Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 467 | 468 | (Page 469) | 470 | 471 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Taarifa iliyotufikia mapema leo,inaeleza kuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la ‘Chamber Squad’, Moses Bushagama ‘Mez B’, amefariki dunia leo asubuhi huko Mkoani Dodoma baada ya kusumbuliwa na Homa ya mapafu kwa muda mrefu. Taarifa ya kifo cha Mez B zimethibitishwa na mama yake mzazi, na kwamba alikuwa amelazwa kwenye Hospitali ya Mwananchi.

  Mez B amewahi kulazwa na kuruhusiwa mara kadhaa katika hospitali ya Dodoma na hivi karibuni alizidiwa na kulazwa mkoani humo mpaka umauti ulivyompata.

  Baadhi ya nyimbo alizowahi kuimba Mez B ni pamoja na ‘Fikiria’, ‘Kama Vipi’, ‘Kikuku’, ‘Shemeji’ ‘Nimekubali’ pamoja na ‘Ghetto langu’ aliyoshirikishwa na Marehemu Albert Mangwea.

  Huyu ni msanii wa pili kufariki kutoka kundi la chamber squad. Miaka miwili iliyopita kundi hilo liliomboleza kifo cha mwenzao Albert Mangwea ‘Ngwea’ huku Mez B akiwa mstari wa mbele wakati wa mazishi yake.

  Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

  0 0

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewataka Watanzania wasikilize na kufuata
  mafundisho yanayotolewa na viongozi wa dini ili Tanzania iwe nchi
  yenye watu waadilifu na wenye hofu ya Mungu.

  Ametoa wito huo leo mchana (Ijumaa, Februari 20, 2015) wakati
  akizungumza na maelfu ya waumini na wananchi waliohudhuria ibada ya
  mazishi ya Askofu Mstaafu Magnus Mwalunyungu kwenye kanisa la Moyo
  Mtakatifu wa Yesu la Tosamaganga, Jimbo Katoliki la Iringa.

  “Leo ni siku ya pekee ya kuwasikiliza viongozi wa dini wakituasa
  tujiandae kwa maisha baada ya kifo. Tukio hili la leo litupe nguvu ya
  kukubali kwamba kifo kipo licha ya kuwa hakizoeleki na kinapotokea
  kinaleta simanzi kubwa,” alisema.

  “Ninawasihi Watanzania wote tufuate mafundisho yanayotolewa na
  viongozi wa dini zetu ili Tanzania iwe na kundi la watu wenye hofu ya
  Mungu, waadilifu na wanyofu kama ambavyo mahubiri ya leo
  yamesisisitiza,” alisema.

  Waziri Mkuu ambaye yuko kwenye ziara ya siku tano ya kikazi mkoani
  Iringa, aliamua kusitisha ziara yake siku ya leo ili aweze kushiriki
  msiba huo. Pia alitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Rais Jakaya
  Kikwete ambaye yuko Kenya kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  Akitoa mahubiri kwenye ibada hiyo, Askofu Damian Dallu wa Jimbo Kuu
  Katoliki la Songea alisema wanadamu wanahangaika na kuogopa kifo kwa
  sababu hawajui baada ya kifo maisha yao yatakuwaje.

  “Askofu Mwalunyungu ameishi kwa miaka 85 na kati ya hiyo, miaka 55
  alikuwa akitumikia kama padre na kwa miaka 22 alimtumikia Mungu aakiwa Askofu. Na hata baada ya kustaafu aliomba awe Parokopale Kidamalai ambako alitumikia kwa miaka minne. Maisha yake yanaendana na neno kutoka kitabu cha hekima kwamba kifo cha mwadilifu ni kupumzika kwa starehe,” alisema.

  Ibada hiyo ya mazishi ilihudhuriwa na Maaskofu wa kanisa katoliki zaidi ya 20.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  IJUMAA, FEBRUARI 20, 2015.

  0 0

  Rais Jakaya Kikwete(kushoto)akipokea bendera ya Afrika Mashariki(EAC)kutoka kwa Rais wa Kenya,Uhuru Kenyatta ikiwa ni ishara ya kumkabidhi Uenyekiti wa  EAC  kwenye  mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika leo.20/2/2015. PICHA NA IKULU.
   Rais Jakaya Kikwete,Naibu Rais wa Kenya,William Rutto na maafisa wengine wakiwa kwenye Jengo la mikutano wa kimataifa la Kenyatta International Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya wakati wa kuimba wimbo wa taifa la Tanzania katika mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika leo.20/2/2015
   Kutoka kushoto ni mgeni mwalikwa,Rais wa Sudani Kusini,Salva Kiir,Rais wa Burundi,Pierre Nkurunziza,Rais Jakaya Kikwete(Tanzania),Rais Uhuru Kenyatta(Kenya)Rais Yoweri Museveni(Uganda)Rais Paul  Kagame(Rwanda)na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC)Dk Richard Sezibera wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano kwenye  mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika leo.20/2/2015


  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia akitoa hutuba yake wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ua wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa LAPF Dar es Salaam jana.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Profesa, Hasa Mlawa, akizungumza katika hafla hiyo.
   Waziri wa Kazi na Ajira Gaudentia Kabaka akichangia jambo kwenye uzinduzi huo.
   Mkurugenzi Mkuu wa LAPF, Eliud Sanga akizungumza machache kwenye uzinduzi huo.
   Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Profesa, Hasa Mlawa (kulia), akimkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia picha yenye nembo ya mfuko huo kwenye  hafla ya uzinduzi wa bodi mpya ya wadhamini ya mfuko wa LAPF na kuiaga bodi iliyomaliza muda wake iliyofanyika makao makuu ya mfuko huo Dar es Salaam jana. 
   Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Profesa, Hasa Mlawa (kulia), akimkabidhi Waziri wa Kazi na Ajira Gaudentia Kabaka picha yenye nembo ya mfuko huo kwenye  hafla ya uzinduzi wa bodi mpya ya wadhamini ya mfuko wa LAPF na kuiaga bodi iliyomaliza muda wake iliyofanyika makao makuu ya mfuko huo Dar es Salaam jana. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia.
   Wajumbe wa bodi ya LAPF iliyomaliza muda wake.
   Wajumbe wapya wa bodi ya LAPF 
   Mgeni rasmi wa uzinduzi huo Waziri Hawa Ghasia (katikati mbele waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya zamani ya LAPF iliyomaliza muda wake. Kushoto kwa waziri Ghasia ni Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka ambaye wizara yake inasimamia mifuko hiyo ya kijamii.
   Mgeni rasmi wa uzinduzi huo Waziri Hawa Ghasia (katikati mbele waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wapya wa  bodi ya LAPF.
   Wageni waalikwa wakiwa kwenye uzinduzi huo.
  Wadau wakiwa kwenye hafla hiyo
  Wanahabari wakichukua taarifa za uzinduzi huo.
  …………………………………..
  Na Dotto Mwaibale
   
  WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia ameitaka bodi mpya ya Mfuko wa LAPF kufanyakazi zao kwa maslahi ya mfuko huo badala ya kupendelea taasisi walizotoka.
  Hayo aliyasema wakati  wa hafla ya uzinduzi wa bodi mpya ya wadhamini ya mfuko wa Pensheni wa LAPF na kuiaga bodi iliyomaliza muda wake iliyofanyika makao makuu ya LAPF  Dar es Salaam jana.

  ” Bodi hii mpya imeundwa katika mfumo wa utatu.
  Kwanza kuna wajumbe ambao wanatoka serikalini, pili wanaotoka chama cha waajiri, na tatu wajumbe kutoka vyama vya wafanyakazi hivyo ninyi wajumbe.
   mna hadhi sawa katika utoaji michango itakayosaidia kuboresha shughuli za Mfuko” alisema Ghasia. 
   
  Ghasia alisema wajumbe hao wote shughuli yao na lengo lao ni moja, nalo ni kusimamia malengo na kazi za mfuko na kuhakikisha wanaasimamia maslahi ya mfuko na siyo eneo ambako kila mmoja wao anatoka. 
   
   “Kwa maneno mengine msifanye kazi kimajimbo”, kwani kufanya hivyo, kutaleta migongano isiyo na tija na kuzorotesha ustawi wa mfuko, ambao kwa sasa ndio mfuko wa hifadhi ya jamii unaokua kwa kasi zaidi nchini” alisema Ghasia.
   
  Alisema anaamini wajumbe hao wote wameteuliwa kwa nia moja moja ya kuhakisha mfuko huo unaongezeka hadi kufikia kilele cha mafanikio cha kuigwa hapa nchini na pengine nje ya nchi na hiyo ndiyo imani kubwa ambayo Rais Jakaya Kikwete anayo kwa LAPF.
   
  Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini wa mfuko huo Profesa, Hasa Mlawa alisema michango ya wanachama imekuwa ikiongezeka pia kwa kiwango cha kuridhisha ambapo mwaka 2011 mfuko ulikusanya Sh. 80.5 bilioni na kiasi hicho kimeongezeka hadi kufikia Sh. 157.6 bilioni mwezi Juni 2014 sawa na ongezeko la asilimia 95.9 kwa kipindi cha miaka mitatu. 
   
  Alisema mambo yaliyofanya kiwango cha michango kuwa juu ni pamoja na ongezeko la wanachama, mishahara, na uwasilishaji wa wakati unaofanywa na waajiri na kuwa kutokana na michango hiyo fedha zilizowekezwa katika vitegauchumi mbalimbali nazo ziliongezeka toka Sh. 387.6 bilioni mwezi Juni 2011 hadi Sh. 748.67 bilioni mwezi Juni 2014 sawa na ongezeko la asilimia 93.2. 
   
  Waziri wa Kazi na Ajira Gaudentia Kabaka ambaye mifuko hiyo ya jamii ipo chini ya wizara yake alisema Serikali itaendelea kulipa madeni yanayodaiwa na mifuko hiyo ili kuifanya iweze kuendelea.

  0 0

  unnamed
  Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Profesa Mark Mwandosya akimkaribisha Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki , Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya Rais kuwasili katika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere akitokea Nairobi Kenya ambapo alihudhuria mkutano wa kilele wa wakuu wa nchi Jumuiya ya Afrika Mashariki.Kushoto ni Waziri wa Elimu na Mafunzo Dkt.Shukuru Kawambwa.(picha na Freddy Maro)

  0 0

  SHIRIKA la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO), mkoani Iringa limetoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 229.9 kwa wajasiriamali wa mkoa huo, katika kipindi cha July mpaka Desembea mwaka jana.

  Akizungumza na uhuru, Kaimu meneja wa SIDO mkoani Iringa, Niko Mahinya alisema lengo la mkopo huo ni kuwawezesha wajasiriamali wadogo kupata mitaji, na kuinua uchumi wao ili waondokane na umaskini.
  Alisema mikopo hiyo ilitolewa kwenye vikundi mbalimbali vya wilaya zote za mkoa wa Iringa na wajasiriamali mmoja mmoja, ambao kupitia SIDO wamefanikiwa kiuchumi.
   “SIDO imekuwa ikitoa mikopo kwa wajasiriamali kwa masharti naafuu tofauti na taasisi nyingine za kifedha ili na riba ndogo ili kukuza mitaji yao, ”alisema.
  Alisema lengo la kutoa mikopo hiyo, ni kuwasaidia wajasiriamali na wananchi wasiokopesheka kwenye mabenki na taasisi nyingine za kifedha.
  Alisema mikopo hiyo ni rahisi zaidi kwa vikundi kwa madai kuwa wanachama wamekuwa wakidhaminiwa na vikundi vyao, ambavyo ikiwa mwanachama huyo atakimbia basi kikundi hicho kitabeba mzigo wa kumlipia.
  Alitaja changamoto kubwa inayowakabili hasa kwa wajasiriamali wa mijini kuwa ni kutorejesha mikopo yao, jambo ambalo linasababisha usumbufu kwa SIDO na kuwafanya wengine wasikopeshwe fedha hizo.
  Hata hivyo alisema kuwa mbali na mikopo hiyo, SIDO imekuwa ikitoa mafunzo ya biashara kwa wajasiriamali, ili iwe rahisi kwao kufanya biashara kwa utaalam na kuweza kukuza biashara zao.
  “Pamoja na mikopo tumekuwa tukitoa mafunzo kwa wajasiriamali wetu na kuwawezesha kushiriki kwenye maonyesho mbalimbali ndani na nje ya nchi, ili kutanua uelewa wa biashara zaidi,”alisema Mahinya.Hata hivyo aliwataka vijana kuwa mstari wa mbele katika kufanya kazi na SIDO ili waweze kuondokana na ugumu wa maisha ambao umekuwa ukiwakabili kwa kuamua kuwa wajasiriamali.
  Alisema ikiwa vijana watajikita kwenye ubunifu wa biashara, itakuwa rahisi kuaminiwa na SIDO na hatimaye kupatiwa mikopo midogo midogo inayoweza kuwafikisha kwenye hatua ya kukopesheka na taasisi nyingine.

   Na Fredy Mgunda,Iringa

  0 0  Majitaka yenye Sumu hatarishi  kutoka Kiwanda cha Nguo cha 21st Century yakitiririka kuingia Mto Ngerengere, Mkoni Morogoro  ambapo Wanachi hutumia maji ya  Mto huo kwa matumizi ya nyumbani. (Picha na OMR)

   Majitaka yenye Sumu hatarishi  kutoka Kiwanda cha Nguo cha 21st Century yakitiririka kuingia Mto Ngerengere, Mkoni Morogoro  ambapo Wanachi hutumia maji ya  Mto huo kwa matumizi ya nyumbani. (Picha na OMR)                 
  Na Victor Mariki – Ofisi ya Makamu wa Rais

   Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira, limetoa amri ya  kfungwa shughuli za  uzalishaji katika Kiwanda cha nguo  cha 21stCentury Limited kilichopo Kihonda Mkoani Morogoro leo  ikiwa ni sehemu ya Utekelezaji  wa Sheria ya Mazingira.

              Hatua hiyo imechukuliwa  kufuatiwa na kupuuzwa  kwa maelekezo na maagizo ya mazingira yaliyokuwa yakitolewa   nyakati tofautit tofauti  na Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa    Morogoro na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Morogo .

              Kiwanda hicho chenye wafanyakazi 1779 kiliagizwa na kuelekezwa tangu mwaka 2006 mamlaka hizo  kutumia mitambo ya kutibu majitaka yake kabla ya kuyatiririsha kwenye Mto Ngerengere ili  kuhepusha jamii inayotumia vyanzo vya maji hayo na madhara ya kiafya.

              Aidha Taarifa ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira ilifafanuwa kuwa mitambo ya kutibu sumu ya majitaka  kiwandani hapo  haina uwezo wa kutosha kutibu sumu zinazozalishwa na shughuli za uendeshaji wa kiwanda hicho.

              Taarifa hiyo iliongeza kuwa kufungwa kwa kiwanda hicho ni sehemu ya Utekelezaji wa Sheria ya Mazingira Na. 20 ya mwaka 2004 pamoja na Kanuni za Mazingira ya mwaka 2007 ambazo zinavitaka viwanda kutibu majitaka yake hadi kufikia viwango vilivyowekwa kabla ya kumwaga au kutiririsha maji hayo kwenye mazingira.           

  0 0
 • 02/21/15--03:01: TAARIFA KWA UMMA

 • UAMUZI WA BODI YA WAKURUGENZI KUHUSU MAOMBI YA TPDC YA  TOZO ZA HUDUMA ZA KUCHAKATA NA KUSAFIRISHA GESI ASILIA

  1.                  Tarehe 1 Septemba 2014, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ilipokea ombi Na. TR-G-14-039 kutoka kwa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuhusu kanuni ya kukokotoa tozo za huduma ya kuchakata na kusafirisha Gesi Asilia, na mapendekezo ya bei ya uchakataji na usafirishaji wa gesi asilia.

  2.                  Kati ya Septemba 2014 na Januari 2015, EWURA ilifanya uchambuzi wa kupitia gharama za ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi asilia, muundo wa mtaji (capital structure)  na  faida ya mtaji, gharama za uendeshaji wa mradi, pamoja na tozo iliyoombwa na TPDC.  
  3.                  Kwa mujibu wa ombi husika, TPDC waliiomba EWURA kuidhinisha vipengele vifuatavyo:
  (a)      kanuni ya kurekebisha tozo za kuchakata na kusafirisha gesi asilia itumike kwa miaka 20 hadi mwaka 2034;
  (b)     tozo kwa huduma ya kuchakata na kusafirisha gesi asilia iwe Dola za Marekani 4.178 kwa uniti (MMBtu) kwa muda wa miaka mitatu ya kwanza;
  (c)      faida kwenye mtaji ya asilimia kumi na nane (18%) na muundo wa mtaji wa asilimia hamsini mkopo na asilimia hamsini fedha za TPDC (50:50); na
  (d)     mwezi Septemba kila mwaka wa tatu utakuwa ni mwezi ambao marekebisho ya tozo kwa miaka mitatu inayofuata yatawasilishwa kwa EWURA.
  4.                  Kwa mujibu wa kifungu 19(2)(b) cha Sheria ya EWURA (Sura ya 414 ya Sheria za Tanzania), tarehe 27 Novemba 2014, EWURA ilianza mchakato wa taftishi kukusanya maoni na hoja za wadau kuhusu uhalali wa ombi lililowasilishwa na TPDC. Wadau waliowasilisha maoni na hoja mbalimbali ni Baraza la Watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji (CCC), Baraza la Ushauri la Serikali kuhusu Huduma za Nishati na Maji (GCC), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Kampuni ya Saruji Tanzania (TPCC), PanAfrican Energy Tanzania Limited, Songas Limited, Maurel & Prom, Wizara ya Fedha, Wizara ya Maji, na Wizara ya Nishati na Madini. Aidha, hoja za wadau na ufafanuzi uliotolewa na TPDC vimezingatiwa na EWURA katika kutoa uamuzi wa ombi hilo.

  5.                  Tarehe  8 Januari na 6 Februari 2015, EWURA ilifanya mikutano na wadau wa karibu (Exit Conference) ambapo EWURA ilisambaza rasimu ya Agizo la EWURA (Draft Order) ili ijadiliwe na kupata maoni ya mwisho; na mkutano huo ulihudhuriwa na  wawakilishi wa Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Maji, Wizara ya Fedha, CCC, GCC, TANESCO, TPDC, PAT, Songas, na TPCC. Asasi zote hizo zilitoa maoni ya mwisho kwenye rasimu ya Agizo la EWURA. Kwa ujumla, EWURA imezingatia maoni yaliyopatikana katika mikutano hiyo na hatimaye kufikia maamuzi kwenye Ombi la TPDC.

  6.                  Katika kikao chake cha tarehe 19 Februari 2015, Bodi ya Wakurugenzi ya EWURA, ilijadili Ombi la TPDC na kufikia maamuzi ya kipindi kifupi cha miezi mitatu (Interim Tariff) ambacho TPDC itakitumia kukamilisha ujenzi na kuwasilisha gharama halisi ambayo EWURA iliyahoji. Maamuzi yaliyotolewa ni kama ifuatavyo:

  0 0

  Rais wa Zanzibar, Dkt. Mohamed Ali Shein, akiweka udongo katika kaburi la marehemu Salmin Awadh Salmin, wakati wa shughuli za maziko yake zilizofanyika katika kijiji cha Makunduchi mjini Zanzibar jana Feb, 2015.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka udongo katika kaburi la marehemu Salmin Awadh Salmin, wakati wa shughuli za maziko yake zilizofanyika katika kijiji cha Makunduchi mjini Zanzibar jana Feb, 2015.
  Baadhi ya Viongozi wa juu wa Serikali, wakiwa ni miongoni mwa waliohudhuria maziko ya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Mjini Zanzibar, marehemu Salmin Awadh Salmin, huko Makunduchi mjini Zanzibar. Marehemu Salmin amezikwa leo Feb, 20, 2015 kijijini kwake Makunduchi Zanzibar.  0 0

   Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Bw. Fred EliyaSaphy (kushoto) akimkaribisha Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa wakati alipowasili na ujumbe wake kutoka wizarani kwa ajili ya shughuli za mafunzo kwa Vijana na ufuatiliaji wa miradi ya vikundi vya Vijana wilayani hum oleo mjini Kibondo.
   Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga(wa kwanza kulia) akielezea jambo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Bw. Fred EliyaSaphy (katika) walipotembelea ofisini kwake leo kwa ajili ya kujitabulisha kabla ya kuanza utekelezaji wa ziara yao wilayani humo. Kutoka kushotoni Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Kibondo Bw. Abel Nuba na wapili kutoka kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa
   Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Kibondo Bw. Moshi Hussen (wa kwanza kushoto) akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Afisa Vijana wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga(wa kwanza kulia) walipofika ofisini kwake leo kwa ajili ya kujitabulisha kabla ya kuanza utekelezaji wa ziara yao wilayani humo. Kutoka kushoto kwa Kaimu Katibu Tawala ni Afisa  Vijana wa Wilaya ya Kibondo Bi. Safi Mtula, Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa, Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurian Masele na Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Kibondo Bw. Abel Nuba .
   Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa akiwasilisha mada kuhusu stadi za masha kwa vijana wa Wilaya za Kibondo na Kakonko katika mafunzo yaliyofanyika leo mjini Kibondo.
   Afisa Vijana wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga akiwasilisha mada kuhusu mwongozo wa mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo Wilayani Kibondo katika warsha iliyoandalliwa na Wizara hiyo na kushirikisha jumla ya Vijana 83 kutoka katika Halmashauri za Kibondo na Kakonko.
  Baadhi ya Vijana kutoka Wilaya za Kibondo na Kakonko wakifuatilia mada zilizokuwa zina wasilishwa na wataalamu kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (hawapo pichani) wakati wa mafunzo kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Stadi za Maisha,Uongozi Bora na Sera ya Maendeleo ya Vijana leo wilayani Kibondo.

  Picha na Frank Shija, WHVUM

  0 0

  Tanzania inaunga mkono kwa dhati Ushirikiano wa Kikanda na muumini mkubwa wa Umoja wa Africa na Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). 
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo  jijini Nairobi mara baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa EAC na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ambaye amekua mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
   "Tunaamini kwamba Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyogawanyika, haitaweza kuchukua nafasi yake kamili na heshima katika familia ya Mataifa ya Afrika na dunia kwa ujumla" Rais amesema na kuongeza kuwa Tanzania inakua kuwa masoko yaliyogawanyika, miundombinu hafifu baina ya nchi, havina nafasi katika dunia ya leo wala ya baadaye. 

  Rais Kikwete amesema na kumpongeza Rais Kenyatta kwa kusimamia utekelezwaji wa maazimio na miradi ya pamoja ya Jumuiya wakati wa kipindi chake cha uenyekiti na kuahidi kuwa Tanzania haitawaangusha wana Afrika Mashariki katika kutekeleza azma yao ya pamoja ya kuendeleza Jumuiya ambayo inaundwa na nchi za Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda. 

  Rais Kikwete amesema katika utekelezaji wa ajenda ya EAC, biashara imeongezeka kwa kiasi kikubwa na kwamba nchi zote wanachama zinayaona matunda hayo. Katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2013 biashara katika nchi za EAC imeongezeka kutoka dola za kimarekani 3, 722.9 hadi dola 5,805.6 ambapo kati ya mwaka 2012 hadi 2013 kumekua na ongezeko la asilimia 6. 
  "Kama biashara isiyo rasmi ingerasimishwa, kwa hakika, ongezeko hili la biashara lingekua juu zaidi ya hapa, hivyo imefikia wakati muafaka kurasimisha biashara isiyo rasmi katika ushirikiano wetu" Rais amesema na kuongeza kuwa " kwa njia hii serikali zitakusanya kodi na hivyo kuna umuhimu wa kuelekeza nguvu katika kusaidia biashara ndogo ndogo na zile zisizo rasmi kwa kuziwekea mazingira mazuri". 
  Rais Kikwete amerejea nyumbani mara baada ya mkutano huo ambao umehudhuriwa na Marais wa nchi zote tano za Jumuiya na Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini ambaye amehudhuria kama mualikwa maalum katika kipindi hiki ambapo mazungumzo ya awali ya kuijadili nchi yake kama inaweza kupata uanachama katika EAC yanaendelea.
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wao Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya pamoja na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakizungumza chemba kabla ya kuingia kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa  Kenyatta International Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya  katika mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Ijumaa Februari 20, 2015
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wao Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya pamoja na Rais Paul Kagame wa Rwanda kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa  Kenyatta International Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya  katika mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Ijumaa Februari 20, 2015
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Naibu Rais wa Kenya, Mhe. William Rutto na maafisa wengine wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa  Kenyatta International Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya wakati wimbo wa Taifa wa Tanzania katika mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Ijumaa Februari 20, 2015
   Kutoka kushoto ni mgeni mwalikwa, Rais wa Sudani Kusini, Mhe Salva Kiir, Rais wa Burundi, Mhe Pierre Nkurunziza, Rais Jakaya Mrisho Kikwete(Tanzania),Rais Uhuru Kenyatta(Kenya)Rais Yoweri Museveni (Uganda) Rais Paul Kagame (Rwanda) na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Balozi Dk Richard Sezibera wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano kwenye  mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete(kushoto)akipokea bendera ya Afrika Mashariki(EAC)kutoka kwa Rais wa Kenya,Uhuru Kenyatta ikiwa ni ishara ya kumkabidhi rasmi Uenyekiti wa  EAC  kwenye  mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika leo Ijumaa Februari 20, 2015 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi. Picha na IKULU

  0 0

  Mgeni Rasmi Waziri wa Fedha wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Saada Mkuya katikati mwenye miwani akiwa katika Picha ya pamoja na viongozi wachuo na Wahitimu wa mahafali ya sita ya Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar). UT3 
  Baadhi ya Wahitimu wa Fani ya Upishi wakiwa wanamsikiliza Mgeni Rasmi Waziri wa Fedha wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Saada Mkuya hayupo pichani wakati wa sherehe ya Mahafali ya Sita ya Chuoni hapo. UT5 
  Baadhi ya Wahitimu wa Fani ya Ukarimu na Uongozi wa Hoteli wakivaa kofia kuashiria kukabidhiwa Stashahada zao katika Mahafali ya sita ya Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar UT6Mwanafunzi Bora Chuoni hapo wa Fani ya Mapokezi ya Wageni “Front Office”Said Shaame Khamis akipokea Zawadi kutoka kwa Mgeni Rasmi Waziri wa fedha wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Saada Mkuya katika Mahafali hayo Yaliyofanyika Maruhubi mjini Zanzibar
  UT7 
  Mgeni rasmi Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa chu hicho.

  ……………………………………………………………
  Na Faki Mjaka- Maelezo Zanzibar
  Waziri wa Fedha wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Saada Mkuya amewataka Wahitimu wa Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar kutoitegemea Serikali katika kupata ajira badala yake wajikite katika kujiajiri wenyewe.

  Amesema nafasi za Ajira Serikalini ni chache hivyo Wahitimu hao wanapaswa kujishughulisha ili wajiajiri wenyewe au kupitia Taasisi Binafsi. Waziri Mkuya ameyasema hayo alipokuwa akitoa hutuba yake kwa Wahitimu wa Mahafali ya Sita ya Chuo cha Maendeleo ya Utalii yaliyofanyika leo kati viwanja vya Chuo hicho Maruhubi Mjini Zanzibar.

  Amesema dhana ya kuitegemea Serikali katika ajira kwa sasa haina nafasi kutokana na uchache wa Ajira na kwamba anaamini Elimu waliyoipata Wahitimu inaweza kuwasaidia katika kujiajiri.

  Ametoa Rai kwa Wahitimu hao kujiunga na Kampuni za Ulinzi ambazo zinatarajiwa kuanzishwa Zanzibar kutokana na kuripotiwa kwa matukio mbalimbali ya kihalifu nchini. Aidha Waziri Mkuya amewashauri Wahitimu hao kutotosheka na kiwango cha Elimu walichofikia badala yake wajiendeleze mbele ili kupata ufanisi katika kazi zao.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Chuo hicho Bi Zulekha Khamis Omar amesema Chuo hicho kinazidi kupiga hatua kimaendeleo nakwamba Wanatarajia kuanzisha Masomo ya Shahada ya Kwanza mwaka 2017-18.

  Amesema mipango ipo mbioni kukamilika kuhusu kuanzishwa kwa Masomo ya Shahada ambapo Chuo hicho kitakuwa Chini ya Chuo Kikuu cha Zanzibar SUZA
  Hata hivyo Bi Zulekha alizitaja Changamoto zinazokabili Chuo hicho kuwa ni pamoja na Uhaba wa Vifaa katika Jiko, na Mmommonyoko wa Ardhi unaotishia Mazingira ya Chuo hicho.

  Chuo hicho kilichoanzishwa mwaka 1992 ili kuongeza ukuaji na Maendeleo ya Utalii Zanzibar kimefanya Mahafali yake ya sita ambapo Jumla ya Wahitimu 511 wa Ngazi za Stashahada na Cheti katika Fani mbalimbali wamehitimu.

  0 0

  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Karume huko Pemba na kupokewa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Ndugu Mwanajuma Majid Abdalla tarehe 20.2.2015. Mama Salma alialikwa Pemba kama Mgeni Rasmi kwenye sherehe ya Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) iliyoandaliwa na Al-Madrasat Jabal- Hiraa.PICHA NA JOHN  LUKUWI   mam2 
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na viongozi mbalimbali waliofika kumpokea wakati alipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Karume huko Pemba kwa ziara ya kikazi ya siku moja kisiwani humo tarehe 20.2.2015. mam3 
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa rasmi kwa kuvishwa shada na wasichana wa Almadrsat Jabal-Hiraa mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Shule ya Utaani huko Wete Pemba ilikofanyika sherehe ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) ambapo Mama Salma Kikwete alikuwa mgeni rasmi tarehe 20.2.2015. mam4 
   Mamia ya wananchi waliohudhuria sherehe ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) kwenye Shule ya Utaani huko Wete Pemba wakisikiliza hotuba ya Mgeni Rasmi Mama Salma Kikwete (hayupo pichani) aliyokuwa akitoa wa viongozi na wananchi waliohudhuria sherehe hizo tarehe 20.2.2015. mam5mam6 
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa nasaha zake kwenye Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) iliyofanyika kwenye Shule ya Utaani huko Wete katika Mkoa wa Kaskazini Pemba huku mamia ya watu wakimsikiliza. Mama Salma alikuwa Mgeni rasmi kwenye sherehe hiyo iliyofanyika tarehe 20.2.2015.
  mam7…………………………………………
  ……………….

  Na Anna Nkinda – Pemba
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amewataka wanawake wa  mkoa wa Kaskazini Pemba kuhakikisha watoto wao wanasoma kwa bidii hadi  elimu ya juu kwa kufanya hivyo wataweza kuzitumia fursa zilizopo na kushika nafasi mbalimbali za uongozi na hivyo kufika ngazi ya maamuzi.

  Mama Kikwete alitoa rai hiyo jana wakati wa sherehe za Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) zilizoandaliwa na  wanawake wa madrasa ya  Jabal – Hiraa na  kufanyika katika viwanja vya shule ya Sekondari Utaani Kaskazini Pemba.

  Mama Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alisema Mtume Muhammad S.A.W. alisimamia umuhimu wa elimu kwa kuona kuwa ili kuweza kuishi na kustawi katika dunia hakuna  budi kupata elimu zote ya ahera na ya duniani ambayo itawezesha kufungua milango ya fursa za duniani na za akhera. 

  “Sisi waislamu tumekuwa tukilalamika kuachwa nyuma kimaendeleo na wenzetu. Sababu kubwa ni kutotia mkazo kwenye elimu na hata pale tunapowasomesha watoto wetu skuli basi tunapuuzia ile ya watoto wa kike. Hili bahati mbaya liko kwetu sisi waislamu wa Afrika”. 

  Mimi nimebahatika kutembea duniani, nimeona wanawake wa kiislamu, tena kutoka nchi za kiislamu wakifanya mambo makubwa, wana vyeo na daraja kubwa kutokana na elimu na ustadi wao. Hawajaacha kuswali, hawajaacha kuolewa, wala kuacha kuwa wake wa kiislamu”, alisema Mama Kikwete. 

  Alitoa mfano wa nchi ya   Misri ambapo asilimia 49 ya wanafunzi wa vyuo vikuu ni wanawake na ni waislamu. Iran asilimia 60 ya wanafunzi wa vyuo vikuu ni wanawake. 

  Alisema wasiposomesha watoto wao haswa watoto wa kike wataendelea kujitumbukiza katika umasikini na hatimaye kuchuma dhambi kwa kuwaonea husda waliofanikiwa. Mtoto wa mama wa kiislamu aliyesoma,  naye ana nafasi kubwa ya  kuwa na mafanikio katika maisha. 

  Kwa upande wa malezi aliwasihi wanawake  hao kuwa chanzo cha mabadiliko kwani wao ndiyo walezi wa watoto na Taifa, wawalee watoto  katika unyenyekevu, kwa imani na kuhakikisha wanavaa mavazi ya heshima yanayokubalika katika jamii yao. 

  Mama Kikwete pia aliwahimiza wanawake hao kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu kwakuwa maisha ya binadamu yanasiasa ndani yake na siasa huleta maendeleo. Kwa wale watakaojitokeza wawaunge mkono na kuchagua amani, usalama na maendeleo. 

  Alihimiza, “Jitokezeni kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura zoezi la kujiandikisha litaanza wakati wowote. Safari hii vitatumika vitambulisho vipya vya kisasa. Wasiojiandikisha na kupata vitambulisho hivi hawataweza kupiga Kura ya Maoni ya Katiba inayopendekezwa wala kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu”.

  Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mwanajuma Majid Abdalla alimshukuru Mama Kikwete kwa kukubali kwake kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo na kumuomba Mwenyezi Mungu amzidishie kheri katika maisha yake. Aliwasisitiza kina mama waliohudhuria sherehe hizo kutenga muda wao kwa ajili ya kwenda madrasa kupata elimu ya ahera  na pia wajifunze elimu ya dunia ambazo zitawasaidia  katika maisha yao .

  “Katika suala la elimu wanawake tuko nyuma kwa madai kuwa tunashughuli nyingi za kifamilia na hivyo kukosa muda wa kujifunza, nawaomba tengeni muda wenu mkajifunze kwani kutokuwa na elimu ya dini na dunia  kutakufanya siku moja  ukashindwa kufanya mambo ya maana pale  utakapokutwa na tatizo ukiwa peke yako”, alisema Mwanajuma.
  Akisoma risala ya madrasa Jabal – Hiraa Khadija Suleiman Muhammed alisema ilianza na wanawake watatu na mwanaumme mmoja ambaye ni Mwenyekiti hadi sasa ina wanafunzi 104  kati ya hao wanawake 63 na wanaume 41.

  Khadija alisema  walimu wa madrasa hiyo wanafundisha kwa njia ya kujitolea  hujipatia kipato kwa kualikwa katika shughuli za Maulid na katika shughuli hizo hutumia mashine za kukodi lakini kama watakuwa na mashine zao zitawasaidia kutatua matatizo waliyo nayo.  Alizitaja mashine hizo kuwa ni boxi mbili za spika, pawa yenye warts 2000, wireless mic mbili na mixer thamani yake ikiwa ni shilingi milioni tatu na laki moja.

  “Tunawakumbusha viongozi wa dini tutumie nafasi tuliyopewa na Mwenyezi Mungu kuielimisha jamii kuacha kuuza au kutumia madawa ya kulevya na kujilinda na ugonjwa wa Ukimwi kwasababu ndiyo janga kubwa kwa taifa letu”, alisema Khadija. 

  Aliyataja mafanikio waliyoyapata kuwa ni wakati madrasa hiyo inaanza walikuwa wanatumia  jengo la mtu lakini hivi sasa wamefanikiwa kupata kiwanja na kujenga jengo la vyumba vinne ambalo halijakamilika lenye  madarasa ya kusomea mawili, chumba cha wageni kimoja, ofisi moja na vyoo viwili.

  Mama Kikwete aliipatia madrasa hiyo mifuko 25 ya saruji ambayo waliihitaji kwa ajili ya kumalizia ujenzi,  vitabu vya kusomeshea vya Mas-hafu na juzuu. Pia aliahidi kuziunga mkono madrasa nyingine sita zilizohudhuria sherehe hiyo.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akivishwa Skafu na Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania,  Abdulkarim Shah (kulia) na Kiongozi wa Skauti, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Feb 21, 2015 kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya Siku ya kuzaliwa Mwanzilishi wa Uskauti Duniani, Lord Rebert Stevenson Smyth Baden-Powell. Picha na OMRSHA2Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti cha Nishani ya Juu, Skauti Barnaba Abel, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya kuzaliwa Mwanzilishi wa Uskauti Duniani, Lord Rebert Stevenson Smyth Baden-Powell, zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Feb 21, 2015. Kulia ni Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania,  Abdulkarim Shah na (kulia kwa Makamu) ni Rais wa Skauti Tanzania, Dkt. Shukuru Kawambwa. Picha na OMRSHA3Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania, Abdulkarim Shah (kulia) na Rais wa Skauti Tanzania, Dkt. Shukuru Kawambwa (kulia kwa Makamu) wakisimama kupokea maandamano ya Vijana wa Skauti, yalipokuwa yakiingia kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya kuzaliwa Mwanzilishi wa Uskauti Duniani, Lord Rebert Stevenson Smyth Baden-Powell, leo Feb 21, 2015. Picha na OMRSHA4 
  Vijana wa Skauti wakipita mbele ya jukwaa kuu kwa maandamano wakati wa sherehe hizo za maadhimisho hayo. Picha na OMR SHA5 
  SHA6Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wananchi na Skauti wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya kuzaliwa Mwanzilishi wa Uskauti Duniani, Lord Rebert Stevenson Smyth Baden-Powell, zilizofanyika leo Feb 21, 2015 kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Picha na OMRSHA7 
  Vijana wa Skauti wakionyesha michezo ya ukakamavu wakati wa sherehe hizo. Picha na OMR SHA8 
  Vijana wa Skauti wakionyesha michezo ya ukakamavu wakati wa sherehe hizo.  SHA10 
  Kikundi cha Kwaya cha Skauti kikiimba wimbo maalum wa maadhimisho hayo. SHA11 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Skauti baada ya sherehe hizo. Picha na OMR

  0 0

  *Asema ni lazima zijengwe mpya, akataa kutoa mchango
  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amepiga marufuku ukarabati wa maabara za
  shule za sekondari na kusisitiza kwamba ni lazima zijengwe mpya kama
  ambavyo Serikali ilielekeza.

  Ametoa agizo hilo leo mchana (Jumamosi, Februari 21, 2015) wakati
  akizungumza na mamia ya wakazi wa kata ya Ilula, mara baada ya kukagua
  ukarabati wa maabara za sayansi kwenye shule ya sekondari Ilula,
  wilayani Kilolo, mkoani Iringa.

  “Mmefanya ukarabati kwenye jengo lililojengwa zaidi ya miaka 20
  iliyopita. Kuna chumba nimekuta ni kidogo mno sababu hakiendani na
  specifications za sasa... chumba kimoja kimepasuka ukuta, hapana! RC
  kama kuna nyingine ya aina hii kazi isiendelee,” alisema.

  “Huu ukarabati mliofanya ni kinyume na maelekezo ya Serikali ya kutaka
  zijengwe maabara mpya. Tulisema zijengwe maabara mpya ili ziweze
  kudumu kwa miaka mingi kidogo. Kuna chumba ceiling board iko chini kwa
  sababu ujenzi ni wa zamani. Ujenzi wa sasa mapaa yako juu zaidi ili
  kuruhusu hewa ya kutosha,” aliongeza.

  “Ningeweza kusema vunjavunja lakini haitakuwa haki kwa sababu kuna
  fedha za watu zimetumika... kwa sasa yatatuhifadhi kwa muda kidogo,
  lakini haya majengo hayatadumu hata kidogo,” alisema.

  Waziri Mkuu pia alikataa kuahidi mchango aliiombwa achangie na
  kuwaeleza kwamba atakuwa tayari kuchangia ujenzi wa jengo jipya na
  siyo ukarabati kwani huo utakuwa ni upotevu wa fedha. Majengo
  aliyoonyeshwa Waziri Mkuu Pinda yalijengwa mwaka 1995 na yalikuwa
  yakitumika kama maabara kwenye sekondari hiyo.

  Alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Bibi Amina Masenza asimamie watu wake
  ili ujenzi wa maabara uweze kukamilika kwa muda uliopangwa. Mkoa huo
  unahitaji mabaara 72 na zilizokamilika ni maabara tano tu huku
  nyingine 53 zikiwa kwenye hatua mbalimbali za ujenzi na 13 bado ziko
  kwenye msingi na moja iko kwenye linta.

  Mapema, akitoa taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Mtendaji wa Kata ya
  Ilula, Bw. Titus Katemo alisema shule ya sekondari Ilula ilijenga
  maabara zake mwaka 1995 kwa nguvu za wananchi na kwamba zilikuwa
  zikitumika toka kipindi chote hicho.

  Alisema ili kuendana na matakwa ya Wilaya, ukarabati wa vyumba vitatu
  ulianza Novemba 15, mwaka jana kutokana na vyumba hivyo kutumiwa na
  watahiniwa wa kidato cha nne wa mwaka 2014 kwenye mitihani ya vitendo.

  “Makisio ya gharama za ukarabati wa vyumba vitatu yalikuwa ni sh.
  38,294,775.00  na tunatarajia ukarabati utakamilika ifikapo tarehe 30
  Machi 2015,” alisema na kumuomba Waziri Mkuu awasaidie awaunge mkono
  kwa mchango kwani kasi ya wananchi kuchangia imekuwa ndogo.

  Waziri Mkuu anaendelea na ziara yake wilayani Kilolo na mchana huu
  anaenda kukagua mradi wa umwagiliaji wa Nyanzwa na pia atazungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMAMOSI, FEBRUARI 21, 2015.

  0 0

   Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi   Dkt. Shukuru Kawambwa (katikati)akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo jipya la Mitihani la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE)  kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa (NACTE) Dkt. Primus Nkwela,Kamishina wa Elimu Profesa Uestella Bhalalusesa,Naibu Katibu Mkuu wa Wizara wa wizara hiyo Consolata Mgimba  na Mwenyekiti wa barabaza la Taifa la Elimu ya Ufundi  Mhandisi Steven Mlote.Hafla hiyo ya Uzinduzi ilifanyika katika makao makuu ya ofisi hizo Mikocheni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
   Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi   Dkt. Shukuru Kawambwa (kulia) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Consolata Mgimba wakizinduzi jengo jipya la Mitihani la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE)  uzinduzi huo ulifanyika  makao makuu ya NACTE Mikocheni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 
   Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi   Dkt. Shukuru Kawambwa  (kushoto)akimsikiliza kwa makini  Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt.Primus Nkwela  wakati alipokuwa akimfafanulia jambo alipokuwa mgeni rasmi kwenye  hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Mitihani lililopo makao makuu ya ofisi hiyo Mikocheni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
   Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt.Primus Nkwela ( aliyesimama) akifafanua jambo mgeni rasmi Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi   Dkt. Shukuru Kawambwa  (kushoto) wakati hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Mitihani lililopo makao makuu ya ofisi hiyo Mikocheni jijini Dar es Salaam,mwishoni mwa wiki.Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Consolata Mgimba.

   Katibu Mkuu waWizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi   Sifuni Mchome akinongonezwa jambo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt.Primus Nkwela  wakati  wa hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Mitihani uliofanyika makao makuu ya ofisi hizo Mikocheni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
   Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi   Dkt. Shukuru Kawambwa (katikati) na  Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi,  Mhandisi Steven Mlote wakimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt.Primus Nkwela wakati alipokuwa akisoma lisala wakati  wa hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Mitihani la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE)  uliofanyika Mikocheni B jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
   Katibu Mtendaji  wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)  Dkt.Primus Nkwela, akisikilizwa jambo na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi   Dkt. Shukuru Kawambwa (kushoto) na wadau wengine  wa elimu wakati alipokuwa akielezea jinsi walivyofanikiwa kujenga jengo hilo jengo hilo wakati wa uzinduzi wa jengo hilo jipya la Mitihani la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE)  uliofanyika Mikocheni B jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

   Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi   Dkt. Shukuru Kawambwa (katikati) akimshukuru Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi,  Mhandisi Steven Mlote  baada ya kumkabidhi zawadi  katika  hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Mitihani la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE)  uliofanyika Mikocheni B jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt.Primus Nkwela.
   Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi   Dkt. Shukuru Kawambwa akionesha cheti halali cha matumizi ya jengo jipya alilolizindua la Mitihani la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE) lililopo makao makuu ya Baraza hilo Mikocheni B  jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt.Primus Nkwela na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi,  Mhandisi Steven Mlote.
  Katibu Mkuu waWizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi   Sifuni Mchome( kulia) akisikilizwa kwa makini na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi  Dkt.Shukuru Kawambwa  (kushoto ) na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt.Primus Nkwela (katikati)alipokuwa akifafanulia jambo wakati wa  hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Mitihani lililopo  Mikocheni B jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
   
  Serikali imesema itaendelea kusaidia upatikanaji wa rasilimali watu na fedha ili kuliwezesha Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kutekeleza malengo yake ya kukuza stadi na maarifa kwa idadi kubwa ya vijana wanaohitimu shule za msingi na za sekondari.
   
  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo jipya la mitihani la baraza hilo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt Shukuru Kawambwa alisema sekta ya elimu hususani Elimu ya Ufundi na Mafunzo Stadi inakuwa kwa kasi kubwa haswa ikizingatiwa kuwa wahitimu wa ngazi za elimu ya msingi na sekondari inaongezeka kila mwaka.
   
  Waziri Kawambwa alieleza kuwa, wahitimu wengi hawapati fursa za kuendelea na masomo hadi ngazi ya vyuo vikuu. “Wahitimu hawa wanahitaji fursa mbali mbali za kukuza stadi na maarifa ambazo zitawasaidia kukabiliana na changamoto za maisha yao ya kila siku na kuingi katika soko la ushindani la ajira ndani nan je ya nchi,”  alielezaa
   
  Kuhusu ongezeko la vyuo vinavyoendesha mafunzo ya Ufundi alisema inaonyesha kuwa hadi sasa kuna idadi ya vyuo takribani 501 na kozi zipatazo 1050 kuanzia ngazi ya Cheti hadi Shahada ya kwanza zinazoendeshwa katika vyuo kwa udhibiti wa  Baraza.
   
  “Huu ni ushahidi tosha kuwa mahitaji ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa vijana wetu ni makubwa ukilinganisaha na uwezo wetu wa kutoa mafunzo hayo. Hivyo, ipo haja kwa baraza kuimarisha Ofisi za kanda ili ziweze kutoa huduma za karibu, kwa wakati na kwa grarama nafuu,” alieleza
   
  Kwa upande wake mwenyekiti wa Braza hilo Injinia Steven Mlote alisema ili kuhakikisha vyuo vinazingatia masharti ya usajili wao na vinatoa elimu bora, Baraza limeweka nguvu kubwa katika kufuatilia na kusimamia ubora wa elimu unatolewa na vyuo vilivyosajiliwa na baraza
   
  “Baraza limefungua ofisi katika kanda 6 kwa ajili ya kusogeza huduma mikoani na kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji. Aidha, kukamilika kwa jengo hili ni utekelezaji wa mkakati  wa kuimarisha huduma za kudhibiti ubora kwa vyuo na uendeshaji mitihani ulioanza kwa kununua mitambo ya kuchapisha mitihani,”
   
  Katika hatua nyingine, mwenyekiti huyo alisema kuwa kutumia Sheria na Kanuni zake, Baraza limetoa notisi ya siku 30 kwa vyuo na taasisi 13 kufungiwa na kufutiwa usajili endapo havitakidhi vigezo vya baraza na pia aliatangaza kutolewa kwa notisi ya kuvishusha hadhi vyuo na taasisi 61.
   

  0 0

   Wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Utalii wakipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Uzalishaji wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL),Castor Massawe (mbele katikati) jinsimalighafi za nafaka zinavyohifadhiwa katika ghala, walipotembelea kiwanda cha TBL, Dar es Salaam juzi.
   Mhandisi Uzalishaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Castor Massawe (katikati) akitoa maelezo kuhusu upishi wa bia kwa njia ya kompyuta wakati wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Utalii walipotembelea kiwanda cha TBL, Dar es Salaam juzi.
   Mhandisi Uzalishaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Castor Massawe (katikati) akitoa maelezo kuhusu uchachuaji wa bia kwa njia ya kisasa wakati wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Utalii walipotembelea kiwanda cha TBL, Dar es Salaam
   Mhandisi Uzalishaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Castor Massawe (katikati) akitoa maelezo kuhusu uchachuaji wa bia kwa njia ya kisasa wakati wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Utalii walipotembelea kiwanda cha TBL, Dar es Salaam
   Mhandisi Uzalishaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Castor Massawe (katikati) akitoa maelezo kuhusu uchujaji wa bia kwa njia ya kisasa wakati wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Utalii walipotembelea kiwanda cha TBL, Dar es Salaam
  Wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Utalii, wakitembelea Kiwanda cha Bia Tanzania cha Dar es Salaam juzi, ikiwa ni sehemu ya mafunzo yao.

  0 0


  DSCF6604
  Baraza Kuu la Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Lindi chini ya Mwenyekiti wake Ndugu Amir M. Mkalipa, wamefanya kikao cha kikanuni leo tarehe 21 Feb. 2018, katika ukumbi wa mikutano wa ofisi kuu ya CCM Mkoa wa Lindi, iliyopo Wailes, Lindi mjini.

  Pamoja na kujadili hoja zingine zinazohusu uimara wa jumuiya mkoani Lindi, changamoto za Vijana na Walimu, suala la migomo ya wafanyabiashara, na kuwataka watendaji wa Serikali kutimiza wajibu na majukumu yao kikamilifu ili kuongeza ufanisi wa Serikali katika kutatua 

  kero za wananchi na kuleta maendeleo ya jamii, lakini pia kikao hicho kimeazimia:-a} Baraza kuu la UVCCM Mkoa wa Lindi imeitaka Serikali kuendelea kuchukua hatua kali kwa watakaobainika kuhusika na mauaji ya Albino. Ni lazima Serikali kushirikiana na wananchi wahakikishe ndugu zetu Albino wanaishi maisha yenye usalama, amani na furaha kwani ni haki yao kikatiba.

  b}Pia, Baraza Kuu la UVCCM Mkoa wa Lindi linampongeza Mhe. Rais na Mwenyekiti wa CCM ndugu Jakaya Kikwete kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM (2010-2015) kwa kukamilisha ujenzi wa barabara ya Kibiti-Mingoyo,Pia inampongeza Mhe Rais Jakaya Kikwete kwa kuteuliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa jumuiya ya Afrika Mashariki.

  Lakini pia, UVCCM inampongeza na kumuunga mkono Mhe Rais kwa uteuzi wa wakuu wa wilaya wapya 27 ambapo baadhi ya wateule hao wanatoka kwenye jumuiya hiyo, jambo ambalo ni heshima kubwa kwa UVCCM, na kudhihirisha kuwa jumuiya hiyo inatimiza wajibu wake wa kuwa tanuru la kuoka viongozi wenye uwezo, waadilifu na wenye kuaminika katika jamii. Pia UVCCM imewapongeza ndugu Mboni Mhita na ndugu Paul Makonda kwa kuteuliwa kuwa wakuu wa wilaya na kuwataka wakatimize wajibu kwa kuwatumikia wananchi kwa uadilifu na ufanisi.

  Pia, UVCCM Lindi inampongeza Kamanda wa Vijana Mkoa Mhe Bernard Membe-Mbunge wa Mtama na Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa kwa kuwa karibu na Vijana na kuiwezesha jumuiya kutimiza majukumu yake.

  C} Mwisho, UVCCM Mkoa wa Lindi inahimiza Halmashauri za wilaya kutenga asilimia 10% ya Mapato yake kwa ajili ya maendeleo ya Vijana na Wanawake, ili vijana wanufaike kwa mikopo na waweze kujiajiri ili kukabiliana na tatizo la ajira na umasikini. Jambo hili lipo kisheria sio ombi, hivyo watendaji husika wa Serikali wahakikishe wanatimiza wajibu wao ipasavyo ama UVCCM itawalazimisha kutimiza wajibu huo.

  Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Lindi, wamepitisha ratiba ya shughuli zao kwa Mwaka 2015 na wataanza ziara ya kutembelea Vijana katika wilaya zote sita (6) za Mkoa wa Lindi.

  0 0

  1
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Chief wa Wahehe , Adam Abdu Sapi Mkwakwa   wakati alipokwenda nyumbani kwa Chief huyo, Kalenga Iringa  Februari 20, 2015 baba yake Chief huyo, Marehemu Abdu Adam Sapi Mkwawa uliotokea hivi karibuni.
  (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  2
    Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akishiriki katika dua mbele ya kaburi la marehemu Abdu Adam Sapi Mkwawa   wakati alipokwenda nyumbani kwa Chief huyo, Kalenga Iringa   kuhani.
  6
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizunbgumza na viongozi wa wilaya ya Kilolo baada ya kusomewa taarifa ya wilaya hiyo Februari 21, 2015. Kushoto ni Mkuu wa koa wa Iringa, Amina Masenza.
  7
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  na mkewe Tunu  wakisalimiana na walimu  wa sekondari ya Ilula kabla ya kukagua ujenzi wa maabara katika shule hiyo akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa.
  8
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua moja ya madarasa ambayo yamegeuzwa kuwa maabara katika Shule ya Sekondari ya Ilula akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa Februari 21, 2015. Kitendo hicho hakikumfurahisha na aliagiza kisirudiwe tena sehemu nyingine ngo mapya yajengwe kwa ajili ya maabara
  9
  Mke wa Waziri Mkiuu, Mama Tunu Pinda akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ilulawilayani Kilolo ambako Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alikagua ujernzi  wa maabara na kuhutubia wananchi. 

  10
  Mkuu, Mizengo Pinda akikagua banio katika mradi wa umwagiliaji maji wa kijiji cha  Nyanzwawilayani Kilolo akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa Februari 21, 2015.
  12
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakikagua shmba la vitunguu la Bw. Furaha Ngalali  (kulia)  wakati walipotembelea mradi wa umwagiliaji wa kijiji cha Nyanzwa wilayani  Kilolo Februari 21, 2015.
  13
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na   Meneja Mipango wa Kamouni ya Mawasiliano ya simu ya VIETTEL TANZANIA LIMITED tawi la Iringa, Salvatory Elikidus katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkiuu, Mizengo Pinda katika kijiji Nyanzwa wilayani Kilolo Februari 21, 20154.  Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Tawi la Iringa,  Tran  Nhat Duy na wapili kushoto ni  Mkuu wa Idara ya Fedha, Vo Ngoc Thang.

  0 0

   Mwenyekiti  wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Taifa, James Mbatia (kulia), akionesha kitabu cha Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akitoa tamko la chama hicho juu sera hiyo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Mosene Nyambabe na kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Zanzibar, Musa Kombo Musa.
   Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Zanzibar, Musa Kombo Musa (kulia), akimkaribisha Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, James Mbatia (katikati), ili azungumze na wanahabari Dar es Salaam leo asubuhi wakati akitoa tamko hilo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Mosene Nyambabe.
   Hapa mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.
   Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
   Wanahabari wakiwa katika mkutano huo.
  Wajumbe wa Halmshauri Kuu (NEC) ya chama hicho waliokuwepo kwenye mkutano huo. Kutoka kulia ni Honest Mombory, Katibu wa Wazee, Ernest Mwasada, Dk.Nderakindo Kessy ambaye pia pia ni Mbunge wa Afrika Mashariki, Angelina Mutahiwa na Esther Komba.

  Dotto Mwaibale
   
  MWENYEKITI wa Chama cha NCCR-Mageuzi Taifa, James Mbatia amesema kuwa uzinduzi wa Sera Mpya ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 ni mpango wa serikali kuwalaghai wananchi kuelekea Uchaguzi Mkuu utakao fanyika Oktoba mwaka huu.

  Pia amesema hali ya elimu nchini ni kama mgonjwa aliyekuwa katika chumba cha wagonjwa mahututi, hivyo serikali isiwe inatoa majibu mepesi kwenye masuala magumu ambayo yanagusa maisha ya watanzania.

  Akizungumza Dar es Salaam leo wakati akitoa tamko la chama hicho kuhusu sera hiyo Mbatia  alisema kuwa mnamo Januari 31 na Februari mosi mwaka 2013, aliwasilisha hoja bungeni kuhusu udhaifu uliopo katika sekta ya elimu.

  Alisema kuwa aliorodhesha athari mbalimbali za udhaifu wa wa elimu itolewayo nchini lakini suala hilo lilionekana kutawaliwa na siasa ambapo haikuwa lengo lake,lengo lilikuwa kuhakikisha kuwa sera mbalimbazi za elimu zinaboreshwa. Mbatia aliongeza kuwa mnamo Februari 13, 2015 mwaka huu Rais Jakaya Kikwete, alizindua Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 lakini ikiwa haijajibu hoja alizokuwa amezitoa.
  Alifafanua kuwa wakati Rais akihutubia alisema kuwa sera hiyo ilitumia miaka saba kukamilika, lakini Mwenyekiti huyo alisema baada ya kuipitia alibaini sera hiyo kuwa na lugha ngumu huku ikiwa na makosa mengine mengi.
  Mbatia alisema anachokiona kwa serikali kuzindua sera hiyo mwaka huu ni mikakati ya kuelekea uchaguzi mkuu,kwani yaliyomo ndani ya sera hiyo yamelenga kuwalaghai wapiga kura.

  Aidha alisema mambo hayo ni pamoja na kutangaza kuwa elimu ya msingi kutolewa bure bila karo na lugha iliyotumika inawachanganya watanzania hivyo ni vigumu kwa wananchi wa vijijini ambao wengi wao hawana elimu kutambua yaliyoandikwa ndani ya sera hiyo.

  “Mfano sera mpya ina matamko mawili ambayo  inawachanganya watanzania kuhusu lugha ya kufundishia,moja inatamka Kiswahili kitatumika kama lugha ya kufundishia ngazi zote za elimu,na ya pili inatamka kuwa Kingereza kitatumka kama lugha ya kufundishia katikan ngazi zote za elimu.

  “Matamko haya mawili, kwanza yanakwepa lawama zinazotokana na malumbano ya muda mrefu kuhusiana na lugha gani inafaa kufundishia, pili imehalalisha mifumo miwili ya elimu ndani ya nchi moja” alisema Mbatia kwa msisitizo .

  Hivyo alisema serikali ilipaswa kutengeneza sera ambayo inazungumza kwa uhakika kuhusu suala la lugha ya kufundishia, kuliko kutoa tamko la sera lisilo na msimamo. Aliweka wazi kuwa wanapendekeza iundwe tume ya kudumu ya elimu nchini itakayoshughulikia pamoja na mambo mengine kuhakikisha ubora wa elimu unapatikana nchini.

  Vilevile alisema wanaiomba serikali kupitia upya sera hiyo kabla haijaanza kutumika ili kuepusha taifa na madhara ambayo yameonesha dalili za kutokea hata kabla haijaanza kutumiaka.(Imeandaiwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

older | 1 | .... | 467 | 468 | (Page 469) | 470 | 471 | .... | 1898 | newer