Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 463 | 464 | (Page 465) | 466 | 467 | .... | 1897 | newer

  0 0


  1
  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa  akifunga rasmi mafunzo ya siku 14 ya wasimamizi na wadadisi wa Sensa ya viwanda 2013 itakayofanyika nchini nzima kuanzia Februari 23,2015. Hafla ya kufunga mafunzo hayo ilifanyika jana eneo la  Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika jijini Dar es salaam.
  2
  Makamu Mkuu wa chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Dkt. Tumaini Katunzi akizungumza na wasimamizi na wadadisi wa Sensa ya Viwanda itakayofanyika nchi nzima kuanzia Februari 23 mwaka huu jana jijini Dar es salaam wakati wa kufunga mafunzo ya wadadisi hao.
  3
  Baadhi ya wadadisi wa Sensa ya Viwanda wakifuatilia hafla ya ufungaji wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kukusanya takwimu za Sensa ya Viwanda ya mwaka 2013 iliyofanyika jana katika Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika eneo la Changanyikeni jijini Dar es salaam.
  4
  Kamishna wa Viapo ambaye pia ni Mwanasheria wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Oscar Mangula akitoa ufafanuzi kwa wasimamizi na wadadisi wa Sensa ya Viwanda (hawapo pichani) kuhusu  Sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia Sensa ya Viwanda ya mwaka 2013 inayotarajia kufanyika nchi nzima kuanzia Februari 23, 2015.
  5
  Baadhi ya wadadisi wa Sensa ya Viwanda wakisaini fomu za viapo vyao mbele ya Kamishna wa Viapo Bw. Oscar Mangula (hayupo pichani) jana jijini Dar es salaam mara baada ya kuhitimu mafunzo  ukusanyaji wa takwimu  za Sensa ya Viwanda 2013 itakayofanyika Februari 23 mwaka huu.
  6
  Wadadisi wa Sensa ya Viwanda 2013 wakiapa mbele ya Kamishna wa Viapo  Bw. Oscar Mangula (hayupo pichani) jana jijini Dar es salaam mara baada ya kuhitimu mafunzo ya siku 14 ya kuwajengea uwezo wa ukusanyaji wa takwimu  za Sensa ya Viwanda 2013 itakayofanyika nchi nzima kuanzia Februari 23 mwaka huu
  .
  ……………………………………………………………………….
  Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
  SERIKALI imesema kuwa maandalizi ya Sensa ya Viwanda ya mwaka 2013 itakayofanyika nchi nzima kuanzia Februari 23 mwaka huu yamekamilika na  kuwataka wamiliki wa viwanda na wadau mbalimbali kutoa ushirikiano kwa wadadisi watakaopita katika maeneo yao kukusanya takwimu wakati wa Sensa hiyo.
  Akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo na kuwaapisha wasimamizi na wadadisi wa Sensa ya Viwanda ya mwaka 2013 iliyofanyika katika Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika jana jijini Dar es salaam ,  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa alisema kuwa maandalizi ya awali ya Sensa hiyo yamekamilika yakihusisha uhamasishaji wa ushiriki wa wenye viwanda kwenye Sensa hiyo, utoaji wa elimu kwa wadadisi na wasimamizi watakaoendesha zoezi hilo.

  Alisema kuwa kutokana na umuhimu wa Sensa hiyo  wamiliki wa viwanda katika maeneo mbalimbali watashiriki kutoa takwimu zitakazojazwa katika madodoso maalum yaliyoandaliwa  ili kuliwezesha taifa kuweka Sera na mipango ya maendeleo inayotokana na takwimu sahihi za viwanda vilivyopo nchini.

  Aliongeza kuwa mafanikio ya Sensa hiyo yatatokana na wamiliki wa viwanda kutambua na kuithamini  Sensa hiyo kwa kutoa ushirikiano wa kuwapatia  takwimu sahihi wadadisi watakaopita katika maeneo yao kukusanya taarifa zinazohusu masuala mbalimbali yakiwemo ya uzalishaji wa bidhaa na masuala ya ajira;

  Dkt. Chuwa alibainisha kuwa upatikanaji wa takwimu sahihi kuhusu Sekta ya Viwanda nchini Tanzania utaiwezesha Serikali kutambua mchango wa viwanda katika ajira, uzalishaji na pato la taifa hivyo kuweka Sera na mipango endelevu ya maendeleo itakayoliwezesha taifa na sekta hiyo  kupiga hatua kimaendeleo.

  “Sensa hii ya viwanda ni muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu, na mafanikio yake yatatokana na wenye viwanda kutupa ushirikiano maana bila  wao kutoa takwimu sahihi mipango ya maendeleo kuhusu viwanda haitatekelezeka kwa sababu ya kukosa takwimu sahihi” Amesisitiza Dkt. Chuwa.

  Kuhusu wasimamizi na wadadisi  watakaoendesha zoezi hilo  litakalofanyika kwa muda wa miezi 3, Dkt. Chuwa aliwataka wafuate  sheria, taratibu na kanuni zilizowekwa  ili kuwezesha upatikanaji wa takwimu bora.

  Naye Mkurugenzi wa shughuli za Takwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Aldegunda Komba akizungumza na wadadisi hao alisema kuwa wadadisi hao wamepewa dhamana kubwa ya kutimiza lengo liliowekwa na Serikali la kuwa na takwimu sahihi kuhusu mchango wa viwanda katika maendeleo ya taifa.

  “Mafunzo tuliyowapatia  kwa vitendo na nadharia yamewajengea uwezo wa kukusanya takwimu bora, tunaomba zoezi hili mlifanye vizuri tunatarajia mtaitumia vizuri elimu mliyoipata kwa kufanya kazi kwa umakini mkubwa kwa manufaa ya taifa letu”. Amesisitiza Bi. Komba.

  Aidha, alibainisha kuwa kukamilika kwa Sensa hiyo kutaliwezesha taifa kutambaua mchango wa Sekta ya Viwanda katika uchumi na pato la taifa. Kwa upande wake Kamishna wa Viapo ambaye pia ni Mwanasheria wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Oscar Mangula akizungumza na wasimamizi na wadadisi wa Sensa hiyo aliwataka kuzingatia  Sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia zoezi.

  Alisema kuwa zoezi hilo litapata mafanikio makubwa kufuatia wadadisi na wasimamizi hao kuzingatia mafunzo na taratibu walizoelezwa huku akibainisha kuwa sheria  itachukua mkondo wake kwa wote watakaoshiriki kwa namna yoyote ile kuvuruga zoezi hilo.

  “Napenda niwaeleze kwamba zoezi hili ni muhimu sana kwa uchumi wa taifa,nawaomba mzingatie yote mliyoambiwa mtakapokuwa mnakusanya takwimu, zingatieni uadilifu na utunzaji wa takwimu mtakazopata kwa kuhakikisha mnaziwasilisha kwa wahusika kwa mujibu wa sheria na si vinginevyo” Alisisitiza.

  0 0

   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akimvisha joho Kamanda wa vijana mkoa wa Kagera Dioniz Malinzi .
    Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akimkabidhi mkuki   Kamanda wa vijana mkoa wa Kagera Dioniz Malinzi wakati wa kumsimika kwenye uwanja wa Uhuru Platform maarufu kama uwanja wa Mayunga.
   Saida Karoli akitumbuiza wakati wa sherehe hizo za usimikwaji wa kamanda wa vijana Dioniz Malinzi kwenye uwanja wa Uhuru,Mayunga Bukoba mjini.
   Wananchi waliofurika kwenye uwanja wa Uhuru Platform ambapo Dioniz Malinzi alisimikwa ukamanda wa vijana mkoa wa Kagera
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wananchi wa Bukoba mjini kwenye uwanja wa Uhuru Platform kwenye sherehe za usimikwaji wa Kamanda wa Vijana mkoa wa Kagera Dioniz Malinzi.

   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimia wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Uhuru ambapo shughuli za kumsimika Dioniz Malinzi kuwa kamanda wa vijana wa mkoa wa Kagera.

   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akimtuza mtoto Amina Mbaraka Chilusadi aliyekuwa akicheza pamoja na Saida Karoli.

   Bibi akisikiliza hotuba kwa makini.
   Boda Boda  wakiongoza msafara wa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kuelekea katika Uwanja wa Mayunga Uhuru Platform tayari kwa kumsimika Kamanda wa Vijana mkoa wa Kagera Dioniz Malinzi
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (kulia) akiwasili uwanjani na gari ya wazi pamoja na Kamanda wa Vijana mkoa wa Kagera Dioniz Malinzi
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa Nape Nnauye akivishwa skafu mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Uhuru Platform tayari kwa shughuli ya kumsimika Kamanda wa Vijana wa CCM mkoa wa Kagera Dioniz Malinzi.

   
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  CONFERENCE THEME

  “The changing Accounting and Economic Landscape:  Opportunities and Challenges for the East African Community”.

  The 1st East Africa Congress of Accountants (EACOA) will be held  at AICC- Arusha- Tanzania from 5th to 7th March 2015.

  The objective of the conference is to create a forum for professional accountants in the region to interact, seek opportunities and to discuss issues impacting the accounting profession in the region.
  The conference is jointly organised by the Accounting Bodies in the Region: OPC Burundi ; Institute of Certified Accountants Kenya (ICPAK); Institute of Certified Accountants of Rwanda (ICPAR); National Board of Accountants and Auditors –Tanzania (NBAA);Institute of Certified Accountants of Uganda (ICPAU), NBAA is the host of the conference.

  Registration and Conference Fee

  Register and pay your fee before 2nd  March, 2015 
  Register and pay your fee before 2nd March, 2015 
  Conference fee: USD 400 or TZS 700,000
  For more details including registration forms please visit our website:
  www.nbaa-tz.org/eacoa.htm

  All enquiries should be addressed to:
  Executive Director,
  National Board of Accountants and Auditors,
  Mhasibu House,
  Bibi Titi Mohamed Street, 
  P.o Box 5128,
  Dar es Salaam, Tanzania 
  Tel:  +255-22 2211890/9
  Fax No. +255 22 2151746
  E-mail: info@nbaa-tz.org
  Telegrams: “ NABAA” 
  Website: www.nbaa-tz.org


  0 0

    fredrick mwakalebela akizungumza na waandishi wa habari
   mwanahabari frank kibiki, aliyewahi kuwa katibu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (uvccm) ngazi ya wilaya kwa zaidi ya miaka 10 na ambaye ni mjumbe wa nec.
   fredrick mwakalebela akiwa na rais wa jamhuri ya muungano ya tanzania.

  na mwanahabari wetu fredy mgunda,iringa.

  wananchi na wananchama wa chama cha mapinduzi (ccm)wa manispaa ya iringa wameendelea na  sitofaham na ni mtu sahihi wa kugombea jimbo la iringa mjini kutokana na wagombea wengi kujitokeza katika harakati hizo.

  wakizun gumza kwa nyakati tofauti wananchi na wanachama hao wamesemakuwa kuna watu ambao tayari wamejijengea majini katika harakati hizo ambao na jesca msambatvangu,fredrick mwakalebela na mahamood madenge wote wanasadikika kuingia kwenye kinyang’anyilo hicho.

  ila mwanahabari frank kibiki, aliyewahi kuwa katibu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (uvccm) ngazi ya wilaya kwa zaidi ya miaka 10 na ambaye ni mjumbe wa nec ameonekana kuvurunga kabisa plani za wanachama kutokana na kuoneka ni kiongozi anayefaa kuigwa na kila lika inayomzunguka.

  wakizunguza kwa nyakati tofauti wanachama wa chama cha mapinduzi wamesema kuwa frank kibiki ndiye mtu pekee anayeweza kureta upinzani kwa mbunge wa jimbo hili mchungaji peter msigwa kutokana na kujiamini kwake.

  wameongeza kwa kusema kuwa  frank kibiki anaushawishi mkubwa kwa jamii tofauti na na watu wengine wanaopanga kugombea jimbo hilo kwa sababu anasiasa safi na sera ambazo zinatekelezeka  kulingana na mazingara ya wananchi wa manispaa ya iringa.

  pia waliongeza kuwa wananchi wanahamu ya kumfahamu frank kibiki kutokana na jina lake kukua kwa ghafla na kuwaguza wanachi wengi hivyo inapelekea siku hadi siku kumtafuta na kutaka kumjua yeye ni nani na anafanya nini.

  walimalizia kwa kusema kuwa kibiki ni mtu pekee ambaye anaweza kuwaweka wanachama cha mapinduzi pamoja kutokana na kutokuwa na kundi hata moja ndani ya chama tofauti na wagombea wanaotarajiwa kugombea jimbo hili.

  kwa upande wake katibu wa ccm mkoani iringa hassani mtenga alisema ipo siku kwenye kura za maoni watu watazimia hii ni kutokana na baadhi ya watu nwanaotarajia kugombea jimbo hili wamekuwa wakitumia pesa nyingi kuwaonga wananchi ili wamchague na akasisitiza kuwa uongozi sio pesa uongozi ni kipaji na uwezo wa mtu binafsi aliopewa na mungu.

  0 0

  Baadhi ya wazazi waliowaleta watoto wao kwa ajili ya zoezi la uandikishaji Vijana Kuingia NSSF- Real Madrid Sports Academy wakijaza na kuwasilisha fomu kwa wasimamizi wa zoezi hilo leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wazazi waliowaleta watoto wao kwa ajili ya zoezi la uandikishaji Vijana Kuingia NSSF- Real Madrid Sports Academy wakijaza na kuwasilisha fomu kwa wasimamizi wa zoezi hilo leo jijini Dar es Salaam.
  Zoezi la uandikishaji watoto watakaoshiriki kuingia katika NSSF- Real Madrid Sports Academy likiendeleajijini Dar es Salaam katika viwanja vya Karume. Zoezi la uandikishaji watoto watakaoshiriki kuingia katika NSSF- Real Madrid Sports Academy likiendeleajijini Dar es Salaam katika viwanja vya Karume.Zoezi la uandikishaji watoto watakaoshiriki kuingia katika NSSF- Real Madrid Sports Academy likiendelea jijini Dar es Salaam leo katika viwanja vya Karume. Zoezi la uandikishaji watoto watakaoshiriki kuingia katika NSSF- Real Madrid Sports Academy likiendelea jijini Dar es Salaam leo katika viwanja vya Karume.Mmoja wa wazazi waliowaleta watoto wao kwa ajili ya zoezi la uandikishaji Vijana Kuingia NSSF- Real Madrid Sports Academy pamoja na mwanae wakijaza fomu kwa wasimamizi wa zoezi hilo leo jijini Dar es Salaam. 
  Mmoja wa wazazi waliowaleta watoto wao kwa ajili ya zoezi la uandikishaji Vijana Kuingia NSSF- Real Madrid Sports Academy pamoja na mwanae wakijaza fomu kwa wasimamizi wa zoezi hilo leo jijini Dar es Salaam .


  Baadhi ya wazazi waliowaleta watoto wao kwa ajili ya zoezi la uandikishaji Vijana Kuingia NSSF- Real Madrid Sports Academy wakijaza na kuwasilisha fomu kwa wasimamizi wa zoezi hilo leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wazazi waliowaleta watoto wao kwa ajili ya zoezi la uandikishaji Vijana Kuingia NSSF- Real Madrid Sports Academy wakijaza na kuwasilisha fomu kwa wasimamizi wa zoezi hilo leo jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wazazi waliowaleta watoto wao kwa ajili ya zoezi la uandikishaji Vijana Kuingia NSSF- Real Madrid Sports Academy wakijaza na kuwasilisha fomu kwa wasimamizi wa zoezi hilo leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wazazi waliowaleta watoto wao kwa ajili ya zoezi la uandikishaji Vijana Kuingia NSSF- Real Madrid Sports Academy wakijaza na kuwasilisha fomu kwa wasimamizi wa zoezi hilo leo jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wazazi waliowaleta watoto wao kwa ajili ya zoezi la uandikishaji Vijana Kuingia NSSF- Real Madrid Sports Academy wakijaza na kuwasilisha fomu kwa wasimamizi wa zoezi hilo leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wazazi waliowaleta watoto wao kwa ajili ya zoezi la uandikishaji Vijana Kuingia NSSF- Real Madrid Sports Academy wakijaza na kuwasilisha fomu kwa wasimamizi wa zoezi hilo leo jijini Dar es Salaam.Moja ya banda linaohusika kusajili kushiriki katika zoezi la uandikishaji watoto watakaoshiriki kuingia katika NSSF- Real Madrid Sports Academy wakiendelea jijini Dar es Salaam leo katika viwanja vya Karume. Moja ya banda linaohusika kusajili kushiriki katika zoezi la uandikishaji watoto watakaoshiriki kuingia katika NSSF- Real Madrid Sports Academy wakiendelea jijini Dar es Salaam leo katika viwanja vya Karume.Baadhi ya watu waliojitokeza kushiriki katika zoezi la uandikishaji watoto watakaoshiriki kuingia katika NSSF- Real Madrid Sports Academy wakiendelea jijini Dar es Salaam leo katika viwanja vya Karume. Baadhi ya watu waliojitokeza kushiriki katika zoezi la uandikishaji watoto watakaoshiriki kuingia katika NSSF- Real Madrid Sports Academy wakiendelea jijini Dar es Salaam leo katika viwanja vya Karume.

   Na Mwandishi Wetu  

  SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kushirikiana na klabu maarufu duniani ya mpira wa miguu ya Real Madrid ya Hispania, leo imeendelea na zoezi lake la usajili wa vijana walio na umri wa chini ya miaka 14 watakaofanyiwa majaribio kwa ajili ya kujiunga na kituo cha michezo cha NSSF-REAL MADRID SPORTS ACADEMY katika uwanja wa Karume mjini Dar es Salaam, huku idadi ya vijana wanaojisajili ikiongezeka. 

   Mchakato huo wa usajili ulianza Oktoba 14 lakini leo idadi ya vijana wanaojitokeza ikiongezeka kwa kasi ambapo jumla ya vijana 257 wamejitokeza kuandikiswa katika viwanja vya karume jijini Dar es Salaam. Akizungumzia zoezi hilo kwa wanahabari katika viwanja vya Karume, Kaimu Meneja Kiongozi wa Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja, Salim Khalfan Kimaro wa NSSF, alisema uandikishaji wa vijana katika zoezi hilo leo umeongezeka kutokana na idadi kubwa kujitokeza kuandikishwa. 

  Akitoa ufafanuzi zaidi Kimaro alisema watoto walengwa ni wale waliozaliwa kuanzia Januari, 2001 hadi Disemba, 2003 na ili mtoto aandikishwe anatakiwa kuambatana na mzazi wake au mlezi anayetambulika kisheria na aje na nyaraka za uthibitisho wake kuwa ni mlezi halali kwa kuonesha vithibitisho vya kisheria. 

   “…Kwa mtoto husika, aje na cheti halisi cha kuzaliwa na kopi yake pamoja na picha ndogo (passport size) zenye rangi ya bluu. Zoezi hili litaendelea tena wiki ijayo tarehe 21 na 22 Februari ambapo baada ya hapo michezo ya majaribio itaanza wiki zinazofuatia,” alisema Khalfan Kimaro. 

  Aidha aliongeza kuwa watoto 30 watakao fuzu kuingia katika kituo cha mafunzo wataandaliwa mazingira kuhakikisha wanaendelea kupata elimu bila kikwazo chochote. Alisema Shirika la NSSF linatoa wito kwa wazazi na walezi kujitokeza kuwaleta watoto wao kujiandikisha ili kuendeleza vipaji vyao kwa fursa iliyotolewa.

  0 0

  Image result for WIZARA YA ARDHI

  Watu wengi wamenunua viwanja/nyumba lakini mali hizo zimeendelea kubaki katika majina ya waliowauzia. Wapo ambao imepita hata miaka kumi tangu wanunue maeneo lakini bado hawajabadili jina kuingia jina lake. Zipo sababu nyingi zinazosababisha hali hiyo lakini moja ni watu kutokujua umuhimu wa kubadili jina kwa haraka. Hapa sizungumzii tu kubadili jina isipokuwa nazungumzia kubadili jina kwa haraka. Kupitia makala haya napenda kuwaamsha watu kuhusu umuhimu mkubwa wa kubadili jina kwa haraka iwapo umenunua nyumba/kiwanja kwa mtu. Ni muhimu sana kufanya hivyo na itakuepusha na mambo mengi.

  1.KAMA HUJABADILI JINA ALIYEKUUZIA BADO NDIYE MMILIKI.

  Ikiwa kutatokea mgogoro wa umiliki wakati ambao umenunua nyumba/kiwanja na hujabadili jina kwenda kwenye jina lako kuna hatari kubwa zaidi ya kupoteza ulichonunua. Hii ni kutokana na ukweli kuwa utapokuwa unatatuliwa mgogoro wa nani mmiliki swali la kwanza huwa ni nani ambaye nyaraka ya umiliki ina jina lake.

  Yule ambaye jina lake linaonekana kwenye hati au leseni ya makazi ndiye hupewa kipaumbele na kwa mujibu wa sheria mwenye jina kwenye hati au leseni ya makazi ndiye mmiliki. Wewe uliyenunua utakuwa na mkataba na jina lako litakuwa kwenye mkataba lakini pamoja na kuwa na jina kwenye mkataba bado huwezi kulinganisha mkataba na hati au leseni ya makazi. Jina linalotokea kwenye hati au leseni ya makazi huwa na nguvu zaidi kuliko lile la kwenye mkataba.


  0 0
 • 02/15/15--21:38: TAUSI LIKOKOLA
 • Tausi Likokola was the first high fashion model to cross over international modeling industry on the 90's with credits from fashion houses such as Gucci, Christian Dior, Issey Miyake, Tommy Hilfger, Escada etc. Tausi also covered numerous fashion magazines and inspired many current models like Flaviana Matata, Millen Magesa, Herieth Paul and others around the globe. Tausi used her name to help her own people in Tanzania in education, HIV/AIDS awareness and positively contributed to Tourism in her country of birth Tanzania as well as business sector and natural resources.

  Tausi withdrew from working actively in the fashion industry to raise a family of her own. Her life journey has taken her from Africa, Europe, Asia, Australia and current in the USA where she calls home. Tausi has published four books and is using her internationally gained experience to work with young girls globally to empower them to full potential. 

  After a decade, Tausi is revisiting her home country Tanzania where she is planning to reconnect with charitable Organizations, visit her first home, schools as well as introducing her perfume ' Tausi Dreams' as first product in a series of other products to follow. Tausi is also scheduled to meet with both political and business leaders to see how further to help her country. Tausi will be escorted with a U.S. based finance managing company Spearpoint with the best investment interests to Tanzania.

  Tausi will arrive at Dar-es-salaam international airport on Friday February 20th 2015.

  For further questions and details please contact;  0 0

   
   Abiria wakishuka toka kwenye ndege mpya ya Shirika la Ndege la Taifa, Air Tanzania (ATCL) aina ya CRJ-100 yenye uwezo wa kubeba abiria 50 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakitoa mkoani Kigoma. Huo ukiwa ni mkakati wa kimaendeleo wa shirika hilo katika kuongeza idadi ya ndege na safari zake. Picha na mpiga picha wetu.
  Meneja wa Air Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Bw James Mbago akizungumza na waandishi wakati wa uzinduzi wa ndege mpya ya shirika hilo aina ya CRJ-100 yenye uwezo wa kubeba abiria 50, mara baada ya ndege hiyo kutua ikitokea mkoani Kigoma. Huo ukiwa ni mkakati wa kimaendeleo wa shirika hilo katika kuongeza idadi ya ndege na safari zake

  SHIRIKA la ndege la Taifa (ATCL) mwishoni mwa wiki iliyopita lilizindua ndege yake mpya aina ya CRJ-100 yenye uwezo wa kubeba abiria 50 ikiwa ni sehemu ya mpango wa shirika hilo kuongeza idadi ya ndege zake sambamba na kuongeza idadi ya safari zake.

  Shirika hilo ambalo kwa sasa linalotoa huduma zake katika mikoa ya Dar es Salaam, Kigoma, Mtwara na visiwa vya Komoro limejipanga kufanya safari za kila siku kati ya mikoa ya Dar es Salaam na Kigoma huku pia likiwa tayari kufanya safari za Mtwara na visiwa vya Komoro mara sita kwa wiki katika siku za Jumatatu, Alhamisi na Jumamosi.

  Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam mara tu baada ya ndege hiyo kutua kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Meneja wa shirika hilo katika kiwanja hicho, James Mbago alisema ndege hiyo imekodiwa kutoka nchini Afrika Kusini kwa jitihada za Serikali ya Tanzania na sasa ipo tayari kuwahudumia wateja wa shirika hilo.

  “Kuja kwa ndege hii kunaongeza idadi ya ndege zetu hadi kufikia mbili na tunashukuru kuona kwamba imepokelewa vizuri na abiria wetu. Ndege yetu nyingine aina ya De-Havilland Dash 8 Q300 kwa sasa inapata matengenezo makubwa kwenye karakana yetu iliyopo hapa hapa uwanja wa ndege,’’ alisema Mbago.

  Kwa mujibu wa Mbago kupona kwa ndege hiyo inayofanyiwa matengenezo kiwanjani hapo kutalifanya shirika hilo lianzishe tena  safari zake za ndani kwa mikoa ya Mwanza, Tabora, Arusha na Mbeya.

  “Muda si mrefu mambo yatakuwa mazuri zaidi…inafurahisha zaidi tunapopata mrejesho mzuri kutoka kwa wateja wetu wanaofurahia huduma za shirika lao mama,’’ aliongeza Mbago. Zaidi, Mbago aliongeza kuwa shirika lake linatarajia ongezeko kubwa la abiria kutokana na ukweli kuwa ndege yao hiyo mpya ina uwezo wa kusafiri kwa haraka zaidi ikilinganishwa na ndege nyingine huku safari zake zikiambatana na huduma nzuri inayotolewa kwa wateja wake.

  Wakizungumza mara tu baada ya kushuka kwenye ndege hiyo, baadhi ya abiria waliotoka Kigoma walisema licha ya kutumia muda mfupi zaidi lakini pia walifurahia huduma nzuri walizozipata kutoka kwa wahudumu wa ndege hiyo.

  “Kwa kweli hii ilikuwa ni moja ya safari zangu za ndege ambayo nimeifurahia sana. ATCL wanahitaji pongezi kwenye hili na zaidi wafikirie kuboresha huduma zaidi ya hapa…sisi abiria tupo tayari kuwaunga mkono kwa sababu ndio wanabeba nembo ya taifa letu,’’ alisema mmoja wa abiria hao aliyejitambulisha kwa majina Gaudence Kashoka.

  0 0

  Mwenyekiti wa muda wa Chama cha Bloggers Tanzania (TBN), Joachim Mushi (kulia) akikabidhi ubani wa fedha shilingi 900,000 na kutoa pole kwa mwanamziki mkongwe, John Kitime (kushoto) ambaye amefiwa juzi na mkewe, tukio hilo lilifanyika jana Kimara eneo la Nguzo ya 800, jijini Dar es Salaam. Mzee Kitime ni mwanachama wa TBN. Mwenyekiti wa muda wa Chama cha Bloggers Tanzania (TBN), Joachim Mushi (kulia) akikabidhi ubani wa fedha shilingi 900,000 na kutoa pole kwa mwanamziki mkongwe, John Kitime (kushoto) ambaye amefiwa juzi na mkewe, tukio hilo lilifanyika jana Kimara eneo la Nguzo ya 800, jijini Dar es Salaam. Mzee Kitime ni mwanachama wa TBN.Mwenyekiti wa muda wa Chama cha Bloggers Tanzania (TBN), Joachim Mushi (kulia) akitoa ujumbe wa pole kwa John Kitime na waombelezaji mara baada ya kukabidhi ubani wa fedha zilizotolewa na wanachama wa TBN jana eneo la Kimara Nguzo ya 800 jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wajumbe wa TBN walifika kumfariji Kitime ambaye pia ni mwanachama wa TBN. Mwenyekiti wa muda wa Chama cha Bloggers Tanzania (TBN), Joachim Mushi (kulia) akitoa ujumbe wa pole kwa John Kitime na waombelezaji mara baada ya kukabidhi ubani wa fedha zilizotolewa na wanachama wa TBN jana eneo la Kimara Nguzo ya 800 jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wajumbe wa TBN walifika kumfariji Kitime ambaye pia ni mwanachama wa TBNBaadhi ya wajumbe wa TBN, wakiwa katika picha na mzee Kitime walipofika kumfariji na kutoa ubani wa TBN. Kutoka kushoto ni Sufian na Othman Michuzi pamoja na Mzee Kitime. Baadhi ya wajumbe wa TBN, wakiwa katika picha na mzee Kitime walipofika kumfariji na kutoa ubani wa TBN. Kutoka kushoto ni Sufian na Othman Michuzi pamoja na Mzee Kitime.Kutoka kushoto ni mjumbe mshauri na Kiongozi wa TBN, Issa Michuzi, baadhi ya wanamuziki wa bandi ya Njenje, Mwenyekiti wa TBN, Mzee Kitime na mwanae akipata picha na baadhi ya waombolezaji marafii waliofika kumfariji. Kutoka kushoto ni mjumbe mshauri na Kiongozi wa TBN, Issa Michuzi, baadhi ya wanamuziki wa bandi ya Njenje, Mwenyekiti wa TBN, Mzee Kitime na mwanae akipata picha na baadhi ya waombolezaji marafii waliofika kumfariji.Baadhi ya wanamuziki wa Njenje pamoja na wajumbe wa Chama cha Bloggers Tanzania (TBN) wakipata picha ya pamoja na mfiwa mwanamziki mkongwe, John Kitime walipofika msibani kumfariji jana Kimara eneo la Nguzo ya 800, jijini Dar es Salaam. Mzee Kitime ni mwanachama wa TBN. Baadhi ya wanamuziki wa Njenje pamoja na wajumbe wa Chama cha Bloggers Tanzania (TBN) wakipata picha ya pamoja na mfiwa mwanamziki mkongwe, John Kitime walipofika msibani kumfariji jana Kimara eneo la Nguzo ya 800, jijini Dar es Salaam. Mzee Kitime ni mwanachama wa TBN.

  0 0

  1Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF Mzee Emannuel Humba akionyesha tuzo yake aliyopewa na mfuko huo kwa kutambua mchango wake akiwa mwanzilishi wa mfuko huo wakati wa hafla ya kuwaaga viongozi na wafanyakazi wastaafu iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee mwishoni mwa wiki , Mzee Emannuel Humba aliwaasa wafanyakazi wa mfuko huo kushikamana na kufanya kazi kwa kujituma ili kuhakikisha mfuko huo unafikia malengo, Katika hafla hiyo Emanuel Humba pia amezawadiwa zawadi mbalimbali. wa pili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF Balozi Ali Mchumo na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo Bw. Michael Mhando.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE)2Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF akitoa shukurani zake kwa uongozi wa NHIF na wafanyakazi kwa ujumla kwa kuwaadalia hafla hiyo ya kuwaaga.3Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF akipokea shada la maua kutoka kwa Balozi Ali Mchumo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF.4 Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti akizungumza katika hafla hiyo wakati akielezea wasifu wa baadhi viongozi wastaafu wa mfuko.
  huo.6Dr Marqus Kalinga Mstaafu wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa akipokea tuzo yake kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF Balozi Ali Mchumo, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Michael Mhando7Athman Rehani Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) akisoma wasifu wa mmoja wa wastaafu.8Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF Balozi Ali Mchumo akikabidhi zawadi kwa mstaafu Andrew Mwilungu aliyekuwa meneja wa NHIF Pwani.10Mstaafu Peter Daniel akitoa shukurani zake mara baada ya kukabidhiwa zawadi zake katika hafla hiyo ya kuwaaga wastaafu wa Mfuko wa Bima Afya ya Taifa, kutoka kushoto wanaofurahia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Michael Mhando12Baadhi ya wafanyakazi wakijadili jambo wakati wa hafla hiyo.13Wafanyakazi wakiwa na nyuso za furaha1416Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Michael Mhando akizunguma katika hafla hiyo.1718Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Michael Mhando kushoto akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Balozi Ali Mchumo kulia na Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti20Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti, Othman Rehani Mkurugenzi wa Afya ya Jamii CHF na Mkurugenzi wa Tiba na Masuala ya Kiufundi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dk.Frank Lekey wakipitia makabrasha wakati wa hafla hiyo.21Balozi Ali Mchumo Akisalimiana na Mkurugenzi Mstaafu wa NHIF Bw. Emannuel Humba.22Balozi Ali Mchumo Mwenyekiti wa Bodi Akiwasili ukumbini hapo huku akiwa ameongozana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu Bw. Michael Mhando.23Baadhi ya wafanyakazi wakimpokea mwenyekiti wa Bodi.24Hapa wakiserebuka kidogo2526Wafanayakzi wakiwa wamejipanga huku wakifurahia jambo wakati wa mapokezi ya viongozi na wafanyakazi wastaafu wakati walipowasili kwenye ukumbi wa Diamond tayari kwa hafla hiyo27 
  Mzee Emanuel Humba pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wakiinga ukumbini hapo huku wakipokelewa na wafanyakazi. 29 
  Baadhi ya maofisa 30 Grace Michael kushoto Hawa Katikati na Catherin wakipozi kwa picha32Wafanyakazi hao wakimpelekea keki Kaimu Mkurugenzi mkuu NHIF Bw. Michael Mhando.33 
  Balozi Ali Mchumo Mwenyekiti wa Bodi akimpongeza Kaimu Mkurugenzi Mkuu Bw. Michael Mhando pamoja na baadhi ya wafanyakazi.31 
  Kutoka kushoto Maofisa wa NHIF Sabina Komba na Luhende Singu wakiwaongoza maofisa wenzao kufungua Shampeni wakati wa hafla hiyo.

  0 0

  index
  Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linapenda kutoa taarifa ya kifo cha Askari wake Praiveti Ahadi Mwaka Mwainyokole kilichotokea tarehe 4 Februari 2015 katika mji mdogo wa Mbalizi, Mkoani Mbeya.
   
  Taarifa za mazingira ya kifo cha Askari huyo zimepotoshwa na baadhi ya Vyombo vya Habari na kusababisha mapokeo tofauti kwa wananchi.
   
  Hali halisi ni kwamba, mnamo tarehe 4 Februari 2015 Askari huyo akiwa na Askari wenzake wanne (4) ambao ni Koplo Bedatu Benard Mloka, Praiveti Thani Hamisi Haji, Praiveti Mzee Buan Mzee na Praiveti Mohamed Juma walivamiwa na kundi la wahuni wakati wakitoka matembezini. Chanzo cha vurugu hizo ni kutokana na Praiveti Rashid Maulid wa Kikosi chao kuibiwa samani kwenye nyumba aliyokuwa amepanga uraiani katika mji mdogo wa Mbalizi, Kitongoji cha Shigamba. Samani alizoibiwa ni pamoja na TV aina ya LG “flat screen” “Inch 20”, radio aina ya Sony moja, Deck aina ya Sangsung, flash moja, extension cable moja na fedha taslimu Tshs 30,000/=.
   
  Askari huyo alitoa taarifa Kituo cha Polisi tarehe 03 Februari 2015 na kupatiwa RB yenye Nambari MBI/RB/285/2015, sambamba na kutoa taarifa Polisi. Kituo hicho cha Polisi kilitoa askari mmoja ambae aliungana na askari Jeshi na wenzake na wakaenda eneo la relini ambako vijana wasio na ajira maalumu hushinda. Waliwakamata vijana saba, mmoja wa vijana hao alikimbia na kwenda kuwapa taarifa wenzao ambao hawakuwepo katika eneo hilo ambapo vijana  sita walifikishwa kituo cha Polisi.
           
  Ilipofika saa tatu usiku askari hao wakiwa katika matembezi ya kawaida walikutana na  kundi la vijana wakiwa na silaha mbalimbali kama nondo na marungu ambao walianza kuwa shambulia huku wakiwashutumu kuwa waliwapeleka wenzao Polisi.
   
  Kwa kuwa kundi la vijana hao lilikuwa kubwa na likiwa na silaha zilizotajwa lilifanikiwa kuwajeruhi,   Askari hao akiwemo Praiveti Ahadi Mwainyokole ambae alijeruhiwa vibaya. Askari hao walikwenda Polisi na wakachukuwa PF3 na kisha kwenda katika hospitali ya Jeshi Mbeya baadaye Praiveti Mwainyokole alifariki muda mfupi baada ya hali yake kutokuwa nzuri kutokana na kupigwa na kitu kizito kichwani hali iliyosababisha damu kuvia kwenye Ubongo.
   
  JWTZ linasikitishwa na mauaji hayo yaliyofanywa kwa Askari wake, na mauaji ya askari wengine katika  maeneo ambako vitendo kama hivyo vimetokea. Ikumbukwe kuwa JWTZ lipo kwa ajili ya usalama na ustawi wa wananchi, hivyo JWTZ linalaani vitendo viovu vinavyofanyika kwa askari wake na linatoa rai kwa vyombo vya sheria kuchukua mkondo wake.
   
  Kimsingi JWTZ halina ugomvi na wananchi kwani kazi yake ya msingi ni kuwalinda ili waweze kutekeleza majukumu yao ya kimaendeleo kwa utulivu na amani kwa ajili ya ustawi wa Taifa letu.
   
  Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Mahusiano
  Makao Makuu ya Jeshi,Upanga

  0 0

  SAM_1097
  Kushoto ni Mkuu wa vipindi vya Radio 5 Mathew Philip na Ashura Mohamed wakiwa katika picha ya  pamoja na wanafunzi wa sekondari walioshiriki katika maadhimisho hayo ya Radio duniani.
   
  Akizungumza na waandishi wahabari hivi karibuni Mkuu wa vipindi wa Radio 5 Bw.Mathew Philip alisema maadhimisho hayo yalidhaminiwa na kituo hicho pamoja na Farm Radio, ikiwa ni kuhadhimisha siku ya Radio duniani ambapo ilifanyika  tarehe 13/2/2015 jijini Arusha.
   
  Bw.Mathew alisema kuwa wakulima pamoja navijana wa kanda ya kaskazini wakiwemo wanafunzi wa shule za sekondari,walipatana  fursa ya kutembelea kituo hicho na kuona namna inavyoendesha vipindi vyake ikiwemo kipindi cha afya ya akili kwa vijana(Positive mood),Fahari yangu kipindi kinacho wagusa wakulima 
   
  Alitoa wito kwa Radio zingine kuwa na utaratibu wa kuhadhimisha siku hiyo kwa kuwa itasaidia kuongeza uaminifu mkubwa na wasikilizaji kwa ujumla
  Kwa upande wake Mtaalamu wa mnyororo wa dhamani kwenye mauzo ya kilimo kutoka Asasi isiyokuwa ya kiserikali la Farm Radio Bw.Terevael Aremu alisema kuwa lengo la kufanya hivyo ni kusisitiza jamii kusikiliza radio hasa vipindi vya elimishi vinavyopatikana katika vituo vya radio hapa nchini na Afrika.
   
  Aidha alisema kuwa Jamii hasa wakulima wakisikiliza radio watapata elimu na taarifa mbalimbali za kile wanachokiitaji kwa wakati sahihi ikiwemo taarifa za hali ya hewa.(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog).
  SAM_1092
  Wakulima pamoja na vijana kanda ya kaskazini wakiwa katika majadiliano mara baada ya kufanya ziara katika kituo cha Radio 5 nakuona namna inavyoendesha vipindi vyake katika maadhimisho siku ya radio duniani iliyofanyika 13/2/2015 jijini Arusha.
  SAM_1093
  Mkuu wa vipindi vya radio 5 Mathew Philip akiteta jambo na mkulima aliyefika katika maadhimisho hayo.
  SAM_1089
  Mtaalamu wa mnyororo wa dhamani kwenye mauzo ya kilimo kutoka Asasi isiyokuwa ya kiserikali la Farm Radio Bw.Terevael Aremu akizungumza katika maadhimisho hayo
  SAM_1091
  Wafanyakazi wa kituo cha radio 5 wakiwa wanafurahia jambo.
  SAM_1105
  Watangazaji mahiri wa kituo cha radio 5 wakiwa katika pozi Semio Sonyo kushoto,katikati Mwangaza Jumanne na Linus Kilembu
  SAM_1102
  Kulia Hilda Kinabo na Semio Sonyo watangazaji wa Radio 5
  SAM_1100SAM_1099
  Mkuu wa vipindi vya radio 5 Mathew Philip pamoja na Mtangazaji Linus Kilembu wakiwa katika majadiliano
  SAM_1109
  Mtangazaji mahiri wa kituo cha Radio 5 Tonnie Kaisoi katika pozi
  Kituo cha Radio 5 chenao yake makuu jijini Arusha imeadhimisha siku ya Radio duniani kwa kuwakutanisha wakulima  na vijana kanda ya kaskazini ikiwa nikuhamasisha vijana kujieleza namna Radio hiyo imesaidia katika kukuza uchumi,kijamii,kisiasa na kiutamaduni.
   

  0 0

  1 
  Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya PSPTB, Bw, Aziz Kilonge akifungua mafunzo ya Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi yaliyofanyika mwishoni mwa wiki kwa kutoa mafunzo kwa walimu ,wataalam wanaosimamia wanafunzi wa fani ya ununuzi na ugavi wanaofanya tafiti kama sehemu ya mafunzo yao ya stashahada ya ununuzi na ugavi mafunzo hayo yamefanyika kaktika ukumbi baraza la Maaskofu TEC jijini Dar es salaam.
  4Wataalamu hao wakiandika mambo muhimu wakati wa mafunzo hayo.57 
  Bw. Godfrey Mbanyi Mkurugenzi wa Mafunzo PSPTB akiandaa mada katika kompyuta yake wakati wa mafunzo hayo. 9 
  Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya PSPTB, Bw, Aziz Kilonge akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu hao mara baada ya kufungua rasmi mafunzo hayo.
  ..................................................................................
  Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi imeendesha mafunzo kwa walimu ,wataalam wanaosimamia wanafunzi wa fani ya ununuzi na ugavi wanaofanya tafiti kama sehemu ya mafunzo yao ya stashahada ya ununuzi na ugavi.Mafunzo hayo yalifunguliwa jana, na mjumbe wa bodi ya wakurugenzi, Bw, Aziz Kilonge, ambaye aliwaasa wataalam hao kuhakikisha kwamba wanasimamia wanafunzi kwa ukamilifu ili kuongeza ubora wa kazi za utafiti zinazofanywa. 

  Aidha, alifafanua kuwa uzingatiaji wa maadili katika kufanya tafiti, ndio msingi na matakwa ya Bodi, ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanafanya tafiti na sio kuchukua kazi zilizofanywa na wanafunzi/watafiti wengine au kufanyiwa na watu wengine.

   Pamoja na kuwajengea uwezo wa kufanya tafiti, pia wanafunzi wanajengewa uwezo wa kuandika ripoti na hata kuwasilisha ripoti katika sehemu zao za kazi. Hivyo lengo kuu ni kuwejengea uwezo wa kutoa huduma bora kwa taifa.Aliwakumbusha wasimamizi hao kuwajengea wanafunzi hao uwezo wa kujiamini na kujieleza kwani ufaulu wa mwanafunzi, unategemea sana uwezo wake wa kuitetea kazi yake, ambapo katika mtihani huo mwanafunzi atawasilisha kazi yake mbele ya wataalam, ili kupima uwezo wake.

  0 0

  FILAMU kubwa ya C.P.U Kitengo cha kutetea Watoto imeingia leo sokoni kwa njia ya mtandao, lengo likiwa ni kuwafikia watu wengi Ulimwenguni, hivyo kwa utaratibu wa kampuni ya usambazaji ya Proin Promotions ni kuuza katika mtandao baadae katika Dvd na njia nyingine.
  Leo Jumatatu tarehe 16.February. 2015 inapatikana mtandaoni unaweza kununua filamu hiyo kwa kutembelea www.proinpromotions.co.tz na kununua filamu ya C.P.U na filamu zingine za Proin Promotions utanunua na kuangalia full HD.
  Sinema ya C.P.U imeshirikisha wasanii zaidi ya 230 huku wasanii wakongwe wenye majina kama Kulwa Kikumba ‘Dude’ Dotnata, Richard Mshanga ‘Mzee Masinde’, Hashim Kambi ‘Ramsey’, Sauda Simba, Subira Wahure, steve Sandhu, Nkwabi Juma, Mohamed Funga funga ‘Mzee Jengua’ Mobby Mpambala wakiwa vinara wa sinema hiyo.

  C.P.U sinema ya kimataifa wiki ya pili itapatikana katika Dvd na kupatikana nchi nzima kutokana na mfumo mpya wa Proin Promotions kuuza kwa njia ya mtandao na wiki inayofuata utaweza kununua katika Dvd, NUNUA NAKALA YAKO HALALI YA C.P.U SASA!.

  0 0

  Naibu Waziri wa Maji ,Amos Makala akitembelea eneo la mradi mkubwa wa Maji unaojengwa katika kijiji cha Kirya wilayani Mwanga.
  Naibu waziri wa Maji Amosi Makala akizungumza jambo na meneja mshauri wa mradi Sharif Saleh mara baada ya kukagua mitambo maalumu kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi wa mradi huo.
  Naibu waziri wa Maji Amosi Makala akifurahia jambo na meneja mshauri wa mradi mkubwa wa maji wa Mwanga Korogwe Sharif Salehmara baada ya kuangalia maadalizi ya ujenzi wa mradi huo.
  Eneo la mradi mkubwa wa maji utakao saidia upatikanaji wa maji katika wilaya za Mwanga,Same na Korogwe .
  Eneo la Bwawa la Nyumba ya Mungu ambalo linatazamiwa kuwekwa mitambo kwa ajili ya uvutaji maji 
  Maeneo mbalimbali amabyo yanatazamiwa kufungwa mashine za kuvuta maji,matanki ya kuhifadhia pamoja na matanki ya dawa kwa ajili ya matibabu ya maji yanatazamiwa kuwekwa.
  Mkuu wa wilaya ya Mwanga Shaibu Ndemanga akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa maji Amosi Makala kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Kirya katika eneo la Njia Panda ulipo mradi huo.
  Baadhi ya wafanyakazi katka mradi huo wakimsikiliza mkuu wa Wilaya ya Mwanga ,Ndemanga.
  Baadhi ya wananchi katika kijiji cha Kirya.
  Naibu Waziri wa maji Amosi Makala akizungumza katika mkutano wake na wananchi wa Kijiji cha Kirya wilayani Mwanga .
  Baadhi ya viongozi walioambatana na Naibu waziri wa maji,Amosi Makala wakati wa ziara yake kutembelea katika eneo hilo kujionea maenedeleo ya ujenzi wa mradi.
  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Moshi.

  0 0
  0 0

  Bwana Harusi Maneno Abdallah na Mkewe Bi Nusrat Tahwa wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunga ndoa hapo jana
   Bwana harusi akielekea kuchukua jiko lake Kimara huku akisindikizwa na wapambe na Mshenga wake
   Dua ikiendelea nyumbani kwa Mwanamke Kimara kabla ya ndoa kufungwa na Maneno kuondoka na Jiko lake.
   Nderemo na vifijo 
  Mtu akilia mara baada ya dada yake kuchukuliwa 
   Kaswida maridhawa akipigwa na watoto wa madrasa
   Akifungishwa Ndoa hapo jana
   Baba wa bi harusi akitoa nasaha kwa watoto wake
  Akimfunua Mkewe mara baada ya kukabidhiwa rasmi hapo jana
  Mdau Maneno akiondoka na jiko lake kuelekea kwake Segerea mara baada ya kufunga ndo hapo jana.Picha na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

  0 0

  Taasisi ya Uongozi wa Afrika kwa Maendeleo Endelevu (UONGOZI Institute) imeandaa  mkutano  wa kikanda  utakaokutanisha viongozi na watunga sera  kutoka  nchi  za Afrika mashariki kuzungumzia changamoto za ukuaji wa miji na kushughulikia hali ya baadaye ya miji ya Afrika.

  Mkutano huu uliopewa jina la, ‘Maisha ya baadae ya nchi za Afrika Mashariki: Jinsi gani tunataka kuishi mwaka 2050’, utafanyika katika hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, Kilimanjaro Hotel tarehe 19 na 20 Februari ambapo Waziri Mkuu wa Tanzania, Mh. Mizengo Pinda (Mb), atakuwa mgeni rasmi.

  Afisa Mtendaji Mkuu wa UONGOZI Institute, Prof. Joseph Semboja alisema kwamba jukwaa hilo linalenga kuangalia na kujadili changamoto na fursa mbalimbali zinazoletwa na ukuaji wa miji  Afrika Mashariki na jinsi gani viongozi wa Afrika wanaweza kukabiliana nazo kwa pamoja. 

  “Kuna uwiano mkubwa wa ongezeko la watu Afrika (na duniani kwa ujumla) wanaoishi mijini na kupelekea msongamano na shinikizo la nyumba, ajira na huduma za kijamii. Ni kwa matokeo haya jukwaa hili limelenga kujadili namna ya kutatua changamoto hizo na kufikiria miji ambayo itatimiza matakwa yetu,” alisema Prof. Semboja. 

  Kwa mujibu wa chapisho la UN-Habitat  ‘Hali ya miji ya Afrika 2014’ , “Afrika Mashariki inashika nafasi ya chini katika miji inayokua duniani lakini ndiyo kanda inayoongoza katika kasi ya ukuaji wa miji yake hivi sasa.  Ifikapo mwishoni mwa muongo huu wa sasa idadi ya wakazi waishio mijini itaongezeka kwa asilimia 50 na jumla ya idadi ya wakazi wa mijini ifikapo mwaka 2040 inatarajiwa kuwa mara tano ya 2010.
  Hivyo basi, ukanda wa Afrika Mashariki utakumbwa na changamoto zitakazotokana na ongezeko kubwa la  idadi ya watu mijini; ongezeko kubwa la madai mapya na ya ziada kwa ajili ya utoaji wa nyumba za kutosha na kwa gharama nafuu na huduma mijini, na pengine muhimu zaidi, fursa ya kuzalisha kipato mijini.”

  “Ni dhahiri kwamba ukuaji wa miji na maendeleo mijini ni matokeo chanya ya maendeleo ya binadamu na ukuaji wa kiuchumi kama tunaweza kuyakabili kiusahihi. Na hii ndiyo maana nzima ya mkutano huu…Kutuweka katika njia sahihi kwa kutambua vipaumbele vya juu na vitu  muhimu kwa ajili ya maendeleo," aliongeza Prof. Semboja. 
  Washiriki wa kongamano hili watatoka: Burundi, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Somalia, Sudan ya Kusini, Tanzania na  Uganda. Waalikwa watakuwa wawakilishi wa ngazi za juu kutoka serikalini, mashirika ya kikanda na kimataifa, miji mikubwa, wasomi, sekta binafsi na asasi za kiraia.


  0 0

   Umati wa waombolezaji ulioshiriki kwenye mazishi ya Mke wa Mwanamuziki Mkongwe hapa nchini,Bw. John Kitime,Marehemu Janeth Joan Chidosa Kitime alizikwa leo kwenye makaburi ya Kinondoni,jijini Dar es salaam.
  Taratibu za mazishi zikiendelea kwenye makaburi ya Kinondoni,jijini Dar es salaam leo.
   Mume wa  Marehemu Janeth Joan Chidosa Kitime,Bw. John Kitime akitoka kuweka shada la maua kwenye kaburi la mkewe wakati wa mazishi yaliyofanyika jioni hii kwenye makaburi ya Kinondoni,jijini Dar es salaam.
  Watoto wa Marehemu wakielekea kuweka shada la maua kwenye kaburi la Mama yao.
   Mfiwa Bw. John Kitime katikati akiwa na Watoto zake mara baada ya Mazishi kwenye makaburi ya Kinondoni,jijini Dar es salaam.
   Wadau mbalimbali wakimfariji mfiwa,Mzee John Kitime mara baada ya mazishi kwenye makaburi ya Kinondoni,jijini Dar es salaam leo.
   Dada Nyota Waziri akimfariji Bw. John Kitime mara baada ya mazishi ya mkewe kwenye makaburi ya Kinondoni,jijini Dar es salaam.
   Anko Kidevu akimfariji rafiki yake Bw. John Kitime.
  Baadhi ya Wanachama wa TBN waliowakilisha kwenye mazishi ya mke wa mwanachama mwenzao,Bw. John Kitime kwenye makaburi ya Kinondoni,jijini Dar es salaam leo.kutoka kulia ni Cathbert Kajuna,Mkala Fundikira,Jennifer Livigha a.k.a ChingaOne,Ahmad na Othman Michuzi pamoja na Muhidin Sufiani.

  0 0


  Mkuu wa wilaya ya Mtwara Mh, Wilman Kapenjama akikabidi funguo ya gari kwa Mshindi wa Promosheni Airtel yatosha Zaidi mkoani Mtwara bw, Sefu Namtapika (60) ambae ni mwalimu mstaafu aliyeibuka na ushindi wa Toyota IST kupitia droo ya kwanza ya promosheni Yatosha zaidi inayoendesha na Airtel. Wanaoshuhudia makabidhiano hayo ni toka kushoto nyuma ni Meneja mauzo wa Airtel mkoa wa Mtwara Bw, Batlomeo Masatu, Afisa Masoko wa Airtel Bi Aminata Keita, na Meneja Biashara wa kanda ya Pwani Bw Albert Majuva.

  Meneja Biashara wa kanda ya Pwani Bw Albert Majuva (wakwanza kulia) akimpongeza Mshindi wa Promosheni ya Airtel yatosha Zaidi mkoani Mtwara bw, Sefu Namtapika ambae ni mwalimu mstaafu aliyeibuka na ushindi wa Toyota IST kupitia droo ya kwanza ya promosheni Yatosha zaidi inayoendesha na Airtel. Anaefuata ni Afisa Masoko wa Airtel Bi Aminata Keita na Meneja mauzo wa Airtel mkoa wa Mtwara Bw, Batlomeo Masatu wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika mkoani humo kwenye viwanja vya mashujaa mwishoni mwa wiki.

  Meneja uhusiano wa Airtel bw, Jackson Mmbando akiongoza umati wa wakazi wa mkoani mtwara waliojitokeza katika viwanja vya Mashujaa kushudia hafla ya makabidhiano ya gari Toyota IST kwa mshindi wa droo ya kwanza ya promosheni ya Airtel yatosha Mzee Sefu Namtapika mwishoni mwa wiki hii.

  Mshindi wa gari aina ya Toyota IST mzee Sefu Namtapika akipongezwa na mke wake Bi… mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake ya gari alilojishindia kupitia promosheni ya Airtel Yatosha zaidi. Hafla ya makabidhiano ilifanyika katika viwanja vya mashujaa mkoani mtwara mwishoni na wiki na kuhudhuriwa na mkuu wa wilaya ya Mtwara mjini mh, Wilman Kapenjama.


older | 1 | .... | 463 | 464 | (Page 465) | 466 | 467 | .... | 1897 | newer