Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46360 articles
Browse latest View live

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NDANI YA JIMBO LA SAME MAGHARIBI MKOANI KILIMANJARO

$
0
0
 ,Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana ukielekea katika kijiji cha Gonjanza kata ya Suji,kuzindua mradi wa masi safi na salama sambamba na kuzungumza na wananchi,wilaya ya Same Magharibi mkoani Kilimanjaro.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpungia mkono mkazi wa kijiji cha Gonjanza kata ya Suji,Msafara wa Kinana ulikuwa ukielekea katika hicho kuzindua mradi wa masi safi na salama sambamba na kuzungumza na wananchi,wilaya ya Same Magharibi mkoani Kilimanjaro. 
Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi ikiwa pamoja na kukagua,kusimamia na kuhimiza ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi Dk.David Mathayo David wakinywa maji ya bomba mara baada ya Katibu Mkuu kuzindua mradi wa maji safi na salama kwa wananchi wa kijiji cha Gonjanza kata ya Suji
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akimtiwsha ndoo ya maji mkazi wa kijiji cha Gonjanza kata ya Suji
 wakazi wa kijiji cha Gonjanza kata ya Suji wakifurahia kupatikana kwa maji katika kijiji hicho,ambapo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi Dk.David Mathayo David walizindua mradi huo 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijibu baadhi ya changamoto za wananchi wa Hedaru waliomsomea kwenye risala yao, Katibu Mkuu alipita Hedaru kushiriki na kukagua ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Hedaru.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi Dk. David Mathayo David wakati wa mapokezi katika kata ya Njoro .Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi ikiwa pamoja na kukagua,kusimamia na kuhimiza ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wananchi wa kata ya Njoro ikiwa ni kituo cha kwanza katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM jimbo la Same Magharibi. 
  Wananchi wa kata ya Njoro wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akiwapongeza kwa uamuzi wao wa kujenga shule ya sekondari katika kata yao.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupanda miti kwenye eneo la shule ya sekondari ya Njoro,jimbo la Same Magharibi ikiwa sehemu ya utunzaji mazingira.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi wakishiriki ujenzi wa madarasa ya shule ya sekondari ya kata ya Njoro. 
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo la Same Magharibi na kuwataka wajumbe hao kuhimiza umoja kati ya wana CCM na kuwapongeza kwa ushindi mzuri wa serikali za mitaa. Katibu Mkuu pia alisisitiza kuwa kutokana na tatizo la maji kuwa kubwa nchi,CCM itahakikisha kwenye ilani yake mpya kuipa kipaumbele cha kwanza maji safi na salama kwa watanzania.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipiga gitaa wakati wa mkutano wa kuwasalimia wananchi kijiji cha Makanye ,jimbo la Same Magharibi.  

 wanancho wakifurahia jambo 
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Unezi Nape Nnauye wakiwa wameongozana na wananchi katika kijiji cha Gonjanza kata ya Suji,wakielekea kuzindua mradi wa maji
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufukia mabomba ya maji katika kijiji cha Gonjanza pamoja na Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi Dk.David Mathayo David

WanaIlboru wadhamiria kurejesha fahari ya Shule yao!!

Rebecca Malope, Solly kuwasili Aprili 4

$
0
0
MUIMBAJI nguli wa Kimataifa wa nyimbo za Injili, Rebecca Malope anatarajia kuwasili Jumaosi ya Aprili 4 akitokea Afrika Kusini kwa lengo la kupanda jukwaa la maadhimisho ya miaka 15 ya Tamasha la Pasaka.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo imekamilika kwa kiasi kikubwa hivyo mashabiki wa muziki wa injili  hapa nchini kujitokeza kwa wingi kufanikisha tamasha hilo ambalo litakuwa ni la aina yake.

Msama alisema mwimbaji mwenzake raia wa Afrika Kusini naye pia anatarajia kuwasili Jumamosi akitokea Afrika Kusini na kundi lake ambalo litatoa burudani kwa wakazi wa Dar es Salaam.Msama alisema Muingereza Ifeanyi Kelechi na Eiphraim Sekeleti wanatarajia siku moja kabla ya kuwasili Malope na Mahlangu.

“Tamasha la mwaka huu lina mambo mengi ambayo yataendana na miaka 15 ya tamasha hilo kubwa hapa Tanzania kwa sababu linashirikisha waimbaji wa Kimataifa na viongozi wakubwa serikalini ambao hufikisha ujumbe wa serikali na neno la Mungu pia,”alisema Msama.

Msama alisema muimbaji Mtanzania anyeishi Kenya Faustine Munishi anatarajia kuwasili Aprili 3 kwa lengo la kufikisha ujumbe wa Neno la Mungu  kupitia waimbaji na viongozi wa dini watakaojitokeza uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kitabu cha Dira na Tumaini Jipya Handeni

$
0
0
Picha juu na chini ni mwandishi wa habari za michezo wa gazeti la Bingwa, Dimba na Mtanzania kutoka Kampuni ya New Habari 2006 Ltd, Sharifa Mmasi pichani akisoma kitabu cha Dira na Tumaini Jipya Handeni kilichoandikwa na Kambi Mbwana, ambaye ni Mratibu Mkuu wa Tamasha la Handeni Kwetu linalofanyika kila mwisho wa mwaka wilayani Handeni, mkoani Tanga. 

MWANDISHI wa Habari za Michezo ambaye pia ni Mratibu Mkuu wa Tamasha la Utamaduni la Handeni Kwetu, Kambi Mbwana, ameandika kitabu chake kinachojulikana kama ‘Dira na Tumaini Jipya Handeni’, kilichoanza kupatikana mapema wiki hii jijini Dar es Salaam na wilayani Handeni, mkoani Tanga.

Kitabu hicho kimeelezea kero na changamoto mbalimbali za wananchi wa Handeni, kama vile shida ya maji, elimu na migogoro ya ardhi kwa ajili ya kushirikisha mawazo ya viongozi wa serikali, wadau na wananchi ili kukabiliana na tatizo hilo wilayani humo na mikoa ya jirani ambapo changamoto hizo zinashabihiana kwa kiasi kikubwa.
Sharifa Mmasi akisoma kitabu cha Dira na Tumaini Jipya Handeni, kilichoandikwa na Kambi Mbwana.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mbwana alisema kwamba kuandika kitabu hicho kuna lengo kubwa la kuelimisha jamii kwa ajili ya kutafuta fursa ya kimaendeleo katika wakati huu ambao wananchi wengi wamekuwa wakilia bila kupata msaada wowote.

“Naijua vizuri wilaya yangu ya Handeni na mkoa wa Tanga kwa ujumla, hivyo nimeamua nitumie kipaji change katika kuandika kitabu hiki ambacho kimeweza kuanika mambo mengi yenye tija kwa serikali na wananchi kwa ujumla, hivyo naomba waniunge mkono kwa kuhakikisha kwamba wanapata kitabu hiki popote kitakapokuwapo.

Kinapatikana kwa bei ndogo mno ya Sh 3500 kwa kuwa sikuwa na lengo la kutajirika kwa kupitia kitabu hiki bali kutoa mawazo yangu na kuelimisha jamii yangu inayonizunguuka, hivyo ni wakatai wa Watanzania wote, bila kusahau wakazi na wananchi wa Handeni kupata nafasi ya kusoma mawazo yangu kwa ajili ya kutafuta namna ya kufika mbali kiuchumi na kiutamaduni, ukizingatia kuwa kitabu kimegusia mambo kadhaa ambayo ni muhimu,” alisema Mbwana.

Kwa mujibu wa Mbwana, maeneo yanapopatikana kitabu hicho kwa jijini Dar es Salaam ni pamoja na ambapo ni Kinondoni Kwa Manyanya, kwenye kituo cha basi kwa muuza magazeti aliyekuwa pembeni ya ghorofa la Mwaulanga, Sinza Kijiweni kwenye studio inayoangaliana na lango la New Habari 2006 Ltd, upande wa wanaokwenda mjini, huku studio hiyo ikiwa karibu na duka la vifaa vya ujenzi. 

Maeneo mengine ni muuza magazeti wa Kimara Mwisho kwenye kituo cha basi cha wanaokwenda mjini, huku Buguruni kikipatikana katika studio ya upigaji wa picha karibu na Hoteli ya New Popex, Buguruni, jijini Dar es Salaam.

Aidha Mbwana alisema kwa wanaotaka kuwasiliana naye juu ya kitabu hicho cha Dira na Tumaini Jipya Handeni wanaweza kumpata kwa +255 712053949 au barua pepe; kambimbwana@yahoo.com.

MALI MUPYA IMEINGIA @AK CLASSIC COSMETICS WAPI WAREMBO WA MUJINI!!?

$
0
0


WADADA WOTE WANAOTAKA KUPIGA MSASA NGOZI ZAO BASI HAPA KIJIWE NDIO HIKI... @AKCLASSIC WANA BIDHAA ADHIMU KWA AJILI YAKO KUANZIA UNYAYONI MPAKA UTOSINI!! NINI KINAKUPA STRESS WEWE? 

JE WATAKA KUNG'AA?AU UNYWELE HAUJAI AMA KUNYONYOKA?UNASWEAT SANA KULIKO KAWAIDA? UNA CHUNUSI NA MABAKA?UNATAFUTA MAKE UP NZURI KWA GHARAMA NAFUU?UNATAKA KUPUNGUA UZITO NA TUMBO LAKO LINASUMBUA? UNA DARK CIRCLE (MIWANI) AMA MICHIRIZI?AU WEUSI WA MAPAJANI ULEEE?AMA UNATAKA KUWA NA RANGI MOJA MWILI MZIMA? 
PITIA BAADHI YA MAMBO YAO HAPA....


TUNAPATIKANA KINONDONI KWA AMANYANYA NA MLIMANI CITY KWA NJE.  
 TUPIGIE  TUPIGIE /0753482909
BIDHAA ITAKUFIKIA POPOTE ULIPO!!



ASILIMIA 40 YA WANAWAKE Z’BAR WANAISHI MAISHA DUNI

$
0
0
DSC_0081
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi (aliyefunikwa mwamvuli) akiwasili kwenye sherehe ya siku ya wanawake duniani iliyoandaliwa na Zanzibalicious Women Group na kufanyika ndani ya ukumbi wa Salama, Bwawani Hotel mwishoni mwa wiki.

Na Mwandishi wetu, Zanzibar
UTAFITI uliofanywa na taasisi ya wanawake nchini Zanzibar ya Zanzibalicious Women umeonyesha kuwa asilimia 40 ya wanawake Zanzibar, wanaishi katika mazingira duni ya umasikini kwa kutojitambua na kukosa elimu ya uelewa jinsi ya kukabiliana na mazingira waliyomo.

Akisoma risala siku ya wanawake mbele ya mgeni rasmi mke wa rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , Mama Mwanamwema Shein , katika siku ya wanawake hafla iliyofanyika hoteli ya Bwawani, Mweka hazina wa Zanzibalicious Women Group, Shekha Hilal alisema hali hiyo ni changamoto kubwa na sasa kunatafutwa namna ya kumfikia mwanamke huyu ambaye ameshagota katika jamii yetu.

“Mama Shein asilimia hii ni kubwa saana, na sisi kama wanawake ambao tayari tumejaaliwa elimu na tunajitambua, ikiwa ni pamoja na tayari tumepiga hatua kimaendeleo katika nyanja mbalimbali, tumeguswa sana sana na suala hili.” Alisema Shekha.

Zanzibalicious ni umoja wa wanawake wanaoishi Zanzibar,ulioanzishwa mwaka 2011,na kusajiliwa rasmi mwaka 2013, ikiambatana na uzinduzi uliofanyika tarehe 28 Machi 2014.
DSC_0227
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mama Mwanamwema Shein akiwasili kwenye sherehe ya siku ya Wanawake duniani iliyoandaliwa na Zanzibalicous Women Group mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Salama, Bwawani Hotel.


Mweka hazina huyo alisema kwamba wanajiuliza maswali mengi kama mwanamke huyo elimu ya kujikwamua imemfikia au kama kuna jitihada zozote za kumfikishia elimu hiyo.“Je hili ni jukumu la serikali peke yake? Au sisi tunatakiwa tujumuike na serikali? mheshimiwa mgeni rasmi tumeona ya kwamba tuungane pamoja na serikali katika kutekeleza suala hili.” Alisema Shekha akielezea nia ya taasisi hiyo ya kuondoa umaskini miongoni mwa wanawake nchini Zanzibar.

Alisema taasisi yao inajipanga kutoa elimu za aina mbili ili awali kumuwezesha kujikimu kupitia ujasiriamali, kwa kumpatia elimu kwa vitendo,kwa mfano:-ushonaji,ufugaji na utengenezaji wa bidhaa mbali mbali na pili kumtoa katika hali ya upweke ili elimu atakayopata imfikishe kwenye mifuko mbali mbali pamoja na mfuko wa Rais Dk. Ali Mohammed Shein .
Alisema katika program hiyo wanatarajia baada ya miaka 2 wanawake 100 watakuwa wanajitegemea wenyewe na kuwa mabalozi katika kuelimisha wanawake wengine zaidi.
DSC_0471
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mama Mwanamwema Shein akisoma hotuba wakati wa sherehe ya siku ya wanawake duniani iliyoandaliwa na Zanzibalicous Women Group na kufanyika ndani ukumbi wa Salama, Bwawani hoteli mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akifuatiwa na Mwenyekiti mstaafu wa Zanzibalicious Women Group, Bi. Ummukulthum Ansel.

“Na kama kila mwanamke akiweza kuelimisha wanawake katika kaya yake ,baada ya miaka kadhaa, Zanzibar itakuwa na wanawake walioweza kujikomboa katika dimbwi hili la kuishi maisha duni.” Alisema.

Akizungumzia mafanikio ya asasi hiyo alisema kwamba imefanikiwa kutoa elimu na kuwawezesha kina mama kuunda vikundi vidogo vidogo vya maendeleo kwa kuanzisha miradi mbalimbali, kwa mfano kina mama wa Chaani na Matemwe. Aidha imetoa misaada ya hali na mali kwa waathirika wa madawa ya kulevya ikiwa ni moja ya kumkwamua mwanamke na kutoa misaada mbali mbali kwa wanawake wasiojiweza ikiwemo hospital kuu ya Mnazi mmoja na kina mama wajane.

Alisema pamoja na mafanikio hayo bado wanawake wanakabiliwa na changamoto za ndoa za utotoni, uzazi salama, ukatili wa kijinsia,mfumo dume, ubaguzi na mimba za utotoni.
Mhe.Mgeni rasmi, Umoja huu umekuwa ukiendesha shughuli zote tokea mwaka 2011 kwa kutegemea michango yetu sisi binafsi.
DSC_0314
Baadhi ya wakinama waliohudhuria sherehe hiyo wakionekana kufurahishwa na hotuba ya Mke wa Rais wa Zanzibar (hayupo pichani).
Changamoto hii imesababisha kutokutimiza kwa malengo yetu kwa muda tulioupanga kutokana na kukosa fedha za kutosheleza utekelezaji wa malengo hayo.
Akijibu risala hiyo Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mama Mwanamwema Shein, ameikumbusha jamii kuunganisha nguvu zao kuwakomboa wanawake kujiendeleza kimaisha na kujiongezea kipato.
Alisema hatua hiyo itaongeza kasi ya kuimarisha ustawi wa familia na jamii hususan wanawake wanaoishi vijijini ambao wanakabiliwa na changamoto zaidi.
Alisema sherehe ya siku ya wanawake duniani inakuwa na maana zaidi kama juhudi zitafanyika kuangalia changamoto na kujipanga kuzifanyia kazi.
“Rai yangu ni kuwa tuwazingatie zaidi akina mama wanaoishi vijijini na wenye mahitaji maalum kutokana na kukosa fursa kama hizo za kuwaendeleza kimaisha”, alisisitiza.
DSC_0344
Mweka hazina wa Zanzibalicious Women Group, Bi. Shekha Hilal akisoma risala kwa mgeni rasmi Mke wa Rais wa Zanzibar (hayupo pichani) Kulia ni Mwenyekiti wa Zanzibalicous Women Group, Bi. Evelyne Wilson.
Aidha, aliongeza kuwa wanawake ni jeshi kubwa ambalo likiandaliwa vyema linaweza kushinda katika mapambano yanayokusudiwa huku akisisitza mshikamano ili kufikia malengo yanayowekwa.
Akizungumzia ujumbe wa sherehe hizo ambao ni kuhamasisha hatua mathubuti kumwendeleza na kumtambua mwanamke, alitoa rai kwa wanawake kushirikiana na serikali katika kampeni za kupambana na madhila wanayokabiliana nayo ikiwa ni pamoja na ukatili wa watoto na wanawake.
Kuhusu uzoefu wake katika maisha na malezi ya watoto, alisema amebahatika kupata watoto 11 ambao amewalea katika mazingira mbalimbali ikiwa ni kwenda na kurudi kazini na kuwa pekee huku mumewe akiwa safarini kikazi.
Aidha, aliwataka wanawake kuwa wastahamilivu katika malezi ya watoto hasa watoto Njiti ambao huzaliwa kabla ya kufikisha muda.
Hata hivyo aliwaonya wanawake wanaojali kujiremba na kuwa sahau watoto na kukumbusha kwa ‘watoto ni wageni’ kwamba wanahitaji matunzo na ukarimu mkubwa kutoka kwa wazazi wao.
IMG_6571
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akizindua Mfuko wa Zanzibalicious Women Group kwa kuchangia shilingi milioni tano, wakati wa maadhimisho ya sherehe ya wanawake duniani visiwani Zanzibar yaliyoandaliwa na Zanzibalicious Women Group na kufanyika katika ukumbi wa Salama uliopo Bwawani Hotel Zanzibar. Kulia ni Mwenyekiti wa Zanzibalicious Women Group, Bi Evelyne Wilson Baruti.
DSC_0082
Mweka hazina wa Zanzibalicious Women Group, Shekha Hilal akinakili majina ya watu waliokuwa wakichangia kwenye harambe ya mfuko wa Zanzibalicous Women Group uliozinduliwa rasmi na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (hayupo pichani).
DSC_0074
Mbunifu nguli wa mavazi Mama wa mitindo, Asia Idarous akinadi moja ya nguo alizotengeneza kwa ajili ya kuchangia mfuko wa Zanzibalicious Women Group.
DSC_0075
Mke wa Naibu Waziri wa Afya serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bi. Zakhia Kombo akitangaza dau la kununua nguo hiyo iliyokuwa ikinadiwa kwenye harambe ya mfuko wa ZWG iliyozinduliwa na Mama Mwanamwema Shein.
DSC_0091
Meza kuu kwenye picha ya pamoja na Zanzibalicous Women Group.
Unaweza kutembelea mtandao wao na kuona shughuli mbalimbali walizozifanya hapahttp://www.zanzibalicious.org/
DSC_0388
Mmoja wa wadhamini ZANLINK wanaotoa udhamini kwa Zanzibalicious Women Group wakisikiliza kwa makini yaliyokuwa yakijiri ukumbini hapo. Kwa picha zaidi bofya link hii

WAKONGWE WA DANSI ABBU OMAR NA FRESH JUMBE WALIVYO BARIKI ONYESHO LA ALLY CHOKI KULE TOKYO,JAPAN

$
0
0
Wanamuziki wa kongwe wa muziki wadansi Abbu Omar Njenga aka Abbu Omar na Fresh Jumbe Mkuu wenye ngome yao nchini Japan,siku ya jumamosi 21 Machi 2015 walitia fora kwa kushiriki jukwaani na kumpa baraka zote mwanamuziki Ally Choki katika onyesho lililofanyika katika ukumbi wa Sonudai-Kanagawa Prefecture, Sagamihara City,Tokyo ,Japan.

Wakongwe hao waliobobea katika muziki kwa maiaka mingi Abbu Omar Njenga mpiga gitaa au mpini na mtunzi aliyewahi kutamba na bendi za UDA JAZZ na mwaka 1981 alijiunga na Simba wa Nyika nchini Kenya na hatimaye kujikita nchini Japan kwa miaka mingi na mwenziwe mkongwe Fresh Jumbe Mkuu aliewahi kuwa mwimbaji mtunzi wa bendi za Dar International (Super Bomboka),DDC Mlimani Park "Sikinde na pia Juwata Jazz band aka Msondo Ngoma ,wakongwe hawa ni mfano wa kuigwa pamoja na kuwa
wameliteka soko la muziki wa kiafrika nchini japani na kungineko lakini wapo mstari wa mbele kuwaunga mkono na kuhakikisha kuwa wanamuziki wa nyumbani Tanzania waingiapo Japan wanateka soko.

 Pia mnaweza kujumuika na mmoja wao at 


Imeripotiwa na Hiroshi Takeuchi
Tokyo,Japan,

William Lukuvi aanza ziara mkoani rukwa.

$
0
0
1
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Manyanya alipowasili uwanja wa ndege wa Sumbawanga kuanza ziara ya kutatua migogoro ya ardhi Mkoani humo.
New Picture (7)
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akimpokea Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi alipowasili eneo la Jangwani mjini Sumbawanga kuweka jiwe la msingi katika nyumba za makazi zinazojengwa na NHC kwa ajili ya kuuzia wananchi.
New Picture (1)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akisalimiana na Kamishna msaidizi wa ardhi kanda ya nyanda za juu kusini Bw. Msigwa mara alipowasili Mkoani Rukwa kutatua migogoro ya ardhi.
New Picture (5)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akitoa msimamo wa dhati wa serikali (kwa wananchi waliofurika kumsikiliza hawapo pichani) wenye nia ya kutatua mgogoro wa ardhi uliopo kati ya mwekezaji na wananchi wa vijiji vya Skaungu na Mawensuzi alipofika katika eneo la Malonje Wilayani Sumbawanga.
New Picture (12)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akihutubia halaiki ya wananchi waliohudhuria sherehe za uwekaji jiwe la msingi kwenye nyumba za makazi zinazojengwa na NHC eneo la Jangwani Mkoani Rukwa. Alisisitiza Halmashauri nchini kutenga ardhi kwa ajili ya NHC kujenga nyumba za gharama nafuu.
New Picture (11)
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akitoa maelezo ya mradi wa nyumba za makazi zinazojengwa na NHC eneo la Jangwani mjini Sumbawanga kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi (hayupo pichani) jana.
New Picture (13)
Mbunge wa Sumbawanga Mhe. Hilal Aeshi akiishukuru NHC kwa kujenga nyumba za makazi eneo la Jangwani kwa ajili ya kuuzia wananchi.
New Picture (4)
Mwenyekiti wa kijiji cha Skaungu Bw. Pascal Mwanakatwe akisoma risala kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi kuelezea mgogoro wa ardhi unaokabili kijiji hicho na mwekezaji kanisa la Efatha baada ya Waziri Lukuvi kufika eneo la Malonje kuwasikiliza wananchi ili serikali ipate mwelekeo wa kutatua mgogoro huo.
New Picture (2)
Watendaji wa sekta ya ardhi wakiratibu mazungumzo ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi alipozungumza na watendaji wa Mkoa wa Rukwa (hawapo pichani ) juu ya migogoro ya ardhi inayowasumbua wananchi.
New Picture (3)
Wananchi wa kijiji cha Skaungu wakimsikiliza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi alipofika kijiji kilichopo kilomita 50 kutoka mjini Sumbawanga kueleza nia ya serikali ya kumaliza mgogoro wa wananchi na Kanisa la Efatha ambalo ni mwekezaji na mmiliki wa mashamba yanayolalamikiwa na wananchi na kukisababisha mauaji ya mara kwa mara.
New Picture (9)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akiweka rasmi jiwe la msingi katika nyumba za makazi zinazojengwa na NHC eneo la Jangwani mjini Sumbawanga kwa ajili ya kuuzia wananchi. Nyumba hizo zinatarajiwa kukamilika mwezi Juni mwaka huu.
New Picture (8)
Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa NHC Bw. Haikamen Mlekio akitoa maelezo ya ujenzi unaofanyika eneo la Jangwani kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi alipowasili kuweka jiwe la msingi la nyumba hizo jana.
New Picture (6)
Kikundi cha ngoma za kifipa kikiburudisha wananchi waliohudhuria sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi nyumba za makazi zinazojengwa na NHC eneo la Jangwani Sumbawanga muda mfupi kabla ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi kuwasili eneo hilo.
New Picture (14)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akisikiliza na kupokea barua za malalamiko ya wananchi waliofurika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa jana ili kuwasilisha kero zao za ardhi.

RAIS KIKWETE APOKEA RIPOTI YA CAG

$
0
0
3
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Profesa Musa Assad akimkabidhidhi Ripoti yake Rais  Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo
4
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikifungua Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali muda mfupi baada ya kukabidhiwa na Mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Profesa Musa Assad(kushoto)ikulu jijjini Dar es Salaam leo.Kulia anayeshuhudia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue5
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maofisa waandamizi kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuju wa Hesabu za Serikali mufa mfupi kabla ya mkuu wa taasisi hiyo Profesa Musa Assad(Watatu kushoto) kuiwasilisha ikulu jijini Dar es Salaam leo.Watano Kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue. (picha na Freddy Maro) 

MEMBE MGENI RASMI TAMASHA LA PASAKA

$
0
0
Mwenyekiti  wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana (hawapo pichani) kuhusu maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika Aprili 5, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi, Jimmy Charles. (Picha na Francis Dande)
 Msama akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya tamasha hilo.
Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Jimmy Charles akifafanua jambo.
………………………………………………………………………………..

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Pasaka litakalofanyika Aprili 5 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika kwa asilimia 97 hivyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi siku hiyo. 

Alisema wameshakamilisha maandalizi ya tamasha hilo, ila kinachosubiriwa ni waimbaji  wa kimataifa Ephraim Sekeleti wa Zambia, Ifeanyi Kelechi kutoka Uingereza, Rebeca Malope na Thori Mahlangu wote kutoka Afrika Kusini pamoja na Faustine Munishi ‘Malebo’ kuanza kuwasili
nchini.

“Tamasha la mwaka huu litakuwa la aina yake kwani tutakata keki, kupiga fataki kama ishara ya kutakiana amani, upendo  na mshikamano na tutaiombea nchi yetu  kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika  Oktoba mwaka huu’’alisema Msama.

Msama aliongeza kuwa tamasha la mwaka huu litabeba ujumbe mahsusi wa ‘amani na upendo ndio amani kwa watanzania’, aidha tamasha hilo pia litatumika kupiga vita maauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi ‘Albino’.Aliongeza kuwa ukiachia mgeni Waziri Membe, pia wageni mashuhuri watahudhuria tamasho hilo akiwemo rais mstaafu ali Hassani Mwinyi ambalo linatimiza miaka 15 tangu kuanzishwa.

MHE. LUKUVI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA NYUMBA MPYA ZA MAKAZI ZA NHC MJINI SUMBAWANGA, APOKEA MALALAMIKO MBALIMBALI YA MIGOGORO YA ARDHI KUTOKA KWA WANANCHI WA MKOA WA RUKWA

$
0
0
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wa tatu kulia na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya wa kwanza kushoto wakikagua mradi wa ujenzi wa nyumba 20 za makazi zinazojengwa na Shirikia la Nyumba la Taifa (NHC) katikati ya Manispaa ya Sumbawanga tarehe 26/03/2015. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Ndugu Nehemia Mchechu nyumba hizo ambazo ni za ghorofa moja zitauzwa baada ya kukamilika ujenzi wake kwa njia ya fedha taslimu na njia ya Mikopo ya benki. 
Waziri wa Ardhi Mhe. William Lukuvi katikati akiweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa nyumba 20 za makazi zinazojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa Mjini Sumbawanga kwa kushirikiana na viongozi wengine wa chama na Serikali Mkoani Rukwa tarehe 26/03/2015.
Waziri wa Ardhi Mhe. William Lukuvi kushoto akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Ndugu Nehemia Mchechu katika hafla fupi ya uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa nyumba za makazi za shirika hilo Mjini Sumbawanga.
Michoro ya mradi huo.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiongea na wananchi (hawapo pichani) wenye malalamiko mbalimbali yanayohusu migogoro ya ardhi Mkoani Rukwa katika ukumbi wa RDC Mjini Sumbawanga tarehe 26/03/2015. Mhe. Lukuvi aliwatangazia wananchi wenye malalamiko sugu wamuandikie wakiambatisha na vielelezo husika na kuviwasilisha kwake ili aweze kuvifanyia kazi, alisema kuwa "..ni muda sasa wa kuponya mioyo ya watu ambao wamezulumika kwa muda mrefu..." Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya. 
Mzee Julius Nkana Mkazi wa Sumbawanga akiwasilisha malalamiko yake ya mdomo na maandishi kuhusu mgogoro wa ardhi kwa Mhe. William Lukuvi. Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya Migogoro takribani yote iliyowasilishwa ilionekana kuibuka kutokana na maeneo mengi yasiyo rasmi ambayo hayajapimwa na kupewa umiliki unaotambulika kisheria. Aliongeza kuwa ipo haja kubwa ya Serikali na mamlaka husika kuimarisha eneo la upimaji wa maeneo na kutoa umiliki wa ardhi kuazia viwanja vya makazi na mashamba kuepusha migogoro ya kuzulumiana ardhi ambayo imekua ikiua  kwa kasi siku hadi siku.
Waziri wa Ardhi Mhe. William Lukuvi kulia akipokea malalamiko ya maandishi ya migogoro ya ardhi kutoka kwa wananchi wa Mkoa wa Rukwa waliopanga mstari katika ukumbi wa RDC.
Zoezi hilo liliambatana na mahojiano mbalimbali ambapo kwa wale wenye malalamiko ambayo kesi zake zipo mahakamani na hazijatolewa uamuzi walishauriwa kuendelea na kesi zao mpaka zitakapomalizika, Ama kwa wale ambao kesi zao zinatatulika zitafanyiwa kazi na Wizara ya ardhi ambapo Waziri husika Mhe. William Lukuvi aliahidi kujibu barua zao za malalamiko, Malalamiko hayo pia yatafanyiwa kazi na Ofisi ya Kamishna wa Ardhi nyanda za juu kusini, Ofisi ya baraza la ardhi Mkoa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimuhoji diwani wa Kata ya Kizwite Ndugu Mavazi (kushoto) kuhusu malalamiko ya muwekezaji Ndugu Azizi Tawaqal (wa pili kushoto) kuhusu madai kuwa wananchi wanamtumia katika kuuza mashamba yaliyonunuliwa na ndungu Aziz Tawaqal licha ya kuwa walishalipwa fidia. Kesi hiyo bado ipo mahakamani na Mhe. Waziri amemuagiza Kamanda wa Polisi Wilaya ya Sumbawanga (OCD) kusimamia sheria kuhakikisha maeneo hayo hayauzwi na hakuna shughuli yeyote inayoendelea mpaka kesi iliyopo mahakamani ikamilike na kutoa uamuzi.     
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa@Rukwareview.blogspot.com)

INDIA YADHAMIRIA KUKABILIANA NA WIZI KUPITIA MASHINE ZA ATM

$
0
0

Katika Mkutano uliofanyika Nchini India, Mbali na maelezo ya jitihada na dhamira kubwa katika kuwekeza katika maswala ya teknolojia kupitia kampeni yao ya DIGITAL INDIA, Pia nchi imepata kuelezea dhamira yao ya kuwekeza zaidi kwa kutoa misaada ya kimasomo ( Scholarships ) kwa wale watakao kuwa wakisomea masomo yatakayo wezesha kukuza na kufanikisha jitihada zao za Digital India.


Aidha, Kwa Upande mwingine – Wameweza kukubali tatizo linalo ambatana na ukuaji wa technolojia ni uhalifu mtandao huku ikielezwa watumiaji wa simu wamefikia asilimia 97% ya raia wa nchini humo, kitu ambacho kinapelekea matumizi mtandao kuingiwa na dosari ya kipekee.


Itakumbukwa India kupitia taarifa inayosomeka kwa "KUBOFYA HAPA" waziri mkuu wan chi hiyo alihimiza wananchi wake kujikita zaidi katika kutengeneza namna ya kukabiliana na uhalifu mtandao ambapo pia iweze kutumika kutoa misaada kwa nchi nyingine.


Katika Kikao cha siku mbili, Kubwa la kiusalama mtandao ni dhamira kubwa ya moja kati ya washiriki wa mkutano huo kuonyesha dhamira yao kubwa ya kukabiliana na tishio la uhalifu kupitia mitandao ( Hasa Wizi wa fedha kupitia ATM) linalo tikisa mataifa mbali mbali hivi sasa.


Katika mazungumzo yangu maalum yaliyo ambatana na mahojianao na vyombo vya habari katika kuangazia dhamira yao hii ya kukabiliana na uhalifu mtandao kupitia wizi wa ATM, Nilipata kuunganisha mawazo na kujua namna gani Taifa la Tanzania tunaweza kuwekeza zaidi kukabiliana na hali hii ambayo pia ni tishio katika Mabenki yetu.


Moja ya mambo muhimu katika hili ambalo nimeona nililete nyumbani ni kuhakikisha tunaongeza aina ya tatu ya utabulisho katika miamala inayofanyika hivi sasa ya kifedha katika ATM zetu zote za mabenki yote. Hili litaongeza usalama katika miamala na pia tayari mataifa yaliyo jaribu aina hii ya suluhisho katika wizi mtandao imeanza kuonyesha matunda.


Natoa Wito kwa mabenki kuangazia hili, na pia na imani kubwa mabenki ya Tanzania yatakaa na kutafakari njia hii rafiki ya kuhakikisha miamala ya wateja wao inaweza kubaki salama ili kuongeza imani kwa wateja wao juu ya fedha zao na wao kutopata hasara kubwa inayopatikana hivi sasa kwenye miamala ya biashara kupia mashine za ATM.

SIMBACHAWENE AIOMBA BENKI YA DUNIA KUISAIDIA TANESCO

$
0
0
00Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (mbele ) akiongoza kikao kilichokutanisha ujumbe kutoka Benki ya Dunia na watalaam wa Wizara ya Nishati na Madini ili kujadili maendeleo ya miradi ya nishati nchini inayofadhiliwa na Benki hiyo, changamoto zake na kupata mapendekezo ya kuboresha miradi hiyo.
……………………………………………………………………………….
Na Greyson Mwase, Dar es Salaam
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene ameliomba Shirika la Fedha Duniani (WB) kulisaidia Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) ili liweze kuimarisha miradi ya usambazaji wa umeme nchini hususan vijijini.
Simbachawene aliyasema hayo wakati alipokutana na ujumbe kutoka Benki ya Dunia na watalaam wa Wizara ya Nishati na Madini ili kujadili maendeleo ya miradi ya nishati nchini inayofadhiliwa na Benki hiyo, changamoto zake na kupata mapendekezo ya kuboresha miradi hiyo.
Alisema kuwa Tanesco inakabiliwa na changamoto ya fedha katika utekelezaji wa miradi ya umeme hususan usambazaji wa umeme vijijini na kupelekea miradi mingi kutokamilika kwa wakati.
Akielezea maendeleo ya shirika hilo la umeme, Simbachawene alisema kuwa shirika hilo limeongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato kwa kubuni mikakati mbalimbali ya ukusanyaji wa mapato hayo na kupunguza hasara zilizokuwa zikijitokeza mara kwa mara.
Akielezea kuhusu upunguzaji wa bei ya umeme nchini, Simbachawene alisema kuwa Serikali imejenga bomba kubwa la gesi kutoka Mtwara hadi jijini Dar es Salaam jambo litakalochangia upatikanaji wa nishati ya umeme ya uhakika na kwa gharama nafuu ambalo ni moja ya utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa.
“ Ili kuhakikisha wananchi wananufaika na sekta mpya ya gesi, serikali ilibuni utaratibu wa kusomesha wataalam pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo ya sayansi katika vyuo vikuu vinavyotoa fani za mafuta na gesi ili kuwa na wataalamu watakaosimamia kwa ufanisi sekta ya gesi na mafuta.,” alisema Simbachawene .
Aliongeza kuwa mara baada ya kuwa na wataalam waliobobea katika masuala ya gesi na mafuta, serikali itaunda taasisi itakayokuwa na kazi ya kutoa ushauri katika masuala ya gesi na mafuta hususan wakati wa uingiaji wa mikataba.


“ Kwa mfano kuna uwekezaji mkubwa unaohitaji mamilioni ya Dola za Marekani, kwa mfano Ujenzi wa Viwanda vya Gesi ya Kimiminika (LNG), uwekezaji huu unahitaji timu ya wataalam watakaohakikisha kuwa maslahi ya nchi yanazingatiwa,” alisisitiza Simbachawene.
Aliongeza kuwa, mbali na kuzalisha wataalam, serikali kwa sasa inaandaa sheria kwa ajili ya sekta za gesi na mafuta ambapo mpaka sasa maoni kutoka kwa wadau mbalimbali yamekusanywa na kujumishwa.
Akielezea kuhusu uwazi katika mikataba ya gesi na mafuta, Simbachawene alisema kuwa Serikali imeweka mkakati wa kuhakikisha kunakuwepo na uwazi katika shughuli zake, moja ya mikakati hiyo ni pamoja na kujiunga na Taasisi ya Kimataifa inayojihusisha na Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Uziduaji (EITI) ambapo taarifa mbalimbali za malipo na makusanyo katika sekta za madini na gesi zimekuwa zikikusanywa na kusambazwa kwa wananchi.
Aliendelea kusema kuwa, Serikali inafuata sheria zinazosimamia utoaji wa taarifa za mikataba. 
Wakati huo huo Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi, Philippe Dongier alisema kuwa Benki ya Dunia ipo tayari kushirikiana na Serikali kupitia Shirika la Tanesco ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata umeme wa uhakika na nchi kutoka katika kundi la nchi masikini dunaiani na kuwa katika kundi la nchi zenye kipato cha kati.
Dongier alisema awali Benki ya Dunia ilijitosa kuisaidia Tanesco ili iweze kutoka kwenye utegemezi wa chanzo kimoja cha nishati ya umeme yaani maji na kutumia vyanzo vingi ikiwa ni pamoja na kupelekea ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi jijini Dar es salaam ambalo mara baada ya ukamilishwaji wake litapunguza gharama ya uzalishaji wa umeme na wananchi wengi kunufaika na nishati hiyo.
Pia Dongier alimpongeza Waziri Simbachawene kwa hatua ya serikali kujenga bomba la gesi na kasi ya uandaaji wa sera kwa ajili ya usimamizi wa sekta mpya za gesi na mafuta na kusisitiza kuwa Benki ya Dunia ipo tayari kushirikiana na Serikali kuhakikisha kuwa malengo yake yanatekelezwa.

SIMBACHAWENE AIOMBA BENKI YA DUNIA KUISAIDIA TANESCO

$
0
0
00Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (mbele ) akiongoza kikao kilichokutanisha ujumbe kutoka Benki ya Dunia na watalaam wa Wizara ya Nishati na Madini ili kujadili maendeleo ya miradi ya nishati nchini inayofadhiliwa na Benki hiyo, changamoto zake na kupata mapendekezo ya kuboresha miradi hiyo.
……………………………………………………………………………….
Na Greyson Mwase, Dar es Salaam
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene ameliomba Shirika la Fedha Duniani (WB) kulisaidia Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) ili liweze kuimarisha miradi ya usambazaji wa umeme nchini hususan vijijini.
Simbachawene aliyasema hayo wakati alipokutana na ujumbe kutoka Benki ya Dunia na watalaam wa Wizara ya Nishati na Madini ili kujadili maendeleo ya miradi ya nishati nchini inayofadhiliwa na Benki hiyo, changamoto zake na kupata mapendekezo ya kuboresha miradi hiyo.
Alisema kuwa Tanesco inakabiliwa na changamoto ya fedha katika utekelezaji wa miradi ya umeme hususan usambazaji wa umeme vijijini na kupelekea miradi mingi kutokamilika kwa wakati.
Akielezea maendeleo ya shirika hilo la umeme, Simbachawene alisema kuwa shirika hilo limeongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato kwa kubuni mikakati mbalimbali ya ukusanyaji wa mapato hayo na kupunguza hasara zilizokuwa zikijitokeza mara kwa mara.
Akielezea kuhusu upunguzaji wa bei ya umeme nchini, Simbachawene alisema kuwa Serikali imejenga bomba kubwa la gesi kutoka Mtwara hadi jijini Dar es Salaam jambo litakalochangia upatikanaji wa nishati ya umeme ya uhakika na kwa gharama nafuu ambalo ni moja ya utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa.
“ Ili kuhakikisha wananchi wananufaika na sekta mpya ya gesi, serikali ilibuni utaratibu wa kusomesha wataalam pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo ya sayansi katika vyuo vikuu vinavyotoa fani za mafuta na gesi ili kuwa na wataalamu watakaosimamia kwa ufanisi sekta ya gesi na mafuta.,” alisema Simbachawene .
Aliongeza kuwa mara baada ya kuwa na wataalam waliobobea katika masuala ya gesi na mafuta, serikali itaunda taasisi itakayokuwa na kazi ya kutoa ushauri katika masuala ya gesi na mafuta hususan wakati wa uingiaji wa mikataba.


“ Kwa mfano kuna uwekezaji mkubwa unaohitaji mamilioni ya Dola za Marekani, kwa mfano Ujenzi wa Viwanda vya Gesi ya Kimiminika (LNG), uwekezaji huu unahitaji timu ya wataalam watakaohakikisha kuwa maslahi ya nchi yanazingatiwa,” alisisitiza Simbachawene.
Aliongeza kuwa, mbali na kuzalisha wataalam, serikali kwa sasa inaandaa sheria kwa ajili ya sekta za gesi na mafuta ambapo mpaka sasa maoni kutoka kwa wadau mbalimbali yamekusanywa na kujumishwa.
Akielezea kuhusu uwazi katika mikataba ya gesi na mafuta, Simbachawene alisema kuwa Serikali imeweka mkakati wa kuhakikisha kunakuwepo na uwazi katika shughuli zake, moja ya mikakati hiyo ni pamoja na kujiunga na Taasisi ya Kimataifa inayojihusisha na Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Uziduaji (EITI) ambapo taarifa mbalimbali za malipo na makusanyo katika sekta za madini na gesi zimekuwa zikikusanywa na kusambazwa kwa wananchi.
Aliendelea kusema kuwa, Serikali inafuata sheria zinazosimamia utoaji wa taarifa za mikataba. 
Wakati huo huo Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi, Philippe Dongier alisema kuwa Benki ya Dunia ipo tayari kushirikiana na Serikali kupitia Shirika la Tanesco ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata umeme wa uhakika na nchi kutoka katika kundi la nchi masikini dunaiani na kuwa katika kundi la nchi zenye kipato cha kati.
Dongier alisema awali Benki ya Dunia ilijitosa kuisaidia Tanesco ili iweze kutoka kwenye utegemezi wa chanzo kimoja cha nishati ya umeme yaani maji na kutumia vyanzo vingi ikiwa ni pamoja na kupelekea ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi jijini Dar es salaam ambalo mara baada ya ukamilishwaji wake litapunguza gharama ya uzalishaji wa umeme na wananchi wengi kunufaika na nishati hiyo.
Pia Dongier alimpongeza Waziri Simbachawene kwa hatua ya serikali kujenga bomba la gesi na kasi ya uandaaji wa sera kwa ajili ya usimamizi wa sekta mpya za gesi na mafuta na kusisitiza kuwa Benki ya Dunia ipo tayari kushirikiana na Serikali kuhakikisha kuwa malengo yake yanatekelezwa.

MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATI YA BARAZA LA USHAURI WA KISIASA LA WATU WA CHINA AWASILI ARUSHA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Ushauri wa Kisiasa la Watu wa China pia Waziri wa Idara ya Kimataifa wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Dk.wakati wa mapokezi kwenye uwanja wa ndege wa KIA.


Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Ushauri wa Kisiasa la Watu wa China pia Waziri wa Idara ya Kimataifa wa kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China amewasili nchini kuja kushiriki kwenye ufunguzi wa Kongamano la Viongozi Vijana wa Afrka pamoja na China litakaloanza leo mjini Arusha.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye  akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Ushauri wa Kisiasa la Watu wa China pia Waziri wa Idara ya Kimataifa wa kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Dk.Wang Jiarui wakati wa mapokezi kwenye uwanja wa ndege wa KIA.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na  Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Ushauri wa Kisiasa la Watu wa China pia Waziri wa Idara ya Kimataifa wa kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Dk.Wang Jiarui mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA ambapo atashiriki kwenye ufunguzi la Kongamano la Viongozi Vijana wa Afrika na China litakaloanza leo mjini Arusha.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Ushauri wa Kisiasa la Watu wa China pia Waziri wa Idara ya Kimataifa wa kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Dk.Wang Jiarui akizungumza  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (kushoto) pamoja na Mkuu wa mkoa wa Arusha Ndugu Daudi Felix Ntibenda kwenye hotel ya Ngurdoto,Arusha.


ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NA UJUMBE WAKE JIMBO LA SAME MASHARIKI.

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo mafupi namna  Tangawizi inavyosindikwa katika kiwanda hicho,ambapo Katibu Mkuu Ndugu Kinana alishuhudia kiwanda hicho kukabidhiwa mashine za kuchakata Tangawizi kutoka SIDO.Kiwanda hicho kilizinduliwa na Rais Kikwete mnamo Oktoba,2012.Katika taarifa iliyosomwa kiwandani hapo inaeleza kuwa kiasi cha fedha zaidi ya shilingi bilioni 500 zimetumika kwa ajili ya ujenzi pamoja na shughuli nyingine za kujenga uwezo ili kuhakikisha kiwanda hicho kinafanya kazi kwa ufanisi.
 Meneja wa SIDO mkoa wa Kilimajaro Bwa.Daniel Njowero akikabidhi nyaraka za mashine mpya za kuchakata Tangawizi kwa Mwenyekiti wa Bodi wa Kiwanda cha Tangawizi,Bwa.Yonaz Yohana Mgonja,huku Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakishuhudia.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kusuka nondo za nguzo za daraja la Mang’a Myamba wakati alipokagua ujenzi wa Daraji hilo Same Mashariki mkoani Kilimanjaro.Ujenzi wa Daraja hilo ni ahadi iliyoitoa Rais Kikwete kwa wananchi wa Same Mashariki katika suala zima la utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010
 Ujenzi wa daraja la Mang’a Myamba,Same Mashariki ukiendelea,Ujenzi wa Daraja hilo ni ahadi iliyoitoa Rais Kikwete kwa wananchi wa Same Mashariki katika suala zima la utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010


Big, Dua Saidi kuanza maisha mapya SHIWATA

$
0
0

MCHEZAJI wa zamani wa Simba na Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars”, Dua Said na muingizaji wa Bongo Movie, Lumole Matovola “Big” na Mwenyekiti wa Wasanii Tanzania  (SHIWATA), Cassim Taalib ni miongoni mwa wasanii 48 walioamua kwenda kuanza maisha ya kijijini.

Wakizungumza katika mkutano wa bodi ya SHIWATA jana, wasanii hao walisema meamua kuungana na wasanii wengine wanaokwenda kuanza maisha mapya katika kijiji cha Wasanii, Mwanzega Mkuranga ambapo watapatiwa mashamba ya kulima bustani na mazao ya muda mfupi.

Dua Said alisema amevutika na kujiji hicho na amekuwa mmoja wa wachezaji wa zamani kuanza maisha ya kijiji cgha wasanii ambayo alisema ni mazuri yenye manufaa kulinganisha na maisha ya mjini.

“Nimefika kijijini Mwanzega na mimi nimejengewa nyumba yangu na SHIWATA, pia nimerekodi filamu ambayo mtaiona katika luninga ni maisha mazuri ya kijijini  ambayo huwezi kufananisha na mjini” alisema Big.

Mwenyekiti wa SHIWATA, Taalib alisema kati ya wanachama 8,000 ambao wamepanga kuhamia Mkuranga kwa ajili ya kilimo na ufugaji watashiriki katika sherehe za kutimiza miaka kumi kutoka ianzishwe na jumla ya nyumba 134 zimejengwa.

 Alisema mtandao huo unasikitishwa na taarifa ambazo siyo za kweli kuwa ndani ya mtandao huo kuna utapeli na kuongeza kuwa wanataarifu wanachama wo wote kwamba mpango huo ni wa kweli, uhakika na uwazi  hakuna mwanachama hata mmoja atakayepoteza haki yake kwa kujiunga na SHIWATA.

Alisema Wanachama waliojiunga na SHIWATA kutoka mwaka 2004 na kufanikiwa kulipa sh. 10,000 za kujiunga na kijiji cha Mwanzega kupitia mtandao huo na kupatiwa hati wanatakiwa kufika ofisini Ilala Bungoni na nyaraka zao zote ili wapelekwe kijijini kukabidhiwa maeneo yao.

Alisema pia wanachama wote waliochangia ujenzi ya nyumba zao kwa kiasi chochote cha fedha kupitia benki wanatakiwa kufika ofisini na nyaraka zao zote ili nao wakakabidhiwe maeneo yao kwa kadri walivyochangia.

Alisema waliochangia katika mgawo wa mashamba katika shamba la Ngarambe na hatajakabidhiwa mashamba yao wanatakiwa wafike ofisini na nyaraka zao ili wakakabidhiwe.

Alisema kijiji ambacho wanaamini kitakuwa kivutio kwa watalii nchini kitapewa jina la Tallywood na kutangazwa nchi mbalimbali duniani na kitakuwa maarufu kwa utengenezaji filamu ambazo zitauzwa ndani na nje ya Tanzania.

RAIS WA ZIMBABWE ROBERT MUGABE AWASILI JIJINI ARUSHA LEO,KUFUNGUA KONGAMANO LA 3 LA VIONGOZI VIJANA WA AFRIKA NA CHINA

$
0
0
 Makamu wa Rais Dk Gharib Bilal akizungumza jambo na Rais wa Zimbambwe,Mh.Robert Mugabe mara mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA,mapema leo mchaa.Rais Mugabe anatarajiwa kufungua  Kongamano la Viongozi Vijana wa Afrika na China litakaloanza leo mjini Arusha.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiteta jambo  na Rais wa Zimbabwe,Mh.Robert Mugabe mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA mapema leo mchana.Rais Mugabe anatarajiwa kufungua  Kongamano la Viongozi Vijana wa Afrika na China litakaloanza leo mjini Arusha..
  Makamu wa Rais Dk Gharib Bilal akimpomkea mgeni wake,Rais wa Zimbabwe,Mh.Robert Mugabe mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa KIA,mapema leo mchana.Rais Mugabe anatarajiwa kufungua  Kongamano la Viongozi Vijana wa Afrika na China litakaloanza leo mjini Arusha.
 Baadhi ya Wanahabari wakihangaika kupata taswira ya kuwasili kwa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ambaye alipokelewa na Makamu wa Rais Dkt.Gharib Bilal na viongozi mbalimbali wa Kitaifa na Kidini
 Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe akiwasili mapema leo mchana
kwenye uwanja wa ndege wa KIA.Rais Mugabe anatarajiwa kufungua  Kongamano la Viongozi Vijana wa Afrika na China litakaloanza leo katika hotel ya Ngurdoto mjini Arusha.

WANAFUNZI WA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA(TPSC) TAWI LATANGA WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO PSPTB

$
0
0
1
Wageni wakiwasili kwenye ofisi za Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi.
New Picture (3)
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa PSPTB, Dr Tesha akitoa hutuba ya ufunguzi kuwakaribisha wanachuo wa mwaka wa pili wa stashahada ya Ununuzi na Ugavi kutoka chuo cha TPSC Utumishi wa Umma tawi la Tanga.
New Picture (4)
Wanachuo wakimsiliza Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Bodi Dr. Tesha.
New Picture (5)
Mkurugenzi ya Mafunzo, Bw. Godfred Mbanyi akielezea juu ya madaraja ya mitihani ya Bodi na taratibu za kufanya mitihani.

New Picture (7)
Bw. Ally Songoro kutoka Kurugenzi ya Taaluma akifafanua jambo, juu ya taratibu za usajili, miiko ya wanataaluma kwa wanachuo waliotembelea Bodi.
New Picture (9)
Bw. Paul Bilabaye kutoka Kurugenzi ya Fedha na Utawala akielezea taratibu za malipo ya huduma mbalimbili zitolewazo na Bodi.
New Picture (10)
Mwanachuo mmoja akiuluza maswali juu ya kazi mbalimbali za Bodi Wataalam wa Ununuzi na Ugavi.
New Picture (11)
Mmoja wa wanachuo akiuliza maswali juu ya kazi mbalimbali za Bodi Wataalam wa Ununuzi na Ugavi.
New Picture (1)
Wanachuo wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye ofisi za Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi.
New Picture (2)
Baadhi ya wanafunzi kwenye picha ya pomoja pamoja na mkurugenzi Mkurugenzi mtendaji wa Bodi Dr. Clemence Tesha na viongozi waandamizi wa Bodi.
.....................................................................
Na Mwandishi wetu
Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imepokea ugeni wa wanachuo sabini wa mwaka wa pili wanaosoma stashahada ya ununuzi na ugavi waliokuja kwenye ziara ya mafunzo kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma tawi la Tanga. Ziara hiyo ya mafunzo ililenga kujua kazi mbalimbali za Bodi ya wataalam wa ununuzi na Ugavi (PSPTB). 

Mkurugenzi mkuu Mtendaji wa PSPTB Dr Clemence Tesha, aliupokea ugeni huo, na kuwashukuru kwa kuona nia ya kufanya ziara ya mafunzo. Aidha aliwaelezea umuhimu wa kuzingatia maadili , kujifunza kwa bidii ili kupata maarifa na ujuzi unaoweza kuhimili soko la ushindani la ajira .Wanachuo pia walielezewa juu ya taratibu za mitihani ya Bodi yenye ngazi ya cheti cha awaliAwali, msingi Msingi na Taaluma.

 Aidha aliwaelezea taratibu za kusajii kwa ajili ya kufanya mitihani ya kitaaluma mara baada ya kumaliza masomo yao na kwamba mhitimu wa stashahada ya ununuzi na ugavi kwa chuo kinachotambuliwa na Bodi anaanzia ngazi ya kwanza ya mitihani ya taaluma. Mitihani ya taaluma ina ngazi tano, ambazo huhitimishwa kwa wanafunzi kufanya mitihaniutafiti.Ziara hiyo pia ilitoa fursa kwa wanachuo hao kujua taratibu za kujisajili kama wataalum wataalam wa Ununuzi na Ugavi kwani ni hitaji la sheria iliyounda Bodi. Aidha walifahamishawa kwamba kuna ngazi mbalimbali za usajili ambazo zinatambua kiwango cha ujuzi na uzoefu wa mtaalam.

“ fanyeni usajili mara mmalizapo chuo ili kutumia fursa za ajira katika fani yenu “ ” alisisitiza. Tambueni kwamba taaluma ya ununuzi na ugavi inaongozwa na misingi ya maadili ambayo inawataka kutambua kuwa mnawajibika kwa umma wa watanzania, taaluama yenu, mwajili wako. Misingi hii ya wajibu ndio inayoifanya taaluma hii iwe ya kipekee. “maadili huanzia

Rais Kikwete Afungua Mkutano wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya mrisho Kikwete akifungua mkutano wa Viongozi wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNICC) jijini Dar es Salaam leo. 
Baadhi ya viongozi wa madhehebu ya dini mbalimbali wakimsikiliza kwa makini Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa akiwahutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Viongozi wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam leo.(picha na Freddy Maro).
Viewing all 46360 articles
Browse latest View live




Latest Images