Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live

WAZIRI CHIKAWE ATUA NCHINI MAREKANI KUSHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA WA KUPAMBANA NA VURUGU NA UGAIDI DUNIANI

$
0
0
mula1 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akikaribishwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula wakati Waziri huyo alipowasili ubalozini hapo jijini Washington DC kujiandaa kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani unaotarajiwa kufanyika jijini humo kesho. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mula2 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati) akimsalimia Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, jijini New York, nchini Marekani, Tuvako Manongi wakati Waziri huyo alipowasili ubalozi wa Tanzania nchini humo uliopo katika Jiji la Washington DC kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani unaotarajiwa kufanyika jijini humo kesho. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mula3 
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula (katikati) akimtambulisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (watatu kulia) Maofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini humo wakati Waziri huyo alipowasili ofisini hapo, jijini Washington DC kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani unaotarajiwa kufanyika jijini humo kesho. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mula4 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wanne kulia) akizungumza na Maofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani baada ya Waziri huyo kuwasili ubalozini hapo jijini Washington DC kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani unaotarajiwa kufanyika jijini humo kesho. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mula5 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati), Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula (kushoto) na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, jijini New York, nchini humo, Tuvako Manongi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumpokea Waziri huyo aliyewasili jijini Washington DC kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani unaotarajiwa kufanyika jijini humo kesho. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

WAZIRI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII, MHE LAZARO NYALANDU ALIPOZUNGUMZA NA WAJUMBE WA KAMATI YA MALIASILI, ARDHI NA MAZINGIRA YA NORWAY

$
0
0
 Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu ( katika kati) akimsikiliza  Mwenyekiti wa Kamati ya  Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira ya Norway, Mhe. Ola  Elvestuen  (kushoto) wakiwa na Balozi wa Norway Nchini Tanzania, Bi.  Hanne-Marie Kaarstad, (kulia) Kabla ya Mkutano  wa Kamati ya  Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira ya Norway  uliofanyika Mpingo House jijini Dar es Salaam.
 Waziri waWizara ya Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu akizungumza na wajumbe wa Kamati ya  Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira ya Norway kwenye Mkutano   uliofanyika Mpingo House jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya  Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira ya Norway, Mhe. Ola  Elvestuen  ( kushoto) akimkabidhi zawadi Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu baada  ya Mkutano  wa Kamati ya  Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira ya Norway uliofanyika Mpingo House jijini Dar es Salaam.

WADAU WA CHANJO YA KUZUIA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI (HPV) WAKUTANA KILIMANJARO.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama akizungumza wakati wa kufungua Mkutano wa Wadau wa Chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi (HPV) katika ukumbi wa Uhuru Hostel mjini Moshi.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia kwa karibu hotuba ya mkuu wa mkoa Gama.
Mwakilishi wa katibu mkuu wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Dkt Neema Rusibamayila akitoa hotuba yake wakati wa mkutano huo wa siku tatu unaofanyika mjini Moshi.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakiwemo Wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wakifuatilia hotuba ya mwakilishi wa katibu mkuu wizara ya Afya,Dkt Rusibamayila.
Mwakilishi mkazi wa Shirika la Afya  Duniani (WHO) Dkt Rusaro Chatora akitoa hotuba yake wakati wa mkutano wa wadau  wa chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa Kizazi (HPV).
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akiteta jambo na Dkt Neema Rusibamayila wakati wa mkutano huo.
Meneja Mpango wa Chanjo taifa Dkt Dafrossa Lyimo akizungumza wakati wa mkutano huo.
Baaadhi ya wawakishi wa Mashirika ya Maendeleo wakifuatilia mkutano huo.
Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro Seveline Kahitwa akizungumza katika mkutano huo;.
Kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt Quaker akifuatilia hotuba zilizotolewa wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
Mwakilishi mkai wa shirika la Afya Duniani Dkt Rufaro Chatora akiwa na Dkt Neema Rusibamayila wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika mkutano huo.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akifurahia jambo na Dkt Chatora.
Washiriki wa mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi ,mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama.
Kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt Endrew Quaker akizungumza na mwakilishi mkazi wa shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt Rufaro Chatora nje ya ukumbi wa mkutano.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

NEWS ALERT: RAIS KIKWETE ATEUA WAKUU WA WILAYA WAPYA 27,WAPYA WAKIWEMO SHABANI KISU,PAUL MAKONDA,FREDRICK MWAKALEBELA

$
0
0
*Atengua uteuzi wa Ma-DC 12, awabadilisha vituo 64, awabakiza 42 kwenye vituo vyao vya zamani.

RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya kwa kuwateua Wakuu wapya 27, kuwahamisha vituo vya kazi 64 na wengine 42 amewabakisha kwenye vituo vyao vya kazi vya zamani.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa OWM TAMISEMI leo mchana (Jumatano, Februari 18, 2015) Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema mabadiliko hayo yamesababishwa na kuwepo kwa nafasi wazi 27 ambazo zilitokana na wakuu wa wilaya watatu kufariki dunia; kupandishwa cheo wakuu wa wilaya watano, kupangiwa majukumu mengine wakuu wa wilaya saba na kutenguliwa kwa uteuzi wa wakuu wa wilaya 12.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema, Rais  Kikwete amewabadilisha vituo vya kazi wakuu wa wilaya 64 na kuwabakiza kwenye vituo vyao vya zamani wakuu wa wilaya 42.

Wakuu wa Wilaya wapya 27 walioteuliwa ni Mariam Ramadhani Mtima anayeenda Ruangwa; Dk. Jasmine B. Tiisike anayeenda Mpwapwa; Pololeti Mgema (Nachingwea); Fadhili Nkurlu anayeenda Misenyi; Felix Jackson Lyaniva anayeenda Rorya na Fredrick Wilfred Mwakalebela anayeenda wilayaya Wanging’ombe.

Wengine na vituo vyao kwenye mabano ni Zainab Rajab Mbussi (Rungwe); Francis K. Mwonga (Bahi); Kanali Kimiang’ombe Samwel Nzoka (Kiteto), Husna Rajab Msangi (Handeni), Emmanuel J. Uhaula (Tandahimba); Mboni Mhita (Mufindi); Hashim S. Mgandilwa (Ngorongoro); Mariam M. Juma (Lushoto); Thea Medard Ntara (Kyela); Ahmad H. Nammohe (Mbozi); Shaban Kissu (Kondoa) na Stephen Zelothe (Musoma).

Wengine ni Pili Moshi (Kwimba); Mahmoud A. Kambona (Simanjiro); Glorius B. Luoga (Tarime); Zainab R. Telack (Sengerema); Bernard Nduta (Masasi); Zuhura Mustafa Ally (Uyui); Paulo Makonda (Kinondoni); Mwajuma Nyiruka (Misungwi) na na Maftah Ally Mohamed (Serengeti).

Wakuu wa Wilaya saba ambao uteuzi wao umetenguliwa lakini watapangiwa kazi nyingine ni Brig. Jenerali Cosmas Kayombo aliyekuwa Simanjiro; Kanali Ngemela E. Lubinga (aliyekuwa Mlele); Juma S. Madaha (aliyekuwa Ludewa); Mercy E. Silla (aliyekuwa Mkuranga); Ahmed R. Kipozi (aliyekuwa Bagamoyo); Mrisho Gambo (aliyekuwa Korogwe) na Elinas A. Pallangyo (aliyekuwa Rombo).

Waziri Mkuu pia aliwataja Wakuu wa Wilaya 12 ambao uteuzi wao umetenguliwa kutokana na sababu za umri, kiafya na kuimarisha utendaji Serikaini na wilaya zao kwenye mabano kuwa ni James K. Ole Millya (Longido); Elias Wawa Lali (Ngorongoro); Alfred Ernest Msovella (Kongwa); Danhi Beatus Makanga (Kasulu); Fatma Losindilo Kimario (Kisarawe); Elibariki E. Kingu (Igunga); Dk. Leticia Moses Warioba (Iringa); Evarista N. Kalalu (Mufindi); Abihudi M. Saideya (Momba); Martha J. Umbulla (Kiteto); Khalid J. Mandia (Babati) na Elias Goroi (Rorya).


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.

JUMATANO, FEBRUARI 18, 2015.

Balozi Seif Ali Idd afungua mkutano wa kikanda wa Ukuaji wa maisha ya baadae kwa miji ya Afrika,jijini Dar leo

$
0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd (wa pili kushoto) akiwa katika meza kuu pamoja na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI,Mh. Hawa Ghasia (kushoto),Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Mh. Said Meck Sadick (wa pili kulia),Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi,Prof. Joseph Sembojo (katikati) pamoja na Dkt. Remy Sietchiping kutoka UN-Habitat wakati wa Mkutano wa Kikanda uliojadili Ukuaji wa maisha ya baadae kwa miji ya Afrika,uliofanyika leo kwenye Hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es salaam. 
 Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi,Prof. Joseph Sembojo akizungumza wakati wa ufunguzi Mkutano wa Kikanda uliojadili Ukuaji wa maisha ya baadae kwa miji ya Afrika,uliofanyika leo kwenye Hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es salaam. 
 Muwakilishi kutoka Shirika la UN-Habitat,Dkt. Remy Sietchiping akifafanua jambo juu ya changamoto mbali mbali zinazoikabili miji mingi ya mikubwa Afrika Mashariki wakati wa Mkutano wa Kikanda uliojadili Ukuaji wa maisha ya baadae kwa miji ya Afrika,uliofanyika leo kwenye Hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es salaam. 
 Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi,Prof. Joseph Sembojo akiteta jambo na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd wakati wa Mkutano wa Kikanda uliojadili Ukuaji wa maisha ya baadae kwa miji ya Afrika,uliofanyika leo kwenye Hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es salaam.Katikati ni Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI,Mh. Hawa Ghasia. 
 Sehemu wa washiriki wakiw katika Mkutano wa Kikanda uliojadili Ukuaji wa maisha ya baadae kwa miji ya Afrika,uliofanyika leo kwenye Hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es salaam.
 Mtoa Mada katika Mkutano huo,Prof. David Simon akizungumza jambo wakati Mkutano wa Kikanda uliojadili Ukuaji wa maisha ya baadae kwa miji ya Afrika,uliofanyika leo kwenye Hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es salaam.
 Mmoja wa wadau wa Mkutano huo akichangia mada.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Kikanda uliojadili Ukuaji wa maisha ya baadae kwa miji ya Afrika,uliofanyika leo kwenye Hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es salaam.
Picha ya pamoja.

Na Chalila Kibuda
Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd,amesema watu wegi waonaishi maeneo ya mijini katika Afrika na dunia nzima wanapata changamoto ambazo ni lazima ziainishwe katika kuweza kuzikabili.

Balozi Idd ameyasema hayo leo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kikanda uliowakutanisha viongozi na watunga sera kutoka nchi za Afrika Mashariki kuzungumzia changamoto za ukuaji wa miji na kushughulikia hali ya baadaye ya miji ya Afrika na jinsi gani tunataka kuishi mwaka 2050,uliofanyika katika ukumbi wa Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

‘’Maeneo ya mjini  katika Afrika yana  fursa lakini maeneo hayo yana changamoto kutokana na ukuaji wa uchumi pamoja na mwingiliano wa kijamii’’amesema Balozi Idd.

Amesema maeneo ya mijini na majiji ni vituo vya fursa za uchumi,Teknolojia na sehemu ya kubadilishana mawazo na uzoefu  na kufanya watu wa vijijini kuvutika zaidi wakiwemo vijana kukombilia mjini kwa ajili ya urahisi wa kupatikana kwa fursa pamoja na huduma mbalimbali.

Balozi Idd amesema watu wanaokwenda katika  majiji wanajifunza njia  mpya za kuishi na kufikiria jinsi ya kuendesha maisha yao kutokana na kuwepo hali hiyo majiji yanapambana dhidi ya umasikini na kuweka mikakati bora  ya kuendesha majiji hayo.

Aidha amesema kushindikana na uimara katika miji na majiji matokeo yake ni umasikini unaingia ,magonjwa na kuwepo hali hiyo inaleta maswali ambayo yanatakiwa kuangalia ni jinsi gani ya kuweza kuyatatua.

Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi wa Afrika kwa Maendeleo Endelevu,Profesa Joseph Semboja amesema jukwaa hilo la leo ni kuangalia changamoto na fursa mbalimbali  zinazoletwa na ukuaji wa miji ya ukanda wa Afrika Mashariki  na jinsi ya viongozi wa Afrika wanavyoweza kukabiliana nazo kwa pamoja.


‘’Kuna changamoto na uwiano mkubwa wa ongezeko la watu Afrika na duniani kwa ujumla wanaoishi mijini na kusababisha msongamano na shinizo la nyumba ,ajira huduma za kijamii’’amesema Prof.Semboja.

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA YALAANI MAUAJI YA MTOTO YOHANA

SERIKALI YASISITIZA MATUMIZI YA TAKWIMU SAHIHI.

$
0
0
  Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Ofisi Bw. Michael Madembwe akizungumza na wazalishaji na watumiaji wa takwimu leo jijini Dar es salaam. Warsha hiyo imewakutanisha wadau hao  kutoka maeneo mbalimbali nchini, kubadilishana uzoefu na kuangalia changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika usambazaji na ukusanyaji wa takwimu nchini.
 Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012,  Hajjat Amina Mrisho Said  akifungua warsha ya siku mbili ya wazalishaji na watumiaji wa takwimu kutoka  Wizara, Idara za Serikali, Wakala, Taasisi za Elimu na Utafiti, Vyuo Vikuu  pamoja na Wadau wa mbalimbali wa maendeleo leo jijini Dar es salaam..
Baadhi ya washiriki wa warsha ya siku mbili ya wazalishaji na watumiaji wa takwimu kutoka  Wizara, Idara, Wakala na Taasisi za Serikali, Vyuo vya  Elimu ya Juu, Taasisi za kiraia,Taasisi za Utafiti na  Wadau wa mbalimbali wa maendeleo leo jijini Dar es salaam.


SERIKALI  YASISITIZA MATUMIZI YA TAKWIMU SAHIHI.
Na. Aron Msigwa 

19/2/2015. Dar es salaam.
SERIKALI imetoa wito kwa watafiti na wataalam kutoka vyuo vikuu, taasisi za elimu na mashirika binafsi kushiriki kikamilifu kuhamasisha  jamii kutumia takwimu sahihi zinazotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu  ili kuwezesha upangaji wa mipango endelevu ya maendeleo inayoendana na hali halisi ya maeneo husika.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakati akifungua warsha ya siku mbili ya wazalishaji na watumiaji wa takwimu kutoka  Wizara, Idara, Wakala na Taasisi za Serikali, Vyuo vya  Elimu ya Juu, Taasisi za kiraia,Taasisi za Utafiti na  Wadau wa mbalimbali wa maendeleo, Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012,  Hajjat Amina Mrisho Said amesema kuwa Serikali itaendelea kuhamasisha matumizi ya takwimu sahihi ili kuongeza uwazi na uwajibikaji. 

 Amesema wadau hao pamoja na mambo mengine wanalo jukumu  la kuielimisha jamii kuelewa mchango wa takwimu katika kufanikisha masuala mbalimbali ya taifa pamoja na uandaaji wa sera za maendeleo.

Bi. Hajjat amesema Serikali kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu imekuwa ikifanya mabadiliko makubwa katika uimarishaji na uboreshaji wa takwimu zinazokusanywa kutoka katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuongeza uwazi na uwajibikaji nchini.

“Tanzania sasa inafanya maboresho na mabadiliko makubwa ya takwimu zake sasa tunazo takwimu mbalimbali  na mkakati wa kuzisambaza takwimu hizo kwa watumiaji ili waweze kuzifanyia kazi unaendelea” Amesema .

Akizungumza kuhusu umuhimu warsha hiyo amesema inalenga kuwaweka pamoja wazalishaji na watumiaji wa takwimu kutoka katika maeneo mbalimbali ili waweze kujadili changamoto mbalimbali, kubadilishana uzoefu na kupeana mrejesho wa matumizi ya takwimu zilizopo hapa nchini.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Ofisi Bw. Michael Madembwe akizungumzia umuhimu wa warsha hiyo  kwa washiriki hao amesema kuwa imewakutanisha wadau hao kwa lengo la kuwajengea uwezo na kupima mafanikio ya shughuli za kitakwimu katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Ameongeza kuwa warsha hiyo ya siku 2 inalenga kuwawezesha wadau hao kuangalia changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika usambazaji na ukusanyaji wa takwimu katika maeneo mbalimbali nchini, kubadilishana uzoefu na kuangalia mahitaji yanayojitokeza pande kwa wazalishaji na watumiaji.

WAZIRI MKUU: WASAIDIENI WAKULIMA WA MPUNGA KUNUFAIKA NA ZANA ZA KISASA

$
0
0
 WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameutaka uongozi wa mkoa wa Iringa utafute njia bora ya kuwasaidia wakulima wanaotumia na skimu ya umwagiliaji ya Magozi katika tarafa ya Pawaga, wilayani Iringa ili waweze kunufaika na matumizi ya zana za kisasa kwenye kilimo cha mpunga.

Akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Katibu Tawala wa Mkoa huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Afisa Kilimo wa Wilaya hiyo na uongozi wa vijiji hivyo, mara baada ya kukagua eneo zima la mradi huo pamoja na zana za kilimo walizonazo leo mchana (Alhamisi, Februari 19, 2015), Waziri Mkuu alisema kwa zana walizonazo hawawezi kufikia lengo lao la uzalishaji wa tani nane kwa ekari moja kama wataendelea na kilimo cha majaruba.

“Hii combine harvester umesema inavuna ekari 12 kwa siku moja, sasa hapa kuna mtu ana robo eka, jirani yake ana nusu eka, pale kuna mwingine ana ekari mbili utawezaje kutumia mashine hii? Kimsingi haiwezekani,” alihoji Waziri Mkuu.

Alimtaka Mkuu wa Mkoa huo, Bi. Amina Masenza awasiliane na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na kupata taarifa wao walifanyaje katika mradi unaohusisha wakulima wadogo na mwekezaji kwenye kilimo cha mpunga wilayani Kilombero.

“Pangeni naye muone jinsi ya kuwachukua baadhi ya wakulima wadogo wa kata hii ili waende huko na kuona wenzao wamefanyaje kwenye kilimo kama chao lakini kinachotumia zana za kilimo za kisasa,” alisema Waziri Mkuu.

“Kikubwa hapa ni kuwaunganisha wawe na ushirika, walime kwa staili ya block farm... lakini wakishavuna kila mmoja apate mgao wake kulingana na eneo lake analomiliki. Mkifanya hivi mtaona tija katika matumizi ya mashine hizi, matumizi ya dawa za kuua magugu na hata matumizi ya mbegu bora,” aliongeza.

Katika skimu hiyo ya umwagiliaji ya Magozi, Waziri Mkuu alikagua mashine ya kupandia mpunga yenye uwezo wa kupanda miche 1,856 kwa ekari moja ama ekari tano kwa siku moja. Pia alikagua mashine ya kupurura mpunga yenye uwezo wa kupurura tani moja nusu za mpunga kwa siku. Vilevile, alionyeshwa mashine mbili za kuvuna mpunga ambapo kila moja ina uwezo wa kuvuna ekari 12.

Waziri Mkuu ambaye aliwasili mkoani Iringa jana jioni (Jumatano) akitokea Dodoma, ameanza ziara ya kikazi ya siku tano katika mkoa huu ili kukagua shughuli za maendeleo.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, FEBRUARI 19, 2015.

Three Young Musicians from Zanzibar receive Andrew Scivener Scholarship

$
0
0
 
Since 2006 DCMA has been receiving grants from the Andrew Scrivener family for the purpose of supporting students of DCMA

The Andrew Scrivener Fund (UK) was established in memory of the late BBC Philharmonic Orchestra violinist to sustain the Music studies of young and talented students from all over Tanzania. Over the years, DCMA has had four intakes of students supported by the Andrew Scrivener Scholarship to study different instruments. This year three DCMA students will receive support from the Fund.

The students receiving scholarship assistance are Rahma Ameir for her study of the violin, Amina Omar for her study of the oud and Said Bhai Said for his study of the qanun.

The Andrew Scrivener Scholarship Fund covers the students' course fees, costs for all study materials, purchase of the student's instrument of specialization and a weekly transport allowance for each of the students. 

This Scholarship has been greatly sought after, with many students applying and seeking the assistance of the award. The expressed criteria for receiving the award is the student's level of need and talent, gender equity and promotion of assisting individuals on learning some specific instruments.

The Dhow Countries Music Academy is a not-for-profit music institution based in Zanzibar that provides quality music education in various instruments as well as music related disciplines such as traditional African Dance, Music Theory as well as providing music courses in several schools.

SERIKALI YA WANAFUNZI CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA (IFM-SO) YAKANUSHA KUMPIGIA DEBE LOWASA.

$
0
0
Serikali ya wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha (IFMSO), kupitia
msemaji wake mkuu ambaye ni Rais wa Serikali ya wanafunzi, ndugu
Clinton Boniface inakanusha taarifa zilizotolewa na gazeti la NIPASHE
toleo namba 0578395 la tarehe 19/02/2015, lenye kichwa cha habari
“WANAFUNZI WA IFM WAMTAKA LOWASA URAIS” na kwamba habari hizo
hazijatolewa na uongozi wa IFMSO, wala hakuna mkutano wowote
uliofanyika katika eneo la chuo cha usimamizi wa fedha kati ya
waandishi wa habari na uongozi wa serikali ya wanafunzi na kutoa tamko
hilo. Pia, kulingana na Katiba ya IFMSO kifungu namba 3, ibara ndogo
ya 1, Katiba inakataza serikali ya wanafunzi (IFMSO) kushiriki katika
mambo yoyote ya kidini au kisiasa, hivyo basi IFMSO inasikitishwa na
taarifa hizo na inaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza
kutokana na taarifa hizo.

Imetolewa na;

…..........
Clinton Boniface.
Rais wa Serikali ya Wanafunzi.
IFM-SO
19/ 02/ 2015.

MKURUGENZI WA CLOUDS MEDIA GROUP,JOSEPH KUSAGA AKANUSHA TAARIFA YA KUUZWA KWA KITUO CHAKE.

$
0
0
Pichani chini ni sehemu ya taarifa hiyo iliyokanushwa na Bwa. Joseph Kusaga,ambayo imekuwa ikisambazwa na baadhi ya watu huku na kule katika mitandao ya kijamii.

Push Observer yazindua teknolojia ya kisasa ya ukusanyaji wa Taarifa ijulikanayo kwa jina la NewsRadar

$
0
0
 Mshauri mkuu wa mradi wa NewsRadar, Romana Gersuni kutoka Ujerumani akielezea jinsi teknolojia hiyo mpya na ya kisasa ya ukusanyaji taarifa mbalimbali ya Push Observer inavyofanyakazi zake.
 mkuu wa mikakati wa kampuni ya Six Telecoms ambayo ni kampuni mama ya Push Observer, Rashid Shamte akielezea faida ambazo watazipata kampuni mbalimbali nchini, husasani za kibiashara kwa kujiunga na huduma ya NewsRadar waliyoianzisha nchii.
Mkurugenzi Mtendaji wa  Kampuni ya Push Mobile Fred Manento akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ufanisi wa mradi wa NewsRadar ambao utawawezesha wafanyabiashara kupata taarifa mbalimbali kwa kutumia mradi huo mpya na wa kisasa nchini
 Afisa Mawasiliano wa kampuni ya Push Observer, Tunu Makamula akiteta jambo na wadau wa kampuni hiyo waliohudhuria semina elekezi na uzinduzi rasmi wa mradi wa NewsRadar ambao utawawezesha wafanyabiashara kupata taarifa mbalimbali kwa kutumia mradi huo mpya na wa kisasa nchini.

Sekta zote Nchini sasa zinaweza kupata taarifa mbali mbali zilizorushwa kwene vyombo vya habari kupitia teknolojia mpya ya usambazaji taarifa ijulikanayo kwa jina la NewsRadar ya kampuni ya Push Observer.

Push Observer Limited ni kampuni ya Tanzania inayomiliki vyombo vya kiinteligencia na teknolojia ya sanaa ya kufuatilia, kukamata na kuchuja vyombo vya habari - magazeti, matangazo (radio & televisheni), Internet na uchambuzi, ripoti ya ushindani kwa ajili ya biashara, serikali na wateja wengineo wa mashirika yasiyo ya kiserikali.

Hivi sasa, Push Observer wanachunguza vituo vya redio 90+, vituo vya televisheni 15+, magazeti (magazeti, majarida, magazeti na majarida) 70+ na machapisho online ikiwa ni pamoja na blogs na mitandao maudhui. Observer ni kampuni ya kiTanzania inayoongoza kidigitali, kwa viwango vya kimataifa na ushirikiano wa kimataifa katika data na uanachama na vyombo kama FIBEP, Nudge, Vision Critical, na Harvard Innovation Labs.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mikakati wa Six Telecoms, Kampuni mama ya Push  Observer, Rashid Shamte alisema kuwa kupitia teknologia hii ya usambazaji ya kisasa, wateja wao wataweza kupata habari taarifa muhimu na mpya masaa ishirini na nne ya wiki. Aliongeza kuwa,tumezindua teknolojia hii kwa wateja wetu kutokana na teknologia ya uchunguzi wa vyombo vya habari kubadilika sana miaka ya karibuni”.

“Huduma hii ya kusambaza taarifa imekuwa ya kisasa, rahisi na ya ubora wa hali ya juu kutokana na uwekezaji wetu katika teknolojia hii. Wana vifaa vya kisasa ambavyo vinaweza kupata taarifa kupitia televisheni, magazeti, mitandao ya kijamii na redio kwa muda muafaka, vifaa hivyo vinauwezo wa kupata taarifa had 350,000 kutoka vyombo mbali mbali. 

Kwa kutambua mahitaji ya wateja wetu kupata habari na taarifa za muhimu tumeamua kuzindua huduma hii na ili kuwahakikishia wateja wetu upatikanaji wa taarifa muhimu na taarifa zinginezo za kwene vyombo vya habari kwa muda muafaka” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Push Observer, Tom Kyalo.

Safari ya Mwisho ya DCP Mstaafu wa jeshi la Polisi Tanzania , Mzee Andrew Michael Kumalilwa huko Tabata Segerea.

$
0
0
 Jeneza lenye Mwili wa marehemu Mzee Andrew Michael Kumalilwa ukiwa tayari kushushwa nyumbani kwake Tabata Segerea ambapo misa ya kumuombea na kutoa heshima za mwisho zilifanyika kabla ya Kwenda kuupumzisha Mwili wake katika Nyumba yake ya Milele.
Askari wa Jeshi la Polisi Tanzania wakiwa wamebeba jeneza lenye Mwili wa aliyekuwa DCP Mstaafu wa Jeshi la Polisi Tanzania Mzee Andrew Michael Kumalilwa  wakiingia katika nyumba yake iliyopo Tabata Segerea kwaajili ya Misa na ndugu, jamaa na marafiki kutoa heshima za mwisho kabla ya kwenda kuupumzisha katika Nyumba yake ya Milele ambapo Marehemu alizikwa katika nyumba kwake Tabata Segerea.
 Mtoto wa Kwanza wa Marehemu Andrew Michael Kumalilwa, Patricia Andrew akiwa mwenye huzuni wakati wa msiba wa marehemu Baba yake ambapo marehemu alikuwa mstaafu wa jeshi la Polisi Tanzania akiwa na Cheo cha DCP.
 Jeneza lililokuwa limebeba Mwili wa Marehemu Mzee Andrew Michael Kumalilwa ukitolewa katika chumba cha kuhifadhia maiti kwaajili ya kuelekea nyumbani Kwake Segerea ambapo mazishi yalifanyika
 Baadhi ya Askari wa Jeshi la Polisi Tanzania wakitoa heshima mbele ya jeneza lililobeba Mwili wa Marehemu Mzee Andrew Michael Kumalilwa ambae alikuwa mstaafu wa jeshi la Polisi kwa ngazi ya DCP
 Ndugu wa marehemu akijadiliana jambo na Mmoja wa Askari wa Jeshi la Polisi wakati wa Kutoa Heshima za mwisho kabla ya kwenda kuupumzisha mwili wa Mzee Andrew Kumalilwa ambae alizikwa nyumbani kwake Tabata Segerea tarehe 14 Februari 2015.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi Tanzania, DCP Simon Siro akitoa maneno mafupi kabla ya kwenda kuupumzisha Mwili wa marehemu Mzee Andrew Kumalilwa katika nyumba yake ya Milele. Marehemu Andrew Kumalilwa alizikwa mnamo tarehe 14 February 2015 huko Nyumbani Kwake Tabata Segerea.

WAZIRI MKUU,MIZENGO PINDA ZIARANI KATIKA JIMBO LA ISIMANI NA KALENGA MKOANI IRINGA

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua matrekta madogo maarufu kwa jina la Power Tiller yanayotumika katika shamba la kilimo cha umwagiliaji la Magozi katika jimbo la Ismani wakati alipolitembelea shamba hilo akiwa katika ziara ya mkoawa Iringa Februari 19, 2015. Watatu kulia ni Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na walimu na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kiwere katika jimbo la Kalenga wakati alipotembelea maabara ya Kemia na Fizikia ya shule hiyo akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa Februari 19, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama mafunzo kwa vitendo ya kumfanyia upasuaji panya yaliyokuwa yakifanywa na wanafunzi wa kidato cha tatu, Rosemary Kapugi (kushoto) na Faudhia Ndunguru Wapili kushoto) wakati alipotembelea maabara ya Baiolojia ya shule ya sekondari ya Kiwere katika jimbo la Kalenga akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa, Februari 19, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua nyumba za walimu katika shule ya sekondari ya Kiwere katika jimbo la Kalenga akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa Februari 19, 2015. Kushoto ni Mkuu wa Shule hiyo, Blandina Nkondola na watatu kulia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Gerlad Guninita.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua nyumba za walimu katika shule ya sekondari ya Kiwere katika jimbo la Kalenga akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa Februari 19, 2015. Kushoto ni Mkuu wa Shule hiyo, Blandina Nkondola na wapili kulia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Gerlad Guninita.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wauguzi wa Kituo cha Afya cha Mlowa katika jimbo la Ismani kabla ya kuzindua kituo hicho akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa Februari 19, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipima mapigo ya moyo ikiwa ni ishara ya kuzindua kituo cha afya cha Mlowa katika jimbo la Isimani akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa Februari 19, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimjulia hali mmoja wa wagonjwa waliolazwa kwenye kituo cha afya cha Mlowa katika jimbo la Isimani akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa Februari 19, 2015.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (kushoto) na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kiwere katika jimbo la Kalenga mkoani Iringa baada ya kuzindua nyumba za walimu shuleni hapo akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa Februari 19, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Airtel yamtangaza Bingwa wa Airtel Trace Music, yamzawadia milioni 50TZS

$
0
0
 Meneja Masoko wa Airtel Aneth Muga (kushoto) akimkabidhi
mshindi wa Airtel Trace Music Stars Nalimi Mayunga hundi ya mfano
yenye dhamani ya sh. 50mil baada ya kuibuka mshindi wa mashindano ya
Airtel Trace Music Stars, pia atapata fursa ya kwenda kuiwakilisha
nchi yetu katika mashindano ya Airtel Trace Stars ya Afrika
yatakayofanyika Mjini Nairobi Kenya mwezi machi,  anaeshuhudia ni
Afisa Uhusiano na matukio  wa Airtel Dangio Kaniki.

  Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Nalimi Mayunga akifurahia
zawadi yake baada ya kuibuka mshindi wa mashindano hayo yaliyofanyika
hivi karibuni. Mshindi huyo pia atapata fursa ya kwenda kuiwakilisha
Tanzania katika mashindano ya Airtel Trace Stars ya Afrika
yatakayofanyika Mjini Nairobi Kenya mwezi machi,

Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Nalimi Mayunga (kati)
akiwaimbia waandishi wa Habari (hawapo pichani) katika hafla ya
makabidhiano  ya zawadi yake hundi ya sh. Milioni 50 kushoto yake ni
Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki (kushoto)  na Meneja
Masoko wa Airtel Aneth Muga (kulia).


 ============   ======  ===========
Airtel yamtangaza Bingwa wa Airtel Trace Music, yamzawadia milioni 50TZS
*       Nyota wa Airtel Trace Music Stars apatikana
Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel leo imemtangaza rasmi mshindi wa
shindano la Airtel Trace Music star, shindano lilidumu kwa muda wa
miezi mitatu maalum kwa wasanii chipukizi kuweza  kuimba na kutuma
nyimbo zao kwa kutumia simu zao za mkononi kama studio kwa  lengo la
kusaka na kuibua vipaji kwa wanamuziki chipukizi nchini.

Akiongea na waandishi wa habari Meneja Masoko wa Airtel Aneth Muga
alisema"Leo tunayofuraha kubwa kumtangaza mshindi wetu wa shindano la
Airtel Trace Music Stars mara baada ya kuchaguliwa na majaji na
kupigiwa kura na watanzania.

"Washiriki watano ni kati ya wengi waliothubutu kuonyesha uwezo wao wa
kushiriki kwa kupiga simu, kuimba na kutuma nyimbo zao na hatimae
majaji wamesikiliza vipaji vyao kama walivyoimba na kuwachagua kuingia
tano bora (top 5)" alifafanua Muga.

Washiriki waliokuwa wamebahatika kuingia tano bora ni   Nalimi Mayunga
  mwenye namba ya ushiriki (55100182), Christopher Kihwele (5510050),
Tracy Eminence (55100420), Beautus Henry (55100106) na Rose Mbuya
(55100366).

Mshindi wetu ni Nalimi Mayunga mwenye namba ya ushiriki (55100182)
ambae amechaguliwa na majaji wetu pamoja na kupigiwa kura nyingi na
wananchi.

Zawadi yake ni milioni Tshs 50mil, na pia atapata fursa ya kwenda
kuiwakilisha nchi yetu katika mashindano ya Airtel Trace Stars ya
Afrika  Nairobi Kenya  yanayoshirikisha nchi 13 barani Afrika ambapo
pia mshindi atakaepatikana atarekodiwa nyimbo zake katika studio za
kimataifa nchini uingereza, na kupewa  mafunzo toka kwa msanii nguli
wa Afrika Akon.

Nchi nyingine zinazoshiriki mashindano haya na zitakazotoa jumla ya
vijana  13 barani Afrika ni pamoja na Kenya, Uganda Zambia,
Madagascar, Malawi, Nigeria, Ghana, Burkina Faso, Chad, Congo
Brazzaville, The Democratic Republic of Congo (DRC), na Gabon

VIONGOZI WAUWAGA MWILI WA MAREHEMU SALMIN AWADH SALMIN BARAZA LA WAWAKILISHI.

$
0
0
SIMA3  
Mwili wa Marehemu Salmin Awadh  ukiingizwa  katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani kwa ajili ya kuagwa rasmi.

  SIMA6SIMA7 
Naibu Katibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai  na Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni Mahmoud Muhammed wakibadilisha mawazo kuhusu msiba huo. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Waziri Mkuu mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Edward Lowasa akiingia katika ukumbi wa baraza la wawakilishi kuuwaga mwili wa aliekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Marehemu Salmin Awadh Salmin aliefariki ghafla jana. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).SIMA2Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na Makamu wa Pili wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakiingia katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi  kuuwaga mwili wa Marehemu Salimn Awadh.

 SIMA8 
Mamia ya wananchi waliohudhuria sala ya kumuombea Marehemu Salmin Awadh Salmin wakiutoa msikitini mwili wa marehemu kuelekea kijijini kwao Makunduchi kwa mazishi. SIMA9 
Msafara uliobeba mwili wa Marehemu Salmin ukiondoka Masjid Noor Muhammad (SAW) kuelekea Makunduchi kwa ajili ya mazishi. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

ASASI YA “AIDS – free” KUSAIDIA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI NDANI YA JESHI LA MAGEREZA

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akisisitiza jambo katika mazungumzo rasmi yaliyofanyika Ofsini kwake leo februari 20, 2015 kati ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza, Polisi na Wasimamizi Wakuu wa Mradi wa “AIDS – free” utakaotekelezwa ndani ya Jeshi la Magereza. mag3 
Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza walioshriki katika mazungumzo rasmi kuhusu Mradi wa “AIDS – free” unaotarajiwa kutekelezwa ndani ya Jeshi la Magereza(wa kwanza kulia) ni Kamishna Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(wa pili kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa pili kushoto) ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Gedion Nkana(wa kwanza kushoto) ni Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Nsajigwa Mwakenja. mag4 
Maofisa Wasimamizi wa Sekta ya Afya kutoka Jeshi la Polisi wakifuatilia mazungumzo rasmi kuhusu Mradi wa “AIDS – free”(wa kwanza kushoto) ni Dkt. Nyanda Lushina(katikati) ni Mrakibu wa Polisi, Husein Yahya.
mag5 
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(meza kuu) akiongoza mazungumzo rasmi yaliyofanyika Ofsini kwake leo februari 20, 2015 kati ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza na Wasimamizi Wakuu wa Mradi wa “AIDS – free” utakaotekelezwa ndani ya Jeshi la Magereza(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

SERIKALI KUAJIRI WALIMU 35,000 - WAZIRI MKUU

$
0
0
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali imepanga kuajiri walimu
zaidi ya 35,000 kwa ajili ya shule za sekondari ili kukabiliana na
tatizo la uhaba wa walimu nchini.

Ametoa kauli hiyo jana jioni (Alhamisi, Februari 19, 2015) wakati
akizungumza na mamia ya wakazi wa kata ya Kiwere, mara baada ya
kukagua ujenzi wa maabara na kuzindua nyumba nne za walimu kwenye
shule ya sekondari ya Kiwere, tarafa ya Kalenga, wilayani Iringa.

Waziri Mkuu alisema walimu hao watagawanywa kwenye shule kulingana na mahitaji yaliyokwishawasilishwa na kwamba watakapopata mgao wao hawana budi kuziangalia kwanza shule zenye miundombinu iliyokamilika kama ilivyo kwa shule hiyo.

Akifafanua kuhusu kasi ya ujenzi wa maabara Waziri Mkuu alisema: “Mkoa
mzima wa Iringa unahitaji kuwa na maabara 318 na zilizo tayari mpaka
sasa ni 108. Lakini kuna nyingine 141 ambazo zimekwishaanza kujengwa
na zimefikia hatua nzuri. Nimeambiwa katika muda mfupi ujao kutakuwa
na maabara 249 zilizokamilika,” alisema.

“RC inabidi uwasukume watu wako ili hizi 69 ambazo bado hazijaanza
kujengwa zikamilike kabla ya Juni mwaka huu kama ambavyo Mheshimiwa
Rais Jakaya Kikwete alikuwa ameelekeza. Alisema hataongeza tena muda
wa ujenzi,” aliongeza.

Alisema elimu ni sekta ya msingi ambayo Serikali imeamua kuipa umuhimu
wa kipekee na kuiweka katika moja ya maeneo sita muhimu ya kipaumbele
chini ya Mpango wa Matokeo Makubwa ya Haraka (BRN).

Waziri Mkuu aliwataka wanafunzi wa shule hiyo wasome kwa bidii na wawe
wasikivu ili waweze kufanya vizuri zaidi kwenye masomo yao.

Mapema, akitoa taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Afisa Elimu wa Wilaya ya
Iringa, Bw. Leonard Msigwa alisema ujenzi wa nyumba hizo nne ambazo
zina pande mbili (four duplex houses) umegharimu sh. milioni 323.2.
Alisema nyumba hizo zenye vyumba vitatu vya kulala, sebule na jiko,
zina uwezo wa kubeba familia nane.

Bw. Msigwa alisema ujenzi wa nyumba ulifanywa shirika la DESWOS la
Ujerumani kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa pamoja
na wananchi. Pia walisaidiwa kujengewa tenki la maji na mabweni mawili
yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 112 kila moja kwa ajili ya
wasichana.

Akifafanua kuhusu hali ya ujenzi wa maabara, Afisa Elimu huyo alisema
hadi sasa wamekamilisha ujenzi wa vyumba viwili vya Kemia na Baiolojia
lakini bado viko kwenye hatua ya kupaka rangi. Alisema mfumo wa gesi
na maji umekwishafungwa ndani ya vyumba vya maabara.

“Ujenzi wa maabara hadi sasa umekwishagharimu sh. milioni 52.8/- na
katika kipindi cha Februari 2015, tumefanikiwa kutengeneza baadhi ya
samani za maabara yaani meza 24 na stuli 96 zenye thamani ya sh.
8,940,000/-,” alisema.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, FEBRUARI 20, 2015.

FUTURE STARS KUSHIRIKI MICHUANO JIJINI KAMPALA

$
0
0


Kituo cha kukuza soka la vijana cha Future Stars Academy(FSA) cha jijini Arusha  kinataraji kushiriki  katika  michuano ya Uganda Junior League inayotaraji kutimua vumbi jijini Kampala mnamo Aprili 24 hadi 26 mwaka huu.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkurugenzi na mwanzilishi wa kituo hicho,Alfred  Itaeli alisema kuwa kituo chao kinataraji kupeleka timu ya watoto ya U-15 katika michuano hiyo kwa lengo la kushindana na kisha kunyakua ubingwa.


Alisema kuwa  ushiriki wao umefuatia kupitia mwaliko walioupata kutoka nchini Uganda kutokana na  nchi hiyo kutambua jitihada za kituo chao za kukuza soka la vijana hapa nchini pamoja na ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki.


Hatahivyo,mkurugenzi huyo alisisitiza ya kwamba katika kuhakikisha wanashriki mashindano hayo kituo chao kimeanza mkakati wa kusaka fedha za nauli na matumizi wakiwa nchini wakati wote wa mashindano kwa kusaka udhamini kutoka kwa wadu mbalimbali wa soka mkoani Arusha na nchini kwa ujumla.


Alisema kuwa wameanzisha tamasha la soka liitwalo “Quiz Night” ambalo linataraji kufanyika mnamo febuari 28 mwaka huu katika viwanja vya TGT jijini Arusha ambapo wanataraji kukusanya fedha za ushiriki katika tamasha hilo ili ziweze kuwasaidia katika safari yao nchini Uganda.


Itaeli,aliwataka wadau mbalimbali wa soka mkoani Arusha ana nchini kwa ujumla kuwapa sapoti katika safari yao kwa kuwa hadi sasa wamekusanya kiasi cha sh,2 milioni  ambapo kwa safari yote nchini humo kinahitajika kiasi cha sh,7 milioni. HABARI kwahisani ya libeneke la kaskazini blog

MWANAMITINDO TAUSI LIKOKOLA AWASILI NCHINI,ATOA CHANGAMOTO KWA WANAMITINDO NCHINI

$
0
0
 Mwanamitindo,Tausi Likokola akiwasili leo wa uwanja wa Ndege Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akitoke nchini Marekani kwa ziara ya siku 10 kushoto ni mama mdogo,Beatrice Likokola
 Mwanamitindo,Tausi Likokola akizungumza na waandishi habari (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere leo Jijini Dar es Salaam.
Mwanamitindo Tausi Likokola akishiriki kucheza ngoma ya asili ya kundi la wanne Star mara baada ya kuwasili wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere leo Jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka)
               
 Na Chalila Kibuda
Mwanamitindo wa Kimataifa (Mtanzania) aishiye Ughaibuni, Tausi Likokola amesema Watanzania wanajitahidi mno katika tasnia ya mitindo, hivyo wanatakiwa  kuwa na ubunifu wa  kipekee kutokana kuwepo kwa ushindani katika tasnia hiyo.
Tausi ameyasema hayo mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam,amesma kwa miaka aliyoishi katika nchi za Ujerumani na Marekani, kwa sasa ndio ameona watanzania wakionesha ubunifu wao  ni mwanzo mzuri na wanaweza kufika mbali.
Tausi amesema anatarajia kufanya ushiriki wa shughuli za kijamii, kwani ndio wajibu wake kama mwanamitindo kutokana na kuwa mchango wake unahitajika katika jamii zenye mahitaji maalum.
Katika ujio wa Mwanamitindo huyo,Tausi anatarajia kutembelea  shirika lisilo la Kiserikali linaloshughulikia  watu wanaoishi na virusi (WAMATA) kutokana na kuwasaidia kwa kila hatua pamoja na kuzuru visiwa vya Zanzibar.
‘’Nimekuja katika ziara yangu hii nitafanya masuala ya kijamii lakini na uzinduzi wa mafuta ya marashi hapa nchini na nimeona uzinduzi huu ni ufanyie nchini kwetu iwe ni fahari yangu’’amesema Tausi .
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live




Latest Images