Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 491 | 492 | (Page 493) | 494 | 495 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Wafanyakazi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel wakiongozwa na Mkurugenzi wa Huduma kwa Jamii,Bi. Adriana Lyamba kubeba mabati kwa ajili ya kupaua darasa litakalotumiwa na wanafunzi wenye ulemavu kwenye shule ya msingi pongwe jijini tanga.
  Mwalimu Mkuu msaidizi wa Shule ya Msingi Pongwe, Mfaume Kamba akitoa maelezo ya ujenzi wa darasa linalojengwa kwa msaada wa kampuni ya simu ya airtel Mkurugenzi wa Huduma za Jamii wa kampuni hiyo,Bi. Adriana Lyamba. 

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imesaidia ujenzi wa darasa kwa ajili ya watoto wenye ulemavu katika shule ya msingi Pongwe iliyopo nje kidogo ya Jiji la Tanga.Darasa hilo limejengwa ikiwa ni jitihada za kampuni hiyo kusaidia maendeleo ya elimu nchini kupitia mpango wa “ Tunakujali” unaohusisha wafanyakazi wake kuchangia katika shughuli za kijamiiMkurugenzi wa Huduma za jamii wa kampuni ya Airtel Bi Adriana Lyamba amefanya ukaguzi wa ujenzi huo na kuahidi kuendelea kusaidia mpango wa elimu kwa makundi yenye mahitaji muhimu hapa nchini.

  Bi Lyamba amesema kuwa msaada huo umetokana na mahitaji ya miundombinu kwa jamii ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu kwenye shule hiyo ambayo kwa Jiji la Tanga ndiyo inatoa elimu kwa watu wenye ulemavu.“sisi Airtel tumeona umuhimu wa wanafunzi wenye ulemavu na tumetambua mahitaji yao ndio maana tumekuja na mpango huu wa ujenzi wa Darasa hapa Pongwe” alisema Bi Lyamba.

  “ujenzi wa Darasa hili ni sehemu ya mpango wetu wa kusaidia ukuaji wa elimu hapa nchini kupitia kampeni yetu ya shule yetu na tunaamini utasaidia makundi yote ya jamii” aliongeza Bi Lyamba.Mwalimu mkuu msaidizi wa shule hiyo Bw. Mfaume Kamba amesema, msaada huo wa ujenzi wa chumba hicho utasaidia sana kupunguza tatizo la wanafunzi wenye mahitaji maalumu kukosa sehemu ya kujifunzi.

  Bw. Mfaume amesema, Jengo hilo ni msaada mkubwa kwa wanafunzi wa awali kwenye shule hiyo ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakisomea nje kutokana na kutokuwepo kwa chumba cha kusomea.“msaada huu ni mkombozi kwetu kwani kwa sasa wanafunzi wetu wa awali watakuwa na mahala pazuri kwa kusomea na kuondokana na adha ya kujifunza wakiwa kwenye mazingira ya nje” alisema Bw. Mfaume.

  Shule hiyo ya Mchanganyiko ya msingi ya Pongwe bado inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na ukosefu wa vyumba vya kutosha vya kujifunzi kwa watu wenye ulemavu na vifaa vyake.

  0 0

  1
  Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu ukitembelea jengo la NHC lililoungua mwaka jana mjini Singida ambapo Shirika linajenga upya jengo jingine katika kiwanja hicho kilichoko katikati ya mji huo. Jana Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia kyando Mchechu ameanza ziara yake ya kutembelea Mikoa ili kuhimiza utendaji kazi wa viwango na kujionea utekelezaji wa miradi ya nyumba za gharama nafuu katika mikoa atakayotembelea ya Singida, Shinyanga, Tabora, Kigoma, Sumbawanga,Katavi na Mbeya. Picha na Muungano Saguya-Shinyanga
  New Picture (2)
  Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu ukiwa eneo la Unyankumi na kupewa maelezo ya mradi wa nyumba za gharama nafuu na Meneja wa NHC Mkoa wa Singida Bw. Ladislaus Bamanyisa ulipotembelea mradi huo kukagua ujenzi wake.
  New Picture (3)
  Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akikagua nyumba za gharama nafuu eneo la Unyankindi Singida na kukuta mmoja wa wanunuzi wa nyumba hizoakiwa amejenga ukuta usilingana na viwango vilivyowekwa na NHC katika miliki zake inazojenga.
  New Picture (4)
  Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu na ujumbe wake wakiwa na mfanyakazi aliyestaafu utumishi wake NHC Dr. Allan Kabogo (wa pili kutoka kulia) walipomkuta eneo la Misigiri Wilaya ya Iramba akiwa anajishughulisha na biashara na huduma za kitabibu. Ujumbe huo ulifurahishwa kuona mstaafu wa NHC anaishi maisha ya furaha na matumaini makubwa.

  New Picture (5)
  Meneja wa NHC Mkoa wa Tabora Bw. Erasto Chilambo akitoa maelezo ya awali kwa ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu ulipotembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Igunga jana.
  New Picture (6)
  Nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Igunga zikiwa katika hatua ya linta tayari kukamilishwa na kuuzwa kwa wananchi wa Wilaya hiyo na maeneo mengine watakaohitaji.
  New Picture (7)
  Utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa nyumba za gharama za nafuu unaotekelezwa na NHC katika mikoa 23 hivi sasa unatoa ajira kwa wananchi wanaozunguka maeneo ya miradi hiyo kama wananchi hawa walivyonaswa na kamera ya NHC Wilayani Igunga jana.
  New Picture (8)
  Meneja wa NHC Mkoani Tabora Bw. Erasto Chilambo akiwatembeza viongozi wa Shirika waliotembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu unaotekelezwa na NHC Wilayani Igunga kwa ajili ya kuuzia wananchi.
  New Picture (9)
  Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akionyeshwa kisima cha maji kinachotumiwa na vikundi vya vijana vya Vijana Tujiajiri na Miti ni Uhai Wilayani Nzega ambavyo vilipewa msaada na NHC wa mashine za kufyatua matofali yanayofungamana.
  New Picture (10)
  Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akiangalia namna mchanga wa kufyatulia matofali yanayofungamana unavyoandaliwa alipotembelea vikundi vya vijana vya Vijana Tujiajiri na Miti ni Uhai Wilayani Nzega jana. Vikundi hivi vilipewa mashine ya kufyatulia matofali na NHC kama sehemu ya kusaidia vijana ajira nchini.
  New Picture (11)
  Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akitoa mchango wa kununua sementi kwa vikundi vya vijana vya Vijana Tujiajiri na Miti ni Uhai Wilayani Nzega ambavyo vilipewa msaada na NHC wa mashine za kufyatua matofali yanayofungamana.Vikundi hivyo sasa vinapata kazi za kuwatengenezea wateja mbalimbali matofali hayo na hivyo kuwa na ajira endelevu.
  New Picture (12)
  Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake wakionyesha na Meneja wa Mkoa wa Tabora Bw. Erasto Chilambo ramani yaeneo lililopewa NHC ili kujenga nyumba za gharama nafuu Wilayani Nzega.
  New Picture (13)
  Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akipewa maelezo na Msimamizi wa mradi wa nyumba za gharama nafuu Bw. Mwikuka juu ya hatua zilizofikiwa katika ujenzi wa nyumba 50 zinazojengwa na NHC eneo la Zongomela Wilayani Kahama.
  New Picture (14)
  Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akisalimiana na mafundi ujenzi alipotembelea mradi wa nyumba 50 za gharama nafuu zinazojengwa na NHC eneo la Zongomela Wilayani Kahama.
  New Picture (15)
  Mkurugenzi wa Usimamaizi wa Mikoa na Utawala Bw. Raymond Mndolwa akishiriki ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Kahama mara baada ya Uongozi wa Shirika kutembelea mradi huo jana.
  New Picture (16)
  Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akisisitiza umuhimu wa kupunguza gharama za ujenzi wa nyumba za gharama nafuu unaofanywa na NHC ili kuwawezesha wananchi wengi kumudu bei ya nyumba hizo alipotembelea nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Kahama ili kuukagua mradi huo jana.
  New Picture (17)
  Mkurugenzi wa redio Kahama FM Bw. Marco Mipawa akimpa maelezo Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu alipotembelea studio hizo ili kufafanua namna wananchi wanavyoweza kununua nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC eneo la Zongomela Wilayani Kahama jana. Ujenzi wa nyumba hizo utakamilika mwezi Agosti mwaka huu na kuuzwa kwa wananchi.
  New Picture (18)
  Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akiongea na wafanyakazi wa NHC Mkoa wa Shinyanga(hawapo pichani) akisisitiza watende kazi zao kwa mtizamo wa kibiashara na kuongeza tija na kwamba hatasita kumuondoa kazini mtumishi yeyote wa Shirika ambaye atashindwa kufikia malengo aliyopewa.
  New Picture
  Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akibatilisha eneo la kujenga nyumba ya biashara mjini Singida kwa Msimamizi wa mradi huo kutoka kampuni ya B.H Ladwa inayojenga jengo hilo. Kwa sasa jengo hilo litajengwa mbele ya jengo la Singida Motel ili kuweza kuvutia wafanyabiashara watakaopanga katika jengo

  0 0

   Makamu wa Rais, Dkt. Bilal (katikati) akikata utepe wa Mradi wa Ujenzi wa Uboreshaji wa Hudumu ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Musoma.Kushoto kwake ni Balozi wa Ufaransa nchini, Melika Berak na viongozi wengine wa chama.
  9
   Makamu wa Rais, Dkt. Bilal akiweka jiwe la Msingi la Mradi wa Ujenzi wa Uboreshaji wa Hudumu ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Musoma.Kushoto ni Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe na katikati ni Balozi wa Ufaransa nchini Melika Berak.
  10
   Mkurugenzi wa Idara ya Ubora wa Maji, Nadhifa Kemikimba akimuonesha Makamu wa Rais, Dkt. Bilal teknolojia ya kusafisha maji kwa kutumia mifupa.
  11
   Baadhi ya washiriki wa maonesho ya Wiki ya Maji Kitaifa

  12
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mbogo Futakamba akizungumza na wananchi juu ya maadhimisho.
  13
   Makamu wa Rais, Dkt. Bilal akimpa kikombe Mkuu wa Idara ya Rasilimali za Maji na Uhandisi wa Umwagiliaji wa Chuo cha Maji, Eng. Pantaleo Tumbo ikiwa ni moja ya zawadi zilizotolewa kwa washiriki wa maonesho ya maadhimisho ya wiki ya Maji.

  Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal akishuka kwenye ndege baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Musoma.2
   Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akiambatana na wenyeji wake baada ya kuwasili mjini Musoma.3
   Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM mkoa wa Mara Adam Ngalawa baada ya kuwasili mjini Musoma.
  4
   Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akisikiliza wimbo wa Tanzania uliokuwa unaimbwa na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kisangula.
  5
   Mkurugenzi Mtendaji ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma, (MUWASA) Mhandisi Said Gantala, akimuonesha Makamu wa Rais, Dkt. Bilal (katikati), ramani ya Mradi wa Ujenzi wa Uboreshaji wa Hudumu ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Musoma. Kushoto ni Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe.
  6
  Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe, akimkaribisha Makamu wa Rais, Dkt. Bilal kuzungumza na wananchi kwenye eneo la mradi.
  7
   Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akizungumza na wananchi.Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara Kapteni Mstaafu Aseri Msangi na kushoto ni Waziri wa Maji, Prof. Maghembe.
  ……………………………………………………………………..
  Hussein Makame-MAELEZO, Musoma
  MAKAMU wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohgamed Ghalib Bilal amesema kuwa kila ahadi ya Serikali iliyotolewa itatimizwa ili kuhakikisha kuwa inaacha kazi nyepesi kwa viongozi watakaokuja katika kuendeleza maendeleo ya Tanzania.
  Dkt. Bilal aliyasema hayo kwenye kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji Duniani ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Mara yakiwa na Kaulimbiu isemayo “Maji kwa Mandeleo Endelevu.
  Katika kilele cha Maadhimisho hayo, Dkt. Bilal aliweka jiwe la Msingi kwenye Mradi wa Ujenzi wa Uboreshaji wa Hudumu ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Musoma ambao utagharimu Shilingi Bilioni 44 hadi kukamilika kwake.
  “Tumewaahidi kupata maji na hilo tutatekeleza.Kila ahadi ya Serikali itatimizwa swali ni muda na wakati lakini kwa kweli hatukusudii kuwaacha njiani, mambo tuliyosema tutayafanya ili tuwaachie watakaokuja kazi nyepesi ya kuendeleza maendeleo ya nchi yetu” alisema Dkt. Bilal.
  Mradi huo mkubwa wa maji unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili, 2015 ambapo Dkt. Bilal alisema mradi huo utakapokamilika itaipatia Manispaa ya Musoma maji ya uhakika kwa asilimia 100.
  Aliongeza kuwa mafanikio ya mradi huo pia ni kuongezeka kwa uzalishaji wa maji kutoka mita za ujazo 10,000 za sasa kwa siku, hadi mita za ujazo 36,000 kwa siku.
  Dkt. Bilal alitoa rai kwa wananchi wa Manispaa ya Musoma na mkoa wa Mara kutunza mradi huo na miradi yote inayoendelea kutekelezwa ili iendelee kuwasaidia wananchi na vizazi vijavyo.
  “Na juu ya haya yote, ni msisitizo katika utunzaji endelevu wa mazingira yetu ili yaendelee kutuhifadhi. Aidha, teknolojia za uvunaji wa maji ya mvua na ujenzi wa mabwawa ni maeneo ambayo yatatuhakikishia kwamba tunakuwa na huduma endelevu ya rasilimali ya maji” alisema.
  Alisema Tanzania haina budi kuwa na mikakati ya makusudi kukabiliana na changamoto hizo, jambo ambalo Serikali imeanza kulifanyia kazi.
  Alifafanua kuwa uhaba wa maji na kutopatikana kwake kwa uhakika kunaleta athari mbaya katika shughuli zote za kiuchumi.
  “Majanga yanayohusiana na maji kama vile, mafuriko na ukame kwa kiwango kikubwa ni maafa yanayojitokeza mara nyingi katika sehemu mbalimbali duniani hivi sasa” alisema Dkt. Bilal na kupngeza kuwa:
  “Vifo, uharibifu wa mali, makazi na miundombinu vina athari kubwa kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja, kikundi, jamii na hata Taifa”
  Hivyo, alitoa wito kwa wadau wote kuunganisha nguvu pamoja katika kukabiliana na athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa kwani, mabadiliko hayo yana athari kuanzia kwenye kupungua kwa misitu na vyanzo vya maji.
  Alitaja athari nyingine kuwa ni kupungua kwa rasilimali za maji juu na chini ya ardhi; kuathirika kwa ubora wa maji ya kunywa; hadi kukua kwa utoaji wa gesi ya ukaa.
  Hata hivyo alisema, Serikali ya Tanzania itaendeleza juhudi za kuhakikisha inawafikishia wananchi maji safi na salama katika maeneo ya nchi ambayo yamekosa huduma hiyo.
  Aliwakumbusha wananchi kuwa wana jukumu kubwa la kutunza vyanzo vya maji popote pale vinapopatikana na kwamba wana kubwa kwenu wananchi ni kutoa mchango unaostahili katika usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji.
  Akimkaribisha Dkt. Bilal, Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe alisema wizara yake itajitahidi na kufanya kila linalowezekana ili katika kipindi kisichozidi miezi mitatu maji yatoke mjini Musoma na wananchi wafurahie huduma hiyo.
  Alisema katika kipindi cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji, viongozi mbalimbali walishiriki katika kukagua miradi ya maji na kutembelea wilaya zote za Mara na kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi ya maji ambayo imekamilika.
  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma, (MUWASA) Mhandisi Said Gantala alisema mradi huo unajengwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Ufaransa kupitia Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD).
  Alisema mradi huo unajumuisha ujenzi wa chanzo kipya cha maji, chujio, mtambo wa kisasa wa kutibu maji na ujenzi wa matenki mapya mawili yenye mita za ujazo 5,500.
  Aliongeza pia kuwa, ujenzi huo utajumuisha ujenzi wa mfumo mpya wa mabomba ya usambazaji maji na ujezni wa miundombinu mingine.
  “Mheshimiwa mgeni Rasmi Serikali ya Ufaransa kupitia Shirika lake la AFD kwa kushirikiana na Benki ya Uwekezaji ya Jumuiya ya Ulaya (EAD) wamekubali kufadhili mradi wa kuondoa majitaka katika manispaa ya Musoma” alisema Mhandisi Gantala.
  Naye Balozi wa Ufaransa nchini Melika Berak alisema kuwa amefurahishwa na ushirikiano anaoupata kutoka Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha wanapunguza tatizo la maji nchini.
  Katika kilele cha maadhimisho hayo ya 27 ya Wiki ya Maji Duniani, washiriki wa maonesho katika maadhimisho hayo walipewa vyeti vya kushiriki na zawadi za vikombe kutokana na makundi washiriki.

  0 0

  Prime Minister of Singapore, H.E. Lee Hsien Loong
   PRESS RELEASE
  H.E. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a condolence message to H.E. Lee Hsien Loong, Prime Minister of Singapore following the death of his father and founding Prime Minister of Singapore, the late Mr. Lee Kuan Yew.

  The message reads as follows:

  “H.E. Lee Hsien Loong,

  Prime Minister of Singapore,

  SINGAPORE.  Your Excellency and dear brother,

  I am writing to extend my deep condolences and that of the government and the people of the United Republic of Tanzania following the death of your father and founding Prime Minister of your nation Mr. Lee Kuan Yew.'

  The demise of Prime Minister Yew is a great loss not only to Singapore but also to all who saw in him an example of a nation builder. The late Yew was admired by the people of Tanzania as a leader whose input in building Singapore is immeasurable, a selfless leader and a friend of all.

  May sincere wish in remembering the late Yew is to emulate him in practice and always embracing his contribution as a leader and role model.

  The People and the Government of the United Republic of Tanzania                        will continue to pray for peace, compassion and strength for the family and the People of Singapore in the time of sorrow and also for the nation as ending’s demise is an immense loss to all Singaporeans.

  Your Excellency,  Please accept my condolences and may the Almighty God rest his soul in eternal peace.  Please accept, Your Excellency the assurances of my highest consideration”.

  Issued by: The Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Dar es Salaam

  23rd March 2015


  0 0

   President Jakaya Mrisho Kikwete escorts Ms. Baronese Lindsay Northover, UK's Parliamentary Under-Secretary of State for International Development after holding talks with her at the State House Behing them is the British High Commissioner to Tanzania Ambassador Diana Melrose
   President Jakaya Mrisho Kikwete and Ms. Baronese Lindsay Northover, UK's Parliamentary Under-Secretary of State for International Development pose for a souvenir photo taken by  the British High Commissioner to Tanzania Ambassador Diana Melrose and another official after  holding talks with at the State House .
   President Jakaya Mrisho Kikwete shakes hands with Ms. Baronese Lindsay Northover, UK's Parliamentary Under-Secretary of State for International Development after holding talks with her at the State House Monday March 23, 2015. Behing them is the British High Commissioner to Tanzania Ambassador Diana Melrose.PHOTO BY STATE HOUSE

  0 0

  Freddy Malima from Dar Es Salaam is the first winner in theongoing #MakeitHappenEAcompetition and will get the chance to take his girlfriend for an all-expenses paid trip to the Mikumi National Park this Easter season as Lumia continues to reward consumers.
  Launched in January 2015, the #MakeItHappenEA aims to empower customers to share their life long desires, and 4 lucky winners will be selected and get a rare opportunity of bring their dream to life.

  Meanwhile, the main prize is only one week away as one lucky consumers stands a chance to win a life changing all expenses paid Experience with friends toCape Town, South Africa courtesy of Lumia.

  To participate, buy any Lumia device*, visit the www.lumialiving.compage where you enter your details and share your dream!

  Winners will be announced on the official Microsoft Lumia social media pages and will be contacted by the Microsoft team to plan how to bring their dream to reality!To learn more about the campaign, follow the #MakeItHappenEA conversations on:
  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akimkabidhi cheti mfanyabiashara mashuhuri,Vicent Laswai kwa niaba ya hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA ) mara baada ya kufanikiwa kufika katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.

  RC Gama akikabidhi zawadi za T-shirt kutoka KINAPA kwa mke wa mfanyabiashara ,Laswai ,Bi Marry Laswai wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Cheti kwa mfanyabiashara huyo baada ya kufanikiwa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.wengine wanao shuhudia ni Mhifadhi mkuu KINAPA,Erastus Rufungulo,na kulia ni mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akimvisha taji ,mfanyabiashara mashuhuri katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ,Vicent Laswai mara baada ya kufanikiwa kufika katika Kilele cha Mlima Kilimanjaro.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama akizungumza mara baada ya kukabidhi Cheti kwa mfanyabiashara Laswai.
  Mfanyabiashara Vecent Laswai akisimulia changamoto na mambo mazuri aliyikutana nayo wakati akipanda Mlima Kilimanjaro na kufika katika kilele cha Uhuru.
  Meneja Maendeleo ya Biashara wa Kibo Palace Hotel ,Charity Githinji akimvisha Laswai tochi maalumu ambayo imekuwa ikitumika wakati wa kupanda Mlima Kilimanjaro 
  Mfanyabiashara Laswai akionesha vifaa alivyokuwa akivitumia wakati wa zoezi la kupanda mlima Kilimanjaro.
  Laswai akipongezwa na mfanyabiashara mwenzake wa Mjini Moshi Ibrahim Shayo maarufu kama Ibra line mara baada ya kufanikiwa kufika kilele cha mlima Kilimanjaro na kurudi salama.
  Baadhi ya wageni waliofika katika hafla fupi ya kukabidhiwa cheti kwa mfanyabiashara Laswai.
  Mhifadhi mkuu Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro,Erastus Rufunguro akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Hotel ya Kibo Homes.
  Mhifadhi mkuu Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro,Erastus Rufunguro akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Hotel ya Kibo Homes.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Kibo Group of Company wakiwa katika hafla hiyo.

  Mr and Mrs Laswai wakifurahia jambo katika hafla hiyo.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akimpongeza Bw,Laswai .
  Mhifadhi mkuu wa KINAPA,Erastus Rufunguro akimpongeza Bw,Laswai.
  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya kasakazini.

  0 0  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akipokelewa na Mkuu mpya wa Wilaya ya Hai,Mh.Anthony Mtaka,mara baada ya kuwasili na kupokelewa wilaya ya Hai tayari kwa kuanza ziara ya wilayani humo.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki kuchimba msingi katika shule ya msingi Modio-Masama Mashariki,Kinana alikagua na kujionea ujenzi mpya wa shule hiyo msingi Modio iliyopata  janga la tetemeko na kubomoka.
   katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akipita kwenye moja ya daraja maarufu sana wilayani Hai,Dara la MNEPO lililopo katika kitongoji cha Kiyungi kijiji cha Mijongweni,wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
   ujenzi wa daraja jipya la MNEPO ambalo lipo katika hatua za mwisho kukamilika ukiendelea
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikagua ujenzi wa daraja jipya la MNEPO ambalo lipo katika hatua za mwisho kukamilika,lililopo katika kitongoji cha Kiyungi kijiji cha Mijongweni,wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na baadhi ya wakazi jamii ya kimasai kutoka kijiji cha Mtakuja,wilayani Hai,mara baada ya kusikiliza mgogoro wao wa ardhi na kampuni ya KADCO,ambapo Ndugu Kinana ameahidi kuutafutia ufumbuzi mgogoro huo ambao umedumu kwa miaka mingi.
   Baadhi ya wakazi jamii ya kimasai kutoka kijiji cha Mtakuja,wilayani Hai,wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kwa staili ya aina yake,alipokuwa akiondoka kijijini hapo mara baada ya kuzungumza nao kusikiliza mgogoro wao wa ardhi na kampuni ya KADCO,ambapo Ndugu Kinana ameahidi kuutafutia ufumbuzi mgogoro huo ambao umedumu kwa miaka mingi. SOMA HAPA KUHUSIANA NA MGOGORO HUO
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiongozwa kukagua chumba kipya cha mionzi,pichani nyuma ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Mh.Leonidas Gama.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akifanya majaribio ya uchunguzi juu ya mkono wake kupitia mashine mpya mionzi,iliyowekwa katika chumba hicho cha mionzi.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa hospitali ya wilaya ya Hai,mara baada ya kukagua chumba kipya cha Mionzi (X-Ray).
   Baadhi ya Wakazi wa mji wa Bomang'ombe  wakishangilia jambo katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini hapo wilayani Hai,mkoa wa Kilimanjaro.
   Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa mji wa Bomang'ombe jioni ya leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Snow View mjini hapo wilayani Hai,mkoa wa Kilimanjaro.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana  akiwahutubia wakazi wa mji wa Bomang'ombe jioni ya leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika  uwanja wa Snow View wilayani Hai,mkoa wa Kilimanjaro.
  Wananchi wa Bomang'ombe wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipowahutubia jioni ya leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini hapo wilayani Hai,mkoa wa Kilimanjaro
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa hospitali ya wilaya ya Hai,kabla ya kukagua chumba kipya cha Mionzi (X-Ray).

  0 0

  WAANDISHI wa Habari Mkoa wa Mbeya hivi karibuni walifanya ziara ya kutembelea kiwanda cha bia TBL Mbeya ambapo pia walipata nafasi ya kushiriki mashindano ya kuonja bia.

  Katika shindano hilo, Mzoefu Saada Matiku ambaye ni mwandishi wa Chanel Ten aliibuka kidedea kwa kupata alama tano kwa tano ikiwa ni mara ya pili tangu apate nafasi kama hiyo kwenye mashindano ya mwaka juzi.

  washindi wengine ni Kenneth Ngelesi wa Tanzania Daima aliyeibuka mshindi wa pili huku Merali Chawe wa Daily news akiibuka kidedea katika nafasi ya tatu.

  Mbali na mashindano hayo Uongozi wa Kiwanda hicho umeilalamikia Serikali kwa kitendo cha kupandisha ushuru kwenye vinywaji katika kila mwaka wa bajeti jambo linaloathiri uzalishaji kwa makampuni binafsi.

  Hayo yalibainishwa  na Meneja wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) Kiwanda cha Mbeya, Waziri Jemedari, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari walipofanya ziara kiwandani hapo Iyunga jijini Mbeya.

  Jemedari alisema uzalishaji wa bidhaa zao katika kiwanda cha Mbeya  umepungua kutokana na ongezeko la Kodi ambapo awali kabla ya kupandishiwa kwa kodi hiyo Kiwanda kilikuwa kinafanya kazi masaa 24 kwa siku 7 lakini sasa kinafanya kazi masaa 24 kwa siku tatu.

  Alisema hadi sasa uzalishaji huo umepungua kwa asilimia 40 ambapo wakati mwingine hulazimika kuzima na kupumzisha mitambo sababu kubwa ni kupungua kwa mauzo baada ya bei kuongezeka.

  Alisema uzalishaji ulikuwa ni Hektolita 12000 hadi 6000 kwa siku lakini sasa hivi umeshuka hadi Hektolita 400 hivyo kusababisha hata kutishia kupunguza watumishi.
  Alisema kitendo cha serikali kupandisha bei kwa mlaji kinaathiri pande nyingi ambapo Mlaji mwenyewe nashindwa kumudu gharama za kununua bidhaa ili hali mzalishaji anaweza anakazalisha kwa wingi lakini sokoni zisinunuliwe.
  “Kama mnavyoona hizo zote ni chupa tupu ambazo zimekosa vinywaji na zilipaswa kuwepo sokoni na hii ni kutokana na kupandisha kodi kiholela, jambo ambalo hata Serikali haijatambua kuwa na yenyewe imekosa mapato” alisema Meneja huyo huku akionesha chupa tupu za bia.

  Aliongeza kuwa serikali ilipaswa kumpandishia kodi mzalishaji na sio mlaji wa mwisho jambo ambalo linaathiri uchumi wa mtu mmoja mmoja.Alisema kwa kufanya hivyo ingekuwa rahisi kwa mzalishaji kuwa na mbinu mbadala ya kukusanya kodi kwa ajili ya kuilipa Serikali tofauti na ilivyosasa ambapo Serikali huongeza gharama ya kodi kwenye bidhaa inayopaswa kwenda sokoni.

  Jemedari alisema katika kunusuru kiwanda kisifungwe uongozi wa tbl umelazimika kupunguza bei ya vinywaji tofauti na bei elekezi inayotakiwa kutokana na kiwango cha kodi ya serikali ambapo Bia moja ilipaswa kuuzwa 2500 lakini kiwanda kimepunguza hadi shilingi 2200.

  Na Mbeya yetu
  Meneja wa Kiwanda akitoa maelekezo.
  Waandishi wa Habari wakipata maelekezo mbali mbali juu ya uzalishaji wa bia.
  Baadhi ya Wataalamu wa Kiwanda cha Bia cha TBL wakiendelea na majukumu yao.
  Picha ya pamoja baada ya kumaliza Ziara.
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akitoa taarifa ya mkutano wa wawekezaji (Round Table Investment Forum) na wakuu wa nchi 5 za ukanda wa Afrika Mashariki utakaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia  Machi 25 hadi 26 mwaka huu.
  Kamishina wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova akitoa taarifa ya hali ya ulinzi na usalama katika jiji la Dar es salaam na vifo vya watu  7 waliopoteza maisha  kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa  zinazoendelea kunyesha katika jiji la Dar es salaam. 
  Na Aron Msigwa –MAELEZO.

  Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa wawekezaji (Round Table Investment Forum) na Marais wa nchi 5 za ukanda wa Afrika Mashariki utakaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia  Machi 25 hadi 26 mwaka huu.  

  Akitoa taarifa ya mkutano huo Mkuu wa wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Saidi Meck Sadiki  amesema kuwa Marais hao Paul Kagame wa Rwanda, Pierre Nkurunzinza wa Burundi, Yoweri Museveni wa Uganda, Uhuru Kenyatta wa Kenya na Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo watahudhuria mkutano huo wakiwa wameambatana na  jumla ya wawekezaji 350. 

  Amesema Tanzania kwa mara nyingine imepata heshima ya kuandaa mkutano huo na kufafanua  kuwa wawekezaji hao wamekwisha anza  kuwasili jijini Dar es salaam kuanzia  Machi 22 , Machi huku marais nchi hizo wakitarajiwa kuwasili jijini humo kuanzia Machi 24,2015.

  Amesema wakiwa nchini Tanzania Marais hao watashiriki kwenye mkutano wa wawekezaji utakaofanyika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Mwalimu J.K.Nyerere kuanzia Machi 23 hadi 26, watatembelea bandari ya Dar es salaam ili kuona namna nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki zinavyoshirikiana katika masuala ya ushuru wa forodha na usafirishaji wa bidhaa mbalimbali.

  Amebainisha kuwa kabla ya kuaondoka nchini  Tanzania Machi 26, 2015 Marais hao pia watatembelea miundombinu ya reli inayotumika kusafirisha mizigo nchi za maziwa makuu kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika usafirishaji wa bidhaa mbalimbali baina ya nchi zao.

  KUHUSU  MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA JIJINI DAR ES SALAAM
  Aidha, kuhusu mvua zinzoendelea kunyesha katika jiji la Dar es salaam  na kusababisha madhara, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki amewataka wananchi kuzingatia agizo la kuhama mabondeni na maeneo mengine hatarishi ili waepuka maafa kufuatia watu 7 kupoteza maisha kutokana na kutokana na athari za mvua zinazoendelea kunyesha.

  Akifafanua kuhusu matukio hayo Mhe. Sadiki amesema maeneo yaliyokumbwa na mafuriko hayo  na kupata maafa hayo ni bonde la Mto Msimbazi na eneo la Buguruni kwa Myamani.

  Amesema kuwa maeneo yaliyokumbwa na mafuriko hayo yameonekana kuwa  na wingi wa takataka ngumu na wingi wa mifuko ya plastiki  iliyotupwa na wakazi hao hali iliyochangia kuziba mifereji inayopeleka maji katika bonde la mto Msimbazi na maji hayo kuhamia kwenye makazi ya watu.
  Ameeleza kuwa kazi ya uokoaji , kumwaga dawa kwenye maji yaliyotuama ili kuzuia athari ya magonjwa ya milipuko, kuzibua mifereji na kukusanya taka katika maeneo hayo inaendelea ili kuruhusu maji kupita kwa urahisi  na kuwataka wakazi hao kuepuka kutupa taka ngumu zinazoziba mifereji ya maji.

  Amesema Serikali inasubiri taarifa kutoka kwa viongozi wa Serikali za Mitaa kwa maeneo ambayo wakazi wake wanaishi kihalali ili waweze kupatiwa misaada ya kibinadamu.

  Kwa upande wake Kamishina wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova amethibitisha vifo vya watu hao 7 waliopoteza maisha kutokana na maeneo yao kukumbwa na mafuriko pamoja na athari ya Umeme.

  Akitoa ufafanuzi wa vifo hivyo amesema kuwa watu 5 wamepoteza maisha kwa kusombwa na maji na wengine 2 wamepoteza maisha kutokana na ajali iliyosababishwa na Lori moja kugonga Transfoma ya umeme eneo la Buguruni Mnyamani.

  Kamishna Kova amesema tayari Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji na Shirika la Ugavi wa Umeme (TANESCO) wameunda kikosi kazi cha uokoaji. Ametoa wito kwa madereva wa magari ya mizigo, mgari binafsi na yale ya abiria kuepuka kupita katika maeneo yaliyojaa maji ili kuepuka ajali na vifo vinavyoweza kuzuilika.


  0 0  Leo Jumanne 24.March 2014 ni siku ya kuzaliwa mdau Hamisi Ally Hamisi tunamuombea kila la heri,Afya njema na maisha marefu,Kijana Hamisi Ally Hamisi alizaliwa siku kama ya leo 24 March,mtaa mchikichi/kongo st.18 Kariakoo jijini Dar akiwa mtoto wa kiume wa alekuwa mchezaji kandanda wa timu za Benfrika,Kongo United "Shetani Wekundu" marehem Bw.Ally Hamisi Ally(RIP) aka De Stefano.

  Hongera sana kijana Hamisi Ally Hamisi kwa siku yako ya Kuzaliwa na endeleza kipaji chako cha kandanda

  wadau mnaweza kuungana nae at www.facebook.com/hamisi.ally.7?fref=ts

  0 0

  DSC_0036

  Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo akipitia kijarida cha maelezo kazi zinazofanywa na taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15. Kulia ni Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Doris Mollel wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa taasisi hiyo uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).


  NAIBU Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi, Mahmoud Thabit Kombo ameitaka jamii kubadili utamaduni na kumshikirisha mwanamme wakati mke wake akienda kujifungua ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha usalama wa mtoto na mama.

  Alisema wanaume wengi hasa wanawake wao wanapokuwa wajawazito na wanakaribia kujifungua wanakosa amani na wengine hukimbia nyumbani au humkimbiza mke na mtoto wao kwa ndugu na jamaa baada ya kujifungua kutokana na kukosa ushauri unaompa ujasiri kuhusu familia yake hiyo mpya.

  Naibu waziri huyo alitoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel mwishoni mwa wiki. Alisema yeye anaamini kwamba moja ya vitu vinavyoweza kupunguza idadi ya vifo kwa watoto wa njiti ni ushiriki wa wanaume na kuwataka watu wa Doris Mollel Foundation kufanya kampeni kubwa ya kubadili tamaduni na wanaume kukalishwa chini kuelekezwa.
  DSC_0069
  Muuguzi wa wodi ya watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mariana Makanda akitoa somo na elimu ya makuzi kwa watoto njiti wanaozaliwa nchini kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa taasisi hiyo.

  Aidha ushiriki wa wanaume katika ujauzito umeelezwa kusaidia kuondoa mashinikizo na ukosefu wa lishe bora kwa wawanake wajawazito kutokana na vitu hivyo kuwa sehemu ya uzazi wa watoto njiti.

  Alisema pamoja na kutoa elimu kwa wanaume na wanawake hasa wauguzi juu ya haja ya wanaume kuona mahangaiko ya wanawake zao, ameitaka jamii kutambua kwamba uzazi katika umri mdogo ni tatizo jingine linalopsababisha uzazi wa watoto njiti.
  Alisema kuhusu mabadiliko katika hospitali na zahanati zetu ili kuwa bora kwa uzazi salama Naibu waziri huyo alitaka taasisi mbalimbali kushirikiana na serikali kuhakikisha kwamba si watoto njiti tu wanakuwa salama bali hospitali na zahanati hizo zinakuwa salama kwa uzazi wa aina zote.

  Awali wakati akimkaribisha Naibu Waziri kufungua taasisi hiyo, Balozi Mwanaidi Sinare, alisema kwamba ipo haja ya zahanati na hospitali za Tanzania zikawa katika hali ya kupokea uzazi wa aina zote ili watoto njiti waweze kuendelea kuishi.
  DSC_0194
  Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo akizungumza kwenye uzinduzi wa taasisi ya Doris Mollel uliofanyika mwishoni mwa juma kwenye hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.

  Wakati huo huo mwasisi wa taasisi hiyo ambaye pia ndiye Mwenyekiti wake, Doris Mollel ambaye ni Mrembo wa Singida 2014/15, ambaye alisema kwamba yeye alizaliwa akiwa njiti na uzito wa kilio 1.2 alisema zaidi ya watoto 200,000 huzaliwa njiti kila mwaka huku elfu 9 wakifariki.
  Alisema wengi wa watoto hao hufariki kwa kukosa huduma muhimu hasa mashine za kuwawezesha kunyonya, kupata joto kuendelea kuishi kabla ya kutoka hospitalini.

  Alisema lengo la kuanzisha taasisi hiyo ni kutafuta fedha za kuweza kusaidia watoto njiti ili kupunguza vifo na kuviondoa. Watoto njiti milioni 15 huzaliwa duniani na kati yao milioni 1 hufa wengi wao kutoka nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania.
  DSC_0112
  Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akielezea makuzi yake baada ya kuzaliwa njiti wa uzito wa kilio 1.2 na kuona kuna umuhimu wa kusaidia watoto njiti wasipoteze maisha kutokana na kukosa vifaa vya kufanya watoto hao waweze kuishi na kufikia malengo kama watoto wengine ambao hawakuzaliwa na wakiwa njiti.

  DSC_0158
  DSC_0171
  Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akimpongeza Balozi Mwanaidi Sinare kwa risala nzuri aliyoitoa wakati wa sherehe za uzinduzi wa taasisi hiyo uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency mwishoni mwa wiki jijini Dar. Kulia ni mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo.
  DSC_0274
  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Rosemary Jairo akizungumza na kumpongeza Doris Mollel wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa taasisi hiyo.
  DSC_0204
  Meza kuu wakijianda kuelekea sehemu maalum ya kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa taasisi hiyo.
  DSC_0218
  Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel na mshirika mwenza wa taasisi hiyo Heena Mujtaba kwa pamoja wakikata utepe kuzindua taasisi yao huku Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo (kushoto) na Balozi Mwanaidi Sinare wakishuhudia tukio hilo.
  DSC_0220
  Sasa imezinduliwa rasmi.
  DSC_0222
  DSC_0228
  Balozi Mwanaidi Sinare (kulia) akimpongeza Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel kwenye uzinduzi huo.
  DSC_0294
  Sehemu ya ndugu, jamaa na marafiki waliohudhuria uzinduzi wa taasisi ya Doris Mollel uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
  DSC_0305
  Baadhi ya wadau waliohudhuria uzinduzi huo.
  DSC_0240
  Meza kuu kwa pamoja wakikata cake maalum wakati wa uzinduzi huo.
  DSC_0250
  Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akimlisha cake mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo wakati wa uzinduzi.
  DSC_0252
  Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akimlisha cake Balozi Mwanaidi Sinare.
  DSC_0254
  Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akimlisha cake Muuguzi wa wodi ya watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mariana Makanda (kushoto).
  DSC_0256
  Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akimlisha kipande cha cake mshirika mwenza wa taasisi hiyo Heena Mujtaba.
  DSC_0258
  DSC_0261
  Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akimlisha kipande cha cake mama yake mzazi Celina Mollel.
  DSC_0048
  Rachel Temu, William Malecela pamoja na mdau wakati wa uzinduzi wa taasisi ya Doris Mollel.
  DSC_0053
  DSC_0040
  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Rosemary Jairo (kulia) Mdau wa Doris Mollel Foundation, Suleiman Saleh pamoja mgeni mwalikwa.
  DSC_0268
  Aliyekuwa Miss Tanzania 1999, ambaye pia ni Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu (kushoto) akifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa taasisi ya Doris Mollel. Kulia ni Miss Tanzania 1998, Basila Mwanukuzi (kulia).
  DSC_0025
  Mtangazaji wa kituo cha Channel Ten na Magic FM, Salma Msangi na rafiki yake wakati wa uzinduzi huo.
  DSC_0080
  Baadhi ya wageni waalikwa akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concepts ambao ni Wachapishaji wa Magazeti ya Jambo Leo, Juma Pinto (wa tatu kulia) na Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Concepts, Benny Kisaka (wa pili kulia) wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye uzinduzi huo.
  DSC_0316
  Mama mzazi wa Doris Mollel , Bi. Celina Mollel (kushoto) katika picha ya pamoja na wadau waliojitokeza kwenye uzinduzi wa taasisi ya Doris Mollel. Kulia ni aliyekuwa Miss Tanzania 1999, ambaye pia ni Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu pamoja na mfanyabiashara maarufu nchini, Bw. Ramesh Patel.
  DSC_0026
  Mjasiriamali Maznat Yusuph Sinare (aliyesimama katikati) akiteta jambo na Balozi Mwanaidi Sinare (kulia) kwenye sherehe fupi za uzinduzi wa Doris Mollel Foundation.
  DSC_0021
  Balozi Mwanaidi Sinare akisalimiana na Mh. Iddi Simba (aliyeipa mgongo kamera yetu) Kulia ni mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo.
  DSC_0321
  Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo (wa pili kushoto) Balozi Mwanaidi Sinare pamoja na mshirika mwenza wa taasisi ya Doris Mollel, Heena Mujtaba.
  DSC_0327
  Pichani juu na chini ni Doris Mollel na familia yake akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau waliohudhuria uzinduzi wa taasisi yake.
  DSC_0331
  DSC_0336
  DSC_0341
  Hoyce Temu katika picha ya pamoja na Rafiki wa Doris Mollel ambaye ni Mlemavu Sophia.
  DSC_0346
  Kutoka kushoto ni Msanii wa filamu nchini, Sinta, Hoyce Temu pamoja na Rachel Temu wakipiga picha kumbukumbu mara baada ya uzinduzi huo kufikia tamati.
  DSC_0350
  Doris Mollel na Sintah.
  DSC_0359
  Mdau Chiku Lweno (kulia) akipozi na Doris Mollel pamoja na baadhi ya wadau waliohudhuria uzinduzi huo.

  0 0

  Balozi wa India nchini Tanzania, Debnath Shaw akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Ofisi za Ask Indus nchini Tanzania, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Ask Indus Global, Abhilash Puljal pamoja na wageni wengine wakishuhudia. Balozi wa India nchini Tanzania, Debnath Shaw akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Ofisi za Ask Indus nchini Tanzania, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Ask Indus Global, Abhilash Puljal pamoja na wageni wengine wakishuhudia.Mkurugenzi Mtendaji wa Ask Indus Global, Abhilash Puljal (kulia) akitoa ufafanuzi ndani ya Ofisi za Ask Indus nchini Tanzania kwa Balozi wa India nchini Tanzania, Debnath Shaw. Mkurugenzi Mtendaji wa Ask Indus Global, Abhilash Puljal (kulia) akitoa ufafanuzi ndani ya Ofisi za Ask Indus nchini Tanzania kwa Balozi wa India nchini Tanzania, Debnath ShawBalozi wa India nchini Tanzania, Debnath Shaw (kushoto) akizungumza mara baada ya kuzinduzi rasmi Ofisi za Ask Indus nchini Tanzania. Kutoka kulia ni Meneja wa Ask Indus nchini Tanzania, A. Prakash na Mkurugenzi Mtendaji wa Ask Indus Global, Abhilash Puljal. Balozi wa India nchini Tanzania, Debnath Shaw (kushoto) akizungumza mara baada ya kuzinduzi rasmi Ofisi za Ask Indus nchini Tanzania. Kutoka kulia ni Meneja wa Ask Indus nchini Tanzania, A. Prakash na Mkurugenzi Mtendaji wa Ask Indus Global, Abhilash Pulja
  Mkurugenzi Mtendaji wa Ask Indus Global, Abhilash Puljal akizungumza katika uzinduzi wa Ofisi za Ask Indus nchini Tanzania. Mkurugenzi Mtendaji wa Ask Indus Global, Abhilash Puljal akizungumza katika uzinduzi wa Ofisi za Ask Indus nchini Tanzania.Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi rasmi wa Ofisi za Ask Indus nchini Tanzania wakifuatilia hotuba anuai. Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi rasmi wa Ofisi za Ask Indus nchini Tanzania wakifuatilia hotuba anuai.Mkurugenzi Mtendaji wa Ask Indus Global, Abhilash Puljal (kulia) akitoa ufafanuzi ndani ya Ofisi za Ask Indus nchini Tanzania kwa Balozi wa India nchini Tanzania, Debnath Shaw. Mkurugenzi Mtendaji wa Ask Indus Global, Abhilash Puljal (kulia) akitoa ufafanuzi ndani ya Ofisi za Ask Indus nchini Tanzania kwa Balozi wa India nchini Tanzania, Debnath Shaw.Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi rasmi wa Ofisi za Ask Indus nchini Tanzania wakifuatilia hotuba anuai. Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi rasmi wa Ofisi za Ask Indus nchini Tanzania wakifuatilia hotuba anuai.Baada ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi rasmi wa Ofisi za Ask Indus nchini Tanzania wakibadilishana mawazo. Baada ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi rasmi wa Ofisi za Ask Indus nchini Tanzania wakibadilishana mawazo.Baada ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi rasmi wa Ofisi za Ask Indus nchini Tanzania wakibadilishana mawazo. Baada ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi rasmi wa Ofisi za Ask Indus nchini Tanzania wakibadilishana mawazo.[/caption][caption id="attachment_56203" align="aligncenter" width="800"]Meneja wa Ask Indus Tanzania, A. Prakash (kulia aliyesimama) akitoa shukrani kwa mgeni rasmi na wageni waalikwa kabla ya kumalizika kwa hafla hiyo. Meneja wa Ask Indus Tanzania, A. Prakash (kulia aliyesimama) akitoa shukrani kwa mgeni rasmi na wageni waalikwa kabla ya kumalizika kwa hafla hiyo.[/caption] Na Mwandishi Wetu, KAMPUNI ya 'Ask Indus Global' imezinduwa huduma zake nchini Tanzania ikiwa ni ofisi itakayo waunganisha wananchi nchini Tanzania juu ya huduma mbalimbali wanazohitaji nchini India wakiwa Tanzania. Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ofisi za Ask Indus Tanzania Limited, Mkurugenzi Mtendaji wa Ask Indus Global, Abhilash Puljal alisema ofisi hiyo ya Dar es Salaam itakuwa kiungo kwa wananchi wanaoitaji huduma za afya, elimu na masuala ya biashara nchini India ambapo kwa sasa wataunganishwa bila usumbufu. Alisema fursa hiyo pia itakuwa ni daraja zuri kwa wafanyabiashara wadogo nchini Tanzania ambao wanahitaji kuagiza bidhaa mbalimbali kutoka nchini India ambapo wataunganishwa na kupata mahitaji yao kwa gharama nafuu na kuepuka mlolongo na gharama za juu. Alisema kampuni hiyo itakuwa msaada mkubwa kwa wagonjwa wanaotegemea huduma za afya kutoka nchini India kwani itakuwa na vifaa vya kisasa vya mawasiliano ambapo mgonjwa anaweza kupata huduma kupitia Ask Indus Tanzania na aweza kupata huduma za awali kuanzia mawasiliano na hospitali, daktari na hata uchaguzi wa hospitali ya kutibiwa kabla ya kuingia gharama za kwenda nchini India tena kwa gharama nafuu. Alisema ofisi hiyo ambayo pia ipo nchini Kenya itakuwa kiungo kikubwa na kuchochea maendeleo kuanzia kwa wafanyabiashara, wananchi wahitaji wa huduma za elimu nchini India kutokea Tanzania na wahitaji wa huduma za afya ambao awali ilichukua muda na gharama kubwa. Akizindua Ofisi hiyo, Balozi wa India nchini Tanzania, Debnath Shaw alisema hiyo ni fursa pekee kwa wananchi Tanzania kuunganishwa kwa huduma mbalimbali kuanzia zile za afya, biashara hasa kwa wafanyabiashara wadogo na wakati pamoja na wahitaji wa huduma za elimu. Alisema kufunguliwa kwa ofisi hiyo mbali na kuchochea maendeleo ya nchi pia ni daraja la kuwaunganisha wananchi wa pande zote juu ya mahusiano ya kiuchumi, kijamii na shughuli nyingine muhimu. Aliwataka wananchi kutumia fursa hiyo ipasavyo ili kuokoa gharama huku wakijipatia mahitaji yao thabiti.

  0 0

  Zifuatazo ni picha za matukio mbalimbali kwenye red carpet wakati wa sherehe ya siku ya wanawake duniani iliyowakutanisha wanawake kutoka kila kona ya visiwani Zanzibar ambayo iliandaliwa na Kikundi cha Wanawake cha Zanzibalicious na kufanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya hoteli ya Bwawani.
  DSC_0148

  DSC_0099
  DSC_0095
  Mbunifu wa mavazi kutoka bara Mama wa mitindo Asia Idarous (kushoto) akipozi na mbunifu wa mavazi kutoka visiwani Zanzibar Matilda Ishungisa wa Malty design.
  DSC_0092
  DSC_0106
  Makamu mwenyekiti wa kikundi cha Wanawake wa Zanzibalicious, Zaning'ha Otembo.
  DSC_0109
  DSC_0111
  DSC_0055
  Mwenyekiti wa kikundi cha Wanawake wa Zanzibalicious Bi. Evelyne Wilson.
  DSC_0057
  DSC_0034
  DSC_0035
  DSC_0041
  DSC_0043
  DSC_0045
  DSC_0052
  Naibu Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe Thuwaiba Kisasi.
  DSC_0066
  Wanaume nao hawakubaki nyuma kutoa sapoti kwa wanawake.
  DSC_0113
  Mama wa mitindo Asia Idarous aking'ara kwenye red carpet.
  DSC_0119
  DSC_0125
  DSC_0128
  Kutoka kushoto ni Make up artist Sada, Mama wa mitindo Asia Idarous na MC wa sherehe ya siku ya wanawake duniani visiwani Zanzibar, Mishi Bomba ambaye pia ni mtangazaji wa Magic FM.
  DSC_0131
  DSC_0134
  DSC_0139
  DSC_0141
  DSC_0143
  DSC_0155
  DSC_0162
  Mke wa Naibu Waziri wa Afya serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bi. Zakhia Kombo (kulia) akiwa na Mama wa mitindo Asia Idarous. Kwa picha zaidi bofya link hii

  0 0

  Rais wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassini Abdalla kushoto akisalimiana na bondia Wang Xin Hua kutoka China mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam jana kwa ajili ya mpambano wake na mohamed Matumla utakaofanyika march 27 katika ukumbi wa diamond jubilee katikati ni Rais wa ngumi za kulipwa nchini PST Emanuel Mlundwa na kulia ni promota wa mpambano uho Jay Msangi Picha na SUPER D BOXING NEWS
  Rais wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassini Abdalla kushoto akisalimiana na bondia Wang Xin Hua kutoka China mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam jana kwa ajili ya mpambano wake na mohamed Matumla utakaofanyika march 27 katika ukumbi wa diamond jubilee katikati ni Rais wa ngumi za kulipwa nchini PST Emanuel Mlundwa .

  bondia Wang Xin Hua kutoka China

  Bondia Wang Xin Hua kutoka China akilakiwa na mwenyeji wake Rais wa ngumi za kulipwa nchini PST Emanuel Mlundwa

  0 0

   Mratibu wa mradi wa ruzuku kwa waandishi wa habari wa mfuko wa waandishi wa habari nchini (TMF) Danstan Kamanzi akizungumza jana mjini Dodoma na kikundi cha waandishi wa habari wanaoandika habari za wasiosikika (Sauti ya mnyonge) kwenye mafunzo ya siku tano ya kuandika habari za mitandao ya jamii yanayofanyika Dodoma hotel.
  Miongoni mwa waandishi wa habari 17 wa kikundi cha waandishi wa habari wanaoandika habari za wasiosikika (Sauti ya mnyonge) wakiwa mjini Dodoma kwenye mafunzo ya siku tano ya kujengewa uwezo wa kuandika habari kwa njia ya mitandoa ya kijamii (social media) yaliyoanza jana. 
  Mratibu wa mradi wa ruzuku kwa wanaandishi wa habari wa mfuko wa waandishi wa habari nchini (TMF) Danstan Kamanzi (kushoto) akimkabidhi mjini Dodoma, Mwenyekiti wa kikundi cha waandishi wa habari wanaoandika habari za wasiosikika (Sauti ya mnyonge) Ramadhan Msangi moja kati ya kompyuta ndogo (tablet) jana kwa ajili ya kufanya shughuli za kikundi hicho.

  0 0

  Wema Sepetu akiwasha gari Jipya la ASX Mitsubishi katika uzinduzi wa gari hilo jijini Dar es Salaam.
   Hili ndilo gari la ASX Mitsubish jipya lililozinduliwa wiki iliyopita katika hoteli ya serena jijini Dar es Salaam 

  Millard Ayo, Wema wasifia gari jipya la 2015 Mitsubishi ASX.
  Mtangazaji wa Clouds FM, Millard Ayo na mwigizaji maarufu nchini, Wema Sepetu wamesifia gari jipya la Mitsubishi ASX la mwaka 2015 linalouzwa na kusambazwa na kampuni ya Diamond Motors (Hansa Group).

  Katika uzinduzi wa kutambulisha gari hilo uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, pamoja na mambo mengine Kampuni ya Diamond Motors wauzaji pekee wa magari kutoka Mitsubishi waliwaalika Millard Ayo na Wema Sepetu kujaribu gari hilo toleo jipya Mitsubishi ASX kabla ya uzinduzi. 

  Mastaa hao walivutiwa na mwonekano wa Mitsubishi ASX lenye vioo vya kisasa juu vyenye mwanga unaomwezesha dereva na abiria kufurahia mwonekano wa pande zote.

  Meneja mauzo wa Diamond Motors, Reena Ganatra alisema Gari hilo lenye luninga ndogo inayocheza DVD, iPods, Bluetooth na sauti kutoka vyanzo mbalimbali ni maalumu kwa vijana wa kisasa na familia kwani Mitsubish ASX  limetengenezwa na teknolojia ya MIVEC yenye kulifanya liwe na nguvu ya 150 ps katika 6,000 rpm na nguvu ya kuzunguka kwa mwendokasi mkubwa na kwamba limetengenezwa maalum kutumia mafuta kidogo. 

  “ASX ni mwanzo tu, tunazo aina nyingine za magari kama kama Pajero ambayo tunakaribia kuyatambulisha sokoni ili kuwapatia watanzania magari imara na yenye kuaminika kutoka Mitsubishi” Alisema Ganatra. 

  ASX toleo la 2015 limebuniwa kwa ubora wa hali ya juu na imara likiwa na bodi gumu pia lina mfumo maalumu usiotegemea funguo hivyo kumfanya mwendeshaji kuwasha injini kwa kubofya kitufe.

   “ASX kutoka Mitsubishi, imetengenezwa maalumu kukidhi mazingira ya Tanzania hasa mijini kama Dar es Salaam ambapo muda wowote dereva wa kawaida anatoka kwenye barabara nzuri na kuingia kwenye barabara zenye makorongo” alisema  Ganatra

  Injini ya gari hilo ambayo ni 2.0-liter imeunganishwa INVECS-III CVT inayoisaidia mwendelezo wake katika kubadili mwendo pamoja na uimara wa usukani unaosaidia mikono ya dereva  kuwa salama hata anapokuwa katika mwendo mkali.

  Hansa Group inayofanya biashara kama Diamond Motors Limited, imekuwa ikifanya kazi ya katika sekta ya usafirishaji tangu mwaka 1980, ikitoa huduma kwa wasambazaji na wadau wa usafiri.Kampuni hiyo huhusika na bidhaa/ huduma mbalimabali. Shughuli za Hansa Group zimesambaa karibu nchi zote za jumuia ya Africa ikitoa huduma kama vile za uchimbaji, Umeme, Mafuta na Gesi, Reli,Ulinzi, Ujenzi, Usafiri, kimataifa na jumuhia za kimataifa. 

  0 0

   Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana ukipokelewa kwa farasi wakati wakiwasili katika kata ya TPC kijiji cha Mikocheni wilaya ya Moshi Vijijni mapema leo asubuhi,tayari kwa kuanza ziara ya jimbo la Moshi Vijijini mkoa wa Kilimanjaro.Ndugu Kinana alizungumza na Wananchi wa kijiji hicho na kuzisikiliza matatizo yao,hasa suala la Ardhi.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wako mkoani Kilimanjaro katika ziara ya siku tisa ya Kusimamia,kuhimiza,Kukiimarisha na kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na  ikiwemo pia kusikiliza matatizo ya wananchi
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake wakiwasili katika kijiji cha Magomeni mapema leo asubuhi,kulia ni Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini Mh.Dkt.Cyril Chami.
   Mkutano ukiendelea katika kijiji cha Mikocheni
   Wananchi wa Mikocheni wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipozungumza nao mapema leo asubuhi,katika jimbo la Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro.
   Wakazi wa kijiji cha Mikocheni wakishangilia jambo wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipozungumza nao na kusikiliza matatizoo yao mbalimbali yakiwemo ya Ardhi.
   Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA tawi la Mikocheni,wilaya ya Moshi Vijijini akitangaza kuhamia chama cha CCM,amapo pia alikabidhiwa kadi mpya ya CCM na kukabidhi kadi yake ya zamani kwa Ndugu Kinana.Pichani kushoto ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisikiliza kwa makini.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiliki kupiga ngoma wakati wakipokelewa katika ukumbi wa CCM mkoa .
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akizunguma katika Mkutano wa Halmashauri kuu ya wilaya na kikao cha jimbo,ambapo Ndugu kinana alipokea taarifa ya chama na taarifa ya utekelezaji wa Ilani 

  0 0

  MBUNGE wa Viti Maalum (CCM), Al Shaimaa Kweigyir, ameitaka serikali kuhakikisha kwamba hukumu za watu wanaokutwa na hatia dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), zinafanyika kwa uwazi, sambamba na kutocheleweshwa ili kulinda roho za Watanzania wanaoendelea kuangamia.
  Picha mbalimbali zikimuonyesha mbunge wa Viti Maalumu, Al-Shaymaa Kweigyir, akiomba mwongozo wa Spika bungeni jana mjini Dodoma, kutaka hatua za haraka zichukuliwe dhidi ya watuhumiwa wa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino). Picha zote na Mpigapicha wetu, Dodoma.
  Akiendelea kutoa ya moyoni
  Akiendelea kuongea kwa msisitizo juu ya mauaji ya albino Tanzania.

  Al-Shaimaa aliyasema hayo bungeni jana akitoa maelezo binafsi kwa kupitia Kanuni ya Kudumu ya Bunge ya (50) 1 inayomtaka mbunge kwa ruhusa ya Spika kutoa maelezo binafsi yanayomhusu au yanayoigusa jamii moja kwa moja.

  Mbunge huyo ambaye pia ni mlemavu wa ngozi alisema kwamba endapo hukumu za kesi za wahalifu wa albino zitahukumiwa mapema na kwa uwazi itatoa funzo kwa wengine wanaofikiria kufanya unyama dhidi ya albino hapa nchini.

  “Na mimi ni mhanga katika jambo hili kwa sababu watu wanaishi kwa mashaka, hivyo naomba hukumu za wahalifu hao ziwe wazi kila mtu aone ili iwe fundisho kwa waliofanya na wale wanaofikiria siku moja wajiingize kwenye unyama huo.

  “Pia naomba sheria za mauaji zirekebishwe ili kulinda haki za walemavu mara baada ya kufanyiwa unyama sambamba na kuwapa adhabu kali wale wote wanaokutwa na hatia dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi,” alisema Kweigyir.

  Kweigyir ni miongoni mwa wabunge wanaopigania haki za kuishi za watu wenye ulemavu wa ngozi, likiwa ni janga lililoshika kasi katika maeneo kadhaa ya Tanzania, hususan katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kunakoonekana kushamiri vitendo vya kuwadhuru na kuwaua walemavu hao wa ngozi.


older | 1 | .... | 491 | 492 | (Page 493) | 494 | 495 | .... | 1897 | newer