Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 492 | 493 | (Page 494) | 495 | 496 | .... | 1897 | newer

  0 0
 • 03/24/15--03:38: KIBONZO CHA NATHAN MPANGALA


 • 0 0

   Mwenyekiti wa kamati ya maafa ya watu waliopatwa na janga la  mvua ya mawe  katika  kata ya Mwakata  ambae ni mkuu wa wilaya ya Kahama,  Benson Mpesya  wa katikati akipokea msaada wa vifaa vya ujenzi  mabati 176  na mifuko ya saruji 130  vilivyotolewa na kampuni ya bia  ya TBL  kulia anayekabidhi ni  meneja mauzo na usabazaji Godwin Zakaria na kushoto ni mjumbe wa kamati Patrick Kalangwa ambae ni mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala lengo la msaada huo ni kuunga mkono ahadi ya Rais Jakaya Kikwete ya kuwajengea nyumba wahanga hao.
   Mwenyekiti wa kamati ya maafa ya watu waliopatwa na janga la  mvua ya mawe  katika  kata ya Mwakata  ambae ni mkuu wa wilaya ya Kahama,  Benson Mpesya  wa katikati akipokea msaada wa vifaa vya ujenzi  mabati 176  na mifuko ya saruji 130  vilivyotolewa na kampuni ya bia  ya TBL  kulia anayekabidhi ni  meneja mauzo na usabazaji Godwin Zakaria na kushoto ni mjumbe wa kamati Patrick Kalangwa ambae ni mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala lengo la msaada huo ni kuunga mkono ahadi ya Rais Jakaya Kikwete ya kuwajengea nyumba wahanga hao.

   Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya  kushoto  ambae ni mwenyekiti wa maafa wa janga la mvua ya mawe lililowapata wananchi wa kata ya Mwakata wilayani Kahama  akipokea msaada wa vifaa vya ujenzi  mabati 176  na mifuko ya saruji  130  toka kampuni ya bia ya TBL , anayekabidhi kulia ni Meneja idara ya mauzo na usambazaji Godwin Zakaria na katikati ni Juma Akida ambae ni meneja mauzo kanda ya ziwa .
  Wananchi wa kijiji cha Mwakata wilayani Kahama wakishusha msaada wa mabati yaliyotolewa na kampuni ya bia tanzania TBL kwa lengo la kuunga mkono ahadi ya Rais Jakaya Kikwete  ya kuwajengea nyumba wahanga wa kata hiyo walioathiriwa na mvua ya mawe ambako  kampuni hiyo imetoa mabati 176 na mifuko ya saruji 130 .

  0 0

  Mjumbe wa Baraza la Wazazi, Taifa na Mbunge wa Korogwe, Steven Ngonyani 'Prof .Maji Marefu' akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma hii leo juu ya tuhuma za yeye kutajwa na mmoja wa wajumbe wa baraza hilo kuwa aliratibu na kulazimisha baadhi ya wajumbe wa baraza hilo kwenda kumuona Mbunge wa Munduli na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa. 

  Naye Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani, alisema yeye alielezwa kuhusiana na safari hiyo na rafiki yake Vioroka Kajoko.

  “Nimekuwa katika jumuiya hii kwa miaka 15. Siko tayari kuchaguliwa kiongozi, marafiki wala maadui. Mimi siko tayari  uomba radhi kwasababu sina kosa nililotenda,”alisema Ngonyani. 

  Alisema hajawahi kumshawishi mtu wala kumlazimisha mtu kumpenda mtu anayempenda yeye.
   Jackline Ngonyani aliyejitambulisha kwa Lowassa kama 'Maji mafupi' na kutoa salam za shukrai kwa wana Ruvuma kwa jinsi Lowassa alivyo shiriki katika mazishi ya Capt.John Komba lakini jana aliwaambia waandishi wa habari kuwa alilazimishwa kushiriki katika msafara huo. Lakini wenzake wanasema yeye alikuwa mmoja wa waratibu.
  Mjumbe wa Baraza Kuu la Wazazi mkoa wa Njombe, Evarist Lupenza,  akizungumza na waandishi wa habari juu ya safari yao kwenda kwa Lowassa. Pamoja nae ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wzazi mkoa wa Mwanza, Malila Lugoye.   Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Dodoma, Dk. Damas Mukassa, akiwaonesha waandishi wa habari picha ambayo mjumbe mwenzao alisema wamelazimishwa kwenda kwa Lowassa jinsi alivyo kula pozi na Lowassa.

  *********************
  VIONGOZI waliotajwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Taifa, Abdallah Bulembo, kuratibu safari ya baadhji ya wajumbe wa jumuia hiyo na baraza la Wazazi Taifa kwenda kumsalimia Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Edward Lowassa leo wamekanusha vikali kuhusika na uratibu wa baraza hilo.

  Jana Bulembo aliwashukia wajumbe waliokwenda nyumbani kwa Waziri Mkuu wa Zamani, Edward lowassa,na kumchakingia fedha na kumshawishi  agombee Urais na kuwataka waombe radhi kutumia jina la baraza hilo na kisha kusubiri  kamati ya maadili.

  Wakizungumza hii leo baadhi ya wajumbe hao wamewataja waratibu walioongoza msafara wao kuwa ni pamoja na Katibu wa CCM Wilaya ya Hanang, Vioroka Kajoro na Mjumbe wa baraza hilo kutoka mkoani Ruvuma, Jackline Ngonyani na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Dodoma, Dk. Damas Mukassa.

  Mjumbe wa jumuiya hiyo kutoka Mkoa wa Njombe, Evarist Lupenza, alisema aliyekuwa akiandika majina ya wajumbe waliokwenda katika ziara hiyo ni Jackline Ngonyani. 

  “Niliwasikia wakisema kwa Mzee ni saa tatu, nikawauliza mnataka kwenda wapi, wakaniambia kuwa wanataka kwenda kumsalimia Lowassa, name nikaandikisha jina kwa ajili ya kwenda huko,”alisema Lupenza.

  Nae Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Mwanza, Malila Lugoye alibainisha kuwa hakuna mtu aliyeshinikizwa katika safari hiyo na ilikuwa ni huru kuamua kwenda au kubaki.

   “Hakuna mtu aliyeshinikizwa kwenda kwa Lowassa kila mtu alikwenda kwa mapenzi yake. Na hakuna mtu aliyetumia jina la Jumuiya wakati tulipokwenda bali watu walijitambulisha mmoja mmoja,”alisema na kuungwa mkono na Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Mkoa wa Mwanza, Malila Lugoye.

  Naye Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani, alisema yeye alielezwa kuhusiana na safari hiyo na rafiki yake Vioroka Kajoko.

  “Nimekuwa katika jumuiya hii kwa miaka 15. Siko tayari kuchaguliwa kiongozi, marafiki wala maadui. Mimi siko tayari  uomba radhi kwasababu sina kosa nililotenda,”alisema Ngonyani.
  Alisema hajawahi kumshawishi mtu wala kumlazimisha mtu kumpenda mtu anayempenda yeye. 

   Dk Mukassa alisema yeye aliratibu ziara hiyo kama mwenyeji wa mkoa wa  Dodoma ambaye anakufahamu nyumbani kwa Lowassa.

   Alisema fedha walizotoa kwa ajili ya kumchangia kuchukua fomu za Sh 600,000 zimetokana na mchango wao wenyewe kama wanachama wa kikundi cha kusaidia cha wajumbe wa jumuiya hiyo.

  “Fedha zile hazikutoka kwenye jumuiya ya chama wala hakuna aliyekwenda pale kuwakilisha jumuiya na niliwaeleza pale mliponiuliza na kila mtu alijitambulisha kama yeye,”alisema.

  0 0

  Balozi wa China nchini Tanzania Mheshimiwa Dr.Lu Youqing (kushoto) akizungumza na Naibu waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mhe. Stephen Masele walipokutana kwenye ukumbi wa ubalozi huo kuzungumzia mkutano wa kimataifa wa viongozi vijana wa Afrika na China unatorajiwa kufanyika kuanzia Machi 27 na kumalizika Machi 31 katika Ukumbi wa Hoteli ya Ngurdoto, mkoani Arusha.002
  Balozi wa China hapa nchini Mheshimiwa Dr.Lu Youqing akipeana mkono na Naibu waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mhe. Stephen Masele mara baada ya kikao chao kufikia tamati ambapo walijadili hatua walizozifikia katika kuandaa mkutano huo wa kimataifa wa viongozi vijana wa Afrika na China unatorajiwa kufanyika kuanzia Machi 27 na kumalizika Machi 31 katika Ukumbi wa Hoteli ya Ngurdoto, mkoani Arusha.003
  Balozi wa China hapa nchini Mheshimiwa Dr.Lu Youqing akijibu swali aliloulizwa na mwandishi wa habari (Hayupo pichani) wakati wa kujadili mustakabali wa uandaaji wa mkutano wa kimataifa wa viongozi vijana wa Afrika na China unatorajiwa kufanyika kuanzia Machi 27 na kumalizika Machi 31 katika Ukumbi wa Hoteli ya Ngurdoto, mkoani Arusha. (Kushoto) ni Naibu waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mhe. Stephen Masele ambaye ni mwenyekiti wa maandalizi ya mkutano huo.

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua kazi ya kuondoa maji ya mafuriko kutoka katika nyumba za watu katika eneo la Buruguruni Mnyamani wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam leo wakati Rais na Mkewe Mama Salma Kikwete na viongozi mbalimbali walipotembelea eneo hili kujionea athari za mafuriko na kuwafariji wananchi.3
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mmoja wa wakazi wa Buguruni Mnyamani Bi.Halima Hamza ambaye nyumba yake imeathiriwa vibaya na maji ya mafuriko wakati Rais na Mkewe Mama Salma Kikwete na viongozi mbalimbali walipotembelea eneo hili kujionea athari za mafuriko na kuwafariji wananchi.4
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimsalimia mtoto Irene ambaye nyumba yao imeathiriwa na mafuriko huko Buguruni Mnyamani leo.56
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mack Sadik akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mfereji ulioziba kutokana na uchafu na kusababisha mafuriko katika makazi ya watu eneo la Buguruni Mnyamani jijini Dar es Salaam leo.

  78
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wakazi wa Buguruni Mnyamani waloathiriwa na mafuriko kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.Rais Kikwete ameahidi kuwasaidia wananchi hao910
  Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipita katika mitaa mbalimbali ya Buguruni leo wakati wa zoezi la kuwafariji waathirika wa mafuriko huko Buguruni Mnyamani leo.
  (picha na Freddy Maro)

  0 0

  Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma Jaji Mstaafu Dkt. Steven James Bwana akiukaribisha ujumbe wa Serikali ya Zimbabwe katika Ofisi ya Tume ya Utumishi wa Umma Tanzania ilipofanya ziara ya Mafunzo nchini Tanzania jana.2
  Katibu Msaidizi wa Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Richard Odongo akiwasilisha mada wakati wa Ziara ya Mafunzo ya Tume ya Utumishi wa Umma ya Zimbabwe ilipoitembelea ofisi ya Tume ya Utumishi wa Umma nchini jana.3
  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi akiukaribisha Ujumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma ya Zimbabwe ulipoitembelea ofisi hiyo jana.4
  Baadhi ya Maofisa wa Ofisi ya Rais-Utumishi na Ujumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma ya Zimbabwe wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa ulipoitembelea ofisi ya Rais-Utumishi.5
  Afisa Tawala Mkuu wa Ofisi ya Rais-Utumishi (wa pili kushoto) Bw. Francis Sangunaa akiwasilisha mada wakati ujumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma ya Zimbabwe ulipoitembelea ofisi hiyo jana.6
  Mkuu wa Mahusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Huduma za Hifadhi ya Jamii nchini Tanzania (SSRA) Bi. Sarah Kibonde akiwasilisha mada wakati ujumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma ya Zimbabwe ulipoitembelea ofisi hiyo jana.7
  Makamu Mwenyekiti wa Tume Ya Utumishi wa Umma ya Zimbabwe Dkt. M. Muchada akipokea zawadi toka kwa Mkuu wa Mahusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Huduma za Hifadhi ya Jamii nchini Tanzania (SSRA) Bi. Sarah Kibonde mara baada ya baada ya kumaliza ziara ya mafunzo katika ofisi hiyo jana jioni.

  0 0

  Nashukuru wote ambao mmekuwa mkifuatilia hatma ya muswada binafsi wa Baraza la Vijana la Taifa niliouwasilisha tarehe 31 Oktoba 2013.
  Vijana na wadau wa maendeleo ya vijana mzingatie kwamba muswada huo hatimaye umepangwa kusomwa kwa mara ya pili na kujadiliwa Bungeni Jumanne tarehe 31 Machi 2015 katika Mkutano wa 19 wa Bunge.

  Muswada huo ulisomwa kwa mara ya kwanza katika Mkutano wa 14 wa Bunge tarehe 21 Disemba 2013. Maoni kutoka kwa wadau yalikusanywa Oktoba 2014 na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii.

  Baraza la Vijana la Taifa pamoja na malengo mengine litawezesha vijana kuanzia kwenye vijiji/mitaa mpaka taifa kuweza kuwa na vyombo vya kuwaunganisha vijana kwa kike na wa kiume kwa ajili ya maendeleo yao na ya taifa.

  Aidha, Baraza hilo litafuatilia pia kwa karibu utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya vijana ikiwemo kuhusu ajira, elimu na sekta zingine katika Halmashauri, Serikali kuu, katika vyombo mbalimbali vya maendeleo na wadau wa maendeleo.

  Pia, Muswada huo utawezeshwa kuanzishwa kwa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na kulipa jukumu Baraza la Vijana kufuatilia kwa karibu utendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana; kuhakikisha kwamba fedha zinatengwa za kutosha na kufika kwa walengwa kuwawezesha vijana kujiajiri, kukuza vipaji vyao na kushughulikia maendeleo yao kwa ujumla.

  Kujadiliwa kwa muswada huo ni hatua ya pekee katika historia ya harakati za vijana nchini kwa kuzingatia kuwa Sera ya zamani ya maendeleo ya vijana ya mwaka 1996 ilitamka kwamba kutaanzishwa  Baraza la Vijana na suala hilo kurudiwa katika Sera mpya ya mwaka 2007.

  Hata hivyo Serikali imekuwa ikikwepa kuhakikisha kwamba matakwa hayo ya sera tajwa yanatekelezwa kwa wakati pamoja na kuwa suala hilo linahusu mustakabali wa maendeleo ya vijana nchini.


  Natambua mchango wa vijana na taasisi zote za vijana mlioshiriki katika maandalizi ya muswada huu, unaitwa binafsi kwa sababu tu ndio neno linalopaswa kutumika kwa mujibu wa Kanuni za Bunge lakini ukweli ni kwamba huu ni muswada wenu; mimi ni mwakilishi.


  John Mnyika (Mb)


  20 Machi 2015.


  0 0

  Wapiga picha katika eneo la Kilima cha Mawenzi wakioneshana uwezo wa kupigana masumbwi hata hivyo chanzo cha ugomvi huo hakikuweza kufahamika mara moja.

  Video na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0


  0 0

  Wakazi wa  Kwa Mangi kata ya Kibosho Kati  wakimsikiliza   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akiwahutubia,Kinana aliwaeleza wananchi hao kuwa kuna baadhi ya watu wamekuwa wakijipitisha pitisha kuomba uongozi,hivyo amewaonya na kuwatahadharisha kutojipitisha pitisha kugombea nafasi za uongozi kabla ya muda kuisha na kutangazwa.
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa  Kwa Mangi kata ya Kibosho Kati ambapo aliwaambia wananchi waache kujipitisha pitisha kugombea nafasi za uongozi kabla ya muda kuisha na kutangazwa.
   Zaidi ya wanachama 335 wamejiunga na CCM kwenye mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na mwanafunzi Elia PeterUlomi wa shule ya sekondari ya Somsom.
  Jengo la chuo cha KVTC kama lionekavyo kwa nje,ambapo  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alitembelea 
   Shamba la Mpunga lililopo Mabogini.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wanafunzi alipotembelea chuo cha KVTC-Kibosho Moshi vijijini.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupanda mti wa kumbukumbu kwenye chuo cha Ufundi KVTC,Kibosho wilaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro.
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki uvunaji wa mpunga kwenye skimu ya umwagiliaji ya Lower Moshi.
    Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini Ndugu Cyril Chami akihutubia wananchi wa kijiji cha Chekereni kata ya Mabogeni. Kata ya Mabogeni ina vijiji 8 na vyote vimeshinda kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa. Jimbo la Moshi Vijijini lina Kata 16 ,shule za sekondari zilizojengwa ni 29.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Chekereni kata ya Mabogini. 

  0 0


   

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

  TAARIFA KWA UMMA KUHUSU AJIRA YA WALIMU WAPYA WA SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI NA VYUO VYA UALIMU MWAKA 2015/16

  JIHADHARI NA MATAPELI

  Kumekuwepo na Tangazo la upotoshaji kuhusu Ajira ya walimu wapya kwa mwaka 2015/16 (TANGAZO No. T.022/15TMS 2015) linalodaiwa kuwa limetolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na kusambazwa kwenye Mitandao ya Kijamii. Taarifa zilizotolewa katika tangazo hilo siyo za kweli na Wizara haihusiki nazo.

  Aidha, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inapenda kuufahamisha umma kuwa ajira ya Walimu wa ngazi ya Cheti, Stashahada, na Shahada hufanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI baada ya kupata kibali cha Ajira kutoka Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Hivyo Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi haihusiki moja kwa moja na zoezi hilo.

  Kutokana na mgawanyo wa majukumu ya Wizara mbalimbali, taarifa sahihi kuhusu ajira mpya za walimu kwa mwaka huu wa fedha zitatangazwa na Mamlaka inayohusika yaani Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI mara watakapokamilisha taratibu zinazotakiwa.

  Imetolewa na:
  Katibu Mkuu,
  WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
  24 Machi, 2015

  0 0

  DSC_0370

  Mtendaji Mkuu wa MO DEWJI FOUNDATION, Gerald Mgesi David akimkabidhi rasmi kijana Paulo Ezekiel (23) msaada wa baiskeli ya magurudumu matatu (tricycle) itakayomsaidia katika kutembelea kwenye shughuli zake za kila siku.

  Na Andrew Chale wa Modewji blog
  Taasisi ya MO DEWJI FOUNDATION inayojishughulisha na miradi ya kusaidia jamii Tanzania katika masuala mbalimbali ikiwemo Afya, elimu na maji mwishoni mwa wiki imeweza kumpatia kijana Paulo Ezekiel (23) msaada wa baiskeli ya magurudumu matatu (tricycle) itakayomsaidia katika kutembelea kwenye shughuli zake za kila siku.

  Tukio hilo la makabidhiano limefanyika katika ofisi za Mo Dewji Foundation jijini Dar es Salaam ambapo Mtendaji Mkuu wa MO DEWJI FOUNDATION, Gerald Mgesi David alikabidhi msaada huo kwa kijana Paulo Ezekieli

  Akizungumza na Modewjiblog, Mtendaji mkuu wa Mo Dewji Foundation amesema, waliguswa na usumbufu aliokuwa anaupata kijana na hivyo kuona ni vyema kumsaidia ili aweze kumudu kuendesha shughuli zake za kila siku. Mo Dewji Foundation imejikita katika kutekeleza miradi ya kijamii ambayo inalenga kusaidia jamii ya kitanzania katika kujikwamua katika hali ya umaskini na kuinua kipato.
  DSC_0399
  Kijana Paulo Ezekiel (kulia) akiwa kwenye mahojiano na mwandishi wa habari wa modewjiblog, Andrew Chale.

  Kijana Paulo Ezekiel:
  Kwa upande wake, kijana Paulo Ezekiel ambaye muda mfupi baada ya kukabidhiwa baiskeli hiyo, alifanya mahojiano maalum na mtandao huu ambapo alieza kuwa, tatizohilo la kulemaa mguu, lilimtokea ghafla wakati yupo mitaa ya Kariakoo kwenye shughuli zake binafsi.

  “Nakumbuka nilikuwa kwenye matembezi maeneo ya Kariakoo, ghafla nilipata kuhisi hali ya kupooza mguu mmoja wa kulia na kupoteza nguvu wasamaria wema waliniokota na kunipeleka Muhimbili” anaeleza Paulo Ezekiel.


  Alieleza kuwa, alikaa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa muda wa miezi sita huku akipatiwa matibabu na baadae aliruhusiwa. “Niliporuhusiwa hali ilikuwa ngumu sana. Kwani nilianza kuomba omba kwa watu msaada ikiwemo kifaa cha kuniwezesha kunisaidia kutembelea. Kule Muhimbili nilikuwa natumia baiskeli kutembelea hivyo nilivyoruhusiwa iliniwia vigumu sana kutumia vifaa vya ulemavu ikiwemo haya magongo.
  Kuna siku katika kuomba omba. Nilikutana na mtu mmoja ambaye alinielekeza kwa Mh. Dewji. Nilipofika kwake msaidizi wake alinitaka nifuatilia kuona kama watafanikisha kwani tayari bajeti ilikuwa imeshafungwa hadi kipindi kingine” alieleza Paulo Ezekiel.
  DSC_0373
  Hata hivyo Paulo Ezekiel alibainisha kuwa, wakati yupo nyumbani kwao, alipigiwa simu juu ya kuitwa kukabidhiwa baiskeli hiyo.
  “Sikuamini kama ningeweza kupata msaada huu. Hadi nilipofika hapa kukabidhiwa namshukuru Mungu pia namuombea kwa Mungu Mh. Mohammed Dewji kwa msaada wake, kwani simjui na wala hanijui..Ilikuwa ni kama bahati kufika katika ofisi yake na kuomba msaada huu asante sana na namuombea maisha marefu Dewji na familia yake, wafanyakazi wake wote popote pale kwani kuniwezesha mimi ni ubinadamu mkubwa sana” alimalizia kijana Paulo Ezekiel.

  Paulo Ezekiel anabainisha kuwa, ilikua vigumu sana kwa yeye kutembelea magongo siku za mwanzoni ambapo anasema hakuwahi kutegemea kama siku moja atakuja kuwa mlemavu.
  “Hujafa, hujaumbika naamini hilo, kwani awali nilikuwa najitafutia riziki zangu za kujikimu kimaisha lakini nilipopata tatizo hili la kupooza mguu na kulemaa ndoto zangu zote zimeyeyuka ila sijakata tama” Hivi ndivyo anavyomalizia Paulo Ezekiel ambaye anaishi Mbagala, Temeke Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
  DSC_0397
  Mwandishi wa habari wa modewjiblog, Andrew Chale (kushoto) akifanya mahojiano na Paulo Ezekiel mara baada ya kukabidhi msaada wa baiskeli ya magudumu matatu.

  Kijana huyu awali alikua akifanya shughuli za kutafsiri Lugha kwa wageni wanaokuja kununua bidhaa kwenye maduka ya Kariakoo na Bandari ya Dar es Salaam hasa wafanyabiashara wanaotoka Congo, Rwanda, Zambia, Malawi, Burundi na maeneo mbalimbali. Paulo Ezekiel ni mtoto wa pili kati ya watoto nne, anatokea Mkoa wa Kilimanjaro na kabila lake ni Mchaga.
  DSC_0317-1024x682
  MO DEWJI FOUNDATION: Ni taasisi iliyoanzishwa na Mbunge wa Singida Mjini (CCM) na mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji maarufu ‘MO’ (pichani) ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya kiongozi bora aliyejitolea kwa kiasi kikubwa katika jamii na kuleta mabadiliko Afrika kwa mwaka 2014.

  Tuzo hiyo aliyotunukiwa MO iitwayo African Philanthropist of the year Award 2014, Ilitolewa na jarida la uongozi la Uingereza, jijini Dubai wakati wa Jukwaa la Viongozi wa Afrika.
  Kabla ya kukabidhiwa tuzo hiyo, sifa kuu aliyokuwa nayo MO kama alivyofafanua wakati wa kukabidhiwa tuzo hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa jarida hilo, Dk Ken Giami alisema wataalamu waelekezi walimchagua Dewji kuwa mshindi kutokana na: Uongozi bora katika Kampuni yake ya Mohammed Enterprises (MeTL GROUP) Pia kigezo kingine kilichompa ushindi ni namna anavyojihusisha na kazi mbalimbali za kijamii.

  Pia Mchango wa MO katika elimu ni sehemu kubwa ya mafanikio yake hususan kwa kuendeleza ujenzi wa shule mbili hadi 12, pamoja na kujitolea kiasi cha zaidi ya Sh520 milioni katika kuendeleza sekta hiyo ya elimu ndani ya jimbo lake hilo la Ubunge la Singida Mjini.
  MO pia amekuwa akisaidia sekta ya afya kwa ushirikiano na Taasisi ya Bilal Muslim Mission ya Tanzania kwa kuwaleta madaktari waliowafanyia upasuaji wagonjwa wa macho na 179 kupata miwani, kusambaza maji safi na salama kwa kuchimba visima vingi vya maji ndani ya jimbo na n.k.

  Kwa sasa MO ndie Bilionea kijana Afrika kwa mujibu wa jarida la Forbes. Unaweza kusoma zaidi kupitia http://www.forbes.com/profile/mohammed-dewji/
  Kwa hali hiyo pia Dewji ameingia katika orodha ya Philanthropist duniani pia waweza kuona watu wengine waliotunukiwa tuzo kama hiyo kupitia hapa: http://en.wikipedia.org/wiki/List_of_philanthropists
  Msomaji wetu unaendelea kuperuzi mtandao wako wa Modewji blog, tutakuletea makala maalum juu ya tatizo hili la kupooza ghafla kwa viungo hadi kusababishia kilema. Endelea kuwa nasi. Asante pia waweza kutuma maoni yako kupitia hapo chini ndani ya mtandao huu ama kupitia simu 0719076376 au 0689858799 au email info@modewjiblog.com

  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii, Said Mtanda (kushoto) akitoa mwongozo wa uchangiaji wakati wa Semina iliyowakutanisha Wadau wa Maendeleo ya Vijana, Kamati ya Maendeleo ya Jamii na Wizara husika, kujadili Muswada wa Sheria ya Baraza la Vijana Tanzania wa mwaka 2015, utakaowasilishwa Bungeni Ijumaa ya tarehe 27/03/2015. Kulia ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara. Semina hii imefanyika tarehe 23-24/03/2015 katika ukumbi wa Pius Msekwa, Mjini Dodoma.
  MT2
  Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii, Said Mtanda (katikati) akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa Semina iliyowakutanisha Wadau wa Maendeleo ya Vijana, Kamati ya Maendeleo ya Jamii na Wizara husika, kujadili Muswada wa Sheria ya Baraza la Vijana Tanzania wa mwaka 2015, utakaowasilishwa Bungeni Ijumaa ya tarehe 27/03/2015. Wengine ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara (kulia) na Katibu wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii, Hanifa Masaninga (kushoto). Semina hii imefanyika tarehe 23-24/03/2015 katika ukumbi wa Pius Msekwa, Mjini Dodoma.
  MT3Muwakilishi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma, Mgaya Ezekiel akichangia wakati wa Semina ya kujadili Muswada wa Sheria ya Baraza la Vijana Tanzania wa mwaka 2015, utakaowasilishwa Bungeni Ijumaa ya tarehe 27/03/2015. Semina hii iliyofanyika tarehe 23-24/03/2015 katika ukumbi wa Pius Msekwa, Mjini Dodoma imewakutanisha Wadau, Kamati ya Maendeleo ya Jamii na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
  MT4Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara(kulia) akifurahia jambo wakati wa Semina iliyowakutanisha Wadau wa Maendeleo ya Vijana, Kamati ya Maendeleo ya Jamii na Wizara husika, kujadili Muswada wa Sheria ya Baraza la Vijana Tanzania wa mwaka 2015, utakaowasilishwa Bungeni Ijumaa ya tarehe 27/03/2015. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii, Said Mtanda. Semina hii imefanyika tarehe 23-24/03/2015 katika ukumbi wa Pius Msekwa, Mjini Dodoma.
  MT5Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara(kulia) akifurahia jambo wakati wa Semina iliyowakutanisha Wadau wa Maendeleo ya Vijana, Kamati ya Maendeleo ya Jamii na Wizara husika, kujadili Muswada wa Sheria ya Baraza la Vijana Tanzania wa mwaka 2015, utakaowasilishwa Bungeni Ijumaa ya tarehe 27/03/2015. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii, Said Mtanda. Semina hii imefanyika tarehe 23-24/03/2015 katika ukumbi wa Pius Msekwa, Mjini Dodoma.MU
  Muwakilishi kutoka YUNA (Youth of United Nations Association), Saidi King’eng’ena akitoa maoni wakati wa Semina ya kujadili Muswada wa Sheria ya Baraza la Vijana Tanzania wa mwaka 2015, utakaowasilishwa Bungeni Ijumaa ya tarehe 27/03/2015. Semina hii iliyofanyika tarehe 23-24/03/2015 katika ukumbi wa Pius Msekwa, Mjini Dodoma imewakutanisha Wadau, Kamati ya Maendeleo ya Jamii na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

  0 0   Na Woinde Shizza,Arusha

  Bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma wanatarajiwa kuwasha moto  ndani ya ukumbi mpya wa kisasa  ujulikanao kwa jina la Flomena uliopo  wilayani hai mkoani Kilimanjaro usiku wa jumatatu ya pasaka .

  Akizungumza na waandishi wa habari muandaaji wa onyesho hilo  Swaum kileo alisema kuwa ameamua kuwaleta bendi hiyo katika uzinduzi huo ili kuweza kuwafurahisha wananchi wa mkoa wa kilimanjaro na mikoa jirani katika sikukuu hiii ya pasaka .  Alisema kuwa  bendi hii inamda mrefu sana aijafika wilayani hai ivyo wameamu kuileta ili wakazi wa wilaya hiyo nao wafurahie mziki wa dance unaofanywa na bendi hiyo . Alitaja kiingilio cha onyesho hiyo kuwa ni shilingi 10000 za kitanzania huku akiwataja wathamini wa onyesho hilo kuwa ni Swaum fashion ,Tbl , libeneke la kaskazini blog pamoja , faraja saloon  pamoja na Radio five.  Kwa upande wa meneja wa bendi ya FM Academia kelvin  mkinga aliema kuwa wamejipanga vyema kuwapa burudani ya kutosha wakazi wa wilaya ya hai mkoa mzima wa Kilimanjaro pamoja na mikoa jirani  na kwa upendeleo watawatambulisha nyimbo zao mbalimbali mpya ambazo wameziandaa na wanatarajia kuzi zindua hivi karibuni.  Alisema kuwa pia wapenzi wake watakuwa na bahati zaidi kwani   show hii ndio itakuwa ya kwanza mara baada ya kutoka katika  shindano lao na bendi ya twanga pepeta kwa upande wa Rais wa bendi hiyo Nyoshi El-Sadat   alisema kuwa timu  yake yote imejipanga vyema kuwapa burudani ya nguvu wakazi wa wilaya ya hai na mkoa mzima huku akisema  kuwa atawapa staili zote za gwasuma ikiwemo ile ya   vundesa  ambapo alisema kuwa wameiboresha na imekuwa ya kiufasaha  zaidi  na ina vinjonjo vingi zaidi ,staili tamu  pamoja na maneno matamu.  “tunatarajia kufanya show  ya kihistoria ambayo aijawai kufanyika  mkoani Kilimanjaro nah iii yote ni kwa ajili ya kuwaburudisha wapenzi wetu wa mziki wa dance wapenzi wetu wa bendi yetu ya fm academia”alisema nyoshi  Aidha alisema kuwa amewaandalia zawadi kubwa wapenzi wake wa mkoa wa huo  pamoja na mikoa jirani kwani watamuoana akiwa na muonekano mpya ambao hawajawai kuuona.

   ni pamoja na kuwaelewesha wapenzi wao nyimbo mpya na kuakikisha wapenzi wao wanajua staili zao zote za  nyimbo hizo na  sio ivyo tu pia alisema kuwa kwa kipindi  hiki wanataka kuwa wakazi wa arusha zawadi ya kuwaletea wasanii wote wa bendi hiyo ambapo alisema wapo 32  na wote watafika jijini Arusha
  chanzo :libeneke la kaskazini blog  0 0

  Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Nsao Shalua (kushoto), akikabidhi bendera ya taifa kwa mshindi wa Airtel Trace Music Stars, Mayunga Nalimi kwa ajili ya kwenda kuiwakilisha nchi katika fainali za Afrika za Airtel Trace Music Stars zitakazofanyika Jumamosi Machi 28, nchini Kenya na kushirikisha nchi 13, katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ofisi za BASATA jijini Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia (katikati), ni Meneja Masoko wa Airtel, Anet Muga.
  Meneja Masoko wa Airtel, Anet Muga. akiongea wakati wa tukio la kumuaga na kumkabithi bendera ya taifa kwa ajili ya kwenda kuiwakilisha nchi katika fainali za Afrika za Airtel Trace Music Stars zitakazofanyika Jumamosi Machi 28, nchini Kenya na kushirikisha nchi 13, katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ofisi za BASATA jijini Dar es Salaam jana. pichani katikati ni Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Nsao Shalua akifatiwa na mshindi wa Airtel Trace Music Stars, Mayunga Nalimi.
  mshindi wa Airtel Trace Music Stars, Mayunga Nalimi akiwa ameshika bendera mara baada ya kukabithiwa na Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), kwaajili ya kuiwakilisha nchi katika mashindano ya muziki ya Airtel Trace Music Stars yatakayofanyika Jumamosi hii nchini Kenya.

  Barasa la Sanaa Tanzania leo limemkabithi bendera mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars Bwana Nalimi Mayunga anayeondoka leo nchi kwenda kuhudhuria mashindano ya Airtel Trace Afrika yatakayoshirikisha washiriki toka nchi 13 barani Afrika yanayofanyika nchini Kenya siku ya Jumamosi tarehe 28 March 2015.

  Mayunga aliibuka mshindi katika kinyanganyiro cha kusaka Wakali wa vipaji vya mziki kupitia shindano la Airtel Trace Music lililozinduliwa na kampuni ya Airtel Tanzania Mwaka Jana mwezi wa kumi na kushirikiksha washiriki mbalimbali kutoka mikoa mbalimbali nchini ambapo fainali ya kumsaka mshindi ilifanyika mwanzoni mwa mwezi wa februari na kumwezesha Mayunga kuwashinda washindani wengine watano na katika fainali hizo na kuondoka na kitita zawadi ya shilingi million 50.


  0 0

  Wafanyakazi wa kampuni ya Megatrade Investment Ltd ya jijini Arusha wakiwa na viongozi wa Chama cha soka wilaya ya Hai kwa ajili ya kukabidhi msaada wa vifaa vya michezo vilivyotolewa kwa vilabu 10 vinavyoshiriki ligi daraja la nne ngazi ya wilaya .
  Meneja Mauzo wa kampuni ya Megatrade Investment Ltd ,kanda ya Kaskazini,Edmund Rutaraka akikabidhi jezi kwa Katibu wa Chama cha soka wilaya ya Hai(HAIDAFA) Cuthbert Mushi huku zoezi hilo likishuhudiwa na wajumbe wa kamati ya utendaji ya chama hicho Fauzia Lema na Marry Munuo(Mwenye kofia) wengine ni wawakilishi wa mauzo wa kampuni ya Megatrade Investment kwa mkoa wa Kilimanjaro,Loserian  Laiser na Filbert Furaha.
  Baadhi ya vifaa vya michezo vyenye thamani ya kiasi cha shilingini Milioni 5 vilivyotolewa na kampuni ya Megatrade Investment ya Jijini Arusha kwa ajili ya vilabu 10 vinavyoshiriki ligi daraja la nne ngazi ya wilaya ya Hai.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini.

  0 0

   Baadhi  ya wanahabari wanaoshiriki  katika warsha ya mtandao  wa kijinsia  Tanzania (TGNP)  wakiwa katika warsha  ya  siku  mbili  jijini  Mbeya.
   Baadhi  ya waraghbishi  wa  ngazi  ya  jamii  kutoka kata ya Msalama wilaya ya  Mbeya  vijijini  wakiwa katika  warsha hiyo.
   Mwezeshaji  wa  warsha  hiyo akiwaonyesha baadhi ya mambo yaliyoibuliwa na  waraghbishi  wa ngazi ya jamii wilaya ya  Mbeya  vijijini.
  ..............................................................................................


  Na  MatukiodaimaBlog

  WAKATI serikali  na  wanaharakati  mbali mbali   wakiendelea  kupiga  vita   mila potofu  za  kurithi  wajane ,baadhi  ya  wanawake  wa kata ya Mlalala  wilaya  ya  Mbeya  vijijini  mkoani  Mbeya  wameeleza  kusikitishwa na vitendo  vya baadhi ya  wajane  kuendelea  kunyanyasika  pale  wanapokataa kurithiwa .


  Hayo  yameelezwa  leo  wa  waraghbishi  wa jamii katika  ngazi ya  kijiji  kutoka kata ya Mlalala  wakati  wakielezea  matokeo ya  tafiti  walizozifanya katika  vijiji  vya kata    hiyo .


  Akizungumza  mbele  ya  washiriki  wa warsha ya  siku  mbili  ya  mtandao  wa  jinsia  Tanzania  (TGNP) inayoendelea  jijini  Mbeya  kwa  kushirikisha   wanahabari   wa  vyombo  mbali mbali  kutoka  mikoa  ya  Mbeya  na  Iringa ,mwakilishi  wa  waraghabishi  hao Bi  Huruma  Mahenge  alisema  kuwa hadi  sasa  tatizo  hilo  bado  ni  kubwa zaidi.


  Kwani  alisema kuwa  baadhi ya  wanawake  wameendelea  kupoteza  mali  zao na  wakati mwingine  kunyanyasika zaidi  kutokana na mila  hiyo ya  wanamke  anapofiwa na mume  kulazimishwa na ndugu  upande  wa  mwanaume  kurithiwa na  mwanandugu  ambae  ameteuliwa na familia ya  upande wa mume.  "Wajane  wamekuwa wakipokonywa mahali mbali mbali  zikiwemo  nyumba , mashamba na  vitu  mbali mbali vya  thamani ama  wakati mwingine  kufukuzwa kabisa  na  watoto iwapo ataonyesha kupingana na maamuzi ya  wanafamilia hao  ya  kurithiwa "alisema  Bi Mahenge  Kuwa  kupitia  kikundi  cha  cha  waraghbishi  wa jamii waliowezeshwa na TGNP  wameanza kupita  katika maeneo  mbali mbali ya  wilaya ya  Mbeya   vijijini  na  kutoa  elimu kupitia matamasha mbali mbali   kama  njia ya  kuelimisha jamii  kuepuka  mila  hizo  potofu.  Alisema hata  kasi ya  maambukizi ya  VVU katika wilaya  hiyo ya  Mbeya  vijijini na mkoa  wa Mbeya kwa  sehemu  yamekuwa yakichangiwa na mila   hizo  za kurithi  wajane.


   Bi Mahenge  mbali  ya  kuipongeza taasisi ya  TGNP kwa kuendelea  kutoa mafunzo  kwa jamii  na  kuijengea  jamii uelewa  kuhusu harakati  za ukombozi wa  mwanamke   kimapinduzi  katika muthadha  wa mjadala  wa madai  ya wanawake katika uchaguzi mkuu 2015  hivi  sasa wanawake ,watoto na  wazee  wameanza kufikiwa na elimu  hiyo kiasi  cha jamii kuanza kuachana na mambo kandamizi  dhidi ya  makundi hayo.
   
  Katika  hatua  nyingine  Bi Mahenge  alisema  kuwa mbali ya serikali kupitia  wizara ya afya na ustawi wa jamii  sera  yake  kutaka wazee wenye  miaka kuanzia  miaka 60  kupatiwa  huduma  za  bure  za matibabu  ila kwa kata  hiyo bado  wazee  wameendelea  kukosa huduma   hiyo ya bure na badala  yake  wanapofika katika maeneo ya  huduma  za afya  husumbuliwa zaidi ama kuandikiwa  dawa za kwenda  kununua.

  Kwa  upande  wake afisa mawasiliano wa  TGNP Bw  Melkizedeck Karol   alisema  kuwa lengo la  mtandao  huu  kutoa  elimu  kwa  wanahabari ni kutaka  kuendelea  kutoa elimu kwa  jamii na kwa pamoja  kuweza  kupaza  sauti  yenye kuleta mabadiliko kwa  jamii  dhidi ya vitendo  vya unyanyasaji wa  kijinsia.


  Bw  Karol  alisema  kuwa  kwa  mwaka  huu TGNP inatoa mafunzo kama  hayo  kwa  wanahabari kutoka kanda  mbali mbali  na  kutaja  maeneo  ambayo  mafunzo kama  hayo  yanaendelea kuwa ni pamoja na Kishapu, Tarime, Morogoro  na Mbeya .

  0 0

     Wananchi wa Kata ya Makuyuni wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye aliwaambia kwa miaka mingi sasa jimbo la Vunjo limekuwa linarudishwa nyuma na ushabiki wa kisiasa na kuwataka wananchi hao kufanya maamuzi sahihi mwaka huu kwa kuichagua CCM.
   katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisikiliza moja ya swali lililokuwa likiulizwa na mmoja wakazi wa himo,Bi.Pepetua Shayo kuhusiana na mradi wa maji uliopo katika eneo hilo,ambapo baadhi ya wananchi wamechukuliwa maeneo yao bila kulipwa fidia yoyote.

   Kijana kutoka chama cha Chadema Membeck Kaigarula akikabidhi kadi ya Chadema kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na kutangaza rasmi kujiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Himo. 
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi kwenye uwanja wa polisi Himo ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa muda umefika sasa wa kufanya maamuzi ya msingi kwa kuchagua kiongozi anayeweza kuleta maendeleo katika Jimbo la Vunjo.
    Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyiaka kwenye viwanja vya polisi himo na kuwaambia wananchi hao wapinzani hawana tena ubavu wa kuongoza kwani kwa zaidi ya miaka mingi sasa wamepata nafasi na hamna walichokifanya kwa wananchi hao wa jimbo la Vunjo.
   Naibu Kamanda wa UVCCM  Moshi Vijijini,Innocent Shirima akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Moshi mjini,Mh.Novatus Makunga,kabala ya kuelekea kwenye mkutano wa hadhara ambapo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alihutubia wakazi wa Vunjo. 
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnaupe pichani kushoto na wajumbe wangine wakitembea kuelekea kwenye uwaja wa mkutano wa hadhara,mjini himo.
   Katibu Mkuu wa CCM akinunua ndizi barabarani Himo wakati akielekea kwenye uwanja wa mkutano wa hadhara
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali kwenye mradi wa vijana wa kijiji cha Oria ,kata ya Kahe Magharibi. 
  Baadhi ya wananchi wakishangilia jambo kwenye uwanja wa polisi Himo ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa muda umefika sasa wa kufanya maamuzi ya msingi kwa kuchagua kiongozi anayeweza kuleta maendeleo katika Jimbo la Vunjo.

  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na Naibu Kamanda wa UVCCM  Moshi Vijijini,Innocent Shirima alipokuwa akiwasili katika kijiji cha Oria,Kata ya Kahe Magharibi,jimbo la Vunjo.

  0 0


  0 0

  Na Mwandishi Wetu, Afrika Kusini.

  MWENYEKITI mpya wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Amina Mwidau, ameongoza wajumbe wa kamati hiyo kwa kufanya ziara nchini ya Afrika Kusini.

  Wakiwa nchini humo walitembelea Bandari ya Durban, ambapo walifanya mazungumzo na viongozi wa juu wa bandari hiyo wakiongozwa na Meneja wake Vusi Khumalo.

  Mwidau ambaye ameambatana na wajumbe kadhaa wa PAC akiwemo Makamu Mwenyekiti Deo Filikunjombe, Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage pamoja na Mbunge wa Mbinga Mashariki, Gaudence Kayombo.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Amina Mwidau akiwa na Meneja wa Bandari Durban nchini Afrika Kusini, Vusi Khumalo wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kikazi nchini humo, Machi 24 na 25 mwaka huu.

  Mwidau akiwa na wajumbe wa PAC, Ismail Rage pamoja na Gaudence Kayombo wakipata maelezo. 

older | 1 | .... | 492 | 493 | (Page 494) | 495 | 496 | .... | 1897 | newer