Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46194 articles
Browse latest View live

RAIS MUSEVENI NA RAIS NKURUNZINZA WAWASILI NCHINI TAYARI KWA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA UKANDA KATI

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Bernard K. Membe (Mb) akimpokea Rais wa Uganda Mhe.Yoweri Kaguta Museveni  alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam. Mhe. Rais Museveni yupo nchini kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Ukanda wa Kati kuhusu Uwekezaji na Viwanda unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuanzia tarehe 25 hadi 26 Machi, 2015.
Rais Museveni akipokea shada la maua kutoka kwa mtoto Balkis Mvungi kama ishara ya kumkaribisha nchini Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Bernard Membe akimpokea Rais wa Burundi Mhe.Pierre Nkurunziza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimatafa wa Mwalimu Julius Njerere.
Rais Nkurunziza akipokea shada la maua kutoka kwa mtoto Balkis Mvungi kama ishara ya kumkaribisha nchini Tanzania.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

TASAF YAWAFUNDA WAANDISHI WA HABARI WA MIKOA YA LINDI NA MTWARA

0
0
 Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF unaendelea kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari ili waweze  kutumia vyombo vya habari vilivyoko kwenye maeneo yao kutangaza habari za Mpango wa kunusuru kaya masikini unaoratibiwa naMfuko huo.

Akifungua mafunzo hayo yanayoendeshwa kwa utaratibu wa Kikao Kazi Mkurugenzi Mtendajiwa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga amesema kazi ya kutokomeza umaskini nchini inahitaji ushiriki wa wadau mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari.

Bwana Mwamanga amesema tangu TASAF ianze kutekeleza Mpango wa kunusuru kaya masikini kumekuwa na mafanikio makubwa hususani katika maeneo ya walengwa ambao wameanza kuboresha maisha yao na katika baadhi ya maeneo walengwa wameanza kukuza shughuli za kiuchumi huku wengine wakiweza kuhudumia kaya zaokinyume na hali ilivyokuwa huko nyuma.

Amewasihi waandishi wa habari kuwatembelea walengwa wa Mpango huo ili kuona namna walengwa hao wanavyonufaika na Mpango huo wa uhawilishaji fedha na kisha kutangaza mafanikio yaliyokwisha patikana huku akisisitiza kuwa hata pale penye changamoto zionyeshwe ili marekebisho yafanyike kwa manufaa ya walengwa
Zifuatazo ni baadhi ya picha za washiriki wa kikao kazi hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo kikuu Huria Mjini Mtwara.
 Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Bwana RenatusMongogwela (mwenye shati nyeupe)akizungumza na ujumbe wa TASAF ulioongozwa na Mkurugenzi mtendaji Ladislaus Mwamangawa, kwanza kushoto kwa kaimu katibu tawala.
  Mkurugenzi Mtendajiwa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga aliyesimama akifungua kikao kazi cha watendajiwa TASAF kutoka maeneo ya utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya maskini na waandishi wa habari wa mikoa ya Mtwara na Lindi (hawapopichani) 
 Washiriki wa kikao kazi cha watendaji wa TASAF  na waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga(hayupo pichani).
 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF bwana  Ladislaus Mwamanga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa TASAF makao makuu baada ya kufungua kikao kazi cha waandishi wa habari wa mikoa ya Mtwara na Lindi.
 Mkurugenzi Mtendajiwa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa TASAF makao makuu baada ya kufungua kikao kazi cha waandishi wa habari wa mikoa ya Mtwara na Lindi.

PRESIDENT KIKWETE OPENS CENTRAL CORRIDOR SUMMIT IN DAR ES SALAM

0
0
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete delivers his keynote address during the opening session of the Central Corridor Presidential Round Table and High Level Industry and investor Forum held at Julius Nyerere International Conference Centre in Dar es Salaam this morning. Third left seated is President Yoweri Kaguta Museveni of Uganda, fourth left is Burundi’s President Pierre Nkurunzinza, and second left is DRC’s Minister for Transport Justin Kaumba Mwana Ngongo.
4
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete speaks with President Yoweri Kaguta Museveni of Uganda(left) and President Pierre Nkurunzinza of Burundi shortly before the commencement Central Corridor Presidential Round Table and High Level Industry and investor Forum held at Julius Nyerere International Conference Centre in Dar es Salaam this morning.5
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete welcomes President Yoweri Kaguta Museveni of Uganda and Pierre Nkurunzinza of Burundi for the Central Corridor Presidential Round Table and High Level Industry and investor Forum held at Julius Nyerere International Conference Centre in Dar es Salaam this morning.

1
23  
(photos by Freddy Maro).

JEMBE FM YA MWANZA YAPEWA LESENI

0
0
DSC_0644
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi leseni kwa redio ya Jembe FM ya jijini Mwanza kwenye ofisi za makao makuu ya TCRA jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).

Na Mwandishi wetu.
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Profesa John Nkoma ametaka matumizi sahihi ya masafa ya radio yanayatumiwa kurusha vipindi vya radio kwa ajili ya maendeleo ya umma.

Kauli hiyo ameitoa jana wakati akikabidhi leseni kwa radio Jembe FM.
Alisema matumizi yasiyo sahihi yatasababisha mamlaka hiyo kunyang’anya leseni walioitoa kwa ajili ya maslahi ya taifa. Alisema pamoja na haja ya kushiriki katika ushindani, kituo hicho kipya kinatakiwa kufuata masharti ya utangazaji ambayo yamo katika leseni waliyoiomba. Alisema radio hiyo ya Mwanza inaongeza ushindani katika eneo hilo katika jumla ya radio FM 12 zinazosikika mjini humo, radio za kitaifa saba, za kikanda 11 na radio ya jamii 1.

Aliwataka kuwa waangalifu na kufuata kanuni za kitaalamua kufanyakazi wanasotahili za kuelimisha na kuburudisha.
DSC_0650
Alisema si radio tu ambayo ina nguvu ndiyo inayoweza kuhimili ushindani lakini pia ufuataji wa kanuni na maadili katika utekelezaji wa majukumu yao. Naye Mkurugenzi Mkuu wa Jembe FM, Dk. Sebastian Ndege amesema kwamba wameanzisha radio hiyo kwa lengo la zaidi ya kuburudisha na kuelimisha bali kusaidia vijana kushika hatamu na kujitengenezea uwezo wa ajira.

Alisema kwamba ili kuhakikisha kwamba wanafanyakazi kitaaluma wameajiri watu ambao wamesomea kazi husika ili kuhakikisha kwamba hawaendi kinyume na leseni yao. Alisema kwamba wanaamini kwamba wana nafasi kubwa ya kujaza mapengo ambayo yapo katika urushaji wa matangazo kwa sasa ili kuhudumia mji wa Mwanza ambao unakua kwa kasi kwa sasa.
DSC_0676
Mkurugenzi wa sheria wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA), Fortunata Mdachi (kushoto) akisisitiza jambo kwa uongozi wa JEMBE FM wakati wa hafla ya kukabidhi leseni kwa uongozi huo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam makao makuu ya ofisi za TCRA. Alisema vipindi vyao vimezingatia haja ya jamii katika uchumi, elimu na afya. 
Aidha amesema kwamba wanategemea kuwa na vipindi vizuri zaidi hasa kutokana na na uzoefu waliokuwa nao hasa wa uandaaji wa njia ya panda.
Jembe FM inamilikiwa na Jembe Media Limited.
DSC_0669
Mkurugenzi Mkuu wa Jembe FM Dk Sebastian Ndege (wa kwanza kushoto) na uongozi wa juu kabisa wa Jembe Media Limited wakimsikiliza kwa makini kabisa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa leseni rasmi ya kurusha matangazo ya redio ya JEMBE FM ya jijini Mwanza.
DSC_0655
Baadhi ya wawakilishi wa kampuni ya Ndege Insurance inayomilikiwa na Dk. Sebastian Ndege waliojumuika kwenye hafla hiyo fupi.
DSC_0665
Maofisa mbalimbali kutoka Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo.
DSC_0683
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma (kulia) akimkabidhi rasmi leseni ya kurusha matangazo ya redio ya JEMBE FM ya jijini Mwanza, Mkurugenzi Mkuu wa Jembe FM, Dk Sebastian Ndege (katikati) katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya ofisi za TCRA jijini Dar. Kushoto ni Mkurugenzi wa sheria wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA), Fortunata Mdachi.
DSC_0712
Mkurugenzi Mkuu wa Jembe FM, Dk Sebastian Ndege akitoa neno la shukrani ambapo pia maeahidi kuwa atafuata masharti na kanuni zote zilizowekwa na mamlaka hiyo.
DSC_0725
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa juu kabisa wa Jembe Media Limited. Kutoka kushoto ni Mwanasheria wa Jembe Media Ltd. Justine Ndege, Mkurugenzi Mkuu wa Jembe FM, Dk Sebastian Ndege pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Jembe Media Ltd, Renata Ndege.
DSC_0733
Mkurugenzi Mkuu wa Jembe FM, Dk Sebastian Ndege na Mwanasheria wa Jembe Media Ltd. Justine Ndege wakionyesha leseni hiyo iliyoambatanishwa na miongozi ya Mamlaka ya Mawasiliano ya TCRA kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) waliohudhuria hafla hiyo.
DSC_0743

MAKALA YA SHERIA: JE INARUHUSIWA KUINGIZA MALI YA WANANDOA KATIKA MALI ZA MIRATHI ILI NDUGU WAZIGAWANE IWAPO MKE/MME AMEFARIKI

0
0

Nimekuwa nikiulizwa maswali mengi kila inapotoka makala. Nami nimeweka ahadi ya kukusanya maswali hayo na kuyajibu na si kuyajibu kwa kumjibu mtu aliyeuliza peke yake , hapana isipokuwa kwa kuyaweka katika makala ili umma wote ufaidike. Haya ni baadhi ya maswali ambayo nimeulizwa na haya ndiyo majibu yake.

1.JE MALI ALIYOPEWA MTU KABLA YA KIFO CHA MAREHEMU NAYO HUHESABIWA KATIKA KUGAWANA MIRATHI.

Yapo mazingira ambapo marehemu huwa amempa mtu/mrithi mali kabla ya kifo. Mara nyingi hii hujitokeza kwa baba au mama na mtoto ambapo baba/mama humpa mali mwanae hata kabla ya kifo. Hampi ile mali kama amemrithisha hapana isipokuwa anaweza kumpa sehemu ya mali pengine ili ajenge au sehemu ya shamba ili alime na wengine huwa wametoa vitu kama magari au hata nyumba. Swali ni je iwapo mtu amepewa vitu kama hivi au amepewa kimojawapo kati ya hivi ni sawa vitu hivi alivyopewa kuhesabiwa wakati wa kugawana mali za marehemu aliyempa mali hizo. Jibu ni ndiyo, sheria inasema iwapo marehemu hakuacha wosia basi wakati wa kugawana mali zake vile vitu ambavyo alivitoa kwa baadhi ya watu/ warithi yafaa vihesabiwa wakati wa mgawanyo wa mali.

Sio kwamba mtu atanyanganywa mali hizo hapana isipokuwa aliyekwishapewa hawezi kupata mgao sawa na yule ambaye hakuwahi kupewa chochote na marehemu wakati wa uhai. Ambaye hakuwahi kupewa chochote yafaa apate mgao zaidi kuliko yule aliyekuwa amepewa na marehermu kabla ya kifo. Isipokuwa hali itakuwa tofauti iwapo marehermu ameacha wosia. Ikiwa marehemu ameacha wosia basi kila mtu atapata kutokana na wosia unavyosema bila kujali nani alikuwa amepewa kabla na nani hakupewa kabla. Wosia utafuatwa hivyohivyo ulivyo.

2. JE INARUHUSIWA KUINGIZA MALI YA WANANDOA KATIKA MALI ZA MIRATHI ILI NDUGU WAZIGAWANE IWAPO MKE/MME NDIYE AMEFARIKI.

Yapo mazingira ambapo mke anaweza kumtangulia mume katika mauti au mme anaweza kumtangulia mke . Lakini mpaka kifo kinamkuta mmoja unakuta tayari kuna mali ambazo zilikuwa zimechumwa na wanandoa kwa pamoja na hivyo kuwa mali za familia. Hapo hapo unakuta kuna warithi kama watoto au ndugu wengine na wanataka mali zote ziingizwe katika orodha ya mirathi na zigawanywe. Swali ni je sheria inasemaje kuhusu jambo hilo. Sheria iko wazi kuwa katika mazingira kama hayo huwezi kuingiza mali zote kwenye mali za mirathi. Kinachotakiwa kufanyika ni kutoa kiwango cha mgao wa mali ambao alikuwa anastahili marehemu kama mgao wake katika mali kama mwanandoa .

Kusoma zaidi BOFYA HAPA

WAZIRI WA ARDHI MHE. WILLIAM LUKUVI AWASILI MKOANI RUKWA LEO, AAHIDI SULUHU YA MGOGORO WA MUDA MREFU WA SHAMBA LA SKAUNGU

0
0
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwasili katika uwanja wa ndege wa Mjini Sumbawanga leo tarehe 25/03/2013 kwa ajili ya ziara ya siku mbili Mkoani Rukwa moja ikiwa kufuatilia migogoro sugu ya ardhi ukiwemo wa shamba la Skaungu ambapo ameonana na wananchi na viongozi wa vijiji kumi vinavyolizunguka shamba hilo ambalo lina mgogoro wa muda mrefu kati ya Mmiliki Ephata Ministry na wananchi hao. Lengo la pili la ziara yake ni kuweka jiwe la msingi katika nyumba za makazi zinazojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katikati ya Mji wa Sumbawanga.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Eng. Stella Manyanya (kulia) akimtambulisha Waziri wa Ardhi Mhe. William Lukuvi kwa viongozi wa Serikali na Chama Mkoa wa Rukwa muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga.
Katika msafara wake Mhe. Waziri aliongozana na Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini Mhe. Aeshi Hillal (Pichani na Mdau Juddy Ngonyani wa Channel Ten), Mbunge wa Jimbo la Kwela Mhe. Ignas Malocha na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Eng. Stella Manyanya. 
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akizungumza na viongozi wa Vijiji kumi vya kata za Mollo na Msandamuungano vinavyozunguka sahamba la Skaungu lenye Mgogoro wa muda mrefu kati ya muwekezaji Ephata Ministry na wananchi wa vijiji hivyo. Mhe. Waziri amesema lengo la kufika kwake Mkoani Rukwa ni kuona maeneo ya mgogoro huo pamoja na kuwasikiliza wananchi na baadae kuonana na muwekezaji huyo kabla ya Serikali kufanya uamuzi wa hatma ya shamba hilo ambalo linadaiwa na wananchi kumega maeneo ya vijiji na hivyo kukosa maeneo ya kulima kutokana na ongezeko la watu. Alieleza kuwa taarifa zote kuhusu shamba hilo zimeshaifikia ofisi yake na kilichobaki ni kutoa uamuzi wa Serikali wa kumaliza Mgogogoro huo.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi alipofika katika Kijiji cha Skaungu kuongea na wananchi alipokelewa na mabango yenye ujumbe mbalimbali unaolenga kuiomba Serikali kusaidia upatikanaji wa ardhi yao ambayo ipo ndani ya shamba la Muwekezaji Ephata Ministry. Mhe. Lukuvi amewatoa hofu wananchi hao kuwa mgogoro huo utapata ufumbuzi kabla ya Serikali ya awamu ya nne haijamaliza muda wake.
 Ujumbe mwingine uliokuwa kwenye mabango hayo.
Ujumbe mwingine ukinyesha kuwa toka Kijiji hicho kianzishwe mwaka 2008 na kupewa hati wananchi hao wamekuwa hawana haki na sehemu ya ardhi yao ambayo ipo ndani ya shamba la Muwekezaji huyo. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Skaungu muda mfupi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Ardhi Mhe. William Lukuvi kuzungumzia lengo la ziara yake katika Kijiji hicho, alisema ni muda sasa kumaliza mgogoro huo.  

 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (kulia) akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Skaungu leo tarehe 25/03/2015. Alisema kuwa mgogoro huo unawanyima usingizi viongozi wa Serikali na imefika wakati sasa kuumaliza. Aliongeza kuwa iwapo Serikali itaamua sehemu ya shamba hilo irudi kwa wananchi basi halitagawiwa kiholela na badala yake utatumika utaratibu maalum kwa kushirikisha Halmashauri na Serikali ya Kijiji kwa kuanza kuwatambua wale wenye hitajio kubwa la ardhi na baadae kuwaangalia wananchi wengine wenye haki ya kupatiwa maeneo hayo.
 Wadau wa Habari Mkoa wa Rukwa wakitoka kuchukua matukio katika Kijiji cha Skaungu, Kutoka kulia ni Juddy Ngonyani (Channel Ten), Nswima Errrrrnest (TBC), Joshua Joel (ITV), Peti Siame (Habari Leo/Daily News), Gurian Adolph Ndingala FM na Mussa Mwangoka (Mwananchi).
 Bi. Anna Msafiri Mwananchi wa Kijiji cha Mawenzusi akitoa kero yake kwa Mhe. Waziri wa Ardhi.
Sehemu ya wananchi wa kijiji cha Mawenzusi ambao pia walipata fursa ya kupaza sauti zao kwa Waziri wa Ardhi Mhe. William Lukuvi.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa@Rukwareview.blogspot.com)

TAHARIRI: TABIA HII YA WAUZA MITUMBA SOKO LA MCHIKICHINI NI UDHALILISHAJI WA KIJINSIA

0
0
Baadhi ya wateja wa nguo wakichagua nguo kwenye soko la Mchikichini
Baadhi ya wateja wa nguo wakichagua nguo kwenye soko la Mchikichini jijini Dar es Salaam.

Na Andrew Chale wa Modewji blog.

Miongoni mwa mambo ya aibu katika jamii ni pamoja na masuala ya udhalilishaji wa kijinsia ukiwemo ule wa maungoni hasa kwa wanawake.Kwa muda mrefu mtandao huu umekuwa ukifuatilia vitendo hivyo vibaya kwa jamii vinavyofanywa na watu waliokosa ustaarabu hasa jamii ya vijana katika maeneo ya mikusanyiko ya watu wengi karibu maeneo mengi ikiwemo jiji la Dar es Salaam.

Miongoni mwa eneo linaloongoza kwa kuwadhalilisha wanawake ni eneo la soko la Mchikichini lililopo Ilala Mkoa wa Dar es Salaam. Mtandao huu umekuwa ukishuhudia vitendo hivyo vibaya kwa jamii ambapo wengi wa vijana wamekuwa wakifanya kwa makusudi kuwadhalilisha wanawake hasa wasichana wadogo kwa kuwashika maungoni (makalio, kifua/maziwa) huku wakiwalazimisha kununua bidhaa zao.

Vitendo hivi vimekuwa ni kama mchezo wa kawaida kwani vijana hao wamekuwa wakiendeleza hali hiyo kwa muda mrefu sasa huku wasichana/wakike hao wanaofanyiwa vitendo hivyo wakiwa hawana wa la kufanya, Mtandao huu tunasema huo ni udhalilishaji na unatakiwa kuchukuliwa hatua za haraka kukomeshwa kwani unakiuka maadili na utu wa mwanamke.
ka - kobe 528
Modewji blogtunatambua ipo mamlaka husika zinazoweza kulichukulia hatua suala hili basi kama zipo zianze sasa kwani udhalilishaji huu huko mbele unaweza kuleta madhara makubwa kwa mtendewa na hata anayetenda kwani akiachwa sasa baadae anaweza kufanya tukio kubwa na likafumbiwa macho ikiwemo kubaka.

Nachelea kuamini kama vijana hawa wanafanya hivi kwa kujiamini ama kuna nguvu ya msukumo nyuma yake? Kipindi cha nyuma sote tumekuwa tukishuhudia vijana hao wakiwachania nguo wanawake waliokuwa wakivaa vimini waliokuwa wakipita katikati ya mitaa ya Kariakoo wakati huo huo wamesahau kuwa nguo hizo wamewauzia wao, tukiacha hilo pia wapo hawa Makondakta wa daladala nao ni miongoni mwa watu wanaoongoza kufanya vitendo vya kidhalilishaji wanawake.

Mtandao huu umeweza kuliona hilo kwa upande wa Makondakta wa Daladala nyingi hasa nyakati za abiria wa kike anapopanda hatua ya kwanza wao wanapeleka mkono kwenye ‘Makalio’ ya Mwanamke na kumvutia ndani ya daladala, yaani kama sapoti ya kumuingiza ndani.

Kondakta anafanya hivyo wakati huo amekaa mlangoni mwa daladala yake, lakini anapopanda mwanaume usogea ndani ama hushuka chini bila hata ya kumshika, lakini akipanda Mwanamke tu utakuta Konda anamshika makalio kuona kwamba ni jambo la kawaida, Hivyo ni wakati sasa wa kubadilika jamani vitu vingine hivi ni kushusha utu wa mwanamke hivyo tubadilike na tuchukue hatua, Asante.

Tuma maoni yakoo hapa kwenye blog hii ama kupitia simu 0719076376

Article 13

0
0


UN yaadhimisha kumbukumbu ya waathirika wa biashara ya utumwa

0
0
Ofisa Habari wa UNIC, Stella Vuzo akisoma hotuba ya ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-moon kwenye maadhimisho ya kumbukumbu kuwakumbuka waathirika wa utumwa na biashara zake zilizoendeshwa eneo la Bahari ya Atlantiki. Ofisa Habari wa UNIC, Stella Vuzo akisoma hotuba ya ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-moon kwenye maadhimisho ya kumbukumbu kuwakumbuka waathirika wa utumwa na biashara zake zilizoendeshwa eneo la Bahari ya AtlantikiMshauri wa Masuala ya Haki za Binadamu wa UN nchini Tanzania, Chitralekha Massey akizungumza na vyombo vya habari katika maadhimisho ya kuwakumbuka waathirika wa utumwa na biashara zake. Mshauri wa Masuala ya Haki za Binadamu wa UN nchini Tanzania, Chitralekha Massey akizungumza na vyombo vya habari katika maadhimisho ya kuwakumbuka waathirika wa utumwa na biashara zake.Ofisa Habari wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Bi. Usia Nkhoma akiwasilisha mada kwa washiriki wa maadhimisho ya kuwakumbuka waathirika wa utumwa na biashara zake. Ofisa Habari wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Bi. Usia Nkhoma akiwasilisha mada kwa washiriki wa maadhimisho ya kuwakumbuka waathirika wa utumwa na biashara zakeOfisa Habari wa UNIC, Stella Vuzo akizungumza na vyombo vya habari kwenye maadhimisho ya kumbukumbu kuwakumbuka waathirika wa utumwa na biashara zake zilizoendeshwa eneo la Bahari ya Atlantiki. Ofisa Habari wa UNIC, Stella Vuzo akizungumza na vyombo vya habari kwenye maadhimisho ya kumbukumbu kuwakumbuka waathirika wa utumwa na biashara zake zilizoendeshwa eneo la Bahari ya Atlantiki.
Baadhi ya washiriki katika maadhimisho ya kumbukumbu kuwakumbuka waathirika wa utumwa na biashara zake zilizoendeshwa eneo la Bahari ya Atlantiki, wakifuatilia mada anuai. Baadhi ya washiriki katika maadhimisho ya kumbukumbu kuwakumbuka waathirika wa utumwa na biashara zake zilizoendeshwa eneo la Bahari ya Atlantiki, wakifuatilia mada anuai.Baadhi ya washiriki katika maadhimisho ya kumbukumbu kuwakumbuka waathirika wa utumwa na biashara zake zilizoendeshwa eneo la Bahari ya Atlantiki, wakifuatilia mada anuai. Baadhi ya washiriki katika maadhimisho ya kumbukumbu kuwakumbuka waathirika wa utumwa na biashara zake zilizoendeshwa eneo la Bahari ya Atlantiki, wakifuatilia mada anuai.Baadhi ya washiriki katika maadhimisho ya kumbukumbu kuwakumbuka waathirika wa utumwa na biashara zake zilizoendeshwa eneo la Bahari ya Atlantiki, wakiangalia picha anuai zinazoelezea juu ya biashara ya utumwa. Baadhi ya washiriki katika maadhimisho ya kumbukumbu kuwakumbuka waathirika wa utumwa na biashara zake zilizoendeshwa eneo la Bahari ya Atlantiki, wakiangalia picha anuai zinazoelezea juu ya biashara ya utumwa.Ofisa Habari wa UNIC, Stella Vuzo akizungumza na baadhi ya vijana kwenye maadhimisho ya kumbukumbu kuwakumbuka waathirika wa utumwa na biashara zake zilizoendeshwa eneo la Bahari ya Atlantiki. Ofisa Habari wa UNIC, Stella Vuzo akizungumza na baadhi ya vijana kwenye maadhimisho ya kumbukumbu kuwakumbuka waathirika wa utumwa na biashara zake zilizoendeshwa eneo la Bahari ya Atlantiki.Baadhi ya washiriki katika maadhimisho ya kumbukumbu kuwakumbuka waathirika wa utumwa na biashara zake zilizoendeshwa eneo la Bahari ya Atlantiki, wakizungumza na vyombo vya habari. Baadhi ya washiriki katika maadhimisho ya kumbukumbu kuwakumbuka waathirika wa utumwa na biashara zake zilizoendeshwa eneo la Bahari ya Atlantiki, wakizungumza na vyombo vya habari.Baadhi ya washiriki katika maadhimisho ya kumbukumbu kuwakumbuka waathirika wa utumwa na biashara zake zilizoendeshwa eneo la Bahari ya Atlantiki, wakiangalia filamu ya mafunzo kwenye maadhimisho hayo. Baadhi ya washiriki katika maadhimisho ya kumbukumbu kuwakumbuka waathirika wa utumwa na biashara zake zilizoendeshwa eneo la Bahari ya Atlantiki, wakiangalia filamu ya mafunzo kwenye maadhimisho hayo.Baadhi ya washiriki katika maadhimisho ya kumbukumbu kuwakumbuka waathirika wa utumwa na biashara zake zilizoendeshwa eneo la Bahari ya Atlantiki, wakifuatilia mada anuai. Baadhi ya washiriki katika maadhimisho ya kumbukumbu kuwakumbuka waathirika wa utumwa na biashara zake zilizoendeshwa eneo la Bahari ya Atlantiki, wakifuatilia mada anuai.[/caption].

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-moon amesema UN itaainisha eneo maalum na la kudumu mahususi kwa ajili ya kuwakumbuka waathirika wa utumwa na biashara za utumwa zilizoendeshwa Bahari ya Atlantiki. Ki-moon ametoa kauli hiyo kwenye hotuba yake maalum aliyoitoa leo kwenye tukio la kumbukumbu ya kuwakumbuka waathirika wa utumwa na biashara zake zilizoendeshwa eneo la Bahari ya Atlantiki. 

 Alisema sehemu hiyo maalum ya kumbukumbu itakayokuwa Jijini New York itatoa fursa kwa watu kutoka mataifa mbalimbali kufika eneo hilo na kujufunza mengi kupitia matukio yaliajiri nyuma kipindi cha utumwa. Alisema kwa taasisi za imataifa ikiwemo UN itatoa fursa kuangalia mikakati yao katika utendaji wa kazi ili kuhakikisha heshima, uhuru na usawa kwa binadamu wote vinalindwa sehemu zote. Alisema kwa mwaka huu maadhimisho ya kumbukumbu kwa biashara ya utumwa inawakumbuka zaidi wanawake ambao waliteseka na wengine hadi kuuwawa kutokana na biashara zautumwa.

 “…Wanawake wengi walipata mateso makubwa kutokana na biashara ya utumwa…walinyanyaswa, walitumika kimapenzi na walilazimishwa kuzaa na hata kuuza watoto wao bila kupenda…,” ilieleza taarifa ya Ki-moon. Alisema biashara ya utumwa bado inaendelea kwa baadhi ya nchi na kutolea mfano kwa mataifa ya Syria na Iraq ambayo hadi leo maelfu ya wanaume, wanawake na watoto wamekuwa wakitekwa kuteswa huku vijana na watoto wakinunuliwa na kutumika kwenye mapigano jambo ambalo ni utumikishaji mbaya. 

 Kwa upande wake Ofisa Habari wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Bi. Usia Nkhoma akiwasilisha mada kwa baadhi ya washiriki wa maadhimisho ya kuwakumbuka waathirika wa utumwa na biashara zake zilizoendeshwa eneo la Bahari ya Atlantiki, yaliyofanyika Dar es Salaam leo aliikumbusha jamii kujifunza kupitia historia. 

 Alisema UN iliamua kutumia siku ya kumbukumbu kuweza kutoa elimu kwa jamii juu ya masuala anuai yanayofanywa kinyume na haki za binadamu kumaliza chembe chembe za utumikiswaji. Aidha katika maadhimisho hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Alliance Francais wa jijini Dar es Salaam washiriki walipata kuona picha za maonesho kuzungumzia biashara ya watumwa pamoja na filamu anuai.

uzinduzi wa ushirika wa jitihada njema zanzibar

0
0

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinbuzi  Mhe. Ali

Mohamed Shein amesema kuanzishwa kwa vikundi vya ushirika (SACCOS) ni
njia moja ya kujiimarisha kiuchumi na kupambana na umasikini Visiwani  
Zanzibar.



Ameyaeleza hayo katika hafla ya uzinduzi wa Ushirika wa Jitihada Njema wa Bandari  ya Zanzibar huko ukumbi wa Hoteli ya Bwawani mjini
Zanzibar.




Amesema uanzishwaji  wa vikundi vya ushirika hasa wa vijana na
kinamama, ni njia ya kuendesha maeneo maalumu ya kufanyia shughuli zao
za Biashara ndogondogo pamoja na kuzitambua rasilimali ambazo ziko
kwenye sekta zisizo rasmi vikiwemo vikundi hivyo.


 Dr. Shein amesema lengo la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ya
awamu ya saba ambayo azma yao ni kuviimarisha vikundi vya ushirika
vinavyokwenda sambamba na ilani ya uchaguzi Mkuu ya Chama cha CCM ya
Mwaka 2010 ambalo amelibainisha wakati alipozinduwa Baraza la nne la
Wawakilishi  tarehe 11 Novemba 2010 katika hutuba yake ya uzinduzi
huo.


Aidha ameeleza kuwa kufanya hivyo ni kuimarisha Mfuko wa Uwezeshaji wa
wananchi kiuchumi ili kukuza uwezo wa kutowa mikopo kwa wananchi na
kuwawezesha kutumia fursa zilizopo katika maeneo yao.
Hata hivyo amesema Serikali itashirikiana nao katika kuzitafutia
ufumbuzi changamoto zinazowakabili ili waweze kupata ufanisi zaidi wa
kuendeleza vikundi vyao.


Wakiwasilisha risala yao wana kikundi cha ushirika wa Jitihada Njema
wameliomba Shirika la Bandari la Zanzibar kuwapatia kiwanja ili waweze
kujenga ofisi yao kwa lengo la kukiendeleza kikundi chao.


Pia wamesema kwamba lengo la Ushirika wao ni kuwapatia mikopo
wananchi, kuutangaza ushirika wao ndani ya jamii ili kuwatengenezea
ajira vijana, kutatuwa changamoto zinazowakabili wanaushirika hao,
kusaidia kujuwa mbinu mbalimbali za elimu na kuwarahisishia
upatikanaji wa Bima ya Afya.



Hata hivyo wamesema tatizo kubwa kwa sasa linalowakabili katika
kikundi cha ushirika wao  ni ukosefu wa ofisi  yenye eneo la kutosha
kwa ajili ya shughuli zao jambo ambalo linawarejesha nyuma kwa kiasi
kikubwa katika utendaji wao  kazi.


Ushirika huo ulianzishwa tarehe 31 Januari, 2004 ikiwa na wanachama
100 na hadi sasa una wanachama 200 na tayari wameshafunga mkataba wa
kupatiwa mikopo na Shirika la Bandari.



IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

TASWA YAWAPIGA MSASA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO 'SUPER D' AKIWEMO NDANI

0
0

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Bw. Dioniz Malinzi, akimkabizi cheti Rajabu Mhamila baada ya mafunzo ya uhandishi wa habari kulia ni mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto na  Katibu Mkuu wa Mchezo wa Riadha nchini Suleiman Nyambu ... (RT)
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akibadilishana mawazo na mwalimu wake wa habari za michezo Salim Said Salim wakati wa mapumziko mafupi ya mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Taswa jana.

Baadhi ya waandishi wa habari za michezo wakifatilia mafunzo hayo.
Waandishi wa habari wakipiga msosi wa mchana
Kocha wa Kimataifa wa mchezio wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila akisalimiana na Katibu Mkuu wa Mchezo wa Riadha nchini Suleiman Nyambu ... (RT) na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Bw.Dioniz Malinzi, 
 

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Bw. Dioniz Malinzi, akimkabizi cheti Rajabu Mhamila baada ya mafunzo ya uhandishi wa habari kulia ni mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto na
Katibu Mkuu wa Mchezo wa Riadha nchini Suleiman Nyambu ... (RT)
Rajabu Mhamila 'Super D akifuatilia kwa m,akini mafunzo ya uandishi wa habari za michezo zilizoandaliwa na chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA zilizofanyika Dar es salaam jana na kudhaminiwa na Times Radio  na Valentino Royal Hotel

ECASSA YAIKUTANISHA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII YA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI

0
0
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF Tanzania, Abubakar Rajab, akimkabidhi zawadi  Mh. Fazila Jeewa waziri wa masuala ya hifadhi ya jamii nchini Mauritius mara baada ya waziri huyo kufungua rasmi warsha juu ya uendeshaji wa bodi za mifuko ya hifadhi ya jamii iliyoandaliwa na taasisi ya hifadhi ya jamii ya Africa mashariki na kati (ECASSA)  inayoendelea huko nchini Mauritius.
Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF (kushoto), akibadilishana mawazo na baadhi ya washiriki wa warsha hiyo.
 Washiriki wa warsha ya Uendeshaji wa Bodi ya Mifuko ya Hifadhi Jamii wakibadilisha mawazo. Wa pili kushoto ni, Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Kanda ya Mashariki, Isaya Mwakifulefule.
Katibu Mkuu wa Taasisi ya Hifadhi ya Jamii ya Africa Mashariki na Kati (ECASSA) Dk. Frederic Ntimarubusa akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Masuala ya Hifadhi ya Jamii nchini Mauritius, Fazila Jeewa kufungua warsha inayoendelea nchini Mauritius.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF Tanzania, Abubakar Rajab, akitoa mada katika warsha juu ya uendeshaji wa bodi za mifuko ya hifadhi ya jamii iliyoandaliwa na Taasisi ya Hifadhi ya Jamii ya Africa Mashariki na Kati (ECASSA)  inayoendelea nchini Mauritius.

Wajumbe wa warsha juu ya uendeshaji wa bodi za mifuko yahifadhi ya jamii kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Burundi, Rwanda, Zambia,Uganda na wenyeji Mauritius wakiwa katika picha ya pamoja na Mh. Fazila Jeewa waziriwa masuala ya hifadhi ya jamii nchini Mauritius mara baada ya ufunguzi wawarsha hiyo iliyoandaliwa na taasisi ya hifadhi ya jamii ya Africa mashariki nakati (ECASSA) juu ya uendeshaji wa bodi za mifuko ya hifadhi ya jamii inayoendelea huko nchini Mauritius.

MKUTANO WA KAMATI YA WATALAAM WA FEDHA, UCHUMI NA MIPANGO WA NCHI WANACHAMA WA UMOJA WA AFRIKA (AU) NA KAMISHENI YA UCHUMI YA AFRIKA (ECA) WAANZA ADDIS ABABA – ETHIOPIA.

0
0
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Hamis H. Mwinyimvua (Kulia) na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Mh.Naimi Azizi wakiwaa kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Watalaamu wa masuala ya Fedha Afrika unaofanyika Mjini Addis Ababa – Ethiopia.
2
Baadhi ya wajumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 8 wa Watalaam wa masuala ya Fedha – Afrika wakijadili jambo wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa ‘United Conference Centre’ Addis Ababa. Kulia ni Nd.Mbayani Saruni na Kushoto ni Bi.Glory Sindilo.
3
Mh.Naimi Azizi Balozi wa Tanzania Nchini Ethiopia (Katikati) na Dkt. Hamis Mwinyimvua (kushoto) wakifurahia jambo na baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 8 wa Watalaamu wa masuala ya Fedha wa Afrika baada ya ufunguzi wa Mkutano huo.

……………………………………………………..
Na Mwandishi wetu
Tanzania inashiriki mkutano wa nane wa Wataalamu wa Fedha, Uchumi na Mipango kwa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) na Kamisheni ya Uchumi ya Afrika (ECA) umeanza nchini Ethiopia kwa kuwakutanisha wataalamu mbalimbali wa masuala ya Fedha kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Afrika.
Mkutano huo wa watalaamu ni maandalizi ya Mkutano wa Mawaziri wa Fedha, Uchumi na Mipango wa Afrika ambao utafanyika kuanzia Machi 30 hadi 31 mwaka huu Addis Ababa nchini Ethiopia.
Katika Ufunguzi wa Mkuatano huo Mh. Abraham Tekeste,Waziri wa Fedha na Uchumi wa Ethiopia alisisitiza kuwa umakini unatakiwa katika utekelezaji wa sera tulizojiwekea, vipaumbele na mikakati ya maendeleo ya kifedha kabla ya kikao cha malengo ya maendeleo endelevu kitakachofanyika Septemba ,2015.
Mkutano huo ambao pamoja na mambo mengine utajadili kanuni na utaratibu wa kamati ya watalaam wa masuala ya fedha, Uchumi na Maendeleo na maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika Afrika, utatanguliwa na uchaguzi wa Mwenyekiti wa kamati ya wataalam na kamati ya Mawaziri wa Fedha, Uchumi na Mipango wa nchi wanachama wa AU, na ECA.

UMOJA WA VYAMA VYA WALIMU WA NCHI ZA AFR/MASHARIKI WAFANYA MKUTANO WA SIKU 4 ZANZIBAR

0
0
Mratibu Msaidizi wa Utafiti na Mafunzo wa Umoja wa Vyama vya Walimu wa Nchi za Afrika Mashariki (FEATU) Bi. Lucy Njura Barimbui akiwasilisha mpango kazi wa miaka 5 ya Mtandao wa Wanawake wa Vyama vya Walimu wa Afrika Mashariki (WNEA) katika Mkutano wa siku 4 uliofanyika Hoteli ya Executive iliyopo Kilimani Mjini Zanzibar.
002
Katibu Mkuu wa chama cha walimu Zanzibar (ZATU) Mussa Omar Tafurwa akichangia kitu katika Mkutano wa mpango kazi wa miaka 5 wa Mtandao wa wanawake wa Vyama vya walimu wa Afr. Mashariki.
003
Naibu Katibu Mkuu wa chama cha walimu Zanzibar (ZATU) Salim Ali Salim akifunga Mkutano wa siku 4 wa Umoja wa vyama vya Walimu wa Nchi za Afrika Mashariki (FEATU) uliofanyika Zanzibar.
 004
Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo wakimba wimbo wa mshikamo mara baada ya kufungwa kwa Mkutano huo.005
Katibu Mkuu wa chama cha walimu Zanzibar Mussa Omar Tafurwa (wakatikati) katika picha ya pamoja ya wajumbe wa Mkutano wa Umoja wa vyama vya Walimu wa Nchi za Afrika Mashariki (FEATU).Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

RAIS KAGAME WA RWANDA AHUDHURIA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA KANDA YA KATI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimraribisha Rais Paul Kagame wa Rwanda kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Kanda ya Kati (Central Corridor Conference) ulioanza jana na kumalizika leo Machi 26, 2015.PICHA NA IKULU.3
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na wageni wake Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Pierre Nkurunzinza kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Kanda ya Kati (Central Corridor Conference) ulioanza jana na kumalizika leo Machi 26, 2015
4
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Paul Kagame wa Rwanda wakiwa kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Kanda ya Kati (Central Corridor Conference) ulioanza jana na kumalizika leo Machi 26, 2015.
6
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Paul Kagame wa Rwanda wakiteta jambo.
7
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Paul Kagame wa Rwanda katika picha ya pamoja na mawaziri wa Tanzania, kenya, DRC na Uganda kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Kanda ya Kati (Central Corridor Conference) ulioanza jana na kumalizika leo Machi 26, 2015
9
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na  Rais Paul Kagame wa Rwanda wakisiliza maelezo toka kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Rished Bade walipotembelea kituo cha kulipia ushuru wa aina zote chini ya paa moja  katika bandari ya Dar es salaam leo Machi 26, 20151011
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na  Rais Paul Kagame wa Rwanda wakiteta jambo walipotembelea  bandari ya Dar es salaam leo Machi 26, 2015
12
Rais Paul Kagame wa Rwanda akipeperusha bendera kuashiria kuzinduliwa kwa safari za treni za mizigo kuelekea Rwanda katika stesheni ya reli ya Dar es salaam akiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho kikwete leo Machi 26, 2015
1415
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na  Rais Paul Kagame wa Rwanda wakiwa katika picha ya pamoja.

CHUO CHA CBE KUANZA KUTOA SHAHADA YA ELIMU KATIKA MASUALA YA BIASHARA.

0
0
h
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) Prof. Emanuel Mjema akizungumza  wakati  wa mkutano wa wadau na wataalam wa elimu kutoka Taasisi za Elimu, vyuo, walimu wa masomo ya Biashara wa shule za Sekondari  waliokutana kupitia Mtaala wa kufundishia mafunzo ya taaluma ya Ualimu katika Biashara leo jijini Dar es salaam
p
Mkurugenzi wa Mafunzo ya awali wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Dkt. Esther Mbise akitoa ufafanuzi kwa wadau wa Elimu kuhusu uandaaji wa mtaala wa kufundishia walimu wa masomo ya Biashara leo jijini Dar es salaam.
y
Menejimenti na watendaji wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano wa wadau na wataalam wa elimu kutoka Taasisi za Elimu, vyuo, walimu wa masomo ya Biashara wa shule za Sekondari na vyuo na  wadau mbalimbali wa Elimu leo jijini Dar es salaam.
…………………………………………………………………………………………………………….
Na.  Aron Msigwa. Dar es salaam.
Chuo cha Elimu ya Biashara Kampasi ya Dar Es salaam (CBE) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu nchini kiko katika hatua za mwisho za kukamilisha Mtaala wa kufundishia Walimu wa masomo ya biashara kwa ngazi ya shahada utakaoanza kutumika katika mwaka masomo utakaoanzia mwezi Septemba 2015.

 Akizungumza wakati wa mkutano wa wadau na wataalam wa elimu kutoka Taasisi za Elimu, vyuo, walimu wa masomo ya Biashara wa shule za Sekondari na vyuo na  wadau mbalimbali wa Elimu leo jijini Dar es salaam, Mkuu wa chuo hicho Prof. Emanuel Mjema amesema chuo chake kimeamua kuanzisha programu hiyo ili kuziba pengo la uhaba wa walimu wa kufundisha masomo ya Biashara wenye taaluma ya ualimu.

Amesema chuo hicho kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kimefikia uamuzi huo kufuatia  utafiti uliofanywa na jopo la wataalamu wa maandalizi ya Mtaala huo  kuanzia mwaka 2012  uliobaini uwepo wa kiwango kikubwa cha uhitaji wa waataalam wa kufundisha masomo ya biashara wenye taaluma ya ualimu.

Prof. Mjema amesema katika utafiti huo ilibainika kuwa asilimia 27 ya walimu wanaofundisha masomo ya Biashara katika maeneo mbalimbali nchini wana taaluma ya ualimu huku asilimia 73 wanafundisha kwa kutumia uzoefu jambo linalochangia  kupungua kwa ubora wa ufundishaji darasani.

“Sisi kama chuo cha Elimu ya Biashara tumeona uhitaji uliopo nchini wa kukosa wataalam wa kufundisha masomo ya Biashara wenye taaaluma ya ualimu ndio maana tumeamua kuanzisha  mtaala huu wa kufundishia wanafunzi wa Shahada ya Elimu katika Biashara ili  tupate wahitimu bora watakaofundisha wanafunzi wetu na kukidhi mahitaji ya soko” Amesisitiza.

Amesema mafunzo yatakayotolewa yatachukua muda wa miaka 3 na kubainisha kuwa katika mahafali ya kwanza ya shahada hiyo wanafunzi wapatao 300 wanatarajia kuhitimu mafunzo hayo. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mafunzo ya awali wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Dkt. Esther Mbise akitoa ufafanuzi kuhusu uandaaji wa mtaala huo amesema timu ya wataalam wa maandalizi ya mtaala huo ilikutana na wadau mbalimbali kutoka Wizara ya Elimu,Taasisi za elimu, wanafunzi, wazazi na Taasisi za Mitaala ya Elimu ili kupata maoni yao na kupata maoni yaliyoanisha maeneo ya kufanyia marekebisho ili kuwa na mtaala bora wenye kukidhi mahitaji ya elimu ya biashara nchini.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya mtaala huo ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Masoko wa CBE akiwasilisha mtaala huo ili upitiwe na wadau wadau waliohudhuria mkutano huo amesema sababu za kuwepo kwa mabadiliko ya kuwepo kwa mtaala huo ni kuwepo kwa mahitaji ya wataalam wa kufundisha masomo ya Biashara wenye taaluma ya Ualimu.

Amesema mtaala huo utakaoanza kutumiwa mwezi Septemba, 2015 utatoa fursa ya wanafunzi wengi zaidi waliohitimu kidato cha sita na vyuo kujiunga katika masomo hayo ya miaka 3 ya Shahada ya Elimu katika biashara.

MGOMO WA WAFANYABIASHARA WATIKISA MKOANI KILIMANJARO.

0
0
Pirika pirika zilizozoeleka katika kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi hazikuonekana katika kituo hicho.
Maduka yaliyopo katika jengo la Halmashauri ya manispaa ya Moshi lenye ghorofa mbili pia hali ilikuwa hivi.
Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa baadhi ya maduka yaliyoko Double road.
Baadhi ya wafanyabiashara wakiwa nje ya maduka yao mara baada ya kuamua kuyafunga kwa kile wanaochodai kufanya mgomo kwa lengo la kumuunga mkono Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara Johnson Minja ambaye kesi yake inasikilizwa mkoani Dodoma.
Maduka yaliyoko kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi yakiwa yamefungwa mara baada ya wafanyabiashara kuamua kufanya mgomo.
Baadhi ya maduka katika jengo ala Neneu Complex yakiwa yamefungwa hakuna huduma iliyokuwa ikitolewa.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

WAZIRI MKUU, MIZENGO PINDA AKUTANA NA UONGOZI WA KAMPUNI YA CHINA MERCHANT GROUP

0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimwonyesha Mwenyekiti wa Kampuni ya China Merchants, Group, Bw. Li Xiaopeng jarida linaloonyesha fursa za uwekezaji nchi lililotolewa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania katika mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Wazri Mkuu jijini Dar es salaam Machi  2015. Kampuni hiyo Inatarajiwa kuanza ujenzi wa bandari ya Bagamoyo hivi karibuni.3
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongozana   na Mwenyekiti wa Kampuni ya China Merchant Group, Bw. Li Xiaopeng (kulia)  na balozi wa China nchini, Lu Youqing baada ya mazungumzo yake na uongozi wa kampuni hiyo  Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dare s salam Machi 26, 2015 . Kampuni hiyo inatarajiwa kuanza ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo hivi karibuni.4
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na  Mwenyekiti wa Kampuni ya China Merchants, Group, Bw. Li Xiaopeng , Ofisini kwa Wazri Mkuu jijini Dar es salaam Machi 26,  2015. Kampuni hiyo Inatarajiwa kuanza ujenzi wa bandari ya Bagamoyo hivi karibuni.
5
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akiwa katika picha ya pamoja    na Mwenyekiti wa Kampuni ya China Merchant Group, Bw. Li Xiaopeng (kulia kwake ) pamoja na ujumbe wake  na balozi wa China nchini, Lu Youqing (kushoto kwake ,baada ya mazungumzo yake na uongozi wa kampuni hiyo  Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dare s salam Machi 26, 2015 . Kampuni hiyo inatarajiwa kuanza ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo hivi karibuni.
6
Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda akizungungumza na Mwenyekiti wa Kampuni ya China Merchant Group, Bw. Li Xiaopeng (watatu kushoto ) pamoja na ujumbe wake  na balozi wa China nchini, Lu Youqing ( kushoto kwake) ,baada ya mazungumzo yake na uongozi wa kampuni hiyo  Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dare s salam Machi 26, 2015 . Kampuni hiyo inatarajiwa kuanza ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo hivi karibuni.

ASKOFU GWAJIMA ATAKIWA KUHOJIWA NA JESHI LA POLISI KUHUSU TUHUMA ZA KASHFA NA MATUSI DHIDI YA KALDINARI PENGO

0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamtaka Askofu JOSEPHAT GWAJIMA wa Kanisa la Ufufuo na Uzima afike haraka katika kituo cha Polisi cha Kati ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa mahojiano kuhusu tuhuma za kashfa na matusi.

"Tumepokea malalamiko ya kukashifiwa na kutukanwa hadharani Mwadhama Kaldinari Polycarp Pengo ambaye ni kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania. Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kama vile WhatsApp na mingineyo kuna sauti iliyorekodiwa (audio) na picha za video (Video Clip) zikimuonyesha Askofu Gwajima akimkashfu na kumtukana kwa maneno makali Kaldinari Pengo katika hali ambayo pia imewaudhi watu wengine".

Baada ya tukio hilo juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanyika katika hali ya kawaida ili kumpata Askofu Gwajima bila mafanikio na hivyo yeye mwenyewe sasa anatakiwa aende akaripoti haraka kwa Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam bila kukosa.

Ni muhimu sana kwa Askofu Josephat Gwajima kuripoti yeye mwenyewe badala ya Kutafutwa au kukamatwa ili ajibu tuhuma hizo kutokana na nafasi yake katika jamii.

Jalada la uchunguzi limefunguliwa na upelelezi wa shauri hili unaendelea ili sheria ichukue mkondo wake.

Imetolewa na: 
S. H. KOVA,
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM 

PSPF WAFANYA KIKAO KAZI NA WATUMISHI WA MANISPAA, DAR NA PWANI

0
0
Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Adam Mayingu, akitoa hotuba ya utangulizi wakati wa kikao kazi cha siku moja ya maafisa na wakuu wa idara za Halmashauri za miji na Manispaa za mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, iliyofanyika makao makuu ya PSPF jijini Dar es Salaam, Alhamisi Machi 26, 2015.

Profesa Hermans Mwansoko, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni, na Michezo, akitoa hotuba ya ufunguzi wa kikao kazi cha siku moja kwa maafisa na wakuu wa idara za Halmashauri na Manispaa za Dar es Salaam na Pwani, kilichoandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, na kufanyika makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam, Alhamisi Machi 26, 2015

Meneja Masoko na Mawasiliano, wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Contatina Martin, akizungumza kwenye kikao hicho

Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Adam Mayingu, akitoa hotuba ya utangulizi wakati wa kikao kazi cha siku moja ya maafisa na wakuu wa idara za Halmashauri za miji na Manispaa za mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, iliyofanyika makao makuu ya PSPF jijini Dar es Salaam, Alhamisi Machi 26, 2015.

Gabriel Silayo, Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Gabriel Silayo, akitoa mada kuhusu uwekezaji wa Mfuko huo, wakati wa kikao kazi hicho


Meneja wa Actuarial Service and Risk Mnagement wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Ibrahim Maftaha, akitoa mada kwenye kikao hicho

Mkurugenzi wa Tehama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Andrew Mkangaa, (katikati), akiongoza kipindi cha maswali na majibu wakati wa kiikao kazi cha siku moja kilichoandaliwa na Mfuko huo kwa maafisa na wakuu wa idara za halmashauri za miji na manispaa za Dar es Salaam na Pwani, na kufanyika makao makuu ya PSPF jijini Dar es Salaam Alhamisi Machi 26, 2015. Kulia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji, Neema Muro na kushoto ni Mkurugenzi wa Uwekezaji, Gabriel Silayo

Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha siku moja cha maafisa na wakuu wa idara za halmashauri za miji na Manispaa za Dar es Salaam na Pwani, wakisoma vipeperushi vyenye maelezo ya huduma mbalimbali za Mfuko wa Pensheni wa PSPF, wakati wa warsha hiyo iliyoandaliwa na Mfuko huo na kufanyika makao makuu ya PSPF jijini Dar es Salaam Alhamisi Machi 26, 2015

Viewing all 46194 articles
Browse latest View live




Latest Images