Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46371 articles
Browse latest View live

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Katiba,sheria na Utawala yaridhishwa na miradi ya TASAF Mbarali

$
0
0
 Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba,Sheria na Utawala wamefanya ziara katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kuona utekelezaji wa shughuli za Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) na kukutana na walengwa wa Mpango wa Kunusuru kaya Masikini unaotekelezwa na mfuko huo.

Wakizungumza na walengwa hao katika kijiji cha Madabaga wabunge hao wameonyesha kuridhishwa na mafanikio makubwa yaliyoanza kupatikana baada ya walengwa kupata fedha chini ya utaratibu wa uhawilishaji fedha unaotekelezwa na Tasaf.

Wakizungumza katika ziara hiyo baadhi ya walengwa wameeleza namna walivyonufaika na fedha zilizokwishatolewa ikiwa ni pamoja na kusomesha watoto,kuboresha makazi yao na kuwa na uhakika wa huduma ya afya na lishe.

Akizungumza kwenye mkutano uliofanyika kijijini Madabaga,mwenyekiti wa kamati hiyo Vedastus Rweyikiza amewahimiza wananchi hao kutumia fursa hiyo kwa ukamilifu ikiwa ni pamoja na kubuni miradi itakayowafanya wawe katika mazingira mazuri hata baada ya mpango huo kumalizika.

Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa Tasaf Ladslaus Mananga,mkurugenzi wa ukaguzi wa mfuko huo,Christopher Sanga alibainisha kuwa jitihada za kuwafikia walengwa wote wa mpango huo zinaendelea ambapo ifikapo katikati ya mwaka huu zaidi ya kaya milioni moja zitanufaika na utaratibu wa uhawilishaji fedha nchini kote.
 Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro(wa tatu kutoka kushoto) akiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba,Sheria na Utawala kabala ya wajumbe hao kutembelea walengwa wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) wilayani Mbarani mkoani humo.Kulia ni mkurugenzi wa ukaguzi wa Tasaf Christopher Sanga.
 MKuu wa wilaya ya Mbarali Gulamhussein Kifu(wa nne kulia) akiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba,Sheria na Utawala kabla ya wajumbe hao kutembelea walengwa wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) wilayani Mbarani mkoani humo.
 Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba,Sheria na UtawalaVedastus Rweyikiza akizungumza jambo baada ya kamati hiyo kukutana na wanufaika wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) katika kijiji cha Madabaga wilayani Mbarani mkoani Mbeya.
 Wanufaika wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) katika kijiji cha Madabaga wilayani Mbarani mkoani Mbeya wakimsikiliza mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba,Sheria na Utawala Vedastus Rweyikiza kabla ya kuanza kugawiwa fedha kwenye mkutano uliofanyika kijijini hapo jana.
 Mmoja wa wanufaika wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) katika kijiji cha Madabaga wilayani Mbarani Hellena Bamba akikabidhiwa fedha kutoka kwa kamati ya mradi ya wilaya(CMC).
 Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba,Sheria na Utawala wakiangalia namna wanufaika wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) katika kijiji cha Madabaga wilayani Mbarani wanavyokabidhiwa fedha.Katikati ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Vedastus Rweyikiza kushoto kwake akifuatiwa na Felix Mkosamali na Willium Ngeleja.

TTCL yatoa Msaada wa Madawati kwa Shule ya Msingi Bunena,Bukoba

$
0
0
Uongozi wa TTCL ukitoa Msaada wa Madawati katika Shule ya Msingi  Bunena leo Ijumaa.TTCL inaamini kutoa msaada huo wa Madawati utasaidia kuboresha Ufanisi wa Shule na hatimaye kupata Matokeo Makubwa sasa katika Sekta ya Elimu. Pia ni Mategemeo ya TTCL kuwa utaleta chachu kwa wadau wengine katika Sekta kuweza kuchangia katika sekta hiyo pana ya Elimu. Hatimae kuondoa Changamoto zinazoikabili sekta ya Elimu hapa Mkoani Kagera na Nchi nzima kiujumla. TTCL pia imeweza kuwahakikishia wadau mbalimbali waliohudhuria hafra hiyo kuwa wataendelea kuwa bega kwa bega katika kuleta maendeleo kadri hali ya kifedha itakavyoruhusu.
Wanafunzi wakikalia dawati moja wapo ambapo dawati moja litakaliwa na Wanafunzi 3 hivyo madawati hayo yatawatosha wanafunzi 150 wa Shule hiyo ya Bunena.

WAKAZI 10000 KUNUFAIKA NA UKARABATI BWAWA LA KALEMAWE

$
0
0
DSC_0001
Mshehereshaji wa kongamano la siku moja lililofanyika jijini Dar kuzungumzia ukarabati na uendeshaji wa bwawa la Kalemawe lililopo wilayani Same mkoani Kilimanjaro, Mtaalamu wa masuala ya fedha wa UNCDF, Bw. Imanuel Muro akisherehesha kongamano hilo. Katikati ni mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Same, Herman Kapufi akifuatiwa na Mkuu wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Bw. Peter Malika.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)

ZAIDI ya watu 10,000 wanaozunguka bwawa la Kalemawe wilayani Same mkoani Kilimanjaro watanufaika na ukarabati wa bwawa hilo na kuwekewa muundo mpya wa kiutawala na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Ukuzaji wa Mitaji (UNCDF).

Bwawa hilo ambalo lipo katika kata za Kalemawe na Ndungu lilijengwa na watawala wa Kiingereza mwaka 1952-1959 kwa ajili ya kusaidia shughuli za kilimo na ufugaji baada ya kuanzishwa kwa hifadhi ya Mkomazi na hivyo wakazi kuzuiwa kwenda katika hifadhi hiyo kwa shughuli mbalimbali.

Taarifa ya kuwepo kwa mradi huo mkubwa, imetolewa na Mkuu wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF) nchini, Bw. Peter Malika wakati akiwakaribisha madiwani wa kata hizo ambao wameitwa katika kongamano la siku moja Dar es salaam kuzungumzia ukarabati na uendeshaji wa bwawa hilo.
DSC_0038
Pichani juu na chini ni Mkuu wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Bw. Peter Malika (kulia) akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Same, Herman Kapufi kufungua rasmi kongamano hilo.


Malika amesema Mfuko huo wa ukuzaji wa mitaji unasaidia ukarabati wa bwawa hilo kupitia mpango wake wa uendelezaji rasilimali kwa kutumia fedha za ndani (LFI) .

Amesema baada ya ukarabati huo, mradi utaendeshwa kwa pamoja kati ya serikali na watu binafsi. Malika alisema ukarabati huo unakidhi lengo la mfuko ambalo ni kuwezesha miundombini inayoleta maendeleo.
“Ukarabati na hatimaye uendeshaji wa bwawa hilo kutasaidia kuleta mabadiliko makubwa ya maendeleo ya mitaji kwa watu binafsi na umma.” alisema
DSC_0026 
Kongamano hilo lililofunguliwa na Mkuu wa wilaya ya Same, Herman Kapufi lilizungumzia masuala ya umiliki, masuala ya kisheria ya taasisi, utawala bora, masuala ya kiufundi ya ukarabati,uvuvi wa samaki wa kibiashara, matumizi ya maji kwa ajili ya umwagiliaji, ufugaji, mabadiliko ya tabia nchi na mazingira, uwezeshaji kiuchumi kwa wanawake, mfumo wa utoaji wa huduma za fedha na masuala mengi mengine ya mipango ya maendeleo endelevu.

Kapufi alisema kwamba pamoja na kushukuru Mfuko wa Mitaji kukubali kuwasaidia, amesema bwawa hilo ni muhimu sana katika kuondoa migogoro na migongano ndani ya jamii pia na mamlaka ya hifadhi ya Mkomazi.
Alisema kurejeshwa kwa hali yake ya zamani kutasaidia wafugaji, wakulima na watumiaji wengine wa bawawa hilo kama wavuvi wa samaki kila mmoja kuwa na nafasi katika matumizi ya bwawa.
DSC_0067
Mkuu wa wilaya ya Same, Herman Kapufi akizungumza kwenye kongamano la siku moja lililofanyika jijini Dar kuzungumzia ukarabati na uendeshaji wa bwawa la Kalemawe lililopo wilayani Same mkoani Kilimanjaro lililoandaliwa na UNCDF.

Aidha alisema ukarabati utakaofanywa na muundo wa uendeshaji wa bwawa hilo utasaidia wilaya pia kufikiria namna ya kutengeneza bwawa jingine katika Mto Ruvu kwa sababu kama hizo za kuwapa uwezo zaidi wananchi katika maendeleo yao kwa kutumia rasilimali maji.

Toka kujengwa kwake katika miaka ya 1950, bwawa hilo lenye urefu wa takaribani kilomita tatu na upana wa mita 200 limepungua ukubwa wake kwa karibu nusu ya uwezo wa awali kwa sababu za kujaa tope, matumizi mabaya, kukosa ukarabati na usimamizi.
Aidha limeota magugu maji ambayo inaua kizazi cha samaki na kuvuruga uvuvi.
DSC_0072
Mkuu wa wilaya ya Same, Herman Kapufi akisisitiza jambo kwenye kongamano hilo lililowakutanisha madiwani wa kata za halmshauri ya wilaya ya Same na wataalam kutoka UNCDF kujadili pamoja kabla ya utekelezaji.
DSC_0082
Pichani juu na chini ni washiriki wa kongamano hilo la siku moja ambao ni madiwani wa kata za Same, mainjinia na wakandarasi kutoka halmashauri ya wilaya ya Same pamoja na wataalam kutoka UNDCF.
DSC_0028
DSC_0096
Washiriki wakitamaza video ya bwawa la Kalemawe lililopo wilayani Same mkoani Kilimanjaro kujionea hali halisi ya bwawa hilo linalohitaji ukarabati.
20140626_124641
Pichani juu na chini ni muonekano wa bwawa la Kalemawe lililopo wilayani Same mkoani Kilimanjaro wakati UNCDF walipotembelea eneo hilo.
20140626_124736

EXCLUSIVE INTERVIEW: 'USHIRIKINA CHANZO CHA MAUAJI YA WATU WENYE ALBINISM' - DK. ALLY POSSI

$
0
0
Na Andrew Chale wa modewji blog.

Dk. Ally Possi ambaye ni Mhadhiri wa chuo kikuu cha Ardhi, Dar es Salaam. Akielezea na kuchambua kwa kina kuhusiana na wimbi la mateso na mauaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi wenye albinism.

Mo dewjiblog, iliamua kufanya mahojiano maalum ilikukuletea wewe msomaji wetu unayeperuzi mtandao wako bora kabisa kujua na kuelewa na nini kifanyike ikiwemo mimi na wewe katika kuchukua hatua.

Suala la mauaji dhidi ya watu wenye albinism:
“JAMII yenye ushirikina ndio yenye kuamini suala la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi ambao wana albinism, hivyo ilikuondoa imani hii potofu ni kutoa elimu katika maeneo yote na kuwalinda popote pale, Jambo hili ni jukumu letu sote” anabainisha Dk. Ally Possi.

Dkt. Possi anabainisha kuwa, Serikali itaendelea kulaumiwa mpaka hapo juhudi za dhati za kukomesha mauaji na vitendo vya kikatili vitakavyochukuliwa na kutokomezwa kabisa.
Fuatilia hapa Mahojiano hayo maalum.
DSC_0391
Mwanasheria na mhadhiri wa chuo kikuu cha Ardhi, Dk. Ally Possi akiwa kwenye ofisi za modewjiblog kabla ya mahojiano na mtandao huu. 

MO DEWJI BLOG : Karibu, mgeni wetu katika mtandao huu wa kijamii unaokuletea habari bora kabisa zilizochambuliwa kwa kina za ndani, nje na makala maalum za kina.
DK. POSSI: Asante, nashukuru sana…
MO DEWJI BLOG: Unadhani nini chanzo na hali ya ongezeko la vitendo hivi kwa sasa hapa Tanzania?
DK.POSSI:“Kwanza mauaji ni.. yanatokana na imani potofu. Imani potofu kwa jamii kuwa ukipata kiungo cha alibino unafanikiwa.
Hii ni imani potofu kwa jamii ya watu wenye kuamini ushirikina.
“Albino ni ulemavu ambao mtu anakosa aina ya vitamin inayoitwa melaniani…
Inakosekana ikiwemo katika ngozi, nywele na macho” anaendelea kubainisha kuwa: Kuwa albinism ni hali ya kurithi kutoka kwa wazazi wote wawili ama mmoja. Ni kwamba baba na mama wanakuwa na vinasaba vinavyokuwa na albinism na vinapokutana wakati wa kutunga mtoto ndipo mtoto mwenye albinism anazaliwa.

MO DEWJI BLOG:Vipi inahusishwa na suala la Imani?
DK. POSSI:“Imani sio dini, Ni imani ya kishirikina.
“Sijui kitu gani ambacho kimetokea kikaleta hiyo imani, kwa kifupi ipo kwenye jamii iliyoendelea na uwezo wake wa kiuchumi ni mdogo na elimu pia.
Pia tunaweza kusema: “Suala hili ni la imani, Imani si ya dini, bali ni ya kishirikina. Kwa sababu kuna mtu anasema yeye muislamu ama mkristo.
Au kuna mtu ana Phd/ Profesa, ama amesoma elimu nzuri tu ama ana pesa anafanya biashara au mfanyabishara au mwanasiasa mwenye elimu yake nzuri lakini ametumbukia kwenye imani hii ya kishirikina.
DSC_0355
Mwanadishi wa habari wa modewjiblog, Andrew Chale akiwa kwenye mahojiano maalum na Dk. Ally Possi.
MO DEWJI BLOG: Kwa nini Kanda ya ziwa mauaji haya yamezidi kwa kasi?.
Dk. POSSI:“Kwanza kuna tatizo: Ofkozi..mauaji hayo Kanda ya ziwa mauaji yameripotiwa sana pia kuna Morogoro pia na sehemu nyingine.
“Serikali imekuwa kimya sana… katika mauaji yametokea husikii kiongozi mkubwa, ukiondoa Rais alivyosema (Machi 2-wakati wa hotuba ya mwisho wa mwezi wa Februari), lakini kiongozi mkubwa wa juu Waziri Mkuu, tangu mtoto Yohana yule wa Geita, Chato kukutwa ameuwawa
Sijasikia kauli nyingine zaidi ya Rais…Ambayo nayo ameitoa wiki mbili hadi moja na nusu, kupita ndio Rais anatoa tamko hilo.
“Nafikiri Serikali imekaa kimya kutoa matamko ama imekuwa ‘slow’ kuchukua maamuzi ama hatua stahiki hasa kwa watuhumiwa huko vijijini.
“Sote tumekaa vijijini ama tuna ndugu vijijini, Mtu anaweza kuibaa Baiskeli kijijini lakini masaa tu, anakamatwa. Lakini watuhumiwa wale wa vijiji wa mauaji ya watu wenye albinism kwa nini ichukue muda wasikamatwe?.
MO DEWJI BLOG:Tuambie inakuaje katika suala la kisheria?.
Dk. POSSI:“Sidhani kama kuna kitu kigumu kuwachukua watuhumiwa vijijini, wakati mtu akiiba baiskeli baada ya muda anakamatwa. Hapa nadhani suala la kisheria lipo kwa watu wote. Sheria inabidi ichukue mkondo wake kwa kuchukua maamuzi stahiki na ya haraka katika kuyafanyia kazi ikiwemo kuwakamata watuhumiwa popote walipo.

Tanesco na Helios Tower Tanzania wafanya warsha ya siku moja juu ya usambazaji wa Umeme

$
0
0
 
Eranus Thompson, Mkuu wa uendeshaji wa Kanda ya Dar Es Salaam na Pwani kutoka Kampuni ya Helios Tower Tanzania akizungumza jinsi Helios Tower wanavyoweza kusambaza umeme unaozalishwa na Tanesco wakati wa warsha ya siku moja na Wafanyakazi wa Shirika la Umeme la Tanzania (Tanesco) iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwl Nyerere.
 Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Usambazaji na Huduma kwa wateja kutoka Tanesco, Mhandisi Sophia Mgonja(mwenye nguo ya rangi nyekundu) akifuatilia warsha kuhusu usambazaji wa umeme iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwl Nyerere jijini Dar Es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Helios na Tanesco waliohudhuria warsha hiyo
 Wafanyakazi wa Tanesco wakifuatilia warsha hiyo.
 Mshauri kutoka Kampuni ya Helios Tower Tanzania, Dama Van Dan Berg akiwasilisha jinsi ya kampuni ya Helios Tower inavyoweza kufanya kazi katika kufunga minara.Picha na Josephat Lukaza - Lukaza Blog

TAARIFA MUHIMU KUTOKA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

$
0
0
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UBORESHAJI WA
DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA
KURA KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA
BIOMETRIC VOTER REGISTRATION (BVR) KATIKA KATA TISA (9) ZA HALMASHAURI YA MJI WA MAKAMBAKO KUANZIA TAREHE 23/2/2015 HADI 3/3/2015

MAFUNZO YA SIKU TATU KWA WAFANYAKAZI WA SEKTA YA AFYA ZANZIBAR

$
0
0
Mkuu wa kitengo cha kufuatilia mwenendo wa maradhi Zanzibar Dkt. Salma Masauni akitoa neno la shukrani mara baada ya kumaliza mafunzo ya siku tatu juu ya kukabiliana na ugonjwa wa Ebola, mafunzo hayo yamezaminiwa na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) huko Hoteli ya Zanzibar Beach Resort.
Mwakilishi kutoka shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO)Tanzania Dkt. Grase Saguti akiwataka wafanyakazi wa sekta ya Afya Zanzibar kuyatumia vyema mafunzo waliyoyapata.
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akiyafunga mafunzo ya siku tutu ya kukabiliana na ugonjwa wa Ebola, mafunzo hayo yanafanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mjini Unguja. Picha na Makame Mshenga- Maelezo Zanzibar.

MAGUFULI ATOA SIKU 14 KWA WAKALA WA MAJENGO KUANZA KUKARABATI OFISI YA MKUU WA WILAYA YA SIHA NA MOSHI

$
0
0

WAZIRI wa Ujenzi Dkt. John Magufuli ametoa siku 14, kwa Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA), kuanza ukarabati wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Siha na Moshi baada ya kubainika majengo hayo kujengwa chini ya kiwango.

Dkt. Magufuli pia ameagiza aliyekuwa meneja wa TBA Mkoa wa Kilimanjaro, Paul Ndossa kusimamishwa kazi mahali alipo ili arejee kujibu tuhuma na kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria.

Waziri huyo alitoa agizo hilo wakati akikagua jengo la mkuu wa Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro baada ya kupewa taarifa za jengo hilo kujengwa chini ya kiwango hali iliyosababisha shughuli za mkuu wa Wilaya ya Siha kuhamishiwa kwenye ofisi za maji za halamashauri hiyo.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji mkuu wa TBA Elius Mwakalinga alisema wakala hao wanasikitishwa na kasoro za kiufundi zilizojitokeza katika jengo hilo na watawachukulia hatua wote waliohusika katika kuchangia majengo hayo kuwa chini ya kiwango.

Mwakalinga amesema tayari TBA imefanya tathmini ya gharama za ukarabati wa jengo la Wilaya ya Siha ambao utafanyika katika kipindi cha wiki 18 na kugharimu shilingi milioni 50.

Majengo ya ofisi za wakuu wa Wilaya za Siha na Moshi yalijengwa kwa usimamizi wa TBA ambapo wahusika walishindwa kuyatumia wakihofia usalama wao baada ya kuona dosari.

President of FC Barcelona visits Etisalat’s stand at the World Congress in Barcelona, Spain

$
0
0
  Barcelona, March 5th, 2015:Mr. Josep Maria Bartomeu, President of FC Barcelona, and the CEO of FCB were welcomed at Etisalat’s stand by Mr. Ahmad Julfar, Etisalat Group CEO during Mobile World Congress (MWC) which was held in Barcelona, Spain from 2-5 March, 2015.


Etisalat is the sponsor and official partner of FC Barcelona.

Mashabiki wamtaka Rose Muhando,Msama apata kigugumizi

$
0
0

MASHABIKI   kadhaa  wa  muziki  wa Injili  Tanzania  wametamka kumtaka  muimbaji  nguli  wa  muziki  wa  Injili  kuwemo  katika  orodha  ya  waimbaji  watakaopanda  jukwaani  kwenye  Tamasha  la  Pasaka  linalotarajia  kufanyika  mwezi  ujao hapa nchini.
 
Voster  Maulid  na Kassim Mtolea wa  jijini  Mwanza  wanampenda kwa kiasi kikubwa muimbaji huyo hasa anapokuwa jukwaani.Mashabiki  hao  walisema  muimbaji  huyo  akifanikiwa  kupanda  jukwaani anasaidia  kuteka  idadi  kubwa ya mashabiki  wanaohudhuria matamasha anayohudhuria.
 
Naye  Method  Millanzi  wa Mtwara  alisema Rose Muhando ni muimbaji asiye na mpinzani Tanzania, hivyo  Kamati ya maandalizi isimuache muimbaji huyo katika mchakato wa tamasha la mwaka huu.Mkurugenzi wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema wamesikiliza kilio cha mashabiki wa muziki huo, wamelipokea suala hilo na watalifanyia kazi.
 
Msama  alisema  yeye  na  kamati  yake  wanaendelea  na  mchakato  wa maandalizi, watatumia  fursa  hiyo kulijadili suala hilo.

SERIKALI YAANZISHA MFUMO WA KIELEKTONIKI KUSIMAMIA UTOAJI WA HUDUMA ZA ARDHI NCHINI.

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akitoa ufafanuzi wa mfumo wa kielektroniki utakaosimamia utoaji wa huduma katika sekta ya ardhi.

Na. Aron Msigwa –MAELEZO.


SERIKALI imeanza kutekeleza mpango wa kusimika mfumo funganishi wa kielektroniki (Intergrated Land Management Information Systeam) utakaosimamia sekta ya ardhi nchini na kupunguza muda, gharama za upimaji na upatikanaji wa hati miliki za ardhi kwa wananchi.

Akizungumzia uanzishwaji wa mfumo huo leo jijini Dar es salaam, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amesema  mfumo huo wa kisasa utawawezesha wananchi kupata hati za umiliki  wa ardhi na taarifa zao za malipo na matumizi ya ardhi katika ngazi za vijiji, wilaya, kanda hadi taifa.

 Amesema utekelezaji wa mradi huo utasimamiwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ufadhili wa Benki ya dunia kupitia ofisi ya Waziri Mkuu na kuongeza kuwa utekelezaji wa mradi huo utafanyika kwa awamu mbili itakayohusisha uundwaji wa programu hiyo na majaribio ya mfumo huo katika kanda zilizochaguliwa za mikoa ya Dar es salaam,Pwani na Morogoro.

Mhe. Lukuvi ameeleza kuwa utekelezaji wa mradi huo mkubwa pia utaambatana na utoaji wa hati mpya za umiliki wa ardhi na kufuta za zamani,  upigaji wa picha za anga kwa mfumo wa Satelite, ujenzi wa kituo cha kutunza kumbukumbu za ardhi kitaifa pamoja na uelimishaji wa jamii kuhusu matumizi ya mfumo huo.

Amesema awamu kwanza itatekelezwa kwa muda wa miaka miwili kuanzia Machi 2015 hadi 2016 na kugharimu kiasi cha dola za Kimarekani milioni 35 huku awamu ya pili ikihusisha uboreshaji wa mfumo huo kutokana na matokeo mazuri yatakayopatikana kwenye awamu ya kwanza ili kuwezesha mfumo huo kusambazwa nchi nzima.

Akitaja faida za kusimikwa kwa mtambo huo nchini amesema utasaidia kuhifadhi  taarifa za wananchi kwa uhakika  na usahihi pamoja na matumizi ya ardhi kote nchini pia  utarahisisha upatikanaji wa hati za umiliki wa ardhi kwa wananchi wengi zaidi tofauti na ilivyo sasa kutokana na ongezeko la kasi ya upimaji wa ardhi

Aidha, amesema mfumo huo utaondoa vitendo vya utoaji wa hati zaidi ya moja kwenye viwanja, kuondoa hati pandikizi na kuongeza uwazi wa taarifa kwa kuwawezesha wananchi wanaomiliki ardhi kupata taarifa zao kupitia  simu za mkononi.

“Nawahakikishia watanzania kiama cha matapeli wa ardhi kimefika ,teknolojia hii ni ya kisasa na Tanzania itakua nchi ya pili barani Afrika kuwa na mfumo wa aina hii, Serikali tumelenga kuondoa kabisa kero na ukiukaji wa maadili  uliokuwa ukifanywa na baadhi ya watendaji wa serikali wasio waaminifu katika utoaji wa hati za viwanja nchini” Amesisitiza.

Amefafanua kuwa kufungwa kwa mitambo hiyo ya kielektroniki katika kanda 7 nchini kutawezesha kila sehemu ya ardhi kupimwa  na kuongeza thamani ya ardhi na mapato ya Serikali yatokanayo na ardhi huku na kueleza kuwa nchi ya Uganda ambayo sasa inatumia mfumo huo imenufaika kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwa na taarifa sahihi za ardhi na matumizi yake.

Amewataka wananchi na watendaji wanaosimamia sekta ya ardhi kote nchini wajiandae kupokea mabadiliko hayo kwa kuanza kutunza kumbukumbu  sahihi za za viwanja wanavyomiliki ambazo zitaingizwa kwenye mfumo huo na wao kupewa hati mpya za kielektroniki.

Pia amewatoa hofu wananchi kuwa zoezi la upimaji wa maeneo ambayo bado hajapimwa hususani yale yenye hati zilizotolewa na vijiji na zile za kimila katika maeneo mbalimbali nchini litaenda sambamba na utoaji wa hati mpya za kielektroniki.

Katika hatua nyingine Mhe. Lukuvi amesisitiza kuwa zoezi la bomoa bomoa linalosimamiwa na wizara yake katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam sasa litafanywa katika mikoa mingine kwa lengo la kusimamia sheria ya ardhi namba 4 ya mwaka 1999 kifungu namba 175(1) inayozuia mwananchi yeyote kuingia na kuendeleza  kwenye ardhi asiyoimiliki kisheria. 

“Naomba wananchi watupe ushirikiano,haki lazima itendeke kazi hii tumeianza katika jiji la Dar es salaam na tunaendelea nayo katika maeneo mengine nchini ambako kuna vitendo vya dhuruma na uvamizi wa ardhi unaofanya na baadhi ya watu kinyume cha sheria”

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NA UJUMBE WAKE AENDELEA NA ZIARA YAKE JIMBO LA KONGWA MKOANI DODOMA.

$
0
0
Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Mkoka wakitazama Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake ukikatiza kwenye moja ya daraja wakati wakielekea katika kijiji hicho cha Mkoka,Wilayani Kongwa mkoani Dodoma,Ndugu kinana aliweka jiwe la msingi la kitega uchumi cha tawi la CCM pamoja na kufungua Ofisi ya CCM Tawi la Mkoka
 Mamia ya Wananchi wa kijiji cha Mkoka wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa kijiji hicho kumsikiliza Katibu Mkuu waa CCM,Ndugu Kinana na Ujumbe wake katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo,wilayani Kongwa mkoani Dodoma.
Kikundi cha ngoma ya asili ya Kigogo,kiitwacho KIFARU kitumbuiza katika uwanja wa kijiji cha Mkoka kabla ya mkutano wa hadhara kuanza.
Mbunge wa jimbo la Kongwa na Naibu Spika wa Bunge,Mh.Job Ndugai akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Mkoka,kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo wilayani Kongwa mkoani Dodoma.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Mkoka,kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo wilayani Kongwa mkoani Dodoma.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia mamia ya wakazi wa kijiji cha Mkoka jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwaja wa kijiji cha Mkoka,Wilayani Kongwa mkoani Dododoma.Ndugu Kinana akiwa amembatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa,Nape Nnauye anaendelea na ziara yake ya siku tisa mkoani humo,akikagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ikiwemo sambamba na kuimarisha uhai wa chama,kusikiliza matatizo ya Wananchi na kuyatafutia ufumbuzi.
Mamia ya wakazi wa kijiji cha Mkoka wakishangilia jambo wakati
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo katika mkutano wa hadhara Wilayani Kongwa mkoani Dododoma.Ndugu Kinana akiwa amembatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa,Nape Nnauye anaendelea na ziara yake ya siku tisa mkoani humo,akikagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ikiwemo sambamba na kuimarisha uhai wa chama,kusikiliza matatizo ya Wananchi na kuyatafutia ufumbuzi.

 sehemu ya umati wa watu wakimsikiliza katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mkoka,Wilayani Kongwa.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwa wamefuatana na wananchi walipokuwa wakiwasili katika uwanja wa Mkoka kwa ajili ya kufanya mkutano wa hadhara,mbali ya Uongozi huo wa juu wa CCM,pia waliambatana Mbunge wa jimbo la Kongwa Mh.Job Ndugai,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mh.Chiku Galawa,Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma,Mh.Addam Kimbisa pamoja na viongozi wengine wa wilaya.
Baadhi ya akina mama wa kijiji cha Chamae kata ya Hogolo wakimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake,wilayani Kongwa.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pichani juu ya jengo akiwa sambamba na Mbunge wa jimbo la Kongwa Mh.Job Ndugai wakishiriki ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Njoge,Kata ya Njoge pamoja na kusalimia Wananchi wa eneo hilo.
Jengo la zahanati hiyo ya Kijiji cha Njoge kama lionekavyo kwa nje,ujenzi wake ukiendelea kwa kasi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Njoge,mara baada ya kushiriki ujenzi wa Zahanati ya kijiji hicho,wilayani Kongwa,mkoani Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma,Mh Adam Kimbisa akizungumza mbele ya wanakijiji cha Njoge na  kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana kwa ajili ya kuwasalimia na kuzisikiliza kero zao.
katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na baadhi ya viongozi wa dini,wakati alipokuwa akiwasili katika kijiji cha Njoge,wilayani Kongwa kwa ajili ya kushiriki ujenzi wa Zahanati ya kijiji na kusikiliza matatizo ya Wananchi hao.
Mbunge wa jimbo la Kongwa Mh.Job Ndugai akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mara baada ya kushiriki ujenzi wa dara la shule ya msingi Mlali,katika kijiji cha Mlali Wilayani Kongwa.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki ujenzi wa matofali kwa ajili ya darasa la shule ya msingi Mlali,katika kijiji cha Mlali Wilayani Kongwa,anaeshuhudia kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mh Chiku Galawa.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizindua mradi wa maji katika kijiji cha Mlali Wilayani Kongwa,mradi huo uliogharimu zaidi ya shilingi milioni mia sita ulianza kujengwa mnamo mwaka 2013 na kutarajiwa kumalizika mei 2014,lakini kwa bahati mbaya mradi huo haukukamilika kwa wakati kutokana na ukosefu wa fedha.Mbunge wa jimbo hilo la Kongwa,Mh.Ndugai alieleza kuwa mradi huo kwa sasa umekwishakamilika kwa asilimia tisini na kwamba mradi huo wa maji safi na salama utawanufaisha wanakijiji wapatao mia saba na zaidi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akitoka kushiriki kupalilia shamba la kijiji katika Kata ya Iduo,wilayani Kongwa
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana wa pilia shoto akishiriki kupalilia shamba la kijiji la Alizeti katika Kata ya Iduo,wilayani Kongwa,shoto kwake ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma,Mh.Adam Kimbisa.

RAIS KIKWETE AZINDUA RASMI STUDIO MPYA ZA AZAM TV JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe akiwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara pamoja na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Azam TV wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam leo Machi 6, 2015.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Naibu Mkurugenzi wa Azam TV Bw. Dunstan Tido Mhando wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam leo Machi 6, 2015.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitangaza rasmi kuzinduliwa kwa studio mpya za stesheni ya Azam TV Tabata Relini jijini Dar es salaam leo Machi 6, 2015. Pamoja naye kwenye kilinge cha utangazaji ni mmiliki wa stesheni hiyo Bw. Saidi Salim Bakhressa.

PSPF YASAIDIA KITUO CHA KULEA WATOTO WALIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU, VINGUNGUTI JIJINI DSM

$
0
0
Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (kulia), akipena mikono na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Vingunguti-Butiama jijini Dar es Salaam, Elvis Bwahama, wakati akikabidhi msaada wa mifuko ya saruji tani 3 na mabati, kwa ajili ya ujenzi kwenye kituo cha kulea watoto walio katika mazingira magumu, cha Lukema. Hafla ya kukabidhin msaada huo kwa kituo hichomnkinacholea watoto 70, ilifanyika Ijumaa Machi 6, 2015. Kushoto ni mwenyekiti wa kituo hicho, Fatuma Ramadhani.

Baadhi ya watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho wakisubiri kukabidhiwa msaada huo

Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (kulia), akiteta jambo na mmoja wa watoto wanaolelewa kwenye kituo cha kulea watoto walio katika mazingira magumu cha Lukema, kilichoko Vingunguti-Butiama jijini Dar es Salaam Ijumaa Machi 6, 2015. Mfuko huo umetoa msaada wa saruji na mabati kwa ajili ya kupanua ujenzi wa kituo hicho kinacholea watoto 70 kwa sasa

Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (kulia), akizungumza jambo wakati alipofika kutoa msada wa saruji na mabati kwa niaba ya Mfuko huo kwa kituo cha kulea watoto waishio katika mazingira magumu, kituo cha Lukema, Vingunguti-Butiama jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Machi 6, 2015.

Mwenyekiti wa Kituo cha kulea watoto walio katika mazingira magumu cha Lukema, kilichoko Vingunguti-Butiama jijini Dar es Salaam, Fatuma Ramadhani, akizungumza kwenye hafla ya kupokea msaada wa saruji na mabati vilivyotolewa na Mfuko huo kwa ajili ya ujenzi.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Vingunguti-Butiama jijini Dar es Salaam, Elvis Bwahame, (kushoto), akizungumza wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano. Kulia ni mkurugenzi wa kituo, Lukondo Mchundo


Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (aliyechuchumaa katika), na mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Vingungjuti-Butiama jijini Dar es Salaam, Elvis Bwahame, (aliyesimama kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto hao

Angalia Video za maswali na majibu za mkutano wa Mhe. Jussa, Sehemu ya kwanza hadi ya Tisa

$
0
0
Muwakilishi wa Jimbo la Stone, Town, Zanzibar Mhe. Ismail Jussa kupitia chama cha wanainchi CUF ambae pia mjumbe wa UKAWA aliweza kuongea na waTanzania waishio. (DMV) na kumuuliza maswali mbali mbali kuhusu mustakabali wa nchi yetu, Siku ya Jumamosi Feb 28, 2015.

Stara T aachia wimbo wa Siku ya Wanawake Duniani

$
0
0

Msanii Stara T, ametoa wimbo mpya UWEZESHWAJI WA MWANAMKE ambao ni maalum kwa ajili ya siku ya kinamama dunia inayoadhimishwa Machi 8 ya kila mwaka.

MKURUGENZI MKUU MPYA WA TBL AKAGUA MAJENGO WALIYOYAKABIDHI KWA CHUO KIKUU CHA STEPHANO MOSHI

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL,Roberto Jarrin akiongozwa na mkufunzi katika Chuo Kikuu Kishiriki cha kumbukumbu ya Stephano Moshi,Gasper Mpehongwa kutembelea vyumba vya madarasa ambavyo vinatumika kwa ajili ya masomo pamoja na mitihanikatika eneo la TBL mjini Moshi.Eneo hilo limetolewa na TBL kwa chuo hicho ikiwa ni kurudisha sehemu ya faida inayopatikana kwa wananchi.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL,Roberto Jarrin akiwa ameambatana na mkuu wa chuo Kikuu Kishiriki cha kumbukumbu ya Stephano Moshi,Profesa Anord Temu,wakati akitembelea majengo ya jengo hilo mjini Moshi.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL,Roberto Jarrinakizungumza wakati wa mkutano wake na waaandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuanza kwa ziara ya kutembelea kiwanda cha kimea cha Moshi nachuo kikuu kishiriki cha kumbukumbu ya Stephano Moshi,
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL,Roberto Jarrinakizungumza wakati wa mkutano wake na waaandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuanza kwa ziara ya kutembelea kiwanda cha kimea cha Moshi na chuo kikuu kishiriki cha kumbukumbu ya Stephano Moshi,
 Meneja Udhamini wa kampuni ya Bia Tanzania,(TBL), George Kavishe  akizungumza na wanahabari (hawako pichani) juu ya msimu wa 14 wa mbio za kimataifa za Kilimanjaro Marathoni 2015 zilizofanyika mkoani Kilimanjaro.
 Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Roberto Jarrin akiwa ameongozana na viongozi wengine wa TBL kutembelea kiwanda cha kutengenezea Kimea kwa ajili ya kutayarisha Bia kilichopo Moshi mkoani Kilimanjaro.
 Baadhi ya viongozi wa TBL wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzimkuu wa TBL ,Roberto Jarrin muda mfupi mara baada ya kutembelea kiwanda cha kuzalisha Kimea cha Mjini Moshi,
 Mkurugenzi mkuu  wa kampuni ya Bia Tanzania ,TBL ,Roberto Jarrin,akizungumza jambo na Mkuu wa Chuo Kikuu kishirki cha kumbukumbu ya Stephano Moshi (SMMUCO), Anord Temu (kushoto) wakati alipofanya ziara kutembelea Chuo hicho ambacho eneo pamoja na majengo yanayomilikiwa na TBL yametolewa kwa chuo hicho.

Gharama za kuunganisha umeme shilingi 177,000. Atakayetoza zaidi ya hapo kufikishwa polisi - Ndassa

$
0
0
 Meneja Miradi kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Khalid James (kulia) akiieleza Kamati ya   Bunge ya Nishati na Madini  hatua iliyofikiwa ya   ujenzi wa miundombinu  ya umeme katika   mikoa ya  Iringa, Dodoma,  Singida hadi   Shinyanga inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Pili. Kamati ya  Bunge inafanya ziara katika  mikoa  ya Dodoma, Singida, Arusha na  Kilimanjaro  kwa  ajili ya kukagua miradi ya umeme   ili kujionea maendeleo  yake pamoja na kuzungumza na wananchi
 Meneja Miradi kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Khalid James (katikati) akitoa maelezo  mbele ya Kamati ya  Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu  maendeleo ya ujenzi wa njia kuu za umeme unaofanywa  na kampuni ya Jyoti Structures Limited kutoka India katika eneo la Nara mkoani Dodoma
Moja ya mrara kwa ajili ya njia  kuu ya umeme  ikiwa chini ya ujenzi  unaosimamiwa na kampuni ya Jyoti Structures Limited kutoka India. Nguzo moja inagharimu  shilingi  milioni 200.



Gharama za kuunganisha umeme  shilingi 177,000.
Atakayetoza zaidi ya hapo kufikishwa polisi – Ndassa

Machi 07, 2015

Na Greyson Mwase, Bahi - Dodoma

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya  Bunge ya Nishati na Madini , Richard Ndassa amewaambia wakazi wa kata ya  Ibihwa iliyopo Bahi mkoani  Dodoma kuwa  gharama  za kuuunganishiwa   huduma  ya  umeme zimeshuka hadi shilingi 177,000 na iwapo  ikatokea wakatozwa zaidi ya kiwango hicho, na watumishi wasio waaminifu basi wana haki ya kumfikisha mbele ya  vyombo  vya kisheria.

Ndassa alisema hayo  wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ilipotembelea wilaya ya Bahi kwa ajili ya  kukagua miradi ya umeme pamoja na kuzungumza na wananchi.

Ndassa alisema kuwa  Serikali imekuwa ikijitahidi kupunguza gharama za kuunganishiwa umeme hasa maeneo ya vijijini kupitia  Wakala wa Nishati  Vijijini (REA)  ili kuhakikisha kila mwananchi  anapata nishati  muhimu na kujiletea maendeleo.

Alisema kuwa kama  juhudi  ya Serikali katika kuhakikisha kila mwananchi anaondokana na umasikini, Serikali  kupitia REA iliamua kupunguza  gharama za kuunganishiwa umeme kwa wananchi wanaoishi  vijijini  ili waweze kupiga hatua kimaendeleo, na kuwataka kuchangamkia  fursa hiyo kwa kujiandaa na uwekezaji wa viwanda vidogo vidogo.

Alifafanua kuwa iwapo watatokea watumishi wasio waaminifu na kutaka kuwatoza fedha zaidi ya kiasi kinachotakiwa kulipwa, basi wana wajibu wa kuwafikisha katika vyomvbo vya  sheria.

“ Iwapo atatokea mtumishi na kuwatoza gharama zaidi ya ile inayohitajika kulipwa kisheria,  basi mna haki  ya  kumfikisha polisi ili afunguliwe mashtaka,” alisema Ndassa

Aliendelea kusema kuwa umefika wakati wa watanzania kuchangamkia fursa mbalimbali  zinazojitokeza mara baada ya kukamilika kwa miradi ya umeme kwani umeme ndio  kitovu  cha ukuaji wa uchumi katika nchi yoyote.

“ Kuna  vijiji ambayo  vimeshaanza kunufaika na huduma ya umeme, nawasihi muanzishe  viwanda vidogo vidogo  vya kukoboa nafaka, kukamua  mafuta ya alizeti ili kujiongezea kipato”, alisema Ndassa.

Wakati huo huo akizungumza kwa niaba ya wakazi wa kata hiyo , Mtendaji wa Kata, Jenipha  William  alisema kuwa katika utekelezaji wa miradi ya umeme  ya REA Awamu  ya Pili pamekuwepo na changamoto  ya vijiji  vingine kurukwa hali inayopelekea wananchi wachache kupata umeme.

Alisema kuwa hali hiyo inapelekea baadhi ya vijiji kupiga hatua kubwa kimaendeleo  huku vijiji  vingine  vikibaki  gizani

Akifafanua jinsi Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) lilivyojipanga  kukabiliana na changamoto hiyo mbele ya Kamati ya Kudumu  ya Bunge ya Nishati na Madini, Meneja wa Tanesco Dodoma, Zakayo  Temu  alisema kuwa  kazi ya kujenga miudombinu ya umeme chini ya REA Awamu ya Pili imekuwa ikifanywa kwa awamu  kulingana na fedha na uwiano na mikoa mingine.

Temu alisema ili kukabiliana na changamoto hiyo, shirika  limetenga bajeti ya mwaka  ujao wa fedha kwa ajili ya  vijiji vilivyokosa umeme.
 


Spika Makinda, Wenyeviti wa Bunge Watembelea Miradi ya NSSF Dar

$
0
0
Meneja Mradi wa NSSF, Mhandisi John Msemwa (mwenye kipaza sauti) akielezea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa zinazojengwa na shirika hilo Kigamboni jijini Dar es Salaam kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni. Meneja Mradi wa NSSF, Mhandisi John Msemwa (mwenye kipaza sauti) akielezea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa zinazojengwa na shirika hilo Kigamboni jijini Dar es Salaam kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni.Meneja Mradi wa NSSF, Mhandisi John Msemwa (mwenye kipaza sauti) akielezea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa zinazojengwa na shirika hilo Kigamboni jijini Dar es Salaam kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni. Meneja Mradi wa NSSF, Mhandisi John Msemwa (mwenye kipaza sauti) akielezea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa zinazojengwa na shirika hilo Kigamboni jijini Dar es Salaam kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni.Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda akitoa shukrani kwa uongozi wa NSSF mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea miradi anuai ya NSSF jijini Dar es Salaam, ambapo aliambatana na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge. Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda akitoa shukrani kwa uongozi wa NSSF mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea miradi anuai ya NSSF jijini Dar es Salaam, ambapo aliambatana na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge.Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Ramadhani Dau (mwenye kanzu) akitoa ufafanuzi kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea miradi mbalimbali ya NSSF ya jijini Dar es Salaam ukiwemo mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni. Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Ramadhani Dau (mwenye kanzu) akitoa ufafanuzi kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea miradi mbalimbali ya NSSF ya jijini Dar es Salaam ukiwemo mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni.Moja ya mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa unaotekelezwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) eneo la Kigamboni. Moja ya mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa unaotekelezwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) eneo la Kigamboni.
Baadhi ya viongozi wa NSSF wakimuongoza Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge katika ziara yao ya kutembelea miradi anuai ya NSSF jijini Dar es Salaam. Baadhi ya viongozi wa NSSF wakimuongoza Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge katika ziara yao ya kutembelea miradi anuai ya NSSF jijini Dar es Salaam.Naibu Katibu Mkuu, Joseph Nyamuanga (wa kwanza kulia) akitoa ufafanuzi kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni. Naibu Katibu Mkuu, Joseph Nyamuanga (wa kwanza kulia) akitoa ufafanuzi kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni.Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge wakitembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni. Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge wakitembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni.Meneja Mradi wa NSSF, Mhandisi John Msemwa akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum (MB) juu ya mradi. Wengine ni Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea miradi mbalimbali ya NSSF ya jijini Dar es Salaam ukiwemo mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni. Meneja Mradi wa NSSF, Mhandisi John Msemwa akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum (MB) juu ya mradi. Wengine ni Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea miradi mbalimbali ya NSSF ya jijini Dar es Salaam ukiwemo mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa KigamboniSpika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge wakitembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni. Mwenye kanzu ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Ramadhani Dau. Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge wakitembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni. Mwenye kanzu ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Ramadhani Dau.Meneja Mradi wa NSSF, Mhandisi John Msemwa (aliyenyoosha mkono) akielezea maendeleo ya mradi huo kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni. Meneja Mradi wa NSSF, Mhandisi John Msemwa (aliyenyoosha mkono) akielezea maendeleo ya mradi huo kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni.Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge wakitembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni. Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge wakitembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni.Meneja Mradi wa NSSF, Mhandisi John Msemwa (wa pili kushoto mbele) akitoa ufafanuzi juu ya mradi huo kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni. Meneja Mradi wa NSSF, Mhandisi John Msemwa (wa pili kushoto mbele) akitoa ufafanuzi juu ya mradi huo kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni.

  SPIKA wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda amelipongeza Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa miradi mikubwa mbalimbali linayoendelea kuwekeza nchini ambayo imekuwa chachu ya maendeleo na kukuza hadhi ya nchini. Spika Makinda ametoa kauli hiyo jana alipokuwa akitembelea baadhi ya miradi mikubwa ya NSSF iliyopo jijini Dar es Salaam, ukiwemo mradi wa ujenzi wa daraja la kubwa la kisasa linalojengwa kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na Mji wa Kigamboni pamoja na mradi mkubwa wa ujenzi wa Mji wa Kisasa unaojulikana kwa jina la Dege ECO Village unaojengwa kwa ubia pamoja na ujenzi wa nyumba za kisasa zenye hadhi mbalimbali kulingana na mahitaji ya watu. 

 Akizungumza wakati akitembelea miradi hiyo, Makinda alisema miradi hiyo mbali na kuleta maendeleo nchini inakuza hadhi ya nchi pamoja na kuirahisishia serikali katika utoaji huduma kwa wananchi wake. Aliiomba Serikali kupitia Wizara mbalimbali na jamii nzima kuendelea kutoa ushirikiano dhidi ya miradi hiyo kwani inachangia maendeleo kuanzia ngazi ya jamii pamoja na taifa kwa ujumla. Aliwataka wananchi kutumia fursa iliyopo ya kununua na kukopa nyumba zinazojengwa na shirika hilo kwani mbali na kujengwa kwa hadhi anuai na kisasa zimepangiliwa jambo ambalo linarahisisha utoaji wa huduma za jamii dhidi yao. 

 Alisema kwa maendeleo ya sasa ni nchi ya Tanzania pekee ambapo raia wake hujenga nyumba wenyewe, kwani mataifa mengi yaliyoendelea nyumba hujengwa na mashirika na kuuzwa kwa raia jambo ambalo huchangia kwa kiasi kikubwa uwepo wa miji iliyopangiliwa tofauti na ilivyo Tanzania. "...Duniani kote watu wanaojenga nyumba wenyewe hadi sasa ni Tanzania tu, na hii ndio chanzo kikubwa cha nchi yetu kuendelea na kuwa na miji ambayo haijapangiliwa (ujenzi holela). Lazima tubadilike unajua ukiwa na mji uliopangiliwa ni rahisi hata kuwahudumia wananchi wako...," alisema Makinda.

 Aidha alishauri uwepo wa utaratibu mzuri wa kukopesha nyumba za kisasa zinazojengwa na NSSF ili wahitaji wapewe na kulipa kwa awamu huku wakimilikishwa nyumba hizo jambo ambalo litaondoa adha ya upatikanaji wa makazi bora kwa wananchi. Katika ziara hiyo Spika Makinda aliambatana na Waziri wa Fedha Saada Mkuya, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Jenista Mhagama , Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka pamoja na Kamati ya Uongozi ya Bunge la Tanzania ambao kwa pamoja walilipongeza Shirika la NSSF na kushauri kuendelea kuwekeza pia katika mikoa mingine inayochipukia kimaendeleo kwa sasa ili kusambaza huduma maendeleo mengine. 

 Awali akitoa taarifa za maendeleo ya ujenzi wa daraja la kisasa la Kigamboni, Meneja Mradi wa NSSF, Mhandisi John Msemwa alisema licha ya changamoto zilizojitokeza mradi huo hadi sasa umekamilika kwa asilimia 75 ya ujenzi wake. Kwa upande wake, Mhandisi Juhus Nyamuhokya wa kampuni ya Ujenzi ya Hifadhi wabia wa NSSF katika ujenzi wa Kijiji cha kisasa cha 'Dege ECO Village' kinachojumuisha ujenzi wa nyumba 7,460 za kisasa zenye hadhi tofauti kulingana na mahitaji alisema ujenzi wake utajumuisha miaka minne ukijengwa kwa awamu tatu.

 Mhandisi Nyamuhokya alisema awamu ya kwanza ya mradi huo inakamilika Desemba 2015, awamu ya pili itakamilika Desemba 2016 huku awamu nyingine ikitarajiwa kukamilika Desemba 2017. Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Ramadhani Dau alimshukuru Spika wa Bunge la Tanzania Anne Makinda pamoja na wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Bunge kwa kutembelea miradi hiyo ambayo ina lengo lakuchochea maendeleo ya taifa na wananchi kiujumla.

MMILIKI WA KAMPUNI YA URBAN AND RULAR ENGINEERING PAMOJA NA WAJUMBE WAKE WAMTEMBELEA BALOZI LIBERATA MULAMULA

$
0
0
 Mkurugenzi na mmiliki wa kampuni ya urban and rular engineering ndugu Awadh Zuberi pamoja na ujumbe wake pichani wamemtembelea Balozi Liberata Mulamula, Kuanzia kushoto ni  ndugu Paula Mwafongo (Afisa Ubalozi uchumi),Bwa. Joseph Mnzanilla ,Mh.Bbalozi Mulamula,Bwa. Awadh Zuberi,Shemuni Halahala pamoja na ndugu Majid Zuberi wakiwa katika picha ya pamoja.
Mkurugenzi wa Urban and Rular  Engineering wa kwanza kulia ndugu Awadh  Zuberi na msaidizi wake Shemuni Halahala wakiwasili  Tanzania house ,ubalozini Washington, D.C.
Viewing all 46371 articles
Browse latest View live




Latest Images