Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel

Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels

Showcase

Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 462 | 463 | (Page 464) | 465 | 466 | .... | 1896 | newer

  0 0

  0 0

  1.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha ikulu mjumbe maalum wa Serikali ya Burundi Sheikh Mohamed Rukara ambaye aliwasilisha ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza leo jioni.Sheikh Mohamed Rukara ni Mkuu wa Utumishi katika serikali ya Burundi.
  2 
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribidhiwa ujumbe maalum Ikulu kutoka  Serikali ya Burundi Sheikh Mohamed Rukara ambaye aliwasilishakutoka kwa Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza leo jioni.Sheikh Mohamed Rukara ni Mkuu wa Utumishi katika serikali ya Burundi.(picha na Freddy Maro)

  0 0  Afisa Matekelezo Mwandamizi(SCO) wa mfuko wa Pensheni wa PSPF Bi. Matilda A. Nyallu  akitoa elimu ya Mpango wa Uchangiaji wa Hiari kwa Askari na watumishi raia makao makuu ya Wizara ya mambo ya ndani jijini Dar es Salaam
   
  Askari na watumishi raia wakifuatilia elimu hiyo iliyokuwa inatolewa na maafisa wa PSPF waliofika makao makuu ya Wizara ya mambo ya ndani kutoa elimu ya  Mpango wa Uchangiaji wa Hiari

  Mfuko wa penseni wa PSPF ulipata fursa ya kukutana na kutoa elimu kuhusu huduma mbalimbali wanazo zitoa na kuweza kuwapa maelezo ya baadhi  ya mafao yanayo tolewa kupitia  Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa (PSS)  kwa Askari na watumishi raia makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani jijini Dae es Salaam.

  Bi. Matilda A. Nyallu ambaye ni Afisa MatekelezoMwandamizi(SCO) wa mfuko wa PSPF  aliweza kutoa rai kwa Askari na watumishi raia wote waweze kujiunga na mfuko wa jamii wa PSPF ili kuweza kupata mafanikiona kunufaika , Pia alitoa mifano michache kwa ambao watajiunga .
   na mfuko huo ambapo kwa Askari na watumishi raia alitaja kuwa wanaweza kupata  mikopo ya kuanzia maisha ambayo itakuwezesha kupata nyumba ambazo wamezijenga kwa ajiri ya mtanzania aweze kununua au kukopeshwa na baadae kuweza kurejesha mkopo huo wa nyumba, pia aliongeza kwa kusema nyumba zote zimewekewa bima endapo tatizo lolote likitokea basi nyumba hizo zitakuwa salama.
  Hata hivyo afisa wa mfuko wa Pensheni Bw.hadji Jamadary aliweza kuwaasa na kuwasisitiza mambo mbalimbali yanoyo tekelezwa na mfuko na kuwataka wawe miongoni mwa watu wenye muamko wa kujiunga ili wengine waweze kuiga mfano kutoka kwao.
  Mfuko wa pensheni ni mfuko wa kijamii unao toa huduma na kukidhi mahitaji ya jamii paspo na gharama zinazo iumiza jamii , kujiunga na mfuko wa PSPF ndiko kutakako kuokoa katika kukuwekea dhamana ya maisha yako iwe ni katika elimu ,makazi,ugonjwa na hata ujasiliamali .Hata hivyo afisa wa mfuko wa Pensheni Bw.hadji Jamadary aliweza kuwaasa na kuwasisitiza mambo mbalimbali yanoyo tekelezwa na mfuko na kuwataka wawe miongoni mwa watu wenye muamko wa kujiunga ili wengine waweze kuiga mfano kutoka kwao.

  Mfuko wa pensheni ni mfuko wa kijamii unao toa huduma na kukidhi mahitaji ya jamii paspo na gharama zinazo iumiza jamii , kujiunga na mfuko wa PSPF ndiko kutakako kuokoa katika kukuwekea dhamana ya maisha yako iwe ni katika elimu ,makazi,ugonjwa na hata ujasiliamali
  .

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akisoma hotuba ya kufunga mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama Tanzania kwa kamati za maadili Mikoa ya Rukwa na Katavi na kufanyika Mjini Sumbawanga tarehe 12-13 Februari 2015. Katika hotuba yake hiyo ameiomba Serikali kutenga fedha ya kutosha ili mafunzo kama hayo yaweze kuwafikia watu wengi zaidi kwa ustawi wa Sheria na Haki nchini.

   Mafunzo hayo ni katika mkakati wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Tanzania kuimarisha tume za maadili nchini kusaidia maadili kwa watumishi wa Mahakama nchini. Kushoto ni Jaji Ferdinand Wambali muwezeshaji wa mafunzo hayo ambae ni Jaji wa Mahakama Kuu na Mkuu wa Chuo cha Mahakama Lushoto .
  Bi Enzel Mtei ambae ni miongoni mwa wawezeshaji wa mafunzo hayo kutoka Tume ya Mahakama Tanzania akimuwakilisha Mtendaji Mkuu wa Mahakama akizungumza muda mfupi kabla ya kuhitimishwa mafunzo hayo. Miongoni mwa maazimio yaliyofikiwa katika mafunzo hayo kwa wanakamati; Mihimili yote ya dola nchini ifanye kazi kwa pamoja ili kutoa haki kwa wakati, Amri halali itakayotolewa namamlaka husika iheshimiwe kuleta usawa wa kisheria nchini na Mahakimu pamoja na wadau wengine wa sheria wawe mfano kwa maadili bora katika jamii.
  Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa katikati na wajumbe wengine wakifuatilia mafunzo hayo.
   Wajumbe wa Kamati ya maadili Mikoa ya Rukwa na Katavi wakifuatilia mafunzo hayo.

   Wajumbe wa Kamati ya maadili Mikoa ya Rukwa na Katavi wakifuatilia mafunzo hayo.(Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa@Rukwareview.blogspot.com)

  0 0

   …NI ZOUK RHUMBA LENYE UTAMU WA MASAUTI
  Wala hakosei kusema ‘kujua kazi ni raha’. Isha Mashauzi anakushuka tena kivingine na wimbo mpya kabisa “Nimpe Nani” unaodhihirisha kuwa anaijua vema kazi yake.

  Hii ni ‘single’ yake ya pili nje ya taarab ukiacha ule wa kwanza “Nimlaumu Nani” uliopigwa katika miondoko ya rhumba. “Nimpe Nani” ni wimbo unaoelea kwenye miondoko ya zouk rhumba lakini ukikolezwa kwa mbali na vionjo vya mduara.

  Wimbo huo wa dakika tatu na nusu ambao umerekodiwa katika studio za C9 Records chini ya producer C9 Kanjenje. Kinanda kimepigwa na Kali Kitimoto na C9, magitaa ya bass na solo yamepigwa na Babu Bomba wa Malaika Band.

  Sauti zote tamu unazozisikia humo ni za Isha Mashauzi kasoro sehemu ndogo sana isiyozidi sekunde 5 iliyotikiwa na Easy Man.

  0 0

  3
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizindua Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 katika hafla iliyofanyika katika shule ya sekondari Majani ya Chai, Kipawa jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt.Shukuru Kawambwa, na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bwana Said Meck Sadik.
  1
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi Dkt.Shukuru Kawambwa, Naibu Waziri wa elimu na ufundi Kassim Majaliwa wakiangalia jaribio la Sayansi lililokuwa likifanywa na mwanafunzi katika shule ya sekondari ya kata ya Majani ya Chai huko Kipawa jijini Dar es Salaam.Awali Rais Kikwete alizindua maabara za sayansi katika shule hiyo na baadaye alizindua Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014.

  (picha na Freddy Maro)

  0 0

  Badhi ya wazazi wakiwasimamia watoto wao katika zoezi la kujaza fomu kwa ajili ya kujiunga na kituo kipya cha michezo cha NSSF-Real Madrid Academy. Badhi ya wazazi wakiwasimamia watoto wao katika zoezi la kujaza fomu kwa ajili ya kujiunga na kituo kipya cha michezo cha NSSF-Real Madrid Academy. 

  SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa kushirikiana na Klabu ya Real Madrid ya Hispania, limezindua mchakato wa usajili wa vijana walio chini ya umri wa miaka 14, watakaochujwa kusaka nafasi ya kujiunga na NSSF–Real Madrid Sports Academy.
  Mchakato huo wa usajili umefanyika leo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam, ambako watoto kutoka Manispaa za Ilala, Temeke na Kinondoni walisajiliwa na kuruhusiwa, zoezi linalotarajia kuendelea leo.
  Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori, aliwaka Watanzaia kuwaleta vijana wao katika mchakato huo, na kwamba hakutakuwa na urasimu utakaowakwamisha kusajiliwa.
  Magori alisema kuwa, jukumu la kama NSSF ni kuratibu usajili wa vijana wasiopungua 500, ambao watafanyiwa mchujo na Real Madrid kupata nyota 30 ambao wataingia rasmi katika darasa la kwanza kabisa la akademi hiyo inayosubiriwa kwa hamu nchini.
  “Wataalamu wanane wa lishe, tiba, afya na soka kutoka Madrid watatua nchini wiki ijayo, kuwafanyia mchujo vijana wapatao 500 tunaotarajia kuwasajili leo, kesho na wikiendi ijayo, ambao watafanya majaribio ya uwanjani Februari 28,” alisema Magori.
  Aliwataka wazazi na walezi wa watoto wenye vipaji, kuhakikisha wanatumia fursa ya kuwafikisha watoto wao kwenye usajili, ili kuwawezesha kupata nafasi ya kuwania kuingia miongoni mwa wakali 30 wa awali watakaofungua darasa la akademi hiyo.
  Alibainisha kuwa, kutokana na uharaka wa uanzishwaji wa kituo, NSSF na Real Madrid hawatoweza kutembelea mikoani kufanya usajili kama huo mwaka huu, badala yake akawataka wazazi wanaoweza kufika na watoto wao Dar es Salaam kufanya hivyo.
  Magori aliongeza kuwa, watoto watakaopata nafasi ya kuingia katika akademi yao watasoma na kujifunza soka, ambapo watakaozivutia timu mbalimbali barani Ulaya watauzwa na wale watakaokwama, watauzwa Afrika, ikiwamo kuunda timu ya NSSF.
  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo wakati wa uzinduzi wa mchakato wa usajili wa vijana walio chini ya umri wa miaka 14, watakaochujwa kusaka nafasi ya kujiunga na kituo kipya cha michezo cha NSSF–Real Madrid Sports Academy.
  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori (katikati) akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Klabu ya Real Madrid, Rayco Ghasia (kulia).
  Mzee Augustino Mtauka akisaini fomu za usajili wa kituo kipya cha mchezo wa soka kinachomilikiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kushirikiana na klabu ya Real Madrid ya Hispania.. Mzee Mtauka alikuwa akisaini fomu hizo kwa niaba ya mjukuu wake Godfrey Oscar (katikati), usajili uliofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam Jumamosi. Kulia ni Msajili Ally Salehe wa Idara ya Elimu ya Michezo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
  Msajili wa Vijana katika Program ya NSSF-Real Madrid Sports Academy, Rachel Kayuni (kulia), kutoka Idara ya Elimu ya Michezo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), akitoa maelekez kwa baadhi ya wazazi na vijana waliokuwa wakisajiliwa kujiunga na kituo hicho cha soka kilicho chini ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kushirikiana na klabu ya Real Madrid ya Hispania. Usajili huo ulifanyika kwenye Uwanja wa Karume.
  Mtoto Osama Rashid akijaza fomu maalum kwa ajili ya kujiunga na kituo cha michezo cha NSSF-Real Madrid Academy. Kulia ni mama yake Tatu Ali akishuhudia.
  Baadhi ya wazazi wakiondoka katika uwanja wa Karume baada ya kuandikisha watoto wao.
  Mwakilishi wa Klabu ya Real Madrid, Rayco Ghasia (wa pili kulia) akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori (kushoto) wakati wa uzinduzi wa zoezi la kuandikisha vijana watakaojiunga na kituo kipya cha michezo.
  Baadhi ya wadau wa soka wakiwa wameleta watoto wao kujisajili katika zoezi hilo.
  Baadhi ya wadau wa soka wakiwa wameleta watoto wao kujisajili katika zoezi hilo.
  Vijana wakiingia katika uwanja wa Karume kwa ajili ya zoezi la kujisajili na hatimaye kujiunga na kituo kipya cha michezo cha NSSF-Real Madrid Academy.
  Mwakilishi wa FIFA katika masuala ya michezo hapa nchini, Henry Tandau (katikati) akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa zoezi la kandikisha vijana watakaojiunga na kituo kipya cha michezo cha NSSF-Real Madrid Academy.
  Mtoto Issa Hashim akijaziwa fomu na Aisha Hashimu.

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya kulia akimkabidhi Katibu Tawala Wilaya ya Kalambo Bi. Mapinduzi Severian Katiba pendekezwa leo tarehe 14 Februari 2015 kwa niaba ya wananchi wa Wilaya hiyo ambao watapata fursa ya kuiona na kuisoma kwa ajili ya kuipigia kura ya maoni mwezi Aprili mwaka huu. 
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akimuonyesha muimbaji wa kikundi cha ngoma za asili ya Kanondo Katiba pendekezwa katika hafla fupi ya kukabidhi Katiba hiyo iliyofanyika katika Wilaya ya Kalambo. \Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akimuonyesha Ndugu Mulele Mulenda Mwanaukawa aliyeshiriki hafla hiyo fupi ya kukabidhi Katiba pendekezwa kwa niaba ya Katibu wa Chadema wa Wilaya ya Kalambo sehemu ya vifungu vya katiba pendekezwa ambavyo vipo na vilikuwepo kwenye rasimu ya Katiba ya Jaji J. Warioba ambpo ni kinyume na inavyodaiwa na UKAWA kuwa vimechakachuliwa.
   Sehemu ya washiriki wa hafla hiyo, Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa.

   Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Kalambo muda mfupi baada ya kukabidhi Katiba pendekezwa. Aliwataka wananchi hao kujitokeza kwa wingi mwezi April kwa ajili ya kuipigia kura  katiba hiyo na kutopotoshwa kwa namna yeyote ile na watu wasioitakia mema nchi yao. Alisema kuwa katiba hiyo ni nzuri kwani imegusa maslahi ya watanzania wote na ustawi wa taifa kwa ujumla. 

  Baadhi ya wananchi wakionekana kujifunika na mwanvuli kufuatia mvua iliyokua ikinyesha mwishoni mwa hafla hiyo.
  (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa)

  0 0

  Sikiliza kibao kipya cha ''MALAIKA FT''kutoka kwa Miss Rahima Jackson akishirikiana na Jae Star, waTanzania ndani ya Wasahington Seattle, Nchini MAREKANI..!

  0 0

  Mwenyekiti wa Chadema Freman Mbowe akiwa anasoma utuba wakati wa ufunguzi wa mkutano wa viongozi wa  chama hicho wa kanda ya kaskazini unaofanyika leo katika  hotel ya new Arusha jijini hapa.
  viongizo wa chadema  akiwemo mwenyekiti wakiwa wanasali kwanza kabla mkutano wa viongozi wa kanda ya kaskazini kuanza.
   Naibu katibu mkuu wa Chadema Salum Mwalimu akiwa anaongea nawaandishi wahabari
   MWENYEKITI wa chama cha demokrasi na maendeleo Chadema Freeman Mbowe amesema kuwa  chama chao kimejipanga kuahakikisha kinahamasisha  kwa  nguvu zote wananchi weweze kwenda kujiandikisha katika  daftari la mpiga kura 

  Alisemakuwa hii itaweza kumsaidia kila mwananchi  kuweza kupata haki yakumchagua kiongozi bora  anaemtaka  katika uchaguzi mkuu  ujao  wa kuwachagua viongozi wakuu ambao ni rais ,wabunge na madiwani.
  Alisema kuwa pamoja ya kuwa tume wamekuwa wananchelewesha kufanyika kwa zoezi hili , wao wamejipanga kikamilifu na pindi ambapo zoezi hili litatangazwa  kuanza rasmi watajitaidi kwa njia yoyote kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha
  Alisema kuwa kwa upande wa kupiga kura katiba wanaendelea na msimamo wao ambao walitangaza awali wa kutoshiriki katika mchakato wa kura ya maoni ya katiba  huku akisisitiza kuwa swala la kutoshiriki katika mchakato wakura za maoni auingiliani kabisa na  kuhamasisha wananchi kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura 

  Alimaliizia kwa kuwasihi wananchi wajitokeze kwa wingi  sana pindi pale ambapo watasikia zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la kudumu limewadia  ili waweze kupata haki yao ambayo itawaruhusu kuchgua kiongozi wanao wataka.
   
  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaliamia na Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa wakati wa Misa maalum ya kumuombea Marehemu Evodius Walingozi, iliyofanyika leo Feb 14 kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na baadhi ya waumini wa dini ya Kikristu wakati wa Misa maalum ya kumuombea Marehemu Evodius Walingozi, iliyofanyika leo Feb 14 kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaliamia na Mwenyekiti wa Bodi ya Madini Wizara ya Fedha Richard Kasesela, wakati walipokutana katika Misa maalum ya kumuombea Marehemu Evodius Walingozi, iliyofanyika leo Feb 14 kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam. Katikati yao ni Mwenyekiti wa Kanisa hilo, Paul Mzuka.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mwenyekiti wa Kanisla la Mtakatifu Joseph, Paul Mzuka, baada ya kuhudhuria Misa maalum ya kumuombea Marehemu Evodius Walingozi, iliyofanyika leo Feb 14 kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam. Picha na OMR.

  0 0  0 0

  Baadhi ya Sehemu za jengo la Jiko la Hoteli ya Kendwa Rocks iliyoko Mkoa wa Kaskazini Unguja ambalo iliuungua moto ulisababishwa na hitilafu za umeme.
  Wahandisi wa Hoteli ya Kendwa wakijaribu kurejesha miundo mbinu ya umeme iliyoathirika kutokana na moto mkubwa uliotokea kwenye Hoteli hiyo.
  Jengo la Jiko la Hoteli ya Kendwa Rocks lililoungua vibaya mwa moto uliosababishwa na hitilafu ya umeme.
    Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimfariji Mwakilishi wa Hoteli ya Gold Zanzibar iliyopo Nungwi  Mkoa wa Kaskazini Unguja Bwana Andrea Azzala baada ya paa la jengo lao kuungua moto.
  Balozi Seif akikaguzwa kuangalia maeneo yaliathirikia kutokana na moto kwenye Hoteli ya Kendwa Rocks Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
  Kulia ya Balozi Seif ni  Msaidizi Menja Mkuu wa Kendwa Rocks Bwana Omar Ibrahim Kilupi, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Kanal Mstaafu Juma Kassim Tindwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Moh’d Aboud Moh’d.
  Balozi Seif akiwafariji wamiliki wa Kendwa Rocks Bwana Ali Ibrahim Kilupi aliyepo mwnzo kushto na msaidizi wake Omar Ibrahim Kilupi baada ya jengo la jiko la hoteli yao kuungua moto.Kati kati ni Waziuri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Moh’d Aboud Moh’d na kushoto kwa Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja Kanal Mstaafu Juma Kassin Tindwa.Picha na – OMPR – ZNZ.
                                                                                                                                                                
  Na Othman Khamis OMPR
  Hitilafu ya umeme iliyotokea mapema  asubuhi imesababisha moto mkubwa   ulioteketeza jengo la jiko, Duka ,sehemu ya burdani ya Hoteli Kendwa Rocks pamoja na Hoteli ya Gold Zanzibar zilizopo katika Kijiji cha Nungwi Mkoa wa kaskazini Unguja.
   
  Moto huo ulioripuka kwa kusaidiwa na upepo mkali uliokuwa ukivuma majira ya saa nne za asubuhi umeteketeza vitu na vifaa mbali  vilivyokuwemo ndani ya majengo hayo na kusabisha hasara inayokisiwa kufikia shilingi za Kitanzania Bilioni Moja { 1,000,000,000/- }.
   
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiambatana pamoja na Waziri wa  Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Mh. Moh’d Aboud Moh’d walifika eneo la tukio kuwafariji wamiliki wa Hoteli hizo.

  0 0
  0 0

       TANZANIAN FOLK MUSIC MADE IN BONGO TO THE WORLD !
                          IMEKUBALIKA KIMATAIFA
  Bendi ya muziki INAFRIKA BAND aka "Wazee wa Indege" kutoka jiji Dar ,ilifanikiwa kulitingisha jiji la Bremen,nchini Ujerumani katika onyesho liliofanyika usiku wa 13 Februari 2015 katika ukumbi mkubwa wa Musik-Theater mjini Bremen,Ujerumani,ambako bendi hiyo kutoka Chang'ombe ilisimama jukwaani na kuziteka nyoyo za maelfu ya wapenzi wa muziki ,aidha bendi ya Inafrika bend imetajwa kuwa bendibora ya muziki wa Folk na radio Funkhaus-Europe .
   
  Vionjo vya mitindo ya muziki wa asili wa makabila ya kitanzania vilivyotumiwa na Inafrika Band katika kuteka yonyo za washabiki kila kuona duniani. Inafrika Band imefanikiwa kuliweka jina ala Tanzania katika tufe la dunia kwa kutumia mitindo yake ya vionjo vya kiasilia.
   
  Inafrika Band ndio bendi kwanza yenye makao Tanzania inayoongoza kufanya tour ndefu duniani wameshafanya ziara katika mabara yote duniani kuanzia Afrika,Austaria,Amerika,Asia ,Europe na visiwa vya Karebiki.
   
  Wakali hawa wa mdundo inayokubalika kimataifa wanatisha na kuzoa washabiki kwa dhoruba kali la mtindo wao wa muziki. Inafrika band inatuwakilisha bado wapo katika ziara ndefu na wanahakikisha kuwa muzikiwa wao unasikika kila kona nje ya mipaka ya kimataifa.msikose kuwasikiliza Inafrika Band (Wazee wa Indege) at http://www.inafrikaband.co.tz pia wape hi at info@inafrikaband.co.tz ii

  0 0

  Naibu Balozi wa Tanzania nchini Oman Juma Othman katikati akiwa kashika Tunzo ya ushiriki wa Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni nchini Oman waliyopewa kutoka Manispaa ya Mji wa Muscat ambao ndio waandaaji wa Maonesho hayo. Kulia kwake ni Kiongozi wa Msafara wa Washiriki kutoka Tanzania Khadija Battashy na kushoto ni Msaidizi kiongozi Masha Hussein na Mkuu wa mambo ya kiufundi wa Msafara Moza Habib. (Picha na Faki Mjaka  Oman)

  0 0

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na Marubani wa Ndege ya Serekali baada ya kuwasili uwanja wa Kamataifa wa Abeid Amani Karume  Zanzibar akitokea Nchini Qatar alikokuwa na ziara ya Kiserekani Nchini humo.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akivishwa shada la mauwa na Vijana walioandaliwa wakati wa mapokezi yake baada ya kumaliza ziara yake Nchi Qatar  
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na Waziri wa Biashara na Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe Nassor Mazrui, alipowasili uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar. 
  Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na Viongozi alipowasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.
               Maalim akisalimia na Wananchi waliofika kumpokea akitokea ziarani Nchi Qatar.
  Maalim Seif akiangaliwa wanafunzi wa Madrasa wakipiga Dufu wakati wa mapokezi yake Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.
  Waandishi wa habari mbalimbali waliofika uwanja wa ndege wakimsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumzia mafanikio ya ziara yake Nchi Qatar 
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ziara yake Nchini Qatar hivi karibuni na kuzungumzia mafanikio ya ziara hiyo kwa waandishi waliofika katika uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume. mkutano huo umehudhuriwa na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali viliko Zanzibar.

  0 0

  3
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikabidhi kikombe kwa washindi bora wa Tunzo ya Rais ya mzalishaji bora Mwaka 2014 uongozi wa Kiwanda cha Saruji Tanga, wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Jumuiya ya wafanyabiashara (Cti). Ghafla hiyo imefanyika jana usiku Februari 14,2015 katika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
   2
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wadau mbalimbali kwenye Ghafla ya  utoaji Tunzo ya Rais ya mzalishaji bora Mwaka 2014 wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na          Jumuiya ya wafanyabiashara (Cti). Ghafla hiyo imefanyika jana usiku Februari 14,2015 katika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
  1
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia maonesho mbalimbali kwenye Ghafla ya  utoajio Tunzo ya Rais ya mzalishaji bora Mwaka 2014 wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na          Jumuiya ya wafanyabiashara (Cti). Ghafla hiyo imefanyika jana usiku Februari 14,2015 katika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.

  5
  Washiriki waliohidhudhia kwenye Ghafla ya  utoaji Tunzo ya Rais ya mzalishaji bora Mwaka 2014 wakimsikiliza Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal alipokua akizungumza kwenye ghafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na Jumuiya ya wafanyabiashara (Cti). Ghafla hiyo imefanyika jana usiku Februari 14,2015 katika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam. (Picha na OMR)
  6
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal katikati akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa Tunzo ya Rais ya mzalishaji bora Mwaka 2014, wakati wa ghafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na Jumuiya ya wafanyabiashara (Cti). Ghafla hiyo imefanyika jana usiku Februari 14,2015 katika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
  7

older | 1 | .... | 462 | 463 | (Page 464) | 465 | 466 | .... | 1896 | newer