Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi kwa kupeleka zege kwenye eneo husika wakati wa ujenzi wa daraja la Kisongo,ambalo lilikuwa kero kubwa kwa wananchi kutokana na barabara ya eneo hilo kulika na mmomonyoko wa udongo.
Ujenzi wa daraja la Kisongo ukiendelea kwa kasi,ambapo pia Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alikagua na kushiriki ujenzi wake.
Baadhi ya wananchi wa Kisongo wakipita juu ya barabara ambayo imeanza kuathirika na mmomonyoko wa udongo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuweka zege wakati wa ujenzi wa kituo cha afya cha Manyire,ujenzi wa kituo hicho unatarajia kuisha mwaka huu ambapo kiasi cha fedha zaidi ya shilingi milioni 500 zitakuwa zimetumika kukamilisha ujenzi huo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa kutoka wilaya ya Arumeru Magharibi Ndugu Mathias Manga wakati wakiwasili kata ya Mlangarini tayari kushiriki ujenzi wa Kituo cha Afya cha kijiji cha Manyire.
Shule ya Sekondari Sokoni II kama ionekanavyo pichani,ikiendelea kujengwa vyumba 12 vya madarasa kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo ambayo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alishiriki ujenzi wake na kuzungumza na baadhi ya wazazu (hawapo pichani).Ujenzi wa vyumba hivyo mpaka vitakapokamilika vinatarajia kugharimu kiasi cha fedha zaidi ya shilingi milioni mia tisa
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Ngaramtoni ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa CCM ya sasa haitofanya makosa, na kuwahakikishia kila atakayefanya makosa itabidi aubebe msalaba wake.
Moja ya shina la wakereketwa la Mateves lililofunguliwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
Mbunge wa jimbo la Arumeru Magharibi Ndugu Goodluck Ole Medeyeakizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nduruma ambao walikuwa na malalamiko juu ya mradi wa maji wa Nduruma kuonekana kupelekwa mashambani badala ya maeneo wanayoishi wananchi.Ndugu Kinana wa pili kushoto alikuwepo kusikiliza malalamiko hayo na kuwapatia majibu.
Mmoja wa Wananchi akitoa malalamiko kuhusiana na mradi wa maji wa kijiji cha Nduruma mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana (hayupo pichani).
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Ngaramtoni ambapo alitoa sababu mbali mbali za dalili za kufa kwa upinzani nchini.
Mbunge wa jimbo la Arumeru Magharibi Ndugu Goodluck Ole Medeye akihutubia wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye viwanja vya shule ya msingi Ngaramtoni,Arusha.