Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 480 | 481 | (Page 482) | 483 | 484 | .... | 1904 | newer

  0 0

  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Raymond Mushi wakati akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Dar esb Salaam terehe 8.3.2015.RAY3 
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipunga mkono ikiwa ni ishara ya kuyapokea  maandamano ya akina mama wa Mkoa wa Dar es Salaam kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani tarehe 8.3.2015. RAY4 Wafanyakazi akina mama kutoka Jeshi la Polisi wakipita mbele ya Mgeni Rasmi Mama Salma Kikwete wakifuatiwa na Jeshi la zimamoto.RAY5Wafanyakazi akina mama kutoka Jeshi la Polisi wakipita mbele ya Mgeni Rasmi Mama Salma Kikwete wakifuatiwa na Jeshi la zimamoto.RAY7RAY10 
  RAY12 
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na mamia ya akina mama kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Dar es Salaam tarehe 8.3.2015. RAY13 
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea zawadi iliyotolewa na akina mama kutoka moja ya wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwee akitembelea mabanda ya maonyesho ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wanawake katika Mkoa wa Dra es Salaam wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani tarehe 8.3.2015. RAY16 
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitazama vijarida mbalimbali vinavyotolewa na wanawake katika mkoa wa Dar es Salaam kuhusiana na nmasuala ya tafiti mbalimbali.
  PICHA NA JOHN  LUKUWI.

  0 0

  SAM_1388
  Wema Sepetu akiwa ndani ya studio za Radio 5 jana mara baada yan kufanya ziara fupi mjengoni hapo akielezea pia kuhusu show yake ya black and white party iliyofanyika jana usiku tarehe 7/3/2015 jijini Arusha kushoto ni mtangazaji mahiri wa kituo hicho Wilfredy akiwa anafanya kipindi na mwanadada huyo, Wanaonekana pichani ni team Wema.(Habari Picha na Pamela Mlollel wa jamiiblog)
  SAM_1387
  Wema Sepetu akiwa anaeleza furaha yake yakuwepo jiji Arusha ambapo amesema jiji la Arusha ni miongoni mwa majiji anayoyapenda, Mwanza ikiwa ya kwanza na Arusha ya pili, Kulia ni msanii Petiman a.k.a Wakuache. 

  SAM_1381
  Mkuu wa vipindi vya Radio5 kulia Mathew Phillip akiwa anakaribisha team Wema.
   
  SAM_1372
  Msafara wa Wema Sepetu ukiingia kwa mbwembwe katika studio za Radio5 zilizopo njiro jijini Arusha.
  SAM_1374
  Muonekano wa Wema Sepetu akiingia mjengoni akiwa katika gari la kifahari la wazi.
  SAM_1393
  Meneja wa Wema Sepetu Martin Kadinda akiwa anatoa neno la shukran kwa wana Arusha kwa mapokezi yao makubwa.
  SAM_1406
  Team mishemishe wakiwa na Wema Sepetu, kushoto; Mwanaisha Suleiman, Wema Sepetu, Mwangaza Jumanne na Hilda Kinabo wakishoo love.
  SAM_1394
  Camera man wa Wema Sepetu akiwa anachukua matukio.
  SAM_1404
  Mtangazaji mahiri wa kituo cha Radio5 Wilfredy akiwa katika picha ya pamoja na mwana dada Wema Sepetu.
  SAM_1407
  Team wema wakiwa wanaondoka katika studio za Radio5.

  0 0

  Karibu katika sehemu hii ya pili ya mazungumzo na Mhe. Samuel Sitta (Mb)
  Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba ya Jamhuri ya Muungano waTanzania mwaka 2014.

  Aliketi nasi kuzungumzia kuhusu kazi zake kama Waziri wa Uchukuzi na pia nia yake ya kugombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu (2015)
  Karibu


  0 0

                 Bendi ya maarufu Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni aka Anunaki aliens bendi hiyo inatarajiwa kutumbuiza katika onyesho maalumu la AFRICA UNITE PARTY litakalofanyika katika ukumbi wa VTS uliopo mtaa wa Augusburger Str.442 D-70327 mjini Stuttgart,nchini Ujerumani.
  Onyesho hilo limeandaliwana shirika la Afrikaktiv e.V wakishirikiana na  shirika la Cabaret du Monde,Ngoma Africa band iliyozoeleka kwa kuwatia kiwewe washabiki wake kilakona duniani wataporomosha muziki moto moto na mdundo wao maarafukama " Extraordinary Bongo Dansi" mdundo unaotingisha bila ya kuwa nampinzani huko ughaibuni, bendi hiyo inadumu katika medani ya muziki kwamuda wa miaka 23 na kufanikiwa kujizolea washabiki kila kona.
  Ticket za onyesho hilo zinapatikana kwa simu ( booking): Call9+49 0)152 12091242 au +49(0)152 106106137 Mnakaribishwa wote,pia usikose kuwasikilizaFFU-Ughaibuni at www.ngoma-africa.com


  0 0

  Dk Hamza Mzige kutoka Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe akimpima moja ya mtoto aliyeletwa kupata huduma katika zoezi hilo lililoendeshwa eneo la Kibugumu Kigamboni jijini Dar es Salaam. Dk Hamza Mzige kutoka Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe akimpima moja ya mtoto aliyeletwa kupata huduma katika zoezi hilo lililoendeshwa eneo la Kibugumu Kigamboni jijini Dar es Salaam.Mratibu wa huduma hizo, Dk. Ali Mzige (wa kwanza kulia) akitoa huduma kwa wagonjwa katika zoezi hilo. Mratibu wa huduma hizo, Dk. Ali Mzige (wa kwanza kulia) akitoa huduma kwa wagonjwa katika zoezi hilo.Mmoja wa wahudumu wa afya akitoa huduma kwa baadhi ya watoto waliofikishwa katika zoezi hilo lililoendeshwa eneo la Kibugumu Kigamboni jijini Dar es Salaam. Mmoja wa wahudumu wa afya akitoa huduma kwa baadhi ya watoto waliofikishwa katika zoezi hilo lililoendeshwa eneo la Kibugumu Kigamboni jijini Dar es Salaam.
  Dk Hamza Mzige kutoka Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe akitoa huduma kwa mmoja wa wateja wake katika zoezi hilo. Dk Hamza Mzige kutoka Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe akitoa huduma kwa mmoja wa wateja wake katika zoezi hilo.Baadhi ya madaktari wakitoa huduma kwa baadhi ya watoto waliofikishwa katika zoezi hilo lililoendeshwa eneo la Kibugumu Kigamboni jijini Dar es Salaam. Baadhi ya madaktari wakitoa huduma kwa baadhi ya watoto waliofikishwa katika zoezi hilo lililoendeshwa eneo la Kibugumu Kigamboni jijini Dar es SalaamBaadhi ya wanajumuiya ya wa Jamii ya Watu kutoka nchini India Bengali wa Dar es Salaam (Bango Sangho) wakitoa baadhi ya zawadi kwa wananchi waliojitokeza kupata huduma za afya. Baadhi ya wanajumuiya ya wa Jamii ya Watu kutoka nchini India Bengali wa Dar es Salaam (Bango Sangho) wakitoa baadhi ya zawadi kwa wananchi waliojitokeza kupata huduma za afya.Baadhi ya wanajumuiya ya wa Jamii ya Watu kutoka nchini India Bengali wa Dar es Salaam (Bango Sangho) wakiwa eneo la Kibugumu Kigamboni jijini Dar es Salaam inapotolewa huduma hiyo. Baadhi ya wanajumuiya ya wa Jamii ya Watu kutoka nchini India Bengali wa Dar es Salaam (Bango Sangho) wakiwa eneo la Kibugumu Kigamboni jijini Dar es Salaam inapotolewa huduma hiyo.Baadhi ya wananchi waliojitokeza kupata huduma za afya bure wakisubiri kuhudumiwa na madaktari. Baadhi ya wananchi waliojitokeza kupata huduma za afya bure wakisubiri kuhudumiwa na madaktari.Balozi wa India nchini Tanzania, Debnath Shaw (kushoto) akisalimiana na Dk Hamza Mzige wa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe ambaye ni miongoni mwa madaktari waliokuwa wakitoa huduma za afya bure kwa watoto wa chini ya miaka mitano eneo la Kibugumu, zoezi hilo lililoendeshwa na Umoja wa Jamii ya Watu kutoka nchini India Bengali. Balozi wa India nchini Tanzania, Debnath Shaw (kushoto) akisalimiana na Dk Hamza Mzige wa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe ambaye ni miongoni mwa madaktari waliokuwa wakitoa huduma za afya bure kwa watoto wa chini ya miaka mitano eneo la Kibugumu, zoezi hilo lililoendeshwa na Umoja wa Jamii ya Watu kutoka nchini India Bengali.Baadhi ya madaktari na wahudumu wa afya wakitoa huduma kwa baadhi ya watoto waliofikishwa katika zoezi hilo lililoendeshwa eneo la Kibugumu Kigamboni jijini Dar es Salaam. Baadhi ya madaktari na wahudumu wa afya wakitoa huduma kwa baadhi ya watoto waliofikishwa katika zoezi hilo lililoendeshwa eneo la Kibugumu Kigamboni jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wananchi waliojitokeza kupata huduma za afya bure wakisubiri kuhudumiwa na madaktari. Baadhi ya wananchi waliojitokeza kupata huduma za afya bure wakisubiri kuhudumiwa na madaktari.Balozi wa India nchini Tanzania, Debnath Shaw (mwenye fulana nyeusi) akipewa maelezo mafupi na Dk. Ali Mzige (wa kwanza kushoto) juu ya zoezi la utoaji huduma za afya bure kwa watoto wa chini ya miaka mitano eneo la Kibugumu lililoendeshwa na Umoja wa Jamii ya Watu kutoka nchini India Bengali. Wengine ni viongozi wa Bango Sangho. Balozi wa India nchini Tanzania, Debnath Shaw (mwenye fulana nyeusi) akipewa maelezo mafupi na Dk. Ali Mzige (wa kwanza kushoto) juu ya zoezi la utoaji huduma za afya bure kwa watoto wa chini ya miaka mitano eneo la Kibugumu lililoendeshwa na Umoja wa Jamii ya Watu kutoka nchini India Bengali. Wengine ni viongozi wa Bango SanghoMratibu wa huduma hizo, Dk. Ali Mzige akizungumza na wanahabari katika zoezi hilo. Mratibu wa huduma hizo, Dk. Ali Mzige akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) katika zoezi hilo.Baadhi ya wanajumuiya ya wa Jamii ya Watu kutoka nchini India Bengali wa Dar es Salaam (Bango Sangho) wakitoa baadhi ya zawadi kwa wananchi waliojitokeza kupata huduma za afya. Baadhi ya wanajumuiya ya wa Jamii ya Watu kutoka nchini India Bengali wa Dar es Salaam (Bango Sangho) wakitoa baadhi ya zawadi kwa wananchi waliojitokeza kupata huduma za afya.

   UMOJA wa Jamii ya Watu kutoka nchini India Bengali wa Dar es Salaam (Bango Sangho) wametoa huduma za afya bure kwa watoto wa chini ya miaka mitano eneo la Kibugumu lililopo Kigamboni jijini Dar es Salaam. 

   Zaidi ya watoto 100 wamepatiwa huduma mbalimbali za afya ikiwemo huduma za vipimo na ushauri, huduma za afya ya kinywa na meno na pia kufanyiwa ukaguzi na ushauri wa lishe suala ambalo limekuwa na changamoto kubwa kwa familia. Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio, Mratibu wa huduma hizo, Dk. Ali Mzige ambaye ni daktari wa watoto amesema Bango Sangho wameamua kuendesha zoezi hilo ili kuwasaidia baadhi ya familia ambazo zimekuwa zikipata changamoto kwa magonjwa anuai yanayowashambulia watoto.

   Alisema zoezi hilo limeendeshwa bure chini ya uratibu wa Umoja wa Jamii ya Watu wa India, Bengali ikiwa ni utaratibu wao wa kujitolea kusaidia jamii katika masuala mbalimbali yanayowakabilia. Alisema mbali ya huduma za vipimo ushauri na huduma za kliniki wazazi pia walipewa ushauri stahiki wa kiafya kwa watoto wao ili kukabiliana na magonjwa nyemelezi yanayowaathiri watoto. 

   Akifafanua zaidi juu ya zoezi hilo, Dk. Mzige alisema idadi kubwa ya watoto waliopatiwa huduma eneo hilo wamebainika kuwa na upungugu wa wekundu wa damu pamoja na upungufu wa uzito jamboa ambalo linaathiri hali ya ukuaji wao kiafya. Alisema waliobainika kuwa na matatizo makubwa kiafya wamepewa rufaa kwenda hospitali za juu kwa msaada zaidi wa kiafya. Alisema pamoja na mambo mengine wanawashauri wazazi kuwatairi mapema iwezekanavyo watoto wa kiume ili kuzuia uwezekano wa kupata maambukizi kwenye njia ya mkojo.

   "...Kwa watoto wa kike tunawashauri mama zao wawasafishe mara kwa mara wanapojisaidia...wengine wanafunga pampasi lakini inakaa muda mrefu inakuwa na unyevu jamboa ambalo linaweza kumsababishia mtoto kupata UTI...maambukizi kwenye njia ya mkojo kwa hiyo hili ni suala ambalo wazazi tunawaelekeza ili kupunguza maambukizi ya magonjwa kwa watoto," alifafanua Dk. Mzige. Aidha alisema mtoto anapopata maambukizi ya mara kwa mara yanamuathiri katika ongezeko la uzito na kukosa hamu ya kula jambo ambalo ni hatari kiafya kwa watoto wengi. 

  Miongoni mwa madaktari waliokuwa wakitoa huduma hizo ni pamoja na wataalamu wa afya ya kinywa na meno, madaktari wataalamu wa watoto pamoja na wataalamu wa vipimo vya maabara. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bango Sangho Dar es Salaam, Amit Nandi alisema wameamua kutoa huduma hilo eneo la nje ya Dar es Salaam ili kutoa fursa kwa wananchi wenye kipato cha chini kupata huduma za afya bure na karibu jambo ambalo litasaidia kupunguza gharama na mzigo kwao. 

  Alisema huduma hizo za afya huzitoa kila mwaka bure kwa jamii ikiwa ni mchango wao kwa jamii ya kawaida ili nayo iweze kupata huduma za afya ambazo zimekuwa changamoto hasa maeneo ya vijijini na nje ya miji. Jamii ya Bango Sangho pia wamesaidia ujenzi wa shule ya msingi na awali ya Kibugumu ikiwa ni mchango kwa jamii.

  0 0

  jan1
  Naibu Waziri Sayansi na Teknolojia January Makamba akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampuni ya na kampuni ya Copyrights Management East Africa Limited (CMEA).
  jan2
  Afisa Mtendaji Mkuu wa CMEA, Paul Matthysse akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa kampuni hiyo yenye lengo la kuwakwamua wanamuziki katika umaskini. CMEA pia  itawawezesha pia watayarishaji wa muziki na wasanii wengine pamoja na vyombo vya habari kupata kufahami takwimu sahihi za nymbo zilizochezwa kwa siku, wiki, mwezi na kwa mwaka.
  Mwanamuziki Mkongwe nchini, John Kitime akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampuni ya inayojishughulisha na Hakimiliki za kazi za wasanii katika nchi za Afrika Mashariki ijulikanayo kwa jina la Copyrights Management East Africa Limited (CMEA).
  …………………………………………………………………………………………..
   
  Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba amewataka wanamuziki nchini kuachana na kutegemea kupata shoo za majukwaani na kupata umaarufu usiokuwa na tija kwa kujiunga na kampuni ya Copyrights Management East Africa Limited (CMEA) ambayo inasimamia haki miliki za kazi za wasanii wa ukanda wa nchi ya Afrika Mashariki.
   
  Naibu Waziri Makamba alisema hayo wakati wa uzinduzi rasmi wa kampuni ya CMEA ambayo ipo chini ya mtayarishaji wa muziki maarufu, Paul Matthysse (P-Funk) ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kamuni hiyo.
   
  Makamba alisema kuwa wanamuziki wengi nchini wanapata umaarufu mkubwa wa bila kipato kutokana na kazi zao bora kwani hawafaidiki na utunzi wa nyimbo zao zinazopigwa kwenye televisheni na vituo vya redio mbalimbali.Alisema kuwa matokeo yake wanapotea katika fani hiyo na kuwa maskini maarufu na faida kubwa kwao ni kupata sifa kwa warembo mbalimbali ambao huwakimbia pale wanaposhuka katika fani.
   
  “Mimi najua muziki na wanamuziki, hakuna mtu anayeweza kunidanganya, wanamuziki wanapata tabu katika utunzi na baadaye kutafuta fedha za kurekodi kwa kukopa au kwa kuombaomba, baadaye watafute fedha za kuwapa madj wa redio na wa vipindi vya televisheni ili wimbo wake uchezwe na kupata shoo mbalimali kwa kipato kidogo,” alisema Makamba.
  Alisema kutokana na  hali ilivyo, mwanamuziki anaishia kukuapata shoo kwa ujira mdogo na akipotea katika fani, anakuwa maskini maarufu.
   
  “CMEA ni sululisho kwenu, kampuni hi itafanyakazi pamoja na Chama Cha Hakimiliki Tanzania (Cosota) kuweza kujua wimbo wako au video yako imechezwa mara ngapi redioni au kwenye televisheni na unastahili kulipwa shilingi ngapi,” alisema.Alisema kuwa hata baada ya kuacha muziki, utaendelea kupata fedha ‘pensheni’ kutokana na wimbo au video yako kuchezwa redioni na kwenye televisheni.
   
  Afisa Mtendaji Mkuu wa CMEA, Paul Matthysse alisema kuwa mbali ya wanamuziki, kampuni yao itawawezeha pia watayarishaji wa muziki na wasanii wengine pamoja na vyombo vya habari kupata kufahami takwimu sahihi za nymbo zilizochezwa kwa siku, wiki, mwezi na kwa mwaka.
   
  Matthysse alisema kuwa kampuni yao imewekeza mitambo ya kisasa inayowezesha kuchapisha na kuhakiki nyimbo pindi zinapochezwa hewani na televisheni na redio na kutoa ripoti za aina mbalimbali zinazohitajika kutumika kwa malengo maalum.
   
  “Pia tunapokea na kuhifadhi nyimbo kwenye mitambo maalum kwa matumizi ya uhakiki, na kudhibiti kiasi cha mirabaha ambacho Cosota kupitia vyombo vya habari inatakiwa kuwalipa wasanii kulingana na idadi kamili ya urushwaji wa kazi zao,” alisema Matthysse.

  0 0


  Mkurungezi mtendaji wa Mwanaharakati Mzalendo Media  Krantz Mwantepele akisaini kitabu cha wageni  mara baada ya kufika katika kituo cha wazee wasiojiweza Msimbazi  kinachosimamiwa na jimbo kuu hapa dar es salaam kanisa la katoliki na kuhudumia wazee wapatao kumi na moja waliokuwa wanaishi katika mazingira magumu.Timu nzima ya Mwanaharakati Mzalendo Media ilikuja hapa kuwaona wazee hawa na kupata nafasi ya kuwafariji na kutoa baadhi ya misaada ya chakula na nguo za kuwasitiri leo siku ya jumamosi tarehe 7/3/2015.
  Mdau Marko Mlonganile akipata nafasi ya kumsalimia mmoja ya wazee wanaopatikana katika kituo hiki na kupata nafasi ya kujua baadhi ya changamoto zinazopatikana katika kituo hiki siku ya jumamosi tarehe 7/3/2015.
  Mdau subilaga james akiwa  katika taswira na mmoja bibi wanaopatikana katika kituo hiki cha wazee wasiojiweza kinachosimamiwa na jimbo kuu Dar es salaam la kanisa katoliki na kuweza kuhudumia wazee wapatao  kumi na moja   siku ya jumamosi tarehe 7/3/2015.


  Bibi ambaye ni mmoja ya wazee wanaotunzwa katika kituo hiki akitabasamu baada ya wadau wa Mwanaharakati Mzalendo Media kutembelea  hapa na kuweza kuwafariji kwa kukaa nao na pia kutoa mahitaji kwa ajili ya chakula na nguo za kuwasitiri katika kituo cha wazee wasiojiweza hapa jijin dar es salaam kituo kinachosimamiwa na jimbo kuu Dar es salaam katoliki   siku ya jumamosi tarehe 7/3/2015


  Bibi akitabasamu baada ya wadau wa Mwanaharakati Mzalendo Media kutembelea  hapa na kuweza kuwafariji kwa kukaa nao na pia kutoa mahitaji kidogo kwa ajili ya chakula na nguo za kuwasitiri katika kituo cha wazee wasiojiweza hapa jijin dar es salaam kituo kinachosimamiwa na jimbo kuu Dar es salaam katoliki   siku ya jumamosi tarehe 7/3/2015


  Baadhi ya wadau toka Mwanaharakati Mzalendo MEDIA wakiongea na mmoja ya wazee aliyelala kitandani ni moja kati ya wanaotunzwa na kituo cha wazee   siku ya jumamosi tarehe 7/3/2015  Moja ya nyumba ambayo inatunza wazee wasiojiweza na ni kituo kinachosimamiwa na kanisa katoliki jimbo kuu dar es salaam


  Mahojiano yakiendelea na msimamizi wa kituo hiki sister angelina hapa akieeleza historia fupi ya kituo na jinsi wanavyowahudumia wazee katika kituo hiki   Mkurungezi wa Mwanaharakati Mzalendo Media Krantz Mwantepele akitoa maelezo kidogo kwa msimamizi wa kituo hiki sister angelina  (hayupo pichani ) na wanaosikiliza kwa makini ni wadau Subilaga na Happy 


  Wadau wa Mwanaharakati Mzalendo MEDIA wakifurahi jambo na msimamizi wa kituo hiki sister angelina 

  Tukikabidhi baadhi ya michango kama mahitaji muhimu ya chakula kwa mismamizi wa kituo cha wazee wasjiojiweza sister angelina  anayeshuhudia ni mdau bensoni 
  Mmoja wa wazee akiongea jambo mdau Marko mlonganile  huku  mkurungezi mtendaji  wa Mwanaharakati Mzalendo media Krantz Mwantepele akisikiliza kwa makini .

  Mkurungezi wa Mwanaharakati Mzalendo Media krantz mwantepele  akikabidhi baadhi ya misaada ya chakula na nguo  kwa msimamizi wa kituo hiki siter angelina  iliyotolewa na wadau wa mtandao wa Mwanaharakati mzalendo Blog
  Mkurungezi  wa Mwanaharakati Mzalendo MEDIA Krantz Mwantepele  akiwa katika picha ya pamoja na wadau   walioshiriki baada ya kumaliza safari ya kuwaona wazee katika kituo hiki na kutoa baadhi ya mahitaji ya chakula na nguo za kuwasitiri


  PICHA ZOTE  NA ALFRED MLONGANILE 


  0 0

  Na Henry Mdimu
  Tangu asubuhi leo nilikuwa busy na awareness za uwanja wa Taifa katika mechi ya watani wa Jadi Yanga na Simba (picha ya pili). Ila jioni hii nilipoangalia simu yangu nikakuta watu wakinilaumu kutokana na tukio la mtoto Baraka Cosmas (picha ya kwanza) ambaye usiku wa kuamkia leo amekatwa mikono yake. 
  Wanasema nilikuwa nakula Bata Uwanja wa Taifa huku watu wanateketea. Hasa alikuwa akiongea mtu anaitwa @hmgeleka. Kwanza nalaani kitendo hicho cha kikatili  na kuzidi kumuomba Rais wangu Mhe Jakaya Mrisho Kikwete aongee na vyombo vyake vya usalama, wasiliache hili lipite hivi hivi. 
  Lakini jingine jamani suala hili sio la mmoja. Kwa sababu nimejitwika ubalozi ndio nilaumiwe kwa hata lililo mbali na mimi? Vita hii ni ya wote, mimi nina wiki mbili tu tangu nianze kazi hii na bado natafuta mtaji wa kuendesha zoezi langu. Tafadhali tutende wote tusinyoosheane vidole, huku tukiwa vijiweni, mmenielewa? #IMETOSHA
   Bango la harakati za "Imetosha!" likiingizwa uwanjani sambamba na ya FIFA ma FIFA Fair Play wakati wa mchezo wa ligi kuu wa watani wa jadi Simba na Yanga Uwanja wa Taifa leo. Chini ni Balozi wa Harakati za Imetosha Henry Mdimu akiongea machache kuhusu harakati hizo zenye lengo la kuhamasisha wadau wote kukomesha vitendo vya mauaji na vya kikatili dhidi ya ndugu zete Albino.
  Wachezaji wa Yanga na Simba wakiingia uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam wakiwa wamevaa fulana maalumu za harakati za "Imetosha!"

   Marafiki wa harakati za "Imetosha!" wakisubiri kuingia uwanjani
  Marafiki wa harakati za "Imetosha!" wakisubiri kuingia uwanjani. Marafiki hao ni mchanganyiko wa wana habari, bloggers, wasanii na wanaharakati wengine 
  Rafiki wa harakati za "Imetosha!" na balozi wa Jay Millions ya VODACOM Zembwela akihamasisha akiwa na marafiki wenzie. Kulia ni mchora katuni maarufu Masoud Kipanya ambaye pia ndiye mwenyekiti wa harakati hizo

  0 0

  Mwenyekiti wa kamati ya mnuso wa wafanyakazi wa Azania Bank tawi la Moshi,Tumsifu Swai akitoa neno la ukaribiho kwa wageni waliofika katika mnuso huo uliofanyika katika Hotel ya Sal Salnero mjini Moshi.
  Meneja wa Azania Bank tawi la Moshi,Hajira Mmambe akizungumza na watoto pamoja na kuwakaribisha wanafamilia wa benki hiyo katika mnuso wa usiku ulioandaliwa mahususi kwa ajili ya wafanyakazi wa benki hiyo pamoja na familia zao.
  Wanafamilia wa Azania Bank tawi la Moshi wakichukua chakula.
  Wafanyakazi wa Azania Bank tawi la Moshi na familia zao wakifurahia msosi wa usiku ulioandaliwa kwa ajili yao.
  Ukafika wakati wa kufungua Champegne,
  Champegne ikagawiwa kwa kila aliyekuwa ukumbini.
  Zikagongwa Cheers kwa waalikwa wote ,akiwemo mwakilishi wa Globu ya Jamii Knda ya Kaskazini akiwa ni mdau wa benki hiyo.
  Keki maalumu kwa ajili ya wafanyakazi wa Benki ya Azania tawi la Moshi na familia zao .
  Wafanyakazi wa Azania Bank tawi la Moshi wakikabidhiwa keki toka kwa Meneja wa tawil hilo Hajira Mmambe (kulia) ikiwa ni sehemu ya sherehe ya wafanyakazi wa benki hiyo baada ya kufanya vyema mwaka 2014/2015.
  Keki ikatolewa kwa wawakishi wa makundi yaliyokuwa yamewakilisha katika tafrija hiyo.
  Azania Bank ikatoa vyeti kwa wafanyakazi wa tawi hil kwa mchango wao waliouonyesha katika kufikia mafanikio katika kipindi cha mwaka 2014/2015.
  Wafanyakazi wote wa Azania Bank tawi la Moshi wakapata nafasi ya picha ya pamoja wakiwa na vyeti vyao.
  Na badae likafuata neno toka kwa Meneja wa tawi hilo,Hajira Mmambe .
  Watoto wa watumishi wa Azania Bank tawi la Moshi wakiwa katika picha ya Pamoja,
  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Knada ya Kaskazini,

  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC) Azza Hamad akizungumza wakati kamati hiyo ilipotembelea Halmashauri ya wilaya ya Karatu.Kulia kwake ni mkuu wa wilaya ya Karatu Omar Kwang.
  Wajumbe wa kamati hiyo Mh ,Tahuida Nyambo na Yahya Issa wakitizama vitabu ,pembeni kulia ni katibu msaidizi wa kamati hiyo Waziri Kizingiti.
  Mjumbe wa kamati ya LAAC,Dastan Mkapa akiwa na Katibu wa kamati hiyo,Dickson Bisire wakifutilia hotuba ya mwenyekiti wa kamati hiyo.
  Wajumbe wa kamati ya LAAC,Mh Agustino Masele pamojan na Mh Menrad Kigola wakifuatilia kwa makini hoja zilizokuwa zikitolewa wakati wa kika hicho na watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Karatu.
  Watendaji wa serikali kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha wakifuatilia jambo katika kikao hicho.
  Baadhi ya watumishi wa Halamshauri ya wilaya ya Karatu wakiwa katika kikao hicho.
  Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu,Lazaro Titus akiongozana na Mwenyekiti wa kamati ndogo ya Bunge ya Hesabu za serikali za Mitaa kwenda kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo.
  Mwenyekiti akikagua jengo la Chuo cha Ualimu cha Ayalabee ambacho kinatajwa majengo yake kujengwa chini ya kiwango.
  Hili ndio jengo la Chuo cha Ualimu cha Ayalabee kama linavyoonekana sehemu ya Paa lake likiwa tayari limebinyea.
  Baadhi ya wananchi walipata fursa ya kutoa madukuduku yao kwa kamati juu ya ujenzi wa Chuo hicho.
  Mbunge wa jimbo la Karatu ,Mch Izrael Natse pia akjazia neno katika eneo la Chuo hicho.
  Jicho la kamati likaona nyufa za kutosha katika jengo hilo kama anavyoonesha mwenyekiti wa kamati hiyo Azza Hamad.
  Maeneo mengine ikabainika kuwa ndiyo yalijengwa siku hiyo wakati kamati inaenda tembelea.
  Hivi ndivyo hali ilivyokuwa kwa baahi ya maeneo.
  Wajumbe wa kamati wakitizama sehemu ya Paa la jengo hilo.
  Kmati ikakagua  Hostel ya wananfunzi ambayo licha ya kukutana na kizuizi cha nyuki bado kamati ilibaini kuwa jengo hilo limejengwa chini ya kiwango pia.
  Kamati ikaelekea kukagua majengo mengine ya chuo hicho.
  Hali ilikuwa ni ile ile.
  Baadae kamati ikafika katika nyumba ya wauguzi na kubaini kuwa licha ya kwamba nyumba hiyo imemalizika bado watumishi wa zahanati hawaishi ndani ya nyumba hiyo na badala yake imetolewa kwa wafanyakazi wa REA,kuweka vifaa vyao .
  Na Dixon Busagaga wa Globu aya Jamii Knada ya Kaskazini.

  0 0

  Msimamizi wa michezo ya kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Mrisho Milao kulia akipata maelekezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mauzo ya mtandao (Online) wa Bayport Financial Services, Zainabu Kalufya, katika uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo ya haraka kwa njia ya mtandao kwa www.kopabayport.co.tz, uzinduzi uliofanyika leo Makao Makuu ya Bayport, jijini Dar es Salaam. Mteja atakayekopa kwa njia ya mtandao anaweza kujishindia Sh Milioni moja kutoka Bayport. Picha kwa Hisani ya Bayport.
  TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services, yenye Makao Makuu yake jijini Dar es Salaam, Tanzania, imezindua tovuti yake ya  www.kopabayport.co.tz, itakayowezesha wateja wake kupata mikopo ya haraka na kwa njia rahisi, huku mteja atakayekopa kwa njia ya mtandao akiweza kushinda jumla ya Sh Milioni moja kutoka kwenye taasisi hii.

  Kwa kupitia tovuti hiyo, watu mbalimbali wanaweza kupata huduma za Bayport, sanjari na kupata mkopo ndani ya saa 24 baada ya kuidhinishwa, huku akijibiwa ombi lake la mkopo, ndani ya masaa mawili tangu alipojisajiri kwa mara ya kwanza.

  Akizungumzia huduma hiyo mpya ya mikopo ya haraka kwa njia ya mtandao jijini Dar es Salaam leo mchana, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema kwamba huduma hiyo sasa itawawezesha wateja wao kukopa mahala popote atakapokuwa, tofauti na awali.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services kitengo cha Huduma kwa Wateja, wakiwajibika wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo ya haraka kwa njia ya mtandao onlinewww.kopabayport.co.tz, jijini Dar es Salaam leo.

  Alisema kuwa lengo la uanzisha kwa tovuti hiyo ya www.kopabayport.co.tzni kutokana na kuweka sera ya mikakati ya kuwapatia huduma hiyo watu wengi iliwaweze kukopa na kujikwamua kiuchumi, ikiwa ni maalum kwa watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni zilizoidhinishwa na Bayport.

  “Bayport sasa imezidi kupiga hatua, kwa sababu mteja wetu hata kama akiwa nyumbani kwake, kwa kupitia huduma yetu hii anaweza kujisajiri na kukopeshwa anachokihitaji kutoka kwetu bila kupata usumbufu wa aina yoyote.
  “Hayani mambo mazuri na naamini ni wakati wa wateja wetu na Watanzania wote kuendelea kuchangamkia huduma zetu za mikopo, ukizingatia ni Bayport pekee inayoweza kukupatia mkopo wa Chagua chochote Bayport italipia, Bima ya Elimu ya Uwapendao, mikopo ya fedha na mingineyo muhimu,” alisema Cheyo.

  Naye Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Mrisho Millao, alisema utaratibu wa kukopa kwa njia ya Internet kutoka Bayport ni mzuri na utarahisisha upatikanaji wa huduma bora kwa wateja wao na Watanzania kwa ujumla.

  “Nimeangalia ni mfumo mzuri na rahisi kwa mteja wa Bayport kupata mikopo ya haraka kwa njia ya mtandao huku ukiwa katika lugha mbili za Kiswahili na Kingereza, huku
  namna ya ushindi wa Sh Milioni moja nao ukiwa ni wa kueleweka, hivyo kila mteja anaweza kushinda kama atakopa kwa njia hii,” alisema Millao.

  Kwa mujibu wa Cheyo, hiyo ni njia rahisi na ya haraka mno inayomuwezesha kumpatia mkopo mteja wao, bila kusumbuka kwenda kwenye tawi kuanza taratibu za kujiunganisha kwenye huduma za mikopo ya taasisi yao.

  Ili mtu aweze kuingia kwenye huduma hiyo, atalazimika kutumia simu yake ya mkononi yenye uwezo wa internet bila kusahau kompyuta, ikiwa hatua rahisi za kumpatia mkopo huo mteja, huku Cheyo akitumia muda huo kuwataka wateja wao na Watanzania kuiunga mkono Bayport ili kujikwamua kiuchumi kutokana na huduma zao za mikopo isiyokuwa na dhamana wala amana.

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa kwa furaha alipowasili uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro Jumapili Machi 8, 2015 kuongoza kilele cha sherehe za Siku ya Wanawake Duniani  iliyoadhimishwa kitaifa mjini humo
   Rais Kikwete akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Mohamed Aziz Abood 
   Rais Kikwete akisalimiana na viongozi wa dini mkoa wa Morogoro
   Rais Kikwete akisalimiana na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez
   Sehemu ya umati uliofurika uwanjani hapo
   Rais Kikwete akiwa meza kuu. Wengine kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro na Mbunge wa Jimbo la Morogoro kusini Mh Innocent Kalogeris, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk Rajab Rutengwe, Waziri Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mhe. Sophia Simba na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez
   Bendi ya Jeshi la Polisi likiongoza maandamano makubwa ya wanawake yakiingia uwanjani
   Rais Kikwete na Meza kuu ikipokea maandamano hayo
   Maandamano
   Kinamama wakisherehekea siku yao
   Rais Kikwete akipungia maandamano
   TTCL wamependeza na miavuli yao.
   Benki ya posta
   Kina baba hawakuwa nyuma


   Msanii Starah Thomas akiimba wimbo maalum akisaidiwa na wanafunzi
   Msanii Peter Msechu akiimba na kucheza na wanafunzi
   Mtoto Miriam Edward akitumbuiza
   Mwanadada hodari  Hazala 'The Ball Juggler' Mohammed akipiga danadana
   Vijana wa Sifa Theatre Troupe wakitumbuiza
   Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk Rajab Rutengwe akisoma utangulizi wa sherehe hizo
   Mwakilishi wa kinamama wajasiriamali wa Morogoro Bi. Emmy Kiula akisoma Risala yao
   Rais Kikwete akipokea risala toka kwa Mwakilishi wa kinamama wajasiriamali wa Morogoro Bi. Emmy Kiula
   Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez akihutubia kwa Kiswahili fasaha
   Rais Kikwete akimpongeza Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez kwa hotuba nzuri, Kushoto ni Waziri Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mhe. Sophia Simba 
   Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Ulaya (EU) Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi pia akihutubia hadhara hiyo kwa Kiswahili fasaha
   Sehemu ya Umati
   Umati wa wakaazi waMorogoro na vitongoji vyake
   Mabalozi wa nchi mbalimbali walihudhuria
   Mabalozi na viongozi wa taasisi mbalimbali zinasohudumia wanawake
   Umati


   Viongozi wa vyama vya siasa wakitambulishwa
   Waziri Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mhe. Sophia Simba akimkabidhi Rais Kikwete tuzo maalum ya Wanawake kwa mchango wake mkubwa wa kujali maslahi yao
   Rais Kikwete akifurhia tuzo yake
   Rais Kikwete akimkabidhi tuzo Celina Ompeshi Kombani  mbunge wa jimbo la Ulanga Mashariki
   Rais Kikwete akimtuza Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe Muhingo Rweyemamu kwa kazi kubwa aliyoifanya kuendeleza elimu ya wasichana alipokuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni
   Mwakilishi wa TAMWA akipokea tuzo kwa kazi nzuri inayofanywa na taasisi hiyo
    Mwakilishi wa TAMWA akipokea tuzo ya pili kwa kazi nzuri inayofanywa na taasisi hiyo

   Tuzo kwa kazi nzuri
   Tuzo kwa masista wanaosaidia kupiga vita ukeketaji 
   Rais Kikwete akihutubia
   Rais Kikwete akifafanua jmbo katika hotuba yake
   Rais Kikwete akiagana na viongozi wa dini
   Baada ya hotuba Rais Kikwete akipiga picha ya pamoja na makundi mbalimbali ya wadu wa Wanawake   Rais Kikwete akitembelea mabanda ya maonesho
   Rais Kikwete akisalimiana na wafanyakazi wa PPF Morogoro
  Rais Kikwete akiongea na mtoto Reuben Boniface mwenye umri wa miaka 9 na manafunzi wa darasa la nne shule ye Elu Children Care
   Rais Kikwete katika banda la WOGE
   Rais Kikwete akikagua banda la Halmashauri ya Mkoa wa Morogoro
  Rais Kikwete akisalimiana na wafanyakazi wa Halmashauri ya Morogoro

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua bei ya mahindi katika soko  la Miembeni mjini Dodoma Machi 8, 2015. Alipita sokoni hapo kukagua upatikanaji wa vyakula. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
  pi2 
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapa maelezo kuhusu kilimo cha zabibu Walimu wa Shule za Kata ya Zuzu, Dodoma waliokwenda shambani kwake Machi 8, 2015 kwa ziara ya kujifunza. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

   Kaimu Mkuu wa Taaluma wa Chuo cha Fedha Chwaka Zanzibar Dkt. Iddi Salum Haji akitoa mafunzo ya Ujasiriamali kwa Wajasiriamali wa Kijiji cha Kitogani kilichopo Wilaya ya Kusini Unguja.(Picha na Miza Othman- Maelezo Zanzibar).
   Kaimu Mkuu wa Idara ya Masomo ya Jumla na Mafunzo Mafupi Zanzibar Nd. Said Mohammed Khamis akitoa ufafanuzi juu ya mafunzo hayo kwa Wajasiriamali wa Kijiji hicho.
   Baadhi ya Wajasiriamali waliohudhuria katika mafunzo ya Ujasiriamali wakisikiliza kwa makini mafunzo hayo.
    Afisa Tawala Wilaya ya Kusini Unguja Bi. Kibibi Mwinyi ambae ndiye Mgeni Rasmi wa kwanza kulia akiwasisitiza Wajasiriamali wa Kijiji cha Kitogani kuyafanyia kazi Mafunzo waliyoyapata  katika Semina hiyo.
   Wakufunzi wa Mafunzo ya Ujasiriamali wakiwa katika picha ya pamoja na Wajasiriamali wa Kijiji hicho.
  Wakufunzi wa Ujasiriamali wakiwa katika picha ya pamoja. (Picha na Miza Othman- Maelezo Zanzibar).


  0 0
 • 03/09/15--10:22: NAFASI ZA KAZI
 • WASAMBAZAJI   DAWA
  Kituo  kinacho  jihusisha  na  tiba asilia  na  huduma  ya  vyakula-lishe  kwa  wenye  kusumbuliwa  na  matatizo  mbalimbali  ya  kiafya, kinatangaza  nafasi   za  kazi  ya  usambazaji  dawa  kwa  wateja  wake  waliopo  katika  maeneo  mbalimbali  ya  jiji  la  Dar  Es  salaam.
  SIFA   ZA  MWOMBAJI :
  1.                       Awe  wa jinsia  ya  kike
  2.                       Elimu  isiyopungua  darasa  la  saba  na  isiyo  zidi  kidato  cha  nne.
  3.                       Awe  msafi, maridadi, mwaminifu  na  anaye  jituma.
  4.                       Awe  anaishi  jijini  Dar  Es  salaam.

  MAJUKUMU   YA  KAZI  :
  Kusambaza  dawa  zetu  kwa wateja  wetu  waliopo  katika  kata  mbalimbali  za  jiji  la  Dar  Es  salaam.
  IDADI   YA   NAFASI  :
  NAFASI   HAMSINI   ( 50  ).
  MALIPO  :
  Shilingi  ELFU  KUMI  KWA  SIKU.
  Andika  maombi  yako  ya  kazi  kupitia  barua  pepe  yetu  ambayo  ni  :

  Maombi  yako  yaelekezwe  kwa   MKURUGENZI  MTENDAJI, NEEMA  RECRUITMENT AGENCY.
  Mwisho  wa  kupokea  maombi  ni  tarehe  21  MACHI  2015.
  Kazi  kuanza  tarehe  30  MARCH  2015

  0 0

  Ukuaji wa Sekta ya TEHAMA umekuwa wa mafanikio na msaada mkubwa katika kuharakisha, kuboresha na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi na kuchangia  kikamilifu katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya Taifa letu. 

  Kwa mfano, wananchi walio wengi sasa wanapata huduma mbalimbali za mtandao kwa kutuma na kupokea pesa; kulipia ankara za maji, umeme na tozo mbalimbali kama vile ada na leseni; na mawasiliano ya simu na intaneti pamoja na elimu mtandao na tiba mtandao.

  Palipo na mafanikio hapakosi changamoto. Pamoja na kwamba tumeshuhudia manufaa na umuhimu wa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika nyanja mbalimbali ikiwemo ya elimu, afya, biashara, miundombinu ya mawasiliano, pia kumekuwepo na changamoto ya matumizi mabaya ya mtandao katika ngazi ya mtu mmoja mmoja, baina ya makundi ya watu na hata kutoka Taifa moja kwenda Taifa lingine kisiasa, kiuchumi, na kiutamaduni.

  Baadhi ya mifano ni pamoja na  suala la wizi wa fedha kwa njia ya mtandao, matukio ya uhalifu kwa kutumia mtandao, uvujaji wa taarifa za siri, upotevu wa haki miliki na matumizi ya saini na ushahidi, mmomonyoko wa maadili, athari za makundi maalumu kama vile watoto na usalama wa miundombinu mbalimbali ya TEHAMA ambapo Serikali imeingia gharama kubwa kuiweka.


  Wakati hayo yakijiri, Kwa sasa kumekua na wimbi kubwa la kurubuni watu kupitia mitandao ambapo majina ya wanasiasa, wanamuziki na wenye majina makubwa yameendelea kutumiaka vibaya katika mitandao ili kufanikisha urubuni wa kuwaibia watu pesa kwa kutumia jina la “VIKOBA” – Chakushangaza zaidi kurasa hizo zinazo onekana zaidi kupitia mitandao yakijamii zinaonekana zimedhaminiwa ili kuweza kusomwa na wengi kitu ambacho  kinapelekea kuonyesha jinsi gani wimbi hili na wahalifu hawa mtandao wamejipanga.


  Watanzania hawanabudi kuwa makini sana na kuwa waangalifu sana wanapo takiwa kuingiza taarifa zao binafsi na wanapo takiwa kufata maelekezo wa kutekeleza miamala kupitia mitandao kwenye vyanzo vyenye utata.


  0 0

   Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa pili kulia), akikabidhi mkataba wa udhamini kwa Meneja wa Bendi ya Walemavu ya Tunaweza, Sixmond Mdeka, katika hafla iliyofanyika kwenye studio ya Ontime Production iliyopo Kijitonyama kwa Ali Maua ‘A’, jijini Dar es Salaam , ambapo Airtel itailipia gharama za kurekodi albamu yao ya muziki. Wanaoshuhudia ni Prodyuza wa studio hiyo, Jaffari Mohamed (kulia) na baadhi ya wanamuziki wa bendi hiyo.

  Waendeleza vipaji vya Walemavu hapa nchini
  • “Tunaweza Band” wawezeshwa kurekodi nyimbo zao mpya.

  Katika kuendeleza shughuli zake za huduma kwa jamii kampuni ya simu za
  mkononi ya Airtel imeendelea kutoa msaada kwa walemavu kupitia kikundi
  cha walemavu kijulikanacho kwa jina la “Tunaweza Band”, kwa
  kuwawezesha kulipia gharama za kurekodi nyimbo zao mpya. Makabidhiano
  ya mkataba huo kati ya kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel na Ontime
  Production yalifanyika katika ofisi za Ontime Production iliyopo
  Kijitonyama kwa Ali Maua ‘A’ jijini Dar Es Salaam.

  Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano Meneja wa Kitengo cha
  Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi, amesema kuwa msaada huo ni
  sehemu ya miradi ya maendeleo ya kijamii ambayo kampuni imeazimia
  kuifanya kulingana na msimamo wa kampuni hiyo wa kuwa karibu na jamiii
  inayowazunguka. 

  “Msaada huu ni sehemu ya azimio tuliloweka la kuwekeza
  katika jamii yetu inayotuzunguka. Watu wanaoishi na ulemavu
  husahaulika katika jamii na hawapati haki zote zinazostahili kwa
  binadamu. Haki za binadamu ni sawa kwa watu wote bila kujali ulemavu
  wao. Kukosa uwezo wa kujihudumia mwenyewe, huleta mateso kwa binadamu
  yeyote yule. Tunafurahi kuwasaidia wenzetu katika jamii hii kwa kuwapa
  uwezo wa kujiongezea kipato kutokana na vipaji walivyonavyo.

  Naye  Meneja wa Bendi ya Walemavu ya Tunaweza, Sixmond Mdeka   alisema
  kuwa amefurahishwa na moyo wa kampuni ya Airtel  kwa kujali walemavu
  hapa nchini kwani wao si wa kwanza kupata msaada huu kutoka Airtel.

  “Nimefurahishwa sana na kitendo cha Airtel kujali walemavu hapa nchini
  na kwa kutusiadia kuongeza vipaji vyetu na vile vile kutuwezesha
  kuongeza kipato chetu kwani baada ya hapa tunauhakika wa kupata
  mikataba ya kurekodi nyimbo zetu nyingine nyingi tu ambazo tunazo.Kwa
  niaba ya  wenzangu wa kikundi cha Tunaweza, napenda kuwashukuru Airtel
  kwa moyo wao wa kujali watu walio katika mazingira magumu, hasa sisi
  walemavu. Msaada huu utatuwezesha na sisi kushirIki katika shughuli
  mbalimbali katika jamii pamoja na kufikia malengo yetu tuliyonayo.

   Mnamo mwezi mmoja uliopita Airtel imewawezesha walemavu wengine kumi
  na tano kuweza kupata mafunzo ya biashara, mtaji na  vibanda vya
  kisasa vya Airtel Money vyenye lengo la kuwawezesha kuwa
  wafanyabiashara wajasiriamali na kuwa mawakala wa huduma ya Airtel
  Money na kutoa huduma mbalimbali ikiwemo kuuza bidhaa za Airtel
  kupitia vibanda hivyo vilivyo katika sehemu mbalimbali jijini Dar es
  Salaam.

  0 0

  Ofisa Mtendaji Masoko wa EATV, Brendansia Kileo (kulia) akifafanua jambo mbele ya wandishi (hawapo pichani), kushoto kwake ni Digital &Branding Manager wa 361 degree, Hurbert Kissas na kulia ni Meneja wa chapa wa vinywaji vikali wa Serengeti Breweries Limited, Shomari Shija.
  Maonyesho ya siku mbili ya Harusi Tanzania maarufu kama ‘Harusi Trade Fair 2015’, yanayotarajiwa kufanyika Machi 13-14 mwaka huu katika ukumbi wa Danken House, uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
   
  Wakiongea na wandishi wa habari  mapema jana Machi 2, wakati wa kutambulisha wadhaamini wakuu wa mwaka huu ambao ni kampuni ya Bia ya Serengeti, kupitia kwa vinywaji vya Baileys ‘Cream with Spirit’ na Johnnie Walker ‘Gold Label’, wandaaji wa maonyesho hayo kampuni ya 361 degree, kupitia kwa Meneja biashara na maendeleo,  Hamis Omary alisema tayari maandalizi hayo yamepamba moto huku washiriki zaidi ya 50, wakitarajiwa kushiriki.
   
  “mwaka huu ni wa sita kwa maonyesho haya. Hivyo tunajivunia mafanikio mbalimbali. Tunashukuru wadhamini wetu kampuni ya bia ya  Serengeti kwa kujitokeza  kudhamini mwaka huu ni faraja kwetu” alisema Hamis Omary.
   
  Aidha, aliwataka watanzania kujitokeza kwa wingi kushuhudia maonyesho hayo kwani ni ya kipekee ambayo yatatoa dira na mwangaza kwa wanaharusi wanaotarajia kuoa, kuoana ikiwemo kupata uzoefu na mipangilio ya shughuli yao ambayo kwa kawaida ni tukio la mara moja katika maisha  ya binadamu.
   
  “Harusi ni tukio zuri, ambalo hutokea mara moja tu, huku likiunganisha familia na jamii pamoja, hivyo nia yetu ni kuwapa maharusi mahitaji yao yoote muhimu kwa pamoja na kwa wakati mmoja, na maonyesho haya ndio sehemu muafaka kwa hilo” alisema Hamis Omary.
   
  Ambapo alisema kuwa, katika maonyesho  hayo wadau wote wa harusi wataonyesha bidhaa zao ambapo kiingilio ni bure kwa watu wote, ila wakati wa maonyesho ya ubunifu wa mavazi ya harusi, yatakuwa na kiingilio cha sh 25,000 kwa kila mtu.
   
  Hamis Omary aliwataja baadhi ya wadau hao ni pamoja na watu wa mapambo (Decorations ), watu wa vyakula (Catering),watu wa matarumbeta, MC, Watengeneza keki, wapamba maharusi na wengine wengi.
   
  Aidha kwa upande wa baadhi ya makampuni ambao ni wadau wa bidhaa za harusi ni pamoja na: 101 STUDIOS, AN NISA ABAYAS, MOIZ HUSEIN STUDIOS, EDNA DESIGN, THE PRINT HOUSE, LOTUS CREATIVE, MANYATA HOUSE OF ACCESSORIES na wengine wengi.
   
  Huku mbunifu wa mitindo, mkubwa ambaye anatamba pia kimataifa, Mustafa Hassanali akitarajiwa kuonyesha mavazi  ya harusi.
   
  Kwa upande wake, Meneja wa chapa ya vinywaji vikali wa kampuni ya Serengeti, Shomari Shija alisema bidhaa zao hizo zenye ubora wa kimataifa, zimekuwa zikipendwa na watu mbalimbali ikiwemo kwenye sherehe hivyo ni muda muafaka kwa watanzania kuendelea kuwaunga mkono na kufurahia muonekano mzuri.
   
  “Kinywaji chetu cha Baileys na Johnnie Walker ni miongoni mwa vinywaji vinavyopendwa sana kwenye harusi mbalimbali. Pia tunaweka chapa ya majina ya wanaharusi kwenye vinywaji vyetu hivyo ni muda muafaka wa kuendelea kutuunga mkono” alisema Shija.
   
  Kwa upande wake, Afisa Masoko Mkuu wa kituo cha televisheni cha EATV, Brendansia Kileo ambao nao ni wadhamini aliwaomba vijana mbalimbali kuendelea kuwaunga mkono kwani kila siku wanatoa vitu vipya ambavyo vinajenga na kutengeneza mustakabali wa maisha yao ikiwemo vipindi bora.
   
  Maonyesho hayo ya Harusi Trade Fair 2015, yanaandaliwa na 361 Degree, huku yakidhaminiwa na kinywaji cha Baileys na Johnnie Walker, East Africa radio/EATV na wengine wengi.
   
  Brand Meneger-Spirit wa Serengeti Breweries Limited, Shomari Shija(mwenye koti jeusi) akifafanua jambo mbele ya wandishi wa habari hawapo pichani) wakati wa utambulisho huo.Meneja wa chapa wa vinywaji vikali wa Serengeti Breweries Limited, Shomari Shija (mwenye koti jeusi) akifafanua jambo mbele ya wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho huo.
   
  Maonyesho haya ya Harusi ambayo hufanyika kila mwaka, huwaleta pamoja wahusika wote wa mambo ya Harusi katika kujenga na kutengeneza mtandao wa kimafanikio baina yao, na ndio maana maonyesho haya yamekuwa ni ya kwanza na ya aina yake Tanzania.
   
  Hivyo ni fursa ya kipekee kwa wenza watarajiwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia namna ya mchakato wa shughuli za harusi zinavyokuwa mwanzo, kati na mwisho.
   
  Ambapo kwa mwaka huu yatapambwa na vitu kama keki, maua, wapiga picha, magauni ya Harusi, bila kusahau mengi na yenye ubunifu katika Harusi.
   
  Ambapo pia kwa maharusi, familia, na wale wote wanaohusika na kamati za Harusi ndio muda muafaka wa kuhudhuria ili kujionea na kujua mengi yahusuyo Harusi na mahitaji yake.
   
  Kwa maelezo zaidi tembelea hapa. http://harusitradefair.com/

  0 0  WAUMINI wa Kikristo waliopata fursa ya kushiriki semina ya neno la Mungu iliyoandaliwa na mtumishi wa Mungu Mwalimu Christopher Mwakasege iliyomalizika jana katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam wamesema wanahamu kubwa na Tamasha la mwaka huu kwa kuwa litakuwa na vitu vya kipekee.

  Wakizungumza leo katika viwanja hivyo, walisema kikubwa ambacho kinaonesha utofauti ni kutimiza miaka 15 tangu kuanza hivyo kuadhimisha miaka hiyo kutakuwa na mambo tofauti yatakayopatikana siku hiyo.

  Waumini hao walisema tamasha hilo ni kubwa hakuna tamasha lingine kubwa kama hilo ambako watanzania pia wanapata nafasi ya kuwaona waimbaji wakubwa wa ndani na nje ambao wamekuwa wakiwasikia tu sauti zao.

  Walisema kuwa kuna njia tofauti za utoaji wa neno la Mungu ambako kwa njia ya uimbaji inawashawishi watu wengi hasa vijana kusikiliza nyimbo na hivyo inakuwa rahisi kumrudia Mungu  hali ambayo inachangia kupungua kwa vitendo viovu.

  “Tunalisubiri kwa hamu kubwa Tamasha la mwaka huu maana linaonekana litakuwa kubwa na tofauti na yaliyopita kwa kweli waaandaji wawe na moyo huohuo wa kutuletea waimbaji mbalimbali wa kutoka nje tunafurahi kuwaona na pia tunapata upako mno tunapowaona wanahubili jukwaani” alisema  mmoja wa mashabiki hao Debora Kaduma.

  0 0  MUIMBAJI  nguli raia wa Afrika Kusini na anayetikisa kwenye muziki wa Injili Afrika, Rebecca Malope ni mmoja wa waimbaji wa Kimataifa waliochomoza kwenye Tamasha la Pasaka linalotarajia kufanyika baadaye mwaka huu hapa Tanzania.

  Kwa mujjibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo Alex Msama  hivi sasa wanaendelea na mchakato  wa maandalizi ya tamasha hilo ambalo linatimiza miaka 15 tangu kuasisiwa kwake.

  Msama alisema sambamba na Malope, Afrika Kusini wanatarajia kutoka waimbaji wengine wawili ambao ni Solly Mahlangu na Keke Phoofolo ambao ni moto wa kuotea mbali. Msama alisema waimbaji hao ni muendelezo wa waimbaji waliokubali kutumbuiza kwenye tamasha hilo ni pamoja na Ephraim Sekeleti, Solomon Mukubwa na wazawa akiwemo Upendo Nkone na Bonny Mwaitege.

  Aidha Msama alisema tamasha la mwaka huu litakuwa ni la aina yake kwa sababu kutakuwa na matukio mengi ambayo yataendana na maadhimisho ya miaka 15 ya Tamasha hilo lililoasisiwa mwaka 2000. 

  “Hivi sasa tunaendelea na mchakato kuelekea Tamasha la Pasaka mwaka huu ambalo litakuwa ni la aina yake kwa sababu tutakuwa na mambo mengi ambayo yatafanana na miaka 15 ya  tamasha letu pendwa linalowalenga wenye uhitaji maalum ambao ni walemavu, yatima na wajane,” alisema Msama.

  Naye Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi, Khamis Pembe alisema wako katika mipango mikubwa ya kufanikisha miaka 15 ya Tamasha la Pasaka ambako wako katika mipangilio ya kuimarisha ulinzi siku hiyo. Pembe  alisema tamasha la mwaka huu litakuwa ni tofauti na yaliyopita kwa kuongeza ukaribu zaidi na jamii yenye uhitaji maalum.


older | 1 | .... | 480 | 481 | (Page 482) | 483 | 484 | .... | 1904 | newer