Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 474 | 475 | (Page 476) | 477 | 478 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Katika harakati za kuhakikisha usafi katika mito na kuzuia mafuriko nyakati za mvua Pichani excavator la Manispaa ya Kinondoni likiwa kazini likisafisha mto Magomeni eneo la Magomeni Makuti.Kuripoti kutoka eneo la tukio ni Afisa Habari wa Manispaa ya Kinondoni Maria.


  0 0


  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa kifo cha Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Captain John Damian Komba kilichotokea jioni ya Jumamosi ya tarehe 28/02/2015. 

  Captain John Damian Komba ni msanii na mdau wa muda mrefu wa sekta ya Sanaa nchini. Amekuwa ni taa na nuru ambayo katika kipindi chote cha uhai wake imeangaza na kutoa mwanga angavu kwenye sekta ya Sanaa.

  Mchango wake katika muziki wa dansi, kwaya na ule wa kiweledi katika kuandaa na kukuza wasanii mbalimbali nchini hautasahaulika kamwe. Ni mdau aliyeacha alama kuu katika muziki wa bendi, kwaya na taarabu na amejitolea kwa kiasi kikubwa katika kuufikisha muziki wa dansi na kwaya mahali ulipo leo.

  Aidha, pamoja na kujiunga na siasa na hatimaye kuwa Mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi, Mheshimiwa Komba hakukoma kuendelea kuipigania sekta ya Sanaa kwani alikuwa ni mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii ambayo kwa mujibu wa kanuni za Bunge ndiyo inayoisimamia na kuishauri Serikali katika masuala yote yahusuyo sekta ya Sanaa na Utamaduni.

  Baraza, wasanii na wadau wote wa Sanaa hatuna budi kuendelea kuenzi mema yote aliyotuachia marehemu John Komba hasa katika kutunga nyimbo za hamasa na ujumbe makini na wenye mashiko kwa jamii yote ya Watanzania. Hakika pengo lililoachwa na Marehemu haliwezi kuzibika, kwani imekuwa ni kama mshumaa uliyozimika ghafla wakati tukiingia kwenye giza.

  Baraza linatoa pole kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Anne Makinda, wabunge na wadau wote wa Sanaa hususan wasanii kwa msiba huu. Ni matumaini ya Baraza kwamba, tutaendelea kuenzi mema yote yaliyotendwa na Marehemu, hasa kudumisha upendo na amani katika tasnia yetu ya Sanaa na taifa kwa ujumla.
  Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Amen

  Godfrey Mngereza
  KATIBU MTENDAJI


  0 0

   Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais Bw.Richard Muyungi (wa tatu kushoto) akiwa na Ujumbe kutoka Marekani, ukiongozwa na Bw. Trigg Talley (kushoto)ambaye pia ni  Mjumbe maalum na Balozi wa masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi walipokuwa katika kikao cha pamoja katika Ofisi  ya Makamu wa Rais, Kujadili kuhusu masuala ya mabadiliko ya Tabianchi na jinsi ambavyo nchi hizo mbili zitakavyoweza kushirikiana kutatua changamoto za mabadiliko ya Tabianchi.(Picha na OMR).
  Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais Bw.Richard Muyungi akieleza jambo, wakati alipokuwa akiongea na Ujumbe Maalum  kutoka Marekani kuhusu Masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi katika kukabiliana na tatizo hili, ambalo Nchi za Afrika zimekuwa zikiathirika zaidi.(Picha na OMR).

  0 0

   Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro Mohamed Lukwele kushoto akimkabidhi Meneja Ukuzaji Biashara na Masoko, Juma Mgori  mkataba wa makubaliano ya kuanza kuendesha mfumo wa ukusanyaji wa mapato anayeshudia katikati ni Meneja miradi wa Selcom Gallus Runyeta. Makabidhiano hayo yamefanyika Morogoro
  Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro Mohamed Lukwele kushoto akionesha mkataba walio saini na kampuni ya Selcom Tanzania baada ya kutiliana saini  kuanza kuendesha mfumo wa ukusanyaji wa mapato katikati ni Meneja miradi wa Selcom Gallus Runyeta. na Meneja Ukuzaji Biashara na Masoko, Juma Mgori  Makabidhiano hayo yamefanyika Morogoro.
   Ofisa Ugavi wa Manspaa ya Morogoro, Vincent Odero kushoto akijadiliana jambo na Meneja miradi wa Selcom Gallus Runyeta. kulia katikati ni Meneja Ukuzaji Biashara na Masoko, Juma Mgori  na Afisa techinolojia habari na mawasiliano 'TEHAMA' wa Manspaa haiyo Innocent Cosma 
   Mwanasheria wa Manispaa ya Morogoro Deusdepith Bishweko  kushoto akiwasomea mkataba Meneja miradi wa Selcom Gallus Runyeta. kulia na Meneja Ukuzaji Biashara na Masoko, Juma Mgori kabla ya kutia saini  kuanza kuendesha mfumo wa ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kielektonik
   Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro Mohamed Lukwele kulia akitia saini mkataba  na kampuni ya Selcom Tanzania na Meneja Ukuzaji Biashara na Masoko, Juma Mgori katikati na kushoto ni Meneja miradi wa Selcom Gallus Runyeta.

  0 0

  SERIKALI imesema itajitahidi kuhakikisha inalipa deni lote la mahindi yaliyonunuliwa kutoka kwa wakulima na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ifikapo Machi 30, mwaka huu.

  Akizungumza na maelfu ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana (Jumapili, Machi 2, 2015) kwenye uwanja wa CCM wa Vwawa wilayani Mbozi, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema Serikali imedhamiria kufuta deni lote.

  “Hapa Mbozi tulikuwa tunadaiwa sh. bilioni 21 lakini tumetoa sh. bilioni 4.5 kwa hiyo tutabakia na deni la kama sh. bilioni 16 ambalo tunajitahidi liwe limeisha ifikapo mwishoni mwa mwezi huu,” alisema.

  “Tunachoweza kuahidi kama Serikali ni kwamba, msimu huu hatutarudia kosa la mwaka jana ingawa mtihani mkubwa tulionao ni wa kushughulika na hifadhi ya chakula kwa kujenga vihenge (SILOS) ili hata kama kuna ziada n tusipate taabu ya kuhifadhi,” aliongeza.

  Alisema alishakwenda Poland kwa maelekezo ya Rais Jakaya Kikwete na wao wameshakuja kuona hali halisi ilivyo. “Tumependekeza vihenge vijengwe kwenye kanda za Mbeya, Rukwa, Dodoma, Dar es Salaam, Arusha au Kilimanjaro na Shinyanga ili iweze kuhudumia kanda ya Ziwa,” alisema.

  Wakati huo huo, Mbunge wa Mbozi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Godfrey Zambi amesema Serikali imekwishalipa zaidi ya sh. bilioni 81 na kwamba deni lililosalia linafikia sh. bilioni 59.

  “Hadi mwishoni mwa mwaka jana, tulikuwa tumeshalipa sh. bilioni 51.5/- na mwaka huu tumepata sh. bilioni 15 kutoka CRDB na hivi majuzi kuna bilioni nyingine 15 zimetoka Hazina… Agizo la Serikali ni kwamba mahindi yote yawe yamelipwa ifikapo Machi 30, naamini tutakamilisha,” alifafanua.

  Alielezea pia tatizo la maji linaloukabili mji wa Mbozi na vitongoji vyake na kueleza kwamba Serikali inashughulikia tatizo hilo katika programu mbalimbali.

  Mapema, akiwa katika ghala la nafaka la NFRA katika makao makuu ya wilaya ya Mbozi, Vwawa, Waziri Mkuu alielezwa kwamba kanda ya Makambako ambayo inajumuisha vituo vya Makambako na Vwawa imezidiwa uwezo na sasa wanalazimika kuhifadhi magunia ya mahindi nje kwa vile maghala yamejaa.

  Meneja wa Kanda hiyo wa NFRA, Bw. Abdillah Nyangasa alisema kanda hiyo ina uwezo wa kuhifadhi tani za nafaka 34,000 ambapo kati ya hizo, tani 22,000 ni maghala ya Makambako na tani 12,000 ni maghala ya Vwawa, Mbozi.

  Hata hivyo, Bw. Nyangasa alisema kanda hiyo kwa sasa kina tani za mahindi 79,496.8 zikijumuisha tani 15,738.9 za msimu uliopita licha ya tani 63,757.8 ambazo zimenunuliwa katika msimu huu.

  “Ili kukabiliana na uhaba wa maghala, kanda yetu hulazimika kufanya hifadhi ya nje (outside storage) kwa kutumia maturubai (tarpaulins) ili mahindi yasiharibiwe na hali ya hewa kama mvua au jua kali,” alisema Bw. Nyangasa.

  Waziri Mkuu anamaliza ziara yake ya siku saba mkoani Mbeya leo kwa kufanya majumuisho na kisha kurejea jijini Dar es Salaam.


  IMETOLEWA NA
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  JUMATATU, MACHI 2, 2015

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakeze Mama Zakhia Bilal na Mama Asha Bilal, wakitoa heshima zao za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Kapteni John Komba, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika leo Machi 2, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Baada ya shughuli hiyo mwili wa marehemu umesafirishwa kuelekea Kijiji cha Litui Wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma kwa maziko.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, wakati walipokutana kwenye Viwanja vya Karimjee baada ya kuhudhuria shughuli za kuaga mwili wa marehemu Kapteni John Komba leo Machi 2, 2015. Baada ya shughuli hiyo mwili wa marehemu umesafirishwa kuelekea Jijini cha Litui Wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma kwa maziko

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, wakati akimkaribisha Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Machi 2, 2015. Balozi Okada alifika ofisini kwa Makamu kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Machi 2, 2015, kwa ajili ya mazungumzo na kumuaga rasmi baada kumaliza muda wake wa kazi nchini.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na Balozi wa Japan nchini Tanzania, aliyemaliza muda wake wa kazi, Masaki Okada, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam. Balozi Okada alifika ofisini kwa Makamu kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.

  0 0


  MAMA wa Katibu wa Mbunge wa Viti Maalum Al Shaimar Kweigyir Semeni Kingaru, anayeitwa Kibibi Haji Pembe, amefariki Dunia leo saa tano asubuhi akiwa na umri wa miaka 80.
  Semeni Kingaru kulia ambaye ni Katibu wa Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaimar Kweigyir, akiwa na mama yake mzazi Bi Kibibi Haji, ambaye amefariki Dunia leo asubuhi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani.

  Mama huyo amefariki nyumbani kwake kijiji cha Misugusugu,wilayani Kibaha, mkoani Pwani, baada ya kuugua kwa muda mrefu.

  Mtoto wa marehemu huyo Kingaru ambaye ni Katibu wa mbunge Al Shaimar aliuambia mtandao huu kuwa mama yake atazikwa kesho saa 10 jioni kijijini hapo kwa ajili ya kumsitiri.

  Alisema kuwa kwa wanaopenda kushiriki kwenye msiba huo watalazimika kushuka katika kituo cha kijiji cha Misugusugu ambapo ndipo sehemu atakapozikwa marehemu mama yake.

  Msiba huo wakati unatokea, Kingaru alikuwa nchini Uganda katika majukumu yake na kulazimika kusitisha shughuli hizo kwa ajili ya kuwahi msiba wa mama yake.

  0 0

  Waziri wa Utalii na Maliasili Razalo Nyarandu akitoa nasaha za kuwaaga wafanyabiashara wa Tanzaia wanaoenda Berlin Ujerumani

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu akitoa nasaha za kuwaaga wafanyabiashara wa Tanzania wanaoenda Berlin, Ujerumani kushiriki maonyesho makubwa Duniani ya biashara maarufu kama ITB kuanzia Machi 4-8 mwaka huu.(Picha zote na modewjiblog)

  Na Andrew Chale wa modewji blog.

  Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu amewataka wafanyabiashara wa Tanzania wanaoenda kushiriki maonyesho makubwa Duniani ya biashara maarufu kama ITB, mjini Berlin, Ujerumani Machi 4 hadi 8, mwaka huu, kubeba uzalendo na kuitangaza Tanzania hususani vivutio vya Utalii na utajiri wa maliasili ili kuvutia wawekezaji.

  Nyalandu aliyasema hayo usiku wa Februari 27, wakati wa halfa fupi ya kuwaaga wafanyabiashara hao ambapo alisema kuwa, kwenda kwao huko kushiriki maonyesho hayo makubwa kabisa duniani, ni fursa kama Tanzania kupata kujitangaza zaidi na kuvutia wawekezaji.
  DSC_0151
  Deputy Head of Mission wa Ubalozi wa Ujerumani, John Reyels akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo.

  “Leo hii tunawaaga hapa. Nyie ndio Tanzania hivyo mnapokuwa huko mjue mmebeba watanzania wengine zaidi ya Milioni 40. Ni wakati wa kuvitangaza vivutio na uzuri wa Tanzania na ilikuongeza soko letu la Utalii na uwekezaji” alieleza Nyalandu.

  Pia aliongeza kuwa, Wizara yake ya Utalii itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha Taifa la Tanzania linafikia malengo yake yaliyokusudiwa ikiwemo kujitangaza ndani na nje ikiwemo kuendelea kuunga mkono juhudi za kupambana na Uharamia dhidi ya meno ya Tembo, wanyama na nyara za serikali kiwemo pembe za ndovu.
  Maofisa wa T.T.B, Devota Mdachi (kushoto) akiwa na Dorothy Masawe (Kulia) wa wizara ya Utalii, wakifuatilia jambo kwa makini wakati wa halfa hiyo
  Afisa wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Devota Mdachi (kushoto) akiwa na Dorothy Masawe (Kulia) kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, wakifuatilia jambo kwa makini wakati wa halfa hiyo.
  DSC_0131
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu akibdilishana mawazo na baadhi ya wageni waalikwa.
  DSC_0202
  Deputy Head of Mission wa Ubalozi wa Ujerumani, John Reyels (kulia), Afisa wa Ubalozi wa Ujerumani kitengo cha habari, John Meirikion (kushoto) wakiteta jambo na mmoja wa wageni waalikwa.

  CEO wa DHL ukanda wa Eastern Africa, Pramod Bagalwadi akisalimiana na Waziri wa Utalii, Razalo Nyalandu
  CEO wa DHL ukanda wa Eastern Africa, Pramod Bagalwadi, akisalimiana na Waziri Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu kwenye hafla hiyo.
  DSC_0103
  Baadhi ya wageni waalikwa ambao ni wafanyabiashara katika sekta utalii wakibadilishana mawazo kwenye hafla hiyo.
  DSC_0237
  DSC_0231
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu katika picha ya pamoja na Afisa wa Ubalozi wa Ujerumani kitengo cha habari, John Meirikion wakati wa hafla hiyo.
  DSC_0222
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu katika picha ya pamoja na wafanyabiashara akiwemo Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton Bw. Florenso Kirambata ( wa pili kushoto).
  DSC_0101
  Mkurugenzi wa Biashara wa Flight Link, Bw. Ibrahim Bukenya akiwa na Deputy Head of Mission wa Ubalozi wa Ujerumani, John Reyels wakati wa hafla hiyo.
  DSC_0145
  Wadau wakifurahi jambo.

  0 0

  Jeneza lenye mwili wa aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM,Marehemu Kapteni John Komba likiwa kwenye viwanja vya Karimjee,jijini Dar es salaam,wakati wa shughuli ya kuaga.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.Kapteni Komba anatarajiwa kuzikwa kijijini Kwake Litui wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma.
   Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Gharib Bilal na wake zake Mama Asha na Mama Zakhia wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
   Rais Mstaafu wa awamu ya pili,Alhaj Ali Hassa Mwinyi akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
   Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa na Mkewe Mama Anna Mkapa wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
   Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina Lowassa wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.

   Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania,Luteni Kanali Samuel Ndomba akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
   Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera na Uratibu wa Bunge,Mh. Jenista Mhagama akitoa heshima za mwisho akifuatana na Naibu IGP,Abdulrahman Kaniki.
   Kingunge Ngombale–Mwiru akitoa heshima za mwisho.
  Kamanda Kova.
  Baadhi wa Waheshimiwa Wabunge wakiifariji familia ya Marehemu.
  Mhe. Ole Sendeka akibubujikwa na machozi kuondokewa na Mbunge mwenzake.
  Familia ya Marehemu.
  Watoto wa Marehemu Kapteni John Komba wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu baba yao.
  Mjane wa Marehemu,Kapteni John Komba,Mama Salome Komba akiaga mwili wa mumewe
  Khadija Kopa.
  Umati wa viongozi mbali mbali pamoja na wananchi wakiwa kwenye viwanja vya Karimjee,jijini Dar es salaam wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Kapteni John Komba.

  Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera na Uratibu wa Bunge,Mh. Jenista Mhagama akitoa salamu za Serikali wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii,Mh. Saidi Mtanda akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya Kamati yake.
  Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Mh. Joshua Nassari akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni.
  Rais Dkt. Jakaya Kikwete akizungumza jambo na Mh. Joshua Nassari.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akitoa salamu za Chama.
  Mh. Muhongo akitoka kuaga mwili wa Kapteni Komba.
  Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa akisungumza jambo na Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana.kushoto ni Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda.
  Mama Regina Lowassa akizungumza jambo na Mama Sophia Kawawa.
  Mh. Mkapa akizungumza jambo na Mh. Anne Makinda.
  Mjane wa Marehemu.

  0 0

  Jeneza lenye mwili wa aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM,Marehemu Kapteni John Komba likiwa kwenye viwanja vya Karimjee,jijini Dar es salaam,wakati wa shughuli ya kuaga.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.Kapteni Komba anatarajiwa kuzikwa kijijini Kwake Litui wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma.
    Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Gharib Bilal na wake zake Mama Asha na Mama Zakhia wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
   Rais Mstaafu wa awamu ya pili,Alhaj Ali Hassa Mwinyi akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
   Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa na Mkewe Mama Anna Mkapa wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
   Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina Lowassa wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
  Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akiifariji familia ya marehemu.
   Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Luteni Jenerali  Samuel Ndomba akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
   Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera na Uratibu wa Bunge,Mh. Jenista Mhagama akitoa heshima za mwisho akifuatana na Naibu IGP,Abdulrahman Kaniki.
   Kingunge Ngombale–Mwiru akitoa heshima za mwisho.
  Kamanda Kova.
  Baadhi wa Waheshimiwa Wabunge wakiifariji familia ya Marehemu.
  Mhe. Ole Sendeka akibubujikwa na machozi kuondokewa na Mbunge mwenzake.
  Familia ya Marehemu.
  Watoto wa Marehemu Kapteni John Komba wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu baba yao.
  Mjane wa Marehemu,Kapteni John Komba,Mama Salome Komba akiaga mwili wa mumewe
  Khadija Kopa.
  Umati wa viongozi mbali mbali pamoja na wananchi wakiwa kwenye viwanja vya Karimjee,jijini Dar es salaam wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Kapteni John Komba.

  Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera na Uratibu wa Bunge,Mh. Jenista Mhagama akitoa salamu za Serikali wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii,Mh. Saidi Mtanda akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya Kamati yake.
  Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Mh. Joshua Nassari akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni.
  Rais Dkt. Jakaya Kikwete akizungumza jambo na Mh. Joshua Nassari.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akitoa salamu za Chama.
  Mh. Muhongo akitoka kuaga mwili wa Kapteni Komba.
  Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa akisungumza jambo na Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana.kushoto ni Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda.
  Mama Regina Lowassa akizungumza jambo na Mama Asina Kawawa.

  Mh. Mkapa akizungumza jambo na Mh. Anne Makinda.
  Mjane wa Marehemu.

  0 0


  0 0

  Mkuu wa kliniki ya Kisukari Hospitali ya Mnazi mmoja Dkt. Faiza Kassim (aliesimama) akizungumza na Waganga wa tiba asili na tiba mbadala kuhusu mashirikiano ya utibabu wa magonjwa ya kisukari na presha.Ili kuepuka mgonjwa mmja kutumia dawa za Hospitali na zile zinazotolewa na waganga hao.  wa3 
  Mmoja wa Waganga wa Tiba asili Bi. Zahra Hassan Ali akichangia katika semina hiyo iliyofanyika ukumbi wa Wizara ya Afya mnazi mmoja Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Uholanzi nchini Tanzania Mhe,Jaap Fredriks alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
  ba2 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na mgeni wake  Balozi wa Jamhuri ya Uholanzi nchini Tanzania Mhe,Jaap Fredriks alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo baada ya mazungumzo yao,[Picha na Ikulu.]

  0 0  0 0

  MENEJA wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Ulrich Urio ametoa wito kwa waandaaji wa Tamasha la Pasaka kuelekeza nguvu zao kupigia kelele wanyama wenye uhitaji maalum wanaomalizwa kila kukicha katika mbuga zetu za hifadhi.

  Kwa mujibu wa Urio wanyamapori hivi sasa katika wakisikia milio ya gari  na bunduki huanza kukimbia hovyo kusaka hifadhi, jambo ambalo linachangia kupoteza maliasili za Tanzania kama Tembo, Faru na wanyama wengineo.

  Urio alisema sambamba na Msama pia wito wa kuwalinda wanyama wetu unatakiwa kuongezewa nguvu pia na Chama cha Kutetea haki za Wanyama kwa sababu hivi sasa idadi kubwa ya wanyama wanauawa na majangili ambao wana nia ovu na Tanzania.

  Alisema wanyama wenye uhitaji kama Tembo sasa hivi hata kuonekana kwake ni kwa nadra kwa sababu ya kuwindwa lakini wanyama kama Simba huranda porini kwa sababu mahitaji yao hayafanani na Tembo.

  Kuhusu mauaji ya wenye ulemavu wa ngozi ‘albino’ alitoa wito kwa vyama na taasisi zinazoguswa na mauaji ya walengwa hao vitoe tiba ama ufuatiliaji wao usiishie kupiga kelele zisizo na mwelekeo na badala yake ziongeze ufanisi kwa kuwalinda ipasavyo wahusika hao.

  Urio alimalizia kwa kumpongeza Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama kwa kuwa karibu zaidi na jamii ambayo ina uhitaji maalum na kumuomba aongeze ufanisi zaidi katika kutekeleza majukumu yake.  

  0 0


  Nimewahi kuandika mara kwa mara kuhusu utaratibu mzuri wa kumwezesha mtu kununua nyumba huku akiwa ameepuka mgogoro. Nilitahadharisha sana kuhusu migogoro ya ardhi ambayo sasa imekuwa janga la kitaifa hapa kwetu. Nakumbuka moja kati ya mambo niliyoeleza ni kuwa utaratibu wa manunuzi ya nyumba/viwanja unatofautiana.Nikasema kwamba tofauti zake zinatokana na ukweli kuwa kila nyumba ina mazingira yake. Hata hivyo sikusema utofauti wa mazingira hayo ila sasa naweza kueleza kwa ufupi utofauti wa mazingira ya kila nyumba unapokuwa katika taratibu za ununuzi.

  1.UTOFAUTI WA KITAALAM KATIKA UNUNUZI NYUMBA.

  Usikurupuke unapohitaji kununua ardhi. Unapaswa kujua kuwa nyumba na viwanja zina taratibu tofauti unapohitaji kununua. Ukikurupuka utalipia gharama ya kukurupuka kwako. Kutokana na hilo ni muhimu tujue kuwa kuna nyumba inayouzwa kwa utaratibu wa kawaida wa mmiliki mwenyewe kumuuzia mnunuzi. Hii mara nyingi huwa haina shida sana kwakuwa unahitaji tu kujiridhisha na baadhi ya mambo ya msingi kama kufanya upekuzi rasmi ( official search) katika mamlaka za ardhi n.k.

  Pili kuna nyumba inayouzwa na wasimamizi wa mirathi. Hii uuzwaji wake hauko sawa na ile inayouzwa na mmiliki halisi. Hawa ni wasimamizi wa mirathi hivyo hata uuzaji wao si uuzaji kama wa mmliki halisi. Utofauti wao upo katika namna ya kuandika mkataba( sale agreement) na nyaraka ambazo wanapaswa kukuonesha wewe mnunuzi . Pia kuna ununuzi wa nyumba ya mkopo ambao sasa ndio mada ya leo. Ununuzi wa nyumba ya mkopo nao si ununuzi kama wa nyumba ya kawaida. Haufanani na nyumba ya kawaida na haufanani na wa nyumba ya mirathi. Unazo tarati bu zake tofauti kabisa na ununuzi mwingine.

  Kusoma zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli katikati akiweka jiwe na msingi kuashiria kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Mwanga-Kikweni-Vuchama-Usangi-Lomwe yenye urefu wa kilomita 40. Kulia kwake ni Waziri wa Maji ambaye pia ni Mbunge wa Mwanga Profesa Jumanne Maghembe, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama pamoja na viongozi wengine wa Wilaya ya Mwanga.
   Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli kushoto akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Musa Iyombe kabla ya kuweka jiwe la msingi katika barabara ya Mwanga-Kikweni-Vuchama-Usangi-Lomwe yenye urefu wa kilomita 40.6. Katikati ni Waziri wa Maji ambaye pia ni Mbunge wa Mwanga Profesa Jumanne Maghembe.
   Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama wakicheza ngoma na kikundi cha ngoma za asili Kikweni kabla ya uzinduzi wa barabara ya Mwanga-Kikweni-Vuchama-Usangi-Lomwe yenye urefu wa kilomita 40.
   . Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma na kikundi cha ngoma cha Msanja group kabla ya kuhutubia mamia ya wakazi wa Usangi kuhusu ujenzi wa barabara ya Kikweni-Usangi-Lomwe ambayo itaanza kujengwa hivi karibuni.
   Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli kushoto akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mama Ana Kilango Malecela katika sehemu ya Kihurio.Dkt. Magufuli ametangaza kujengwa kilomita tatu za lami katika eneo hilo pamoja na kuifanyia maandalizi ya kujengwa kwa kiwango cha lami barabara ya Mkomazi-Same yenye urefu wa km 96.
   Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiwahutubia mamia ya wakazi wa Kihurio Same Mkoani Kilimanjaro.
   Wakazi wa Usangi waliojitokeza kumsikiliza Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli
   Waziri wa Ujenzi akiwahutubia wakazi wa Gonja wakati akipita kukagua barabara ya Kihurio hadi Gonja maore Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro.

   Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiagana na wananchi wa Usangi mara baada ya kuwahutubia.
  Picha ya Pamoja Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli katikati akiwa pamoja na Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama, pamoja na Viongozi wengine wa Wilaya na Chama cha Mapinduzi mara baada ya kuhitimisha ziara yake katika Wilaya za Same na Mwanga mkoani Kilimanjaro.Picha zote kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano-Wizara ya Ujenzi

  0 0

  Meneja wa Benki ya Exim Tawi la Morogoro, Bi Anna Wesiwasi (wapili kulia) akipeana mkono na Mkurugenzi wa Kituo cha Amani cha watoto wenye ulemavu, Padri Beatus Sewando (watatu kulia) mara tu baada ya kuzindua jengo la kituo hicho kilichokarabatiwa na benki hiyo jana mkoani Morogoro. Akishuhudia ni Afisa Mauzo wa Benki hiyo Vick Haji (Kulia).

  Na Mwandishi wetu, Morogoro

  BENKI ya Exim Tanzania imefanya ukarabati wa majengo ya kituo cha watoto wenye ulemavu cha Amani kilichopo eneo la Chamwino mkoani Morogoro ikiwa ni muendelezo wa jitihada za benki hiyo kuboresha maisha ya jamii.

  Kupitia sera yake ya kurudisha sehemu ya faida yake kwa jamii, benki hiyo pia imejipanga kutoa misaada zaidi ikilenga mipango yenye kuleta maendeleo kwa jamii hapa nchini hususani katika maeneo ambayo benki hiyo tayari imefungua matawi yake.

  Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya ukarabati wa majengo ya kituo hicho iliyofanyika mkoani humo mwishoni mwa wiki iliyopita, Meneja wa tawi la benki hiyo mkoani Morogoro, Bi Anna Wesiwasi alisema msaada huo pia unalenga uboreshaji wa maisha ya watoto wanaoishi kwenye kituo hicho kwa kuwa wataishi kwenye makazi salama, safi na bora kwa afya zao.

  “Benki ya Exim siku zote tunaamini kuwa watoto wenye ulemavu wanahitaji kupewa matumaini zaidi na kwa kushiriki kwetu kwenye mipango ya maendeleo kama huu ndio tunatekeleza hiyo imani yetu kwa vitendo na zaidi tunazidi kuwa karibu na jamii inayotuzunguka jambo ambalo ni muhimu katika ulimwengu wa kibiashara kwa sasa kuona kwamba benki inarudisha sehemu ya faida yake kwa watu inao wahudumia,'' alisema Bi Wesiwasi

  Kwa mujibu wa Bi Wesiwasi, benki hiyo inaamini kuwa watoto ndio wateja wao wa kesho kama sio wa sasa na hivyo basi benki hiyo itajitoa kwa hali na mali kuhakikisha kwamba wanapata maisha bora kwa sasa .

  Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo,  Mkurugenzi wa kituo hicho, Padri Beatus Sewando alisema uamuzi wa benki hiyo kusaidia kituo cha watoto wenye ulemavu ni kitendo kinachotakiwa kuigwa na taasisisi, mashirika na watu mbalimbali hapa nchini.

  “Tunashukuru sana kuona wenzetu wa benki ya Exim wameonyesha mfano kwa kuitikia kilio chetu.Msaada huu utawahakikishia  watoto wetu hapa kituoni kuwa na makazi bora na salama kwaa afya zao…naomba wengione waige mfano huu,’’ alitoa wito

  0 0


  masaki 
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Balozi wa Japan Mhe.Masaki Okada ikulu jijini Dar es Salaam wakati balozi huyo alipokwenda kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi nchini.(picha na Freddy Maro)

older | 1 | .... | 474 | 475 | (Page 476) | 477 | 478 | .... | 1897 | newer