Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YAKUTANA NA VIONGOZI WA SIASA JIJINI DAR LEO.

$
0
0

 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Damian Lubuva akizungumza wakati wa mkutano na Viongozi wa Vyama vya Siasa uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa JB Belmonte,Jijini Dar es salaam.Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Julius Malaba na kulia ni Kamishina wa Tume yaTaifa ya Uchaguzi,Prof. Amon Challigha
Sehemu ya Viongozi wa Vyama vya Siasa waliohudhulia Mkutano huo wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Damian Lubuva (hayupo pichani) leo kwenye Ukumbi wa JB Belmonte,Jijini Dar es salaam.
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini,Jaji Francis Mutungi akichangia mada katika mkutano huo wa Viongozi wa Vyama vya Siasa uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa JB Belmonte,Jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha UDP,Mh. John Momose Cheyo akiwa na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi CCM,Ndg. Nape Nnauye wakati wa mapumziko mafupi ya mkutano huo.
Mwenyekiti wa CHADEMA,Mh. Freeman Mbowe akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Chama cha ACT,Ndg. Samson Mwigamba.
Eeehh....bwanaaaaa upoooo........?? Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi,Mh. James Mbatia akifurahi jambo na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi CCM,Ndg. Nape Nnauye.Katikati ni Katibu Mkuu wa CHADEMA,Dkt. Wilbroad Slaa.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

MKUU WA MKOA WA RUKWA AONANA NA VIONGOZI NA WAJUMBE WA MFUKO WA CHANGAMOTO ZA MILLENIA (MCAT), AWAPONGEZA KWA KAZI NZURI YA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA NCHINI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na viongozi na wajumbe wa Mfuko wa Changamoto za Millenia Tanzania (MCA-T) wakiongozwa na mwenyekiti wake ambae pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi  Dr. Servaciaus Likwelile (kulia)  ofisini kwake leo tarehe 12 Februari 2015. Katika salam zake ameishukuru Serikali na mfuko huo kwa kazi nzuri inayofanyika Mkoani Rukwa na taifa kwa ujumla hususani katika ujenzi wa miundombinu ya barabara za lami, Pamoja na hayo ameiomba Serikali na wafadhili wa MCC kusaidia pia katika ujenzi wa barabara muhim za Wampembe iliyopo Wilaya ya Nkasi, barabara ya bondeni kwa ajili ya kuunganisha ukanda wa bonde la Ziwa Rukwa unaoongoza kwa uzalishaji wa mpunga na Mikoa ya Katavi na Mbeya, barabara ya Kasesha kwa ajili ya kuunganisha Mkoa wa Rukwa na Zambia na barabara ya kuelekea Kalambo Falls yalipo maporomoko ya Mto Kalambo ambayo ni ya pili kwa urefu barani Afrika.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (kulia) akiendesha kikao ofisini kwake mapema leo tarehe 12 Februari 2015 kati yake na viongozi na wajumbe wa Mfuko wa Changamoto za Millenia Tanzania (MCA-T) .
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akitoa zawadi ya kanga kwa Katibu Mkuu Wizara ya fedha na uchumi Dr. Servaciaus Likwelile pamoja na viongozi wengine na wajumbe wa Mfuko wa Changamoto za Millenia Tanzania (MCA-T), Kanga hiyo ni ishara ya mafanikio ya miaka 40 ya Mkoa wa Rukwa 1974-2014.    
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa (kulia) alipata fursa ya kuwaalika viongozi na wajumbe wa Mfuko wa Changamoto za Millenia Tanzania (MCA-T) kwa ajili ya chakula cha usiku walipowasili Mkoani Rukwa tarehe 11 Februari 2015. Anaechukua chakula ni Mwenyekiti wa mfuko huo ambae pia ni Katibu Mkuu Wizara ya fedha na Uchumi Dr. Servaciaus Likwelile.
Picha ya pamoja.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA YAENDESHA MAFUNZO YA SIKU MBILI KWA KAMATI ZA MAADILI ZA MIKOA YA RUKWA KATAVI

$
0
0
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Jaji Kakusulo Sambo akisoma hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo mapema leo tarehe 12 Februari 2015. Mafunzo hayo ya siku mbili yanayoshirikisha Mikoa ya Rukwa na Katavi yanafanyika Mkoani Rukwa. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya na Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Ibrahim Msengi. 
Jaji wa Mhakama Kuu ambae pia ni Mkuu wa Chuo cha Mahakama Lushoto Jaji Ferdinand Wambali akiendesha mafunzo hayo ambayo yameanza leo tarehe 12 Februari na yatamalizika kesho tarehe 13 Februari 2015 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa (RDC).
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Ibrahim Msengi akitoa shukurani za Mikoa ya Rukwa na Katavi kwa kuletewa mafunzo hayo ambayo ni muhimu kwa Kamati za maadili za Mikoa hiyo katika utekelezaji wa majukumu yake ya siku.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Ndugu Iddi Kimanta (wa kwanza) na Katibu Tawala Wilaya Kalambo Bi Mapinduzi Severian ambao ni Wajumbe wa Kamati ya maadili Mkoa wa Rukwa wakifuatilia mafunzo hayo.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati za maadili Mkoa wa Rukwa na Katavi wakifuatilia mafunzo hayo.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa (wa kwanza) na wajumbe wengine wa Kamati za Maadili Mikoa ya Rukwa na Katavi wakifuatilia mafunzo hayo.
Mafunzo yakiwa yanaendelea.
Picha ya pamoja.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa@Rukwareview.blogspot.com)

Rais Kikwete akutana na Viongozi wa Taasisi ya Siti Binti Saad

$
0
0
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad Bibi Nasra Mohamed Hilal(wanne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mizengo Pinda pamoja na mlezi wa Taasisi hiyo Rais Mstaafu awamu ya pili Mhe.Ali Hassan Mwinyi ikului jijini Dar es Salaam leo.(picha na Freddy Maro)

5 YEARS ANNIVERSARY

Umeisikia kampeni ya EATV, East Africa Radio iitwayo “Zamu Yako 2015″?

$
0
0
DSCN9941 
Mkuu wa vipindi wa East Africa Radio, Nasser Kingu (kushoto) akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuzindua kampeni ya Zamu yako 2015, Kulia kwake ni Mkuu wa Masoko Eatv & East Africa Radio, Alex Galinoma

KITUO cha Televisheni chenye ushawishi mkubwa kwa vijana  nchini Tanzania, EATV, sambamba na kituo chake cha East Africa Radio,  mapema leo wamezindua rasmi kampeni kubwa na ya aina yake ijulikanayo kwa jina la ZAMU YAKO 2015.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa vipindi East Africa Radio, Nasser Kingu alibainisha kampeni hiyo inamalengo mahususi kwa Taifa ikiwemo vijana kwa ujumla juu ya kuwakumbusha na kuwaelimisha vijana kuhusiana na umuhimu pamoja na uwezo walionao katika kufanya maamuzi sahihi kwenye masuala makubwa ya kitaifa hususani yanayohusu siasa za Tanzania.
“Kampeni hii ina dhamira ya kuhimiza vijana kutumia fursa waliyonayo katika kufanya maamuzi na mambo mbalimbali.
Kwanza kushiriki kikamilifu katika zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ya maoni katika  mchakato wa kutafuta katiba mpya, na mwisho kushiriki kikamilifu katika zoezi la kupiga kura ili kuchagua viongozi wao ambao ni madiwani, wabunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania” alibainisha Kingu.
Aidha Kingu alisema EATV na East Africa Radio, imekuwa na mvuto mkubwa sana kwa vijana hivyo lengo la kampeni hiyo itafanikiwa kwani inawalenga na kuwagusa moja kwa moja vijana.
Kingu pia aliweza kutoa takwimu kadhaa, ambapo alisema kwa Tanzania, umri rasmi wa kupiga kura ni kuanzia miaka 18 na kuendelea, kwa mujibu wa sense ya mwaka 2012, Jumla ya watu Milioni 22, (22,424,136) wanatazamiwa  kushiriki zoezi hilo kwa mwaka huu.
“Katika idadi hiyo ya wapiga kura, vijana wenye umri wa miaka 18 mpaka 40 peke yao  ni 15,293,681. Idadi ambayo ni sawa na asilimia 68.20 ya wapiga kura wote.
Hii ina maanisha kwamba hatma ama mustakabali wa Taifa hili uko mikononi mwa vijana. Na ndio maana vituo vyetu Tv na Radio vinaaminika zaidi na vijana,  hivyo tunaendesha kampeni hii kwa kutambua umuhimu na nguvu ya vijana katika taifa letu.
Ikumbukwe pia hii si mara ya kwanza kwa vituo vyetu kuwa na kampeni kama hii, mwaka 2010, tulikuwa na kampeni ya kuwataka vijana kuacha kulalamika  na kutumia kura yao” alifafanua Kingu.
Kampeni hiyo inatarajiwa kufanywa na vituo hivyo kupitia vipindi vyao mbalimbali kila siku, ikiwemo kufanya mahojiano na wananchi, vijana, vingozi wanasiasa, watu maalufu na wengineo wengi ambao pia watakuwa wakialikwa kwenye studio za vipindi vya vituo hivyo, kwa zaidi ya mwaka mzima.

Mazungumzo na Mhe. Balozi Mustafa Nyang'anyi Pt II

$
0
0
Karibu sana na asante kwa kujiunga nasi katika kipindi hiki cha HUYU NA YULE
Tumepata fursa ya kuongea na Mhe. Balozi Mustafa Nyang'anyi
Tumefanya mazungumzo naye ya sehemu nne, kueleza safari yake kimaisha
Tunaendelea na sehemu ya pili ya mazungumzo yetu, ambapo Mhe Balozi Nyang'anyi anaanza kuelezea namna
1: Alivyoingia kwenye siasa (ubunge mwaka 1970)
2: Alivyopata taarifa za kwanza za uteuzi wake serikalini. Hapa napo pana mvuto wake kusikiliza.
3: Nafasi alizoshika kama naibu waziri na waziri kamili
4: Nafasi ya ukuu wa mkoa
5: Na hata harakati zake na pia alivyopata nafasi ya kuja kusoma Chuo Kikuu Havard
KARIBU
Kama ulikosa sehemu ya kwanza ya mazungumzo yetu,
Huyu na Yule ni kipindi kinachotayarishwa na Vijimambo Blog na kuzalishwa na Kwanza Production
Kwa mawasiliano, maoni ama ushauri, tafadhali wasiliana nasi kupitia kwanzaproduction at gmail.com

Mahojiano na Omar Ally Mwenyekiti wa Zanzibar Diaspora Association

$
0
0
Sikiliza kwa makini Mahojiano na Omar Ally, Mwenyekiti wa Zanzibar Diaspora Association, akiongelea njia nzuri kuhusu  maendeleo ya kuinua wana ZADIA pamoja na Zanzibar kwa ujumla.

Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, NHC mafunzoni Afrika Kusini

$
0
0
Ujumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi , Maliasili na Mazingira ukiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati, Abdulkarim Esmail Hassan Shah (Mafia), Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki na kuambatana na uongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa wakisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Tumaini Thika jana. Kamati hiyo iko katika ziara ya mafunzo nchini humo.
Ujumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi , Maliasili na Mazingira uliofuatana na uongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa ukiwa katika picha ya pamoja nje ya Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, jana. Kamati hiyo iko katika ziara ya mafunzo nchini humo.
Mjumbe wa Kamati ya Maliasili na Mazingira Benedict Ole Nangoro, (kulia) akijadiliana jambo na Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani cha Shirika la Nyumba la Taifa, Fatuma Chillo.
Ujumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi , Maliasili na Mazingira uliofuatana na uongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa ukiwa katika picha ya pamoja nje ya Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, jana. Kamati hiyo iko katika ziara ya mafunzo nchini humo
Ujumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi , Maliasili na Mazingira ukiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati, Abdulkarim Esmail Hassan Shah (Mafia), Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki uliofuatana na uongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa ukisikiliza maelezo ya namna mashine ya ufyatuaji matofali ya Hydraform inavyofanya kazi kutoka kwa Mtaalamu wa kampuni ya Hydraform ya Afrika Kusini, jana. Kamati hiyo iko katika ziara ya mafunzo nchini humo.
Ujumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi , Maliasili na Mazingira uliofuatana na uongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa ukisikiliza maelezo ya namna mashine ya ufyatuaji matofali ya Hydraform inavyofanya kazi kutoka kwa Mtaalamu wa kampuni ya Hydraform ya Afrika Kusini, jana. Kamati hiyo iko katika ziara ya mafunzo nchini humo.
Ujumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi , Maliasili na Mazingira uliofuatana na uongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa ukisikiliza maelezo ya namna mashine ya ufyatuaji matofali ya Hydraform inavyofanya kazi kutoka kwa Mtaalamu wa kampuni ya Hydraform ya Afrika Kusini, jana. Kamati hiyo iko katika ziara ya mafunzo nchini humo.
Ujumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi , Maliasili na Mazingira uliofuatana na uongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa ukisikiliza maelezo ya kutoka kwa Mtaalamu wa kampuni ya Hydraform ya Afrika Kusini, jana. Kamati hiyo iko katika ziara ya mafunzo nchini humo.
Ujumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi , Maliasili na Mazingira uliofuatana na uongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa ukisikiliza maelezo ya kutoka kwa Mtaalamu wa kampuni ya Hydraform ya Afrika Kusini, jana. Kamati hiyo iko katika ziara ya mafunzo nchini humo.
Katika picha ya pamoja nje ya ofisi za Kampuni za Hydraform Afrika Kusini leo.
Ujumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi , Maliasili na Mazingira uliofuatana na uongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa ukisikiliza maelezo ya namna mashine ya ufyatuaji matofali ya Hydraform inavyofanya kazi kutoka kwa Mtaalamu wa kampuni ya Hydraform ya Afrika Kusini, jana. Kamati hiyo iko katika ziara ya mafunzo nchini humo.

PATA OFFER YA VALANTINE @AK CLASSIC COSMETICS

$
0
0
WALE MABINGWA WA COSMETICS ZA UKWEE, #AKCLASSICOSMETICS WAMEWAANDALIA VALENTINE SPECIAL!! KWA AJILI YA WALE WOTE WANAOWAJALI NA KUWAENZI WAPENDWA WAO
PATA PACKAGE MAALUM KWA AJILI YA MPENZI WAKO KWA BEI YA PUNGUZO KABISA... BIDHAA PENDWA ZA VICTORIAs SECRETS, KAMA LOTION,SHOWERGEL,LIPSTICK,
LIPGLOSS,DEODRANT,PERFUMES N.K!!
KUONA PICHA ZA BIDHAA ZAIDI...
                          INGIA
            www.akclassic.blogspot.com

KARIBUNI DUKANI MJIONEE MAMBO KADHA WA KADHA
KAMA BODY SHAPER,TIBA ZA CHUNUSI,BIDHAA ZA KUPUNGUZA UNENE NA UZITO,BIDHAA ZA KUNG'ARISHA N.K
TUPO MLIMANI CITY KARIBU KABISA NA PETROL STATION YA TOTAL!
TUPIGIE 0753482909

 BIDHAA ZINAWEZA KUKUFIKIA MPAKA ULIPO!!



 

Tamasha la Pasaka kamili kusaidia jamii

$
0
0
WAANDAAJI wa Tamasha la Pasaka wamesema wataendelea kusaidia jamii katika kila tamasha lao litakapofanyika.
 
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Dar es Salaam  leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya miaka 15 ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama ilieleza kuwa kwa miaka yote hiyo wamekuwa mstari wa mbele kusaidia jamii.
 
"Tumedhamiria kwa dhati kusaidia jamii kwa namna mbalimbali, hii haitakuwa mara ya kwanza kwetu kufanya hivyo, tulisaidia matamasha yaliyopita, tutaendelea na juhudi hizo kila tutakapopata nafasi, “ alisema Msama katika taarifa hiyo.
 
Alisema katika miaka yao 15 wamesaidia sehemu mbalimbali ikiwemo waathirika wa mabomu yaliyotokea kwenye kambi ya jeshi Gongo la Mboto, Dar es Salaam.

Pia alisema Tamasha la Pasaka wamewahi kusaidia fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima nakuwasaidia mitaji ya biashara wanawake wajane. “Tangu mwanzo tulishajionesha kwamba tuna dhamira ya dhati na ndio maana tunafurahia sana kila mwaka kwamba nasi tunashirikiana na jamii na hata mwaka huu tutafanya hivyo,” alisema Msama.
 
Pia alisema kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali wamekuwa wakitoa semina za kusaidia wajane, yatima na vijana wasio na ajira ikiwa ni pamoja na kuwapa mbinu za kufanya biashara na kuachana na dawa za kulevya.

"Mimi naamini mtoaji wa vyote ni Mwenyezi Mungu, hivyo ni busara upatapo kidogo ugawane na wasiojiweza ili kuongeza thawabu yako.

Kuhusiana na tamasha la mwaka huu, alitamba kuwa wamewaandalia mashabiki wa muziki wa Injili mambo mazuri  yatakayowaburudisha na kuridhika.

Serikali na Wadau binafsi washauriwa kuwasaidia Wajasiriamali wa Kitanzania

$
0
0
 
 Balozi wa Tanzania nchini Oman Ali Ahmed Saleh kushoto Aliyekaa kwenye kiti akipata burudani ya Msewe iliyoandaliwa kwa ajili yake na Kikundi cha Sanaa cha Zanzibar mara baada ya Balozi huyo kumaliza ziara yake ya kuwatembelea Watanzania na kushauriana nao mambo mbalimbali ya kukuza soko katika Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea Mjini Mascut nchini humo. Picha na Faki Mjaka.
 Wasanii wa Kikundi cha Sanaa cha Zanzibar wakicheza Ngoma aina ya Uringe kwa Balozi wa Tanzania nchini Oman (hayupo pichani) mara baada ya Balozi huyo kuwatembelea Watanzania na kushauriana nao mambo mbalimbali ya kukuza soko katika Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea Mjini Mascut nchini humo.
  Mjasiriamali wa Mavazi mbalimbali ikiwemo ya Kimasai Bi Anna Matinde akitoa ufafanuzi wa bidhaa zake kwa Balozi wa Tanzania Nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh kulia.Balozi Saleh alifanya ziara ya kuwatembelea Watanzania hao na kushauriana mambo mbalimbali ya kukuza soko katika Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea Mjini Mascut nchini humo. Picha na Faki Mjaka-Mascut Oman.

Na Faki Mjaka, Muscat, Oman  

Serikali na Wadau binafsi wameshauriwa kuwasaidia Wajasiriamali wa Kitanzania ili waweze kuziweka bidhaa zao katika Vifungashio (Package) vyenye mvuto na kiwango cha ubora wa kimataifa.

Kufanya hivyo kutawawezesha Wajasiriamali hao kupata soko la Bidhaa zao kwa Wateja wadogo na wakubwa katika nchi mbalimbali duniani.

Ushauri huo umetolewa na Balozi wa Tanzania nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh alipowatembelea Wajasiriamali wanaoshiriki katika Maeonesho ya Kimataifa ya Sanaa,Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea katika Mji wa Muscat nchini Oman.

Amesema licha ya Tanzania kufanya vyema katika Maonesho hayo kuna baadhi ya changamoto ambazo zinahitaji kupatiwa ufumbuzi ili Tanzania izidi kupata sifa ya bidhaa zake kimataifa.

Changamoto hizo ni pamoja na uwezo mdogo wa kuziweka bidhaa wanazozitengeneza katika Vifungashio (Package) ambavyo ubora wake haujafikia kiwango kinachotakiwa cha kimataifa.

Balozi Saleh amefahamisha kuwa mbali na bidhaa hizo ikiwemo zile za Viungo kupata Soko kutoka kwa Wakaazi wa Oman lakini inakuwa ngumu kupata Soko kwa Wateja wa Maduka Makubwa (Supermarkets) ambao wangenunua bidhaa hizo kwa ujumla.

Ameongeza kuwa Wateja wa Maduka Makubwa wanahitaji bidhaa zilizowekwa katika Package ambazo zinaonesha kuwa zimepitia katika maabara ya kisayansi na kupata vigezo vyote vinavyohitajika kimatumizi.

“Naamini tukiwa na Package zenye ubora wa kimataifa zinazoonesha Warrant, muda wa matumizi basi hata Order za Wateja wa Supermarkets tungepata za kutosha ” Alisema Balozi Saleh

Aidha Balozi Saleh amewashauri Wajasiriamali hao kuziweka bidhaa zao katika Vifungashio (Package) hata zile ambazo bado hawajafikiria kuziweka ikiwemo zile za Vinyago na Viatu ili kuvutia zaidi Wateja.

“Tumezoea kwetu kuwa Vinyago haviwekwi kwenye Package ila navyo vinatakiwa viwekwe pamoja na vitu vingine ili wateja wahamasike na Ubora wa Bidhaa zetu” Alishauri Balozi Saleh

Hata hivyo Balozi Saleh ameishukuru Serikali ya Oman kwa mashirikiao yake makubwa na Tanzania na kwamba fursa hiyo iliyopatikana itakuwa na Matunda mazuri kwa Tanzania kutokana na kujitangaza vyema kwa Wageni na Wenyeji wa Oman.

Kwa upande wao Wajasiriamali hao Walimshukuru Balozi Saleh na Ofisi yake kwa kuwa karibu nao na kushauriana nao kila muda jambo ambalo linawapa faraja kubwa.

TWANGA PEPETA KUFANYA ONYESHO MAALUM LA VALENTINE DAY.

$
0
0
BENDI ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ usiku wa kesho itafanya onyesho maalum ya kusherekea siku ya wapendanao ‘Valentine Day’, kwenye ukumbi wao wa nyunmbi Mango Garden, Kinondoni.

Mkurugenzi wa bendi hiyo Asha Baraka amesema kuwa pia onyesho hilo watatambulisha nyimbo zao mpya zilizoko kwenye chati. Pia mkurugenzi huyo alisema kuwa bendi hiyo itapiga nyimbo zao zote za zamani zilizovuma wakati huo. Aliwataka mashabiki wa bendi hiyo kujitokeza kwa wingi kuhudhuria onyesho la aina yake ambalo  litabubikwa na zawadi kibao za Valentine.

“Tumejianda vizuri kwa onyesho la Valentine. Onyesho hili limeboreshwa zaidi ya lile la kumpongeza mwanamuziki wao kongwe Lwiza Mbutu lililofanyika wiki iliyopita ambalo iliudhuriwa na umati wa mashabiki,” alisema Asha.

“Tunaomba watu wajitokeze kwa wingi waje waangalie onyesho letu  maalum  kwani ukizingatia kwamba Valentine Day hufanyika mara moja kwa mwaka,” alisema Asha. Naye mratibu wa onyesho hilo Joseph Kapinga amesema kuwa maandalizi yote yamekamilika kilichobaki ni muda kufika ili mashabiki wapate uhondo.

Onyesho hilo limeandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts kwa hisani ya Dodoma Wine, Freditto Entertainment, CXC Africa na Saluti5. Mratibu huyo amesema kuwa siku hiyo Twanga Pepeta pia itapiga nyimbo zao za zamani zilizowapatia umaarufu. Baadhi ya nyimbo hizo ni Kisa Cha Mpemba, Fainali Uzeeni, Mtu Pesa, Safari 2005, Aminata, Busu  la mwaka2000, Nusu la kufunga mwaka na nyinginezo.

Bendi hiyo inayotamba kwa staili ya Kisigino pia itapiga nyimbo zao kama Nyumbani ni Nyumbani, Dunia Daraja,‘Mwana Dar es Salaam’, ‘Shida ni Darasa’, ‘Rafiki Adui’, ‘Mwisho wa Ubaya ni Aibu’, ‘Nazi Haivunji Jiwe’, ‘Sitaki Tena’ na ‘Ganda la Miwa”. Bendi hiyo inaundwa na wanamuziki kama Kalala Junior, Dogo Rama, Saleh Kupaza, Luiza Mbutu, Badi Bakule, Rama Pentagon, Frank Kabatano na Kalala Junior.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA UONGOZI WA KAMPUNI YA NARI YA CHINA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Meneja Mkuu wa Kampuni ya NARI ya China, Bw. Bao Tianhua, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Feb 13, 2015 kwa mazungumzo. Katikati ni Katikati ni Mkurugenzi wa Bosandra Professionals Co Ltd, Bora Joachim. 

Mhe. Dkt. Bilal, leo amekutana na Uongozi wa Kampuni hiyo ya NARI kutoka Nchini China ambayo pia inajishughulisha na Uwekezaji wa Miundombinu ya Umeme  Nchini Tanzania kwa kushirikiana na Wakala wa Umeme Vijijini.
 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Meneja Mkuu wa Kampuni ya NARI ya China, Bw. Bao Tianhua, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Feb 13, 2015 kwa mazungumzo.  
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Meneja Mkuu wa Kampuni ya NARI ya China, Bw. Bao Tianhua, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo Feb 13, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Kampuni ya NARI ya China mara baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwake Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Picha na OMR

MBUNGE MH. JOSHUA NASARI AONGOZA MAZISHI YA ALIYEKUWA MWANAFUNZI WA IFM EMMANUEL P. PALLANGYO ,SING'ISI MERU ARUSHA

$
0
0

Mbunge wa Arumeru Mashariki Mh. Joshua Nasary akitoa salamu za Pole kwa wafiwa wote wakati wa mazishi ya Marehemu Emmanuel Pendael Pallangyo aliyefariki Tarehe 7.02.2015 na kuzikwa kijijini kwao Sing'isi Meru tarehe 12.02.2015 .

Mh. Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasary akiweka Shada la maua katika Kaburi la Marehemu Emmanuel Pendael Pallangyo aliyefariki Tarehe 7.02.2015 na kuzikwa tarehe 12.02.2015 kijijini kwao Sing'isi Meru
Msaidizi wa Askofu Mkuu wa Jimbo la Kaskazini   Paulo Urio akimaliza Ibada Makaburini kwa kutoa Mbaraka kwa watu wote waliofika katika mazishi ya Marehemu Emmanuel Pendael Pallangyo yaliyofanyikia kijijini kwao Sing'isi Meru.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa Makaburini wakati wa mazishi.
Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Arumeru Mashariki Mh.  Joshua Nasary akiwa na kwenye msiba wa Marehemu Emmanuel Pallangyo ambaye alikuwa ni Mwanafunzi wa IFM nyumbani kwao Sing'isi Meru.
Mmoja wa wanafamilia akisoma Wasifu wa Marehemu Emannuel Pendael Pallangyo
Msaidizi wa Askofu mkuu wa Jimbo la Kaskazini   Paulo Urio akiongoza Ibada ya Mazishi ya Marehemu Emmanuel Pendael Pallangyo kijijini kwao Sing'isi Meru.
Baadhi ya viongozi wa Dini kutoka Madhehebu Mbalimbali wakiwa wanaimba na waombolezaji wengine wakati wa ibada ya  Mazishi.
Mkuu wa jimbo la KKT kaskazini  Zelote Pallangyo akitoa Mahubiri wakati wa Misa ya mazishi ya Marehemu Emmanuel Pallangyo kijijini kwao Sing'isi Meru.
 Aliyeteuliwa kuzungumza kwa niaba ya Familia Bwana Exaud Assery Pallangyo akitoa salamu za shukurani za pekee kwa watu wote waliohudhuria Mazishi ya Mpendwa wao Emmanuel Pendael Pallangyo aliyefariki Tarehe 7.02.2015 Jijini Dar es salaam na kuzikwa Tarehe 12.02.2015 Nyumbani kwao Sing'isi Meru.
Baadhi ya ndugu wa Marehemu Emmanuel Pendael Pallangyo aliyefariki tarehe 7.02.2015 wakiwa na simanzi wakati wa Ibada ya Mazishi kijijini kwao Sing'isi Meru
Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika Ibada ya Mazishi ya Marehemu Emmanuel Pallangyo kijijini kwao Sing'isi Meru.
Mwili wa Marehemu Emmanuel Pendael Pallangyo ukipelekwa Makaburini kijijini kwao Sing'isi Meru kwa ajili ya Mazishi.
Baba wa Marehemu Mzee Pendael T.  Pallangyo kushoto akiweka Shada la maua katika Kaburi la Mwanae Emmanuel Pendael Pallangyo.

Baba wa Marehemu Mzee Pendael T.  Pallangyo akitoa Salam zake za Mwisho kwa Mwanae Mpendwa Emmanuel Pallangyo
Kaka Mkubwa wa Marehemu Elisante Pallangyo, akifuatiwa na Dada zake Eliakunda  Pallangyo, Magreth Pallangyo pamoja na Sarah Pallangyo wakitoa Heshima za Mwisho  katika Mwili wa Marehemu Emmanuel Pendael Pallangyo Kijijini kwao Sing'isi Meru  Arusha.

WATAALAM WA KUJITOLEA KUTOKA JAPAN WATUA NCHINI KUTOA HUDUMA KATIKA SEKTA MBALIMBALI

$
0
0
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi (katika kiti kikubwa) akiongea na wataalam wa kujitolea kutoka nchini Japani waliomtembelea ofisini kwake kujitambulisha
 Wataalam wa kujitolea kutoka nchini Japani wakipiga makofi kumshukuru Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi mara baada ya kuwakaribisha nchini kufanya kazi sekta mbalimbali.
 Sehemu ya wataalam wa kujitolea kutoka nchini Japani waliokuja nchini kutoa huduma kwa kujitolea katika maeneo mbalimbali wakitoka nje ya Ofisi ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma baada ya hafla fupi ya kuwakaribisha nchini.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi (wa nne toka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa kujitolea kutoka nchini Japani waliokuja kwa ajili ya kutoa huduma katika maeneo mbalimbali nchini.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA UONGOZI WA KAMPUNI YA MWANANCHI COMMUNICATION

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communication, Francis Nanai,  wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Feb 13, 2015 kwa mazungumzo na kujitambulisha rasmi baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo. Kushoto ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni hiyo, Bakari Machumu.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communication, Francis Nanai wakati walipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Feb 13, 2015 kwa mazungumzo na kujitambulisha rasmi baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo na kuelezea kazi zinazofanywa na kampuni hiyo.

Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa juu wa Kampuni ya Mwananchi Communication, Mkurugenzi Mtendaji Francis Nanai  (wa pili kushoto) Mhariri Mtendaji Bakari Machumu (kulia) na Mshauri wa Kampuni hiyo, Teddy Mapunda (kushoto) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo, Feb 13, 2015.

Halmashauri ya mufindi yapewa wiki 3 kujenga kizimba cha takataka soko kuu mafinga

$
0
0
-->
Katibu wa CCM Wilaya ya Mufindi, Miraji Mtaturu
 vijana wa mafinga wakishangila uwepo wa Katibu wa CCM Wilaya ya Mufindi, Miraji Mtaturu


Na Fredy Mgunda,Mafindi.

Halmashauri ya mufindi yapewa wiki 3 kujenga kizimba cha takataka soko kuu mafinga pia kusambaza maji katika vyoo vya halmashauri vilivyopo sokoni hapo.

Wiki tatu hizo zimetolewa na Katibu wa chama cha mapinduzi wilayani mufindi Miraji Mtatulu baada ya kufanya ziara ya kushtukiaza katika soko hilo na kubaini kuwapo kwa kizimba kinacho tumiwa kuhifadhi taka hakijajengwa kwa utalamu ikiwa kinauchafu na maji ya muvua nayo yanapita hapo hali inaypelekea kuhatalisha afya za wafanyabiashara katika eneo hilo hususani mlipuko wa magonjwa.

Pia mtatulu ametoa wiki tatu kwa halmashauri kukarabati miundo mbinu ya choo ambapo choo hiyo imekuwa ikitumiwa pasipo maji huku usafi wake nao ukiwa hafifu na kwaupande wa choo ya mtu binafsi ametakiwa kuweka maji vyooni na kuboresha usafi ndani ya wiki hizohizo tatu.

Nao wafanyabiashara wamemtaka kuchukua hatua stahiki kutokana na baadhi ya wataalamu wa serikali kuchukulia maneno ya wanasiasa ni siasa pia kutakiwa kuaahidi kama mambo hayo yasipofanyika ni hatua gani atachukua au nini afanyiwe,
"utatuaminisha vipi kuwa wewe utalifanyia kazi suala hili ikiwa hawa wataalamu wengi wao huamini maneno yanayozungumzwa na wanansiasa ni siasa" Akijibia amesema Ilikuonyesha amejitoa kufanya kazi ya jamii yeye hana tofauti na shehe,Mchungaji, au Padrii hivyo atahukumiwa siku ya mwisho hivyo hawezi acha ahukumiwa kwasababu ya uzembe wa baadhi ya watendaji waliopewa jukumu la kufanya kazi hiyo.

Kwa upande wa katibu wa soko hilo FREDRICK MNG'ONG'O Ameibua changamoto ambayo kwasasa iliyokuwa mupango wa wafanyabiashara hao kujakugomea kitendo cha Serikali kupandisha kodi kwa asilimia mia huku TRA wakijipangia tuu kiasi cha kulipia kuwa ni mara 2 ya malipo ya mwaka jana jambo ambalo limewafanya wafanyabiasha wote kuitaka halmashauri kuandaa mkutano utakaotolea ufafanuzi juu ya swala hilo ikiwa na kuanika hadharani viwango vya ushuru kwa kila biashara ili kuondokana na rushwa za lazima huku wakimtaka na katibu huyokuhudhuria kutoa ushauriwake.

Mara baada ya kikao katibu amewataka wananchi kutokukichukia chama kilichopo madarakani kwani wanaokifanya chama hichohicho kutopendwa ni wafanyakazi wa sekta mbalimbali kutofanya kazi zao kwa maadili pia chama hicho hakiwatumi watumishi hao kuwaibia wananchi kwa maana ya kuwafisadi wananchi"Wananchi kwa pamoja tunatakiwa kuwawajibisha watendaji kwani wao ndio hawafanyikazi na chama kama chama kinafanya ipasavyo na sasa naanza na hawa ambao wao hawafanyi kazi za wananchi.

Katika kusisitiza na kujazia kuwa lazima baada ya wiki tatu anakagua tena kama yametendewa kazi amesema halmashauri inaweza kutumia fedha zitakazo ludishwa na waliozichukua kauli hiyo ilishangiliwa na wafanyabiashara waliokuwapo katika mkutano huo,kauli hiyo imekuja wakati baadhi ya wafanyakazi wa halmashauri hiyo wakiwa wamefikishwa mahakama ya wilaya ya mufindi kwa makosa ya uhujumuuchumi katika halmashauri hiyo.

NOEL OLE VAROYA CHADEMA ATANGAZA KUWANIA KITI CHA UBUNGE ARUSHA

$
0
0
NOEL PIC
Katika picha ni Noel Olevaroya akihutubia Maelfu ya wananchi katika moja ya harakati zake katika mkutano wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Aliyewahi kuwa mwenyekiti wa vijana na mjumbe Wilaya ya Arusha kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Noel Olevaroya (37) ametangaza rasmi kupeperusha bendera ya chama hicho kwa kuwania nafasi ya ubunge katika jimbo la Arusha mjini

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha Noel Olevaroya alisema kuwa nia yake ya kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la Arusha ni msukumumo kutoka kwa Mungu baada ya kumaliza nafasi yake ya uwenyekiti wa vijana na mjumbe wilaya ya Arusha mwaka 2014

Alieleza kuwa msukumo huo ulikuwa ukimsumbua sana na ndipo aliamua kutii sauti ya Mungu kwa kutangaza kuwania nafasi hiyo ya kugombea kiti cha ubunge katika jimbo la Arusha mjini ambapo kwasasa jimbo hilo lipo mikononi mwa Godbless Lema

Aidha alisema kuwa Mbunge anafursa nzuri sana ya kusaidia wananchi hata kwa kupitia mfuko wa jimbo,mshahara hali ambayo itasaidia kuwainua wananchi na kupunguza umaskini

Alitoa wito kwa vijana wa Arusha kusikiliza sauti ya Mungu kwa kuwachagua viongozi bora wenye hofu ya Mungu kwa maslahi ya Nchi yetu
(Habari na Pamela Mollel wa jamiiblog)

TANGAZO LA MSIBA WA NDG ANDREW MICHAEL KUMALILWA (DCP MSTAAFU).

$
0
0
Marehemu Andrew Michael Kumalilwa enzi za uhai wake.
Familia ya Bwana Andrew Michael Kumalilwa inasikitika kutangaza kifo cha wa baba yao mpendwa Bwana Andrew Michael Kumalilwa  kilichotokea tarehe 09 Februari 2015 Jijini Dar Es Salaam.
Marehemu Andrew Michael Kumalilwa alizaliwa mnamo tarehe 10 Machi 1938 na aliwahi kushika nyazifa mbalimbali ikiwepo ya Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Tanzania (DCP) na msiba upo nyumbani kwake Tabata Segerea na Mazishi yatafanyika Kesho (LEO) Nyumbani Kwake Segerea.
Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi - Amina
Timu nzima ya Lukaza Blog inapenda kutoa pole kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki kwa kuondokewa na Mpendwa wao. Mungu awatie nguvu katika Kipindi hiki Kigumu
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live


Latest Images