Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 507 | 508 | (Page 509) | 510 | 511 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Paroko wa Kanisa Katoliki Paroki ya Mwananyamala, Focus Masawe,  akizindua Kadi maalumu na tiketi kwa ajili ya harambee kuchangia ujenzi na ukarabati wa Kanaisa hilo jijini Dar es Salaam juzi
   Paroko wa Kanisa Katoliki Paroki ya Mwananyamala, Focus Masawe,  akionyesha Kadi maalumu na tiketi kwa ajili ya harambee kuchangia ujenzi na ukarabati wa Kanisa hilo baada ya kuzindua rasmi

   Waumini wa Kanisa Katoliki Paroki ya Mwananyamala wakiimba wakati wa uzinduzi uuzaji wa tiketi na kadi Maalumu ya  harambee ya kuchangia ujenzi na ukarabati wa Kanisa hilo juzi

   Wanakwaya wa Paroko wa Kanisa Katoliki Paroki ya Mwananyamala, wakiimba wakati wa uzinduzi uuzaji wa tiketi na kadi Maalumu ya  harambee ya kuchangia ujenzi na ukarabati wa Kanisa hilo juzi.

   Waumini wa Kanisa Katoliki Paroki ya Mwananyamala wakiimba wakati wa uzinduzi uuzaji wa tiketi na kadi Maalumu ya  harambee ya kuchangia ujenzi na ukarabati wa Kanisa hilo juzi

  Waumini wa Kanisa Katoliki Paroki ya Mwananyamala wakiimba wakati wa uzinduzi uuzaji wa tiketi na kadi Maalumu ya  harambee ya kuchangia ujenzi na ukarabati wa Kanisa hilo juzi


  0 0

  Mgeni rasmi wa hafla hiyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju (kulia) akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu katika hafla ya wanahabari na wahariri waliohitimu mafunzo ya ubobezi katika kuandika habari za dawa za kulevya na uandishi wa habari za maendeleo ya malengo ya milenia wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa vyeti. Mgeni rasmi wa hafla hiyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju (kulia) akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu katika hafla ya wanahabari na wahariri waliohitimu mafunzo ya ubobezi katika kuandika habari za dawa za kulevya na uandishi wa habari za maendeleo ya malengo ya milenia wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa vyeti.Mwakilishi wa Mmoja wa Mataifa na Mkuu wa Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa Tanzania, Dk. Jama Gulaid (kulia) akimpongeza mmoja wa wanahabari kabla ya kupokea cheti chake katika hafla ya wanahabari na wahariri waliohitimu mafunzo ya ubobezi katika kuandika habari za dawa za kulevya na uandishi wa habari za maendeleo ya malengo ya milenia wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa vyeti. Mwakilishi wa Mmoja wa Mataifa na Mkuu wa Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa Tanzania, Dk. Jama Gulaid (kulia) akimpongeza mmoja wa wanahabari kabla ya kupokea cheti chake katika hafla ya wanahabari na wahariri waliohitimu mafunzo ya ubobezi katika kuandika habari za dawa za kulevya na uandishi wa habari za maendeleo ya malengo ya milenia wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa vyeti.Mgeni rasmi wa hafla hiyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju (katikati) akizungumza katika hafla ya wanahabari na wahariri waliohitimu mafunzo ya ubobezi katika kuandika habari za dawa za kulevya na uandishi wa habari za maendeleo ya malengo ya milenia wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa vyeti. Mgeni rasmi wa hafla hiyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju (katikati) akizungumza katika hafla ya wanahabari na wahariri waliohitimu mafunzo ya ubobezi katika kuandika habari za dawa za kulevya na uandishi wa habari za maendeleo ya malengo ya milenia wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa vyeti.Dk. Jama Gulaid Mwakilishi wa Mmoja wa Mataifa na Mkuu wa Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa Tanzania akizungumza katika hafla ya wanahabari na wahariri waliohitimu mafunzo ya ubobezi katika kuandika habari za dawa za kulevya na uandishi wa habari za maendeleo ya malengo ya milenia wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa vyeti. Dk. Jama Gulaid Mwakilishi wa Mmoja wa Mataifa na Mkuu wa Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa Tanzania akizungumza katika hafla ya wanahabari na wahariri waliohitimu mafunzo ya ubobezi katika kuandika habari za dawa za kulevya na uandishi wa habari za maendeleo ya malengo ya milenia wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa vyeti.Mwakilishi wa Mmoja wa Mataifa na Mkuu wa Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa Tanzania, Dk. Jama Gulaid (kulia) akimpongeza mmoja wa wanahabari kabla ya kupokea cheti chake katika hafla ya wanahabari na wahariri waliohitimu mafunzo ya ubobezi katika kuandika habari za dawa za kulevya na uandishi wa habari za maendeleo ya malengo ya milenia wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa vyeti. Mwakilishi wa Mmoja wa Mataifa na Mkuu wa Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa Tanzania, Dk. Jama Gulaid (kulia) akimpongeza mmoja wa wanahabari kabla ya kupokea cheti chake katika hafla ya wanahabari na wahariri waliohitimu mafunzo ya ubobezi katika kuandika habari za dawa za kulevya na uandishi wa habari za maendeleo ya malengo ya milenia wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa vyeti.Baadhi ya wanahabari hao wakielezea changamoto na namna walivyonufaika na mafunzo hayo ya ubobezi katika kuandika habari za dawa za kulevya na uandishi wa habari za maendeleo ya malengo ya milenia wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa vyeti. Baadhi ya wanahabari hao wakielezea changamoto na namna walivyonufaika na mafunzo hayo ya ubobezi katika kuandika habari za dawa za kulevya na uandishi wa habari za maendeleo ya malengo ya milenia wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa vyeti.
  Mwakilishi wa TMF, Bi. Radhia akizungumza katika hafla ya kukabidhiwa vyeti kwa wanahabari wabobezi katika kuandika habari za dawa za kulevya na uandishi wa habari za maendeleo ya malengo ya milenia wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa vyeti. Mwakilishi wa TMF, Bi. Radhia akizungumza katika hafla ya kukabidhiwa vyeti kwa wanahabari wabobezi katika kuandika habari za dawa za kulevya na uandishi wa habari za maendeleo ya malengo ya milenia wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa vyeti.Ofisa Habari wa UNIC, Stella Vuzo (aliyesimama) akizungumza kutoa shukrani kwa washiriki wa hafla hiyo. 
  Ofisa Habari wa UNIC, Stella Vuzo (aliyesimama) akizungumza kutoa shukrani kwa washiriki wa hafla hiyo.Baadhi ya wanahabari hao wakielezea changamoto na namna walivyonufaika na mafunzo hayo ya ubobezi katika kuandika habari za dawa za kulevya na uandishi wa habari za maendeleo ya malengo ya milenia wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa vyeti. Baadhi ya wanahabari hao wakielezea changamoto na namna walivyonufaika na mafunzo hayo ya ubobezi katika kuandika habari za dawa za kulevya na uandishi wa habari za maendeleo ya malengo ya milenia wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa vyeti.Meza kuu ikiwapongeza baadhi ya wanahabari hao wakielezea changamoto na namna walivyonufaika na mafunzo hayo ya ubobezi katika kuandika habari za dawa za kulevya na uandishi wa habari za maendeleo ya malengo ya milenia wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa vyeti. Meza kuu ikiwapongeza baadhi ya wanahabari hao wakielezea changamoto na namna walivyonufaika na mafunzo hayo ya ubobezi katika kuandika habari za dawa za kulevya na uandishi wa habari za maendeleo ya malengo ya milenia wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa vyetiBaadhi ya wanahabari hao wakielezea changamoto na namna walivyonufaika na mafunzo hayo ya ubobezi katika kuandika habari za dawa za kulevya na uandishi wa habari za maendeleo ya malengo ya milenia wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa vyeti. Baadhi ya wanahabari hao wakielezea changamoto na namna walivyonufaika na mafunzo hayo ya ubobezi katika kuandika habari za dawa za kulevya na uandishi wa habari za maendeleo ya malengo ya milenia wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa vyeti.Baadhi ya wanahabari hao wakielezea changamoto na namna walivyonufaika na mafunzo hayo ya ubobezi katika kuandika habari za dawa za kulevya na uandishi wa habari za maendeleo ya malengo ya milenia wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa vyeti. Baadhi ya wanahabari hao wakielezea changamoto na namna walivyonufaika na mafunzo hayo ya ubobezi katika kuandika habari za dawa za kulevya na uandishi wa habari za maendeleo ya malengo ya milenia wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa vyeti.Ofisa Habari wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Bi. Usia Nkhoma akitoa matangazo katika hafla ya wanahabari na wahariri waliohitimu mafunzo ya ubobezi katika kuandika habari za dawa za kulevya na uandishi wa habari za maendeleo ya malengo ya milenia wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa vyeti. Ofisa Habari wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Bi. Usia Nkhoma akitoa matangazo katika hafla ya wanahabari na wahariri waliohitimu mafunzo ya ubobezi katika kuandika habari za dawa za kulevya na uandishi wa habari za maendeleo ya malengo ya milenia wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa vyetiBaadhi ya wanahabari na wahariri pamoja na wageni waalikwa walihudhuria katika hafla ya waliohitimu mafunzo ya ubobezi katika kuandika habari za dawa za kulevya na uandishi wa habari za maendeleo ya malengo ya milenia wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa vyeti. Hafla hiyo ilifanyika ofisi za UN jijini Dar es Salaam juzi. Baadhi ya wanahabari na wahariri pamoja na wageni waalikwa walihudhuria katika hafla ya waliohitimu mafunzo ya ubobezi katika kuandika habari za dawa za kulevya na uandishi wa habari za maendeleo ya malengo ya milenia wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa vyeti. Hafla hiyo ilifanyika ofisi za UN jijini Dar es Salaam juzi.Baadhi ya wanahabari na wahariri waliohitimu mafunzo ya ubobezi katika kuandika habari za dawa za kulevya na uandishi wa habari za maendeleo ya malengo ya milenia wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa vyeti. Hafla hiyo ilifanyika ofisi za UN jijini Dar es Salaam juzi. Baadhi ya wanahabari na wahariri waliohitimu mafunzo ya ubobezi katika kuandika habari za dawa za kulevya na uandishi wa habari za maendeleo ya malengo ya milenia wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa vyeti. Hafla hiyo ilifanyika ofisi za UN jijini Dar es Salaam juzi.

  SERIKALI imesema inaandaa mswada wa sheria ambayo itawalinda watoaji wa taarifa za masuala ya uhalifu ikiwa ni jitihada za kuimarisha mapambano dhidi ya vitendo mbalimbali vya uhalifu nchini Tanzania. Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. George Masaju alipokuwa akitoa vyeti kwa baadhi ya waandishi wa habari waliokuwa katika mpango wa kuandika habari za dawa za kulevya pamoja na mafanikio na changamoto za mpango wa milenia.

   Akizungumza katika hafla hiyo iliyoandaliwa kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa (UN) na Mfuko wa Wanahabari Tanzania (TMF), Masaju alisema kwa sasa ni Sheria ya Makosa ya Rushwa (ufisadi) tu ndiyo inayowalinda watoaji wa taarifa hizo kwani imekataza wao kutajwa tofauti katika maeneo mengine ya sheria. Alisema katika sheria hiyo mpya inayokusudiwa kutungwa na Serikali itapanua wigo wa ulinzi kwa watoaji wa taarifa kutotajwa endapo watatoa taarifa juu ya makosa yoyote jambo ambalo alisema litasaidia katika mapambano ya uhalifu. 

  "Serikali inaandaa muswada wa Sheria ya kuwalinda watoa taarifa wa vitendo vya uhalifu (whistle blowers protection bill) ili kuimarisha mapambano dhidi ya uhalifu wa aina zozote nchini. Kwa sasa ni watoa taarifa wa makosa ya rushwa (ufisadi) tu ndio wanatamkwa katika sheria ya kuzuia na Kupambana na Rushwa, 2007 kulindwa wasitajwe," alisema Mwanasheria Mkuu. 

   Aidha alisema Sheria mpya ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya ya Mwaka 2015 ambayo imepitishwa na Bunge hivi karibuni imetungwa kwa kuzingatia mapungufu ya sheria za nyuma hivyo itakuwa na nguvu zaidi ya kupambana na uhalifu huo tofauti na ilivyokuwa awali. Alikiri kuwa sheria ya awali ilikuwa na mapungufu kadhaa jambo ambalo lilichangia sheria hiyo kushindwa kufanya kazi kikamilifu katika mapambano. 

  Alisema miongozi mwa mapungufu kwa sheria iliyokuwa ikitumika awali ni pamoja na kutotoa adhabu kulingana na ukubwa wa kosa, na haikuainisha masharti bora ya udhibiti wa madawa ya kulevya kama ilivyo kwa sheria mpya. Alisema sheria mpya imeanzisha Baraza la Taifa la Kudhibiti Dawa za Kulevya ambapo mwenyekiti wake ni Waziri Mkuu wa Tanzania na wajumbe wake watatoka pande zote za Muungano yaani Tanzania Bara na Visiwani, alisema kazi kubwa ya balaza hilo ni kusimamia utekelezaji wa Sera ya Udhibiti wa Dawa za kulevya.

   "Sheria iliyopo ina udhaifu wa adhabu, haitoi adhabu kulingana na ukubwa wa kosa kwenye baadhi ya makosa, hivyo kusababisha kukosekana kwa mizania ya haki. Sheria mpya imeweka kima cha kuanzia cha adhabu iwe ni faini au kifungo. ...Mfano sheria mpya imeweka adhabu ya faini isiyopungua milioni 50 na isiyozidi milioni 500 au kifungo kisichopungua miaka 7 na kisichozidi miaka 30 au vyote kwa pamoja." 

  Alifafanua Masaju katika hotuba yake. Jumla ya waandishi wa habari 18 walipata mafunzo ya namna ya kuripoti habari za dawa za kulevya pamoja na kuripoti habari za malengo ya milenia baada ya kuwezeshwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)kwa kushirikiana na mfuko wa wanahabari Tanzania (TMF) na kukabidhiwa vyeti na mgeni rasmi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Masaju.

  0 0

  Waziri mkuu Mstaafu ,Fredrick Sumaye akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine mbalimbali wakiwemo waandaji buda mfupi kabla ya kuanza kwa mbio za Km 21 Katika gate la kuingilia hifadhi ya taifa ya Ngorongoro.
  Waziri mkuu Msaatfu Fredirick Sumaye akikimbia sambamba na rais wa shirikisho la riadha Tanzania,RT,Athony Mtaka(Kushoto kwake) mkuu wa mkoa wa Arusha ,Daud Ntibenda,pamoja na mkuu wa wilaya ya Karatau Omary Kwaang kuashiria kuanza kwa mbio za Ngorongoro Marathoni.
  Maratibu wa Mbio ,Meta Paul akiwa na mmoja wa wasiamamizi ,Leila wakati wakiwaandaa wanariadha kuanza mbio za Km 21 katika lango la kuingilia hifadhi ya taifa ya Ngorongoro.
  Mbio zikianza rasmi.
  Baaadhi ya washiriki katika mbio hizo ,walikuwemo pia wadhamini kama Maremga Investment,hapa Marenga mwenye truck suit nyeusi akijaribu kukimbiza upepo.
  Awawli mbio zikiwa bado ndio zimeanza kundi la wakimbiaji lilionekana wote wanakimbia kwa karibu.
  Muda ulivyosonga na hatua ndivyo zilivyo ongezeka.
  Hatimaye wakaanza kuachana mmoja baada ya mmoja,
  Wengine wakaamua kwenda pamoja ili kupeana moja.
  wengine wakafunguka zaidi.
  Hatimaye wakapatikana wakimbiaji watatu wakaongoza hadi mwisho wa mbio na hawa ni ,Joseph Theofily(katikati),George Gerald (kulia) na Emanuel Giniki.
  Mkimbiaji raia wa Kenya ambaye jina lake halikufahamika mara moja akijaribu kuonesha umahiri wake katika mbio hizo.
  Msichana pekee aliyekuwa akiongoza ni Failuna Abdi .
  Nyuma ya Failuna alikuwepo Nathalia Elisante.
  Mshindi wa kwanza katika Mbio za Ngorongoro Maratahoni 2015 ,Joseph Theofily akimaliza mbio hizo katika uwanja wa Mazingira Bora akitumia muda wa 1:03:09.
  Mshindi wa Pili katika mbio hizo ,George Gerald akihitimisha mbio hizo akitumia muda wa 1:03:36
  Mshindi wa tatu ,Emanuel Giniki akikalimilisha mbio kwa muda wa 1:03:42.
  Giniki akijaribu kupoza koo mara baada ya kumaliza mbio.
  Mkimbiaji wa klabu ya riadha ya Holili,Osward Moris akihitimisha mbio.
  Mshindi wa kwanza kwa kina dada Failuna Abdi akihitimisha mbio katika nafasi ya kwanza baada ya kutumia muda wa 1 :10:25
  Mgeni rasmi katika mbio hizo ,Waziri mkuu Mstaafu ,Fredirck Sumaye akiingia uwanjani huku akihitimisha mbio za km 21 .


  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.


  WANARIADHA wa Tanzania Joseph Theofily wa klabu ya riadha ya Holili ya mkoani Kilimanjaro na Failuna Abdi wa klabu ya riadha ya Winning Spirit ya jijini Arusha wamefanikiwa kupeperusha vyema Bendera ya taifa baada ya kuibuka washindi wa kwanza katika mbio za kimataifa za
  Ngorongoro Marathoni kwa upande wa wanaume na wanawake.

  Mwanariadha Theofily alifanikiwa kumaliza mbio za km 21 akitumia muda wa saa 1:03:09 na kujinyakulia kitita cha sh Mil, 1. mbele ya wakongwe wengine kutoka nchi za Kenya ,Uganda na Malawi huku Gabriely Gerald wa klabu ya Winning Spirit ya jijini Arusha akishika nafasi ya pili akimaliza mbio akitumia saa 1:03:36 na kujinyakulia kitita cha sh laki 5.

  Emanuel Giniki alifanikiwa kushika nafasi ya tatu na kujinyakulia zawadi ya sh 250,000,nafasi ya nne ikichukuliwa na Ezekiel Therop huku mwanariadha Mohamed Msenduki wa klabu ya Wining Spirit ya jijini Arusha akimaliza nafasi ya tano.

  Mwanariadha wa kike Failuna aliyerejea hivi karibuni kutoka nchini Brazil kushiriki mashindano ya mbio za Km 15 ambazo alifanikiwa kumaliza mbio hizo katika nafasi ya saba,aliwaongoza wakongwe kama Banuelia Bryton ,Marry Naali Jackline sakilu na Catherine Range akimaliza mbio katika nafasi ya kwanza kwa kutumia muda wa saa
  1:10:25.

  Failuna aliyejinyakulia zawadi ya kitita cha kiasi cha sh Mil,1. alifuatiwa kwa karibu na mpinzani wake Nathalia Elisante aliyetumia muda wa 1:14:40 na kuzawadiwa kitita cha sh 500,000 huku nafasi ya tatu  ikichukuliwa na Magdalena Crispine aliyetumia muda wa 1:15:56, nafasi ya nne na tano ikienda kwa Anjelina Tsere na Merry Naali.

  Mbio za kimataifa Ngorongoro Marathoni zinafanyika zikiwa na lengo la kuwawezesha watoto wa jamii ya kimasai kupata elimu ikiwemo kumalizia shule ya Endulen iliyoko Ngorongoro na kutangaza urithi wa utalii kupitia hifadhi ya taifa ya Ngorongoro huku ikishirikisha pia mbio za Kilomita tano kwa wafanyakazi wa taasisi mbalimbali pamoja na  Km 2.5 kwa wanafunzi.


  Kwa picha zaidi ingia hapa,

  www.dixonbusagaga.blogspot.com

  0 0

  mic1
  mic2
  Katibu msaidizi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (NACTE) Mhe. Alex Mkondola akikagua timu za Bandari na IFM wakati wa mchezo wa Ufunguzi kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwishoni mwa juma(Picha kwa Hissani ya Miss Demokrasia Tanzania).


  Na: Faraja Nyota.

  Fainali za kwanza za michezo ya vyuo vya elimu ya kati NACTE TANZANIA, zimezinduliwa siku ya jumamosi tarehe 18 kwenye viwanja vya chuo kikuu cha Dar es Salaam, ambapo Mgeni Rasmi aliyefanya Uzinduzi huo ni Katibu msaidizi wa NACTE, Mhe. Alex Mkondola.

  Ufunguzi huo ulizihusisha timu zilizokuwa kundi A, pamoja na zile za kundi B zilizopo kwenye viwanja vya Chuo cha Mwalimu Nyerere Memorial-Kigamboni, katika mchezo wa mpira wa miguu uwenye msisimko mkubwa ukilinganisha na michezo mingine.

  akizungumza wakati wa Uzinduzi huo Mgeni rasmi aliwaasa washiriki wote kuitumia michezo hii kama sehemu ya wao kubadilishana mawazo pamoja na kuijenga miili yao kimichezo ” jambo hili la uwepo wa hii michezo ni jambo la kujivunia kutokana na kwambsasa wale wote wenye vipaji mtaviendeleza lakini kubwa ikiwa ni kubadilishana mawazo miongoni mwenu, isipokuwa natarajia kwamba mtaitumia michezo hii kushiiki kwa utulivu ili iweze kuleta tija na iwe ya msisimko kila mwaka” alisema Mkondola.

  Michezo hiyo inahusisha juma ya vyuo 18 vilivyofanikiwa kuingia hatua hiyo baada ya kufuzu kuvuka katika hatua ya awali ya makundi 11 yaliyokuwa na timu 10 kila kundi katika idadi ya vyuo 115 vya Dar es salaam na Pwani.
  Michuano hiyo inatazamiwa kufanyika june 21 kwenye viwanjia vya chuo kikuu cha Dar es Salaam UDSM ambapo timu zilizopo kwenye michuano hiyo ni pamoja na  kundi A lenye timu za Mwalimu Nyerere Memorial Academy
  Bandari College, College of Social Science, National Institute of Transport, Institute of Finance Management
  Kilimanjaro Institute College.

  timu zinazounda kunda B ni pamoja na St. Joseph College, College of Business Education, Elimu ya Watu Wazima, 
  Tanzania Institute of Accountancy (TIA) Muhimbili Medical Schools, College of Engineering and Technology huku kundi a mwisho likiwa na timu za Njuweni Institute of Hotel, Catering & Tourism Management, Tanzania Revenue Authority
  University of Dar es Salaam Business School, Bagamoyo College of Arts (TaSUBa), Dar es salaam City College(DACICO), Dar es Salaam Institute of Tecknology (DIT)

  0 0

   Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mungereza (kushoto), akizungumza wakati wa hafla ya kumtangaza mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika, Mayunga Nalimi (katikati), katika tafrija iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia (kulia),
   Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mungereza (kushoto), akimkabidhi tuzo mwimbaji Mayunga Nalimi baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika, katika tafrija iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia (kulia), ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso.

   Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mungereza (kushoto), akimpongeza mwimbaji Mayunga Nalimi baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika, katika
  tafrija iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia (kulia), ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso.

  0 0

  Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile kushoto kwake kwa pamoja wakifuatilia kwa makini mkutano wa 10 wa kisheria wa kundi la Afrika (Afrikca Group Constituency) uliokuwa ukiendelea mjini Washington DC.
  Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akiwa na Katibu Mkuu wa kwa pamoja wakifuatilia kwa makini mkutano wa 10 wa kisheria kundi la Afrika (Afrikca Group Constituency) uliokuwa ukiendelea mjini Washington DC.
  Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile kushoto kwake kwa pamoja wakifuatilia kwa makini mkutano wa 10 wa kisheria wa kundi la Afrika (Afrikca Group Constituency) uliokuwa ukiendelea mjini Washington DC.
  Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile kushoto wakifuatilia semina iliyokuwa ikitolewa kuhusu uimarishaji wa makazi mijini.


  Wakati Mikutano ya Benki ya Dunia na Shirika la kifedha la kimataifa ikiendelea hapa Mjini Washington Dc. Mawaziri wa fedha wameweka misimamo yao juu ya sera ambazo zinawekwa na Benki ya Dunia.

  Akizungumza na vyombo vya habari,waziri wa fedha wa Tanzania Mhe. Saada Salum Mkuya alisema” Sisi kama nchi tuliwasilisha nini tunaona katika utekelezaji wa mipango ya Benki. Tumeshukuru sana Benki ya Dunia kwa kuendeleza mipango ya kuweza kusaidia nchi za kiafrika ,hususan kwenye mipango ya kujenga miundo mbinu ya kiuchumi kama vile barabara,   kilimo pamoja na miundo mbinu ya maji na umeme”.

  “Lakini vilevile tumeonyesha wasiwasi wetu kutokana na sera ambazo Benki ya Dunia imeziweka, kama vile kuangalia sera zile za watu wa kiasili ya kiafrika, sisi tumehisi mbali ya nia nzuri na njema ya Benki hii ya Dunia, lakini inaweza kuwa ni kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya nchi zetu kwa sababu sera hiyo inaweza kutumika kuigawa nchi ambayo misingi yake imekuwa ikijengwa kwa umoja kutoka uhuru”.Alisistiza Mkuya.

  Hakuishia hapo aliendelea kutoa mfano kuwa “sisi watanzania tumekuwa wamoja ingawa tuna lugha mbalimbali kutokana na makabila tofauti. Lakini tumekuwa pamoja kwa kipindi cha miaka 50.Kwa hiyo tumeona sera hiyo isije ikatumika kwa ajili ya kuwa kigezo cha utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini . Sisi kama wa Afrika na viongozi wa Afrika tunashirikiana kuona kuwa sera zinazowekwa hazitukwamishi”.

  Hali hii ya kudai uasilia (indigenous) imeibuka zaidi katika miongo hii miwili, wakati kukiwa kumejitokeza watu wanaodai kuwa wao hawatambuliki na hoja hii inaihusu hasa nchi ya Tanzania.

  Mawaziri wa Fedha kutoka Afrika wamejadili mambo mbali mbali ambapo ni pamoja na masuala ya maendeleo na mahusiano yao na Benki ya Dunia.

  Katika Mkutano huo wa kisheria Mkurugenzi Mtendaji ndiye ambaye amewasilisha maazimio ya Benki katika kipindi cha miezi sita.Aliongeza Mkuya.

  Aidha katika mkutano huo pia walizungimzia suala la Ebola. “Kwa kweli wamekubali kusaidia nchi zile ambazo zimekumbwa na gonjwa hili lakini wamezitaka nchi za afrika na zenyewe kushirikiana katika kupambana na gonjwa hili”.Alimalizia Mkuya.

  Mikutano hiyo bado inaendelea hapa mjini Washington DC. Hali ya hewa ni baridi kiasi.

  0 0

   Makamu Mwenyekiti wa chama cha wapagazi nchini(TPO) Loshiye Mollel
  akizungumza katika mkutano wa wapagazi na mfuko wa NHIF mkoa wa Arusha.
   Mfamasia wa NHIF Mshindo Msulle akitoa mada huu ya huduma za NHIF hasa maduka ya dawa ambayo wanaweza kupata madawa pindi watakapokosa hospitali.
  Afisa matekelezo wa mfuko wa bima ya afya mkoa wa Arusha, Desderius
  Buhiye alitoa elimu juu ya huduma zinazotolewa na NHIF


  Zaidi ya vijana  20,000 wanaofanya kazi ya kubeba mizigo ya
  watalii,(wapagazi) katika Mlima Kilimanjaro na Meru ,wametakiwa kujiunga na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) ili kujihakikisha huduma bora ya afya .

  Meneja wa NHIF mkoa Anisia Ngweshem alitoa wito huo , katika mkutano wa Wapagazi , ulioandaliwa na chama cha wapagazi(TPO),uliofanyika katika ukumbi ya Golden View jijini hapa.

  Ngweshem alisema, NHIF ina huduma bora za kuwapatia matibabu watanzania ikiwepo huduma mpya ya kulipia kwa mwaka 76,800 makundi maalum. Akizungumzia huduma za afya kwa wapagazi, Mwenyekiti wa bodi ya TPO AlexLemenge alisema chama hicho, kinaandaa utaratibu wa kuhakikisha wapagazi wote wanajiunga na mifuko ya bima za afya.  Alisema utaratibu huo, utaondoa matatizo ya wapagazi kufariki kwa kukosa
  huduma bora za afya kutokana na kazi ngumu wanayofanya kubeba mizigo ya watalii na kupanda milima.

  Awali Makamu mwenyekiti wa TPO, Loshiye Mollel aliomba serikali kuwaunga mkono wapagazi ili waweze kupata maslahi bora ambayo ndio yatawapatia huduma bora za za afya.

  "tumekuwa na mgogoro na makampuni ya utalii kwa zaidi ya mwaka sasa,
  tunaomba yatekeleze maelekezo ya serikali kulipa ujira kwa siku kati ya Tsh
  12,000 hadi 15,000 lakini hadi sasa ni makampuni 28 tu kati ya Zaidi ya 400
  ndio yanalipa"alisema.

  Katika mkutano huo, wapagazi waliunga mkono, mpango wa kujiunga na NHIF
  huku wakitaka uongozi wa TPO kwa kushirikiana na taasisi nyingine
  kushinikiza malipo bora kwa kazi yao. kwa hisani ya libeneke la kaskazini blog.


   Baadhi ya wapagazi wakiwa mkutano wao wa kanda mjini Arusha.ukumbi wa golden View.

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki akizungumza na watendaji , waganga wakuu wa wilaya na mkoa wa mkoa wa Dar es salaam leo wakati akizindua Mpango Kazi wa kuharakisha kupunguza vifo vya akina mama na watoto walio chini ya miaka 5 kwa mkoa wa Dar es salaam.
   Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akizungumza na watendaji , waganga wakuu wa wilaya na mkoa wa Dar es salaam leo kueleza nafasi yake katika kusimamia utekelezaji wa wakati Mpango Kazi wa kuharakisha kupunguza vifo vya akina mama na watoto walio chini ya miaka 5 kwa mkoa wa Dar es salaam.
   Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dkt. Grace Maghembe akiwasilisha mpango Kazi wa Kuharakisha kupunguza vifo vya akina mama, Watoto wachanga na watoto walio chini ya umri wa miaka 5 kwa mkoa wa Dar es salaam.  
  Baadhi ya watendaji wa mkoa , waganga wakuu wa wilaya na mkoa  wa Dar es salaam waliohudhuria uzinduzi wa Mpango kazi wa Kupunguza Vifo vya akina mama wajawazito na Watoto chini ya miaka 5 leo wakimsikiliza Mkuu wa mkoa huo Mhe. Sadiki Meck Sadiki (hayupo pichani) Picha/Aron Msigwa.  RC DAR ES SALAAM AZINDUA MPANGO KAZI WA KUHARAKISHA KUPUNGUZA VIFO VYA AKINA MAMA NA WATOTO CHINI YA MIAKA 5  AKEMEA WATUMISHI WAZEMBE.

  Na. Aron Msigwa – MAELEZO.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki amezindua Mpango  Kazi wa kuharakisha kupunguza vifo vya akina mama na watoto walio chini ya miaka 5 kwa mkoa wa Dar es salaam na kukemea tabia ya baadhi ya watumishi wasio waadilifu wanaotumia lugha za kuudhi, kejeli na vitendo vya unyanyasaji kwa akina mama wajawazito wanaofika kupata huduma za uzazi katika hospitali, vituo vya afya na Zahanati.

   Akizungumza  katika kikao kilichowahusisha watendaji wa mkoa , waganga wakuu wa wilaya na mkoa wa Dar es salaam leo jijini Dar es salaam, Mhe. Sadiki amesema watumishi wa afya  wa mkoa huo wanao wajibu wa kutekeleza majukumu yao na kutimiza malengo yaliyowekwa na Serikali ya kuwapatia huduma bora za afya akina mama wajawazito na watoto walio na umri chini ya miaka 5 yaliyowekwa na mkoa.

  Amesema kuwa katika kutekeleza mpango kazi huo Serikali haitasita kuwachukulia hatua za kinidhamu na kisheria watumishi wa afya watakaobainika kushiriki katika vitendo ubadhirifu na wale watakaosababisha kwa namna moja au nyingine vifo vya mama wajawazito na watoto chini ya miaka 5 watakaofika hospitalini kupata huduma za afya na kupoteza maisha yao kutokana na uzembe wa watumishi katika vituo husika.

  Amebainisha kuwa mkoa Dar es salaam pamoja na mambo mengine umeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa inawafikia akina mama na watoto na kuwapatia huduma bora akina mama wajawazito wanaofika katika vituo vya afya vya Serikali kupata huduma za uzazi ili kukabiliana na vifo vya akina mama na watoto vinavyotokea.

  Ameeleza kuwa Tanzania imekuwa ikitekeleza malengo ya millennia (MDG)ambayo yalipangwa kukamilika ifikapo Desemba 2015 na kuongeza kuwa katika utekelezaji wa malengo hayo bado inakabiliwa na changamoto za kupunguza vifo vya wajawazito ambavyo amesema kwa takwimu za mwaka 2013 zinaonyesha vifo 410 kwa kila vizazi hai 100,000.

  “ Tanzania katika jambo hili tumepiga hatua japo bado tunakabiliwa na changamoto ya kuendelea kupunguza vifo hivyo kufikia 133 kwa kila vizazi hai 100 if ikapo mwezi Desemba 2015” 

  Amesema akiwa kiongozi wa mkoa huo atahakikisha lengo hilo linatimiza kabla ya muda uliopangwa na kuwataka watendaji wa afya kwa ngazi zote kutimiza wajibu wao ipasavyo na kuzitumia rasilimali zilizopangwa kutekeleza malengo yaliyopangwa ili kuhakikisha kuwa vifo vinavyotokana na uzazi na vile vya watoto wachanga vinapungua . 

  “Nachoweza kusema, uwezo wa kukabiliana na changamoto hii tunao tukiunganisha nguvu zetu kwa mazingira tuliyonayo  ya taasisi za Serikali na Binafsi bado tunayo nafasi nzuri ya kutimiza malengo yaliyowekwa, kwa sasa tunaendelea na mkakati wetu wa kuongeza wodi za kujifungulia akina mama wajazito  wilaya ya Temeke, Ilala na Kinondoni ili kuongeza wigo wa huduma za afya” Amesemaa.

  Ametoa wito kwa wataalamu wa afya kuendelea kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa akina mama wajawazito ili waweze kuelewa umuhimu wa kuhudhuria Kliniki kabla na baada ya kujifungua za afya kupitia mpango wa TIKA utakaoanzishwa katika jiji la Dar es salaam utakaowawezesha kupata huduma za afya kwa mwaka mzima kwa gharama nafuu.

  Katika hatua nyingine Mhe. Sadiki amewataka wakurugenzi wa manispaa za Dar es salaam kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya motisha kwa watumishi wa afya wanaotumia muda mwingi kazini wakiwahudumia wagonjwa hususani akina mama wachanga na watoto chini ya miaka 5 wa mkoa huo.

  Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dkt. Grace Maghembe awali akiwasilisha Mpango  Kaziwa Kuharakisha kupunguza vifo vya akina mama, Watoto wachanga na watoto walio chini ya umri wa miaka 5 kwa mkoa wa Dar es salaam  amesema  kuwa licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali toka kuzinduliwa kwake miaka 2 iliyopita na Rais Jakaya Kikwete umepata mafanikio.

  Amesema kuwa pamoja na kuongezeka wa idadi ya wazazi wanaojifungua kutoka 97,807 hadi 134,838 mwaka 2012 hadi 2014 vifo vya uzazi vimepungua kutoka 123 hadi 99 katika vizazi hai 100,000.

  Amesema mafanikio zaidi ya huduma ya afya ya mama na mtoto katika mkoa wa Dar es salaam bado yanakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo  kiwango kidogo cha matumizi ya huduma ya uzazi wa mpango wa asilimia 47, kiwango kidogo cha asilimia 51 ya wajawazito wanaohudhuria Kliniki angalau mara 4 chini ya lengo kitaifa ambalo ni asilimia 90.

  Aidha ameeleza kuwa mkoa unaendelea kuchukua hatu mbalimbali za kuhakikisha kuwa huduma ya afya ya mama na mtoto inaimarika katika jiji la Dar es salaam kwa kuiweka huduma hii kuwa kipaumbele cha mkoa na kuongeza usimamizi shirikishi wa huduma za afya, mafunzo kazini kwa watumishi, kuongeza vitendea kazi, dawa na vifaa tiba pamoja na kuhamasisha ushiriki wa wadau na wafadhili mbalimbali.

  0 0

  On Friday the 24th April 2015, His Excellency Dr. Jakaya Mrisho Kikwete will officially launch the much anticipated photographic book which celebrates and covers the historic journey of the 50 years of the United Republic Of Tanzania.

  The book will be launched at The Serena Hotel, which is located at the heartbeat and the city center of Dar es Salaam, Tanzania.

  The book, which comprises of over 444 pages describing in detail the historic journey of Zanzibar and then Tanganyika (Tanzania Mainland), covering the rich historical background and the political journey prior to the Union in 1964 and also the political journey of the factual events from 1964 until 2014.

  This book is believed to be the only book of excellence in terms of its contents about the Photographic Journey of the Union and has been published, written and edited by Tanzanians. The most exceptional story of this book is that it has been blessed by both the existing Presidents, Dr Jakaya Mrisho Kikwete and Dr. Ali Mohamed Shein by both having agreed to do the foreword for this book. Furthermore, it remains to be the only book that carries the foreword of both the Presidents of the United Republic of Tanzania and Zanzibar respectively and furthermore they are the current Presidents in power. 

  This book is anticipated to bring a lot of excitement to the general public and our fellow Tanzanians in terms of using the book for historical research and educational purpose. Some of the pictures that have been published in this book are appearing in public for the first time.

  In addition to the above, the book will serve as a catalyst to promote tourism, investment and business aspect of Tanzania as special chapters on cultural tourism and business institutions has been incorporated.

  For more information call Maryam on  0778 004 658 for interviews with writers and publishers. 

  OR  CLICK THE  THE FOLLOWING LINK FOR HIG RES IMAGES AND PHOTOS


  0 0


  0 0

  SAD6Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia ukanda wa Afrika Bw. Makhatar Diop na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier,wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya alipokuwa akitoa msimamo wa Tanzania katika mkutano huo uliofanyika mjini Washington DC.
  Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akipiga mahesabu ya haraka haraka na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile, baada ya kuulizwa swali na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia ukanda wa Afrika Bw. Makhatar Diop,( hayupo kwenye picha).Kulia ni Bw. Rished Bade Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania na kushoto ni Gavana msaidizi wa Benki kuu ya Tanzania Bi. Natu Mwamba.
  sad2Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia ukanda wa Afrika Bw. Makhatar Diop pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier wakitafuta kitu cha kumuuliza Waziri wa fedha (hayupo kwenye picha)katika mkutano uliofanyika mjini Washington DC.
  sad3Ujumbe wa Mkutano huo kutoka pande zote mbili yaani Tanzania na Benki ya Dunia, wakiwaangalia wajumbe waliokuwa wakijitambulisha.sad4Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akijibu maswali aliyokuwa akiulizwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia ukanda wa Afrika Bw. Makhatar Diop aliyeko mbeleyake.Kulia kwa Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile akifuatiwa na Bw. Rished Bade Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania.
  sad5Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akijibu maswali aliyokuwa akiulizwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia ukanda wa Afrika Bw. Makhatar Diop aliyeko mbeleyake.Kulia kwa Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile akifuatiwa na Bw. Rished Bade Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania.
  Picha zote na Ingiahedi C. Mduma – Washington DC.

  0 0

  Mkuu wa Wialaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda akikagua Mazingira ya Soko la ndizi la Lililopo Mabibo akiwa ameambatana na Viongozi wa wafanyabiashara wa soko hilo leo alipofika kusikiliza kilio chao.Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ametembelea Soko hilo leo mara baada ya viongozi wa soko hilo kufikisha kilio chao cha muda mrefu  kwake na Ndipo alipoamua kufika mara moja kuwasikiliza.

  Wafanyabiashara hao kilio chao kikubwa kwa Mkuu wa wilaya hawajui hatma ya biashara yao Sokoni hapo kwa kuwa  eneo wanalofanyia biashara sio rasmi kwajili ya soko  ni Mali ya Kiwanda cha Urafiki.Wafanyabiashara hao wakimweleza zaidi Mkuu wa wilaya wamesema Kutokana na kutokutambulika kwa eneo hilo kama eneo la soko kunawanyima fursa mbalimbali ikiwemo Mikopo kwa kuwa eneo hilo halitambuliki.

  Wafanyabiashara ambao wapo takribani 10000 hao wakieleza zaidi walisema wako hapo kwa muda mrefu lakini hawajui hatma ya maisha yao.Pia Miundombinu ya Soko haifai kabisa hali inayosababishwa kutokutambulika kama sehemu ya soko.
   Mkuu wa Wialaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Akipatiwa Maelezo zaidi kuhusu eneo la Soko hilo kutoka kwa Mwenyekiti wa Soko Hilo Ndugu Idd Pazi kwa niaba ya Wafanyabiahara wa Soko Hilo.
   Mkuu wa Wialaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Ndizi lililopo Mabibo leo.Aidaha Mkuu wa Wialya wakati akijibu amewaambia amepokea kwa mikono Miwili Kilio chao Atalifanyaia kazi kwa haraka kwa kushirikiana na ngazi mbalimbali za Maamuzi na Mapema atawajibu.Mkuu wa Wilaya akieleza zaidi amesema Ngumu sana kwake  kutoa ahadi ambayo itakuwa ngumu kutekelezeka kwa kuwa Eneo hilo ni Mali ya Kiwanda cha urafiki na kiwanda kimebinafsishwa ni ngumu kuaahi kama watalipata eneo hilo kwajili ya Soko Bila kujua Mipango ya Kiwanda kuhusu eneo hilo. 
   Mkuu wa Wialaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda alitumia Mkutano huo na Wafanyabiashara kuwaeleza Mipango na Mikakati yake iliyokwisha kuanza na ambayo ataianzaisha hivi karibuni kwajili ya Kutatua kero zinazowakabili wakazi wa wilaya ya Kinondoni.Akieleza Zaidi Mh Makonda amesema kwenye ofisi yake kila siku ya Jumanne ni  siku ya Kumwona Mkuu wa Wilaya kwahiyo ametoaa rai wa wakazi wote wa kinondoni wenye matatizo Mbalimbali Kufika ofisini kwake kila Jumanne Kumwona.Pia kwa wale wakazi wa Kinondoni wenye migogoro ya Ardhi Kufika ofisini kwake kila siku ya Ijumaa yuo kwajili ya kutatua kero za wanakinondoni
   Baadhi ya Wafanyabiashara wa Soko hilo wakimsikiliza kwa makini 
   Mkuu wa Wialaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Wakati ikajibu baadhi ya Kero za wafanyabiashara hao.
   Mkuu wa Wialaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Akipokea Baadhi ya Zawadi alizopewa na wafanyabiashara wa Soko la Ndizi la Mabibo.

  0 0

  Baadhi ya washiriki wa mkutano wa masuala ya Ugunduzi wa Digitali Afrika wa mwaka 2015 'Innovation Africa Digital (IAD) uliyofanyika nchini Zimbabwe ambapo Huawei ikiwa mshiriki iliahidi kushirikiana na nchi za Afrika katika kukuza sekta ya Teknohama. 

  KAMPUNI nguli katika sekta ya  teknolojia  ya habari na mawasiliano ya Huawei imeomba uwepo wa ushirikiano baina yake na mataifa ya Afrika hususani katika nyanja za teknolojia ya habari na mawasiliano (TEKNOHAMA).


  Kwa mujibu wa Makamu wa Raisi wa kampuni hiyo katika ukanda wa Mashariki na Kusini Bw David Wang, hatua hiyo inalenga kutimiza adhma ya pamoja baina ya kampuni hiyo na mataifa ya Afrika katika kuunganisha bara hilo katika mfumo wa mawasiliano.

  “ Ili kufanikisha adhma hii ya kuunganisha bara hili katika mfumo wa mawasiliano, Huawei tunategemea zaidi ushirikiano kutoka kwenye serikali za mataifa ya Afrika,’’ alisema  Bw Wang kwenye Mkutano wa mwaka wa masuala ya uvumbuzi wa digitali (IAD) uliofanyika mjini  Victoria Falls, Zimbabwe hivi karibuni.

  Kama mdau maalumu kwenye mkutano huo, kampuni hiyo ilipata fursa ya kuonyesha uvummbuzi wake kwenye masuala ya TEKNOHAMA pamoja na vifaa vyake. Kwa mujibu wa Bw Wang, ili kuenda sambamba na kaulimbiu 'UpatikanajiNafuu’ ya mkutano huo , Huawei  kwa sasa wanatengeneza mtandao wa miundombinu ya mawasiliano, ikiwemo mitandao wa LTE kwa ajili ya taifa laZimbabwe.

  Mradi huo unalenga  kuziba pengo la maendeleo ya kidigitali kwa kuongeza eneo linalofikiwa na mtandao wa mawasiliono nchini humo pamoja na huduma kwa bei nafuu. “Lakini pia kwenye hili vipaji vya TEKNOHAMA ni muhimu sana kwa maendeleo ya bara hili. Huawei inajikita zaidi pia kwenye kuandaa vipaji hivi kwenye bara hili.’’ Alisema

  Akielezea zaidi Bw Wang alisema mnamo mwezi Oktoba mwaka huu Huawei kwa kushirikiana na Serikali ya Zimbabwe watatekeleza mpango wa kijamii wa kampuni hiyo uitwao “Mbegu kwa ajili ya baadae’ utakaotoa fursa kwa wanafunzi 10 kutoka nchini humo kupata mafunzo ya TEKNOHAMA katika makao makuu ya kampuni hiyo nchini China.

  Akizungumza kwenye Mkutano huo, Waziri wa TEKNOHAMA, Posta nahuduma za usafirishaji nchini  Zimbabwe Bw. Supa Mandiwanzira alionyesha kutambua kampuni ya Huawei kama nguli wa masuala ya TEKNOHAMA ulimwenguni na yenye utaalamu na uzoefu kiutandawazi katika kutoa hudumanafuu za masuala ya TEKNOHAMA nchini humo.

  Mkutano huo wa siku mbili (kutoka Aprili 14-16)ulihusisha washiriki 500,wakiwamo watunga sera, mashirka simamizi, watoa huduma na watumiaji wa kuu wa TECNOHAMA kutoka Afrika na sehemu nyingine dunia, kwa lengo la kutoa huduma muhimu kwa wanahisa , ili kuboresha mazingira ya teknolijia hiyo na kukuza maendeleo ya sekta hiyo.


  0 0

   Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philip Mangula (kushoto), akihutubia katika mkutano wa wajumbe wa Halmshauri kuu ya CCM, matawi, wenyeviti wa serikali za mitaa na wajumbe wao na mabalozi wa chama hicho wilaya ya Ilala, uliohusu utekelezaji wa ilani na mchakato wa uchaguzi mkuu uliofanyika Dar es Salaam leo asubuhi. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala, Asaa Simba.
   Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala, Asaa Simba akimkaribisha Mangula kuzungumza na wanaccm wa wilaya ya Ilala.
   Mbunge wa Jimbo la Ilala,  Mhe Mussa Azan 'Zungu' akitoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM katika jimbo hilo mbele ya Mangula na viongozi wengine kwenye mkutano huo. Kwa habari kamili na picha zaidi

  0 0

  SAM_2087
  Mratibu wa Kambi ya matibabu Arusha katika kituo cha kutoa huduma kwa
  wanawake (MMC)kilichopo mkabala na Hoteli ya Impala, ambapo ushauri huo unatolewa, Austin Makani akizungumza na waandishi wa habari  juu ya ujio wa madaktari bingwa kutoka India kwaajili ya kuwaona wagonjwa wenye matatizo ya Moyo,Tumbo,Upasuaji wa saratani,Mishipa ya fahamu na uti wa mgongo,Shida za Figo,Mifupa,upasuaji wa jumla na upasuaji wa kupunguza uzito,zoezi hilo litafanyika kwanzia tarehe20-22 Aprili 2015(Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
  SAM_2071
  Madaktari bingwa kutoka India
  SAM_2085
  Daktari bingwa kutoka India katika hospitali ya Apollo Abhijit Singh akizungumza jambo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Arusha katika kituo cha MMC Health.
  SAM_2084
  Wagonjwa wakiwa wanasubiria kupata huduma
  SAM_2091
  Mmiliki wa mtandao wa http://jamiiblog.co.tz Pamela Mollel akiwa katika picha ya pamoja na Madaktari bingwa kutoka India
  SAM_2077
  Sehemu ya waandishi wa habari wakiwa kazini
  SAM_2075

  MADAKTARI bingwa kutoka hospitali ya  SPS Apollo iliyopo  Ludhiana

  nchini India wamewasili nchini na kuanza kutoa huduma ya ushauri bure
  kwa magonjwa makubwa ambayo yamekuwa yakiwasumbua watu wengi na
  kuwalazimu  kwenda kutibiwa nchini India.

  Akizungumza na waandishi wa habari katika kituo cha kutoa huduma kwa
  wanawake (MMC) ambapo ushauri huo unatolewa, Mratibu wa Kambi hiyo ya
  matibabu Arusha, Austin Makani alisema kuwa , madaktari bingwa hao
  wanatoa ushauri kwa wagonjwa wenye matatizo ya Figo , Moyo, tumbo,
  saratani, mishipa ya fahamu, uti wa mgongo, upasuaji wa kawaida na wa
  kupunguza uzito.

  Austin alisema kuwa,  ujio wa madaktari hao watano kutoka  nchini
  India umeratibiwa na kituo  cha kutoa huduma kwa wanawake (MMC) kwa
  kushirikiana na hospitali ya SPS Apollo iliyopo Ludhiana nchini India
  na wamefikia hatua hiyo baada ya kugundua kuwa wagonjwa wengi
  wanaoenda kutibiwa nchini India wanasumbuliwa na magonjwa hayo.

  Alisema kuwa, uwepo wa madaktari hao bingwa kwa siku tatu utasaidia
  sana wananchi wa jiji la Arusha kufika na kupewa ushauri bure juu ya
  magonjwa yanayowasumbua na hivyo kuokoa gharama ya kusafiri hadi
  nchini India kufuata huduma hizo.

  ‘hapa sisi wanachofanya madaktari hawa bingwa ni kusikiliza wagonjwa
  na baada ya kupata maelezo wanapata ushauri bure wa kwenda kupima
  kulingana na ugonjwa alionao na baada ya kurudisha majibu ndipo
  tunamwandikia dawa ya kutumia na kama ugonjwa wake unahitaji kutibiwa
  India tunampunguzia  gharama  kidogo ya kwenda kutibiwa India ‘alisema
  Austin.

  Alisema kuwa, uwepo wa kambi hiyo ya matibabu jijini Arusha unatoa
  fursa pia kwa wagonjwa waliokuwa wakatibiwe nchini India kutokana na
  magonjwa yanayowasumbua na kuweza kupata ushauri wa haraka na wakti
  mwingine kuepuka gharama za kusafiri.

  Wakizungumza  katika kituo hicho, Madaktari hao bingwa ,Abhijit Singh
  na Atul Behll kutoka hospitali ya SPS Apollo India  walisema kuwa
  ,changamoto kubwa iliyopo katika nchi za kiafrika ni watu wengi
  kutokuwa na utamaduni wa kwenda kupima afya zao ,hivyo aliwataka
  wananchi wa mkoa wa Arusha na mikoa jirani kufika kwa wiki ili kupata
  ushauri juu ya afya zao.

  Walisema kuwa,nchini India  kuna watanzania wengi wanaopata matibabu
  kutokana na magonjwa yaliyotajwa ,hivyo wakaona kuna umuhimu mkubwa
  kwa wao kuwafikia na kuweza kutoa ushauri bure na hatimaye kupunguza
  gharama za kwenda nchini India.

  0 0

   Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja na Shughuli za Kanda wa Bohari ya Dawa (MSD),  Edward Terry (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ukumbi wa Idara Habari Maelezo jijini Dar es Salaam mipango ya MSD na mambo mengine. Kushoto ni Ofisa Uhusiano wa MSD, Etty Kusiluka.
   Etty Kusiluka akitoa ufafanuzi wa masuala kadhaa.
   Mkutano na wanahabari ukiendelea.
  Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

  Dotto Mwaibale
  WASIMAMIZI  wa vituo vya afya, zahanati, hospitali za wilaya, mkoa na hospitali za rufaaa wametakiwa kuwa makini katika kusimamia utoaji wa dawa na vifaa tiba ili kutoa matumizi ya dawa na vifaa tiba ili kuhakikisha vinatosheleza idadi ya watu katika eneo husika.

  Wito huo ulitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa huduma kwa wateja na shughuli za kanda wa Bohari ya Dawa (MSD),  Edward Terry wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam katika ukumbi wa wa idara habari maelezo.

  "Wasimamizi wa vituo vya afya na hospitali huleta maoteo ya dawa na vifaa tiba kulingana na idadi ya watu walionao kwenye maeneo yao na mara nyingi uangalia magonjwa yanayoshambulia zaidi maeneo hayo hivyo hakutakiwi kuwa na uhaba wa dawa endapo usimamizi mzuri utazingatiwa, alisema Terry.


  Akitolea mfano wilaya ya Iramba, Igunga, Bariadi, babati , Arumeru na Sumbawanga kutokuwa na tatizo la dawa ambapo hufuata kanuni na sheria za uagizaji wa dawa kutoka bohari ya dawa pamoja na kutumia vyanzo vingine vya mapato kuongezea bajeti inayotolewa na serikali.

  Pamoja na hilo  Teryy aliongeza kuwa usimamizi makini wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ndiyo utakaofanya changamoto ya ukosefu wa dawa kwenye hospitali na vituo kukoma.

  "MSD imeboresha huduma na kumpatia mteja taarifa muhuimu zinazomhusu kwa kuziweka wazi taarifa hizo kwenye mtandao ambapo atapata fursa ya kupata taarifa hizo muda wowote.

  Alitaja taarifa hizo kuwa ni pamoja na orodha ya dawa na vifaa tiba zilizopo gharani, bei zake na picha za kifaa husika. Taarifa zingine zilizopo kwenye mtandao wa MSD ni pamoja na mgawo wa fedha kwa kila kituo na hospitali uliotolewa na serikali, fomu ya malalamiko na mrejesho.

  Terry aliongeza kuwa baadhi ya  hospitali na vituo vya afya  na wafanyakazi wasio waaminifu ambao wanadiliki kuzichepusha dawa akitolea mfano taarifa ya hivi karibuni katika kituo cha afya cha Kawawa mkoani Mtwara ambapo alikamatwa ofisa wa kituo cha afya akipakia dawa kwenye pikipiki bila maelezo ya sehemu anapozipeleka.

  Alisisitiza wananchi na wanahabari kuwa walinzi shirikishi  katika utoaji wa taarifa za upotevu wa dawa kwenye vituo vya afya na hospitali ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.

  "Tunaposambaza dawa kwenye vituo vya afya na hospitali huwa tuna makabidhianao kati ya MSD na kamati ya afya ya eneo husika, hivyo wananchi wanapoambiwa hakuna dawa waonyeshwe fomu ya makabidhiano ya mwisho ya dawa, taarifa ya mgawanyo wa dawa na hati ya maombi ya kuagiza dawa hizo,"alisema Terry huku akiongeza kuwa MSD imeanza kubandika orodha ya dawa zote katika mbao za matangazo ya dawa zote zilizokabidhiwa katika kituo husika.

  Pia alizikumbusha hospitali kuwasilisha mahitaji ya dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendnishi vya maabara katika ofisi za msd za kanda Kanda kabla ya Aprili 30 mwaka huu, maombi hayo yaambatinishwe na kivuli cha mpango wa manunuzi kama unavyoonekana katika vitabu vya halmshauri , Council comprehensive Health plan (CCHP), cha ili mahitaji hayo yashughulikiwe kwa wakati. (Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habari za jamii.com)  0 0


    
   .Mkurugenzi wa Hazina Foundation William Mungai na mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Mufindi Community Walefare Amina Rajab wakikabidhi kabati likiwa na madawa mbalimbali kwa  kituo cha Makalala kilichoko mafinga liganga.


    Mkurugenzi wa Hazina Foundation William Mungai na mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Mufindi Community Walefare Amina Rajab, wakiwa katika picha ya pamoja na walimu na wanafunzi walemavu wa kituo cha Makalala kilichoko mafinga liganga.


  NA DENIS MLOWE, MUFINDI

  JAMII imewatakiwa kuacha tabia ya kuwaficha walemavu bali kutoa taarifa za watoto hao waliopo kwenye familia mbalimbali kwa lengo la kupata huduma bora  hasa katika sekta ya elimu na afya.

  Hayo yamezungumzwa na mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Mufindi Community Walefare Amina Rajab wakati wa kutoa msaada wa madawa mbalimbali na nguo kwa walemavu wanaolelewa na kituo cha Serikali cha Makalala kilichoko Luganga Mafinga kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Hazina Foundationi ya mjini humo, William Mungai ambaye ni mjumbe wa mkutano mkuu wa Chadema na Mgombeo ubunge jimbo la Mufindi Kaskazini.

  Amina alisema kuwa kuna wazazi wengi wana kasumba ya kuwaficha watoto wenye ulemavu bila kujua kuwa wanahaki sawa na watoto wasiowalemavu na wakipatiwa elimu wanaweza kuwa wakombozi wa familia hasa katika masomo ya ufundi.

  Alitoa wito kwa serikali kuona umuhimu wa kutumia vituo mbalimbali vinavyolea watoto wenye ulemavu kuhakikisha vinawejengea miundo mbinu rafiki na uboreshaji mipango na mfumo wa utoaji elimu, afya na usafiri kulingana na tofauti za umri wa watoto nchini.

  Aliongeza kuwa walemavu wanayo haki ya kuishi na kujitegemea iwapo jamii itawajengea uwezo badala ya kuwafungia ndani na kuwaona kama ni mkosi katika familia  ila kugundua vipaji walivyonavyo na kuiwezesha serikali kuwaingiza katika mipango mbalimbali ya kuwapatia huduma

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Hazina Foundationi, William Mungai aliomba jamii kubadilika sasa na kuondokana na dhana potofu ya kuwatenga walemavu katika shughuli za kijamii

  Alisema kuwa bado elimu zaidi inahitajika kwa jamii ili kuweza kuondokana na mila zisizo na maana za kuwatenga na kuwadharau walemavu katika jamii.

  Naye Rahel Kumbo  ambaye ni Mlezi wa kituo cha Makalala kinachofadhiliwa na serikali alitoa wito kwa jamii kuwa walemavu wasifichwe majumbani na badala yake  wapelekwe hospitalini mapema ili wapate matibabu na kuwapatia elimu katika shule husika za walemavu.

  Alisema kuwa licha ya nia ya serikali kutaka watoto walemavu wapelekwe shule bado mazingira ya kujifunza katika shule nyingi hayawavutii watoto hawa hali inayosababisha baadhi yao kukacha masomo licha ya kuwa na vipaji vikubwa.

  Alisema kuwa serikali imejenga sana shule za kata lakini ujenzi wa shule za walemavu hasa upande wa sekondari umekuwa kikwazo kwa baadhi ya watoto kwa kuwa hali zao za kimaumbile zinawapa ugumu kurandana na hali ya mazingira ya shule.

  Alitoa wito kwa serikali kuwa makini na suala zima la ujenzi wa shule unaoendelea kuangalia na walemavu wanapaswa kujengewa vyoo vya kukidhi haja zao,maana hali hiyo ikiendelea walemavu watapata magonjwa mengi na kushindwa kuhudhuria masomo yao.

  0 0

  DSC00268KIJANA MWENYE UMRI WA MIAKA 20 ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA FADHIL SIKAPUNDWA, MKAZI WA NAMTAMBALALA WILAYANI MOMBA ALIUAWA PORINI KWA KUPIGWA FIMBO SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA WATUHUMIWA WALIOTAMBULIKA KWA MAJINA YA 1. SHADRACK SIMBEYE (16) 2. JOB JOHN (21) NA 3. MASUOD SIMWAKA (18) WOTE WAKAZI WA NAMTAMBALALA WILAYANI MOMBA.

  TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 19.04.2015 MAJIRA YA SAA 19:00 JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA NAMTAMBALALA, KATA YA NZOKA, TARAFA YA NDALAMBO, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA, CHANZO CHA TUKIO HILO NI TUHUMA ZA WIZI WA VIATU, SIMU NA NGUO. WATUHUMIWA WAMEKAMATWA NA UCHUNGUZI ZAIDI WA TUKIO HILI UNAENDELEA.

  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI KUFANYA HIVYO NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAJENGE TABIA YA KUWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA WATUHUMIWA WANAOKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
   
  KATIKA TUKIO LA PILI:
  MWANAMKE MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA IYENGA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA PILLY MGALA ALIMUUA MUME WAKE AITWAYE AMADI MWASHAMBWA, (42) MKAZI WA KIJIJI CHA IYENGA KWA KUMCHOMWA KISU KIFUANI.

  AWALI MNAMO TAREHE 19.04.2015 MAJIRA YA SAA 21:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA IYENGA, KATA YA ISANSA, TARAFA YA IGAMBA, WILAYA YA MBOZI MWANAMKE HUYO ALIMJERUHI MUME WAKE KWA KUMCHOMA KISU KIFUANI NA KUPELEKEA KUKIMBIZWA KATIKA ZAHANATI YA KIJIJI CHA IYENGA KWA MATIBABU. KUTOKANA NA MAJERAHA ALIYOYAPATA MNAMO TAREHE 20.04.2015 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAPATIWA MATIBABU.

  CHANZO CHA TUKIO HILO NI UGOMVI ULIOTOKANA NA WIVU WA KIMAPENZI BAADA YA MAREHEMU KUMTUHUMU MKE WAKE KUWA SIO MWAMINIFU KATIKA NDOA YAO. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO NA MSAKO MKALI UNAENDELEA WA KUMTAFUTA.

  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANDOA KUTATUA MIGOGORO YAO KWA KUKAA MEZA MOJA NA KUFIKIA SULUHISHO ILI KUEPUKA VITENDO VYA KUJICHUKULIA SHERIA VINAVYOWEZA KUSABABISHA MADHARA NA MATUKIO KAMA HAYA YA MAUAJI.


  TAARIFA ZA MISAKO:
   JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA KIJANA MMOJA MKAZI WA FOREST YA ZAMANI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA EMANUEL SAMWEL (28) AKIWA NA NOTI BANDIA AMBAZO KAMA ZINGEKUWA HALALI ZINGEKUWA NA THAMANI YA TSHS 325,000/=.

  MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 20.04.2015 MAJIRA YA SAA 16:00 JIONI HUKO ENEO LA ISYESYE, KATA YA ISYESYE, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA MBEYA AKIWA KWENYE HARAKATI ZA KUJARIBU KUWEKA PESA HIZO KWENYE AKAUNTI YAKE YA TIGO-PESA KWENYE DUKA LA MARY PATRICK (32) MFANYABIASHARA NA MKAZI WA ISYESYE.

  NOTI HIZO ZILIKUWA NA NAMBA DT. 2937833 NOTI 6, BV 2937839 NOTI 10, DT 4243042 NOTI 4, BF 1547948 NOTI 5, BV 4243044 NOTI 8, AA 4243045 NOTI 18, DT 1547949 NOTI 5 NA BC 2937831 NOTI 10. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.

  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA PINDI WAONAPO VIASHIRIA VYA UHALIFU AU WANAPOMTUHUMU MTU/WATU ILI HATUA STAHIKI ZICHUKULIWE DHIDI YAO.


  Imesainiwa na:[AHMED Z. MSANGI – SACP]KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

  0 0

  wak1
  Mkuu wa Makazi ya Mishamo, Fredrick Nisajile akizungumza na maofisa wake (kushoto) kabla ya kuanza kugawa vyeti vya uraia kwa raia wapya wa Tanzania kijijini Ilangu katika Makazi ya Mishamo, yaliyopo wilayani ya Mpanda Vijijini, Mkoa wa Katavi. Zaidi ya watu 152,572 katika Makazi ya Mishamo, Katumba na Ulyankulu waliokuwa wakimbizi wa Burundi wa mwaka 1972 walioomba uraia 2008 na kupewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2010, wanastahili kupokea vyeti hivyo kama raia wapya wa Tanzania. 

   Hata hivyo, Makazi ya Katumba na Ulyakulu tayari wamekamilisha zoezi la ugawaji wa vyeti hivyo, na sasa ni zamu ya raia wapya wa Makazi ya Mishamo kuwawiwa ambapo Serikali ya Tanzania inashirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR) katika ugawaji wa vyeti hiyo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  wak2
  Afisa Uhamiaji, Philimon Msenya (kushoto) akichukua alama ya vidole kwa raia mpya wa Tanzania, Bukuru Yohana kabla ya kupewa cheti chake cha uraia katika ugawaji wa vyeti hivyo kwa raia wapya zaidi ya 52,565 katika Makazi ya Mishamo yaliyopo wilayani ya Mpanda Vijijini, Mkoa wa Katavi.

   Zaidi ya watu 152,572 katika Makazi ya Mishamo, Katumba na Ulyankulu waliokuwa wakimbizi wa Burundi wa mwaka 1972 walioomba uraia 2008 na kupewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2010, wanastahili kupokea vyeti hivyo kama raia wapya wa Tanzania. Hata hivyo, Makazi ya Katumba na Ulyakulu tayari wamekamilisha zoezi la ugawaji wa vyeti hivyo, na sasa ni zamu ya raia wapya wa Makazi ya Mishamo kuwawiwa ambapo Serikali ya Tanzania inashirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR) katika ugawaji wa vyeti hiyo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  wak3
  Mkuu wa Makazi ya Mishamo, Fredrick Nisajile akizungumza na wazee wa Kijiji cha Ilangu katika Makazi hayo, ambao ni raia wapya wa Tanzania wakati wakisubiria kupewa vyeti vyao vya uraia. Wazee hao wametengewa sehemu maalum ili kupewa kipaumbele kutokana na umri wao ili waweze kupewa vyeti hivyo kwa uharaka zaidi. 

  Zaidi ya watu 152,572 katika Makazi ya Mishamo, Katumba na Ulyankulu waliokuwa wakimbizi wa Burundi wa mwaka 1972 walioomba uraia 2008 na kupewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2010, wanastahili kupokea vyeti hivyo kama raia wapya wa Tanzania. Hata hivyo, Makazi ya Katumba na Ulyakulu tayari wamekamilisha zoezi la ugawaji wa vyeti hivyo, na sasa ni zamu ya raia wapya wa Makazi ya Mishamo kuwawiwa ambapo Serikali ya Tanzania inashirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR) katika ugawaji wa vyeti hiyo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  wak4
  Raia wapya wa Tanzania wa Kijiji cha Ilangu katika Makazi ya Mishamo, wakiwa wameweka foleni ndefu ili waweze kugawiwa vyeti vyao vya uraia kijijini hapo, wilayani Mpanda Vijijini, mkoani Katavi, leo. Zaidi ya watu 152,572 katika Makazi ya Mishamo, Katumba na Ulyankulu waliokuwa wakimbizi wa Burundi wa mwaka 1972 walioomba uraia 2008 na kupewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2010, wanastahili kupokea vyeti hivyo kama raia wapya wa Tanzania. 

  Hata hivyo, Makazi ya Katumba na Ulyakulu tayari wamekamilisha zoezi la ugawaji wa vyeti hivyo, na sasa ni zamu ya raia wapya wa Makazi ya Mishamo kuwawiwa ambapo Serikali ya Tanzania inashirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR) katika ugawaji wa vyeti hiyo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  wak5
  Raia wapya wa Tanzania wa Kijiji cha Ilangu katika Makazi ya Mishamo, wakiwa wameweka foleni ndefu ili waweze kugawiwa vyeti vyao vya uraia kijijini hapo, wilayani Mpanda Vijijini, mkoani Katavi, leo. Zaidi ya watu 152,572 katika Makazi ya Mishamo, Katumba na Ulyankulu waliokuwa wakimbizi wa Burundi wa mwaka 1972 walioomba uraia 2008 na kupewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2010, wanastahili kupokea vyeti hivyo kama raia wapya wa Tanzania. 

  Hata hivyo, Makazi ya Katumba na Ulyakulu tayari wamekamilisha zoezi la ugawaji wa vyeti hivyo, na sasa ni zamu ya raia wapya wa Makazi ya Mishamo kuwawiwa ambapo Serikali ya Tanzania inashirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR) katika ugawaji wa vyeti hiyo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  wak6
  Afisa Operesheni wa Idara ya Wakimbizi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Stephen Daniel (kushoto) akiwaelekeza raia wapya wa Tanzania katika Kijiji cha Ilangu, Makazi ya Mishamo, kuwasilisha vyeti vya kliniki vya watoto wao ili waweze watoto wao kuwekwa kwenye kumbukumbu ya Serikali. Watoto wote waliozaliwa baada ya mwaka 2010 ni raia wa Tanzania wa kuzaliwa, hivyo hawatapewa vyeti vya uraia kama wanavyopewa wazazi wao. 

   Zaidi ya watu 152,572 katika Makazi ya Mishamo, Katumba na Ulyankulu waliokuwa wakimbizi wa Burundi wa mwaka 1972 walioomba uraia 2008 na kupewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2010, wanastahili kupokea vyeti hivyo kama raia wapya wa Tanzania. 

  Hata hivyo, Makazi ya Katumba na Ulyakulu tayari wamekamilisha zoezi la ugawaji wa vyeti hivyo, na sasa ni zamu ya raia wapya wa Makazi ya Mishamo kuwawiwa ambapo Serikali ya Tanzania inashirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR) katika ugawaji wa vyeti hiyo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

  0 0

  Mlinzi wa Bonite akiwa ameshikilia bunduki yake aina ya Short Gun ,muda mfupi baada ya kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi ambao walifanikiwa kupora fedha 


older | 1 | .... | 507 | 508 | (Page 509) | 510 | 511 | .... | 1897 | newer