Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 483 | 484 | (Page 485) | 486 | 487 | .... | 1897 | newer

  0 0

  unnamed (4)Dear Friends.
  Napenda kutoa taarifa kwamba kumekuwa na tapeli mmoja ambae amekuwa akitumia picha zangu kwa kufungua facebook accounts kwa majina mbali mbali kama Justin Stan,James Brown,Onesmo,Felister Julius, Anthony Yohana au Yohana Anthony na mengineyo mengi.

  Mtu huyu amekuwa akijenga urafiki na watu wasiotambua kuwa ni TAPELI katika mtandao wa kijamii wa Facebook.

  Urafiki ukiwa umekamilika kwa maana ya friends request kutoka kwake and acceptance kutoka kwa victim amekuwa akiwaambia marafiki zake hawa wa Facebook kuwa yeye ni muajiriwa sehemu mbali mbali tofauti katika kila account hizi za facebook kama kwa mfano kwingine akidai anafanya Vodacom Mlimani City, kwingine akidai anafanya Tanesco Makao Makuu,PPF na sehemu nyingine kadhaa na amekuwa akiwaahidi kwamba ana watu wenye uwezo wa kuwaunganishia kazi sehemu hizo kwa sharti la wanaotaka kazi kujikusanya na kufikia idadi ya watu watano na wakilipa kiasi cha shilingi 50,000 kila mmoja basi watapata nafasi za kazi hizo.

  Wakati mwingine amekuwa akiwa wadanganya baadhi ya watu kuwa yupo mkoani kikazi au akihudhuria semina na kwamba mdogo wake anashida ya dharura ya pesa kama shilingi 25,000 au 30,000 na kuomba marafiki wamtumie na kuwaahidi atawarudishia mara atakapokua free, amekuwa akitoa namba mbali mbali za simu mojawapo zikiwa hizi 0785412653 na 0688081032. Wale walioshtuka amekuwa akiwatukana matusi makubwa ya nguoni bila uoga.

  Natoa tahadhari kwa watu wote kujihadhari na kufanya urafiki na watu msio wajua, kuzingatia umakini haswa katika mambo ya pesa, pia kujua watu wa namna hii ni wengi sana online haswa kwenye social media. Nashauri uki suspect mtu wa design hii basi wasiliana na polisi na ikibidi kumtengenezea mtego wa kumnasa.

  Vijana tunatakiwa tuchape kazi kwa nguvu na sio kutafuta njia za mikato. Hakuna hadithi yeyote niliyowahi kuisikia ya aliyefanikiwa katika maisha kwa njia ya mkato. Mwana fundi ni kusoma kwa bidii ili elimu yako ikupatie ajira.

  Mwisho naomba marafiki zangu wooote mnisaidie kurepost message hii kwani naamini itawaokoa wengi (vulnerable) ambao kwa namna moja au nyingine wanaweza kuwa hawajui utapeli huu wa online.

  Picha hiyo hapo juu ni yangu na ndio amekuwa akiitumia kwenye account nyingi za facebook. Mimi ninaamini Mungu na hivyo huyu bwana Siku zake 40 zipo karibu. Napenda pia kwa namna ya kipekee nawashukuru wale wote (zaidi ya 10) waliotumia muda wao kunitafuta na kunipa taarifa hizi muhimu walipomshtukia Tapeli huyu.

  Mwenyezi Mungu awabariki saana.
   

  0 0

  IMG_0207
  CHAI BORA the leading Tea packing company in Tanzania, with over 300 employee operating countrywide distribution from head office based in Dar-es-Salaam, Companies factory is based in Mafinga Irringa region the main Tea growing area, CHAI BORA is happy to pack the Tea growing region to keep the freshness of Taste and aroma. Company Brands are known to public, accepted with ISO quality certification and TBS standards. Company is managed by multi talent team of managers who are well experience in the region and in the Tea business. Company has also been nominated as one of the Super brands in East Africa region.

  In addition to the known Tea brands such Luxury and Supreme blends, company also introduced masala Tea, Tangawizi Tea and AMOR (creamer based instant tea) Last year.

  CHAI BORA is proud to introduce its instant coffee brand with the name of CAFÉ BORA into the market. Company offers café bora in sachets format and Tins of 50gram and 100gram, now available in all the supermarkets in Tanzania. Café Bora come with 100% pure instant coffee produced from the best of Robusta and Arabica coffee.

  In late 2014, company acquired the DABAGA tomato sauce business based in Irringa, company is in the process of revamping and upgrading the infrastructure and arranging the business funding. Dabaga is known to Tanzanian consumers as one of the pioneering Tomato sauce business in Tanzania known for its sweet taste, use of fresh Local tomatoes helping thousands of local farmers in southern regions since early 1994. 
  CHAI BORA is pleased to associate with Dabaga and unleash its full potential and brings products that will exceed the expectations of Tanzanian and international consumers.

  Management Team of Chai Bora is energized, more than excited to service market. We are a Team with Integrity, have passion in what we do and most of all driven by the consumer expectations. We are thankful to the consumer support and trade support. Our promise is to offer consumers with Great Tea and food products in East Africa.

  0 0


  BI GLADNESS MARTIN BRUSH PASIPOTI YAKO NA VITU VYAKO VINGINE AMBAVYO ULIPOTEZA AMA KWA KUDONDOSHA AU KUPORWA POCHI YAKO BASI HATI YAKO HIYO NA VITU VINGINE MBALIMBALI VIMEOKOTWA NA VIPO KATIKA MIKONO SALAMA.

  YEYOTE ANAE MFAHAMU MHUSIKA AME TAARIFA AFIKE OFISI YA MTENDAJI KATA-TABATA MSIMBAZI SOKONI, ATAKABIDHIWA. 

  KWA MAELEZO ZAIDI PIGA 0713624583 

  0 0
  0 0

  Familia ya Marehemu Robert Mwang'onda wa Mabibo jijini Dar es Salaam wanapenda kutangaza kupotelewa na ndugu yao Nsajigwa Kennedy Mwang'onda ambaye aliondoka nyumbani Mabibo CCM - Karibu na Chuo Cha Usafirishaji toka tarehe 26-2-2015. Anamatatizo la kupoteleza Kumbukumbu.
  Atakayemuona awafahamishe kwa simu namba 0715 919 168 Frank Mwang'onda, 0682 822 111/ 0754 631 888.
  Au atoe taarifa kituo chochote cha Polisi kwa URP/RB/2331/2015.

  0 0

  *Nakala zaidi ya 650,000 kusambazwa kwenye taasisi
  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema hadi kufikia Februari 26, mwaka huu, Serikali imekwishasambaza jumla ya nakala 1,341,300 za Katiba Inayopendekezwa Kwenye mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.


  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam, jana jioni (Jumatano, Machi 11, 2015) Waziri Mkuu alisema
  Zanzibar imepatiwa nakala 200,000 na kuongeza kuwa nia ya Serikali ya
  kuchapisha nakala milioni mbili iko palepale.


  Hata hivyo, Waziri Mkuu alibainisha kwamba nakala 658,700 zilizobakia
  zitagawanywa Kwenye wizara zote za Tanzania Bara na Zanzibar,
  Mahakama, Bunge, Baraza la Wawakilishi, taasisi za Serikali, Tume
  zote, taasisi za dini, asasi za kiraia, vyombo vya sheria, vyuo vya
  elimu ya juu, vyama vya siasa na na taasisi zinazojitegemea ili
  kuongeza wigo wa usambazaji kwa wananchi wengi zaidi.


  “Lazima nikiri kwamba kuzisambaza na kuzifikisha kwa walengwa ni jambo
  moja na kuhakikisha kwamba zinasomwa ni jambo jingine. Wito wangu kwa
  Watanzania wote ni kuhakikisha wanasoma na kuielewa Katiba
  Inayopendekezwa ili wanapokuja kupiga kura waelewe ni nini wanafanya,”
  alisema.


  “Niwasihi sana Watanzania wenzangu, wasikubali kurubuniwa juu ya
  kilichoandikwa Kwenye Katiba Inayopendekezwa, na tena mtu asikubali
  kuombwa kuomba auze nakala yake. Tusikubali watu warubiniwe kirahisi.
  Kila mmoja ahakikishe anaisoma na kuielewa, na wenye mitandao na blogs
  watumie fursa hii kuusambazia umma nakala za Katiba hii ili watu wengi
  zaidi waweze kuisoma,” alifafanua.


  IMETOLEWA NA
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S.  L. P. 3021,
  11410 - DAR ES SALAAM
  ALHAMISI, MACHI 12, 2015.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kahama,Mh. Benson Mpesya akisalimiana na Muwakilishi wa kampuni ya Airtel mkoa wa Shinyanga,Ezekiel Nungwi wakati Kampuni hiyo ilipofika kuwaona wahanga wa mafuriko na kuwapelekea Baadhi ya Vitu mbali mbali.kampuni hiyo ya Airtel imetoa,sabuni ,mabati ,maharange ,mchele ,mafuta kwa Wahanga hao.
  Mkuu wa Wilaya ya Kahama,Mh. Benson Mpesya akiwapongeza wafanyakazi wa Kampuni ya Simu ya Aitel kwa moyo wao wa kuwasaidia waathilika wa mafuriko katika kijiji cha mwakata ambapo Wilayani Kahama yaliyotokea hivi karibuni.Airtel imetoa msaada wa vitu mbali mbali kama vile sabuni ,mabati ,maharange ,mchele ,mafuta.
  Sehemu za Nyumba zilizoathiliwa na Mafuriko hayo.

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetembelea wahanga wa mfuriko ya mvua katika wilaya ya kahama mkoani shinyanga kwa kuwapatia msaada wa mahitaji muhimu yanayoitajika kwa sasa. Zaidi ya watu 35 walifariki na kuwaacha mamia wakiwa hawana makazi ya kukaa kufatia mvua kubwa iliyonyesha mwanzoni mwa mwezi machi mwaka huu

  Akionge wakati wa makabithiano ya msaada huu, Meneja mauzo wa Airtel Shinyanga Bwana Ezekiel Nungwi alisema” Tunaungana kwa pamoja katika maafa haya na kutoa pole kwa familia zilizopoteza marafiki na wanafamilia kutokana na mafuriko haya.

  Tunatambua pia mafuriko haya yamewaacha wakazi wengi bila makazi, huku mazao yao kuharibiwa na mifugo yao kufa hivyo tunaungana kwa pamoja kutoa msaada kwa namna tutakayoweza . Leo kwa niaba ya Ofisi yetu ya kanda ya Shinyanga tunatoa msaada wa mabati, mablanketi, magodoro pamoja na chakula vyenye thamani ya shilingi milioni 3 na kuwaomba watanzania kuungana nasi kuwasaidia ndugu zetu wa kahama ili kuepuka milipuko ya magonjwa isitokee na kuwawezesha kurudi kufanya shughuli zao za kawaida mapema iwezekanavyo.

  Sambamba na mchango huu, tunapenda kuzindua namba maalumu itakayowawezesha watanzania kuchangia. Tunachukua fulsa hii kuwaomba wateja wetu kuchangia kwa kutuma ujumbe wenye neno MAAFA kwenda namba 15626 , ujumbe huu utalipiwa shiling 256 na pesa hiyo itaingia kwenye mfuko wa kuchangia wahanga wa mafuriko mkoani Shinyanga,

  Akiongea kwa niaba ya wakazi wa Kahama helen Benjamin Alisema” Tunawashukuru sana Airtel kwa msaada huu ulikuja wakati tunauhitaji zaidi, Tunawashukuru kwa kuanzisha namba itakayowapa fulsa watanzania kuchangia, napenda kuwaomba watanzania kushiriki kwa kuchagia na kwa makampuni mengine kujitolea na kutusaidia katika hali ngumu ambayo imetuweka kwenye hatari kupata milipuko ya magojwa na zaidi tumekosa makazi na shughuli zetu za kiuchumi zimeteketea. Tunawashukuru waliojitolea mpaka sasa na tunaomba muendelea na moyo huo wa kujitolea.  0 0

  Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Profesa Juma Athumani Kapuya akizungumza na watendaji wa Wakala wa Majengo nchini (TBA) kuhusu utekelezaji wa ujenzi wa nyumba za Serikali, wakati walipotembelea ofisi za Wakala jana jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli.
  Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akieleza jambo kwa Kamati ya Bunge ya Miundombinu (hawapo pichani) kuhusuiana na mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa miradi mbalimbali na hatua zilizochukuliwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Elius Mwakalinga akiongozana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Prof. Juma Kapuya, wakati Kamati hiyo ilipotembelea nyumba za watumishi wa Serikali eneo la Ada Estate jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Push Mobile Media, Freddie Manento akifafanua jambo kuhusiana na huduma ya ‘Online Bulk Messaging’ inavyofanya kazi. Huduma hiyo itamwezesha mtumiaji kutuma ujumbe mmoja kwa watu wengi na katika muda muafaka.
  Mkuu wa Mauzo na Masoko wa kampuni ya Push Mobile Media Limited, Ezekiel Mukundi (Kulia) akielezea umuhimu wa huduma ya “online bulk Messaging’ kwa sekta mbalimbali. Kushoto ni Daniel Buchafwe ambaye ni Mkuu wa Idara ya Ufundi.
  Mkuu wa Idara ya Ufundi wa Kampuni ya Push Mobile Media Daniel Buchafwe akielezea jinsi ya huduma ya “online bulk messaging” inavyofanyakazi. Kulia ni Mkuu wa Mauzo na Masoko wa kampuni ya Push Mobile Media Limited, Ezekiel Mukundi.

  Kampuni inayoongoza kwa huduma ya teknolojia ya mawasiliano, Push Mobile Media imezindua huduma ya ujumbe kwa njia ya mtandao wa internet ijulikanyo kwa jina la “Bulk Messaging” kwa lengo la kumwenzesha mtumiaji kufikisha ujumbe mmoja kwa watu wengi na katika muda muafaka.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Push Mobile Media, Freddie Manento alisema kuwa huduma hiyo itamwezesha mtumiaji kufikisha ujumbe muhimu kwa gharama nafuu ikiwa katika sekta mbalimbali na kwa mtu binafsi.

  Manento alisema kuwa lengo kubwa ya kuanzisha huduma hiyo ni kuwawezesha wafanyabiashara na sekta nyingine kufanya mawasiliano ya haraka zaidi na kujitangaza.

  “Kama ni mfanyabiashara, utaweza kujitangaza pia kwani wateja watapata taarifa muhimu utakazo wapa kwa muda muafaka na wao kuutumia katika maendeleo ya biashara zao,” alisema Manento. “Ili kupata huduma hiyo, unatakiwa kujiunga kupitia mtandao wetu, www.pushgw.com na kufungua akaunti yako,” alisema Manento.

  Alisema kuwa makampuni au taasisi yanaweza kutumia huduma hii kuwapa taarifa wafanyakazi, wateja wao kuhusiana na biashara na taarifa nyingine. “Kwa watu binafsi, unaweza kutumia huduma hii kutoa taarifa za shughuli mbalimbali ikiwa pamoja na harusi na hata kwa waandishi wa habari wanaweza kutumia taarifa hii kwa lengo la kuwasiliana na wahariri wao kwa kile wanachokifanya katika sekta hiyo,” alisema.

  Mkuu wa Idara ya Mauzo na Masoko wa Push Mobile Media Limited Ezekiel Mukundi alisema kuwa huduma hiyo ni rahisi kwani mtumiaji anaweza kutuma ujumbe kwa kiasi cha sh 16 kwa kutegemea na ukubwa wa ‘bando’ analotaka.

  Alisema kuwa kwa upande wa sekta ya afya, huduma hii inawezwa kutumiwa na madaktari kuwakumbusha wagonjwa kuhusiana na siku ya kupata matibabu. “Unachotakiwa kufanya ni kujiunga na huduma hii kwa njia ya mtandao na kuweka namba za simu ya mkononi kwa watu wanaotakiwa kupata taarifa na kutuma, watapata kwa haraka zaidi na kwa muda unaofaa,” alisema Mukundi.


  0 0

  *Una sehemu 14 ikiwemo ya Mahakama ya Kadhi
  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali itawasilisha Bungeni Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wenye sehemu 14 likiwemo suala la Mahakama ya Kadhi.

  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam, jana jioni (Jumatano, Machi 11, 2015) Waziri Mkuu alisema
  Serikali inakusudia kuwasilisha muswada huo kwenye mkutano ujao wa
  Bunge unaotarajiwa kuanza Jumanne ijayo, (Machi 17).

  Hata hivyo, Waziri Mkuu amewasihi Watanzania waondoe hofu iliyoenezwa
  na tetesi kwamba muswada huo una lengo la kuiingiza mahakama hiyo
  kwenye Katiba Inayopendekezwa na kuwataka wazipuuze tetesi hizo.

  “Hakuna ukweli wowote kwenye jambo hilo kwa sababu Bunge la Katiba
  lilikwishavunjwa na Bunge lijalo halina mamlaka ya kufanya hivyo. Hili
  ni Bunge la sasa haliwezi kubadili maamuzi ya awali… Jambo hili halina
  ujanjaujanja au njama zozote za kuliingiza Kwenye Katiba
  Inayopendekezwa,” alisema.

  “Hizo ni hofu za kweli zilizosambaa na inategemea jinsi mtu
  alivyoelewa suala zima. Kikubwa ni kutambua kwamba Mahakama ya Kadhi
  zimekuwa zinafanya kazi hapa nchini tangu mwaka 2012 lakini kwa
  kuendeshwa na wao wenyewe na siyo Serikali,” alisema.

  Alisema kinachoombwa kwenye marekebisho hayo ya sheria ni kutambuliwa
  kwa maamuzi yanatolewa na Mahakama ya Kadhi pindi yanapofikishwa
  kwenye vyombo vya umma au taasisi za Serikali. “Sehemu ya tano ya
  muswada huo ndiyo inaongelea Mahakama ya Kadhi. Na mapendekezo yao
  yanaomba maamuzi yanayotolewa kuhusu ndoa, mirathi au talaka
  yanapokuja kwenye taasisi nyingine yaheshimiwe,” alifafanua Waziri
  Mkuu.

  Akitoa mfano, Waziri Mkuu alisema: “Kuna mama mmoja alipewa talaka na
  katika maamuzi ya talaka ile, alipaswa kupewa nyumba. Alipokwenda kwa
  Kamishna wa Ardhi ili abadilishe jina kutoka majina ya awali na kuwa
  la huyo mama akaulizwa haya maamuzi yametolewa wapi, sisi
  hatuyatambui… hili lilileta usumbufu mkubwa kwa wahusika.”

  Akifafanua zaidi, Waziri Mkuu alisema kwa mara ya kwanza, suala la
  Mahakama ya Kadhi liliibuliwa mwaka 1998 na Bw. Augustine Lyatonga
  Mrema na Bw. Yusuph Ramia (marehemu) ambao walitaka Bunge lijadili
  hoja yao ya kutaka Serikali ianzishe mahakama hiyo.

  “Bunge liliunda Kamati iliyoongozwa na Bw. Arcado Ntagazwa na baada ya
  mjadala mrefu halikufikia tamati. Serikali ikalifuatilia lakini pia
  haikufikia mwisho. Mwaka 2005 likaingizwa kwenye Ilani ya Chama cha
  Mapinduzi na Chama kikaitaka Serikali ifuatilie kuona tatizo ni nini.”

  “Kwenye mkutano wa Bunge la Bajeti, tarehe 30 Juni 2009, Waziri wa
  Katiba na Sheria ndiye alikuja na hiyo hoja na kuahidi kuifuatilia
  Reinstatement Act ya mwaka 1964 sura ya 375 na kuona Serikali itafanya
  nini katika suala hilo.”

  “Wakati huo ndiyo nilikuwa nimeteuliwa Uwaziri Mkuu kwa hiyo nikaanza
  nalo kwa kuunda timu ya viongozi wa dini ili tulijadili kwa kina suala
  hili kwani kama Serikali kuna masuala ambayo inaamini ni lazima
  iendelee kuyasimamia na kubwa likiwa ni amani na utulivu wa nchi
  yetu,” alisema.

  Alisema katika vikao hivyo walikubaliana kwamba kuendelea kudai suala
  hilo liingizwe kwenye Katiba haikuwa sahihi kwa sababu ni suala la
  imani zaidi na kwa msingi huohuo, walikubaliana kwamba zianzishwe na
  wao wenyewe na kisha wazipangie majukumu ni nini zitafanya.

  “Tulikubaliana kwamba mahakama hizo zisiguse masuala ya jinai bali
  zihusu masuala ya binafsi tu ambayo ni ndoa, talaka, mirathi, malezi
  ya watoto na wakfu. Tulisema jambo hili liwe ni la hiari na lisiwe la
  lazima,” alisema.

  “Msingi wa mjadala ulikuwa mahakama hizi zisiwe kama Mahakama ya Ardhi au Mahakama ya Biashara kwamba mishahara na ofisi zao vigharimiwe na Serikali, hapana… kwa hiyo fikra kwamba Serikali ilikuwa inakataa kuzianzisha hazikuwa sahihi. Ndiyo maana Waislamu walikubali
  kuziansisha kwa hiari yao wenyewe na kwa gharama zao wenyewe,”
  alisema.

  “Nimeongea na Kadhi Mkuu hivi majuzi akaniambia kwamba hadi sasa
  mahakama hizo zimekwishaamua kesi zisizopungua 2,000 na zisizozidi
  3,000.”

  Akielezea juhudi za kukutana na wadau wa pande zote mbili, Waziri Mkuu
  alisema Februari 3, mwaka huu alikutana na Kamati ya Amani ya Mkoa wa
  Dar es Salaam yenye wajumbe 25 ambao ni Waislamu na wajumbe 25 ni
  Wakristo lakini katika kikao hicho walihudhuria wajumbe 55.

  “Wao walijadiliana peke yao, kisha wakakutanisha pamoja na mimi
  nikapewa majumuisho ya mkutano huo. Lakini wakashauri kwamba uitishwe mkutano mkubwa zaidi wenye wadau kutoka nchini nzima ili nao wajadili suala hili. Ndipo Machi 3, mwaka huu nikakutana na Kamati ya Maadili na Haki za Binadamu iliyokuwa na wajumbe 55 wa taasisi tofauti za
  Kiislamu na wajumbe 34 wa Madhehebu ya Dini ya Kikristo.”

  “Mkutano ulikuwa mkali na ubishani mwingi wengine wakidhani kwamba
  wameitwa kushiriki kikao hicho ili kubariki suala la Makahama ya Kadhi
  liingizwe kwenye Katiba inayopendekezwa lakini hatimaye, tulielewana
  na kufikia muafaka juu ya marekebisho yanayotarajiwa,” alisema.

  IMETOLEWA NA
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S.  L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM
  ALHAMISI, MACHI 12, 2015.

  0 0

  1
  Baadhi ya watalaam kutoka Kampuni ya Elektro Merl ya nchini Austria ambao walileta na kufunga makontena ya umeme wa jua pamoja na mfumo wa usambazaji umeme kwa vijiji 10 vilivyo mbali na gridi ya taifa, pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, wakikagua moja ya makontena ya umeme wa jua katika Kijiji cha Lobilo, wilaya ya Kongwa, mkoani Dodoma hivi karibuni.
  2
  Makontena ya umeme wa jua yaliyopo katika Vijiji vya Lobilo na Silale, Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma. Makontena haya ni sehemu ya Mradi unaotekelezwa na Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, ambapo upo katika hatua ya majaribio na unalenga kuvipatia umeme vijiji vilivyo mbali na mfumo wa gridi ya Taifa.
  3
  56
  Baadhi ya nyumba za wananchi katika Vijiji vya Lobilo na Silale, wilayani Kongwa, mkoa wa Dodoma, zilizounganishiwa huduma ya umeme wa jua kupitia makontena maalum.

  …………………………………
   Na Veronica Simba – Dodoma
  Jumla ya Vijiji 10 katika Wilaya za Kongwa, Mlele na Uyui vimeunganishiwa umeme kupitia Mradi wa makontena ya kuzalisha umeme kutokana na jua.Mradi huo unatekelezwa na Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, ambapo upo katika hatua ya majaribio na unalenga kuvipatia umeme vijiji vilivyo mbali na mfumo wa gridi ya Taifa.

  Wizara ya Nishati na Madini wiki hii, ilisaini makubaliano ya kukamilika kwa awamu ya kwanza ya Mradi na Kampuni ya Elektro-Merl ya nchini Austria ambayo ndiyo ilileta na kufunga makontena 14 ya umeme wa jua pamoja na mfumo wa usambazaji umeme kwa nyumba zilizoko katika vijiji husika.

  Akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano hayo, Mwakilishi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Styden Rwebangira alisema wananchi waliounganishiwa umeme huo wa jua, watapata huduma hiyo bure kwa kipindi cha miaka miwili ya mwanzo ambayo ni ya matazamio.

  Alisema kuwa, baada ya miaka miwili, kuanzia tarehe waliyosaini makubaliano, wananchi wa vijiji husika wataanza kuchangia fedha kidogo kwa ajili ya ununuzi wa vifaa mbalimbali kama betri na paneli vinavyotumika katika mradi huo, ambavyo vina ukomo wa kutumika.

  “Vifaa hivi vina gharama kubwa sana, hivyo inabidi kuwa na utaratibu wa kukusanya fedha za kutosha ili kuweza kununua vifaa vingine pindi vilivyopo vinapofikia ukomo wake wa kutumika. Hivyo kila mwananchi anayetumia huduma hii inabidi achangie gharama,” alisema Mhandisi Rwebangira.

  Aidha, aliongeza kuwa, ili kuhakikisha mradi unatoa matokeo yaliyotarajiwa, inabidi uendeshwe na mtu au kampuni yenye utaalamu wa masuala ya umeme, mitambo ya umeme jua pamoja na uzoefu na ufahamu wa kutosha kuhusu mitambo ya aina hiyo.

  “Hivyo, kila baada ya miaka miwili, ukiacha kipindi cha majaribio ambapo mradi utakuwa chini ya Wizara, atachaguliwa mtaalamu au kampuni kupitia njia ya ushindani ambaye atalipwa kwa utaratibu utakaokubaliwa katika mkataba,” alisema Rwebangira.

  Kwa upande wake, Ofisa wa Wizara aliyefika kushuhudia utiaji saini makubaliano ya kukamilika kwa awamu ya kwanza ya mradi, Paul Kiwele alisema Wizara ilifanya tathmini ya kuchagua vijiji kwa ajili ya majaribio ya mradi huo ambapo vigezo mbalimbali vilitumika.Kiwele alivitaja vigezo hivyo kuwa ni pamoja na Kijiji husika kuwa mbali na gridi ya Taifa, kutokuwa katika mpango wa kufikiwa na miradi ya umeme ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) hivi karibuni.

  Alitaja vigezo vingine kuwa ni nyumba za Kijiji husika kuwa karibu pamoja na uwepo wa matumizi ya kiwango cha umeme utakaozalishwa.“Aidha, kwa kuwa mradi huu ni wa majaribio, ililengwa kupata mikoa mitatu tofauti ili uzoefu utakaopatikana utumike katika uendelezaji teknolojia hii katika maeneo mengine ya nchi,” alisema.

  Naye, Mtaalam kutoka Kampuni ya Elektro Merl, Mhandisi Hannes Merl akizungumzia mkataba uliosainiwa na Wizara pamoja na Kampuni yake, Januari mwaka jana kuhusu utekelezaji wa mradi husika, alisema mbali na kufunga makontena 14 ya umeme wa jua pamoja na mfumo wa usambazaji umeme, mkataba pia ulihusisha ufungaji wa waya, taa, swichi na soketi moja kwa kila nyumba iliyofikiwa.

  Mhandisi Merl alisema kila kontena lina uwezo wa kuzalisha kWp 13.75 ambapo kila nyumba ya makazi na huduma za biashara zimetengewa W 250 na taasisi za kijamii zimetengewa W 500.

  Aliongeza kuwa, wananchi wanaweza kuunganisha mashine ndogo ndogo za kusaga, kuchomelea, kuranda na kuchana mbao pamoja na nyinginezo kutoka katika makontena hayo hivyo kunufaika na shughuli za kiuchumi.

  Pia, Mhandisi Merl alisema mradi umetoa jokofu kwa kila zahanati na vituo vya afya vilivyopo katika vijiji vinavyonufaika na mradi huu. Aidha, alisema kuwa mradi umefunga taa za mitaani kwa kila kijiji kitakachonufaika na mradi husika.

  Kwa upande wao, baadhi ya wananchi katika vijiji vilivyonufaika na mradi huo wa makontena ya umeme wa jua, waliishukuru na kuipongeza Serikali kwa wazo zuri la kuwapelekea wananchi hao umeme wa jua ili nao waweze kunufaika kwa namna mbalimbali kutokana na uwepo wa nishati hiyo muhimu.

  “Ninaishukuru sana Wizara ya Nishati na Madini kuona matatizo yetu na kusikia kilio chetu. Imekuwa kama ndoto. Umeme huu umeniwezesha kuendesha biashara ya saluni kwa njia ya kisasa kabisa. Situmii tena Mkasi kunyoa wateja wangu kama hapo awali. Sasa ninatumia mashine za kunyolea na ninapata wateja wengi, hivyo kuboresha kipato changu na maisha yangu kwa ujumla,” alisema Lazaro Kutamika, mkazi wa Kijiji cha Lobilo, Wilaya ya Kongwa, mkoani Dodoma.

  Wizara ya Nishati na Madini imekuwa ikitumia mbinu mbalimbali katika jitihada za kuwafikishia wananchi huduma ya umeme. Kwa kupitia mradi huo wa makontena ya kuzalisha umeme kutokana na jua, Serikali inafanya majaribio ya kuvipatia umeme vijiji vilivyo mbali na mfumo wa gridi ya Taifa kwa kutumia teknolojia husika.

  Vijiji vilivyonufaika na mradi huo kwa awamu ya kwanza ni pamoja na Lobilo, Leganga, Ngutoto na Silale vya mkoa wa Dodoma. Vingine ni Tura, Loya na Lutende vilivyoko mkoa wa Tabora. Aidha, kwa mkoa wa Katavi, vijiji vilivyonufaika ni Nsenkwa, Mapili na Ilunde.

  0 0

   2
  Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC),Mhe. Zitto Kabwe akiongoza kikao cha kamati hiyo jijini Dar es Salaam wakati wa uwasilishi wa hesabu za Shirika la Umeme la Tanzania (Tanesco) lilipowasilisha ,kulia ni Mbunge wa Tabora Mjini Ismail Aden Rage.
  4
  Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco, Dk. Mighanda Manyihi akijitambulisha kwa wajumbe kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) katika kikao cha kuwasilisha hesabu za shirika hilo kilichofanyika jijini Dar es Salaam,kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Mhandisi. Felchesmi Mramba.
  5
  Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Mhandisi. Felchesmi Mramba, akijitambulisha kwa wajumbe kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) katika kikao cha kuwasilisha hesabu za shirika hilo kilichofanyika jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco, Dk. Mighanda Manyihi.
  89
  Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kutoka Sudani Kusini wakifuatilia utendaji kazi wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kwa upande wa Tanzania, katika kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco)liliwasilisha ripoti ya hesabu zake. ( Picha na Lorietha Laurence-Maelezo)
  1
  Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Mhandisi. Felchesmi Mramba, akiwasilisha ripoti ya hesabu za shirika hilo kwa wajumbe kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) katika kikao cha kilichofanyika jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco, Dk. Mighanda Manyihi.

  0 0

  unnamed

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (Wasita kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma muda mfupi baada ya Rais kuwaapisha ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.kutoka kjushoto ni Bibi Salome Mollel(Kamishna),Bibi Evelyne Itanisa(Kamishna),Bw. Mgeni Mwalimu Ally(Kamishna),Mwenyekiti wa Tume Dkt.Stephen James Bwana, Bwana George Yambesi(Kamishna),Bwana Yahya Fadhili Mbila (Kamishna) na Bibi Adieu Nyondo (Kamishna).(picha na Freddy Maro)

  0 0

  jkm1 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na kuwafariji waathirika wa Mvua ya Mawe,iliyonyesha hivi karibuni katika Kijiji cha Mwakata,Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga,leo Machi 12,2015.jkm2  
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na kuwafariji waathirika wa Mvua ya Mawe,iliyonyesha hivi karibuni katika Kijiji cha Mwakata,Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga,leo Machi 12,2015.jkm3 
  Maelfu ya Wakazi wa Kahama wakimsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipokuwa akiwahutubia mara baada ya kutembelea na kujionea athari ya Mvua ya Mawe kwa wananchi wa Kijiji cha Mwakata,Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga,leo Machi 12,2015.

  0 0


  It is two years today since the sudden loss of our beloved Ibrahim Werrema John, who passed away on March 13, 2013 in Dar es salaam.

  Your wife Agatha Ibrahim John, your parents Mr & Mrs John Keraryo, brothers, sisters, nephews and nieces, inlaws and friends can’t forget your fond memories of kindness, friendship and amazing sense of humor. You were a wonderful leader on others and inspirational to every one of us.

  With still remember that sad final moment when you left us with disbelief and tearful eyes. We have leant to remember you with smiles not tears as we believe we will see each other once again; When God call us we hope to be right by your side and reunite. “Whosoever believeth in Christ shall never perish, but have eternal life”.(John 3:16)

  As we remember you in this day, we promise to continue all the good things that you had already set for us to accomplish. In our hearts you will always stay.

  Your life was a blessing, your memory a treasure.
  You are loved beyond words and missed beyond measure.
  We hope to be re-united forever in eternity. AMEN

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara jioni ya leo katika uwanja wa sabasaba, wilayani Kondoa, wakati wa ziara ya siku tisa iliyomalizika leo mkoani Dodoma ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

  Katika ziara yake hiyo aliyoambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ilikuwa ya mafanikio makubwa, kwani msafara wake umetembelelea Wilaya 7 na majimbo 9 ya uchaguzi kwa kuzunguka jumla ya Km, 2289.

  Akizungumza katika mkutano wa kuhitimisha ziara hiyo mjini Kondoa, Nape alisema kuwa katika mkoa huo tayari wamefanya mikutano 91, ambapo 82 ya hadhara na 9 ya ndani. Pia wamekagua jumla ya miradi 73 ikiwemo 62 ya maendeleo na 11 ya chama,Nape akaongeza kuwa katika ziara hiyo imefanikiwa kuongeza wanachama wapya wapatao 8245

  Kesho Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Nape Nnauye wanaanza ziara ya kikazi katika Mkoa wa Arusha, ambapo wataanzia Jimbo la Monduli linaloongozwa na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ambaye ni mbunge wa jimbo hilo.
   Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Zabein Mhita akijiandaa kupiga magoti ikiwa ni ishara ya kumuomba Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kusaidia kutatua tatizo la maji katika Mji wa Kondoa
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nauye akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa sabasaba,jioni ya leo wilayani Kondoa.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kinyasi, Kata ya Kwadelo, ambapo amemshauri Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi pamoja na wakuu wa mikoa minne ya Dodoma, Manyara, Morogoro na Tanga kukka pamoja kupata suluhisho la migogoro inayoendelea ya Wakulima na Wafugaji pamoja na askari wa Wanyamapori kuwashambulia wananchi na hata kufikia kuwaua kwa risasi ambazo maganda yake walimuonesha Komredi Kinana katika mkutano huo. 
  Ndugu Kinana akihutubia katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kondoa.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akivalishwa mgolole ikiwa ni heshima kubwa ya wazee wa kijiji cha Changaa,wilaya ya Kondoa
  Mkuu mpya wa Wilaya ya Kondoa, Shaban Kisu akijitambulisha wakati wa mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Changaa, Kondoa leo. Kisu ambaye alikuwa mtangazaji wa TBC ameteuliwa hivi karibuni na Rais kushika wadhifa huo.
  Mkuu mpya wa Mkoa wa Dodoma Mh.Chiku Galawa akijitambulisha wakati wa mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Changaa, Kondoa leo. Mh.Galawa alikuwa mkuu wa mkoa wa Tanga.
   Mbunge wa Jimbo la Kondoa Zabein Mhita akielezea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wakati wa mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Changaa.
  Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Kinyasi, Kata ya Kwadelo, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipowahutubia,Kinana amemshauri Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi pamoja na wakuu wa mikoa minne ya Dodoma, Manyara, Morogoro na Tanga kukaa pamoja kupata suluhisho la migogoro inayoendelea ya Wakulima na Wafugaji pamoja na askari wa Wanyamapori kuwashambulia wananchi na hata kufikia kuwaua kwa risasi ambazo maganda yake walimuonesha Komredi Kinana katika mkutano huo.
  Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Kinyasi, Kata ya Kwadelo, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipowahutubia,
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akionyesha maganda ya risasi yaliyotumiwa na askari Nyama Pori na kuwajeruhi wananchi
  Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Kinyasi, Kata ya Kwadelo, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipowahutubia,
  Wananchi wa Kata ya Kwadelo wakinyoonsha mikono juu kukikubali Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuliko vyama vingine vya siasa.
  Baadhi ya Wazee wa kijiji cha Kwadero wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana haonekani pichani akishiri kuweka jiwe la msingi kwa ofisi ya CCM wilayani Kondoa.
  Moja ya Jengo la Kituo cha Kilimo ambalo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana pia alikagua.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya Mhe. Lediana Mg'ong'o

  Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu akitoa taarifa kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya inayoshughulikia masuala ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya walipotembelea Makao Makuu ya PSPF, jijini Dar es salaam.Kushoto ni viongozi wa Kamati hiyo Mhe. Diana Chilolo, Makamu Mwenyekiti na Lediana Mg’ong’o, Mwenyekiti wa kamati hiyo.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya Mhe. Lediana Mg'ong'o akisisitiza jambo wakati akizungumza na viongozi na watendaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF wakati kamati anayoiongoza ilipotembelea makao makuu ya mfuko huo leo jijini Dar es salaam.Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSPF, Bw. George Yambesi na Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu.

  Wajumbe wa Kamati ya ya Bunge ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa mfuko wa Pensheni wa PSPF mara baada ya kuhitimisha ziara yao makao makuu ya mfuko huo jijini Dar es salaam.

  0 0

  ka1Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (wapili kushoto) akimkabidhi kadi ya pikipiki Mwenyekiti wa Makatibu Kata wa CCM Wilaya ya Nachingwea, Ally Napepa. Waziri Chikawe alikabidhi pikipiki 35 kwa makatibu kata wilayani humo kwa ajili kazi ya uendeshaji wa shughuli za chama ikiwemo kuwahamasisha wananchi katika kata zao kujiandisha ili kuipigia kura ya ndiyo Katiba iliyopendekezwa na Bunge, pamoja na kujiandaa na uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu. Makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi za CCM wilayani humo. Kulia ni Katibu wa CCM wilaya hiyo, Mussa Liliyo. Picha na Felix Mwagara.
  ka2Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kulia) akiwasisitiza Makatibu Kata wa CCM Wilaya ya Nachingwea, kuzitumia kwa uangalifu pikipiki 35 alizowakabidhi kwa ajili ya kazi za uendeshaji wa shughuli za chama ikiwemo kuwahamasisha wananchi katika kata zao kujiandisha ili kuipigia kura ya ndiyo Katiba iliyopendekwa na Bunge, pamoja na kujiandaa na uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu. Makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi za CCM wilayani humo. Picha zote na Felix Mwagara.

  0 0

  Na Abdulla Ali na Mwanaisha Moh’d Maelezo-Zanzibar.
         

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Haji Omar Kheri amesema Serikali itaendelea kutoa elimu madereva  wa daladala ili waweze kufuata sheria za barabarani na kuepusha ajali zisizo za lazima.


  Hayo ameyaeeleza katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Wilaya ya Magharibi Unguja wakati akijibu swali la mwakilishi wa Jimbo la Wawi Mhe. Saleh Nassor Juma.


  Amesema Serikali imeamua kutoa elimu hiyo kutokana na baadhi ya madereva wa daladala kuwa wakaidi wa kufuata na kutii sheria, jambo linalopelekea kuwepo kwa misongamano ya gari isiyo ya lazima katika vituo vya daladala, ambapo hurejesha nyuma harakati za abiria wakati wa safari zao.


  Aidha Waziri huyo ameliomba Jeshi la Polisi kusimamia sheria za  barabarani kikamilifu ili kuepusha ajali za mara kwa mara na zisizo za lazima.


  Wakati huo huo nae Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii, na Michezo Mhe. Bihindi Hamad Khamis amesema Serikali ina mpango wa kujenga viwanja vya kisasa vya mpira wa miguu na mikono kwa kila Mkoa wa Zanzibar.


  Amesema kwa sasa Serikali imeshaanza mchakato wa kujenga viwanja vya   mikoa ya Kaskazini Pemba na Kaskazini Unguja ambapo kwa upande wa Kaskazini Unguja kitajengwa katika kijiji cha Nungwi na kwa upande wa Kaskazini Pemba kitajengwa katika kijiji cha  Kinyasini.


  Amefahamisha kuwa lengo la kujenga viwanja hivyo ni kukuza Sekta ya Michezo na hadi sasa Baraza la Michezo Zanzibar limeshasajili rasmi vyama 33 vya michezo kwa ajili ya kuunga mkono hatua hizo za kukuza sekta za michezo nchini.


  Vile vile amempongeza Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mhe. Mohamedraza kwa kuwa mstari wa mbele katika kukuza Sekta ya Michezo Nchini kwa kujenga viwanja 2 vya mpira wa miguu vyenye Taa  katka Jimbo lake na kuwataka viongozi wengine  wa Serikali na Sekta Binafsi kuiga mfano huo.             

  IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO-ZANZIBAR


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri Mkuu wa Misri, Ebrahim Mehlep, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Sharm El- Sheikh, kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa kuhusu maendeleo na Uchumi wa nchini Misri.
  Picha zote na OMR
  2
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na mwenyeji wake, Waziri Mkuu wa Misri, Ebrahim Mehlep, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Sharm El- Sheikh, jana kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa kuhusu maendeleo na Uchumi wa nchini Misri

older | 1 | .... | 483 | 484 | (Page 485) | 486 | 487 | .... | 1897 | newer