Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 479 | 480 | (Page 481) | 482 | 483 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akifanya mahojiano na Ephraim Kibonde wa Kipindi cha Maisha ni Nyumba cha Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwenye uzinduzi wa nyumba za makazi za Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria kwenye uzinduzi wa nyumba za makazi za Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
  Michael Chilongani wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwafafanulia jambo wageni waliofika katika uzinduzi wa nyumba za makazi za Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
  Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Maagi akiwafafanulia jambo wageni waliofika katika uzinduzi wa nyumba za makazi za Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
  Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, Abdulkarim Shah akibadilishana mawazo na wageni waliofika katika uzinduzi wa nyumba za makazi za Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
  Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria kwenye uzinduzi wa nyumba za makazi za Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
  Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria kwenye uzinduzi wa nyumba za makazi za Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
  Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria kwenye uzinduzi wa nyumba za makazi za Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
  Sophia Mwema wa Shirika la Nyumba la Taifa akibadilishana mawazo na mmojawapo wa wageni waliofika katika uzinduzi wa nyumba za makazi za Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
  Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria kwenye uzinduzi wa nyumba za makazi za Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
  Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria kwenye uzinduzi wa nyumba za makazi za Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
  Mbunge wa Lushoto, Henry Shekifu akijadiliana jambo na mwenzake kwenye uzinduzi wa nyumba za makazi za Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
  Gibson Mwaigomole wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwafafanulia jambo wageni waliofika katika uzinduzi wa nyumba za makazi za Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
  Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria kwenye uzinduzi wa nyumba za makazi za Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.
  David Shambwe, Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara, David Shambwe akishuhudia namna shughuli hiyo inavyoendelea. Picha zaidi za tukio hili tutawaletea.
  .......................................................................................................................
  TAARIFA YA UUZWAJI WA NYUMBA ZA VICTORIA PLACE, DAR ES SALAAM
  Kwa mara nyingine tena Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo (Ijumaa, 6, Machi, 2015) limezindua rasmi mauzo ya nyumba katika mradi wake mpya wa Victoria, jijini Dar es Salaam. Mradi unatarajiwa kugharimu kiasi cha zaidi ya Sh 11 bilioni mpaka utakapomalizika.
  Mradi huu upo Victoria Kijitonyama, takribani kilomita 7 kutoka Jijini Kati, una nyumba 127 za kuuzwa zilizopo kwenye majengo pacha ya ghorofa 13. Mradi huu uko sehemu yenye huduma zote muhimu za kijamii jijini Dar es Salaam zikiwamo za kiafya, shule, maduka, na masoko. Mbali na huduma katika ujirani, mradi wenyewe utakuwa na maeneo ya biashara katika ghorofa ya chini (ground floor) na ghorofa ya kwanza, ambapo tunatarajia kuwepo na huduma nyingine za kijamii kama vile “Supermarkets”, Migahawa n.k
  Kadhalika, Mradi huu unatarajiwa kuboresha maisha ya wanunuzi wa nyumba hizi kwani umejikamilisha kwa huduma za wakazi,kwa kuwa na maeneo mawili ya , mazoezi (gym), mabwawa ya kuogelea mawili (swimming pools) na eneo la watoto kuchezea.Zaidi ni kwamba, nyumba zipo ndani ya uzio kwa ajili ya usalama watumiaji na kuna maegesho ya magari ya kutosha.
  Mradi una nyumba 127 tu zinazouzwa, zenye ukubwa tofauti, idadi ya vyumba tofauti na bei tofauti. Nyumba hizi zina vyumba kuanzia viwili hadi vinne, na bei zake zinaanzia Tshs165,150,000/= hadi 306,445,000/= kabla ya kodi ya Ongezeko la thamani(VAT). Ukubwa wa nyumba unaanzia mita za mraba 90 hadi 167. Mbali na vyumba vya kulala, kila nyumba ina jiko kubwa la kisasa, choo cha pamoja na eneo la kufulia na kuanikia nguo.
  Sifa za ziada za mradi huu ni kuwa na eneo maalum la kukusanyia taka, sehemu iliyotengwa maalum kwaajili ya kufanyia mazoezi, bwawa la kuogelea na eneo kubwa la ziada la maegesho ya magari.
  Nyumba hizi ni Bora na za Kisasa. Tunawahamasisha na kuwakaribisha watanzania wote walio nchini na walio nje ya nchi, wafanye mawasiliano na makao makuu ya shirika, ofisi zetu za mikoa, au kupitia barua pepe na kukamilisha taratibu mapema kwa ajili ya kuweza kuingia kwenye mchakato ulio wazi wa manunuzi.

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM,ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania mapema leo asubuhi katika ukumbi wa White House,mjini Dodoma.Ndugu Kinana amewataka wasomi hasa wanafunzi wa vyuo vukuu nchini kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za juu za chama hicho.

  Kinana amesema kuwa chama cha mapinduzi CCM kimejipanga kutumia vijana hasa wasomi kwa kuleta changamoto mpya ndani ya chama hicho,ambapo amewatoa hofu ya kushiriki kwenye siasa hata kama hawana fedha na kuwa kujaribu si kushindwa na watakuwa wamejitambulisha kwenye majukwaa ya siasa na kutoa mifano kwa baadhi ya vijana ambao walijaribu na siku ya mwisho waliibuka washindi kwa kuwabwaga baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho na serikalini wakiwemo madiwani.
   Baadhi ya Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania wakishangilia jambo ndani ya ukumbi wa wa White House kabla ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kuzungumza nao mambo mbalimbali.
   Sehemu ya meza kuu.
  13
  Viongozi wa kikundi cha vijana wasomi cha New Generation Network cha mjini Dodoma  wakionyesha cheki ya shilingi milioni 10 waliyokabidhiwa na afisa vijana mkoa wa Dodoma Tumsifu Mwasamale  kutoka mfuko wa vijana  wa  Wizara ya Habari, Michezo, Utamaduni na Maendeleo ya vijana.  Huku Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na viongozi wengine wakipiga makofi.
   Mkutano ukiendelea ndani ya ukumbi wa White House mjini Mdodoma.
  Pichani kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mh Chiku Galawa akiwa pamoja na Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Dodoma mjini,Mh.Bi Fatuma Mwenda pamoja na Mkuu mpya wa Wilaya ya Dodoma mjini,Mh.Betty Mkwassa wakisubiri kumpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana nje ya ukumbi wa White House mapema leo asubuhi.Nduugu Kinana anaendelea na ziara yake wilaya ya Dodoma mjini na vitongoji vyake.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akisalimiana na Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Dodoma mjini,Mh.Bi Fatuma Mwenda,pichani kati anaeshuhudia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mh.Chiku Galawa.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na Mkuu mpya wa Wilaya ya Dodoma,Mh.Betty Mkwassa.

  PICHA NA MICHUZI JR-DODOMA.

  0 0

   *Waziri Mkuu aomba Watanzania wamuunge mkono

  SERIKALI ya Japan imetoa msaada wa dola za Marekani 90,286 sawa na sh. milioni 160/- kusaidia ujenzi wa shule ya awali kwenye shule ya msingi Kakuni, iliyopo kijiji cha Kibaoni, wilayani Mlele, mkoa wa Katavi.

  Japan imetoa msaada huo ikiwa ni sehemu ya mchango wake katika shule mpya ya msingi Kakuni ambayo Waziri Mkuu Mizengo Pinda alianzisha wazo la kuijenga kama njia ya kumshukuru Mungu na kuwashukuru wananchi waliosaidia kumfikisha hapo alipo. Waziri Mkuu Pinda alisoma darasa la kwanza hadi la nne katika shule ya msingi Kakuni mwaka 1957 hadi 1960.

  Akizungumza kwenye hafla fupi ya utiaji saini mkataba wa msaada huo uliofanyika jana jioni (Ijumaa, Machi 6, 2015) kwenye ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni na kushuhudiwa na Waziri Mkuu mwenyewe, Kaimu Balozi wa Japan, Bw. Kazuyoshi Matsunaga alisema Serikali yake imeamua kutoa msaada huo kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995 inayosema elimu ni haki ya kila mtoto.

  Alisema sera ya elimu iliongezewa uzito na Mpango wa Kuendeleza Elimu ya Msingi Awamu ya Pili (PEDP II) ambao unasisitiza kwamba kila shule ya msingi ni lazima iwe na shule yake ya awali kama njia thabiti ya kuhimiza upatikanaji wa elimu ya awali hapa nchini.

  “Mojawapo ya changamoto inayoikabili sekta ya elimu hapa Tanzania ni kukosekana kwa mazingira mazuri ya shule katika hatua za mwanzo za makuzi ya watoto wengi. Kwa mfano, kata ya Kibaoni ina shule tatu za msingi ambazo ni Kakuni, Ilalangulu na Milumba lakini hakuna shule ya awali hata moja, jambo ambalo hufanya watoto wote walundikane kwenye darasa mojawapo kwenye shule ya msingi Kakuni,” alisema.


  Alisema anaamini mchango walioutoa utasaidia kuboresha viwango vya elimu ya awali katika kata ya Kibaoni. Mchango huo wa sh. milioni 160/- unatarajiwa kutumika kujenga madarasa mawili ya awali, ofisi ya walimu wa shule hiyo, eneo la michezo, bwalo dogo la chakula na jiko. “Natambua kuwa ujenzi wa shule peke yake hauinui kiwango cha elimu, bali kuongeza uandikishaji wa watoto, kuongeza walimu na kuboresha maslahi yao ni chachu nyingine muhimu katika kuinua kiwango cha elimu,” alisema.

  Utiaji saini huo ulifanywa na Kaimu Balozi huyo pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mlele, Bw. William Mwakalambile. Wengine waliokuwepo ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dk. Ibrahim Msengi na Katibu Tawala wa mkoa huo, Mhandisi Emmanuel Kalobelo.

  Akizungumza katika hafla hiyo fupi, Waziri Mkuu Pinda aliishukuru Serikali ya Japan kwa msaada huo ambao alisema utachangia kwa kiasi kikubwa kuitimiza ndoto yake aliyokuwa nayo ya kuisaidia jamii iliyomsomesha.

  “Wazo la ujenzi wa shule mpya ya msingi Kibaoni lilitokana na ukweli kwamba nilisoma na kumaliza kwenye shule hii ya Kakuni. Nikiwa ni mtumishi wa Serikali, ni Mbunge na sasa hivi ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nilijiuliza hivi shule hii ninaweza kuiacha hivi hivi? Hakuna jambo ambalo naweza kufanya na kuisaidia jamii ya wanakijiji na kata nzima ya kwetu?,” alisema Waziri Mkuu katika mada fupi aliyoiwasilisha jana.

  “Niliwaza pia kufanya ukarabati lakini nikabaini kuwa eneo la shule halitoshi kwani idadi ya wanafunzi waliopo ni kubwa kuliko eneo la shule hiyo. Hivi sasa shule ina wanafunzi wapatao 770. Madarasa yamechakaa na nyumba za walimu pia zimechakaa,” alisema.

  Alisema alipeleka maombi kwenye Serikali ya Kijiji cha Kibaoni ambayo ilitoa ekari 65 kutoka eneo lililokuwa ni mashamba ya bega kwa bega na kisha akawasilisha ombi maalum kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda (wakati huo) ambayo hivi sasa ni Mlele ili kuomba ushauri na usimamizi wa jumla katika kuisimamia ndoto hiyo.

  Alisema aliishirikisha Halmashauri kuandaa michoro inayotolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na OWM-TAMISEMI, na kuwataka waandae mapendekezo ya bajeti kwa kuzingatia taratibu za kiuhandisi na ujenzi na makisio ya awali yalikuwa sh. bilioni 1.3/-.

  Alisema alipeleka barua kuomba michango kwa watu binafsi, mashirika ya umma, taasisi, mabenki na balozi mbalimbali ambao hadi sasa wamekwishamchangia sh. milioni 816.6 na dola za Marekani 210,000 na kwamba hadi sasa kwenye akaunti ya ujenzi amebakiza kiasi cha sh. milioni 182 na dola za Marekani 60,189.

  “Katika kuanza zoezi la kukusanya fedha mwaka 2013, Ubalozi wa China ulikuwa wa kwanza kuitikia maombi yetu na ulitoa Dola za Marekani 200,000 ambazo zilikuwa sawa na sh. milioni 320. Pia ubalozi ukamteua mkandarasi wa barabara ya kutoka Nkasi – Kibaoni – Mpanda asaidie katika ujenzi wa shule ili kupunguza gharama,” alisema.

  Hadi sasa majengo yaliyokamilika ni madarasa 14, jengo la utawala lenye ofisi za walimu na maktaba mbili (wanafunzi na walimu), jengo la TEHAMA la wanafunzi lenye darasa moja, ukumbi mdogo na ofisi ya mwalimu na jengo moja la choo lenye matundu 48. Pia ujenzi wa nyumba sita za walimu uko kwenye hatua ya msingi. Nyumba hizo zinajengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

  Waziri Mkuu aliwaomba Watanzania watakaoguswa na jambo hili wamsaidie kutimiza ndoto yake kwani bado anakabiliwa na kazi ya kuweka umeme, maji, kujenga nyumba nane za walimu, choo kingine chenye matundu 48, bwalo na jiko, karakana nne za ufundi, vitabu na TABLETS za wanafunzi, kituo cha walimu cha mafunzo ya muda mfupi na utunzaji taarifa (Resource Centre), viwanja vya michezo vya kisasa vinavyozingatia michezo yote, mfumo wa uvunaji maji ya mvua, mfumo wa maji safi na maji taka, nyumba mbili za walinzi na uzio wa shule.

  Alitaja vitu vingine ambavyo bado vinahitaji kuchangiwa ni meza za walimu – za ofisini na darasani, viti vya walimu – vya ofisini na darasani, madawati ya shule ya msingi na ya awali, meza na viti vya maktaba zote mbili, meza na viti vya bwalo – shule ya msingi na shule ya awali.

  (mwisho)
  IMETOLEWA NA
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S.  L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM
  JUMAMOSI, MACHI 7, 2015.

  0 0

  UT1 
  Kaimu Mkuu wa Idara ya Utamaduni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Afisa Bw. Habibu Msami akimkaribisha Mgeni rasmi kufunga kikao kazi cha kumi cha sekta ya Utamaduni jana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mgeni rasmi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi.
  UT2 
  Mgeni rasmi wakati wa kufunga kikao kazi cha sekta ya utamaduni akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi akizungumza na wadau wa utamaduni kuwapongeza kuwa na ushirikiano katika kutekeleza majukumu yao. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Utamaduni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Afisa Bw. Habibu Msami
  UT3 
  Afisa Utamaduni kutoka Kiteto Bibi. Bihawa Masawika akitoa neno la shukrani wakati wa kufunga kikao kazi cha kumi cha sekta ya Utamaduni jana Jijini Dar es Salaam.
  UT4 
  Afisa Utamaduni kutoka Wilaya ya Mbogwe Mkoa wa Geita Bw. Athanas Michael akiimba shairi la kuhamasisha kudumisha Utamaduni wakati wa kufunga kikao kazi cha kumi cha sekta ya Utamaduni jana Jijini Dar es Salaam.
  UT5 
  Mshairi kutoka Chama cha Umoja wa Washairi Tanzania (UWASHATA) Bw. Issa Amiri Kilimo akiimba shairi la kuipongeza Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa kushirikiana na wadau wa utamaduni kuhamasisha masuala ya utamaduni wakati wa kufunga kikao kazi cha kumi cha sekta ya Utamaduni jana Jijini Dar es Salaam.

  UT6 
  Baadhi ya Maafisa Utamaduni kutoka Wilaya mbalimbali za Tanzania Bara wakifuatilia matukio yaliyokua yakiendelea wakati wa kufunga kikao kazi cha kumi cha sekta ya Utamaduni jana Jijini Dar es Salaam.(Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo)……………………………………………………………..
  Na: Genofeva Matemu – Maelezo
  Maafisa Utamaduni na wadau wa utamaduni wametakiwa kuuenzi utamaduni wa watanzania kwa kutekeleza na kusimamia utamaduni ulio sahihi na kuacha kuiga tamaduni zisizokuwa zetu.Rai hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi alipokua akifunga kikao kazi cha kumi cha Maafisa Utamaduni kutoka Halmashauri zote Tanzania Bara.

  Bw. Mushi amesema kuwa kikao kazi hicho kilichosimamia kauli mbiu isemayo Fani za Sanaa zielimishe Umma Maudhui ya Katiba pendekezwa kimefanyika wakati muafaka hasa ukizingatia taifa lipo kwenye hatua ya kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ambalo litatumika pia kupigia kura katiba pendekezwa.

  “Sanaa ni shughuli pana kwa kuwa inaweza kufikisha ujumbe kwa haraka katika jamii hasa kwa kutumia fani mbalimbali kama muziki, ngojera, ngoma, maigizo na kadhalika hivyo kwa kupitia fani za Sanaa Umma utaelewa maudhui ya katiba pendekezwa na kufanya maamuzi sahihi ya kuipigia kura katiba pendekezwa”, alisema Bw. Mushi.

  Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Idara ya Utamaduni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Afisa Utamaduni Bw. Habibu Msami amesema kuwa kikao kazi cha kumi cha Sekta ya Utamaduni kimekuwa na mafanikio chanya kwani washiriki wamepata fursa ya kujadili kwa kina masuala mtambuko yanayoikabili sekta hiyo.

  “Ni hakika kuwa tutakapotoka hapa tutakua mfano mzuri katika Halmashauri na Asasi zetu kwa kuzingatia mambo ya msingi na kuhakikisha tunautetea, tunaulinda na kuuendeleza utamaduni wetu kwa ajili ya ujenzi wa Taifa”, alisema Bw. Msami.

  Naye Afisa Utamaduni kutoka Kiteto Bibi. Bihawa Masawika amesema kuwa kikao kazi cha sekta ya utamaduni kimewawezesha kupata maarifa yatakayowawezesha kuwa wahamasishaji wakubwa na kuwa chachu na mabalozi wazuri katika kutekeleza na kuendeleza masuala ya utamaduni nchini.

  0 0


  pi2
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Kaimu Balozi wa Japan Nchini, Kazuyoshi Matsunaga   baada ya kushuhudi utiaji saini wa makubaliano ya Japan ya msaada Japan wa shilingi milioni 160    kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali ya Kakuni wilayani Mlele Machi 6, 2015 kweye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  pi3
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akiwa katika picha ya pamoja  na Kaimu Balozi wa Japan nchini, Kazuyoshi Matsunaga (kulia kwake) baada ya kushuhudi utiaji saini wa makubaliano ya  msaada wa  Japan wa  shilingi milioni 160    kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali ya Kakuni wilayani Mlele Machi 6, 2015 kweye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa katavi, Dkt. Ibrahim Mzengi na wapili kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa huo, Mhandisi Kalobelo. Wapili kulia ni Kaimu  Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mlele, William Mwakalambile.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  ……………………………………………………………………
  *Waziri Mkuu aomba Watanzania wamuunge mkono
  SERIKALI ya Japan imetoa msaada wa dola za Marekani 90,286 sawa na sh. milioni 160/- kusaidia ujenzi wa shule ya awali kwenye shule ya msingi Kakuni, iliyopo kijiji cha Kibaoni, wilayani Mlele, mkoa wa Katavi.

  Japan imetoa msaada huo ikiwa ni sehemu ya mchango wake katika shule mpya ya msingi Kakuni ambayo Waziri Mkuu Mizengo Pinda alianzisha wazo la kuijenga kama njia ya kumshukuru Mungu na kuwashukuru wananchi waliosaidia kumfikisha hapo alipo. Waziri Mkuu Pinda alisoma darasa la kwanza hadi la nne katika shule ya msingi Kakuni mwaka 1957 hadi 1960.

  Akizungumza kwenye hafla fupi ya utiaji saini mkataba wa msaada huo uliofanyika jana jioni (Ijumaa, Machi 6, 2015) kwenye ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni na kushuhudiwa na Waziri Mkuu mwenyewe, Kaimu Balozi wa Japan, Bw. Kazuyoshi Matsunaga alisema Serikali yake imeamua kutoa msaada huo kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995 inayosema elimu ni haki ya kila mtoto.

  Alisema sera ya elimu iliongezewa uzito na Mpango wa Kuendeleza Elimu ya Msingi Awamu ya Pili (PEDP II) ambao unasisitiza kwamba kila shule ya msingi ni lazima iwe na shule yake ya awali kama njia thabiti ya kuhimiza upatikanaji wa elimu ya awali hapa nchini.

  “Mojawapo ya changamoto inayoikabili sekta ya elimu hapa Tanzania ni kukosekana kwa mazingira mazuri ya shule katika hatua za mwanzo za makuzi ya watoto wengi. Kwa mfano, kata ya Kibaoni ina shule tatu za msingi ambazo ni Kakuni, Ilalangulu na Milumba lakini hakuna shule ya awali hata moja, jambo ambalo hufanya watoto wote walundikane kwenye darasa mojawapo kwenye shule ya msingi Kakuni,” alisema.

  Alisema anaamini mchango walioutoa utasaidia kuboresha viwango vya elimu ya awali katika kata ya Kibaoni. Mchango huo wa sh. milioni 160/- unatarajiwa kutumika kujenga madarasa mawili ya awali, ofisi ya walimu wa shule hiyo, eneo la michezo, bwalo dogo la chakula na jiko. “Natambua kuwa ujenzi wa shule peke yake hauinui kiwango cha elimu, bali kuongeza uandikishaji wa watoto, kuongeza walimu na kuboresha maslahi yao ni chachu nyingine muhimu katika kuinua kiwango cha elimu,” alisema.

  Utiaji saini huo ulifanywa na Kaimu Balozi huyo pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mlele, Bw. William Mwakalambile. Wengine waliokuwepo ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dk. Ibrahim Msengi na Katibu Tawala wa mkoa huo, Mhandisi Emmanuel Kalobelo.
  Akizungumza katika hafla hiyo fupi, Waziri Mkuu Pinda aliishukuru Serikali ya Japan kwa msaada huo ambao alisema utachangia kwa kiasi kikubwa kuitimiza ndoto yake aliyokuwa nayo ya kuisaidia jamii iliyomsomesha.

  “Wazo la ujenzi wa shule mpya ya msingi Kibaoni lilitokana na ukweli kwamba nilisoma na kumaliza kwenye shule hii ya Kakuni. Nikiwa ni mtumishi wa Serikali, ni Mbunge na sasa hivi ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nilijiuliza hivi shule hii ninaweza kuiacha hivi hivi? Hakuna jambo ambalo naweza kufanya na kuisaidia jamii ya wanakijiji na kata nzima ya kwetu?,” alisema Waziri Mkuu katika mada fupi aliyoiwasilisha jana.

  “Niliwaza pia kufanya ukarabati lakini nikabaini kuwa eneo la shule halitoshi kwani idadi ya wanafunzi waliopo ni kubwa kuliko eneo la shule hiyo. Hivi sasa shule ina wanafunzi wapatao 770. Madarasa yamechakaa na nyumba za walimu pia zimechakaa,” alisema.

  Alisema alipeleka maombi kwenye Serikali ya Kijiji cha Kibaoni ambayo ilitoa ekari 65 kutoka eneo lililokuwa ni mashamba ya bega kwa bega na kisha akawasilisha ombi maalum kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda (wakati huo) ambayo hivi sasa ni Mlele ili kuomba ushauri na usimamizi wa jumla katika kuisimamia ndoto hiyo.

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Paul Makonda baada ya kuwasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni leo Machi 7, 2015 akitokea Kigali Rwanda, alikohudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kati ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe Sophia Mjema. PICHA NA IKULU
   Mwenyekiti wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea kwa furaha  shahada la maua baada ya kuwasili Kigali, Rwanda, tayari kwa mkutano  na viongozi wenzake wa Jumiya hiyo katika mkutano wa tisa wa wakuu wa nchi hizo kujadili miradi iliyoko katika Ukanda wa Kaskazini (Northern Corridor Integration Projects)  katika Hoteli ya Serena mjini Kigali. 
  Mkutano wa leo pia umehudhuriwa na wakuu wa nchi za Kenya, Uganda na wenyeji Rwanda. Mbali na nchi hizo na mbali na Tanzania, nchi za Burundi na Sudan Kusini pia zilialikwa kuhudhuria mkutano huo. Mkutano huo ni ulijadili hatua za utekelezaji wa miradi mbali mbali iliyokubaliwa kulingana na maelekezo yaliyotolewa katika mkutano wa nane wa namna hiyo uliofanyika Nairobi, Kenya, Desemba 11, mwaka jana, 2014.
   Mwenyekiti wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na mwenyeji wake Rais Paul Kagame wa Rwanda kabla ya kuanza kwa mkutano wa tisa wa wakuu wa nchi hizo kujadili miradi iliyoko katika Ukanda wa Kaskazini (Northern Corridor Integration Projects)  katika Hoteli ya Serena mjini Kigali. 
   Mwenyekiti wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi wenzake wa Jumiya hiyo katika mkutano wa tisa wa wakuu wa nchi hizo kujadili miradi iliyoko katika Ukanda wa Kaskazini (Northern Corridor Integration Projects)  katika Hoteli ya Serena mjini Kigali..


  Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame amesema kuwa hatua ya Mwenyekiti wa Nchi Wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuhudhuria Mkutano wa Tisa wa Nchi Zilizoungana Kutekeleza Miradi ya Miundombinu Ukanda wa Kaskazini za Northern Corridor Projects ni hatua muhimu katika kufungua utekelezaji wa miradi ya miundomninu katika kanda nyingine za EAC.

  Aidha, Rais Kagame amemshukuru Rais Kikwete kwa uamuzi wake kuhudhuria Mkutano huo uliofanyika leo, Jumamosi, Machi 7, 2015, katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena mjini Kigali, Rwanda. Rais Kikwete amefanya ziara hiyo ya siku moja kuhudhuria Mkutano huo kwa mwaliko wa Rais Kagame.

  Naye Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema kuwa ni jambo la kufurahisha kwamba Rais Kikwete ameweza kuhudhuria Mkutano wa leo, kwa sababu sasa njia imefunguka kuanza kazi ya utekelezaji wa miradi kwenye Ukanda wa Kati wa Central Corridor unaokatisha katikati ya Tanzania.

  Marais Kagame na Kenyatta walikuwa wanazungumza wakati wa hotuba za ufunguzi za Mkutano huo uliofanyika kwa kiasi cha saa mbili unusu mara baada ya Rais Kikwete kuwasili Kigali akitokea Dar es Salaam kiasi cha saa sita mchana.
  Akifungua Mkutano huo, Rais Kagame alisema: “Nawashukuru waheshimiwa marais wote kwa kuja. Lakini hasa hasa, namshukuru sana mwenyekiti wetu wa EAC Rais Kikwete kwa kupata muda wa kuja kujiunga nasi katika mkutano huu.”

  Aliongeza Rais Kagame huku makofi yakiendelea kumkaribisha na kumshangilia Rais Kikwete: “Kuwepo kwake hapa leo, kunaongeza matumaini kuwa miradi mbali mbali na mingi zaidi katika kanda mbali mbali za nchi zetu wanachama wa EAC, sasa inaweza kutekelezwa kwa haraka zaidi. Nakushukuru sana Mheshimiwa Rais.”
  Mbali na Marais Kikwete, Kagame na Kenyatta, Mkutano wa leo pia umehudhuriwa na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini, Makamu wa Rais wa Pili wa Burundi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia.

  Nchi za Kenya, Uganda,Rwanda na Sudan Kusini ndizo wanachama wa Northern Corridor na kwenye mkutano wa leo, Burundi pia imetangaza kuwa imeamua kuwa mshiriki kamili wa mikutano ya Ukanda huo badala ya kuwa msikilizaji kwa muda mrefu.

  Akizungumza katika Mkutano huo, Rais Kenyatta amesema: “Tunafurahi sana kwamba Mwenyekiti wetu wa EAC yuko nasi leo kwa sababu uwepo wake utaongeza msukumo wa kutuwezesha kuanza utekelezaji wa miradi mingine hasa katika Ukanda wa Kati. Tanzania ina mengi kuchangia katika jambo hilo. Kwa mfano, umeme mwingi ambao utaanza kuzalishwa na Tanzania mwaka huu, unahitajika kwa nchi zote za EAC na Northern Corridor.”

  Rais Kikwete ambaye alikuwa msikilizaji tu kwa sababu Tanzania inaendelea kuwa mwanachama wa EAC bila kuwa mshirika wa Northern Corridor amezugumza kwa ufupi tu akisema kuwa kwa sababu yeye ni mwalikwa na msikilizaji asingeweza kusema mengi.
  Amewaambia viongozi wenzake: “Nakushukuru Rais Kagame kwa kunialika. Kama unavyojua, mimi ni msikilizaji tu na hivyo siwezi kusema sana. Lakini napenda kuwapongezeni nyote kwa kazi mnayoifanya. Sote tunajua kuwa hakuna utengamano bila kuendeleza miundombinu.”

  Ameongeza Rais Kikwete: “Kinachoendelea kule Northern Corridor kitasaidia sana katika mawazo na utekelezaji wa kazi ambayo tunajiandaa kuianza kwenye Ukanda wa Kati. Nawatakieni mafanikio zaidi na kasi ya Mwenyeji Mungu katika utekelezaji wa miradi yenu.”

  Chini ya Northern Corridor nchi hizo zimebuni miradi 14, ambayo baadhi yao imeanza kutekelezwa ikiwa ni pamoja na kuanzisha visa moja ya kusafiria ya watalii. Nchi hizo ziliunda kundi hilo mwaka mmoja na miezi tisa iliyopita na wakuu wa nchi wanachama hukutana kila baada ya miezi miwili kwa mashauriano na maamuzi.
  Rais kikwete amerejea nyumbani usiku wa leo baada ya kumalizika kwa Mkutano huo.
   

  0 0

  ???????????????????????????????
  Wafanyakazi wa kampuni ya Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha wakiwa katika picha ya pamoja jana katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kitaaluma ili waweze kuandika habari za kuboresha maisha ya jamii kwa kupata maendeleo kuelekea uchaguzi mkuu,mafunzo hayo yanaendeshwa na shirika lisilo la kiserikali la BBC Media Action, aliyevalia shati la blue ni mkufunzi mwandamizi Pendael Omari wa shirika hilo(Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
  ???????????????????????????????
  Mkufunzi mwandamizi Pendael Omari wa shirika lisilo la kiserikali la BBC Media Action akiwa anatoa ufafanuzi katika mafunzo hayo yaliyokuwa yakifanyika katika ofisi za Radio 5,mafunzo hayo yalidumu kwa takribani wiki mbili
  ???????????????????????????????
  Mtangazaji maarufu wa kituo hicho Ernest Matundiro a.k.a Prince de la ville kushoto akiwa anaandika vipengele muhimu katika uandishi wa habari,kulia ni Mhariri wa kituo hicho Monica Nangu.
  ???????????????????????????????
  Msimamizi mkuu wa vipindi vya Radio 5  kulia Mathew Philip akiwa anafatilia mafunzo kwa ukaribu zaidia,kushoto ni mtangazaji wa kituo hicho Wilberd Kiwale
  ???????????????????????????????
  Mkufunzi mwandamizi Pendael Omari akiwa anatoa ufafanuzi kwa Mhariri Mkuu Philip Magesse katika mafunzo hayo jana
  ???????????????????????????????
  Mtangazaji wa kituo hicho Yakubu Simba
  ???????????????????????????????
  Mtangazaji machachari wa kituo hicho Godfrey Thomas a.k.a GT
  ???????????????????????????????
  Mmiliki wa mtandao wa kijamii wa http://jamiiblog.co.tz/ Pamela Mollel akiwa anafanya mahojiano na mkuu wa vipindi vya Radio 5  Mathew Philip kuhusu mafunzo hayo
  ???????????????????????????????
  Mtangazaji wa kituo hicho Clara Moita wakiwa katika majadiliano na mkuu wa vipindi vya Radio 5 Mathew Philip
  ???????????????????????????????
  Wafanyakazi wa Radio 5 katika pozi

  Wafanyakazi wa Radio 5 jijini A rusha wamepatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kitaaluma ili waweze kuandika habari za kuboresha maisha ya jamii kwa kupata maendeleo kuelekea uchaguzi mkuu,mafunzo hayo yanaendeshwa na shirika lisilo la kiserikali la BBC Media Action,

  Akizungumza mapema jana katika mafunzo hayo Mkufunzi mwandamizi Pendael Omari wa shirika lisilo la kiserikali la BBC Media Action alisema kuwa lengo la kufanya mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa kitaaluma pindi wanapokuwa katika kazi zao

  Alisema kuwa mafunzo hayo yatawezesha pia upatikanaji wa utawala bora kwa kuwa vyombo vya habari vitaelimisha wananchi umuhimu wa kuchagua viongozi watakaoleta maendeleo

  Kwa  upande wake Msimamizi mkuu wa vipindi vya radio hiyo  Mathew Philip  alisema kuwa mafunzo hayo yamewajengea uwezo wa kufanya kazi kwa kuwa walikuwa wakifanya mafunzo kwa vitendo zaidi 

  Pia alisema kuwa kupitia mafunzo hayo wamepata ufahamu wa namna ya kutafuta habari za kupigia kura maoni pamoja na uchaguzi mkuu bila upendeleo kwa kumpa msikilizaji nafasi ya kusikika na kumpa elimu

  Mafunzo hayo yalifanyika katika ofisi za radio 5 kwa muda wa wiki mbili 
  (Habari na Picha Pamela Mollel wa jamiiblog)

  0 0

    Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimpa zawadi maalum mwanafunzi Ali Hemed Ali.
   Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi zawadi iliyotolewa na wanafunzi wa Mahusiano ya Kimataifa Mwalim Fakih Kombo Faki katika sherehe za mahafali ya saba ya Chuo cha Utawala wa Umma Zanzibar.
   Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwahutubia wahitimu wa kada tofauti wa Chuo cha Utawala wa Umma Zanzibar. Sherehe hiyo imefanyika Tunguu Wilaya ya kati Unguja.
  Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi (wakatikati) waliokaa katika picha ya pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri zaizi Chuoni hapo.  (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
    Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipoke mandamano ya wahitimu wa kada tofauti waliomaliza mafunzo yao ya Diploma katika Chuo cha Utawala wa Umma Zanzibar.
   Mwanafunzi Mbarouk Kheir Othman akisoma risala ya wanafunzi katika sherehe za mahafali ya saba ya Chuo cha Chuo cha Utawala wa Umma Zanzibar.
   Wahitimu wa kada ya mahusiano ya kimataifa wakimsikiliza Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipokuwa akiwahutubia mara baada ya kuwatunuku vyeti katika sherehe za mahafali ya saba ya Chuo hicho.
    Baadhi ya wageni walikwa katika sherehe hizo.


  0 0

  pi4 
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na viongozi wa mkoa wa Dodoma bada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Februari 7, 2015. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Galawa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

  DI1 
  Mkuu wa Wilaya ya Mjini Magharibi Bw.Ayoub Mohamed Mahmoud akiongea na Viongozi mbalimbali wa Dini na kuwataka kuhubiri amani na utulivu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea upigaji kura ya maonikwa Katiba Inayopendekezwa pamoja uchaguzi Mkuu
  DI3 
  Mbunge wa WAWI kupitia chama cha wananchi CUF Mh. Hamad Rashid Mohamed akiongea na viongozi wa Dini mbalimbali na kuwaasa kuisoma, kuielewa Katiba Inayopendekezwa na kuacha kupotoshwa kwa kusomewa vipengele vya Katiba hiyo bila kupewa ufafanuzi, wakati wa mkutano ulioratibiwa na Kamati ya Amani na Utulivu Tanzania kushirikisha viongozi wa Dini leo Zanzibar.
  DI4Mwenyekiti wa Kamati ya Amani na utulivu Tanzania Sheikh Noman Thabit Jongo akiwaeleza viongozi wa Dini mbalimbali suala la amani na utulivu katika kuelekea katika kuipigia kura ya maoni Katiba Inyopendekezwa na kuwaasa kuwaelimisha waumini wao juu ya ubora wa Katiba Inayopendekezwa kwani imegusa makundi yote katika Jamii
  DI5 
  Katibu wa Kamati ya Amani na utulivu Tanzania Padri. Damas Mfoi akiongea katika mkutano wa Kamati ya Amani na Viongozi wa Dini mbalimbali Zanzibar na kuwaasa kusambaza ujumbe wa Amani na kuepuka mambo yoyote yatakayoashiria uvunjifu wa amani hasa katika kipindi hiki Taifa likielekea katika Mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya na Uchaguzi Mkuu.
  DI6 
  Baadhi ya Viongozi mbalimbali wa Dini Zanzibar wakifuatilia Mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika Mkutano huo
  DI7 
  Mmoja ya Mjumbe wa Mkutano akifanya rejea katika Katiba Inayopendekezwa wakati wa uwasilishwaji wa Mada katika Mkutano huo.(PICHA NA HASSAN SILAYO)

  …………………………………………………………………………..
  Na Hassan Silayo.

  Viongozi wa Dini nchini wameaswa kuhubiri suala amani na utulivu nchini hasa katika kipindi hiki taifa likielekea upatikanaji wa Katiba Mpya na Uchaguzi Mkuu.Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Mjini Magharibi Bw. Ayoub Mohamed Mahmoud wakati wa mkutano wa Kamati ya amani Tanzania na Viongozi wa Dini Mbalimbali leo Zanzibar.

  Bw. Ayoub alisema kuwa suala la amani na utulivu linamhusu kila mtu kwenye jamii na Taifa kwa ujumla hivyo ni budi kuepuka vishawishi vya uvunjifu wa amani hasa katika wakati huu wa kuelekea upatikanaji wa Katiba Mpya na Uchaguzi Mkuu.

  “ kama tunavyofahamu sasa taifa linaelekea katika mambo makubwa mawili ya upatikaji wa Katiba Mpya na Uchaguzi Mkuu hivyo ninyi kama viongozi wa Dini hamna budi kuhubiri Amani na Utulivu ili Taifa kwa ujumla liweze kufikia dhamira na malengo yaliyowekwa” Alisema Ayoub.

  Aidha Bw. Ayoub aliongeza kuwa nchi yetu ina sheria, kanuni na taratibu zinazotuongoza hivyo wananchi hawana sababu ya kugombana hasa kwenye mambo yanayolenga kuliletea taifa maendeleo kwani hatuna pengine pa kwenda pindi machafuko yanapotokea.
   Akizungumzia kuhusu mchakato wa Katiba Inayopendekezwa Bw. Ayoub alisema kuwa wananchi hawana budi kujitokeza katika kuipigia kura ya maoni Katiba Inayopendekezwa kwani katiba hii imegusa makundi yote katika jamii.

  Pia Bw. Ayoub aliwaasa viongozi wa dini kuisoma katiba hii kifungu kwa kifungu, ibara kwa ibara ili kwenda kutoa elimu kwa waumini wao ili kuepuka upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu wasioitakia mema nchi yetu.

  Naye Mbunge wa WAWI kupitia tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) Mh. Hamad Rashid Mohamed alisema kuwa amekuwa akishangazwa na baadhi ya watu wanaopita mitaani na kutoa upotoshaji wa baadhi ya vipengele vilivyo katika Katiba Inayopendekezwa bila kuangalia madai yaliyopelekea kuanzishwa kwa mchakato wa upatikaji wa Katiba MpyaMh. Rashid alisema kuwa maaandamano mengi yaliyokuwa yakifanyika kudai upatinaji wa Katiba Mpya yalitaka uwepo wa Tume huru ya uchaguzi,Mgombea huru na matokeo ya Tume kuhojiwa mahakamani na si suala la Serikali tatu au Serikali ya Mkataba jambo ambalo limejumuishwa vyema katika Katiba Inayopendekezwa na kutoa fursa pana zaidi ya kile walichokuwa wakidai.

  Alieleza kuwa wananchi hawana budi kusoma na kuelewa maudhui yaliyomo Katiba Inayopendekezwa ili kuona fursa zinazopatikana na jinsi gani Katiba hiyo imegusa maisha ya kila kundi katika Jamii ikiwemo watoto, wavuvi, walemavu, vijana, wanawake na wazee.
   Pia Mh. Rashid alisema kuwa viongozi wa dini hawana budi kuhubiri amani hasa katika kipindi hiki cha upatinaji wa Katiba Mpya na kuwaepuka wale wote wanaotaka kulipeleka taifa katika hali uvunjifu wa amani kwa kuhubiri chuki hasa juu ya Katiba Inayopendekezwa.

  Akizungumzia kuhusu suala la amani na utulivu katika mchakato huu wa Upatikanji wa Katiba Mpya Mwenyekiti wa Kamati ya Amani na Utulivu Tanzania Sheikh Noman Thabiti Jongo alisema kuwa njia pekee ya kuepuka uvunjifu wa amani ni kwa kuisoma na kuielewa Katiba Inayopendekezwa na kuacha kusikiliza chuki zinazoenezwa na baadhi ya watu kuhusu mchakato huu.

  Naye Katibu wa Kamati ya amani na Utulivu Padri Damas Mfoi aliwataka viongozi wote wa dini katika nafasi zao kuhubiri amani na utulivu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea upatikanaji wa Katiba Mpya na Uchaguzi mkuu.

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akimwagilia maji zao la nyanya la vijana wajasiriamali wa CCM katika Kijiji cha Nkulabi, Mpunguzi, Dodoma. Kinana aliwapongeza vijana hao wanne kwa kuamua kuanzisha shamba hilo ambalo mazao yake yanawasaidia kujikimu kimaisha.Kinana aliwataka vijana wengine kuiga mfano huo.

  Copy and WIN : http://bit.ly/copynwin
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa amebeba maji kwenye madumu aliposhiriki umwagiliaji maji katika shamba la nyanya la vijana wajasiriamali wa CCM katika Kijiji cha Nkulabi, Kata ya Mpunguzi, Jimbo la Dodoma Mjini leo wakati wa ziara yake,Kinana yupo mkoani Dodoma kwa ziara ya siku tisa ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi, kuimarisha uhai wa chama na kusikiliza kero za wananchi pamoja na kuzitafutia ufumbuzi.

  Copy and WIN : http://bit.ly/copynwin
   , akishiriki kuchimba mtaro wa mradi wa maji katika Kata ya Nzuguni

  Copy and WIN : http://bit.ly/copynwin
   Kinana akishiriki ujenzi wa chumba cha darasa katika Shule ya Sekondari Lukundo mjini Dodoma leo. 
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Dodoma, ambapo ametoa ushauri kwa Katibu Mkuu Kiongozi, kuwasimamisha mara moja watumishi wanaotajwa kwenye sakata la Escrow kama CCM ilivyowasimamisha viongozi watatu waliotajwa kwenye sakata hilo.

  Copy and WIN : http://bit.ly/copynwin
   Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwajibika.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Dodoma mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya  Barafu,Nape aliwaambia wakazi hao kuwa makini na wapinzani kwani wamekuwa wakihangahika na fedha za wafadhili ambazo hawaitakii mema nchi yetu.
   Baadhi ya wanachama wapya waliojunga na CCM wakila kiapo  wakati wa mkutano huo

  Copy and WIN : http://bit.ly/copynwin
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (wa tatu shoto) akiongoza kula kiapo cha CCM wakati wa mkutano huo. 
    Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Ndugu Adam Kimbisa akiwahutubia wakazi wa Dodoma mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Barafu.
   Pichani ni baadhi ya Wafuasi wa chama cha CCM na wananchi wakishangilia jambo kwenye mkutano huo.

  0 0

  Hotuba ya Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari aliyoitoa wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbinga ,Marehemu Captain John Damiano Komba ,Nassar alitoa hotuba hiyo kwa niaba ya kambi rasmi ya Upinzania Bungeni. 

  0 0

   

  Mwenyekiti wa Kamati  ya Kudumu ya Bunge ya  Nishati na Madini, Richard Ndassa akitoa maagizo kwa Wakandarasi, Wataalamu kutoka  Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), Wizara ya Nishati na Madini na  viongozi mbalimbali kwenye majumuisho  ya ziara ya kamati hiyo, baada ya kufanya ukaguzi wa miradi ya umeme mkoani Singida pamoja na kuzungumza na wananchi.
  Mwenyekiti wa Kamati  ya Kudumu ya Bunge ya  Nishati na Madini, Richard Ndassa (katikati) akisisitiza  jambo  katika eneo la mradi wa kuzalisha umeme kwa njia ya  upepo lililopo Kisesile wilayani Singida Mjini  mara  kamati hiyo  ilipotembelea mradi huo ili kujionea maendeleo yake pamoja na kuzungumza na watendaji wa eneo hilo.  Na Greyson Mwase, Singida.

  Mkuu wa Kitengo cha Miundombinu  na  Nishati  kutoka Shirika la Maendeleo la  Taifa (NDC)  Pascal Malesa  amesema kuwa serikali inatarajia kutumia   Dola za Marekani  Milioni 132 kwa ajili ya kukamilisha mradi wa kuzalisha umeme wa upepo wenye uwezo  wa Megawati 50 ifikapo  mapema mwaka 2016.

  Malesa aliyasema hayo mbele ya Kamati ya  Kudumu ya Bunge  ya Nishati na Madini  iliyofanya ziara ya kutembelea mradi wa kuzalisha  umeme kwa njia ya upepo unaojengwa  katika eneo la  Kisesile  nje kidogo ya  Singida  Mjini. Kamati ya  Bunge ya Nishati na Madini  ipo mkoani  Singida kwa ajili ya kukagua miradi ya umeme ili kujionea maendeleo yake pamoja na kuzungumza na wananchi.

  Alisema mradi huo  unatekelezwa kwa ubia kati ya  Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) lenye asilimia 60, Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) lenye  asilimia 20 na kampuni ya  Power Pool  East  Africa Limited yenye asilimia 20 chini ya kampuni ya ubia iitwayo  Geo  Wind Power  Tanzania  Limited  (Geo Wind)  iliyoundwa mwaka 2011.

  Malesa alieleza kuwa gharama hizo zinahusisha utekelezaji wa mradi huo  awamu ya kwanza kwa ajili ya kuzalisha megawati 50 ambayo itahusisha ujenzi  wa msongo wa umeme  wa kilovolti 220 umbali wa kilomita 12 na kuunganisha kwenye  gridi ya  taifa.

  Alisema  fedha hizo ni  mkopo kutoka  Benki ya  Exim  ya  China na  kuongeza  kuwa kwa  sasa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) linafuatilia mkopo  huu chini  ya  udhamini wa Serikali  kupitia  Wizara ya  Fedha  baada ya kukamilisha  vigezo vyote  vya mradi vilivyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya kupata mkopo  wa masharti nafuu na kuviwasilisha benki ya Exim ya  Serikali ya watu wa  China.


  Alieleza kuwa baada ya  Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya   Fedha  kuwasilisha maombi  ya mkopo kwenye Benki ya Exim  ya China mwaka 2013,  ujumbe wa kwanza kutoka  benki hiyo  uliwasili Tanzania mapema Machi 2014 na kufanya uhakiki wa awali wa mradi.

  Alisema pamoja na uhakiki wa mradi huo, ujumbe  huo ulifanya mazungumzo  na  Wizara ya  Fedha na wanahisa wa mradi na kuongeza kuwa ujumbe wa pili  kutoka Benki ya Exim  ulifika Tanzania mapema Mei, 2014 na kufanya  uhakiki wa kina wa mradi ikiwa ni pamoja na kutembelea eneo la mradi mkoani Singida  na kufanya mazungumzo na uongozi wa mkoa wa Singida.

  Akielezea hatua iliyofikiwa kuhusu mkopo, Malesa aliieleza kamati kuwa baada ya  Serikali kupitia NDC kutimiza masharti  yote  ya mkopo  na  Benki ya  Exim  kutoka  China  kufanya uhakiki wa mradi,  benki hiyo iliridhia  kutolewa kwa mkopo wenye masharti nafuu tangu mwezi  Septemba mwaka jana  kwa ajili ya ujenzi wa mradi huu.

  Aliongeza kuwa hivi sasa Serikali kupitia  Wizara ya  Fedha iko katika majadiliano  ya masharti ya mkopo na kusisitiza kuwa NDC inafuatilia majadiliano hayo  ili kuhakikisha kuwa yanasainiwa mapema ili kuanza ujenzi mara moja  ili kuendana na  Mpango wa Matokeo Makubwa  Sasa (BRN) ambao umeeleza wazi  kuhusu lengo la  serikali  kutekeleza na kukamilika kwa mradi huu mwaka 2016.

  Akielezea matarajio ya mradi huo Malesa alisema mara baada ya kukamilika kwa mradi huo, mradi utaimarisha  uwezo wa Gridi ya Taifa hasa wakati  wa kiangazi  kwa kuzalisha  umeme wa  uhakika na hivyo kusaidia uhifadhi  bora wa maji katika bwawa la Mtera na hivyo kupunguza makali ya mgawo  wa umeme nchini.

  “ Mradi utalipunguzia Taifa mzigo wa kutumia  fedha za kigeni  kuagiza mafuta  ya  dizeli yanayotumika kwenye mitambo ya kufua umeme wa dharura”, alisema Malesa
  Malesa aliongeza kuwa vilevile  mradi utajenga uwezo wa kitaalam  kwa watanzania  kupitia progamu za kubadilishana uzoefu pamoja na ujuzi na kuongeza uhifadhi wa mazingira.

  Alisema mradi utaingiza Dola za Marekani  milioni 23.2 kwa mwaka kutokana  na mauzo ya umeme na kutoa ajira zipatazo 2,200 na kusisitiza kuwa mradi utalipa kodi mbalimbali serikalini  ikiwa ni pamoja na  Kodi ya Ongezeko la Pato (VAT) na nyinginezo.

  Akielezea changamoto za mradi  Malesa alisema ni pamoja na kuchelewa kwa upatikanaji wa mkopo kwa masharti nafuu  kutoka Benki ya Exim ili kugharamia  ujenzi wa mradi na kuongeza kuwa  hali hiyo inatokana na Benki ya Exim kubadilisha  sera za riba nafuu kutoka asilimia  moja hadi mbili na muda wa mkopo kupungua kutoka miaka 25 hadi 20 huku  Wizara ya  Fedha  ikipendelea riba kuwa asilimia moja kama ilivyokuwa awali.

  Akielezea mikakati ya kukabiliana na changamoto hiyo Malesa alisema kuwa NDC ikishirikiana na wanahisa wenzake, inafuatilia kwa karibu  sana upatikanaji wa mkopo  kutoka Benki ya  Exim mapema iwezekanavyo hasa ikizingatiwa kuwa mradi huu unatekelezeka kwa faida kwa kuzingatia masharti mapya  ya Benki ya Exim.

  Akielezea suala la  fidia kwa wananchi waliopisha mradi huo  Malesa alisema kuwa jumla ya shilingi milioni 418 zililipwa kama  fidia kwa wakazi waliopisha mradi  huo katika awamu  mbili tofauti.

  Akielezea chagamoto wakati wa ulipaji wa fidia, Mkuu wa wilaya  ya  Singida Mjini anayehamishiwa katika wilaya ya Urambo Queen Mlozi, alisema  wapo wakazi sita wasiokuwa waaminifu walilipwa zaidi ya mara moja huku baadhi yao wakilipwa bila kuwa na  maeneo.

  Mlozi alisema suala la watuhumiwa hao ofisi yake imeshalikabidhi katika Ofisi ya  Taasisi  ya Kuzuia  na Kupambana na  Rushwa (Takukuru) kwa hatua zaidi. Wakati huohuo  akizungumza kwa niaba ya Kamati ya  Kudumu ya  Bunge ya Nishati na Madini, Mwenyekiti wa kamati hiyo  Richard Ndassa aliitaka serikali kuharakisha mchakato wa mkopo kutoka  Benki ya  Exim ili mradi huo  uanze mara moja na mkoa wa Singida uanze kunufaika na mradi huo.

  Ndasa alisema  kuwa mbali na uwezo wa kuzalisha megawati 50, mradi huo una uwezo wa kuongeza hadi megati 300 kiasi ambacho ni kikubwa kwenye  Gridi ya  Taifa.

  Alisema mbali na  kupunguza tatizo la mgawo wa umeme,  mradi huo pia utapelekea punguzo la bei ya umeme kutoka  shilingi za kitanzania senti 30 ya awali hadi senti 13 na hivyo kuchangia kwenye  ukuaji wa uchumi wa nchi.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Times Radio Fm, Mr. Rehure Nyaulawa (kushoto) akimkabidhi msaada wa mashuka Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala Dk, Sophinias Ngonyani (kulia) mara baada ya Timu nzima ya Kipindi cha Maskani kilipopiga hodi hospitalini hapo kutoa misaada ya mashuka yapatayo 200 kwa ajili wodi ya akina mama na watoto. 

  Msaada huo ilikuwa ni kuunga mkono maadhimisho ya wanawake duniani inayoadhimishwa leo Machi 8, duniani kote. Wanaoshuhudia ni Mbunge wa Kinondoni Mhe. Idd Azzan na Mkurugenzi wa Mazinat Bridal Maza Sinare. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ni 'Uwezeshaji Wanawake, Tekeleza Wakati ni Sasa'. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.
  Wakifurahia msaada.
  Mtangazaji wa Kipindi cha Maskani ya Times Fm, Stanslaus Lambat (wa kwanza kulia) akiendelea kurusha matangazo live toka eneo la tukio.
  Mtangazaji wa Kipindi cha Maskani ya Times Fm, Sandra Temu akiongea machache mara baada ya makabidhiano kufanyika.
  Viongozi wakifuatilia kwa makini.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Times Radio Fm, Mr. Rehure Nyaulawa alisema kuwa Times Kupitia kipindi cha Maskani walifika kuungana na watu wote duniani kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambayo hufanyika Machi 8 kila mwaka.
  Kila mmoja anatambua changamoto zinazoikabili sekta ya afya hapa nchini hivyo wa kutambua hilo wameamua kuwa mfano bora kwa jamii kwa kuchangia mashuka 200 kwa ajili ya wodi ya akinamama na watoto kwenye hospitali ya Mwananyamala.

  Mbunge wa Kinondoni Mhe. Idd Azan akitoa shukrani kwa uongozi wa Times Fm kwa kujitoa kutoa msaada katika jimbo lake.
   Mbunge waa Kinondoni Mhe.Idd Azzan akiongea na mtangazaji wa Kipindi cha Maskani cha Times Fm Sandra Temu mara baada ya kufika katika hospitali kuungana nao kutoa msaada wa mashuka kwa ajili ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani.
  Mtayarishaji wa Kipindi Cha Maskani Zhora Zuri (wa kwanza kushoto) akitoa maelezo machache mara baada ya kuingia katika hospitali ya Mwananyamala kutoa msaada. Pembeni ni Watangazaji wa kipindi hicho Sadra Temu, Stanslaus Lambat (mwenye shati nyeupe) na rafiki yao mwenye tisheti nyeusi.
  Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala Dk, Sophinias Ngonyani (katikati) akitoa  maelezo kwa Mbunge wa Kinondoni Mhe. Idd Azzan na Mkurugenzi Mtendaji wa Times Radio Fm, Mr. Rehure Nyaulawa mara baada ya Timu nzima ya Kipindi cha Maskani kilipopiga hodi hospitalini hapo kutoa misaada ya mashuka yapatayo 200 kwa ajili wodi ya akina mama na watoto. Msaada huo ilikuwa ni kuunga mkono maadhimisho ya wanawake duniani inayoadhimishwa leo Machi 8, duniani kote.
  Wakunga wa hospitali ya Mwananyamala wakiwa wameshika mashuka mara baada ya kukabidhiwa.
  Umati wa Watu waliofika kushuhudia makabidhiano hayo.
  Mbunge wa Kinondoni Mhe. Idd Azzan na Mkurugenzi Mtendaji wa Times Radio Fm, Mr. Rehure Nyaulawa wakitandika kitanda mara baada ya Timu nzima ya Kipindi cha Maskani kilipopiga hodi hospitalini hapo kutoa misaada ya mashuka yapatayo 200 kwa ajili wodi ya akina mama na watoto. Msaada huo ilikuwa ni kuunga mkono maadhimisho ya wanawake duniani inayoadhimishwa leo Machi 8, duniani kote.
   Mmoja ya akinamama akitoa shukrani kwa uongozi wa Times Fm kwa masaada waliotoa.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Times Radio Fm, Mr. Rehure Nyaulawa akiongea na wafanyakazi wa Maznat Bridal mara baada ya Timu nzima ya Kipindi cha Maskani kilipopiga hodi hospitalini hapo kutoa misaada ya mashuka yapatayo 200 kwa ajili wodi ya akina mama na watoto. Msaada huo ilikuwa ni kuunga mkono maadhimisho ya wanawake duniani inayoadhimishwa leo Machi 8, duniani kote.
   Mtayarishaji wa Kipindi cha Maskani ya Times Fm, Zhora Zuri akitoa maelekezo kwa Mtangazaji wa Kipindi hicho Sandara Temu.
  Mbunge wa Kinondoni Mhe. Idd Azzan akiongea na Mtayarishaji wa Kipindi cha Maskani ya Times Fm, Zhora Zuri.
  Timu ya Maznat Bridal ikiwakilisha.

  0 0

   Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Rukia Mtingwa (kushoto) akiwaongoza baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo katika tukio la  kujitolea damu lililoandaliwa na benki hiyo kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani jijini Dar es Salaam jana.
    Meneja Mahusiano ya Kibiashara wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Lukemelelo Kaduma (katikati) akijitolea damu ikiwa ni sehemu ya matukio ya wafanyakazi wa  NBC kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani jijini Dar es Salaam mwishoni jana. Anayemtoa ni mtaalamu wa damu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS), Peter Chami na kushoto ni mkazi wa Jiji la Dar es Salaam, Benard Elikana.
   Mmoja wa wafanyakazi wa  Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Jolanda Songoro (kushoto) akijitolea damu ikiwa ni sehemu ya matukio ya wafanyakazi wa  NBC kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani jijini Dar es Salaam mwishoni jana. Anayemtoa ni mtaalamu wa damu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS), Peter Chami.
   Meneja wa Idara ya Mikopo Midogo wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Jacob Samuel (kulia) akijitolea damu pamoja na baadhi ya wafanyakazi wenzake ikiwa ni sehemu ya matukio ya wafanyakazi wa  NBC kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani jijini Dar es Salaam jana. Anayemtoa ni mtaalamu wa damu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS), Peter Chami.

   Mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya NBC, William Tendwa naye akishiriki tukio lililoandaliwa na benki hiyo la kujitolea damu kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.
   Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC wakijitolea damu ikiwa ni sehemu ya matukio ya wafanyakazi hao kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani jijini Dar es Salaam jana. Anayewatoa damu kushoto ni mtaalamu wa damu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS), Peter Chami.
   Mkazi wa Jiji la Dar es Salaam, Bernard Elikana akiungana na baadjhi ya wafanyakazi wa NBC kujitolea damu kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani. Kulia ni Petert Chami wa Damu Salama.
   Mkazi wa Mwananyamala Dar es Salaam Subira Omar akijitolea damu katika tukio lililoandaliwa na Benki ya NBC kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani jana. Anayemtoa ni Peter Chami kutoka Damu Salama (NBTS)

   Mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya NBC, John Nyaindi  naye akishiriki tukio lililoandaliwa na benki hiyo la kujitolea damu kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani. Kushoto ni Daudi Mkawa kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama.
  Mtaalamu wa damu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Peter Chami (kulia) akimuandaa mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya NBC, Georgia Mwita ili aweze kumtoa damu katika  tukio hilo jijini Dar es Salaam jana.

  0 0

  LEO katika maswali matano kuelekea miaka 15 ya Tamasha la Pasaka linalotarajia kufanyika baadaye mwaka huu hapa Tanzania,  Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi ni shabiki mkubwa wa tamasha hilo lililoasisiwa tangu mwaka 2000 ambaye anakiri aliwahi kuhudhuria baadhi ya matamasha hayo na kujionea waimbaji wa Tanzania wanavyofikisha ujumbe wa neno la Mungu kupitia uimbaji.
   
  Swali: unaizungumziaje sikukuu hii kubwa kuliko zote kwa Wakristo hapa duniani, ukiwa ni muamini wa dini hiyo?
   
  Jibu: Nawaomba Watanzania kujiandaa kusherehekea Sikukuu hiyo ambayo ni kubwa zaidi ya zote duniani kwani tunasherehekea kufufuka kwa Bwana Yesu Kristo aliyefufuka kwa ajili ya kuwakomboa waumini mbalimbali ulimwenguni.
   
   Swali: Nini wito wako kwa waumini katika sikukuu hiyo muhimu zaidi?
   
  Jibu: Wito wangu kwa waumini kwanza ni kutambua maana ya Pasaka na kwanini tunasherehekea sikukuu hiyo adhimu hapa duniani.
   
  Pili nawaomba Watanzania wenzangu kujua maana ya Pasaka kwani hata Wakristo baadhi hawatambui maana ya Pasaka na kwanini tunasherehekea sikukuu hii muhimu ya kukumbuka ufufuko wa kipenzi chetu.
   
  Swali:Nini wito wako kwa Tamasha la Pasaka ambalo linatimiza miaka 15 tangu kuasisiwa kwake na Kampuni ya Msama Promotions?
   
  Jibu: wito wangu kupitia Tamasha la Pasaka ambalo ni ufufuko wa  Bwana Yesu Kristo, Watanzania tulitumie kutenda mema yanayomfurahisha na kumpendeza Mungu, kwani sasa hivi kuna matukio mengi machafu yanayomuudhi na kumchukiza Mungu, hivyo ni nafasi yetu kumpigia magoti na kumuomba.
   
  Kwani tamasha hilo la muziki wa Injili si la Wakristo pekee, linashirikisha mashabiki mbalimbali wa muziki huo wenye mwelekeo wa kuzungumza na Mungu kupitia Waimbaji wanaopanda jukwaani ambao wanapaza sauti zao zinazokwenda mbali zaidi kwa lengo la kumpigia magoti na kumuomba Mungu.
   
  Swali: Unawaasa nini Watanzania kupitia tamasha hilo ambalo lina mlengo wa kusaidia jamii zenye uhitaji maalum kama yatima, walemavu, wajane na wenye shida zinazofanana na hizo ambazo zinahitaji msaada kutoka kwa wenye huruma kama Alex Msama?
   
  Jibu: Wito wangu kwa Watanzania ni kuongeza upendo  ili kuilinda amani yetu tuliyonayo tuliyoachiwa na muasisi wa taifa hili, marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alituasa tupendane kwani hata maandiko matakatifu yanatueleza juu ya upendo baina ya wanadamu.
   
  Amani na upendo linatakiwa lizingatiwe kwa sababu, tunashirikiana na nchi jirani kupitia waimbaji na hata viongozi kadhaa ambao wanashiriki kwenye tamasha hilo ambalo linakusanya nchi kadhaa za Afrika zikiwemo Afrika Kusini, Zambia, Kenya, Rwanda na moja ya bara la Ulaya ambayo ni Uingereza, jambo ambalo ni la kujivunia zaidi kwa sababu inaonesha sala zetu zinafika kwa Mungu ipasavyo kwani kadri siku zinavyozidi kwenda mbele idadi ya wageni kupitisa tamasha hilo wanazidi kuongezeka, hivyo ni nafasi yetu kuitunza na kuithamini tunu hiyo muhimu tuliyopewa na Mungu.
  Kanuni ya utu, binaadamu wote ni ndugu moja, mambo ya kuuana wenyewe kwa wenyewe, uhasama, ufisadi, mauaji ya albino na machafu mengine yanayochafua taswira na uongozi wa mataifa mbalimbali hasa Tanzania iliyogubikwa na wingu hilo zito yatapungua kupitia Tamasha la Pasaka ambalo ndio nguzo kuu ya kuondoa udhaifu huo.
   
  Swali: Nini changamoto iliyoko mbele hasa kwa masuala kama upitishwaji wa Katiba pendekezwa, uchaguzi Mkuu na mengineyo yanayoendelea kabla ya maendeleo hayo?
   
  Jibu:Tamasha la Pasaka mwaka huu lina changamoto nyingi kwani inatakiwa tujitafakari kwa kiasi kikubwa tulipofikia na tunakokwenda kwani tunatakiwa turudi katika umoja wetu tulioachiwa na baba wa Taifa Mwalim,u Julius Kambarage Nyerere kwani Tanzania si wakabila bali ni Taifa moja, hivyo tuachane na mifumo ambayo itaondosha umoja wetu na kutugombanisha kwa kuchonganishwa na watu wachache wasioitakia mema nchi yetu.
   
  Uchaguzi mkuu wa mwaka huu una changamoto nyingi sana ambazo zisisababishe tutoke kwenye mstari wa amani na upendo tulioachiwa na waasisi wetu kwa sababu ya wachache wenye uchu wa madaraka ambao watatusababishia machafuko ambayo yataigharimu nchi yetu.
   
   Wito wake kwa waimbaji wa Tanzania ni kuongeza juhudi ili kulinda na kufanikisha maendeleo ya muziki huo ambao lengo lake ni kumfikishia Mungu kilio chetu wanadam hasa kwa matukio yanayomchukiza.

  0 0


  Ikiwa leo ndiyo Siku ya Wanawake Duniani, wanawake wa Ghala la Kuhifadhi Madawa la Taifa (MSD) jana walisherehekea siku hiyo kwa aina yake baada ya kuifanya katika eneo lao la kazi.
  Akizungumza na akina mama hao, Victoria Elangwa ambaye ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, alisema wameamua kufanyia sherehe hizo eneo la kazi ili akina mama hao wapewe elimu kuhusu afya ya uzazi, ujasirimali pamoja na kukabiliana na msongo unaowakabili wafanyakazi katika maisha yao ikiwa ni pamoja na sehemu ya kazi.

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (MSD),  Bw. Cosmas Mwaifani akifungua sherehe hiyo kabla ya kumkabribisha mgeni rasm, Bi. Helen Mwakipunda ambaye ni Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, aliwapongeza akina mama hao kwa kuadhimisha sherehe hiyo kwa aina ya tofauti.
  "Nawapongeza kwa kuamua kuadhimisha siku yenu kwa kuwaalika watoa mada ya afya, ujasiramali na msongo unaoweza kumkabili mtu akiwa kazi na nyumbani," alisema mkurugenzi huyo.Naye mgeni rasmi, Bi. Mwakipunda aliwapongeza akina mama hao na kuwaambia wazidi kujitokeza katika nafasi mbalimbali za uongozi  kwa sababu wanaweza.

  "Hivi sasa wanawake tumeweza kupigania haki zetu mbalimbali na kuondokana na ukandamizwaji uliokuwepo huko nyuma wa kutoshirikishwa kwenye masuala ya mirathi na mambo mengine," alisema Mwakipunda.

  Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akina wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Matlida Ngarina akitoa mada ya juu ya magonjwa ya aliwata akina mama kuwa na utamaduni wa kujichunguza matiti yao mara kwa mara ili kubaini kama kuna uvimbe wowote.

  Dk. huyo aliongeza kuwa, kufanya hivyo kutawasaidia kujiepusha na kansa ya ziwa ambayo imekuwa aikiua wanawake wengi hivi sasa.

  Aliwaeleza wanawake hao maradhi mbalimba ya via vya uzazi na kuwashauri wawape somo mabinti zao wasijihusishe na mapenzi wakiwa na umri mdogo kwani baadaye hupatwa na saratani ya kizazi. 
   Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (MSD), Bw. Cosmas Mwaifani akifungua sherehe za Siku ya Akina Mama Duniani zilizofanyika.
  Bw. Mwaifani akimkaribisha mgeni rasmi wa sherehe hizo, Bi.Helen Mwakipunda ambaye ni Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
  Bi. Mwakipunda akizungumza na wafanyakazi wa (MSD) wakati wa sherehe hizo
   Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akina kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili,.Matlida Ngarina aliyeAlikwa kwa ajili ya kutoa mada kuhusiana na magonjwa ya akina mama, akizungumza na wafanyakazi wa (MSD)
   Mjasiriamali maarufu wa saluni jijini Dar es Salaam, Maza Sinare akitoa mada kuhusu ujasiriamali wakati wa sherehe hizo. Sinare alialikwa mahususi kwa ajili ya kuwafundisha akina mama wa MSD namana wanavyoweza kuanzisha biashara zao huku wakiendelea kufanya kazi.
  Dr. Chris Mauki, akiwazungumza na akina mama wa MSD namna wanavyoweza kukabiliana na msongo wa mawazo sehemu ya kazi
   Afisa Habari wa (MSD),Etikusi Siluka ambaye siku hiyo alikuwa mshehereshaji wa sherehe hizo akizungumza jambo
  Mmoja wa wafanyakzi wa (MSD) akimuuliza swali, Dk. Ngarina kuhusiana na uvimbe wa titi kwa wanawake.
   Mfanyakazi wa (MSD), Gendi Machumani akimuuliza swali Dk, Ngarina kuhusiana na magonjwa ya njia ya uzazi kwa mwanamke.
   Baadhi ya wafanyakazi wa (MSD), wakimsikiliza kwa makini Bi, Mwakipunda aliyekuwa mgeni rasmi.
   Mgeni rasmi katika sherehe hizo, Bi. Mwakipunda akicheza muziki wa Nani Kama Mama wakati wa sherehe hizo.
   Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (MSD), Bw. Mwaifani akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa (MSD) pamoja na mgeni rasmi kulia kwake, Bi. Mwakipunda.
   Wafanyakazi wa (MSD) ambao wapo kwenye Club ya mazoezi ya MSD, wakifanya mazoezi katika sherehe hizo.
   Wafanyakazi wa hao wakiwapigia makofi wenzao waliokuwa wakifanya mazoezi ya viungo.

  0 0


  Akina mama Wa Citizen Foundation wakiongozwa na askari polisi wa kituo cha cahng'ombe wakati wakifanya maandamano kutoka kituoni hapo kwenda kukabidhi msaada wa magodoro hospitali ya temeke.

   Akina mama wa Citizen Foundation wakiwa nje ya Hospitali ya Wilaya ya Temeke na walikokwenda kukabidhi magodoro.

   Mwenyekiti wa Citezen Foundation, Lilian Wasira akimkabidhi moja ya magodoro, Amosi Kabelege ambaye ni Msimamizi Mkuu wa Hospitali ya Temeke.
   Mwenyekiti wa Citizen Foundation, Lilian Wasira akimkabidhi maji ya kunywa, Bi. Ashura aliyelazwa hospitalini hapo.
  Mganga mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Temeke, Amani Malima alimshukuru Mwenyeti wa Citezen Foundation kwa masaada wa magodoro waliotoa hospitalini kwake jana.

  Akina mama wa Kikundi cha Citizen cha Tabata jijini Dar es Salaam, jana kilitoa magodoro 50 na katoni 25 za maji na 25 za soda aina ya Cocacola ikiwa ni kuadhimisha Siku ya Akina mama Duniani.

  Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo, Mwenyekiti wa kikundi hicho, Lilian Wasira alisema wameguswa sana na tatizo la akina mama kujifungulia sakafuni ndiyo maana wakaona watoe msaada huo.

  Lilian alisema, wameamua kufanya hivyo badala ya kusherehea siku hiyo kwenye kumbi za burudani huku wenzao wakijifungulia sakafuni.

  Mwenyekiti huyo alisema hawataishia Temeke tu bali wanatarajia kufanya harambee nchi nzima kuwahamasisha wadau mbalimbali kuhakikisha huduma ya afya inaboreshwa. Magodoro hayo yana thamani shilingi milioni 2,740,000.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akifungua pazia kuashiria ufunguzi wa Hotel ya Park Hyatt Zanzibar iliyopo Mambo Msiige Mji Mkongwe wa Zanzibar (kulia) Kaimu Waziri wa Fedha na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini (katikati) Mmiliki wa Hoteli hiyo Sheikh Ali Sayeed  Albawardy [Picha na Ikulu.]sh2 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akikata utepe kama ishara ya ufunguzi wa Hotel ya Park Hyatt Zanzibar iliyopo Mambo Msiige Mji Mkongwe wa Zanzibar (kulia) Kaimu Waziri wa Fedha na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini (kushoto) Mmiliki wa Hoteli hiyo Sheikh Ali Sayeed  Albawardy [Picha na Ikulu.]sh3 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akifuatana na Sheikh Ali Sayeed  Albawardy mmiliki wa Hotel ya Park Hyatt Zanzibar alipotembelea sehemu mbali mbali za Hoteli hiyo iliyopo Mambo Msiige Mji Mkongwe wa Zanzibar baada ya kuifungua rasmi leo.sh4 
  Wasoma utenzi Amina Mohamed na Khadija Ridhiwani (kulia) walipokuwa wakitoa burudani hiyo mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pamoja na viongozi mbali mbali wakati wa sherehe za Ufunguzi wa Hotel ya Park Hyatt Zanzibar iliyopo mtaa wa Mambo Msiige Mji Mkongwe wa Zanzibar leo .
  sh5 
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini akiwa Kaimu waziri wa Fedha alipokuwa akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Hotel ya Park Hyatt Zanzibar kwa wananchi pamoja na kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein azungumze na Wananachi baada ya kuifungua Hoteli hiyo iliyopo mtaa wa Mambo Msiige Mji Mkongwe wa Zanzibar leo sh6 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  akitoa hutuba yake wakati alipokuwa akizungumza na wananchi na Viongozi mbali mbali na wawekezaji walioalikwa katika ufunguzi wa  Hotel ya Park Hyatt Zanzibar yenye hadhi ya juu  katika mtaa wa Mambo Msiige Mji Mkongwe wa Zanzibar leo.sh7 
  Baadhi ya waalikwa mbali mbali wakiwemo wawekezaji na wafanyabiashara wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  alipokuwa akizungumza na wananchi na Viongozi mbali mbali na wawekezaji walioalikwa katika ufunguzi wa  Hotel ya Park Hyatt Zanzibar yenye hadhi ya juu  katika mtaa wa Mambo Msiige Mji Mkongwe wa Zanzibar leo .sh8 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akiaagana na Sheikh Ali Sayeed  Albawardy baada ya kumalizika kwa sherehe za ufunguzi wa Hotel ya Park Hyatt Zanzibar iliyopo Mambo Msiige Mji Mkongwe wa Zanzibar (katikati) Meneja Mkuu wa Hoteli hiyo Bi Mercela Heeendoerfer,[Picha na Ikulu.]

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akivishwa chombo chenye dawa aliposhiriki kupulizia dawa za kuua wadudu katika mradi wa shamba la zabibu eneo la Chinangali II, Wilaya ya Chamwino leo.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki kupulizia dawa ya kuua wadudu katika mradi wa shamba la zabibu wa Chinangali II, wilayani Chamwino, mkoani Dodoma leo.
  Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Farida Mgomi, na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM kupitia Vijana, Deo Ndejembi wakishiriki kupulizia dawa za kuu wadudu katika shamba la zabibu la Chinangali II, wilayani Chamwino, mkoani Dodoma leo.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Mtera,Mh.Livingstone Lusinde ndani ya wilaya ya Chamwino mapema leo.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Mtera,Mh.Livingstone Lusinde ndani ya wilaya ya Chamwino mapema leo.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiweka jiwe la msingi Ofisi ya CCM Wilaya.
  Ndugu Kinana akipanda mti  mbele ya Ofisi ya Wilaya ya Chamwino inayojengwa.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndug Kinana akiingia ukumbini kuendesha mkutano wa Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Chamwino
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndug Kinana akizungumza katika mkutano maalum wa jimbo la Chilonwa,wilaya ya Chamwino leo.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (katikati), akishiriki kuchimba shimo la choo cha Shule Mpya ya Msingi ya Kikwete, eneo la Chamwino Ikulu, Jimbo la Chilonwa wakati wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, katika Wilaya ya Chamwino, Mkoa wa Dodoma leo.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi-Taifa Nnape Nnauye akimpogeza mmoja wa watoto kundi la Nyota Njema aliyekuwa akipiga ngoma yenye asili ya kigogo kwa ustadi.
  Nyota njema Kikundi cha ngoma za asli ya kabila la Wagogo linaloshirikisha watoto wanaopiga kwa ustadi ngoma kiktumbuiza baada ya Kinana kuwasili kushiriki ujenzi wa Shule ya Msingi ya Msanga B, wilayani Chamwino.Katikati ni mtoto Jamima Juma mwenye umri wa miaka mitatu

  Copy and WIN : http://bit.ly/copynwin
  Nyota njema Kikundi cha ngoma za asli ya kabila la Wagogo linaloshirikisha watoto wanaopiga kwa ustadi ngoma kiktumbuiza baada ya Kinana kuwasili kushiriki ujenzi wa Shule ya Msingi ya Msanga B, wilayani Chamwino.Katikati ni mtoto Jamima Juma mwenye umri wa miaka mitatu

  Copy and WIN : http://bit.ly/copynwin
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akitazama kikundi cha ngoma za asili ya kabila la Kigogo linalowashirikisha watoto kiitwacho Nyota Njema,alipokwenda kushiriki ujenzi wa shule ya msingi ya Msanga B,Wilayani Chamwino.
  Sehemu ya jengo la Zahanati ya kijiji cha Mahampha katika kata ya Chilonwa,Wilayani Chamwino,ambapo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alishiriki ujenzi wa zahanati hiyo
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiungana na vikundi vya ngoma kupiga ngoma alipowasili kwenye mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Majereko, wilayani Chamwino leo.
   Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano huo wa hadhara.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana Katibu Mkuu wa CCM,akihutubia katika mkutano huo, ambapo alisema CCM ni chama pekee nchini kinachowajali wanawake kwa kuwapatia nafasi nyingi za uongozi. Leo ni maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ambayo kitaifa imeadhimishwa mkoani Mororo na mgeni rasmi alikuwa Rais Jakaya Kikwete.
  Copy and WIN : http://bit.ly/copynwin

older | 1 | .... | 479 | 480 | (Page 481) | 482 | 483 | .... | 1897 | newer