Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live

SERIKALI HAITORIDHIA KUWAACHA WAPANGAJI NA WAFANYABIASHARA KATIKA JENGO LA TRENI KUEPUSHA MAAFA

$
0
0
Na Abdulla Ali   Maelezo-Zanzibar.    
                                         
Serikali haitoridhia kuwabakisha Wapangaji na Wafanyabiashara katika jengo la Treni ili kuepusha maafa na kuokoa maisha ya Wananchi na mali zao.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Zanzibar Mhe. Ramadhan Abdulla Shaaban wakati wa mkutano wa mzungumzo ya pamoja kati ya Wapangaji na  Wafanyabiashara wanaolitumia jengo hilo na Serikali uliofanyika katika ofisi ya Mamlaka ya Mji Mkongwe iliopo Forodhani Mjini Zanzibar.  

Waziri huyo amesema kuhamishwa kwa Wakaazi na Wafanyabiashara katika jingo hilo sio jambo la mjadala kama wanavyotaka wao bali ni wajibu wao kufuata maagizo ya serikali ili kuepukana na vifo visivyo vya lazima na hasara za mali zao pindi jengo hilo litakapo poromoka na kupelekea kuitupia lawama serikali pale majanga yatakapotokezea. “Hili si jambo la majadiliano kama mnavyotaka nyinyi”, alieleza Waziri Ramadhan.  

Ametanabahisha kuwa serikali imeshachukua hatua mbalimbali za kulijenga tena jengo hilo ikiwemo kutafuta mafundi, wahandisi pamoja na vifaa vya ujenzi na inategemewa hivi karibuni kuanza rasmi kwa ujenzi huo.

Aidha waziri ramadhan amewataka Wapangaji na Wafanyabiashara hao kutokaidi agizo la Serikali kwa usalama wa mali na maisha yao kwani jengo hilo linaonekana halitoweza kuhimili mvua za Masika zinazotarajiwa kuanza mwezi machi mwaka huu na badala yake linaweza kuporomoka kutokana na mvua hizo.

Jengo la Treni liliopo Darajani Mjini Zanzibar lina wakaazi 57 wakiwemo Wapangajia na Wafanyabiashara ambapo kwa sasa hali yake hairizishi baada ya kupasukapasuka na kutishia usalama wa maisha ya watu wanaoishi humo pamoja na wapita njia.

IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI GEORGE SIMBACHAWENE AFUNGUA MKUTANO WA KUJADILI NISHATI ENDELEVU NCHINI KWA WOTE

$
0
0
 Waziri wa Nishati na Madini  George Simbachawene akifungua mkutano  kwa ajili ya  kujadili nishati endelevu  nchini kwa wote ( Tanzania Sustainable  Energy for  All)  ulioshirikisha  sekta binfasi,  wataamu  kutoka Wizara ya Nishati na Madini pamoja na wadau wa nishati nchini.  Mkutano huo uliofanyika katika hoteli ya   Protea jijini  Dar es Salaam  lengo lake lilikuwa ni kubadilishana uzoefu kwa ajili ya kuboresha  sekta ya umeme  nchini. 
 Meneja   Hifadhi kutoka Shirika la WWF Nchini Dk. Amani Ngusaru  akitoa hotuba ya kumkaribisha  Waziri wa Nishati na Madini George  Simbachawene (hayupo pichani)
Sehemu ya wadau wa mkutano  kwa ajili ya  kujadili nishati endelevu  nchini kwa wote ( Tanzania Sustainable  Energy for  All)  ulioshirikisha  sekta binfasi,  wataamu  kutoka Wizara ya Nishati na Madini pamoja na wadau wa nishati nchini wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa inatolewa na  Waziri wa Nishati na Madini  George  Simbachawene  ( hayupo pichani)

NAPE ATEMBELEA OFISI ZA MAJIRA LEO

$
0
0
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye (kulia) akisisitiza CCM kuendelea kuimarisha ushirikiano na uwazi na vyombo vya habari, mwishoni mwa mazungumzo yake na wahariri wa magazeti ya kampuni ya BTL,  Wachapishaji wa Magazeti ya Majira, Bussines Times na Sports Starehe,  Wapili kushoto ni Mtahiriri wa Majira Eckland Mwaffisi na Mhariri Mtendaji wa Kampuni hiyo, Imma Mbuguni. Picha zote na Bashir Nkoromo).
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye (kulia) akizungumza na uongozi wa Kampuni ya Bussines Times, Wachapichaji wa Magazeti ya Majira, Bussines Times na Sports Starehe, akiwa katika mwendelezo wa ziara ya vyombo vya habari aliyoaianza wiki iliyopita mjini Dar es Salaam. Kushoto ni Mtahiriri wa Majira Eckland Mwaffisi na Mhariri Mtendaji wa Kampuni hiyo, Imma Mbuguni. 
 Nape akimsalimia Meneja Uhusiano wa Bussines Times Ltd, Julieth Lamosai, baada ya kutambulishwa kwake na Mbunguni wakati wa ziara hiyo
 Nape akienda na Mbunguni kwenye ukumbi kwa ajili ya mazungumzo.


 Meneja Usambazaji wa BTL,  Sophia Mshangama akiuliza ni namna gani CCM kama chama tawala kimejenga misingi ya kushirikiana na wadau katika masuala ya kuinua uchumi, wakati ziara hiyo. Kushoto ni Mhariri wa Sport Starehe. Charles Mateso
 Baadhi ya wafanyakazi wa BTL wakimsikiliza Nape wakati wa ziara hiyo
 Baadhi ya wahariri wakimsikiliza Nape alipozungmza nao wakatai wa ziara hiyo

 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye (kushotia), akisalimiana na Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Bussines Times, Imma Mbuguni, alipowasili katika Ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam,  akiwa katika mwendelezo wa ziara ya vyombo vya habari aliyoaianza wiki iliyopita .

 nape akisalimiana na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Uchapaji cha Bussines Times (BTL), Omari Holaki baada ya kuwasili ukumbini kuzungumza na uongozi wa kampuni hiyo
Mhahiriri wa Majira Eckland Mwaffisi (kulia) na Mhariri Mtendaji wa Kampuni hiyo, Imma Mbuguni, wakiwa tayari kumsikiliza Nape ukumbini wakati wa ziara hiyo.
 Meneja Biashara wa BTL Lecil Moshi akiluliza swali ili kupata ufafanauzi kutoka kwa Nape wakati wa kikao chake na uongozi wa kampuni huyo.

MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA ZANZIBAR YAFANYIKA LEO

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake wakati  wa Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Sheria sherehe zilizofanyika leo katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja (kulia) Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu,Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Othman Chande (kushoto) na Waziri wa katiba na Sheria Abubakar Khamis Bakary
sh7Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu alipokuwa akisema machache na kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ali azungumze na Wananchi, Mahakimu na Wanasheria katika sherehe za Kilele cha Siku ya Sheria Zanzibar zilizofanyika leo katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja.sh2Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mohamed Othman Chande (mbele) wakiongoza maandamano wakati wa kilele cha siku ya Sheria Zanzibar sherehe zilizofanyika leo katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Zanzibar.sh3Mahakimu na Wanasheria wakiwa katika maandamano wakati wa kilele cha siku ya Sheria Zanzibar sherehe zilizofanyika leo katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Zanzibar ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
sh4Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu (kushoto) alipowasili katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Zanzibar katika kilele cha siku ya Sheria Zanzibar(katikati) Waziri wa Katiba na Sheria Abubakar Khamis Bakary.sh5Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Jaji Mkuu wa Mahakama kuu Tanzania Shaaban Ally Lila (kushoto) alipowasili katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Zanzibar katika kilele cha siku ya Sheria Zanzibar(katikati) Waziri wa Katiba na Sheria Abubakar Khamis Bakary.
sh6Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi (kulia) akifuatiwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu,Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Othman Chande (kushoto) na Waziri wa katiba na Sheria Abibakar Khamis Bakary wakiwa wamesimama wakati Wimbo wa Taifa ukipigwa katika maadhimisho ya kilele cha Siku ya Sheria zilizofanyika leo katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja.sh8 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipeana mkono na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu baada ya kikizindua kitabu cha Mwaka wa Sheria leo katika Sherehe za Siku ya Sheria zilizofanyika  viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja.
[Picha na Ikulu.]

VIONGOZI WA KANISA LA ANGLICAN WATEMBELEA SHAMBA LA WAZIRI MKUU ZUZU DODOMA KUJIFUNZA KILIMO BORA CHA ZABIBU NA EMBE

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwaongoza viongozi wa Kanisa la Anglican kutembelea malisho ya ng’ombe  kwenye shamba lake  lililopo  Zuzu Dodoma Februari 9, 2015. Baadhi ya viongozi hao ambao walikwenda kujifunza kwa lengo la kuanzisha shamba linalofanana na hilo Dodoma ni Askofu Dickson Chilongani wa Dayosisi ya Dodoma (wapili kushoto), Askofu Maimbo Mndolwa wa Dayosisi ya Tanga (kulia kwake) na kulia ni Re. Canon, Johnson Chinyongole ambaye ni Katibu Mkuu wa Kanisa hilo. ANGLI4 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwaongoza viongozi wa Kanisa la Anglican kutembelea shamba lake la zabibu lililopo Zuzu Dodoma Februari 9, 2015. Baadhi ya viongozi hao ambao walikwenda kujifunza kwa lengo la kuanzisha shamba linalofanana na hilo Dodoma ni Askofu Dickson Chilongani wa Dayosisi ya Dodoma (kushoto), Askofu Maimbo Mndolwa wa Dayosisi ya Tanga (wapili kushoto) na  kulia ni Re. Canon, Johnson Chinyongole ambaye ni Katibu Mkuu wa Kanisa hilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)ANGLICAN1

CHRISTIAN BELLA 'KING OF THE BEST MELODIES' AAHIDI MAKUBWA SHOO YA VALENTINE'S DAY, DAR LIVE

$
0
0
Christian Bella (kulia) akijibu baadhi ya maswali ya wanahabari (hawapo pichani) kuhusu maandalizi ya shoo yake ya Valentine kwenye Ukumbi wa Dar Live.
Bella akisisitiza jambo kwa wanahabari (hawapo pichani).
Christian Bella (kulia) akiwapa vionjo vya wimbo wake mpya wa 'NASHINDWA' wanahabari (hawapo pichani). Kushoto ni mmoja wa viongozi wa Malaika Band, X-Bass Babu Bomba.
Bella akitoa vionjo vya wimbo wa 'NANI KAMA MAMA' kwa wanahabari.
Bella akiwa na Mhariri wa Gazeti la Risasi Jumamosi, Erick Evarist.
X-Bass Babu Bomba na Bella katika pozi na Mpiga Picha wa GPL, Musa Mateja.
X-Bass Babu Bomba na Bella wakiwa katika picha ya pamoja na Mhariri Mwandamizi wa GPL, Walusanga Ndaki.
X-Bass Babu Bomba na Bella wakipozi na Shafii Mohamed wa GPL.
X-Bass Babu Bomba na Christian Bella katika pozi ndani ya GPL.

PREZIDAA wa Bendi ya Malaika Music, Christian Bella 'King of the Best Melodies' amewaahidi shoo kali mashabiki wake watakaohudhuria katika Ukumbi wa Kisasa wa Dar Live, Jumamosi ijayo ambayo ni Siku ya Wapendanao 'Valentine's Day'. Staa huyo ameyasema hayo hivi punde wakati wa mkutano na wanahabari wa vyombo mbalimbali uliofanyika katika ofisi za Global Publishers.

Bella amesema atakuwepo ndani ya kiwanja hicho mapema kuanzia saa 7 mchana na atapiga picha za red carpet na mashabiki wake watakaohudhuria sambamba na kuzungumza nao mawili-matatu. Mbali na kuwahi ukumbini, Bella amewaandalia nyimbo zake zote kali za mapenzi kama vile Msaliti, Safari Siyo Kifo, Nakuhitaji pamoja na wimbo bora uliofunga mwaka wa Nani Kama Mama.

Kuonyesha kuwa utakuwa Usiku wa Wapendanao, Bella amewaandalia mashabiki wake zawadi ya wimbo mpya uitwao NASHINDWA ambao atauchia kwa mara ya kwanza huku video akienda kuifanyia nchini Afrika Kusini wiki ijayo. Mbali na Bella usiku huo ambao ni maalum kwa wapendanao, mkali wa muziki wa Mwambao, Mfalme Mzee Yusuf naye atakuwepo katika kuwaburudisha mashabiki wote watakaokuwepo ukumbini hapo.

Usiku huo Mzee Yusuf atashuka na kundi lake la Jahazi Modern Taarab na kuangusha ngoma zake zote kali za mapenzi kama vile My Valentine, Wapendanao, Tiba ya Mapenzi,  Wasiwasi Wako pamoja na hii ambayo ni habari ya mjini kwa sasa ya Mahaba Niue.

:MOTO MKUBWA UMEZUKA KATIKA MOJA YA JENGO MTAA WA LIBYA/MOSKI-KARIAKOO JIJINI DAR

$
0
0
Moto Mkubwa umezuka mapema leo kwenye moja ya nyumba pichani iliopo mtaa wa Libya na Moski -Kariakoo jijini Dar,na kupelekea mali kadhaa kuteketea.Kikosi Kazi cha Globu ya Jamii kilkuwepo eneo la tukio na kukuletea kila kilichojiri ,lakini kwa taarifa kutoka kwa mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio walieleza kuwa chanzo cha moto huo bado hakijafahamika rasmi,Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio kuhakikisha amani na utulivu unakuwepo huku kikosi cha zimamoto na magari nayo yaliendelea  kuwasili kupambana na moto huo..
Mmoja wa wapiga picha akitazama kwa mshangao moto mkubwa uliokuwa ukiendelea kuwaka kwa nguvu na kuteketeza baadhi ya mali zilizomo ndani ya jengo hilo lililopo mtaa wa Jamuhuri na Moski-Kariakoo jijini Dar.
 Moto uliozuka mapema leo na kuteketeza majengo matatu ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika makutano ya Mtaa wa Libya na Mosque jijini Dar es Salaam.

Moto huo ulioanza majira ya saa tatu asubuhi kwa kuanza kufuka moshi na baadae kuwaka na kuteketeza eneo lote la juu ya majengo hayo.
Akizungumza leo na waandishi wa habari katika eneo la tukio Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina wa Jeshi la Polisi Suleiman Kova amesema vikosi vya uokoaji na Zima Moto vimefanya ushirikiano katika kuzima moto huo baadhi ya maeneo na kuokoa maduka katika majengo hayo.

 ‘’Vikosi vya zima moto vimefanya ushirikiano kwa kuleta magari sita ya kuzima na uzimaji na kufanikisha kuuzima moto ambao ulikuwa mkubwa’’amesema Kova.

Kova amesema kuwa vikosi vya ukoaji vya zima moto vimefanya kazi kwa ushirikiano ambavyo ni  Zima moto za Uwanja wa Ndege,Zima Moto ya Kampuni ya Ulinzi ya Altimate,Night Support ,pamoja  na Kikosi cha Zima moto ya Jiji.

Amesema kuwa  chanzo cha moto bado hakijafahamika mpaka sasa.Amesema uchunguzi wa kubaini chanzo cha moto huo bado unaendelea .Aidha Kamanda Kova amesema thamani ya vitu vilivyoungua katika majengo hayo bado wanaendelea na uchunguzi lakini hakuna maafa katika moto huo.

Naye Kamishna msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Kanda Maalum ya Dar es salaam,Jeswald Nkongo amewataka wananchi kutoa taarifa mapema pindi waonapo matukio ya moto na sio kudharau kwa kuamini kuwa moto ni mdogo na wanaweza kuudhibiti.
 Baadhi ya Polisi kutoka Jeshi la Polisi na Kikosi cha Zimamoto vikiwasili eneo la tukio mtaa Libya na Moski.
 Baadhi ya wasamaria wema wakiondoa gari iliokuwa jirani na jengo linaloteketea kwa moto
 Baadhi ya Polisi kutoka Jeshi la Polisi wakiwa katika eneo la tukio,huku wananchi nao wakishuhudia tukio hilo la kusikitisha.
Moja ya Gari  la zimamoto likiwa limewasili eneo la tukio hivi punde.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Airtel yazindua promosheni ya Airtel yatosha Zaidi kwa Wakazi wa Mwaza

$
0
0
Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde akiongea na waandishi wa habari ( pichani hawapo) wakati wa kuzindua promosheni ya Airtel yatosha Zaidi jijini Mwanza, Promosheni ya Airtel yatosha inawawezesha wateja wa Airtel kujishindia gari Aina ya Toyota IST moja kila siku. kushoto Afisa Masoko wa Airtel Rebecca Mauma na Kulia ni Afisa Mauzo kanda ya Ziwa Emmanuel Raphael.
 Afisa Masoko wa Airtel Rebecca Mauma (kushoto) akifafanua jambo wakati wa kuzindua promosheni ya Airtel yatosha Zaidi jijini Mwanza, Promosheni ya Airtel yatosha inawawezesha wateja wa Airtel kujishindia gari Aina ya Toyota IST moja kila siku. katikati ni Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde akifatiwa na Afisa Mauzo kanda ya Ziwa Emmanuel Raphael 
 Wanahabari wa vyombo mbalimbali Jijiji Mwanza wakifatilia utambulisho wa promosheni ya Airtel yatosha Zaidi jijiini Mwanza wakati wa mkutano wa kuzindua na kuitambulisha promosheni hiyo kwa wakazi wa mwanza
 Wanahabari wa kutoka vyombo vya habari Mwanza wajadili kuhusu promosheni ya Airtel yatosha Zaidi wakati wa kuzindua promosheni ya Airtel yatosha Zaidi jijini Mwanza, Promosheni ya Airtel yatosha inawawezesha wateja wa Airtel kujishindia gari Aina ya Toyota IST moja kila siku

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi kwa wakazi wa Mwanza wakati ziara yake yenye lengo la kuwaelimisha wateja wake juu ya promosheni hiyo kambambe inayowawezesha wateja wake kujishindia gari Aina ya Toyota IST kila siku
Promosheni ya Airtel yatosha Zaidi iliyozinduliwa Jumatatu wiki iliyopita mpaka sasa imewawezesha wateja wa 3 kutoka katika mikoa mbalimbali kujishindia magari  aina ya Toyota IST kufatia droo iliyochezeshwa ijumaa iliyopita chini ya usimamizi wa bodi ya mchezo ya kubahatisha Tanzania
Akiongea kwa niaba ya Airtel Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde alisema” Tunayofuraha kuitambulisha kwenye wakazi wa mkoa wa Mwanza promosheni yetu ya Airtel Yatosha  Zaidi ninayomuwezesha wateja wetu kuendelea kufurahia vifurushi vya huduma ya Airtel yatosha huko wakijishindia Toyota IST Moja kila siku. 
Mpaka sasa tunao washindi wa tatu ambao wamepatikana kupitia droo iliyochezeshwa siku ya Ijumaa iliyopita, wewe pia unayo nafasi ya kuibuka mshindi kwa kujiunga tu na vifurushi vya Airtel yatosha vya siku, wiki au Mwezi namba yako itaingia moja kwa moja kwenye droo, hakuna makato yoyote wala gharama ya ziada ni kwa matumizi yako yakaawaida ya kila siku tunakuwezesha kushinda zawadi nono.
Akitangaza majina ya washindi Bi Jane Matinde alisema washindi wetu katika droo yetu ya kwanza ni pamoja na Ramadhani Dilunga, Mkulima  Mkazi wa mkoa wa Pwani, Namtapika Kilumba, mwalimu Mstaafu na mkazi wa mkoa wa Mtwara  pamoja na Mwajabu Churian , mfanyabiashara na mkazi wa Mbagala Jijini Dar es Saalam. Bado kuna magari 57 yamebaki kwa wewe mteja wa Airtel kujishindia
Natoa wito kwa wakazi wa Mwanza na watanzania kwa ujumla kujiunga katika vifurushi hivi kwa kupiga *149*99* au kwa kununua Vocha ya Airtel Yatosha au kwa kupitia huduma ya Airtel Money na kupata vifurushi vya sms, muda wa maongezi na internet zaidi kulinganisha na zifurushi vingine sokoni lakini zaidi Airtel yatosha inakupati nafasi ya kushinda Toyota IST kila siku aliongeza Matinde
Kwa upande wake mkazi wa Mwanza Bwana Selestine Bundala alisema” tumefurahia sana promosheni hii kwani inatupa nafasi ya kujishindia bila kutuma ujumbe mfupi wala kujibu maswali lakiini zaidi inampaita mshindi gari la kisasa na kumwezesha kufanya shughuli zake kirahisi, nawapongeza Airtel sana na mimi pia naendelea kuvitumia vifurushi hivi kwani vinarahisisha huduma za mawasiliano na kuzifanya kuwa za gharama nafuu.
Droo ya pili ya promosheni ya Airtel yatosha zaidi itafanyika ijumaa hii ambapo washindi saba wa wa wiki hii watatangazwa. Na washindi watatu wa wiki iliyopita watabithiwa magari yao siku ya Jumatano.

Waziri Mwakyembe azungumzia Kenya kuzuia magari ya Tanzania Viwanja vya Ndege

$
0
0
 Picha zote Kushoto ni Katibu Mkuu Joyce Mapunjo, Katikati Waziri Dkt Harrison Mwakyembe na Kulia ni Naibu Waziri Dkt Abdallah Juma Saadala. Huyo mwenye suti na tai nyekundu kwenye picha hizo mbili ni Naibu Katibu Mkuu Amantius Msole.


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UAMUZI WA SERIKALI YA KENYA KUZUIA MAGARI YA KITALII YALIYOSAJILIWA TANZANIA KUINGIA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JOMO KENYATTA KWA AJILI YA KUCHUKUA NA KUSHUSHA WATALII

Tarehe 22 Desemba, 2014, Serikali ya Jamhuri ya Kenya ilitoa amri ya kuzuia magari ya kitalii yenye usajili wa Tanzania kwenda kuchukua na kushusha watalii wanaotumia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta wakiwa njiani kuja kutembelea vivutio vya utalii katika Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. 

Baada ya uamuzi huu wa Serikali ya Kenya, Waziri wa Maliasii na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu alifanya majadiliano na Waziri wa masuala ya utalii wa Serikali ya Kenya siku ya tarehe 16, Januari, 2015 ili kutafuta ufumbuzi wa kadhia hii. Matokeo ya mkutano wa Mawaziri hawa yalikuwa ni kusitishwa kwa muda katazo lililotolewa na Serikali ya Kenya kwa makubaliano kuwa yafanyike mazungumzo baina ya pande hizi mbili ndani ya kipindi cha wiki tatu kuanzia tarehe 16 Januari, 2015 ili kurekebisha Mkataba wa Ushirikiano katika sekta ya utalii wa mwaka 1985 kati ya nchi zetu mbili.

Kufuatia makubaliano hayo Wizara ya Maliasili na Utalii iliiomba Wizara ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki iandae kikao hicho cha pamoja katika muda uliopangwa. Kwa kuzingatia historia na uzito wa suala lenyewe, Wizara ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki iliona umuhimu wa kuhusisha Wizara zingine husika za Uchukuzi, Mambo ya Nje, Viwanda na Biashara, Fedha, Ulinzi, Mambo ya Ndani, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira na Viongozi wa Sekta Binafsi ili kupata msimamo wa nchi wa pamoja kabla ya mkutano na Kenya.


Hivyo, vikao vya wataalam vimefanyika Dar es Salaam na Arusha hadi wiki ya kwanza ya mwezi huu wa pili kwa maandalizi ya kikao cha mwisho cha Mawaziri upande wa Tanzania kabla ya kukutana na wenzetu wa Kenya. Pamoja na kushauriana na Waziri mhusika wa Kenya (Masuala ya Afrika Mashariki, Biashara na Utalii, Bi. Phyllis Kandie) kusogeza mbele tarehe ya mkutano wa pamoja ili kuruhusu muda wa kutosha kwa majadiliano ya ndani na wadau, Bi. Kandie alimwandikia Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, Dkt. Richard Sezibera na kumnakili Waziri Nyalandu, kurejesha amri yake ya awali ambayo alisema inaendana na Sheria ya utalii na kanuni za uchukuzi za Kenya.

Serikali ya Tanzania kimsingi imesikitishwa na uamuzi huo wa Serikali ya Kenya kwani haujengi wala hauendani na dhamira njema ya Mkataba wa Kuanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kuenzi njia ya mazungumzo, maelewano na maridhiano katika kufikia maamuzi. Suala la kurekebisha mkataba ulioingiwa na nchi hizi mbili kwa hiari miaka 30 iliyopita, si jepesi la kujadiliwa na Mawaziri wawili tu na kuwekeana ukomo wa muda katika kulipitia. Serikali ya Tanzania itaendelea na mchakato iliouanzisha wa kuhusisha wadau wote na kufikia uamuzi ambao itauwasilisha kwa Serikali ya Kenya kupitia vikao rasmi vya Jumuiya.

Pamoja na kwamba amri hii ya Serikali ya Kenya inaenda nje ya mkataba wa 1985 kwa kuvihusisha hata viwanja vya ndege kuwa sehemu ya vivutio vya utalii, Serikali ya Tanzania itaheshimu na kuzingatia amri hiyo ili kulinda undugu na urafiki uliopo kati ya nchi zetu huku tukitafakari hatua za kuchukua ili kuondoa bughudha kubwa itakayotokea kwa watalii na wasafiri wetu wanaopitia uwanja huo wa Jomo Kenyatta. Aidha Tanzania itachukua hatua ya kuwafahamisha watalii na wageni wote wenye nia ya kutembelea vivutio vya kitalii vya Tanzania kutumia viwanja vingine vya ndege ili kuepuka kadhia na gharama zisizo za lazima.

Kwa upande wa Tanzania, viwanja vya ndege hasa vile vya Kimataifa vitaendelea kuwa sehemu ya malango ya kuingilia na kutokea kwenda kokote iwe ndani ya Jumuiya au nje ya Jumuiya na havitavichukuliwa kama vivutio vya utalii. Tanzania haitazuia magari ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki au nchi nyingine yoyote kuingia katika viwanja vyake vya ndege kuleta au kuchukua watalii wanaopitia katika viwanja hivyo na kwenda katika nchi zao.

Mkataba wa mwaka 1985 kati ya Tanzania na Kenya ulilenga kutoa mwongozo wa ushirikiano katika Sekta ya Utalii kati ya nchi zetu mbili. Aidha, makubaliano hayo yalielekeza maeneo muafaka kwa ajili ya kubadilishana watalii huku ikizingatiwa kuondoa bugudha kwa watalii. Maeneo hayo ni pamoja na miji ya mipakani pamoja na miji rasmi iliyopendekezwa na kukubalika na pande zote mbili ikiwemo Nairobi ambako kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Jomo Kenyatta kipo.

Mwisho, Tanzania itaendelea kuenzi undugu na urafiki uliojengeka kwa zaidi ya miaka 50 tokea uhuru kati ya nchi zetu mbili na suala dogo kama hili halitaweza kuteteresha uhusiano wetu mzuri.


WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
10 FEBRUARI, 2015.

MAKAMU WA RAIS MHE. DKT. BILAL AONGOZA WANANCHI WA MKOA WA DAR ES SALAAM KWENYE MAZISHI YA FAMILIA KAPTEN DAVID MPILA LEO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akitoa heshima za mwisho kwenye majeneza yenye miili ya Familia ya marehemu Kapten David Mpila waliofariki kwa kuteketea na moto nyumbani kwao Kipunguni, wakati wa mazishi yao yaliyofanyika leo Februari 10,2015 katika makaburi ya Airwing Ukonga Dar es salaam.BIL2 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimfariji mama mzazi wa marehemu bibi Celina Mpila mke wa marehem Kapten David Mpila waliofariki kwa kuteketea na moto, wakati wa mazishi yao yaliyofanyika leo Februari 10,2015 katika makaburi ya Airwing Ukonga Dar es salaam.             (Picha na OMR)

PADRE MUNISHI AWEKWA WAKFU KUWA PAROKO KANISA KATOLIKI BALTIMORE MD

$
0
0
IMG_0279Baba padre Honest Munishi akiwekwa wakfu kuongoza kanisa la Katoliki la St.Edward Baltimore Md nchini Marekani katika misa iliyoongozwa na Askofu Dennis Madden wa jimbo la kuu la Baltimore, Jumapili Februari 8,2014. Padre Munishi amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Padre Evod Shao aliyemaliza muda wake IMG_0276Padre Munishi katika ibada. IMG_0284Padre Munishi akitia saini mbele ya askofu baada ya kusimikwa kuwa paroko mpya wa kanisa la Baltimore Md. IMG_0288Baba askofu wa jimbo kuu la Baltimore akimtambulisha padre Munishi kwa waumini wake. IMG_0301Balozi Liberata Mula mula aliongoza watanzania kwenye ibada hiyo kulia kwake ni mwambata wa kijeshi nchini Marekani na Canada Kanal Adolph Mutta. IMG_0307Kikosi cha wanajumuiya wa Kenya wakiimba kumpongeza padre Mushi wakati wa matoleo. IMG_0333Mwenyekiti wa Jumuiya ya wakatoliki watanzania Bw.Pius Mutalemwa na mkewe. IMG_0334Kushoto Bw.Gervas Wambura na katibu wa Jumuiya ya wakatoliki Dan Steven. IMG_0339Mama Mhando. IMG_0354Kikundi maalum kikitumbuiza baada ya ibada. IMG_0369Mwakilishi kutoka ofisi ya Meya wa Baltimore akitoa hotuba. IMG_0376Padre Munishi akiwashukuru wote waliomkaribisha na kumpokea kwa ukarimu mkubwa. IMG_0415Kutoka kushoto kiongozi mkuu wa Padre Munishi, Askofu wa jimbo kuu la Baltimore Dennis Maden, balozi Mula mula na padre Munishi baada ya ibada ya misa kumalizika . Kwa picha zaidi bofya umgana na Sundayshomari.com

Tanzanian Dentist Dr. Talib Ali on the TOP Doctors Interviews - Sedation Dentistry

$
0
0
Dr. Talib Ali, a top dentist from Avatar Dental Care in Leesburg, Virginia, discusses the benefits of Sedation Dentistry on the TOP Doctors Interviews which are seen on CNN Headline News, CNBC, FOX News and other networks. Call Avatar Dental Care Today and set your consultation with Dr. Talib Ali at 703-669-8600 or visit http://www.avatardental.com/ or his office at:
Avatar Dental Care
545 G. East Market Street
Leesburg, VA 20176

HAPPY BIRTHDAY – BENEDIKT FULBRIGHT MAKULILO

$
0
0
 My dearest son, Benedikt

Today is your 4thBirthday. It is another February 10th of the year. You were born at 5:42pm Pacific Standard Time. Your birth is a blessing and that’s why you are Benedikt. You have helped us to be better human beings by reflecting our lives as parents. Both Marie and I are thankful to God every day to have such a wonderful little guy.


For the past four years we haven’t settled into one area for a long time. You know it was because of job change. I am proud of you whenever we moved you adopted quickly and enjoyed the area. There is a big possibility to have another move this summer. If I get accepted into my PhD studies, obvious we will move to another state. You will enjoy more to the new area, play with snow which you’ve not experienced in your four years. We’ll have so much fun.


On your first birthday’s letter, I promised one thing. I promised to take you to Tanzania when you are older enough so that you can meet all my family members and know my roots. I remember you had a dream and said we were together in Tanzania and you milked a cow….yes, when we are there you will milk cow. I think this year we can work out and take you to Tanzania. Unfortunately you will not meet Babu (your grandfather). He is already in heaven with his three children; Scolastica, Stanslaus and Vincent. Though you’ll not meet him, you will get opportunity to see his legacy which I am very much proud of his accomplishments as a committed father, a non-corrupt personnel, religious and above all the only person who valued education to his children than any person I have ever seen in this world. 


Recently we have not been able to play soccer and run many times as we used to. We have to go back to our routine of going to the park and have more fun. I know when you go to school you will learn other kind of sports. I have no problem with any sport of you and enjoy playing. What I promise is: I will support you in any sport, take you to practice and attend your games. The most important thing is have fun and enjoy the talents you have been given by God. But if you want to be professional in any sport, remember hardworking and prayers will take you to another level. Talent is nothing if you don’t work hard on it. Always remember to pray and ask for God blessings no matter what, whether you are in success or hard time.


Nothing in this world comes easy. You will face so many challenges. You will fail and loose so many things. The best thing is to learn from your failures and challenges you face to make you a better person and a winner. This is one of the reason when you and I compete on running I don’t let you win every time. I give you opportunity to work harder. This is what Carl Brashear said “It is not a sin to be knocked down; it’s a sin to stay down”. Always get up and do it again. Don’t allow failure and challenges steal your dreams and achievements. 


For the past year, you started saving some money (pennies and quarters) in your pig bank for ice-cream. You didn’t touch a single coin, you were determined to have enough money for ice-cream. You managed to have like $20 for such a period. I’m very much proud of you son in that accomplishment. To me is not about how much money you have collected and saved. It is about discipline, commitment and long term goals you have. Many of us hard time to have such discipline. 


You and I have our own tradition for your birthday. We are going to the bus ride as we have been doing in all other birthdays. And this letter is another gift for you. I have kept all letters I have written to you. I’m going to publish it into a book titled “THE BENEDIKT FACTOR”. You are the really factor of my life. You are the game changer. 

You have given me opportunity to look life into a different angle as a father and husband. You’ve helped me to know how important mothers are to children. As most men we take things for granted. But being in the labor room for your birth and see how mothers go through, I have different and most positive perspective on women and mothers. I know without you, things would be different.



You are the best my little crazy guy.



Nakupenda Sana

HAPPY BIRTHDAY BENEDIKT FULBRIGHT MAKULILO

Your loving Baba

Ernest

Tanzania bloggers network (TBN) yatoa rambirambi kwa mwanahabari wa familia ya watu sita waliofariki kwa ajali ya moto

$
0
0
 Mwenyekiti wa muda wa Chama cha Bloggers Tanzania (Tanzania Bloggers Network - TBN ), Joachim Mushi (kulia) akitoa poe na kisha kukabidhi ubani wa fedha shilingi laki tano (500,000/-) jana zilizotolewa kwa mwanahabari wa Kitulo FM ya Njombe Bw. Conrad Mpila kama pole toka TBN baada ya kupoteza ndugu watano wa familia moja katika ajali ya moto iliyotokea hivi karibuni na kuua watu sita eneo la Kipunguni jijini Dar es Salaam. Katikati ni mmoja wa wajumbe wa TBN, Dotto Mwaibale. TBN ilishiriki katika mazishi ya marehemu hao sita waliozikwa jana katika makaburi ya Airwing, Dar es Salaam. Picha na Francis Dande.
 "Tupo nawe katika wakati huu mgumu..." anasema  Mwenyekiti wa muda wa Chama cha Bloggers Tanzania (Tanzania Bloggers Network - TBN ) Bw. Joachim Mushi wakati anakabidhi ubani huo
"Pole sana Conrad", Bw Mushi anamfariji mfiwa.

TANGAZO LA KUPOTELEWA NA MTOTO

$
0
0
DUZE DAVID TUSEKELEGE .
MTOTO WA KIUME DUZE DAVID TUSEKELEGE  MWANAFUNZI WA KIDATO CHA TATU KATIKA SHULE YA SEKONDARI AMKA ILIYOPO IGAWILO UYOLE MKOANI  MBEYA AMETOWEKA NYUMBANI MAENEO YA SOWETO KWA MAMA JOHN TANGU TAREHE 04 JANUARY 2015. 

MTOTO HUYO NI MWEUPE WA KIMO CHA WASTANI, TUNAOMBA MTU YEYOTE ATAKAYE MUONA ATOE TAARIFA KATIKA KITUO  CHA POLISI KILICHO KARIBU. TAARIFA YA POLISI NI RB 71/2015 YA TAREHE 08/01/2015  AU ATUTAARIFU KWA  NAMBA ZA SIMU ZIFUATAZO – 0756 033 340,  0764 504 904 ,  0784 509 808  AU 0719 011 099.


Mwingereza atajwa Tamasha la Pasaka

$
0
0
MWIMBAJI wa kimataifa raia wa Uingereza, Ayobami David  ni mmoja wa waimbaji wanaopenekezwa sana na mashabiki waalikwe katika onesho la miaka 15 ya Tamasha la Pasaka nchini.
 
Ayobami ni mwimbaji ambaye anafanya vizuri katika muziki huo wa Kumtukuza Mungu kupitia nyimbo mbalimbali.Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama alisema katika taarifa yake kuwa mwaka huu wanataka kutoka kivingine.
 
“Mashabiki wamekuwa wakiomba tumualike Ayobami, bado tunapokea maoni mbalimbali na kulingana na vigezo vyetu tutajipanga,” alisema Msama. Alisema kwa kuwa wameamua kukuza muziki huo hapa nchini, wataalika wasanii mbalimbali wa kimataifa ili kulifanya tamasha la mwaka huu liwe la aina yake.
 
Alisema wamekuwa wakiwatumia katika matamasha yake yaliyoasisiwa tangu mwaka 2000, waimbaji kutoka Kenya, Zambia, Afrika Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na wa hapa nchini.
 
“Niliyoeleza mwanzoni yanakamilika, kwa sababu nilidhamiria kuliboresha zaidi Tamasha la Pasaka kwa kuwashirikisha waimbaji wa Kimataifa, mashabiki wakae mkao wa kula kupata ladha tofauti katika tamasha la mwaka huu,” alisema Msama.  
 
Baadhi ya waimbaji waliopata kutumbuiza Tamasha la Pasaka tangu lianzishwe ni Rebecca Malope, Keke Phoofolo (Afrika Kusini), Ephraim Sekereti (Zambia), Faraja Ntaboba (DRC) na Sarah K, Paul Mwai (Kenya).

MKUU WA SHULE YA SEKONDARI ADAIWA KUMKIMBIA MBUNGE CHIKU ABWAO.

$
0
0
 Mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha demokrasia na maendeleo chadema CHIKU ABWAO akikagua jengo lilokumbwa na ajali ya moto


 Mbunge  CHIKU ABWAO akiwa katika eneo la nje ya jengo liloungua

Mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha demokrasia na maendeleo chadema CHIKU ABWAO alisikitiswa na uongozi wa shule  ya sekondari ya idodi kushindwa kumpokea kama mbunge na mama aliyeguswa na ajali ya moto katika shule kwa kuwa alikuwa ameshatoa taarifa kabla hajaenda katika shule hiyo.

Kitendo hicho kiliwafanya baadhi ya wanahabari wa manispaa ya iringa waliokuwa wameongozana na mbunge huyo walikasilishwa kitendo kilichofanywa na uongozi wa shule ya sekondari ya idodi na walianza kuhoji je? angekuwa mkuu wa mkoa,mkuu wa wilaya na waziri au mbunge wa jimbo hilo wangemfanyia hivyo.

Licha ya hujuma alizopewa ambazo zinasadikika kuwa za kisiasa mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha demokrasia na maendeleo chadema CHIKU ABWAO aliendelea na zoezi lake la kutoa msaada wa shilingi milioni moja ili kusaidia majukumu mengine ya shule hiyo kutokana tathimini fupi iliyotewa na baadhi ya walimu.

Akizungumza mbele ya wanafunzi wa shule   CHIKU ABWAO amesema kuwa ameguswa na ajali hiyo ya moto ndio maana ameamua kujitolea kutoa msaada huo.

aidha ABWAO ameishauri serikali kujenga mabweni kwa mtindo nyumba za kawaida ili kuwawezesha  wanafunzi kuishi kumi katika bweni moja tofauti na sasa ambapo wanafunzi wanaishi zaidi ya mia na ishirini katika bweni moja.

Lakini  ABWAO akasisitiza kuweka ulinzi mzuri kwenye mabweni kwa kuwa suala kama hilo limekuwa likijitokeza mara kwa mara katika shule hiyo na kuomba wakandarasi watakao kuwa wanapewa tenda za kujenga mabweni ya shule kuhakikisha wanaweka vifaa maalum vya kuzimia moto.

Alipotafuta mkuu wa shule kwa njia ya simu na kuulizwa kwanini umemkimbia mbunge alijibu kwa kusema kuwa alikuwa na majukumu mengine kwa hiyo sio lazima kumpokea mbunge wakati kuna majukumu mengine makubwa zaidi ya yeye.

Umeme kichocheo cha ukuaji wa uchumi nchini - Simbachawene Greyson Mwase na Rhoda James, Dar es salaam

$
0
0
Waziri wa  Nishati na Madini, George  Simbachawene amesema kuwa nishati ya  umeme ni  kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi wa nchi hivyo  serikali ipo  tayari kushirikiana na wadau mbalimbali  ili kuhakikisha kuwa nishati ya umeme inakuwa ni  ya uhakika.


Simbachawene aliyasema hayo kwenye ufunguzi wa mkutano  uliokutanisha wadau wa nishati kutoka sekta binafsi, asasi za kiraia na wataalamu kutoka  Wizara ya Nishati na Madini,  katika  hoteli ya Protea  jijini  Dar es salaam. Lengo la mkutano huo lilikuwa ni kubadilishana ujuzi na uzoefu katika  usimamizi wa miradi ya umeme.


Alisema kuwa, Serikali  imekuwa ikiandaa mikakati mbalimbali  ya  kuhakikisha wananchi wote wanapata nishati ya umeme  ya uhakika na kwa gharama nafuu na kusisitiza kuwa ili kufikia lengo  hilo, Serikali imebuni  vyanzo mbalimbali kama vile umeme wa jua, upepo, tungamotaka,  jotoardhi na  gesi asilia kulingana na Sera ya Nishati ya Mwaka  2003.


“ Umeme wa Gridi ya  Taifa pekee hautoshi kabisa katika kuhakikisha wananchi wote wanaunganishwa na huduma ya umeme  ndio maana  Serikali imebuni  vyanzo  vingine ili   kuhakikisha kuwa yale maeneo ambayo  hayajafikiwa na  umeme wa gridi ya   taifa, wanapata umeme na kupunguza  umasikini kupitia nishati hiyo, “alisema Simbachawene.


Wakati huohuo, Meneja Uhifadhi kutoka Shirika la Kimataifa linaloshughulikia masuala ya  utunzaji wa mazingira na maisha ya wanyamapori (WWF; World  Wide Fund for  Nature) Nchini  Dk. Amani  Ngusaru akizungumzia hali ya umeme duniani alisema kuwa  takribani watu bilioni 1.6 hawana  nishati ya uhakika ya umeme huku bilioni 2.4 wakiwa hawana nishati ya uhakika kwa ajili ya kupikia. Aliongeza kuwa kwa  upande wa Tanzania kwa kipindi cha miaka 10 Serikali imefanya  jitihada mbalimbali katika kuhakikisha inapunguza upungufu wa umeme nchini.


Akizungumzia  changamoto katika utekelezaji wa miradi ya  umeme nchini Dk. Ngusari alisema teknolojia, fedha za uendeshaji na ukosefu wa  ujuzi  zinazuia upatikanaji  wa umeme wa uhakika. Akielezea mchago wa WWF katika nishati ya umeme Dk. Ngusari alieleza kuwa, WWF imekuwa ikisaidiana na  Serikali katika kuongeza upatikanaji wa nishati mbadala na  kuongeza matumizi ya bayomass.

FURAHI NA UMPENDAE GROOVEBACK J'MOSI HII @ EAST 24

Balozi wa Japan asaini mkataba wa mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kukamulia mafuta ya alizeti wilayani Chato.

$
0
0
BALOZI wa Japan nchini Masaki Okada leo ametiliana saini na halmashauri ya wilaya ya chato mkoani geita ujenzi wa kiwanda cha kukamulia mafuta ya alizeti kitakachojengwa wilayani chato mkoani geita.

Akizungumza katika hafla hiyo balozi Okada amesema serikali ya japan imeamua kutoa msaada wa dola za Marekani 95,124 sawa na shilingi milioni 165 za Tanzania kugharamia mradi huo.

“Mradi huu ni wa kipekee katika miradi toka mfoko wa grant assistance for grassroots human security projects GGHSP kwani unalenga kuhamasisha kilimo cha alizeti wilayani chato na hivyo kuibua fursa mpya za ajira  na kuwawezesha wananchi kutumia mafuta yasio na lehemu” ,amesisitiza balozi Okada.

Akizungumza katika hafla hiyo mbunge wa chato, ambae pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli amemshukuru balozi Okada kwa misaada mbalimbali anayoitoa hapa nchini na katika jimbo la chato ili kuibua fursa za kiuchumi na  kuharakisha maendeleo.

Amewataka wajenzi wa kiwanda hicho kukijenga kwa viwango vya ubora unakubalika na kumaliza kazi hiyo kwa wakati ili kuanza uzalishaji wa mafuta kwa haraka . “kiwanda hiki kitakapokamilika kitakuwa na uwezo wa kutengeneza lita 1600 za alizeti kwa saa moja na kukamua gunia 80 za alizeti na hivyo kuwezesha mafuta ya alizeti kusambazwa ndani na nje ya nchi na kukuza uchumi”, amefafanua waziri Dkt. Magufuli.

Naye mkurugenzi wa halamashauri ya wilaya ya chato  Clement Berege amemhakikishia balozi  kuwa msaada wa kiwanda cha kutengeneza mafuta ya alizeti utasimamiwa kikamilifu ili uwe na manufaa kwa jamii ya chato na wananchi kwa ujumla.

Katika hatua nyingine balozi Okada amesaini mkataba wa kutoa magari mawili ya kusafirisha wagonjwa ambulance katika hospitali ya taifa ya muhimbili ili kupunguza changamoto ya usafirishaji wagonjwa.

Naye kaimu mkurugenzi mtendaji wa hospitali ya taifa ya muhimbili Dkt. Hussein kidanto amemshukuru balozii wa japan kwa msaada huo wenye thamani ya shilingi milioni 70 na kuahidi hospitali hiyo iko kwenye mkakati wa kuanzisha kitengo cha ambulance ili kusafirisha kwa haraka wajawazito, wagonjwa na waathirika wa ajali na hivyo kuwafikisha katika hospitali hiyo kwa wakati.

IMETAYARISHWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO WIZARA YA UJENZI
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live




Latest Images