Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 460 | 461 | (Page 462) | 463 | 464 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Aliyekaa kutoka kushoto Afisa mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais bi Emelda Teikwa,kulia Injinia Ladslaus Kyraruzi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, aliyesimama kushoto Bw. Fred Manyika kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, na Aliyesimama kulia Bw. Balisi Gopolang mtaalam wa masuala ya hali ya hewa kutoka nchini Botswana wakijadili jambo...katika mkutanao wa maandiilizi wa mkutano wa Dunia wa mabadiliko ya Tabia nchi unaendelea mjini Geneva Uswiss..( Picha na Evelyn Mkokoi)

  0 0  0 0

  “ Dr. Evans Rweikiza adressing the press during the official launching of Tanzania Financial services for Undeserved Settlements(TAFSUS) at Giraffe Hotel Dar es Salaam." .

  0 0


   Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi.

  Na Andrew Chale wa modewjiblog
  Mshindi wa Januari 2015 wa shindano la wazo la biashara 3N anatarajiwa kutangazwa siku ya Alhamisi ya Februari 12 kuanzia saa tano asubuhi jijini Dar es salaam.

  Kwa mujibu wa Dk. Reginald Mengi kupitia kurasa wake wa twitter, alitangazia umma kuwa Shindano hilo jipya lijulikanalo kwa kifupi -3N, ikiwa ni kifupisho cha ‘Nitabuni wazo la biashara, Nitatekeleza, na Nitafanikiwa’, ambapo mshindi wa kwanza wa mwezi Januari anatarajiwa kutangazwa siku hiyo ya alhamisi Februari 12. Dk. Mengi aliweka ujumbe huo twittter : “Kutokana na sababu zisizozuilika mshindi wa Januari wa shindano la 3N atatangazwa Februari 12 saa 5 asubuhi. Samahani kwa usumbufu wowote”.

  Kwa mujibu wa Dk. Mengi awali mshind I alitakiwa kutangazwa Jumatano ya leo ya Februari 11, kabla ya kusogeza mbele hiyo Februari 12.
  Shindano hilo litakuwa linafanyika kila mwezi kwa muda wa miezi sita kuanzia Januari Mosi 2015, hadi Juni 30, 2015, na mshindi wa kila mwezi atajishindia ruzuku ya shilingi milioni 10 atakazozitumia kutekeleza kwa vitendo wazo lake la biashara.

  Shindano hilo, linawashirikisha Watanzania pekee, litaendeshwa kwa njia ya mtandao wa kompyuta ambapo mshiriki atatuma wazo lake la biashara kwa anuani ya twita @regmengi Shindano la Wazo la Biashara. Katika mchujo wa kwanza jopo la wataalamu litateua mawazo 10 bora Zaidi na waliotoa mawazo hayo watafanyiwa usaili kwa njia ya simu ili jopo hilo lijiridhishe kama mawazo waliyoyotuma ni yao binafsi, na kama wamejipanga vizuri kutekeleza kibiashara.

  Kutokana na mawazo hayo 10 teule, jopo litachagua wazo moja kuwa mshindi. Hii ni mara ya tatu kwa Dkt. Mengi kuendesha shindano kwa kutumia mtandao wa kompyuta wa twitter kwa kuamini kwake kuwa mitandao ya kijamii ina nguvu kubwa katika kuchochea ujasiriamali hasa kwa kizazi cha sasa. Shindano la kwanza na la pili lililoendeshwa mwaka jana lilikusudiwa kushawishi mawazo ya kuondoa umaskini katika taifa lenye utajiri mkubwa, lakini watu wake wengi wakiwa bado wametopea katika lindi la umaskini.
   
  Awali akizungumza katika uzinduzi wa shindano hilo, Dkt. Mengi alisema shindano hilo limelenga kuhimiza watu kuwa na upeo mkubwa wa kuona fursa za kibiashara na kuzitumia kujikwamua kiuchumi. Pia alisema shindano hilo ni mchango wake binafsi wa kuunga mkono jitihada za serikali na sekta binafsi za kuwakomboa wananchi kiuchumi kwa njia za ujasirimali, kwani amesema Sera zote mbili za kitaifa za Elimu ya juu na maendeleo ya viwanda vya kati na vidogo zina vipengele vya kuchochea na kuendeleza utamaduni wa ujasirimali wa mtu mmoja mmoja.

  “Kwa muda mrefu nimekuwa nikishawishi uwepo wa moyo wa ujasirimali miongoni mwa wa Watanzania na hasa kwa vijana. Ni ndoto yangu kuona uchumi wetu unakua kwa kasi kiasi cha kuzalisha zaidi ya mamilionea 100 kila mwaka wanaoendesha biashara halali,” alisema. Alisema kuwa na wazo sahihi la biashara, katika muda muafaka na eneo sahihi ni muhimu zaidi kuliko ruzuku ya fedha.

  “Nataka vijana watambue kwamba wanaweza kuanza na kitu kidogo na kukua kufikia kampuni kubwa kabisa ya kimataifa unayoweza kufikiria,” alisema na kusisitiza kwamba anaamini siku moja mazingira ya ujasirimali nchini Tanzania yakuwa miongoni mwa mazingira bora kabisa barani Afrika.

  Amesisitiza kuwa Shindano hilo liko wazi kwa watanzania wote na wanachotakiwa kufanya ni kuhakikisha wanapeleka wazo lao la biashara kwa Dk Mengi kupitia mtandao wa kompyuta wa twita, kwa kumtag Dk Mengi kwenye @regmengi.

  Aidha amesema ni wale tu watakaomtag ndio watafikiriwa na jopo la wataalamu, na kusisitiza kuwa maamuzi ya jopo la Wataalamu yatakuwa ni ya mwisho.
  Washindi wa kila mwezi wataarifiwa kwa kutumiwa ujumbe mfupi kwa kupitia akaunti zao za twita (DM) na kupewa ruzuku yao katika sherehe fupi itakayohudhuriwa na waandishi wa habari.

  0 0

  Na Miza Kona  Maelezo-Zanzibar .
                                                                     
  Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein amesema uhuru wa mahakama ni suala la msingi na lenye umuhimu mkubwa katika kujenga utawala bora nchini.

  Hayo ameyasema huko Victoria Garden Wilaya ya Mjini Unguja katika maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar, Dkt Shein amesema ili Mahkama iendelee kuwa huru mihili mengine haipaswi kuingilia katika maamuzi yake kama ilivyo hapa nchini hivyo ni muhimu kwa majaji, wanasheria, mahakimu, mawakili na wahusika wa kada ya sheria kutekeleza majukumu yao bila ya hofu na upendeleo kwa kuzingatia katiba na sheria ziliopo.

  Rais Shein amesema uhuru huo utakuwepo  pindi patakapokuwa na taasisi zilizo huru  zilizowekwa kikatiba na kisheria  zenye kufanya kazi zake kwa uadilifu na mashirikiano.

  Amewataka wananchi kufanya jitida ya kuzielewa sheria mbali mbali zilizopo ambazo ni muhimu katika kusimamia maisha ya kila siku kwani Mahkama ina dhamana ya kutekeleza majukumu yake bila ya kuingiliwa kutokana na uhuru uliopewa kwa kuzingatia sheria.


  “Mahkama inatakiwa kuwa chombo au taasisi huru, uhuru kwa maana ya kuwa huru wale wote waliopewa jukumu na katiba la kutoa haki ya kuamua mtu kuwa mkosa au hana hatia lazima awe huru kutokana na shindikizo bila ya kujali anakotoka, Mahkama iwe huru kutokana shindikizo la Kisiasa, Kiutawala na Kihisia ikiwa inataka kufanya kazi zake kwa uadilifu unaofuata sheria mama ambayo ni Katiba pia Mhkama haitakiwi kulazimishwa au kupokea vitisho vya aina yoyote” , amefahamisha Dkt Shein.

  Akizungumzia kuhusu suala la Rushwa nchini Dkt Shein amesema kuwa tafiti mbali mbali zilizofanywa nchini na mashirika ya Kimataifa kuhusu tatizo la Rushwa na Uhujumu wa Uchumi zinaonyesha kuwa mambo hayo ndio yanayokwamishwa maendeleo ya nchi zinazoendelea hivyo amewataka wananchi kuongeza kasi ya mapambano katika kuchukia Rushwa na kuwa mstari wa mbele katika kulinda mali na maslahi ya Umma.

  Nae Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Abubakar Khamis Bakari amesema ucheleweshaji wa kesi Mahkamani unasababisha mashahidi na wazee kuwa wagumu katika kutoa mashirikiano hata hivyo chombo husika kinaendela kufanya mbinu za kulitatua tatizo hilo.

  Mapema Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othaman Makungu amesema uhru wa Mahkama ni kutoa haki bila ya upendeleo, woga wala kupokea rushwa na kufuata misingi ya sheria katika utoaji wa haki.

  Ametanabahisha kuwa dhana ya kufuata sheria ndio kigezo muhimu katika utawala bora kwani hupelekea kuwepo kwa uwazi na uwajibikaji kwa watumishi wa umma hivyo amewataka watumishi hao kufuata sheria kikamilifu katika kuwahudumia wananchi ili waweze kupata haki zao bila usumbufu wa aina yoyote.

  Amesema kuwa wasimamizi wa sheria watoe  haki bila ya upendeleo na kuitumia sheria bila ya kuogopa na kumhofia mtu yeyote kwani ndiko kutakowafanya watu kuridhishwa na maamuzi yanayotolewa na Mahakama na kuepusha vurugu jambo litakalopelekea nchi kuwa yenye amani na usalama.

                                      IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0

   Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Saleh M. Jidawi (wa kulia waliokaa) na Meneja wa Kampuni ya Simed International Services ya Uholanzi Nd. Michor Pleijzer wakitia saini mkataba wa uboreshwaji wa wodi ya wazazi na watoto Unguja na Pemba huku wakishuhudiwa na Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman na Balozi wa Uholanzi Nchini Tanzania Mr. Jaap Frederiks katika hafla iliyofanyika Wizara ya Afya Mjini Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
    Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Saleh M. Jidawi  (kulia)na Meneja wa Kampuni ya Simed International Services ya Uholanzi Nd. Michor Pleijzer wakibadilishana hati za makubaliano  ya uboreshwaji wodi ya wazazi na watoto za Unguja na Pemba katika hafla iliyofanyika Wizara ya Afya Mjini Zanzibar.
   Balozi wa Uholanzi Nchini Tanzania Mr. Jaap Frederiks akizungumza na baadhi ya watendaji wakuu wa Wizara ya Afya kabla ya utiaji saini makubaliano ya uboreshwaji wa wodi ya wazazi na watoto Unguja na Pemba, hafla hiyo imefanyika Wizara ya Afya Zanzibar.
  Balozi wa Uholanzi Nchini Tanzania Mr. Jaap Frederiks (wakatikati mbele walio simama)katika picha ya pamoja ya viongozi wa Wizara ya Afya ya Zanzibar wakiongozwa na Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman wa mbele kulia. Sherehe hiyo ilifanyika Wizara ya Afya Mjini Zanzibar.(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
  Na Abdulla Ali  Maelezo-Zanzibar   .
                                      
  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kuokoa maisha ya Wanawake na Watoto kwa kuimarisha Miundombinu ya Afya.
  Hayo ameyaeleza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dr. Saleh M. Jidawi wakati akisaini Mkataba kwa ajili ya utekelezaji wa kuanza kwa mradi wa kuimarisha Afya za Mama na Watoto uliyofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo iliyopo Wilaya ya Mjini Unguja.

  Mkataba huo uliosainiwa na Wizara ya Afya Zanzibar kupitia Katibu Mkuu Dr. Saleh M. Jidawi kwa pamoja na Meneja wa Kampuni ya Simed International ya Uholanzi Nd. Michor Pleijzier uliofanyika siku ya tarehe 11/02/2015 ni miongoni mwa muendelezo wa utekelezaji wa mradi huo ambao awali ulitiwa saini mnamo tarehe 23/12/2014.

  Dr. jidawi amesema kuwa dhamira kuu ya mradi huo ni kuimarisha afya za kina mama na watoto waliozaliwa chini ya mwaka mmoja pamoja na kutoa huduma kwa watoto wengine. Ametanabahisha kuwa utekelezaji wa mradi huo unakwenda sambamba na utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya 2020 uliotafsiriwa na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Zanzibar (MKUZA ii).

  Amesema kuwa mradi huo unajumuisha maeneo mbalimbali ya utekelezaji ikiwemo upatikanaji wa vifaa, tiba, ukarabati wa vifaa, uboreshaji wa miundombinu pamoja na utoaji wa ushauri elekezi kwa Hospitali ya Mnazi Mmoja. Amesema sambamba na hayo mradi huo unakusudia kuviboresha vituo vya Afya 19 vya Unguja na Pemba ili vipate kutoa huduma bora kwa jamii.

  Ametanabahisha kuwa kwa upande wa Hospitali ya Mnazi Mmoja mradi huo utajumuisha vitengo mbalimbali vikiwemo chumba cha upasuaji, maabara, duka la dawa, chumba cha wagonjwa mahututi cha watoto na wazazi, kitengo cha huduma za X-ray, wodi za wazazi, kitengo cha kutakasisha vifaa tiba, eneo maalumu la kuteketeza taka za hospitali pamoja na kitengo cha wagonjwa wa nje (OPD).

  Dr. Jidawi ameeleza kuwa mradi huo wa sekta ya Afya unaakisi maazimio ya Serikali zote mbili ambazo ni Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Uholanzi kwa kufanya kazi pamoja katika nyanja mbalimabali za kimaendeleo ikiwa ni pamoja na uchimabaji wa gesi, uhifadhi wa mwambao wa bahari, uendelezaji wa bandari pamoja na uhifadhi wa Mji Mkongwe.

  Nae Balozi mdogo wa Uholanzi Nd. Jaap Frederiks ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuharakisha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya mradi huo na kazi iliyobakia ni kuanza rasmi kwa maazimio ya mradi huo ambao utachukua takriban Miezi 33 hadi kukamilika kwake. 

  Mradi huo utagharimu shilingi Bilioni 19.5 Tsh, ambapo asilimia 50% ya fedha hizo zimetolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na 50% zilizobaki zimetolewa na Serikali ya Uholanzi, zaidi ya gharama hizo pia Serikali ya Uholanzi imetoa fedha kwa ajili ya uandaaji wa michoro pamoja na ushauri elekezi uliogharimu shilingi Milioni 720 Tsh.
   
  IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0

  NA KAMBI MBWANA, DAR ES SALAAM.

  JAMHURI ya Muungano wa Tanzania, inatarajiwa kufanya Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu kwa nafasi mbalimbali. Ni katika Uchaguzi huo, Watanzania watapata fursa ya kuwachagua madiwani, Wabunge na Rais.


  Uchaguzi huo utafanyika Bara na Visiwani nao watachagua wawakilishi wao wanaoamini kuwa watakuwa na msaada nao kuhakikisha kwamba Zanzibar inapiga hatua.


  Joto kali na msisimko wa aina yake umeshika kasi kutokana na uchaguzi huo. Mengi yanasemwa. Mengi yanasikika pia. Ieleweke kuwa, kila mtu ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa.

  Yoyote anaweza kuwa mbunge au diwani kama sheria inavyosema katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, wale wenye sifa zilizotajwa kwenye urais, nao wana haki hiyo.


  Hata hivyo lazima tufahamu urais si jambo dogo. Ni Mungu pekee anayebariki jambo hilo, ukizingatia kwamba ni nafasi moja inayoshikwa na mtu mmoja, iwe Tanzania au kwingineko kwenye utaratibu huo.

  Tatizo si kugombea nafasi hiyo nyeti ya urais. Tatizo hawa wapambe wa urais wanaojitoa akili kwa kushabikia mambo yasiyokuwa na kichwa wala miguu, hususan kwa wakati huu.


  Vita ya urais ipo katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya wanachama wake wengi kutajwa au kuonyesha nia ya urais mwaka huu. Hadi sasa, wanachama zaidi ya nane wameonyesha nia ya kuwania urais badaye mwaka huu na kuibua joto na msigano wa hali ya juu.


  Baadhi ya wanachama hao ni pamoja na Bernard Membe, Samuel Sitta, Dkt Asha-Rose Migiro, Steven Wassira, January Makamba, Khamis Kigwangwallah, Edward Lowassa, Lazaro Nyalandu na wengineo.  Si dhambi kuonyesha nia ya kuwania nafasi yoyote ya uongozi, lakini ustaarabu unatakiwa ili kudhihirisha hekima yako, busara yako na namna gani ulivyojaliwa uwezo wa kupambanua mambo kwa mitazamo tofauti.

  Sheria zifuatwe. Kwa mfano, wapo watu wanaotajwa kutumia fedha nyingi kushawishi  waungwe mkono katika vijiwe vya kahawa, pombe za kienyeji au katika nyumba za ibada.


  Wale wanaotumia muda mwingi kufanya vikao vya kuungwa mkono bara na visiwani na kupewa majina ya ‘wapambe wa urais’. Jamii inajiuliza maswali mengi dhidi ya watu hao.


  Ikulu kuna nini? Kwanini wahahe usiku na mchana sanjari na kutumia fedha nyingi bila kujua wanapozitoa ili tu watimize ndoto zao? Fedha hizo wamezipa majina mengi mazuri. Leo wanaziita sadaka, rambirambi, takrima au msaada katika mambo mbalimbali ili wasieleweke vibaya.


  Ni fedha chafu kama fedha nyingine. Na zinatolewa na watu wachafu wenye nia chafu, ndio maana baadhi yao huona ni sahihi kusaka nafasi ya urais kwa kutumia fedha nyingi kuwanunua wapambe, wakitaka waimbiwe nyimbo nzuri ili waonekane umuhimu wao.


  Watu hao hawana dhamira ya dhati ya kuwakomboa Watanzania. Wanataka waende Ikulu wakafanye biashara zao na kugawana vyeo wao na wapambe wao wanaotoka povu kuwasafisha mabwana wakubwa hawa wanaotaka Ikulu kwa udi na uvumba.


  Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kulikemea suala hilo ma kusema Ikulu ni Mahala patakatifu. Utakatifu wa Ikulu ya Nyerere, unanajisiwa na hawa wasaka urais kwa fedha.


  Tumeshuhudia kundi likijipambanua dhidi ya wengine, wakiona wao wana nafasi nzuri zaidi ya kupata nafasi ya kuingia Ikulu. Kujiamini huko kumetokana na kuamini wamefanikiwa kuwanunua watu  ambao pengine ndio wenye uwezo wa kuwapitisha katika vikao vya CCM.

  Wanahangaika mchana na usiku kuwawekea mabwana wakubwa wao mazingira mazuri, bila kujua kwamba hawapo sahihi. Muda wa  uchaguzi bado, kampeni za mapema za nini.

  Anapojitokeza mtu hadharani kuanza kumpigia kampeni mtu ni jambo linaloibua maswali mengi na kuhoji uhalali wao na shauku hiyo ya urais. Wiki iliyopita, tulishuhudia baadhi ya wabunge kusimama hadharani mjini Dodoma kwa ajili ya kumpigia debe Lowassa.

  Wabunge kama vile Stephen Ngonyani Profesa (Maji Marefu), John Komba, Mary Chatanda na wengineo walijitoa akili kwa kumsafisha Lowassa na kumtaka agombee urais kwa madai Watanzania wana imani naye.

  Wabunge hawa wana uhakika gani kama Watanzania wote wana imani na Lowassa? Na walitumwa waseme hilo hadharani ili waandishi waone na kuandika kwenye vyombo vyao?

  Basi bora CCM iruhusu kampeni kuliko kuachia vitendo hivi hadharani vikiendelezwa na upande mmoja, maana unawanyima haki wengine katika mchakato huo wa urais.

  Najiulizaa tu, kwani muda wa kampeni umefika? Kwani hawa wabunge na wapambe wote wa urais hawajui wakati bado? Hizi ni rafu na zinatakiwa ziangaliwe upya ili kulinda heshima ya chama.

  Wana CCM wote, wabunge, madiwani na viongozi wa serikali wanapaswa kuisimamia ilani ya  Uchaguzi wa chama chao kuwapatia maendeleo Watanzania, kuliko kuelemea kwenye kampeni za mapema za urais.

  Majimbo yao yamekuwa na changamoto nyingi na pengine wapiga kura wao wamekata tamaa na maisha. Badala ya kubuni, kusimamia miradi ya maendeeleo, wapo ‘busy’ kuwanadi wasaka urais kinyume cha sheria na maadili ya CCM.

  Hivi wabunge hawa na wapambe wengine wa Lowassa hawajui kama ni makosa kufanya kampeni mapema? Wasubiri muda ufike ili wajinafasi. Ikumbukwe Lowassa ni kati ya makada wa CCM walioadhibiwa kwa rafu za mbio za kumrithi Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

  Pamoja na kuadhibiwa huko, bado wapambe wanajitoa akili. Wanaona wanayo haki kuliko wengine. Najiuliza tu, hivi kila mmoja akisimama kumpigia debe mgombea wake wakati huu serikali itafanya kazi?

  Lowassa asimame, Membe ashangiliwe na Makamba hali kazalka. Basi hii itakuwa nchi ya vituko isiyoheshimu taratibu zake ilizojiwekea ili kuepusha mikanganyiko kwa mambo nyeti kama urais.

  Wakati nasema haya, nakumbuka namna gani nchi iliyumba kabla ya makada hao wa CCM kuadhibiwa. Walipishana makanisani, misikitini na katika vijiwe vya bodaboda, wakijificha kwenye kivuli cha kusaidia jamii. Fedha nyingi zilitolewa na baadhi yao kwa kivuli cha misaada.

  Viongozi wa CCM wakawatia hatiani na kuwapunguza makali yao. Je, wangapi wamepunguza kasi baada ya adhabu hiyo? Na wanaoendelea ndio kusema wapo juu ya sheria kuliko wote?

  Ni wakati wa wapambe hao wa urais kujitathimini upya. Wajiangalie mara mbilimbili juu ya mambo wafanyayo? Si kweli kama Watanzania wote wanaamini wanachotaka wapambe hao.
    Wapunguze joto na haraka. Wasubiri muda wa kutangaza nia ufike na kupitishwa pia na chama chao ili wawanadi vizuri.

  Hata wakitaka kuwabeba mgongoni ruhusa. Wakitaka kuwafuta viatu au kuwabebea mikoba yao pia hawatakatazwa. Si wakati huu.

  Haraka hizi ndio zinazosababisha baadhi ya vitendo viovu, matusi, kejeli na chuki kwa baaadhi ya makundi hayo ya urais. Baadhi yao wamekosa busara na uvumilivu katika suala hilo.

  Fuatilia vyombo vya habari bila kusahau mitandao ya kijamii. Hali ni mbaya na yapo makundi yanayofanya kampeni za wazi kabisa. Nyimbo za wagombea zinatungwa na kusambazwa kwa nguvu zote.

  Hizo si kampeni, zinaitwaje. Hizo si rushwa nguvu hizi zinatoka wapi na faida yake ni nini? Wasanii wanaokwenda studio kurekodi nyimbo za mapambio kabla ya muda wanapata wapi pesa? Na kama wanatoa wenyewe kwa mapenzi yao, mara ngapi wamekemewa?

  Ifikie wakati tuwe na subira na uvumilivu. Hili litajenga heshima ya CCM na Taifa kwa ujumla katika kutafutwa mrithi wa JK, rais anayemaliza muda wake baadaye mwaka huu.

  Purukushani hizo zinaangaliwa na watu wote, wakiwamo wapinzani wanaosubiri kuona nani anasimamishwa na CCM katika urais mwaka huu. Wanataka kuona na kujipanga pia. Huenda wanatumia muda huo kujiridhisha juu ya wanaotajwa na mapungufu yao ili wawabane kirahisi, hususan atakapoteuliwa mtu mchafu na asiyekuwa na mvuto.

  Sina shaka na wanaotaka urais Tanzania. Shaka yangu ni vitendo viovu vilivyoshika kasi vya kufanya kampeni mapema. Ni mwanzo wa kuingiza choko choko endapo baadhi watamwagwa kwa kufanya kampeni mapema.

  Hawa hawa wapambe waliojitoa akili watasimama hadharani kupinga uamuzi huo na kuibua migogoro,  wakati wanajua sheria na miiko yote, wakiwamo viongozi wa chama wanaotumika pia katika harakati hizi.

  Ya nini haraka? Tusubiri muda ukifike na kuamua hatma ya nchi yetu, huku tukiomba apatikane mtu bora na mwenye maadili, bila kusahau ndoto za kuliletea maendeleo Taifa letu. Mungu atamuinua Mtanzania mmoja kwa ajili ya kugombea nafasi hiyo kwa CCM na kuungana na wengine wa upinzani ili kumpata rais wetu mpya.

  Atakuwa ni chaguo la Watanzania wote. Si kama hivi inavyoaminishwa na wapambe kila uchao. Wayafanyayo yapo kwa maslahi yao si ya Watanzania wote. Katika harakati hizo, wajisemee wao na si Watanzania wote.

  Mwisho natoa rai kwa CCM juu ya kuwamulika wapambe au wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali za uongozi za udiwani, ubunge na urais kuhakikisha wanafuata sheria za chama chao.

  Wasubiri mchakato huo ufunguliwe rasmi. Wasijitoe akili kwa kufanya kampeni kabla ya muda. Watakaobainika, majina yao yatupwe bila kuangalia wangapi watalia au watacheka. Hili litakiletea chama heshima na kudhihirisha ukongwe wake na kisima cha kupika viongozi wenye maadili.
  kambimbwana@yahoo.com+255712053949
  Mwisho

  0 0

  MULO1
  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akiweka jiwe la Msingi katika Wodi ya Watoto, Zahanati ya Lugeye. 
  MULO3 
  Walio kaa chini wananchi wa Nyanguge wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Mwanza.
  ………………………………………………………………………………………
  Na: Atley Kuni- Mwanza.

  Wazee katika Mkoa wa Mwanza, wamemshauri Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, kuanza kulima zao la alizeti ili kuuwezesha mkoa huo kuinuka kuichumi kutokana na hali mbaya ya mazao kama pamba kupoteza umaarufu kwenye sekta ya uchumi wa mkoa huo.
   Wakizungumza katika kikao kilicho wakutanisha wazee hao na mkuu wa mkoa hivi karibuni katika hoteli ya Mwanza, wazee hao walisema kutokana na hali isiyoridhisha kwa zao kama pamba ambalo ndilo lilikuwa zao kuu la uchumi wa mkoa huu kupoteza umaarufu ni vema sasa jamii ikabadilika na kuhamishia nguvu zake kwenye zao la alizeti.

  Akizungumza kwa niaba ya wazee wenzake, aliyekuwa Mkuu wa kwanza wa wilaya ya Ilemela, Jared John Gachocha, alisema, haoni sababu ya mkoa wa Mwanza kushindwa kutilia mkazo zao la alizeti ambalo gharama zake za uzalishaji ni nafuu zaidi ukilinganisha na pamba.” Mh. Mkuu wa mkoa mimi nadhani kipindi hiki tushughulike kufa na kupona kwenye alizeti, sioni kwa nini wenzetu wa Singida watupite katika hili, zao la alizeti ni rahisi mno kulilima halina usumbufu halihitaji mbolea nyingi, haliitaji maji mengi na maandalizi yake kwakweli ni rahisi lakini pia faida yake ni kubwa” alisema na kuongeza kuwa “hali hiyo itasaidia mkoa kujitosheleza kwa mafuta lakini pia kuweza kuuza kwa watu wengine.

  Mbali ya zao la alizeti wazee hao pia walimuasa mkuu huyo wa mkoa, kuelekeza nguvu zaidi kwenye masuala ya ufugaji, wakisema kuwa tupo nyuma sana katika masuala ya mifugo huku wakitolea mfano nchi ya Kenya kwamba Ng’ombe anauwezo wakutoa maziwa lita hadi 20 tofauti na Tanzania, hali inayo walazimu wazee hao kumuasa mkuu wa mkoa kuwataka wafugaji kuachana na ufugaji wa kizamani na badala yake watafute mitamba itakayoweza kuleta tija kwa wafugaji. “Ni ukweli usiopingika kwamba hapa kwetu kumpata ng’ombe anayeweza kukupatia lita 10 za maziwa ni nadra sana hivyo tuwashawishi wakulima waweze kutafuta mitamba ambayo itakuwa niya kisasa ili waweze kukuza uchumi wao lakini uchumi wa mkoa kwa ujumla.

  Awali akizungumza mkuu wa Mkoa wa Mwanza, kabla yakuanza kupokea maoni ya wazee hao, alisema mkoa wa Mwanza wenye watu Milioni mbili na laki saba na mia saba sabini na mbili mia tano na tisa, huku mkoa ukiwa unachangia Trioni 4.9 katika pato la taifa, Watu wake milioni moja uchumi wao unategemea zaidi katika Sekta ya Uvuvi, “Wazee wangu nimewaiteni tusaidiane kuongoza mkoa huu, mkoa huu ni mkubwa na changamoto tulizo nazo ni nyingi” alisema Mulongo na kuongeza kuwa, “kati ya watu mil. 2.7, watu Milioni moja wanategemea ziwa kuanzia mvuvi ziwani hadi mparuaji na mchuuzi mdogo mdogo wa mtaani sasa hali ya ziwa letu kwa upande wa uzalishaji sio salama sana, tuna kwendaje lazima tujipange kisawasawa alisema Mulongo.

  Mkuu wa mkoa wa Mwanza toka amewasili mkoa wa Mwanza, ameweka utaratibu wakukutana na watu wa makundi mbali mbali mkoani hapa ili kufahamu changamoto ambazo zipo ili waweze kuzitatua kwa kushirikiana kwa pamoja, makundi ambayo tayari yamekutana na mkuu huyo wa mkoa hadi sasa ni pamoja na, Wananchi wa kawaida kwa kuzungumza nao kwenye mikutano ya hadhara na kusikiliza kero zao na kuzipatia ufumbuzi, Wafanya biashara wadogo ambao alifanikisha kufanyika kwa uchaguzi wao, wakuu wa taasisi za umma zilizoko mkoani hapa, viongozi wa dini, viongozi wa kisiasa na asasi zisizo za kiraiya.

  Mkoa wa Mwanza ni mkoa wa pili kwa uchangiaji wa pato la taifa kwa asilimia 9.15% ukitanguliwa na Mkoa wa Dar Es Salaam, huku wastani wa pato la mwananchi wa kawaida ikiwa ni Tshs. 910,824 kwa mwaka.

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua jengo la upasuaji katika hospitali ya rufaa ya Mawenzi mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro muda mfupi baada ya kulifungua jana.Kulia ni Naibu Waziri wa Afya Dkt.Steven Kebwe.KJ2 
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wauguzi wa hospitali ya rufaa ya Mawenzi mjini Moshi muda mfupi baada ya kufungua jengo la upasuaji na kuweka jiwe la msingi kuzindua ujenzi wa wodi ya mama na watoto katika hospitali hiyo jana.(wanne kulia ni Naibu waziri wa Afya Dkt.Steven Kebwe,wanne kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama,Kushoto ni Mbunge wa Vunjo Agustino Lyatonga Mrema,na wapili kushoto ni Mbunge wa Moshi Vijijini Dkt.Cyril Chami. KJ3KJ4 
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt.Ramadhan Dau pamoja na wadau wengine wakitazama ramani ya jengo jipya la kitega uchumi la NSSF mjini Moshi Kilimanjaro Commercial Complex wakati wa hafla ya ufunguzi jana. KJ6 
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na chipikizi wa Tanzania Girl Guides wakati wa hafla ya ufunguzi wa jengo la kitega uchumi la NSSF mjini Moshi jana.Tanzania Girl Guides,UMATI,Tanzania Red Cross ni wadau wa NSSF katika mradi huo. KJ7 
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt.Ramadhani Dau baada ya hafla ya ufunguzi wa jengo jipya la kitega uchumi la NSSF mjini Moshi jana.Katikati ni Waziri wa Kazi na Ajira Mh.Gaudensia Kabaka(picha na Freddy Maro)

  0 0


  Upo wakati kwenye ndoa ambapo mmoja wanandoa anaweza akawa anataka kuuza au kubadili jina la nyumba/kiwanja bila ridhaa ya mwenzake ilihali nyumba hiyo ni ya familia. Lakini pia nje ya hilo kuna mazingira ambayo mtu anaweza kuwa si mwanandoa lakini ana maslahi katika nyumba au kiwanja cha mtu fulani na anataka kuzuia nyumba/ kiwanja hicho kisibadilishwe jina au kisiuzwe. Kisheria jambo hilo linaruhusiwa na huitwa zuio( Caveat).

  Hili sio zuio la kwenda mahakamani kama mazuio tuliyoyazoea.Hili ni zuio jingine kama nitakavyolieleza. Aidha kuzuia hati isibadilishwe kimsingi ni sawa na kuzuia nyumba isiuzwe. Hii ni kwakuwa hakuna namna ambavyo mnunuzi anaweza kununua kitu ambacho hakiwezi kubadilika na kuingia katika jina lake. Ikiwa mke ana wasiwasi kuwa mume anaweza kumzunguka na kuuza mali ya familia au mume ana wasi wasi juu ya uwezekano wa mke kuuza basi wanayo ruhusa ya kuweka zuio ili hati ya nyumba isibadilishwe. Yapo mambo mengi kuhusu hili nitaeleza baadhi.


  0 0

  Serikali imeanza kusambaza nakala milioni mbili za Katiba Inayopendekezwa nchini kote ili kuwawezesha wananchi kuisoma na kushiriki katika Kura ya Maoni iliyopangwa kufanyika tarehe 30 Aprili mwaka huu.

  Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro amesema leo (Jumatano, Februari 11, 2015) jijini Dar es Salaam kuwa kati ya nakala hizo zilizochapwa jijini Dar es Salaam, nakala 1,800,000 zinasambazwa Tanzania bara na nakala 200,000 zinasambazwa Tanzania Zanzibar.

  Kwa mujibu wa Waziri Migiro, hadi kufikia jana (Jumanne, Februari 10, 2015), jumla ya nakala 707,140 zilikuwa zimesambazwa katika mikoa 12 ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar ambayo imepata nakala 200,000 na kuwa kazi hiyo inaendelea vizuri na inatarajiwa kukamilika katika muda mfupi ujao.

  Mikoa hiyo na nakala ziliozosambazwa katika mabano ni Katavi (15,640), Rukwa (27,040), Ruvuma (47,740), Mbeya (78,640), Simiyu (34,840), Mara (52,540), Tabora (58,540) na Kigoma (41,440). Mikoa mingine ni Kagera (54,340), Geita (36,940), Mwanza (57,040) na Pwani ambapo usambazaji umeanza kwa wilaya ya Mafia ambayo imepata nakala 2,400.

  “Idadi ya nakala ya Katiba Inayopendekezwa kwa kila mkoa inategemea na wingi wa kata katika mkoa, ndiyo maana baadhi ya mikoa unaona imepata nakala nyingi,” amesema Dkt. Migiro ofisini kwake wakati akiongea na baadhi ya waandishi wa Habari waliotaka ufafanuzi kuhusu hatua iliyofikiwa katika kazi ya uchapishaji na uasambazaji wa nakala za Katiba Inayopendekezwa.

  Kwa mujibu wa Waziri Migiro, kuna zaidi kata 3,800 nchini kote na lengo la Serikali ni kusambaza nakala 300 katika kila kata ambazo zitasambazwa kwenye vijiji, vitongoji na mitaa kupitia Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Miji, Manispaa na Majiji.

  Kuhusu taasisi za elimu na dini, Waziri Migiro amesema Serikali imepanga kusambaza nakala 658,400 kwa taasisi za elimu, dini, vyama vya siasa na asasi za kiraia na kuwa usambazaji huo utaanza hivi karibuni.

  Pamoja na usambazaji huo, Waziri Migiro amewakumbusha wananchi ambao bado hawajapata nakala za Katiba Inayopendekezwa, kuisoma kupitia tovuti ya Wizara ya Katiba na Sheria (www.sheria.go.tz) na tovuti ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (www.agctz.go.tz).

  0 0


  0 0

  DSC_8983

  Balozi wa Japan nchini, Mh. Masaki Okada (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Hussein Kidanto wakitiliana saini mkataba wa fedha za ruzuku shilingi milioni 70/ zilizotolewa na serikali ya Japan kwa ajili ya kununua magari mawili ya wagonjwa (Ambulance). Tukio hilo lilishuhudiwa na viongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na Mkurugenzi wa Hospitali hiyo aliyemaliza muda wake Dkt. Marina Njelekela.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).

  Na modewjiblog team.

  Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli ameishukuru Japan kupitia Balozi wake alioko nchini kwa kusaidia miradi inayochangia maendeleo ya moja kwa moja hususani afya, elimu na maji. Dk. Magufuli alisema hayo jana katika makazi ya Balozi wa Japan Nchini, Masaki Okada yaliyopo Masaki Jijini Dar es Salaam wakati wa kutiliana na saini za mkataba wa fedha za ruzuku zitakazoenda kusaidia maendeleo kwa jamii ikiwemo Jimbo la Chato na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

  Katika hafla hiyo, Dk. Magufuli aliambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Wilaya ya Chato, pamoja na Wakurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akiwemo Mkurugenzi wa zamani wa hospitali hiyo Dk. Marina Njelekela pamoja na wa sasa Dk. Hussein Kidanto.
  DSC_8984
  Balozi Okada na Mkurugenzi Dkt. Kidanto wakibadilishana hati za mikataba hiyo. Dk. Magufuli alishuhudia utiaji wa saini wa mikataba hiyo ambapo Balozi Okada alitoa kiasi cha sh milioni 70, kwa ajili ya ununuzi wa magari ya kisasa ya kubebea wagonjwa (Ambulance) kwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambayo mpaka sasa inadaiwa wana Ambulance moja pekee.

  Mbali na kiasi hicho cha fedha, Pia Dk. Magufuli alishuhudia utiaji wa saini huo ambapo Balozi huyo alitoa sh milioni 165, kwa ajili ya kujenga kiwanda cha kukamulia mafuta ya Alizeti yenye viwango vya Kimataifa.

  Dk. Magufuli alishukuru kwa niaba ya Serikali na pia akiwa kama Mbunge wa Chato, alisema Japan imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia juhudi za maendeleo kwa wananchi mbalimbali wa mijini na vijijini. Hata hiyvo Dk. Magufuli alishtushwa na hali ya Hospitali hiyo ya Taifa kuwa na Ambulance moja pekee wakati wao Halmashahuri ya Chato hadi sasa wameweza kuwa na Ambulance tatu.
  DSC_8991
  Balozi wa Japan nchini, Mh. Masaki Okada (kulia) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Chato mkoani Geita, Ndugu Clement Berege wakitiliana saini mkataba wa fedha za ruzuku shilingi milioni 165 kwa ajili ya kujengea kiwanda cha kukamulia mafuta ya Alizeti wilayani Chato mkoani Geita.

  “Nimeshtushwa sana na hili la kusikia kuwa mna Ambulance moja pekee. Yaani hata Chato pale tuna Ambulance tatu. Naomba Mkurugenzi mpya, uendelee kuomba kwa mabalozi wengine ili tuweze kupata Ambulance nyingi zaidi pia wanahabari mtusaidie kwa hili.” Alisema Dk. Magufuli. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Chato, alipogeza Japan, kwa msaada wao kwani utaenda kusaidia Halmashauri ya Chato kama ulivyokusudiwa.
  “Wakazi wa Chato ni wakulima, wafugaji na wavuvi, hivyo kwa msaada huu pia utakuwa chachu ya maendeleo hasa kwa kilimo cha Alizeti.” Alisema Mkurugenzi huyo.
  DSC_0393
  Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli akitoa shukrani kwa serikali ya Japan inayowakilishwa na Balozi Masaki Okada baada ya kushuhudia utiaji saini wa mikataba ya fedha za ruzuku shilingi milioni 235 sawa na dola za Kimarekani 136,015 zilizotolewa na serikali ya Japan.

  Japan imekuwa ikisaidia mara kwa mara wilaya ya Chato, ambapo mwaka 2013, Japan walitembelea huko na kujionea shida mbalimbali kwa wakulima wa Alizeti hivyo wameona kusaidia msaada huo. Mbali na kusaidia mashine hiyo ya Alizeti Japan pia imekuwa ikisaidia maendeleo mbalimbali ikiwemo shule za msingi, Sekondari na huduma za afya kwa Hospitali iikwemo wodi ya akina mama.

  DSC_0347
  Mkuu wa wilaya ya Chato, Bw. Rodrick Mpogolo akizungumza kwenye hafla hiyo ambapo pia alimshukuru Balozi Mh. Masaki Okada kwa kutengeneza ajira wilayani kwake kupitia msaada huo.
  DSC_0342
  Pichani juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa na waandishi wa habari waliohudhuria hafla hiyo fupi iliyofanyika nyumbani kwa Balozi Mh. Masaki Okada jana jijini Dar.
  DSC_0382
  DSC_0399
  Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli akiteta jambo na Balozi wa Japan nchini, Mh. Masaki Okada mara baada ya hafla fupi ya utiaji saini wa mikataba ya fedha za ruzuku kwa ajili ya kuendeleza miradi inayochangia maendeleo ya moja kwa moja nchini.
  DSC_0405
  Waziri wa Japan nchini, Mh. Masaki Okada akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mara baada ya kuhitimisha zoezi la utiaji saini wa mkataba wa fedha za ruzuku kwa ajili ya kununua magari mawili ya wagonjwa (Ambulance) zilizotolewa na serikali ya Japan.
  DSC_0415
  Balozi wa Japan nchini, Mh. Masaki Okada katika picha ya pamoja na Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli pamoja na viongozi wa halmashauri ya Chato.

  0 0


  Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Kijerumani ya Kreissparkasse Tubingen, Christoph Gogler, (wapili kushoto0, akimkabidhi mfano wa hundi ya euro 2,000, mkurugenzi mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya TPB, jijini Dar es Salaam, Jumatanoi Feb 12, 2015. Benki hiyo YA kIJERUMANI NA tpb, pia wamesaini makubaliano ya ushirikiano baina yao. Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Kijerumani ya Kreissparkasse Tubingen, Christoph Gogler, (wapili kushoto0, akimkabidhi mfano wa hundi ya euro 2,000, mkurugenzi mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya TPB, jijini Dar es Salaam, Jumatanoi Feb 12, 2015. Benki hiyo YA kIJERUMANI NA tpb, pia wamesaini makubaliano ya ushirikiano baina yao.Mkurugenzi Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi, (Kulia), na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Kijerumani ya Kreissparkasse Tubingen, Christoph Gogler wakitia saini makubaliano ya ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili za kifedha malao makuu ya TPB, jijini Dar es Salaam, Jumatano Feb. 11, 2015. Ujerumani itakuwa ikitoa mafunzo kwa wafanyakazi wa TPB ili kuwajengea uwezo katika fani mablimbali hsusan huduma kwa wateja. Pia taasisi hiyo imeipatia TPB eURO 2,000 kwa madhumuni hayo hayo. Mkurugenzi Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi, (Kulia), na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Kijerumani ya Kreissparkasse Tubingen, Christoph Gogler wakitia saini makubaliano ya ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili za kifedha malao makuu ya TPB, jijini Dar es Salaam, Jumatano Feb. 11, 2015. Ujerumani itakuwa ikitoa mafunzo kwa wafanyakazi wa TPB ili kuwajengea uwezo katika fani mablimbali hususan kitengo cha huduma kwa wateja. Pia taasisi hiyo imeipatia TPB EURO 2,000 kwa madhumuni hayo hayo.Mwanasheria wa TPB, Mystica Mapunda Ngongi, (Kulia) na mwakilishi na msauri wa taasisi ya Kijerumani ya SBFIC, Clause Thiele, wakisaini ili kuthibitisha makubaliano hayo. Mwanasheria wa TPB, Mystica Mapunda Ngongi, (Kulia) na mwakilishi na msauri wa taasisi ya Kijerumani ya SBFIC, Clause Thiele, wakisaini ili kuthibitisha makubaliano hayo.Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi (wapili kulia) akipokea hundi yenye thamani ya Euro 2,000 kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Kreissparkasse Tübingen ya Ujeruman, Dk. Christoph Gögler. Fedha hizo ni kwaajili ya kuendeshea mafunzo kwa wafanyakazi wa Benki hiyo, kulia ni Mwakilishi wa Benki hiyo, Claus Thiece na kulia kwae ni Meneja Rasilimali watu wa TPB, Peter Mapigano. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi (wapili kulia) akipokea hundi yenye thamani ya Euro 2,000 kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Kreissparkasse Tübingen ya Ujeruman, Dk. Christoph Gögler. Fedha hizo ni kwaajili ya kuendeshea mafunzo kwa wafanyakazi wa Benki hiyo, kulia ni Mwakilishi wa Benki hiyo, Claus Thiece na kulia kwae ni Meneja Rasilimali watu wa TPB, Peter Mapigano.
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Kreissparkasse Tübingen ya Ujeruman, Dk. Christoph Gögler (kushoto) pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi wakisaini hati ya makubaliano ya ushirikiano wa taasisi hizo. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Kreissparkasse Tübingen ya Ujeruman, Dk. Christoph Gögler (kushoto) pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi wakisaini hati ya makubaliano ya ushirikiano wa taasisi hizo.Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Kreissparkasse Tübingen ya Ujeruman, Dk. Christoph Gögler (kushoto) akizungumza na wanahabari katika hafla ya ukabidhi hundi yenye thamani ya Euro 2,000 kwa Benki ya Posta Tanzania (TPB) leo Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Kreissparkasse Tübingen ya Ujeruman, Dk. Christoph Gögler (kushoto) akizungumza na wanahabari katika hafla ya ukabidhi hundi yenye thamani ya Euro 2,000 kwa Benki ya Posta Tanzania (TPB) leo Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi.

  0 0

  Msafara wa Rais Jakaya Kikwete ukiwasili katika jengo la Kitega Uchumi la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ,NSSF kwa ajili ya ufunguzi rasmi wa jengo hilo.
  Baadhi ya wananchi waliohudhuria sherehe hiyo ya uzinduzi wa jengo la kitega uchumi la NSSF.
  Kikundi cha Ngoma kikitoa burudani.
  Mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii,NSSF ,Ramadhan Dau akizungumza wakati wa sherehe ya uzinduzi wa jengo hilo la kitega uchumi.
  Wawakilishi wa Red Cross ambao pia ni wabia katika jengo hilo.
  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama akizungumza wakati wa sherehe ya uzinduzi wa jengo hilo la NSSF.
  Waziri wa kazi na Ajira ,Gaudensia Kabaka akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo hilo.
  Wawakilishi wa Girl Guides ambao pia ni wabia katika jengo hilo wakifurahia jambo.
  Rais Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Jengo la Kitega Uchumi la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii,NSSF mkoani Kilimanjaro.
  Viongozi wa UMATI toka kulia ni Mkurugenzi wa fedha stephen lutashubila akifuatiwa na Mkurugenzi wa UMATI ,Lulu Ng'wanakilala na anayemfuatia ni  Meneja Utetezi na Ukusanyaji Rasilimali wa UMATI ,Meshack Mollel.
  Baadhi ya viongozi wa taasisi mbalimbali wakiwa katika sherehe hiyo ya uzinduzi wa jengo jipya la kisasa la Kitega Uchumi la NSSF.
  Rais Kikwete akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa jengo la kitega uchumi la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF .
  Rais Kikwete akizungumza na mstahiki meya wa manispaa ya Moshi ,Jafary Michael wakati akitembelea jengo hilo.
  Jengo jipya la kisasa la kitega uchumi la NSSF linavyoonekana kwa ndani.
  Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa UMATI wakiwa ni wabia katika jengo hilo.
  Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wafanya kazi wa Red Cross wakiwa na wabia katika Jengo hilo.
  Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Wahandisi walioshiriki katika ujenzi wa jengo hilo.
  Rais Kikwete akiwa katika picha ya Pamoja na wafanyakazi wa NSSF mkoa wa Kilimanjaro.
  Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo wa vyama vya siasa.
  Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Girl Guides .
  Rais Kikwete akizungumza na Mshereheshaji katika uzinduzi wa Jengo la kitega Uchumi la NSSF,Peter Mavunde .
  Rais Kikwete akiondoka mara baada ya kuzindua jengo hilo la kitega Uchumi.
  Rais Kikwete akizungumza na Mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ,NSSF,Ramadhan Dau.
  Msafara wa Rais Kikwete ukiondoka katika jengo jipya la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF muda mfupi mara baada ya Rais kuzindua rasmi jengo hilo.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0

  H1Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Henry Riaya (kulia) akisaini Waraka wa Brighton Declaration kuhusiana na usawa wa kijinsia katika michezo, hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo (jana) kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bi. Juliana Yassoda.H2Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Maendeleo ya Michezo Bi Juliana Yassoda wa kwanza kushoto akisaini Waraka wa Brighton Declaration kuhusiana na usawa wa kijinsia katika michezo, hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo (jana).wa kwanza kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Henry Riaya.H3Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Henry Riaya (kulia) akisisitiza jambo mbele ya wanahabari hawapo pichani kuhusiana na Waraka wa Brighton Declaration kuhusiana na usawa wa kijinsia katika michezo
  H4Baadhi ya wanahabari wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Henry Riaya hayupo pichani akizungumza na wanahabari hawapo pichani katika hafla ya kusaini Waraka wa Brighton Declaration kuhusiana na usawa wa kijinsia katika michezo.Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Benjamin Sawe -WHVUM

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi wa Saudi Arabia, Hani Abdullah Mominah, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo Feb 12, 2015 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Saudi Arabia, Hani Abdullah Mominah, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo Feb 12, 2015 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi wa Saudi Arabia, Hani Abdullah Mominah, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika wakati Ofisini kwa Makamu Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo Feb 12, 2015 wakati Balozi huyo alipofika kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini. Picha na OMR

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaapisha Balozi mpya wa Tanzania nchini Kenya na Naibu Katibu mkuu wa Wizara ya Fedha. Katika hafla hiyo iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Kikwete amemwapisha Bwana John Haule kuwa balozi mpya wa Tanzania nchini Kenya na Dkt.Hamisi Mwinyimvua ameapishwa kuwa naibu katibu mkuu wa Wizara ya Fedha.
  Balozi mpya wa Tanzania nchini Kenya Bwana John Haule akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo.
  Balozi mpya wa Tanzania nchini Kenya Bwana John Haule akipeana mkono na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mara baara ya kula kiapo Ikulu jijini Dar es salaam leo.
  Naibu Katibu mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Hamisi Mwinyimvua akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiirekebisha tai ya mtoto Amani Mwinyimvua(11) muda mfupi baada ya kumwapisha Baba yake Hamis Mwinyimvua kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha katika hafla iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi(picha na Freddy Maro)

  0 0

   Balozi wa Iran nchini Tanzania,Mh.Mehdi Aghajafari akimpokea Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh.Dkt.Mahadhi Juma Maalim (Mb) alipowasili katika hafla ya kusherehekea siku ya Taifa la Iran iliyofanyika kwenye makazi ya Balozi huyo Jijini Dar es Salaam jana usiku.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh.Dkt.Mahadhi Juma Maalim (Mb) akizungumza mbele ya wageni mbalimbali walioalikwa katika hafla ya siku ya Taifa la Iran iliyofanyika kwenye makazi ya balozi wa Iran Jijini Dar es Salaam.
   Balozi wa Syria nchini, Mhe.Abdulmonem Annan (kushoto) Jaji mkuu wa Tanzania,  Mhe. Mohamed Chande Othman (katikati) na Balozi wa Yemen nchini, Mhe.Abdulla Hassan Alamri wakimsikiliza kwa makini Mgeni Rasmi kwenye hafla ya Siku ya Iran, Naibu waziri Dkt. Mahadhi.
   Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Hassan Simba Yahaya (kulia) akiwa na Maafisa kutoka Wizara hiyo Bw. Mkumbwa Ally (kushoto) na Bw. Leonce Bilauri (katikati) wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri (hayupo pichani) katika hafla hiyo.
   Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe.Dkt.Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akisalimiana na Balozi wa Syria nchini Mhe. Abdulmonem Annan kwenye sherehe hizo.
   Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe.Mohamed Chande Othman akizungumza jambo na  Mhe.Dkt.Mahadhi kwenye hafla ya siku ya Iran.
  Picha na Reuben Mchome
  ================================================
  STATEMENT BY HON. DR. MAHADHI JUMA MAALIM, (MP) DEPUTY MINISTER OF FOREIGN AFFAIRS AND INTERNATIONAL COOPERATION OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA ON THE OCCASION OF THE NATIONAL DAY OF THE ISLAMIC REPUBLIC OF IRAN DAR ES SALAAM, 11TH FEBRUARY, 2015
  Your Excellency Ambassador Mahdi, Aghajafari Ambassador of the Islamic Republic of Iran;
  Your Excellency Juma Alfani Mpango, Ambassador of the Republic of Congo and Dean of the Diplomatic Corps;
  Your Excellency Nasri Abujaish, Ambassador of the State of Palestine, and Dean of the Arab Group
  Your Excellencies Ambassadors and High Commissioners;
  Your Excellencies Heads of Diplomatic Missions;
  Your Excellencies Heads of International Organizations;
  Distinguished Guests;
  Ladies and Gentlemen,
  I feel very honoured to stand before you on this special evening when we mark the auspicious event of the 36th National Day of the Islamic Republic of Iran. Indeed it is a particular privilege to join you all this evening as I represent the Government and the people of the United Republic of Tanzania to celebrate this historic day in the history of your beautiful country Your Excellency.
  Your Excellency,
  Distinguished Guests,
  Ladies and Gentlemen,
  At this juncture, allow me therefore, on behalf of the Government and the People of the United Republic of Tanzania, to take this opportunity to extend to Your Excellency, and through you to the Government and the People of the Islamic Republic of Iran, our profound and heartfelt congratulations on the occasion of celebrating the 36th Anniversary of the Islamic Revolution of your country.
  Your Excellency,
  As we join you in this auspicious occasion, I wish to express my satisfaction on the bilateral relations that so happily exist between our two countries and our peoples despite being geographically separated by a long distance.
  Such a good relationship can be traced back 1,000 years ago, when Iranians, then under the Shiraz Empire sailed to East Africa.
  Tanzania and Iran also have a connection of culture, where there is some similarities of words in both Swahili as well as Persian languages. The Swahili words, "chai" = tea, "achari" = pickle, "serikali" = government, "diwani" = councillor, "sheha" = village councillor, are some of the words also used in Persian bearing testimony to the older connections with Persian merchants. 
  Your Excellency,
  Distinguished Guests,
  Ladies and Gentlemen,
  Our two countries already have a good framework for bilateral cooperation.
  This is the Joint Permanent Commission (JPC), to coordinate cooperation in the trade, economic, technical and cultural spheres. We are all aware of the inherent obstacles that have militated against the role initially envisaged for the Joint Commission. It is our duty, to learn from our experiences and work together to find ways to make (JPC) arrangement more effective to strengthen our cooperation.
  The two countries maintain good cooperation in different sectors; these include health, agriculture, culture, and from vocational to higher education. The two countries are geared to expand and strengthen cooperation in many areas of mutual interests of both countries.
  At the Government level there have been exchange of visits at the national levels, to mention a few and recent ones include the then First Vice President of the Islamic Republic of Iran who visited Tanzania in 2012 and the then Minister of Information, Youth, Culture and Sport Dr. Emmanuel Nchimbi visited Iran in 2012. Last week Hon. Dr. Mohammad Javad Zarif, Foreign Minister of Iran, was in our country for a two day official visit.
  At global spheres, both countries have been cooperating in all matters of common concerns in Non Alignment Movements (NAM) and United Nations (UN). Allow me at this occasion to reaffirm our commitment to strengthen the close cooperation that exists between our two friendly countries and people.
  Your Excellency,
  In contemporary world, we all recognize the power and position of private sector.
  Thus, the existing friendly relations between our two countries are set to be the corner stone for further expansion and deepening in trade and investment between our private sectors. The just recent visit by Hon. Dr. Zarif to Tanzania with heavy weight CEOs and other prospective investors from Iran to Tanzania set a stepping stone for forging a close economic cooperation between the two countries by increasing trade and investments. Investors from Iran had fruitful discussions with their counterparts organized by Tanzania Chambers of Commerce, Industries and Agriculture (TCCIA).
  Through this spirit of enhancing strong cooperation, Tanzania invites more investors from Iran to come to Tanzania to explore opportunities for investment for mutual benefit of both countries. We can expand economic relations to include areas like agribusiness, agro-processing, iron ore and ore extraction and processing, banking and tourism. To walk the talk, I am very happy to note that during the visit by Hon. Zarif, Tanzania and Iran have signed Bilateral Agreement on the Promotion and Protection of the Investments between the two Countries. On the same vein, the third round of negotiations on Avoidance of Double Taxation and Prevention from Fiscal Evasion (DTA) are underway.
  Your Excellency,
  Distinguished Guests,
  Ladies and Gentlemen,
  Your Excellency, once again, it is an honour for me to share with you this celebrations of your great country National Day, and I wish to reiterate our sincere congratulations to Your Excellency and  through you, to the Government and brotherly people of the Islamic Republic of Iran, for marking 36th anniversary of your great Islamic Revolution.
  We wish you more success in the coming years and decades.
  Thank you all for listening.

  0 0

  DSC_0333
   
  “NILIAMUA kuanzisha Msama Promotions baada ya kuona muziki wa Injili umesahaulika na unashuka thamani yake.“Hivyo kwa kushirikiana na wenzangu nikaona ni busara kuuinua ili tuwe kama wenzetu Afrika Kusini ambao wana waimbaji wa nyimbo za Injili wanaotamba kama Rebecca Malope, Itani Madima, Steve Kekane, Vuyo Mokoena na wengine wengi,” hiyo ni kauli ya Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama.
   
  Msama ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, anasema alitaka watu wajue na kutambua kuwa muziki wa Injili unaweza kupigwa kama burudani katika kumbi mbalimbali za starehe na kuondoa dhana potofu kwamba muziki huo wa Injili haufai kupigwa katika kumbi hizo.
   
  “Kupeleka muziki wa Injili kwenye kumbi ambazo hupigwa muziki wa miondoko mingine ya kidunia si dhambi kama baadhi ya watu wanavyofikiri,” anasema.Anasema ni zaidi ya miaka 15 tangu walipoanzisha Tamasha la Pasaka wakati wa sikukuu hiyo kila mwaka na sasa jamii imelikubali na limekuwa gumzo kubwa kwa jamii.
   
  Anasema pia dhamira yao nyingine ya kuanzisha tamasha hilo ilikuwa kusaidia jamii kwa namna mbalimbali kutokana na fedha za viingilio, lakini pia kuwapa ajira vijana kutokana na tamasha hilo.“Ninachoweza kusema ni kwamba mwaka huu tumedhamiria kwa dhati kusaidia jamii kwa namna mbalimbali kutokana na fedha zitakazopatikana kwenye viingilio vya tamasha.
   
  “Haitakuwa mara ya kwanza kwetu kusaidia, tumefanya hivyo miaka ya nyuma na tutaendelea na juhudi hizo kila tutakapopata nafasi ya kufanya hivyo, “ anasema.Anatolea mfano kuwa miaka ya nyuma wamesaidia watu mbalimbali ikiwemo  waathirika wa mabomu yaliyotokea kwenye kambi ya jeshi Gongo la Mboto, Dar es Salaam. Pia anasema wamepata kutoa fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji ya biashara wanawake wajane.
  Msama anabainisha kwamba kutokana na dhamira hiyo, ndiyo maana wamekuwa mstari wa mbele kuandaa matamasha ya muziki wa Injili, lengo likiwa ni kusaidia masuala mbalimbali.Anasema mwanzoni wakati wanaanza tamasha hilo mwaka 2000, wamewahi kuandaa matamasha kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee kwa ajili ya kuchangia watoto yatima wa mikoa ya Morogoro na Pwani, ambao wazazi wao walifariki kwa ugonjwa wa Ukimwi, ambapo yote waliyopanga yalifanikiwa.
   
  Pia anasema fedha wanazopata wamekuwa wakitumia kusomesha yatima na kuwatafutia ajira mbalimbali wasiojiweza ikiwa ni pamoja na wengine kupata mafunzo ya kunadi vitu kupitia kampuni yake ya udalali ya Msama Auction Mart. Mkurugenzi huyo anasema mpaka sasa wanasomesha wanafunzi katika shule mbalimbali Dar es Salaam.
   
  Pia anasema kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali wamekuwa wakitoa semina za kusaidia wajane, yatima na vijana wasio na ajira ikiwa ni pamoja na kuwapa mbinu za kufanya biashara na kuachana na dawa za kulevya.
  Anasema wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha huduma wanazotoa zinawafikia walengwa.
   
  “Mimi naamini mtoaji wa vyote ni Mwenyezi Mungu, hivyo ni busara upatapo kidogo ugawane na wasiojiweza ili kuongeza thawabu zako.
  “Ndiyo maana tumekuwa tukijitolea kuwasaidia wasiojiweza ikiwa ni pamoja na  kuwasomesha yatima na wasiojiweza na tumekuwa mstari wa mbele kutoa ajira kwa  baadhi ya vijana wa Tanzania,” anasema.
   
  Mkurugenzi huyo wa kampuni hiyo iliyo mstari wa mbele kuinua muziki wa Injili nchini, anawaasa vijana kuwa na moyo wa ujasiri na uvumilivu na wa kupenda kujituma kufanya kazi ili kufikia lengo la kupiga hatua kimaendeleo.Anasema vijana wengi wamekuwa wakipenda kukaa na kubweteka badala ya kufanya kazi na kuwa wabunifu.
  “Binafsi sipendi maendeleo yangu peke yangu, bali napenda pia kuwa mstari wa mbele kushirikiana na wenzangu,” anasema.
   
  Kuhusiana na tamasha lenyewe anatamba kuwa wamewaandalia mashabiki wa muziki wa Injili mambo mazuri yatakayowaburudisha na kuridhika.Anaeleza kuwa tamasha la mwaka huu 2015 ambalo lipo katika hatua za awali za maandalizi litafana kwa vile kutakuwa na waimbaji wengi wa muziki wa Injili watakaowapa mashabiki vionjo mbalimbali.
   
  Anasema anatarajia tamasha hilo litahudhuriwa na maaskofu wa madhehebu mbalimbali aliosema wameanza kufanya mazungumzo na baadhi yao, ambao wapo katika kamati yake ya maandalizi.
  Anajinasibu kuwa tamasha hilo litafana kwa vile kutakuwa na 
  waimbaji wengi wa muziki wa Injili watakaowapa mashabiki vionjo mbalimbali. 
   
  Kwa mujibu wa Msama, mpaka sasa wadau wa muziki wa Injili wa mikoa ya Mbeya, Mwanza, Arusha, Dodoma, Tanga, Dar es Salaam, Mtwara, Shinyanga na Zanzibar ndiyo ambao wameomba kufanyika tamasha hilo mikoani mwao.
   
  “Tutaheshimu mno maoni ya wapenzi wa tamasha hili kutoka sehemu mbalimbali na kila watakalotushauri tutalifanyia kazi, lengo kubwa ni kiboresha tamasha letu,” anasema Msama.Pia Msama anasema, kampuni yake ipo katika mkakati wa kujenga kiwanda cha kisasa kwa ajili ya kuzalisha bidhaa zinazohusiana na kazi za wasanii.

older | 1 | .... | 460 | 461 | (Page 462) | 463 | 464 | .... | 1898 | newer