Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live

The 6th Steering Committee meeting of the East African Community Medicines Regulatory Harmonization (EAC-MRH)


MFUMUKO WA BEI WAONGEZEKA KIDOGO KUTOKA ASILIMIA 4.0 MWEZI JANUARI, 2015 HADI KUFIKIA ASILIMIA 4.2 MWEZI FEBRUARI, 2015.

$
0
0
 Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Epraim Kwesigabo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya kuongezeka kwa Mfumuko wa Bei nchini kwa mwezi Februari, 2015. Kulia kwake ni Kaimu Meneja wa Takwimu za Ajira na Bei wa Ofisi hiyo Bi. Ruth Minja.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa kazini wakati Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Epraim Kwesigabo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu akizungumza nao leo jijini Dar es Salaam kuhusu taarifa ya kuongezeka kwa Mfumuko wa Bei nchini kwa mwezi Februari, 2015. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)
========  ======  =========
MFUMUKO WA BEI WAONGEZEKA KIDOGO KUTOKA ASILIMIA 4.0 MWEZI JANUARI, 2015 HADI KUFIKIA ASILIMIA 4.2 MWEZI FEBRUARI, 2015.
 
Na: Veronica Kazimoto,
Dar es Salaam,
09 Machi, 2015.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Februari, 2015 umeongezeka  kwa asilimia 4.2 kutoka asilimia 4.0  mwezi Januari mwaka 2015.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Epraim Kwesigabo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ambapo amesema kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2015 imeongezeka kidogo ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2015.

“Kuongezeka kwa Mfumuko wa Bei wa mwezi Februari, 2015 kumechangiwa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Februari, 2015 zikilinganishwa na bei za mwezi Februari, 2014, amesema Kwesigabo”.

Bidhaa za vyakula zilizoonyesha kuongezeka mwezi Februari, 2015 zikilinganishwa na bei za mwezi Februari, 2014 ni pamoja na bei za mchele (asilimia 18.5), unga wa mihogo (asilimia 9.3), nyama (asilimia 8.9), samaki (asilimia 12.4) na maharagwe kwa asilimia 7.1.

Kwa upande wa bidhaa zisizo za vyakula zilizoonyesha kuongezeka mwezi Februari, 2015 zikilinganishwa na bei za mwezi Februari, 2014 ni pamoja na bei za mavazi ya wanaume (asilimia 4.7), mavazi ya wanawake (asilimia 3.3), mkaa (asilimia 5.1), mashuka (asilimia 3.1) na gharama za kumuona daktari kwa asilimia 11.2.

Akizungumzia kuhusu Mfumuko wa Bei kwa kipimo cha mwezi Mkurugenzi Kwesigabo amesema kuwa Mfumuko wa Bei wa mwezi Februari, 2015 unaopimwa kwa kipimo cha mwezi umeongezeka kwa asilimia 1.6 ukilinganisha na ongezeko la asilimia 1.0 mwezi Januari, 2015.

Aidha, Kwesigabo amesisitiza kuwa Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi kufikia 154.83 mwezi Februari, 2015 kutoka 152.43 mwezi Januari, 2015 ambapo kuongezeka kwa fahirisi kumechangiwa na kuongezeka kwa bei za bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula.

Kwa upande wa thamani ya shilingi, Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Epraim Kwesigabo amesema uwezo wa Shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia Shilingi 64 na senti 59 mwezi Februari, 2015 kutoka mwezi Septemba, 2010 ikilinganishwa na Shilingi 65 na senti 60 ilivyokuwa mwezi Januari, 2015.

Hata hivyo, Mfumuko wa Bei nchini Tanzania una mwelekeo unaofanana na baadhi ya nchi nyingine za Afrika Mashariki kwa kuwa Mfumuko wa Bei wa mwezi Februari, 2015 nchini Uganda umeongezeka hadi asilimia 1.4 kutoka asilimia 1.3 mwezi Januari, 2015; na nchini Kenya, Mfumuko wa Bei wa Mwezi Februari, 2015 umeongezeka hadi asilimia 5.61 kutoka asilimia 5.53 mwezi Januari, 2015.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA SHIRIKA LA SIMU LA VIETNAM

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Makamu wa Rais wa Shirika la Simu Vitnam (VIETTEL) Hoang Son, wakati Makamu huyo alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Machi 9, 2015 kwa mazungumzo akiwa ameongozana na ujumbe wake.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Makamu wa Rais wa Shirika la Simu Vitnam (VIETTEL) Hoang Son (wa pili kushoto kwake)  na ujumbe wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Viettel Global, Tao Duc Thang, Mshauri wa Viettel Tanzania, Francis Mndolwa na  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Nguyen Thanh Quang, wakati Makamu huyo alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Machi 9, 2015
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Kampuni ya Viettel, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika leo Ofisini kwake Ikulu. Picha na OMR

TFDA takes chairmanship of EAC Medicines Regulatory Harmonisation Programme

$
0
0
The Director General of Tanzania Food and Drugs Authority and Chairperson,  Mr. Hiiti B. Sillo, giving welcoming remarks to the 6th Steering Committee Meeting of the EAC Medicines Regulatory Harmonization (EAC-MRH) Programme at Lemigo Hotel, Kigali, Rwanda on 5thMarch 2015.
 The Deputy Secretary General for Productive and Social Sectors, EAC Secretariat, Honourable Jesca Eriyo, officiating the 6th Steering Committee Meeting of the EAC-MRH Programme at Lemigo Hotel, Kigali, Rwanda on 5th March 2015.
 Participants of the 6th Steering Committee Meeting of the EAC-MRH Programme at Lemigo Hotel, Kigali, Rwanda in a group photo, 5th March, 2015.
 The Heads of EAC Partner States’ National Medicines Regulatory Authorities taking and responding to questions from the media after issuing a Press Statement on domestication and implementation of the EAC harmonised regulatory guidelines, requirements and standards on Medicines Evaluation and Registration, Good Manufacturing Practice and Quality Management System at Lemigo Hotel, Kigali, Rwanda on 6th March 2015.

Rais Dkt. Kikwete afungua Mkutano wa Mwaka wa Wahasibu Wakuu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESSAG)

$
0
0
JK2 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Mkutano wa Mwaka wa Wahasibu Wakuu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika(ESSAG) uliofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere International Conference Centre JNICC jijini Dar es Salaam leo.(picha na Freddy Maro).
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Wahasibu Wakuu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika(ESSAG) uliofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere International Conference Centre JNICC jijini Dar es Salaam leo. Walioketi meza kuu kutoka kulia ni Waziri wa Fedha Mh.Saada Mkuya, Katibu Mkuu wizara ya Fedha Servacius Likwelile, manaibu katibu wakuu hazina Dkt.Hamisi Mwinyimvua na Bi.Dorothy Mwanyika.

KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE JIMBO LA MTERA KWA KIBAJAJ.!

$
0
0
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizindua mradi wa maji uliojengwa kwa msaada wa shirika la Oxyfarm katika kijiji cha Mvumi mission,jimbo la Mtera wilayani Chamwino.Pichani kulia ni Mbunge wa jimbo la Mtera,Livingstone Lusinde a.k.a Kibajaji akishihudia tukio hilo adhimu. Kinana amelishukuru shirika hilo kwa kukamilisha ujenzi wa mradi  wa kisima hicho kwa muda mfupi
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizindua mradi wa maji uliojengwa kwa msaada wa shirika la Oxyfarm katika kijiji cha Mvumi mission,jimbo la Mtera wilayani Chamwino.Pichani kulia ni Mbunge wa jimbo la Mtera,Livingstone Lusinde a.k.a Kibajaji
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wakazi wa kijiji cha Mvumi mission,jimbo la Mtera mapema leo mara baada ya kuzindua mradi wa maji uliojengwa kwa msaada wa shirika la Oxyfarm
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wajumbe wa mkutano mkuu wa Jimbo la Mtera,katika kijiji cha Mvumi Mission ,wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na viongozi wengine wa wilaya na mkoa wa Dodoma wakikagua mradi wa ujenzi wa madarasa shule ya Msingi Suli yaliyogharamiwa na shirika la Neigbourhood kutoka Korea ya Kusini,kwa kiasi cha shilingi bilioni tatu,ujenzi huo pia unahusisha vyumba vya  walimu pamoja zahanati ya kijiji cha Suli. 
 Mbunge wa jimbo la Mtera,Livingstone Lusinde a.k.a Kibajaji akimwagilia maji mti alioupanda katika shule ya sekondari Fufu,ambapo Katibu Mkuu wa  CCM,ndugu Kinana alikagua bweni la wasichana na kupanda miti katika suala zima la kulinda mazingira. 
 Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria mkutanno huo wa hadhara.
Mbunge wa jimbo la Mtera,Livingstone Lusinde a.k.a Kibajaji akiwahutubia wananchi wa Fufu,jimbo la Mtera wilayani Chamwino jioni ya leo.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wananchi wa Fufu,jimbo la Mtera wilayani Chamwino jioni ya leo.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia baadhi ya  wakazi wa kijiji cha Manzase kata ya Fufu,,jimbo la Mtera wiyani Chamwino mkoani Dodoma,leo jioni katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Manzase.
 Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Manzase Kata ya Fufu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia mapema leo jioni katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Manzase.

MZEE YUSSUF NA ISHA MASHAUZI WATHIBITISHA RASMI MTANANGE WA JAHAZI NA MASHAUZI CLASSIC

$
0
0
Hatimaye wakurugenzi wa Mashauzi Classic na Jahazi Modern Taarab, wamefanya mkutano na waandishi wa habari na kuthibitisha kuwepo kwa onyesho la pamoja la makundi hayo yenye nguvu katika muziki wa taarab.

 Onyesho hilo litafanyika mwezi huu Jumapili tarehe 22 ndani ya ukumbi wa Travertine Hotel Magomeni. Mkurugenzi wa Jahazi, Mzee Yussuf na mkurugenzi wa Mashauzi Classic, Isha Ramadhan maarufu kama Isha Mashauzi, wamesema siku hiyo hatumwi mtoto dukani. 

 Wakiongea katika mkutano huo wa waandishi wa habari uliofanyika Jumatatu jioni katika hotel ya Travertine Hotel, wakurugenzi hao ambao wote ni waimbaji nyota, wakasema onyesho hilo si mpambano lakini pia sio la masihara kwani kila bendi imejipanga kuhakikisha inaangusha burudani iliyokwenda shule.
Kutoka kushoto ni  Meneja wa Mashauzi Classic Ismail Rashid, Isha Mashauzi, Mzee Yussuf na Seif Magwaru meneja wa Jahazi Modern Taarab.

WAKUU WA MIKOA YA MBEYA NA RUKWA WAMTEMBELEA MTOTO ALBINO ALIYEKATWA KIGANJA

$
0
0
Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya, Dk. Mpoki Ulisubisya akiwaongozwa Wakuu wa Mikoa ya Mbeya na Rukwa kuelekea Wodini kumjulia hali Mtoto Baraka aliyekatwa kiganja cha mkono wa kulia na watu wasiojulikana kijijini kwao juzi.
Mtoto Baraka aliyekatwa kiganja cha mkono wa kulia na watu wasiojulikana kijijini kwao juzi akiwa amelala kitandani akiendelea kupatiwa matibabu.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stellah Manyanya akiwa anamwangalia kwa jicho la huruma Mtoto Baraka aliyekatwa kiganja cha mkono wa kulia na watu wasiojulikana na kutokomea nacho akiwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.
Wakuu wa Mikoa ya Mbeya na Rukwa wakimjulia hali Mtoto Baraka aliyekatwa kiganja cha mkono wa kulia na watu wasiojulikana kijijini kwao juzi.
Wakuu wa Mikoa ya Mbeya na Rukwa sambamba na viongozi wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya wakiwa wameinamisha nyuso zao huku wakisali kuwaombea watu wenye ulemavu wa ngozi ili wasipate madhara baada ya kumtembelea Mtoto Baraka aliyekatwa kiganja cha mkono wa kulia na watu wasiojulikana kijijini kwao juzi.
Mama mzazi wa mtoto Baraka,Prisca Shabani akiwa na jeraha kichwani baada ya kupigwa na watu waliomkata kiganja mtoto wake, akiwa anawasikiliza wakuu wa mikoa ya Mbeya na Rukwa waliomfika kuwajulia hali katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya wanakopatiwa matibabu.
.Waandishi wa habari wakichukua maelezo kutoka kwa wahanga wa tukio la kukatwa kiganja kwa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (albino).


Na Mbeya yetu

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro aliongozana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhandisi Stella Manyanya walifika Hospitalini baada ya mtoto huyo kufikishwa kwa ajili ya matibabu zaidi.

Mtoto huyo mkazi katika kijiji cha Ikonda kata ya Chitepa wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa alihamishiwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya baada ya kukatwa kiganja chake akitokea kituo cha Afya cha Kamsamba wilayani Momba mkoani hapa.

Akizungumza kwa masikitiko makubwa mama wa mtoto huyo, Prisca Shaban(28) alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa saba usiku alipokuwa anarudi ndani akitokea nje kujisaidia alivamiwa na mtu ambaye hakumfahamu na kisha akamsukumia ndani kabla ya kumpiga kichwani kwa rungu na kisha kupoteza fahamu.

Alisema akiwa amepoteza fahamu mtu aliyekuwa amemvamia ndipo alipata nafasi ya kuingia ndani na kutekeleza adhma yake ya kumkata kiganja mtoto huyo ambaye ni mmoja kati ya watoto watatu wenye ualbino katika familia hiyo na kuondoka nacho.

Alisema wakati hayo yakitokea mumewe aliyemtaja kwa jina la Cosmas Lusambo alikuwa amekwenda kulala nyumbani kwa mke mdogo kwani ilikuwa zamu ya kwenda kulala huko kwa usiku huo lakini baada ya kusikia mayowe ya kuomba msaada alikwenda kuungana na familia yake na kumpeleka mtoto kituo cha afya cha Kamsamba kutokana na kuwa jirani na kijiji chao.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya, Akizungumza baada ya kumtembelea Baraka katika wodi ya watoto kwenye hospitali ya rufaa kanda ya Mbeya, alioneshwa kusikitishwa na tukio hilo na kuahidi kulifanyia kazi ili wahusika wapatikane na kuchukuliwa hatua.

Alisema ni tukio ambalo linasikitisha ambalo linazidi kuendeleza vitendo vya aibu kwa kuwafanyia ukatili wa kinyama albino kwa ujinga wa watu wachache wanaowadanganya watu kuwa viungo vyao ni bahati ya kuleta utajiri.

Mhandisi Manyanya mbali na kuzungumza na familia ya waathirika wa janga hilo pia aliongoza sara fupi ya kuwaombea albino hospitalini hapo alionesha pia kusikitishwa na mwenendo wa mashitaka ya watu waliofanya ukatili dhidi ya albino akisema mahakama zimekuwa na milolongo mirefu inayokatisha tama wadau wa kupinga ukatili huo.

Mkuu huyo wa mkoa alishauri pia kuangaliwa upya kwa sheria inayohusu masuala ya hukumu za kifo akisema ikibidi inapaswa kubadilishwa ili iweze kutoa haki kwa watu wanaofanya ukatili dhidi ya wenzao.

Alisema sheria ya sasa kumtaka rais pekee kuwa mtu wa mwisho kutoa uamuzi kunyongwa kwa mtu aliyehukumiwa inakosa nguvu ya kutekelezwa kutokana na majukumu mengi aliyonayo na kushauri kuwa ni vyema vyombo vya sheria vipewe mamlaka ya mwisho ya kutekeleza adhabu hiyo.

UNESCO, TIE na OUT wafadhili kozi kuboresha mitaala ya elimu Afrika

$
0
0
Ofisa mwakilishi wa Naibu Waziri wa Elimu, Anne Kilango Malecela akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa programu hiyo ya uboreshaji mitaala. 
 Ofisa mwakilishi wa Naibu Waziri wa Elimu, Anne Kilango Malecela akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa programu hiyo ya uboreshaji mitaala.Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania, Profesa Tolly Mbwette akizungumza katika hafla maalumu ya uzinduzi wa awamu ya nne ya programu hiyo jana Dar es Salaam. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania, Profesa Tolly Mbwette akizungumza katika hafla maalumu ya uzinduzi wa awamu ya nne ya programu hiyo jana Dar es Salaam.Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues aizungumza katika hafla ya uzinduzi wa programu hiyo jana jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues aizungumza katika hafla ya uzinduzi wa programu hiyo jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa leo Dar es Salaam. Baadhi ya washiriki wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa leo Dar es Salaam.Baadhi ya washiriki wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa leo Dar es Salaam. Baadhi ya washiriki wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa leo Dar es Salaam.
Meza kuu katika hafla ya uzinduzi wa programu hiyo ya uboreshaji mitaala ikifuatilia mada anuai. Meza kuu katika hafla ya uzinduzi wa programu hiyo ya uboreshaji mitaala ikifuatilia mada anuai.
Mmoja wa waratibu wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa leo Dar es Salaam akifundisha kwa washiriki. Mmoja wa waratibu wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa leo Dar es Salaam akifundisha kwa washiriki.Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) akiteta jambo na mmoja wa waratibu wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na kuboresha mitaala ya elimu Afrika. Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) akiteta jambo na mmoja wa waratibu wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na kuboresha mitaala ya elimu Afrika.Baadhi ya washiriki wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa leo Dar es Salaam. Baadhi ya washiriki wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa leo Dar es Salaam.Baadhi ya washiriki wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa leo Dar es Salaam. Baadhi ya washiriki wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa leo Dar es Salaam.Baadhi ya washiriki wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa leo Dar es Salaam. Baadhi ya washiriki wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa leo Dar es Salaam.Mmoja wa waratibu wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa leo Dar es Salaam akifundisha kwa washiriki. Mmoja wa waratibu wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa leo Dar es Salaam akifundisha kwa washiriki.Baadhi ya washiriki wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa leo Dar es Salaam. Baadhi ya washiriki wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa leo Dar es Salaam.Mmoja wa waratibu wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa leo Dar es Salaam akifundisha kwa washiriki. Mmoja wa waratibu wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa leo Dar es Salaam akifundisha kwa washiriki.Baadhi ya washiriki wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa leo Dar es Salaam. Baadhi ya washiriki wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa leo Dar es Salaam.Baadhi ya maofisa toka meza kuu wakizungumza katika hafla ya uzinduzi wa programu hiyo ya uboreshaji mitaala ikifuatilia mada anuai. Baadhi ya maofisa toka meza kuu wakizungumza katika hafla ya uzinduzi wa programu hiyo ya uboreshaji mitaala ikifuatilia mada anuai.[/caption] SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) wamewezesha kozi kwa baadhi ya nchi za Afrika yenye lengo la kuboresha mitaala ya elimu.

 Akizungumza kwa niaba ya Naibu Waziri wa Elimu, Anne Kilango Malecela katika hafla ya uzinduzi wa programu hiyo ya uboreshaji mitaala, aliipongeza UNESCO pamoja na taasisi zingine zilizounganisha nguvu kuhakikisha kozi hiyo ya uboreshaji mitaala inafanyika. Alisema njia pekee ya kuendelea kuboresha elimu yetu ni kutumia wataalamu wa elimu hasa wanaohitimu katika kozi maalumu za ubunifu na uandaaji mitaala kuiboresha mitaala hiyo kwa kuzingatia mahitaji halisi taifa moja hadi lingine. 

Alisema awamu ya nne ya mafunzo hayo ya uboreshaji mitaala ambayo imezinduliwa leo jijini Dar es Salaam na kujumuisha wanafunzi 100 kutoka nchi 23 ambazo ni pamoja na Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Zambia, Swaziland, Niger, Senegal, Cameroon, Burkina Faso, Togo, Chad, Ivory Coast, Nigeria, Hong Kong, Liberia, Sudan Kusini, Sierra Leone, Benin na wenyeji Tanzania. 

Aidha Kilango katika hotuba yake ameiomba UNESCO pamoja na mashirika wafadhili wa programu hiyo kuangalia uwezekano wa kuipanua zaidi na kuboresha programu hiyo ili kuwa na manufaa zaidi jambo ambalo alisema Serikali ipo tayari kutoa ushirikiano wowote kufaniisha jambo hilo. Hata hivyo aliwataka wahitimu wa mafunzo hayo kutumia nafasi walioipata ipasavyo pamoja na kuifanyia kazi kitaaluma mara baada ya mafunzo hayo.

 Alisema elimu ya utaalamu wa mitaala ni muhimu kwa taifa lolote hivyo kutumia utaalamu walioupata kuzishauri mamlaka kuboresha elimu kulingana na maitaji. UNESCO katika hafla hiyo iliwakilishwa na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues ambaye aliwataka wanafunzi watakao pata mafunzo hayo kutumia elimu ya utaalamu ipasavyo ili kuboresha elimu.

Benki ya Exim yaadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa kupinga ukatili dhidi ya wafanyakazi wa ndani.

$
0
0
 Katibu mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali inayojishughulisha na masuala ya maendeleo ya jamii (CODERT), Hellen Kayanza akifafanua jambo wakati wa shughuli iliyoandaliwa na Benki ya Exim jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambayo husherehekewa Machi 8 kila mwaka. 

Wakati wa shughuli hiyo wafanyakazi wa kike wa benki hiyo walitoa wito kwa wanawake nchini kutumia maadhimisho ya mwaka huu kutokomeza ukatili dhidi ya wafanyakazi wa ndani. Wanaotizama ni Meneja mwandamizi wa kitengo cha rasilimali watu wa benki ya Exim, Joan Mbakileki na Mkuu wa matawi wa benki hiyo, Elizabeth Mayengoh. 
Mkuu wa matawi wa Benki ya Exim, Elizabeth Mayengoh (kulia), akikabidhi zawadi kwa Katibu mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali inayojishughulisha na masuala ya maendeleo ya jamii (CODERT), Hellen Kayanza (wa pili kulia) wakati wa shughuli iliyoandaliwa na Benki ya Exim jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambayo husherehekewa Machi 8. 

Wakati wa shughuli hiyo wafanyakazi wa kike wa benki hiyo walitoa wito kwa wanawake nchini kutumia siku hiyo kutokomeza ukatili dhidi ya wafanyakazi wa ndani. Wanaotizama ni Mkuu wa matawi wa benki hiyo, Agnes Kaganda (kushoto) na Meneja mwandamizi wa kitengo cha rasilimali watu wa benki ya Exim, Joan Mbakileki.

NSSF yang'ara mashindano ya mbio za Kilimanjaro marathon

$
0
0
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Cresentius Magori (wa tatu kulia) akishiriki kwenye mbio za Kilimanjaro. Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Cresentius Magori (wa tatu kulia) akishiriki kwenye mbio za Kilimanjaro.Baadhi ya wafanyakazi wa NSSF- Kilimanjaro wakishiriki kwenye mbio za Kilometa 5. Baadhi ya wafanyakazi wa NSSF- Kilimanjaro wakishiriki kwenye mbio za Kilometa 5.Baadhi ya Wafanyakazi wa NSSF - Kilimanjaro wakimalizia kukimbi mbio za kilometa 5. Baadhi ya Wafanyakazi wa NSSF - Kilimanjaro wakimalizia kukimbi mbio za kilometa 5.

MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeshiriki kwenye Mbio za nyika za zinazoendelea kuwa maarufu mwaka hadi mwaka Kilimanjaro ambazo zimefanyika kwa mwaka wa 13 mfululizo. NSSF ilishiriki ikiwa kama mdhamini wa mbio za KM 5 ambazo zilishirikisha washiriki zaidi ya 3500. Pamoja na udhamini huo NSSF ilipata nafasi ya kutoa elimu kwa wakazi mbalimbali wa Mkoa wa kilimanjaro walioshiriki na kutembelea kwenye banda lao.

Mrembo Miss Tanzania aongoza wakazi wa dar katika zoezi la uchangiaji damu

$
0
0
Mshindi wa tatu wa Miss Tanzania 2014,Doris Mollel akishiriki zoezi la uchangiaji damu katika ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Siku ya wanawake Duniani,iliyofanyika Buguruni Chama jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto Ofisa Muuguzi kutoka Benki ya Damu Salama,Selina Joseph. Zoezi hilo la uchangiaji damu liliandaliwa na Mrembo huyo. 

Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani,mrembo Doris Mollel ambaye ni Miss Tanzania namba tatu kwa mwaka 2014 ameongoza mamia ya watanzania katika zoezi la kizalendo la kuhamasisha kuchangia damu kwa watanzania kwa ajili ya wagonjwa mbalimbali,zoezi ambalo limefanyika jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki. 

Zoezi hilo ambalo lilikuwa linaongozwa na mpango wa taifa wa damu salama kwa udhamini wa kampuni ya METL lilikuwa na lengo la kupata damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya Mama na Mtoto kwani matatizo ya damu katika hospitali za Tanzania yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku,jambo lililompelekea mrembo huyo kuamua kujitoa kuhamasisha watanzania kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo. 

Zoezi hilo lilifanyika Machi 8 mwaka huu katika maeneo ya Buguruni Chama kwa muda wa siku nzima,ambapo jumla ya uniti 65 za damu zimepatikana kiwango ambacho kimetajwa kuwa kinatia matumaini kwa mrembo huyo kufanikiwa katika kuwahamasisha watanzania kujitokeza kwa wingi. 
Akizungumza na wanahabari kuhusu kitu kilichomsukuma kuendesha zoezi hilo,Doris alisema kuwa ameamua kufanya hivyo baada ya kugundua kuwa wakina mama wengi pamoja na watoto hufariki dunia wakati wa kujifungua kutokana na kukosa damu ya kuongezewa,jambo ambalo amesema ni lazima watanzania kuungana kwa pamoja kutafuta damu ya kutosha katika kila hospitali ili kuiondoa hali hiyo ambayo inaweka hatarini maisha ya mama na mtoto wa kitanzania. 

Amesema kuwa swala la kujitolea damu ni swala la kizalendo zaidi na moyo wa kujitoa kwa kuwa kila mtanzania anaweza kuwa na uhitaji wa damu muda wowote hivyo ni lazima watanzania wawe na utamaduni wa kuchangia damu mara kwa mara kwani itasaidia endepo kutatokea uhitaji wa damu katika mahospitali yetu. 



Aidha amewataka watanzania wengine ambao wanauwezo wa kuhamasisha watu wengine kuchangia damu wafanye hivyo kwani kuna uhitaji mkubwa sana wa damu katika mahospitali ya kitanzania na kufanya hivyo ni kuokoa maisha ya watanzania wengi wenye uhitaji wa damu hiyo. 

Doris Mollel alijizolea umaarufu mwaka 2014 baada ya kufanikiwa kushika nafasi ya tatu katika shindano la Miss Tanzania mwaka huo ambapo aliwashinda warembo wengine waliokuwa wanawania taji hilo.
 Mtoto wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Mh. Said Meck Sadick,Bi Mariam Meck Sadick akiungana na wananzania wengine kwenye zoezi la kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Mrembo Doris Mollel.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakishiliki zoezi la uchangiaji damu katika kusherehekea Siku ya wanawake Duniani,iliyofanyika Buguruni Chama jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mpiga Picha wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd,John Dande akipima uzito tayari kwa kushiriki zoezi la uchangiaji damu,ikiwa ni sehemu kuunga mkono sherehe za Siku ya wanawake Duniani.zoezi hilo lilifanyika Buguruni Chama jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Picha na John Dande.

MEET AND GREET PARTY YA TANZANIA BLOGGERS ASSOCIATION SERENA HOTEL

Article 0

WAZIRI MKUU AKUTANA NA BALOZI WA KUWAIT NCHINI,/ PIA AFANYA MAZUNGUMZO NA MAKAMU WA RAIS WA KAMPUNI YA CONTRACTUS YA POLAND

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na balozi wa Kuwait nchini, Mhe Jaseem Al Najem kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Machi 9, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na balozi wa Kuwait nchini, Mhe. Jaseem Al Najem, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Machi 9, 2015. Katikati ni Ofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Batholomeo Jungu.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Contractus ya Poland, Bw. Witold Kartzewski (wapili kulia) na watendaji wa kampuni hiyo, Daniel Junusz (kulia) na Honorata Musloviska Ofisini kwake jijini Dar es salaam Machi 9, 2015. Kampuni hiyo pamoja na mambo mengine bingwa katika ujenzi wa vihenge vya kisasa vyenye uwezo wa kuhifadhi tani nyingi za nafaka. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

DCB COMMERCIAL BANK WADHAMINI MASHINDANO YA TANZANIA BANKERS & PUBLIC FUNDS CUP‏‎

$
0
0

 wa Tatu kutoka (kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji  wa DCB  Commercial Bank Plc  Bw. Edmund Mkwawa wa pili kutoka (kulia) ni Mkurugenzi Mkuu wa My way Entertainment Paul Mganga,wa Kwanza (kulia) ni Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya Tanzania Bankers and Public Funds Cup 2015 David Manoti, wa pili  (Kushoto) Samweli Mahendeka Agency Banking Manager ambaye pia ni Kapteni wa Timu ya Benki ya DCB wa tatu (kushoto) ni ni Product Development and Marketing Manager wa DCB Commercial Bank Plc Bw. Boyd Mwaisame na anayemfuatia  ni Chief Treasury Manager ambaye pia ni Mlezi wa Timu ya DCB Commercial Bank Plc Bw.Samwel E. Dyamo wakiwa katika Mkutano na waandishi wa Habari makao makuu ya DCB Commercial Bank Plc Leo.
 Mkurugenzi Mtendaji  wa DCB  Commercial Bank Plc  Bw. Edmund Mkwawa akiongea na Waandishi wa Habari Makao makuu ya DCB , alithibitisha kuwa DCB Commercial Bank watashiriki katika mashindano ya Tanzania Bankers and Public Funds Cup 2015 ambapo Timu yao tayari imesha anza kufanya mazoezi ya kujiandaa na mashindano hayo tangu mwezi wa pili mwaka huu 2015 na kuwa timu ipo katika hari nzuri sana si kwa kushiriki tuu lakini pia kutoa upinzani mkubwa watakazokutana nazo na hata kunyakua kikombe.

 Pia Bwana. Mkwawa amesema kuwa DCB pamoja na kushiriki kwao lakini wameamua kudhamini mashindano hayo ili kuweza kufanikisha kwa ufasaha zaidi na kuongeza kuwa lengo kubwa la DCB Commercial Bank kupitia udhamini na ushiriki wa mashindano hayo ni kupanua wigo mkubwa wa kimahusiano na kibiashara kwa ukaribu zaidi baina ya Benki,Mifuko ya kijamii na Jamii kwa ujumla.  Mwisho alitoa wito kwa wananchi mbalimbali kufika katika viwanja ambapo mashindano yatafanyika ili kujipatia Huduma Bora za Benki ya DCB na kujiunga na huduma mbalimbali zitolewazo na Benki hiyo katika Banda lao  maalum ambalo litakuwa katika viwanja hivyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa My Way Entertainment Bw.  Paul Mganga akiongea na waandishi wa Habari Makao makuu ya DCB Commercial Bank leo, alisema kuwa wanatarajia kuwa na mwitikio Mkubwa wa Taasisi za Kifedha na Mifuko ya Jamii katika Mashindano ya Tanzania Bankers Cup and Public Funds Cup kwa kujiunga na mashindano haya kama ilivyo DCB Benki ambao wameweza kuwa wa kwanza kuthibitisha wanashiriki mashindano hayo na Kudhamini pia na kuwashukuru kwa hilo, alihimiza kuwa Taasisi zengine za Kifedha na Mifuko ya Kijamii kuwa na mwitikio mkubwa wa mashindano hayo, kwani Michezo hujenga afya Bora na kukuza akili kama ilivyo kauli mbiu ya Mashindano haya"Tuungane katika Michezo, Michezo ni Afya , Michezo ni Ajira" Mwisho aliishukuru Benki ya DCB kuonesha mwamko mkubwa katika Swala la Michezo na kuomba Taasisi nyengine za Kifedha na Mifuko ya Jamii kuwa na mwamko huo. 
 
 Product Development and Marketing Manager wa DCB Commercial Bank Plc Bw. Boyd Mwaisame akisisitiza Jambo wakati wa Mkutano huo wa Benki ya DCB na waaandishi wa Habari juu ya Mashindano ya Tanzania Bankers and Public Funds Cup alisema kuwa ndani ya viwanja vya michezo kutakuwa na Banda maalum la DCB Commercial Bank ambapo huduma mbalimbali za Benki hiyo zitatolewa eneo hilo.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano ya Tanzania Bankers and Pensions Funds Cup 2015 Bw. David Manoti alitoa wito kwa vyombo vya habari , wadau wa Michezo, na wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika mashindano haya yatakayofanyika katika viwanja vya wazi ili kuweza kujionea burudani ya pekee itakayokuwa inaendelea katika viwanja hivyo.
Mkutano na waandishi wa Habari  Makao Makuu ya Benki ya DCB juu ya Ushiriki wao na Kudhamini mashindano hayo ukiwa unaendelea ambapo Mashindano hayo yanatarajia kuanza Rasmi 28 Machi 2015.

MKUU WA WILAYA KINONDONI AFANYA ZIARA HOSPITALI YA MWANANYAMALA NA PALESTINA KUANGALIA UTENDAJI WAKE

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akipewa maelekezo kutoka kwa mtaalamu wa maabara Dokta  Mniko Kimori.

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akiongea na akinamama waliopo katika wodi ya uzazi wakieleza uhaba wa majengo kusababaisha msongamano.
Akipokelewa na Mkunga...
Akiongea na wagonjwa...
Akionyeshwa X-Ray na mmoja ya wagonjwa...
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akiongea na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Palestina, Dkt. Benedicto Luoga iliyopo Sinza jijini Dar es Salaama akisoma taarifa ya hospitali mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza jana kuangalia jinsi utendaji wake wa Kazi. 
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akiongea akina mama aliyowakuta wakipata huduma katika hospitali ya Mwananyamara mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza jana kuangalia jinsi utendaji wake wa Kazi. Pembeni ni Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala Dk. Sophinias Ngonyani (kulia).
Akinamama wakifurahia kuongea na mkuu wa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akiongea  mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza jana kuangalia jinsi utendaji wake wa Kazi. 
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala Dk. Sophinias Ngonyani (kulia) akimuongoza Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza jana kuangalia jinsi utendaji wake wa Kazi.  
Wananchi walifika kupata huduma katika hospitali ya Mwananyamala wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda (hayupo pichani) mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza jana kuangalia jinsi utendaji wake wa Kazi.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akisalimiana na mmoja ya madokta wa hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza jana kuangalia jinsi utendaji wake wa Kazi.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akiongea akina mama aliyowakuta wakipata huduma katika hospitali ya Mwananyamara mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza jana kuangalia jinsi utendaji wake wa Kazi. 
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akionyeshwa jinsi X-Ray inavyofanya kazi.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akipata maelezo mara baada ya kuingia chumba cha maabara ya hospitali ya Mwananyamala mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza jana kuangalia jinsi utendaji wake wa Kazi.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala Dk. Sophinias Ngonyani akitoa maelezo kwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza jana kuangalia jinsi utendaji wake wa Kazi. 
Madokta wa hospitali ya Mwananyamala wakishauriana jambo.
Uhaba wa jengo na Vitanda ndiyo chanzo cha kuwalaza watoto watano kitanda kimoja.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akiongea na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Palestina, Dkt. Benedicto Luoga iliyopo Sinza jijini Dar es Salaama mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza jana kuangalia jinsi utendaji wake wa Kazi. Pembeni ni Katibu Tawala wa Manispaa ya Kinondoni.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Palestina iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam kuangalia jinsi utendaji wake wa Kazi.
Waandishi wa Habari walioambatana na Mkuu wa Wilaya wakifuatilia.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Palestina, Dkt. Benedicto Luoga akitoa maelezo machache.

Tatizo la mgawo wa umeme Arusha kumalizika Juni

$
0
0
  • Ni baada ya kukamilika kwa mradi wa umeme wa bilioni 72.5
    Wateja wapya 30,000 kuunganishwa
Na Greyson Mwase, Arusha

Meneja Mradi wa  Kusambaza  Umeme unaojulikana kwa jina la  Electricity  V unaofadhiliwa na  Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Mhandisi  Florence Gwang’ombe amesema kuwa  tatizo la kukatika katika kwa  umeme katika mkoa  wa Arusha litakwisha mapema Juni mara baada ya kukamilika kwa  kituo cha kupooza na kusambaza umeme  kilichopo katika eneo la Njiro, nje kidogo ya jiji la  Arusha.

Mhandisi Gwang’ombe aliyasema hayo mbele ya Kamati ya Kudumu  ya Bunge ya Nishati na Madini  iliyofanya ziara katika kituo hicho ili kujionea maendeleo yake pamoja na kuishauri  serikali  jinsi ya  usimamizi wake.

Alisema mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho mbali na kuboresha upatikanaji wa  nishati ya umeme katika jiji  la Arusha,  wateja wapya wapatao  30,000 wanategemewa kuunganishiwa umeme kutoka katika kituo hicho.

Akielezea   mradi huo  kwa ujumla Mhandisi  Gwang’ombe alisema kuwa  mradi huo unaofadhiliwa na  Benki ya Maendeleo  ya Afrika (AfDB) kwa  mkopo wa kiasi cha shilingi za kitanzania 72,588, 506,400 unahusisha  ujenzi wa njia za umeme wenye  urefu wa kilomita 480 za msongo wa kilovoti 33 na ufungaji wa transfoma 102 za kusambaza umeme zenye ukubwa wa 33/0.4 kV.

Alisema pia mradi huu unahusisha ujenzi na ukarabati wa vituo vya kupoozea umeme vya  Ilala, Sokoine katika mkoa wa Dar es  Salaam  na  upanuzi wa kituo cha  kupoozea umeme cha Njiro.


Alisisitiza kuwa mradi  unatekelezwa na Mkandarasi  National Contracting  Company ambaye alishinda zabuni  ya ujenzi  na ukarabati wa vituo vya kupoozea umeme katika mikoa ya Dar es  Salaam na  Arusha  na mkandarasi  Eltel Networks TE AB ambaye alishinda zabuni  ya ujenzi na ukarabati wa mifumo   ya kusambazia umeme  katika mikoa ya Shinyanga na  Mwanza.

Akielezea   hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa  kituo cha kupoozea umeme cha Njiro,  Mhandisi Gwang’ombe alisema kazi zinazoendelea katika kituo hicho ni pamoja na ufungaji wa transfoma mbili  na ufungaji wa mitambo  ya kisasa kwa ajili ya kuendesha  na kulinda mifumo ya umeme.

Aliongeza kuwa uagizaji na utengenezaji wa vifaa umekamilika  kwa asilimia 85,  kazi za ujenzi  zimekamilika kwa  asilimia 76 pamoja na kumalizika kwa kufunga na kuunganisha  vifaa na mifumo  ya umeme.

Alisisitiza kuwa mradi huu unategemewa kuongeza ukuaji wa uchumi katika mkoa wa Arusha pamoja na mikoa mingine   kama Shinyanga na Mwanza kwani utachochea ukuaji   wa viwanda vidogo vidogo na biashara katika maeneo husika pamoja na  kuongeza fursa za ajilra kwa wananchi.

Aliendelea kusema kuwa mradi huo utaboresha  huduma za jamii kwa wananchi kutokana na  upatikanaji wa umeme mashuleni, mahospitalini na kwenye maeneo mengine ya  jamii  husika na hivyo kupunguza umasikini  kwa wananchi  jambo ambalo linaendana na malengo ya siasa ya nchi.

Akizungumzia lengo la  mradi,  Mhandisi Gwang’ombe alisema kuwa lengo la mradi  ni kuongeza  uwezo wa kusambaza umeme wenye kiwango  kinachotakiwa na  usiokatikakatika na kulisaidia Shirika la Umeme Nchini (Tanesco)  kuweza kuwafikia na kuwapatia umeme  wenye uhakika wateja wengi zaidi  ambao bado hawajapatiwa huduma ya umeme.

Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Nchini  (Tanesco), Mhandisi Felchesmi Mramba aliiambia  Kamati ya Bunge kuwa  ongezeko la wateja wa kawaida  na  viwanda lilisababisha ongezeko la kasi la matumizi  kufikia Megawati 70 hali iliyopelekea shirika   kuboresha  na kujenga vituo  vya  kupoozea na kusambazia umeme.

Mhandisi Mramba alisema, kabla ya  ujenzi wa kituo hicho, hali ya umeme katika jiji la Arusha ilikuwa ni mbaya hali iliyopelekea ujenzi wa kituo hicho na kusisitiza kuwa Shirika limeamua kufanya  mapinduzi katika sekta ya umeme kwa kuhakikisha linashirikiana na wawekezaji  mbalimbali na wataalamu wake katika ujenzi wa vituo vya kuzalisha na kusambaza umeme ili kuzalisha nishati  ya umeme ya uhakika

EU, UN WAFAGILIA JUHUDI ZA KUBORESHA HALI ZA WANAWAKE TANZANIA

$
0
0
un2
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitoa salamu za Umoja wa Mataifa kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake duniani ambapo kitaifa ilifanyika mkoani Morogoro miwshoni mwa juma.

Na Modewjiblog team, Morogoro
SERIKALI ya Tanzania imepongezwa na Umoja wa mataifa kwa juhudi zake kubwa inazofanya katika kuhakikisha kuna usawa wa jinsia nchini humu.
Kauli hiyo imetolewa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakati alipopewa nafasi ya kuhutubia umati wa watu waliokusanyika kusherehekea siku ya wanawake duniani ambayo kitaifa ilifanyika Morogoro.

Alisema mbele ya Rais Jakaya Kikwete kwamba kazi kubwa iliyofanywa na serikali ya awamu ya nne ya kutekeleza maazimio ya kimataifa kuhusu usawa wa jinsia umeifanya Tanzania kuwa moja ya mataifa yanayostahili kupigiwa mfano.

Akitoa salamu za Umoja wa Mataifa kutoka kwa Katibu Mkuu Ban Ki Moon, mratibu huyo alisema kwamba katika bara la Afrika Tanzania imefanya makubwa katika kuhakikisha usawa wa jinsia na wanawake kuwezeshwa katika masuala mbalimbali yakiwemo ya kisiasa na utawala.
un6
Balozi wa Jumuiya ya Ulaya nchini, Filiberto Ceriani Sebregondi akisoma risala wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake duniani ambapo kitaifa ilifanyika mkoani Morogoro.

Alisema Tanzania imepiga hatua kubwa katika masuala ya usawa kijinsia na kutolea mfano wa kuwapo kwa asilimia 36 ya wanawake Bungeni.
Aidha amesema kuanzishwa kwa mifumo inayohakikisha kwamba wanawake wanapata nafasi sawa katika masuala ya uongozi, elimu na pia kupitishwa kwa sheria kali ya kukabiliana na masuala ya unyanyasaji na ukatili dhidi ya wanawake.

Aidha alisema kwamba miaka 20 iliyopita hali haikuwa sawa lakini kwa sasa kuna mabadiliko makubwa japo yanatakiwa mengi zaidi ili kukabiliana na changamoto zilizopo sasa.

Hata hivyo ameitaka serikali kufanya juhudi zaidi katika kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake na wasichana na kuhakikisha kwamba wanawake wanakuwa na sauti katika ngazi zote za utawala kuanzia katika kaya.

IMG_9262
Msanii nguli wa muziki nchini, Starah Thomas akiimba wimbo maalum katika siku ya kimataifa ya wanawake duniani ambapo kitaifa ilifanyika mkoani Morogoro.
Amesema hali hiyo inatokana na ukweli kuwa bado yapo maeneo ambapo mwanamke amekuwa akidharauliwa na pia kulazimishwa kufanya mambo ambayo ni kinyume na uhuru wa mwanadamu na haki zake za msingi.
Mambo hayo ameyataja kama haki za urithi , umiliki wa ardhi, ndoa za utotoni na ukeketaji.
Aidha kuna utata katika utekelezaji wa mifumo ya sheria inayotakiwa kumlinda mwanamke.
Mratibu huyo alisema kwamba maadhimisho hayo yanatoa nafasi ya kuchambua mafanikio, kuangalia changamoto na kutazama fursa zilizopo katika kuleta mafanikio katika juhudi za kuleta usawa wa jinsia kwa kutekeleza maazimio ya Beijing.
Naye Balozi wa Jumuiya ya Ulaya nchini Filiberto Ceriani Sebregondi amesema kwamba ameridhishwa sana na namna Tanzania inavyotekeleza mchakato wa kuelekea usawa wa wanawake na maendeleo kwa wote.
IMG_9302
Msanii Peter Msechu akitoa burudani sambamba na baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari Morogoro kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake duniani ambapo kitaifa ilifanyika mkoani Morogoro.
Amesema Jumuiya hiyo imefurahishwa na nafasi wanayopewa kusaidia Tanzania kufikia ustawi wa jamii kwa kuleta usawa kwa wanawake na wanaume.
Jumuya hiyo imesema kwamba inaamini mchango wake unasaidia kuweka hali bora zaidi kwa wanawake.
Amesema jumuiya hiyo kwa bajeti ya sasa wamechangia zaidi ya shilingi bilioni 14 katika miradi ambayo inasaidia wanawake moja kwa moja katika masuala ya wanawake katika ardhi na kilimo,ufundi stadi, fursa za ajira na kuzuia ukatili kwa wanawake.
Alisema kwamba mwaka 2014, walifanikisha mafunzo kwa maofisa jamii 63, dawati la jinsia 150, waendesha mashtaka 200, kamati za shule 200, watu wanaojitolea 6000, pamoja na wazazi na waangalizi kutoka Tanzania na Zanzibar.
Aidha jumuiya hiyo iliwezesha wanawake 8000 wa Mtwara na Kigoma kupata mikopo, mafunzo ya biashara na kumiliki ardhi.
IMG_8516
Wanafunzi mbalimbali wa shule za sekondari mkoani Morogoro wakifurahia burudani zilizokuwa zikitolewa kwenye uwanja wa Jamuhuri yalipofanyika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani na kufikia kilele chake machi 8 mwaka huu.
Aidha wamesaidia zaidi kuendeleza mafunzo dhidi ya mila na tamaduni zinazodhalilisha wanawake mkoani mwanza na Mara.
Katika mkoa wa Morogoro wamesaidia wafumaji wa Ifakara na kuwajengea uwezo wa kuongeza kipato chao.
Aidha wamefanikisha ujenzi wa makazi katika mji Kilosa kwa wale waliovurugwa na Masika.
Katika wilaya ya Kilosa mradi huo ulitumia shilingi bilioni 13.8 kusaidia ujenzi wa shule mbili na zahanati kupeleka umeme na maji.
IMG_8970
Kudhihirisha kuwa hata wanawake wanaweza: Mtaalamu wa Danadana Tanzania nzima hakuna, Hazala Charles Mnjeja a.k.a Ronaldo akitoa burudani kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Amesema miradi inayosaidiwa na Umoja wa Ulaya imelenga kuhakikisha kwamba wanawake na watoto wanapata nafasi ya kuchangika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Aidha ameshauri watanzania kusimama kidete kuhakikisha kwamba ukatili dhidi ya wanawake na watoto unamalizwa na kuanza kutengeneza jamii inayothamini utu na usawa.
Aidha balozi huyo ametaka kuanzishwa kwa mfumo wa kushughulikia migogoro ya ardhi ili kutoa nafasi wanawake waweze kushiriki kikamilifu katika uchumi unaotokana na ardhi.Alisema kuendelea kwa migogoro hiyo kunawanyima nafasi wanawake kuendelea kwa kuwa ardhi ni mtaji mkubwa kwao.
IMG_8976
IMG_9034
Sehemu ya umati wa wakazi wa Morogoro waliohudhuria kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani wakiwemo kina baba ambapo kitaifa ilifanyika mkoani Morogoro.
IMG_8364
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu (kushoto) na Afisa Habari wa Ubalozi wa Jumuiya ya Umoja wa ulaya Tanzania (EU), Susanne Mbise wakiwa kwenye picha ya pamoja na mtoto Miriam Edward aliyeambata na mama yake mzazi ndani ya viwanja vya Jamuhuri kwenye kilele cha sherehe za maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kitaifa yalifanyika mkoani Morogoro.
IMG_9355
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akifurahi jambo wakati akiwapongeza Sister Stella Mgaya (wa pili kulia) wa Kituo cha kupambana na ukeketaji cha Masanga (TFGM) Tarime, mkoani Mara na Mkurugenzi wa Kituo hicho, Sista Germaine Baibika (wa pili kushoto) baada ya kutunikiwa tuzo ya kutambua mchango wao wa kupambana na ukeketaji kwa wasichana wilayani Tarime. Kulia ni Balozi wa Jumuiya ya Ulaya nchini, Filiberto Ceriani Sebregondi.
IMG_8539
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akisalimiana kwa furaha na Mkuu wa wilaya ya Morogoro mjini, Jordan Rugimbana wakati wa sherehe za kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kitaifa yalifanyika mkoani Morogoro.
IMG_9337
Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye picha ya pamoja na baadhi ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania pamoja na viongozi wa serikali.
IMG_9330
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiteta jambo Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya zoezi la picha ya pamoja wakati wa sherehe za kilele cha maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake duniani.
IMG_8415
Baadhi ya raia wa kigeni na wakazi wa Morogoro wakiingia kwenye lango kuu la uwanja wa Jamuhuri mkoani Morogoro kushiriki sherehe za siku ya wanawake duniani.
DSC_0508
Rais wa VICOBA, Tanzania Bi. Devotha Likokola akizungumza na baadhi ya vikundi mbalimbali vya wanawake vilivyoshiriki kwenye maonyesho ya siku ya wanawake duniani mkoani Morogoro na kuwataka kujiunga na VICOBA ili waweze kupanua mitaji na wigo wa biashara zao.
IMG_8467
Afisa Utumishi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Kanda ya Mashariki Esuvatie Masinga akitoa elimu ya kutambua Haki na wajibu kwa mdau wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania kwenye banda lao wakati wa maadhimishi ya siku ya wanawake duniani ambapo kitaifa ilifanyika mkoani Morogoro.
IMG_8367
Afisa Habari wa Jumuia ya Umoja wa ulaya Tanzania (EU), Susanne Mbise akijadiliana jambo na Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu (kulia) pamoja na Stephaine Raison ambaye ni Afisa Mawasiliano wa UN Women (Katikati).

Rais Kikwete akutana na Mkuu wa Majeshi wa Malawi

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Mkuu wa majeshi ya ulinzi wa Malawi Jenerali Ignacio Emmanuel John ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Malawi na Tanzania.Jenerali Ignacio Emmanuel John Maulana(kushoto) na mwenyeji Jenerali Davis Mwamunyange(kulia) ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Malawi Jenerali Ignacio Emmanuel John Maulana na ujumbe wake ikulu jijini Dar es Salaam leo(picha na Freddy Maro).
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Malawi na Tanzania.Jenerali Ignacio Emmanuel John Maulana(kushoto) na mwenyeji Jenerali Davis Mwamunyange(kulia) ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live




Latest Images