Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 3 | 4 | (Page 5) | 6 | 7 | .... | 1897 | newer

  0 0


  THE Board of Directors of Tanzania Standard (Newspapers) Limited (TSN) has appointed Mr Gabriel Nderumaki (pictured), the company’s Acting Managing Editor effective December, 24, this year.

  According to a statement issued by the company yesterday, Mr Nderumaki takes over from Mr Mkumbwa Ally, after expiry of his contract with the company on December 15.

  The new acting Managing Editor has been with TSN for over 20 years and served in senior editorial positions including Sports Editor, News Editor and Business Editor.

  “I am ready for the new challenge and looking forward to getting maximum co-operation from readers, government, private sector and all other stakeholders,” Mr Nderumaki.

  He pledged that under his leadership, TSN who are the publisher of Daily News, Sunday News, Habari Leo, Habari Leo  Jumapili and SpotiLeo, will continue to publish well researched educative and informative, as opposed to unreasonable sensational articles.
  “We will continue to publish informative stories in support of the government’s initiatives to improve the lives of Tanzanians and when necessary provide constructive criticism, as opposed to unreasonable sensational articles.
   
  “To investors and those in the private sector, we will continue writing balanced and educational stories about their role in national development,” he said.

  TSN is a registered company and has been in the newspapers industry for more than 70 years. The company is currently wholly owned by the government

  0 0  0 0


  Sam Machozi a..k.a Sam Mapenzi akiongozaji waimbaji wenzake Aneth Kushaba (kushoto) sambamba na Sony Masamba wakitoa burudani ya aina yake Ijumaa ya mwisho kwa mwaka 2012 katika kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar es Salaam. (Picha na Mo Blog).
  Sura mpya ya SKYLIGHT Band ikifanya yake Jukwaani katika show ya mwisho ya Band hiyo kwa Mwaka 2012 iliyofanyika Ijumaa ya tarehe 28 mwezi huu katika kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar es Salaam. Si mwingine ni Binti mdogo mwenye kipaji cha aina yake mshindi wa pili katika shindano la Epiq Bongo Star Search 2012 Salma Yusuf sambamba na Meneja wa Band hiyo Aneth Kushaba AK 47 wakiwapa raha mashabiki wa bendi hiyo.
  Carolina mama njoo tucheze pamoja..... Moja ngoma inayobamba mujini ya SKYLIGHT BAND katia vituo mbalimbali vya radio hapa nchini. Mungu akipenda Usikose Ijumaa hii ya kwanza kwa Mwaka 2013.
  Palikuwa hapatoshi..... kwa raha zao.
  "Gere Mama Gere..... Wanionea Gere....." Binti mwenye kipaji sauti ya kasuku Salma Yusuf akiwazungusha mashabiki wa SKYLIGHT BAND kwa mduara akipigwa tafu na Joniko Flower pamoja na Sony Masamba katika ukumbi wa Thai Village jijini Dar.
  Pichani Juu na Chini Wake kwa Waume wakizungusha mduara huku wengine wakimwaga radhi hapo kati..Hapo chacha.
  Chezea Salma Yusuf wewe ulizoe kumuona kwenye TV wakati wa EBSS 2012 njoo umuone Live Ijumaa akitambulishwa rasmi kwa mashabiki wa SKYLIGHT BAND.
  Wadau wakishow love katika ukumbi Thai Village Masaki jijini Dar.
  Vijana Watanashati wakipata Ukodak...Single Ladies mpooooo??? Kazi kwenu.
  SKYLIGHT BAND ilipata ugeni kutoka The B Band ya Banana Zorro. Pichani ni Aneth Kushaba AK 47 akishow love na baadhi ya wasanii wa The B BAND.
  Mdau King Kif akishow Love na Aunty Ezekiel a.k.a Mrs. Demonte pamoja na rafiki yake katika usiku wa SKYLIGHT BAND.
  Mdau Eric Ndalu katika pozi.
  Kati ya Vijana hawa wawili walikuwa wakisheherekea siku yao ya kuzaliwa ndani ya Kiota cha Thai Village na SKYLIGHT BAND.
  Wadau wakipata Ukodak mbele ya Camera yetu.
  Sam Machozi a.k.a Sam Mapenzi na rafiki yake Mwinyi wakishow love.
  Wadau wa SKYLIGHT BAND.
  Mbavu nene zilihakikisha Ulinzi na Usalama unakuwepo.

  0 0
 • 12/31/12--00:37: New Year Events

 • The Good Life East Africa’s New Year’s Eve Party Lineup (Tanzania)

  So The Good Life knows that many of you are waiting until the very last minute to make a plan for New Year’s Eve, so being the good citizens that we are, we are going to help you make your decision for tonight by listing all of the places and parties that The Good Life will be tonight. Karibu!


  Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro.


  This year Moet & Chandon has partnered with the Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro, to ensure that there is something for everyone under one roof this New Year's Eve.  For those that are looking for a quiet yet intimate way to bring in the New Year, the award winning Oriental Restaurant provides the perfect destination for reflection of this past year's highlights and for declaring resolutions for the year to come. The Oriental will be transformed with amazing decor from Moet & Chandon and all guests will receive a complimentary glass of Moet & Chandon to toast the New Year. Space is very limited so guests are encouraged to book in advance. 0764 70 1234


  For those that want to bring in the New Year with banging beats, Rouge Night Club, located at the Hyatt Regency offers an exclusive destination for music and entertainment on New Year's Eve.  With one of the best sound and light systems in all of East Africa, guests at Rouge will be treated to a delightful sensory session. All guests at Rouge will be greeted and treated with a complimentary glass of Moet & Chandon in the Moet Lounge located on the rooftop of Rouge.  In the Moet Lounge guests can dance the night away and bring in 2013 with style. Admission: 50,000/= 0764 70 1234. 

  Akemi

   It is a night in the stars and with the stars at Dar’s Revolving Restaurant.  Tonight at Akemi guest will enjoy a 5-course set dinner menu, a complimentary glass of Moet & Chandon in the Moet Lounge, a live band and DJ, and of course a view like no other to welcome in the New Year. $100 +255 687 360 360 info@akemidining.com. 

  Club 327                      


  Hennessy and Club 327 have created a New Year’s Eve party for those of you that love good as DJ Topspin from the United States will be the Soul Controller and is guaranteed to keep you on the dance floor all night long.  When you want to cool your heels why not take a seat in one the 3 Moet-Hennessy Ultra VIP suites. 30,000/=  +255789236052. 


  Mlimani City


  If you are like Belvedere and consider yourself fashionable and fabulous then Mlimani City is your destination tonight for the annual Grown & Sexy: New Year’s Eve party.  DJ Global from Uganda has the music covered so come out to party the night away with some of the biggest names in fashion and entertainment. 30,000/= / VIP 50,000/= 0767 558 619


  Wherever you go tonight The Good Life encourages you to be responsible and bring in 2013 safely. Happy New Year!

  www.Facebook.com/TheGoodLifeEA / www.Twitter.com/TheGoodLifeEA  0 0


  0 0


  Utamaduni wa watanzania kujiunga na huduma za Bima nchini kama njia mojawapo ya kukabiliana na gharama za majanga na matukio mengine ya asili ikiwemo kifo umeaonekana kuongezeka kufuatia kuwepo kwa urahisi wa kukata na kujiunga na bima kupitia simu za mkononi. Kuongezeka kwa utamaduni huo wa kukata bima kunasaidia kuondokana na dhana ya kwamba kukata bima ni sawa na kujitakia majanga jambo mbalo hata hivyo halina ukweli na badala yake bima imekuwa msaada mkubwa kwa wanajamii katika kumudu gharama zitokanazo na majanga na matukio mengine yasiyoweza kuepukika.

  Kuwepo kwa urahisi huo ni matokeo ya ubia wa kibishara kati ya kampuni ya Bima ya Heritage na Kampuni ya Vodacom Tanzania ambapo sasa mteja wa Vodacom ameewezeshwa fursa rahisi na ya uhakika ya kujiunga na huduma za bima kupitia simu za mkononi kutumia huduma ya M-pesa. Hii ni huduma ya kwanza na ya aina yake inayopatiakana Tanzania pekee. “Tumeshuhudia mageuzi makubwa katika sekta ya bima nchini tangu tulipoanzisha utaratibu wa kukata bima kupitia simu za mkononi huku mteja akifanya malipo ya bima yake kwa njia ya M-pesa, tunaamini ubia huu umekuwa wa faida kubwa kwa jamii.”Amesema  Mkuu wa Kitengo cha huduma za bima wa kampuni ya Heritage Tanzania, Bw. Joseph Mardai.

  “Ni wazi sasa upo urahisi na jamii inaanza kuona umuhimu wa bima. Tayari watu kadhaa wameshafanikiwa chini ya mpango huu ambapo kampuni ya Heritage Tanzania imeweza kuwalipa wanufaika wa bima hizo za Upendo na Faraja kiasi cha fedha kusaidia gharama za mazishi kwa urahsi zaidi kupitia M-pesa, hakuna usumbufu wala gharama za ziada.”Ameongeza Mardai.

  Mardai amesema mabadiliko ya kifikra yanayoanza kuonekana hivi sasa nchini kuhusu huduma za bima hasa kwa bima zinazohusisha vifo kutasadia kwa kiwango kikubwa namna jamii inavyoweza kuondokana na hofu na mzigo mkubwa wa kugharamia shughuli za mazishi na matibabu “Hakuna anaependa kuzungumzia kifo lakini tunapogundua kwamba hakuna mwenye uwezo wa kukizuia wala kutambua ni wakati upi kitamfika ni dhahiri tunapaswa kutafakari namna bora ya kupunguza mzigo kwa familia zetu katika kugharimia shughuli za mazishi.” Amesema Mardai Na kuongeza kuwa “Huduma za Faraja na Upendo inatoa namna bora ya kupata suluhisho.”


  Chini ya utaratibu wa ukataji wa bima kwa njia ya M-pesa mteja anaweza kukata na kulipia bima yake wakati wowote na mahali popote na hata kupokea fidia ya malipo ya bima yake pale tatizo lililokatiwa bima linapotokea ambapo fedha hizo hupokelewa na wanufaika aliowaandikisha kwenye mkataba wa bima.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza amesema ubunifu katika Vodacom unaendelea kudhihirisha azma ya kampuni hiyo katika kubadil na kurahisisha maisha. “Tumekuwa na dhamira hiyo ya kuhakikisha teknolojia ya simu za mkononi haishii katika kupiga na kupokea simu au kutuma ujumbe mfupi wa maneno tunataka kuona maisha ya watu yakiwa rahisi na mepesi zaidi kupitia simu zao za mkononi. Huduma hii ya Bima ni uthibitisho mmojawapo wa dhamira inayotuongoza katika biashara.”Amesema Meza.

  “M-pesa imeleta mapinduzi makubwa hapa nchini jinsi jamii inayoishi, hatuna sababu yakurudi nyuma tutaendelea kuongoza katika ubunifu na kuziunganisha huduma mbalimbali katika mfumo wa M-pesa ili kuzileta karibu na wananchi.”Alisema Meza na kuongeza “Tayari kwa sasa biashara nyingi zimeshaunganishwa na mfumo wa M-pesa kuanzia usafiri wa anga, malipo kwenye maduka makubwa – Supermarkets, uchangijaji katika mifuko ya hifadhi ya jamii, malipo ya ving’amuzi n.k.” 
  Hivi karibuni kampuni ya Heritage ililipa wateja wake wawili wa kwanza kabisa tangu kuanza kwa huduma ya bima kwa kwa njia ya M-pesa.

  Wateja hao ni  mke wa Bw. Mathias Mahunda, Bi. Fransisca Mahunda ambae mumewe alikuwa mteja aliyekuwa na Bima ya Upendo aliyefariki dunia Novemba 17, mwaka huu ambae alilipwa kiasi cha sh, milioni mbili. Mwengine aliyenufaika na bima hiyo ni mke wa marehemu Kulwa Mtangaki, Bi. Julieth Mtangaki, ambaye mumewe marehemu Bw. Mtangaki alifariki dunia Novemba 12 kwa ajali na bima yake ya Faraja iliwezesha mkewe kupewa kiasi cha sh. 200,000 kama kusaidia gharama za Maziko.

  Katika hatua nyengine wateja mbalimbali wa Vodacom wamekuwa wakinufaika na huduma za bima kwa kupatiwa Sh. 200,000 kama promohseni ya kufanya miamala kumi ndani ya kipindi cha mwezi mmoja.
  “Kila mteja wetu anaefanya miamala kumi kwa mwezi tunamzawaidia bima ya Sh. 200,000 katika mwezi unaofuata ambayo hudumu kwa kipindi cha mwezi mmoja na anaweza kunufaika na fidia ya bima iwapo atakutwa na umauti ndani ya kipindi hicho cha mwezi mmoja fedha ambazo hulipwa kwa wanufaika anaowapendekeza.”Alisema Meza.

  Mteja hupaswa kuandikisha majina ya wanufaika wake kupitia utaratibu unaoelezwa kwenye ujumbe mfupi wa maneno anaotumiwa kujulishwa kuhusu kuingiziwa kiasi hicho cha fedha (200,000) katika akaunti ya bima. 

  0 0


  Kocha mpya wa Simba Patrick Liewing atua Dar


  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

  Kocha mpya wa Simba, Mfaransa, Patrick Liewing pichani, aliyeshika nguo nyekundu mkononi, amewasili leo saa saba za mchana kwa ajili ya kuinoa timu ya Simba.

   Uongozi wa Simba, kwa kupitia Katibu Mkuu wao, Evodius Mutawala, alikuwa miongoni mwa wadau wa michezo waliompokea Liewing katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.

  Kocha huyo anawasili huku akiikuta timu ya Simba ikiwa chini ya Jamhuri Kihwelo Julio, kocha ambaye amekuwa na mapenzi makubwa na klabu hiyo kila wakati kwa kitendo chake cha kukubali kuinoa timu hiyo.

  Mengi juu ya ujio wa kocha huyo raia wa Ufaransa, yatasikika baada ya kufanya mazungumzo ya mwisho na kuingia makubaliano rasmi ya kuinoa Simba, yenye kipindi kikubwa cha kurudisha imani kwa wapenzi na wanachama wao.

  Simba ilimaliza mzunguuko wa kwanza wa ligi ya Tanzania kwa kushika nafasi ya tatu, nyuma ya timu ya Yanga na Azam FC.Habari picha kwa hisani ya http://handenikwetu.blogspot.com

  0 0


  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akikabidhi Mbuzi kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Tushikamane Children Care Trust Fund Bw. Gratho Messy Mbele (wa kwanza kulia) na Mkuu wa Shule ya Tushikamane Bi. Euphrosine Mtundu, kama zawadi kwa watoto yatima wa kituo hicho ambapo panapo majaliwa hapo kesho atajumuika nao kupata chakula cha mchana. Anayeshuhudia tukio hilo ni Diwani wa Kata ya Tabata Hajati Mtumwa Mohamedi (wa pili kushoto)
  Mstahiki Meya Jerry Silaa akikabidhi ndoo ya mafuta kwa kituo hicho chenye lengo la kuhudumia watoto yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi kwa kuwapa mahitaji muhimu kama vile elimu, afya, chakula, malazi, mahitaji ya shule, pamoja na huduma za kisaikolojia na ulinzi dhidi ya manyanyaso.

  Viongozi wa kituo hicho wakimshukuru Mstahiki Meya Jerry Silaa.

  Meya wa Manispaa Mstahiki Jerry Silaa akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi wa kituo hicho mara baada ya kukabidhi zawadi za vyakula ikiwa ni mchango wake kwa vijana hao katika kusherehekea mwaka mpya 2012/2013.

  Kila mwaka wakati wa sherehe za mwaka mpya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala yeye binafsi hutoa sadaka kwa wahitaji kwa kumshukuru Mungu kwa kumuwezesha kumaliza mwaka salama.

  Leo Mstahiki Meya Jerry Silaa ametoa chakula kwa kituo cha Watoto Yatima na watoto Yatima na watoto Waishio Katika Mazingira Hatarishi cha Tushikamane Children’s Care Trust Fund ambapo pamanapo majaliwa hapo kesho atakula chakula pamoja nao.

  Asasi hiyo ya Tushikamane Children’s Care Trust Fund ilianzishwa mwaka 2001 na kupata usajili wa kudumu mwaka huo huo ili iweze kujiendesha kwa mujibu wa sheria za nchi.

  0 0


  Mwaka 2012 ndio huoo umetokomea, ni vizuri kuangalia yaliyopita ili kujitayarisha na yajayo. Muziki wa nchi yetu ulitawaliwa na muziki wa Bongoflava, Taarab, muziki wa bendi, matarumbeta, muziki wa Enjili, na muziki wa kiasili. Si siri kuwa muziki wa Bongoflava ndio uliokuwa ukitawala katika vyombo vya habari na sehemu nyingi za maonyesho ukifuatiliwa na muziki wa Taarab na muziki wa enjili. 

  Katika muziki wote huu jambo lililokuwa wazi ni kuwa waimbaji ndio waliokuwa wakipewa kipaumbele katika tasnia hii. Waimbaji katika aina zote za muziki uliotajwa hapo juu ndio waliotajwa na kupewa sifa kwa ubora wa muziki. Kumekuweko na mashindano kadhaa ambayo yote yamejikita katika kutafuta vipawa vya waimbaji japo mara nyingi yamejitambulisha kama mashindano ya kusaka vipaji mbalimbali. 

  Hakuna ubishi muziki wa dansi na muziki wa asili ndio muziki uliopewa muda mchache sana katika vyombo vya habari. Na hata katika muziki huo, bendi ambazo zimejikita kufuata mipigo ya Kikongo vilipewa nafasi zaidi ya bendi ambazo zimejichagulia njia nyingine za muziki wao.

  Kuna sababu kadhaa ambazo zimefanya muziki wa bongoflava kuchukua nafasi zaidi katika vyombo vya habari, la kwanza ni uwingi wa kazi za bongoflava zinazorekodiwa. Karibu kila mji una studio ya aina moja au nyingine, na katika studio hizo kazi nyingi zaidi zinazorekodiwa ni aina hiyo ya muziki, hivyo kutokana na uwingi wa kazi hizo ni wazi kabisa ndizo ambazo zitaendelea kutawala anga la vyombo vya habari, na pia ni kutokana na mfumo wa vyombo vyetu vyote kujikita katika mfumo wa aina fulani tu za muziki.

  Kwa mtizamo wangu heka heka za muziki wa Enjili zilipungua 2012. Yale matamasha makubwa ya muziki huo yalipungua sana, na hata nyimbo za kushtua jamii hazikuwa nyingi  kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
  Muziki wa Taarab haujaleta mabadiliko kimuziki, mengi yaliyofanywa katika 2012 ni marudio tu ya ubunifu uliofanyika nyuma. Kama vile uanzishwaji wa kucheza show katika taarab, upigaji wa gitaa na kuliachia pekee yake kama ilivyokuwa kwa bendi kuachia gitaa la rhythm miaka kabla ya tisini na zile video za kucheza mbele za viwanja vya hoteli. Kumekuweko tu ubunifu wa misemo na mipasho, jambo tena ambalo limesababisha kuenziwa zaidi kwa waimbaji tu katika fani hiyo pia.

  Bendi ziko katika wakati mgumu, wakati wanamuziki wengi wa bendi wakilalamika kuwa muziki wa bendi haupigwi, kumekuweko na jitihada ndogo za bendi kurekodi nyimbo mpya, maelezo mengi yamekuwa ni kuhadithia enzi ambapo muziki wa bendi ulitawala na kuona kama hiyo ni sababu tosha ya muziki huo kurushwa hewani. Bendi chache zilizorekodi hazijaja na  nyimbo zilizoweza kuteka umma wa wa Tanzania na hivyo kusababisha muziki huu kukosekana katika anga za muziki. Matangazo mengi ya muziki wa dansi yamekuwa ni kutangaza rap mpya au kupatikana kwa msanii mpya, lakini kiujumla hakujakuwa na kitu kipya katika muziki wa bendi.

  Muziki asili pia umekosekana kwenye vyombo vya habari kwa kuwa si vikundi vingi vya muziki huu vyenye uwezo wa kulipia gharama za studio ambao muziki huu unastahili kurekodiwa. Studio nyingi zimejengwa kwa ajili ya muziki wa aina ya Bongoflava tu, zile studio za kuweza kuruhusu kundi la muziki wa asili kurekodi gharama yake huwa ni kubwa sana. 

  Kundi la Makirikiri lilitakiwa kuwa elimu tosha kwa wasanii wa muziki wa Kiasili, kuwa na muziki huo ukifuata taratibu nzuri ya kurekodiwa unauza vizuri sana, bahati mbaya kuna vikundi sasa vimeacha muziki na ngoma zao, vinaiga uchezaji wa  Makirikiri.

  Pengine watu watasema nimesahau muziki wa kwaya, sijausahau, kwa kweli muziki huu umebaki  hasa kwenye muziki wa Enjili. Hapo zamani ulikuwa ukitumika sana kwenye siasa na kampeni , lakini kwa mwaka 2012 hali imekuwa mbaya kwa muziki huu.

  Pamoja na kuwa wengine wangeweza kusema tunasonga mbele katika muziki, kwangu mimi naona tunarudi nyuma kitaaluma. Tasnia inaingiza pesa nyingi zaidi, na hata kuna wasanii walioingiza pesa nyingi sana, lakini  kwangu hilo si kipimo cha maendeleo katika tasnia hii.

  Kama nilivyoanza kusema washika maikrofon wamekuwa ndio alama ya muziki wa Tanzania. Muziki ni zaidi ya kuimba. Katika kuimba sauti nzuri ya muimbaji ni muhimu, na ninashukuru kwa hilo tunao waimbaji wazuri wengi sana, lakini ule muziki unaomsindikiza muimbaji ni muhimu sana kwani ule hauna mipaka wala lugha, na ndio unaoweza kutufungulia mlango wa soko la kimataifa. 

  Wengi tunapenda sana muziki wa kutoka Kongo, Nigeria, South Africa, pamoja na kuwa hatujui hata moja wanaloliongelea tunaupenda muziki huo kutokana na mpangilio wa vyombo vyao. Kutokujali wapigaji katika mfumo wa nchi yetu ndio unatupelekea kuwa watu wa ‘copy and paste’ wa upigaji wa muziki wa nchi nyingine. Ukiorodhesha nyimbo zote zilizotikisa nchi hii kwa mwaka 2012 utagundua asilimia kubwa ya muziki uliotumika ulikuwa ni wa kunakili kutoka muziki wa nchi nyingine, Nigeria, Congo na Afrika Kusini ndio wamekuwa waalimu wetu wakuu.

  Ushauri kwa maproducer wa Bongoflava, kuangalia pia muziki wetu wa asili humu ndani ya nchi ili tuje tumalize 2013 na kitu chetu ambacho Wanaigeria, Wakongo nao pia waige toka kwetu. Inawezekana sana maana wimbo wa Weekend wa Afro70 uliwahi kuweko katika  kumi bora 1972, Nigeria.

  Muziki wa Enjili pamoja na kuwa ndio unaotegemewa kutufundisha maadili, ulikuwa na kasoro moja kubwa nayo ni kukosa maadili kwa kucopy na kupaste. Nyimbo nyingi zilizokuwa maarufu na kuteka hisia za maelfu ya watu zilikuwa ni kuiga moja kwamoja kutoka Afrika ya kusini. Najiuliza je ndio kilichopunguza moto wa muziki huu 2012? Kulikuwa hakuna za kukopi? Wanamuziki wa Enjili kama ilivyo kwa ushauri kuhusu Bongoflava, ni muda wa kurudi nyuma na kutumia raslimali ya utamaduni iliyoko kuleta mabadiliko na kukuza soko la muziki huo.

  Tasnia ya muuziki wa Tanzania katika tafiti moja wapo umeitwa ‘the radio-driven contemporary music industry’. Kwa maneno rahisi, tasnia ambayo imekuwa inaendeshwa na radio. Radio zimekuwa na uwezo wa kumpandisha na kumshusha mwanamuziki, kumtafutia soko, kumzibia soko na kadhalika. Hali hii ikisindikizwa na rushwa ambayo imetapakaa katika jamii yetu, unapata picha kuwa kungeweza kukawa na sura bora au tofauti ya muziki hali isingekuwa ilivyo. Kuna ripoti za watu kutoa hongo nyimbo za wenzao zisipigwe, hongo ili nyimbo zipigwe, visasi vya kuzuia nyimbo zisipigwe na kadhalika. 

  Na katika jamii ambayo imekuwa na kawaida ya kutegemea vyombo vya habari kujua muziki gani mpya na mzuri, uwanja huu si uwanja ulio tambarare hata kidogo. Bahati mbaya inaonekana wenye vyombo hivi wako mbali na ukweli unaoendelea katika vyombo vyao au kwa kutokujua au kupuuza. Janga hili limevikumba hata vyombo ambavyo vinaendeshwa na taasisi za dini. Wanamuziki wa muziki wa Enjili nao pia wanalia kudaiwa rushwa na watangazaji wa radio za Enjili!.  

  Nakumbuka siku niliyopata nafasi kuongea na kiongozi mmoja wa dini ambaye Kanisa lake linaendesha kituo cha radio, nilipata mshangao baada mkuu huyo, kuanza kutetea watangazaji wake badala ya kuamua kufanya uchunguzi wa tuhuma.

  Umefika muda wa radio kuanza kujigawa kimuziki. Ni kichekesho mji kuwa na vituo vya radio 30 halafu vyote vinapiga aina hiyohiyo ya muziki, wakati kuna aina mbalimbali za watu. Ajabu ni kuwa wenye radio wanajua kuwa katika nchi nyingine unaweza kukuta radio iliyoamua kupiga aina fulani tu ya muziki, Jazz Radio, Country music Radio, Classic Music Radio, lakini hilo limekuwa gumu kwao kutekeleza hapa. Kuwe na utofauti, Wasikilizaji tuko wa aina tofauti.

  Vyombo vya habari viijitahidi kupata wataalamu husika wa aina tofauti za muziki, muziki unaviingizia vyombo hivyo mabilioni ya fedha, vyombo vya habari  viupe heshima yake. Bila muziki hakuna radio.Magazeti yamekuwa mstari wa mbele katika kutangaza aina mbalimbali za wasanii na sanaa. Pamoja na hongera kwa kazi nzuri lakini bado kuna nafasi kubwa ipo tupu, hakuna wataalamu wa uandishi wa habari za muziki. 

  Hivyo habari nyingi za muziki zinaandikwa na waandishi kama wapenzi wa muziki na si wataalam wa uandishi wa muziki, jambo ambalo liko tofauti na uandishi wa michezo kwa mfano soka. Unaweza ukasoma habari ya soka ambapo mwandish atakueleza nafasi za wachezaji, kama ni faulo, ni nini kilisababisha, na kama ni goli lilikuwa ni la kichwa au kona au penalty, hili haliko katika muziki. Utaambiwa tu  bendi ilipagawisha, au msanii fulani ateka nyoyo za wapenzi, na maelezo ya juu juu kama yale, kunahitajika kuanzishwa mafunzo ya elimu ya uandishi wa kazi za sanaa. 

  Hili litapunguza hata vurugu kama zilizotawala  mwaka huu ya wapiga picha kufikia hata kulala chini ili tu wapate picha ya nguo za ndani za msanii na hayo ndio kuwa maelezo makuu ya onyesho zima la muziki.Ikiwa kulikuwa na mchango wa serikali katika muziki, basi ulikuwa mdogo au ulikuwa ni kwa shughuli maalumu lakini si kwa kutengeneza mazingira ya kuwezesha unafuu kwa wanamuziki kwa ujumla. 

  Idara ya Utamaduni imeendelea kupata bajeti ndogo ambayo imefanya Baraza La Sanaa La Taifa kuendelea kubaki Dar es Salaam tu, likibangaiza kuweko kwa kutegemea kutoa vibali mbalimbali kwa wasanii, na nguvu zake kuonekana Dar es Salaam tu. Na kwa kuwa hakuna Maafisa Utamaduni Mkoa, na Maafisa Utamaduni Wilaya na Manispaa wako chini ya serikali za mitaa hivyo kuwa wizara tofauti na Waziri wa Utamaduni, nguvu za serikali katika utamaduni ni 0. 

  COSOTA chombo ambacho shughuli yake ilikuwa ni kulinda hakimiliki za wasanii na ambacho kilikuwa chini ya wasanii, kwa kinyemela kabisa kimerudishwa katika mikono ya serikali, lakini bado kinakusanya mirabaha 'kwa niaba ya wasanii' huku kukiwa na bodi isiyo na uwakilishi wa wasanii kuanzia 2007. Swali utakusanyaje pesa kwa iaba yangu lakini huniruhusu kujua ni kiasi gani umekusanya, unazitumiaje na ukiulizwa unakuwa mkali!!!!!!? Kuna wasanii wamekuwa wakidai kurudishiwa COSOTA, ushauri wangu wasanii wakae wajipange  na kuelewa vizuri sheria ya Hakimiliki kabla ya kujitwishwa zigo hilo la miba.

  Katika miezi 6 ya mwisho ya 2012 kumejitokeza spidi kali ya Mamlaka ya Ukusanyaji wa Mapato kutengeneza mazingira ya kukusanya mapato kutokana na mauzo ya kazi za muziki na filamu. Kimsingi kulipa kodi ni wajibu wa kila mwananchi na wasanii ni wananchi pia, lakini taratibu zake ndio zinanipa utata, hasa pale ambapo kwa muda mrefu imekuwa ikitangazwa kuwa njia hii itasaidia wasanii kwa kupunguza kuibiwa.

  Sentensi hii inaonyesha wazi anaeiongelea aidha hajui mfumo wa biashara ya kazi muziki, au kwa makusudi anapotosha ili kuficha kitu. Wasanii wengi huwa wamekwishalipwa kwa kazi ambazo zimesambaa na ziko barabarani zinaibiwa, wanaoibiwa ni wasambazaji. Hivyo kulinda kazi hizo unamlinda msambazaji si msanii. 

  Pia kuanza kukusanya kodi kwa kazi hizi kumepewa jina ‘kurasmishwa  kwa kazi ya usanii’, kuna mabilioni wasanii wanatakiwa walipwe na watumiaji wa kazi za sanaa, kama radio na TV, mapromota, waajiri na kadhalika  hakuna anaeliongelea hilo wala hakuna anaetamka takwimu hizo. Kuna kazi ya kurudisha mitaala ya masomo ya sanaa mashuleni, kurudisha vyuo vya walimu wa sanaa, kurudisha maafisa utamaduni kuwa chini ya Wizara ya Utamaduni kuwawezesha kufanya kazi zao kadri ya sera ya Utamaduni, na mengine mengi ya aina hiyo ndio ningeona kurasimisha kazi za sanaa, lakini kukusanya kodi tu kwa kazi ambazo hata hivyo mikataba yake mingi inautata na kuita urasimishaji si sahihi.
   
  Katika nchi nyingi critics au watu ninaoweza kuwaita kiswahili wakosoaji, huwa ni muhimu katika maendeleo ya sanaa, watu hawa hupata heshima kutokana na kuweza kuangalia mapungufu katika kazi za sanaa na kuyasema, jambo ambalo hupelekea wasanii kujirekibisha na kutengeneza kazi bora zaidi. Hapa kwetu kutoa ushauri ni kutafuta matusi, toka kwa wasanii wenye kazi husika, vyombo vya habari na hata sehemu ya jamii, umefika muda wahusika kuchukua uchambuzi kama changa moto za kuboresha kazi.

  Niliyoyataja hapa yote yako wazi ninachotegemea ni kuona 2013, hatua zinaanza kupigwa kurekibisha, ili wanamuziki wa nchi hii nao wapate nafasi sawa na wengine wa nchi nyingine.

  John Kitime
  31.12.2012
  Sinza, Dar es Salaam


  0 0

  Wapendwa ndugu,jamaa na marafiki popote pale mlipo,yamebaki masaa kadhaa kuuaga mwaka 2012,ambao kwa hakika ulikuwa na changamoto nyingi za kimaisha,dhoruba za hapa na pale wengi zilitukumba,lakini kwa kudra za Mwenyezi Mungu akatushika mkono akatuinua na maisha yakaendelea.

  Binafsi mpaka dakika hii namshukuru Mungu nikiwa mwenye afya njema kabisa.Maisha ya sasa Wanadamu wengi wamekuwa dhaifu kwa mambo mengi,lakini Mungu ndiyo njia sahihi wa kumtumia katika sala zako kuyashinda majaribu na madhaifu ya Dunia.Yako mengi ambayo naweza nikayaandika hapa lakini bado yasitoshe pia.Nasema asanteni kwa ushirikiano wenu mkubwa kwa namna moja ama nyingine,kama kuna mahali nilikosea,tukakwaruzana kidogo basi "NAFSI NI NYONGE" Tusameheane na maisha  yaendelee.

  Tunahamia mwaka mwingine mpya kabisa 2013,basi na tuendelee na ushirikiano huu tuliokuwa nao kwa mambo mbalimbali yenye kujenga na kuleta tija katika maisha yetu,Mwaka 2013 uwe wa kuhakikisha kweli sote pia tumehamia kwenye mfumo wa kidijitali,tushauriane,tuelemishane tunyooshane njia iliyo sahihi ili kila mmoja kila wakati abaki nafsini mwake mwenye furaha daima,Pia tumtangulize Mungu kila wakati kwa kila jambo ili pia azidi kuzibariki kazi za mikono yetu daima.

  Kwa Blogaz wenzangu,changamoto nyingi tumekumbana nazo 2012,ikiwemo tatizo kuu la KUKOPY NA KUPASTE.! Na nyinginezo nyingi tuzijuazo zinatusumbua kwa namna moja ama nyingine,basi ni nyema 2013 iwe ya kuzitafutia ufumbuzi,kama si kuzimaliza kabisa basi angalau tuendelee kuzipunguza ili kuzimaliza kabisa,huku suala la kujituma na ubunifu vikiwa ndio ngao kuu ya mabadiliko miongoni mwetu.Ushirikiano tuliokuwa nao umeonesha tuna uwezo mkubwa wa kuisadia jamii inayotuzunguka na hata serikali pia kwa namna moja ama nyingi,basi tusimame kidete kuhakikisha ushirikiano huu hauteteleki ama haupotei kirahisi,badala yake tuiimarishe zaidi kila kona .

  Natoa shukurani za dhati kabisa kwa makampuni na wadau mbalimbali ambayo/ambao kiukweli yametoa mchango mkubwa kuhakikisha tunasonga mbele na libeneke hili ,si vibaya nikiyataja makampuni hayo kuwa ni Serengeti Breweries Ltd,Airtel,Bayport,Msama Promotions Ltd,kampuni ya R&R,Dada Teddy Mapunda,Hoyce Temu,Blogaz wote (bila kinyongo) na wengine waliotupa hatua ya kusogea kwa namna moja ama nyingine,Mungu awabariki sana.

  Asanteni 
  Nawatakia heri ya sikukuu ya Mwaka mpya.

  0 0


   Afisa Uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde akiongea na waandishi wa habari wakati wa kuendesha droo ya mwenzi  wa washindi wa Amka Millionea, Ambapo moja kati ya washindi ni  bw Rickson Richard kutoka Arusha aliyejishindia shillingi million 15. pichani  Katikati ni Meneja Bidhaa Francis Ndikumwami akifatiwa na Mwakilishi wa Bodi ya Bahati nasibu ya taifa bw Sadiki Elimsu. 
   Meneja Bidhaa Francis Ndikumwami na Mwakilishi wa Bodi ya Bahati nasibu ya taifa bw Sadiki Elimsu wakitafuta washindi wa mwenzi wa promosheni ya Amka Millionea ambapo Ambapo moja kati ya washindi ni bw Rickson Richard kutoka Arusha ambaye amejishinid kitita cha shillingi million 15.  wakishuhudia ni waandishi wa habari , kulia ni Afisa Uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde

  Afisa Uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde akiongea na Mshindi wa Amka Millionea bw Rickson Richard (19) kutoka Arusha  mara baada ya kuibuka kuw mshindi wa shillingi million 15 wa promosheni ya Amka millionea, Katikati ni Meneja Bidhaa Francis Ndikumwami akifatiwa na Mwakilishi wa Bodi ya Bahati nasibu ya taifa bw Sadiki Elimsu
    

  =======  ========  ========  =======

  Airtel yawazawadia washindi wa mwenzi wa “Amka Millionea” promosheni shilingi million 30
  ·         Washindi wawili wapatikan, Kila mmoja aondoka na kitita cha shilling million 15
  2 January 2013  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayotoa huduma nafuu na yenye wigo mpana zaidi wa mawasiliano, leo iwatangaza washindi  wa mwenzi wa promosheni “Amka Millionea” wa pesa taslimu  million 30 mara baada ya kuibuka washindi kupitia droo iliyofanyika leo asubuhi ambapo kila moja ameibuka na  kitita cha shilingi milioni 15 pesa taslimu.

  Akitangaza washindi hao mara baada ya droo iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde alisema” Airtel inawapa nafasi nyingine watanzania  kushiriki na Kushinda fedha taslimu kwa kupiti promosheni yetu hii kabambe ya “Amka Millionea” iliyozinduliwa mwanzoni mwa mwenzi December, mpaka sasa wateja zaidi ya 300 wamejishindia zawadi za pesa taslimu zenye thamani  zaidi ya shilingi million 120.  Promosheni ya Amka millionea inawazawadia wateja wa Airtel  Kila siku , kila wiki na leo tunashuhudia wateja wawili wa mwisho wa mwenzi wakiibuka kuwa washindi wa shilingi million kumi na tano kila mmoja.

  Tunaendelea kuwajali na kuwazawadia wateja wetu nchi nzima kuhakikisha washindi wengi wanapatikana, tunaendelea kuimarisha dhamira yetu ya kutoa huduma bora zenye viwango vya juu na kudhihirisha kauli mbiu yetu ya jisikie huru, aliongeza Matinde

  Akiongea kwanjia ya simu mara baada ya kutangazwa mshindi, Rickson Richard  mkazi wa Arusha na mwanafunzi wa kidato cha tano  katika shule ya Lyamungo high school alisema’ nimefurahi kuibuka mshindi wa milioni 15 wa promosheni ya Amka millionea, pesa hizi ntazitumia katika masomo yangu shule na kumsaidia baba yangu ambaye ndiye aliyenipa pesa za kuchezea promosheni hii.  nawaambia watanzania  ­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­waamini wanaweza kushinda na kujiunga kwani mimi nimecheza na nimeshinda kwa Bahati nao pia wananafasi ya kujishindia kama mimi.

  Tunapenda kuwajulisha kuwa promosheni hii bado inaendelea na kukupa nafasi ya kuwa mmoja kati ya washindi wa mamilioni ya fedha  kila siku, kila wiki, kila mwezi  au mshinid wa zawadi kubwa moja itatolewa mwisho wa promosheni. 

  Ili mteja aweze kushiriki inabidi atume neno WIN/SHINDA kwenda namba 15595 bure , Baada kujiunga mteja atakuwa atapata ujumbe kutoka 15656 na kupata maswali ambayo atajibu na akipata sahihi atapata ponti 20 akikosea atapata ponti 10. Na kwakila ujumbe atakaotuma atatozwa kiasi cha shilingi 350 pamoja na kodi.  0 0


  Habari za leo wadau wote na poleni na kazi, Tulikuwa tunaomba mtusaidie kutuwekea uzinduzi wa kupiga Kura kupitia Mtandaoni. Tunatanguliza Shukurani zetu. Asanteni

  Ili kuongeza ushiriki wa wananchi , Bodi ya Miss Utalii Tanzania imezindua Rasmi upigaji Kura wa kumpata mshindi wa taji la Miss Utalii Tanzania 2012/13 kupitia tovuti. Fulusa hii ni kwa watu wote ndani na Nje ya Tanzania. 

  Bofya Link Hii kumpigia Kura Mrembo wa Mkoa wako ashinde: http://misstourismorganisation.blogspot.com/p/meet.html

  0 0


  0 0

  Mkazi wa Kigogo jijini Dar, ambaye jina lake halikujulikana mara moja akikatiza barabarani na ndoo zake akielekea kutafuta maji.

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azzan (kulia), akimkabidhi funguo mshindi wa Toyota Noah, Ramadhan Salum Pazi.
  Idd Azzan (kulia) akimkabidhi faili la gari mshindi wa Noah, Ramadhan Pazi.
  Ramadhan Pazi akiingia katika gari lake aina ya Toyota Noah.
  ...Akiwa ndani ya gari lake.
  Idd Azzan akimsaidia Pazi kuwasha gari lake.
  --
  MSHINDI wa Bahati Nasibu ya 'Timiza Ndoto Yako, Jishindie Toyota Noah' ambayo ilikuwa inaendeshwa na Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd, Ramadhan Salum Pazi, mkazi wa Buguruni-Rozana jijini Dar es Salaam, leo amekabidhiwa gari lake aina ya Toyota Noah. Makabidhiano hayo yamefanywa na Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azzan nje ya ofisi za Global Publishers. Bahati Nasibu hiyo iliyokuwa inaendeshwa kupitia magazeti ya Global ambayo ni Uwazi, Risasi, Championi, Amani, Ijumaa na Ijumaa Wikienda ilifika mwisho Desemba 20 mwaka jana ambapo bwana Ramadhani Pazi aliibuka kidedea.

  0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina Lowassa wakiwapungua mikono wageni waalikwa wakati wa hafla ya Chakula cha Mchana aliyoiandaa kwa ajili ya kusherehekea Mwaka Mpya wa 2013,iliyofanyika nyumbani kwake Monduli.
  Mbunge wa Jimbo la Kilindi,Mh. Beatrice Shelukindo (wa pili kulia) akiambatana na Mbunge wa Jimbo la Bariadi,Mh. Andrew Chenge wakati wakiwasili kwenye hafla ya Chakula cha Mchana iliyokuwa imeandaliwa na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa kwa ajili ya kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2013.
  Wafanyabiashara maarufu jijini Arusha,Papa King na Mdau Mathias (MNEC) wakiwasili kwenye hafla hiyo.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akihutubia wageni mbali mbali waliohudhulia hafla ya Chakula cha Mchana aliyoiandaa kwa ajili ya kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2013,iliyofanyika nyumbani kwake,Monduli.
  waalikwa wakipata Chakula nyumbani kwa Mh. Lowassa.

  0 0

  INTERNET CAFE INAYOMILIKIWA NA MSANII WA MZIKI WA BONGO FLEVA , MIONDOKO YA HIP HOP NCHINI ,EMMANUEL SIMWIGA AKA IZZO BIZNESS INATARAJIWA KUZINDULIWA KESHO JIJINI MBEYA, INTERNET CAFE HIYO AMBAYO IKO NDANI YA CHUO CHA TEOFILO KISANJI UNIVERSITY (TEKU) , ITAZINDULIWA RASMI  KESHO TAR 4 
  NA MHESHIMIWA MBUNGE WA MBEYA ,JOSEPH MBILINYI,

  0 0


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein amemteuwa Profesa Ali Seif Mshimba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Viwango la Zanzibar(Zanzibar Bureau of Standards) katika Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar.
   
  Kwa mujibu wa Taarifa iliotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee imeeleza kuwa Rais amefanya uteuzi huo kwa   uwezo aliopewa  chini ya kifungu 8(2)(a)  cha Sheria ya Viwango namba 1 ya mwaka 2011.
   
  Uteuzi huo umeanza jana.
   
  IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
  3/1/2013

  0 0  Dar inachangia asilimia 80 ya mapato. Kitovu cha Uchumi. Dar inachangia 90% ya ufisadi. Uti wa mgongo wa ufisadi nchini'
  Imeandikwa na Mh Zitto Kabwe.
  Malumbano kati ya wananchi wa Mtwara na Serikali kuhusu matumizi bora ya utajiri wa nchi yameendelea kwa takribani wiki moja sasa. Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na Waziri wa Nishati na Madini kuwaita Watanzania wa Mtwara Wahaini, wapuuzi na watu hatari, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania naye aliingia kwenye mjadala huo kwa kuonya watu wanaowaunga mkono watu wa Mtwara na kuwaita watu wanaotafuta umaarufu wa kisiasa na wanaotaka kugawa nchi. Siku moja baada ya hotuba ya Rais, Waziri wa Nishati na Madini alifanya mkutano na waandishi wa habari kueleza suala lile lile ambalo bosi wake alilielezea usiku wa kuamkia mwaka mpya 2013. Hii ni dalili ya Serikali kuweweseka.
  Katika kauli ya Serikali, ambayo haikuwa na jipya zaidi ya wimbo ule ule wa ‘kugawa nchi’ ‘umaarufu wa kisiasa’ nk, Serikali ilitaka kuonyesha umma kuwa watu wa Mtwara hawana shukurani. Kwamba miaka yote toka Uhuru watu wa Mtwara wamekuwa wakilishwa na Pamba, Kahawa, Chai, Tumbaku, Sukari, Kidatu nk. Kwamba watu wa Mtwara na Lindi hawakuchangia hata kidogo kwenye hazina ya Taifa. Hivyo wao kupigia kelele gesi yao ni uchoyo na roho mbaya na kukosa shukurani. Kauli ya Serikali ni kauli ya chombo kinachoendelea kukosa ‘legitimacy’ ya kuongoza taifa. Ni kauli ya kukata tamaa. Ni kauli hatari sana dhidi ya Watanzania waliojitolea damu kulinda uhuru wa nchi yetu.
  Moja, Serikali katika kauli yake haitaji kabisa kwamba toka Uhuru watu wa Mtwara na Lindi wamekuwa wachangiaji wakubwa sana katika uchumi wa Taifa kupitia zao la Korosho. Takwimu za Uzalishaji wa Korosho zinaonyesha kwamba kuanzia mwaka 1965 mpaka 2011 Korosho imeliingizia Taifa fedha kigeni jumla ya dola za Kimarekani 4.58 bilioni ( Cashewnuts Sub-sector study 2003, Hali ya Uchumi 2012, Cashewnuts Tanzania Report 2010). Katika Mwaka wa Uchumi unaoishia Novemba 2012, Korosho imeliingizia Taifa jumla ya dola za Kimarekani 151 milioni. Katika mwaka 2011 zao hili liliingiza dola 130 milioni wakati Pamba iliingiza dola 53 milioni tu. 
  Licha ya Zao la Korosho kuingiza fedha hizi za kigeni  (sawa ni shilingi trilioni 7.2) kwa nchi mikoa ya Lindi na Mtwara ipo miaka 50 nyuma kimaendeleo kulinganisha na mikoa mingine ya Tanzania. Serikali inataka kufuta historia ya mchango wa zao la Korosho kwenye uchumi wa nchi yetu kwa sababu ya uroho wa gesi asilia. Kwa nini kauli rasmi ya Serikali haijataja Korosho kabisa? Kauli hii ilipitishwa na ngazi zote za Serikali? Mawaziri wa Serikali wanaotoka mikoa ya Lindi na Mtwara walikubali kauli kama hii itoke dhidi ya wananchi wao wanaoteseka na zao la Korosho miaka nenda miaka rudi?
  Pili, Serikali imesahau kabisa mchango wa watu wa Lindi na Mtwara katika ulinzi wa Taifa letu. Moja ya sababu ya mikoa ya Lindi na Mtwara kuwa nyuma kimaendeleo ni juhudi za ukombozi wa kusini mwa Afrika. Kambi ya wapigania uhuru wa Msumbiji ilikuwa Nachingwea. Kambi ya Frelimo iliwekwa kwenye Shamba la Mkonge kilometa 17 tu kutoka mjini Nachingwea ambapo ilikuwa makao makuu ya ukombozi wa Msumbiji. Rais Samora Machel, Rais Joaqim Chissano na Rais Guebuza waliendesha mapambano kutoka kusini mwa Tanzania. 
  Makaburu wa Afrika Kusini na Wareno walikuwa wanashambulia nchi yetu na mikoa hii miwili ya Lindi na Mtwara ikawa ‘buffer zone’. Wakati Dar es Salaam inaendelea kwa kila aina ya maendeleo, mikoa ya Lindi na Mtwara ilikuwa inalinda ili wanaoishi Dar es Salaam na mikoa mingine waishi wa amani na starehe. Serikali inapimaje mchango huu wa mikoa hii? Tunaipima kwa fedha? Uroho wa gesi asilia kuzalisha umeme wa kufurahisha walalaheri asilimia 14 nchini ndio inaifanya Serikali kusahau kabisa ‘sacrifice’ ya watu wa Mtwara katika kulinda uhuru wa Taifa letu?

  Tatu, Serikali inasema lazima bomba lije Dar es Salaam kwa sababu Dar ndio inazalisha asilimia 80 ya Mapato ya Serikali. Kwanza huu ni uwongo. Ni aibu Serikali kujitetea kwa uwongo. Dar es Salaam ni kituo tu cha kukusanyia mapato ya Serikali. Uzalishaji mkubwa wa nchi yetu wenye kuzalisha kodi unafanyika nje ya Dar es Salaam. Walipa kodi wakubwa wengi Ofisi zao Kuu zipo Dar es Salaam lakini uzalishaji wao unafanyika nje ya Dar es Salaam. 
  Serikali itoe orodha ya walipa kodi wakubwa 100 tuone uzalishaji halisi wa mapato hayo unafanyika wapi. Hata hivyo inawezekana kuwa ikawa kweli Dar es Salaam inakusanya asilimia 80 ya mapato ya nchi. Basi na tuseme Dar es Salaam inachangia asilimia 90 ya ufisadi wote nchini. Kashfa zote kubwa za Ufisadi zinafanyika Dar es Salaam na fedha nyingi za ufisadi zinatumika Dar es Salaam.
  Mwisho, maandamano ya watu wa Mtwara ni kielelezo tosha kwamba watu wa mikoa ya Lindi na Mtwara wamechoshwa na longolongo za Serikali. Wananchi wa Mtwara na Lindi wanataka Uwajibikaji wa Serikali kuhusu utajiri wa nchi. Mtanzania yeyote mwenye tahadhari ya nchi yetu kutokuwa na laana ya rasilimali ataungana mkono na watu wa Lindi na Mtwara kudai maendeleo. 
  Nilitoa mfano wa Mgodi wa Golden Pride ambao umemaliza dhahabu yote tani 76 katika eneo la Lusu wilayani Nzega. Kampuni ya Resolute ya Australia iliwekeza dola 370 milioni kuanzia mwaka 1998 (mkataba wao ulisainiwa 25th June 1997). Katika kipindi cha uhai wa mgodi, miaka 14,  Kampuni hii imeuza dhahabu ya thamani ya dola za kimarekani 3.3 bilioni. Kabla Serikali haijawaita watu Mtwara wahaini, wapuuzi na watu hatari, iwaambie watu Watanzania kodi kiasi gani imekusanywa kutoka mgodi huu katika kipindi cha miaka 14. Mpaka mwaka 2008, kwa mujibu wa Taarifa ya Kamati ya Bomani, kampuni hii ilikuwa imelipa mrahaba wa dola 11 milioni na kodi nyingine dola 16 milioni. Serikali itwambie ilipofika Disemba 2012 kodi kiasi imekusanywa kutoka kampuni hii?
  Pia watu wa Mtwara na Lindi wameona historia ya bomba la Songosongo. Hata kodi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa (0.3%) ilikuwa inalipwa Halmashauri ya Manispaa Ilala na kampuni ya Pan Africa Energy. Ilichukua juhudi za mbunge wa Kilwa Kaskazini Murtaza Mangungu kuingilia kati ndio kodi ikaanza kulipwa Kilwa ambapo uzalishaji unafanyika. Watu wa Mtwara ni werevu, wanajua wafanyalo. Wanataka utajiri wa nchi unufaishe nchi kwa kuanzia kule utajiri ulipo. Kuna dhambi gani?
  Uwajibikaji katika uvunaji wa Rasilimali ya Gesi ndio chanzo cha maandamano ya watu wa Mtwara. Serikali isikimbilie kulaumu wanasiasa kwamba ndio wamechochea maandamano haya. Haya ni maandamno ya wananchi wakitaka Serikali yao iwajibike kwao. Serikali ithubutu kufanya ubabe wa kujenga bomba la gesi bila ridhaa ya Wananchi wa Lindi na Mtwara. 
  Wananchi wanapohitaji uwajibikaji ni wajibu wa Serikali kuwajibika kwao ni sio kuwaita wahaini, wachochezi, watu hatari, wapuuzi. Watu wa Mtwara wamechangia maendeleo ya Taifa letu kwa jasho na damu. Serikali ina wajibu wa kuwasikiliza, kuwaelimisha na kupata mwafaka. Kauli ya Serikali imewatukana watu wa Mtwara na Lindi. Hawatakubali kudhalilishwa. Hawatakubali historia yao kufutwa. Hawatakubali waendelee kubaki nyuma kimaendeleo. Serikali ifikirie tena.

  0 0


  Umati wa watu kutoka kila pande ya dunia unatarajiwa kukusanyika  pamoja mwezi wa pili Mjini Zanzibar kusherekea miaka 10 ya tamasha la muziki la Sauti za Busara. Tamasha hili litaanza tarehe 14 mpaka 17 Februari 2013 ndani ya Ngome Kongwe Zanzibar. Tamasha litavutia idadi kubwa ya wenyeji na wageni kutoka mataifa mbali mbali kwa mwaka2013.  Tamasha litasherekea mafanikio yake ya kuwajumuisha wasanii na watazamaji pamoja kutoka kila pande ya Afrika na kwengineko kwa utajiri wetu wa utamaduni na uzoefu,  kukuza utamaduni na maendeleo katika jamaii kwa miaka 10 iliyopita. 


  Sauti za Busara ni tukio la kipekee la kila mwaka Afrika mashariki na linajulikana kama ‘ Tamasha rafiki  zaidi duniani’.  Katika toleo hili litajumuisha wasanii 200:  zaidi ya vikundi ishirini na tano kutoka Afrika mashariki na kwingineko;  utaalamu wa kutumia vyombo vya umeme na asilia  vyote hivi vitaonekana moja kwa moja kwenye jukwaa la Sauti za Busara. Ndani ya Ngome Kongwe itakuwa ni siku tatu mfululizo kwa muziki wa moja kwa moja, ratiba  hii itaendelea  kuanzia Ijumaa mpaka Jumapili ikiambatana na shoo kuanzia saa kumi na moja jioni mpaka saa saba usiku

  .

  Tamasha pia litajumuisha filamu za miziki ya kiafrika: kumbukumbu, video za muziki na maonyesho ya moja kwa moja ya onyesho, yote haya tumelenga kukuza utajiri na utofauti wa muziki wa kiafrika hii itaonyeshwa ndani ya ukumbi wa Amphitheatre Ngome Kongwe Kiingilio katika tamasha kwa Watanzania ni 3,000/- TSh. Orodha ya wasanii wa kimataifa watakao shiriki Tamasha la 10 la Sauti za Busara ni Cheikh Lo kutoka Senegal,  ni mwimbaji, mwandishi, mpiga Gitaa, Kora, ngoma na ni kivutio Afrika magharibi na kati, aliunda aina yake ya  kipekee. Cheikh Lô alizaliwa mwaka 1955, wazazi wake ni watu wa Senegal mji wa Bobo Dioulasso, Burkina Faso, sio mbali na mpaka wa Mali,mahali alipokulia wanaongea Bambara (Lugha ya  Mali), Wolof (Lugha ya Senegal) na kifaransa.    Wakati wa utotoni alikuwa anasikiliza aina zote za muziki hususani miziki ya Congo ijulikanayo kama rumba ni muziki unaojulikana sana Afrika. Miaka 21 alianza kuimba na kupiga kora na Orchestra Volta Jazz mjini  Bobo Dioulasso. Youssou N'Dour  aliitambua sauti yake ndipo alipomsaidia kukuza kipaji chake baada kukutananaye  kwa mara ya kwanza  mwaka 1989. "Kila alipokuwa akiimba vibwagizo nilivutiwa na sauti yake," N'Dour alisema, " lakini nilitokea kumfahamu kupitia nakala yake 'Doxandeme'.  Niliisikiliza sauti yake "wow" – Niliona kitu kupitia sauti yake ambayo ilikuwa safari kutoka Burkina, Niger, Mali".

  Katika Tamasha la miaka 10 ya Sauti za Busara itakutanisha bendi bora (Best of the Best) ambazo zilipendwa na mashabiki wa muziki kwa miaka tisa iliyopita ikiwemo bendi Mama na kiongozi wa rumba Tanzania wanaojulikana kama DDC Mlimani Park Orchestre (Sikinde) Nao wakati wa Taarab asilia Zanzibar na Afrika Mashariki kwa ujumla wajulikanao kama Culture Musical Club wataonyesha cheche zao kwenye Tamasha la kumi la Sauti za Busara, kundi hili lililojizolea umaarufu sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi kama Marekani, Japan na kwingineko.

  Wasanii wengine ni Khaira Arby (Mali), Comrade Fatso na Chabvondoka (Zimbabwe),  Atongo Zimba (Ghana),  N'Faly Kouyaté (Guinea),  Nathalie Natiembe (Reunion),  Nawal & Les Femmes de la Lune (Comoros / Mayotte), Wazimbo (Mozambique)The Moreira Project (Mozambique / Afrika Kusini), Owiny Sigoma Band (Kenya / UK), Mokoomba (Zimbabwe), Msafiri Zawose & Sauti Band (Tanzania), Mani Martin (Rwanda), Burkina Electric (Burkina Faso / USA),  Lumumba Theatre Group (Tanzania), Sousou & Maher Cissoko (Senegal / Sweden), Super Maya Baikoko (Tanzania), Peter Msechu (Tanzania)   na wengineo wengi.

  Sauti za Busara itaandaa Movers & Shakers networking forum kwa wenyeji na wageni wataalam  katika sanaa. Mtandao huu utachukuwa nafasi  katika kujadil maendeleo,  kubadilishana mawazo  na ubunifu katika kiwanda cha sanaa kanda ya Afrika Mashariki na kwingineko. It’s not just the festival that puts on a show; the local community is encouraged to take part by hosting Busara Xtra fringe events. These includetraditional ngoma drum and dance, fashion shows, dhow races, open-mic sessions, after-parties and performances of Zanzibar’s oldest taarab orchestras as arranged by the local community. 

  Si tamasha pekee linalofanya maonyesho: wenyeji nao wanapewa moyo wa kuhodhi matukio mbalimbali yajulikanayo kamaBusara Xtra. Matukio hayo yanajumuisha ngoma za asili, maonyesho ya mavazi, mashindano ya ngalawa, taarabu asilia na mengineyo mengi ambayo yanaandaliwa na wenyeji.

  http://busaramusic.org/SzB2012pics/               www.busaramusic.org/SzB2011pics     
  * Hi-res photos available for media on request

older | 1 | .... | 3 | 4 | (Page 5) | 6 | 7 | .... | 1897 | newer