Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live

Rais Kikwete akagua vijiji vilivyoathiriwa na Mvua Chalinze

0
0
7
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma wakiwasili kwa helikopta katika kata ya Chalinze wakitokea jijini Dar es Salaam jana, kukagua uharibifu ulioletwa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali na kuharibu makazi ya watu na kujeruhi ambapo kaya 47 zikiathirika katika vijiji vya Msoga na Tonga.(picha zote na Freddy Maro)
2
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete pamoja na viongozi wa kata Ya Chalinze wakikagua baadhi ya nyumba zilzoharibiwa vibaya baada ya kuangukiwa na miti kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha katika kata ya Chalinze na kuathiri kaya 47.Rais Kikwete alikagua uharibifu huo, kuzungumza na kuwafariji wana vijiji hao na kuahidi kuwasaidia katika janga hilo
3
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakizungumza na wana vijiji waliopatwa na dhoruba la mvua.
45
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwafariji wana vijiji hao na kuahidi kuwasaidia katika janga hilo

  Na Freddy Maro Chalinze,Bagamoyo.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jana aliwafariji na kuahidi kuzisaidia kaya 40 ambazo nyumba zao ziliharibiwa vibaya na mvua mkubwa iliyoambatana na upepo mkali wiki iliyopita huko Chalinze,wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.

Katika ziara hiyo Rais Kikwete ambaye alikuwa amefuatana na mkewe mama Salma Kikwete alikagua Shule ya msingi Chalinze, Ofisi ya CCM, na nyumba kadhaa za wanakijiji ambazo ziliharibiwa vibaya na mvua hizo na kujeruhi baadhi ya wanavijiji walioangukiwa na nyumba zao.
 “Nimepata taarifa ya maafa yaliyotokea, sikuwepo kwahiyo nimekuja kuwapa pole.Poleni sana Kwa wale ambao nyumba zimeharibika serikali inao utaratibu wa kusaidia.Mkurugenzi akipata taarifa atajua jinsi gani ya kuwasaidia.Lakini kuna misaada tunayoweza kutoa.Nasikia Mbunge ametoa msaada wa chakula na dawa pamoja na matibabu.

Lakini Kwenye serikali tunao wajibu wetu.Mkurugenzi yupo taarifa zipilekwe kwake kwa uhakika ilitujue la kufanya.Poleni sana tutaendelea kusaidiana,” alisema Rais Kikwete ambaye pia ni Mkazi wa kijiji cha Msoga, kata ya Chalinze.

Mvua mkubwa iliyoambatana na upepo mkali wiki liyopita iliharibu kabisa majengo nane katika kata ya Chalinze ambapo kuta zilibomoka mabati kuezuliwa na upepo mkali na miti kuangukia nyumba na kujeruhi wana kijiji kadhaa ambao walitibiwa katika hospitali ya Tumbi.Kaya 47 kutoka vijiji vya Msoga na Tonga ziliathirika na mkasa huo.

MKUTANO MKUU WA JUMUIYA YA WAWEKEZAJI WA SEKTA YA UTALII ZANZIBAR (ZATI) WAFANYIKA MJINI UNGUJA.

0
0
mku1Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya ya wawekezaji wa sekta ya Utalii Zanzibar (ZATI) Bi. Pamela Mattheuu (aliesimama) akielezea hali ya Utalii ilivyo kwa sasa na kupanga mikakati ya kuitangaza zaidi sekta hiyo, huko Hoteli ya Double Tree by Hilton Shangani Mjini Zanzibar.
Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Abdulla Juma (Mabodi) akifungua Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya wawekezaji wa sekta ya Utalii Zanzibar (ZATI) katika Hoteli ya Double Tree by Hilton Shangani Mjini Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar). mku4 
Baadhi ya wanachama wa Jumuiya hiyo wakimsikiliza mgeni rasmin Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Abdulla Juma (Mabodi) kayupo pichani alipokuwa akifungua mkutano huo. mku5 
Mmoja wa wanachama wa ZATI Simai Mohamed Saidi akiuliza suali katika Mkutano huo uliofanyika Double Tree by Hilton Shangani Mjini Zanzibar.
mku6 
Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Abdulla Juma (Mabodi) wakatikati katika picha ya pamoja na Mwenyekiti Mstaafu wa Jumuiya ya (ZATI) Abdulsamad Said (kulia) na kushoto Makamu wake mstaafu Boby Mckena. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

MKAKATI WA KUENDELEZA ENEO LA MAPOROMOKO YA MTO KALAMBO MKOANI RUKWA WACHUKUA SURA MPYA, MKUU WA MKOA HUO AKAGUA UJENZI WA GETI LA KUINGILIA KATIKA MAPOROMOKO HAYO

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akitoa baadhi ya maelekezo kwa fundi anaejenga geti litakalotumika kutoza ushuru kwa watalii wa nje na wa ndani watakaofika kuona maporomoko ya mto Kalambo (Kalambo Falls) ambayo ni maporomoko ya pili kwa ukubwa barani Afrika. 

Maporomoko hayo ambayo yapo Mkoani Rukwa mpakani na nchi jirani ya Zambia yamekuwa yakinufaisha zaidi upande Zambia ambao wamejenga miundombinu kadhaa kuwawezesha na kuwavutia wanaofika kuona maporomoko hayo. 

Mto unaotengeneza maporomoko hayo upo nchini Tanzania na hata muoenekano mzuri unapatikana kutokea upande wa Tanzania. Kufuatia hali hiyo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya ameamua kusimamia kidete kuhakikisha miundombinu kadhaa inajengwa katika eneo hilo la maporomoko ili rasilimali hiyo adimu iweze kutambulilaka na kutoa mchango wa kiuchumi kwa taifa na Halmashauri husika ya Wilaya ya Kalambo.
Jengo ambalo litatumika kama geti la kuingilia katika maporomoko ya Mto Kalambo na ambalo pia litatumika kama eneo la kutoza ushuru kabla ya watalii kuingia kushuhudia maporomoko hayo likiwa katika hatua ya ujenzi wa awali.
 Afisa Habari Mkoa wa Rukwa Ndugu Hamza Temba akifurahia maajabu ya maporomoko ya Mto Kalambo.
 Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Ndugu Frank Maten(Kulia) na baadhi ya watalii wa ndani waliofika kuangalia maporomoko hayo wakifurahia maumbile ya asili ya eneo hilo. 
Picha ya pamoja.
(Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa@Rukwareview.blogspot.com)

Mazungumzo na Mhe. Balozi Mustafa Nyang'anyi....Sehemu ya mwisho

0
0
Karibu sana na asante kwa kujiunga nasi katika kipindi hiki cha HUYU NA YULE
Tumepata fursa ya kuongea na Mhe. Balozi Mustafa Nyang'anyi
Tumefanya mazungumzo naye ya sehemu nne, kueleza safari yake kimaisha
Na katika sehemu hii ya nne na ya mwisho ya mazungumzo yetu, Mhe Balozi Nyang'anyi anaanza kuelezea.

1:Tukio la ugaidi la Septemba 11, 2001  - walivyopata taarifa (kama wanadiplomasia), na kilichofuata
2: Jukumu la kukuza mwanya wa biashara kati ya Marekani na Afrika, ambalo lilisababisha kupitishwa kwa muswada wa sheria wa AGOA
3: Siku yake ya kawaida kama Balozi inavyokuwa na alizimudu vipi?
4: Kituo chake kipya cha kazi huko Abu Dhabi Julai 2002
5: Utata juu ya wajibu wa ofisi za ubalozi kwa wananchi wake
6: Maisha baada ya kustaafu
7: Kazi yake kama Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Ndege Tanzania (ATC)
8: Nani alioshirikiana  na kuhusiana nao kwa urahisi zaidi
9: Maisha yake ya kisiasa na BUSARA ZAKE
KARIBU
Kama ulikosa sehemu za awali, unaweza kuangalia Sehemu ya kwanza hapa, sehemu ya pili hapa na sehemu ya tatu hapa

THE MOHAMED AMIN AFRICA MEDIA AWARDS - CALL FOR ENTRIES

0
0
MAAMAS_MOSOUND_LOGO-2
Mohamed Amin Africa Media Awards – Celebrating Excellence
AFRICA24 MEDIA, the Pan African, international quality, multi-platform content provider, joins MoSound, East Africa’s premiere events company, to debut our new awards program that will honor the best quality, most innovative content, and rising platforms that are changing the face of Africa.

May 20-22 in Nairobi, Kenya we are inviting the continent’s media to learn at 6 daily workshops; discuss, at 3 daily symposiums; and win at our gala dinner. Today we start accepting nominations from both content makers, and their fans, on our awards website, www.mohamedaminama.com.
Awards will be given in the following categories:
BEST NEWSCAST
BEST SPORTS CONTENT
BEST USE OF VISUAL CONTENT IN SOCIAL MEDIA
BEST MAGAZINE PROGRAM
BEST CSR INITIATIVE PRESENTATION
BEST MOBILE PHONE CONTENT FEATURING AFRICAN IMAGES MOST INNOVATIVE PROGRAM
BEST DOCUMENTARY
STUDENT AWARD: I AM AFRICA
MAAMA’S BEHIND THE SCENES AWARD
PEOPLE’S CHOICE AWARD (VOTED AMONG ALL CATEGORIES)

Detailed descriptions and criteria for each award are available on the website. Workshops will feature expert instruction from international media professionals on Sports Event Coverage; News Writing; Effective Use of Social Media; Camerawork Innovation; Line Producing Newscasts; and Presenting on Talk Shows. Symposiums will line up prominent featured speakers to discuss Television Production Standards; Reporting on Crises/Disasters/Political Conflict in Africa; Media Freedom/Responsibility.


All categories are open to content in any language spoken in Africa, and encouraged from media organizations LARGE and small. Awards will include paid contracts to produce content for current and future AFRICA24 MEDIA productions.

A panel of respected judges will be announced in March, as well as our exciting venues and daily excursions to see some of the top tourists spots in Nairobi. Enter your productions or those you admire today, and you could wind up a finalist, with an all expense paid trip to Nairobi to participate in the 3-day event and be honored at the gala dinner.

The event has been officially announced from Chester House in Nairobi, where the renowned photographer and video journalist Mohamed Amin kept his office until his death in a plane crash in 1996. The Camerapix/ AFRICA24 MEDIA founder was passionate about quality television and trained many young Africans who found venerable careers in media here.

 His reports of the mid-80’s Ethiopian famine led to relief efforts that saved millions. His coverage of the rise and fall of Idi Amin, the assassination of Tom Mboya, the Soviet training base in Zanzibar and the coronation of Bokassa as Emperor of the Central African Republic, go down in journalistic lore. But he also favored Africa with dozens of coffee table books, beautiful travelogues and annual coverage of the East African Safari rally.

If my Dad was alive today, his son Salim says, “he would surely embrace every form of media, to reach people, to tell new stories, and to drive his business.”

He would also be proud that an event named after him would provide training and important dialogue about his profession. And he would be impressed that AFRICA24 MEDIA is offering prizes that include contracts to produce content for his company.

Africa’s current generation of TV professionals, as well as those about to launch their careers, can be proud to participate in categories honoring innovative programs, social media and, of course, the student award!
A video press release is also available at www.mohamedaminama.com

UNCDF CALL FOR INVESTMENT (PROJECT) PROPOSALS IN TANZANIA

0
0
uncdf 11
This United Nations Capital Development Fund (UNCDF) call for investment proposals is the first in Tanzania under the Local Finance Initiative (LFI) programme which is being implemented in partnership with the government of Tanzania through the Prime Minister’s Office – Ministry of Regional Administration and Local Governments (PMO-RALG).

MAKALA YA SHERIA: JIHADHARI, HAUTARURUHUSIWA KUFANYA TRANSFER AU KUPATA HATI IKIWA UNA MKATABA WA SERIKALI ZA MITAA.

0
0

Hapo awali niliandika namna sheria isivyowaruhusu viongozi wa serikali za mitaa kuandaaa na kusimamia mauzo na manunuzi ya nyumba au viwanja. Nikasema kitu hicho hakiruhusiwi katika sheria na wanaofanya hivyo hakika wako katika makosa makubwa. Nikasisitiza kuwa wewe ambaye mkataba wako umeandikiwa serikali za mitaa ujue wazi kuwa mkataba wako wa manunuzi hauna hadhi kisheria. Huu ni ukweli ambao nitazidi kuusema ili kuwaepusha watu na usumbufu na ili watu wasiendelee kuingia katika utapeli huu. Ndio, huu ni utapeli na ni jinai. Ni sababu hizihizi zinazowaingiza watu wasio na hatia kwenye migogoro ya ardhi na kuwapotezea hela zao.

1.HUWEZI KUFANYA TRANSFER UKIWA NA MKATABA WA SERIKALI ZA MITAA.

Kwa wale ambao waliwahi kufanyia mikataba yao ya manunuzi ya nyumba/viwanja serikali za mitaa halafu wakaamua kwenda ardhi kubadili jina watakuwa wamekutana na hiki kitu ninachoongelea hapa. Ikiwa ulifanya manunuzi ya ardhi na ukasimamiwa na serikali za mitaa basi ujue huwezi kubadilisha jina kutoka kwa aliyekuuzia kuingia jina lako. Na hapo ni vyote yaani hati au leseni ya makazi. Huwezi kabisa kubadilsha kimojawapo kati ya hivyo ikiwa mkataba wako ni wa serikali za mitaa.

Kusoma zaidi BOFYA HAPA

MSAMA PROMOTIONS LTD YAMWAGA MISAADA KWA VITUO VYA WATOTO YATIMA, YALAANI MAUAJI YA ALBINO YANAYOENDELEA NCHINI

0
0
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. Alex Msama akikabidhi vyakula mbalimbali kwa Halima Ramadhan Mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Mwandaliwa kilichopo Tegeta jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, ikiwa ni moja ya misaada inayotolewa katika vituo mbalimbali vya kulelea watoto yatima wakati wa msimu huu wa maadalizi ya Tamasha la Pasaka linalotimiza miaka 15 tangu lianzishwe.

Msama amekabidhi misaada hiyo kwa vituo vitano vya kulelea watoto waishio katika mazingira magumu,makabidhiano ya misaada hiyo ilifanyika kwenye ofisi za kampuni hiyo,Kinondoni jijini Dar.

Msama alisema kuw maandalizi ya tamasha hili yanaendelea vyema mpaka sasa,na kwamba tamasha hilo linatarajiwa kufanyika jijini Dar April 7 2105,ambapo litashirikisha waimbaji mbalimbali wa Kimataifa na wa Nchini,aliongeza kuwa ili kunogesha zaidi tamasha hilo pia kutakuwepo na michezo mbalimbali itakayochezwa ikiwemo na kukabidhi zawadi na vikombe kwa washiriki wa tamasha hilo.

katika hatua nyingine Bwa.Alex Msama amelaani matukio ya mauaji ya Albino hapa nchini,ameiomba Serikali kutilia mkazo katika janga hilo ambalo limekuwa likiibua na kuzua gumzo miongoni mwa jamii,hivyo ameiomba Serikali kuwashughulikia ipasavyo wahusika wote waliofanya na wanaofanya ukatili huo ambao ni kinyume kabisa na maadili ya nchi yetu,na ikibidi kukomesha kabisa matukio hayo ambayo yamekuwa yakilitia aibu Taifa letu.



WAZIRI MKUU AAHIDI BWAWA LA KUTUNZIA MAJI NYANZWA

0
0
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema anakubaliana na ombi la wakazi wa Nyanzwa na Igunda wilayani Kilolo, mkoani Iringa kuhusu ujenzi wa bwawa la kuhifadhia maji yatakayovunwa msimu wa mvua ili yasaidie kuongeza eneo la mradi wa umwagiliaji.

Ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akiwahutubia wakazi wa vijiji vya Nyanzwa na Igunda, mara baada ya kukagua mradi wa umwagiliaji wa Nyanzwa ambao ni maarufu kwa kilimo cha vitunguu.

“Huu mradi ni wa siku nyingi. Nimewauliza wataalamu niliokwenda nao wakasema ujenzi wa bwawa ndiyo suluhisho pekee la kuokoa mradi huu na kwamba ni jambo linalowezekana kama fedha zipo.”

Aliutaka uongozi wa mkoa uandae mpango kazi na wauweke kwenye bajeti ya mwaka ujao wa fedha ili mradi huo uweze kuombewa fedha kwenye bajeti kuu ya Serikali.  ia aliwataka wakazi wa eneo hilo wakitunze chanzo cha maji kwa kuweka mipaka ili watu wasikivamie na hatimaye kukiharibu.

“Tengeni eneo kwa kuweka mipaka. Mkurugenzi simamia uwekaji wa mipaka kwenye chanzo hiki ili tukilinde kwani uharibifu wa mazingira utakiharibu kabisa,” alisisitiza.

Akiwa katika ukaguzi wa eneo la mradi, Waziri Mkuu alikutana na mkulima mmoja wa vitunguu Bw. Furaha Ngalali (32) ambaye alimweleza kwamba mwaka jana alifanikiwa kulima ekari tatu za vitunguu ambazo zilimpatia kiasi cha milioni 6/- huku kila gunia akiwa ameliuza kwa sh. 70,000/-.

“Gharama kwa kila ekari ni karibu sh. 600,000/- kwa hiyo kwa ekari tatu ni sh. milioni 1.8/-. Tukivuna vitunguu tunaandaa bustani ya mbegu na pia humu tunapanda maharage,” alisema Bw. Ngalali alpoulizwa Waziri Mkuu analima eneo hilo mara ngapi kwa mwaka.


Alipoulizwa soko la vitunguu wanapata wapi, Bw. Ngalali alisema wanunuzi huwa wanavifuata huko huko Nyanzwa na kwamba wengi wao hutoka Dar es Salaam, Mbeya na Songea. Kijiji cha Nyanzwa kipo umbali wa kilometa 36 kutoka Ruaha Mbuyuni ilipo barabara kuu ya kuelekea Dar es Salaam na Mbeya.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka wakazi wa vijiji vya Nyanzwa na Igunda wajikite kwenye ufugaji wa nyuki kwani hauna gharama kubwa na unawawezesha wananchi kuinua kipato chao kwa haraka.

“Wakati mkisubiri ujenzi wa bwawa ili muongeze uzalishaji wa mbogamboga ni vema mkaangalia suala la ufugaji nyuki… licha ya kutumika kama sehemu ya kujiingizia kipato, pia ufugaji nyuki ni njia mojawapo ya utunzaji wa misitu,” alisema.

“Hapa mlipo kuna msitu mkubwa wenye migunga na mibuyu mingi tu. Yote hii imechanua maua mengi mno. Lazima tutumie uwepo wa misitu hii kama fursa ya kipekee ya kujiingizia kipato kwa kuweka mizinga ya nyuki. Unaweza usipate mahindi au vitunguu lakini asali ikawasaidia kuwapa kipato. Hivi sasa lita moja ya asali imefikia sh. 15,000/- hadi sh. 20,000/- na tena mtapata nta ambayo pia ina bei nzuri tu,” alisema.

Alisema kwa sasa asali inauzwa kwa bei ghali kwenye nchi mbalimbali baada ya kuongezeka kwa mahitaji yake na hasa ikizingatiwa kwamba inatumika kama dawa ya kutibu magonjwa mbalimbali na pia kwenye baadhi ya vipodozi.

Mapema, akisoma taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Mtendaji wa Kijiji cha Nyanzwa, Bw. Hekima Masanula alisema skimu ya umwagiliaji ya Nyanzwa ilijengwa mwaka 1960 wakati huo kwa kutumia banio la miti na magunia ya mchanga. Ilikuja kuboreshwa miaka ya 90 kwa ufadhili kutoka Jumuiya ya Ulaya na Serikali ya Sweden.

“Hata hivyo, skimu hii ambayo inahudumia wakulima 3,469 wakiwemo wanaume 1,662 na wanawake 1,807; inakabiliwa na uhaba wa maji kwani ni hekta 256 tu ambazo zinamwagiliwa kwa sasa wakati eneo lote la mradi ni hekta 940,” alisema Bw. Masanula.

Alisisitiza ombi la kujengewa bwawa kama njia pekee ya kuwakwamua wakazi hao kutokanana shida ya maji inayowapata hasa wakati wa kiangazi.

WALIMU ZAIDI YA 200 WALUNDIKANA MANISPAA YA IRINGA

0
0
 WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Bw. Ahmed Sawa akae pamoja na Afisa Elimu wake na kuwapunguza walimu 230 waliozidi mahitaji ya walimu kwenye manispaa hiyo na badala yake wawapangie kwenda vijijini.

Ametoa agizo hilo jana jioni (Jumapili, Februari 22, 2015) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa kata ya Ipogolo waliofika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Ipogolo, nje kidogo ya Manispaa ya Iringa.

“Manispaa inahitaji walimu 534 lakini waliopo ni 764. Hapa kuna ziada ya walimu 230 tena kw shuke za msingi... Mkurugenzi kaa na Afisa elimu wako muwaondoe walimu waliozidi na kuwapangia waende vijijini ambako kuna mahitaji zaidi,” alisema.

“Kwa upande wa shule binafsi nako pia tatizo ni lile lile. Walimu wamezidi. Mahitaji ni walimu 75 waliopo ni walimu 142 ... wanaozidi ni walimu 67,” alisema Waziri Mkuu.

“Sina tatizo na walimu wa shule binafsi kwa sababu wao wana mfumo wao wa ajira lakini hawa wa shule za Serikali ni lazima muwaondoe tena haraka sana. Waondoeni waende vijijini kwenye mahitaji makubwa sababu ualimu ni ualimu tu, siyo lazima mtu awe mjini ndiyo afundishe vizuri,” alisema.


Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliupongeza uongozi wa mkoa wa Iringa kwa kuwa na ufaulu wa juu kwenye shule za msingi lakini akawataka wajiulize ni kwa nini ufaulu huo umeanza kushuka tangu mwaka 2013.

“Mwaka 2010 kiwango cha ufaulu kilikuwa asilimia 77; mwaka 2011 kilikuwa asilimia 87; mwaka 2012 kilipanda na kufikia asilimia 97. Lakini mwaka 2013 kilishuka hadi asilimia 82 na mwaka jana ni kama kipo palepale kwani kilikuwa asilimia 82.5. Kaeni mjiulize kumetokea nini na mtafanya nini ili kurudi tena kwenye asilimia 97 au zaidi.”

Akizungumzia suala la afya, aliwaeleza wananchi hao kwamba ameuagiza uongozi wa mkoa kupitia watoa tiba wake waweke utaratibu wa kutoa elimu walau kila baada ya miezi miwili au mitatu ili wananchi wapate ufahamu wa magonjwa makuu yanayosumbua hivi sasa.

Akifafanua magonjwa ya akinamama, Waziri Mkuu aliyataja magonjwa hayo kuwa ni saratani ya matiti, saratani ya shingo ya uzazi na tatizo la fistula wakati kwa upande wa akinababa alisema wao wanahitaji kupatiwa elimu zaidi kuhusu ugonjwa wa tezi dume.

“Matatizo haya yanatibika lakini ni lazima watu waeleweshwe kwamba wakiwahi kwenda hospitali matatizo haya yanatibika lakini wakichelewa inakuwa tatizo zaidi,” alisema.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, FEBRUARI 23, 2015.

AMIN SALMINI AAHIDI KUIBORESHA OFISI YA SERIKALI YA MTAA KATA YA TABATA, WAKIFANYA SHEREHE YA KUWASHUKURU WAPIGA KURA WAO.

0
0
 Mtoto wa Rais Mstaafu wa awamu ya tano Zanzibar, Amin Salmin, akimkabidhi Cheti, Mwenyekiti wa UWT ambaye pia ni Kaimu Katibu wa CCM wa Tabata Relini, Shahani Mtwawa, wakati wa Sherehe maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwashukuru Wapiga Kura wa CCM, waliofanikisha kuchaguliwa kwa Viongozi wa Serikali ya Mtaa huo wa Kata ya Tabata. Sherehe hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika Ofisi za Serikali ya Mtaa Kata ya Tabata, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake mgeni rasmi huyo, aliahidi kuiboresha Ofisi hiyo ya Serikali ya Mtaa wa Tabata kwa kununua Fenicha za ofisi zisizopungua gharama ya Sh. M 1.5. Picha na Sufianimafoto.com
 Mtoto wa Rais Mstaafu wa awamu ya tano Zanzibar, Amin Salmin, akisaini katika kitabu cha wageni, mara tu baada ya kuwasili kwenye ofisi hizo.
 Mtoto wa Rais Mstaafu wa awamu ya tano Zanzibar, Amin Salmin, akimkabidhi Vifaa vya michezo (Jezi na Mpira)  Katibu Mwenezi wa Kata ya Tabata Relini, Ramadhan Mazongera,  wakati wa Sherehe maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwashukuru Wapiga Kura wa CCM, waliofanikisha kuchaguliwa kwa Viongozi wa Serikali ya Mtaa huo wa Kata ya Tabata. Sherehe hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika Ofisi za Serikali ya Mtaa Kata ya Tabata, jijini Dar es Salaam.
 Mtoto wa Rais Mstaafu wa awamu ya tano Zanzibar, Amin Salmin, akimkabidhi Vifaa vya Michezo (Jezi na Mpira) Mwakilishi wa Tawi la CCM la Mti Mgandisho Tabata, Bakari Mpakala, wakati wa Sherehe maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwashukuru Wapiga Kura wa CCM, waliofanikisha kuchaguliwa kwa Viongozi wa Serikali ya Mtaa huo wa Kata ya Tabata. Sherehe hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika Ofisi za Serikali ya Mtaa Kata ya Tabata, jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya Kinamama waliojitokeza kwenye sherehe hiyo.

  Mtoto wa Rais Mstaafu wa awamu ya tano Zanzibar, Amin Salmin, akikabidhi Meza na Viti, kwa  Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Tabata, Elisante Msangi (kulia)  wakati wa Sherehe maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwashukuru Wapiga Kura wa CCM, waliofanikisha kuchaguliwa kwa Viongozi wa Serikali ya Mtaa huo wa Kata ya Tabata. Sherehe hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika Ofisi za Serikali ya Mtaa Kata ya Tabata, jijini Dar es Salaam.
 Mtoto wa Rais Mstaafu wa awamu ya tano Zanzibar, Amin Salmin, akimtunza mwimbaji wa kundi la Segere lililokuwa likitoa burudani, wakati wa Sherehe maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwashukuru Wapiga Kura wa CCM, waliofanikisha kuchaguliwa kwa Viongozi wa Serikali ya Mtaa huo wa Kata ya Tabata. Sherehe hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika Ofisi za Serikali ya Mtaa Kata ya Tabata, jijini Dar es Salaam.
 Wasanii wa kundi la Segere wakiimba wakati wakitoa burudani katika Sherehe maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwashukuru Wapiga Kura wa CCM, waliofanikisha kuchaguliwa kwa Viongozi wa Serikali ya Mtaa huo wa Kata ya Tabata. Sherehe hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika Ofisi za Serikali ya Mtaa Kata ya Tabata, jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya kinamama wa CCM wakiserebuka wakati wa sherehe hiyo.
Mtoto wa Rais Mstaafu wa awamu ya tano Zanzibar, Amin Salmin, akimkabidhi Cheti, Katibu CCM Tawi la Tabata, Siza Mazongela,  wakati wa Sherehe maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwashukuru Wapiga Kura wa CCM, waliofanikisha kuchaguliwa kwa Viongozi wa Serikali ya Mtaa huo wa Kata ya Tabata. Sherehe hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika Ofisi za Serikali ya Mtaa Kata ya Tabata, jijini Dar es Salaam.

CALL FOR ARTISTS 2015 : KARIBU MUSIC FESTIVAL 6th (Fri) – 8th (Sun) NOVEMBER 2015, BAGAMOYO TANZANIA

0
0
Karibu Cultural Promotions Organization in collaboration with Legendary Music Entertainment and Promotions Company Limited are organizing the 2nd edition of the “Karibu Music Festival”, an annual Three (03) Days International cultural event aiming at African Culture Promotion to the world, as well as introducing other countries’ culture to Africa, and building up friendship/collaboration opportunities among all participants. In the aspects of music, dance, paintings, theater, crafts, and many others, all artists who can share our passion and goal together, you are welcomed to participate in this event to present your great talents and promote yourself!
The festival involves International artists from Africa, Europe, America, and Asia who will perform at the main stage and conduct their unique Workshop classes. This will be 100% LIVE performance among 3 days!! It will also feature Musicians selling and showcasing their CDs (Albums), craftsmen and artisans selling unique products, cultural food and drink vendors, Also a Cinema and graffiti venues for more art adventures. The big Live performance stage with the high quality sound system from Legendary Music will be set nearby the College of Arts and Culture Bagamoyo-TASUBA, from 6th(Fri) to 8th (Sun) of November 2015.
 Let us share the wonderful moment on the stage!!!
APPLICATIONS ONLINE www.karibumusic.org

Airtel kuendelea kusaidia walemavu hapa nchini kwa kuwaongezea vitendea kazi

0
0
Afisa masoko wa Airtel Haruna Ndyanabo (wa pili Kulia) akimkabidhi Rukia Salum (wapili Kushoto) mmoja kati ya walemavu waliowezeshwa na Airtel kwa kupatiwa vibanda vya kisasa vya Airtel Money ili kuweza kijipatia kipato na kuendeleza Maisha yao ya kila siku. Wakishuhudia ni baadhi ya walemavu wengine waliowezeshwa na Airtel katika mtaji huo.
Afisa masoko wa Airtel Haruna Ndyanabo (kushoto) akimkabidhi Peter Gwikama mmoja kati ya walemavu waliowezeshwa na Airtel kwa kupatiwa vibanda vya kisasa vya Airtel Money ili kuweza kijipatia kipato.
Afisa masoko wa Airtel Haruna Ndyanabo (Kulia) akimkabidhi Josephine John mmoja kati ya walemavu waliowezeshwa na Airtel kwa kupatiwa vibanda vya kisasa vya Airtel Money ili kuweza kijipatia kipato.


Katika kuendeleza shughuli zake za huduma kwa jamii kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imekabidhi simu za mkononi kama kitendea kazi kwa walemavu waliowezeshwa na Airtel kwa kupatiwa vibanda vya kisasa vya Airtel Money vyenye lengo la kuwawezesha kuwa wafanyabiashara wajasiriamali na kuwa mawakala wa huduma ya Airtel Money na kutoa huduma mbalimbali ikiwemo kuuza bidhaa za Airtel kupitia vibanda hivyo vilivyo katika sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Simu hizo zilibabidhiwa kwenye muendelezo wa mafunzo yao ya ujasiriamali yanayofanyika katika ukumbu wa Machinga Complex .

Akiongea wakati wa hafla ya makabidhiano, Afisa masoko wa Airtel Tanzania Haruna Ndyanabo alisema, “Airtel imeendelea kutoa mchango kwa jamii kwa kuhakikisha walemavu hao wanafikia ndoto zao, kwa kuendelea kuwapatia mafunzo mbali mbali ili kuhakikisha wanakuwa wafanyabiashara madhubuti na tunaamini msaada wetu utasaidia kuboresha maisha yao kwa kuwaongezea uwezo wakujiongezea kipato”.

“Kwani watu wanaoishi na ulemavu wanakabiliana na hali ngumu ya uchumi kuliko makundi mengine katika jamii” ukizingatia kwamba ulemavu siyo kigezo chakutoweza kufanya kazi.

Aliongeza kwa kusema “Shabaha ya kampuni ya Airtel hapa nchini sio tu biashara bali pia kuona maisha ya jamii zinazotuzunguka yananufaika na uwepo wetu kazi inayofanywa kupitia mfuko wa jamii wa Airtel na ndio maana tupo mstari wa mbele katika kusaidia nyanda tofauti hapa nchini.

Simu hizo zilikabidhiwa mbele ya mwenyekiti wa Taasisi ya haki za binadamu na maendeleo ya kiuchumi bw. Abubakar Rakesh.

Mwenyekiti huyo alisema,” tunayofuraha kuona baadhi ya wenzetu wakiwezeshwa ili kuweza kukidhi mahitaji yao na kuongeza kipato chao.

Tutaendelea kuwashukuru Airtel kwa misaada yao endelevu na kwa kukiwezesha kikundi hiki kuweza kujiendeleza. Wito wangu kwa wanachama wenzangu ni kutumia nafasi hii vizuri, kuweka jitihada katika kazi zao ili kufanya vyema na kufanikiwa katika biashara zao.”

WAWAKILISHI KUTOKA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM WAONANA NA MKUU WA MKOA WA RUKWA KUJADILI UANZISHWAJI WA CHUO HICHO MKOANI RUKWA

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na wawakilishi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mapema leo tarehe 23 Februari 2015 ofisini kwake kujadili mchakato wa uanzishaji wa Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Mkoani Rukwa. Chuo Kikuu hicho kitaleta maombi maalum kwa uongozi wa Mkoa wa Rukwa kuomba kupatiwa kambi ya Kianda iliyokuwa ikitumiwa na Kampuni ya Aasleaf Bam International iliyokuwa ikijenga barabara ya Laela - Sumbawanga kwa kiwango cha lami. Kwa upande wa Uongozi wa Mkoa wa Rukwa unaona kuna haja kubwa ya kuanzishwa kwa Chuo Kikuu Mkoani humo kuweka chachu ya elimu na kusogeza huduma hiyo muhim zaidi kwa wananchi. Kushoto kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ni Katibu Tawala Mkoa huo Ndugu Smythies Pangisa. 
Dkt. Joseph Kihedu ambaye ni muhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema amefurahishwa na muamko wa Serikali ya Mkoa wa Rukwa katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya elimu pamoja na kiu yao kubwa ya kuona Mkoa unakua na Chuo Kikuu. Alisema kuwa endapo Chuo Kikuu hicho kitapewa maeneo hayo bila shaka hakitasita kuanzisha Tawi  la Chuo hicho Mkoani Rukwa mbapo itakua ni fursa kubwa kwa chuo hicho kujitanua zaidi katika kutoa elimu yenye ubora nchini. Kutoka kushoto ni wawakilishi wengine kutoka chuo hicho ambao ni Ndugu Michael John na Bi. Brenda Kazimili. 

Majadiliano yakiwa yanaendelea. Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya alisema Serikali ya Mkoa haitosita kutoa ushirikiano wa taasisi yeyote ya elimu ya juu ikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yenye lengo la kuwekeza katika elimu Mkoani Rukwa. Amekitaka Chuo Kikuu hicho cha Dar es Salaam kuendelea na nia yake ya kuomba maeneo hayo na kusema kuwa Serikali ya Mkoa itatoa majibu sahihi kwa kile kitakachowezekana.(Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa@Rukwareview.blogspot.com)

Kinana: Tamasha la Pasaka litumike kuiombea amani Tanzania

0
0
mfuko2
KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana ametoa wito kwa waandaaji wa Tamasha la Pasaka, Kampuni ya Msama Promotions kuongeza ufanisi kwa kuongeza chachu kwa waimbaji kuiombea amani Tanzania hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.
 
Kwa mujibu wa Kinana sambamba na hilo kwa pamoja tuiombee nchi yetu umoja, amani, mshikamano ambako tamasha hilo litumike kumuomba Mungu kufanikisha umoja kwa Watanzania ulioasisiwa  na baba wa Taifa Mwalim Julius Kambarage Nyerere.Kinana alitumia fursa hiyo kuwatakia heri na fanaka Wakristo wote duniani heri na fanaka katika sherehe hizo ambazo ni kumbukumbu kubwa kwao ambayo haifanani na nyingine za kijamii.
 
Aidha Kinana alimpongeza Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama kwa kuwaunganisha Watanzania wa madhehebu mbalimbali na kuwa kitu kimoja na kudumisha mshikamano katika jamii. 
 
Kinana alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa mashabiki na wapenzi wa tamasha hilo kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha mipangilio ya Msama katika kuisaidia jamii ya Watanzania.
 
Kinana ni mmoja wa Makatibu wa CCM wanaotekeleza majukumu yake ipasavyo kwa kuweza  kurudisha heshima ya chama kilichopoteza mwelekeo, hivi sasa CCM imerudisha heshima kama ilivyokuwa kwenye uongozi wa baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MKURANGA WAPEWA MSAADA WA VIFAA VYA KUPIMIA MACHO

0
0
Afisa Mkazi wa taasisi isiyo ya Kiserikali ya  Brien Holden Vision Institute Eden Mahayo (Pwani.kushoto)akimkabidhi msaada wa sanduku la vifaa vya kupimia macho Kaimu Mkurugenzi wa  manispaa ya Mkuranga  Mbenjamin Majoya  kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi 122 za  Mkuranga  ambapo wanafunzi hao watapata huduma ya kupima na kutibiwa macho bure.hafa hiyo ilifanyika hivi wilayani 002mkuranga mkoa wa Pwani.
Matroni wa haospitali ya wiraya ya Mkuranga Mkuranga Rosemary Magombola  akisoma moja ya maneno kwenye kibao maarumucha kupimia macho mara baada ya kukabidhiwa msaada huona taasisi isiyo ya kiserikali ya  Brien Holden Vision Institute Eden  kwa ajili ya wanafunzi wa shuleza msingi 122  .Kulia ni  Mratibu wa taifa  wa huduma za macho Dkt.Nkundwa Mwakyusa (kushoto) Mratibu wa mradi huo kwa watoto wa shule za msingi toka taasisis ya ya  Brien Holden Vision Institute Eden ,Rebecca Kasika.
Afisa maendeleo ya jamii ya mji wa kibaha mkoa wa pwani akikabidhiwa na Mashine ya kupimia macho na   Afisa Mkazi wa taasisi isiyo ya Kiserikali ya  Brien Holden Vision Institute Eden Mahayo (kushoto)   wakati wa hafla ya kukabidhi wa msaada wa  vifaa vya macho vyenye thamani ya shilingi milioni 11.4  kwa ajili ya kuwahudumia wanafunzi  wa Wilaya hiyo ya Kibaha ambao watanufaika na  huduma hiyo ya  upimaji  macho pamoja na  matibabu bure
Wafanyakazi wa hospitali ya Kibaha kitengo cha macho wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa ya  Brien Holden Vision Institute Eden,mara baada ya kukabidhiwa msaada wa vifaa vya macho vyenye thamani ya shilingi milioni 11.4.
*********** 
NA MWANDISHI WETU
TAASISI isiyo ya Kiserikali ya Brien Holden Vision  imetoa msaada wa vifaa vya kupimia macho wa zaidi ya sh milioni 11.4 kwa Wilaya za Mkuranga  na Kibaha ziliyopo mkoani Pwani mwishoni mwa wiki.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa msada huo ,Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya hiyo  Benjamin Majoya alisema  msaada huo utasaidia  katika kupandisha  kiwango cha taaluma kwa wanafunzi  katika Wilaya  hiyo kutokana  na idadi ya watoro  darasani kupungua  kuanzia mwaka huu.
  
Alisema kupungua kwa idadi ya wanafunzi watoro kutakwenda sambamba na kuongezeka kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi watakaojiunga na elimu yasekondari mwaka ujao.

Majoya alisema  msaada uliotolewa na Taasisi hiyo umekuja kwa wakati mwafaka  kwa wakati amabo ulikuwa ukihitajika hivyo  mbali ya kuwasaidia wanafunzi wa shule za msingi  lakini pia utawasaidia wananchi wote wa Wilaya hiyo.
  
Alibainisha kuwa  msaada huo unaojumuisha mashine zote za kupimia macho pamoja kutengenezea miwani  za aina mbalimbali  utasaidia kuondoa tatizo la uoni hafifu ambalo hapo awali wazazi walikuwa na imani potofu kwamba huenda watoto wao  wamerogwa .
  
Akielezea ukubwa wa tatizo hilo ,alisema kuwa uoni hafifu umekuwa sababu ya mwanafunzi kutokufanya vizuri kitaaluma kutokana na kuugua mara kwa mara hivyo kusababisha utoro.
  
“Tunaishukuru sana Taasisi ya BrienHolden Vision kwa msaada  waliotupatia na tunaahidi  kuutumia kwaajili ya wananchi ,na ifahamikie kwamba hii itabaki kuwa mali ya hospitali ya Wilaya ya Mkuranga  ’”alihitimisha Majoya.

 Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Eden  Mashayo alisema  lengo la Taasisi yake ni  kuwajengea uwezo wa kuona wanafunzi pamoja na walimu lakini pia kutoa mafunzo kwaajili ya walimu  ili waweze kuwapima wanafunzi  wapate huduma stahiki ili kuondokana na tatizo hilo..
  
Mashayo aliahidi ushirikiano baina ya  Taasisi yake ,Wizara ya Afya,Wilaya ya mkuranga  na kwa kuleta mtaalamu wa masuala ya macho kila mwezi mara mbili ambaye atakuwa akiwahudumia wakazi wa eneo hilo ili kuondokana na tatizo la uoni hafifu  ambalo litapungua kwa asilimia 10 .

Kwa  upande wake Mkuu wa Mratibu wa  huduma za macho Taifa kutoka Wizara ya Afya Dk Nkundwe Mwakyusa alisema kuwa  mradi huo unaosaidia shule za Msingi  bagamoyo na Kibaha umeshahudumia  shule 121 katika awamu ya kwanza na awamu ya pili utahudumia shule 116 .

Akizungumzia  changamoto zinazowakabili alisema kuwa  huduma hizo hazipewi kipaumbele  kwasababu serikali inajua tu kunawafadhili .

Hata hivyo alibainisha kuwa  ili kutatuua changamoto hizo  na kuifanya jamii iwe na uelewa sahihi juu ya magonjwa  ya macho mikakati iliyopo huenda mambo yakabadilika  na mwaka huu jamii itaanza kupata taarifa sahihi kuhusu magonjwa ya macho.

Naye  daktari Mtalamu wa macho  Gilbert Massawe wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga na Afisa Maendeleo ya jamii mji wa kibaha Leah Rwanji waliishukuru Wizara ya Afya sambamba na Taasisi ya
Brien Holden Vision   kwa msaada wao na kubainisha kuwa utasaidia kupunguza idadi ya utoro kwa wanafunzi kwa asilimia 10.

RAIS KIKWETE AMKABIDHI H.H. THE AGA KHAN HATI YA CHUO KIKUU CHA AGA KHAN KILICHOPO DAR ES SALAAM

0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Kiongozi wa madhehebu ya Ismailia duniani Mtukufu Aga Khana baada ya kumkabidhi hati ya Chuo Kikuu cha Aga Khan kilichopo Dar es salaam leo February 23, 2015 Ikulu jijini Dar es salaam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza  Kiongozi wa madhehebu ya Ismailia duniani Mtukufu Aga Khana akiongea baada ya kumkabidhi hati ya Chuo Kikuu cha Aga Khan kilichopo Dar es salaam leo February 23, 2015 Ikulu jijini Dar es salaam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Kiongozi wa madhehebu ya Ismailia duniani Mtukufu Aga Khana hati ya Chuo Kikuu cha Aga Khan kilichopo Dar es salaam leo February 23, 2015 Ikulu jijini Dar es salaam

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongeqa kwa furaha na Kiongozi wa madhehebu ya Ismailia duniani Mtukufu Aga Khana akiongea baada ya kumkabidhi hati ya Chuo Kikuu cha Aga Khan kilichopo Dar es salaam leo February 23, 2015 Ikulu jijini Dar es salaam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki na Kiongozi wa madhehebu ya Ismailia duniani Mtukufu Aga Khana tayari kwa  kumkabidhi hati ya Chuo Kikuu cha Aga Khan kilichopo Dar es salaam leo February 23, 2015 Ikulu jijini Dar es salaam. PICHA NA IKULU

Nyambui alilia riadha ifufuke upya

0
0
 MKURUGENZI wa Masoko wa Isere Sports, Abbas Ally Isere akionesha jezi zitakazotumiwa na wanariadha ikiwa ni makubaliano ya Kampuni yake kuagiza vifaa vya riadha na kuviuza kwa bei ya chini 
========  =========  ============
Na Mwandishi Wetu,Morogoro
MAOFISA michezo na Maofisa Elimu wa mikoa ya Tanzania wameombwa kushirikiana na wenyeviti wa mchezo wa riadha kufufua mchezo huo kutoka ngazi ya shule za msingi na Sekondari.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui akizungumza katika mkutano Mkuu wa Mwaka wa tathmini wa mashindano ya Shule za Msingi (UMITASHUMTA) na Shule za Sekondari (UMISETA) yanayosimamiwa na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)alisema imefika wakati kila mdau achangie kufufua mchezo huo.

Alisema mchezo huo ambao zamani ulitangaza Tanzania katika mashindano mbalimbali duniani unazidi kupoteza umaarufu kwa sababu hakuna mikakati madhubuti ya kufuatilia wanamichezo wenye vipaji kutoka ngazi ya shule za msingi hadi vyuo vikuu.

Nyambui alisema kwa mara ya mwisho mwaka jana Tanzania ilishiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika Scotland ikiwa ni baada ya miaka 40 kutoka na mchezaji Basil John mita 1500 kushika nafasi ya nane kati ya 12 walioingia fainali.

Alisema mchezo wa riadha hauna wafadhili kama ilivyo michezo ya soka lakini amejitahidi kushawishi kampuni ya Isere Sports isaidie kuwauzia wachezaji wa riadha vifaa kwa bei ya chini.

"Tumekubaliana na Kampuni ya Isere Sports iagize na kuwauzia wetu vifaa vya michezo kwa bei ya kawaida ili wamudu kununua viatu na jezi za " alisema Nyambui.
Meneja Masoko wa Isere Sports, Abbas Ally Isere alisema ni kweli wamefikia makubaliano hayo na yeye kama mtanzania anayehitaji vipaji vionekane atajitahidi kuhakikisha vifaa vya riadha anaviagiza na kuviuza kwa bei ya chini.
Mikoa inayotamba kutoa wanariadha wengi ni Manyara, Arusha, Mara, Mtwara, Dodoma, Mbeya, Kanda ya Ziwa na mikoa nyingine.

WANAHABARI WAWAFARIJI YATIMA ,JIJINI ARUSHA

0
0
 Waandishi wa Habari wa Arusha wakitoa Zawadi zao za "Valentine's day" kwa watoto wa kituo cha Huruma Children's Trust Kwa Morombo, Jijini Arusha, kama ishara ya Upendo na Kuwajali watoto yatima katika siku hii muhimu ya Wapendanao. Kushoto aliyesimama ni Mratibu wa Shughuli hiyo Bi. Jane Edward Kutoka TV1 -Arusha. Zawadi hizo zilitolewa Tarehe 14.02.2015 Jumamosi.
 Wakurugenzi wa Wazalendo 25 Blog Bw. Gadiola Emanuel na Jamii Blog Bi. Pamela Mollel tukitoa zawadi kwa mmoja wa watoto wa Huruma Children's Trust Centre Kwa Morombo, Jijini Arusha. kama ishara ya Upendo katika Sherehe ya siku ya wapendanao
 Mkurugenzi wa Jamii Blog Bi. Pamela Mollel Akitoa Zawadi kwa Mmoja wa Mtoto katika kituo cha watoto yatima cha Huruma Children's Trust Centre Kwa Morombo, Jijini Arusha katika siku ya Wapendanao.
 Mwandishi wa Habari wa Tanzania Daima Bw. Ferdinand Shayo na Mwandishi Huru na Mmiliki wa Blog ya Wazalendo 25 Blog Bw. Gadiola Emanuel Wakishusha mzigo ambao ni moja ya zawadi ya Upendo kwa Watoto yatima wa Kituo cha Huruma Children's Trust Centre, Kwa Morombo, Jijini Arusha. Tarehe 14/ 2/2015 Jumamosi.


Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Wanahabari kutoka vyombo mbali mbali vya habari nchini wametembelea kituo cha watoto yatima cha Huruma Children  Center kilichopo Mtaa wa Morombo  na kuwafariji pamoja na kuwapeleka zawadi
Katika Ziara hiyo iliyoandaliwa na Kampuni ya jamii media ambao ni wamiliki wa  jamiiblog.co.tz  ililenga kuwakutanisha Wanahabari na makundi maalumu katika jamii ikiwa ni njia ya kujitoa kwa jamii na kuwa faraja kwa waliokosa faraja.

Mkurugenzi wa Jamii media ,Pamela Mollel amesema kuwa mbali na kuripoti matukio mbali mbali yanayojiri nchini Wanahabari wana jukumu la kuisaidia jamii kwasababu wao ni sehemu ya jamii .
Pamela Mollel ameeleza kuwa suala la kujitoa kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu ni jukumu la kila Mtanzania ili kuwasaidia kuwa na maisha bora na kuisaidia jamii pia.

Mwandishi wa Kituo cha TV 1 Mkoani hapa Jane Edward ameeleza kuguswa na watoto hao wenye vipaji lukuki ambavyo vikiendelezwa wanaweza kuwa tunu ya taifa na kuliletea taifa ushindi katika sanaa na michezo.
“Watoto hawa licha ya kuwa yatima wana uwezo mkubwa ambao ukitumiwa vizuri unaweza kulisaidia taifa letu wengine ni wabunifu mashirika binafsi ,serikali na mtu mmoja mmoja kuwaunga mkono watoto hao” Alisema Jane Edward 

Mmiliki wa blogu ya Wazalendo 25 Blog Bw. Gadiola Emmanuel anasema kuwa ni wakati sasa kwa wanahabari kuwa mfano wa kuigwa katika kuisaidia jamii na kuongoza mabadiliko wanayoyataka kuyaona badala ya kuwa wasemaji peke yake hususani katika masuala ya kijamii ushiriki wao utaleta mabadiliko chanya na ushawishi mkubwa.
 Siku ya Wapendanao Pamoja na Watoto Yatima ...........katika kituo cha Huruma Children's Trust Centre Kwa Morombo, Jijini Arusha.
 Hapa ni Bwenini la watoto wa kiume wa kituo cha watoto yatima cha Huruma Children's Trust Centre Kwa Moromboo, Jijini Arusha.
 Pamela Mollel Akimlisha mtoto yatima katika kituo cha Huruma Children's Trust Centre Kwa Moromboo, Jijini Arusha.
 Sema Hellooooooo........
 Bi. Jane Edward wa TV1 -Arusha akimlisha mmoja wa Watoto yatima katika kituo cha Huruma Children's Trust Centre Kwa Moromboo, Jijini Arusha.
 Mdau wa Habari na IT wa Palace HoteL Arusha Bw. Ricki Justin akitoa zawadi kwa mmoja wa watoto yatima wa kituo cha Huruma Children's Trust Centre Kwa Moromboo, Jijini Arusha
 Ricki na Gadiola Emanuel wakikabidhi mzigo kwa mmoja wa watoto yatima wa kituo cha Huruma Children's Trust Centre Kwa Morombo, Jijini Arusha.
 Mratibu wa Shughuli hii na Mwandishi wa Kituo cha Runinga cha TV1 Bi. Jane Edward akitoa moja ya zawadi kwa Matron wa kituo cha watoto yatima cha Huruma Children's Trust Centre Kwa Morombo, Jijini Arusha.
 Kushoto ni Pamela Mollel wa Jamii Blog na Kulia ni Jane Edward wa TV1- Arusha wakimkabidhi Matron wa watoto yatima wa kituo cha Huruma Children's Trust Centre Kwa Morombo, Jijini Arusha.
 The CEO wa Wazalendo 25 Blog Bw. Gadiola Emanuel na Mratibu Bi. Jane Edward wa TV1 -Arusha wakipata historia fupi ya kituo cha Huruma Children's Trust Centre Kwa Moromboo, Jijini Arusha.
Muonekano wa kituo cha Huruma Children's Trust Centre Kwa Moromboo, Jijini Arusha. Picha Zote na Ferdinad Shayo , Gadiola Emanuel na Pamella Mollel.

SERIKALI NA WADAU MBALIMBALI KUENDELEA KUTOA ELIMU KWA MAKUNDI YALIYO KATIKA HATARI YA KUPATA MAAMBUKIZI YA VVU.

0
0
fat1 Mkurugenzi wa Udhibiti na Uhakiki wa Wizara ya Afya  Dkt.Mohamed Ally Mohamed akionyesha moja ya chapisho lenye taarifa za tafiti za watu walio katika makundi maalum  na hali ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi  katika mikoa 7 lililotambulishwa leo jijini Dar es salaam.fat2Mkurugenzi wa Udhibiti na Uhakiki wa Wizara ya Afya  Dkt.Mohamed Ally Mohamed (katikati) akimkabidhi Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho (kushoto) chapisho lenye taarifa za utafiti  kwa watu walio katika makundi maalum  na hali ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi  katika mikoa 7  leo jijini Dar es salaam.fat4Mkurugenzi wa Udhibiti na Uhakiki wa Wizara ya Afya  Dkt.Mohamed Ally Mohamed (katikati) akimkabidhi Meneja  Mpango wa Tume ya Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP) Dkt. Robert Josiah (kushoto) chapisho lenye taarifa za utafiti  kwa watu walio katika makundi maalum  na hali ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi  katika mikoa 7  leo jijini Dar es salaam.fat5Mkurugenzi wa Udhibiti na Uhakiki wa Wizara ya Afya  Dkt.Mohamed Ally Mohamed (katikati) akiwa ameshika chapisho lenye taarifa za utafiti  kwa watu walio katika makundi maalum  na hali ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi  katika mikoa 7  akiwa na baadhi ya watendaji wanaoongoza taasisi za kupambana na Ukimwi nchini . fat6 
Picha ya pamoja ya washiriki hao baada ya uzinduzi wa chapisho.
………………………………………………………

Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
Dar es salaam.
SERIKALI imesema kuwa itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya Afya kutoa elimu kwa makundi ya watu wanaotumia dawa za kulevya na wale wanaojihusisha na biashara ya ngono katika maeneo mbalimbali nchini  ili kukabiliana na maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi .
 
Akizungumza kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Serikali leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Udhibiti na Usalama wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt.Mohamed Ally Mohamed wakati wa kutambulisha matokeo ya tafiti za watu walio katika makundi maalum yaliyo katika hatari ya kuambukizwa  Virusi vya Ukimwi  katika mikoa 7 iliyofanyiwa utafiti ambayo ni Dar es salaam, Mwanza, Mbeya, Iringa, Mara, Tabora na Shinyanga.
 
Akitambulisha matokeo hayo Dkt. Mohamed amesema kuwa hali ya maambukizi  mapya miongoni  mwa wanaume na wanawake katika maeneo yaliyofanyiwa utafiti imekuwa ikipungua kwa kasi ndogo licha ya juhudi kubwa  zinazofanywa na Serikali kwa na wadau mbalimbali kukabiliana na maambukizi hayo kutokana na makundi hayo kutobadili tabia. 
 
Amesema maeneo mbalimbali yaliyofanyiwa utafiti na wataalam wa Wizara ya Afya, taasisi za kitaifa na Kimataifa zinazojihusisha na Ukimwi yameonesha uwepo wa tabia hatarishi zinazochangia maabukizi mapya ya VVU yakihusisha  makundi watu walio katika makundi maalum ya wanawake wanaofanya biashara ya ngono, wanaume wanaofanya ngono ya jinsia moja pamoja na watu wanaojidunga dawa za kulevya.
 

Amefafanua kuwa katika mikoa 7 ambayo imefanyiwa utafiti huo hali ya maambukizi ya VVU kwa wanawake imeonekana kuwa kubwa pamoja na ongezeko la wanaume wanaofanya ngono na wanaume wenzao huku idadi ya wanaojidunga dawa za kulevya ikikadiriwa kuwa kati ya 7,000 hadi 10,000.
 
“Hali ya maambukizi katika mikoa ulikofanyika utafiti ni kubwa, wanawake wana maambukizi makubwa,  idadi ya wanaojidunga dawa za kulevya inakadiriwa kuwa kati ya 7,000 hadi 10,000 huku kiwango chao cha maabukizi ya VVU kwa asilimia kikiwa asilimia 15.5 kiwango hiki ni kikubwa” Amesema Dkt. Mohamed.
 
  Kwa upande wake Meneja  Mpango wa Tume ya Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP) Dkt. Robert Josiah akizungumzia kuhusu tafiti hizo amesema kuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za taifa na kimataifa ilifanya tafiti tatu za makundi yaliyo katika hatari ya kuambukizwa VVU ili kubaini makisio ya idadi ya watu walio katika makundi hayo.
 
Dkt.Robert ameeleza  kuwa tafiti hizo zilifanyika katika vipindi tofauti kuanzia mwaka 2013 hadi 2014 kwenye mikoa yenye viwango vya juu vya maabukizi ya VVU na kueleza kuwa mkoa wa Iringi unaongoza kwa kuwa na asilimia 9.1, ukifuatiwa na Mbeya 9.0%, Shinyanga 7.4%, Dar es salaam 6.9%, Tabora 5.1%, Mara 4.5% na Mwanza 4.2.
 
Amesema kwa kutumia matokeo hayo Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeweza kubaini changamoto mbalimbali na hali ya maambukizi ya VVU miongoni mwa makundi ya watu walio katika makundi hatarishi kwa lengo la kubaini mbinu mbalimbali za kutoa huduma za kinga, tiba na matunzo kwa watu walio katika makundi hayo.
 
“Kwa upande wetu tutatumia takwimu hizi kuboresha huduma ztu na kupanga mipango mbalimbali ya kupunguza maambukizi ya Ukimwi nchini, lengo la NACP ni kuhakikisha kuwa Tanzania inaondokana na maambukizi ya VVU” Amesema.
 
Naye Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho akizungumzia matokeo ya tafiti hizo amesema kuwa ipo haja ya tafiti zinazofanyika nchini kuendelea kutazama jinsia zote ili kupata uhalisia katika jamii kwa makundi maalum.
Ametoa wito kwa Serikali na wadau mbalimbali kuzitumia takwimu zilizopatikana ili kufanya mabadiliko ya mbinu na njia za kukabiliana na maambukizi mapya ya VVU nchini Tanzania.
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live




Latest Images