Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 502 | 503 | (Page 504) | 505 | 506 | .... | 1898 | newer

  0 0

  ais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza askofu Mpya wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu wakati wa ibada ya kumweka wakfu iliyofanyika katika kanisa kuu la Parokia ya Mama mwenye Huruma, Ngokolo, mjini Shinyanga leo.
  ---------------------------------
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumapili, Aprili 12, 2015 ameungana na maelfu ya waumini wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Shinyanga, kuhudhuria Ibada rasmi ya kumweka wakfu na kumsimika Askofu mpya wa Jimbo hilo, Mhashamu Baba Askofu Liberatus Sangu.  Rais Kikwete amewasili kwenye Kanisa Kuu la Mama Mwenye Huruma, Ngokolo, mjini Shinyanga kiasi cha saa sita unusu mchana kwa ajili ya Ibada hiyo iliyohudhuriwa pia na maaskofu wakuu, maaskofu na maaskofu wasaidizi 38, akiwamo Askofu Mkuu wa Jimbo la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo na Rais wa Mabaraza ya Kipapa na Katibu Mwambata wa Uenezaji Injili Ulimwenguni Askofu Mkuu Protase Rugambwa kutoka Makao Makuu ya Kanisa Katoliki, Vatican.  Askofu Sangu ambaye amewekwa wakfu na kusimikwa kwenye Siku ya Huruma ya Mungu Duniani anakuwa Askofu wa nne wa Jimbo la Shinyanga na anachukua nafasi iliyoachwa wazi tokea Novemba 6, 2012, wakati aliyekuwa Askofu wa Jimbo hilo, Baba Askofu Aloysius Balina alipofariki dunia.  Kwa miaka karibu mitatu, jimbo hilo limekuwa chini ya Usimamizi wa Kitume wa Askofu Mkuu Yuda Tadei R’uaichii wa Jimbo Kuu la Mwanza.

  Askofu Sangu mwenye umri wa miaka 52 baada ya kuwa amezaliwa Februari 19, mwaka 1963, katika Kijiji cha Mwazye, Jimbo Katoliki la Sumbawanga, Mkoa wa Rukwa, alipata daraja la upadrisho Julai 3, mwaka 1994. Wakati anateuliwa na Baba Mtakatifu Francesco kuwa Askofu Februari 2, mwaka huu wa 2015, alikuwa na daraja la Mosinyori.             Akikabidhi Jimbo hilo kwa Askofu mpya, Askofu Mkuu R’uaichii amesema kuwa Jimbo la Shinyanga ni moja ya majimbo makubwa zaidi ya Kanisa Katoliki nchini, likiwa na kilomita za mraba karibu 30,000 na waumini Wakatoliki wanaokaridiwa kufikia 300,000 katika Mkoa ambao idadi kiasi ya wakazi wake bado wanaamini  imani za jadi.  Amesema kuwa Jimbo hilo lina parokia 29, mapadre wa Jimbo 52, mapadre wa Kitawa 18 na hivyo kulifanya jimbo hilo kuwa na jumla ya mapadre 70 na “jeshi kubwa” la watawa 70.

  Kwenye sherehe hizo zilizohudhuriwa na viongozi wengi wa Serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Ali Lufunga, Askofu Sangu amepewa zawadi ya sh milioni 18, fimbo ya kiuchungaji na ng’ombe 10 wa maziwa na Wakatoliki wa Jimbo hilo. Rais Kikwete amerejea Dar es Salaam jioni ya leo baada ya kumalizika kwa Ibada hiyo.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa salamu zake za pongezi muda mfupi baada ya kumalizika kwa ibada ya kumweka wakfu askofu mpya wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu katika Kanisa Kuu Parokia ya Mama Mwenye Huruma Ngokolo Mjini Shinyanga.


  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na maaskofu wa Katoliki muda mfupi Baada ya ibada ya kumweka wakfu askofu mpya wa jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Baba Askofu Liberatus Sangu(wapili kulia pembeni ya Rais) huko Ngokolo mjini Shinyanga leo. Picha na Freddy Maro

  0 0

  1
  Rais Jakaya Kikwete akikabidhi tuzo ya Meya Bora Tanzania kwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda baada ya kushinda tuzo hiyo kitaifa iliyoandaliwa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa nchini (ALAT) katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam juzi. Kulia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Agrey Mwanri.
  3
  Rais Jakaya Kikwete akizungumza baada ya kukabidhi Tuzo ya Meya Bora Tanzania, Yusuph Mwenda (kulia) baada ya kushinda tuzo hizo zilizoandaliwa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa nchini (ALAT) katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya NMB, Tom Boghols na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Hawa Ghasia (wa pili kushoto).
  4
  Rais Jakaya Kikwete akitoa maelekezo kwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (kulia) kuhusu namna bora ya matumizi ya trekta baada ya kumkabidhi Meya huyo baada ya kushinda Tuzo ya Meya Bora Tanzania kwenye hafla iliyofanyika Dar es Salaam hivi karibuni. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki na Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya NMB, Tom Boghols (wa pili kulia).
  5
  Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akijaribu kuendesha trekta alilokabidhiwa na Rais Jakaya Kikwete baada ya kushinda tuzo ya Meya Bora Tanzania.
  …………………………………………………………………
  Na Mwandishi Maalum,
  Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda ameshinda Tuzo ya Meya Bora Tanzania na kuzishinda Halmashauri 168 zote nchini.
  Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo na Rais Jakaya Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, Meya wa Manispaa hiyo, Yusuph Mwenda amesema siti ya kushinda tuzo hiyo ni kufanya kazi kwa pamoja kati yake Madiwani, Watendaji na kuwahsirikisha wananchi wake.
  Meya Mwenda alisema kuwa Halmashauri yake imekuwa ikifanya kazi kwa uwazi zaidi kwa kuwashirikisha wananchi wake katika mikakati ya kimaendeleo ikiwemo kuwashirikisha katika miadi mbalimbali ya Halmashauri hiyo na hivyo kujikuta kazi yake inakuwa rahisi na kupata mafanikio makubwa kwa muda mfupi.
  Mwenda alisema kuwa Manispa yake imekuwa mstari wa mbele katika kusimamia na kuitekeleza miradi yake kwa bidii kubwa ikiwemo ukusanyaji mapato na usimamizi mzuri wa matumizi ya mapato hayo katika miradi hiyo.
  “Ushirikiano ‘team work’ kati yangu na madiwani, Madiwani na Watendaji, Ofisi ya Mkuu wa Wialaya na Mkuu wa Mkoandio siri ya mafanikio. Lakini kubwa zaidi ni wananchi wenyewe, kupitia wao tumeweza kuwa na mendeleo zaidi.” Alisema Mwenda.
  Aidha Meya Mwenda alisema kuwa Halmashauri yake imefanikiwa kufikia malengo yake kutoka na kuongezeka kwa mapato ya ndani kwa aslimia 360 kutoka shilingi Bilioni 10 mwaka 2011/ 2011 mpaka kufikia Bilioni 36 mwaka jana na kuiwezesha Manispaa hiyo kusimamia vema miradi yake yenyewe.
  Aliitaja miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa Barabara, Madara, Zahanati, Shule, matumizi ya Teknohama pamoja na ujenzi wa Kituo kikubwa cha daladala cha kisasa cha Sinza ambacho ujenzi wake umegharimu shilingi bilioni 4.06.
  Aidha alisema Halmashauri yake imeweza kuongeza fedha za miradi yake ya maendeleo kutoka Bilioni 3.2 kwa mwaka 2011 mpaka kufikia Bilioni 16 na hivyo kuifanya kuwa ya kwanza nchini kusimamia miradi yake kwa fedha za mapato ya ndani kwa asilimia kubwa.
  Hii ni mara ya kwanza kufanyika kwa shindano la Tuzo za Meya Bora Tanzania chini ya Jumuiya ya Serikali za Mitaa nchini (ALAT) ambazo zilikuwa katika makundi mawili makuu ambayo ni Tuzo ya Maendeleo ya Halmashauri na Tuzo ya Jumla ambazo zilifanyika juzi na kuhudhuriwa na Rais Jakaya Kikwete.

  0 0

  SAM_1775
  MKUU  wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda akiwa anafungua mkutano ulioandaliwa na mfuko wa mafao ya kustaafu wa GEPF kwa wadau wake jijini Arusha uliolenga kujadili maswala mbalimbali ya mfuko wa mafao ya kustaafu (GEPF) sambamba na mabadiliko katika mfuko huo.(Habari Picha na Pamela Mollel wa http://jamiiblog.co.tz/)
  SAM_1760 
  Meneja masoko wa mfuko wa GEPF Aloyce Ntukamazina akizungumza katika mkutano na wadau kutoka sekta mbalimbali uliofanyika jijini Arusha uliolenga kujadili maswala mbalimbali ya mfuko wa mafao ya kustaafu (GEPF) sambamba na mabadiliko katika mfuko huo.
  SAM_1759
  MKUU  wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda akiwa anasoma kipeperushi chenye maelezo kuhusu mfuko wa GEPF,kushoto Meneja masoko wa mfuko wa GEPF Aloyce Ntukamazina,kulia ni meneja kanda ya kaskazini Dennis Kaitwa
  SAM_1765
  Kushoto Mwalimu Jonuis Lowassa kutoka idara ya utumishi wa walimu(KTSD)wilaya ya Mounduli na Longido SAM_1779
  Afisa masoko GEPF Clement Oning'o ambaye alikuwa Mc wa shughuli hiyo akitoa utaratibu katika mkutano huo.
  SAM_1769
  Afisa muajiri Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Siraji Msophe akifurahia jambo katika mkutano huo
  SAM_1770
  MKUU  wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda wakiwa wanateta jambo na Meneja masoko wa mfuko wa GEPF Aloyce Ntukamazina
  SAM_1761
  Wadau wakiwa katika mkutano huo
  SAM_1762
  Kushoto Afisa rasilimali watu na utawala Halmashauri ya wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Isaial Bayege akiwa ananukuu baadhi ya mambo katika mkutano huo ulioandaliwa na mfuko wa GEPF jijini Arusha
  SAM_1763
  Kulia ni Afisa Rasilimali watu katika chuo cha Nelson Mandela Bi.Honorina Mashingia
  SAM_1783
  Meneja masoko wa mfuko wa GEPF Aloyce Ntukamazina akizungumza na waandishi wa habari kutoka  vyombo mbalimbali kuhusu mfuko wa GEPF jijini Arusha
  SAM_1785
  Meneja kanda ya kaskazini kutoka mfuko wa GEPF Dennis Kaitwa akizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha
  SAM_1780
  Washiriki wa mkutano huo wakiwa katika picha ya Pamoja na mgeni Rasmi MKUU  wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda
  MKUU wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda ameitaka mifuko ya jamii kuendelea kutoa elimu zaidi kwa wananchi kujiunga na mifuko hiyo ili kuweka akiba ambayo itasawasaidia kwa maisha yao ya baadaye.
  Aliyasema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa wadau kutoka sekta mbalimbali uliofanyika mjini hapa uliolenga kujadili maswala mbalimbali ya mfuko wa mafao ya kustaafu (GEPF) sambamba na mabadiliko katika mfuko huo
  .
  Alisema kuwa, mifuko hiyo ina manufaa makubwa sana kwa jamii hususan kipindi cha kustaafu ambacho huwa ni kipindi kigumu sana kwa asilimia kubwa ya wastaafu ambapo wengi wao mifuko hiyo huwasaidia sana kuondokana na maisha magumu yanayowakabili.

  Ntibenda alisema kuwa, kuna idadi kubwa sana ya wastaafu ambao wangependa kujiunga na mifuko hiyo ila kinachowawia ugumu ni kutopata elimu ya kutosha juu ya kujiunga na mifuko hiyo ambayo ina manufaa makubwa sana kwao.

   Meneja masoko wa mfuko wa GEPF Aloyce Ntukamazina alisema kuwa ,mfuko huo umeanza kutoa elimu nchi nzima juu ya mabadiliko ya mfuko huo ambapo wamezindua mafao mapya manne ambayo ni fao la elimu,uzazi,fao la kuanza maisha ,na fao la kujikimu ambapo mafao hayo yote ni yataanza kutumika katika mfuko huo hivi sasa.

  Aloyce amesema kuwa,mfuko huo wamekuwa wakijitahidi sana na kukabiliana na changamoto ya wajiri kutofikisha mafao ya wafanyakazi kwenye mifuko kwa wakati ambapo mfuko huo wamekuwa wakijitahidi kuhakikisha makato hayo yanafika kwa wakati na muda ulipangwa .

  Aidha washiriki wa mkutano huo, wakizungumza kwa nyakati tofauti waliutaka usimamizi wa mifuko hiyo kuongeza mifuko zaidi ili wananchi wawe katika hali nzuri ya kiuchumi kwa kutumia mifuko mbalimbali na kuondokana na kusongamana kwenye mifuko michache iliyopo .

  Meneja wa mfuko huo kanda ya kaskazini ,Denis Kaitwa amesema kuwa wamekuwa wakikabiliwa na changamoto kubwa ya kutoa elimu kutokana na asilimia kubwa ya wananchi kuwa wagumu kujiunga na mifuko hiyo ambayo ina manufaa makubwa kwa maisha yao.

  Kaitwa alisema kuwa,kupitia mkutano huo utawawezesha wadau hao kutoa elimu zaidi kwa wafanyakazi wao na hatimaye kuweza kutambua umuhimu wa kujiunga na mfuko huo wa GEPF ambao una manufaa makubwa kwa jamii.

  0 0

  Mgeni rasmi wa mpambano wa fainali kugombea pikipiki Gongo la Mboto, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa (mwenye miwani) akikabidhi zawadi ya mshindi wa kwanza wa kombe la pikipiki lililoandaliwa na Lucas Lutanilwa. Mgeni rasmi wa mpambano wa fainali kugombea pikipiki Gongo la Mboto, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa (mwenye miwani) akikabidhi zawadi ya mshindi wa kwanza wa kombe la pikipiki lililoandaliwa na Lucas Lutanilwa.Mgeni rasmi wa mpambano wa fainali kugombea pikipiki Gongo la Mboto, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa (mwenye miwani) akikabidhi zawadi ya mshindi wa kwanza wa kombe la pikipiki lililoandaliwa na Lucas Lutanilwa. Mgeni rasmi wa mpambano wa fainali kugombea pikipiki Gongo la Mboto, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa (mwenye miwani) akikabidhi zawadi ya mshindi wa kwanza wa kombe la pikipiki timu ya Mazombi FC lililoandaliwa na Lucas Lutanilwa.Mwakilishi wa Timu ya Vijana Jogging Club akipokea zawadi ya fedha baada ya kuibuka washindi wa tatu katika Luta CUP Gongo la Mboto. Mwakilishi wa Timu ya Vijana Jogging Club akipokea zawadi ya fedha baada ya kuibuka washindi wa tatu katika Luta CUP Gongo la Mboto..Mgeni rasmi wa mpambano wa fainali kugombea pikipiki Gongo la Mboto, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa (wa pili kulia) akizungumza kabla ya kuanza kwa mtanange huo kati ya Timu ya Mazombi FC na Sobibo FC. Mgeni rasmi wa mpambano wa fainali kugombea pikipiki Gongo la Mboto, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa (wa pili kulia) akizungumza kabla ya kuanza kwa mtanange huo kati ya Timu ya Mazombi FC na Sobibo FC.
  Washindi wa nne wakipokea haki yao pia. Washindi wa nne wakipokea haki yao pia.Washindi wa nne wakipokea haki yao pia. Washindi wa nne wakipokea haki yao piaMgeni rasmi wa mpambano wa fainali kugombea pikipiki Gongo la Mboto, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa (mwenye miwani) akifuatilia mpambano kati ya Timu za Mazombi FC na Sobibo FC. Mazombi walifanikiwa kutaa ubingwa baada ya kuifunga Sobibo 1-0. Mgeni rasmi wa mpambano wa fainali kugombea pikipiki Gongo la Mboto, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa (mwenye miwani) akifuatilia mpambano kati ya Timu za Mazombi FC na Sobibo FC. Mazombi walifanikiwa kutaa ubingwa baada ya kuifunga Sobibo 1-0.Mgeni rasmi wa mpambano wa fainali kugombea pikipiki Gongo la Mboto, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa () akikagua timu ya Mazombi FC kabla ya mpambano kuanza. Mgeni rasmi wa mpambano wa fainali kugombea pikipiki Gongo la Mboto, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa () akikagua timu ya Mazombi FC kabla ya mpambano kuanza.Mgeni rasmi wa mpambano wa fainali kugombea pikipiki Gongo la Mboto, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa (wa pili kulia) akikagua timu ya Sobibo FC kabla ya mpambano kuanza. Mgeni rasmi wa mpambano wa fainali kugombea pikipiki Gongo la Mboto, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa (wa pili kulia) akikagua timu ya Sobibo FC kabla ya mpambano kuanza.Timu ya Sobibo FC katika picha ya pamoja kabla ya mpambano kuanza. Timu ya Sobibo FC katika picha ya pamoja kabla ya mpambano kuanza.Timu ya Mazombi FC katika picha ya pamoja kabla ya mpambano kuanza. Timu ya Mazombi FC katika picha ya pamoja kabla ya mpambano kuanza.Mashabiki mbalimbali wa Gongo la Mboto wakifuatilia mpambano wa fainali kugombea pikipiki Gongo la Mboto. Mashabiki mbalimbali wa Gongo la Mboto wakifuatilia mpambano wa fainali kugombea pikipiki Gongo la Mboto.Baadhi ya wachezaji na mashabiki na Timu ya Vijana Jogging Club wakishangilia baada ya kuibuka washindi wa tatu katika Luta CUP Gongo la Mboto. Baadhi ya wachezaji na mashabiki na Timu ya Vijana Jogging Club wakishangilia baada ya kuibuka washindi wa tatu katika Luta CUP Gongo la Mboto.

    MEYA wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa jana alilazimika kutoa zawadi ya pikipiki baada kuvutiwa na ushindani mkubwa uliokuwepo katika mchezo wa fainali wa mpira wa miguu kugombea pikipiki aina ya Boxer. Meya Slaa alilazimika kutoa pikipiki hiyo baada ya timu za Mazombi FC na Sobibo FC zote za Gongo la Mboto kuonesha ushindani mkali katika mchezo wa fainali uliofanyika katika Uwanja wa Kampala Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam. 

   Slaa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mchezo huo ameahidi kuwakabidhi pikipiki mpya timu ya Sobibo FC ambayo ilishika nafasi ya pili katika mchezo huo wa fainali ambapo timu ya Mazombi FC iliibuka mshindi na kukabidhiwa pikipiki mpya aina ya Boxer iliyotolewa na muandaaji wa mashindano hayo Lucas Lutanilwa.

   "...Kutokana na ushindani mkubwa uliooneshwa na timu zote mbili natamka kwamba hata washindi wa pili Sobibo FC nao ninawazawadia pikipiki kama waliopata wenzao ili kuleta kiu ya kupenda michezo zaidi kwa vijana wetu," alisema Slaa akizungumza alipokuwa akikabidhi pikipiki kwa mabingwa Masombi FC. Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani kwa pande zote mbili timu ya Mazombi imefanikiwa kutwaa ubingwa na kukabidhiwa pikipiki mpya baada ya kuifunga Sobibo FC goli 1-0 lilipatikana dakika 70 ya kipindi cha pili cha mchezo huo.

   Timu zote mbili pia zilikabidhiwa seti mojamoja ya jezi kwa kuweza kufika fainali, hata hivyo washindi wa nne na tatu wa Mashindano hayo yaliyopewa jina la Luta Cup walipewa zawadi za fedha taslimu kama pongezi. Timu ya Vijana Jogging Club walifanikiwa kutwaa ushindi wa tatu na kujinyakulia fedha taslimu katika mashindano hayo.

  0 0

  Wanafunzi wa shule ya sekondari Handeni iliyopo wilayani Handeni wakisoma vitabu vilivyotolewa na Kampuni ya Airtel shuleni hapo kwa ajili ya masomo ya sayansi vyenye thamani ya sh.milioni mbili.
  Meneja wa Mauzo wa Kampuni ya Simu za Mikononi ya Airtel Kanda,Aluta Kweka kulia akimkabidhi Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Handeni Muhingo Rweymamu vitabu vya masomo ya sayansi vilivyotolewa na kampuni hiyo vyenye thamani ya sh.milioni mbili anayeshuhudia katikati ni Mwalikishi wa Afisa Elimu wilaya ya Handeni,Ally Mwinyuma ambaye alimuwakilisha pia Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo.
  Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Handeni,Ally Adamu kulia akimkabidhi kitabu mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule hiyo Aisha Juma cha Fizikia ambavyo vilitolewa na kampuni ya simu za mikononi nchini Airtel vyenye thamani ya sh.milioni mbili.

  Uongozi wa shule ya sekondari ya Kutukutu iliyopo wilayani kilosa mkoani Morogoro, umeishukuru kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa msaada wa vitabu vya masomo ya sayani.

  Msaada huo wenye thamani ya shilingi milioni mbili umekabidhiwa hivi karibu na wawakilishi wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ikiwa ni mpango wa SHULE YETU unaosimamiwa na kampuni hiyo.

  Akipokea msaada huo kwa niaba ya walimu na wanafunzi wa shule hiyo mkuu wa shule ya sekondari Kutukutu Finyilise Elias amesema, utasaida kuongeza ufaulu wa wanafunzi wake wanaosomea masomo ya sayansi.

  Mwalimu Finyilise amesema, kumekuwa na ufaulu wa kusuasua kwa wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne hasa kwenye masomo ya sayansi hivyo msaada huo utasaidia kuongeza ufaulu shuleni hapo. “ Wanafunzi wetu wanaosomea michepuo ya sayansi wamekuwa na ufaulu mdogo sana na hii inatokana na ukosefu wa vitabu vya masomo hayo kwa muda mrefu sasa” alisema Mwalimu Mkuu huyo.

  “msaada huu utatusukuma haraka kwenye ufaulu wa kiwango cha juu wa masomo ya sayansi kwani mwitikio wa wanafunzi wetu ni mkubwa na tunatarajia tutapata matokeo ya haraka kutokana na msaada huu wa vitabu” aloingeza Mwalimu Finyilise.

  Awali akikabidhi msaada wa vitabu hivyo, Meneja wa Airtel Mkoani Morogoro Bw. Omar Bongo amesema, hatua hiyo ni kuwawezesha wanafunzi wa shule za sekondari kupata maarifa ya masomo ya sayansi kwa vitendo. “Sisi wa Airtel tumekuja hapa kusukuma gurudumu la maendeleo mbele kupitia elimu na hasa vitabu vya kujifunzia, mkazo wetu kwa sasa ni masomo ya Sayansi na tumeleta vitabu vya kujifunzia. Alisema Bw. Bongo.

  Shule hiyo ya sekondari kutukutu yenye wanafunzi zaidi ya 300 bado inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na vyumba vya maabara na mazingira mazuri ya kujifunzia.

  0 0

  ZURII HOUSE OF BEAUTY AND BONGO DEEJAYS PRESENT!!
  Londons Rugby 7's After Party, Appearing Live, Bongo Flava recording artist from Tanzania most famous for his song "Number One". Diamond Platnumz will be preforming with his WCB dancers and special guests at the Royal Regency Banquet Hall for one night only.
  THE ROYAL REGENCY
  501 HIGH STREET NORTH
  MANOR PARK 
  For Front Row V.I.P Tables and Info Please Contact our Ticket Hotline: 07853482158 or 07421167123
  Dont be left out, tickets are running out quickly. We are counting down to the most Epic event of the Year!!
  IN SUPPORT OF ALBINO CRUELTY IN TANZANIA. TOGETHER WE SAY: "IMETOSHA"
  Follow the link below or clck "Buy Tickets" to get your tickets A.S.A.P


  Buy tickets for Diamonds are forever UK live concert

  0 0

   Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade (kulia) akikata utepe kwenye boksi lililokuwa na Mtaala utakaotumia katika mafunzo hayo wakati wa ufunguzi uliofanyika leo jijini Dar es Salaam kushoto ni Mkuu wa Chuo cha uongozi wa Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo

   Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade (kulia) akionesha mtaala utakaotumika katika mafunzo ya washiriki 150 waliodahiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kushoto ni Mkuu wa Chuo cha uongozi wa Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo

   Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade(wa sita kutoka Kulia) na Mkuu wa Chuo cha uongozi wa Kodi Prof. Isaya Jairo (ITA) (wa Tano kutoka kushoto) wakiwa katika Picha ya Pamoja na washiriki wa Mafunzo hayo baada ya kuyazindua leo Jijini Dar es Salaam. 

   Baadhi ya washiriki wa Mafunzo hayo wakifuatilia hotuba zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa ufunguzi wa Mafunzo hayo.
  Picha na Hassan Silayo-MAELEZO.


   - Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo akiwakaribisha wageni katika hafla ya ufunguzi wa Mafunzo ya ukusanyaji kodi kwa waajiriwa wapya Leo Jijini Dar es Salaam.

   Mkuu wa Chuo cha uongozi wa Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo akimkaribisha Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Mafunzo hayo na kuwataka washiriki kushiriki kikamilifu kwenye kipindi cha mafunzo ili waweze kuwa na mbinu thabiti za ukusanyaji kodi kwa maslahi ya Taifa
   Naibu Mkurugenzi kitengo cha Rasilimali Watu Bw. Victor Kimaro akiwaeleza washiriki wa Mafunzo namna mchakato ulivyofanyika na kuwataka kuthibitisha ubora wao katika kipindi chote cha mafunzo
   
   - Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Rished BADE akiongea na washiriki wa Mafunzo ya ukusanyaji kodi na kuwataka kufanya kazi kama watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania na kutumia fursa hiyo kujiimarisha kiutendaji kabla ya kuanza kazi rasmi ya ukusanyaji kodi inayohitaji uadilifu na ueledi wa hali ya juu katika kuitekeleza, wakati wa hafla iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam

  0 0

   Mshauri wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Phocus Lasway akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Kebwe Stephen Kebwe (kulia) wakati wa ziara ya Kiwanda cha Dar es Salaam cha TBL kilichopo Ilala. Kushoto ni Mkurugenzi wa Usalama na Chakula wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Raymond Wisenge. Wizara ilionesha kuridhishwa na viwango vinavyozingatiwa na TBL katika uzalishaji wake.
   Meneja Mdhibiti Viwango wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Conchesta Ngaiza (kulia) akimuelezea jambo Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Kebwe Stephen Kebwe wakati wa ziara ya Kiwanda cha Dar es Salaam cha TBL kilichopo Ilala. Kushoto ni Mkurugenzi wa Usalama na Chakula wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Raymond Wisenge. Wizara ilionesha kuridhishwa na viwango vinavyozingatiwa na TBL katika uzalishaji wake.
   Meneja wa Kiwanda cha Dar es Salaam cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Calvin Martin akimuelezea jambo Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Kebwe Stephen Kebwe wakati wa ziara ya Kiwanda cha Dar es Salaam cha TBL kilichopo Ilala. Wizara ilionesha kuridhishwa na viwango vinavyozingatiwa na TBL katika uzalishaji wake.
   Meneja wa Kiwanda cha Dar es Salaam cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Calvin Martin (kulia) akimuelezea jambo Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Kebwe Stephen Kebwe. Wizara ilionesha kuridhishwa na viwango vinavyozingatiwa na TBL katika uzalishaji wake.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye koti) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali a wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na watumishi wa wizara hiyo baada ya ziara ya Kiwanda cha Dar es Salaam cha TBL kilichopo Ilala. Wizara ilionesha kuridhishwa na viwango vinavyozingatiwa na TBL katika uzalishaji wake.


  Wizara ya Afya yaridhishwa na viwango TBL

  Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeonesha kuridhishwa na viwango vinavyozingatiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika uzalishaji wa bia zake.

  Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri  wa Wizara hiyo Dk Kebwe Stephen Kebwe wakati wa ziara ya kiwanda hicho ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa wizara yake kutembelea maeneo yaliyo katika utaratibu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

  “Hapa TBL tumegundua kuna uwelewa  wa hali ya juu kwa watumishi, wafanyakazi, wasimamizi na menejimenti  ya kampuni hii kwa kweli viwango ni vizuri na hasa katika ufuatiliaji wa wa afya za wafanyakazi,” alisema na kuongeza kuwa walijionea uzalishaji wa bia mbalimbali kiwandani hapo kwenye chupa na kadhalika.

  Kwa mujibu wa Naibu Waziri huyo, malengo mwaka huu ni kufanya usimamizi katika maeneo mbalimbali yanayotoa huduma kwa wananchi kama viwanda na kuogeza ni lazima viwanda viendane na viwango vinavyotakikana kisheria na kimataifa na kwamba wizara yake sasa hivi haikai na kusubiri ripoti za mezani bali wanatembelea maeneo yaliyo chini yao ili kujihakikishia kuhusu suala la viwango.

   Naibu Waziri huyo, ambaye aliambatana na viongozi mbalimbali kutoka wizarani na Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA), aliwapongeza viongozi wa TBL kwa kujipanga vizuri  katika utendaji  wao.

  “Tumetembelea viwanda mbalimbali lakini hapa mmejipanga vizuri zaidi, alisema baada ya kupokea maelezo mbalimbali kutoka kwa viongozi wa TBL waliokuwepo kwenye ziara hiyo.

  Dk. Kebwe pia aliipongeza TBL kwa kuwa mstari wa mbele katika kuwajali wafanyakazi kwa kuanzisha Programu ya Ukimwi katika sehemu ya kazi ambayo pamoja na mambo mengine inalenga kuhamasisha upimaji wa mara kwa mara na pia kuhumiza matumizi ya kinga dhidi ya ugonjwa huo.

  Katika maelezo ya utangulizi, Naibu waziri huyo alielezwa kuwa TBL ina utaratibu wa kupima wafanyakazi wake mara moja kwa mwaka na kwa kipindi cha kuanzia Aprli mwaka jana hado Machi mwaka huu zaidi ya asilimia 83 ya wafanyakazi walipima afya yao kuona kama wameathirika au la.

  “Hii ni dalili nzuri sana na nawapongeza kwa hatua hii na ni matumaini yangu kuwa kuanzia sasa na kuendelea mtaanza kupima mara mbili kwa mwaka nivyo sheria inavyotaka,” alisema.

  Meneja wa Kiwanda Cha Dar es Salaam, Calvin Martin, alisema wamefarajika mno kwa ujio huo wa Naibu Waziri ili aweze kujionea namna kampuni hiyo imekuwa ikizingatia suala la viwango katika uzalishaji wake.

  “Tumewaonesha maeneo yote na wameonesha kuridhishwa na viwango na haua ambazo bidhaa zetu zinapitia kabla ya kwenda kwa mlaji,” alisema na kuongeza kuwa wana nia ya kuendelea kuboresha viwango vyao ili kampuni hiyo iendelee kuwa bora zaidi. 

  0 0

  Familia aliye kuwa waziri mkuu  wa Tanzania  hayati Edward Moringe Sokoine wakiwa katika ibada maalumu ya maadhimisho ya kifo chake  nyumbani kwake monduli juu, siku ambayo huadhimishwa April 12 kila mwaka
  Wake wa  aliye kuwa  waziri mkuu  wa Tanzania  hayati Edward Moringe Sokoine  , wakiweka  mashada ya maua kwenye kaburi la  mume wao nyumbani kwake eneo la monduli Juu wilayani monduli mkoani Arusha wakati wa maadhimisho ya siku ya kifo chake siku ambayo huadhimishwa April 12 kila mwaka.

  Watoto wa kiume wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, Kutoka kushoto:  Joseph Sokoine,Tumaini Sokoine na Ibrahimu Sokoine wakiweka shada la maua kwenye kaburi la baba yao nyumbani kwake eneo la Monduli Juu Wilayani Monduli mkoani Arusha wakati wa maadhimisho ya siku ya kifo chake jana.

  Watoto wa kike wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, Kutoka kushoto:  Maria Sokoine,Joyce Sokoine ,Mbunge wa Viti Maalum Namelock Sokoine na Seki Sokoine wakiweka shada la maua kwenye kaburi la baba yao nyumbani kwake eneo la Monduli Juu Wilayani Monduli mkoani Arusha wakati wa maadhimisho ya siku ya kifo chake jana.
   Mbunge wa Viti Maalum, Namelock Sokoine akiwa na kaka yake ibrahim Sokoine katika kumbukumbu ya kifo cha baba yao aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania.
   Mbunge wa Viti Maalum na Mtoto wa  aliye kuwa waziri mkuu  wa zamani   hayati Edward Moringe Sokoine, Namilock Sokoine akiongea na baadhi ya wazee wa kimaasai baada ya misa maalumu ya maadhimisho ya kifo  cha Sokoine amabayo yalifanyika  nyumbani kwa marehemu eneo la Monduli juu wilayani Monduli mkoani Arusha jana.
   Mbunge wa viti maalu, Namelock Sokine akizungumza na wadau 

  0 0

   Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais-Utumishi Mhe.Celina O.Kombani (Mb) akiwa katika hafla fupi ya kuwaaga wanamichezo wa ofisi yake wanaoelekea katika mashindano ya Meimosi 2015 mkoani Mwanza.
   Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais-Utumishi Mhe.Celina O. Kombani (Mb)akiagana na wachezaji  wa Ofisi ya Rais-Utumishi wanaokwenda katika mashindano  ya Meimosi 2015 yatakayofanyika jijini Mwanza.
  Kaimu Katibu Mkuu-Utumishi Bw.HAB Mkwizu (kushoto) akiagana na wachezaji  wa Ofisi ya Rais-Utumishi wanaokwenda kuiwakilisha ofisi katika mashindano  ya Meimosi 2015 yatakayofanyika jijini Mwanza.

  0 0

   
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua kitabu cha Programu ya Uongozi na Maadili  katika Chuo cha Kumbukumbu ya Nyerere Kigamoni jijini Dar es salaam leo. Kushoto kwake  ni Waziri wa Elimu Dkt Shukuru Kawambwa na kulia kwake ni Mkuu wa Chuo hicho Profesa Shadrack Mwakalila. 
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsimika rasmi Mzee Pius Msekwa kuwa Mwenyekiti wa Kibweta cha Mwalimu Nyerere cha Uongozi na  Maadili wakati wa uzinduzi wa Kozi Maalum ya Maadili na Uongozi katika Chuo cha Kumbukumbu ya Nyerere Kigamoni jijini Dar es salaam leo.
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza  Mzee Pius Msekwa akitoa shukurani baada ya kusimikwa rasmi kuwa Mwenyekiti wa Kibweta cha Mwalimu Nyerere cha Uongozi na  Maadili wakati wa uzinduzi wa Kozi Maalum ya Maadili na Uongozi katika Chuo cha Kumbukumbu ya Nyerere Kigamoni jijini Dar es salaam leo. Kushoto kwake  ni Waziri wa Elimu Dkt Shukuru Kawambwa na kulia kwake ni Mkuu wa Chuo hicho Profesa Shadrack Mwakalila.
   Rais Jakaya Mrisho Meza kuu akiwa imesimama na meza kuu  kuimba wimbo wa Taifa baada ya uzinduzi wa Kozi Maalum ya Maadili na Uongozi katika Chuo cha Kumbukumbu ya Nyerere Kigamoni jijini Dar es salaam leo. Kushoto kwake  ni Waziri wa Elimu Dkt Shukuru Kawambwa na kulia kwake ni Mkuu wa Chuo hicho Profesa Shadrack Mwakalila.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akielekea kwenye uwanja wa shughuli tayari kuzindua Kozi Maalum ya Maadili na Uongozi katika Chuo cha Kumbukumbu ya Nyerere Kigamoni jijini Dar es salaam leo. Pamoja naye ni Mkuu wa Chuo hicho Profesa Shadrack Mwakalila. PICHA NA IKULU

  0 0

  Jumla ya kaya masikini elfu Tisa 277 zimetambuliwa na Halmashauri ya wilaya ya Mufindi, katika utekelezaji wa hatua ya awali ya kuzibaini kaya masikini kwenye vijiji na mitaa ikiwa ni mpango wa awamu ya tatu wakuzinusuru kaya masikini unaoratibiwa na mfuko wa maendeleo ya jamii nchini Tasaf kuputia Halmashauri hiyo.

  Taarifa ya Ofisi ya habari na Mawasiliano ya Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kwa vyombo vya habari, imetanabaisha kuwa, wawezeshaji wapatao 72 walijengewa uwezo wa kubaini vigezo kwa kaya masikini, ambapo hojaji zilifanyiaka na jumla ya vijiji 82 na mitaa 12 walifanya dodoso na kuzibaini kaya masikini elfu tisa 277.

  Taarifa  hiyo imeeendele kubainisha kuwa, tayari kaya hizo zimepelekwa Tasaf makao makuu ili kufanyiwa uchambuzi wa mwisho unaozingatia vigezo kwa njia ya teknolojia ya kompyuta na mara baada ya kurejea kwa kaya teule, zoezi litakalofuata ilitakuwa ni uandikishaji  kabla ya kuziwezesha kifedha, ambapo kila kaya inatarajia kupata shilingi elfu 38 na 100 kila mwezi kwa kipindi cha miaka mitatu.

  Pamoja na uwezeshaji huo katika ngazi ya kaya, mpango huo pia unakusudia kuibua na kutekeleza miradi ya msingi ya huduma za kijamii kwenye  sekta za Afya, Elimu na Maji katika maeneo ambayo kaya hizo zimetambuliwa.

  Aidha, masharti makuu kwa kaya zitakazo teuliwa na kupatiwa fedha kwa kipindi chote cha miaka mitatu ya mradi zitalazimika kuzizalisha kwa kujiunga kwenye vikundi vya kuweka na kukopa au kuanzisha biashara ya kujiingizia kipato huku wale watakaoshindwa kutekeleza masharti hayo wataondolewa.

  Katika hatua nyingine timu ya maofisa iliyokuwa ikiendesha zoezi la hojaji ya kuzitambua kaya hizo lilikabilina na changamoto kadhaa ikiwa ni pamaoja na uwelewa mdogo kuwa fedha hizo ni za bure, kuzihusisha Fedha hizo na Asasi maalufu ya(Free Mason) baadhi ya kaya kupatikana maeneo yasiyofikika kwa urahisi asanjari na baadhi ya wananchi kukana kwamba wao si masikini licha ya kutanjwa na wakazi wenzao.

  0 0


   
  Dar es Salaam, 13 April 2015 Finali ya shindano la Airtel Trace Music Stars Afrika lililoshirikisha washiriki kutoka nchi 13 barani Afrika chini ya majaji mahiri akiwemo  Akon, Devyne Stephens na Lynnsha  mwisho mwa wiki hii watashirikiana kumtanga rasmi mshindi wa Airtel Trace Afrika.


  Airtel kupitia taarifa yake iliyotumwa na ofisa uhusiano wake Jane Matinde imesema “Shughuli nzima ya kumtangaza mshindi itaonyeshwa  kupitia chanel ya Trace inayopatikana katika kituo cha DSTV #325  siku ya jumamosi tarehe 18 April 2015

  Shindano hilo kabambe la  Airtel Trace music star lilihusisha washiriki wengi walioshiriki kupitia kupiga simu na kurekodi mojakwa moja ambapo jumla ya simu zaidi ya milioni mbili na laki tatu  za washiriki wote zilipigwa na kufanya namba ya washiriki wa shindano hili kubwa Afrika kuweza kuzidi mashindano ya Ulaya na marekani kama vile ya voice na idols.

  Washiriki 13 kutoka nchi za Afrika waliingia katika kinyanganyiro cha kutafuta mshindi tarehe 28 machi 2015.  Usikose kushuhudia shindano hilo la kusisimua lenye vionjo vya kila aina, mbwembwe na bashasha tele.

  Finali hizi za Airtel Trace Stars zitaonyeshwa siku ya Jumamosi ambapo watazamaji na majaji  watachagua na kutangaza mshindi ambaye atapata dili la kurekodi , kupata mafunzo ya muziki kutoka kwa mwanamuziki nguli wa nchini Marekani lenye thamani ya zaidi ya dola za kimarekani 500,000/=

  Progam hii ya finali itarushwa siku ya Jumamosi ya tarehe 18 April kuanzia saa tatu Usiku na kurudia siku ya Jumapili tarehe 19 Aprili kuanzia saa kumi jioni katika chaneli ya Trace urban.  Kipindi kitadumu kwa muda wa dakika tisini.

  0 0
  0 0

  WA15Mwanafunzi mshiriki wa semina ya kuzuia mimba za utotoni kwa wanafunzi wa shule za sekondari katika Wilaya ya Temeke akiwasilisha majibu ya majadiliano ya kikundi chao katika siku ya kwanza ya semina hiyo.
  WA7Baadhi ya wanafunzi na walimu wa Shule za Sekondari kutoka Wilaya ya Temeke wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi, Afisa Elimu-Sekondari wa Wilaya ya Temeke Ndugu Donald Chavila wakati akifungua semina hiyo inayofanyika Kibasila Sekondari. (PICHA NA JOHN  LUKUWI). 
  WA10Baadhi ya wanafunzi kutoka Shule za Sekondari katika Wilaya ya Temeke wakisikiliza kwa maini baadhi ya mada zilizokuwa zikitolewa wakata wa semina ya kuzuia mimba za utotoni kwa wanafunzi wa Sekondari katika wilaya hiyo. Semina hiyo ya siku 5 inafanyika Kibasila Sekondari na ilifunguliwa rasmi tarehe 13.4.2015.WA11Washiriki wa semina wakiwa wamegawanyika katika vikundi mbalimbali ili kujadili mojawapo ya mada iliyokuwa imetolewa na baadaye kila kundi kuwasilisha kwenye semina hiyo.WA13Washiriki wa semina wakiwa wamegawanyika katika vikundi mbalimbali ili kujadili mojawapo ya mada iliyokuwa imetolewa na baadaye kila kundi kuwasilisha kwenye semina hiyo.

  0 0

  Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Zanzibar Dkt. Andymicheel Grimany akifungua semina ya ushajishaji juu ya usalama wa chakula iliyoandaliwa na Bodi ya chakula na Dawa iliyofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
  7
  Baadhi ya washiriki wa semina ya ushajishaji juu ya usalama wa chakula wakifuatilia mada zilizowakilishwa kwenye semina hiyo.
  6
  Meneja wa Kiwanda cha Maziwa cha Azam Zanzibar Kirtikumar Dave akichangia katika semina ya ushajishaji juu ya usalama wa chakula iliyoandaliwa na Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni.
  5
  Mkuu wa Idara ya Huduma za Maabara Bodi ya chakula, Dawa na Vipodozi Nadir Khamis Hassan akitoa mada katika semina ya ushajishaji juu ya usalama wa chakula katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni.
  4
  Mrajisi wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar Dkt. Burhan Othman Simai akitoa ufafanuzi wa baadhi ya masuala yaliyoulizwa katika semina ya ushajishaji juu ya usalama wa chakula iliyofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni, (kulia) Mwakilishi wa WHO Zanzibar Dkt. Andymicheel Grimany.
  3
  Mshiriki wa semina ya ushajishaji juu ya usalama wa chakula  iliyofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni Saleh Mohd Haji akitoa amchango wake.
  2
  Afisa Mipango  Idara ya Sera na Utafiti katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi Omara Ali Omar akitoa mada ya Usalama wa chakula katika uzalishaji kwa upande wa Mifugo katika Semina ya  siku moja ya ushajishaji juu ya usalama wa chakula iliyoandaliwa na Bodi ya chakula na Dawa Zanzibar iliyofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani.

  ……………………………………………………………………..
  Na Fatma Kassim
  MWAKILISHI wa Shirika la afya ulimwenguni WHO Zanzibar Dk Andymicheel Grimany amesema kuwa maradhi mengi yanayotokea kwa binaadamu chanzo chake ni ukosefu wa  usalama wa chakula.
  Amesema kuwa kunaumuhimu wa kuzingatia uimarishaji wa chakula tokea kikiwa shambani uhifadhi wake hadi kufikia walengwa hakizingatii ubora na usalama wa chakula.
  Hayo ameyaeeleza katika mkutano wa maadhimisho ya siku ya Afya Duniani uliowakusanyisha wadau mbali mbali katika uliofanyika katika Zanzibar Beach Resort ambapo ujumbe wa mwaka huu ni ubora wa usalama wa chakula.
  Alisema kuwa chanzo kikubwa cha maradhi yanayotokana na chakula ni pamoja na Ebola iliyotokea katika nchi za Afrika Magharibi pamoja na miripuko ya maradhi mabali mbali yanayotokea hapa nchini ikiwemo maradhi ya kuharisha.
  Alifahamisha kuwa hivi sasa ulimwenguni kote kunaongozeko kubwa la matatizo  yanayotokana na ukosefu wa ungalizi mzuri wa vyakula vinayotokana na kilimo, Mifugo na hata katika utaarishaji wake na kusababisha maradhi kwa watumiaji.
  Kwa upande wa Mrajis wa Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar Dk Burhan Othman Simai amesema kuwa ni vyema wafanyabiashara hapa nchini kufuata taratibu za kisheria zilizowekwa ili kupunguza ongezeko la matatizo ya kiafya kwa watumiaji wa bidhaa hizo.
  Alisema hivi sasa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya uekezaji wa bidhaa ya mifugo zikiwemo minofu ya kuku ambao baadhi yao hawafati taratibu za uuzaji kwa kuwahifadhi kwenye mafriji na badala yake baadhi yao husambaza kwa kutumia baskeli jambo ambalo linahatarisha afya za wananchi
  Alifahamisha kuwa Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi itaendelea kufanya uchunguzi pamoja na kudhibiti bidhaa zisizofaa kwa matumizi ya mwanadamu sambamba na kuzitaka taasisi zote pamoja na wananchi nchini kujenga ushirikiano kwa lengo la kudhibiti bidhaa zisizofaa.
  Wakitoa mada walufunzi mbali mbali wa mkutano huo walisema kuwa kunachangamoto mbali mbali zinaikabili Bodi hiyo ikiwemo Zanzibar kugeuzwa jaa la bidhaa zisizofaa kwa matumizi ya mwanadamu, ongezeko wa ghala zisizosajiliwa pamoja na uelewa mdogo wa jamii juu ya kazi zinazofanywa na Bodi hiyo.
  Walisema ni jukumu la wafanyabiashara wa chakula kujua sheria mbali mbali zinazosimamia masuala ya chakula sambamba na kutambua kuwa jukumu la usalama wa chakula ni lao.
  Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi ni chombo halali kilicho chini ya Wizara ya Afya na kina mamlaka ya udhibiti wa ubora wa usalama wa Chakula Dawa na Vipodozi pamoja na vifaa Tiba.
  Tangu kuanzishwa kwa Bodi hiyo mwaka 2007 zaidi ya tani 1000 zimeangamizwa na zaidi ya asilimia 80 ya bidhaa ya chakula hutegemewa kutoka nje ya nchi.

  0 0

   Wanafunzi wa Carman Ainsworth High School iliyopo Michigan watembelea ubalozi wa Tanzania Washington DC, na kupata fursa ya kuonana na Mhe balozi Liberata Mulamula.
                        Baadhi ya wanafunzi wakimsikiliza kwa makini Mhe, balozi Leberata Mulamula.
                               Mhe, balozi Liberata Mulamula akitoa historia fupi ya Tanzania.

                        Mhe, balozi Liberata Mulamula akiwashukuru wageni wake kwa kuchagua ubalozi wa Tanzania kama sehemu mojawapo ya ziara yao hapa mjini Washington DC.

  0 0


  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana, kuhusu tume aliyoiunda kwa ajili ya kuchunguza ubovu wa barabara katika wilaya hiyo.
  Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.

  Na Dotto Mwaibale

  MKUU wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda ameunda tume ya wajumbe saba wakiwamo wawili kutoka serikalini kwa ajili ya kuchunguza ubovu wa barabara katika wilaya hiyo.

  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana Makonda amesema amechukua hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wakilalamikia ubovu wa barabara katika wilaya ya Kinondoni kuwa zinajengwa chini ya kiwango.

  Alisema wananchi hao wanasema barabara hizo zinajengwa chini ya kiwango kwani lami inawekwa leo lakini haimalizi miezi sita inabanduka na kuacha mashimo ambayo yamekuwa ni sehemu ya maisha ya kawaida kwa barabara ndani ya wilaya hiyo.

  Makonda alisema katika wilaya hiyo barabara nyingi mitaro yake haipitishi maji kama inavyotakiwa, mitaro mingine imechimbwa mifupi kuliko mahitaji halisi, barabara kujengwa nyembamba kutoka kushoto kwenda kulia bna kuwa ujenzi wa barabara hizo hauendani na kasi ya mahitaji na kukua kwa mji.

  Alisema kutokana na hali hiyo kwa kuwa si mtaalamu wa masuala ya barabara ameamua kuunda tume huru ya wataalamu itakayojumuisha wasanifu, wahandisi, wataalamu wa mikataba, ugavi na manunuzi na watu wengine kutoka vyombo mbalimbali ili wachunguze.

  "Tume hii na vyombo hivyo vingine tumevipatia kazi ya kuchunguza usanifu wa barabara kama unazingatia viwango, taratibu za manunuzi na kutoa tenda kama zinazingatiwa, wakandarasi wetu wazalendo kama wanawajibika ipasavyo au kuna njama yoyote inafanywa ili kuhujumu kazi waliyopewa na kama wahandisi wetu wanatimiza wajibu wao ipasavyo kamtika mchakato mzima wa usanifu na ujenzi ili kuhakikisha ubora wa barabara unafikiwa" alisema Makonda.

  Makonda alisema Tume hiyo itafanyafakazi kwa siku 21 kuanzia kesho Aprili 15 mwaka huu na kukabidhi ripoti yake ofisini kwake mbele ya waandishi wa habari Mei 5 mwaka huu saa 5 asubuhi na kuwa matokea ya ripoti hiyo ndiyo yatakayotoa majibu ya kupanua wigo wa uchunguzi kwenye kandarasi nyingine za ujenzi wa shule za serikali, ofisi za umma za wilaya hiyo.

  Wajumbe wanaounda tume hiyo ni Mhandisi Julius Mamilo ambaye atakuwa mwenyekiti , Mhandisi Ronald Rwakatare (Katibu), John Malisa, Abednego Lyaga, Mhandisi Patrick Balozi na wajumbe wengine wawili kutoka vyombo vingine vya serikali vinavyoshughulikia uchunguzi.
  (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

  0 0
 • 04/14/15--13:30: Article 0


older | 1 | .... | 502 | 503 | (Page 504) | 505 | 506 | .... | 1898 | newer