Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWAJULIA HALI WANANCHI WALIOANGUKIWA NA NYUMBA ZAO KWA UPEPO NA MVUA KUBWA MSOGA.

$
0
0

LIB1 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete (wa pili kulia), Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli na baadhi ya Viongozi, wakati alipowasili Kitongoji cha Mnazi Mmoja, Msoga jana kwa ajili ya kuwafariji wananchi waliokubwa na maafa kwa kuangukiwa na nyumba zao kutokana na Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha juzi. Katika tukio hilo jumla ya watu 12 walijeruhiwa na jumla ya nyumba 128 kubomoka. Picha na OMR
LIB2 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete (kulia), wakati alipowasili Kitongoji cha Mnazi Mmoja, Msoga jana kwa ajili ya kuwafariji wananchi waliokubwa na maafa kwa kuangukiwa na nyumba zao kutokana na Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha juzi. Katika tukio hilo jumla ya watu 12 walijeruhiwa na jumla ya nyumba 128 kubomoka. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli (kulia) wakiongozwa na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete (wa pili kushoto),  baadhi ya Viongozi, wakati alipowasili Kitongoji cha Mnazi Mmoja, Msoga jana kwa ajili ya kuwafariji wananchi waliokubwa na maafa kwa kuangukiwa na nyumba zao kutokana na Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha juzi. Katika tukio hilo jumla ya watu 12 walijeruhiwa na jumla ya nyumba 128 kubomoka. Picha na OMR LIB4 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji Bi.Fatuma Janga na baadhi ya majeruhi wakati alipowatembelea jana Feb 17, 2014 baada ya kuangukiwa na nyumba zao kutokana na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha juzi kijijini  hapo. Picha na OMR

Ziara ya Waziri Simbachawene Mtwara na Lindi

$
0
0
chaw1 
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara, Alfred Luanda (aliyesimama), akiwasilisha taarifa fupi ya hali ya mmomonyoko wa ardhi uliosababisha mazingira ya hatari kwa Kiwanda cha kuchakata gesi asilia cha Maurel & Prom Tanzania (M&P), kilichopo Mnazi Bay – Mtwara. Wanaosikiliza ni Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa tatu kutoka Kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu (katikati), na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Nishati na Madini walioongozana na Waziri.
chaw5 
Sehemu ya Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara.
chaw6 
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, akikagua sehemu ya Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara wakati wa ziara aliyoifanya mwanzoni mwa wiki mkoani humo.
chaw7 
Matanki ya kuhifadhia maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali, yaliyopo katika eneo la Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara. Katika ziara yake mtamboni hapo, Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene aliagiza maji hayo yatumike pia kuwasaidia wananchi wanaoishi maeneo jirani.
chaw8 
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara wakati wa ziara yake Mtamboni hapo mwanzoni mwa wiki.

Baadhi ya Wafanyakazi/Vibarua katika Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara, wakiendelea na kazi wakati Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene alipofanya ziara kukagua maendeleo ya Mradi huo mwanzoni mwa wiki. chaw12 
Baadhi ya Wafanyakazi/Vibarua katika Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara, wakiendelea na kazi wakati Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene alipofanya ziara kukagua maendeleo ya Mradi huo mwanzoni mwa wiki.
Sehemu ya Mtambo wa kuchakata gesi wa Madimba mkoani Mtwara. chaw15 
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kulia) akijadili jambo na mmoja wa wasimamizi wa Mtambo wa kuchakata gesi wa Madimba – Mtwara, wakati wa ziara yake mwanzoni mwa wiki kukagua maendeleo ya Mradi.

Baadhi ya nyumba wanazoishi wafanyakazi wa Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara chaw3 
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa pili kutoka Kulia) akikagua nyumba za wafanyakazi wa Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara. Pamoja naye ni Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Bomba la gesi, Mhandisi Kapuulya Musomba (Kushoto – sambamba na Waziri) na Mkuu wa Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud (Kulia kwa Waziri.
chaw4Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Bomba la gesi, Mhandisi Kapuulya Musomba (kushoto), akifafanua jambo kwa Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa pili kutoka kushoto) wakati akikagua nyumba za wafanyakazi wa Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara.

…………………………………………………………………..

* Aahidi umeme kwa wana-MsimbatiNa Veronica SimbaWaziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene amefanya ziara mkoani Lindi na Mtwara mwanzoni mwa wiki kukagua miradi mbalimbali iliyo chini ya Wizara yake ambapo aliahidi huduma za umeme na maji kwa wananchi mbalimbali.
 Akiwa Madimba mkoani Mtwara, baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa mtambo wa kuchakata gesi, Waziri Simbachawene alimwagiza Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Bomba la gesi, Mhandisi Kapuulya Musomba kutoa huduma ya maji safi kwa wananchi wanaozunguka maeneo hayo.“Kutokana na taarifa yenu, mtakuwa na hifadhi ya maji ya kutosha hapa. Pamoja na matumizi yenu mbalimbali, hakikisheni mnatoa huduma ya maji kwa wananchi wanaozunguka mtambo,” alisema Waziri.
 Vilevile, Waziri Simbachawene alitoa ahadi ya umeme kwa Kijiji cha Luvula kilichoko Msimbati. Alisema Kijiji hicho na vingine 15 vilivyo jirani na Kiwanda cha kufua umeme cha Mnazibay, vitapatiwa umeme kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu.
 “Tunaendelea na zoezi la kusambaza umeme nchi nzima. Lengo letu ni kuhakikisha idadi ya watanzania wanaopata umeme inaongezeka zaidi na zaidi ili kuwezesha lengo la nchi yetu kufikia uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kama dira ya maendeleo inavyoonesha,” alisema.Ziara hiyo ya Waziri Simbachawene, ni ya kwanza kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara tangu aliposhika wadhifa wa Uwaziri wa Nishati na Madini, Januari mwaka huu.

Makamu wa Rais akagua mzani wa Kisasa wa Vigwaza na kufungua barabara ya Msoga – Msolwa km 10

$
0
0
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli kushoto akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal kuhusu Mzani wa kisasa wa Vigwaza uliopo Mkoani Pwani ambao umekamilika kwa asilimia 99.8.
Mzani wa Kisasa wa Vigwaza kama unavyoonekana. Mzani huu utapima magari kwa haraka zaidi kwa muda wa sekunde 30 kwa kila gari tofauti na mizani ya sasa inayotumia dakika moja na nusu mpaka mbili.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akihutubia wananchi katika Mzani wa Vigwaza mara baada ya kuukagua.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli pamoja na Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete, akikata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya Msoga-Msolwa km 10 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.
Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akizungumza mara baada ya kutoa pole kwa wananchi wa kijiji cha Msoga, Chalinze mkoani Pwani walioathirika na kimbunga kikali kilichosababisha kubomoka kwa nyumba zaidi ya 40 katika kijiji hicho pekee.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akicheza ngoma pamoja na kikundi cha ngoma cha Msoga kusherehekea ufunguzi wa barabara ya Msoga-Msolwa yenye urefu wa km 10. Barabara hiyo itapunguza msongamano wa magari katika eneo la Chalinze.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na watumishi wa TANROADS mara baada ya kukagua Mzani wa Vigwaza.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli kulia akisalimiana na Waziri wa Elimu ambaye pia ni Mbunge wa Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa kabla ya ukaguzi wa Mzani wa Vigwaza.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo akiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli wakielekea kwenda kumpokea Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal katika eneo la mzani wa Vigwaza mkoani Pwani. Picha zote kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini GCU-Wizara ya Ujenzi.

ZIARA YA WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI NCHINI SINGAPORE

$
0
0
Ujumbe wa NHC ulipokutana na baadhi ya wawekezaji wakubwa wa sekta ya uendelezaji Miliki wa Singapore ili kuwahamasisha kuwekeza vitega uchumi vya hoteli nchini Tanzania. Ujumbe huu umekutana na Bw. Henry Ngo ambaye ni Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bonvest na Hoteli ya Sheraton Singapore ambao pia wamewekeza Zanzibar Hoteli ya Kitalii.
NHC2 
Ujumbe wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa William Vangimembe Lukuvi ukiwa katika Mamlaka ya Uendelezaji wa nchi ya Singapore(Urban Redevelopment Authority –URA) kujionea namna mamlaka hiyo inavyoratibu ukuaji wa sekta ya nyumba kwa kuweka mipango madhubuti ya matumizi bora ya ardhi kulingana na mahitaji ya Taifa hilo linalotegemea zaidi utalii.
NHC3 
Mchoro unaoonyesha ramani ya nchi ya Singapore ulioko Makao Makuu ya Mamlaka ya Uendelezaji nchi hiyo ukionyesha majengo mbalimbali yaliyoko katika nchi hiyo yenye uhaba mkubwa wa ardhi.
NHC4 
Ujumbe wa Tanzania ukiangalia ramani yenye matumizi mbalimbali yaliyotengwa kwenye ardhi ya Taifa la Singapore. Katika nchi hiyo hakuna uwezekano wa mtu yeyote kuvamia kipande chochote cha ardhi kwa kuwa kila ardhi imepangiwa matumizi yake na kusimamiwa na sheria madhubuti.
NHC5 
Ujumbe wa Tanzania ukitizama maeneo yaliyoendelezwa yenye matumizi mbalimbali nchini Singapore kwenye jengo la makumbusho ya kihistoria ya hatua za ukuaji wa mji huo.
NHC6 
Kamishna wa Ardhi Dk Moses Kusiluka(kushoto)na watendaji wa NHC na Wizara wakipata maelezo kwa njia ya video ya namna mji wa Singapore ulivyopangwa kulingana na ardhi iliyopo na mahitaji ya Taifa hilo.
NHC7 
Ujumbe wa Tanzania ukiangalia kwa chini mchoro wenye ramani ya nchi ya Singapore na jinsi matumizi ya ardhi yanavyoratibiwa ulipotembelea Mamlaka ya Uendelezaji nchi ya Singapore jana.
NHC8 
Makamu wa Rais wa Shirika linalosimamia mipango Miji la Singapore Bw. Anandan Karunakaran(aliyeinama) akimueleza Waziri Lukuvi maeneo mapya yaliyotengwa kwa ajili ya uendelezaji mpya wa mji wa Singapore baada ya kufukia vipande vya bahari(land reclamation) ili kukidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye ya idadi ya watu wa nchi hiyo.

MAMILIONI YA DOLA YAIBIWA KATIKA MABENKI KUPITIA WIZI MTANDAO

$
0
0
Baada ya kikao kilichofanyika wiki iliyopita chuo kikuu cha Stafford ambapo Rais Obama wa marekani alikutana na wafanya biashara, Wanasheria na wasimamizi washeria kujadili hali ya mtikisiko wa maswala ya usalama mitandao, Inadhihirisha wazi bado kuna safari ndefu kukabiliana na wimbi hili la uhalifu mtandao duniani kote.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba Tishio la uhalifu mtandao na utayari wa kukabiliana nao bado kuna kutowiana ipasavyo ingawa jitihada bado ni kubwa kuweza kukabiliana na uhalifu huu unaokua kwa kasi ya pekee duniani kote.

Nategemewa kuwasilisha mada itakayoangazia jitihada za mataifa makubwa 8 dhidi ya uhalifu mtandao na athari za jitihada hizo kwa mataifa mengine katika mkutano wa mwaka utakaofanyika Nchini Croatia unaounganisha wataalam wa maswala ya usalama mitandao kutoka mataifa kadhaa ambapo patajadiliwa mambo kadhaa ya kiusalama mitandao – Taarifa Zaidi za mkutano zinaweza kupatikana kwa "KUBOFYA HAPA"
 
Wakati haya yakijiri na mikakati Zaidi ikiendelea ya kukabiliana na wimbi kubwa la uhalifu mtandao hivi sasa makampuni yanayojihusisha maswala ya fedha yameonekana yakiathirika Zaidi na uhalifu mtandao – Hii ni kwamujibu ya ripoti maalum iliyotolewa na kampuni ya Kaspersky Lab.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA KITAIFA KUHUSU WATOTO WALIO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizindua Vitabu vya Miongozi kuhusu huduma za Watoto walio katika Mazingira Hatarishi na Sheria ya Mtoto No, 21 ya mwaka 2009, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa kuhusu Watoto walio katika mazingira hatarishi, lililofanyika leo Feb. 18, 2015 kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha Vitabu vya Miongozi kuhusu huduma za Watoto walio katika Mazingira Hatarishi na Sheria ya Mtoto No, 21 ya mwaka 2009, baada ya kuzindua rasmi vitabu hivyo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa kuhusu Watoto walio katika mazingira hatarishi, lililofanyika leo Feb. 18, 2015 kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid (kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akimkabidhi Waziri wa Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia, Vitabu vya Miongozi kuhusu huduma za Watoto walio katika Mazingira Hatarishi na Sheria ya Mtoto No, 21 ya mwaka 2009, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa kuhusu Watoto walio katika mazingira hatarishi, lililofanyika leo Feb. 18, 2015 kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa dare s Salaam, Said Meck Sadik na Kulia kwa Makamu ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akimkabidhi Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia, Vitabu vya Miongozi kuhusu huduma za Watoto walio katika Mazingira Hatarishi na Sheria ya Mtoto No, 21 ya mwaka 2009, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa kuhusu Watoto walio katika mazingira hatarishi, lililofanyika leo Feb. 18, 2015 kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa dare s Salaam, Said Meck Sadik na Kulia kwa Makamu ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akimkabidhi Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Ummy Mwalimu, Vitabu vya Miongozi kuhusu huduma za Watoto walio katika Mazingira Hatarishi na Sheria ya Mtoto No, 21 ya mwaka 2009, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa kuhusu Watoto walio katika mazingira hatarishi, lililofanyika leo Feb. 18, 2015 kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa dare s Salaam, Said Meck Sadik na Kulia kwa Makamu ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na mwanafunzi, Zulfa Said, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa kuhusu Watoto walio katika mazingira hatarishi, lililofanyika leo Feb. 18, 2015 kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed  Gharib Bilal, akizungumza wakati akifungua rasmi Kongamano la Kitaifa kuhusu Watoto walio katika mazingira hatarishi, lililofanyika leo Feb. 18, 2015 kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Picha na OMR


  Baadhi ya wanafunzi waliowawakilisha wanafunzi wenzao katika Kongamano hilo, wakifuatilia kwa makini matukio yaliyokuwa yakiendelea ukumbni hapo.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Banana Zorro (kulia) na msanii wa maigizo, Angelina Leonard, na baadhi ya washiriki katika Kongamano hilo wakimsikiliza Makamu wa Rais wakati akihutubia.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi walioshiriki Kongamano hilo, baada ya ufunguzi.
 Mtoto Rahma Fadhili, mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya Sekondari ya Jitegemee, ambaye ni msanii wa kundi la sanaa la Mpoto Theatle, akiigiza kama Chokoraa aliyekataliwa na Baba mzazi jukwaani mbele ya mgeni rasmi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi.
 Wasani wa kundi la Sanaa la Mpoto Theatle, wakiigiza jukwaani kutoa ujumbe maalum kuhusu Kongamano hilo, la Kitaifa kuhusu Watoto walio katika mazingira hatarishi, lililofanyika leo Feb. 18, 2015 kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

 Msanii wa kundi la Mpoto Theatle, Angelina Leonard, akitoa ujumbe kuhusu unyanyasaji wa watoto wakati wa Kongamano hilo. Picha na OMR
Wasanii wa bendi ya B-Band, wakiongozwa na Banana Zorro ( wa pili kulia) wakitoa burudani wakati wa Kongamano hilo. Picha na OMR.

HOTUBA YA  MHE. DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL, MAKAMU WA RAIS WA  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,  KWENYE KONGAMANO LA KITAIFA KUHUSU WATOTO WALIO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI, UKUMBI WA MWL. JULIUS NYERERE,
DAR ES SALAAM,  TAREHE 18  FEBRUARI 2015


Mhe. Dkt. Seif Seleman Rashid (Mb)
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii;

Waheshimiwa Mawaziri mliopo;

Mhe. Said Mecky Sadick
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam;
Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali;

Waheshimiwa Mabalozi wa Nchi mbalimbali;

Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa;

Wawakilishi wa Wadau mbalimbali;

Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya;

Waheshimiwa Wakurugenzi wa Halmashauri;
Ndugu Wanahabari;

Ndugu Wananchi;

Wageni Waalikwa;

Mabibi na Mabwana.

Awali ya yote napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma kwa kutupa uzima na afya njema, na kuweza kukusanyika hapa katika Kongamano hili muhimu. Nitumie nafasi hii pia kukushukuru wewe binafsi Mhe. Dkt. Seif Seleman Rashid, na uongozi mzima wa Wizara wa Afya na Ustawi wa Jamii, kwa heshima kubwa mliyonipa, kunialika kufungua kongamano hili.

Mheshimiwa Waziri;
Shughuli ya leo ni muhimu na imekuja wakati muafaka kwa kuwa Taifa letu bado linakabiliwa na ongezeko la watoto walio katika mazingira hatarishi pamoja na matukio ya ukatili, unyanyasaji, utelekezaji na unyonyaji dhidi ya watoto. Hivyo tuna kila sababu kukaa na kuumiza vichwa, ili kupata namna bora ya kuondokana na matatizo haya katika jamii yetu.

Ndugu Washiriki wa Kongamano;
Mabibi na Mabwana;
Nchi yetu kama zilivyo nchi nyengine za Kusini mwa Jangwa la Sahara imeathiriwa kwa kiasi kikubwa na janga la UKIMWI, umaskini, migogoro ya kijamii, ukatili na unyanyasaji. Matatizo haya yamesababisha ongezeko kubwa la watoto walio katika mazingira hatarishi kutokana na kudhoofika kwa mifumo ya kijamii ya utoaji huduma katika ngazi ya familia. Taarifa za tafiti na chambuzi mbalimbali zinaonesha kwamba wapo watoto milioni 2.5 ambao ni yatima kutokana na janga la UKIMWI (TDHS 2010). Matokeo ya zoezi la utambuzi wa watoto walio katika mazingira hatarishi uliofanyika katika halmashauri 111, unaonesha kuwa wapo watoto 897,913 wakiwemo wasichana 422,019 na wavulana 475,894 wanaoishi katika mazingira hatarishi (Taarifa ya utambuzi hadi 2013).  

Vile vile Utafiti wa Hali ya Ukatili na Unyanyasaji (VAC 2009) uliofanyika Tanzania, umeonesha kuwa watoto watatu  kati ya 10 wa kike, na mtoto mmoja  kati ya saba  wa kiume, wamefanyiwa ukatili wa kingono kabla hawajafikisha umri wa miaka 18. Utafiti huo umeonesha pia robo ya watoto wote wa kiume na wa kike, wamefanyiwa ukatili wa kimwili kabla ya kufikisha umri wa miaka 18. Takwimu hizi zinatuonesha kwamba watoto wetu hawako katika hali ya usalama jambo linaloathiri makuzi na maendeleo yao na Taifa zima kwa ujumla  kwa sababu watoto ndio Taifa la kesho.

Ndugu Washiriki wa Kongamano;
Mabibi na Mabwana;
Hali ya watoto wetu nchini hairidhishi kwa kuwa watoto walio wengi na hasa wale walio katika mazingira hatarishi wanakumbwa na vidokezo vya hatari katika umri mdogo. Vidokezo hivyo ni pamoja na afya duni, lishe duni, malezi duni ndani ya familia au kaya, watoto kuishi na kufanya kazi mitaani, kukinzana na sheria, vitendo vya ukatili kama vile kubakwa, kupigwa, kutumikishwa nk. Watoto hawa wako katika hatari zaidi ya kuathirika katika makuzi yao kimwili kiakili na kisaikologia jambo ambalo si jema kwa maendeleo na maisha yao ya baadae. Vilevile watoto wengine  wanapoteza maisha na wengine wanapata ulemavu wa kudumu, kwa mfano wale wanokatwa sehemu za viungo vyao kutokana na imani potofu zilizopo katika jamii. Nafarijika sana kuona kwamba mmetambua umuhimu wa kuwashirikisha watoto katika Kongamano hili ili wao wenyewe waweze kuzungumza yale yanayowasibu. Rai yangu ni kwamba, ujumbe utakaowasilishwa na watoto hawa, upewe kipaumbele na mapendekezo yao, yaingizwe katika mikakati ya utekelezaji wa mpango huu.

Ndugu  Washiriki;
Mabibi na Mabwana;
Serikali yenu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imefanya jitihada kubwa katika kukabiliana na hali ya ongezeko la watoto walio katika mazingira hatarishi pamoja na matukio ya ukatili na unyanyasaji wa watoto. Hata hivyo utekelezaji wa jambo lolote haukosi changamoto. Nimearifiwa kwamba zipo changamoto kadhaa zinazokabili utekelezaji wa mradi huu  ambazo ni; Uhaba wa rasilimali, Jamii kutoona umuhimu wa kusaidia malezi, Matunzo na ulinzi kwa watoto walio katika mazingira hatarishi, Kiwango cha umaskini katika ngazi ya familia/kaya, Majanga mbalimbali ukiwemo UKIMWI, Wazazi kutengana na kuvunjika kwa ndoa pamoja na baadhi ya mila na desturi zenye madhara. Yote haya yamesababisha kuwepo ongezeko la watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na matukio ya unyanyasaji na ukatili kwa ya watoto.

Ndugu Washiriki;
Mabibi na Mabwana;
Wito wangu katika kukabiliana na changamoto hizi, nawaomba wadau mbalimbali waendelee kushirikiana na kusaidia Serikali katika kuandaa na kutekeleza miradi mbalimbali ya Malezi, Matunzo, Ulinzi na Usalama kwa watoto.  Nitumie nafasi hii pia, kupongeza mashirika na taasisi ambazo kwa njia moja ama nyingine, zimekuwa mstari wa mbele kusaidia miradi mbalimbali ya kuboresha maisha ya watoto wetu. Kipekee, napenda kushukuru mashirika yafuatayo kwa misaada yake mbalimbali ikiwemo ya fedha na utaalamu. Mashirika hayo ni pamoja na; Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Masuala ya Wanawake (UN Women), Shirika la Misaada la Watu wa Marekani (USAID), Abbot Fund, Save the Children, Plan International, World Vision, European Union, Catholic Relief Service pamoja na wadau wengine wote ambao wanashirikiana na Serikali katika kutekeleza mipango mbalimbali ya kuwahudumia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi tangu mwaka 2000. Napenda pia kuwapongeza Viongozi na watendaji katika halmashauri zote za Tanzania Bara kwa kazi wanayoifanya ya usimamizi na utekelezaji wa Mpango wa Huduma kwa Watoto Walio Katika Mazingira Hatarishi. Hongereni sana, ongezeni bidii, msirudi nyuma. 

Ndugu Washiriki;
Mabibi na Mabwana;
Naamini kwamba tumekusanyika pamoja katika Kongamano hili ili kuweza kutafakari kwa pamoja hali ya watoto walio katika mazingira hatarishi hapa nchini. Hivyo mijadala yenu katika siku tatu hizi ichambue na kuangalia mambo yafuatayo;
1.       Majukumu ya kila mmoja wenu katika kuboresha hali ya
          malezi, matunzo na ulinzi kwa watoto hao,
2.       Hali ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Watoto
          Walio katika Mazingira Hatarishi (2013 – 2017) na namna
          ya kukabiliana na changamoto zinazojitokeza,
3.       Kutumia vyombo vya habari katika kutoa hamasa na
mafunzo kwa umma juu ya umuhimu wa malezi na ulinzi wa watoto,
4.       Kuandaa mikakati endelevu ya kuimarisha upatikanaji wa rasilimali kwa ajili ya huduma kwa watoto walio katika mazingira hatarishi, na
5.       Uimarishaji wa mifumo ya ulinzi na usalama kwa watoto.

Ndugu Washiriki wa Kongamano;
Mabibi na Mabwana;
Kongamano la leo litupe fursa ya kutambua kwamba jukumu la kulea, kutunza na kulinda watoto wetu ni letu sote, hivyo kila mmoja wetu anapaswa kuendelea kutekeleza wajibu huu muhimu kwa kasi zaidi na kuhakikisha kuwa masuala ya watoto hawa, yanapewa kipaumbele na kuingizwa katika mipango ya maendeleo katika ngazi zote. Ni imani yangu kwamba washirika wetu wa maendeleo, watazidi kuunga mkono juhudi zetu za kuboresha maisha ya watoto walio katika mazingira hatarishi. Napenda pia niwakumbushe  viongozi wa wizara mbalimbali kwamba tunao wajibu wa kutekeleza matamko tuliyojiwekea wakati wa Uzinduzi wa Mpango Kazi wa Pili wa kitaifa wa Huduma kwa Watoto Walio katika Mazingira Hatarishi na Uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Hali ya Ukatili na Unyanyasaji kwa Watoto nchini.

Ndugu Washiriki wa Kongamano;
Ndugu Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Kwa kuhitimisha hotuba yangu, natoa wito kwa wananchi wote kila mmoja wetu awajibike ipasavyo katika suala zima la kulea na kutunza watoto wetu ipasavyo. Sisi sote tuna jukumu la kuhakikisha kwamba watoto wetu wanaishi katika hali ya usalama na wanalelewa na kukuzwa katika maadili mema.

Baada ya kusema hayo, kwa heshima kubwa na taadhima natamka kwamba; Kongamano la Kitaifa la Watoto Walio Katika Mazingira Hatarishi,  limefunguliwa rasmi.
Nawatakia majadiliano mema. Tuwajibike Kuwalinda Watoto Wetu
Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.

UN YATAKA JUHUDI ZAIDI KUKABILI MAUAJI YA ALBINO

$
0
0
DSC_0233
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza na binti wa miaka 19 ambaye ni mlemavu wa ngozi na kutosikia, Masalu Masuka ambaye anaishi katika kituo cha watoto walemavu cha Buhangija baada ya kukimbia kwao Bariadi kukwepa wauaji wa albino. Binti huyo alijifungua mtoto wake akiwa kituoni hapo bila msaada wa muuguzi.

MRATIBU wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, na Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Maendeleo la umoja huo (UNDP), Alvaro Rodriguez amehimiza serikali kuchukua hatua zaidi kukabili mauaji ya watu wenye albinism.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo kufuatia taarifa ya kutekwa na kuuawa kwa binti mwenye albinism wa umri wa mwaka mmoja, Yohana Bahati, alisema pamoja na juhudi zilizopo sasa za kukabili mauaji dhidi ya watu wenye albinism lazima ziongezwe.
Maiti ya Yohana Bahati (1) aliyetekwa Februri 15 mwaka huu imekutwa katika kijiji cha Shilabela Mapinduzi , kilomita chache kutoka nyumbani kwao Ilelema.

Mwili huo umekutwa na polisi katika hifadhi ya Biharamulo jana Februari 17, 2015 majira ya saa 9 alasiri huku ikiwa imenyofolewa miguu na mikono. Mama yake, Ester Jonas (30) bado hoi hospitalini Bugando akitibiwa majeraha yaliyotokana na mapanga wakati akijaribu kumuokoa mtoto wake.
DSC_0386
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiwa amembeba mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Ghoke Maliwa anayelelewa kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga alipofanya ziara ya kukitembelea kituo hicho hivi karibuni mkoani humo.

Aidha dada yake Tabu bahati (3) bado yuko katika ulinzi wa polisi wakati dada yao mkubwa Shida Bahati (12) akiwa kwa ndugu zake kijiji kingine. Alisema katika taarifa yake kwamba katika kipindi cha miezi miwili Tanzania imeshuhudia kutekwa nyara kwa watoto wawili katika kanda ya ziwa. Desemba mwaka jana mtoto Pendo alitekwa na kusababisha kizaazaa kikubwa lakini pamoja na juhudi za kumtafuta mtoto huyo mpaka leo hajulikani alipo.


Taarifa hiyo imesema kwamba Umoja wa Mataifa unasikitishwa na vitendo hivyo vya kikatili dhidi ya watoto hao wawili. Mashambulio dhidi ya watu wenye albinism yanaelezwa kuwa yanasababishwa na imani za kishirikina na kwamba kutoka mwaka 2000 hadi sasa watu wenye albinism 74 wameshauawa.

“ Mashambulizi haya yanaambatana na ukatili mkubwa, na wakati serikali inafanya kila juhudi kukabili tatizo hili, juhudi kubwa zinastahili kufanywa ili kukomesha mauaji na kulinda kundi hilo dogo la watu ambao wako katika hatari kubwa “ inasema sehemu ya taarifa hiyo.
DSC_0351
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisoma ujumbe unaosema “DREAM BIG” kwenye T-shirt ya mtoto Agnes Kabika mwenye ulemavu wa ngozi anayelelewa kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi alipofanya ziara ya kutembelea kituo hicho hivi karibuni.

Umoja wa Mataifa umesema kwamba mashambulio dhidi ya albino hayavumiliki, si halali kwa namna yoyote na yanaweza kukomeshwa. Wakati taifa hili linaelekea katika uchaguzi, yapo madai kuwa maisha ya watu wenye albinism wako katika hatari kubwa. Mratibu huyo amesema kwamba pamoja na kupongeza juhudi za serikali katika kukabiliana na wimbi hilo la mauaji hayo, Umoja wa Mataifa unataka Mamlaka husika kuhakikisha haki za raia zinalindwa na utawala wa sheria unazingatiwa.

“ Tunataka mwaka 2015 kuwa mwaka ambapo haki za Watanzania wote zitaheshimiwa wakiwemo albino” Taarifa imesisitiza. Mratibu huyo wa umoja wa Mataifa amesema kwamba amezungumza na Mkuu wa Mkoa wa Geita Fatma Mwassa na chama cha Maalbino nchini TAS.

Amesema Mkuu huyo wa mkoa alimhakikishia kwamba wanafanya kila linalowezekana kukomesha madhila dhidi ya maalbino, huku TAS ikitaka kuhakikisha kwamba huu ni mwaka wa kukomesha mauaji. Aidha Mratibu wa The Same Sun (UTSS) nchini, Vicky Ntetema, amemweleza mratibu huyo wa Umoja wa Mataifa mashaka yake wakati taifa linaelekea katika uchaguzi mkuu.

Wasanii wa Filamu Nchini watakiwa kutokuwa makontena ya biashara haramu

$
0
0
 Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fisoo akizungumza na wasanii wa bongo movie wanaotarajia kwenda nchini Uingereza kurekodi filamu na kampuni ya Didas Entertainment iliyopo nchini Uingereza. Kulia ni Mama wa Didas Bi. Nuru Idrisa  
 Kutoka kulia Msanii Yusuph Mllela, Afisa kutoka Bodi ya Filamu Bibi Beatrice Msumari, Msanii Esha Buhet na Msanii Husna Athumani wakimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu walipofika ofisini kwake kwa ajili ya kuwaaga wasanii hao wanaotarajia kwenda nchini Uingereza kurekodi filamu na kampuni ya Didas Entertainment.
 Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fisoo kulia akimpa mkono msanii Yusuph Mllela baada ya neno la kuwaaga wasanii watatu (Yusuph Mllela, Esha Buhet na Husna Athumani) wanaotarajia kwenda nchini Uingereza kurekodi filamu na kampuni ya Didas Entertainment.
 Msanii wa Bongo Movie Bi. Esha Buhet kushoto akifurahi wakati wa kuagana na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fisoo kwa ajili ya kuanza safari ya kwenda nchini Uingereza kurekodi filamu na kampuni ya Didas Entertainment. Katikati ni Mama wa Didas Bi. Nuru Idrisa.
Msanii Husna Athumani akipokea mkono wa pongezi kutoka kwa Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fisoo (kulia) wakati wa kuwaaga wasania wanaotarajia kwenda nchini Uingereza kurekodi filamu na Kampuni ya Didas Entertainment. Katikati ni Mama wa Didas Bi. Nuru Idrisa.          (Picha zote na: Genofeva Matemu – Maelezo)         

MAANDALIZI YA MIAKA 15 YA TAMASHA LA PASAKA,BAISKELI 100 KUTOLEWA KWA WALEMAVU MIKOA KUMI

$
0
0

 
Msama ameongeza kuwa hivi sasa wako katika mazungumzo na waimbaji wa muziki wa injili kutoka nje ya nchi hasa kule Afrika Kusini na Uingereza, waimbaji ambao wako katika mazungumza na kampuni ya Msama Promotion ni Solomon Mahlangu, Rebecca Malope, Keke Pofolo na wengine wote kutoka nchini Afrika Kusini.

Msama alisema kuwa idadi ya mikoa ambayo imeomba iandae onesho la miaka 15 ya Tamasha la Pasaka sasa imefikia 17,amesema Tamasha la Pasaka kwa mwaka huu litakuwa la aina yake tangu walipoanzisha tamasha lao mwaka 2000.
 
“Tumepokea maombi ya wadau kutoka mikoa 17 wakitaka tupeleke Tamasha la Pasaka mikoani kwao. Tunachofanya kwenye kamati yangu ni kupokea maoni kwa njia mbalimbali kwa wadau wetu wa huko.
 
 “Lakini si kupendekezwa au kuombwa tu na wadau ndiyo kigezo cha kupewa nafasi, lazima tuangalie na mazingira ya mkoa husika katika mambo ya matamasha,” alisema Msama.Aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Morogoro, Rukwa,  Mara, Singida, Arusha, Ruvuma, Mbeya, Iringa, Tanga, Dar s Salaam, Mtwara, Mwanza, Dodoma, Tabora, Shinyanga, Kilimanjaro na Zanzibar.
 
 Alisema kamati yake inatarajia kukutana Jumatano wiki hii na kufanya tathmini ya maombi kwa wadau wao wa maeneo hayo ili kupata mikoa sahihi ambayo tamasha hilo litafanyika mwaka huu.
 
Tamasha la Pasaka linaandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es Salaam, ambayo pia huandaa Tamasha la Krismas kila mwaka, lakini wanataka Tamasha la Pasaka mwaka huu liwe bora zaidi kwa sababu wanasherehekea miaka 15 tangu waanzishe tamasha hilo.

Vijana wilayani Kasulu wapewa somo kuhusu fursa za Mfuko wa Maendeleo ya Vijana

$
0
0

kas1 
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mhe. Dani Makanga (watatu kutoka kulia kabla ya mabadiliko) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo walipomtembelea ofisini kwake leo. Kutoka kulia ni Afisa Utamaduni na Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Bw. Mbogo, Afisa Vijana kutoka Wizara ya
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mhe. Dani Makanga akizungumza na wajumbe kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo waliofika ofsini kwake kwa ajili ya kujitambulisha kabla ya kuendelea na ratiba yao ya mafunzo kwa Vijana wa Halmashauri za Kasulu na Bihigwe leo mjini Kasulu. Katikati ni Mkuu wa msafara huo ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa na wa kwanza kushoto ni Afisa Vijana wa wizara hiyo Bi. Amina Sanga. kas3 
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Bw. Bernard Ntikabuze (kushoto) akiagana na akipeana mkono na Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga wakati walipotembelea ofisini kwa Mkurugenzi huyo leo. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa.
kas4 
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu Bw. Muguha Titus Muguha akizungumza na Vijana wanaoshiriki mafunzo kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (hawapo pichani) yanayotolewa na wataalamu kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Kutoka kulia ni Afisa Vijana wa Wizara hiyo Bi. Amina Sanga, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria Bibi. Esther Riwa, Mkuu wa Kituo cha Maendeleo ya Vijana Sasanda kilichopo Mbeya Bw. Laurian Massele na Afisa Vijana wa Mkoa wa Kigoma Bw. Edward Manase
kas5 
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa akitoa mada kuhusu Sera ya Maendeleo ya Vijana na Stadi za Maisha kwa baadhi ya Vijana wa Halmashauri za Kasulu na Buhigwe leo katika Ukumbi wa Kituo cha Utamaduni Wilayani Kasulu.
kas6 
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa akitoa mada kuhusu Sera ya Maendeleo ya Vijana na Stadi za Maisha kwa baadhi ya Vijana wa Halmashauri za Kasulu na Buhigwe leo katika Ukumbi wa Kituo cha Utamaduni Wilayani Kasulu.
Baadhi ya Vijana wakifuatilia mada zilizokuwa zilizokuwa zikiwasilishwa na Mkuu Mkuu wa Kitengo cha Sheria Kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa haypo pichana leo mjini Kasulu. kas8 
Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga akitoa maada kuhusu Mwongozo wa Mkopo wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo Wilayani Kasulu wakati wa mafunzo kwa Vijana wa Halmashauri za Kasulu na Buhigwe.Jumla ya Vijana 66 wamehudhuria mafunzo hayo.
kas9 
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Bw. Bernard Ntikabuze akizungumza na ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo walipofika ofisini kwake ili kujitambulisha kabla ya kuendelea na ratiba ya mafunzo na ukaguzi wa miradi Wilayani hapo leo.

Rais Kikwete apokea hati za utambulisho kutoka Malawi,Kuwait.Afrika ya Kusini na Kenya

$
0
0
1
Baliozi mpya wa Malawi nchini Tanzania Mhe. Hawa Ndilowe akiwasilisha kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete hati za Utambulisho ikulu jijini Dar es Salaam Februari 18, 2015.Katikati anayeshuhudia ni Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage Juma.
2
Balozi Ndilowe akiwa katika picha na Rais Kikwete na kufanya naye mazungumzo baada ya kuwasilisha hati za utambulisho.
3
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Baliozi mpya wa Malawi nchini Tanzania Mhe. Hawa Ndilowemara mara baada ya kuwakilisha hati za Utambulisho.
4
Balozi mpya wa Kuwaiti nchini Tanzania Mhe.Jasem Ibrahim Al-Najem akiwasilisha kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete hati za utambulisho ikulu jijini Dar es Salaam Februari 18, 2015.
5
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania akiwa katika picha na Rais Dkt.Jakaya Kikwete.
6
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania na Rais Dkt.Jakaya Kikwete.wakiwa katika mazungumzo baada ya kuwasilisha hati za utambulisho.
7
Balozi Mpya wa Afrika ya Kusini nchini Tanzania Mhe.Thamsanqa Dennis Mseleku akiwasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo. Katikati anayeshuhudia ni Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage Juma.
8
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na balozi mpya wa Afrika ya Kusini nchini Tanzania Thamsanqa Dennis Mseleku baada ya kuwasilisha hati zake za utambulisho na kufanya naye mazungumzo.
910
Balozi Mpya wa Kenya nchini Tanzania Mhe.Chirau Ali Mwakwere akiwasilisha Kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete hati zake za utambulisho ikulu jijini Dar es Salaam leo. . Katikati anayeshuhudia ni Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage Juma.
.1111
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na balozi mpya wa Kenya nchini Tanzania Chirau Ali Mwakwere wakikumbatiana na kwa furaha muda mfupi baada ya balozi huyo kuwasilisha hati zake za utambulisho ikulu jijini Dar es Salaam leo. (picha zote na Freddy Maro)

Mfumo wa Mtandao wa Upatikanaji Taarifa za Ardhi Zanzibar wazinduliwa

$
0
0
3
Mgeni rasmi katika Uzinduzi huo Balozi Antilla akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mfumo wa Mtandao wa Upatikanaji Taarifa za Ardhi Zanzibar.
4
Wa Tatu (Kulia) ni Meneja wa mradi wa ZALIS Nd. Moh’d Zahran akitoa maelezo ya kitaalamu kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi (Kulia) na Mgeni rasmi Balozi Antilla wa (Katikati). 
1
Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Zanzibar. Ali Khalid Mirza akiwasilisha Hotuba yake kwa mgeni rasmi Balozi wa Finland nchini Tanzania Bi Sinnika Antilla (Kulia) katika Uzinduzi wa Mfumo wa Mtandao wa Upatikanaji Taarifa za Ardhi Zanzibar unaojulikana kama (Zanzibar Land Information Service) (ZALIS) uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Ardhi iliyoko Forodhani Mjini Zanzibar.
2
Kulia ni mgeni rasmi wa Uzinduzi huo Balozi wa Finland nchini Tanzania Bi Sinnika Antilla akiwasilisha hotuba yake kwa katibu mkuu wa Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati (Kushoto) wakati wa uzinduzi huo.

5
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi akiwa katika Mkutano na Vyombo vya Habari mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi huo.
…………………………………………………………………………….
(Picha na Miza Othman Maelezo-Zanzibar)
Balozi wa Finland nchini Tanzania Bi Sinnika Antilla amesema Zanzibar itaondokana na umasikini pindi itakua na utekelezaji juu ya Sera ya Utunzaji na Utumiaji mzuri wa Ardhi.
 Hayo ameyaeleza katika ukumbi wa Idara ya Ardhi iliyoko Forodhani Mjini Zanzibar wakati wa Uzinduzi wa Mfumo wa Mtandao wa Upatikanaji Taarifa za Ardhi Zanzibar unaojulikana kama (Zanzibar Land Information Service) (ZALIS).  Amesema huo utakuwa na lengo la kushughulikia changamoto za Ardhi na kuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi kwa kuweka sera nzuri za mazingira nchini Zanzibar.
 Aidha amefahamisha kuwa ZALIS ina lengo la kuhakikisha kuwa Ardhi inatumika vizuri pamoja na kuwepo uongozi ulio bora wa Ardhi nchini Zanzibar ili ije iwe ni urithi mzuri na wenye manufaa kwa vizazi vijavyo.Balozi Antilla ameipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuanzisha Mtandao wa Serikali (E-Government) uliorahisisha kufanikiwa kwa mradi huo pamoja na kuushukuru uongozi wa Idara ya Ardhi kwa ushirikiano wao katika kufanikisha mradi huo wenye malengo makubwa ya kijamii na kiuchumi kwa nchi hizo mbili.
 Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Zanzibar Nd. Ali Khalid Mirza amesema mradi wa ZALIS umepelekea kuwepo kwa matumizi mazuri ya maliasili hususan Ardhi na Misitu ambapo hadi sasa zaidi ya 40% ya Ardhi ya Zanzibar imefanyiwa usajili na asilimia zaidi ya 30% ya Ardhi hiyo inatumika kwa ajili ya kilimo jambo ambalo limeimarisha kilimo na kupelekea kukua kwa kiasi kikubwa uchumi wa wananchi wa Zanzibar.

Amefahamisha kuwa mradi wa mtandao huo utasaidia kutunza kumbukumbu kwa njia iliyo salama ya mtandao na kuepusha kupotea kwa taarifa za wateja pamoja na kuwataka watendaji wa Idara hiyo kuwapa elimu wananchi wasio na uelewa juu ya matumizi na umuhimu wa mtandao huo.Ametanabahisha kuwa kuna changamoto nyingi zinazoikabili idara hiyo wakati wa usajili ikiwemo baadhi ya wananchi kutokuwa na vyeti vya kuzaliwa pamoja na baadhi ya Ardhi kuwa na migogoro ya mirathi hivyo kushindwa kuzifanyia usajili kwa wakati. 
 Amesema usajili wa Ardhi ulianza mnamo mwaka 2013 ukianzia na Mji Mkongwe, Mikoroshoni, Miembeni na maeneo mengine mbalimbali Unguja na Pemba na hadi sasa bado unaendelea hivyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo ili kuzifanya Ardhi zao kuwa katika hali ya usalama kutokana na Dhulma na Wizi jambo ambalo kwa sasa limekithiri kwa kiasi kikubwa nchini.

RED CUP PARTY ZANZIBAR NDANI YA PALM BEACH BWEJUU FEB 28

$
0
0
RCP 
Ile party ya kijanja inayosubiriwa kwa hamu kubwa na watu mbalimbali wa ndani na nje ya Zanzibar Maarufu kama ‘RED CUP Party’ kufanyika Februari 28 ndani ya Hoteli ya Palm Beach iliyopo Bwejuu, Unguja.

Akielezea mwandaaji wa shoo hiyo ya kijanja, Djzoro ON Mix Man amesema tayari mipango yote imekamilika na tiketi zimeanza kuuzwa kwa sasa. “Party ya kijanja ya RED CUP Party, kwa sasa ni gumzo na tiketi zimeshaanza kuuzwa. Kwa kiingilio cha sh 10,000/= kwa wanaume na sh 5000/=, kwa wanawake. Pia kwa wanaotaka tiketi wanaweza kuwasiliana kupitia simu namba 0658775755.” Alibainisha Djzoro ON Mix Man
10982328_795315397225783_1381477172125504952_o 
Djzoro ON Mix Man aliongeza kuwa, Party hiyo inayotarajiwa kufanyika katika hoteli ya Palm Beach iliyopo Bwejuu nje ya mji wa Unguja. Wameandaa magari yatakayoondokea Ngome Kongwe majira ya saa 6. Ambapo pia, kama utakuja na usafiri wako mlangoni kwenye shoo, kiingilio kitakuwa sh elf 5 tu sambamba na michezo mbali mbali pamoja na swimming pool.

“Hii shoo ni ya aina yake kwani ni Kimataifa, tayari set up ya swimming pool ipo tayari kwajili ya REDCUP na usiku zitawaka taa mbali mbali za kupendeza. Jipange kwa kingilio cha elf 5 mlangon au kwa bus kubwa kutoka NGOME KONGWE mpaka PALM BEACH na shiling elf 10 kwa wanaume na elf 5 kwa wanawake karibu sana” alisema. Djzoro ON Mix Man.
Eneo litakalofanyika Red Cup Party 
Eneo litakalofanyika Red Cup Party.
tiketi zipo tayari 
Tiketi zipo tayari.

TBL YAKABIDHI MSAADA WA KISIMA CHA MAJI JIMBO LA MPENDAE,ZANZIBAR

$
0
0
 Mwakilishi wa Jimbo la Mpendae, Said Mohammed Dimwa akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kisima cha maji kwa wananchi wa Mpendae kilichochimbwa kwa udhamini wa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Wa pili kulia ni Meneja Uhusiano wa TBL, Doris Malulu.
Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),  Doris Malulu akigongeana glasi za maji na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mpendae baada ya uzinduzi wa kisima kilichochimbwa kwa msaada na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),  katika Jimbo hilo. Haflahiyo ilifanyika  Zanzibar, mwishoni mwa wiki.
 Mwakilishi wa Jimbo la Mpendae, Zanzibar, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Uvuvi na Misitu,  Mohammed Dimwa akimshukuru Ofisa Uhusiano wa TBL, Doris Malulu baada ya kisima cha maji kilichochimbwa kwa msaada na TBL,  katika Jimbo hilo. Hafla hiyo Zanzibar, mwishoni mwa wiki.
 Mwakilishi wa Jimbo la Mpendae na Naibu Waziri wa Uvuvi na Misitu, Said Mohammed Dimwa akimtwisha ndoo ya maji mama mkazi wa Jimbo la Mpendae, Zanzibar baada ya uzinduzi wa kisima cha maji kilichochimbwa jimbo humo kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Kisima hicho kilizinduliwa mwishoni mwa wiki.
Wageni waalikwa wakinywa maji  baada ya Mwakilishi wa Jimbo la Mpendae, Mohammed Dimwa kuzindua kisima cha maji kilichochimbwa kwa msaada na Kampuni ya Tanzania (TBL),  katika Jimbo hilo. Hafla hiyo ilifanyika  Zanzibar, mwishoni mwa wiki.

MAKALA YA SHERIA: MFANO WA JINSI WOSIA UNAVYOKUWA/UNAVYOANDIKWA.

$
0
0


Wapo watu ambao shida yao ni kuandaa wosia lakini tatizo ni waanzeje. Je waandike kama barua, je waandike kama makala, je waandike kama maombi ya zabuni, je waandike kama notisi, waandikeje hasa. 

Wapo watu ambao wameshaandika wosia lakini wameandika hovyohovyo tu bila mpangilio maalum. Ikumbukwe kuwa wosia mbovu usio katika taratibu na mpangilio wa kisheria ni wosia ambao baada ya kufa kwako unaweza kuleta ugomvi mkubwa na hatimaye inaweza kuamuliwa kuwa wosia huo si halali hata kama ni kweli uliuandika na hivyo kusababisha yale yote uliyotaka yafanyike baada ya kufa kwako yasifanyike. 

Aidha hili ni tatizo ambalo makala haya yaweza kusaidia kulimalia kwa atakayesoma. Mfano huu au sample hii hapa chini ni ya kitaalam na ya kisheria hivyo mtu anaweza kuinakili hivihivi ilivyo na akaitumia kuandalia wosia wake.

Kusoma zaidi BOFYA HAPA

HII HAPA ORODHA KAMILI YA MABADILIKO YA WAKUU WA WILAYA WALIOTEULIWA LEO NA RAIS KIKWETE

JIPATIE NAKALA YAKO YA GAZETI LA UWAZI MIZENGWE YA UCHAGUZI KILA IJUMAA

MWANZA KU-JEMBEKA NA SAUTI SOL JUMAMOSI HII FEB 21 NDANI YA JEMBE BEACH

$
0
0
Hatimaye ule mpango mzima wa kuzifungulia burudani ulioasisiwa na redio mpya ya jijini Mwanza JEMBE FM na kubatizwa jina 'JEMBEKA' unaanza rasmi jumamosi ya wiki hii tarehe 21/02/2015 ndani ya kiota cha burudani cha kitalii Jembe Beach Mwanza.

Burudani itakayo fungua mpango huo wa 'JEMBEKA' ni kutoka kwa kundi maarufu Afrika Mashariki lililovuka mipaka na sasa muziki wake kuchezwa hadi barani Ulaya kundi la Sauti Sol toka nchini Kenya ambao watapiga muziki LIVE.

Vijana wa Nyumbani JJ Band nao watakuwepo ndani ya Jembe Beach Resort kwaajili ya kumwaga burudani ya kijanja zaidi ya vile ulivyowazoea.
Kiingilio ni shilingi 10,000/= kwa tiketi za awali na Tshs 15,000/= ukinunua getini.

Tiketi zinapatikana ofisi za Jembe Fm zilizopo PPF Plaza Mwanza.
Ni chini ya udhamini wa K Vant Gin, Coca cola, ikiwezeshwa na Jembe ni Jembe, Jembe Fm, Jembe Djz na G.SENGO BLOG.

WAZIRI MKUU PINDA AANZA ZIARA YA MKOA WA IRINGA

$
0
0
1
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza  baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Nduli kuanza ziara ya kikazi mkoani Iringa Februari 18, 2015
2
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama ngoma  ya kikundi cha Mangala  baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Nduli kuanza ziara ya kikazi mkoani Iringa Februari 18, 2015.
3
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na viongozi wa mkoa wa Iringa baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Nduli kuanza ziara ya kikazi mkoan Iringa Februari 18, 2015.
5
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua maabara ya Chuo Kukuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa wakati alipotembelea Chuo hicho akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa Februari 18, 2015. Kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Profesa Rwekaza Mkadala.
6
Waziri Mkuu, Mizengo  Pinda akimsikiliza Mtalaamu wa Mifumo ya computer wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa, Ibrahimu Mwahu wakati alipokagua maabara ya chuo hicho akiwa katika zaiara ya mkoa wa Iringa Febtuari 18, 2015. Kulia kwake ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dr. Shukuru Kawambwa.
7
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na viongozi wa mkoa wa Iringa baada ya kupokea taarifa ya mkoa wa Iringa kwenye ikulu ya Iringa Februari 18, 2015. Kushoto ni Mkuu wamkoa wa Iinga , Amina Masenza. Mheshimiwa Pinda yuko katika ziara ya kikazi mkoani Mbeya.
8
Badhi ya viongozi wa mkoawa Iringa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipozungumza nao Februari 18, 2015 akiwa katika ziara mkoa wa Iringa Februari 18, 2015. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

MWANAMUZIKI WA BONGO FLAVA MWANA FA AKITETA JAMBO NA WAZIRI CHIKAWE NCHINI MAREKANI

$
0
0
fa1 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akizungumza na mwanamuziki mkongwe wa Bongo Flava, Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA wakati mwanamuziki huyo alipokutana na Waziri huyo jijini Washington DC katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani. 

Waziri Chikawe yupo nchini humo kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani, na kwa upande wa Mwana FA yupo nchini Marekani kwa ajili ya matembezi yake binafsi hata hivyo alienda ubalozini hapo kwa ajili ya kumsalimia Balozi. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
fa2 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia), Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula wakiwa katika picha ya pamoja na mwanamuziki mkongwe wa Bongo Flava, Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA wakati mwanamuziki huyo alipokutana na Waziri huyo jijini Washington DC katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani. 

Waziri Chikawe yupo nchini humo kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani, na kwa upande wa Mwana FA yupo nchini Marekani kwa ajili ya matembezi yake binafsi hata hivyo alienda ubalozini hapo kwa ajili ya kumsalimia Balozi. Kulia ni rafiki wa mwanamuziki huyo ambaye pia ni mfanyabiashara, Swalah Saidi. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images