Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 499 | 500 | (Page 501) | 502 | 503 | .... | 1898 | newer

  0 0

  paroko  wa  kanisa la  anglikana  ludewa  Andrew  Hiluka kushoto akilishwa  chakula na mbnge  wa   jimbo la  Ludewa Deo  Filikunjombe kulia  huku mkuu wa  mkoa  wa Njombe Dr Rehema Nchimbi akimsaidia kushika sahani ya  chakula jana  baada ya  mbunge  huyo na mkuu  wa  mkoa  kuwaandalia chakula wagonjwa  wote  wa  hospitali ya  wilaya ya Ludewa.
  Mbunge  wa  Ludewa  Filikunjombe  akiongoza  msafara  wa  viongozi  mbali  mbali  akiwemo mkuu  wa  mkoa wa Njombe Dr Nchimbi kutembelea   wagonjwa hospitali ya wilaya ya  Ludewa
  Filikunjombe na Rc njombe wakitoa msaada  wa  vitu mbali mbali kama sabuni , mafuta na taulo kwa  wagonjwa  waliyelazwa hospitali ya wilaya ya  Ludewa jana
  watoto  wa mbunge Filikunjombe   wakishirikiana na  Rc  njombe  kutoa msaada kwa wagonjwa
  Dr  nchimbi na filikunjombe  wakitoa maada wa  chakula na vitu mbali mbali kwa  mgonjwa

  mtoto  wa  filikunjmbe akitoa maada wa chakula kwa  mgonjwa
  rc njombe  kulia akimlisha chakula  mgonjwa huku  mbunge  filikunjombe  akimsaidia  kushika bakuri
   mbunge Filikunjombe  akimsikiliza mkuu  wa mkoa  wa Njombe Dr nchimbi  wakati akizungumza na  wagonjwa katika hospitali  ya  wilaya ya  Ludewa

   katibu  mwenezi mkoa  wa njombe honoratus  mgaya na mkuu  wa mkoa wa njombe dr  nchimbi wakitoa chakula kwa wagonjwa
   mkuu  wa  wilaya ya  ludewa bw anatory chowa  akitoa maada wa  vitu mbali mbali kwa mgonjwa  hospitali ya ludewa
  filikunjombe  akiwa amempakata  mtoto katika  hospitali ya wilaya ya  ludewa
   filikunjombe akitoa msaada  wa  chakula
   mkuu  wa  mkoa  njombe  akila  chakula  na mgonjwa
   filikunjombe  akila  chakula na mgonjwa

   DC Ludewa akila  chakula na mgonjwa 
  mwanahabari  wa  TBC Iren Mwakalinga  akila  pasaka na  wagonjwa  hospitali ya  wilaya ya Ludewa    mbunge  wa Ludewa  Deo  Filikunjombe wa  pili  kulia akishiriki  kula chakula   na  wauguzi pamoja na mmoja kati  ya wanawake waliolazwa  katika  wodi la  wanawake waliojifungua kwenye  hospitali ya  wilaya ya Ludewa  wakati  wa  sikukuu ya pasaka
   mwalimu  DOMINIC HAULE  AKILA  CHAKULA NA  WAGONJWA
   MBUNGE FILIKUNJNOMBE KATIKATI AKILA  CHAKULA NA MUUNGUZI NA MGONJWA  KUSHOTO


   ZIARA  YA  MBUNGE FILIKUNJOMBE NA RC  NJOMBE KWENDA  KULA  CHAKULA NA  WAGONJWA
  FILIKUNJOMBE  AKIFURAHI WAKATI WAUGUZI  WA  WAGONJWA  WAKIMSHANGILIA

  FILIKUNJOMBE  AKILA  CHAKULA NA MGONJWA 
  NA MATUKIODAIMABLOG 
  MKUU wa  mkoa  wa Njombe Dr Rehema Nchimbi amempongeza mbunge Ludewa  mkoani Njombe Bw Deo Filikunjombe kwa kutumia sikukuu  ya pasaka  kuwaandalia  chakula watu wenye matatizo  wakiwemo wafungwa wa  gereza la Ludewa  na wagonjwa waliolazwa  katika Hospitali  ya wilaya ya Ludewa  huku akiagiza Halmashauri ya  Ludewa kuanzisha  huduma ya chakula kwa  wagonjwa .

  Dr Nchimbi alitoa  pongezi  hizo jana wakati  alipoungana na mbunge  huyo na viongozi  mbali mbali  wa  mkoa na wilaya ya  Ludewa   kushiriki hadla  hiyo ya mbunge  kula chakula pamoja  na wagonjwa  na  kuwapa misaada  mbali  mbali kama ulivyoutaratibu  wake kwa  kila sikukuu kula na wagonjwa na wafungwa .

  Alisema  utaratibu  unaotumiwa na  mbunge huyo  ni utaratibu  mzuri  ambao  unapaswa  kuigwa na wabunge  wengine nchini kwa kuyatembelea makundi  mbali mbali ya  kijamii wakati wa  sikukuu ama  siku  nyingine badala ya kusherekea sikukuu kwa  kufanya anasa.

  'kweli  ni jambo la kumpongeza   sana  mbunge Filikunjombe  kwa  huu utaratibu  ambao amekuwa akiufanya  binafasi niliposikia mbunge  anakuja  kufanya jambo hili kubwa la  kula  na  wagonjwa  pasaka  niliamua  kufunga  safari na mimi  kuja   kushiriki zoezi hili na  kumtia  moyo  zaidi mbunge kwa   hili si  wabunge  wote ambao  wanakawaida  ya  kutembelea  na  kuwafariji  wagonjwa na  wafungwa  kama  hivi 'alisema mkuu huyo

  Hata  hivyo  mkuu  huyo  wa  mkoa  alisema  kuwa  katika   kumuunga mkono  mbunge  Filikunjombe kwa  wazo   hilo  zuri  kwa  upande  wake  anachangia ngunia 5 za  mahindi  ili  kuwaanzishia wagonjwa wanaofika  kujifungua  huduma ya chakula kwa  kipindi chote wawapo  hospitalini hapo kama  njia ya kuepusha wagonjwa  kuwa na  mawazo ya  wapi  watapata  chakula

  kwani  alisema  si  wagonjwa   wote  wanaofika   kusubiri muda  wa   kujifungua  hospitalini hapo  wanauwezo wa  kiuchumi hivyo  kuiagiza halmashauri ya  wilaya ya  Ludewa  kuangalia   uwezekano  wa  kuchangisha chakula kwa wananchi  ili  kusaidia  huduma ya chakula kwa   wagonjwa .


  Alisema wilaya ya Ludewa na  mkoa wa Njombe kwa  ujumla hauna  shida ya chakula kama   ilivyomikoa  mingine   hivyo uwezekano  wa  kuanzisha utaratibu  wa kutoa  chakula kwa wagonjwa unawezekana .


  Akishukuru kwa  msaada  huo  wa  chakula  kwa niaba ya wagonjwa  wengne waliolazwa hospitalini hapo  paroko  wa  kanisa la  anglikana  ludewa  Andrew  Hiluka alisema   kuwa alichokifanya  mbunge huyo  ni  moja kati ya baraka  kubwa  kwake na kuwa baadhi ya wanasiasa  wanapoteza nafasi  zao   kutokana na  kuwa na roho mbaya  na uchoyo kwa  wale   waliowachagua.

  Kwani  alisema  Ludewa  imepata   kuwa na wabunge zaidi ya  watano   ila wakati  wa  sikukuu kama   hizo  wabunge  hao  walikuwa wakitoka  nje ya Ludewa ama kujifungia na familia  zao kula sikukuu tofauti na Filikunjombe  ambae  amekuwa  ni  mbunge  wa aina yake kwa  siku ya  sikukuu  kuandaa chakula  cha pamoja na  wagonjwa kwa  kula nao  chakula wodini .

  Paroko  Hiluka alitoa   wito  kwa  wananchi  wa   jimbo la  Ludewa  kuendelea kumchangua kwa  miaka mingine  zaidi mbunge Filikunjombe kwani ametambua  mahitaji  sahihi  ya  wana  Ludewa  kwa kusaidia  maendeleo ya   jimbo   hilo pia kuwagusa wote  wenye  matatizo mbali mbali ambao ni nje ya ahadi  zake za ubunge .

  Alisema  ni  kipindi  cha  Filikunjombe kasi kubwa ya   maendeleo  imeonekana kwa  kila mwananchi  wa  wilaya   hiyo na nje ya wilaya lakini pia  ni  mbunge  pekee  kusomesha   sekondari watoto  yatima  zaidi ya 700 katika  wilaya   hiyo kwa  kila mwaka  huku wabunge waliopita labda aliyejitiahidi  kusomesha basi haikuzidi watoto 2 kwa miaka yote  mitano .

  Nae mbunge Filikunjombe alisema  kuwa utaratibu   huo  wa  kula  chakula na  wagonjwa amekuwa akiufanya kila mwaka toka  alipoingia madarakani  mwaka 2010  na kuwa   iwapo  wananchi  wa jimbo  hili watamchagua ataendelea  kuwaletea maendeleo lakini  pia  kuwasaidia watu wenye matatizo kwani anachoamini na  kuendelea  kuamini  kuwa  wazima na wagonjwa  wote ni  wapiga kura  wake na  kuwa furaha yake  ni  kuona wagonjwa  wanapona ili waweze  kumchagua  tena.

  0 0

  IMG-20150406-WA0061Maafisa wa Jeshi la Polisi Tanzania wakipokea mwili wa hayati mzee Eddis Mgawe ulipowasili Jumatatu kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Daresalaam Tanzania (JIA) kutoka Washington Dc. Mzee Mgawe alikuwa ni kamishna mstaafu wa Jeshi la Polisi nchini na alifariki dunia wiki iliyopita nchini Marekani alikokuwa anawatembelea wanae.

  0 0

  Mwanamuziki Ali Kiba akizikonga nyoyo za mashabiki waliofurika Dar Live katika shoo yake ya Mwana Dar Live iliyokuwa ikipigwa kwa 'Live Band'.
  Ali Kiba na mdogo wake Abdul Kiba wakichekecha na kucheketua.
  Mashabiki wa Ali Kiba wakishow love.
  Ali Kiba na mdogo wake Abdul Kiba wakizidi kuwapagawisha mashabiki waliofurika ndani ya Dar Live Sikukuu ya Pasaka.
  Mashabiki wa Ali Kiba wakicheza staili mpya ya Chekecha Cheketua.
  Shabiki wa Ali Kiba akiwa na tisheti kuonyesha kuwa yeye ni 'Team Kiba'.

  Ali Kiba akizidi kulitawala steji la kupanda na kushuka la Dar Live.
  Wapiga vyombo wa Ali Kiba wakiwa kazini.
  Mwanamuziki Msaga Sumu akiwarusha mashabiki wa Dar Live katika shoo ya Mwana Dar Live Sikukuu ya Pasaka.
  Nyomi ikimpa shangwe Msaga Sumu.

  Isha Mashauzi na kundi lake la Mashauzi Classic wakilishambulia jukwaa la Dar Live katika shoo ya Mwana Dar Live.

  Isha Mashauzi akifanya yake stejini.

  Mwanamuziki wa Bongo Fleva anayefanya vizuri katika tasnia hiyo, Pamela Daffa 'Pam D' akiwarusha mashabiki wa Dar Live kwa songi lake kali la Nimempata.

  Vijana wa Pam D wakifanya yao stejini.

  Pam D akizidi kuwadatisha mashabiki.

  Mshindi wa kitita cha shilingi milioni 10/- kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Shamila Ramadhani (kushoto) akikabidhiwa hundi yake na Balozi wa promosheni hiyo, Hillary Daud ‘JayMillions’ baada ya kuibuka mshindi wa kitita hicho kupitia promosheni hiyo. Katikati ni mume wa mshindi huyo Abdallah Mahoka. Makabidhiano hayo yalifanyika jana wakati wa Tamasha la Mwana Dar Live, kwenye ukumbi wa Dar Live. Ili  mteja kujua kama  ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.

  Mshindi wa milioni 10 za JayMillions, Shamila Ramadhani na mumewe wakionesha mfano wa hundi ya fedha hizo.

  JayMillions akipozi na baadhi ya wadau wa Dar Live sambamba na warembo alioambatana nao baada ya kutoa mahela.
  MSANII wa kizazi kipya anayetamba na wimbo wa Chekecha Cheketua, Ali Saleh ‘Kiba’ amewapagawisha vilivyo mashabiki wake waliojitokeza katika shoo ya Mwana Dar Live kwenye Sikukuu ya Pasaka katika Ukumbi wa Taifa wa Burudani, Dar Live, Mbagala jijini Dar es Salaam.
  Ali Kiba akiwa sambamba na mdogo wake Abdul Kiba waliangusha bonge la burudani huku wakiimba nyimbo zao zote kwa kutumia vyombo vya jukwaani ‘live band’.
  Shoo hiyo ilisindikizwa na Isha Mashauzi akiwa na Mashauzi Classic, Msaga Sumu na Pamela Daffa 'Pam D' ambao walitoa burudani ya nguvu na kuzikonga nyoyo za mashabiki waliofurika ndani ya ukumbi huo.
  Shoo ya MWANA DAR LIVE ilidhaminiwa na VODACOM TANZANIA, huku wadhamini wengine wakiwa SKYY VODKA, RED BULL, VITA MALT, VALEUR BRANDY, GRANTS,
  JÄGERMEISTER NA GLOBAL PUBLISHERS LTD.


  0 0

  unnamed
  Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
  Waandishi wa habari nchini wameazimia kuboresha Fani ya Uandishi na Utayarishaji wa Vipindi Vinavyohusu Watu wenye Ulemavu wa Akili ili kuzidi kutetea Maslahi na Haki za Watu hao.
  Maazimio hayo wameyatoa katika Semina ya Siku mbili ya kuwajengea Uwezo waandishi hao iliyoandaliwa na Jumuiya ya Watu wenye Ulemavu wa Akili Zanzibar (ZAPDD) kwa Msaada wa Mwenvuli wa Asasi za Kiraia.
  Wamesema kuna kila haja ya kuboresha Habari na Vipindi wanavyotoa kutokana na Jamii ya Watu wenye Ulemavu wa akili kukumbwa na Changamoto nyingi na hivyo kukoseshwa haki zao za Msingi.
  Aidha wameazimia kuongeza Ushirikiano wa karibu baina yao na Jumuiya ya ZAPDD ili kuona Jamii hiyo inawezeshwa kama zilivyokuwa jamii nyingine nchini.
  Awali akitoa mada katika Semina hiyo Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu Ally Uki aliwataka Wanahabari hao kuwasaidia Walemavu hao wa Akili kwa kufichua maovu wanaotendewa ili Jamii ipate uelewa na kulinda haki zao.
  “Ndugu zangu hawa Walemavu wa Akili Hawapewi haki ya Kutoa Ushahidi Mahakamani, Hawawezi kupiga kura, Wananyanyaswa na Kubakwa hivyo jitihada zenu ndio zitakazochangia kupata haki zao” Alisema Uki.
  Kwa Upande wake Mdau wa Jumuiya ya ZAPDD Khalid A. Omar ameziomba Taasisi za Kiraia na Kijamii kuendelea kuihimiza Serikali kuongeza kasi ya kuzifanyia mapitia Sheria ambazo zinawakandamiza Watu wenye Ulemavu wa Akili.
  Ameongeza kuwa ni vyema Taasisi hizo pia zisaidie kuishawishi Serikali kutenga Bajeti ya Angalau Asilimia 5%  ya gharama ya Sekta ya Afya ziende kwa Watu wenye Ulemavu.
  Akifunga Mafunzo hayo Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya ZAPDD Tamrin Ali Said amesema wamelazimika kufanya kazi na Wanahabari wakiamini kuwa Mchango wao ni mkubwa katika kusaidia MApambano dhidi ya haki za Watu wenye Ulemavu wa Akili.
  Tunajua Umuhimu wenu Waandishi ndio tukawaita hapa ingawa kuna Makundi mengine kama Viongozi wa Dini na Wasanii ambao nao tutafanya kazi kwa pamoja katika kusaidia kuwapatia haki zao Watu wenye Ulemavu wa Akili.
  “Tunakuombeni sana Mujitolee katika kuandika na kutayarisha Vipindi vyenu ambavyo kwa hakika Mungu atakulipeni pale mnapofichua Ukandamizwaji wa haki za Watu wenye Ulemavu wa Akili” Aliomba Makamu Mwenyekiti.
  Jumuiya ya Watu wenye Ulemavu wa Akili Zanzibar ZAPDD kwa sasa ina wanachama zaidi ya 2,600 ambapo imejikita zaidi katika kutetea haki na fursa Watu wenye Ulemavu wa Akili nchini.

  0 0

   Waziri Membe akitoa msaada kwenye kituo hicho
   Waziri Membe pamoja na Mkewe Mama Dorcas Membe katika picha ya Pamoja na Masista wanaolea watoto yatima katika kituo hicho.
    Waziri Membe akizungumaza wakati wa ziara yake kituoni hapo. Kulia ni Mama Dorcas Membe. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Paul Makonda akifuatiwa na Padri Timoth Maganga wa Kanisa Katoliki la Kigogo Mburahati.
  Padri Timoth Maganga wa Kanisa Katoliki la Kigogo Mburahati akitoa shukrani zake za pekee kwa Waziri Membe kutembelea kituoni hapo.
  Msimamizi wa Nyumba ya Furaha na Amani, Sista Bakitha akiongea machache kumkaribisha Mhe. Membe mara baada ya kufika kituoni hapo akiambatana na mkewe Dorcas na familia yake kwa jumla kusherehekea Siku Kuu ya Pasaka pamoja na Watoto Yatima na Wazee wanaolelewa kwenye kituo cha Nyumba ya Furaha na Amani.
   Mama Dorcas Membe akiwatuza watoto wa kituo hicho pesa wakati wakicheza kuwakaribisha kituoni hapo. 
   Watoto yatima wakiwa na walezi wao.
   Akinamama walemavu na wasiojiweza wanaolelewa katika kituo hicho.
   Waziri Membe akikata keki pamoja na Sista Bakitha kama ishara ya kusherehekea Siku Kuu ya Pasaka pamoja na Watoto Yatima na Wazee wanaolelewa kwenye kituo cha Nyumba ya Furaha na Amani. Pembeni ni Mama Dorcas Membe nae akifurahia
   Waziri Membe akilishwa keki na mmoja ya watoto wanaolelewa katika kituo.
   Waziri Membe akiwalisha keki watoto.
  Mama Dorcas Membe akiwalisha watoto keki.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) akimtazama kwa furaha mmoja wa watoto yatima wanaolelewa kwenye kituo cha Nyumba ya Furaha na Amani kilichopo Kigogo Mburahati, Jijini Dar es Salaam. Waziri Membe alikitembelea kituo hicho wakati wa Siku Kuu ya Pasaka.
  Mhe. Membe pamoja na Mkewe Mama Dorcas Membe wakipata maelezo juu ya watoto waishio katika kituo hich kutoka kwa Sista Mary Bakhita.
  ---
  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe ametoa wito kwa Watanzania kujenga utamaduni wa kuwasaidia watu wasiojiweza waliopo kwenye jamii wakiwemo watoto yatima, walemavu, wazee na wajane.

  Waziri Membe ametoa wito huo hivi karibuni alipotembelea Kituo cha Kulelea Watoto Yatima na Wazee cha Nyumba ya Furaha na Amani kilichopo Mburahati Jijini Dar es Salaam.

  Mhe. Membe alisema kuwa katika jamii za watu kumekuwa na makundi ambayo yanahitaji msaada mkubwa kutoka kwa watu wengine ambao kwa namna moja au nyingine wamejaaliwa kipato kidogo na afya. Alisema kuwa ni wajibu wa watu wa aina hiyo kuwasaidia wale wanaohitaji kama vile watoto yatima, walemavu, wazee na wajane.

  Waziri Membe ambaye alikuwa amefuatana na Mke wake, Mama Dorcas Membe aliguswa sana na historia ya baadhi ya watoto yatima aliowatembelea kituoni wakiwemo wale waliotupwa jalalani na kuokotwa wakiwa kwenye hali mbaya.

  “Lipo kundi linalopata mateso na matatizo katika jamii zetu tunazoishi. Ni vizuri Watanzania tukajenga utamaduni wa kutembelea sehemu kama hizi ili kujionea wenyewe hali halisi.

  Kwa kweli ni hali ya kusikitisha kuona baadhi ya watoto walitupwa na kuokotwa jalalani na wengine tayari wakiwa wamepata majeraha ya kung’atwa na mbwa. Hivyo ni wajibu wetu sote kuwasaidia kwa chochote kidogo tunachojaaliwa kupata”, alisema Waziri Membe.

  Aidha, Mhe. Membe aliwapongeza na kuwasifu Masista wa Shirika la Mama Theresa ambao ndio wasimamizi wa kituo hicho kwa kuwalea watoto, vijana na wazee wenye matatizo mbalimbali na kuwaomba waendelee kujipa moyo katika kazi hiyo kwani ni njia moja wapo ya kumtumikia Mungu.

  Awali akimkaribisha Waziri Membe kituoni hapo, Sista Mkuu wa Kituo hicho, Sista Mary Bakhita, alisema kuwa wamefurahia sana ziara hiyo ya Mhe. Membe hususan katika Siku Kuu ya Pasaka kwani ni faraja kubwa kwao kwa Watoto na Wazee wanaolelewa kituoni hapo.

  “Tumefarijika sana kula pasaka pamoja nawe Mhe. Waziri. Watoto na Wazee hawa wanajisikia vizuri pale wanapotembelewa na tunaomba uendelee na moyo huo huo”, alisema Sista Bakhita.
  Wakati wa ziara hiyo Mhe. Membe na familia yake walitoa zawadi mbalimbali kwa kituo hicho ikiwemo vyakula, sabuni na fedha kiasi cha shilingi milioni 10 kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali kituoni hapo.

  0 0

   
  Kamanda wa jeshi la zimamoto mkoa wa iringa akikabidhi mbuzi kwa kaimu mkuu wa kituo cha Sister Theresa, Sister Sister Winfrida Mhongole  katika makabidhiano yaliyofanyika kituoni hapo.

  NA DENIS MLOWE,IRINGA

  JESHI la Zimamoto mkoani Iringa limesheherekea sikukuu ya pasaka  na watoto  wanaoishi katika kituo cha kulea yatima cha Sister Theresia  kilichoko Tosamaganga mkoani Iringa kwa kuwapatia misaada mbalimbali.

  Akikabidhi msaada huo Kamanda wa Jeshi la Zimamoto mkoa wa Iringa Inspekta Kennedy Komba alisema lengo kubwa la jeshi hilo ni kuwa karibu zaidi na jamii katika kutoa misaada ambayo itawasaidia yatima walioko katika vituo mbalimbali mkoani hapa.
   
  Alisema yatima wanakabiliana na mazingira magumu katika kupata mahitaji muhimu hasa chakula, afya na malazi hivyo ni jukumu la kila mmoja kuweza kuwasaidia kuondokana na hali ya utegemezi.
   
  “Tumeamua kugawa msaada huu kwa kuguswa na matatizo mbalimbali wanayokabiliana nao vituo vingi vya kulelea watoto hapa nchini katika harakati zetu za kuhahikisha watoto yatima wanapata mahitaji muhimu katika maisha yao ya kil siku huu ni mwanzo tu wa jeshi la zimamoto katika kuwa karibu na jamii na hii tunafanya kila mwaka kuweza kurudisha pia katika jamii kile ambacho jeshi hilo linapata” alisema Komba
   
  Alisema msaada uliotolewa wa mchele kilo hamsini, mbuzi, mafuta ya kupikia, sabuni na kuwapatia kifaa cha kuzimia moto (Fire extinguisher) baada ya kuwapa mafunzo ya jinsi ya kutumia vyote vikiwa na jumla ya thamani ya shilingi laki 250,000.
   
  Komba alisema jeshi la zimamoto litakuwa likitoa msaada wa aina hiyo kila mara ili kujiweka karibu na jamii kuweza kutambua shughuli wanazofanya na kuwataka wadau wengine kuiga jeshi hilo katika kuwasaidia watoto yatima.
   
  “Jamii ya Kitanzania yatakiwa kuunga mkono tabia ya kuwasaidia watoto yatima na kuwaimiza kupenda masomo yao na jamii kutowatumia kama watoto wa kazi za ndani na kuwahudumia kwa kila jambo wanalofanya kuliko kutumia muda mwingi katika matumizi ya anasa” alisema Komba
   
  Kwa upande wake kaimu msimamizi wa kituo hicho Sister  Winfrida Mhongole  alilishukuru jeshi la zimamoto kwa msaada huo na kuwataka wadau wengine wawe na moyo wa kujitolea kwa watoto yatima wanaolelewa katika vituo tofauti mkoani hapa.

  Alisema kituo kina jumla ya watoto 280 ambao mbali na hao watoto 72 wanaishi kituoni hapo na wengine wako katika shule mbalimbali wakisoma zikiwemo za msingi na sekondari.

  Alisema watoto hao wamepokelewa kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo ya Iringa, Mbeya, Njombe, Morogoro, Dar es Salaam na Morogoro.

  “Mbali na mapato yatokanayo na shughuli za kilimo tunazozifanya kama kituo, kituo hiki kinaendeshwa kwa michango ya wahisani mbalimbali wa ndani na nje. Kwa kweli hatuna wafadhili wa kudumu,” alisema na kuomba wahisani waendelee kujitokeza kuwasaidia.

  0 0

  Waimbaji wa Glorious Worship Team (GWT) wakiwa stejini wakati wa kumsifu Mungu na kumwabudu.
  Glorious Worship Team wakizidi kumwabudu Mungu katika Ukumbi wa Victoria Petrol Station.
  Mpiga gitaa la sauti nzito (base) wa GWT, Emmanuel Materu akicharaza gitaa hilo. Pembeni yake ni waimbaji wenzake.
  David Silomba (kulia) pamoja na Paul Clement wakiendelea kutoa burudani.
  Kutoka kulia ni mwimbaji David Silomba akiimba sambamba na Editha Salum. Katikati ni Mpiga gitaa la sauti nzito (base), Emmanuel Materu.
  Davina Lema (kulia) na Mary Igoti wakimwabudu Mungu wakati wa hafla ya Mtoko wa Pasaka.
  Mwimbaji Editha Salum akizidi kumtukuza Mungu.
  Dk. Mponzi pamoja na familia yake wakiwa na wadau wengine wa GWT wakati wakifuatilia matukio mbalimbali ukumbini hapo.
  Ester Peter (kulia) akiimba pamoja na Salome Shemakulenge.
  Mlezi wa GWT, Eric Shigongo akisalimiana na mmoja wa wadau wa GWT.
  GWT wakiendelea kumsifu na kumwabudu Mungu kwa nyimbo.
  KIKUNDI cha kumsifu na kumwabudu Mungu cha Glorious Worship Team (GWT) katika Sikukuu ya Pasaka kilitoa burudani ya nguvu kwenye hafla ya kumsifu na kumwabudu Mungu iliyokwenda kwa jina la 'Mtoko wa Pasaka' na kufanyika Ukumbi wa Victoria Petrol Station, Mikocheni jijini Dar es Salaam.

  Katika hafla hiyo, GWT walimsifu na kumwabudu Mungu kwa nyimbo ikiwa ni muendelezo wa programu yao ya Sunday Celebration ambayo hufanyika kila Jumapili kuanzia saa 9 alasiri baada ya ibada.

  Akizungumza na mtandao huu, Mkurugenzi wa GWT, Emmanuel Mabisa amesema wiki hii katika Sunday Celebration Season 4 ndani ya Ukumbi wa Victoria Petrol Station, Mjasiriamali na Mtunzi mahiri wa Vitabu, Eric Shigongo ataendelea kutoa somo lake la Siri za kutoka kuwa Mwajiriwa hadi kuwa Mwajiri.

  Katika somo hilo, Shigongo atatoa bure vitabu vyake zaidi ya 200 alivyoahidi kuvitoa kwa watu waliowahi kufika ukumbini katika Sikukuu ya Pasaka. Waimbaji mahiri wakiwemo; Upendo Nkone, Carvary Band, The Jordan Moses Zamangwa (Mosax), na Masanja Mkandamizaji watakuwepo kutoa burudani siku hiyo ya Aprili 12, mwaka huu.

  0 0

  President Jakaya Kikwete and his entourage leave the UN Headquarters in New York, after holding talks with the UN Secretary General Mr Ban Ki-moon at the UN Headquarters in New York.
   STATE HOUSE PHOTOS
  —————————
  The Chairman of the United Nations High-level Panel on the Global Response to Health Crisis President Jakaya Kikwete on Monday met and held talks with UN Secretary General Ban Ki-moon in New York.

  This was the first time President Kikwete met the UN Chief since he appointed him to chair the panel, whose 0ther members include those from Brazil, Switzerland, Indonesia, Botswana and the United States.

  President Kikwete and Mr Ban Ki-moon reviewed the  terms of reference of the panel which  is mandated  to come up with  recommendations to strengthen  national and international systems to prevent and manage future health crises, taking into account lessons learned from the response to the outbreak of Ebola virus.

  In carrying out its work, the Panel will undertake a wide range of consultations, including with representatives from the affected countries and communities, the UN system, multilateral and bilateral financial institutions and regional development banks, Non-Governmental Organizations, countries supporting the response effort, other member states, health care providers, academic and research institutions, the private sector, and other experts.
  The panel will hold its first meeting in early May and is expected to submit its final report by the end of the year to the UN Secretary General, who will make the report available to the General Assembly, and undertake further action as appropriate.

  0 0

  B8
  Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Hamid Ameir akiweka shada la mauwa katika kaburi la Marehemu Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume,baada ya kisomo cha  hitma na dua iliyoombwa na wananchi wa Zanzibar katika Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo asubuhi,[Picha na Ikulu.]B11Balozi Ali Karume (Mtototo)  kwa niaba ya familia akiweka shada la mauwa katika kaburi la Marehemu Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume,baada ya kisomo cha  hitma na dua iliyoombwa na wananchi wa Zanzibar katika Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo asubuhi,[Picha na Ikulu.]
  B12
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein pamoja na Viongizi wengine wakiitikia Dua iliyoombwa na Mufti Mkuu wa zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (kulia) baada ya kisomo cha hitma iliyosomwa leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.B14Baba Askofu wa Anglikan wa Kanisa la Mkunazini Michael Hafidh akiomba dua wakati Viongozi mbali mbali waliofika katika kaburi la aliyekua Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,baada ya kisomo cha hitma iliyosomwa leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.

  B1Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Vuai Ali Vuai maara alipowasili katika viwanja vya Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja kubhudhuria katika Hitma ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume Iliyofanyika leo asubuhi.[Picha na Ikulu.]B2Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein(katikati) akiwaongoza Viongozi mbali mbali pamoja na Wananchi katika Kisomo cha hitma ya aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini UngujaIliyofanyika leo asubuhi.[Picha na Ikulu.]B3Baadhi ya Viongozo wakisoma hitma akiwemo aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume(kushoto) Balozi Ali Karume katika ukumbi  wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja Iliyofanyika leo asubuhi.B4Waislamu na wananchi mbali mbali wakiwa katika kisomo cha hitma ya 
  aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja Iliyofanyika leo asubuhi.B5Akinamama wa Mitaa mbali mbali ya Mji wa Unguja wakiwa katika kisomo cha Hitma ya aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja Iliyofanyika leo asubuhi.B7Mke wa Rais Zanzibar Mama Mwanamwema Shein(katikati) akiwa na  Mama Shadya Karume Mke wa Rais Mstaafu wa Zanzibar(wa tatu kulia) Mama Fatma Karume (wa pili kulia) Mke wa Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mama Zakia Bilali (kushoto) Bi Khadija Aboud (wa pili kushoto)Mjumbe wa Kamati Kuu wa CCM,katika hitma ya kumuombea dua Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,iliyosomwa leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.

  0 0


  0 0
 • 04/07/15--11:54: Tangazo la Shukrani
 • The Late Angela Gaya Novatus Matiku


  IN EVELASTING MEMORY


  Dear Angela, it's been a year since you left us, it all happened so sudden, we didn't get to say "GOODBYE". Our lives have changed without you here. Although physically you are not with us, you are always in our hearts and minds. You were a special gift from GOD, a true Angel just as your name.  We thank almighty GOD for the time you spent with us. We miss you so much but we always take courage and hope through the bible verse from Revelation 21:4;

  “He will wipe away every tear from their eyes, and death shall be no more, neither shall thAere be mourning, nor crying, nor pain anymore, for the old order of things has passed away.”

  You are deeply missed and remembered  by your parents Rtd. Brig. Gen Novatus Matiku and Zania Matiku; son Jason Phoenix; brothers Wakondya, Sode and Silvanus; sister Sylvia; in laws Beatrice Chiomba, Aika Makindara, Asupya Nalingigwa and Amanda Chris Shayo; nephews Humphrey, Hudson, Abihudi and Aikondya; nieces Andetta, Zanella and Amona; friends and relatives.


  We believe that someday we'll see you again, until then; you will forever live in our hearts.  0 0

  IMG_2176

  Meneja Mwendeshaji wa kampuni ya Shamy Tours and Travel Agent Zanzibar, Bw. Khamis Mwinjuma Simba akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo katika sekta ya utalii Zanzibar na Tanzania kwa ujumla wakati wa zoezi la kugawa zawadi za vinyago kwa wageni waalikwa zaidi ya 300 waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Mgahawa mkubwa unaotoa huduma za chakula cha Kitanzania unaomilikiwa na mpishi maarufu duniani mtanzania, Issa Kasuwi Kapande almaarufu kama ‘Chef Issa’ nchini Sweden katika mji wa Trollhattan.Unaweza kutembelea tovuti yao kwa anauni hiiwww.shamytours.co.tz

  Na Mwandishi Maalumu,Trollhattan, Sweden
  KAMPUNI ya kupokea wageni ya Zanzibar ya Shamy Tours and Travel Agent Zanzibar, imefungua ofisi nchini Sweden ambayo itakuwa inashughulikia masuala ya watalii na wageni mbalimbali wanaotaka kuingia Tanzania na visiwani Zanzibar.

  Meneja Mwendeshaji wa Kampuni ya Shamy, Khamis Mwinjuma Simba akizungumza mjini hapa alisema kwamba kampuni yake kupitia Bodi ya Utalii ya Sweden wamepata kibali na leseni ya kuanzishwa kwa branchi ya kampuni hiyo yenye makao makuu yake mjini Zanzibar , mtaa wa Malindi.

  Kampuni hiyo ambayo tangu kuanzishwa kwake ina miaka minne sasa ilifanya uzinduzi wa branchi yake hivi karibuni, kazi iliyofanywa na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Dora Msechu wakati akizindua mgahawa wa Mtanzania, Issa Kapande wiki iliyopita.
  Simba alisema kwamba tangu kuanzishwa kwake wamepata maendeleo makubwa hasa katika kukabiliana na changamoto za soko na kwamba kwa kuanzishwa kwa tawi hilo wanaangalia kufikia nchi 30 za Ulaya zinazotumia viza ya Ulaya.
  IMG_2100
  Alisema kuwa na ofisi nchini Sweden kumeamsha mori wa kuongeza mafanikio ya kampuni ili kusaidia juhudi za Wizara ya Utalii Zanzibar katika kuhakikisha kwamba sekta ya Utalii inaendesha uchumi wa Zanzibar.

  Alisema wizara kama wizara imefanya juhudi kubwa kuhakikisha utalii unakua na kuleta mafanikio kwa Zanzibar na hivyo ni wajibu wao kama Shamy Tours kuhakikisha kwamba wanatoa fursa walizowezeshwa na wizara hiyo kutanua shughuli zao ili kuihakikishia mapato serikali kwa kuingiza wageni wengi zaidi.

  "Tumepata faida kubwa kama Shamy Tours kutoka kamisheni ya utalii hasa usajili, kupewa hati za uendeshaji na vipeperushi na machapisho mbalimbali na hasa chapisho la Karibu Zanzibar linalohusu Zanzibar," alisema Simba na kuongeza kuwa kwa kusaidiwa huko wameweza kusonga mbele na katika miaka minne kwa kushirikiana na Issa Kapande, Mtanzania mbaye amefungua mgahawa wa Kitanzania nchini Sweden, wameweza kuanzisha branchi nchini Sweden.

  Alisema pamoja na kuzindua ofisi yao, wameitumia siku ya ufunguzi wa mgahawa wa Issa Kapande kukutana na wadau mbalimbali wa masuala ya utalii nchini Sweden na kuwapatia zawadi halisi za Kitanzania kuwapa ushawishi wa kuja nchini.
  IMG_2182
  Balozi wa Shamy Tours and Travel Agent nchini Sweden, Bi. Anab akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo wakati wa zoezi la kukabidhi zawadi kwa wageni waalikwa zilizotolewa na kampuni hiyo kwenye hafla ya uzinduzi wa mgahawa mkubwa unaotoa huduma za chakula cha Kitanzania unaomilikiwa na mpishi maarufu duniani mtanzania, Issa Kasuwi Kapande almaarufu kama ‘Chef Issa’ nchini Sweden.

  Baadhi ya zawadi hizo ni vinyago vya kimakonde taswira za Wamasai na vipeperushi mbalimbali. Alisema kuwapo kwa Shammy Tours nchini Sweden kutakuza biashara ya utalii.
  Alisema mipango ya kuanzisha ofisi nchini Sweden ilianza zamani wakati Issa Kapande akifanya shughuli zake katika Hoteli ya African House miaka sita iliyopita na kushika kasi katika miaka miwili iliyopita ambapo Issa Kapande alifika Zanzibar mara mbili kukamilisha ushirikiano uliozaa ofisi hiyo ya Sweden.

  Alisema pamoja na kujitangaza katika nchi zaidi ya 30 za Ulaya kupitia ofisi hiyo ya Sweden Shamy Tours inatarajia kushiriki katika maonesho ya utalii Afrika Kusini yatakayofanyika Mei mwaka huu, Urusi Juni mwaka huu na London, Uingereza Novemba mwaka huu.
  Alisema ushiriki wao ni sehemu ya kutafuta masoko na kuitangaza Tanzania, nchi ya visiwa vya Zanzibar, mlima Kilimanjaro na mbuga ya Serengeti.
  IMG_2194
  Unaweza kutembelea tovuti yao kwa anauni hiiwww.shamytours.co.tz

  0 0

  Baadhi ya wanasemina wakiwa katika Picha ya pamoja

   Kilimo na Ufugaji wa Kisasa kwa maendeleo ya Jamii na kukataa umasikini kwa kujiajili ndiyo kauli kuu iliyotawala katika Semina ya Kilimo na Ufugaji wa kisasa iliyofanyika Jijini Dar es salaam ambapo washiriki walipata mafunzo na Elimu Bora juu ya Kilimo bora cha kisasa pamoja na ufugaji Semina iliyo ongozwa na Mjasiriamali mwanamke ambaye amethubutu Bi. Mary David Kinong'o.

  Katika Semina hiyo kulikuwa na mafunzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kilimo cha kisasa cha kutumia Green houses ambapo , wanasemina walipata elimu ya umuhimu wa kilimo hicho ambacho hakichukui nafasi kubwa na kinaweza kufanyika mahali popote na kwa gharama nafuu ambapo kilimo kama cha Nyanya, Matunda na Mboga mboga kinaweza kikafanyika katika Green Houses.

  Pia walipata elimu juu ya ufugaji wa Samaki, Kuku, Kware pamoja na Matumizi ya Mashine za Kisasa za Kutotolea mayai Incubator, Chicken Cages za kisasa ambazo zinasaidia kuwatunza kuku vizuri na kupata faida zaidi, Mashine za kunyonyolea kuku na kutengenezea chakula cha kuku ili mfugaji asipate shida wakati wa kutafuta wapi apate mahali pa kufanya hayo na badala yake kuwa nayo mwenyewe nyumbani.

  Mwisho Mwendesha semina Bi. Mary David Aliwasisitiza watanzania kuwa wanaweza kuwa wajasiliamali na kujitegemea pia kupata kipato kikubwa kama wakifuata hatua bora za kilimo na ufugaji wa kisasa.

  Tembelea Libeneke lake la: www.kukuprojecttz.blogspot.com


   Mjasiriamali na Muandaaji wa wa Semina ya Kilimo na Ufugaji wa Kisasa Bi. Mary David Kinong'o akitoa Maelezo juu ya Kilimo na Ufugaji wa kisasa ambapo aliwasisitiza Vijana na watu wote kujiunga na ujasiliamali na kuunda vikundi mbalimbali ili kujiendeleza kiuchumi.
  Mmoja wa wajasiliamali ambaye pia ni Mkulima na Mfugaji akichangia uzoefu wake wa jinsi alivyo nufaika na mafunzo kama haya na mpaka sasa anajitegemea na Kupata kipatochake na kuwasaidia wengine.
  Wa kwanza Kulia ni Stella mmoja wa akina dada  ambaye amekuwa mfano mzuri wa kuigwa katika semina hiyo akieleza ujuzi  wake umuhimu wa mikutano kama hii ambapo yeye anafanya kilimo cha Mpunga ambapo alianza na kuvuna Gunia Mbili na sasa amefikisha mpaka Tani 100 na zaidi baada ya kupata elimu Bora ya Kilimo.
  Bwana Daniel Ambaye ni Mkulima na Mfugaji akichangia uzoefu wake katika maswala ya kilimo.
  Mwendeshaji msaidizi wa Semina Hiyo Bwana Saidi akitoa mafunzo ya juu ya kuanzisha kilimo kwa kutumia Green House pamoja na faida zake 
  Bize akichukua yale ya Muhimu kabisa katika semina hiyo.
   Wanasemina wakiwa wanasikiliza kwa makina mada mbalimbali ambazo zilikuwa zikitolewa katika Semina ya Kilimo na Ufugaji wa kisasa
   Semina ikiwa inaendelea

  0 0

  MWANAHABARI WA SIKU NYINGI NA ALIYEWAHI KUWA MPIGA PICHA WA KAMPUNI YA TSN (WACHAPISHAJI WA MAGAZETI YA DAILY NEWS,SUNDAY NEWS NA HABARI LEO), BW. BERNARD RWEBANGIRA (PICHANI) AMEFARIKI DUNIA USIKU WA KUAMKIA LEO NA MSIBA UPO NYUMBANI KWAO MBEZI BEACH, JIJINI DAR ES SALAAM.

  MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMINA
  0 0


  0 0

  Mchezaji wa zamani wa klabu ya Barcelona Patrick Kluivert akiwaongoza wachezaji wenzake akiwepo Simao Sabrosa muda mfupi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)
  Wachezaji wa Barcelona wakielkea upande wa watu mashuhuri katika uwanja wa ndege wa Kiamtaifa wa Kilimanjaro (KIA)
  Mchezaji Luis Garcia(kulia) akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro .kushoto ni mratibu wa safari ya wachezaji wa zamani wa klabu ya Barcelona Royco Garcia.
  Wachezaji wa zamamni wa klabu ya Barcelona wakijadiliana jambo katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro muda mfupi mara baada ya kuwasili na ndege ya shirika la ndege la KLM.
  Simao Sabrosa mchezaji wa zamani wa klabu ya Barceona akiwa katika eneo la mapumziko katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro.
  Mchezaji Patrick Kluivert akizingumza kwa simu muda mfupi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro KIA jana usiku .
  Meneja maendeleo wa KiboPalace Hotel ,Charity Githinji akiteta jambo na wachezaji wa zamani wa klabu ya Barcelona walioanza kuwasili nchini kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya wachezaji wa zamani wa Tanzania.

  0 0


  Bishop Hiluka aliyekuwa Katibu wa Taff aliyeng’olewa na Bodi ya Taff .
    Rais wa Taff Simon Mwakifwamba aliyekuwa anatakiwa kung’olewa na katibu wake.

  :- Kwa kusuka mipango ya kumng’oa Rais Mwakifwamba
  NI kikao kilichochukua zaidi ya saa nane kujadili agenda kadhaa lakini iliyoonyesha kuwa ni hatari na kuchukua muda wa wajumbe ilikuwa ni mikakati inayosemekana kusukwa na katibu Bishop Hiluka kutaka kumng’oa rais wa shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifwamba, hatimaye Bodi kwa kupiga kura ikafikia muafaka kuwa katibu aachie ngazi na Rais aendelee na uongozi.

  Awali Bishop alikataa kujiudhuru kwa maelezo kuwa mwenye mamlaka ya kumuwajibisha ni Bodi ya Taff na si Rais wala makamu wake, jambo lilozua mjadala mkubwa baada ya Mwakifwamba kusema kuwa wajumbe wa Bodi haikuwa rahisi kumtambua yeye bila ya yeye kumtambulisha na wajumbe wakampitisha.


  Uhasama uliopo inasemekana kuwa Katibu amekuwa akitoa siri za shirikisho kwa wapinzani na wasilitakia mema shirikisho, jambo ambalo lilimshitusha Rais na kuanza kufanya kazi kwa taadhali huku akimwangalia katibu wake, baada ya kufikia hatua hiyo ndipo Bodi ilipokutana leo ikiwa na nia ya kujadili baadhi ya mikataba ya Taff na wadau wanaotaka kufanya nao kazi.


  Kikao kilibadili mwelekeo baada ya katibu kuleta agenda ya mpasuko ndani Taff ambapo Rais alipinga kuwa agenda hiyo haikuwepo katika agenda zilizopo jambo lililoonyesha kuwa watu hawa hawana mawasiliano pamoja kuwa ni watu wanaotegemea kiutendaji na kuonyesha hofu kubwa hasa pale Mwakifwamba aliposema kuwa hawezi kufanya kazi na Bishop.


  FC iliongea na Katibu Bishop Hiluka baada ya kufikia maamuzi yaliyofikiwa kupigiwa kura za kumtoa katika nafasi yake ya ukatibu wa Taff, alisema kuwa kwake imekuwa nafuu kwani inampa nafasi ya kufanya kazi zake nyingine zenye maslahi tofauti pale sehemu kubwa ya kujitolea na bado kuna majungu.


  “Taff hali ni mbaya tusidanganyane, nimekuwa na mtafaruku mkubwa sana na Mwakifwamba  kiutawala kwani mwenzangu  amekuwa akitengeneza platform ndani ya Taff kunipaka matope na kuzusha mambo ambayo hayana ukweli wala faida kwa tasnia ya filamu Tanzania,”anasema Bishop.


  Bishop anasema kuwa aliomba kujiudhuru zaidi ya mara tatu lakini bodi ya Taff  imekuwa ikimzuia ikitaka asiondoke hadi asimamie uchaguzi upite ndio wangeweza kuangalia njia ya kumpata katibu mwingine hivyo hata alipoambiwa ajiudhuru alisema kuwa alishaomba mara nyingi sana kufanya hivyo akazuiwa.


  “Lakini leo wakaniambia nipumzike nimepata amani kwani nimekuwa nikikosa hata pesa kwa ajili ya familia ya kwa ajili ya Taff, siku za hivi karibuni nilipunguza kabisa kufika ofisini na kuangalia kazi zangu zinazonipa riziki tena kwa amani,”anasema Bishop.  Katibu kasisitiza pia kuwa hata safari alizokuwa akienda Dodoma alikuwa akilipiwa na Bodi ya Filamu kwani yeye ni mjumbe wa Bodi hiyo kwa kifupi Taff hakuna fedha zaidi ya umaarufu tu ambao anasema kwake hauna faida.


  FC ilirudi kwa Mwakifwamba ambaye alikuwa mlengwa mkubwa, alisema kuwa Bishop amekuwa hatari sana akitumika na maadui wa Taff kubomoa shirikisho kwa nguvu zote kwa alibadilika ghafla katika utendaji na kuacha kabisa kufika ofisini.


  “Nimekuwa nikimshangaa sana katibu wangu tunapanga mipango ya kuikomboa tasnia ya filamu hii kwa nia njema kabisa lakini mwenzangu anatumika na maadui kuiteketeza Taff, hivi karibuni alipanga fitina vya kuning’oa uongozi,”anasema Mwakifwamba.


  Mwakifwamba anasema kwa makusudi kabisa amekuwa akimkana katika vikao mbalimbali sambamba kutoandika barua za sehemu husika ikiwa ndio moja ya kazi zake kutofika ofisini bila taarifa tofauti awali alipokabidhiwa ofisi.


  “Leo nilikuwa tayari kuachia ngazi kwani si rahisi kufanya kazi na Yuda Isikalioti ukiwa naye kila siku hilo aliweza Bwana Yesu pekee kwani alikuwa Mungu, maamuzi ya Bodi yametenda haki kwa maslahi ya Taff si yangu wala ya Bishop,”anasema Mwakifwamba.


  Rais huyo amezidi kusisitiza kuwa katibu wake alikuwa akizunguka katika vyama wanachama wa shirikisho kumwaga sumu kwa kumchafua na hata kuwaandaa baadhi ya wajumbe siku ya mkutano mkuu uliofanyika mwaka mwezi wa tatu kumng’oa kwa kuficha nyaraka za ofisi.


  “Hivi karibuni tumeshindwa kuandika barua iliyohitajiwa na Cosota kuipeleka WIPO kwa makusudi kabisa bila sababu za msingi si rahisi kufika huko tuendako kwa stahili hii, bora apumzike na kuwaachia nafasi wengeine wenye spidi ya maendeleo,”anasema Mwakifwamba.


  Wajumbe walioshiriki katika mkutano huo ni John Lister Manyanya, (Mjumbe), Ally Baucha (Mjumbe), John Kallage (Mjumbe) Paul Mtendah (Mjumbe), Deo Songa Njelekela (Makamu wa Rais Taff), Emmanuel Myamba (Mjumbe), Bishop Hiluka (Katibu) na Simon Mwakifwamba (Rais wa Taff).


  Kati ya wajumbe wote ambao hawakupiga kura ni wawili tu ambao walisema hakuna sababu ya kupiga kwani tayari idadi ilipiga kuamuru ajiudhuru kubwa hivyo kuanzia leo Bishop Hiluka si katibu mtendaji wa Taff  Bodi imewajibisha hili kujenga amani na utendaji wa upendo kwa watendaji wa Taff.
  0 0

  MWANAMKE MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA NGWALA WILAYANI CHUNYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ELIZA SWEETY (44) ALIUAWA KWA KUCHOMWA KISU SEHEMU ZA SHINGONI, MGUU NA MKONO WA KUSHOTO NA MKE MWENZA WAKE AITWAE PAULINA EFESTI MWAMBE (46) MKAZI WA NGWALA.
  TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 06.04.2015 MAJIRA YA SAA 20:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA NGWALA, TARAFA YA SONGWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
  INADAIWA KUWA, CHANZO CHA TUKIO HILO NI WIVU WA KIMAPENZI KWANI PAULINA EFESTI MWAMBE AMBAYE NI MKE MWENZA ALIKUWA AKIMTUHUMU MAREHEMU KUPENDWA ZAIDI NA MUME WAO AITWAE GERVAS MWAIPOSI (50) MKAZI WA NGWALA. MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA UPELELEZI ZAIDI UNAENDELEA.
  KATIKA TUKIO LA PILI:
  MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 03 ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA AIRICH JACKSON MKAZI WA IGAWILO ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAPATIWA MATIBABU KATIKA KITUO CHA AFYA IGAWILO BAADA YA KUGONGWA NA MKOKOTENI.
  TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 07.04.2015 MAJIRA YA SAA 15:30 ALASIRI HUKO IGAWILO, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO. JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
  TAARIFA ZA MISAKO:
  KATIKA MSAKO WA KWANZA, JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WANNE WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. VICTOR EDGAR (24) MKAZI WA ILEMI 2. JAMES PASCHAL (21) MKAZI WA PAMBOGO 3. RULES KAJIGILI (27) MKAZI WA MAKUNGULU NA 4. IKE MWAKYAMBIKI (30) MKAZI WA MAKUNGULU WAKIWA NA BHANGI KETE 35 NA MISOKOTO 24 SAWA NA UZITO WA GRAM 295.
  WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 07.04.2015 MAJIRA YA SAA 13:30 MCHANA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA HUKO ENEO LA MAKUNGULU, KATA YA RUANDA, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
  KATIKA MSAKO WA PILI, JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA MAPELELE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MARTHA FUNGO (60) AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 03 NA MTAMBO MMOJA WA KUTENGENEZEA POMBE HIYO.
  MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 07.04.2015 MAJIRA YA SAA 08:00 ASUBUHI KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA HUKO ENEO LA MAPELELE, KATA YA NSALALA, TARAFA YA USONGWE, WILAYA YA KIPOLISI MBALIZI, MKOA WA MBEYA.
  KATIKA MSAKO WA TATU, JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA ILEMBO ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FRANK JOHN (34) MVUVI AKIWA NA NYAVU ZA KUVULIA SAMAKI AINA YA KOKOLO ZILIZOPIGWA MARUFUKU KUVULIA SAMAKI KATIKA ZIWA RUKWA.
  MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 07.04.2015 MAJIRA YA SAA 08:00 ASUBUHI KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA HUKO KATIKA KIJIJI CHA ILEMBO, KATA YA GALULA, TARAFA YA SONGWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA ZINAENDELEA.
  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA NA POMBE MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA WAVUVI KUACHA KUTUMIA NYAVU ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA MAENDELEO YA VIUMBE VYA MAJINI.
  [AHMED Z. MSANGI – SACP]
  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Sayansi,Teknolojia na Mawasiliano,Profesa Patrick Makungu akizungumza na waandishi wa habari leo juu ya utumiaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) katika semina iliyofanyika leo katika hoteli ya New Afrika,Jijini Dar es Salaam.
   Makamu Mkuu wa Chuo cha Bagamoyo.Profesa Costa Mahalu akizungumza na waandishi wa habari leo juu ya utumiaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) katika semina iliyofanyika leo katika hoteli ya New Afrika,Jijini Dar es Salaam.
  Meneja Mradi wa Idara ya Uchumi na Mendeleo ,Mazingira na Utalii wa Afrika Kusini,Rolda Rapotu akizungumza na  katika semina ya wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano iliyofanyika  leo katika hoteli ya New Afrika ,Jijini Dar es Salaam

  =========  ==========  ===========

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
  Wizara ya Sayansi,Teknolojia na Mawasiliano imesema itaendelea kudhibiti matumizi ya mtandao katika kuhakikisha hatumiki vibaya kwa watumiaji.

  Hayo ameyasema leo Katibu Mkuu wa Wizara ya Sayansi,Teknolojia na Mawasiliano,Profesa Patrick Makungu wakati wa Semina ya Maendeleo ya Jamii na Utumiaji Teknolojia ya Habari na Mawasiliano iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya New Africa,Jijini Dar es Salaam.
  Makungu Wizara ya Sayansi,Teknolojia na Mawasiliano imepitisha sheria ya matumizi ya mitandao katika kulinda ili kulinda matumizi hayo yasitumike vibaya na kuharibu sura ya nchi.Amesema kuwa tafiti mbalimbali za mitandao  zimeanza 2010 hali ambayo zinaendelea na kufanya hivyo itasaidia nchi kupata maendeleo katika sekta ya mawasiliano.
  Naye Mratibu wa Semina ya Maendeleo ya Jamii na Utumiaji Teknolojia ya Habari na Mawasilino,Profesa Benson Nindi amesema mradi huo wanafanya katika kutoa elimu juu ya utumiaji wa mitandao na serikali ya Tanzania inatakiwa kutunga sera ambayo itasaidia wananchi kwenda kasi na teknolojia ya habari na mawasiliano.

  0 0

  Wasimamizi wa redio za jamii wakisikiliza kwa makini wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
   Mwenyekiti wa Mtandao wa redio za Jamii, Joseph Sekiku akiongea machache kabla ya kuwagawia wasimamizi wa redio za jamii wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkaazi wa UNESCO nchini Tanzania Bi Zulmira Rodrigez, akiwagawia wasimamizi wa redio za jamii katiba iliyopendekezwa iliwekwa kwa nji ya sauti.

  Wakurugenzi na viongozi mbalimbali wa Radio za jamii wamethibitisha kupokea na kuanza kurusha Katiba Inayopendekezwa kwa njia ya sauti, makala na michezo ya radio iliyoandaliwa na Kampuni ya Focus Media na COMNETA zenye maudhui ya katiba inayopendekezwa.

  Wakizungumza na Focus Media ambao ndio waandaaji na wasambazaji wamekiri kwamba wamepokea kwa wakati muafaka, kwani hawakuwa na chanzo sahihi cha kupata maudhui yanayohusu elimu ya uraia na uchaguzi mkuu na kura ya maoni.

  Baadhi ya wasimamizi wa radio zilizo katika mtandao wa radio za kijamii Community Media Network of Tanzania ambao wamethibitisha kupokea vitendea kazi hivyo ni Bw. Ali Khamis Mtwana, Mkurugenzi Mtendaji wa Tumbatu Island Community Radio, Bw. Anton Masai Triple A FM Arusha, Dr. Lazaro Ole Mongoi Mkurugenzi Mtendaji wa IDEA Radio, Henry Bernard, Adelina Lweramla, Jackson Mollel, wa ORS FM Arusha, Edwin Mpokasye, Radio Fadhila Mkurugenzi Radio Kwizera- Ngara.

  Vipindi vinapokuwa vikiruka hewani wasikilizaji wamekuwa wakishiriki kwa kupiga simu na kuuliza maswali ilikuelewa zaidi Katiba Inayopendekezwa.

  Wengine wanapiga simu kupongeza na mnamichezo ya radio ilivyoratibiwa vizuri na ikielimisha jamii juu ya mambo mbalimbali muhimu.
  ILI KUSIKILIZA VIPINDI HIVI VYENYE MAUDHUI YA KATIBA INAYOPENDEKEZWA TEMBELEA 
  www.facebook.com/KatibaInayopendekezwaTanzania

older | 1 | .... | 499 | 500 | (Page 501) | 502 | 503 | .... | 1898 | newer