Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

Cheki shoo ya Julio batalia alioifanya escape one.

$
0
0

Pokea performance ya Julio Batalia kwenye Show iliyofanyika escape 1 tarehe 7 february j'mosi kwenye Utambulisho wa Video mbili Kaunyaka ya Chege na Temba na Vuvula ya Madee ali.video zilizotengenezwa na director Adam Juma...Julio aliperfom ngoma zake mbili Haina Noma na special for you na pia kuwapa kionjo cha ngoma yake mpya inayoitwa (Tetemesha) ambayo imefanyika wakati wa safari ya South Africa akiwa na Chege,Madee na Temba na kufanikisha kurekodi na producer mkubwa Dj maphorisa wa UHURU UHURU..Ngoma mpya ya Julio (Tetemesha) inategemewa kutoka march ama april mwanzoni ikiambatana na video.

INTRODUCING WIMBO WA MWANADADA JANEDIVA VIDEO

MKUTANO WA KUJADILI NAMNA YA KUKABILIANA NA MAAFA MBALIMBALI WAFANYIKA ZANZIBAR.

$
0
0
 -Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akisalimiana na Viongozi mbalimbali alipoingia katika mkutano wa kujadili namna ya kujiandaa kukabiliana na maafa mbalimbali yanayoweza kutokea Mkutano uliofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni Zanzibar.
 Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akisalimiana na Command Surgeo Usafricom Philip C Knight Sheen alipoingia katika mkutano wa kujadili namna ya kujiandaa kukabiliana na maafa mbalimbali yanayoweza kutokea Mkutano uliofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni Zanzibar.
 Baadhi ya Viongozi wa Nchi Tano za mataifa mbalimbali walioshiriki katika mkutano wa kujadili namna ya kujiandaa kukabiliana na maafa mbalimbali yanayoweza kutokea Mkutano uliofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni Zanzibar.
 Command Surgeo Usafricom Philip C Knight Sheen akitoa hotuba yake katika mkutano wa kujadili namna ya kujiandaa kukabiliana na maafa mbalimbali yanayoweza kutokea Mkutano uliofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni Zanzibar.
 Waziri wa Nchi Afisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohd Aboud Mohd kitoa hotuba yake katika mkutano wa kujadili namna ya kujiandaa kukabiliana na maafa mbalimbali yanayoweza kutokea Mkutano uliofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni Zanzibar.
 Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akitoa hotuba katika mkutano wa kujadili namna ya kujiandaa kukabiliana na maafa mbalimbali yanayoweza kutokea Mkutano uliofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni Zanzibar.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akiwa katika Picha ya pamoja na Viongozi wa Nchi tano za mataifa mbalimbali waliohudhuria mkutano wa kujadili namna ya kujiandaa kukabiliana na maafa mbalimbali yanayoweza kutokea Mkutano uliofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni Zanzibar.PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA UONGOZI WA CHUO KIKUU CHA TUMAINI IKULU LEO

$
0
0
 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na baadaye katika mazungumzo na uongozi wa juu wa Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es salaam uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo February 9, 2015. Ujumbe huo umeongozwa na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la kilutheri Tanzania Dkt Alex Malasusa pamoja  na Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Nyumba la taifa (NHC) na Mwenyekiti wa Harambee ya chuo hicho ambacho kinamilikiwa na kanisa la KKKT. PICHA NA IKULU

WANANCHI WATAKIWA KUWA NA MWAMKO WA KUSOMA NA KUZIJUA SHERIA KUPATA HAKI ZAO

$
0
0
Na Miza Kona        Maelezo-Zanzibar                                                      

Wananchi wametakiwa kuwa na mwamko wa kuisoma sheria ili waweze kuijua na kupata haki zao pamoja na kuepukana na vitendo mbali mbali vinavyokwenda kinyume na sheria.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Bi Harusi Miraji Mpatani wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huko ofisini kwake Migombani Zanzibar.

Amesema wananchi wamekuwa ni wagumu wa  kufuata sheria kutokana na uelewa mdogo waliokuwa nao wa kutojua haki zao za msingi jambo linalopelekea kwenda kinyume na sheria hizo pamoja na kuwepo kwa kesi nyingi zikiwemo za udhalilishaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Amesema kituo cha Huduma za Sheria kipo kwa ajili ya kuwasaidia Wazanzibar kuweza kuelewa na kujua haki zao pamoja na masuala ya sheria na haki za binadamu kwa kuwapatia elimu sahihi na ufafanuzi wa sheria hizo.

Amefahamisha kuwa kituo pia kinatoa msaada wa sheria na huduma kwa wananchi wasiojiweza wakiwemo Walemavu, Masikini ,Wanawake na Watoto pamoja na kuwaelimisha wananchi na kutatua migogoro.

“Elimu ya vitendo vya udhalilishaji wa watoto inaendelea kutolewa lakini bado vitendo hivyo vinazidi kuongezeka vijijini hivyo jamii iwe na mwamko wa kuwafichua na kuwachukulia hatua wale wote wanaofanya vitendo hivyo”, ameeleza Mkurugenzi huyo.

Akizungumzia kuhusu ucheleweshaji wa kesi mahakani Mkurugenzi huyo amesema kuwa kuna kesi nyingi mahakamani ambazo bado hazijatolewa hukumu kutokana na kukwama  kwa kesi hizo mahakamni hapo na nyengine kukosa ushahidi hivyo kituo kinafuatilia tatizo hilo kwa wahusika na kulitafutia ufumbuzi.

Ameeleza kituo kina miradi miwili inayosimamia haki za watoto katika Wilaya ya Kaskazini A na Wilaya ya Maghariri Unguja chini ya ufadhili ya Umoja wa Ulaya (EU) pamoja na Save The Children ambayo inapinga unyanyasaji wa watoto na kusimamia haki za binadamu.

Bi Harusi amefahamisha kuongezeka kwa watumiaji wa kituo hicho ni faraja kubwa ambayo inapelekea kupata matumaini mazuri ya maendeleo ya utoaji wa huduma za kituo kwani katika mwaka 2013 wateja waliofika kituoni hapo ni 3000 lakini kwa mwaka jana zaidi ya wateja 4000 walifika kupata huduma katika kituo hicho.

Aidha Bi Harusi amewataka wananchi kufuatilia Katiba iliyopendekezwa ili waweze kuielewa na kufanya maamuzi sahihi wakati ukifika pamoja na kutumia kituo hicho cha sheria kwani kinatoa huduma zake bure ili kuwasaidia wananchi kupata haki zao.

Kituo cha Huduma za Sheria kinatarajia kuazimisha miaka 23 tangu kuanzishwa kwake na kauli mbiu ni “Kutojua Sheria Sio Kukaa kimya”. 

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDD AISHUKURU SERIKALI YA MAREKANI

$
0
0
 
Na Miza Othman      Maelezo- Zanzibar                                               

Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi ameishukuru Serikali ya Marekeni  kwa msaada wao katika  kuimarisha na kujikinga na maafa mbali mbali pindi yanapotokea Visiwani Zanzibar.

Hayo ameyaeleza leo huko ukumbi wa Zanzibar Beach Resort  wakati wa ufunguzi wa mkutano ulioandaliwa na Idara ya Kuzuia Maafa Zanzibar kwa ajili ya kutoa elimu  kwa wananchi  ili kujua namna ya  kujijkinga na maafa wakati yanapotokea.

Balozi Seif amesema Serikali ya Marekani kwa kushirikiana na Idara ya Maafa ya Zanzibar imetoa msaada wa kiufundi na kifedha ambao umerahisisha katika kutatua matatizo ya kimaafa yanayoikabili Zanzibar.

Amesema serikali ya Zanzibar imekuwa ikikumbwa na vitisho mbalimbali vya maafa ikiwemo mafuriko, ukame na ajali za meli hivyo  ameishukuru Nchi hiyo kwa kujitolea katika kutoa elimu juu ya kujikinga na maafa wakati yanapotokea katika maeneo yao kwa itasaidia kwa kiasi kikubwa kupambana na majanga hayo.

Balozi Seif ametanabahisha kuwa Lengo la Mkutano huo ni kuimarisha Miundombinu na kukabiliana na maafa katika Nchi za Afrika.

Hata hivyo ameviomba vyombo vya habari kutoa habari zitakazowaelimisha wananchi juu ya kujikinga na maafa yanapotokea ili kupunguza vifo vya mara kwa mara ambavyo vinatokana na hali hiyo.

Aidha amesema Serikali inashirikiana na wadau wengine wa maendeleo ikiwemo Jeshi na Asasi za Kijamii kuhakikisha wananchi wanaishi salama kwa  kuwatafutia vifaa vya uokozi kwa ajili ya kupambana na maafa wakati yanapotokea.
 
Aidha Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Zanzibar Ali Juma Hamad amesema kutokana na hatuwa zinazochukuliwa katika kupambana na maafa hadi sasa Zanzibar imeshapiga hatuwa katika kupambana na hali hiyo.

“Kila Nchi ni lazima kufanya majaribio wakati wakutokea maafa je, wananachi wanaweza kujikinga na maafa hayo”, alisema Mkurugenzi Ali Juma Hamad.

Hata hivyo amezitaka taasisi za Serikali na binafsi kuzidisha juhudi katika kutoa elimu ya  kupambana na maafa wakati yanapotokea ambapo  Jumla ya Nchi Tano kutoka Afrika zimeshiriki katika kutowa elimu juu ya kujikinga na maafa.
  
                                                                      IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

RAIS KIKWETE AKUTANA NA RAIS WA KANISA LA SEVENTH DAY ADVENTIST DUNIANI DKT TED N.C. WILSON IKULU

$
0
0
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika mazungumzo na kiongozi wa  Rais wa kanisa la Seventh Day Adventist (SDA) duniani, Dkt. Ted N.C. Wilson aliyemtembelea pamoja na ujumbe wake wa viongozi wa kanisa hilo kutoka nchi 11 za Afrika Ikulu Jumamosi February 7, 2015, Usiku jijini Dar es salaam.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo na kupata chakula cha usiku na kiongozi wa  Rais wa kanisa la Seventh Day Adventist (SDA) duniani,  Dkt. Ted N.C. Wilson aliyemtembelea pamoja na ujumbe wake wa viongozi wa kanisa hilo kutoka  nchi 11 za Afrika Jumamosi February 7, 2015, usiku Ikulu jijini Dar es salaam. PICHA NA IKULU.


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone:255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz              

Fax: 255-22-2113425



PRESIDENT’S OFFICE,
      STATE HOUSE,
              1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kanisa la Seventh Day Adventist (SDA) duniani limeipongeza Tanzania na Watanzania kwa kulinda amani nchini na pia kusaidia kuleta na kuinua kiwango cha amani na utulivu katika nchi nyingine katika eneo la Mashariki na Kati la Afrika.

Aidha, Kanisa hilo limepongeza msimamo na sera ya Serikali ya Tanzania ya kuvumilia na kulinda uhuru wa watu kuabudu dini yoyote waitakayo na kamka mtu anataka kuamua kutokuwa na dini.

Pongezi hizo kwa Tanzania zilitolewa usiku wa jana, Jumamosi, Februari 7, 2015, na Kiongozi wa Kanisa hilo la SDA duniani, Rais wa the General Conference of the Seventh Adventist Church, Dkt. Ted N.C. Wilson na viongozi wenzake wakiwemo kutoka nchi za Afrika 11 wakati walipokutana kwa mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, na baadaye kula naye chakula cha usiku Ikulu, Dar Es Salaam.

Katika mazungumzo na Rais Kikwete na baadaye wakati wa hotuba yake kwenye chakula, Dkt. Wilson alimwambia Rais Kikwete: “Nataka kukupongeza na kukushukuru sana kwa kudumisha amani katika Tanzania na katika nchi nyingine za Afrika.”
Aliongeza: “Historia yako na ile ya Tanzania katika eneo hili inajulikana duniani pote. Hakuna shaka kuwa mmefanya juhudi kubwa kulinda na kudumisha amani hapa kwenu na nje ya nchi yenu. Kwetu sisi amani na utulivu ni mambo muhimu kwa sababu yanasaidia kueneza neno na injili ya Mungu katika hali salama kabisa.”

 Kiongozi huyo wa SDA aliongeza: “Aidha, tunakushukuru sana wewe na kuipongeza sana nchi ya Tanzania kwa uvumilivu wa imani za kidini na pia kwa kuweka, kulinda na kudumisha uvumilivu na uhuru wa kuabudu ambako kila mtu ana haki ya kuamua anaabudu nini. Asante, Mheshimiwa Rais na nchi yako, kwa kuinua kiwango cha uhuru na uvumilivu.”

Dkt. Wilson na viongozi wa SDA kutoka nchi mbali mbali duniani walikuwa nchini kushiriki katika mkutano wa kidini ujulikanao kama Blessings in Mission East and Central Africa ambao ulifanyika jana kwenye Uwanja wa Taifa mjini Dar Es Salaam. Dkt. Wilson alimweleza Rais Kikwete kuwa Kanisa lake limefanya mkutano mzuri na wa kuvutia na kuwa inakadiriwa kuwa kiasi cha watu 40,000 kutoka ndani na nje ya Tanzania walishiriki mkutano huo.


Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

8  Februari, 2015

 

ZANZIBAR KUANZA ZOEZI LA KUPIGA DAWA MAJUMBANI.

$
0
0
 Meneja kitengo cha kumaliza Malaria Zanzibar Bw. Abdalla Suleiman Ali akizungumza na waandishi wa habari juu ya zoezi la upigaji dawa ya kuuwa Mmbu wa Malaria zoezi hilo litaanza tarehe 15/02/2015 mpaka 26 kwa Unguja na Pemba ni tarehe 28 mwezi huu, Dawa itayotumika ni ACTELIC ambayo ipo salama kwa binadam taarifa hiyo kaitoa Ofisini kwake mwanakwerekwe Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga -Maelezo Zanzibar.

Na Makame Mshenga -Maelezo Zanzibar.

Jumla ya nyumba 34,874 zimelengwa kupigwa dawa ya Malaria katika zoezi linalotarajiwa kuanza februari 15 hadi 28 kwa Unguja na Pemba ni 28.

Akizungumza na waandishi wa habari Meneja kitengo cha kumaliza Malaria Zanzibar Bw. Abdalla Suleiman Ali alisema.''kutokana na mafanikio makubwa katika kupambana na Malaria ambapo takwimu zinaonyesha malaria imeshuka chini ya asilimia moja Zanzibar

mafanikio hayo yamepelekea kitengo kinachoshuhuliki malaria kubadilisha utaratibu wa upigaji dawa kwa kuelekeza nguvu zaidi kwenye maeneo ambayo bado wagonjwa wanaripotiwa ingawa kwa idadi ndogo.

Wilaya za Unguja ni- Wilaya ya kati Shehia 23 Kaskazini ''A'' Shehia 1 ambayo ni Mkokotoni Kaskazini ''B'' Shehiya 15 Magharibi Shehia 12 na Kusini Shehia 12  

Upande wa Pemba Shehia tisa zitapigwa dawa ambazo ni Wilaya ya Micheweni Shehia ya Tumbe, Kinyasini na Makangale, Mkoani Shehia za Wambaa na Michenzani Wete Shehia za Ukunjwi na Junguni na Chake Chake ni Shehia za Ngagoni na Mgelema.

HYUNDAI yashiriki Mkutano wa Kimataifa wa Teknolojia ya Mitambo ya Ujenzi.

$
0
0
Meneja Mauzo wa Hyundai, Bw. Alen Nkya (kushoto) akijadiliana na Meneja Mradi wa Dangote Industries, Mhandisi Markus Abayo (kulia) kuhusu mitambo ya ujenzi ya kisasa katika Mkutano wa Kimataifa wa Teknolojia uliofanyika Nairobi. Anayeshuhudia (katikati) ni Afisa Mikopo wa Hyundai, Bw. Manase Mpayo. Dangote Industries wanatumia mitambo ya Hyundai Excavator, Wheel Loader na Forklift katika miradi ya cement, n.k.

UWANJA WA MCHEZO WA GOFU WAZINDULIWA ZANZIBARI

$
0
0
4
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dk.Mwinyihaji Makame Mwadini akitoa hutuba ya ufunguzi wa kiwanja kipya cha Mchezo wa Gofu kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika Hoteli ya Sea Cliff  iliyopo Kiombamvua Wilaya ya Kaskazini B. Mkoa wa Kaskazini Unguja.
5
Msimamizi na Mtengenezaji wa  ujenzi wa kiwanja kipya cha mchezo wa Gofu Bw.Peter Matkovich kutoka Afrika Kusini alipokuwa akitoa shukurani zake wakati wa sherehe za ufunguzi wa kiwanja hicho  jana katika Hoteli ya Sea Cliff  iliyopo Kiombamvua Wilaya ya Kaskazini B. Mkoa wa Kaskazini Unguja.
2
Mwenyekiti wa Kampuni ya Sea Cliff Resort and Spa Zamzibar Bw.Subhash Patel (kushoto) akibadilishana mawazo na  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dk.Mwinyihaji Makame Mwadini baada ya kufungua kiwanja kipya cha Mchezo wa Gofu jana alipomuwakilisha  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika Hoteli ya Sea Cliff iliyopo Kiombamvua Wilaya ya Kaskazini B. Mkoa wa kaskazini Unguja.

6
Baadhi ya wageni mbali mbali kutoka Ndani na nje ya Zanzibar wakiwa katika sherehe za Ufunguzi wa kiwanja kipya cha mchezo wa Gofu kilichofunguliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dk.Mwinyihaji Makame Mwadini kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika Hoteli ya Sea Cliff iliyopo Kiombamvua Wilaya ya Kaskazini B. Mkoa wa kaskazini Unguja.
1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dk.Mwinyihaji Makame Mwadini akisalimiana na wageni waliohudhuria  katika ufunguzi wa Kiwanja kipya cha Mchezo wa Gofu jana uzinduzi alioufanya kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika Hoteli ya Sea Cliff iliyopo Kiombamvua Wilaya ya Kaskazini B. Mkoa wa kaskazini Unguja.
Picha na Ikulu

MAKALA YA SHERIA: JE WAJUA WOSIA WA MANENO NI WOSIA HALALI KISHERIA?

$
0
0
Wosia ni jambo kati ya mambo ambayo huwasumbua watu wengi. Sababu ya kuwasumbua wengi ni lile lile tu kuwa ufahamu wa mambo ya sheria haujawa wa kutosha katika jamii. Tatizo la wosia limepelekea magomvi makubwa ya kifamlia hasa wakati wa misiba au baada ya misiba.

Pia wakati mwingine ni tatizo hili hili ambalo limewafanya baadhi ya watu tena ndugu kugombea maiti. Kama watu wanaelewa vyema habari ya wosia na haki za kila mtu katika wosia sioni haja ya ndugu kugombea maiti au baadhi ya mambo ambayo marehemu pengine ameyatolea ufafanuzi kabla ya kifo chake.

Kuna wosia wa aina mbili,. Kwanza wa maandishi na pili wa maneno. Leo sisi tunaangalia wa maneno lakini kwanza wosia ninini.

NAPE: HAKUNA MGOMBEA ATAKAYEPITISHWA CCM KWA PRESHA ZA MAKUNDI, NI KWA KUKIDHI VIGEZO VYA KANUNI NA KATIBA ZA CHAMA TU

$
0
0
NA BASHIR NKOROMO.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema, hakuna kitakayempitisha kugombea urais 2015, kwa presha za makundi au wapambe.

Akizungumza kwa nyakati tofauti katika vyumba vya habari vya magazeti ya Habari Corporation, na Mwananchi Communication Ltd, jijini Dar es Salaam, leo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema, mfumo wa CCM katika kuwapata wagombea ni imara kiasi kwamba hautaweza kuathiriwa na presha za makundi wakati wa kuteua mgombea urais katika uchaguzi mkuu mwaka huu.

Amesema, ni vigezo vinavyozingatia kanuni na katiba ya Chama tu ndivyo vitakavyomuwezesha anayetaka kupeperusha bendera ya CCM kupitishwa na Chama, vinginevyo haitawezekana hata kama ana makundi yenye presha kiasi gani.

"Chama hiki kina mfumo na taratibu ambazo haziwezi kusukumwa na presha za wapambe wa mgombea yeyote, na hata kumbukumbu zinaonyesha kwamba katika chaguzi zilizopita, wamewahi kuwepo wagombea wenye makundi yenye presha kiasi cha kudhaniwa ndio wangeteuliwa, lakini baada ya kufika mbele ya taratibu na kanuni waliachwa na nafasi kupewa wengine", alisema Nape.

Alisema, kanuni na taratibu ndizo mwamuzi wa mwisho katika kuteua wagombea wa CCM, "Sisi tukisema wanaotaka nafasi hii njooni mjipime hapa, mmojawapo akijaiona hatoshi lakini kwa ujanja akaongeza matofali kupata urefu... huyo taratibu zitatumia kuondoa matofali ili abaki kama alivyo kuona kama anatosha", alisema Nape.

"Na katika utaratibu huu wa kuondoa matofali ndiyo watajitokeza baadhi yao kulalamika kwa sababu itauma kidogo", alisema.
HABARI KATIKA PICHA
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiingia katika ofisi za Kampuni ya Habari Corporation Ltd, kendelea na ziara katika vyombo vya habari aliyoianza wiki iliyopita. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma wa CCM, Godfrey Chongolo
 Nape akisalimiana na Mhariri Mkuu wa Habari Corporation Denis Msaky baada ya kuingia chumba cha habari
 Nape akisalimiana na Matinyi ambaye ni mmoja wa wahariri katika kampuni hiyo ya Habari Corporation, wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania, Rai na Dimba
 Napa kisalimiana na Mhariri wa Msanifu wa Habari wa Mtanzania Hamis Mkotya.

 Nape akiwa katika chumba cha habari cha Mtanzania
 Nape akitazama picha iliyomvutia katika chumba cha habari cha Mtanzania, ambayo alionyeshwa na Msaky.
 Picha yenyewe ni ya Rais wa sasa Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa na Muasisi wa Habari Corporation, Jenerali Ulimwengu
 Nape akionyeshwa chumba cha habari cha chenye mkusanyiko wa madawati mbalimbali ya magazeti ya Mtanzania Rai na Dimba
 Nape akisalimiana na Mhariri wa habari za Siasa Sarah Mosi
 Nape akisalimiana na Mhariri wa habari wa Mtanzania, Bakari Kimwanga
 Nape akisalimiana na John Mlinda
 Nape akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Usanifu
 Nape akiwa katika picxha ya pamoja na wasanifu wa kurasa
 Mhariri Mtendaji wa New Habari Corporation, Absalom Kibanda akimkaribisha Nape
 Mhariri Mtendaji wa New Habari Corporation Absalom Kibanda, akitambulisha kwa Nape uongozi wa magazeti ya kampuni hiyo.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati akizungumza na uongozi wa New Habari Corporation Ltd, hasa kuhusu masuala ya wagombea Urais
 Nape akizungumza zaidi
 Nape akizungumza mambo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Habari Corporation, Hussein Bashe baada ya mazungumzo ya ndani
 Wakuu wa New Habari Corporation wakiagana na Nape nje ya ofisi za kampuni hiyo
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akikaribishwa na Mhariri Mkuu wa Mwananchi, Bakari Machumu baada ya kuwasili kwenye ofisi za Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd leo
 Bakari Machumu akimkaribisha Nape ofisini kwake. Kushoto ni Chongolo
 Nape na Machumu akiwa katika chumba cha habari cha magazeti ya Mwananchi na The Chitizen
 Nape akizindikizwa na Machumu wakati wakienda ukumbini kwa ajili ya mazungumzo zaidi
 Nap0e akizungumza na uongozi wa magazti ya kampuni ya Mwananchi Communications Ltd
 Nape akisisitiza jambo wakati akizungumza na uongozi wa magazeti ya kampuni ya Mwananchi Communications Ltd
 Nape akimpatia zawadi ya kalenda ya CCM, Bakari Machumu, mwishoni mwa mazungumzo
 Haya kwaherini mbaki salama...
 "Mimi pia nipo hapa" Angetile Oseah akimwambia  Nape baada ya kukutana wakati akiondoka ofisi za Mwananchi Communication Ltd.
 Nape akiagana na Bakari Machumu mwishoni mwa mazungumzo. Picha na Bashir Nkoromo

WAKILI: MAHAKAMA IMEMTENDEA HAKI MACHA

$
0
0
NA MWANDISHI WETU
UPANDE wa utetezi katika kesi iliyokuwa ikimkabili mfanyabiashara Hans Macha, umesema Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imetenda haki kwa kuthibitisha kuwa mteja wao alinunua nyumba kihalali kutoka kwa mlalamikaji Ramadhani Balenga.

Kauli hiyo ya upande wa utetezi, imekuja ikiwa ni siku chache baada ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Devotha Kisoka kutoa hukumu iliyothibitisha kwamba Macha alinunua nyumba kihalali kutoka kwa Balenga.

Wakili wa Macha, Deo Ringia alidai mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam, kwamba mahakama hiyo imetenda haki kwa sababu ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri ulikuwa na mashaka na wa kuunga unga.

Alidai kwa upande wao, wamepokea hukumu hiyo kwa furaha zaidi kwani haki imetendeka.

"Haki imetendeka na mteja wetu amepumua. Tumeipokea hukumu kwa furaha zaidi kwani haki imetendeka kwa sababu hata usahahidi wa upande wa Jamhuri ulivyokwenda ulikuwa na mashaka na wa kuunga unga," alidai.

Wakili Ringia alidai atazungumzia zaidi hukumu hiyo ambayo Hakimu Moshi aliisoma kwa kifupi, baada ya kupata nakala yake.

Novemba, mwaka jana, mahakama hiyo ilimuona Macha ana kesi ya kujibu na kutakiwa kuwasilisha utetezi wake, baada ya upande wa Jamhuri kufunga ushahidi wake.

Macha wakati akijitetea aliita mashahidi takriban 10 ambapo, alikanusha tuhuma hizo kwa madai ni za uongo na kuiomba mahakama kuyatupilia mbali mashitaka hayo.

Alidai tuhuma hizo ni za uongo kwa sababu Balenga anafahamu kwamba alimuuzia nyumba hiyo.

SAFARI TV SHOW EP5

$
0
0
SAFARI ni kipindi kinachofundisha na kuburudisha kinachohusu suala zima la ujasiriamali endelevu. Kipindi hiki kikiwalenga vijana na watu wa kila rika. Ni kipindi kinachokuelezea namna ya kujenga au kukuza kipato ili kuondokana na adha za ajira, na kwa wale waliokata tamaa kinahamasisha kwa kukuonesha mbinu mbali mbali na fursa za kujikwamua kimaisha. 

TIPER kuongeza uwezo wa kuhifadhi mafuta kufikia mita za ujazo 213,000

$
0
0
 Mafundi wa kampuni ya kuhifadhi mafuta ya Tanzania International Petroleum Reserves Limited (TIPER), wakitengeneza paa katika moja ya matanki mapya ya kampuni hiyo, wakati kampuni hiyo ikitaraji kuongeza uwezo wa kuhifadhi mafuta maradufu baada ya kukamirika kwa ukarabati wa matanki yake wawili ya mita za ujazo 36,600 kila moja ifikapo machi mwaka huu.
Miongoni mwa matanki ya kampuni ya ya kuhifadhi mafuta ya Tanzania International Petroleum Reserves Limited (TIPER) yanayofanyiwa marekebisho, wakati kampuni hiyo ikitaraji kuongeza uwezo wa kuhifadhi mafuta maradufu baada ya kukamirika kwa ukarabati wa matanki yake wawili ya mita za ujazo 36,600 kila moja ifikapo machi mwaka huu 
 
Kampuni ya kuhifadhi mafuta ya Tanzania International Petroleum Reserves Limited (TIPER) inatarajia kuongeza uwezo wake wa kuhifadhi mafuta mara mbili zaidi baada ya kukamilika kwa ukarabati wa matanki yake mawili, yenye mita za ujazo 36,600 kila moja, ifikapo mwezi Machi mwaka huu.
 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo jana, mradi huo uliozinduliwa mapema mwaka jana,  unawakilisha uwekezaji wa Dola za kimarekani milioni 11 (Takribani 19bn/-) na utapelekea kuongezeka kwa uwezo wa kuhifadhi mafuta kutoka mita za ujazo 141,000 na kufikia mita za ujazo 213,200 mara baada ya kukamilika.
 
“Zaidi ya hayo, muundo mpya wa muunganiko wa bomba utaongeza ufanisi wa kupokea mafuta ya ‘Automotive Gas Oil’ (AGO) kutoka kwenye ‘Single Point Mooring’ (SPM) kutoka kwenye kiwango cha mtiririko ‘flow rate’ cha mita za ujazo 1,500 kwa saa mpaka kufikia mita za ujazo 2,000 kwa saa, ambacho ni kiwango cha kasi zaidi,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa TIPER, Bw. Daniel Belair.
 
Ili kukidhi ukuaji wa mahitaji ya bidhaa ya mafuta, Bw. Daniel Belair alisema kuwa kampuni hiyo ina mpango wa kutengeneza matanki mapya ili kuongeza uwezo wa kuhifadhi mafuta kwa mita za ujazo 100,000 zaidi ili kufikia mita za ujazo 313,200 katika siku zijazo. 
 
Kufuatia mradi huo, Bw. Belair alisema kuwa TIPER ina mpango wa kutandaza mabomba mapya ya kusafirisha mafuta kati ya Kigamboni na Kurasini.
 
“Mradi huu utaongeza ufanisi wa kusukuma kwa kasi zaidi bidhaa kwa wateja wetu waliopo Kurasini,” alisema huku akiongeza kuwa uwekezaji huo utagharimu kati ya Dola za kimarekani milioni 12 na 16.

Wakati huohuo kampuni itawekeza kiasi kingine cha Dola za kimarekani milioni 2 ili kubadilisha mfumo uliopo wa kupampu kwa kuweka pampu zenye uwezo mkubwa zaidi na wenye kuaminika na pia mita za utiririkaji ‘flow meters’ zitaongezwa.

Kupitia taarifa hiyo, Bw. Blair aliweka bayana mpango wa kampuni hiyo wa kutenga kiasi cha dola za kimarekani milioni 2 zitakazotumika kufanyia marekebisho mpango wake wa kukabiliana na dharura ‘Emergency Response Plan’ ili kwenda sambamba na uwezo huo mpya. Alisema kuwa kitengo cha kupambana na janga la moto pia kitaimarishwa zaidi.
 

SERIKALI YAIPONGEZA BENKI YA ACCESS KUFUNGUA TAWI LAKE JIJINI MBEYA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Abbas Kandoro akizungumza na wateja pamoja na wafanyakazi wa Benki ya Access wakati alipokuwa mgeni rasmi katika sherehe za uzinduzi wa tawi la benki hiyo jijini Mbeya mwishoni wa wiki iliyopita. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Mhe. Dk. Norman Sigallah King na kutoka kushoto ni Ofisa Masoko Mwandamizi wa Access Bank, Jonas Muganyizi Bisheko, Meneja wa Mkoa wa Benki ya Access Mbeya, Emmanuel Venance na Mwakilishi wa Benki ya Access kutoka Makao makuu jijini Dar es salaam, Sebastian Gaissert. (PICHA ZOTE NA CATHBERT ANGELO KAJUNA WA KAJUNASON BLOG-MBEYA).
Mwakilishi wa Benki ya Access kutoka Makao makuu jijini Dar es salaam, Sebastian Gaissert, akitoa hotuba yake katika sherehe za uzinduzi wa tawi la benki hiyo mkoani Mbeya.
Meneja wa Mkoa wa Benki ya Access Mbeya, Emmanuel Venance akizungumza machache wakati wa sherehe za uzinduzi wa tawi la benki hiyo mkoani Mbeya. Habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

Benki ya Exim yawaasa wateja wake kutumia fursa zilizopo katika sekta ya gesi nchini

$
0
0
 
 BENKI ya Exim imetoa wito kwa wateja wake kutumia vyema fursa ya ugunduzi uliopo katika sekta ya gesi  nchini kwani ina uwezo wa kubadilisha muundo wa uchumi uliopo na kujenga uchumi mpya uliojengeka katika utegemezi wa gesi asilia ambao utakua na matunda makubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya kibenki na biashara.

Wito huo ulitolewa na Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa benki hiyo, Bw. Dinesh Arora wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam hivi karibuni maalum kwa ajili ya wateja wake wakubwa.

Zaidi ya hayo, Arora alieleza kuwa sekta ya gesi inaambatana na fursa nyingi ambazo zinaweza kutumiwa na wadau mbali mbali waliopo katika sekta binafsi. Alitaja maeneo yenye fursa kuwa ni pamoja na matengenezo ya vifaa, ujenzi, huduma za mazingira na Mafunzo ya Ufundi.

“Ni imani yetu kama benki ya Exim kuwa, katika siku zijazo, kutakuwa na ongezeko kubwa la mahitaji ya makazi, sehemu za burudani, utalii, elimu na huduma za afya. Jukumu kubwa la sekta binafsi itakuwa ni kukuza uhusiano na sekta ya gesi na kugundua na kuzitumia fursa,” alisema.

Akizungumzia juu ya ukuaji wa uchumi nchini, Arora alisema kuwa makampuni yanahitaji mipango na mikakati ya kifedha ya muda mrefu ili kuweza kufikia mahitaji na malengo yao ya ukuaji.

 “Kama benki ya tano kwa ukubwa Tanzania, Benki ya Exim inatoa huduma za kibenki za uwekezaji katika mfumo wa ushauri na ‘intermediary’ ili kuzalisha na kuongeza mtaji kwa njia ya ‘debt and equity’ kwa wateja wakubwa,” alisisitiza..

Arora aliendelea kuwaasa wateja kutumia kitengo cha benki hiyo cha huduma za kibenki za uwekezaji, ambacho kwa sasa kina huduma mpya zilizotengenezwa maalum ili kukidhi mahitaji mahsusi ya wateja wake, zikiwemo Project Financing, Debt na Equity Syndication services na Private Equity na M & A Advisory Services.

Arora alisema kuwa benki yake imejenga uwezo mzuri katika suala hilo na piaimeongeza nguvu zaidi katika muundo wake wa uongozi ili kusaidia katika kurahisisha uwepo wa uhusiano wa kimataifa  na kuongeza  mtandao na wawekezaji. “Tumejiimarisha zaidi na tumefanya maombi ya vibali mbalimbali stahiki na pia tumeungana na wawekezaji,” alisema.  
  
Akizungumzia huduma zinazopatikana katika kitengo hicho cha huduma za kibenki za uwekezaji, Arora alisema moja ya huduma zinazotolewa na kitengo hicho ni pamoja na ushauri bora wa kimkakati kwa wateja wake.

“Muundo wa benki yetu unaturuhusu kuwahudumia wateja wetu na kuwapatia ufumbuzi wa mahitaji yao ya kimkakati na kifedha katika nyanja zote. Tunawiwa kuwa mshauri nambari moja kwa wateja wetu ikiwa ni pamoja na makampuni binafsi, taasisi za fedha, mamlaka za umma, wawekezaji na wakopeshaji,” alisema.

MHE. WAZIRI SAMUEL SITTA KUUNGURUMA MKUTANO WA KUJADILI KATIBA -MASWALI YOTE KUJIBIWA LIVE -WOTE MNAKARIBISHWA WASHINGTON DC -JUMAPILI FEB 22

Meli Kubwa yenye Urefu wa Mita 244 yatia nanga Bandari ya Dar

$
0
0
Meli kubwa MSC Martina yenye urefu wa mita 244 na upana wa mita 32.2 ikiwa na uwezo wa kubeba makontena 2,411 imefanikiwa kutia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka, Mhandisi Madeni Kipande amesema, mafanikio hayo ni juhudi zilizofanywa na Mamlaka kuzitangaza bandari zake pamoja na uboreshwaji wa huduma.

“Ujio huu wa meli kubwa za mizigo kama hizi ni faraja kubwa sana kwetu kwani pia utaongeza uingiaji wa mizigo kwa wingi na hatimaye kuleta unafuu kwa mtumiaji wa mwisho,” alisema Mhandisi Kipande. MSC Martina Kampuni ya Mediterranean Shipping Company (MSC) ni miongoni mwa meli kubwa na za kisasa ambazo zimefanikiwa kutia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam na kupakia na kupakua mzigo.

Meli nyingine kubwa na ya kisasa kuja nchini kwa mara ya kwanza ilikuwa ni Maersk Cubango mali ya Maersk Line iliyokuwa na urefu wa mita 250 na upana wa mita 38 ikiwa na uwezo wa kubeba kontena 4,500.

Mhandishi Kipande ameomba ushirikiano uliopo kati ya Mamlaka na mawakala wa meli uendelee ili kuleta ufanisi zaidi na amewataka mawakala wengine kuleta meli kubwa kama walivyofanya, Maersk and Mediterranean.

Kwa upande wake Nahodha aliyeingiza meli hiyo ndani ya Bandari ya Dar es Salaam, Abdulah Mwingamno alisema mabadiliko ya teknolojia yameongeza uwezo wa Bandari ya Dar es Salaam kuhudumia meli kubwa zaidi.

“Tuliweza kuingiza meli yenye urefu wa mita 250 ya kampuni ya Maersk iitwayo Maersk Cubango na sasa tumeingiza meli nyingine kubwa ya kampuni ya MSC iiitwayo MSC Martina yenye urefu wa mita 244, haya ni mafakio makubwa kwetu,” alisema.

Nahodha Mwingamno aliongeza kwamba meli hiyo ya mizigo iliingia salama katika lango la Bandari ya Dar es Salaam bila tatizo lolote kama ziingiavyo meli nyingine. Alisema kwamba ujio wa meli hiyo na kufanikiwa kutia nanga katika bandari yetu bila tatizo lolote ndio kumefungua milango kwa meli hiyo na nyingine za aina hiyo kuanza safari zake kuja Dar es Salaam.

“Tunatarajia ujio wa meli kubwa zaidi ya hii yenye urefu wa mita zipatazo 260 katika bandari yetu kwenye miezi ya Machi na Aprili mwaka huu,” alisema. Naye mwakilishi wa kampuni ya meli hiyo ya MSC nchini, Ndugu Ahmed Kamal alisema kwamba wanatarajia kuleta meli kubwa zaidi nchini, kwani kampuni yao ina meli kubwa zaidi zinazotia nanga katika bandari nyingine Duniani. 

“Hii ni meli kubwa ya kwanza ya kampuni yetu kuja nchini lakini lengo letu ni kuleta meli kubwa zaidi ya hii nchini,” amesema Kamal.

Meli nyingine kubwa zaidi zilizowahi kutia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam zilikuwa na urefu wa mita 220 na mita 234,  zikiwa na uwezo wa kubeba makontena kati ya 2800 na 3000. Awali meli zilizokuwa zinaruhusiwa kuingia katika bandari ya Dar es Salaam hazikutakiwa kuzidi urefu wa mita 234.

Imetolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)
S.L.P. 9184
Dar es Salaam

GUMZO LA JIJI LA NEW YORK NA VITONGOJI VYAKE NI "OMMY DIMPOZ KWA POZ " A.K.A SUPER HANDSOME LIVE UP CLOSE AND PERSONAL -FEB 21

$
0
0


TICKETS ON SALE NOW FOR $40 *** THEY WILL BE MORE AT THE DOOR $50
SEATED 3 -COURSE DINNER
FIRST CLASS SERVICE
RED CARPET PAPARAZZI 
DRESS READY FOR ACTION
HIGH LEVEL SECURITY 
**********************************************************

Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images