Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 464 | 465 | (Page 466) | 467 | 468 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Mwili wa baba wa msanii wa muziki wa kizazi kipya Dully Sykes,Marehemu Ebby Sykes ukiswaliwa nyumbani  kwa kaka wa marehemu maeneo ya Kawe jijini Dar leo mchana.Marehemu Ebby Sykes amezikwa jioni hii kwenye makabiri ya Kisutu.
   Mwili wa Marehemu Ebby Sykes ukipandishwa kwenye gari kwa safari ya kwenda kwenye mazishi,makaburi ya Kisutu jijini Dar jioni hii.
   Msanii wa muziki wa kizazi kipya Dully Sykes akiwa amepanda gari lililobeba mwili wa Marehemu baba yake kwa safari ya kwenda kupumzishwa kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar leo
  Baadhi ya wasanii pamoja na ndugu na jamaa waliofika kwenye msiba wa marehemu Ebby Sykse

  0 0

  3
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na   Chifu mpya wa Wahehe, Chifu Adam Abdu Mkwawa, Mtwa Adam wa Pili (14), wakati wa mazishi ya baba yake aliyekuwa Chifu wa Kabila la Wahehe, Chifu Abdu Mfwimi Adam Mkwawa leo  katika eneo la Nyumba ya Makumbusho ya Chifu Mkwawa, Kijiji cha Karenga Februari 16, 2015.
  56
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa pole mjane wa aliyekuwa Chifu wa Kabila la Wahehe, Chifu Abdu Mfwimi Adam Mkwawa leo  Kijiji cha Karenga Februari 16, 2015.
  8
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya aliyekuwa Chifu wa Kabila la Wahehe, Chifu Abdu Mfwimi Adam Mkwawa leo  katika eneo la Nyumba ya Makumbusho ya Chifu Mkwawa, Kijiji cha Karenga Februari 16, 2015
  ………………………………………
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Februari 16, 2015, ameungana na mamia ya waombolezaji kumlaza katika nyumba yake ya milele, Chifu wa Kabila la Wahehe, Chifu Abdu Mfwimi Adam Mkwawa.

  Aidha, Rais Kikwete ameshuhudia kutawazwa kwa Chifu mpya, Chifu Adam Abdu Mkwawa, Mtwa Adam wa Pili, kijana wa miaka 14, ambaye yuko darasa la saba na ambaye anachukua nafasi ya baba yake ambaye aliaga dunia juzi, Jumamosi, Februari 14, 2015. twa Adam wa Pili ni mtoto pekee wa kiume na pia ni mtoto sita na wa mwisho wa Chifu Abdu Adam Mkwawa ambaye ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 65.

  Rais Kikwete amewasili katika eneo la Nyumba ya Makumbusho ya Chifu Mkwawa, Kijiji cha Karenga, kiasi cha saa saba kujiunga na mamia ya waombolezaji na kushuhudia kutawazwa kwa Mtwa Adam wa Pili, ambaye amekuwa chifu kwa kupewa mkuki na ngao, ambavyo vilitumiwa na Chifu Mkwawa mwenyewe, na baadaye kukalishwa kwenye kiti cha uchifu.
   Kwa vile hajafikisha umri wa miaka 20 ambao ndio umri rasmi wa kuwa Chifu wa Wahehe, ameapishwa pia chifu wa muda, Chifu Hassan Adam Sapi (Mahinya), ambaye atashikilia kiti cha uchifu kwa niaba ya Mtwa Adam wa Pili, mpaka hapo atakapofikisha umri wa miaka 20, miaka sita kutoka sasa.

  Wakati mmoja wakati wa sherehe ya kutawazwa, Rais Kikwete amelazimika kumbembeleza na kumtuliza Mtwa Adam Abdu Mkwawa, ambaye alizidiwa na hisia na kuanza kubujikwa na machozi.

  Baada ya kutawazwa kwa chifu mpya, yameanza mazishi ya chifu aliyeaga dunia ambaye amezikwa kwa heshima na taratibu zote za dini ya Kiislam lakini pia akapigiwa risasi tatu kwa kutumia gobole kwa mujibu wa mila na tamaduni za Kabila la Wahehe.

  Baada ya kumalizika kwa mazishi ya Marehemu Chifu Abdu Mfwimi Adam Mkwawa, Rais Kikwete amekwenda nyumbani kwa marehemu kutoa pole kwa wafiwa akiwemo mama mjane.
   Rais Kikwete amewasili Mkoani Iringa asubuhi ya leo, akitokea Dar es Salaam, ambako anafanya ziara ya kikazi ya siku mbili. Rais Kikwete ataondoka Iringa kesho, Jumanne, Februari 17, kurejea Dar es Salaam.

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu warsha maalumu iliyoandaliwa na kampuni hiyo katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yatakayofanyika Machi 7, 2015 ukumbi wa Mlimani City. Wengine kutoka kushoto ni maofisa wa Trumark,  Antu Mandoza na Nuru Lyau.
   Mratibu wa Warsha hiyo Antu Mandoza (kulia), akisisitiza 
  jambo wakati akizungumza na wanahabari. Kushoto ni Mratibu Msaidizi wa warsha hiyo, Nuru Lyau.
   Ofisa wa Kampuni ya Trumark, Zulekha Samwix (kulia), akichangia jambo wakati wa mkutano huo.
  Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
  …………………………………………..
  Na Dotto Mwaibale
   
  KAMPUNI ya TruMark ya jijini Dar es Salaam imeandaa warsha yenye lengo la kumjengea mwanamke uwezo wa kutambua changamoto na kuzigeuza kuwa fursa.
   
  Hayo yamemwa Dar es Salaam leo na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Agness Mgongo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
  Mgongo alisema warsha hiyo itafanyika Machi 7, 2015 katika ukumbi wa mikutano wa  Mlimani City ikiwa ni siku moja kabla ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
   
  ‘Tunataka tumjengee mwanamke uwezo wa kujiamini, kujithamini na kutambua kuwa changamoto anazozipata ni fursa zitakazomfanya aweze kupambana na makali ya maisha na kisha kujiendeleza bila kumtegemea mwanaume’ alisema Mgongo.
   
  Aidha Mgongo alisema kuwa warsha hiyo itajumuisha shuhuda na maonesho ya bidhaa na kazi za mikono kutoka kwa wanawake waliofanikiwa kupitia changamoto mbalimbali walizozipitia.‘Siwezi kuwataja ila watakuwepo wanawake ambao walikumbwa na changamoto mbalimbali lakini hawakukata tamaa na mwisho wa siku wakafanikiwa,’ alisema Mgongo.
   
  Naye kwa upande wake Mratibu Mkuu wa warsha hiyo, Antu Mandoza alisema kuwa kutakuwa na kiingilio cha sh. 50,000 ambayo asilimia 10 ya fedha zitazopatikana zitaelekezwa katika kuwaandaa wasichana kujitambua mapema kabla ya kuingia katika soko la ajira.
   
  ‘Tutaenda katika shule mbalimbali za wasichana kuwafundisha mbinu nbalimbali za kuwa wajasiriamali na kujiajiri punde wanapohitimu masomo yao’ alisema Mandoza.

  0 0

  DSC_0358
  Benki ya NMB imetoa msaada wa madawati 40 na meza za walimu wenye thamani ya sh. milioni 5 katika shule za msingi  Mwaramu,iliyomo wilayani humo,huku msaada huo ukiwa umetokana na faida inayopata benki hiyo.

  Akiongea baada ya kukabidhi msaada huo,meneja wa benki  hiyo kanda ya kaskazini, Vicky Bishubo alisema benki hiyo imeamua kutoa msaada wa madawati hayo baada ya kuona shule nyingi zikikosa madawati na wanafunzi wake wakikaa chini kwenye sakafu.

  Alisema kutokana na hali hiyo wanafunzi wengi wamekuwa hawazingatii masomo pindi wawapo darasani kwa sababu ya ukosefu wa vitendea kazi vya madarasani hususani madawati.

  ‘’leo benki ya NMB imeamua kutoa msaada wa madawati 40 , meza za walimu na viti wenye thamani ya shilingi milioni 5 ,tumeamua kufanya hivyo kutokana na uhitaji wa shule husika napenda niwahakikishie kuwa benki yenu imetenga zaidi ya shilingi bilioni 1 kwa ajili ya kuirudishia jamii faida kidogo inayopata’’alisema Bishubo

  Bishubo aliongeza kuwa,benki hiyo iliamua kutoa msaada wa madawati hayo ya wanafunzi ili kuweza kutoa motisha kwa wanafunzi hao kuweza kusoma kwa bidii kwa madai kuwa kutokuwepo kwa vitendea kazi mashuleni ni moja ya sababu zinazopelekea wanafunzi wengi kufeli.

  "Msaada huu wa madawati  umetokana na faida kidogo ambazo benki inapata hivyo tumeona katika faida hizo ni jambo jema kutoa msaada wa aina hii kwa ajili ya kuweza kuendeleza watoto kielimu kwani wao ndiyo Taifa la kesho," alisema Bishubo.


  Naye Meneja wa NMB tawi la Hai Merdadi Malisa alisema benki hiyo imejipanga kusaidia jamii  katika wilaya hiyo kwa kutoa msaada pindi inapohitajika na kuwataka wananchi kufungua akanti katika benki hilo ili kuiwezesha benki hiyo kupata faida zaidi.
  Kwa upande wake Mkuu wa Hai , Novatus Makunga aliipongeza benki ya NMB kwa kutoa msaada huo na kuwataka wadau wengine wa elimu kuiga mfano wa benki hiyo kwa kutoa mchango kama huo ili kupunguza ya madawati wilayani huo.

  Alisema wilaya ya Hai inakabiiwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya upungufu wa madawati hata hivyo alisema taitizo hilo lipo kwa baadhi ya shule za msingi na wilaya ipo kwenye mkakati wa kukabiliana nalo.

  ‘’Changamoto ya madawani ipo sana katika wilaya yetu ya Hai ila tunajitahidi kukabiliana nayo kwa kuwatumia wadau mbalimbali hususani nyie wa NMB ,najua benki itakuwa imepokea maombi mengi lakini tunawapongeza kwa kuona umuhimu wa kutoa katika shule ya msingi Mwaramu iliyopo wilaya yangu,alisema

  Aliwataka wadau wengine wa elimu kuiga mfano wa benki ya NMB,kwa kuisaidia serikali kupunguza changamoto zilizopo kwenye shule mbalimbali hapa nchini hasa za msingi ambako ndiko tatizo kubwa lilipo.

  ‘’Kupatikana kwa madawati haya naimani kutaongeza ari ya ufaulu kwa wanafunzi sambamba na walimu kuongeza ari ya ufundishaji katika shule hii’’alisema Makunga

  habari hii kwa hisani ya libeneke lakaskazini blog

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua dawati  lenye ubora uliothibitishwa na Shirika la Viwango Tanzania lililouiniwa na kutengenezwa na Kampuni ya EDOSAMA HARDWARE ya jijini Dar es salaam, ofisini kwake Februari 16, 2015. Dawati hilo linalotengenezwa kwa mbao laini ambazo zimebanwa  bila kutumia misumari linakadiriwa kugharimu sh. 80,000/=. Wengine pichani  kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Eric Shigogo, Mkuu wa Idara ya Mikopo ya Benki ya TIB, Masanja Kungu, Ofisa Mazingira, Daniel Kapakala na Mkurugrnzi Msaidizi wa Kampuni hiyo,Edward Saguda.shig2 
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua dawati  lenye ubora uliothibitishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) lililobuniwa na kutengenezwa na Kampuni ya EDOSAMA HARDWARE ya jijini Dar es salaam. Dawati hilo linalotengenezwa kwa mbao laini ambazo zimebanwa  bila kutumia misumari linakadiriwa kugharimu sh. 80,000/=. Wengine pichani  kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Eric Shigogo, Mkuu wa Idara ya Mikopo ya Benki ya TIB, Masanja Kungu,  Ofisa Mazingira, Daniel Kapakala na Mkurugrnzi Msaidizi wa Kampuni hiyo,Edward Saguda.  shig3 
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua dawati  lenye ubora uliothibitishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) lililobuniwa na kutengenezwa na Kampuni ya EDOSAMA HARDWARE ya jijini Dar es salaam. Dawati hilo linalotengenezwa kwa mbao laini ambazo zimebanwa  bila kutumia misumari linakadiriwa kugharimu sh. 80,000/=. Wengine pichani  kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Eric Shigogo, Mkuu wa Idara ya Mikopo ya Benki ya TIB, Masanja Kungu,   na Mkurugrnzi Msaidizi wa Kampuni hiyo,Edward Saguda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  na1Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kushoto) akitoa maelezo ya kumkaribisha Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu (Kulia) wakati alipofanya ziara ya kujitambulisha kwa Tume ya Mipango.
  Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kushoto) akimkabidhi zawadi za vitendea kazi Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu alipofanya ziara ya kujitambulisha kwa Tume ya Mipango. na6 
  Naibu Katibu Mtendaji (Miundombinu na Huduma), Mhandisi Happiness Mgalula (Kushoto) akimkabidhi zawadi Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu alipofanya ziara ya kujitambulisha kwa Tume ya Mipango.

  …………………………………………………………………
  Na Saidi Mkabakuli.

  Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu amefanya ziara ya kujitambulisha kwa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ambayo ni moja taasisi anazoziratibu.

  Akizungumza wakati wa ziara hiyo Dkt. Nagu alitoa wito kwa Tume ya Mipango ijielekeze katika kujibu changamoto kuu za kiuchumi zinazowakabili watanzania kwa sasa ikiwemo umaskini miongoni kwa Watanzania walioko vijijini,  ukosefu wa wa viwanda vya kuongeza thamani mazao hasa kipindi hiki Tanzania inapoelekea kwenye uchumi wa gesi.
  Dkt. Nagu aliasa Tume ya Mipango kufanya tafiti mbalimbali za kiuchumi na kijamii zitakazotoa majibu ya changamoto hizo.

  “Kwa kuwa moja ya majukumu ya Tume ya Mipango ni kuandaa mipango ya maendeleo ya muda mrefu, kati na ile ya kila mwaka na pia kufanya tafiti mbalimbali za kiuchumi na kijamii, napenda kusisitiza kuwa mipango inayoandaliwa ijielekeze katika kujibu changamoto hizo kubwa zinazowakabili wananchi wetu ili kuhakikisha kuwa tunafikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025,” alisema Dkt. Nagu.

  Kwa mujibu wa malengo makuu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, serikali imejipanga kuhakikisha maisha bora na mazuri kwa kila mtanzania, utawala bora unaozingatia sheria, na kujenga uchumi imara, wa kisasa na ushindani.

  Akizungumza wakati wa kumkaribisha Dkt. Nagu, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango alisema kuwa majukumu ya msingi ya Tume ya Mipango ni kutoa dira na mwongozo wa uchumi wa Taifa pamoja na kubuni sera za uchumi na mikakati ya mipango ya maendeleo ya Taifa; usimamizi wa uchumi na kufanya utafiti katika nyanja za uchumi na maendeleo ya jamii.

  Dkt. Mpango aliongeza kuwa kwa sasa Tume ya Mipango inafanya kazi ya kuratibu utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2014/15 pamoja na uandaaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2015/16 na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2016/17.

  “Vilevile, Tume ya Mipango tumejidhatiti katika kuandaa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2016/17 – 2020/21 ambao utajikita katika kuifikisha tanzania kuwa ni nchi ya viwanda,” alisema Dkt. Mpango.

  Kwa mujibu wa Dkt. Mpango, tangu kuundwa upya kwa Tume ya Mipango mwaka 2008, imefanikiwa kukamilisha kazi kubwa za kitaifa ikiwemo kufanya mapitio ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, kuandaa Mpango Elekezi wa Miaka 15 (2011/12 – 2025/26 pamoja na kuandaa Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12 – 2015/16) na kuratibu utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Idadi ya Watu 2006.

  Kazi nyingine ni pamoja na kuandaa Mipango ya Maendeleo ya Taifa kila Mwaka, kuandaa mfumo wa ufuatiliaji na utekelezaji wa miradi ya Matokeo Makubwa Sasa na kuratibu uanzishwaji wa President Delivery Bureau (PDB), Kuandaa Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji katika Sekta ya Umma (Public Investiment Management – Operational Manual – PIM-OM), na kufanya tafiti mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

  0 0

  Kufuatia kifo cha Mtanzania Robert  Mpwata (a.k.a Ricardo) kilichotokea mji wa Schotten hapa ujerumani,  Mazishi  yanategemea kufanyika Marbug hapa ujerumani, lini na mahali tutawaletea taarifa zaidi wiki ijayo inayoanza Jumatatu ya tarehe 16.02.15,  watanzania tunaendelea kuomba uvumilivu wenu kwani jambo hili limechukua muda mrefu  kwa sababu kila kitu kilikuwa mikononi mwa  polisi.

  Watanzania wote ambao tupo katika UTU e.V Whattsupp Group tumekubaliana kw apamoja kuchanga pesa  kwa ajili ya kusaidia gharama za mazishi h ivyo tunawaomba watanzania wote Ujerumani na sehemu mbali mbali nje ya ujerumani msaada wa hali na mali ili kuweza kufanikisha Mazishi ya Mtanzania mwenzetu. asanteni sana kwa uvumilivyu mkubwa. Michango yote ipelekwe kwenye acc inayoonekana hapo chini

  Name des Kontoinhabers: Mfundo Peter
  Name des Kreditinstitutes: Spakasse Alzenau
  IBAN: DE84795500000008273377
  BIC: BYLADEM1ASA
  Asanteni

  0 0

  DSC_0254
  Balozi wa India nchini, Mh. Debnath Shaw akikata utepe kuzindua moja ya majengo ya shule ya msingi Kibugumo yaliyokarabatiwa na umoja wa jamii ya watu kutoka India Bengali waliopo hapa Tanzania, BANGO SANGHO kwenye hafla fupi iliyofanyika mwishoni mwa wiki Kigamboni jijini Dar. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mbunge wa jimbo la Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile (wa tatu kushoto), Mwenyekiti wa umoja wa jamii ya watu kutoka India Bengali waliopo hapa Tanzania, BANGO SANGHO, Amit Nandy (wa pili kushoto) Pintu Dutta na Dipankr ambao ni wajumbe wa umoja huo.
  DSC_0255
  DSC_0260
  Balozi wa India nchini, Mh. Debnath Shaw na Mbunge wa jimbo la Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile wakikagua moja ya jengo la darasa lililokarabatiwa na kuwekwa madawati mapya na umoja wa jamii ya watu kutoka India Bengali waliopo hapa Tanzania, BANGO SANGHO.
  DSC_0266
  DSC_0003
  Balozi wa India nchini, Mh. Debnath Shaw akisalimiana na Daktari bingwa wa Afya ya jamii na familia, Dkt. Ali Mzige kwenye hafla fupi ya kukabidhi madawati 50 pamoja majengo mawili ya shule ya msingi Kibugumo yaliyokarabatiwa na umoja wa jamii ya watu kutoka India Bengali waliopo hapa Tanzania, BANGO SANGHO. Katikati ni Mbunge wa Kigamboni Dk Faustine Ndungulile. (Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).


  WANAFUNZI 150 waliokuwa katika dhiki ya elimu shule ya msingi Kibugumo kutokana na kulazimika kusoma wakiwa wameketi sakafuni wamekabidhiwa madawati yatakayowawezesha kusoma kwa raha.

  Madawati hayo yamekabidhiwa jana na umoja wa jamii ya watu kutoka India Bengali waliopo hapa Tanzania, BANGO SANGHO mbele ya shuhuda ya balozi wa India nchini, Debnath shaw. Pamoja na madawati hayo taasisi hiyo ilikabidhiwa madarasa mawili yaliyokarabatiwa.

  Akipokea msaada huo Kaimu Ofisa elimu wa Manispaa ya Temeke Angelina Nasazwa, alisema umekuja wakati muafaka hasa kwa kuangalia changamoto nyingi zilizopo katika shule hiyo, ikiwemo miundombinu ya madarasa na ofisi.
  DSC_0026
  Balozi wa India nchini, Mh. Debnath Shaw (wa pili kulia) akiteta jambo na Mbunge wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile (kulia) kwenye hafla fupi ya kukabidhi madawati 50 pamoja majengo mawili ya shule ya msingi Kibugumo yaliyokarabatiwa na umoja wa jamii ya watu kutoka India Bengali waliopo hapa Tanzania, BANGO SANGHO.

  Alisema kukabidhiwa kwa madawati na majengo hayo kunapunguza shida iliyopo na kufanya mazingira ya kusomea kwa wanafunzi wengi kuwa rafiki. Aidha pamoja na kutoa shukrani kwa umoja wa Bango Sangho na pia kwa balozi mwenyewe kwa kusaidia shule hiyo, ofisa huyo alisema kwamba jumuiya hizo zimefanya vyema kuwakumbuka watoto hao ambao walikuwa na changamoto kubwa za kusoma wakiwa wameketi huku wakiwa hawajui kwamba kwa matatizo hayo wamekuwa wakikosa haki zao za msingi za elimu bora.

  Hata hivyo pamoja na kupokea misaada hiyo aliwataka watu Bango Sangho kuendelea kutoa ushirikiano kwa shule hiyo ambayo inakabiliana na changamoto nyingi. Naye Mbunge wa Kigamboni Dk. Faustine Ndungulile aliwapongeza watu wa Bango Sangho kwa kuiona shule hiyo ya Kibugumo na kusema wananchi wa Kibugumo watauenzi msaada huo kwa kutunza madawati na madarasa hayo ambayo yamepatikana kutokana na kujinyima kwa wanachama wa Bango Sangho.
  DSC_0036
  Balozi wa India nchini, Mh. Debnath Shaw akipokea zawadi ya maua kutoka kwa mmoja watoto wa shule ya msingi Kibugumo iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Alisema mchango wa wanajumuiya ya Bango Sangho ni muhimu hasa kipindi hiki cha mabadiliko ya sera ya elimu itakayoanza kutumika mwakani, ambayo inatarajia kuleta mapinduzi makubwa ya elimu nchini.

  Mbunge huyo ameahidi kuendeleza ushirikiano na jumuiya hiyo huku akiahidi ushirikiano pia katika uendesha kliniki kwa wanafunzi wa shule ya Kibugumo. Bango Sangho ni jumuiya ya wananchi wa India wanaoishi nchini Tanzania ambao hujishughulisha na masuala ya utamaduni na kidini na wakati mwingine hutoka na kusaidia jumuiya zingine hasa watoto.

  Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Amit Nandy akimkaribisha mgeni rasmi balozi wa India kuzungumza machache, alisema pamoja na majukumu ya jumuiya hiyo katika masuala ya kidini na utamaduni,wamekuwa wakishirikiana na taasisi nyingine kwa ajili ya maendeleo ya jamii.
  DSC_0047
  Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Kibugumo, Mzamilo Ally (kushoto) akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Balozi wa India nchini Tanzania, Mh. Debnath Shaw kuzungumza na wageni waalikwa.

  Alisema walikabidhiwa jukumu la kusaidia shule hiyo miaka miwili iliyopita na kwamba wanashukuru wametimiza azma hiyo na sasa wanataka kufanya matibabu bure kwa wanafunzi kama kamati ya shule na serikali ya eneo hilo itakubali. Awali Mwalimu Tatu Mhina akisoma risala ya kuukaribisha ugeni huo shuleni Kibugumo, alisema bado wana changamoto kubwa kubwa kutokana na shule hiyo kuwa na wanafunzi 1000 huku wengi wao wakiwa na tatizo la miundombinu, madarasa, ofisi za walimu na madawati.

  Alisema pamoja na kwamba bado wana madarasa lakini madarasa yamechakaa na hivyo kuhitaji kuangaliwa. Aidha baadae mwalimu huyo katika mahojiano alisema kwamba wanachangamoto ya chumba cha kompyuta na umeme na kwamba wanafundisha somo la tehema bila uhalisia.
  DSC_0137
  Mwalimu Tatu Mhina wa shule ya msingi Kibugumo akisoma risala iliyoandaliwa na walimu wa shule hiyo kwa mgeni rasmi Balozi wa India nchini (pichani meza kuu).

  Pamoja na kuomba ushirikiano pia mwalimu Tatu alisema upo uwezekano wa shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1975 wakati wa kamepni za vijijini vya ujamaa, kupata umeme kwa kuwa nguzo zimepita karibu kinachotakiwa kwa wahusika kuliona hilo.

  Naye balozi wa India nchini amesema amefurahishwa kushuhudia uhusiano mzuri uliopo kati ya wakazi wa Kibugumo na jamii ya India inayoishi nchini Tanzania kupitia Bango Sangho.
  Alisema ushirikiano huo anatarajia kuona ukiendelea kwa manufaa ya jamii zote mbili za Kibugumo na Bango Sangho.
  DSC_0190
  Balozi wa India nchini, Mh. Debnath Shaw akizungumza na wazazi, walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Kibugumo kwenye hafla ya kukabidhi madawati 50 na majengo mawili yaliyokarabatiwa na umoja wa jamii ya watu kutoka India Bengali waliopo hapa Tanzania, BANGO SANGHO.
  DSC_0228
  Baadhi ya wajumbe wa umoja wa jamii ya watu kutoka India Bengali waliopo hapa Tanzania, BANGO SANGHO wakimsikiliza mgeni rasmi kwenye hafla hiyo.
  DSC_0231
  Mbunge wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi madawati 50 pamoja na majengo mawili yaliyokarabatiwa na umoja wa jamii ya watu kutoka India Bengali waliopo hapa Tanzania, BANGO SANGHO katika shule ya msingi Kibugumo iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
  DSC_0168
  Mwenyekiti wa umoja wa jamii ya watu kutoka India Bengali waliopo hapa Tanzania, BANGO SANGHO, Amit Nandy akielezea nia na madhumuni ya umoja huo ambao utaendelea kusaidia jamii zenye uhitaji kwa ajili ya maendeleo ya Taifa ikiwa ni pamoja na kudumusha ushirikiano baina ya nchi ya Tanzania na India.
  DSC_0103
  Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Temeke, Angelina Ngasazwa akitoa neno la shukrani kwa umoja wa jamii ya watu kutoka India Bengali waliopo hapa Tanzania, BANGO SANGHO kwa msaada walioutoa shule ya msingi Kibugumo.
  DSC_0245
  Mbunge wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile akiongoza ugeni huo kuelekea eneo la tukio kwa ajili ya zoezi la kukabidhi majengo mawili yaliyokarabatiwa na umoja wa Bango Sangho.


  0 0

  Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais, Dk. Julius Ningu (katikati)  ambaye pia ni Mgeni Rasmi katika  Warsha ya Mafunzo ya  kuandaa vigezo vya mikakati ya Kitaifa ya kupunguza Gesijoto,  akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Warsha hiyo njee ya Ukumbi wa Stella Maris Mkoani  Bagamoyo leo . Kulia kwake ni Mkufunzi kutoka UNDP- New York,  Dk. Deborah Cornland na kushoto  kwake ni Mkufunzi kutoka Carboni Africa- Nairobi  Faith Nangabo. (Picha na OMR)

  Mkurugenzi  Idara ya Mazingira, Ofiisi ya Makamu wa Rais, Dk. Julius Ningu akifungua  Warsha ya Mafunzo ya kuandaa vigezo vya mikakati ya Kitaifa ya kupunguza Gesijoto Mkoani Bagamoyo leo . wa kwanza kushoto  ni Mtaalam wa Nishati na Mabadiliko Tabianchi kutoka UNDP- Dar es Salaam, Bw. Abbas Kitogo na wa kwanza  kulia  ni Dk. Deborah Cornland kutoka UNDP- New York.


  0 0

  DSC_0255
  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha, Nyerembe Munasa akizungumza katika ufunguzi wa kuadhimisha siku ya redio duniani iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Arusha.

  “Mnatakiwa kutafiti, kutathmini na kupeleka taarifa zenye tija na kuhamasisha vijana kujituma kufanya kazi kwa bidii ili kuondoa wimbi la umaskini kwa wananchi na hasa vijana, mkitekeleza wajibu wenu kwa kujua nini mnachofanya mtachochea mabadiliko kwa haraka katika jamii”.

  Akizungumzia fursa zilizopo, Mkuu huyo wa Wilaya ya Arumeru ametoa wito pia kwa vyombo vya habari hususani radio za jamii kuwawezesha vijana wa Kitanzania kutambua na kutumia fursa zilizopo za uchumi wa gesi na mafuta ili kujiondoa katika umaskini unaolalamikiwa kusababishwa na ukosefu wa kazi.

  “Pamoja na utengenezaji wa vipindi vyenye kuelimisha jamii redio jamii lazima ziwajibike kibinafsi na kijamii hadi ngazi ya taifa kwa kuwapa vijana taarifa zilizosheheni fursa zilizopo na namna ya kuzifanyia kazi, ili vijana waondokane katika migogoro na maandamano yasiyokuwa na tija kwa sababu watakuwa wanajua nini cha kufanya ndani ya sheria na utengamano wa amani”.
  DSC_0242
  Amesema vyombo vya habari jamii iwapo vitatumia vyema Katika kuwashirikisha vijana vina uwezo na nguvu kubwa kubadilisha fikra za wananchi kwa kutengeneza vipindi ambavyo vitachochea mawazo endelevu kwa kuzingatia mila na utamaduni wa taifa la Mtanzania kuwakomboa vijana kuepukana na utamaduni tegemezi unaosababisha kulemaa kwa vijana kutafuta njia za mkato na kutopenda kufanya kazi jambo ambalo linasababisha mwendelezo wa umaskini nchini.

  Akizungumza kwa wakilishi wa redio za jamii, waandishi na wadau wengine wa habari mjini hapa, Munasa alisema majukumu matatu ya utangazaji wa redio, yamekuwa hayafikiwi inavyotakiwa kutokana na wengi wa wahusika kutofahamu vyema majukumu yao au kutowajibika kikamilifu.

  “Utakuta mwandishi wa habari hasa watangazaji anaingia studio hajajiandaa kwa kufanya utafiti wa somo linalozungumziwa, hana mwongozo wa kipindi (script), hana mpango kazi wa kipindi (programme matrix) na wala mlolongo wa uendeshaji wa kipindi kinapoanzia na kuishia, hili ni tatizo sio utangazaji!”

  DSC_0223
  Baadhi ya washiriki kutoka redio mbalimbali za jamii nchini wakimsikiliza mgeni rasmi wakati akifungua rasmi sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani.

  Pamoja na kuwakumbusha watangazaji umuhimu wa kutangaza katika vyombo vya habari hususan redio mkuu huyo wa wilaya aliwataka washiriki kubadili mtazamo wa muziki kwa kupiga muziki wa asili kwa lengo la kupeleka ujumbe mzito na wenye manufaa kwa taifa badala ya muziki uliojaa mahadhi ya mapenzi na matusi.

  “Muziki una nguvu kubwa katika maisha ya binadamu watangazaji lazima mfahamu na mjue namna ya kuupangilia kutokana na vipindi mnavyovitayarisha na muda wa aina ya muziki husika. Sio wakati wote ni wakati wa kusikiliza muziki wa mapenzi, kwa sababu redio husikilizwa na watu mbalimbali kwa sababu mbalimbali pia.”

  Suala la mpangilio wa muziki, kuuelewa na thamani yake katika redio na umma lilielezwa kwa undani zaidi na nguli wa masuala ya muziki katika vyombo vya habari Masoud Masoud ambaye alisema kuwa watangazaji wa kisasa wamekuwa hawaelewi maana ya muziki na faida zake Katika kuendeleza taifa kitamaduni na kimaendeleo.
  DSC_0012
  “Vijana wengi wamekuwa wakitayarisha muziki wanaoupenda wao na sio unaopendwa na kufufaisha umma, wakati umefika kwa kutafuta mbinu au jitihada zozote za kuwafundisha muziki ni nini, unachezwa wakati gani na kwa manufaa ya nani.” Sherehe hizo ambazo huandaliwa kila mwaka tarehe 13 Februari, ziliandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na ujumbe wa mwaka huu ni “Nguvu ya Redio na Ushiriki wa Vijana katika Maendeleo”.

  Ujumbe kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Irina Bokova katika kuadhimisha siku hiyo na kusomwa kwa niaba yake na mwakilishi wa UNESCO nchini Bokosha Spencer umesisitiza nguvu ya radio katika kujihusisha na masuala ya kijamii kwa vijana wenye umri chini ya miaka 30, ambao ni zaidi ya nusu ya idadi ya watu duniani .
  DSC_0258
  Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akifurahi jambo na baadhi ya washiriki kutoka redio mbalimbali za jamii wakati Mkuu wa Wilaya ya Arumeru akibariki ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyofanyika jijini Arusha mwishoni mwa wiki.

  “Vijana wanawake na wanaume hawashirikishwi vema katika vyombo vya habari - hutengwa mara nyingi kunakoashiria kusahaulika kwa mapana yake katika masuala ya kijamii, kiuchumi na kidemokrasia. Redio kama chombo cha mshikamano, kinachokuza elimu na utamaduni ushirikishwaji wa vijana ni muhimu”. Bokova aliitaka jamii kuwasaidia vijana kwa kuwapa sauti kubwa zaidi na kujenga hisia ya jamii kwa njia ya usambazaji wa habari kwa kutayarisha na kusikiliza vipindi vya redio.
  DSC_0007
  Bw. Spencer Bokosha akisoma hotuba kwenye maadhimisho ya siku ya redio duniani kwa niaba ya Mkuu wa ofisi ya Shirika la UNESCO, Tanzania Zulmira Rodriguez.
  DSC_0061
  Mwenyekiti wa mkutano wa sherehe maadhimisho ya siku ya redio duniani ambaye pia ni Meneja wa Maadili wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. Allan Lawa akiendesha akitoa mada chokonozi ni kwa namna gani radio inaweza kutumika kama jukwaa la ushiriki kwa vijana katika mabadiliko ya kidemokrasia? Utafiti unaogusa Watanzania wakielekea katika uchaguzi mkuu.
  DSC_0158
  Mwandishi mkongwe na mkufunzi wa tasinia ya habari kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Ayub Rioba akitoa mada Je uwekaji huru wa mawimbi ya radio kumesababisha mambo mabaya zaidi kuliko mazuri: Mitazamo na matarajio kuhusiana na ushiriki wa vijana wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani.
  DSC_0147
  Makamu Mwenyekiti wa mtandao wa redio za jamii nchini (COMNETA) ambaye pia ni Meneja wa redio jamii Sengerema FM ya mkoani Mwanza Bw. Felician Ncheye, akiwasilisha mada inayohusu ushiriki wa vijana katika vipindi vya Redio, ambapo amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa Redio za jamii kuhakikisha zinawafikia watu wote kwenye jamii huku wakiwalenga vijana ambao ndio wana idadi kubwa ambayo inaweza kuchochea mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi na kitamaduni.
  DSC_0091
  Meneja wa Redio Kahama FM, Marco Mipawa akichangia mada ya kuonesha nguvu za vijana na vyombo vya habari vya jamii pamoja na kujadili kanuni bora zilizojitokeza katika utekelezaji wakati sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani zilizofanyika mwishoni mwa wiki jijini Arusha.
  DSC_0136
  Mwandishi wa habari mkongwe, mzee Gervas Moshilo akitoa mada ya Uandishi wenye maadili na uwakilishi wa vijana kupitia vyombo vya habari wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani.
  DSC_0054
  Meza kuu ikifuatilia mada na michango mbalimbali iliyokuwa ikitolewa na washiriki.
  DSC_0183
  Pichani juu na chini ni watangazaji wa redio za kijamii walioshiriki kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani wakichangia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye maadhimisho hayo.
  DSC_0123
  DSC_0219
  Mshehereshaji kwenye madhimisho ya siku ya redio duniani, Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua rasmi maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).

  Na Mwandishi wetu, Arusha
  Vyombo vya habari hususan redio za jamii zimetakiwa kutanguliza uzalendo na kutetea maslahi ya taifa ili kuliepusha taifa katika migogoro na mitafaruku inayoweza kusababisha machafuko nchini hasa katika kipindi cha uchaguzi mkuu ujao. Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Arumeru mkoani Arusha Nyerembe Munasa wakati wa kuadhimisha Siku ya Redio duniani iliyofanyika mwishoni mwa wiki.

  Akizungumza na watangazaji wa redio za jamii na wadau mbalimbali wa habari nchini katika ufunguzi wa maadhimisho hayo Munasa alisema redio ina nguvu kubwa kuchambua na kutengeneza mustakabali wa taifa na hasa vijana iwapo itatumika vizuri badala ya kuwa chanzo cha matatizo na uchochezi mambo ambayo yanaweza kulisambaratisha taifa.
  Amewataka waandishi na watangazaji wa redio jamii kuzingatia maadili ya kazi zao kwa lengo la kuleta mabadiliko katika maisha ya Watanzania na kujenga taifa endelevu .


  0 0

  HOYCETEMUNAWALEMAVU2
  Former Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu on field during the recording of her TV talk show.
  She also has her own talk show, Mimi na Tanzania (Me and Tanzania), which focuses on CSRs, fundraising, and supporting women and children through the promotion of human rights, gender equality, and access to healthcare and education. 

  Please nominate her on this category: “Journalists, reporters, presenters who stand out in their field”
  International Women’s Day just around the corner, MISA’s is looking to choose 2015 Women to Watch. So, who better to ask for nominations then motivated, inspirational women such as Hoyce Temu, I hope you will agree with me.
  You can nominate as many women as you like, from any of the 11 SADC countries in which MISA operates, that’s: Angola, Botswana, Lesotho, Namibia, Malawi, Mozambique, South Africa, Swaziland, Tanzania, Zambia and Zimbabwe.
  To nominate Hoyce Temu, simply email at this address (alexandrapeard@gmail.com) or info@misa.org with the name of your nominations, contact details for them (such as an email address or phone number) and a short explanation of their background and why you are nominating them - a sentence or two is all we need.
  HOYCETEMUNAWALEMAVU8
  MISA’s is interested in showcasing women across a range of fields whose work / interests and passions touch on the issues of free expression and access to information. Some examples might include:
  -Artists and performers who use their art to advocate for human rights / speak out against injustice etc.
  -Civil society representatives
  -Journalists, reporters, presenters who stand out in their field(GOR FOR THIS ONE AND PLEASE NOMINATE HOYCE TEMU)
  -Women in fields or roles traditionally male dominated such as camera operators, news anchors, sound technicians etc.
  -Human rights lawyers
  -Citizen journalists
  -Women in ICT, creating new platforms for expression, improving access to ICT etc.
  -Children / youth who are ‘rising stars’ in the media or human rights fields
  Untitled1
  Picha mbalimbali za Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akiwa katika kazi za kijamii na kuwasaidia watu wenye matatizo mbalimbali kupitia kipindi chake cha Mimi na Tanzania kinachorushwa kupitia Runinga ya Channel Ten kila Jumapili.

  0 0

  Ujumbe wa Tanzania chini ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ukionyesha namna Serikali ya Singapore inavyoratibu upatikanaji wa nyumba kwa wananchi wake ulipotembelea Bodi ya Maendeleo ya Nyumba ya Singapore jana.Jumla ya nyumba 900,000 zimeshajengwa na Bodi hii na kupatiwa wananchi kupitia ruzuku ya serikali na nyumba 50,000 zinapangishwa kwa wananchi kwa kodi isiyozidi asilimia 5. Taifa la Singapore lina watu milioni 5.4 na asilimia 99 ya watu wan chi hiyo wamewezeshwa kumiliki nyumba.
  luk2 
  Ujumbe wa Tanzania ukitembelea vyumba vya mfano vya ukubwa tofauti vinavyojengwa na Bodi ya nyumba ya Singapore kwa ajili ya kuuzia au kupangisha wananchi kulingana na uwezo, mahitaji na ukubwa wa familia. Vyumba hivi vipo Makao Makuu ya Bodi ya Nyumba ya Singapore ambavyo ni kivutio kwa wageni wanaotembelea jengo hilo kujifunza namna ya kuhudumia watu wa kada mbalimbali wanaohitaji nyumba.
  luk3 
  Ujumbe wa Tanzania ukielezwa historia ya hatua mbalimbali za maendeleo ya sekta ya nyumba nchini Singapore walipotembelea Bodi ya Maendeleo ya nyumba nchini humo jana.
  luk4 
  Ujumbe wa Waziri Lukuvi ukiwa katika mji wa kisasa wa Punggol wenye ukubwa wa kilomita za mraba kumi ambao una nyumba zilizojengwa na Bodi ya Maendeleo ya Nyumba Singapore kwa ajili ya wananchi wa kipato cha kati na chini. Katika eneo hili nyumba zimewekewa miundombinu ya kisasa na zina watu wanaofikia 250,000. Hapa ni ghorofa ya pili ya jengo mojawapo lililojengwa katika mji huu wa kisasa.
  Mojawapo wa majengo ya kisasa katika mji wa Punggol nchini Singapore yanayokaliwa na wananchi waliouziwa na Bodi ya Nyumba ya Singapore kupitia mifuko ya jamii na ruzuku ya serikali luk6luk7 
  Ujumbe wa Tanzania ukiwa eneo la Punggol Point Park ambalo ng’ambo yake ni bandari ya nchi ya Malaysia inayopakana kwa karibu na nchi ya Singapore.
  luk8 
  Ujumbe wa Waziri William Vangimembe Lukuvi ukiingia Wizara ya Mambo ya Nje ya Singapore ulipotembelea Wizara hiyo jana.
  luk9 
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.William Vangimembe Lukuvi akiweka saini kwenye kitabu cha wageni muda mfupi baada ya kuingia Wizara ya Mambo ya Nje ya Singapore. Kulia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. Angela Kairuki.
  luk10 
  Mh. Waziri Lukuvi akisalimiana na Waziri wa Nchi Mwandamizi wa Mambo ya Nje wa Singapore Bw. Masagos alipotembelea Wizara hiyo jana.
  luk11 
  Ujumbe wa Tanzania ukiwa katika mazungumzo na Waziri wa Nchi Mwandamizi Mambo ya Nje wa Singapore. Katika mazungumzo hayo Tanzania imeiomba Serikali ya Singapore kuwekeza nchini Tanzania hususan kwenye sekta ya nyumba, kusaidia upangaji wa miji mikubwa na kuanzisha safari za ndege kuja Tanzania ili kuvutia utalii. Nchi ya Singapore hupokea ndege 5800 kwa wiki kutoka nchi mbalimbali duniani na ina zaidi ya ndege 200 zinazoenda mataifa mbalimbali duniani hivyo kuwa kivutio kikubwa kuliko Tokyo Japan.
  luk12 
  Waziri William Lukuvi akimpa zawadi ya kahawa na chai ya Tanzania, Waziri Mwandamizi wa Nchi ya Singapore Bw. Masagos kama ishara ya kutangaza bidhaa za Tanzania
  luk13 
  Ujumbe wa Tanzania ukiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mwandamizi wa Mambo ya Nje wa Singapore mara baada ya kumaliza ziara fupi ya kutembelea Wizara hiyo jana kuvutia ushirikiano wa kiuchumi na nchi ya Singapore.
  luk14 
  Ujumbe wa Tanzania ukipata maelezo ya jinsi Shirika la Mipango Miji nchini Singapore la Surbana linavyokabiliana na uhaba wa ardhi katika nchi hiyo. Katika maelezo yake Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo Bw. Pang Yee Ean alisema mipango ya ardhi ya Singapore huhuishwa kila baada ya miaka mitano ili iendane na hali ya uchumi na mahitaji na kuna nidhamu ya hali ya juu katika upangaji na matumizi ya ardhi ya nchi hiyo.

  0 0

  Na Abdulla Ali Maelezo-Zanzibar.                            

  Idara ya Ardhi na Mazingira inatarajia  kufanya Uzinduzi wa Mfumo wa Mtandao wa Upatikanaji Taarifa za Ardhi Zanzibar (Zanzibar Land Information Service) (ZALIS) itakayosaidia upatikanaji wa taarifa sahihi za Ardhi nchini. 

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara hiyo uzinduzi huo  utafanyika siku ya Jumatano ya tarehe 18/02/2015 katika jengo la Ardhi liliopo Forodhani Mjini Zanzibar.

  Kwa mujibu taarifa hiyo imesema mtandao huo wenye teknolojia rahisi itakayosaidia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa habari na taarifa zote za Ardhi ikiwemo usajili, utambuzi, upimaji, uhaulishaji eneo, kijografia, mipaka na kuongeza ufanisi wa shughuli zote ardhi kwa kiasi kikubwa.

  Sambasamba na hayo taarifa hiyo imeeleza kuwa mfumo wa ZALIS utarahisisha upatikanaji wa taarifa na takwimu zinazohitajika Kijamii na Kiuchumi juu ya masuala ya Ardhi na kuzifanya shughuli hizo kuwa rahisi na nyepesi zaidi.

  Aidha Serikali ya Finland kupitia Wizara yake ya Mambo ya Nchi za Nje imekuwa ikiisaidia Zanzibar katika masuala mbalimbali ikiwemo Maji, Mazingira, Misitu pamoja na Ardhi kwa zaidi ya miaka 10 hadi sasa.

  Taarifa hiyo imefahamisha kuwa Shughuli za usajili wa Ardhi zilizinduliwa rasmi mnamo mwaka 2013 na Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein  zikiwa zinaendelea vizuri nchini. 

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo imeeleza maendeleo ya usajili wa Ardhi yamekuwa yakiendelea vizuri nchini ambapo hadi sasa jumla ya vikataa 34,000 vimeshapatiwa usajili wa kudumu.

  Taarifa hiyo imesema hadi sasa tayari kumeshaanzishwa Sera ya Taifa ya Ardhi, Mkakati wa Kitaifa wa Maendeleo ya Matumizi ya Maeneo ya Ardhi, Mipango Kimkoa Kaskazini na Kusini, Upitiaji wa Sheria zinazohusu Ardhi na Sera ya Mazingira na ile ya Misitu zimeshafanyiwa mapitio na marekebisho.

  Mfumo wa ZALIS umefadhiliwa na Serikali ya Finland ambao umegharimu zaidi ya shilingi milioni 100 ambapo mgeni rasmi katika Uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Balozi wa Finland nchini Tanzania Bi. Sinnika Antilla.  

       
     IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

  0 0

   Waziri wan chi ofisi ya Rais mahusiano na uratibu Dokta Mary Nagu (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya TASAF kushoto kwake ni mkurugenzi mtendaji wa TASAF Ladislau Mwamanga (mwenye suti  nyeusi).
   Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Ladislaus Mwamanga akimtembeza Waziri wan chi Ofisi ya Rais Dokta Mary Nagu katika jingo linalotumiwa kuhifadhi kumbukumbu za walengwa wa Mpango wa Kunusuru kaya maskini.
   Waziri wa nchi ofisi ya Rais Dokta Mary Nagu akzungumza na menejimenti ya TASAF katika ziara yake katika taasisi hiyo .

  Karibu TASAF hivyo ndivyo anavyoelekea kusema mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus Mwamanga  alipomkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Dokta Mary Nagu ambaye amefanya ziara ya kujitambulisha katika taasisi hiyo.

  0 0

    Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Saleh Mohamed Jidawi akitoa maelezo wakati wa Hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya uchunguzi na upasuaji wa macho kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China.  Wa kwanza (kushoto) ni Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman na (wakatikati) ni Balozi mdogo wa China aliepo Zanzibar Xie Yuanliang.
   Balozi Mdogo wa China Xie Yuanliang akimkabidhi Waziri wa Afya Rashid Seif Suleima msaada wa vifaa vya matibabu ya macho uliotolewa na Serikali ya nchi yake. Hafla hiyo ilifanyika Makao Mkuu ya wizara ya Afya Mnazimmoja mjini Zanzibar.
  Waziri wa Afya wa Zanzibar Rashid Seif Suleiman akitoa shukrani  baada ya kupokea msaada wa dawa za matibabu ya macho uliuotolewa na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China katika Hafla iliyofanyika Wizarani Mnazimmoja.Picha na Makame Mshenga Habari Maelezo Zanzibar.

  0 0

  Umati wa watu ukiwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam wakati wa mazishi ya baba yake mzazi ambaye pia ni msanii mkongwe mzee Ebby Sykes.
   Waziri Mkuu mstaafu jaji Joseph Warioba akiweka udongo.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akiweka udongo katika kaburi la msanii mkongwe mzee Ebby Sykes.
   Mbunge wa Chalinzi, Ridhiwani Kikwete akiweka udongo.
   Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu akiweka udogo katika kaburi la mzee Ebby Sykes
   Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu akiweka udongo katika kaburi la mzee Ebby Sykes.
   Dully Sykes (wa pili kushoto) akiwa ndani ya kaburi la baba yake mzee Ebby Sykes wakati wa mazishi yake.
   Ndugu na jama wakishiriki mazishi.

  Baadhi ya waombolezaji wakishiriki mazishi ya msanii mkongwe, Ebby Sykes yaliyofanyika leo kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)

  0 0

  Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JIHIL ENTERPRISES ya India Nd. Jilesh H. Babla wakitiliana saini mkataba wa makubaliano ya kuanzishwa kwa ofisi ya uwakala wa Utangazaji Utalii wa Zanzibar Nchini India. (Picha na Makame Mshenga Maelezo-Zanzibar)BAR2 
  Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JIHIL ENTERPRISES ya India Nd. Jilesh H. Babla wakikabidhiana mkataba wa makubaliano ya kuanzishwa kwa ofisi ya uwakala wa Utangazaji Utalii wa Zanzibar Nchini India baada ya kumaliza kusaini. (Picha na Makame Mshenga Maelezo-Zanzibar)
  BAR3 
  Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Nd. Saleh Ramadhan Ferouz akijibu maswali ya waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa tukio hilo. (Picha na Makame Mshenga Maelezo-Zanzibar)
  BAR4 
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar na Wa 3 kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JIHIL ENTERPRISES ya India Nd. Jilesh H. Babla na viongozi wengine kutoka Wizara ya Habari pamoja na Kamisheni ya Utalii Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja.


  (Picha na Makame Mshenga Maelezo-Zanzibar)
  ……………………………………………………………………………….
  Na Abdulla Ali Maelezo-Zanzibar
  Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar imetia saini mkataba wa makubaliano ya kuanzishwa kwa ofisi ya uwakala wa Utangazaji Utalii wa Zanzibar Nchini India.

  Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Nd. Ali Mwinyikai wakati wa kutia saini Mkataba huo katika ukumbi wa Wizara hiyo iliyopo Kikwajuni Mjini Zanzibar.
  Mkataba huo umetiwa saini tarehe 17/02/2015 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Nd. Ali Mwinyikai na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JIHIL ENTERPRISES ya India Nd. Jilesh H. Babla.

  Katibu huyo amesema kuwa uanzishwaji wa ofisi ya utalii nchini India haukuja kwa bahati mbaya ila ni utekelezaji wa ilani na malengo yaliyopangwa na kutekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyopo madarakani kwa upande wa sekta ya Utalii kwa lengo la kuitangaza zaidi Zanzibar kiutalii.

  Amesema ofisi hizo zitafanya kazi kama mabalozi wa kuutangaza Utalii wa nchi zao kwa kuwapatia habari watalii wote ambao wana nia ya kuzitembelea nchi husika pamoja na kutoa ushawishi mkubwa utakaowafanya wananchi wa nchi hizo kuwa na maamuzi sahihi ya kuzitembelea nchi hizo.

  Aidha Katibu huyo amesema kuwepo kwa ofisi za Utalii nchini India itasaidia kujenga uhusiano mzuri na wa kudumu baina ya Zanzibar na wadau mbalimbali wa Utalii walioko nchini India jambo ambalo linakosekana katika masoko yaliyopo hivi sasa ispokua soko la Itali.
  “Tuna kila sababu za Zanzibar nayo kutumia mfumo huu wa utangazaji wa Utalii kwani unaweza kuleta tija kubwa kwa haraka ukilinganisha na mifumo mengine ya utangazaji”, ameeleza Katibu Mwinyikai. 

  Amesema mpango huo umelenga kuimilikisha Sekta ya Utalii kwa wanachi wote wa Zanzibar ili kuhakikisha kuwa uwepo wa sekta hiyo unawafaidisha wananchi wa Zanzibar Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni.

  Ametanabahisha kuwa kupanuka kwa wigo wa masoko ya Utalii kutaongeza kazi ya utekelezaji wa dhana ya Utalii na kuondokana na utegemezi wa soko la Ulaya ambalo linatishia uhakika wa kuwepo kwake kutokana na athari za Kiuchumi na Kifedha zinazojitokeza siku hadi siku.

  Nd. Mwinyikai amefahamisha kuwa kutokana na hali hiyo Serikali ya Zanzibar imeamua kuongeza nguvu na kubadilisha mikakati ya utafutaji wa masoko mengine ikiwa ni pamoja na yale yanayochipukia yakiwemo ya Nchi za China, India, Urusi na Uturuki.

  Nae mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Jihil Enterprises ya India ambae pia ni mzaliwa wa Zanzibar anaeishi Mumbai India Nd. Jilesh H. Babla amesema ameamua kuwa wakala wa Utalii wa Zanzibar Nchini India kwa lengo la kuitangaza Zanzibar kiutalii kwani Zanzibar ina vivutio vingi vya Kiutalii zikiwemo Fukwe na Mandhari mazuri ya Kisiwa hicho pamoja na sehemu za kihistoria.

  Amesema ameamua maamuzi ya kizalendo kuwa Wakala wa Zanzibar Nchini India kwani hadi sasa hakuna wazalendo wanaoishi nje ya Nchi waliyojitikeza kufanya kazi hiyo pamoja na kuvitaka vyombo vya habari Zanzibar kufikisha ujumbe uliyo sahihi kwa wananchi juu ya Utalii wa Zanzibar ili kukuza Utalii wa nchi na hatimae kupelekea kukua kwa uchumi wa nchini.

  Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dr. Ahmada H. Khatib amesema wazo la kuwa na Ofisi ya Utalii Nchini India lilitokana na matokeo ya ziara rasmi ya Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliyoifanya Nchini China na India tarehe 27/05/2013 hadi 02/06/2013 ambayo ilijumuisha Mawaziri mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

  Amesema pamoja na kuwa takwimu za idadi ya watalii wanaotembelea Zanzibar bado zinakumbana na changamoto za kutokuwa sahihi hata hivyo idadi ya sasa inaonyesha kuwa India hutoa watalii zaidi ya 98,000 kwa kila mwaka hivyo ipo haja ya kuwepo kwa wakala wa Utalii wa Zanzibar Nchini humo.

  Amefahamisha kuwa makisio ya jumla ya kuendesha Ofisi hiyo Mjini Mumbai, India inakadiriwa kufikia zaidi ya Dola 100,000 za kimarekani kwa Mwaka ambapo Dola zipatazo 27,000 ni za kuendeshea Ofisi hiyo kila mwezi.

  0 0  Kuomba talaka si dhambi. Kama lingekuwa dhambi sheria isingeruhusu jambo hilo kwakuwa si kawaida ya sheria kuhamasishi madhambi. Ni kwasababu hii nasema kuwa atakayeona amebanwa basi aombe talaka. Si kosa hata kidogo kufanya hivyo isipokuwa ndivyo tunavyoelekezwa na sheria zetu tunazozipenda na kuziheshimu sana.

  1. KUVUNJIKA KWA NDOA.

  Kuvunjika kwa ndoa kwa mujibu wa sheria zetu za Tanzania kuna mazingira mengi. Baadhi ya mazingira hayo ni yale yaliyoorodheshwa kifungu cha 12 (a-e) cha Sheria ya ndoa ambayo ni pamoja na kifo cha mmoja wa wanandoa,  talaka ambayo tunaiongelea lakini pia yapo mazingira mengine mengi.

  2. AINA ZA TALAKA

  Talaka twaweza kuzigawa katika makundi mawili nayo ni, talaka itolewayo nje ya mahakama ambayo hutokana na ndoa zilizo katika mfumo wa kimila na nyingine ni talaka itolewayo  mahakamani ambayo sisi hapa tutaiongelea.

  Kusoma zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  NA KAMBI MBWANA, DAR ES SALAAM.

  JOTO la kisiasa limezidi kupamba moto. Hii ni kutokana na harakati za kuimarisha kambi za wagombea wa nafasi mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu nchini kote.

  Wameanza mchaka mchaka wa udiwani, ubunge bila kusahau urais. Kwa nafasi ya urais, tumeshuhudia watu wanaojiandaa kuvutana na kustawisha makundi yao ili iwe chachu yao ya kurithi kiatu cha Rais wa Awamu ya nne, Profesa Jakaya Mrisho Kikwete.

  Ingawa nafasi za ubunge na udiwani zinawaniwa pia na watu kutoka kwenye vyama vya upinzani, lakini ni wazi kuwa joto na mtifuano mkubwa upo katika Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Kila chama kina taratibu zake. Hata hivyo, kutokana na maridhiano yao waliyopa jina la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) vyama vinne vya upinzani vikiongozwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama Cha Wananchi CUF, NCCR Mageuzi na NLD vimetangaza kusimamisha mgombea mmoja kila jimbo la uchaguzi au kata.

  Huo ndio msimamo wa wapinzani. Wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanaamini kuwa vyama vya upinzani mwaka huu watafanya vizuri katika Uchaguzi Mkuu, endapo CCM haitajisahihisha na wafalme wake majimboni.

  Ni kutokana na hilo, nadiriki kusema kwamba, uchaguzi wa mwaka huu utakuwa mgumu. Katu CCM isitarajie mteremko. Ili iweze kujua namna gani inafanya vizuri katika uchaguzi huo, ni lazima iwapime wabunge na wagombea wake hususan kwa nafasi za ubunge.

  Licha ya kuwapo katika Bunge litakalomalizika baadaye mwaka huu, bado wana ndoto za kuingia kwenye uchaguzi wa mwaka huu kutetea nafasi zao, bila kuangalia jinsi walivyochokwa na wananchi wao.

  Hii ni kwasababu baadhi ya wabunge wamechokwa. Na hata kama wanakubalika, haina haja ya kuendelea kuwavumilia ili waendelee kutawala katika majimbo yao, maana hakuna umuhimu huo.

  Yapo majimbo yenye changamoto na shida nyingi. Wananchi hawajui nini hatma ya maisha yao. Shida ya maji, afya duni, elimu duni na kilimo kisichokuwa na tija ni mtihani mzito kwao.

  Wakati wabunge hao wakijigamba kama wanapendwa au wanakubalika, wananchi wao hawana cha kujivunia. Wameendeleaa kupiga miayo  na kudanganywa kila ufikapo uchaguzi. Mtazamo wa wabunge hao utaleta madhara makubwa kwa CCM.


  Wananchi watapiga kura za chuki. Wana uwezo wa kuwaondoa wabunge hao mizigo na kuwapa wapinzani kwa njia ya sanduku la kura. Watafanya hilo bila kuangalia heshima ya CCM iliyojiwekea tangu mwaka 1977.

  Hili si sahihi. Na linapaswa kupingwa vikali. CCM Makao Makuu bila kusahau viongozi wake waliosambaa Tanzania nzima, lazima wajipange ili kulinda hadhi ya chama hiki mbele ya hadhira.

  Iwaite wabunge wake na kuwahoji nini wamewafanyia wananchi wao. Iwahoji kwanini wanataka kugombea tena ubunge. Kwa wale waliokaa madarakani kwa miaka mitano, walau wanaweza kuonewa haya, ukizingatia kuwa vipindi viwili ni halali, tukiamini upo uwezekano wa kusimamia yale aliyoanzisha.

  Wale waliokaa madarakani miaka 10 kuendelea, wasichekewe. Kama walishindwa kufanya kwa miaka yote waliyokaa madarakani, watawezaje kutekeleza kwa miaka mitano ijayo?

  Huu si muda wa kupotezeana muda. Wabunge mizigo na wanaotawala kwa manufaa ya matumbo yao na familia zao wasionewe huruma. Kwa bahati mbaya, CCM ina mfumo mzuri, ila unaharibiwa na rushwa na kuoneana haya.

  Makatibu wa CCM wa Mikoa na wilaya ndio wanaoweza kumpitisha mbunge mzigo asiyekuwa na jipya kwa uongozi wake.Badala ya makatibu hao kusimamia sheria, kanuni na maadili ya chama, wamebakia kuhujumu wengi na kunufaisha wachache wao.

  Katibu anashindwa kusimamia hata yale yaliyokuwa kwenye ilani ya chama chake kwa kumuogopa mbunge aliyekuwa madarakani kwa zaidi ya vipindi viwili, huku anachojua ni kuunda mtandao usiokuwa na tija.

  Wabunge hao na makatibu ndio wanaokiweka chama katika nafasi ngumu kwenye chaguzi zake. Unawezaje kumshawishi mwananchi ampigie kura mbunge aliyekaa madarakani miaka 10 bila kutatua shida za wapiga kura wake?

  Wanaona jinsi akina mama wanavyotumia muda mwingi kutafuta maji kwa umbali mrefu, hali ya kuwa mbunge amechimba kisima karibu na nyumba yake. Katika shida zote walizokuwa nazo, hakuna hata moja inayomuhusisha mtoto wa mbunge, mke au familia yake ya karibu.

  Kwani wapiga kura ndio wameumbiwa shida? Hawana haki ya kuishi vizuri kutokana na serikali yao makini iliyochaguliwa kwa mapenzi makubwa? Inakera na kuumiza kichwa. Kwa akili zao wameamua kuidhalilisha CCM.

  Viongozi wetu wawe na haya na huruma pia. Ubunge usitumike kama mradi wa mtu mmoja, hali ya kuwa hana uwezo wa kuwaletea maendeleo wananchi wake. Wanaoongoza kwa kutegemea busara ya kiti cha katibu na viongozi wenzake wa CCM katika jimbo husika.

  Ni zaidi ya ujinga na upuuzi. Tanzania si shamba la bibi. Tunahitaji kuwa na viongozi na si watawala tu. Mfumo mbovu usiokuwa na dhamira ya maendeleo ya watu wao, huchochea chuki kwa Watanzania dhidi ya CCM, moja ya chama kikongwe barani Afrika.

  Tujipime na kujisahihisha pia. Viongozi wa CCM wa matawi hadi Taifa waangalie mbinu ya wabunge mizigo wa muda mrefu na waliochokwa. Wakati nasema haya, natambua wapo Watanzania wenye uwezo wa kuongoza kwa kushirikiana na wananchi wao.

  Lakini wanashindwa kwasababu ya ghiriba, chuki za kimtandao dhidi ya wafuta viatu wa mabwana wakubwa walioyafanya majimbo ni kampuni zao binafsi.

  Fanya ziara katika mikoa mbalimbali ujionee hali ilivyokuwa ngumu. Wapo Watanzania ambao hata mlo wao wa siku ni tatizo. Watoto wao wanakwenda shuleni wakiwa na nguo zenye matobo.

  Na yapo maeneo ambayo wanafunzi wetu wanakaa chini. Pamoja na kukaa chini kwa wanafunzi, kukosa huduma bora za afya, ajabu wapo wabunge wanaojiandaa tena kugombea ubunge.

  Huu ni zaidi ya ujinga. Tunapaswa kujitafakari upya kwa ajili ya kuunda Tanzania yenye neema. CCM iangalie hawa wabunge waganga njaa. Wabunge wachumia tumbo wasioridhika na madaraka.

  Ngazi za kiuongozi zinajulikana. Ukishafikia ngazi ya ubunge, ukakaa madarakani miaka 10 ni dhahiri unapaswa kuachia ngazi na kupisha wengine waendeleze yale uliyofanya. Vinginevyo labda urais maana ndio nafasi iliyobakia.

  Huo ndio ukweli wa mambo. Maana yapo majimbo kwenye wilaya yanayoonekana ni vichaka. Hakuna dhamira ya kuwaletea maendeleo wananchi wao. Hasira zinawapanda wananchi hao na kuamua kusimama kidete kubadilisha viongozi na kuwapitisha wapinzani, wakiamini ndio sehemu ya kuwapunguzia kero zao zilizochosha watu.


  Ifikie wakati wabunge na viongozi wao wa CCM wajitafakari upya. Wajipime kama wanayo shauku ya kuwatumikia wananchi wao. Ikiwa wameona ni ngumu, basi wakae pembeni kwa maslahi ya chama tawala.

  Ikiwa hawataki kwa ridhaa yao basi walazimishwe ili kupunguza chuki kwa wananchi waliopania kubadilisha mfumo wa uongozi katika maeneo yao. Wananchi wasilazimishwe waamini kuwa adui wao ni CCM. Adui yao ni viongozi wabovu waliokuwapo kwenye CCM. Na viongozi hawa wanaweza kuiondolewa na CCM ikaendelea kuheshimika ndani na nje ya nchi.
  kambimbwana@yahoo.com+255712053949

  0 0

  Wajasiriamali, Wasanii na Waandishi wa Habari waliopata nafasi yakwenda Oman kwa ajili ya kuutangaza Utamaduni wao wakipokelewa na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar.
  Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Bi Hindi Hamadi wa mwanzo kulia akiwasalimia wasanii hao baada ya kuwasili uwanjani hapo.
  Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimuhoji mmoja kati ya Wasanii waliyopata bahati ya kwenda nchini Oman kwa ajili ya maonyesho hayo. 

  Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar,Bi. Hindi Hamadi Khamis (katikati) akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Zanzibar wa Abeid Karume akisubiri kuwasili kwa Wajasiriamali, Wasanii na Waandishi wa Habari waliokuwa nchini Oman kwa ajili ya maonyesho ya Tamasha la Utamaduni yaliyofanyika nchini humo.
  (Picha na Miza Othman Maelezo, Zanzibar)

older | 1 | .... | 464 | 465 | (Page 466) | 467 | 468 | .... | 1898 | newer