Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 504 | 505 | (Page 506) | 507 | 508 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Uongozi wa Mamlaka zinazohusika na  uwekezaji Tanzania na Wawekezajia kutoka Egypt wakati ujumbe huo ulipofika Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo April 15, 2015.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katikati akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Wawekezajia kutoka Egypt baada ya mazungumzo yao wakati ujumbe huo ulipofika Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo April 15, 2015.
   
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katikati akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Wawekezajia kutoka Egypt baada ya mazungumzo yao wakati ujumbe huo ulipofika Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo April 15, 2015.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mr. Joe Kawkaban kiongozi wa Ujumbe wa Wawekezajia kutoka Egypt baada ya mazungumzo yao wakati ujumbe huo ulipofika Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo April 15, 2015.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Wawekezajia wa CPU wakati alipokutana na ujumbe huo Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo April 15, 2015.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katikati akiwa katika picha ya pamoja na Wawekezajia wa CPU baada ya mazungumzo yao Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo April 15, 2015. (Picha na OMR)

  0 0

  Katibu asasi ya Vijana ya Boys & Girls Bw,Johnson Jacob kutoka Bariadi akionyesha igizo lilikuwa likionyesha wajibu wa Vijana  kwa Familia ikiwamo kuwalinda na kuwapatia mahitaji yao muhimu.
  Mtaalamu wa Stadi za Maisha Bw,Robert Semkiwa akiwafundisha waratibu wa ukimwi na maafisa Vijana wanaohudhuria Warsha ya siku tatu inayohusu Stadi za maisha na Afya ya uzazi jinsi ya kukabiliana na Msongo wa Mawazo na njia gani za kutumia kukabiliana nao.
  Waratibu wa Ukimwi na maafisa Vijana wakiwa katika mjadala wa pamoja wakipambanua kwa kina stadi mojawapo katika stadi tatu za maisha ya kujitambua leo jijini Mwanza.kundi ili lilikuwa likijadili jinsi ya kukabili mihemko kwani ni  hatua mojawapo kijana anayoipitia katika maisha yake.


  Mwakilishi wa Vijana kutoka kamati ya kudhibiti Ukimwi manispaa ya Shinyanga Bw,Rigobert Rwehumbiza akielezea wajibu binafsi kwa kijana kwa washiriki wenzie katika warsha ya siku nne ya stadi za maisha na afya ya uzazi.

  0 0

  CCiV3FEWIAEKkRE
  Na Zainul Mzige wa modewjiblog
  Mbunge wa Nzega ambaye amejitokeza kutangaza nia ya kugombea urais nchini ambaye pia amekuwa mtetezi mkuu wa wananchi wa jimboni kwake kupitia migodi mbalimbali Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla (Mb) ameandika kitabu kiitwacho "Tanzania tunayoitaka" yakiwa ni mawazo yake binafsi ambacho anatarajia kukisambaza Tanzania nzima.

  Kigwangalla katika kitabu chake amezungumzia fikra mpya za kuleta mapinduzi ya kiuchumi na kijamii kutokana na urithi wa rasilimali, utamaduni na utajiri wa nguvu kazi.

  “Kuna mambo misingi minane niliyoipendekeza, ambayo yakifanyiwa kazi tutapata Tanzania Tuitakayo”, amesema Kigwangalla.
  10649905_10152917376443243_2689156129216005815_n
  "Misingi hiyo inaunda mfumo mpya wa politikoikonomi unaoitwa Ujamaa wa Kiafrika wenye Vionjo vya kibepari. Misingi imepewa jina la 'Kigwanomics.', ameongeza Kigwangalla.

  Kitabu hicho cha "Tanzania tunayoitaka" kwa mujibu wa Kigwangalla mwenyewe ameeleza kuwa kinapatikana katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma na Iringa huku juhudi zikiendelea kusambaza Tanzania nzima.

  Pata nakala ya kitabu cha Kigwangalla ambacho kipo mtaani kwako.

  0 0

  DSC_0348

  Mwenyekiti wa mtandao wa Redio Jamii nchini (COMNETA) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Redio ya Jamii ya Wilayani Karagwe ya FADECO FM, Bw.Joseph Sekiku akizungumza katika hafla fupi ya kumuaga Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT) ambaye amemaliza muda wake, Prof. Tolly Mbwete (katikati) iliyoandaliwa na Mtandao wa Redio za Jamii nchini (COMNETA). Kushoto ni Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu.
  DSC_0359
  Katibu wa mtandao wa Redio Jamii nchini (COMNETA), Riziki Leisuya akisoma risala fupi wakati wa hafla ya kumuaga Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Tolly Mbwete.
  DSC_0386
  Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT) ambaye amemaliza muda wake, Prof. Tolly Mbwete akipokea risala iliyosomwa na Katibu wa mtandao wa Redio Jamii nchini (COMNETA), Riziki Leisuya wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyoandaliwa na WanaCOMNETA.
  DSC_0373
  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania ambaye amemaliza muda wake, Prof. Tolly Mbwete (wa pili kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Mhariri wa Sibuka FM, Anita Balingilaki kwa niaba ya Wanamtandao wa Redio Jamii nchini Tanzania (COMNETA) kama ishara ya kumuaga rasmi wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na wanamtandao huo ya kumtaki kheri katika majukumu mapya anayoenda kufanya nchini Addis Ababa.

   Kushoto ni Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu na Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa mtandao wa Redio Jamii nchini (COMNETA) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Redio ya Jamii ya Wilayani Karagwe ya FADECO FM, Bw.Joseph Sekiku akifutiwa na Mshauri wa UNESCO, Balozi mstaafu Mh. Christopher Liundi.
  DSC_0430
  Mshauri wa UNESCO, Balozi mstaafu Mh. Christopher Liundi akitoa wasifu wa Prof. Tolly Mbwete kwenye hafla hiyo fupi.
  DSC_0436
  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT) ambaye amemaliza muda wake, Prof. Tolly Mbwete katika picha ya pamoja na wakufunzi na washiriki wa warsha ya siku tatu kutathmini mradi wa demokrasia na Amani (DEP) yenye lengo la kuimarisha ushiriki wa redio za jamii nchini kuelekea uchaguzi 2015 na kura ya maoni kwa wanamtandao wa Redio Jamii nchini (COMNETA) iliyoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na kufadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) ambayo imemalizika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT).  MTANDAO wa Radio za Kijamii nchini Tanzania (COMNETA) na Chuo Kikuu Huria (OUT) kwa umoja wao zimepongeza mchango mkubwa wa aliyekuwa Makamu Mkuu wa chuo hicho Profesa Tolly Mbwete kwa jitihada zake za kuziunganisha redio jamii na chuo kuhakikisha taarifa zinawafikia walio wengi hasa vijijini.

  Katika hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa OUT hivi karibuni mtandao wa COMNETA umesema jitihada za Profesa Mbwete kuziunganisha taasisi hizo mbili zimefanikishwa kwa kiasi kikubwa kufikisha taarifa za kozi mbalimbali zinazoendesha chuoni na kwa bei nafuu kwa Watanzania wengi ambao umesaidia kukifahamu na hatimae kujiunga na chuo.

  Akisoma risala fupi iliyotayarishwa na COMNETA, Katibu wa mtandao huo Riziki Leisuya alisema kwamba makubaliano na mashirikiano kati ya Comneta na OUT yaliyowezeshwa na Profesa Mbwete yamezaa matunda mengi baina ya pande hizo mbili kiasi cha kulishawishi Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu ,Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kukubali kujenga studio ya redio katika chuo hicho ili kurahisisha mawasiliano kwa kutayarisha vipindi lakini pia itatumika na wanafunzi wanaochukua taaluma ya uandishi kufanya mazoezi kwa vitendo kuboresha mafunzo yao.

  “Comneta kupitia redio zake imefanikiwa kupeleka habari wilayani na vijijini kwa kukitangaza chuo kwa watu wasiojiweza jambo ambalo limesababisha ongezeko la idadi ya wanafunzi chuoni hapo kutokana na unafuu wa gharama” iliongeza risala hiyo iliyosomwa na Riziki.

  Profesa Mbwete ambaye muda wake wa utumishi chuoni hapo umefikia kikomo kwa sasa amechaguliwa kuwa Mkuu wa Vyuo Vikuu vya Kikanda (Pan African Universities-PAU) na Umoja wa Nchi huru za Afrika kuanzia mwezi Januari mwaka 2015.

  Akiwashukuru na kuwaaga wana-Comneta ambao walihudhuria ulingo wa siku tatu kutathminimradi wa demokrasia na Amani (DEP) Profesa Mbwete alisema amefarijika na ushirikiano uliopo kati ya taasisi hizo mbili ambao umekuwa na mafanikio ya kipekee kwa umma wa Tanzania na kuahidi kumkabidhi atakayechukua nafasi yake kuendeleza ushirikiano huo na kumshauri ofisi ya COMNETA iendelee kwa mkataba wa ushirikiano kwa miaka mitatu na kila mwaka kuufanyika mapitio na mrejesho.

  Naye Balozi Christopher Liundi ambaye ni mshauri wa Unesco akimzungumzia Profesa Mbwete alisema kwamba Profesa Mbwete anastahili pongezi kutokana na jinsi alivyoimarisha Chuo Kikuu Huria na kuimarisha ushirikiano kati ya Chuo hicho na Comneta kwa kutoa ofisi ambayo mtandao wa redio za jamii unaitumia kwa kutekeleza majukumu yake kama jitihada za kutoa uwezo kwa mtandao huo.

  “Profesa Mbwete alikuwa mstari wa mbele kupanua chuo na namshukuru sana kwa kauli yake ya kuipa COMNETA miaka mingine mitatu kutumia ofisi iliyotolewa na chuo chini ya usimamizi wake. Ninaamini kwamba huko aendako atapeperusha bendera ya Tanzania na ataiwakilisha vizuri kwenye PAU, nina matarajio makubwa sana kutoka kwake,’ alisema Balozi Christopher Liundi.

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini Philemoni Ndesamburo akimtambulisha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi Jafary kuwa mrithi wake wa kiti cha ubunge katika jimbo hili wakati wa uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi oktoba.
  Ndesamburo akizungumza na wananchi wa Moshi mara baada ya kumtangaza mrithi wake katika jimbo la Moshi mjini.


  0 0

   Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe akiwahutubia wananchi Manyoni Mjini.
   Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo Anna Mghwira, akiwahutubia wakazi wa Manyoni Mjini.
   Wakazi wa Mji wa Singida wakishangilia viongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo wakati waa mkutano huo jijini humo leo.
   Viongozi wakiimba wimbo wa taifa.

  Zitto akizungumza na wakazi wa Mji wa Singida leo.

  CHAMA cha ACT-Wazalendo kimesema kinaweza kuunganisha nguvu na vyama vingine vya upinzani ili kukiondoa chama cha mapinduzi kwenye uchaguzi mkuu ujao ambapo alisema shauku kubwa ya wananchi ni kutaka kujua msimamo wa ACT Wazalendo katika kushirikiana na vyama vingine vya siasa ili kufanikisha malengo ya kuiondoa CCM katika madaraka.

  Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Singida na Kiongozi wa ACT wazalendo Zitto Kabwe wakati akihutubia mamia ya wananchi katika uwanja wa shule ya msingi ukombozi.

  "Tumedhamiria kuleta mapinduzi ya kiuchumi kwa kuubomoa mfumo  unaonyonya wananchi. Msimamo wetu upo wazi na tumeueleza mara kadhaa"alisema na kuongeza

  “ACT- Wazalendo tunaunga mkono juhudi zozote za kushirikiana kwa vyama na hili linathibitishwa na jina letu Alliance na msimamo wetu kuhusu mabadiliko ya Katiba. Kubwa tunataka ushirikiano utakaonufaisha wananchi na sio ushirikiano wa kugawana nafasi za uongozi,” alisema Zitto.

  Kiongozi huyo wa ACT alisema chama hicho hakina tatizo na kipo tayari kushirikiana na chama chochote kilichokuwa  tayari kushirikiana nao ikiwemo Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

  Alisema umoja huo ni lazima uwe na malengo ya kujenga uchumi shirikishi wenye kuzalisha ajira nyingi na bora, wenye mfumo wa hifadhi ya jamii kwa wananchi wote na wenye kutokomeza umasikini.

  Alikanusha chama hicho kutoa  kauli yeyote dhidi ya UKAWA kama inavyoaminishwa na baadhi ya watu, bali wameweka wazi kuwa lazima misingi ya kiitikadi na kifalsafa izingatiwe katika ushirikiano wowote.

  "Tupo tayari kwa umoja kwani ni moja ya misingi mikuu 10 ya chama chetu na umoja ni nguvu,” alisema Zitto.

  Akizungumzia hali ya umaskini kwa mkoa wa Singida, Zitto alisema pamoja na hali ya umaskini Serikali ya CCM, imeshindwa kupunguza umasikini, nchini kwa kiasi kikubwa na kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

  Alisema ripoti ya maendeleo ya binadamu imeonyesha kuwa Tanzania imeshuka kufikia daraja la chini la nchi zenye kiwango kidogo zaidi cha maendeleo ya binadamu.

  “Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya UNDP kuhusu Maendeleo ya Binadamu duniani ya mwaka 2014 ambayo imeiweka Tanzania katika kundi la nchi zenye maendeleo ya binadamu ya kiwango cha chini.  Lakini kinachoshitusha ni kushuka kwa nafasi saba zaidi katika Kipimo cha maendeleo ya binaadamu, (HDI), ukilinganisha na mwaka 2013.

  “Ushahidi mzuri wa jambo hili ni ule unaotolewa na kipimo cha Maendeleo ya Binadamu (HDI), ambacho hupima maendeleo ya binadamu katika nchi kwa kuzingatia mkusanyiko wa vigezo vya umri wa kuishi, elimu na kipato,” alisema Zitto. 

  Alisema katika ngazi ya mikoa, ripoti hiyo  inaonyesha tofauti kubwa ya viwango vya maendeleo ya binadamu ndani ya Tanzania.

  Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Iringa, Ruvuma, Mbeya, na Tanga ndiyo mikoa yenye kiwango cha juu cha maendeleo ya binadamu.

  “Singida inazalisha alizeti na sasa hivi tunajua kwamba watu wanaojali afya zao, wanapenda kula mafuta ya alizeti na ukiongelea mafuta ya alizeti, basi yale yaliyo bora yanatokana katika mkoa huu. Lakini pamoja na fursa hiyo ambayo inaweza kuitumia ili kuinua hali ya maisha ya wananchi,” alisema

  Alisema Mkoa wa Singida una madini lakini jambo la kushangaza bado umekuwa mkoa wa kwanza kwa umaskini huku madini hayo yakishindwa kuwanufaisha wananchi hasa wanaozunguka vijiji vya Sambaru na Londoni.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Anna Mghwira,  alisema sasa umefika wakati ni lazima nchi iwe huru kwa kuwa na misingi imara itakayoimarisha demokrasia nchini.

  “Rais aitishe Bunge maalumu ili kufanya marekebisho madogo ya Katiba kuruhusu uchaguzi huru na wa haki lakini pia Wajumbe wa Tume waombe kazi na wawe wataalamu.

  Alisema ACT inashauri kuitishwa kwa Bunge Maalumu ni kutokana Bunge la sasa la 10 lina uhai wa mkutano mmoja kabla ya kuvunjwa.

  “… hivyo Katibu wa Bunge atangaze nafasi za wajumbe wa Tume, kamati ya Bunge ya Katiba Sheria na Utawala itafanya mahojiano ya wazi na kupata majina 22 yatakayopelekwa bungeni,” alisema Anna


   Mkazi wa Manyoni Mjini Mzee ambaye jinalake halikupatikana maramoja akichukua picha za video kwa kutumia simu mkutano wa ACT-Wazalendo.
   Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, akisalimiana na mzee ambaye alitumia muda mwingi kuwapiga picha za ideo viongozi hao wakiwa kwenye mkutano Manyoni mjini.
   Zitto akisalimiana na wakazi wa Manyoni Mjini.
   Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe na Mwenyekiti wa Chama hicho Anna Mghwira wakizindua tawi la chama hicho kwenye Kijiji cha Kintintu wilayani Manyoni mkoani Singida. 
   Zitto akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kintintu mara baada ya kuzindua tawi la chama hicho
   Viongozi wa ACT -Wazalendo wakishangilia na wananchi wa wilayani Manyoni baada ya kuzindua tawi la Manyoni Mjini.

  0 0
 • 04/16/15--02:32: Article 12
 • Untitled-1 copy
  KWA MATUKIO MBALIMBALI YANAYOHUSU MASUALA YA SIASA ZIKIWEMO HABARI MAKALA FUPIFUPI , VITUKO , KUJIFAGILIA NA UWAJIBIKAJI WA WANASIASA KWA JAMII TEMBELEA www.politikstz.blogspot.com ILI UPATE KUJUA, KUELIMIKA NA KUBURUDIKA. PIA UNAWEZA KUTUTUMIA HABARI, MATUKIO YA PICHA NA MAKALA FUPIFUPI LAKINI ZISIWE HABARI ZA KUCHAFUA HALI YA HEWA AMA KUMCHAFUA MTU TUTUMIE KWA EMAIL HII .politikstz@gmail.comTUTASHUKURU KWA USHIRIKIANO WENU.

  0 0

  Meneja Ufundi Idara ya Petroli EWURA Ndugu Gerald Maganga akiwasilisha moja ya mada katika Semina kwa Wafanyabiashara wa Mafuta Mikoa ya Rukwa na Katavi katika ukumbi wa Moravian Centre Mjini Sumbawanga tarehe 15 April 2015. Kushoto ni Afisa Uhusiano EWURA Ndugu Wilfred Edwin. Miongoni mwa mada zilizowasilishwa katika Semina hiyo ni Udhibiti na Kanuni za Ukokotoaji wa bei za Mafuta, Ubora wa Miundimbinu, Usalama na Utunzaji wa Mazingira katika Sekta ya Mafuta ya Petroli, Faida za kutumia Mafuta yenye kiwango kidogo cha Sulphur na Sheria na Kanuni katika udhibiti wa Sekta ya Petroli nchini.
  Afisa Biashara Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Ndugu Paul Nganyanyuka akichangia moja ya mada katika Semina hiyo ya EWURA na wafanyabiashara ya mafuta Mikoa ya Rukwa na Katavi iliyofanyika katika Ukumbi wa Moravian Centre mjini Sumbawanga tarehe 15/04/2015.
   Sehemu ya wajumbe katika Semina hiyo ambao ni wafanyabishara wa vituo vya mafuta Rukwa na Katavi, Mtoa huduma Serikalini GPSA na Maafisa Biashara kutoka Mikoa ya Rukwa na Katavi. (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

  0 0
 • 04/16/15--03:30: VACANCIES

 • Dira Newspaper Co Ltd. publisher of Dira ya Mtanzania and Pata Habari is looking for motivated and highly experienced individuals to fill the position of:

  POSITION: EDITOR (4 POSTS)


  MAIN RESPONSIBILITIES

  . To coordinate the newspaper
  . Maintain production schedules and report on the progress
  . Assist with the layout and design of the publication
  . Deciding which stories and articles are to be published


  QUALIFICATION AND EXPERIENCE

  Professional: Diploma in Journalism
  Academic: Basic University Degree in Journalism
  Experience: 3-5 years Journalistic working experience

  MODE OF APPLICATION
  Interested and suitably qualified individuals should forward their applications enclosing a detailed CV and copies of professional certificates by May 6, 2015 to;

  Human Resources Manager,
  Dira ya Mtanzania
  P.O. Box 105497
  Dar es Salaam.

  0 0

   Ujumbe kutoka Tanzania ukifuatilia kwa karibu mkutano huu. (African Group one Constituency
   Ujumbe kutoka Tanzania ukifuatilia kwa karibu mkutano huu. (African Group one Constituency)
   Gavana wa Benki kuu Prof. Benno Ndulu akifuatilia kwa makini mkutano wa kundi la Afrika unavyoendelea. (African Group one Constituency)
   Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya  akishiriki katika mkutano huu wa kundi la Afrika. (African Group one Constituency)
   Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya akifuatilia kwa karibu majadiliano ya mkutano huu wa kundi laAfrika. (African Group one Constituency).
  Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya akichangia Mada  katika mkutano huu wa kundi laAfrika. (African Group one Constituency).


  “Shirika la fedha la kimataifa (IMF) hujishughulisha na kutoa ushauri wa kisera kwa nchi wanachama na kutoa mikopo na misaada ya kifedha. Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum aliyaeleza hayo mjini hapa. Akishiriki kikao cha kundi la Africa(African Group one Constituency). Kundi hili hukutana kila kunapokuwa na mikutano ya Shirika la Fedha la Kimataifa na Benki ya Dunia kwa lengo la kuwezesha nchi za Afrika kuwa na sauti moja na kujua hatua ambazo Nchi za Afrika zimefikia kuhusiana na Taasisi zake za kifedha.

    Mhe. Mkuya alichangia mada mbalimbali zilizohusu kundi hilo akilenga zaidi maendeleo na muelekeo mzuri wa mafanikio ya kifedha katika nchi ya Tanzania. 

   Waziri wa Fedha  wa Tanzania Mhe. Saada Salum Mkuya ni Gavana katika mkutano huu akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha  na Mlipaji Mkuu wa Serikali  Dr. Servacius Likwelile ambaye ni  Gavana msaidizi kwa upande wa Benki ya Dunia (WB), aidha  Gavana wa Benki kuu Prof. Benno Ndulu ni Gavana msaidizi kwa upande wa Shirika la Fedha la Kimataifa(IMF).

   Katika Mkutano huu Magavana hawa ndio wenye maamuzi ya juu na nguvu kubwa ya kuweza kuyashawishi mashirika  ya kifedha kuhusu nini kifanyike.  Mkutano huu uliofanyika leo, umeangalia uhalisia na vigezo vinavyotolewa na Shirika la Fedha la kimataifa katika kuimarisha taasisi za kifedha katika nchi wanachama Afrika.  

  Katika mkutano huu, mambo muhimu yaliyojadiliwani pamoja na maendeleo katika kundi hilo na mabadiliko ya maboresho katika Benki ya Dunia. Wakijadiliana katika mkutano huo wajumbe hao wameshauri Shirika la fedha la kimataifa pamoja na taratibu zake, liangalie namna ya kulegeza masharti ya mikopo ili nchi wanachama ziweze kufanya mabadiliko ya kifedha kwa urahisi.

   Mikutano hiyo bado inaendelea hapa mjini Washington DC. na nchi wanachama wanaendelea kufika kwa wingi.

  Imetolewa na Msemaji :Wizara ya fedha
   Ingiahedi C.Mduma
  Washington DC
  15/04/2015.
  0 0

  Afisa Mchambuzi wa Mifumo ya Computer wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Amos Madaha akizungumza katika semina ya siku nne ya matumizi ya fomu mbalimbali za uandikishwaji wa wapiga kura (BVR) ya mafunzo kwa zaidi ya wachambuzi 500 yanayofanyika jijini Dar es Salaam.
   Afisa Mchambuzi wa Mifumo ya Computer wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Adolf Kinyero akizungumza katika semina ya siku nne ya matumizi ya fomu mbalimbali za uandikishwaji wa wapiga kura (BVR) ya mafunzo kwa zaidi ya wachambuzi 500 yanayofanyika jijini Dar es Salaam. 
  Zaidi ya wachambuzi 500 wamekutanishwa na NEC kwa ajili ya mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya mfumo wa BVR.

  0 0

  DSC_0392
  Mtaalamu wa mawasiliano Mradi wa uwezeshaji wa demokrasia (DEP) kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Nicodemus Marcus akizungumza wakati wa kufunga warsha ya siku tatu ya kutathmini mradi wa uwezeshaji wa demokrasia na amani (DEP) kwa wanamtandao wa Redio Jamii nchini (COMNETA) yenye lengo la kuimarisha ushiriki wa redio za jamii nchini kuelekea uchaguzi 2015 na kura ya maoni iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na kufadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria Tanzania jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 

  Wa pili kushoto ni Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji  Mwalimu,akifuatiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania, Prof. Tolly Mbwete, Mwenyekiti wa mtandao wa Redio Jamii nchini (COMNETA) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Redio ya Jamii ya Wilayani Karagwe ya FADECO FM, Bw.Joseph Sekiku na Mshauri wa UNESCO, Balozi mstaafu Mh. Christopher Liundi.

  DSC_0158
  Mhariri wa Redio Kwizera FM ya Ngara mkoani Kagera, Seif Omary Upupu akichangia mada wakati wa warsha ya siku tatu ya kutathmini mradi wa uwezeshaji wa demokrasia na amani (DEP) kwa wanamtandao wa Redio Jamii nchini (COMNETA).
  DSC_0166
  Mhariri wa Sibuka FM, Anita Balingilaki akishiriki kuchangia mada kwenye warshi hiyo.


  Aidha wametambua kwamba redio za jamii ndio mhimili mkubwa wa kupata taarifa mbalimbali za uchaguzi zilizofanyiwa kazi hasa uwapo wa watoa habari wa kuaminika katika jamii. Pia alisema redio hizo zimeanza kuona umuhimu wa kufuata maadili, ushirikishaji kijinsia, utoaji wa nafasi kwa makundi mbalimbali wakiwemo walemavu na vijana katika kazi.

  Hata hivyo alisema kwamba mapungufu yaliyojitokeza yalisababishwa na viongozi wa redio kupuuzia suala la uwajibikaji na pia kuwakoesha vitendea kazi watumishi husika na umbali wa maeneo ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi kutoka katika ofisi zilizopo redio husika.

  Viongozi pia katika tathmini walishauriwa kuwapa motisha watendaji wao kwani walionekana kulalamikia suala la kukosa motisha katika kazi ambazo wanastahili kuzifanya ili kufuata maelekezo ya mradi wa DEP.

  Wakati huo huo Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu (THRDC) moja ya taasisi inayotetea usalama wa waandishi wa habari maeneo ya kazi imewataka washiriki katika warsha wasipofuata maadili hawataweza kufanyakazi zao vyema ikiwa ni pamoja na kuingia katika migogoro na wadau wa habari. 

  Naye Balozi Christopher Liundi mshauri wa UNESCO amesisitiza pia haja ya kufuata maadili na pia kuhakikisha redio za jamii zinajijenga kupitia mtandao wao na kujiuza kwa umma.

  Aidha alishauri kwamba ripoti ya UTPC igawiwe kwa wadau wote kwani imetengeneza msingi wa utendaji kazi katika radio za jamii ambazo kwa sasa zinakuja kasi katika kuhabarisha mambo mbalimbali kwa jamii hasa vijijini.
  Katika tathmini hiyo ya mradi wa DEP walikuwepo wawakilishi kutoka Ofisi ya Msajili, Tume ya taifa ya uchaguzi (baba nay a Visiwani), Under the same Sun, Human Rights Defenders Coalition(THRDC) na taasisi nyingine zinazogusa masuala ya uchaguzi na amani.
  DSC_0289
  Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu akifafanua jambo kwa washiriki wa warsha hiyo.
  DSC_0020
  Pichani juu na chini ni baadhi ya Wanamtandao wa redio jamii 28 nchini (COMNETA) waliohudhuria warsha hiyo ya siku tatu ya kutathmini mradi wa uwezeshaji wa demokrasia na amani (DEP) kwa wanamtandao wa Redio Jamii nchini (COMNETA) yenye lengo la kuimarisha ushiriki wa redio za jamii nchini kuelekea uchaguzi 2015 na kura ya maoni iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na kufadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  DSC_0018DSC_0288
  Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu akizungumza na wanamtandao wa redio jamii nchini (COMNETA) waliohuhduria warsha ya siku tatu ya kutathmini mradi wa uwezeshaji wa demokrasia na amani (DEP) iliyomalizika mwishoni mwa juma lililopita katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) jijini Dar es Salaam. 

  Kushoto ni Makamu mwenyekiti wa COMNETA ambaye pia ni Meneja wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Telecentre Sengerema FM, mkoani Mwanza Bw. Felician Ncheye pamoja na Mwenyekiti wa Gender and Media in Southern, Tanzania Chapter (GEMSAT) Dominica Haule.
  DSC_0284
  Mratibu wa Mradi wa uwezeshaji wa Demokrasia na Amani (DEP) kutoka ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Bi. Beatrice Stephano akizungumzia ushiriki wao na majukumu kwenye mradi wa DEP kwa wana-COMNETA.
  DSC_0028
  Makamu mwenyekiti wa COMNETA ambaye pia ni Meneja wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Telecentre Sengerema FM, mkoani Mwanza Bw. Felician Ncheye (kulia) akiwa na wadau kutoka Under the Same Sun walioshiriki kutoa mada kwenye warsha hiyo.

  Na Mwandishi wetu
  SHIRIKA la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini limetoa wito kwa redio za jamii kujikita zaidi katika kutoa hamasa ya ushiriki wa wananchi katika mchakato wa uchaguzi ukiwamo kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.

  Akizungumza matumaini ya Umoja huo katika tathmini ya mradi wa Uwezeshaji wa Demokrasia (DEP) kwa Redio za Kijamii nchini Tanzania zinazounda umoja wa COMNETA, chini ya ufadhili wa UNESCO, mtaalamu wa masuala ya mawasiliano wa UNDP Nicodemus Marcus alisema kwamba redio hizo zina kazi 5 muhimu kuelekea uchaguzi.

  Alisema pamoja na kutekeleza makubaliano kati ya Umoja wa Mataifa na redio hizo kuhusu elimu kuelekea uchaguzi mkuu unaozingatia maadili ya uandishi na uwajibikaji katika mradi huo ni matumaini ya UNDP kwamba redio hizo zitatimiza wajibu wa kuhakikisha kwamba uchaguzi unafanyika kwa amani na makundi mbalimbali yanajitokeza kupitia vyama vyao vya kisiasa kuwania uongozi.

  Akifafanua alisema kwamba hamasa ya watu kujitokeza kujiandikisha katika daftari la wapiga kura, kushiriki katika kura ya maoni,Kujitokeza kwa wingi katika upigaji kura, kuendeleza amani kuelekea katika uchaguzi mkuu na kuhamaisha makundi kuwania uongozi ni mambo matano ambayo Umoja wa Mataifa unategemea redio hizo zitafanya.

  Aidha alisisitiza haja ya redio hizo kufuata makubaliano ya kuendesha elimu kwa uadilifu mkubwa ili wasijiingize katika matatizo yoyote yale yatakayokwamisha kazi ya kutoa elimu kwa umma kuelekea uchaguzi mkuu na mchakato wake.

  Naye Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu ambaye taasisi yake ndiyo inayosimamia redio za jamii alisema kwamba Tathmini ya mradi wa uwezeshaji wa demokrasia (DEP) kwa radio za kijamii, umeonesha kuwapo kwa changamoto hasa katika utekelezaji wa makubaliano.
  Alisema kati ya redio 28 zilizomo katika umoja wa Comneta ni redio kama 8 zilizofanya juu ya kiwango na kuonesha kwamba inawezekana kuhabarisha umma.

  Ufanisi wa redio hizo umeoneshwa katika ripoti ya Umoja wa Vilabu vya waandishi wa UTPC uliopewa kazi ya kufuatilia utekelezaji wa makubaliano ya mwaka jana kuhusu uendeshaji wa vipindi mbalimbali vya uchaguzi katika mradi wa DEP. Alisema redio zilizofanya vyema ni pamoja na Mpanda iliyopata alama 80 huku redio nyingine za Fadeco FM , Fadhila FM, Sibuka FM, Mazingira FM, Kwizera FM Kyela FM na Micheweni zikiwa na alama 60.

  Pamoja na changamoto hiyo Bi. Rose Haji Mwalimu alisema wamejifunza kwamba kumekuwepo na kuboreka kwa vipindi kiasi ya kwamba watu wengi wanavutiwa kusikiliza redio hizo na wengine wakitaka kufanyanao kazi.

  0 0

   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (kulia)  akiwa katika mazungumzo na ugeni kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania uliomtembelea leo Ofisini kwake ukiongozwa na Balozi Lu Youqing  (kushoto)  kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya China na Tanzania katika kuimarisha  shughuli za Mipango Miji ,Usimamizi wa Matumizi endelevu ya Ardhi . 
   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (kulia) akimweleza  Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing  (kushoto) namna Wizara yake inavyoendelea  kuimarisha  shughuli za Mipango Miji ,Usimamizi na Matumizi endelevu ya Ardhi katika maeneo mbalimbali nchini.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimkaribisha Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing  alipomtembelea  ofisini kwake  leo jijini Dar es salaam na kufanya mazungumzo  ya kuimarisha  ushirikiano kati ya Tanzania na China katika masuala ya uendelezaji wa Ardhi na Mipango miji. 

  0 0

   Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi akizungumza na Balozi wa Uingereza hapa nchini Bi. Dianna Melrose wakati balozi huyo alipomtembelea Mheshimiwa Lukuvi ofisini kwake kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu uendelezaji wa  uendelezaji wa sekta ya ardhi nchini Tanzania. Picha/ Nanyaro,Clarence - Wizara ya Ardhi.

  0 0

   Kamishna wa Forodha na Ushuru kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Tiagi Masamaki Kabisi akiwaeleza waandishi wa Habari juu ya faida za Mfumo mpya wa Uondoshaji Mizigo bandarini(TANCIS) ikiwa unasaidia katika kufanya makadirio ya kodi sahihi kulingana na taarifa sahihi zilizoletwa kwa kutumia mfumo huo, pia utasaidia wateja kujua sehemu mizigo yao ilipo na pia wanapaswa kulipa kiasi gani kulingana na mzigo wa mteja, wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam.

   Ofisa Mwandamizi wa Forodha kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Felix Tinkasimile akiwaeleza waandishi wa habari namna mfumo mpya wa uondoshaji mizingo unavyoongeza uwazi na uwajibikaji utakaosaidia kuzuia upoteaji wa mizigo bandarini ikiwemo Magari na Makontena , wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam.

   Kaimu Meneja wa Kituo cha Huduma cha Forodha kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Kasty Phelician akiwaeleza waandishi wa Habari majukumu ya kituo hicho ikiwemo kutoa tathnimi ya kodi unayopaswa kulipwa kwa kupitia na kuhakiki nyaraka zote kutoka kwenye kadhia zinazotumia mfumo wa TANCIS ikiwamo viwango vya ushuru wa forodha vinavyopaswa kutozwa.
   Meneja wa Forodha Bandari ya Dar es Salaam kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)Bw.Burton Kaissy akiwaeleza waandishi wa Habari namna wanavyoshirikiana na Taasisi mbalimbali kurahisisha usafirishaji wa mizigo yote inayoenda nje nchi

  Baadhi ya waandishi wa Habari wakimsikiliza Meneja wa Forodha Bandari ya Dar es Salaam kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)Bw.Burton Kaissy wakati wa Ziara iliyofanyika katika mamlaka hiyo kuona jinsi mfumo wa TANCIS unavyofanya kazi.PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO. 

  0 0

   Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akiongozana na viongozi wa dini ya kiislamu (kulia) Mwakilishi wa Mufti wa Tanzania katika Mafunzo hayo Sheikh Abubakar Zuber na kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwinyibaraka Sheikh Issa Othman wakati akilelekea kufungua Mafunzo ya kuwajengea uwezo Viongozi wa dini ya Kiislamu ili kuimarisha usalama nchini.Mafunzo hayo yaliandaliwa na Taasisi ya Mwinyibaraka na kufanyika jijini Dar es Salaam jana.(Picha na Frank Geofray wa Jeshi la Polisi)
   Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu, akizungumza na  viongozi wa  dini ya kiislamu waliohudhuria katika mafunzo ya kuwajengea uwezo Viongozi wa dini hiyo.Mafunzo hayo yaliandaliwa na Taasisi ya Mwinyibaraka na kufanyika jijini Dar es Salaam jana.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akizungumza  na Katibu wa Jumuiya ya Wanazuoni wa kiislamu Sheikh Khamisi Mataka katika Mafunzo ya kuwajengea uwezo Viongozi wa dini ya Kiislamu ili kuimarisha usalama nchini.Mafunzo hayo yaliandaliwa na Taasisi ya Mwinyibaraka na kufanyika jijini Dar es Salaam jana.

  0 0

   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kati Kati akishindikizwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Said Mohd Dimwa Kulia yake mara baada ya kuhudhuria Mkutano wa pamoja  kati ya Uongozi wa Kampuni inayohusika na masuala ya Teknolojia ya Kisasa ya mawasiliano ya Baharini  { SRT } na watendaji wa sekta ya Habarini hapo Zanzibar Ocean View.
    Afisa Mkuu wa Mradi wa Teknolojia ya Kisasa ya mawasiliano ya Baharini  wa Kampuni ya { SRT } kutoka Nchini Uingereza  Bwana Simon Tucker akielezea umuhimu wa kifaa cha mawasiliano kinachotumika katika vyombo vya usafiri Majini kwenye Mkutano wa pamoja na watendaji wa Sekta ya Baharini hapa Zanzibar.

  Wa Pili kutoka Kulia waliokaa ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Kulia ya Balozi ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Said Mohd Dimwa na wa kwanza kulia ni Bwana Lazaria Moh’d Said.
  Balozi Seif akizungumza na Wanahabari   mara baada ya kuhudhuria Mkutano wa pamoja kati ya Uongozi wa Kampuni inayohusika na masuala ya Teknolojia ya Kisasa ya mawasiliano ya Baharini  { SRT } ya Nchini Uingereza na  watendaji wa Taasisi zinazohusika na sekta hiyo hapo Zanzibar.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Zanzibar ikiwa ni sehemu ya Dunia hii  inahitaji kuendelea kuwa salama na tulivu kutokana na mazingira yake yaliyozunguukwa na Bahari pembe zote.

  Alisema mfumo wa kisasa wa mawasiliano unaotumika katika mataifa mbali mbali Duniani uliolenga zaidi katika maeneo ya bahari  yenye kutoa utajiri mkubwa kwa   asilimia 90% ya Uchumi wa Dunia unafaa kutumika ili kuondoa shaka katika udhibiti wa uvamizi wa vitendo vya kiharamia.

  Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akizungumza na Wanahabari wa Vyombo mbali mbali hapa Nchini mara baada ya kuhudhuria Mkutano wa pamoja kati ya Uongozi wa Kampuni inayohusika na masuala ya Teknolojia ya Kisasa ya mawasiliano ya Baharini  { SRT } ya Nchini Uingereza na  watendaji wa Taasisi zinazohusika na sekta hiyo hapo Zanzibar Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar.

  Alisema yapo matukio kadhaa ya uvamizi wa vyombo vya Baharini yaliyowahi kuibuka  na kuripotiwa katika ukanda wa Pembe ya Afrika ambayo yalikuwa yakitekelezwa na maharamia kutokana na udhaifu wa mawasiliano uliokuwepo wakati huo.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliridhika na kukubaliana na Mfumo wa kisasa waTeknolojia ya mawasiliano ya Baharini  unaotumiwa na Kampuni ya          { SRT } ya Nchini Uingereza katika Mataifa mbali mbali Duniani ambao umesaidia kupunguza wimbi la uharamia katika maeneo ya Baharini.

  Akiwasilisha mada ya mfumo wa utendaji kazi wa Kampuni hiyo kwenye  Mkutano huo Afisa Mkuu wa Mradi wa Teknolojia ya Kisasa ya mawasiliano ya Baharini  wa { SRT }  Bwana Simon Tucker alisema  kifaa maalum cha Mawasiliano huwekwa kwenye chombo cha Baharini ambacho husaidia kutoa taarifa za mawasiliano.

  Bw. Simon alisema chombo hicho kidogo kinachoweza kuwekwa kwenye boti au hata meli za uvuvi na abiria kinauwezo wa kusafirisha mawimbi ya mawasiliano kwa zidi ya meli 40.

  Othman Khamis Ame
  Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar. 

  0 0

      Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Mhe.Dkt.Pindi Chana akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa Kompyuta katika  Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu  kilichopo Manispaa ya Ilala,leo jijini Dar es Salaam.
      Meneja Masoko na Maendeleo ya Bidhaa wa DCB Commercial Bank,Bw.Boyd Mwaisame akifafanua jambo  wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa Kompyuta katika  Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu  kilichopo Manispaa ya Ilala,leo jijini Dar es Salaam.
      Baadhi ya Wanafunzi wa  Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu wakisikiliza kwa makini risala iliyo kuwa ikisomwa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Mhe.Dkt.Pindi Chana leo Jijini Dar es Salaam.
  0  Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Mhe.Dkt.Pindi Chana (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu  kilichopo Manispaa ya Ilala,leo jijini Dar es Salaam.( Picha na Emmanuel Massaka)

  Na Bakari Issa,Dar es Salaam.


  Benki ya Biashara ya DCB imetoa msaada wa Kompyuta kwa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu  kilichopo Manispaa ya Ilala,kwa lengo la kutoa elimu katika Chuo hiko chenye wanafunzi wenye ulemavu.


  Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo wa Kompyuta kwa Chuo hicho,Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Mhe.Dkt.Pindi Chana amesema  umuhimu wa Vyuo hivi unatokana na lengo la kuanzishwa kwake aambalo ni kutoa maarifa na stadi zitakazowawezesha wananchi kujiajiri,kujitegemea  ili kuondokana na ujinga,umaskini na maradhi hatimaye waweze kuchangia kuinua uchumi wa taifa.


  Pia,Dkt.Chana amewahasa wazazi kuacha kuwaacha watoto wao kukaa nyumbani bila kujishughulisha na shughuli yeyote pindi wanapomaliza masomo yao na badala yake kuwashughulisha watoto hao ili kujiepuka kujiingiza kwenye makundi yasiyofaa.


  Kwa upande wake,Meneja Masoko na Maendeleo ya Bidhaa wa DCB Commercial Bank,Bw.Boyd Mwaisame amesema  Benki imekabidhi msaada huo kutokana na kuguswa na matatizo mengi yanayojitokeza katika jamii likiwemo la ukosefu wa vitendea kazi . kwa watoto wenye Ulemavu.


  Naye, Mkuu wa  Chuo hiko,Bi.Pulcheria M. Ndamgoba ametoa  shukrani kwa msaada huo wa Kompyuta katika Chuo hiko na kuahidi kukitumia vizuri katika kutoa elimu chuoni hapo,huko Kiongozi wa  Wanafunzi wa Chuo hiko,Ridhwan Omary akitoa msisitizo kwa Benki hiyo kuwasaidia kujengea viwanja vya michezo.

  0 0

   Daktari Edna Kiogwe akieleza juu ya umuhimu wa elimu ya Hedhi kwa jamii nzima wakati wa semina na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St. Anthony.
  Mkurugenzi mtendaji wa Kasole Secrets Hyasintha Ntuyeko ambeye pia ni muandaaji wa siku ya Hedhi Duniani kwa Tanzania akielezea umuhimu wa kutunza Mazingira wanapokuwa Hedhi na kuithamini miundombinu.
   Kutoka kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa Kasole Secrets Hyasintha Ntuyeko ambao pia ni watengenezaji wa Pads za Glory, Katikati ni Mlezi wa wanafunzi Hilda Minja na Sara Mugele ambaye ni Dean of students  Shule ya Sekondari ya St. Anthony.
   Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St. Anthony wakiwa wanafuatilia kwa makini Semina hiyo.
   Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St. Anthony wakifurahia Pads za Glory walizopewa ikiwa ni ishara ya kusherehekea sikukuu ya Hedhi Duniani.
  Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St.Anthony wakifurahia zawadi za Glory Pads baada ya Semina.

  Kufahamu zaidi juu ya Hedhi salama Bofya www.hedhisalama.com  0 0older | 1 | .... | 504 | 505 | (Page 506) | 507 | 508 | .... | 1897 | newer