Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

RAIS WA ZIMBABWE ROBERT MUGABE AFUNGUA KONGAMANO LA VIJANA AFRIKA NA CHINA,RAIS KIKWETE ATUNUKIWA TUZO YA HESHIMA .

$
0
0
  
Mgeni Rasmi wa Kongamano la tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China, Rais wa Zimbabwe,Robert  Mugabe akihutubi usiku huu kweye kongamano hilo kwenye moja ya ukumbi wa mikutano katika hotel ya Ngurdoto mjini Arusha.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza usiku huu kwenye moja ya ukumbi wa mikutano katika hotel ya Ngurdoto mjini Arusha,ambapo Kongamano la tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China linafanyika na mgeni rasmi ni Rais wa Zimbabwe,Robert Mugabe.
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe (aliyeshikwa  mabepa) akiwasili usiku huu kwenye moja ya ukumbi wa mikutano katika hotel ya Ngurdoto mjini Arusha,kwa ajili ya kufungua kufungua  Kongamano la tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China.
 RAIS Jakaya Kikwete  akipewa tunzo  ya Heshima ya juu ya Kuhamasisha Amani na Utulivu katika Bara la Afrika na Rais wa Umoja wa Vijana Afrika (PAYU),Francine Furaha Muyumba .Tuzo hiyo imetolewa na Umoja wa Vijana  wa  Umoja wa Afrika,pichani kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mh.Mboni Mhita
  Rais Jakaya Kikwete akitoa salamu zake kwa washiriki wa   Kongamano la tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China,ambalo mgeni rasmi ni Rais wa Zimbabwe,Robert Mugabe.
  Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na baadhi ya washiriki wa Kongamano la tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China,ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Zimbabwe,Robert Mugabe,kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana 
 Rais Jakaya Kikwete akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipowasili jioni ya leo kwenye moja ya ukumbi wa mikutano katika hotel ya Ngurdoto mjini Arusha,kwa ajili ya kutoa salamu kwa washiriki wa   Kongamano la tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China,ambalo mgeni rasmi ni Rais wa Zimbabwe,Robert Mugabe.Pichani kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Mh.Stephen Masele.

DMV ALL STARS WATUA VOA.

$
0
0
IMG_6367Sunday na Ebreezy, Domi, Aj Ubao na Prince Heri.Jiandae kusikiliza mahojiano yao katika Jukwaa la Vijana la VOA. IMG_6371Aj Ubao na Domi wakijiandaa kupiga acapella. IMG_6379San Tized na Prince Heri katika acapella. Kwa picha zaidi ungana na sundayshomari.com IMG_6384IMG_6387

HOSPITALI YA MT,MERU YAKABILIWA NA UPUNGUFU WA MASHUKA YA KUJIFUNIKIA WAGONJWA

$
0
0
3Mwenyekiti wa kikundi cha Upendo Family Group ,Faustine Mwanadago (kushoto)akimkabidhi msaada wa katoni ya maji muuguzi mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Arusha,Mt Meru,Sifael Masawe jana kikundi hicho kilipofanya ziara ya kutembelea wagonjwa hospitalini hapo,jumla ya mashuka 300 na maji katoni 10 zenye thamani ya zaidi ya sh,2 milioni zilikabidhiwa ,anayeshuhudia pembeni ni makamu mwenyekiti wa kikundi hicho,Jasmine Kiure(Habari Picha na moses mashalla wa jamiiblog.co.tz/)
1Mwenyekiti wa kikundi cha Upendo Family Group ,Faustine Mwanadago (kushoto)akimkabidhi msaada wa mashuka na maji muuguzi mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Arusha,Mt Meru,Sifael Masawe jana kikundi hicho kilipofanya ziara ya kutembelea wagonjwa hospitalini hapo,jumla ya mashuka 300 na maji katoni 10 zenye thamani ya zaidi ya sh,2 milioni zilikabidhiwa ,anayeshuhudia pembeni ni makamu mwenyekiti wa kikundi hicho,Jasmine Kiure.

Hospitali ya mkoa wa Arusha,Mt Meru inakabiliwa na upungufu mkubwa wa mashuka ya kujifunikia kwa ajili ya wagonjwa mbalimbali   waliolazwa hospitalini  hapo hali ambayo imepelekea baadhi ya wagonjwa hao kulala bila kujifunika nyakati za usiku.

Kwa sasa hospitali hiyo ina jumla ya vitanda 500 na mashuka 300 wakati wastani wa kitanda kimoja kinatakiwa kuwa na  mashuka 8.

Akizungumza na waaandishi wa habari mara baada ya kupokea msaada wa jumla ya mashuka 100 na katoni kumi za maji kwa ajili ya wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo,muuguzi mfawidhi wa hospitali hiyo,Sifael Masawe alisema kuwa tatizo la uhaba wa fedha kutoka serikali kuu limechangia kukosekana kwa huduma mbalimbali hospitalini hapo yakiwemo mashuka.

Alisema kuwa  kwa nyakati tofauti baadhi ya wagonjwa hushindwa kujifunika mashuka nyakati za usiku  kutokana na uhaba wa mashuka hayo na kuwataka wadau mbalimbali mkoani Arusha kujitokeza kuokoa hali hiyo.

Akikabidhi misaada ya mashuka na maji kwa ajili ya wagonjwa waliolazwa katika wodi wa akina mama hospitalini hapo ,mwenyekiti wa kikundi cha Upendo Family,Faustine Mwandago alisema kwamba misaada hiyo imegharimu kiasi cha zaidi ya sh,2 milioni.

Mwandago,alisema kuwa lengo la kukabidhi misaada hiyo ni kuonyesha upendo kwa watu wenye mahitaji mbalimbali sanjari na  kulienzi jina la kikundi chao kwa vitendo huku akiwataka wadau wengine kuwaunga mkono.

TAHARIRI: TCRA IZIMULIKE BLOGS ‘UCHWARA’ NA KUZICHUKULIA HATUA KALI

$
0
0
11039142_10200327749914253_7953568182828634952_n
"Screen shot" ikionyesha moja ya habari zilizorushwa kwenye moja ya blog uchwara kuhusiana na taarifa za uzushi wa kifo cha mchungaji Gwajima.
…Ni zile zinazoandika habari za uongo, matusi

Na Andrew Chale wa Modewji blog.

Miongoni mwa mambo ambayo Tanzania tunapitia kwa sasa ni pamoja na teknolojia mbalimbali ikiwemo mawasiliano ya simu, intaneti vyombo vya habari na mengine mengi, Lakini mawasiliano hayo kwa sasa ikiwemo Intaneti wapo wanayoyatumia vibaya.

Kupitia BLOG, mtandao ambao mtu anaweza kutengeneza chombo chake cha kutolea taarifa ama kufanyaia jambo lolote lile liwafikie wengi kwa mema, lakini kwa sasa hilo halipo kwani licha ya kuwa kila mtu anaweza kuanzisha blog imetoa mwanya kwa wengine kuzitumia blog hizo kinyume na matarajio.

Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na BLOG nyingi ambazo asilimia kubwa mtu yoyote anaweza kuanzisha tena bure kama ilivyo akaunti yako ya Email, watu wanaoziendesha BLOG hizo wamekuwa wakiongoza kwa kuweka habari za uongo, upotoshaji, habari zinazoenda kinyume na maadili, pamoja na habari ambazosi za kweli.

Tunaamini wapo watu wanaofanya shughuli hizi za BLOG, ambao ni Ma-blogger wazuri tu licha ya kuwa si wanahabari, lakini kwenye blog zao wana weka ‘POST’ habari nzuri na zinazoendana na maadili pia wamekuwa wakitoa habari za kuelimisha jamii, kuifunza jamii na wanapata wasomaji wanaotembelea wengi sana kiasi cha hata kupewa matangazo na baadhi ya Makampuni binafsi ya kibiashara, Serikali na watu wengine, lakini shida ni kwenye hizi ‘Blog uchwara’ ambazo kila kukicha wao kazi yao kukopi na ku-paste habari za kwenye magazeti na kuzipa ‘kiki’ kwenye blog zao wengine habari hizo hizo za kwenye magazeti wao kazi yao kubadilisha kichwa cha ‘habari tu ilimradi apate wasomaji wengi? Jamani kweli hii ni haki?, tena kichwa hicho cha habari hakiendani na maadili ya Mtanzania ama kinakiuka maadili hii si sawa, TCRA, muamke na kuchukua hatua kali.
1
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Profesa John Nkoma.
Tunaamini Mamlaka yaa Mawasiliano Tanzania (Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA), ( https://www.tcra.go.tz/) mpo na mnafuatilia lakini sijui kama mnaliona hili ni tatizo ama si tatizo.

Tukumbuke huko nyuma kulikuwa na mitandao kama hii tena ya watanzania ambao waliifungua ambapo walianza kuweka picha za kawaida na baadae ikawa inabadilika kuwa wanaweka picha za utupu… wakaachiwa hivi hivi baadae wakawa wanaweka picha za viongozi wakiwemo viongozi wakuu wa Nchi mwisho wa siku Mamlaka husika wakaja kukumbuka shuka wakati mambo yamekua si mambo.

Hivyo ni wakati sasa kwa TCRA, kuchukua hatua blog zote zinazoendana kinyume na maadili ikiwemo kupotosha, kuweka pichaa za ngono na kugombanisha watu basi zichukuliwe hatua.
Mtandao huu unaamini kuwa na unaungana na wadau wote wanaendelea kutoa maoni yao juu ya kuzitaka blog hizi zichukuliwe hatua. Kwani mpaka tunaandika habari hii ni pamoja na baada ya Mdau Yusuph Mhoja kuchukizwa na moja ya habari kwenye miongoni mwa blog hapa nchini. (Tazama picha), ambapo Mdau huyo aliuliza: “Hivi huyu mwandishi anajua kiswahili kweli? Yuko mochwari kwani amefariki huyo?” wakati anajiuliza hayo, hii ni kuwa inawatokea watu wengi sana wanaapokutana na habari kwenye hizo blog uchwara.

Wadau waliochangia mada ya Mhoja: Pendi Mahundi yeye alieleza hivi: “hahaha.... hili ndiyo tatizo kubwa la kila mtu mwenye kisimu cha TECNO bongo kujifanya blogger and a self-appointed journalist... UJINGA mtupu, huwa naziona habari kwenye viblogu mpaka kichefu chefu... full of attention-seeking sensationalism... utakuta heading: HATARI, Vilio na majonzi, Breaking news, Unbelievable..kisa tu kutaka watu wazisome blog zao.” Alieleza Mahundi.
Hata hivyo wachangiaji wengine waliomba serikali kupitisha mswada wa habari na sheria ya ICT ili kukomesha wandishi wa viblog uchwara.
IMG-20150310-WA0045
Modewji blog tunaamini pia Mtandao wa wanabloga Tanzania (Tanzania Blogger Network-TBN) wapo kwani kuna misemo mingi ya zamani inayosemwa, ikiwemo ule wa SAMAKI MMOJA AKIOZA…? Jibu watatupatiaa TBN ama kama si lao basi bomu likilipuka tusimtafute mchawi huko mbeleni.

Hata hivyo, mtandao huu wa Mo dewji blog tunaungana na TCRA na kusema kuwa: “ #Ukipata ujumbe wa chuki, matusi au uongo, FUTA DELETE KABISA!.
Tuandikie maoni yako kupitia kwenye mtandao huu hapo chini ama kupitia simu 0719076376 au 0714940992.

WENGI WAHAMASIKA KATIKA MATEMBEZI YA KUPIGA VITA MAUAJI YA ALBINO - IMETOSHA, JIJINI DAR LEO

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe na Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaymar Kweigyr wakiongoza matembezi ya hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam kuanzia viwanja vya Biafra mpaka Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam.
Matembezi yakiendelea.
Wadau kutoka sekta mbali mbali wakishiriki kwenye Matembezi ya hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam kuanzia viwanja vya Biafra mpaka Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam.Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaymar Kweigyr, Balozi wa Harakati ya Imetosha, Henry Mdimu, Mwakilishi wa Chama cha Albino Tanzania (TAS), Abdillah Omar sambamaba na wadau wengine wakishiriki kuimba wimbo 'Tanzania Tanzania' kabla ya kuanza kwa shughuli nzima ya hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini, iliyofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es salaam.
Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaymar Kweigyr akicheza muziki wa sambamba na Mwanamuziki wa Reggae,Jhiko Manyika "Jhikoman" wakati wa shughuli nzima ya hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini, iliyofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es salaam.Kulia ni Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network ambao ni wadau wakubwa wa harakati ya Imetosha, Joachim Mushi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Matembezi ya Hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini (Imetosha), Ally Masoud "Kipanya" akimkaribisha Balozi wa Harakati ya Imetosha, Henry Mdimu ili kuzungumza na Watanzania waliofika kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam leo.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

President Kikwete Conferred Leadership Award in Arusha

$
0
0
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with Zimbabwe's President Robert Mugabe in Arusha shortly before president Mugabe officiated the opening of the 3rd Africa-China Young Leaders Forum yesterday.
The President of Pan African Youth Union Ms.Francine Muyumba presents a Leadership Excellence Award to President Dr,Jakaya Mrisho Kikwete in recognition for his outstanding leadership in the continent especially in promoting youth development.(photos by Freddy Maro)

BALOZI MDOGO MPYA INDIA, NA BALOZI MPYA WA OMAN WAKUTANA NA DK.ALI MOHAMED SHEIN IKULU ZANZIBAR

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana  na Balozi Mdogo mpya wa India anaefanyia kazi zake Zanzibar Satendar Kumar  alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kujitambulisha.
2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na  Balozi Mdogo mpya wa India anaefanyia kazi zake Zanzibar Satendar Kumar  alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kujitambulisha
3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na  Balozi  Mdogo mpya wa India anaefanyia kazi zake Zanzibar Satendar Kumar  alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo baada ya mazungumzo yao aliyefika kujitambulisha,
4
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana  na Balozi Mdogo mpya wa Oman  aliyepo  Zanzibar Mhe,Ali Abdulla Al-Rashdi  alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kujitambulisha,
5
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na  Balozi Mdogo mpya wa Oman  aliyepo  Zanzibar Mhe,Ali Abdulla Al-Rashdi alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kujitambulisha,
6
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na  Balozi  Mdogo mpya wa  Oman  aliyepo  Zanzibar Mhe,Ali Abdulla Al-Rashdi alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo baada ya mazungumzo yao aliyefika kujitambulisha.[Picha na Ikulu.]

AIRTEL YAKARABATI DARASA SHULE YA MSINGI USHINDI

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa tatu kulia), akizungumza kabla ya kukabidhi Darasa la Chekechea lililokarabatiwa kwa udhamini wa Wafanyakazi wa Airtel, kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Ushindi iliyopo Mikocheni ‘B’, jijini Dar es Salaam jana. Kutoka (kulia) ni Mwenyekiti wa Shule hiyo, Jumanne Konara na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Elias Katunzi, Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto) na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa tatu kulia), akimkabidhi Mtendaji wa Serikali ya Mtaa wa Mikocheni ‘B’, Suleiman Sagong’o, Darasa la Chekechea lililokarabatiwa kwa udhamini wa Wafanyakazi wa Airtel, kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Ushindi iliyopo Mikocheni ‘B’, jijini Dar es Salaam jana. Kutoka (kulia) ni Mwenyekiti wa Shule hiyo, Jumanne Konara na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Elias Katunzi, Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto) na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kulia), akifungua mlango wa Darasa la Chekechea lililokarabatiwa kwa udhamini wa Wafanyakazi wa Airtel, kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Ushindi iliyopo Mikocheni ‘B’, jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia (kutoka kushoto) ni Mwenyekiti wa Shule hiyo, Jumanne Konara, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Elias Katunzi, Mtendaji wa Serikali ya Mtaa wa Mikocheni ‘B’, Suleiman Sagong’o na baadhi ya wafanyakazi wa Airtel.


SHOW YA LADY JAY DEE NA ALI KIBA ILIVYOBAMBA KIOTA CHA M.O.G BAR & RESTAURANT

$
0
0
DSC_0035
Mwanamuziki Lady Jay Dee akitoa burudani na Machozi Band Ijumaa ya tarehe 27 mwezi huu ndani ya kiota chake cha Mog Bar & Restaurant (Nyumbani Lounge) katika show anazofanya mara moja kwa mwezi kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi ambapo Ijumaa hiyo alimualika Msanii machachari wa Bongo Flava Ali Kiba kwa ajili ya kukonga nyoyo za mashabiki wake ndani ya kiota hicho.
DSC_0033
DSC_0058
Vijana watanashati wenye vipaji vya aina yake wa Machozi Band wakipiga Back Vocal kumpa sapoti Lady Jay Dee a.k.a Komando Binti Machozi. Kutoka kushoto ni Faraja, Omirady pamoja na Chiqitita.
DSC_0089
Pichani juu na chini ni mashabiki wa Machozi Band wakimtunza manoti Lady Jay Dee.
DSC_0083
DSC_0078
DSC_0046
Umati wa mashabiki wa Machozi Band wakipata burudani kutoka kwa band hiyo inayoongozwa na Lady Jay Dee.
DSC_0048
DSC_0065
DSC_0066
DSC_0204
Msanii nyota nchini, Ali Kiba akitoa burudani ya aina yake ndani ya kiota cha M.O.G Bar & Restaurant baada ya kutikia mualiko wa msanii mwezake Lady Jay Dee na kufanya Live Music bila kutumia CD na kuwafanya mashabiki kupagawa zaidi.
DSC_0217
Ali Kiba akiendelea kuwaburudisha mashabiki wake Machozi Band.
DSC_0219
Warembo walipagawajem sasa.
DSC_0248
Twende kazi hapo sasa.
DSC_0253
Mrembo akijinafasi kwa Ali Kiba.
DSC_0275
#ChekechaCheketua.......Wadada wakichizika na mauno ya Ali Kiba na style yake mpya.
DSC_0283
Mwanadada hakukubali kabisa na kuamua kupanda jukwaani kulipiza mauno ya Ali Kiba.
DSC_0284
Picha inajieleza jinsi Ali Kiba alivyokonga nyoyo za mashabiki wake.
DSC_0296
Lady Jay Dee: Nimemkuta analia, kajilaza, sababu amechoka.....Mengi amevumilia, yalomkwaza, anataka kuondoka....ana siku ya pili sasa, hajarudi nyumbani kulala,...namuonea huruma sana, haya....mapenzi hayana maana
Lady Jay Dee: who the single girl.....who the single boy, Ali Kiba: i am a single boy.......Ali Kiba: who the single girl, .......Lady Jay Dee: i am a single girl.......Lady Jay Dee: who the single boy, Lady Jay Dee na Ali Kiba:....mi na we single boy.
DSC_0300
Tumefunika mbaya mtu wangu....ndio ishara waliyokuwa wakipeana Ali Kiba na Lady Jay Dee.
DSC_0281
DSC_0256
DSC_0010
Binti mrembo binti kwenye kipaji Faraja wa Machozi Band akiwapa raha mashabiki wa Band hiyo Ijumaa ya mwisho wa mwezi huu ndani kiota cha Mog Bar & Restaurant (Nyumbani Lounge).
DSC_0142
Mkali wa Reggae na Dance Hall nchini Double D akiwarusha mashabiki wake ndani ya kiota cha M.O.G Bar & Restaurant.
DSC_0158
Mkali wa Reggae na Dance Hall nchini Double D katika hisia kali za kuwapa raha mashabiki wake.
DSC_0144
Vijana wakijiachia vilivyo baada ya Reggae za Double D kuwakolea ndani ya kiota cha M.O.G Bar & Restaurant.
DSC_0170
Omirady wa Machozi Band akitoa burudani kwa mashabiki wa Band hiyo katika show inayopigwa mara moja kwa mwezi na kuwateka mashabiki wengi ndani ya kiota cha M.O.G Bar & Restaurant.
DSC_0015
Msanii Chiqitita wa Machozi Band akitoa burudani kwa mashabiki wa band hiyo (hawapo pichani).
DSC_0059
Mashabiki wa machozi band wakipata Ukodak.
DSC_0193
Sehemu ya umati wa mashabiki wa Live Band uliofurika Ijumaa ya mwisho wa mwezi huu ndani ya M.O.G Bar & Restaurant kushuhudia show ya wakali wa muziki nchini Lady Jay Dee na Ali Kiba.
DSC_0001
Hawa jamaa ndio wanaohakikisha Lady Jay Dee anakuwa salama siku zote.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGA KONGAMANO LA 3 LA VIJANA WA TANZANIA NA CHINA, JIJINI ARUSHA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake jana Machi 29, 2015 wakati akifunga rasmi Kongamano la tatu la Vijana wa Tanzania na China, lililohusu masuala ya Uongozi, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Ngurdoto jijini arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la China na Afrika, Chen Lin, baada ya Makamu kufunga rasmi Kongamano la tatu la Vijana wa Tanzania na China, lililohusu masuala ya Uongozi, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Ngurdoto jijini arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo, wakati akiondoka ukumbini hapo baada ya kufunga rasmi Kongamano la tatu ya Viajana wa Tanzania na China, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.

RAIS KIKWETE AWASILI MAREKANI KWA MWALIKO WA UMOJA WA MATAIFA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Jumapili, Machi 29, 2015 amewasili jijini New York, Marekani kwa mwaliko wa Umoja wa Mataifa.

Miongoni mwa mambo mengine, Rais Kikwete amefunguia rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa, na Jumatatu Machi 30, 2015 amealikwa kuhutubia Baraza la Umoja wa Mataifa la Uchumi na Jamii (ECOSOC - UN).
Rais Kikwete akilakiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatifa Dkt Mahadhi Juma Maalim alipowasili jijini New York, Marekani. 
Rais Kikwete akisalimiana na Waziri wa WAZIRI wa Kazi na Ajira, Mhe. Gaudensia Kabaka anayefuatiwa na Waziri wa Fedha wa Zanzibar Mhe. Omar Yussuf Mzee ...
Jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
Rais Kikwete akikata utepe kufungua rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

KITUO CHA JIMOLOJIA KUWEZESHA UONGEZAJI THAMANI MADINI NCHINI

$
0
0
Mkandarasi wa kampuni ya Kiure Engineering iliyofanya Ukarabati Mkubwa katika kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC) cha Jijini Arusha, Oswald Modu ( wa tatu kulia) akimkabithi funguo za vyumba mbalimbali vya kituo hicho, Mkurugenzi wa Manunuzi Wizara ya Nishati na Madini Amon Makachayo (wa tatu kushoto). Wengine wanaoshuhudia ni baadhi ya watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini na Wafanyakazi wa kampuni ya Kiure Engineering.
002
Mratibu wa Kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC) Mussa Shanyangi (wa pili kulia), akiwaonesha Mkurugenzi wa Manunuzi Wizara ya Nishati na Madini Amon Makachayo (wa pili kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Habari na Teknolojia Francis Fungameza namna mashine ya kukata mawe inavyofanya kazi.
003
Baadhi ya Wanafunzi katika kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC) waki polish mawe wakati wa mafunzo. Wanafunzi hao wako katika mafunzo ya ukataji na unga’rishaji madini katika kituo hicho.004
Meneja Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) Idrisa Yahya (kushoto) akimweleza jambo Mkandarasi wa Kampuni ya Kiure Engineering Oswald Modu(wa tatu kulia) wakati wa ukaguzi wa jingo la kituo hicho kabla ya makabidhiano rasmi kufanywa.
005
Baadhi ya wanafunzi wa kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC) kilichopo Jijini Arusha. Wakiwa katika mafunzo ya kunga’risha madini. Kituo hicho kitawezesha shughuli za Uongezaji Thamani kufanyika chuoni hapo.006
Sehemu ya Jengo la kituo cha Jimolojia Tanzania TGC, inavyoonekana pichani baada ya Ukarabati Mkubwa kufanywa na Kampuni ya Kiure Engineering. Jengo hilo limekabidhiwa rasmi kwa kituo hicho mwishoni mwa wiki.007
Meneja Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) Idrisa Yahya (katikati) na ujumbe wa Wizara na Mkandarasi wa Kampuni ya Kiure Engineering wakikagua mfumo wa CCT katika kituo cha Jimolojia Tanzania. (TGC).
008
Baadhi ya Vinyango vilivyochongwa kwa madini yam awe katika kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC).

………………………………………………………………………………
Na Asteria Muhozya, Arusha

Imeelezwa kuwa kukamilika kwa ukarabati mkubwa wa kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC) cha Jijini Arusha ni mafanikio makubwa kwa Wizara ya Nishati na Madini hususan katika tasnia ya Uongezaji Thamani Madini nchini kwani kitawezesha shughuli hizo kufanyika nchini.
Hayo yamebainishwa na Meneja Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) Idrisa Yahya mwishoni mwa wiki wakati wa makabidhiano ya kituo hicho baada ya kukamilika kwa ukarabati mkubwa uliofanywa na kampuni ya Kiure Engineering .
“Mkandarasi amejitahidi kufanya kazi katika muda tuliokubaliana na kazi imefanyika kama ilivyotakiwa. Hivi sasa tutautaja kama mradi uliokamilika”, alieleza Idrisa.
Aliongeza kuwa, mradi wa SMMRP utaendelea kukisaidia kituo hicho ili kiweze kutimiza malengo yake na kuhakikisha kinatoa taaluma katika masuala ya uongezaji thamani madini na hivyo kuwezesha sekta ya madini kuchangia zaidi katika pato la taifa.  Alisema kuwa, SMMRP imelenga katika kukiwezesha kituo hicho kuwa bora katika mafunzo ya uongezaji thamani madini nchini kutokana na umuhimu wa shughuli hizo kufanyika nchini badala ya madini hayo kusafirishwa nje ya nchi yakiwa ghafi. 
“Tumelenga katika kukiunganisha kituo hiki na vyuo vingine duniani vinavyotoa taaluma katika masuala haya ili kupata uzoefu na kubadilishana taaluma. Tunataka kituo hiki kifanye kazi iliyokusudiwa na kisimame peke yake hivyo lazima kiweke mipango mizuri. Kwa upande wa wizara ina budi kutenga bajeti ya kituo hiki kiendelee ili kutimiza malengo tunayoyatarajia”, alisisitiza Idrisa.
Kwa upande wake Mratibu wa kituo hicho Musa Shanyangi alisema kuwa, kituo hicho kinatarajia kuanza muhula mpya wa masomo ifikapo mwezi Juni mwaka huu katika fani za ukataji madini, masuala ya jimolojia, mafunzo ya usanifu na utengenezaji wa mapambo ya vito.
“Hivi sasa tunao wanafunzi 15 wanawake wanaosoma fani ya kukata na kung’arisha madini. Wanafunzi hawa walianza mafunzo tangu Novemba 2014 na wanasoma kwa ufadhili wa Serikali kwa kushirikiana na Chama cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (TAMIDA)” alisema Shanyangi.
Aidha, Shanyangi aliishukuru Serikali kwa kutambua shughuli za uongezaji thamani madini nchini kwani zitaongeza wigo wa ajira, kipato cha mtu mmoja mmoja, kuwezesha ukuaji wa shughuli za kiuchumi kupitia sekta hiyo ikiwemo pia kuchangia katika pato la taifa. Shughuli za uimarishaji na uendelezaji wa kituo hicho zinafanyika chini ya Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP). Kituo kitakuwa na maabara ya utambuzi wa madini ya vito, maktaba ya jimolojia na makumbusho ya madini ya vito.

WAZIRI LUKUVI AFANYA ZIARA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA DAR

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu ambaye alikuwa akitoa maelezo mafupi kuhusu utendaji wa Shirika hilo leo asubuhi. Waziri Lukuvi yuko katika ziara ya siku mbili kushuhudia utendaji wa Shirika hilo ambapo leo na kesho atatembelea baadhi ya miradi ya NHC iliyopo jijini Dar es Salaam na kisha baadaye kuzungumza na wafanyakazi wa NHC. Picha za Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Jamii.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akisalimiana na James Rhombo, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa NHC, wakati akikaribishwa Makao Makuu ya NHC. Kulia na Felix Maagi, Hamad Abdallah na Raymondo Mndolwa. 
 Waziri Lukuvi akisindikizwa na Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa, Haikamen Mlekio kuingia kwenye ofisi za makao makuu ya NHC leo.
 Waziri Lukuvi akisalimiana na Felix Maagi, Mkurugenzi wa Fedha wa NHC, wakati akikaribishwa Makao Makuu ya NHC. Kulia kwa Maagi ni James Rhombo, Hamad Abdallah na Raymondo Mndolwa. 
 Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mikoa na Utawala wa Shirika la NYumba la Taifa Raymond Mndolwa, akimsindikiza Waziri Lukuvi kuingia ukumbini NHC ambapo alipata fursa ya kuwasalimia wafanyakazi wa shirika hilo.

 Waziri Lukuvi akisalimiana na wafanyakazi wa NHC
 Waziri Lukuvi akisalimiana na wafanyakazi wa NHC
 Wakurugenzi wa NHC
 Wafanyakazi wa NHC wakimsikiliza Waziri Lukuvi (hayupo pichan)

Wafanyakazi wa NHC wakimsikiliza Waziri Lukuvi (hayupo pichan)
 Waziri Lukuvi akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHC
 Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya NHC katika picha.

ZITTO KABWE AZINDUA CHAMA CHA ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPARECY (ACT)

$
0
0
 Mwenyekiti wa Chama cha  Alliance for change and Transparecy (ACT)  Anaa Elisha    Akiwashukuru wanachama wote alioshiriki walio kiunga Mkono chama hicho nawaliotoka vyama vingine wakiwemo viongozi na Taasisi Mbalimbali.

Kiongizi MKuu wa chama  hicho na akiliyekua Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zitto Kabwe. akizungumza na wanachama Mbalimbali toka Nje na Ndani ya Dar es Salaa  katika uzinduzi wa chama hicho na kuwaomba wanachama popote walipo waipigie  Kura ya Hapana  Katiba Pendekezwa.

Msanii Afande Sele akiwa na wanachama wa Alliance for change and Transparecy (ACT) katika Picha ya pamoja kwenye Uzinduzi wa Chama hicho
Baadhi ya wajumbe na Viongozi wa Chama hicho wakimsikiliza Zitto Kabwe alipo kua akizindua Mkutano wa Chama hicho(wa tatu kushoto) ni Baba wa  Kiongizi MKuu wa chama  hicho na akiliyekua Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zitto Kabwe.,
Msanii  wa Makomando Said Christopher akisalimia Viongozi alipopanda juukwaani na mwenzake
 Mwenyekiti wa Chama cha  Alliance for change and Transparecy (ACT)  Anaa Elisha akisalimiana na Kiongizi MKuu wa chama  hicho na akiliyekua Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zitto Kabwe mara alipo maliza kuzungumza na wafuasi wa chama hicho.
 Mwenyekiti wa Chama cha  Alliance for change and Transparecy (ACT)  Anaa Elisha akisalimiana na Askofu Mstaafu wa Jimbo la Kigoma Angilikana Gerald Mpango  baada ya kuzungumza na Wanachama
Kikundi cha Ngoma ya Asili ya Kutoka Kigoma kwa jina maarufu kwa Mkoa huo wa kigoma inaitwa Usambere ikitoa burudani katika uzinduzi huo
Wanachama wa chama hicho kwa makundi mbalimbali wakiingia katika ukumbi kwa nyakati tofauti
Wafuasi wa Chama hicho wakiwa na mabango wakiingia Ukumbini
Wafuasi wa Chama hicho wakiwa na mabango yenye Ujumbe tofauti wakiingia Ukumbini
Wafuasi wa Chama hicho wakiwa na mabango yenye Ujumbe tofauti wakiingia Ukumbini
Wanakikundi wa kasimbo Asili, toka Mkoa wa Kigoma Kijiji cha Nyarubanda Kataa ya Mkigo Wilaya ya Kigoma wakitoa salam ya Chama hicho wakiwa wanajiandaa kuingia kwa Nyimbo za Ali ya Mkoa wao katika Mkutano wa Uzinduzi wa Mkutano wa  Alliance for change and Transparecy (ACT)
Baadhi ya Wafuasi wa Chama hicho wakiingia Ukumbini
Afande Sele akiwa Jukwaani akitumbuiza
Wasanii wa Kikundi cha Makomando wakitoa Burudani, kulia ni fred felix na Said Christopher.
Wafuasi wa chama hicho wakijiandikisha na kupatakadi ya Uanacha
Wanachama
Mamia wajitokeza Uzinduzi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Zitto Kabwe akisoma Fomu ya Chama hicho inayomtaka kila mwanacha Ngazi ya juu atangaze Mali zake
Kasimbo Asilia ikitoa Burudani katika Mkutano wa chama cha Alliance for change and Transparecy (ACT)  katika
Ukumbi wa Diamondi Jubilee Dar es Sallam leo mara baada ya chama hicho kufanya Uzinduzi 
Vikundi mbalimbali Vikitoa maigizo katika Uzinduzi wa Chama hicho.
Wanachama wakijipanga wakati Viongozi wa Chama hicho Kitaifa wakitarajia kuingia katika Ukumbi wa  Diamondi Jubilee
Wanachama wakijipanga mikono wakati Viongozi wa Chama hicho Kitaifa wakitarajia kuingia katika Ukumbi wa  Diamondi Jubilee na baadhi ya wanachama wakipunga mikono kwa kuonyesha alama ya chama chao
 (kulia) akiwapungia mikono wanachama alipokua akiingia katika Ukumbi wa Diamondi Jubilee Dar es Sallam leo (kushoto) ni  Kiongizi MKuu wa chama  hicho na akiliyekua Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zitto Kabwe.
Ulipoimbwa wimbo wa Mungu Ibariki.
Wanachama wakiimba Wimbo wa Taifa
.Katibu Mkuu ACT Tanzania Samson Mwigamba akizungumza na wanachama alipokua akifafanua jambo.

Jamii itoe ushirikiano kukomesha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini

$
0
0
Na. Johary Kachwamba - MAELEZO, DODOMA

JAMII imetakiwa kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi nchini katika kutoa taarifa zitakazo fanikisha kukamatwa kwa wote walioshiriki mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani  Mhe. Pereira Silima bungeni mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mhe. Al -Shaimaa Kwegyir, Mbunge wa Viti Maalum aliyehoji kuchelewa kwa taarifa ya kupatikana kwa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi, Pendo Emmanuel.

“Pendo alitekwa kutoka mikononi mwa mama yake mzazi, hii changamoto ni kubwa sana, tunaomba jamii itusaidie kutoa taarifa zitakazo saidia kufanikisha kukamatwa kwa wahusika, tushirikiane kwa pamoja kukomesha tatizo hili” alisema Mhe. Silima

“tangu kutekwa kwa mtoto Pendo watu 14 wanashikiliwa na jeshi la polisi akiwemo baba mzazi, uchunguzi bado unaendelea na watuhumiwa watafikishwa mahakamani hivi karibuni, ila Pendo bado hajapatikana” aliongezea Mhe. Silima

Aidha akijibu Swali la msingi la Mhe. Salumu Barwany, Mbunge wa Lindi Mjini, aliyehoji idadi ya kesi za mauaji ya walemavu wa ngozi na sababu za kuchelewa kutolewa hukumu. Mhe. Silima alisema kesi 10 zinaendelea kisikilizwa mahakama mbalimbali

“kati ya mwaka 2006 hadi 2015 jumla ya matukio 56 ya uhalifu dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi yaliripotiwa nchini. Matukio 41 yalihusisha vifo 43, matukio 13 yalihusisha majeruhi 13 na matukio 2 ya kupotea kwa watu wenye ulemavu wa ngozi” alifafanua Mhe. Silima

“kesi 46 kati ya matukio 56 zilifikishwa Mahakamani ambapo kesi 10 zenye watuhumiwa 12 zilitolewa hukumu ya kifo na kumi ziko chini ya upelelezi. Aidha kesi 26 watuhumiwa wake waliachiwa huru kwa kukosa ushahidi” aliongezea Mhe. Silima

Kuchelewa kwa hukumu au upelelezi wa baadhi ya kesi zilizotajwa kunachangiwa na sababu mbalimbali kama vile matokeo ya uchunguzi wa DNA toka Mamlaka ya Uchunguzi na/au mashahidi kutopatikana kwa urahisi na kwa wakati.

UJAMAA INTELLECTUALS NETWORK WATOA MSAADA KATIKA KITUO CHA KULELEA YATIMA CHA MAUNGA CENTRE JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
 
 Mwasisi na Mratibu Mkuu wa Kikundi cha Ujamaa Intellectuals Network Bw. Lusekelo Mwandemange akikabidhi msaada kwa Bi. Zainab Bakary Maunga wa kituo cha kulelea yatima cha Maunga Centre.
Bi. Mwajuma Njaritta  kutoka kikundi cha Ujamaa Intellectuals Network akimkabidhi mmoja wa watoto Msaada wa vitabu kwa niaba ya watoto wengine katika kituo cha kulelea yatima cha Maunga Centre. 
 Baadhi ya Misaada iliyotolewa na kikundi cha Ujamaa Intellectuals Network.
 Mwanzilishi na Mkuu wa kituo cha kulelea yatima cha Maunga kilichopo karibu na Kituo cha Polisi cha Hananasif  Kinondoni Bi. Zainab Bakari Maunga akitoa shukurani zake kwa kikundi cha Ujamaa Intellectuals Network kwa kuleta misaada mbalimbali katika kituo hicho.
 
 Mwasisi na Mratibu Mkuu wa kikundi cha Ujamaa Intellectuals Network Bw. Lusekelo Mwandemange akizungumza jambo wakati wa kutoa misaada hiyo na kuongeza kwamba huu ni mpango ambao wanaufanya kwa nchi nzima lengo ni kuwasaidia watu wasiojiweza, na pia ametoa ahadi ya kuendelea kutoa ushirikiano na kuendelea kusaidia zaidi kwa wale wasiojiweza.
 
 Katibu Mkuu wa Kituo cha kulela yatima cha Maunga akitoa neno la Shukurani baada ya kupokea misaada hiyo na kuwasihi watu wengine waguswe ili waweze kusaidia kama hawa walivyofanya
 Mmoja wa watoto akitoa Shukurani zake kwa niaba ya watoto wenzake baada ya kupokea Msaada huo.
 Baadhi ya watoto wakiwa pamoja na wanakundi wa Kikundi cha Ujamaa Intellectuals Network
Picha ya pamoja baada ya kukabidhi msaada huo

TUZO YA HESHIMA KUTOLEWA KWA BABA WA TAIFA HAYATI JK NYERERE NA HAYATI NELSON MANDELA, JIJINI DAR

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU TUZO YA JAMII ITAKAYOTOLEWA TAREHE 13 APRIL 2015 KATIKA UKUMBI WA JULIUS NYERERE INTERNATIONAL CONVENTION CENTRE, JIJINI DAR ES SALAAM



MGENI RASMI: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta Jakaya Mrisho Kikwete



WAGENI WAALIKWA:

Mara baada ya Hafla ya Tuzo ya Jamii ambapo Washindi wote watapewa Tuzo na Mgeni Rasmi, Kutakuwa na Dhifa ya Kitaifa ya Tuzo ya Jamii ambayo itahudhuriwa na wageni wafuatao:



  • Wapewa Tuzo,
  • Familia za wapewa Tuzo,
  • Viongozi Waandamizi wa Serikali,
  • Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania,
  • Viongozi wa vyama vya siasa na kijamii na Wafanyabiashara,
  • Taasisi zisizo za kiserikali,
  • Watu Mashuhuri na
  • Wawakilishi kutoka makundi yenye mahitaji maalum ambapo kwa mwaka huu watawakilishwa na Watu wenye Ulemavu wa Ngozi-Albino



MUHIMU:

Tanzania Awards International Ltd imepanga kufanya hafla ya utoaji wa Tuzo ya Jamii na kisha Dhifa ya Kitaifa ya Tuzo ya Jamii siku ya tarehe 13 ya mwezi April ya kila mwaka kwa malengo ya kuadhimisha Kumbumbuku ya siku ya kuzaliwa  Baba wa Taifa,  Hayati Mwalimu Julius Kambarege Nyerere.



Kuhusu Tanzania Awards International Limited

Tanzania Awards International Limited ni kampuni iliyosajiliwa kisheria nchini Tanzania kwa Malengo ya Kufanya tafiti mbalimbali, Kutoa ushauri wa kisheria na kijamii, kuandaa na kuratibu matukio pamoja na Uandaaji na Utoaji wa Tuzo Ya Jamii.



Maana ya Tuzo ya Jamii

Tuzo ya Jamii ni Tuzo inayotolewa kwa Taasisi na Watu binafsi kutokana na Mchango na Jitihada zao katika kusaidia na kutetea maslahi ya Jamii.





Malengo ya Tuzo ya Jamii

  • Kutambua, Kuthamini, Kuunga Mkono na Kutoa Tuzo kwa Taasisi au Mtu Binafsi kutokana na Mchango na Jitihada zake katika kusaidia na kutetea maslahi ya Jamii.



  • Kuikumbusha Jamii kuona umuhimu, kujali na Kuunga Mkono jitihada zinazofanywa na Taasisi au Mtu Binafsi katika kuleta Ustawi na Maendeleo ya Jamii



VIPENGELE VYA TUZO YA JAMII 2015

Vipengele vya Tuzo ya Jamii, hubadilika kila mwaka kulingana na aina na matokeo ya Utafiti unaofanywa na Tanzania Awards International Limited. Kwa mwaka huu (2015), Tuzo ya Jamii itakuwa na Vipengele Vikuu vinne (4) vifuatavyo:



  1. Tuzo ya Jamii 2015
  2. Tuzo ya jamii –Tuzo ya Heshima
  3. Tuzo ya Jamii ya Haki za Binadamu
  4. Tuzo ya Jamii kwa Mwanasiasa mwenye mafanikio katika siasa za Tanzania



UFAFANUZI WA KILA KIPENGELE CHA TUZO YA JAMII 2015



  1. Tuzo ya Jamii 2015

Tuzo hii itatolewa kwa Taasisi au Mtu Binafsi kutokana na mchango na jitihada zake katika kusaidia na kutetea Jamii.



Mshindi wa Tuzo hii ya Jamii atapatikana kwa:



(a)   Mhusika mwenyewe kuwasilisha vielelezo au ushahidi wa mchango wake huo kwa Jamii

AU

(b)   Kwa jamii kupendekeza jina la mhusika kupitia mitandao ya kijamii

AU

(c)    Kwa Kamati ya Tuzo ya Jamii kufanya utafiti, kuchambua na kuteua jina moja miongoni mwa yale yaliyopatikana kupitia kipengele (a) na (b)



Mshindi wa Tuzo ya Jamii 2015 atatangazwa rasmi siku ya Hafla ya Tuzo ya Jamii itakayofanyika tarehe 13 April 2015 katika Ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre, Jijini Dar es Salaam



2. Tuzo ya Jamii-Tuzo ya Heshima

Watakaopewa Tuzo ya Jamii-Tuzo ya Heshima ni:

(a)  Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na



(b)Hayati Nelson Mandela –Rais wa Kwanza Mzalendo wa Jamhuri ya Afrika ya Kusini

Tuzo hii ya Heshima kwa mwaka huu itatolewa kwa Waasisi hao wawili kutokana na Jitihada na Mchango wao wa kipekee na uliotukuka katika kutetea na Kulinda Maslahi ya Wanyonge







3. Tuzo ya Jamii ya Haki za Binadamu

Tuzo hii inatolewa kwa Taasisi au Mtu Binafsi kutokana na Mchango na Jitihada zake katika Kuelimisha, kulinda, kutetea na Kuimarisha Utawala Bora nchini Tanzania



Vigezo vinavyotumika kwa mwaka huu katika kumpata mshindi wa Tuzo ya Jamii ya Haki za Bianadamu, ni hivi vifuatavyo:



·         Weredi wa Taasisi au Mtu Binafsi katika kufanya uchunguzi, Utafiti na kutoa taarifa zake kwa uhuru, pasipo upendeleo wowote kwa Serikali, Chama, Kikundi au mtu Binafsi

·         Mchango wa Mtu Binafsi au Taasisi katika Kuelimisha Jamii,  kulinda, kutetea na kuhamasisha juu ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania.



·         Mchango wa Mtu Binafsi au Taasisi katika kulinda, kuhifadhi na kuhamasisha juu Amani, utulivu, Usalama wa Raia na Mali zao na Utii wa Sheria kwa ujumla



  1. Tuzo ya Jamii ya Mwanasiasa Mwenye Mafanikio katika siasa za Tanzania



Mshindi wa Tuzo hii atatangazwa siku ya hafla ya Tuzo ya Jamii baada ya mwanasiasa husika kupigiwa kura nyingi kupitia mtandao wa Push mobile ambapo mpigaji wa kura anatakiwa aende sehemu ya kuandika ujumbe mfupi wa maneno katika simu yake ya Mkononi na kuandika namba ya Mwanasiasa husika, alafu anatuma namba hiyo kwenda 15522.



Vigezo vitakavyotumiwa na wapiga kura kupitia namba 15522 ni hivi vifuatavyo:



  • Uadilifu, Uaminifu, Heshima na Utii kwa Jamii na sheria za nchi kwa Amani ya nchi yetu



  • Jitihada binafsi katika kulinda na kutetea Muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar, Umoja wa Kitaifa na Kijamii



  • Uzoefu wa Uongozi wa Umma, Taasisi za Kimataifa na Mchango wake kwa Jamii.



  • Matarajio, Mipango na nia ya Dhati ya Kuleta Maendeleo na Mafanikio kwa Watanzania



Orodha ya Wanasiasa wanaowania Tuzo ya Jamii ya Mwanasiasa Kijana na Mtu Mzima Mwenye Mafanikio katika siasa za Tanzania imepatikana baada ya wanajamii kupendekeza mara nyingi jina la Mwanasiasa husika kupitia Mtandao wa Push Mobile na mitandao mingine ya kijamii. Kamati ya Tuzo ya Jamii, baada ya kupitia majina yote yaliyopendekezwa kupitia mbalimbali ikiwemo Push Mobile, imepata orodha ifuatayo:



WATU WAZIMA

JINA LA MWANASIASA
NAMBA YA KUMPIGIA KURA
MHE. MIZENGO PETER PINDA
MM01
MHE. PROF. SOSPETER MWIJARUBI MUHONGO
MM02
MHE. DR. WILBROD PETER SLAA
MM03
MHE. ASHA-ROSE MTENGETI MIGIRO
MM04
MHE. SAMIA HASSAN SULUHU
MM05
MHE. JAMES FRANCIS MBATIA
MM06
MHE. DR. JOHN POMBE MAGUFULI
MM07
MHE. DR. HARRISON GEORGE MWAKYEMBE
MM08
MHE. PROF. IBRAHIM HARUNA LIPUMBA
MM09
MHE. STEPHEN MASATU WASIRA
MM10
MHE. BALOZI LIBERATA MULAMULA
MM11
MHE. BENARD KAMILIUS MEMBE
MM12
MHE. EDWARD NGOYAYI LOWASSA
MM13



VIJANA

JINA LA MWANASIASA
NAMBA YA KUMPIGIA KURA
MHE. JANUARY YUSUPH MAKAMBA
MK01
MHE. ZITTO ZUBERI KABWE
MK02
MHE. MWIGULU LAMECK NCHEMBA
MK03
MHE. HALIMA JAMES MDEE
MK04
MHE. SAADA SALUM MKUYA
MK05
MHE. LAZARO SAMUEL NYALANDU
MK06
MHE. ESTHER AMOS BULAYA
MK07
MHE. UMMY ALLY MWALIMU
MK08
MHE. NAPE MOSES NNAUYE
MK09
MHE .MBONI MHITA
MK10
MHE. DAVID ZACHARIA KAFULILA
MK11
MHE. VICKY PASCHAL KAMATA
MK12
MHE. JOHN JOHN MNYIKA

UN KUENDELEA KUISAIDIA TANZANIA KUTATAU CHANGAMOTO ZA MAENDELEO

$
0
0
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile (katikati) akiwasili katika ukumbi wa mikutano kwenye hoteli ya Hyatt Regency akiwa ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo (kulia) pamoja na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez kwa ajili ya kuzindua rasmi ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania, uzinduzi uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Nyuma yao ni Mkurugenzi wa Programu kutoka Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF), Dk. Tausi Kida.

DSC_0207Mshehereshaji wa uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania, Taji Liundi akiitambulisha meza kuu kwa wageni waalikwa (hawapo pichani) waliohudhuria uzinduzi huo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

DSC_0209Meza kuu Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo, Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez.
Na Mwandishi wetu
UMOJA wa Mataifa umesema kwamba utaendelea kuisaidia serikali ya Tanzania katika kutanzua changamoto za maendeleo zinazoikumba nchi hii.
Kauli hiyo imetolewa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja huo (UNDP), Alvaro Rodgriguez wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya maendeleo ya Binadamu ya mwaka 2014 mwishoni mwa wiki.
Ripoti hiyo imeandaliwa na Taasisi ya utafiti wa masuala ya kiuchumi na jamii- ya ESRF kwa ufadhili wa UNDP na inagusia changamoto za Maendeleo .
Katika hotuba yake amesema kwamba Umoja wa Mataifa unaona juhudi za serikali katika kuwakwamua wananchi katika umaskini na kutokana na hali hiyo wataendelea kusaidia mipango mbalimbali ya maendeleo pamoja na utafiti wenye kulenga kutoa suluhu kwa changamoto za maendeleo ya wananchi.
Ripoti hiyo ambayo inazungumza: “mabadiliko ya kiuchumi kwa maendeleo ya watu” imesheheni mipango mbalimbali ya maendeleo na shida zake na namna ya kukabiliana na shida hizo.
Katika utafiti huo imeelezwa kuwa pamoja na uchumi wa Tanzania kukua kwa kasi umaskini bado ni kero kubwa kutokana na kukosekana kwa uhusiano kati ya ukuaji wa kiuchumi na kufutwa kwa umaskini miongoni mwa wananchi wa kawaida.
Kuanzia mwaka 2001 uchumi wa Tanzania umekuwa ukikua kwa zaidi ya asilimia 6.
Mratibu huyo wa UN nchini amesema kwamba kutokana na kasi ya uchumi kutoenda sambamba na uchumi ndio maana UN inashirikiana na serikali kuona namna bora ya ukuaji uchumi kwenda sawa na uondoaji wa umaskini miongoni mwa wananchi waliowengi.
Wakati huo huo serikali imesema imefurahishwa na uzinduzi wa ripoti hiyo ambayo inatumaini itasaidia katika kuboresha sera na kujibu masuala muhimu ya kukabiliana na umaskini nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dk. Servacius Likwelile katika tukio hilo la uzinduzi wa ripoti.
Alisema serikali inaamini kwamba mambo yaliyomo katika ripoti hiyo yatasaidia katika harakati zake za kukabili umaskini ikiwa ni pamoja wa mipango ya maendeleo kwa kuzingatia dira ya taifa ya maendeleo ifikapo mwaka 2025.
Tanzania inajipanga kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 ikitegemea viwanda katika uchumi wake badala ya kilimo kama ilivyo sasa.
Alisema kwamba serikali imefurahishwa na jinsi ripoti ilivyojikita katika kuainisha maendeleo ya watu na sehemu kubwa ya ushauri utazingatiwa kwa mipango mipya ya maendeleo.
Ripoti ya maendeleo ya watu ni mkakati wa serikali ya Tanzania ulianzishwa Machi 2013 kwa lengo la kutafiti namna bora ya kunasua wananchi katika umaskini wakati taifa likiendelea kukuza uchumi.
Mradi huo unatekelezwa na taasisi ya ESRF ikishirikiana na Wakala wa taifa wa Takwimu (NBS), Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa serikali ya Zanzibar na kitivo cha uchumi cha chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Mradi huo unafadhiliwa na UNDP na umejikita zaidi katika kuangalia vipaumbele katika maendeleo, mambo yanayojitokeza, fursa na changamoto.
Ripoti hii inapatikana kwenye anuani zifuatazo
DSC_0241
DSC_0201Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akisoma risala kwenye uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania uliofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.
DSC_0247Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile akikata utepe kuzindua rasmi Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania uliofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia uzinduzi huo ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo (kulia).
DSC_0259Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akizindua chapisho la Kiswahili la Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania huku mgeni rasmi na Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF wakishuhudia tukio hilo.
DSC_0271Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo akizundua chapisho la kingereza la Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.
DSC_0277Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile (katikati), Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo kwa pamoja wakionyesha ripoti hiyo kwa waandishi wa habari na wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo.
DSC_0290Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo (kulia), Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile (katikati) na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez wakipitia nakala za ripoti hiyo mara baada ya kuzinduliwa rasmi jijini Dar.
DSC_0297Mgeni rasmi kwenye picha ya pamoja na wadau waliofanikisha maandalizi ya ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania.
DSC_0451Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo (katikati) akiteta jambo na Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP nchini Tanzania, Philippe Poinsot (kushoto) wakati wa kupiga picha ya kumbukumbu. Kulia ni Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Amon Manyama.

Wananchi watakiwa kudai Risiti kwenye vituo vya Petroli na Dizeli

$
0
0
Na. Johary Kachwamba - MAELEZO, DODOMA

Serikali  imewahimiza Wananchi kudai risiti pindi wanunuapo mafuta kwenye vituo vya kuuza Petroli na Dizeli ili kurahisisha ukusanyaji wa Kodi ya Mapato, Aidha kutokuchukua risiti ni kosa kisheria hivyo wote muuzaji na mnunuzi  wanastahili adhabu kwa mujibu wa sheria.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Nchemba amesema hayo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mhe. Rukia Ahmad, Mbunge wa Viti Maalum aliyehoji kwanini Serikali isitoze kodi kwa jumla pale vituo hivyo vinaponunua mafuta

Mhe. Nchemba amesema ulipaji wa kodi ya mapato hususani kwa makampuni yanayouza mafuta unafuata mfumo wa wafanyabiashara kujikadiria wenyewe na kulipa kodi kama ilivyoainishwa kwenye Sheria ya Kodi ya Mapato sura 132, kisha ukaguzi wa hesabu kufuata baadaye.

“baada ya kubaini kuwa kuna udhaifu katika utoaji risiti ambao husababisha upotevu wa mapato, Serikali imeanzisha mfumo wa matumiz ya mashine ya kodi ya kielektroniki kwenye biashara mbalimbali ikiwa ni pamoja na vituo vya kuuza mafuta” Mhe. Nchemba.

Hata hivyo mfumo wa matumizi ya mashine za kodi za kielektroniki katika kutoa risiti za mauzo umetekelezwa kwa awamu mbili, awamu ya kwanza iiwahusu wafanyabiashara waliosajiliwa na kodi ya ongezeko la thamani (VAT) wakati awamu ya pili inahusu wafanyabiashara wengine waliobaki

“vituo vingi vya mafuta nchini havijasajiliwa na kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwa kuwa mafuta ya Petroli na Dizeli hayatozwi kodi ya VAT” aliongezea Mhe. Nchemba

Kodi za Ushuru wa bidhaa, ushuru wa mafuta na ushuru wa Petroli hukusanywa Forodhani mara tu bidhaa hizi zinapoingizwa nchini, isipokuwa kwa mafuta ya Petroli na Dizeli yanayoenda nchi za jirani. Kodi hizi ulipwa forodhani na makampuni yanayoagiza mafuta ya Petrol na dizeli kwa kuzingatia kiasi cha ujazo wa lita zilizoingizwa nchini kabla ya kuuza kwenye vituo vya mafuta.

NANI KUIBUKA KINARA WA TUZO ZA FILAMU TANZANIA!

$
0
0
  Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifwamba(kulia) akielezea jambo kwa wana habari(hawapo pichani) wakati wa kutangaza walioingia katika hatua ya mwisho ya kushindania Tuzo za Filamu Tanzania leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na wana habari uliofanyika katika hotel ya New Africa ya jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tuzo hizo Caroline Gul na mmoja wa wadhani kutoka International Eye Hospital Dr. Recep Yujel.
Jaji mkuu katika mchakato wa mchujo Issa Mbura kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akitoa ufafanuzi wa vipengere 11 vilivyoainishwa kushindaniwa. 
 Afisa Masoko kutoka EATV/EA Radio Happy Shame ambao ni moja ya wadhamini wa tuzo hizi akitoa neno kwa niaba ya wadhamini wa Tuzo za Filamu Tanzania.
  Mwakilishi kutoka Push Mobile Bwana Ezekiel akielezea namna ya upigaji kura ili kupata washindi tuzo hizi kubwa nchini.
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images