Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 484 | 485 | (Page 486) | 487 | 488 | .... | 1896 | newer

  0 0


   Watatu toka kushoto ni Richard Kasesela alipokua akiwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa George  Bush Intercontinental uliopo Houston, Texas nchini Marekani kwa ajili ya Pazi Reunion itakayofanyika siku ya Jumamosi March 14, 2015 katika uwanja wa mpira wa kikapu wa Pilgrim uliopo katika kanisa la Lutheran lililopo Houston. Wengine katika picha ni wenyeji wake waliompokea,  kutoka kushoto ni Willy Crrusa, Aika na Flora Mochiwa maarufu kama Madikodiko. Mchezaji mwingine anayekuja kwenye maadhimisho hayo ya Pazi toka nje ya Marekani ni Atiki Matata anayekuja siku ya Ijumaa March 13, 2015 akitokea Uingereza. Picha na VIJIMAMBO
   Richard Kasesela akitest uwanja wa mpira wa kikapu mara tu alipowasili uwanjani hapo mara tu baada ya kutoka uwanja wa ndege kushoto ni Davis mchezaji mwingine wa mchezo huo, Flora Mochiwa na Willy Crrusa wakiangalia kama bado wamo. Richard Kasesela richa ya kuwa mchezaji wa Pazi pia aliwahi kuwa Rais wa chama cha mpira wa kikapu Tanzania.
   Wachezaji wa mpira wa kikapu wakipata picha ya pamoja na Richard Kasesela.
   Mdau toka Columbus, Ohio akiwa tayari kushuhudia Pazi Reunion itayaofanyika siku ya Jumamosi March 14, 2015 ndani ya jiji la H-Town.
   Willy Crrusa katika picha ya pamoja na Andrew wakati wakiwa ndani ya madikodiko.
   Wageni wakipata chakula huku maongezi yakiendelea.
  Andrew akipata picha ya pamoja na Richard Kasesela.

  0 0

  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akizungumza na wageni waliofika ofisini kwake kumjulisha kuhusu Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni lililoandaliwa na Kilimanjaro Dialogue Institute litakalofanyika nchini Tanzania na kuhusisha nchi 18 tarehe 21 na 22 Machi mwaka huu. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel, wakwanza kulia ni Bw. Ramadhani Madabida na anayefuata ni Rais wa Kilimanjaro Dialogue Institute Bw. Ali Akkiz.
  2
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (watatu kushoto) akizungumza na waandaaji wa Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni lililoandaliwa na Kilimanjaro Dialogue Institute na kuhusisha nchi 18 zikiwemo France, USA, South Africa, Iraq, Mozambique, na Thailand. Kulia ni Rais wa Kilimanjaro Dialogue Institute Bw. Ali Akkiz na wapili kulia ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara.
  3
  Bw. Ramadhani Madabida (kulia) akifafanua jambo walipokutana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara wakwanza kushoto kumpa taarifa ya Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni lililoandaliwa na Kilimanjaro Dialogue Institute litakalofanyika nchini Tanzania tarehe 21 na 22 Machi mwaka huu na kuhusisha nchi 18. katikati ni Rais wa Kilimanjaro Dialogue Institute Bw. Ali Akkiz.
  4
  Rais wa Kilimanjaro Dialogue Institute Bw. Ali Akkiz (wapili kulia) akielezea jinsi walivyojiandaa kufanikisha Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni litakalohusisha nchi 18 walipokutana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (wapili kushoto). Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel, na kulia ni Bw. Ramadhani Madabida.5
  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akizungumza na waandaaji wa Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni litakalofanyika nchini Tanzania tarehe 21 na 22 Machi mwaka huu na kuhusisha washiriki kutoka nchi 18 zikiwemo Tunisia, Central Africa, Romania, Nigeria, kongo, Kenya na Uganda. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Utamaduni Bibi. Lily Beleko na kulia ni Rais wa Kilimanjaro Dialogue Institute Bw. Ali Akkiz.
  Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo

  0 0

  DSC_0576

  Msimamizi wa mradi wa FAO kijiji cha Kiroka mkoani Morogoro, Ajuaye Sigalla, akitoa muhtasari wa maendeleo ya mradi FAO unaotekelezwa na wanakikundi wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI) mbele ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Filiberto Sebregondi walipofanya ziara ya kugagua miradi yao ya maendeleo mkoani Morogoro.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog)

  Na Mwandishi wetu, Morogoro.

  BALOZI wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi ametembelea skimu ya umwagiliaji ya Kiroka na kusema kwamba atahakikisha kwamba kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwamo serikali wataendelea kusaidia wananchi kujiinua kiuchumi.

  Akiwa katika skimu hiyo inayosaidiwa na Shirika la Chakula duniani (FAO) ametaka miradi ya maendeleo nchini kutowaacha nyuma wanawake na watoto kwani wao ndio msingi wa maendeleo ya kijamii kuanzia ngazi ya kaya hadi Taifa.

  Balozi huyo ambaye anatarajiwa kurejea Ulaya mwaka huu baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi nchini amesema kwamba kuwapo kwa asilimia 60 ya wafaidika na mradi huo wa Mpunga kuwa wanawake kumesaidia sana kuamsha maendeleo ambayo yanatakiwa kuendelea kusimamiwa.

  "Wanawake wamefanikiwa kupeleka watoto wao shuleni. kuwapatia chakula kinachostahiki na kupata kipato na katika hili ni vyema wasiachwe nyuma kimaendeleo" alisema balozi huyo.
  DSC_0633
  Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Filiberto Sebregondi akizungumza na wanakikundi wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI) wanaofadhiliwa na FAO wakati wa ziara ya kutembelea miradi inayofadhiliwa na wadau wa maendeleo ambapo mradi wa Kiroka unafadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la FAO huku mradi wa makazi mapya kwa waathirika wa mafuriko Kilosa ukifadhiwa na Ubalozi wa Umoja wa Ulaya. Kushoto kwake ni Msimamizi wa mradi wa FAO kijiji cha Kiroka mkoani Morogoro, Ajuaye Sigalla.

  Alisema kwamba amefurahishwa sana na mradi huo na kusema kwamba Umoja wake utaendelea kushirikiana na mashirika ya Umoja wa Mataifa na serikali katika kuhakikisha kwamba mwananchi wa kawaida wa Tanzania anapata maisha bora.

  Mradi wa Kiroka ambao unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya FAO na benki ya NMB ikishirikiana na RaboBank umelenga kuboresha kilimo cha Mpunga na pia kuwawezesha wakulima hao kuwa na nafasi ya kupata fedha za kuendeleza majukumu yao.


  Ili kufanikisha hilo wakulima wanapatiwa elimu ya fedha na pia utunzaji wa nafaka wa pamoja na mikakati ya mauzo.
  DSC_0643
  Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Filiberto Sebregondi akifafanua jambo wakati akitoa salamu kwa wanakikundi wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI). Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa kijiji cha Kiroka, Mbaraka Mnebe, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez pamoja na Msimamizi wa mradi wa FAO kijiji cha Kiroka mkoani Morogoro, Ajuaye Sigalla.

  Mradi huo ulioanza 2004 na kutarajiwa kuisha Juni mwakani unatekelezwa 2018 umelenga kufungua fursa kwa wanawake na wanaume na kuongeza uzalishaji, kusaka masoko, kupata njia ya kupata mikopo na kujenga uwezo wa kufanikisha shughuli za maendeleo kwenye skimu.
  Mradi huo unatarajiwa kutumia dola za Marekani 737,000 hadi utakapokamilika.

  Wakizungumza na balozi huyo kuelezea mazingira yao wakulima walishukuru msaada unaotoka katika mashirika ya kimataifa na kuwaomba kusaidia kuwapatia fursa zaidi za maendeleo kwa elimu wanayoipata.
  Wamesema mabadiliko yaliyosababishwa na elimu yamewafanya wazalishe Mpunga kwa wingi katika eneo dogo na kufungua fursa za masoko kwa hifadhi na utafutaji masoko wa pamoja.
  DSC_0595
  Katibu wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI), Muhidin Kigadu akielezea mafanikio waliyoyapata tangu walipoanza kupewa mafunzo ya kilimo bora yanayofadhiliwa na Shirika la FAO mbele ya ugeni huo.

  Mradi huo ambao ulianza na Watu wa Sua kama watoa elimu sasa wanapigwa msasa na Taasisi ya maendeleo mjini na Vijijini (RUDI) kwa lengo la kuhakikisha kwamba wanatumia mfumo wa Asia wa ulimaji wa Mpunga kwa kutumia maji kidogo huku wakihifadhi ghalani kusubiri bei nzuri.

  Katika ziara hiyo ya karibuni ya Balozi huyo akiambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, viongozi hao walipata nafasi ya kusikiliza changamoto za wakulima katika mradi huo ambapo uzalishaji sasa umeongezeka kutoka gunia tano kwa eka kufikia gunia 25 kwa kulima kitaalamu.

  Katibu wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI), Muhidin Kigadu alisema mradi huo ambao ulianza Februari 21,2012 umewajengea uwezo wakulima wa mlimani kutengeneza makinga maji huku wakulima wa kwenye skimu wakilima kilimo cha mashadidi.
  IMG_9373
  Mwenyekiti wa kijiji cha Kiroka, Mbaraka Mnebe akielezea jinsi skimu ilivyowasaidia kuinua maisha ya wananchi kwa kuwapatia elimu iliyowaletea mafanikio makubwa yaliyowezesha kulima kisasa na kubadilisha maisha yao hasa katika makazi na huduma za jamii na kuwapeleka watoto shule.

  Alisema wanawashukuru wahisani kwa kuwawezesha kurejesha uoto wa kijani ikiwa na pamoja na kuwa na kilimo cha matunda.
  Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Kiroka, Mbaraka Mnebe amesema skimu imewasaidia kuinua maisha ya wananchi kwa kuwapatia elimu iliyowaletea mafanikio makubwa yaliyowezesha kulima kisasa na kubadilisha maisha yao hasa katika makazi na huduma za jamii na kuwapeleka watoto shule.
  Aidha wakulima wamefanikiwa kununua vyombo vya usafiri vya moto kama Pikipiki na kuachana na Baiskeli.
  DSC_0607
  Mwanachama wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI), mkoani Morogoro, Bi. Asha Bogasi akitoa ushuhuda jinsi maisha yao yalivyobadilika mpaka wanaweza kusaidia na waume zao kusomesha watoto wao kutokana na skimu ya mradi huo.

  Hata hivyo amesema pamoja mafanikio hayo wanachangamoto hasa ya masoko na elimu ambayo wanadhani wanaihitaji zaidi huku akisisitiza zaidi kwamba elimu inatakiwa hata kama wamemaliza mradi na wahisani kuondoka.

  Mradi bado ambao haujakamilika kwani kati ya hekta 147 za mradi ni kama hekta 40 zinazotumuka kwa kuwa miundombinu haijatawanyika vya kutosha katika hekta zote.
  DSC_0661
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akijibu hoja mbalimbali zilizotolewa na kuwapa pongezi za kuweza kubadilisha maisha yao kupitia kilimo cha kisasa kinachofadhiliwa na FAO kwa wanachama wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI) alipofanya ziara ya kukagua mradi huo kijijini hapo.
  DSC_0588
  Wanachama wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI) wakiwa wamekusanyika kwenye shule ya msingi Kiroka wakati wa ugeni wa Shirika la Umoja wa mataifa na Ubalozi wa Umoja wa Ulaya ulipowatembelea kukagua miradi yao.
  DSC_0573
  DSC_0647
  Mratibu mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na Balozi wa Umoja wa Ulaya wakiondoka kijijini hapo mara baada ya kukutana na kuzungumza na Wanachama wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI).

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akilakiwa kwa furaha na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa wakati wa mapokezi  yaliyofanyika Makuyuni, tayari kuanza ziara mkoani Arusha leo.ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza
  kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

  Lowassa amewafagilia Kinana na Nape kwa kazi nzuri wanaoifanya ya kuzunguka mikoa mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha uhai wa chama ambapo alimshauri Komredi Kinana kupunguza kasi wanayokwenda nao kwani ni kubwa. Pia alisema hakuna katibu wa chama aliyefanya kazi kubwa ya kukiimarisha chama kama Kinana.
   Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa wakati wa mapokezi yaliyofanyika Makuyuni, tayari kuanza ziara mkoani Arusha leo.ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa  kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza  kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akivishwa skafu na vijana wa chipukizi mara baada ya kuwasili Makuyuni,wilayani Monduli tayari kwa kuanza ziara ya siku 8 Arusha
    Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akijadiliana jambo na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa wakati wa mapokezi  yaliyofanyika Makuyuni, tayari kuanza ziara mkoani Arusha leo.ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza
  kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
    Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizinduw mradi wa umeme vijini (REA) katika kijiji cha Lolkisale,Wilayani Monduli mkoani Arusha
   Baadhi ya Wananchi wakishangilia jambo wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia katika kijiji cha Lolkisale,ambapo pia alizindua mradi wa umeme vijijini (REA).
  Pichani kulia,Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Mbunge wa jimbo la Monduli,Edward Lowassa (kushoto) wakishiriki kupaka rangi jengo la hospitali ya wilaya,jengo hilo hadi kukamilika zinatarajia kutumia kiasi cha fedha shilingi bilioni tisa
   Pichani kulia,Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Mbunge wa jimbo la Monduli,Edward Lowassa (kushoto) wakishiriki kuweka vitofali katika jengo la hospitali ya wilaya,jengo hilo hadi kukamilika linatarajia kutumia kiasi cha fedha shilingi bilioni tisa
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipokelewa kwa shangwe na wananchi wa Monduli mjini
   ,Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi jengo la kitega uchumi CCM wilaya ya Monduli mkoani Arusha
   Baadhi ya Wananchi wa Mji wa Monduli wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana Monduli mjini.

   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na baadhi ya wakulima wa mpunga wakishiriki kwa pamoja upaliliaji wa shamba la Mpunga,Mto wa Mbu,wilaya Monduli mkoani Arusha.
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akiwa sambamba na Mbunge wa jimbo la Monduli,Edward Lowassa wakitoka kushiriki kupalilia shamba la Mpunga,Mto wa Mbu wilayani Monduli mkoani Arusha.

   Baadhi ya Wafuasi wa chama cha CCM wakishangilia jambo .

  Mbunge wa jimbo la Monduli,Edward Lowassa akihutubia katika uwanja wa barafu,Mto wa Mbu wilaya ya Monduli mkoani Arusha.
   Lowassa wakishangiliwa alipkuwa akihutubia katika mkutano huo
   Nape Nnauye akihutubia katika mkutano huo
  Komredi Kinana akihutubia katika mkutano huo

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Elimu na Ufundi Mhe. Anne Kilango Malecela, Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dr Alex Gehaz Malasusa, Mwenyekiti wa Harambee hiyo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Nehemia Mchechu na wachangiaji wakubwa katika harambee hiyo iliyofanyika usiku huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam ambapo jumla ya shilingi bilioni 1.6 kati ya shilingi bilioni 2 zinazohitajika zilipatikana. Michango hiyo ni ya kufanikisha upanuzi wa chuo hicho katika awamu ya pili.

   Rais Kikwete katika picha ya pamoja na wakuu wa majimbo ya KKKT, Wachungaji, Wainjilisti na wafanyakazi wa Parish na viongozi wengine
   Rais Kikwete katika picha ya pamoja na wakuu wa majimbo ya KKKT, Wachungaji, Wainjilisti na wafanyakazi wa Parish na viongozi wengine
   Rais Kikwete akipongezwa kwa kufanikisha harambee hiyo
  Rais Kikwete katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya harambee hiyo iliyoongozwa na mwenyekiti wake Mzee Arnold Kilewo ( wa kwanza kulia mbele) baada ya harambee hiyo iliyofanyika usiku huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam ambapo jumla ya shilingi bilioni 1.6 kati ya shilingi bilioni 2 zinazohitajika zilipatikana. Michango hiyo ni ya kufanikisha upanuzi wa chuo hicho katika awamu ya pili.

  0 0


       WASANII,WATAYARISHAJI, WASAMBAZI,WATAMAZAJI NA WAANDISHI
                              WOTE   MNAKARIBISHWA


  Asalaam Alaaikum Warhmatullah Wabarakatuhu

  Tunapenda kuwajulisha wadau wa maadili movies nchini kutakuwa na mkutano wa mkubwa utakaofanyika tarehe 31 Mai 2015 kuanzia saa 2.00 asubuhi ukumbi wa Jaffar Complex uliopo  Mnazi mmoja jijini Dar es salaam  

  AGENDA ZA MKUTANO
  Kuandaa daftar la orodha ya wasanii na kuchagua rasmi aina ya mfumo wa filamu zetu na mengineyo
   
  Kuchagua uongozi wa wa muda uliona mpangilio rasmi na kuupa majukumu likiwepo la 
  1. Kuanzisha mtandao wenye hamasa na mwelekeo kwa wassii wote wa maadili Africa mashariki na Africa kwau ujumla
  2. Kushirikiana na kujenga na kuunga mkono kuimarisha soko la filamu

  Tunapenda kuaalika waandishi wa habari watunzi waongozaji  wasambazaji na hata watazamaji wa filamu za maadili wasanii wote nchini tunawaalika ila stara ya mavazi kwa wanawake izingatie muhimu kwa wanawake  

  "Maadili Movies Lengo ni kusimamia ulinzi wa maadili mema kupitia filamu za Kitanzania, kuazisha, kuendeleza na kuhamsisha uwepo na ukuwaji wa filamu zenye heshima, zinazozingatia maneno, matendo na mavazi yenye maadili."
  Tuwe pamoja wana 
  • BURUNDI
  • RWANDA  
  • KENYA 
  • UGANDA
  • CONGO
  • TANZANIA na AFRICA KWA UJUMLA 
  Kwa mawasiliano ya simu kwa wale watakaoshiriki kutoka nchi tofauti tofauti pamoja na nchini ,Tafadhali tuwasiliane kwa simu kwa namba zifutazo:

  0 0


  0 0

  Zitto Kabwe .

  Mwanamapinduzi na Rais wa zamani wa Burkina Faso Thomas Sankara alisema kuwa ili kuleta mabadiliko ya kimapinduzi ni lazima kuwa na hali fulani ya uendawazimu. 

  Ila tusiufikirie uendawazimu huu wa kuokota makopo bali ule ukichaa mzuri wa kuamini katika mambo au misingi fulani na kuisimamia kwa dhati pamoja na changamoto nyingi.

  Kwa kuamini kwa dhati katika mabadiliko haya na kutaka kuboresha maisha ya wanakigoma, mwaka 2005 nilikuja kwenu kuwaomba ridhaa ya kuwatumikia kama mwakilishi wenu Dodoma. Nikiwa na umri wa miaka 29 tu. Labda ulikuwa ni msukumo wa matumaini yangu makubwa yanayoambatana na ujana yaliyowashawishi, kwani mliniamini na kunipa kazi hiyo ya heshima kubwa ya kuwawakilisha.

  Mwaka 2010 mliniamini tena, naamini kutokana na utekelezaji wangu mzuri wa kazi na mafanikio tuliyoyaweza kuyapata katika jimbo letu. Hivyo kwa miaka kumi tumekuwa bega kwa bega katika safari hii ya pamoja ya kujenga na kuiendeleza jimbo letu, na leo nimekuja kuwashukuru kwa fursa mliyonipa kwani safari yetu inafikia mwisho. Fursa mliyonipa ni ya kipekee kwani ilikuwa fursa si tu ya kuwatumikia ninyi bali kulitumikia Taifa langu.


  0 0

   makundi mbalimbali ya kijamii ya mikoa ya Kaskazini, inayojumuisha mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Arusha na Manyara wakiwawanaandamana kwa pamoja kuelekea kwa mbunge wa jimbo la monduli  hii leo


  Katibu wa Chama cha Wasioona Mkoa wa Kilimanjaro  (TLB), Protas Soka Akisoma risala kwa niaba ya makundi hayo mbele ya mbunge wa jimbo la monduli
   Viongozi mbalimbali wa makundi ya kijamii wakiwa wanamkabidhi waziri mstaafu ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Monduli Edward Lowasa bahasha yenye fedha taslimu shilingi milioni mbili laki tano sitini na saba elfu na mia sita zilizochagwa na wananchi   kwa ajili ya kwenda kuchukuwa fomu ya kugombea nafasi ya Urais.
  Kwa picha zaidi na habari kamili BOFYA HAPA

  0 0

  Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege (kushoto) akimkabidhi balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 fedha waliyoitoa kusaidia harakati za imetosha jana jijini Dar es Salaam. Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege (kushoto) akimkabidhi balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 fedha waliyoitoa kusaidia harakati za imetosha jana jijini Dar es Salaam.Balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu (kulia) akizungumza na wanahabari kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa shilingi milioni 10 zilizotolewa na Makampuni ya IPTL na PAP kusaidia kampeni maalumu kupinga mauaji ya watu wenye albino. Kushoto ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege. Balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu (kulia) akizungumza na wanahabari kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa shilingi milioni 10 zilizotolewa na Makampuni ya IPTL na PAP kusaidia kampeni maalumu kupinga mauaji ya watu wenye albino. Kushoto ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege.Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege (wa pili kulia) akizungumza na wanahabari katika hafla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 10 kusaidia harakati za imetosha jana jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu. Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege (wa pili kulia) akizungumza na wanahabari katika hafla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 10 kusaidia harakati za imetosha jana jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu.Baadhi ya viongozi na wajumbe wa kamati ya utendaji ya Imetosha Foundation wakipiga picha na hundi ya shilingi milioni 10 fedha iliyotolewa na Makampuni ya IPTL na PAP kusaidia kampeni maalumu kupinga mauaji ya watu wenye albino. Wa kwanza kushoto ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege. Baadhi ya viongozi na wajumbe wa kamati ya utendaji ya Imetosha Foundation wakipiga picha na hundi ya shilingi milioni 10 fedha iliyotolewa na Makampuni ya IPTL na PAP kusaidia kampeni maalumu kupinga mauaji ya watu wenye albino. Wa kwanza kushoto ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege.Balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu (kulia) akizungumza na wanahabari kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa shilingi milioni 10 zilizotolewa na Makampuni ya IPTL na PAP kusaidia kampeni maalumu kupinga mauaji ya watu wenye albino. Kushoto ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege. Balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu (kulia) akizungumza na wanahabari kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa shilingi milioni 10 zilizotolewa na Makampuni ya IPTL na PAP kusaidia kampeni maalumu kupinga mauaji ya watu wenye albino. Kushoto ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege.

   KAMPENI maalumu za kupinga mauaji ya watu wenye u-albino nchini inayojulikana kama 'Imetosha' iliyoanzishwa na balozi wa kujitolea, Henry Mdimu, chini ya Imetosha Foundation zimezidi kushika asi baada ya makampuni ya IPTL na PAP kutoa shs milioni 10 kusaidia kampeni hizo. Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege jana alimkabidhi balozi Mdimu mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10 kama ishara ya kuunga mkono kampeni hizo za kutoa elimu kutokomeza imani potofu zilizojengeka kwa baadhi ya wanajamii juu ya watu wenye albino. 

  Akizungumza katika hafla hiyo fupi Bw. Makandege alisema matukio ya mauaji au kukatwa viungo kwa watu wenye ulemavu wa ngozi yaani albino yamefika hatua ya kutisha nchini Tanzania, hususani katika kanda ya ziwa hivyo kuna kila sababu kila mmoja bila ubaguzi kushiriki kusaidia mapambano hayo. Alisema ulemavu wa ngozi waliyonao watu wenye albino ni mapungufu ya kibaiolojia ambayo ni mapenzi ya Mungu hivyo imani potofu zinazoendelea hazina budi kupigwa vita kwa nguvu zote. 

  "...Kuna minongono mitaaani kwamba watu wanatenda matukio hayo wana imani potofu kwamba ukitumia kiungo cha mtu mwenye albinism, ndipo utafanikiwa. Kama kweli viungo vyao vingekuwa vinaleta utajiri, basi watu wenye albinism wangekuwa matajiri namba moja duniani," alisema Makandege akizungumza. 

   "...Sisi IPTL na PAP tumeguswa sana na jambo hili. Kwa wote wanaofanya matendo haya, mnapaswa kuwa na hofu ya Mungu mkijua kuwa siku ya kihama, kila mtu atajibu na kuhukumiwa kwa matendo yake. Tunakubaliana kabisa na wenzetu IMETOSHA Foundation kwamba, imefika wakati kila Mtanzania, na hata wageni waishio Tanzania, kusema IMETOSHA na kusimama kidete kuwalinda hawa ndugu zetu," alisisitiza kiongozi huyo wa IPTL. 

  Aidha kampuni za IPTL na PAP zimeyataka makampuni mengine nchini na watu binafsi kuungana kwa kuchangia harakati hizi za imetosha ili kusaidia kampeni ya imetosha kupita mikoa ya kanda ya ziwa kupaza sauti na kuielimisha jamii juu ya uwepo wa imani potofu zinazoendeleza mauaji ya watu wenye u-albino. Kwa upande wake Balozi wa Imetosha, Mdimu aliishukuru kampuni za IPTL na PAP kwa moyo wauliouonesha wa kusaidia harakati hizo na kumtaka kila Mtanzania kwa nafasi yake kusaidia kupaza sauti kwamba imetosha mauaji na unyanyasaji wanaoupata watu wenye ualbino. Alisema mauaji haya yanamgusa kila Mtanzania na kuendelea kuichafua nchi yetu hivyo kumtaka kila mmoja kupaza sauti yake kupinga vitendo hivyo. 

  Machi 28, 2015 Imetosha Foundation inatarajia kufanya matembezi ya hisani kuchangisha fedha zaidi ili kusaidia kampeni za kukomesha mauaji ya watu wenye u-albino kabla ya kuanza rasmi safari za kuzunguka katika mikoa ya kanda ya ziwa pamoja na wasanii waliojitolea kueneza elimu hiyo kwa jamii moja kwa moja.

  0 0

  Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani), jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki kuhusiana na ujio wa mwimbaji nyota kutoka Afrika Kusini Thori Mahlangu (Obrigado). (Picha Francis Dande)
   Msama akifafanua jambo.
   
  Na Loveness Mboje

  RAIA  wa Afrika Kusini ambaye ni Mwanamziki wa nyimbo za injili, Thori Mahlangu (Obrigado), amethibitisha kuwa mmoja wa waimbaji wa kimataifa watakaotumbuiza katika Tamasha Pasaka litakalofanyika Aprili 5.

  Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema kuwa sambamba na mwimbaji huyo ataambatana na waimbaji wengine 16 kutoka nchini humo huku Faustine Munishi maarufu kwa jina la Malebo na Solomon Mukubwa  kutoka nchini Kenya nao watakuwepo.

  Msama alisema kuwa viingilio vya tamasha hilo kwa watoto vitakuwa shs. 2,000 viti vya kawaida shs.5,000 VIP B, shs. 10000 VIP A shs. 20,000 kwa watu wakubwa na kuongeza kuwa mara baada ya tamasha hilo, Aprili 12 itakuwa ni zamu ya wakazi wa jiji la Mwanza katika Uwanja wa  CCM Kirumba.

  Aidha kwa upande wa waimbaji wazawa  Msama amesema kuwa mwimbaji Joshua Mlelwa ambaye alikuwa mwimbaji wa Upendo Group  naye atapamba tamasha hilo ambalo linasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki.

  Tamasha hilo linatimiza miaka 15 tangu lianzishwe
  na linatarajiwa kuhudhuriwa na watu mbalimbali kutoka nchi za Kenya, Uganda,Rwanda, Afrika Kusini Uingereza na wenyeji Tanzania.

  0 0

   Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt. Primus Nkwela (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye Makao makuu ya ofisi hizo  Mikocheni B jijini Dar es Salaam, Wakati akiutangazia Umma juu ya kukaribisha maombi ya kujiunga na mafunzo ya Ualimu kwa mwaka wa masomo 2015/2016 kwa vijana waliomaliza kidato cha Nne  Oktoba 2014. na wengine wenye sifa mbalimbali  kama zinavyopatikana kwenye  tovuti ya baraza hilo:www.necte.go.tz.Waombaji  watakao omba kabla ya tarehe 10 Aprili 2015 wataruhusiwa kujiunga  na mafunzo mnamo Aprili 15 2015 kwenye vyuo mbali mbali kama vinavyopatikana kwenye tovuti yao.Kulia ni Katibu msaidizi wa Baraza hilo Ramadhani Samainda.
  .Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt. Primus Nkwela (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari pichani katika Makao makuu ya ofisi hizo  zilizopo Mikocheni B jijini Dar es Salaam, wakati akiutangazia Umma juu ya kukaribisha maombi ya kujiunga na mafunzo ya Ualimu kwa mwaka wa masomo 2015/2016 kwa vijana waliomaliza kidato cha Nne  Oktoba 2014. na wengine wenye sifa mbalimbali  kama zinavyopatikana kwenye  tovuti ya baraza hilo:www.necte.go.tz.Waombaji  watakao omba kabla ya tarehe 10 Aprili 2015 wataruhusiwa kujiunga  na mafunzo mnamo Aprili 15 2015 kwenye vyuo mbalimbali kama vinavyopatikana kwenye tovuti yao.

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (wa pili kulia)akishiriki ujenzi wa tanki la maji katika Kijiji cha Sakala, wilayani Ngorongoro.Ndugu Kinana na ujumbe wake wako kati wa ziara ya siku tisa mkoani Arusha ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
   Komredi Kinana akisaidiana na Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro, Telele kujenga vyumba vya madarasa ya kidato cha nne na cha tano katika Shule ya Sekondari Samunge, wilayani Ngorongoro.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM kijiji cha Wasso Ndugu Revocatus William Parapara. Awali ndugu Revocatus William Parapara alikuwa Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Ngorongoro kwa takribani miaka 15.
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akilakiwa kwa ngoma ya kabila la Watemi (Wasonjo) alipowasili katika Kijiji cha Samunge, wilayani Ngorongoro, aliposhiriki ujenzi ujenzi wa vyumba vya madarasa ya kidato cha nne na cha tano katika Shule ya Sekondari ya Samunge wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
   Wajumbe wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ngorongoro wakiwa katika mkutano na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mjini Loliondo
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza katika mkutano huo.

   Komredi Kinana akiingia kwenye mkutano wa hadhara katika Mji wa Waso, wilayani humo
   Nape Nnauye akihutubia katika mkutano huo wa hadhara
   Komredi Kinana akipatiwa zawadi ya fimbo  Kinana akihutubia katika mkutano huo.
   Komredi Kinana akiangalia ngoma wakati wa mapokezi katika mkutano wa hadhara mjini Wasso, wilayani Ngorongoro.
   Vijana wa jamii ya kimasai wakitumia simu kupiga picha wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akihutubia katika KJijiji cha Ngaresero, wilayani Ngorongoro.


   Komredi Kinana akivishwa pambo lenye shanga katika Kijiji cha Ngaresero

   Mmoja wa wanachama wapya wa CCM akipatiwa kadi na Komredi Kinana baada ya kujiunga katika Kijiji cha Ngaresero, wilayani Ngorongoro.  0 0

   Vijana wa Kigoma wakiwa na bango wakimsubiri Mhe. Zitto Kabwe "Mirumbani" alipokwenda jimboni huko kutoa Ahsante kwa kumchagua kuwa mbunge wao kwa vipindi viwili
   Mhe. Zitto Kabwe "Mirumbani" alipokwenda jimboni huko kutoa Ahsante kwa kumchagua kuwa mbunge wao kwa vipindi viwili
   Mhe. Zitto Kabwe "Mirumbani" akitoa  Ahsante kwa wananchi wa jimboni kwake kwa kumchagua kuwa mbunge wao kwa vipindi viwili
    Mhe. Zitto Kabwe "Mirumbani" akiwa amebebwa na  wananchi wa jimboni kwake alipokwenda kuwashukuru kwa kumchagua kuwa mbunge wao kwa vipindi viwili.
    Mhe. Zitto Kabwe "Mirumbani" akicheza ngoma na  wananchi wa jimboni kwake alipokwenda kuwashukuru kwa kumchagua kuwa mbunge wao kwa vipindi viwili
    Mhe. Zitto Kabwe "Mirumbani" akihutubia  wananchi wa jimboni kwake alipokwenda kuwashukuru kwa kumchagua kuwa mbunge wao kwa vipindi viwili
    Mhe. Zitto Kabwe "Mirumbani" akikabidhi gari la wagonjwa katika kituo cha Afya cha kijiji cha Nyarubanda  jimboni kwake alipokwenda kuwashukuru kwa kumchagua kuwa mbunge wao kwa vipindi viwili.

  0 0


  0 0

   Timu ya Pazi wanaume wakipata picha ya pamoja na mashabiki wao walipokua nyumbani kwa madikodiko ambaye pia ni mmoja wa waratimu wa tamasha hili la kumbukumbu ya timu hiyo iliyowika miaka mingi katika ukanda wa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla. Tamasha hili lililobeba jina la Pazi Reunion litafikia tamati leo Jumamosi March 14, 2015 kwa mechi kadhaa na kuakumbuka na kuaenzi viongozi na wachezaji wa timu hiyo waliotangulia mbele ya haki.
   Pazi Queens wakiwa katika picha ya pamoja leo patakua hapatoshi.
  Patrick Mwigula kutoka South Carolina na Atiki Matata kutoka Uingereza wachezaji wa Pazi waliowika miaka ya nyuma wakijadili mchezo wa leo kama walivyokutwa na kamera ya Vijimambo.
   Atiki Matata na Richard Kasesela wakipata picha ya pamoja.
  Kulia ni Masawe shabiki wa Pazi wa miaka mingi si mazoezi si mechi alikua hakosekani uwanjani hapa akisalimiana na Richard Kasesela mara tu walipoonana baada ya kupoteana kwa miaka mingi.
  Kutoka kushoto ni Emmanuel, Patrick na Kasesela wakikumbushana enzi zao za Pazi.
  Wachezaji wa Pazi toka shoto ni Vitalis Gunda toka Maryland, Richard Kasesela toka Tanzania na Willy Crrusa toka Houston, Texas wakikumbushana enzi zao. Kwa picha zaidi Bofya HAPA

  0 0
  0 0

  Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa akizungumza muda mfupi kabla ya wagombea wa nafasi mbalimbali wa SHIMIWI Mkoani Rukwa kuanza kunadi sera zao tarehe 13/03/2015. Katika salam zake ameahidi kutoa ushirikiano kwa uongozi wa SHIMIWI utakaochaguliwa ili kusukuma gurudumu la maendeleo ya michezo Mkoani Rukwa.
  Msimamizi wa Uchaguzi Ndugu Erasmus Rugarabamu ambae pia ni Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa  akitoa maelekezo na taratibu mbalimbali za uchaguzi huo wa kuwachagua viongozi wa Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Mkoani Rukwa  tarehe 13/03/2015. 
  Sehemu ya washiriki wa uchaguzi huo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa, Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Sumbawanga, Kalambo na Nkasi.
   Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Ndugu David Mlongo akitoa baadhi ya maelekezo kwa washiriki.
  Mwenyekiti mpya wa Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Mkoani Rukwa Ndugu Godfrey Haule akinadi sera zake muda mfupi kabla ya zoezi la upigaji wa kura kuanza. Mwenyekiti huyo ameshinda kwa jumla ya kura 47 kati ya kura 95 zilizopigwa.
  Makamu Mwenyekiti mpya wa SHIMIWI Mkoani Rukwa Ndugu Furahi Kisogole akinadi sera zake muda mfupi kabla ya zoezi la upigaji wa kura. Mgombea huyu ameshinda kwa jumla ya kura 75 kati ya kura 95 zilizopigwa.
  Katibu mpya wa Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Mkoani Rukwa Ndugu Lusungu Nyagawa akinadi sera zake muda mfupi kabla ya zoezi la upigaji wa kura kuanza. Mgombea huyu ameshinda kwa jumla ya kura 39 kati ya kura 95 zilizopigwa.
  Katibu Msaidizi mpya wa SHIMIWI Mkoani Rukwa Bi. Asha Kanondo Ally akinadi sera zake muda mfupi kabla ya zoezi la upigaji wa kura. Mgombea huyu ameshinda kwa jumla ya kura 54 kati ya kura 95 zilizopigwa.
  Katika nafasi pekee ilyokuwa na mgombea mmoja ni ile ya Mwekahazina ambayo Ndugu Dotto Leonard pichani akinadi sera zake kabla ya uchaguzi ameshinda kwa kura za ndio 89 dhidi ya kura 16 za hapana  kati ya kura 95 zilizopigwa.
  Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa SHIMIWI Ndugu Leonard Mihayo Kariba akinadi sera zake muda mfupi kabla ya zoezi la upigaji wa kura. Mjumbe huyu alishinda kwa jumla ya kura 47 katika kura 95 zilizopigwa.
   Upigaji wa kura.
   Zoezi la upigaji kura. 
  Zoezi la uhesabuji wa kura likiendelea.
  (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Michael Mhando akizungumza na Waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusiana na zoezi la upimaji afya na kukusanya damu salama kwa ushirikiano na Mpango wa damu salama katika mikoa sita nchini.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Michael Mhando akizungumza na Waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusiana na zoezi la upimaji afya na kukusanya damu salama kwa ushirikiano na Mpango wa damu salama katika mikoa sita nchini. Kushoto ni Afisa Uhusiano wa Mpango wa taifa wa Damu Salama, Rajab Mwenda.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Michael Mhando akizungumza na Waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusiana na zoezi la upimaji afya na kukusanya damu salama kwa ushirikiano na Mpango wa damu salama katika mikoa sita nchini. Kushoto ni Afisa Uhusiano wa Mpango wa taifa wa Damu Salama, Rajab Mwenda na kulia ni Mkurugenzi wa Rasilami watu na Utawalawa wa NHIF, Beatus Chijumba.
  Baadhi ya maofisa wa NHIF walioshiriki mkutano huo na waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini. 
  **********

  0 0

  1
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia katika mkutano wa Kiuchumi na maendeleo wa Misri, uliofunguliwa jana Machi 13, 2015 na Rais wa Misri, Abdel-Fattah El- Sisi, mjini Sharm El-Sheikh, Misri.
  2
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) akiwa na baadhi ya viongozi kutoka mataifa mbalimbali wakati akiwa katika mkutano wa Kiuchumi na maendeleo wa Misri, uliofunguliwa jana Machi 13, 2015 na Rais wa Misri, Abdel-Fattah El- Sisi, mjini Sharm El-Sheikh, Misri
  3
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais wa Misri, Rais wa Misri, Abdel-Fattah El- Sisi, wakati walipokutana kwa mazungumzo baada ya mkutano huo, uliofanyika jana Machi 13, 2015 mjini Sharm El-Sheikh, Misri.
  6
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Wawekezaji wa Misri wanaotaka kuwekeza katika Sekta ya Viwanja Wilayani Mkuranga, wakati alipokutana nao kwa mazungumzo leo, Machi 14, 2015 mjini Sharm El- Sheikh, Misri, alikohudhuria mkutano wa Kiuchumi na maendeleo wa Misri, uliofunguliwa jana Machi 13, 2015 na Rais wa Misri, Abdel-Fattah El- Sisi, mjini Sharm El-Sheikh, Misri.
  7
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na wageni wake Wawekezaji wa Misri wanaoataka kuwekeza katika Sekta ya Viwanda Wilayani Mkuranga, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika leo Machi 14, 2015 mjini Sharm El- Sheikh, Misri alikohudhuria mkutano wa Kiuchumi na maendeleo wa Misri, uliofunguliwa jana Machi 13, 2015 na Rais wa Misri, Abdel-Fattah El- Sisi, mjini Sharm El-Sheikh, Misri. Picha na OMR

older | 1 | .... | 484 | 485 | (Page 486) | 487 | 488 | .... | 1896 | newer