Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live

HAPPY BIRTHDAY BLOGGER CATHBERT ANGELO KAJUNA

$
0
0
Napenda kumshukuru Mungu kwa kunifikisha leo Aprili 10 siku yangu ya kuzaliwa... Hakika Mungu ni mwema kwa kila jambo. Pia napenda kuishukukuru familia yangu, ndugu jamaa na marafiki kwa kuwa pamoja nami mpaka leo. Asanteni sana.

TPB wazinduwa Tawi jipya Kimara Mwisho Dar es Salaam

$
0
0
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya hafla ya uzinduzi wa tawi dogo la Benki hiyo lililopo Kimara Mwisho jijini Dar es Salaam. Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya hafla ya uzinduzi wa tawi dogo la Benki hiyo lililopo Kimara Mwisho jijini Dar es Salaam.Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Posta Tanzania (TPB), Profesa Lettice Rutashobya (kulia) akimkabidhi kadi ya TPB mteja wa kwanza kuhudumiwa katika tawi jipya dogo la Benki hiyo lililopo Kimara Mwisho jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Posta Tanzania (TPB), Profesa Lettice Rutashobya (kulia) akimkabidhi kadi ya TPB mteja wa kwanza kuhudumiwa katika tawi jipya dogo la Benki hiyo lililopo Kimara Mwisho jijini Dar es Salaam.Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi (kulia) akimpongeza mteja wa kwanza kuhudumiwa katika tawi jipya dogo la Benki hiyo lililopo Kimara Mwisho jijini Dar es Salaam. Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi (kulia) akimpongeza mteja wa kwanza kuhudumiwa katika tawi jipya dogo la Benki hiyo lililopo Kimara Mwisho jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) wakitoa huduma kwa baadhi ya wateja waliofika katika hafla ya uzinduzi wa tawi jipya dogo la Benki hiyo lililopo Kimara Mwisho jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) wakitoa huduma kwa baadhi ya wateja waliofika katika hafla ya uzinduzi wa tawi jipya dogo la Benki hiyo lililopo Kimara Mwisho jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) wakitoa huduma kwa baadhi ya wateja waliofika katika hafla ya uzinduzi wa tawi jipya dogo la Benki hiyo lililopo Kimara Mwisho jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) wakitoa huduma kwa baadhi ya wateja waliofika katika hafla ya uzinduzi wa tawi jipya dogo la Benki hiyo lililopo Kimara Mwisho jijini Dar es Salaam.Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi akisaini katika kitabu cha wageni cha Ofisi ya TPB tawi dogo jipya la Benki hiyo lililopo Kimara Mwisho jijini Dar es Salaam. Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi akisaini katika kitabu cha wageni cha Ofisi ya TPB tawi dogo jipya la Benki hiyo lililopo Kimara Mwisho jijini Dar es Salaam.Meneja Mkuu Utawala na Huduma wa Benki ya Posta Tanzania, Diana Myonga (kulia) akifafanua jambo kwa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi kwenye hafla ya uzinduzi wa Tawi dogo la TPB lililopo Kimara Mwisho jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Teknolojia na Uendeshaji wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Jema Msuya. Meneja Mkuu Utawala na Huduma wa Benki ya Posta Tanzania, Diana Myonga (kulia) akifafanua jambo kwa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi kwenye hafla ya uzinduzi wa Tawi dogo la TPB lililopo Kimara Mwisho jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Teknolojia na Uendeshaji wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Jema Msuya.Baadhi ya wateja wa kwanza wa tawi jipya dogo la TPB lililopo Kimara Mwisho jijini Dar es Salaam wakihudumiwa. Baadhi ya wateja wa kwanza wa tawi jipya dogo la TPB lililopo Kimara Mwisho jijini Dar es Salaam wakihudumiwa.Baadhi ya wateja wa kwanza wa tawi jipya dogo la TPB lililopo Kimara Mwisho jijini Dar es Salaam wakihudumiwa. Baadhi ya wateja wa kwanza wa tawi jipya dogo la TPB lililopo Kimara Mwisho jijini Dar es Salaam wakihudumiwa.Muonekano wa tawi jipya dogo la TPB lililopo Kimara Mwisho jijini Dar es Salaam. Muonekano wa tawi jipya dogo la TPB lililopo Kimara Mwisho jijini Dar es Salaam

MGOMO WA MADEREVA WA VYOMBO VYA USAFIRISHAJI WATIKISA NCHI LEO

$
0
0
Madereva wa Vyombo vya Usafirishaji katika maeneo mbalimbali hapa nchini, leo wameingia katika Mgomo wa kutotoa huduma hiyo, kwa kile kinachoelezwa Madereva hao kutakiwa kurudi vyuoni kwa mafunzo zaidi ya usalama barabarani.

Hali ya mgomo huo, umepelekea adha kubwa kwa abiria wa vyombo hivyo, hasa wale waliokuwa wakielekea mikoani, kwani katika Stendi kuu ya Mabasi ya Ubungo jijini Dar es salaam, hakuna basi hata moja lililoondoka huku daladala nazo zikiwa hazionekani kabisa vituoni.

Uongozi wa Madereva hao umeomba kukutana na Uongozi wa Juu Serikalini ili kulizungumzia swala hilo la kuwataka Madereva hao kurudi mafunzoni, kwani wao wanadai kuwa kazi wazifanyazo si za kudumu na hivyo watakaporudi mafunzoni hali ya maisha yao itatetereka.
Mabasi ya Abiria yaendayo Mikoani yakiwa yameegeshwa tu kwenye maeneo yake katika Kituo kikuu cha Mabasi Ubungo jijini Dar.
Wakina mama hawa wakiwa wamemshikilia Mgonjwa wao waliekuwa wakimsafirisha kwente mkoani, wakiondoka stendi ya kuu ya Mabasi Ubungo baada kukosa usafiri kutokana na mgomo wa vyombo hiyo leo.
Huku Ubungo mambo yako namna hii, ni mwendo wa kupiga mguu tu.
Mijadala ikiendelea kwa wadau mbalimbali wanaofanya shughuli zao katika kituo kikubwa cha Mabasi cha Ubungo jijini Dar.
Mara lori likazuiliwa na watu hawa, wakidai kuwa amepakia abiria hivyo anatakuwa kuwashusha kama anataka kuendelea na safari yake.

HAKUNA HAKI YA MTU KUKATAA KUTII SHERIA

$
0
0
indexNa Masanja Mabula -Pemba .
Rais  wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Haki za watu Mhe Agustino Stephen Ramadhan amesema kuwa hakuna haki ya mtu kukataa kutii Sheria na kuwataka wananchi  kujiepusha na vitendo vya  kujichukulia sheria mikononi mwao .

Amesema kuwa katika nchi yenye misingi ya Utawala Bora jamii inapaswa kuiachia mahakama kutoa tamko juu ya mambo ambayo  yanakinzana na jamii kwa lengo la kuhakikisha kwamba jamii inapata haki kwa mujibu wa sheria .

Akizungumza kwenye  mahafali ya tatu ya wasaidizi wa sheria wa majimbo  Zanzibar yaliyofanyika kwenye ukumbi wa ZSSF nje kidogo ya Mji wa Chake Chake , amesema kuwa mahakama ndio chombo ambacho kinatafsiri  sheria na kutoa haki .

Rais huyo ambaye pia Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu Tanzania ametumia fursa hiyo kuwataka wasaidizi wa Sheria kuwahudumia wananchi wanyonge kuweza kupata haki zao na kujiepusha kutumia elimu waliyoipata kwa maslahi yao binafsi .

“Hakuna uhuru wa mtu kukataa kutii sheria , hivyo jamii mnakiwa kutojichukulia sheria mikononi mwao bali waiache mahakama kutoa tamko juu ya masuala yanayoikinza jamii kwa lengo la kulinda amani ” alisisitiza .
Aidha amepongeza juhudi zinazochcukuliwa na kituo cha sheria  Zanzibar kwani kimeweza kuleta mawimbi ya matumaini kwa jamii na kubomoa ukuta wa maovu , wanyinge pamoja na maonevu wanayofanyiwa wananchi hasa maskini.

Amefahamisha kwamba katika misingi ya demokrasia na utawala sheria uhuru wa maoni ya wananchi unazingatiwa na kuongeza kwamba taasisi binafsi zinaweza kuchangia kuongezeka  kwa uhuru wa wananchi .

“Kituo cha huduma za sheria Zanzibar imekuwa ni moja ya taasisi ambazo zinachangia kukua kwa uhuru wa maoni wa  wananchi hasa katika nchi zinazofuata utawala wa Sheria ” aliongeza Jaji Agustino Ramadhan .
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini wa kituo cha huduma za sheria Zanzibar Pr Chris Maina Pita amesema kuwa kituo hicho kimekuwa mstari wa mbele kuwaelimisha wananchi elimu ya Sheria ili waweze kuisaidia jamii yao inayowazunguka .

Amesema kuwa kituo hicho kimeanda motisha kwa wasaidizi wa sheria wanaofanya vizuri katika masomo yao na ambao wanataka kujiendeleza zaidi kusoma Elimu wa Sheria kwamba kinadhamini gharama za masomo wa wanafunzi hao katika chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali .
“Kituo kimeandaa mfuko kwa ajili ya wanasaidizi wa Sheria ambao wanataka kujiendeleza zaidi kielimu katika vyuo vikuu , chuo kinagharamia gharama za masomo kwa wanafunzi hao , na tayari wafadhili wameanza kuingi a fedha katika mfuko huo ” alifahamisha .

Mapema Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Harusi Miraji Mpatani amesema kuwa tayari kituo hicho kimetoa wasaidizi wa Sheria 197 huku wengine 82 wakiwa wanaendelea na masomo yao .
Mpatani ameeleza kuwa kituo kinaridhiwa na utendaji wa kazi wa wasaidizi hao wa Sheria wa Majimbo Zanzibar kwani wameweza kusaidia wananchi kupata haki .

OFISI ZA TAASISI ZA SERIKALI KUFUNGIWA LUKU

$
0
0
ni2
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kulia) akimpokea Balozi wa Marekani Nchini, Mark Childress (kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za Wizara ya Nishati na Madini.
………………………………………………………………………………………………..
Na Greyson Mwase, Dar es Salaam 
Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene amesema kuwa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) lina mpango wa kufunga mita za LUKU katika ofisi za taasisi zote za serikali kama moja ya mikakati yake katika ukusanyaji wa mapato.
Simbachawene aliyasema wakati wa kikao chake na Balozi wa Marekani Nchini, Mark Childress aliyemtembelea ofisini kwake lengo likiwa ni kujadili hatua iliyofikiwa ya utekelezaji wa mpango wa kuboresha sekta ndogo ya umeme na miradi ya Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC).Alisema kuwa kama mkakati wa kuhakikisha kuwa shirika la Tanesco halijiendeshi kihasara, shirika hilo limeweka mkakati wa ukusanyaji wa mapato, moja ya mkakati ikiwa ni kufunga mita za Luku kwenye Taasisi za Serikali, Binafsi na wateja wa kawaida.
“Tunaamini shirika likitekeleza mkakati huo, litapunguza hasara na kuwa tegemezi kwenye serikali kupitia ruzuku.” Alisema Simbachawene. Alisema pia Tanesco itaingia mkataba na Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco) kwa ajili ya ukusanyaji wa madeni yake ya nyuma na kuendelea kulipia ankara zake za kila mwezi. Akizungumzia hatua iliyofikiwa ya utekelezaji wa miradi ya MCC Awamu ya Pili , Simbachawene alisema kuwa kazi ya uandaaji wa miradi imekamilika na kuwasilishwa katika Bodi ya MCC nchini Marekani kwa ajili ya kupata idhini ya kufadhili miradi
Alitaja mikoa itakayofaidika na miradi ya MCC Awamu ya Pili kuwa ni pamoja na Pwani, Tabora, Shinyanga na Morogoro pamoja na kuboresha utendaji kazi wa Tanesco. 
Wakati huohuo Balozi wa Marekani Nchini, Mark Childress alisema kuwa amefurahishwa na hatua ya utekelezaji wa miradi ya MCC Awamu ya Pili na kusisitiza kuwa Marekani ipo tayari kushirikiana na nchi ya Tanzania kupitia miradi ya umeme ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata umeme wa uhakika ambao una mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

RAIS KIKWETE APOKEA RIPOTI YA OPERESHENI TOKOMEZA

$
0
0

WACHEZAJI WA BARCELONA WAMTEMBELEA RAIS KIKWETE IKULU

UN. TAASISI IMARA KATIKA UTATUZI WA MIGOGORO

$
0
0
Kutoka kushoto ni Reginald Munisi, Mwenyekiti, United Nations Association of Tazania, Mr. Alvaro Rodriguez, Mratibu Mkazi, Umoja wa Mataifa Tanzania, Balozi Dr. Agustine Mahiga, Balozi Mstaafu wa Tazania Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wakiwa katika Maadhimisho ya Miaka 50 Taasisi ya Umoja wa Matifa (UNA) pamoja na maadhimisho ya miaka 70 ya umoja wa Mataifa (UN) yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Reginald Munisi, Mwenyekiti wa UNA Tanzania akitoa maneno ya ufunguzi katika mkutano mkuu wa UNA Tanzania.
Washiriki katika mkutano mkuu wa UNA Tanzania.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

UMOJA wa Mataifa (UN) ni taasisi imara katika kusimamia maendeleo ya wananchi pamoja na kutatua migogoro mbalimbali ya nchi ya vita kwa nchi wanachama wa umoja huo.

Hayo ameyasema leo Balozi Agustine Mahija wakati wa Maadhimisho ya Miaka 50 Taasisi ya Umoja wa Matifa (UNA) pamoja na maadhimisho ya miaka 70 ya umoja wa Mataifa (UN) iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mahija alisema Umoja wa Mataifa (UN) umekuwa mstari wa mbele katika kutatua migogoro ikiwa ni kufanya wananchi waishi maisha ya amani kwa kuanzisha baraza la usalama wa Umoja wa Matiafa ambalo limekuwa likishughulikia migogoro mbalimbali.

Amesema UN imeweza kuweka malengo mbalimbali ya kiuchumi kwa nchi 195 zilizo katika umoja huo katika kuweza kuondokana na umasikini kwa kubuni miradi ambayo yameleta tija kwa mataifa mbalimbali.

Naye Mwenyekiti waTaasisi ya Umoja wa Mataifa UNA Tanzania. Reginald Munisi amesema katika kuelekea uchaguzi vyombo vinavyoshughulikia ulinzi visijihusishe na siasa ili wananchi waweze bkupiga kura kwa amani.
Munisi amesema vyombo vya ulinzi vikijihusisha na siasa wananchi watashindwa kushirika katika uchaguzi wa kuchagua viongozi wao ambao ndio wanawategemea katika maendeleo ya nchi.

Aidha alisema UNA Tanzania itatoa eli kwa vyombo vya ulinzi katika kuelekea uchaguzi ikiwa ni lengo la kuwafanya wananchi waweze kupiga kura kwa amini na kuweza kuwapata viongozi wao.
Mr. Alvaro Rodriguez, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa, na Mgeni Rasmi, Tanzania akifungua mkutano mkuu wa UNA Tanzania.
 Washiriki katika picha ya pamoja.
 Balozi Dr. Agustine Mahiga akizungumza na waandiahi wa habari.
Reginald Munisi, Mwenyekiti wa UNA Tanzania, akizungumza na waandishi wa habari.
Mr. Alvaro Rodriguez, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mgeni Rasmi akizindua kipengele cha "Ask the UN RC" katika wavuti ya UNA Tanzania - www.una.or.tz
---


Polisi watumia mabomu ya machozi kutuliza vurugu Iringa mjini

$
0
0
Mpita njia  eneo la Ipogolo akipiga  picha kwa simu moto  uliokuwa  ukiwaka barabarani.

Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia FFU mchana huu wametumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi waliokuwa wameziba barabara ya Iringa -Kilolo kwa kuchoma mataili

Wananchi hao wamefikia uamuzi huo Baada ya mtoto kugongwa na gari kwa zaidi ya saa Moja bila maiti kutolewa.

Kutokana na hali hiyo wananchi hao wa Eneo la Ipogolo walilazimika kuchoma moto barabara hiyo huku waliochoma mataili Kabla ya Polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya
 Na  MatukiodaimaBLOG

VURUGU  kubwa  zimetokea leo   katika  eneo la Ipogolo  mjini Iringa na  kupelekea askari wa   kikosi cha kutuliza  ghasia  (FFU)  kutumia  mabomu ya machozi  kuthibiti vurugu    baada ya mtoto wa  miaka kata 6 kugongwa na gari  wakati  akifanya biashara ya  kuuza mbogo mboga .


  Wananchi wanaosadikika  kuwa na  hasira kali  walianza kuwashambulia  askari  polisi waliofika kuchukua mwili huo kwa mawe  kwa madai ya  kuchelewa  kufika  eneo la  tukio.

Wakizungumzia  tukio   hilo kwa mwandishi wa habari hizi  baadhi ya  wananchi   walisema  kuwa  mtoto   huyo  aligongwa  majira ya saa 7 mchana na zaidi ya saa  moja baada ya  kutoa taarifa  polisi  ndipo  walipofika  eneo la  tukio jambo lililowakwaza  wananchi hao .


Walisema  kuwa  mbali ya  polisi  hao  kufika  pia tayari  baadhi ya askari  waliopo eneo hilo la stendi kuu ya Ipogolo  kwa  kushirikiana na  wananchi  walifanikiwa  kulikamata  gari  ambalo  lilisababisha ajali  hiyo .


Alisema  Neema Sanga  kuwa wakati  tukio  la kugongwa  mtoto  huyo  likitokea  alikuwa jirani na eneo hilo katika  msiba  na kuwa  wakati  akiwa ameingia ndani ya nyumba  hiyo  yenye msiba  kusaidia  kugawa  chakula ghafla  alipata taarifa  kuwa wananchi  wameanza vurugu kwa  kuchoma  moto matali katika barabara  hiyo  kuu ya  Iringa- Kilolo.

Hata   hivyo  alisema  kuwa  tukio  hilo  lilichukua  zaidi ya dakika 45  polisi  hao wa FFU  kufika na kuanza  kutuliza  vurugu  hizo kwa  kupiga mabomu ya machozi  kuwatawanya  wananchi zaidi ya 500  waliokuwa  wamekusanyika eneo hilo kuzuia  magari  kuendelea kupita katika  barabara  hiyo  huku  baadhi yao  wakitaka  kufunga  barabara  kuu ya  Mbeya  - Iringa ambayo haihusiki ka bisa na   eneo  lililotokea  tukio hilo.

" Ni  kweli  mtoto kagongwa na gari na kufa  tukio ambalo ni kusikitisha sana na  polisi baada ya  kupigiwa simu  wamefika  eneo la  tukio na  kuchukua maiti ya  mtoto  huyo lakini  tunajiuliza kwanini  vijana hao kuanza  kuwapiga mawe  polisi na kufanya  vurugu  wakati gari  lililogonga mtoto huyo  likiwa  limekamatwa .."  alihoji Bi  sanga

 Kuwa kwa  upande  wake hakuona  sababu za  polisi  kupigwa  wala  wananchi hao kuchoma moto  barabara wakati ajali  hiyo kama ajali nyingine na tayari  gari  lililosababisha ajali  likiwa  limekamatwa .

Bi  Sanga  alisema  wakati  mwingine  polisi  wanalalamikiwa kuwa wanatumia  nguvu  zaidi  ila kwa  tukio   hilo lawama  zake anazipeleka kwa  wananchi wenzake ambao walionyesha  kufanya vurugu kwa kuchomo moto  barabara  hiyo ya lami na   kupiga  polisi huku  wakitambua  wazi  polisi si  waliosababisha ajali  hiyo.

 Huku kwa  upande  wake mmoja  John Kalinga  akiomba  serikali kupitia  wizara ya miundo  mbinu  kuangalia   uwezekano  wa  kuweka matuta katika eneo hilo kwa madai kuwa  hii ni ajali ya  pili  kutokea na kusababisha  vifo  toka  eneo hilo  lilipowekwa  lami .

Mwandishi  wa habari hizi  alishuhudia baadhi ya  vijana  wakikimbilia kujificha katika nyumba  moja  iliyopo eneo hilo ambayo  ilikuwa na msiba   huku baadhi yao  wakijifungia  katika maduka  na bar  zilizopo eneo hilo kabla ya  polisi  kuwafuata na  kuwakamata   huko  walikojificha na  kuwaacha   wale  waliokimbilia msibani .

Kamanda  wa  polisi  wa  mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi hakuweza  kupatikana  kuzungumzia tukio  hilo  huku idadi ya vijana  waliokamatwa  kwa tuhuma za  kuhusika katika  vurugu  hizo zaidi ya 20  walionekana  wakipagiwa katika magari  ya  polisi.

Askari  wa FFU wakiwa katika msako  wa  kuwasaka  waliohusika na  vurugu hizo eneo la Ipogolo  mjini Iringa
Moshi wa  bomu la machozi  ukiwa angani
Moshi  ukiwa  umetanda  angani
Bomo  la machozi  likilipuka  angani 
Askari  wa zimamoto  wakizima moto katikati ya  barabara  ya  Iringa - Kilolo  leo
Askari  wa zimamoto  wakifungua  barabara
Askari  wa FFU  wakiwa kazini
Askari  wa Zimamoto akitoa  taili  lililokuwa  likiwaka barabarani
Wananchi  waliokuwa  msibani  wakishuhudia msako  mkali wa  polisi
Barabara  ikiwa  imefungwa
Askari  wa jeshi la  Zimamoto na  uokoaji mjini Iringa  akisaidia kumvusha  mzee  ambae  alikuwa akikimbia mabomu na  kujificha mtaroni
Mzee  huyo  akimpongeza  askari kwa  wema  wake
Baadhi ya  watuhumiwa wa  vurugu hizo  wakipakiwa katika gari la  FFU

Magari ya  polisi  yakisafirisha  watuhumiwa wa vurugu kwenda  kituo  cha polisi kati
Wananchi  wakiwa katika  vurugu  hizo  huku baadhi yao  wakishuhudia

Mkurugenzi wa Mwananchi Communications Limited Francis Nanai azindua asasi ya TAYL

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited, Francis Nanai akizungumza wakati akizindua asasi ya kuendeleza vijana katika masuala ya uongozi ijulikanayo kwa jina la Tanzania- Asia Young Leaders (TAYL).
Mjumbe wa Kamati Kuu na mmoja wa muasisi wa asasi ya TAYL, Ismail Biro akizungumzia historia na malengo ya asasi hiyo wakati wa uzinduzi uliofanyika kwenye hotel ya New Africa jijini.
Wajumbe na wanachama wa asasi hiyo walifuatilia uzinduzi. 

MBOWE AKABIDHI AMBULANCE MBILI KWA HOSPITALI YA WILAYA YA HAI NA HOSPITALI YA MACHAME.

$
0
0
Magari mawili ya kubebea wagonjwa(Ambulance) yaliyotolewa na Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe yakiwasili katika viwanja vya soko la Kuni kwa ajili ya kukabidhiwa kwa viongozi wa hosptali ya wilaya ya Hai pamoja na hosptali ya Machame inayosimamiwa na kanisa la KKKT.
Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe akiwa amembeba mtoto mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Kuni na kulakiwa na wananchi katika jimbo hilo.
Magari ya wagonjwa yaliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Hai kwa ajili ya wagonjwa jimboni humo.
Mbunge Mbowe akiwa amembeba moja ya watoto waliofika uwanjani hapo kwa ajili ya kushuhudia msaada wa magari ya wagonjwa yaliyotolewa na mbunge huyo kwa watu wa jimbo la Hai.
Muonekano wa ndani wa magari hayo ya kubebea wagonjwa .
Baadhi ya viongozi mbalimbali waliohudhuria shighuli ya makabidhiano iliyofanyika katika uwanja wa Kuni ,Bomang'ombe wilayani Hai.
Wananchi wakiwa wamezingira magari hayo wakiyatizama kwa karibu.
Mbunge wa jimbo la Hai ,akiuzungumza juu ya msaada huo kwa watu wa jimbo la Hai.
Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe akikabidhi nyaraka mbalimbali za magari hayo kwa Baba Mchungaji Asanterabi Swai ambaye pia ni mkuu wa jimbo kwa niaba ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT).
Mmoja wa viongozi wa Machame Hosptal ,Swai akifurahia msaada wa gari hilo la wagonjwa kwa hosptali yake.
Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe akikabidhi funguo wa gari kwa mganga mkuu wa wilaya ya Hai,Dkt Paul Chawote ,msada uliotolewa kwa ajili ya hosptali ya wilaya ya Hai.
Watumishi wa hosptali ya wilaya ya Hai,wakiondoka katika viwanja hivyo mara baada ya kukabidhiwa gari hilo.
Wananchi wakifurahia msaada huo.
Baadhi ya wananchi waliofika kushuhudia makabidhiano ya msaada huo wa magari ya kubebea wagonjwa.
Mbunge wa Jimbo la Hai ,Freeeman Mbowe akizungumza na wananchi mara baada ya kukabidhi msaada wa magari mawili ya kubebea wagonjwa.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

IMETOSHA yaendeleza mkakati wake kimataifa kusafisha jina la nchi

$
0
0
Mkakati wa kutokomeza unyanyapaa na mauaji ya watu wenye ualbino nchini, uitwao IMETOSHA, jana ulianza rasmi kujitokeza kimataifa baada ya kushiriki katika pambano la kimataifa la kirafiki kati ya nyota wa zamani wa Barcelona na Veterani wa Afrika Mashariki.

Katika mpambano huo wa kimataifa uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mkangara, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadick na maafisa kutoka katika mkakati huo walipata nafasi ya kuongea na wachezaji hao nyota wa Barcelona kuhusiana na dhana iliyoko katika nchi za nje ambako inaaminika Tanzania wanauana wenyewe kwa wenyewe kutokana na imani za kishirikina.
Akiongea baada ya mpambano huo ambapo Barcelona waliibuka washindi, Balozi na muasisi wa mkakati huo unaoelekea na sura ya kizalendo na kitaifa, Bw. Henry Mdimu alisema kulikuwa na haja wachezaji hawa warudi na ujumbe kwao wenye majibu ya maswali wanayojiuliza kuhusiana na mauaji ya albino na kukosa majibu.

"Maneno haya ya kwamba sisi tunauana kwa imani za kishirikina, ingawa matukio mengi yapo kanda ya Ziwa lakini nchi nzima inachafuka kwa hiyo haja ya kusafisha jina la nchi kwa mataifa ya nje ipo na sisi IMETOSHA tumeamua kuchukua jukumu", alisema Balozi huyo ambaye pia ana ualbino.

Mdimu alibainisha kwamba katika mkakati wa kimataifa wameanza kwa kuanzisha tovuti (imetosha.or.tz) ambayo itakuwa ikionesha matukio mbali mbali yanayopinga mauaji na unyanyapaa ili wanaoamini vingine waone kwamba unyanyapaa na mauaji kwa watu wenye ualbino si kitu ambacho watanzania kama taifa wanakifurahia.

Balozi huyo pia alitoa wito kwa kila mtanzania kuuunga mkono mkakati wa IMETOSHA ili katika miaka 20 ijayo  kizazi kijacho kiwe na jamii yenye watu wenye ualbino wanaoishi kwa amani katika nchi yao.
Wachezaji wa zamani wa timu ya Barcelona ya Hispania wakiongozwa na Patrick Kluivert (aliebeba mtoto) wakiingia uwanjani tayari kwa kukipiga na timu ya Tanzania Veterans katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. hadi mwisho wa mchezo, Barcelona ya Hispania ilishinda bao 2-1.
Mchezaji wa zamani wa timu ya Barcelona ya Hispania, Patrick Kluivert akifurahia jambo na Mtoto Sharifa mwenye Ualbino kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Tanzania Veterans uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. 
 
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mkangara (wa pili kulia) akizungumza jambo na Mchezaji wa zamani wa timu ya Barcelona ya Hispania, Patrick Kluivert wakati akiwasalimia wachezaji hao kabla ya kuanza kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Tanzania Veterans, uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jana.Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadick.
Sehemu ya Wachezaji wa timu ya Tanzania Veterans na Barcelona wakiwa kwenye picha ya pamoja na Watoto wenye Ualbino mbele ya Bango la Mkakati wa kutokomeza unyanyapaa na mauaji ya watu wenye ualbino nchini, uitwao IMETOSHA.Habari/Picha na Othman Michuzi

MBIO ZA KIMATAIFA ZA NGORONGORO MARATHONI SASA KUFANYIKA APRILI 18 MWAKA HUU.

$
0
0
Waandaaji wa mbio za kimataifa za Ngorongoro Maratahoni katika mkutano na wanahabari kuzungumzia maandalizi ya mwisho ya mbio hizo zinazotarajia kufanyika Aprili 18 mwaka huu ,Karatu mkoani Arusha.
Mkurugenzi wa Zara Tanzania Adventure na Zara Charity,Zainab Ansel akizungumza na wanahabari kuhusu maandalizi ya mbio hizo ambazo zinadhaminiwa na Shirika lisilo la kiserikali la Zara Charity .

Mratibu wa Mbio za Kilimanjaro Marathoni Meta Peter akizungumzuia wanariadha wa Tanzania ambao wanartarajia kushiriki Mbio hizo huku akisema mbio za mwaka huu zitashirikisha wanariadha walioshiriki mbio za dunia za Nyika mwaka huu watakao toana jasho na wakimbiaji kutoka nchini Kenya,Uganda na Malawi.
Muongozaji wa Mbio hizo kutoka kampuni ya Zara Tour ,Frances Kilawe akizungumza historia ya Mbio hizo.
Mwakilishi wa shirika lisilo la kiserikali la Zara Charity Datus Mmary akizungumzia lengo la mbo hizo ambao awali ilikuwa ni kuchangia katika kutokomeza Marelia na mbio za mwaka huu zitakuwa ni kwa ajili ya kuchangia elimu hasa kwa watoto wa jamii ya wafugaji.
Mwakilishi wa kampuni ya Bonite Bottlers ,Leonard Makule akizungumzia juu ya udhamini wa kampuni hiyo katika mbio za kimataifa za Ngorongoro Marathoni 2015.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

ZIARA YA CHAMA CHA ACT-WAZALENDO NDANI YA NYANDA ZA JUU KUSINI

$
0
0
 Viongozi wa Chama cha ACT –Wazalendo wakiangalia mazao ya wakulima waKijiji cha Mkongotema wilayani Songea vijijini jimbo la Peramiho jana
aliposimamishwa kijijini hapo ili afungue tawi la chama hicho jana.
wakazi wa mji wa Makambako mkoani Njombe wakifuatilia yaliyokuwa yakjiri kwenye mkutano huo wa hadhara jana, wakati wa ziara ya chama hicho inayoendelea mikoa ya nyanda za juu kusini.
 Askari wa jeshi la polisi wakiimarisha ulinzi kwenye mkutano wa chama
cha ACT-Wazalendo mjini Njombe jana.
 Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Samson Mwigamba akiwahutubia wakazi wa mji wa Makambako mkoani Njombe jana, wakati wa ziara ya chama hicho inayoendelea mikoa ya nyanda za juu kusini.
 Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa Njombe wakifuatilia
kwa makini huku wakinyeshewa na mvua.
  Kiongozi wa Chama cha Alliance For Change and Transparency (ACT-Wazalendo) Zitto Kabwe, akiwahutubia wakazi wa mji wa Makambako mkoani Njombe jana, wakati wa ziara ya chama hicho inayoendelea mikoa ya nyanda za juu kusini.
   Kiongozi wa Chama cha Alliance For Change and Transparency (ACT-Wazalendo) Zitto Kabwe, akisalimiana na Wananchi mara baada ya kumaliza wahutubia wakazi wa mji wa Makambako mkoani Njombe jana, wakati wa ziara ya chama hicho inayoendelea mikoa ya nyanda za juu kusini.
   Kiongozi wa Chama cha Alliance For Change and Transparency (ACT-Wazalendo) Zitto Kabwe, akiondoka mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara ndani ya mji wa Makambako mkoani Njombe jana, wakati wa ziara ya chama hicho inayoendelea mikoa ya nyanda za juu kusini.
  Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Samson Mwigamba akiwahutubia wakazi wa mji wa Makambako mkoani Njombe jana, wakati wa ziara ya chama hicho inayoendelea mikoa ya nyanda za juu kusini.
 Kiongozi wa Chama cha Alliance For Change and Transparency
(ACT-Wazalendo) Zitto Kabwe, akiwahutubia wakazi wa mji wa Njombe huku akinyeshewa na mvua mjni humo jana ambapo wakazi waliojitokeza
walikubali kulowa ili kumsikiliza.



Rais Jakaya Kikwete ametakiwa kuitisha Bunge Maalum haraka
iwezekanavyo ili ili liweze kufanya marekesho madogo ya katika ili
kuruhusu uchaguzi ufanyike kwa uhuru na haki.

Kauli hiyo imetolewa na CHAMA cha Alliance For Change and Transparency
(ACT-Wazalendo), wakati akizungumza kwa nyakati tofauti Mkoani Njombe
na Mji Mdogo wa Makambako wakati wa ziara ya chama hicho ya kuimarisha
chama hicho mikoani.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo,
Anna Mghwira,  alisema sasa umefika wakati ni lazima nchi iwe huru kwa
kuwa na misingi imara itakayoimarisha demokrasia nchini.
“Rais aitishe Bunge maalumu ili kufanya marekebisho madogo ya Katiba
kuruhusu uchaguzi huru na wa haki lakini pia Wajumbe wa Tume waombe
kazi na wawe wataalamu.

“Kwa nini ACT tunashauri kuitwa Bunge Maalumu ni kutokana na uhai wa
Bunge la 10 umebaikisha mkutano mmoja kabla ya kuvunjwa.
“… hivyo Katibu wa Bunge atangaze nafasi za wajumbe wa Tume, kamati ya
Bunge ya Katiba Sheria na Utawala itafanya mahojiano ya wazi na kupata
majina 22 yatakayopelekwa bungeni,” alisema Anna

Alisema baada ya kukamilka kwa mchakato huo huo, Bunge litapiga kura
kuchagua watu 11 ambao majina yao watapelekwa kwa Rais ambaye naye
atawatangaza kuwa makamishna wa Tume huru ya uchaguzi pamoja na
kumteua mwenyekiti kutoka miongoni mwa makamishna hao waliopitishwa na Bunge.

Alisema kutokana na hali hiyo ili kuweza kuwa na tume huru ya
Uchaguzi, Tanzania inaweza kutumia mfumo uliotumiwa na nchi ya
Msumbiji ambayo kila chama kinateua mwakilishi au kufuata utaratibu wa
kutangaza majina kupitia Bunge.

“Kama tukifanikiwa kupata tume huru ni wazi mwaka huu tutakuwa na na
Uchaguzi huru na haki kuliko miaka yote iliyopita,” alisema.

Kwa upande wake Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, alisema
kuporomoka kwa maadili ya Taifa kutokana na kukosekana na viongozi
wanaipinga rushwa kwa vitendo kama ilivyokuwa ikifanywa na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Moringe Sokoine.

Kutokana na kukosekana kwa uadilifu kwa viongozi ni wazi sasa Taifa
linashindwa kusukumwa na viongozi waliopo Serikalini na badala yake
wanaimba uadilifu huku wakishindwa kutekeleza kwa vitendo.
“Kesho nchi inakumbuka kifo cha Sokoine, ambaye alifariki Aprili 12,
mwaka 1984 yaani kesho (leo) lakini kifo chake ni wazi kwetu
 
ACT-Wazalendo tunamkumbuka kwa uwajibikaji wake kwa vitendo.
“… leo nchi inayumba ufisadi kila kukicha umekuwa ukitamalaki  jambo
ambalo lilipigwa na Sokoine kwa kuikata rushwa na hata kupinga uhujumu
uchumi kwa makusudi nab ado nchi ilisimama katika uadilifu kama
tunavyoamini ACT,” alisema

Alisema kama Sokoine angakuwa hai hakuna kiongozi wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), ambaye angetembea barabarani na kufanya wanayofanyika
sasa.
 
Azimio la Songea
Alisema akiwa Mbunge aliwasilisha hoja mbalimbali ikiwemo utekelezaji
wa azimio la Songea ambalo lilitaka uwazi na wajibikaji kwa Serikali.
“Nilipokuwa bungeni nilisema kuwa mikataba yote ni lazima iwe wazi
lakini nilikosa kuungwa mkono na wabunge wenzangu na si hilo tu
nilisema mishahara ya ya wabunge ikatwe kodi pia sikuungwa mkono je
kisa langu ni nini.

“Tulishindwa kutekeleza suala la mikataba ya madini ambapo leo hii
wawekezaji wananufaika na madini lakini wananchi wakibaki kuwa
watazamaji jambo hili si jema. Nayi hapa Njombe mna madini  mengi
mengi  kule kwa rafiki yangu Filikunjombe,” alisema.

Zitto alisema si kazi yake kutoa matusi kwani hatua yake ya kuhamia
chama kipya cha ACT-Wazalendo, kusiibue malumbano ila waachiwe
Watanzania ndio waamuzi wa “Leo tumewaleta chama mbacho hamtojutia kwa kuunga mkono kama ikitokea kuwaambia tunakwenda bungeni hatuchukui posho basi hatuchukui kweli
kuliko ilivyo sasa,” alisema

MTANDAO WA KUTETEA HAKI ZA BINADAMU WAHAMASISHA AMANI KABLA YA UCHAGUZI MKUU

$
0
0
SAM_1708
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Husna Mwilima aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Arusha, Daudi Ntibenda,akifungua mkutano wa kujadili masuala ya ulinzi na usalama kuelekea uchaguzi mkuu, ulioandaliwa na mtandao wa utetezi wa haki za binadamu uliofanyika jijini Arusha(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
SAM_1679 
Onesmo Ole Ngulumwa, Mratibu wa Mtandao wa Kutetea Haki za binadamu akizungumza katika mkutano huo wa kujadili masuala ya ulinzi na usalama kuelekea uchaguzi mkuu, ulioandaliwa na mtandao wa utetezi wa haki za binadamu,kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Husna Mwilima aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Arusha, Daudi Ntibenda, kushoto Mwakilishi kutoka taasisi ya kuhamasisha masuala ya amani nchini Marekani, Steve Hege 
SAM_1695 Mwakilishi kutoka taasisi ya kuhamasisha masuala ya amani nchini Marekani, Steve Hege akizungumza katika mkutano huo.

Waandishi wa habari hapa Nchini wametakiwa kuwaelimisha jamii juu ya umuhimu wa amani katika nchi ya Tanzania tunapoelekea uchaguzi mkuu kwa kuandika na kutangaza amani hali itakayosaidia uchaguzi kufanyika kwa amani

Akizungumza katika mkutano wa siku mbili wa kujadili masuala ya ulinzi na usalama kuelekea uchaguzi mkuu,uliofanyika jijini Arusha mwisho mwa wiki, ulioandaliwa na mtandao wa utetezi wa haki za binadamu. Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoa Arusha Husna Mwilima alisema kuwa uvunjifu wa amani una madhara makubwa sana katika nchi

Alisema kuwa vyombo vya habari vinajukumu kubwa la kuelimisha umma madhara ya vita hasa tunapoelekea uchanguzi mkuuu wa Rais,wabunge na madiwani,huku akitaka Tanzania kuiga mfano wa Kenya ambapo vyombo vya habari vya nchi hiyo vilikuwa vikitangaza na kuandika amani kipindi cha uchaguzi

Mwilima amewaomba viongozi wa vyama vya siasa, dini na taasisi zisizo za kiserikali kushirikiana kueleza wafuasi wao juu ya umuhimu wa kutunza amani wakati wa uchaguzi mkuu.


Kwa upande wake Mratibu wa Mtandao wa Kutetea Haki za binadamu Onesmo Ole Ngulumwa alisema kuwa marekebisho ya baadhi ya mambo kabla ya uchaguzi mkuu ni muhimu ili kufanyika uchaguzi salama na yenye kujali demokrasia  Pia aliongeza kuwa kwa kuwepo kwa amani itasaidia sana wananchi kupiga kura katika hali ya kiusalama zaidi.



SAM_1686

Wadau kutoka Taasisi za kiraia 
SAM_1681
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha, Onesmo Ole Nangole kulia akifatilia mkutano huo
SAM_1709
Amani Golugwa mwenyekiti  wa CHADEMA mkoa wa Arusha akifatilia mkutano kwa umakini wakati mgeni rasmi akizungumza katika  mkutano huo
SAM_1685
Kiongozi wa dini akiwa anafatilia mada SAM_1683
Kiongozi wa dini akiwa anafatilia mada
SAM_1715
Picha ya pamoja
SAM_1719
Wadau wakipiga picha ya pamojana mgeni rasmi.

AJALI TENA:ajali ya basi la abiria na lori la Fuso Ruaha Mbuyuni leo,wengi wadaiwa kupoteza maisha.

$
0
0
Habari zilizotufikia punde zinaeleza kuwa watu kadhaa ambao idadi yao bado haijafahamika, wanasemekana wamepoteza maisha baada ya basi la abiria liitwalo Nganga linalofanya safari zake kati ya Iringa na Kilombero kugongana uso kwa  uso na lori aina ya Fuso na kisha magari hayo kuteketea kwa moto  maeneo ya milimani kilomita  kadhaa kutoka Ruaha Mbuyuni kuelekea Morogoro, majira ya saa mbili asubuhi leo. Pichani ni basi hilo la Nganga wakati na bada ya kuteketea kwa moto. Tunaendelea kufuatilia taarifa hizi na tutazileta mara zitapopatikana. 

WATANZANIA WAISHIO NJE KUTOPIGA KURA OKTOBA - PINDA

$
0
0
*Waziri Mkuu aomba Watanzania waiombee nchi yao

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Watanzania waishio ughaibuni hawataweza kupiga kura wakiwa nje ya nchi kwenye uchaguzi wa Oktoba mwaka huu, kwa sababu kuna mambo kadhaa ambayo Serikali inabidi iyatekeleze kabla ya zoezi hilo kufanyika.

Ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumamosi, Aprili 11, 2015) wakati akizungumza na baadhi ya Watanzania waishio Uingereza kwenye makazi ya Balozi wa Tanzania nchini humo, Balozi Peter Kallaghe, yaliyoko Highgate, Kaskazini mwa Jiji la London.

Akizungumza na Watanzania hao ambao baadhi yao walitoka miji ya Leicester na Manchester, Waziri Mkuu alisema mambo makuu ambayo yanahitaji kuzingatiwa kabla hawajaweza kupiga kura ni pamoja na marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi Na. 1 ya mwaka 1985 pamoja na uandikishwaji wa Watanzania wana-Diaspora kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

"Najua suala kubwa ambalo mnatamani kulisikia ni hili la Watanzania kuweza kupiga kura kutokea huku mliko. Hili inawezekana lisifanikiwe wakati huu kwa sababu kuna mambo muhimu ya kuzingatia kubwa likiwa ni marekebisho ya sheria na hili zoezi la uandikishaji wapigakura kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura. Ili mwananchi aweze kupiga kura ni lazima awe ameandikishwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura," alisema.

"Itabidi tuangalie kama mashine za BVR nazo zitapaswa kupelekwa kwenye kila ubalozi ili watu wetu waweze kujiandikisha au itafutwe njia nyingine ya kufanikisha hilo jambo.... lakini watu wa Tume wanaamini kwamba jambo hilo linaweza kufanikiwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2020," aliongeza.

Waziri Mkuu ambaye aliwapatia nakala zisizopungua 40 za Katiba Inayopendekezwa, alitumia fursa hiyo kuwasisitizia wasome kwa makini Katiba hiyo ili wawe na uelewa mpana na kisha wailinganishe na Katiba ya mwaka 1977 ambayo inatumika hivi sasa ili waweze kubaini kama kweli haina kitu kama ambavyo watu wengine wanadai.

"Moja ya changamoto zinazotukabili huko nyumbani ni mjadala kuhusu Katiba Inayopendekezwa... wako watu wanaosema kwamba hakuna kitu kipya kabisa kwenye Katiba Inayopendekezwa, lakini mimi nasema hayo ni mawazo yao binafsi," alisema.

Akifafanua kuhusu Katiba hiyo, Waziri Mkuu alisema: "Mimi nilikuwa sehemu ya Bunge Maalum la Katiba, ni kweli tulibadili baadhi ya vipengele lakini kwa nia ya kuiboresha. Ninawasihi kila mmoja wenu aisome na kuangalia kama kweli hamna kitu au kuna kitu kipya ikilinganishwa na Katiba inayotumika hivi sasa. Angalieni na pimeni, je kuna kitu kimeboreshwa au la?"

Aliwasihi waendelee kuiombea nchi ya Tanzania ili iendelee kuwa na amani na utulivu na hasa katika kipindi hiki ambacho inakabiliwa na uchaguzi wa madiwani, wabunge na Rais. "Ninawasihi muendelee kuiombea nchi yetu ili ipate viongozi wazuri ambao watajali maslahi ya wengi," aliongeza.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, APRILI 12, 2015.

HAFLA YA CHAKULA KWA WANAKAMATI MBALI MBALI WA SHEREHE ZA MAPINDUZI YAFANYIKA

$
0
0
za1Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Viongozi katika  chakula cha usiku  kilichoandaliwa rasmi kwa Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa katika kufanikisha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar  ya miaka 51  katika viwanja Ikulu Mjini Unguja jana.za2Waalikwa walioshiriki katika chakula cha usiku  kilichoandaliwa rasmi kwa Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa katika kufanikisha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar  ya miaka 51  katika viwanja Ikulu Mjini Unguja jana.za3Waalikwa walioshiriki katika chakula cha usiku  kilichoandaliwa rasmi kwa Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa katika kufanikisha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar  ya miaka 51  katika viwanja Ikulu Mjini Unguja jana.za4Baadhi ya waalikwa katika  katika chakula cha usiku  kilichoandaliwa rasmi kwa Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa katika kufanikisha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar  ya miaka 51  katika viwanja Ikulu Mjini Unguja jana wakifuatilia kwa makini taratibu wakati wa chakula hicho ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.za5Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akichukua chakula wakati wa hafla maalum kwaHalmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa katika kufanikisha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar  ya miaka 51  katika viwanja Ikulu Mjini Unguja jana.za6Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzinbar Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Viongozi mbali mbali walishiriki katika  hafla maalum ya chakula cha usiku kwa Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa katika kufanikisha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar  ya miaka 51  katika viwanja Ikulu Mjini Unguja jana.za7Baadhi ya Viongozi wakichukua chakula katika hafla ya chakula cha Usiku  kilichoandaliwa rasmi kwa Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa pamoja kamati mbali mbali zilizofanikisha Sherehe hizo hafal ilifanyika jana viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.za8Baadhi ya waalikwa wakichukua chakula katika hafla ya chakula cha Usiku  kilichoandaliwa rasmi kwa Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa pamoja kamati mbali mbali zilizofanikisha Sherehe hizo hafal ilifanyika jana viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.za9Kikundi cha JKU Morden Taarab kiitumbiza wakati wa chakula cha Usiku  kilichoandaliwa rasmi kwa Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa pamoja kamati mbali mbali zilizofanikisha Sherehe hizo hafal ilifanyika jana viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.za10Baadhi ya wasanii waliofanikisha kutoa burudani katika sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibarwakiwa katika hafla yachakula cha Usiku  kilichoandaliwa rasmi kwa Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa pamoja kamati mbali mbali zilizofanikisha Sherehe hizo hafal ilifanyika jana viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.za11Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini akitoa neno la Shukurani kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati wa hafla ya chakula cha Usiku  kilichoandaliwa rasmikwa Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa pamoja kamati mbali mbali zilizofanikisha Sherehe za maiaka 51 ya mapinduzi matukufu ya Zanzibar zilizofanyika viwanja vya Ikulu.za12Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Viongozi baada ya kumalizika kwa hafla ya chakula cha usiku  kilichoandaliwa rasmi kwa Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa katika kufanukisha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibarya miaka 51  katika viwanja Ikulu Mjini Unguja jana,[Picha na Ikulu.]

SEREKALI YATAKIWA KUTOWAFUKUZA WATOTO WA KIKE WENYE UJAUZITO MASHULENI

$
0
0


Serikali imetakiwa kutazama upya uwezekano wa kubadili  sheria inayomnyima haki ya kuendelea na masomo mwanafunzi wa kike pindi anapopata ujauzito akiwa shuleni.


Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Afisa elimu taaluma ,mkoa wa Arusha,Kabesi katundu Kabeja wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa umoja wa wakuu wa shule za msingi kutoka nchi ya Kenya uliofanyika katika hotel ya Leons iliyopo Sakina kwa Idi ,jijini hapa,ambapo walimu zaidi ya 1000  kutoka nchini  humo walikutana.


Alisema  hatua ya sasa ya kumfukuza shule mwanafunzi wa kike mwenye ujauzito ni kumnyanyapaa na kumkosesha fursa ya kupata elimu,hivyo alisema ni vema serikali katazama upya sheria hiyo kandamizi.


Aliitaka serikali kuiga nchi jirani ya kenya ambayo sheria yao inaruhusu msichana huyo  kuendelea na masomo pindi anapokuwa amejifungua.


‘’Hapa kwetu sheria zinakataza mwanafunzi mwenye ujauzito kuendelea na masomo lakini serikali tumeiomba serikali ibadili sheria hiyo ili kutoa fursa kwa mwanafunzi mwenye ujauzito kuendelea na masomo pindi anapojifungua,alisema Kabeja.


Kwa upande wake mwenyekiti wa  umoja kutoka nchini Kenya ,Wintred Mbinyasila ,alisema mkutano huo ambao umekuwa ukifanyika kila mwaka unalenga kubadilishana mawazo na mwaka huu lengo ni kujifunza teknolojia ya kufundishia.


Hata hivyo alisema nchi ya Kenya imepiga hatua kubwa suala la elimu kwa mtoto wa kike baada ya kuruhusu mwanafunzi huyo pindi anapokuwa na ujauzito kuendelea na masomo  baada ya kujifungua.


‘’Serikali huchukua hatua kali kwa mtu mzima aliyempa ujauzito mtoto wa kike ila kama alipata ujauzito kutoka kwa mwanafunzi mwenzake ,sheria inaruhusu kuendelea na masomo kwa masharti ya kutoa matunzo  pindi akifikia umri wa mtu mzima’’alisema


Naye mjumbe wa shirikisho la walimu wakuu wa nchi za Afrika mashariki ,Anjelina Kitigwa alisema mkutano huo unasaidia sana kubadilishana uzoefu na kujadili changamoto zilizopo hali itakayosaidia  kuinua elimu katika nchi za afrika mashariki.

MWENYEKITI WA KIJIJI ASABABISHIA FAMILIA SABA KUKOSA MAHALA PA KUISHI BAADA YA KUBOMOA NYUMBA ZAO

$
0
0
 Baadhi ya mashamba ya migomba yaliyofyekwa na kijiji kwa madai kuwa shamba hilo lipo ndani ya eneo la kijiji,

Baadhi ya wahanga waliovunjiwa nyumba zao wakiwa katika mabaki ya nyumba hizo ,katika kijiji cha Sakila wilayani Arumeru.


FAMILIA saba zenye watu zaidi ya 30 katika kijiji cha Sakila,wilayani Arumeru mkoani hapa,hazina mahala pa kuishi  kutokana na nyumba zao kubomolewa na mwenyekiti wa kijiji hicho kwa madai kuwa zilijengwa bila kufuata utaratibu.


Aidha familia hizo wakiwemo watoto wadogo zimelazimika kulala kwenye mabaki ya nyumba hizo licha ya baridi kalli na mvua zinazonyesha wilayani humo baada ya kukosa mahala pa kujikimu.


Akizungumzia kadhia hiyo mmoja wa wahanga hao,Samson Joseph Nasary(70) alisikitishwa na hatua ya mwenyekiti wao Richard Mbise akiwa na kundi la watu zaidi ya 20 kuvamia makazi yao na kubomoa nyumba zao huku wakimwaga akiba kidogo ya chakula walichokuwa nacho .


Alisema tukio hilo limetokea April 2 mwaka huu ambapo askari wa kampuni ya ulinzi ya Kifaru ndio walikuwa wakitekeleza zoezi hilo wakiongozwa na uongozi wa kijiji hicho.


‘’Eneo hilo ni mali ya baba yetu mzee Joseph Mareu Nasary aliyeishi hapa tangu mwaka 1948 na baada ya kufariki alituachia  urithi  tukiwa tunaishi hapa,wakati kijiji kinaanza mwaka 1976 /77 sisi tayari tunaishi hapa sasa tunasikitika sana leo hii kuvamiwa na kuvunjiwa nyumba zetu wakisema eti tumevamia’’alisema


Naye mkazi mwingine Peter Mafie alilalamikia hatua ya mwenyekiti huyo kuamuru kufyekwa kwa  migomba yake na mazao aliyootesha kwenye shamba lake bila kushirikishwa .


Alieleza kuwa kabla ya kumchagua mwenyekiti wao,aliwahidi kuwa angewasaidia kutatua mgogoro huo bila kuondolewa kwenye makazi yao,suala ambalo lilichangia wao kumchagua kwa kishindo.

Hata hivyo wameshangaa baada ya kumchangua amewageuka na kubomoa nyumba zao.


Wengine waliobomolewa nyumba zao ni,Lightnes Charles ambaye ni mjane,David Israel,Lucas Akyo ,Visenti Mathias ,Joshua Shayo,Deatres Sakwera na Selian Juma wote wakazi wa kijiji hicho.



Aidha wameitaka serikali akiwemo mbunge wao Joshua Nasary kuwasaidia wapate haki yao ya kurejeshewa makazi hayo kwani kwa sasa wanaishi kwa kubangaiza na kulala mahala pasipo stahili.


Kwa upande wa mwenye kiti,Richard Mbise alikiri kubomoa nyumba za wakazi hao akisisitiza kuwa alikuwa akitekeleza amri ya mahakama ya ardhi ya wilaya iliyotoa ushindi kwa kwa uongozi wa kijiji.


Hata hivyo alisisitiza kuwa wananchi hao walivamia eneo hilo  lililotengwa kwa ajili ya huduma mbalimbali za kijiji ikiwemo ujenzi wa zahanati na shule na kuanzisha makazi.


Aliongeza kuwa  uongozi wa kijiji ulijaribu mara kadhaa kuwaondoa katika eneo hilo lakini walikuwa wakaidi hadi suala hilo walipoamua kulifikisha mahakamani.

habari na libeneke la kaskazini blog

Viewing all 46340 articles
Browse latest View live




Latest Images