Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NDANI YA JIMBO LA ARUMERU MASHARIKI

0
0
 Akina mama wakiusimamisha msafara wa Komredi Kinana iliwaeleza tatizo la kutopatikana maji tangu wazaliwe katika Kijiji cha Shimbumbu, Jimbo la Arumeru Mashariki, mkoani Arusha.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akilakiwa na akina mama waliobeba ndoo tupu ikiwa ni ishara ya kuelezea tatizo la maji linalowakabili wakazi wa Kijiji cha Shimbumbu  Jimbo la Arumeru Mashariki,wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Wakazi wa eneo hilo wamedai kuwa wamekuwa na tatizo hilo la maji tangu wazaliwe kiasi cha kuwafanya walazimike kubadilishana maji na kokoto zinazotokana na kuuvunja mlima wa mawe uliopo kijijini hapo.

Komredi Kinana ambaye katika ziara yake ameambatana na Katibu wa Itikadiu na Uenezi, Nape Nnauye, amewaahidi wananchi wa eneo hilo kuwasaidia kukamilisha mradi wa maji utakaogharamiwa na Serikali ili mlima huo unusurike. Eneo hilo kwa hivi sasa linaoongozwa na Mbunge Joshua Nassari wa Chadema.
 Akina mama wakiwa na ndoo wakati wa mkutano na Komredi Kinana karibu na mlima unaopasuliwa mawe kupata kokoto za kubadilishana maji.
 Komredi Kinana akihutubia katika mkutano uliofanyika Kata ya Mbungu, alikozaliwa yeye.
 Komredi Kinana akihutubia katika mkutano uliofanyika Kata ya Mbuguni, alikozaliwa yeye.
 Wazee wa kabila la Wameru, wakimvisha mgolole ikiwa ni ishara ya kumkaribisha kuwa mzee wa kimila wa kabbila hilo.
 Nape akivishwa mgolole kiwa ni heshima ya wazee kumkaribisha kimila katika Kijiji cha Shimbungu
 Bibi kizee adelela Muungule (78)  akiwa miongoni mwa akina mama wa Kijiji cha Shimbungu, Jombo la Arumeru Mashariki. Bi Adelela amesema kuwa tangu utotoni wamekuwa wakiteseka kupata maji ambvapo walikuwa wanatembea umbali mrefu kuata maji katika mto mmoja uliopo mbali na kijiji hicho.

 Komredi Kinana akisalimiana na wauguzi wa Hosptali ya Wilaya ya Tengeru, alipokwenda kukagua jengo jipya la upasuaji pamoja na ujenzi wa jengo la kuhifadhia maiti..
 Komredi Kinana akitoka kukagua jengo la upasuaji katika hospitali hiyo.
 Komredi Kinana akiruka msingi alipokwenda kukagua jengo la kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Tengeru, Jimbo la Arumeru Mashariki, Mkoa wa Arusha.
 Baadhi ya walimu wa Chuo cha Ualimu cha  Patandi wakiwa na bango linaloelezea kuwa aliwahi kusoma hapo, ambapo awali ilikuwa inaitwa West Meru Middle School. Kinana alisoma katika shule kuanzia darasa la tano hadi la saba kati ya mwaka 1967-1968.
 Komredi Kinana akielezea mazingira ya eneo la shule hiyo aliyosoma jinsi ililivyokuwa tofauti na lilivyo sasa.
 Komredi Kinana akitia saini kwenye kitabu cha wageni cha chuo hicho.
 Msafara wa Kinana ukipita karibu na majengo ya chuo hicho enzi hizo kilivyokuwa shule ya kati alisoma Komredi Kinana.
 Wananchi wakimlaki Komredi Kinana alipowasili katika Kijiji cha Sing'isi kuzungumza na wananchi

 Komredi Kinana akizungumza na wananchi ambapo aliwahidi kuumaliza mgogoro wa ardhi kati ya wana Kijiji na Wawekezaji wanaohodhi ardhi na kuwaacha wananchi wakiteseka kwa kutokuwa na mashamba.

 Komredi Kinana akishiriki ujenzi wa jengo la mashine ya kukobolea mbunga katika  Kata ya Usa River Lekitatu, Jimbo la Arumeru Mashariki


 Komredi Kinana akizungumza na mmoja wa vijana wa Kata ya Mbuguni ambapo yeye alizaliwa, alipofika kukagua mradi wa maji na kuzungumza na wananchi
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara ambapo alikemea kitendo cha Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nayalandu kutembea na viongozi wa dini  kwenye misafara yake mikoani, ili wawe wanamsafisha na tuhuma za kushindwa kutatua migogoro ya ardhi kati ya Hifadhi za Taifa na Wananchi.
 Komredi Kinana akimpongeza aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Wilaya ya Arumeru, John Palangyo kwa kitendo chake cha kuihama CUF na kujiunga na CCM, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Mbuguni, Wilayani Arumeru.
 Komredi Kinana akihutubia katika mkutano huo
 Komredi Kinana akihutubia katika mkutano uliofanyika Kata ya Mbungu, alikozaliwa yeye.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiagana na Mkuu wa Kwanza wa Majeshi mstaafu wa kwanza, Jenerali Sarakikya katika Kijiji cha , Nkoanekoi, Jimbo la Arumeru Mashariki baada ya kumaliza kuhutubia na kutatia kero mbalimbali za wananchi wa kijiji hicho kinachokabiliwa na tatizo la maji, barabara mbovu pamoja na umeme.
 Komredi Kinana akivishwa mgogole na wazee wa Kata ya Mbuguni
Wazee wa Kata ya Mbuguni wakimvisha zawadi ya mgolole, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ikiwa ni heshima ya wazee hao wa Kata aliyozwa Komredi Kinana.



















 Komredi Kinana akihutubia katika mkutano uliofanyika Kata ya Mbungu, alikozaliwa yeye.
 Komredi Kinana akihutubia katika mkutano uliofanyika Kata ya Mbungu, alikozaliwa yeye.

MKUU WA MKOA WA RUKWA ENG. STELLA MANYANYA AKAGUA UJENZI WA MRADI WA MAJI SAFI NA MAJI TAKA SUMBAWANGA MJINI

0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akipata maelezo ya mradi wa Maji Taka katika Manispaa ya Sumbawanga kutoka kwa Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Sumbawanga (SUWASA) Ndugu Zakaria Ngunda alipofika kutembelea mradi huo tarehe 19/03/2015. 

Ujenzi wa mradi wa Maji Taka umeshakamilika na kinachosubiriwa hivi sasa ni magari matatu kwa ajili ya kuzolea taka za vyooni zitakazomwagwa katika mtambo huo  ili uanze kufanya kazi. Miradi yote mikubwa ya Maji Safi na Maji Taka Mjini Sumbawanga inagharimu zaidi ya fedha za Kitanzania shilingi bilioni 30.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na Wakandarasi wanaojenga mradi Maji Safi na Maji Taka Mjini Sumbawanga ambao ni Techno Fab na Mkandarasi mshauri GKW ambapo amewataka kuongeza kasi kumaliza mradi huo ambao upo nyuma ya wakati. Amemuagiza Mkandarasi anaejenga kukamilisha ujenzi huo kwa kipindi cha miezi miwili ijayo licha ya kuomba kuongezewa muda wa miezi sita ili aweze kukamilisha kazi hiyo. 

Alisema kuwa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ni lazima uende na wakati kuhakikisha huduma muhimu zinawafikia wananchi kwa wakati na hivyo kupisha malalamiko ya wananchi kwa Serikali yao. Kwa upande mwingine ameuagiza uongozi wa Maji Safi na Maji Taka Mjini Sumbawanga kumfikishia taarifa za Mkandarasi Herken Builders Ltd aliyojenga mradi wa maji wa visima nane na "pumps" ambazo hazifanyi kazi aweze kumchukulia hatua stakihi ikiwepo kumuandikia barua kuwa hastahiki kufanya kazi katika Mkoa wake wa Rukwa. 
 Mradi wa Bwawa la kuchujia Maji Taka Mjini Sumbawanga ukiwa umekamilika. 
 Sehemu ya Bwawa hilo.
 Sehemu ya Mradi wa Maji Safi ambao ni Chujio la kuchuja Maji Safi kabla ya kwenda kwa walaji.
 Sehemu ya Mradi wa Maji Safi.
Picha nyuma ni sehemu pia ya ujenzi wa mradi mkubwa wa Maji Safi unaoendelea katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga. (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

‘Kishkwambi’ Kutoka Huawei

0
0
Katika kile kinachooneka na ni kujipanga vyema, kampuni gwiji la mawasiliano duniani Huawei imeanza kutangaza kuja na kitu kipya na kikubwa zaidi hivi karibuni.  Tunaweza kusema huu ni mwaka wa Huawei, au tuseme huu ni msimu wa Huawei kufanya yao kwani ni mwezi huu huu wamezindua bidhaa kali na tumeanza kusikia minong’ono ya kuwa ku na mengine yanakuja.  Tofauti na tulivyozoea kuwa wanatangaza uzinduzi wa bidhaa ila sasa hivi wanakuja na “kishkwambi”. Hakuna ajuaye kishkwambi ni nini kwani inaweza kuwa ni bidhaa mpya au inaweza kuwa ni zawadi kwa wapenzi wake laki ni inaonekana wazi kuwa ni jambo kubwa.
Alipoulizwa na mwandishi wa habari hii, Meneja Bidhaa wa kampuni hiyo, Joseph Lyimo alisema kuwa ‘kishkwambi’ ni habari ya mjini, maalumu kwa wapenzi wao na kuwaomba watanzania wote watembelee kurasa zao za mitandao ya kijamii kujua zaidi pia tovuti maalumu ya kishkwambi hapahttp://huawei.kishkwambi.co.tz/

Kampuni ya Huawei yenye makao makuu yake nchini China, imekuwa mstari wa mbele kufikisha teknolojia ya kisasa kwa watu duniani kote. Kwa hapa nchini wamekuwa wakitoa simu za bei nafuu na hivyo kufanya watanzania wengi kupata teknolojia hiyo. 

WAHARIRI, TAMWA WAKUTANA KUFANYA TATHMINI UKATILI UNAOSABABISHWA NA POMBE

0
0
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Gladness Munuo (katikati) akionesha ripoti ya utafiti juu ya matumizi ya pombe na inavyochangia unyanyasaji wa kijinsia kwa Wilaya ya Kinondoni. Kulia ni Mwakilishi wa Shirika la IOGT ambalo ndio wawezeshaji wa utafiti huo. Wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa Shirika la IOGT. Ripoti hiyo imezinduliwa leo jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Shirika la IOGT nchini Tanzania (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kabla ya uzinduzi wa ripoti ya matumizi ya pombe na athari katika vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia.
Mwakilishi wa Shirika la IOGT nchini Tanzania (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kabla ya uzinduzi wa ripoti ya matumizi ya pombe na athari katika vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia.
Kiongozi Mkuu wa Utafiti juu ya matumizi ya pombe uliofanyika Wilaya ya Kinondoni, Dk. Severine Kessy (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari namna utafiti ulivyoendeshwa. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Gladness Munuo. Utafiti huo uliendeshwa na Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) kwa kushirikiana na Shirika la IOGT.
Kiongozi Mkuu wa Utafiti juu ya matumizi ya pombe uliofanyika Wilaya ya Kinondoni, Dk. Severine Kessy (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari namna utafiti ulivyoendeshwa. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Gladness Munuo. Utafiti huo uliendeshwa na Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) kwa kushirikiana na Shirika la IOGT.
Kiongozi Mkuu wa Utafiti juu ya matumizi ya pombe uliofanyika Wilaya ya Kinondoni, Dk. Severine Kessy akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari namna utafiti ulivyoendeshwa. Utafiti huo uliendeshwa na Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) kwa kushirikiana na Shirika la IOGT.
Kiongozi Mkuu wa Utafiti juu ya matumizi ya pombe uliofanyika Wilaya ya Kinondoni, Dk. Severine Kessy akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari namna utafiti ulivyoendeshwa. Utafiti huo uliendeshwa na Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) kwa kushirikiana na Shirika la IOGT.
Baadhi ya waandishi wa Habari waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa ripoti hiyo wakifuatilia matukio na ufafanuzi juu ya ripoti hiyo.
Baadhi ya waandishi wa Habari waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa ripoti hiyo wakifuatilia matukio na ufafanuzi juu ya ripoti hiyo.Baadhi ya waandishi wa Habari waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa ripoti hiyo wakifuatilia matukio na ufafanuzi juu ya ripoti hiyo.
Baadhi ya waandishi wa Habari waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa ripoti hiyo wakifuatilia matukio na ufafanuzi juu ya ripoti hiyo.

PINDA AWEKA JIWE LA MSINGI LA MRADI WA AJI WA BUNDA

0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua eneo la chanzo cha maji cha mradi wa maji wa Bunda katika  katika ziwa Victoria kwenye kijiji cha Nyabehu mkoani Mara  ikiwa ni moja ya shughuli za wiki ya maji, Machi 20, 2015. Kulia kwake ni Mbunge wa Bunda na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephene Wasira.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
3
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiweka jiwe la Msingi la Mradi wa Maji wa Bunda katika  kijiji cha Nyabehu mkoani Mara ,Machi 20, 2015 ikiwa ni moja ya shughuli za wiki ya Maji. . Wapili kushoto ni Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe na kushoto ni Mbunge wa Mwibara, Kange Lugora.  Wapili kulia ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephene Wasirra.
5
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua   moja kati ya mashine tisa za kusukuma  maji katika mradi wa Maji wa Bunda  uliopo kwenye ziwa Victoria katika kijiji cha Nyabihu  wilayani Bunda ikiwa ni moja ya shughuli za wiki ya maji Machi 20, 2015. Kulia kwake ni Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe.

Mwinyi aitwa Pasaka

0
0
RIAS Mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi ameombwa kuhudhuria kwa mara nyingine katika Tamasha la Pasaka linaloadhimisha miaka 15 mwaka huu.Mwinyi ndiye mgeni muasisi  wa tamasha hilo ambako kwa mara ya kwanza alikuwa mgeni rasmi kwenye tamasha la mwaka 2000.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo Alex Msama anapenda rais huyo mstaafu ahudhurie siku hiyo kwa kuwa yeye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi muasisi ambaye pia ni mlezi, hivyo akihudhuria atajionea maendeleo yake.

“Nitapenda sana iwapo rais Mwinyi atahudhuria siku ya Tamasha ili aweze kushuhudia muendelezo wa Tamasha tangu alipolizindua mwaka 2000,” alisema Msama. Alisema hadi sasa maandalizi yamekamilika hivyo mashabiki wa nyimbo za injili wakae mkao wa kula wakisubiria tamasha hilo mapema mwanzoni mwa mwezi ujao.

“Mashabiki wakae tayari maandalizi yamekamilika, tunachosubiri ni siku yenyewe ifike, waimbaji maarufu watakuwepo wakisufu na kuabudu, hivyo ni wakati wenu mzuri wa kwenda kupata neno la Mungu kwa njia ya uimbaji,” alisema.

Tamasha hilo la kimataifa litakalobeba waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili ndani na nje ya nchi litafanyika mwezi ujao Dar es salaam na baadae kwenda katika baadhi ya mikoa. Waimbaji watakaohudhuria Tamasha hilo ni pamoja na Jessica Honore,  Joshua Mlelwa, Upendo Nkone, Kwaya ya Kijitonyama na  John Lisu. Kwa upande na waimbaji kutoka je  ya Tanzania atakuwepo Rebecca Malope na Solly Mahlangu (Afrika Kusini), Faustin Munishi (Kenya).

KIKOSI CHA KMKM KUPATIWA MADAKTARI BINGWA

0
0
imagesAli Issa na Miza Othman Maelezo- Zanzibar.  
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema inatarajia kuajiri Madaktari Bingwa na Wazalendo katika Kikosi maalumu cha kuzuia Magendo Zanzibar KMKM ili kukidhi haja ya Madaktari katika hospitali ya KMKM iliyopo Kibweni Mjini Unguja.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za Serikali Haji Omar Kheri katika Baraza la Wawakilishi wakati akijibu Swali la Mwakilishi wa Wawi Salehe Nassor Juma aliyetaka kujua lini Serikali itaajiri Madaktari Bingwa kwa kikosi hicho
Waziri Heri amesema Uajiri huo utafanywa katika Msimu mpya wa Ajira kufuatilia upungufu wa Madaktari waliopo ili kusaidia kupunguza mzigo wa kuhudumia Wagonjwa katika Hospitali kuu ya Rufaa ya Mnazi mmoja.
Amesema Wataajiri Vijana Wazalendo ambao wamesomea fani husika na Ueledi mkubwa wa kutibu Wananchi Hospitalini hapo ambapo Uajiri huo utakwenda sambamba na Programu ya Wamarekani ambao wamekubali kuisaidia hospitali hiyo kwa kutoa Wataalamu wao.

“Kuna mpango wa kupata madaktari bigwa wawili kutoka marekani ili kuisaidia Hospitali yetu ya KMKM iliyopo kibweni Zanzbar” alisema Waziri Kheri.
Aidha Waziri huyo amesema kuwa watanunua Mashine moja ya Uokozi baada ya ile iliyopo kuharibika ambapo Mashine hiyo itatumika kwa kutilia Gesi vifaa vya uokozi.
Hata hivyo amesema watalazimika kununua Mashine nyingine ili kuziweka katika vituo vya uokozi pale uchumi utakavokuwa unaruhusu kufanya hivyo.
Kikosi maalumu cha KMKM kinatoa huduma za jamii ikiwemo Afya ,katika kambi zake zote ambapo Hospitali ya Kibweni ni hospitali kubwa na yakisasa inayotoa huduma za rufaa ili kusaidiana na hospitali kuu ya Rufaa ya Mnazi mmoja.

KIONGOZI WA EXTRA BONGO BAND ALLY CHOKI KULITINGISHA JIJI LA TOKYO! WHITE PARTY

0
0


APEWA MAPOKEZI MAZURI NA KUPANDA JUKWAANI NA WAKONGWE
                                    FRESH JUMBE NA ABBU OMARY

Ukumbi: Sonudai-Kanagawa Prefecture, Sagamihara City,


Tokyo,Japan.
Mwanamuziki mahili wa muziki wa dansi Ally Choki ambaye pia ni kiongozi wa bendi ya Extra Bongo aka "Wazee wa Kizigo" anatarajiwa kutingisha jukwaa siku ya Jumamosi 21.Machi 2015 ambapo wanamuziki wa Eagle's Vission watakuwepo kumsindikiza Ally Choki anayefuatana na Super Nyamwela.Katika onyesho hilo.

wakongwe wawili wa muziki wa dansi watanzania wanaoishi Japan wanamuziki Fresh Jumbe Mkuu na Abbu Omary watakuwepo jukwaani kuwapa baraka zote wadogo zao Ally Choki na Super Nyamwela katika ukumbi wa Sehemu inaitwa Sonudai-Kanagawa Prefecture, Sagamihara City pembeni kiduchu ya Jiji la Tokyo.

Madhumuni ya ziara ya Ally Choki na Super Nyamwela ni kuangalia ushirikiano na uwezekano wa soko la muziki wa dansi wa Tanzania "Bongo Dansi" ili muziki huo uweze kushika kasi kubwa na soko Japan na mashariki ya mbali kwa ujumla,Pia uwezekano wa bendi ya Extra Bongo kufanya ziara za kimataifa. Wadau msikose
kujitokeza kwa wingi katika Onyesho hili waswahili usema 'Chereko Chereko na mwenye mwana"

MAKAMISHNA WA POLISI WAPYA WAAPISHWA

0
0
Kamishna wa Polisi Elice Mapunda akila kiapo mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu baada ya kupandishwa cheo na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka Naibu Kamishna wa Polisi kuwa Kamishna wa Polisi. Katikati ni Msemaji wa Jeshi hilo Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Advera Bulimba. Hafla hiyo fupi ilifanyinyika jana Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Polisi Diwani Athumani akila kiapo mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu baada ya kupandishwa cheo na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka Naibu Kamishna wa Polisi kuwa Kamishna wa Polisi. Hafla hiyo fupi ilifanyinyika jana Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akimpongeza Kamishna wa Polisi Elice Mapunda mara baada ya kula kiapo mbele yake kufuatia kupandishwa cheo na Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka Naibu Kamishna wa Polisi kuwa Kamishna wa Polisi. Hafla hiyo fupi ilifanyinyika jana Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Polisi Diwani Athumani akila kiapo mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu baada ya kupandishwa cheo na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka Naibu Kamishna wa Polisi kuwa Kamishna wa Polisi. Hafla hiyo fupi ilifanyinyika jana Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi).


Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, amewapandisha vyeo maafisa watatu (3) wa Jeshi la Polisi kutoka cheo cha Naibu Kamishina wa Polisi (DCP) kuwa Kamishina wa Polisi (CP) na maafisa wengine 14 kutoka cheo cha Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) kuwa Naibu Kamishina wa Polisi (DCP).

Maofisa waliopandishwa vyeo kutoka cheo cha Naibu Kamishina wa Polisi (DCP) kuwa Kamishina wa Polisi (CP) ni pamoja na Kenneth Kasseke, Elice Mapunda na Diwani Athumani.

Maofisa wengine waliopandishwa cheo kutoka Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) kuwa Naibu Kamishina wa Polisi (DCP) ni pamoja na Godluck Mongi, Ally Lugendo, Salum Msangi, Faustine Shilogile, Maulid Mabakila, Albert Nyamhanga, Daniel Nyambabe, Salehe Ambika, Robert Boaz na Gabriel Semiono. Pia wamo kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu Charles Mkumbo, kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Valentino Mlowola, kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas na kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala Maria Nzuki.

Aidha, mhe. Rais amempandisha Juma Yusuf Msige kutoka cheo cha kamishina msaidizi wa Polisi (ACP) kuwa kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP).

Kufuatia kupandishwa vyeo kwa maafisa hao wa Jeshi la Polisi, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu katika hafla fupi ya kuwaapisha makamishina hao wapya, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutambua mchango wa Jeshi la Polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao.

Aidha, IGP Mangu amewapongeza maofisa wote waliopandishwa vyeo na kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi mkubwa ili kuwa chachu ya mabadiliko katika kuimarisha usalama wa raia na mali zao. IGP Mangu aliongeza kuwa, cheo ni dhamana na kuwataka kuwa mfano mzuri katika utekelezaji wa majukumu yao na usimamizi kwa walio chini yao.

Imetolewa na:
Advera Bulimba -SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

MAELEZO BINAFSI YA MHE. ZITTO ZUBEIR KABWE, MB KUHUSU UANACHAMA WAKE KATIKA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) NA HATMA YAKE KAMA MBUNGE KATIKA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

0
0
Mh. Zitto Kabwe

SERIKALI INAHITAJI WAMAFUNDI SANIFU 10,000 WA MAABARA (LABORATORY TECHNICIANS) MPYA ZIONAZOJENGWA NCHINI.

0
0
Waziri wa TAMISEMI Mhe.Hawa Ghasia akijibu swali kwa niaba ya Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais na Menejimenti ya Utumishi wa Umma lililoulizwa na Mhe. Yahya Issa (Mb )wa Chwaka tarehe 20.03.2015.Mjini Dodoma.
003
Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya wakiwa wamesimama ndani ya Bunge mara baada ya kutambulishwa kwa uwepo wao,Mjini Dodoma tarehe 20.03.2015.

Na Anitha Jonas – MAELEZO,Dodoma.
Serikali imesema inauhitaji wamafundi sanifu 10,000 wa maabara
(Laboratory Technicians) mpya zionazojengwa nchini.
Hayo yameyasema na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bungeni Mjini Dodoma, Mhe.Hawa Ghasia alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Chwaka, Yahya Kassim
Issa (CUF).
Katika swali lake Issa alitaka kujua kwa nini Serikali huwapa mikataba
watumishi waliostaafu wakati wapo vijana wengi ambao hawana kazi. 
Waziri Ghasia alisema Serikali hutoa mikataba kwa baadhi ya kada ambazo bado hazijitoshelezi kutokana na kuwa na wataalamu wachache.
“Kwa mfano kwa sasa Serikali ina mahitaji makubwa wa mafundi sanifu wa
maabara kwa ajili ya kusimamia maabara zetu zinazojengwa walipo kwa
sasa hawafiki 1,000 wakati mahitaji ni 10,0000,” alisema Ghasia.
Awali akijibu swali la Msingi la Mbunge huyo, Ghasia alisema sio sera
ya Serikali kuwaajiri wastaafu isipokuwa pale tu inapoonekana ni kwa
manufaa ya umma kutokana na mahitaji makubwa katika sekta husika.
Alisema vijana na wasomi waliohitimu vyuo mbalimbali hapa nchini
hupatiwa ajira kulingana na mahitaji ya bajeti iliyopo.
Waziri Ghasia alisema Kwa mujibu wa Kifungu cha 17 (1) cha Sheria ya Pensheni kwa Watumishi wa Umma sura namba 371, mtumishi wa umma anayo hiari ya kustaafu kwa hiyari akifikisha umri wa miaka 55.

KINANA ATIKISA JIMBO LA ARUSHA MJINI,WANANCHI WAMPOKEA KWA SHANGWE.

0
0
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijibu hoja mbali mbali zilizoletwa na kamati ya soko la  Kilombero ikiwa pamoja na kupandishiwa kodi bila utaratibu maalum.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wananchi wa Arusha kwenye soko la Kilombero ambapo walisalimu wananchi waliojitokeza kwa wingi.
 Wananchi na Wafanyabiashara mbalimbali katiko soko la Kilombero wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipozungumza nao ikiwemo pia na kuyasikiliza matatizo mbalimbali yanawakabili katika soko hilo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na viongozi wengine wa chama na serikali wakila chakula kwa Mama Lishe wa soko la Kilombero,jijini Arusha,pichani kulia ni Mbunge wa Viti Maalum Vijana,Mh.Catherine Magige.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakinywa kahawa mara baada ya kumaliza kuwasalimu na kuzindua shina la wakereketwa wajasiriamali Oysterbay, Unga ltd, Arusha.

Ameongeza kuwa CCM ni chama kinachotakiwa kuwasemea na kuwatetea wanyonge na siyo kuwakandamiza na kuwaonea  “Lazima viongozi na watendaji wa serikali na chama wawajibike kwa wananchi ambao ndiyo walioingia mkataba na CCM ambayo iliunda serikali inayotekeleza ilani yake” amesema .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana yuko katika ziara ya kikazi ya mkoa wa Arusha akikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010, inayotekelezwa na serikali ya CCM huku akihimiza uhai wa Chama hicho akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na viongozi wengine wa CCM kuelekea kwenye soko la Kilombero,jijini Arusha,kusikiliza kero na matatizo mbalimbali yaliyopo ndani ya soko hilo.

HARAKATI YA IMETOSHA KUFANYA MATEMBEZI YA HISANI MACHI 29,YAPEWA MCHANGO WA MIL. 10 KUTOKA TDL

0
0
Kampuni ya Tanzania Distilleries LTD (TDL),imechangia kiasi cha sh.milioni 10 kwa harakati ya Imetosha inayopiga vita mauaji ya watu wenye Ualbino,ambayo itafanya matembezi ya hisani machi 29 mwaka huu yatakayofanyika kuanzia katika viwanja vya Biafra na kuishia katika Viwanja vya Leaders Klabu,Kinondoni jijjni Dar es Salaam.

Akizunguma na waandishi wa habari wakati kutangaza kutoa mchango huo,Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo,David Mgwassa amesema kupinga mauaji ya watu wenye ulemavu ni jukumu la kila mtanzania,hivyo TDL kama watanzania wameona umuhimu kuchangia harakati hizo,kwani hata sifa mbaya zinazopatikana nje ya nchi hazilengi mtu mmoja au kundi fulani. 

Amesema watu wengine wajitokeze kuunga mkono harakati hizo ili kuwa sehemu ya watu ambao wanaguswa na suala la mauji ya watu wenye ualbino.

Matembezi hayo yataongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mathias Chikawe ambapo ujumbe wa serikali utatolewa katika harakati zinazoendelea za kukomesha mauaji ya watu hao wenye Ualbino.

Akizungumzia Matembezi hayo,Balozi wa Harakati ya Imetosha,Henry Mdimu amesema matembezi hayo hayalengi kukusanya fedha wanachohitaji ni watu washiriki matembezi hayo.

mdimu amesema kuwa harakati hiyo ni ya kutoa elimu katika mikoa ambayo mauji ya watu wenye ualbino ili kuweza kubadilisha hali hiyo na isiendelee kuwepo.

"Hatulengi masuala ya fedha tunachotaka wananchi wafikishiwe elimu na watu wanaofanya hivyo washindwe kufanya kutokana na elimu iliyotolewa kuanzia katika familia"amesma Mdimu.

Amesema harakati hizo zimetokana na nguvu ya wadau ambao wamejitolea nguvu zao katika kuweza kukomesha mauaji ya watu wenye Ualbino hapa nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Distilleries LTD,David Mgwassa (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza kuchangia kiasi cha shilingi milioni 10 kwa Mfuko wa Imetosha Foundation.Kushoto ni Balozi wa Harakati ya Imetosha,Henry Mdimu na kulia ni Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network,Joachim Mushi.
Balozi wa Harakati ya Imetosha,Henry Mdimu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO jijini Dar es salaam leo,wakati wa kutangaza matembezi ya hisani yatakayofanyika Machi 29 kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es salaam na kuongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mh. Mathius Chikawe.Wengine pichani toka kulia ni Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network,Joachim Mushi,Katibu wa Harakati ya Imetosha,Salome Gregory pamoja na Mwanamuziki Mkongwe nchini,Jhiko Manyika "Jhikoman".
Sehemu ya Wajumbe wa Harakati ya Imetosha waliofika kwenye Mkutano na Waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es salaam,wakiwa kwenye picha ya pamoja.

UMOJA WA VYAMA VYA WANAFUNZI ELIMU YA JUU KUTOKA VYUO MBALIMBALI KANDA YA KASKAZINI WAMUOMBA PROF.MUHONGO KUGOMBEA URAIS 2015

0
0
IMG_8515
UMOJA wa Vyama vya wanafunzi Elimu ya juu kutoka vyuo mbalimbali kanda ya kaskazini Kilimanjarona ,Arusha ,wajitokeza kumshawishi Prof. Sos peter Muhongo Kugombea Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania  Mwaka 2015.(Picha na Jamiiblog).
IMG_8521Akizungumza kwa niaba ya vijana wenzake Mwenyekiti wa vijana hao Charles Ngereza kutoka chuo cha uhasibu Arusha amesema kuwa kinachowafanya kumshawishi prof Sos peter kugombea urais ni kutokana na kuwa kiongozi bora kwa wananchi na mtu anayejali matatizo ya wananchikatika kuwapatia huduma
IMG_8509
Pia wanasema kuwa amekuwa akiwezesha  uchumi kujitegemea na kupinga ulanguzi katika sekta ya uwekezaji pamoja na kutetea vijana katika uwekezaji na kupata ajira.
IMG_8515
Vijana hao ambao ni umoja wa vyama vya wanafunzi wa elimu ya juu katika picha kutoka kushoto ni NELSON WILSON MACHUMU ,TUMAIN UNIVARSITY. 2 DAUD HIPOLITY SHAYO CHUOCHA UHASIBU (IAA)3 SARAH AMINIRABI MUSHI ARUSHA UNIVARSITY 4CHARLES NGEREZA CHUO CHA UHASIBU  ARUSHA.5HOBESHIJUVENARY MAKUMIRA UNIVARSITY PAMOJA NA RAHMA YUSUPH SENGEZA CHUOCHA JOMO KENYATA

BENKI YA CBA YATOA MSAADA WA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 3 KWA SHULE YA SINGISI ARUSHA

0
0
IMG_8466
Meneja Masoko wa bank ya CBA  Bw. Sollomon Kawiche akisoma hutuba wakati walipokuja kutoa msaada chek ya fedha Shiling Million Tatu na laki Nane katika Shule ya msingi na Ufundi Singisi kwa ajiliya kununua vifaa vya umeme vya kujifunzia kwa wanafunzi wa ufundi shulen hapo.Aliyeko kulia ni mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Singisi Janeth Ayo na watatu kulia ni meneja  wa Kanda CBA Juliana Mwansuva(Picha na Jamiiblog)
IMG_8493
Meneja wa Kanda wa Bank ya CBA Juliana Mwamsuva akimkabidhi Mwalimu mkuu washuleya msingi singisi  Janet Ayo Chek ya shiling Million tatu na laki nane kwaajili ya kununua vifaa ya umeme kwawanafunzi wa ufundi shulen hapo.aliyekokushotoni meneja masoko Sollomon Kawiche
IMG_8486
Diwani wa Kta ya seela Singisi Mh Peter kiungai akimkabidhi cake Meneja masoko wa bank ya cba kama ishara ya pongezi ya kutoamsaada shuleni hapo
IMG_8490
IMG_8463(1)
Kikundi cha utamaduni cha wanafunzi katika shule ya Msingi Singisi kikitumbuiza mbele ya ugeni uliokuja kutoa msaada shuleni hapo.

President Kikwete Arrives in Namibia for Presidential inauguration

0
0
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete and his wife Mama Salma Kikwete receive bouquet of flowers shortl after they arrived at Hosea Kutako International airport in Windhoek Namibia to attend the 25th Independence Anniversary -Silver Jubilee and the inauguration of the 3rd President of the Republic of Namibia Dr.Hage Geingob.(Photos by Freddy Maro)

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI MATEMBEZI YA HISANI YA KUCHANGIA UJENZI WA KANISA LA KIGANGO CHA MT. DOMINIC SAVIO TEMEKE MIKOROSHINI, DAR ES SALAAM.

0
0
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki na kuongoza matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kigango cha Mt. Dominic Savio, lililopo Temeke Mikoroshini. Matembezi hayo yamefanyika leo Machi 21, 2015 asubuhi kuanzia Chang’ombe Polisi hadi Temeke Mikoroshini, jijini Dar es Salaam.  
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokelewa na mwakilishi wa Askofu Titus Mdoe, Padri Mushi (mwenye kanzu nyeupe) na baadhi ya viongozi wa Kanaisa wakati alipowasili eneo la mwisho wa matembezi ya hisani ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kigango cha Mt. Dominic Savio, lililopo Temeke Mikoroshini. Matembezi hayo yamefanyika leo Machi 21, 2015 asubuhi kuanzia Chang’ombe Polisi hadi Temeke Mikoroshini, jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla fupi ya matembezi ya hisani ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kigango cha Mt. Dominic Savio, lililopo Temeke Mikoroshini. Matembezi hayo yamefanyika leo Machi 21, 2015 asubuhi kuanzia Chang’ombe Polisi hadi Temeke Mikoroshini, jijini Dar es Salaam
 Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sofia Mjema, akizungumza kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, wakati wa hafla fupi ya matembezi ya hisani ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kigango cha Mt. Dominic Savio, lililopo Temeke Mikoroshini. Matembezi hayo yamefanyika leo Machi 21, 2015 asubuhi kuanzia Chang’ombe Polisi hadi Temeke Mikoroshini, jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya Saa yenye picha yake kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya matembezi hayo, Paroko wa Parokia ya Chang’ombe, Benedict Mushi, wakati wa hafla fupi ya matembezi ya hisani ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kigango cha Mt. Dominic Savio, lililopo Temeke Mikoroshini. Matembezi hayo yamefanyika leo Machi 21, 2015 asubuhi kuanzia Chang’ombe Polisi hadi Temeke Mikoroshini, jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya picha yake iliyochorwa na Msanii, Florian Ludovic (hayupo pichani) kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya matembezi hayo, Paroko wa Parokia ya Chang’ombe, Benedict Mushi, wakati wa hafla fupi ya matembezi ya hisani ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kigango cha Mt. Dominic Savio, lililopo Temeke Mikoroshini,  matembezi hayo yamefanyika leo Machi 21, 2015 asubuhi kuanzia Chang’ombe Polisi hadi Temeke Mikoroshini, jijini Dar es Salaam.  Picha hiyo iliuzwa kwa mnada kiasi cha Sh. Milioni 2.5. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimina na kumpongeza, msanii aliyechora picha yake, Florian Ludovic, wakati wa hafla fupi ya matembezi ya hisani ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kigango cha Mt. Dominic Savio, lililopo Temeke Mikoroshini. Picha hiyo iliuzwa kwa mnada kiasi cha Sh. Milioni 2.5.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Mzee Thomas Wambura Kyangombe (miaka 99) baada ya kushiriki matembezi hayo ya hisani ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kigango cha Mt. Dominic Savio, lililopo Temeke Mikoroshini. matembezi hayo yamefanyika leo Machi 21, 2015 asubuhi kuanzia Chang’ombe Polisi hadi Temeke Mikoroshini, jijini Dar es Salaam. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa katika picha ya pamoja yam zee Thomas Wambura Kyangombe (miaka 99) na mtoto mdogo kuliko wote walioshiriki matembezi hayo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa kanisa hilo na wanakamati wa uchangiaji wa ujenzi huo

ZIARA YA WAZIRI WA ARDHI MH. WILLIAM LUKUVI BABATI MKOANI MANYARA

0
0
1a
Mkuu wa mkoa wa Manyara ,Mhe.Joel Nkaya Bendera akizungumza katika kikao cha viongozi wa wilaya zote za mkoa huo kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Babati,kushoto ni Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe.William Lukuvi na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Babati,Crispin Meela.Mhe.Bendera amesisitiza nidhamu ya kazi katika kuhudumia wananchi na ameapa kuwaondoa watendaji wabovu mkoani humo.
2a
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe.William Lukuvi akizungumza katika kikao cha viongozi wa wilaya zote za mkoa wa Manyara kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Babati.Ameuagiza uongozi wa mkoa huo kumaliza migogoro ya ardhi ifikapo mwezi Mei mwaka huu.
3a
Baadhi ya watendaji wa sekta ya Ardhi Kanda ya Kaskazini na baadhi ya waheshimiwa wabunge akiwemo Mbunge wa Kiteto,Benedct Ole Nangoro na Mbunge wa Viti Maalum,Pauline Gekul wakifatilia maelekezo ya Mhe Lukuvi alipozungumza na watendaji wa mkoa wa Manyara jana.

5a
Wananchi wa mkoa wa Manyara wakimsikiliza Waziri wa Ardhi(hayupo pichani)alipokutana nao kusikiliza kero za migogoro ya ardhi inayosababishwa na watendaji wa sekta hiyo kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Babati.
6a
Wananchi wa mkoa wa Manyara wakipeana maelekezo yaliyotolewa na Waziri wa Ardhi ya namna ya kuwasilisha malalamiko yao kwa maandishi alipokutana nao kusikiliza kero za migogoro ya ardhi inayosababishwa na watendaji wa sekta hiyo kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Babati.
7a
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe.William Lukuvi akizungumza na wananchi wa mji wa Babati waliojitokeza kuwasilisha kero zao zinahusu migogoro ya ardhi.Kikao hicho kilihudhuriwa pia na wabunge wa mkoa wa Manyara.
8a
Katibu Tawala wa mkoa wa Manyara,Mhandisi Omar Chambo akisoma taarifa ya migogoro ya ardhi mkoani humo kwa Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe.William Vangimembe Lukuvi kwenye ziara yake ya kusikiliza kero za ardhi.

KINANA KUHITIMISHA ZIARA YAKE JIJINI ARUSHA LEO

0
0
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa barabara ya Mwanama- Olorien ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami,Ndugu Kinana pia aliitembelea na kuikagua barabara hiyo.
 Ujenzi wa barabara ya Mwanama- Olorien ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami ukindelea ambapo Ndugu Kinana pia aliitembelea na kuikagua. 
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akitembelea kiwanda cha General Tyre eneo la Themi,jijini Arusha,ambapo Kiwanda hicho Serikali imeamua kukifufua na kuanza kuzalisha upya bidhaa zake kupitia shirika la Maendeleo la Taifa (NDC),pichani kati ni Kaimu Mkuregunzi wa NDC,Bwa.Mlingi Mkucha na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha,Onesmo Ole Nangolo.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akisikiliza malalamiko ya baadhi ya waliokuwa wafanyakazi wa kiwanda cha shirika la General Tyre,ambao Ndugu Kinana ameahidi kuyafanyia kazi na kuhakikisha wafanyakazi hao wanapata haki yao.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye sambamba na viongozi wengine wa chama hicho wakitembelea kiwanda cha nguo cha Kiltex,ambapo kimefungwa na kusimamisha uendeshaji wake,ambapo kwa miaka mitatu kiwanda hicho  kiligeuzwa kuwa ghala la kuhifadhia nafaka,hku mitambo yake yote ikiwa imeondolewa na kupelekwa kusikojulikana,
 Mlinzi Mkuu wa Kiwanda cha Kiltex,Mathias Mahundi akifafanua jambo kwa  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana,na kulia ni Mkuu mpya wa Wilaya ya Arumeru na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh.Asnah Mwilima.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizunguza na Halmashauri kuu ya CCM Wilaya,mapema leo jijin Arusha,ambapo pia alipokea taarifa za kazi ya chama na serikali.

WAFANYABIASHARA MANISPAA YA SUMBAWANGA WALALAMIKIA KODI MBALIMBALI SERIKALINI, MKUU WA MKOA WA RUKWA ENG. STELLA MANYANYA AWATAKA KUWA WAZALENDO KULIPA KODI KWA HIARI KUJENGA NCHI YAO

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akisikiliza risala ya umoja wa wafanyabiashara wa Manispaa ya Sumbawanga iliyokuwa ikisomwa kwake na Mwenyekiti wa umoja huo Ndugu Willington Kiziba Ndyetabura (Kulia). Katika risala hiyo yalikuwepo malalamiko mbalimbali ikiwemo ya matumizi ya mashine za EFD ambapo ni pamoja na gharama kubwa za mataengenezo, Ada ya ukaguzi wa majanga ya moto(Fire), Kupanda mara mbili kwa kodi ya mapato kwa wafanyabiashara wadogo na Ulinzi na Usalama kwa wafanyabiashara. Wafanyabiashara hao walihoji n ivigezo gani vilivyotumika kupandishwa kwa kodi hiyo. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na umoja wa wafanyabiashara wa Manispaa ya Sumbawanga tarehe 19/03/2015 katika mkutano wa pamoja wa kusikiliza kero zao mbalimbali uliofanyika katika ukumbi wa Upendo View katikati ya Mji wa Sumbawanga. Wafanyabiashara hao waliomba kuonana na Mkuu huyo wa Mkoa ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka wafanyabiashara hao kuwa wazalendo kwa kulipa kodi kwa hiari ili kuchangia maendeleo ya Mkoa na taifa kwa ujumla.

 Katika kujibu kero zao mbalimbali alisema kuwa, zile kero ambazo haziwezi kutatuliwa mpaka yafanyike mabadiliko ya sheria atayachukua na kuyafikisha sehemu husika na pindi marekebisho yatakapohitajika yatafanyiwa kazi, aliwataka pia wafanyabishara hao watii sheria mbalimbali za kodi ikiwemo kuchangia ada ya ukaguzi wa majanga ya moto ili kuimarisha jeshi la zimamoto ambalo linahitaji maboresho makubwa kwa usalama wa wananchi na malizao.

Kuhusu hali ya ulinzi na usalama katika Mkoa wa Rukwa alisema kwa sasa hali ni shwari ukilinganisha na kipindi cha nyuma ambapo hivi karibuni wahalifu mbalimbali waliokuwa wakisumbua wamekamatwa. Aliwataka wafanyabiashara hao kuwa walinzi namba moja wa amani katika Mkoa wa Rukwa kwa kutoa taarifa zozote zenye dalili za uhalifu au za watu wanaowatilia mashaka. 
Sehemu ya wafanyabiashara wa Mjini Sumbawanga wakifuatilia moja ya mada katika Mkutano huo.
 Washiriki wa Mkutano huo ambao ni wafanyabiashara wa mjini Sumbawanga.
 Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Rukwa Ndugu John Ernest Palingo akijibu baadhi ya hoja kutoka kwa wafanyabiashara hao. Ndugu Palingo alisema Mashine za EFD zina manufaa makubwa kwa mfanyabiashara kwani pamoja na kutunza kumbukumbu za kibishara pia husaidia makisio sahihi ya kodi kwa mfanyabishara kuepusha makadirio ya juu ambayo hupelekea kumnyonya mfanyabiashara.  
 Sehemu ya wafanyabiashara waliohudhuria katika mkutano huo.
Mmoja ya wafanyabishara akiuliza swali katika mkutano huo.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa@rukwareview.blogspot.com)
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live




Latest Images