Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 482 | 483 | (Page 484) | 485 | 486 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mwanasheria mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu (pichano) mapema leo hii ametangaza kuvuliwa uanachama kwa mbunge wa Jimbo la Kigoma Kasikani,Zitto Kabwe baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam kutupilia mbali pingamizi la mbunge huyo la kuzuia asijadiliwe.

  "Kwa mujibu wa katiba ya chama cha CHADEMA, mwanachama yoyote anapofungua kesi mahakamani dhidi ya chama chake, endapo atashindwa katika kesi hiyo atakuwa amejiondoa uanachama wake, kwahiyo natangaza rasmi rasmi Zitto Kabwe sio mwanachama tena wa Chadema.
  Kwa upande wake Zitto Kabwe amesema hawakuwa na wito wa mahakamani leo na Jaji wa kesi kahamishiwa Tabora na hawana taarifa ya Jaji Mpya, pia kaongeza kuwa Mwanasheria anafuatilia na atatoa statement.

  Licha ya kutupilia mbali kesi ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, Mahakama kuu imemtaka kulipa gharama zote za kesi toka ilivyoanza.

  Mwaka jana Zitto Kabwe aliweka pingamizi mahakamni kuzuia kikao cha Kamati Kuu kumjadili na hoja yake ilikuwa ni kupinga kuitisha kamati kuu kabla shauri lake kusikilizwa na Baraza Kuu.

  CHANZO: EATV.COM

  0 0


  ka1
  Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum Jimbo la  Singida, Martha Mlata (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya  Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Dkt. Miganda Manyahi (kulia), jijini Arusha kabla  ya kuanza kwa ziara kwenye miradi ya  umeme. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini  inafanya  ziara katika miradi ya umeme iliyopo katika mikoa  ya Arusha na Kilimanjaro ili  kujionea hatua  ya utekelezwaji wake pamoja na kuzungumza na watendaji.
  ka2
  Mwenyekiti wa  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini  Richard Ndassa (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha,  Daudi Felix Ntibenda (kulia) mara baada ya Kamati  hiyo kuwasili ofisini  kwake kwa ajili ya kupokea taarifa ya mkoa kabla ya kuanza kwa ziara kwenye miradi ya umeme.
  ka3
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha,  Daudi Felix Ntibenda ( wa nne kutoka kushoto waliosimama mbele), Mwenyekiti wa  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini  Richard Ndassa ( wa tano kutoka kushoto waliosimama mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kudumu  ya Bunge ya Nishati na Madini na wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini mara baada ya kumalizika  kwa kikao.
  ka4
  Meneja Mradi wa  Kusambaza  Umeme unaojulikana kwa jina la  Electricity  V unaofadhiliwa na  Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Mhandisi  Florence Gwang’ombe (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini  Richard Ndassa (kulia) mara baada ya kamati hiyo kuwasili kwenye eneo la mradi huo ili kujionea maendeleo ya utekelezwaji wake.
  ka5
  Mtaalam kutoka Kampuni ya Sweco International AB,  Pal Aberg (kushoto) akiielezea Kamati ya Kudumu ya  Bunge ya Nishati na Madini  hatua iliyofikiwa ya  ujenzi wa kituo cha kupooza na kusambaza umeme cha Njiro kilichopo nje kidogo ya jiji la Arusha.
  ka6
  Kamati ya Kudumu ya  Bunge ya Nishati na Madini  ikiendelea na ziara katika eneo la kituo cha kupooza na kusambaza umeme kilichopo Njiro nje kidogo ya jiji la Arusha.

  ka7 
  Mtaalam kutoka Kampuni ya Sweco International AB,  Pal Aberg (kulia) akitoa maelezo mbele ya Kamati ya Kudumu ya  Bunge ya Nishati na Madini  kwenye eneo la kituo cha kupooza na kusambaza umeme cha Njiro kilichopo nje kidogo ya jiji la Arusha.
  ……………………………………………………………………………

  Ni baada ya kukamilika kwa mradi wa umeme wa bilioni 72.5Wateja wapya 30,000 kuunganishwa
  Na Greyson Mwase, ArushaMeneja Mradi wa Kusambaza Umeme unaojulikana kwa jina la Electricity V unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Mhandisi Florence Gwang’ombe amesema kuwa tatizo la kukatika katika kwa umeme katika mkoa wa Arusha litakwisha mapema Juni mara baada ya kukamilika kwa kituo cha kupooza na kusambaza umeme kilichopo katika eneo la Njiro, nje kidogo ya jiji la Arusha. Mhandisi Gwang’ombe aliyasema hayo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyofanya ziara katika kituo hicho ili kujionea maendeleo yake pamoja na kuishauri serikali jinsi ya usimamizi wake.

  Alisema mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho mbali na kuboresha upatikanaji wa nishati ya umeme katika jiji la Arusha, wateja wapya wapatao 30,000 wanategemewa kuunganishiwa umeme kutoka katika kituo hicho.
   Akielezea mradi huo kwa ujumla Mhandisi Gwang’ombe alisema kuwa mradi huo unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa mkopo wa kiasi cha shilingi za kitanzania 72,588, 506,400 unahusisha ujenzi wa njia za umeme wenye urefu wa kilomita 480 za msongo wa kilovoti 33 na ufungaji wa transfoma 102 za kusambaza umeme zenye ukubwa wa 33/0.4 kV.

  Alisema pia mradi huu unahusisha ujenzi na ukarabati wa vituo vya kupoozea umeme vya Ilala, Sokoine katika mkoa wa Dar es Salaam na upanuzi wa kituo cha kupoozea umeme cha Njiro.

  Alisisitiza kuwa mradi unatekelezwa na Mkandarasi National Contracting Company ambaye alishinda zabuni ya ujenzi na ukarabati wa vituo vya kupoozea umeme katika mikoa ya Dar es Salaam na Arusha na mkandarasi Eltel Networks TE AB ambaye alishinda zabuni ya ujenzi na ukarabati wa mifumo ya kusambazia umeme katika mikoa ya Shinyanga na Mwanza.Akielezea hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa kituo cha kupoozea umeme cha Njiro, Mhandisi Gwang’ombe alisema kazi zinazoendelea katika kituo hicho ni pamoja na ufungaji wa transfoma mbili na ufungaji wa mitambo ya kisasa kwa ajili ya kuendesha na kulinda mifumo ya umeme.

  Aliongeza kuwa uagizaji na utengenezaji wa vifaa umekamilika kwa asilimia 85, kazi za ujenzi zimekamilika kwa asilimia 76 pamoja na kumalizika kwa kufunga na kuunganisha vifaa na mifumo ya umeme.

  Alisisitiza kuwa mradi huu unategemewa kuongeza ukuaji wa uchumi katika mkoa wa Arusha pamoja na mikoa mingine kama Shinyanga na Mwanza kwani utachochea ukuaji wa viwanda vidogo vidogo na biashara katika maeneo husika pamoja na kuongeza fursa za ajilra kwa wananchi.

  Aliendelea kusema kuwa mradi huo utaboresha huduma za jamii kwa wananchi kutokana na upatikanaji wa umeme mashuleni, mahospitalini na kwenye maeneo mengine ya jamii husika na hivyo kupunguza umasikini kwa wananchi jambo ambalo linaendana na malengo ya siasa ya nchi.

  Akizungumzia lengo la mradi, Mhandisi Gwang’ombe alisema kuwa lengo la mradi ni kuongeza uwezo wa kusambaza umeme wenye kiwango kinachotakiwa na usiokatikakatika na kulisaidia Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) kuweza kuwafikia na kuwapatia umeme wenye uhakika wateja wengi zaidi ambao bado hawajapatiwa huduma ya umeme.

  Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), Mhandisi Felchesmi Mramba aliiambia Kamati ya Bunge kuwa ongezeko la wateja wa kawaida na viwanda lilisababisha ongezeko la kasi la matumizi kufikia Megawati 70 hali iliyopelekea shirika kuboresha na kujenga vituo vya kupoozea na kusambazia umeme.

  Mhandisi Mramba alisema, kabla ya ujenzi wa kituo hicho, hali ya umeme katika jiji la Arusha ilikuwa ni mbaya hali iliyopelekea ujenzi wa kituo hicho na kusisitiza kuwa Shirika limeamua kufanya mapinduzi katika sekta ya umeme kwa kuhakikisha linashirikiana na wawekezaji mbalimbali na wataalamu wake katika ujenzi wa vituo vya kuzalisha na kusambaza umeme ili kuzalisha nishati ya umeme ya uhakika.

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kijiji cha Misisi kata ya Misisi,wilayani Bahi mapema leo,mkoani Dodoma akiwa ziarani ndani ya jimbo la Bahi.

  Ndugu Kinana amezungumza na wananchi hao waliokuwa wamebeba mabango na kuzuia msafara wake,kutokana na matatizo yaliyokuwapo katika kijiji hicho na kukosa ufumbuzi kwa muda mrefu.Wananchi hao walikuwa na lalamiko lao moja kubwa lililohusu shule yao ya msingi ya Msisi,ambayo madarasa yake mawili yaliezuliwa paa (kama yaonekanavyo pichani) na mengine kubomoka kabisa kufuatia mvua kubwa ilionyesha na kusababisha madhara hayo.

  Shule hiyo ya msingi Msisi ilipatwa na dhahma hiyo mnamo mwaka 2011,na mpaka leo haikuwahi kufanyiwa ukarabati wa aina yoyote huku walimu na wanafunzi wakipigwa na jua wakati wa masomo.Ndugu Kinana baada ya kusikiliza lalamiko hilo kutoka kwa wanakijiji hao,alianzisha harambee ya papo kwa papo iliyohusu viongozi wa CCM mkoa na Wilaya waliokuwa kwenye msafara huo na kuichangia shule hiyo na kufanikiwa kupata fedha na vifaa vya ujenzi ambavyo vitapelekea kuanza upya kwa ujenzi wa madara hayo,Aidha Wananchi wa kijiji hicho walimshukuru Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana kwa harambee alioifanya na kupelekea kupatikana kwa misaada hiyo.

  Ndugu Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wapo kwenye ziara ya siku tisa mkoani Dodoma ya kukagua,kuhimiza na kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010 pamoja na kusikiliza matatizo ya wananchi na kuyatafutia ufumbuzi.
   Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Msisi akiwa amebeba bango lake kichwani.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akisoma moja ya bango lililokuwa limebebwa na mmoja wa wananchi wa kijiji cha Msisi,Wilaya ya Bahi lililohusu shule ya msingi ya kijiji hicho kukosa madarasa ya kusomea wanafunzi,kufuatia mvua mkubwa kuezua mapaa.
    Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mh Chiku Galawa na Mbunge wa Jimbo la Bahi,Mh Omari Badwel wakishiriki uchimbaji wa mitaro na kufukia bomba za maji,katika kijiji cha Nguji kata ya Mundemu wilaya ya Bahi mkoani Dodoma.Mradi huo wa maji unatarajiwa kuhudumia zaidi ya watu elfu tatu,aidha mradi huo uliogharimu kiasi cha fedha zaidi ya Milioni mia saba unatarajiwa kukamilika Aprili 15,2015.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipokelewa katika kijiji cha Mundemu wilaya ya Bahi mkoani Dodoma 
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wananchi wa Bahi mara baada ya kumaliza kuzungumza na Halmashauri kuu ya Wilaya ya Bahi,ambapo pia Wananchi waliruhusiwa kuuliza maswa na kupatiwa majibu papo kwa papo.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikagua chanzo cha maji (kisima) chenye ujazo wa lita 16 kwa saa,kinachotumia umeme wa jua
   Pichani kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki kupalilia majani katika shamba la mizabibu la Lubala Succoss,katika kata ya Ilindi,wilaya ya Bahi

   Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndgu Kinana alipokuwa akizungumza nao jioni ya leo katika kijiji cha kangogo kata ya Babayu,amapo pia alishiriki ujenzi wa nyumba ya waalimu.
   Baaddhi ya Wanahabari wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,uliofanyika katika kijiji cha Chonde,wilaya ya ya Bahi mkoa wa Dodoma.


  Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Chonde wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipowahutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara,wilayani Bahi mkoa wa Dodoma.
   Wanachi wa kijii cha Chonde wakishangilia wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokabidhiwa Mkuki na kuvalishwa mgolole ikiwa ni ishara ya kuwa mmoja wa machifu wa kabila la Wagogo
    Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiendesha trekta ikiwa ni ishara ya kuzindua mradi wa matrekta katika kijiji cha Chonde,Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma jioni ya leo.
    Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiendesha trekta,wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipozindua mradi huo wa matrekta katika kijiji cha Chonde,Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma jioni ya leo.
    Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Chonde wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipowahutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara,wilayani Bahi mkoa wa Dodoma.

  0 0

  WATEJA wa taasisi ya Kifedha ya Bayport inayojihusisha na mambo ya mikopo wanaweza kujishindia jumla ya Sh Milioni moja, endapo wataamua kukopa kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz, uliozinduliwa rasmi jana, jijini Dar es Salaam.
  Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, pichani, akisisitiza jambo katika moja ya matukio ya kikazi ya taasisi hiyo nchini Tanzania.

  Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport, Ngula Cheyo, alisema kwamba kuanzishwa kwa huduma hiyo mpya na ya haraka ni sehemu ya kuwapatia wateja wao na Watanzania kwa ujumla huduma bora na za kiwango cha juu.
  Alisema uzinduzi wao wa huduma ya kukopa kwa mtandao (online), utawawezesha kwa kiasi kikubwa wateja wao kushinda Sh Milioni Moja, baada ya kuchezeshwa kwa droo ya kumtafuta mshindi.

  “Sasa mtu anaweza kukopa kwa njia rahisi na kwa haraka zaidi endapo atakopa kwa njia ya internet, huku akiweza kujishindia Sh Milioni kutoka Bayport Financial Services.“Naamini sasa wateja wetu wataendelea kufurahia huduma nzuri kutoka kwetu kwa ajili ya kurahisisha maisha, ukizingatia kuwa mikopo ya Bayport haina dhamana wala amana,” alisema.

  Naye Msimamizi wa Michezo ya kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania, Mrisho Millao, alisema kwamba mfumo wa ukopaji kwa njia ya mtandao ya Bayport ni rahisi na nzuri, hivyo kila mtu anaweza kukopa na kujishindia zawadi hiyo ya Sh Milioni moja.

  “Kila mtu anaweza kukopa na kushinda kutokana na mfumo uliokuwapo kuwa rahisi, maana mteja anaweza kutumia njia mbalimbali zenye mtandao kama vile kompyuta na simu za mikononi ambapo baada ya kutuma maombi, yatapokewa kwa haraka na wahudumu wao,’ alisema Millao.

  Bayport ni taasisi ya kifedha inayojihusisha na mambo ya mikopo ambapo imefanikiwa kufungua ofisi katika mikoa na wilaya mbalimbali za Tanzania ili kuwafikishia karibu huduma zao.

  0 0

  th1 
  Mmoja wa wakunga wa jadi Bi. Namboto Sheha Kombo akielezea jinsi wanavyofanya kazi zao za ukunga katika mkutano uliofanyika Hospitali ya Kivunge Mkoa wa kaskazini “A” Unguja.
  Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahamoud Thabit Kombo akizungumza na wakunga wa jadi, na kuwataka washirikiane na watalaam wa Afya katika kazi zao ili kupunguza vifo vya Akinamama na watoto. th3 
  Msaidizi daktari dhamana Hospitali ya Muembe ladu Ruzuna A.M. Shamte akifahamisha kitu katika mkutano wa wakunga wa jadi na watalam wa afya huko Kivunge Mkoa wa kaskazini “A” Unguja. th4 
  Baadhi ya Wakunga wa Jadi na watalam wa Afya waliofika katika mkutano wa kukuza mashirikiano huko Kivunge Mkoa wa kaskazini “A” Unguja wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahamoud Thabit Kombo (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao. th6 
  Dkt. Dhamana Hospitali ya Kivunge Khamis Hamad Ali akitoa nasaha zake katika mkutano wa Wakunga wa Jadi na watalam wa Afya wa kukuza mashirikiano katika kufanya kazi zao. Picha na Makame Mshenga- Maelezo Zanzibar.

  …………………………………………………………………………………….
  Na Abdulla Ali Maelezo-Zanzibar                              
  Dawa za Kienyeji wanazopatiwa kina mama wajawazito kutoka kwa  Wakunga wa Jadi wakati wa kujifungua husababisha matatizo ya kiafya kwa watoto wanaotarajiwa kuzaliwa pamoja na akina mama hao.

  Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahamoud Thabit Kombo wakati akizungumza na Wakunga wa Jadi wa Vijiji vya Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja katika ukumbi wa mikutano wa Hospitali kuu ya Mkoa wa Kaskazini Unguja iliyopo katika kijiji cha Kivunge mkoani hapo.

  Amesema kuwa dawa hizo hua zinahatarisha zaidi maisha ya kina mama wajawazito na watoto wanaotarajiwa kuzaliwa hususan kwa akina mama wenye viashiria hatari wakati wa ujauzito ikiwemo maradhi ya Presha na Sukari ambayo yanaweza kusababisha kupoteza uhai wao kwa haraka zaidi.
  Naibu Waziri huyo amesema ipo haja kwa Wakunga wa Jadi kuwafikisha kina mama wajawazito katika Vituo vya Afya pindi wanapobaini kuwa kina mama hao wana matatizo ya kiafya au mtoto kuleta matatizo wakati wa kujifungua na kuacha kung’ang’ania kuwazalishia nyumbani ili kuokoa maisha ya mtoto na mama mja mzito.

  Kwa upande wake Daktari Dhamana wa Hospitali ya Kivunge Nd. Khamis Hamad Ali amesema ipo haja kwa Wakunga wa Jadi kushirikiana na Wizara ya Afya Zanzibar ili kufanikisha zoezi la uzalishaji wa kina mama kwa usalama zaidi pamoja na kuwaomba Wakunga hao kwenda nao wagonjwa katika vituo vya afya kwa kupata uangalizi wa kitaalamu zaidi.

  Amesema watoto wengi hupata matatizo ya magonjwa yakiwemo ya Kifafa na Utaahira kutokana na uchungu mkali unaowapata kina mama wakati wa kujifungua hususan kwa wale wanaojifungulia kwa Wakunga wa Jadi kwani wakunga hao huwa hawana vifaa vya kupunguza makali ya uchungu wa kina mama hao ikiwemo sindano maalum wanazochomwa kina mama kwa ajili ya kupunguza uchungu huo.

  Sambamba na hayo Dkt. Khamis amesema inaripotiwa kuwa 5% – 15% ya wanawake wote Duniani huwa wanapata matatizo wakati wa kujifungua pamoja na kuwaomba kina mama kuwa wawazi kuelezea matatizo waliokwisha kuyapata kabla ya siku za kujifungua kufika pindi wanapokwenda katika vituo vya afya ili kurahisisha uzalishaji huo.
  Nae Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Muembe Ladu Zanzibar Dkt. Ruzuna Abdulrahman Moh’d amesema ipo haja kwa Wakunga wa Jadi kupatiwa Taaluma na Elimu ya kisasa ili waendelee kuisaidia Serikali kwa kuwazalisha kina mama wajawazito kwa njia za kisasa na zilizo salama zaidi.

  Ametanabahisha kuwa dawa za kienyeji zinaweza kutumika kwa kina mama waliokwisha kujifungua ikiwa mtoto amezaliwa bila ya matatizo yoyote ya kiafya. Nao Wakunga wa Jadi wa Wilaya Kaskazini “A” Unguja wamesema kuwa akina mama wengi waja wazito huwa wanakimbia kwenda kuzalia Hospitali ili kukimbia manyanyaso wanayoyapata kutoka kwa madaktari hususan kutoka kwa madktari wadogo na hivyo kuwaomba madaktari hao kujirekebisha kitabia ili kuokoa maisha ya kina mama na watoto kwa maendeleo ya Taifa.

  Aidha wamewaomba madaktari kutoka serikalini kuendelea kutoa elimu ya uzazi kwa akina mama na Wakunga wa Jadi pamoja na kuwaasa wananchi wenzao hususan kina mama kwa kuyasikiliza na kuyafanyia kazi yale yanayotolewa na Wataalamu wa Afya kwa lengo la kujiongezea ujuzi katika kazi yao ya uzalishaji wa akina mama.

  0 0

  Mgombee ubunge jimbo la songea mjini kwa tiketi ya chama cha maendeleo (chadema) Frederick Fussi akisisitiza jambo katika mkutano wake na waandishi habari.
  ---------------------------------------

  OFISA  Mshauri  wa masuala ya Uchumi, Biashara na Uongozi Frederick Fussi ambaye pia ni kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ametangaza nia ya kugombea ubunge wa jimbo la Songea Mjini kupitia Chama hicho huku akielezea vipao mbele ambavyo atavitekeleza endapo akipewa ridaha kutoka kwa wananchi.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana mchana kwenye Hotel ya Agopal ya mjini Songea ,Fussi aliesema kuwa ameamua kutangaza nia ya kutaka kugombea jimbo hilo akiwa na lengo la kutaka kurudisha umiliki wa Halmashauri ya manispaa ya songea mikononi mwa wananchi wenyewe kwa kuwashirikisha kwenye miradi mbalimbali ya utekelezaji.
  Mwandishi wa habari wa The guardian Gedeone Mwakaosi akimuuliza swali mgombea ubunge ambaye haonekani pichani.
  --------------------------------------- 

  Alisema kuwa matamanio ya wapiga kura ni kutaka kuitambua Halmashauri yao jinsi inavyoweza kuwasaidia katika shughuli mbalimbali za maendeleo pamoja na huduma za jamii katika kupunguza baadhi ya matatizo yanayowakabili wananchi wa jimbo hilo.

  Kada huyo wa CHADEMA alisema kuwa katika utendaji wake atazingatia mahitaji ya makundi yote ndani ya jamii ikiwemo kufuatilia fedha za miradi mbalimbali ambayo baadhi ya wananchi walidai kuwa imekuwa ikitekelezwa kwa viwango vya chini kwa baadhi ya miradi kushindwa kukamilika kwa wakati.
  Waandishi wa habari pichani pamoja na wanachama wa CHADEMA wakimsikiliza mgombe ubunge ambaye hayupo pichani katika mkutano huo.
  --------------------------------------- 

  Fussi  ambaye amedai kuwa ana elimu ya Shahada ya kwanza katika fani ya Uchumi na uongozi wa siasa ambayo aliipata kwenye chuo kikuu cha Mwalimu Nyerere alisema kuwa  uchunguzi alioufanya kwa zaidi ya miaka miwili amebaini kuwa  kuna baadhi ya mapungufu ya kiutendaji ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea hasa kwa upande wa usimamizi wa miradi.
  Mgombe ubunge jimbo la songea mjini kwa tiketi ya chama cha maendeleo (CHADEMA) Frederick Fussi akiongea jambo katika mkutano wake na waandishi habari pamoja na wanachama wa chama hicho.
  ---------------------------------------
  Alisema kuwa licha ya kuwepo na mapungufu ya kiutendaji  ndani ya manispaa hiyo bado kumekuwepo na tatizo la miundo mbinu ya barabara pamoja na usafi wa mazingira ambao umeonekana kuwa ni kero kubwa kwa wakazi wa manispaa hiyo.

   Alisema kuwa wananchi wakimpa ridhaa ya kuwawakilisha kwenye Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania  atajitahidi kutengeneza fursa za ajira hasa kwa makundi mbalimbali yakiwemo ya  vijana na akina mama kwa kuishawishi serikali itakayokuwepo madarakani kuhakikikisha inaleta wawekezaji wa viwanda na vitu mbalimbali vikiwemo vya utalii kwa kuwa jimbo hilo limebahatika kuwa na sehemu za kumbukumbu ya mashujaa wa vita vya majimaji. 

  0 0

  Tarehe 08/03/2015, Dr. Wilbroad Slaa Katibu Mkuu wa Chadema kupitia kwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Ndugu Mabere Marando alitoa tuhuma kwa Serikali na kuwahusisha baadhi ya viongozi wa juu wa CCM kuwa wanapanga njama za kumdhuru Katibu Mkuu huyo wa Chadema.
   
  Kimsingi tuhuma hizi ni za kipuuzi, lakini uongo huu usipojibiwa unaweza kugeuzwa kuwa ajenda na Chama hiki cha Chadema kwa kukosa ajenda zingine za maana. Hakuna asiyejua kuwa Chadema kwa sasa kinapumulia mashine, hivyo maneno na matendo yao kwa sasa lazima yalenge kujaribu kujinasua na balaa la kufa kwa chama chao.
  Ni vizuri Watanzania wakakumbuka historia ya tuhuma lukuki zilizowahi kutolewa na Katibu Mkuu huyu wa Chadema toka aanze siasa na ambazo zote zilikuja thibitika kuwa ni za uongo. Hapa nitawakumbusha baadhi.

  Akiwa Singida katika kampeni za Urais za mwaka 2010, Dk. Slaa aliwatangazia wananchi mkutanoni kwamba kulikuwa kumekamatwa lori kubwa la mizigo (semi-trela) lililojazwa karatasi za kura za Urais zilizokuwa tayari amepigiwa kabisa mgombea Urais wa CCM, Dk. Jakaya Kikwete.

  Katika kuonyesha kwamba alikuwa na uhakika wa jambo hilo, alisoma hadi namba za lori hilo na tela lake kutoka kwenye karatasi aliyokuwa ameshika mkononi, kisha akasema kuwa lori hilo lilikamatwa katika mji mdogo wa Tunduma, mkoa wa Mbeya wakati likiingia nchini kutoka Lusaka, Zambia.

  Lakini baada ya polisi kuchukua hatua za haraka wakitumia namba za lori na tela lake alizokuwa amezisoma na kulikamata, kisha wakalipekua hadharani huku wananchi wakishuhudia palepale Tunduma, kilichokutwa ndani ya lori ilikuwa shehena ya vipodozi vya kina mama na sabuni za manukato.

  Baada ya siku chache huku akiwa amesahau yote, Dk. Slaa akatangaza tena kuwa mgombea Urais wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alikesha katika hoteli ya Lakairo, Mwanza akiweka mikakati ya kuiba kura siku ya uchaguzi huo wa mwaka 2010 ili ashinde. Siku chache alisema kura zimeingizwa na zimeshapigwa, hapa amesahau anadai ndio kwanza mpango unapangwa.

  Aliwataja watu wengine aliodai walikuwa pamoja na Rais Kikwete kuwa ni aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz na Mkurugenzi wa Hoteli hiyo iliyopo katika jiji la Mwanza, Lameck Airo. Lakini wakati Dk. Slaa akisema uongo huo, Rais Kikwete siku nzima na usiku wake wote alikuwa Mtwara akiendelea na kampeni zake za Urais.


  Hata Rostam Aziz naye kwa siku hiyo pamoja na usiku wake wote alikuwa Igunga akiendelea na kampeni zake za Ubunge, na pia hata Airo naye siku nzima na usiku wote huo alikuwa jimboni kwake Rorya akifanya kampeni zake za kugombea Ubunge. Baada ya kushindwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Dk. Slaa aliwaambia waandishi wa habari kwamba alikuwa na ushahidi wa matokeo ya Urais ya kituo kwa kituo ya nchi nzima yakionyesha kuwa alishinda.

  Akasema, chama chake kingeyasoma hadharani na kuwakabidhi waandishi wa habari ili wananchi waujue ukweli kuwa alidhulumiwa ushindi wake, kazi iliyofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi na haki yake akapewa aliyekuwa mgombea Urais wa CCM, Jakaya Kikwete.
  Lakini kwa vile alikuwa akiwatangazia uongo wananchi, Dk. Slaa hadi leo hajawahi kuyasoma matokeo hayo ya kughushi, badala yake alipowaita tena waandishi wa habari akatangaza kuwa Tanzania isingetawalika mpaka arudishiwe haki yake. Hapo ndipo ghasia zikiwemo za mauaji za Chadema zilipoanza hadi leo.

  Januari, 2011 aliwaambia waandishi wa habari kwamba alikuwa na mkanda unaothibitisha kuwa mauaji ya Januari 5, mwaka huo yaliyofanyika katika jiji la Arusha kutokana na maandamano ya vurugu ya wafuasi wa Chadema yalifanywa kwa makusudi na polisi, na kwamba wafuasi wake hawakufanya fujo wala vurugu zo zote.

  Alisema mkanda huo angeuonyesha mbele ya waandishi wa habari ndani ya siku tatu au mbili baada ya Polisi Makao Makuu, kuonyesha unaothibitisha kwamba wafuasi wa Chadema walifanya vurugu ikiwemo kutaka kuvamia Jengo la Makao Makuu ya Polisi la Mkoa na kupora silaha zilizokuwa humo, wawafungulie wahalifu waliokuwa ndani na kulichoma moto jengo lenyewe. Lakini tokea kipindi hicho hadi sasa ikiwa tayari imeshapita miaka minne, Dk. Slaa siyo tu ameshindwa kuuonyesha mkanda huo “ndani ya siku tatu ama mbili” alizokuwa ameahidi, bali amethibitisha kwamba alichosema kwa Watanzania ulikuwa ni uongo na uzushi.

  Mwaka 2011, Dr. Slaa alikwenda mbali kwa kuzusha kwenye mkutano wa hadhara kuwa aliyekua Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wakati huu Brig. Gen. mstaafu Yohana Balele amefariki dunia. Akajaribu kuwaaminisha wananchi pale kuwa ni kweli, baadae ikagundulika kuwa Mkuu huyo wa Mkoa ni mzima na wala haumwi. Haikujulikana mara moja sababu za Dr. Slaa kumzushia kifo Mkuu huyo wa Mkoa.

  Julai 2012, Dr. Slaa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika walizusha kwamba wanafuatiliwa na baadhi ya Maafisa wa Idara ya Usalama wa Taifa ili wauawe, lakini walipotakiwa kupeleka ushahidi wao katika vyombo vya dola ili kusudi watuhumiwa wachunguzwe na hatimayewakamatwe na kuruhusu Sheria ichukue mkondo wake, wote waligoma na kudai hawapo tayari kushirikiana na Jeshi la Polisi.

  Waliendelea na msimamo huo hata pale Dk. Slaa alipolazimishwa kwenda Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na kuhojiwa, lakini akashindwa kutoa uthibitisho wake mwenyewe wala wa Mnyika kwa sababu walidai suala hilo limezungumzwa katika kikao cha Kamati Kuu ya Chadema.

  Mwaka 2012, Dr. Slaa akiwa ziarani Ifakara wilayani Kilombero mkoa wa Morogoro, alidai kuwa CCM imeingiza silaha kutoka nje ya nchi kontena zima, ili zitumike kuwadhuru viongozi wa Chadema, jambo ambalo hata hivyo hadi leo ameshindwa kulitolea uthibitisho wala kielelezo chochote. Wanaomfahamu vizuri endapo ingekuwa kweli angeita waandishi wa habari, akatoa ushahidi wake na kuwakabidhi ili wautumie kuandika madai hayo, lakini kwa sababu ulikuwa ni uongo ndiyo maana hakutoa karatasi yoyote hadi leo.

  Juzi bila aibu anaibuka na tuhuma zingine za eti kutaka kuuawa. Kupanga kumdhuru Dr. Slaa, ili CCM ipate nini kwa kudhurika kwake? Kwa umri wake, afya yake na kadhalika, kwa nini CCM ipange kumdhuru mzee huyu? Huu ni mwendelezo wa tabia yake ya kuzusha mambo ya uongo kila anapoona anachuja kisiasa. Ni busara kwa umri wake akatumia muda wake mwingi KUMRUDIA MWENYEZI MUNGU. Lakini hata mtu aliyetumika kuufikisha uongo huo kwa umma, naye ana historia ya kuzusha mambo na kusema hata asiyoyaamini.

  Marando aliwahi kuitisha kikao na waandishi wa habari na kudai Katibu wa Itikadi na Uenezi alifaidika na pesa za EPA, alipobanwa na mteja wake aliyekuwa akimtetea mahakamani kwa kesi hiyo hiyo ya EPA, akaruka yale matamshi yake kwa maandishi na kudai ilikuwa ni shinikizo la Chama chake kusoma yale maneno lakini hata yeye hayaamini.

  Lakini ni Marando huyu huyu ambaye akipanda kwenye majukwaa ya siasa anadai swala la EPA ni ufisadi mkubwa sana kwa nchi na akishuka tu jukwaani, anakimbia mahakamani kwenda kuwatetea watuhumiwa hao hao wa EPA aliowaita majukwaani mafisadi wa EPA. Mzee huyu naye ni mnafiki.

  Hebu tujiulize, ni lini Mabere Marando aliacha rasmi kazi yake ya awali ya ukachero mpaka aaminike leo kufanya kazi afanyayo? Nani alimtumia kujaribu kusambaratisha chama cha NCCR-Mageuzi miaka ya mwanzo ya mfumo wa vyama vingi nchini? Hivi ni kweli Marando ni wa kuaminiwa leo?

  Natoa wito kwa Watanzania bila kuingilia utaratibu wa Sheria na vyombo vya Serikali kufuatilia uongo huu mpya, Watanzania nawaomba wampuuze na kupuuza uongo huu. Usitupotezee muda, tuendelee na mambo ya msingi ya kujenga nchi yetu.

  Nimshauri pia babu yangu Dr. Slaa, kwa umri wake, wenzake wakifikisha umri huu wa uzee wanatumia muda wao kumrejea Mwenyezi Mungu badala ya yeye kuendelea kutunga uongo na uzushi kila kukicha. Namwomba mwenyezi Mungu ampe kuiona busara hiyo.

  Imetolewa na:-Nape Moses Nnauye, KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,ITIKADI NA UENEZI

  0 0


   MRATIBU WA KIBIKI CUP HARUNA SALEH AKIWA NA MDAU WA SOKA FRANK KIBIKI

  Mratibu wa KIBIKI CUP Haruna Saleh akiwa na mdau wa soka FRANK KIBIKI na wanahabari
   
  NA MWANDISHI WETU, IRINGA
  LIGI inayoshirikisha  watoto walio chini ya umri wa miaka 16, inaloitwa  Iringa Kibiki Childrens Cup 2015 yenye lengo la kupinga mauaji ya walemavu wa ngozi (Albino) inatarajia kuanza kutimua vumbi jumamosi ikishirikisha timu nane za manispaa ya Iringa.
  Mratibu wa ligi hiyo, Haruna Salehe alisema lengo la mpira huo ni kukuza vipaji vya watoto na kueneza ujumbe wa kupinga ukatili na mauaji yanayofanywa kwa walemavu wa ngozi nchini.
  Alisema ligi hiyo iliyobuniwa na kuendeshwa na mwandishi wa habari wa gazeti la Uhuru, inatarajia kushirikisha timu nane za watoto katika manispaa ya Iringa.
  “Lengo kubwa ni kukuza vipaji na kueneza ujumbe wa kupinga ukatili wa kijinsia hasa kwa wenzetu walemavu wa ngozi ambao wamekuwa wakiuawa kila siku bila huruma jambo ambalo, hatutaki liendelee kwenye jamii yetu,”alisema.Alisema michuano hiyo itakuwa ikifanyika katika uwanja wa mwembetogwa ambao ni wa wazi ili watu wengi wapate nafasi ya kushiriki.
  Kwa upande wake, mdau wa soka na mwanahabari wa gazeti hilo, Frank Kibiki alisema ameamua kubuni ligi hoyo ili kupanda mbegu ya kupenda michezo na kutambua vipaji vya soka tangu utotoni, ili iwe rahisi kuwapata wachezaji bora siku zijzo.
  “Mpira ni ajira na huu hauna dini, kabira wala rangi, watu wote hata watoto wanaweza kushiriki kwenye mpira hivyo tumebuni jambo hili ili kuendelea kukuza vipaji huku tukibeba ujumbe wa kupinga ukatili kwa wenzetu wenye ulemavu wa ngozi,”alisema.
  Kibiki ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa soka kushiriki kwenye michuano hiyo ili kusaidia kuibua vipaji na kulifanya soka la Iringa kuwa endelevu.
  Alisema tayari shirikisho la Soka, manispaa ya Iringa wametoa Baraka za kuanza kwa ligi hilo, ambalo watoto wameshaewa mafunzo ya kuwa waamuzi na washika vibendera hiyo wao wenyewe watajiongoza.
  Kwa upande wao wadau wa soka, manispaa yaa Iringa waliitaka serika kutambua mchango na kuwekeza kwenye soka ili kusaidia kupandisha timu zilizopo na kuendelea kuibu vipaji ikiwemo michuano ya watoto.

  0 0

   DSC_0144

  Kaimu Balozi wa Japan, Bw. Kazuyoshi Matsunaga akisoma risala fupi mbele ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia) wakati wa hafla fupi ya utiaji saini mkataba wa msaada wa shilingi milioni 160 kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali ya Kakuni wilayani Mlele Machi 6, 2015 kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
  *Waziri Mkuu aomba Watanzania wamuunge mkono.

  SERIKALI ya Japan imetoa msaada wa dola za Marekani 90,286 sawa na sh. milioni 160/- kusaidia ujenzi wa shule ya awali kwenye shule ya msingi Kakuni, iliyopo kijiji cha Kibaoni, wilayani Mlele, mkoa wa Katavi.

  Japan imetoa msaada huo ikiwa ni sehemu ya mchango wake katika shule mpya ya msingi Kakuni ambayo Waziri Mkuu Mizengo Pinda alianzisha wazo la kuijenga kama njia ya kumshukuru Mungu na kuwashukuru wananchi waliosaidia kumfikisha hapo alipo. Waziri Mkuu Pinda alisoma darasa la kwanza hadi la nne katika shule ya msingi Kakuni mwaka 1957 hadi 1960.

  Akizungumza kwenye hafla fupi ya utiaji saini mkataba wa msaada huo uliofanyika (Ijumaa, Machi 6, 2015) kwenye ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni na kushuhudiwa na Waziri Mkuu mwenyewe, Kaimu Balozi wa Japan, Bw. Kazuyoshi Matsunaga alisema Serikali yake imeamua kutoa msaada huo kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995 inayosema elimu ni haki ya kila mtoto.

  Alisema sera ya elimu iliongezewa uzito na Mpango wa Kuendeleza Elimu ya Msingi Awamu ya Pili (PEDP II) ambao unasisitiza kwamba kila shule ya msingi ni lazima iwe na shule yake ya awali kama njia thabiti ya kuhimiza upatikanaji wa elimu ya awali hapa nchini.

  “Mojawapo ya changamoto inayoikabili sekta ya elimu hapa Tanzania ni kukosekana kwa mazingira mazuri ya shule katika hatua za mwanzo za makuzi ya watoto wengi. Kwa mfano, kata ya Kibaoni ina shule tatu za msingi ambazo ni Kakuni, Ilalangulu na Milumba lakini hakuna shule ya awali hata moja, jambo ambalo hufanya watoto wote walundikane kwenye darasa mojawapo kwenye shule ya msingi Kakuni,” alisema.

  Alisema anaamini mchango walioutoa utasaidia kuboresha viwango vya elimu ya awali katika kata ya Kibaoni. Mchango huo wa sh. milioni 160/- unatarajiwa kutumika kujenga madarasa mawili ya awali, ofisi ya walimu wa shule hiyo, eneo la michezo, bwalo dogo la chakula na jiko. “Natambua kuwa ujenzi wa shule peke yake hauinui kiwango cha elimu, bali kuongeza uandikishaji wa watoto, kuongeza walimu na kuboresha maslahi yao ni chachu nyingine muhimu katika kuinua kiwango cha elimu,” alisema.
  DSC_0168
  Baadhi ya watendaji ofisi ya Waziri Mkuu waliohudhuria hafla hiyo fupi ya utiaji saini mkataba wa msaada na Ubalozi wa Japan wa shilingi milioni 160 kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali ya Kakuni wilayani Mlele Machi 6, 2015 kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam.
  Utiaji saini huo ulifanywa na Kaimu Balozi huyo pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mlele, Bw. William Mwakalambile. Wengine waliokuwepo ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dk. Ibrahim Msengi na Katibu Tawala wa mkoa huo, Mhandisi Emmanuel Kalobelo.
  Akizungumza katika hafla hiyo fupi, Waziri Mkuu Pinda aliishukuru Serikali ya Japan kwa msaada huo ambao alisema utachangia kwa kiasi kikubwa kuitimiza ndoto yake aliyokuwa nayo ya kuisaidia jamii iliyomsomesha.
  “Wazo la ujenzi wa shule mpya ya msingi Kibaoni lilitokana na ukweli kwamba nilisoma na kumaliza kwenye shule hii ya Kakuni. 

  Nikiwa ni mtumishi wa Serikali, ni Mbunge na sasa hivi ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nilijiuliza hivi shule hii ninaweza kuiacha hivi hivi? Hakuna jambo ambalo naweza kufanya na kuisaidia jamii ya wanakijiji na kata nzima ya kwetu?,” alisema Waziri Mkuu katika mada fupi aliyoiwasilisha jana.
  “Niliwaza pia kufanya ukarabati lakini nikabaini kuwa eneo la shule halitoshi kwani idadi ya wanafunzi waliopo ni kubwa kuliko eneo la shule hiyo. Hivi sasa shule ina wanafunzi wapatao 770. Madarasa yamechakaa na nyumba za walimu pia zimechakaa,” alisema.
  DSC_0148
  Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dkt. Ibrahim Mzengi (wa kwanza kushoto) akiwa na watendaji wa mkoa wa Katavi na wilaya ya Mlele alioambatana nao kwenye hafla hiyo fupi. Katibu Tawala wa Mkoa huo, Mhandisi Kalobelo (wa pili kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Mlele, William Mwakalambile (wa pili kulia) pamoja na Afisa Mipango wa wilaya ya Mlele, Seif Mohamed Makome (kulia).
  Alisema alipeleka maombi kwenye Serikali ya Kijiji cha Kibaoni ambayo ilitoa ekari 65 kutoka eneo lililokuwa ni mashamba ya bega kwa bega na kisha akawasilisha ombi maalum kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda (wakati huo) ambayo hivi sasa ni Mlele ili kuomba ushauri na usimamizi wa jumla katika kuisimamia ndoto hiyo.
  Alisema aliishirikisha Halmashauri kuandaa michoro inayotolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na OWM-TAMISEMI, na kuwataka waandae mapendekezo ya bajeti kwa kuzingatia taratibu za kiuhandisi na ujenzi na makisio ya awali yalikuwa sh. bilioni 1.3/-.
  Alisema alipeleka barua kuomba michango kwa watu binafsi, mashirika ya umma, taasisi, mabenki na balozi mbalimbali ambao hadi sasa wamekwishamchangia sh. milioni 816.6 na dola za Marekani 210,000 na kwamba hadi sasa kwenye akaunti ya ujenzi amebakiza kiasi cha sh. milioni 182 na dola za Marekani 60,189.
  “Katika kuanza zoezi la kukusanya fedha mwaka 2013, Ubalozi wa China ulikuwa wa kwanza kuitikia maombi yetu na ulitoa Dola za Marekani 200,000 ambazo zilikuwa sawa na sh. milioni 320. Pia ubalozi ukamteua mkandarasi wa barabara ya kutoka Nkasi – Kibaoni – Mpanda asaidie katika ujenzi wa shule ili kupunguza gharama,” alisema.
  PG4A5435 (1)
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akishuhudia utiaji saini mkataba wa msaada wa Japan wa shilingi milioni 160 kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali ya Kakuni wilayani Mlele Machi 6, 2015 kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam baina ya Kaimu balozi wa Japan nchini, Kazuyoshi Matsunaga (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Mlele, William Mwakalambile (kulia). Waliosimama nyuma yao kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dkt. Ibrahim Mzengi, Katibu Tawala wa Mkoa huo, Mhandisi Kalobelo na Kulia ni Afisa Mipango wa wilaya ya Mlele, Seif Mohamed Makome.
  Hadi sasa majengo yaliyokamilika ni madarasa 14, jengo la utawala lenye ofisi za walimu na maktaba mbili (wanafunzi na walimu), jengo la TEHAMA la wanafunzi lenye darasa moja, ukumbi mdogo na ofisi ya mwalimu na jengo moja la choo lenye matundu 48. Pia ujenzi wa nyumba sita za walimu uko kwenye hatua ya msingi. Nyumba hizo zinajengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
  Waziri Mkuu aliwaomba Watanzania watakaoguswa na jambo hili wamsaidie kutimiza ndoto yake kwani bado anakabiliwa na kazi ya kuweka umeme, maji, kujenga nyumba nane za walimu, choo kingine chenye matundu 48, bwalo na jiko, karakana nne za ufundi, vitabu na TABLETS za wanafunzi, kituo cha walimu cha mafunzo ya muda mfupi na utunzaji taarifa (Resource Centre), viwanja vya michezo vya kisasa vinavyozingatia michezo yote, mfumo wa uvunaji maji ya mvua, mfumo wa maji safi na maji taka, nyumba mbili za walinzi na uzio wa shule.
  Alitaja vitu vingine ambavyo bado vinahitaji kuchangiwa ni meza za walimu – za ofisini na darasani, viti vya walimu – vya ofisini na darasani, madawati ya shule ya msingi na ya awali, meza na viti vya maktaba zote mbili, meza na viti vya bwalo – shule ya msingi na shule ya awali.
  DSC_0186
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akishuhudia tukio la kubadilishana hati za mkataba wa msaada baina ya Kaimu balozi wa Japan nchini, Kazuyoshi Matsunaga (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Mlele, William Mwakalambile (kulia).
  DSC_0134
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitoa neno la shukrani kwa Serikali ya Japan mara baada ya hafla ya utiaji saini wa mkataba wa msaada huo.
  DSC_0215
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda akifanya 'Power point presentation' ya hatua ya ujenzi wa shule mpya ya msingi Kibaoni aliyoijenga kutokana na michango ya wadau wa maendeleo kama kurudisha fadhila kwa jamii yake iliyomsomesha kijijini kwake.
  DSC_0244
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Balozi wa Japan nchini, Kazuyoshi Matsunaga (kulia kwake) baada ya kushuhudia utiaji saini mkataba wa msaada wa Japan wa shilingi milioni 160 kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali ya Kakuni wilayani Mlele Machi 6, 2015 kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dkt. Ibrahim Mzengi na wapili kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa huo, Mhandisi Kalobelo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mlele, William Mwakalambile.

  0 0

  NITALALA UZEENI BY DJ CHOKAWakati tukiisubiri siku ya Ijumaa ya tarehe 13 March 2015 kuusikiliza Wimbo Mpya kutoka kwa DjChoka Alioubariki jina la "NITALALA UZEENI", Basi Tunakupa nafasi ya Kumsikiliza Dj Choka akiuzungumzia Kiundani wimbo huo ambao anaamini Kuwa Mashabiki wake Watauelewa sana haswa Vijana.
  Akizungumza na DjHaazu wa Mambo Jambo Radio Arusha Kupitia Kipindi cha DUNDO Choka amesema NITALALA UZEENI ni wimbo flani unaoelezea Zaidi jinsi ambavyo Watu wanaHustle kila kukicha na Kula Bata huku wakiamini Hakuna kulala Kwani Kulala kuko Uzeeni.
  Ngoma hiyo imefanywa pale AM Records na amewapa Shavu Vijana Wapya kwenye Game ambao ni Young Mlunya na Big Y Na wawili wengine ambao wanajulikana ni Country Boy na Climax Bibo.
  Hata hivyo Choka amezungumzia pia Ukimya aliokuwa nao kwenye Utoaji wa Zile Project zake kuwa ni Majukumu na kukaa Karibu na Familia huku akihakikisha kuwa anakaa karibu zaidi na Mwanaye ili asije akaitwa Uncle na Mwanae kwa kukaa Mbali naye.
  Kitamu zaidi ni kwamba Kuna Mbali na hiyo Pia Kuna Project Zingine Zinazofuata Soon Kupitia Mikono ya Maproducer tofauti ambao Tayari ameshakaa nao Sawa ambao ni Mesen Selekta, NahReal na Kwakuwa hana Mpango wa Kufanya Kubum Kubaa sana ila lazima afanye Mkono Mmoja wa KubumKuban kutoka Kwa Producer Mkali wa Hip-Hop Toka Arusha DAZ NALEDGE Toka DabMusic
  PATA NAFASI YA KUMSIKILIZA DJ CHOKA AKIZUNGUMZA NA DJHAAZU KWA KU-CLICK LINK HII>>> DJ CHOKA NDANI YA MAMBOJAMBO RADIO NA @DJHAAZU

  0 0

  Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini Mwa Afrika, (MISA) imemtangaza mrembo mwenye vipaji vingi hapa nchini, Jokate Mwegelo, kuwa miongoni mwa wanawake tisa waliofanya mambo makubwa katika jamii kwa ukanda wa nchi za Kusini mwa Afrika ijulikanayo kwa jina la “Misa’s Women to Watch’.

  Kwa mujibu wa taraifa iliyotolewa na MISA wakati wa siku ya wanawake Duniani, Jokate ambaye ni mfanyabiashara, mwanamitindo, mtangazaji, mwanamuziki, mbunifu wa mavazi na muigizaji wa filamu amepata nmafasi hiyo kutokana na juhudi zake katika kuelimisha jamii na hasa afya ya watoto na kuwawezesha wanawake.

  Taarifa hiyo imesema kuwa Jokate ambaye kwa sasa ana miaka 24, ameweza  kuweka msukumo mkubwa katika jamii mbali ya kujihusisha katika masuala ya ujasiliamali kupitia nembo yake ya Kidoti.

  “Ni mfano wa wanawake walioamua kujiajiri pamoja na kuwa na elimu ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam katika masuala ya Siasa, kwa umri wake mdogo, ameweza kujihusisha na masuala ya afya ya mama na watoto na masuala ya elimu,” ilisema taarifa hiyo.

  Akizungumzia hatua hiyo ya kutambulika, Jokate alisema kuwa utambuzi wake kutoka Misa ni faraja kubwa na amepata amasa kubwa ya kuendelea na harakati zake katika elimu, biashara, afya na kuwawezesha watoto wa kike.

  “Nimeamua kuitumikia jamii kutokana na vipaji vyangu, nashukuru kuona taasisi kama Misa inanitambua na kuniweka katika kundi la wanawake tisa waliofanya mambo makubwa katika jamii, hii inaonipa taswira kuwa kile ninachokifanya kinajulikana na ndiyo lengo langu katika jamii,” alisema Jokate.

  Alifafanunua kwa kusema kuwa taarifa hiyo imempa changamoto na kuwa mbunifu zaidi wa nini cha kufanya katika maisha ya kila siku na hasa katika kujikwamua kimaisha yeye binafsi na kwa jamii nzima.

  Mbali ya Jokate, orodha hiyo pia imemtaja Miss Tanzania 2013/14 Happiness Watimanywa kutokana na mkakati wake katika masuala ya jamii, Teresa Chirwa Ndanga (Mwandishi wa habari za uchunguzi Malawi), Josephine Chinele,(Mwandishi, Malawi), Nashilongo Gervasius (Mwandishi, Namibia), Oshosheni Hiveluah (Mtengenezaji filamu,  Namibia), Mary Pais Da Silva (Mwanasheria wa Haki za Binadamu Swaziland),  Noxolo Nkabinde (Mwandishi , Swaziland) na Judith Mulenga mwanaharakati wa haki za watoto nchini Zambia.

  0 0

  Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati akimtangaza mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Uingereza, Ifiyani Karechi atakayeshiriki katika tamasha hilo litakalofanyika Aprili 5 kwenye Uwanja wa Taifa. (Picha na Francis Dande).  


   Alex Msama.

  0 0  1.     Shirika la Under The Same Sun (UTSS) linalaani vikali kitendo cha kinyama cha kukatwa kiganja cha mkono wa kuume cha mtoto mwenye albinism Baraka Cosmas Rusambo (6); aidha, Prisca Shaaban, mama wa mtoto huyo kujeruhiwa vibaya kwa mapanga kichwani kwenye shambulio la kikatili linalohusishwa na imani za kishirikina lililotokea usiku wa Jumamosi Machi 7, 2015 kwenye Kijiji cha Kipeta, Kata ya Kiseta wilaya ya Sumbawanga Vijijini mkoani Rukwa. Waathirika hao kwa sasa wanapata matibabu kwenye Kituo cha Afya cha Kamsamba wilayani Momba mkoani Mbeya.

  2.    Wauaji hao wametokomea kusikojulika na kiganja cha mtoto huyo, huku Jeshi la Polisi likishikilia watu saba wakituhumiwa kuhusika na shambulio hilo. Aidha jeshi hilo limewahamishia mahali salama watoto wengine wawili wenye albinism wa familia hiyo kwa ajili ya usalama wao. 

  3.    Pamoja na hatua zilizochukuliwa na viongozi mbalimbali wa Serikali dhidi ya matukio hayo ya kinyama kama vile Mh. Mizengo Pinda (Mb) – Waziri Mkuu ya kufungia leseni za waganga wa jadi na hatimaye kuruhusiwa siku 30 kabla uchaguzi mkuu wa mwaka 2010; Mh. Mathias Chikawe (Mb) 

  – Waziri wa Mambo ya Ndani la kupiga marufuku wapiga ramli chonganishi; na, hivi juzi Mh. Jakaya Kikwete – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyeapa kutokomeza unyama huo, bado matendo haya ya kinyama yanaendelea kuiandama Tanzania, nchi inayotambulika kuwa kisiwa cha amani na kimbilio la kila aliyevurugikiwa na amani nchini mwao.

  4. Tunadhani ni wakati mzuri sasa wa kuja pamoja Serikali na wadau wote ikijumuisha mashirika ya kutetea haki za binadamu ya nje na ndani ya nchi, mashirika ya kidini, waandishi wa habari, mashirika ya watu wenye ulemavu, wanasiasa, watu binafsi na wengineo ili kutafuta suluhu ya pamoja na ya kudumu kwa maslahi na usalama wa nchi yetu Tanzania.

  5.     Ni wakati muafaka wa kufanyia kazi kauli na ahadi za Mh. Jakaya Kikwete Rais wa Tanzania alizozitoa wakati akifanya mkutano na viongozi wa Chama cha Albino Tanzania (TAS) Machi 5, 2015 Ikulu jijini Dar es Salaam kwamba serikali itafanya kila iwezalo ikiwa ni pamoja na kuunda kamati ya pamoja ya wadau kutafuta njia muafaka ya kukomesha mauaji haya yanayoiaibisha Jamhuri yetu ya Tanzania. Mkutano ulikubaliana pia kufanyiwa mapitio kwa sheria zinazohusu uchawi na waganga wa jadi, vizuri utekelezaji wa kazi hiyo ukaanza mara moja.

  6.    Tunapendekeza pia Waheshimiwa Wabunge wote wa maeneo yaliyoathirika na kadhia hii walau kufanya kikao cha pamoja kujadili namna ya kutokomeza unyama huo na hatimaye, kwa umoja wao, kuliomba Bunge la Jamhuri kujadili kadhia hii na kuielekeza Serikali na vyombo vyake hatua na mbinu stahili za kuchukua. 

  7.     Aidha, kutekelezwa kwa sheria zilizopo bila shuruti ni jambo la msingi sana. Kwa msingi huo, tunashauri waliokutwa na hatia na hatimaye kuhukumiwa na mahakama zetu kwa mujibu wa sheria za Tanzania, basi adhabu zao zitekelezwe bila kigugumizi chochote.

  Imetolewa na Under The Same Sun
  Machi 11, 2015

  Kwa maelezo zaidi wasiliana na:
  Vicky Ntetema, Mkurugenzi Mtendaji UTSS-TZ
  Taasisi Road, Mikocheni B, Kwa Warioba
  P.O. Box 32837, Dar es Salaam, Tanzania
  T:  +25522278024 Fax:  +255222782356
  Mob: +255753177752/ +2557658600136  0 0

   Mwenyekiti wa Unity Women Foundation (UWF), Maryam Ajmy akiwa akikusanya misaada waliyokuwa wakitoa katika hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam kutoa msaada kwa wanawake ikiwa ni kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanyika hivi karibuni.  
  Mwenyekiti wa Unity Women Foundation (UWF), Maryam Ajmy akiwa na wanaumoja wenzake wakiingia hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam kutoa msaada kwa wanawake ikiwa ni kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanyika hivi karibuni.   
  ---
  Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
  Unity Women Foundation (UWF), umetoa msaada kwa wanawake wagonjwa katika hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam.
  Akizungumza na baada ya kutoa msaada katika Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika hivi karibuni, Mwenyekiti wa UWF, Mariam Shamo amesema wanawake wanatakiwa kujitoa kwa wanawake wenzao wenye matatizo kwa siku zote kutokana na kuwepo kwa wanawake wengine hawana msaada wa mtu yeyote.
  Mariam amesema wanawake siku ya wanawake itumike kwa kwa kufariajiana na kuendelea na kuweza kuona kuona mabadiliko na kuweza kutatua changamoto zetu zinazotukabiri.Amesema wanawake wenye uwezo wasaidie na kuwatembelea wanawake wenzao katika wodi mbalimbali na kutoa msaada hata kama ni kidogo lakini kinathamani yake.
  Aidha amesema kama UWF wataendelea kutoa kuwafariji wagonjwa kila muda ili nao waweze kujua wanawake wa nje yao wanatambua matatizo yao.

  0 0

   Kontena la Lori hilo likiwa limewekwa pembeni baada ya kuondolewa kwenye eneo la Ajali.
  Picha na mdau Baraka wa Chibiriti

  Watu zaidi ya 30 wanasadikiwa kupoteza na maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya sana katika ajali mbaya iliyotokea mapema leo asubuhi,maeneo ya Changarawe,Mafinga Mkoani Iringa,iliyohusisha Lori la Mizigo na Basi la abiria la Kampuni ya Majinja lililokuwa likitokea Mkoani Mbeya kuelekea jijini Dar es salaam.


  Ajali hiyo imetokea baada ya Lori hilo la Mizigo lililokuwa likitokea Jijini Dar kuelekea Mbeya kuligonga na kuliangukia basi hilo wakati lililokuwa likikwepa shimo kubwa lililopo katikati ya barabara wakati wakiwa kwenye mwendo walipokuwa wakipishana. 

  Hali ya Uokoaji wa maiti na majeruhi walionasa kwenye ajali hiyo bado ni tete na hasa kutokana na ukosefu wa Gesi ya kukata basi hilo kukosekana eneo lote la Mafinga,Juhudi zinafanyika ili kuweza kuokoa majeruhi pamoja na maiti.

  Globu ya Jamii inaendelea kufuatilia kwa ukaribu tukio hili ambalo ni la kusikitisha sana na ni msiba mkubwa kwa taifa,na tutaendelea kujuzana kupitia hapa hapa.

  Mungu azipokee na kuzilaza mahala pema peponi roho za marehemu wote katika ajali hii na awajaalie kupona kwa haraka majeruhi wote - Amin.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mheshimiwa Amina Masenza kufuatia ajali mbaya ya barabarani iliyotokea tarehe 11 Machi, 2015 Mafinga katika Mkoa wa Iringa katika eneo lijulikanalo kwa jina la Changarawe, ambayo imepoteza uhai wa watu zaidi ya 40 waliokuwa wakisafiri kwa basi hilo na wengine kadhaa kujeruhiwa.


  Ajali hiyo imetokea baada ya basi la Kampuni ya Majinja Express walilokuwa wakisafiria watu hao kutoka Mbeya kwenda Dar es Salaamkugongana na lori lililokuwa likitokea Dar es Salaamkwenda Mbeya, hivyo kusababisha kontena lililokuwa limebebwa na lori hilo kuliangukia basi.


   “Nimeshtushwa, nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana kufuatia taarifa za vifo vya watu zaidi ya 40 huku wengine kadhaa wakijeruhiwa katika ajali hii mbaya ambayo imesababisha simanzi na majonzi makubwa kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu”, amesema Rais Kikwete akiomboleza msiba huu.


  “Huu ni msiba mkubwa, na Taifa kwa ujumla limepata pigo kubwa, hivyo naomba upokee salamu zangu za rambirambi kutoka dhati ya moyo wangu kutokana na ajali hii iliyotokea Mkoani kwako. Naomba, kupitia kwako, rambirambi zangu  na pole nyingi ziwafikie watu wote waliopotelewa ghafla na wapendwa wao.  Namuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema azipokee na kuzilaza Roho za Marehemu wote mahala pema peponi, Amina”, ameongeza kusema Rais Kikwete.


  Katika Salamu zake hizo, Rais Kikwete amewahakikishia wafiwa wote kuwa yuko pamoja nao katika kuomboleza msiba wa ndugu na jamaa zao, lakini amesema, pamoja na machungu yote ya kupotelewa na ndugu na jamaa zao, anawaomba wafiwa wawe na moyo wa uvumilivu na subira wakati huu wanapoomboleza vifo vya wapendwa wao.  

  Aidha, Rais Kikwete amehitimisha rambirambi zake kwa  kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema watu wote waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo wapone haraka, ili waweze kuungana tena na ndugu na jamaa zao.


  Imetolewa na;

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu – Dar es Salaam.  11 Machi, 2015


  0 0
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale amesema hakuna ufisadi wowote wala malipo tata yaliyofanywa na wizara ya ujenzi kwa makandarasi  na wahandisi washauri katika bajeti ya mwaka 2011/2012.

  Eng. Mfugale amesema fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya kasma maalum ya ujenzi wa miradi ya barabara nchini kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 252 kilitumika  kulipa madai ya Makandarasi na Wahandisi washauri.

  Eng. Mfugale amesisitiza kuwa Serikali inajenga barabara kwa kuzingatia vipaumbele vya maendeleeo na hulipa makandarasi na wahandisi washauri ili kuwezesha kazi hizo kufanyika kwa wakati na kwa kuzingatia mikataba.

  Eng. Mfugale ametoa ufafanuzi huo kufuatia baadhi ya vyombo vya habari kunukuliwa kuwa kumekuwa na ubadhirifu ,au matumizi tata katika malipo ya wakandarasi Wizara ya Ujenzi na kusisitiza kuwa suala hilo lilishajadiliwa na kupatiwa ufumbuzi na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), katika kikao chake cha Agosti 22 mwaka 2013.

  Amewataka watumishi  wa TANROADS kote nchini kuendelea na shughuli zao za ujenzi na usimamizi wa  barabara  bila kuvunjika moyo kwani  hakuna ubadhirifu wowote.

  Zaidi ya km 35,000 za barabara hapa nchini  zinasimamiwa na TANROADS kupitia mameneja wake katika mikao 25 nchini kote ambapo takriban KM 11,154 zinajengwa kwa kiwango cha lami katika kipindi  hiki.


  IMETAYARISHWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA UJENZI.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Mohamed Gharib Bilal (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es salaam,Profesa Hudson Nkotagu kuhusu uzalishaji wa Digrii 4 zinazozalishwa chuo kikuu cha Dar es Salaam,wakati wa Mkutano wa Jitihada za Nchi za Afrika za kuzalisha mafuta na Gesi Katika Vyuo vya mafunzo Stad,uliofanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julias Nyerere Jijini Dar es salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Mohamed Gharib Bilal akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Chuo cha Ufundi (VETA) wakati alipotembelea kwenye banda la veta wakati wa Mkutano wa jitihada ya Nchi za Afrika za Kuanzisha Mafunzo ya Mafuta na Gesi katika Vyuo vya Ufundi Stadi,Mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mwelim Nyerere Jijini Dar es Salaam leo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Mohamed Gharib Bilal akifungua Mkutano wa siku mbili kuhusu jitihada za chi za Afrika za kuanzisha Mafunzo ya Mafuta na Gesi katika Vyuo vya Ufundi Stadi, Mkutano huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Julias mwalim Nyerere Jijini Dar es Salaam leo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Mohamed Gharib Bilal akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Mkutano wa siku mbili kuhusu jitihada za chi za Afrika za kuanzisha Mafunzo ya Mafuta na Gesi katika Vyuo vya Ufundi Stadi, Mkutano huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Julias mwalim Nyerere Jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

  Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Shaaban Ali Lila akimwapisha Mhe. Lenatus Ishengoma (kulia) kuwa Naibu Msajili wa Mahakama ya Tanzania leo jijini Dar es salaam. Wanaoshuhudia kiapo hicho ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Othman Chande (kushoto) na Mhe. John Kahyoza, Msajili Mahakama Kuu ya Tanzania.
  Mhe. Elizabeth Mkwizu akisaini hati ya kiapo cha kuwa Naibu Msajili wa Mahakama mbele ya Jaji Kiongozi Mhe. Shaaban Ali Lila baada ya kuapishwa leo leo jijini Dar es salaam.
  Naibu Msajili wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Hussein Shaaban Mushi akipokea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwongozo wa utendaji kazi wa Mahakama kutoka kwa Jaji Kiongozi Mhe. Shaaban Ali Lila mara baada ya kuapishwa kuwa Naibu Msajili wa Mahakama ya Tanzania leo jijini Dar es salaam.


  0 0

   Basi la Majinja Express likiwa limeharibika vibaya baada ya kuangukiwa na kontena katika ajali iliyotokea nje kidogo ya mji wa Mafinga jana eneo la Changalawe barabara kuu ya Iringa Mbeya.
  Msululu wa magari ukiwa unasubiri kuondolewa kwa maiti katika eneo la ajali (Picha zote na Denis Mlowe).

  42 WAPOTEZA MAISHA MUFINDI KWA AJALI


  NA DENIS MLOWE, MUFINDI


  HUZUNI na majonzi yametawala katika mji mdogo wa Mafinga baada ya ajali mbaya ya basi la abiria la Majinja Express lilokuwa likitokea jijini Mbeya kuelekea Dar Es salaam kugongana uso kwa uso na kisha kudondokewa na Kontena na kusababisha watu 42 kufariki dunia katika ajali iliyotokea eneo la Changarawe barabara kuu ya Iringa kwenda Mbeya.


  Ajali hiyo ambayo hatazamiki mara mbili imetokea majira ya 3.30 asubuhi km 5 kutoka mjini Mafinga kwa lori lenye namba T689 APJ likiendeshwa na dereva aliyejulikana kwa jina la Maka Sebastian (26)mali ya CIPEX Company kwa kontena kuangukia basi la Majinja Express lenye namba T438 CDE likiendesha na dereva Baraka Gabriel (37).


  Katika ajali hiyo waliofariki dunia papo hapo walikuwa 37 na watano wamefariki wakiwa hospitali ya wilaya ya Mufindi na inasemekana wengi wao ni wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam waliokuwa wakitokea jijini Mbeya kati ya hao walofariki ni wanaume 32 wanawake 7, watoto 3 na majeruhi 22.


  Mmoja wa abiria wa basi hilo,Musa Mwasege akisimulia chanzo cha ajali hiyo alisema kuwa chanzo ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa  basi alilopanda kwa kuwa katika mwendo kasi licha ya ubovu wa barabara hiyo kuwa na mashimo mengi yanayosababisha ajali.


  “Sehemu iliyotokea ajali kwa kweli ni mbovu hivyo dereva wetu baada ya kupunguza mwendo akawa anazidi kuongeza na kutumbukia katika shimo na kusababisha kugonga uso kwa uso na roli hilo na kisha kontena kutuangukia baada ya hapo sikutambua lolote hadi nilipofika hospitali” alisema.


  Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza akizungumza katika eneo la ajali alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni ubovu uliokithiri wa barabara hiyo na ni tukio la kuhuzunisha sana kwa wa watanzania na kuagiza wakala wa barabara kuanza matengenezo ya barabara hiyo.


  Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi, amekiri kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa chanzo cha ajali ni ubovu wa barabara kutokana kuwa na mashimo mengi.


  “Hapa tusitafute mchawi nani katika hii ajali chanzo kikubwa ni ubovu wa barabara hivyo ni jukumu la mamlaka husika kurekebisha tatizo la barabara.” Alisema.


  Kamanda Mungi aliwataja abiria waliokuwemo katika basi hilo kuwa ni Esta Emanuel Lusekelo, Jerimiah Wakison, Doto Katuga, Diga Solomon, Theresia Kaminyage, Frank Chiwango, Luteni Sanga, Alfred Sanga, Juliana Bukuku, Esta Fide, Paulina Justin.


  Wengine ni Catherine Mwajengi, Zira Kasambala, Rebeka Kasambala, Mbamba Ipyana, Dulile Kambala, Frank Mbaule, Mustapha Ramadhan, Bwana Mussa, Shadrak Msigwa, Mathias Justin, na aliyejulikana kwa jina moja la Elias. 


  Naye mganga mkuu mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Mufindi Boaz Mnenegwa alikiri kupokea maiti 37 na majeruhi 22 zilizotokana na ajali hiyo na kusema kuwa majeruhi watano walifariki mara baada kufikishwa kituoni hapo.

  Alisema kuwa kutokana ufinyu wa nafasi katika chumba cha kulaza maiti hospitalini hapo maiti 32 zilisafirishwa kuelekea katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa na majeruhi waliokuwa mahututi wawili wote wa kiume walipewa rufaa ya kwenda kutibiwa  katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa.

  0 0

   Sehemu ya umati wa Wananchi waliojitokeza katika mkutano huo kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (hayupo pichani),wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi hao na kuwaasa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili kupata nafasi ya kushiriki katika upigaji kura ya maoni ya Katiba inayopendekezwa.

  Mbunge wa Jimbo la Chemba (kondoa kusini),na Naibu Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh Juma Nkamia akizungumza na wananchi wa jimbo lake katika kijiji cha Itolwa Wilayani Chemba,Mh.Nkamia kupitia Wizara yake alikabidhi hundi za fedha zenye thamani ya shilingi Milioni 52 kwa vikundi tisa vya vijana vinavyojishughulisha na  ujasiliamali.Katika mkutano huo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana (pichani shoto) pia aliwahutubia wananchi hao.
  Katibu Mkuu Ndugu Kinana akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mrijo wilayanii Chemba,alipokwenda kukagua mradi wa ujenzi wa soko la Kimataifa,Wiayani Chemba mkoani Dodoma.
  Wananchi wa Kijiji cha Babayu wakimpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwasili katika wilaya ya Chemba tayari kuendelea na ziara yake ya siku tisa mkoani Dodoma
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana pichani shoto akitoka kupanda mti na kukagua wodi ya akina  Mama na  Watoto,itakayokuwa ina uwezo wa kuwahudumia wanakijiji wapatao zaidi ya  elfu moja kilichojengwa katika zahanati ya Kelema,wilaya ya Chemba,Mradi wa ujenzi wa jengo hilo ni ulianza mnamo mwaka 2013 na kutarajiwa kumalizika mnamo mwaka 2015,ambapo zitatumika kiasi cha fedha zaidi ya shilingi milioni 42
  Baadhi ya ya wafuasi wa CCM wakisubiri kumpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana katika kijiji cha Mapango
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mapango,wilaya ya Chemba,ambapo walieleza tatizo lao kubwa linalowakabiri katika kijiji hicho ni ukosefu wa maji,ambapo katibu Mkuu,Kinana aliahidi kuhakikisha kijiji hicho kinapata maji safi na salama kwani tayari utandikaji wa mambomba ya maji ulikwishaanza. 
  Mmoja wa wananchi akiwa amebeba picha ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana katika kijji cha Songolo,walipokuwa wakimpokea.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na wananchi 
  katika kijiji cha Songolo,walipokuwa wakimpokea.

  Katibu Mkuu wa CCM,akiondoka kwenye mkutano mara baada ya kuwasalimia wananchi katika kijiji cha Songolo,kulia kwake ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Mh.Adam Kimbisa

older | 1 | .... | 482 | 483 | (Page 484) | 485 | 486 | .... | 1897 | newer