Pichani kulia ni Meneja Ubunifu wa Ofa za Kampuni ya Tigo,Bwa.David Sekwao akizungumza na mmoja wa washindi wa promosheni ya Ascend Y200 kwa njia ya simu iliyozinduliwa rasmi mnamo Oktoba 2012,inayomuwezesha mteja kununua samrtphone yenye kiwango na hadhi ya aina ya Ascend Y200 kwa punguzo la hali ya juu,Pichani kati ni Meneja wa Tigo,Bwa.William Mpinga na Muwakilishi kutoka michezo ya Bahati Nasibu nchini,Bwa.Bakari Maggid wakishuhudia tukio hilo lililofanyika leo kwenye hotel ya Holiday Inn,jijini Dar
Pichani kati ni Meneja wa kampuni ya Tigo,Bwa.William Mpinga akifafanua kuwa kwa "Mara nyingine tena Tigo inaendelea kuweeka tabasamu katika nyuso za thamani za wateja wetu kwa kuwapa fursa ya kujifunza na kuonja tamaduni mpya.Tunayo furaha kwa mara ya pili kuwa na shindano letu la Promosheni yetu bomba ya ‘Ascend Y200’ na kutangaza washindi mbalimbali ambao wataondoka hivi karibuni Dar-es-salaam kwenda China.
Siyo kwamba tunabadilisha tu namna wateja wetu wanavyowasiliana kupitia aina hii mpya ya smartphone zenye ubora wa hali ya juu katika nyanja mbalimbali za mawasiliano, bali pia tunabadilisha maisha ya Watanzania kwa kubadilisha uzoefu na kumbukumbu za maisha yao kwa kuwapatia bidhaa bora zenye thamani katika maisha yao yote." alisema Bw William Mpinga, Meneja wa Kampuni ya Tigo.
TIGO YAMPELEKA CHINA MSHINDI MWINGINE WA DROO YA ‘ASCEND Y200’..
Dar es Salaam Tanzania Machi 11, 2013: Tigo Tanzania leo hii imetangaza Washindi wa awamu ya pili ya droo ya ‘Ascend Y200’;
Simon Richard Simon (36) mkazi wa Ubungo, Dar-es-salaam na Frederick Wilfred Mgaya (24) mwanafunzi chuo Kikuu Kishiriki cha Tiba cha KCMU-Moshi na mkazi wa Moshi mkoani Kilimanjaro; wamejishindia zawadi ya kugharamiwa na Tigo gharama zote za kutembela miji mikubwa nchini China.
Meneja Usanifu na Ofa wa kampuni ya Tigo Bw. David Sekwao alisema “Promosheni ya ‘Ascend Y200’ ilizinduliwa rasmi mnamo mwezi Oktoba mwaka 2012 kwa 2012 inayomuwezesha mteja kununua smartphone yenye kiwango na hadhi ya juu aina ya ‘Ascend Y200’ kwa punguzo la hali ya juu. Droo ya kwanza ya Promosheni ya ‘Ascend Y200’ ilifanyika mnamo Disemba 19, mwaka 2012, ambapo washindi wawili wenye bahati safari ya kutembelea miji mbalimbali mashuhuri nchini China zilizogharamiwa na Tigo. Kutakuwa na droo nyingine tano ambapo jumla ya washindi wawili watachaguliwa katika kila droo, na kufanya idadi yao kuwa jumla ya washindi kumi.”
Aliongeza kuwa, zawadi hiyo ya safari ya China kwa washindi hao itajumuisha, Malazi, posho ya chakula kwa siku 3 katika hoteli ya Dragon Hotel iliyopo katika jiji la Guangzhou China, kutembelea vivutio mbalimbali kwa nusu siku jijini Guangzhou, mapumziko ya siku nzima katika milima ya Lotus nchini humo, pesa za matumizi binafsi kiasi cha Dola 200 za Kimarekani kwa kila mshindi pamoja na gharama zote za usafiri wa ndege.
Kigezo cha kushiriki shindano la Promosheni ya ‘Ascend Y200’, wateja wa Tigo wanatakiwa kununua smartphone yenye kiwango na hadhi ya juu aina ya ‘Ascend Y200’ kwa punguzo la hali ya juu katika duka lolote laTigo lililosajiliwa na kujiunga na pakeji ya A-Smart.
"Mara nyingine tena Tigo inaendelea kuweeka tabasamu katika nyuso za thamani za wateja wetu kwa kuwapa fursa ya kujifunza na kuonja tamaduni mpya.Tunayo furaha kwa mara ya pili kuwa na shindano letu la Promosheni yetu bomba ya ‘Ascend Y200’ na kutangaza washindi mbalimbali ambao wataondoka hivi karibuni Dar-es-salaam kwenda China.
Siyo kwamba tunabadilisha tu namna wateja wetu wanavyowasiliana kupitia aina hii mpya ya smartphone zenye ubora wa hali ya juu katika nyanja mbalimbali za mawasiliano, bali pia tunabadilisha maisha ya Watanzania kwa kubadilisha uzoefu na kumbukumbu za maisha yao kwa kuwapatia bidhaa bora zenye thamani katika maisha yao yote." alisema Bw William Mpinga, Meneja wa Kampuni ya Tigo.
Mpinga aliendelea kufafanua kuwa, "Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wateja wetu wote wa Tigo kwa mchango wao katika kukuza na kuendeleza promosheni hii na pia kuwaomba wale wote ambao bado hawajanunua smartphone yenye kiwango na hadhi ya juu aina ya ‘Ascend Y200’ kwa punguzo la hali ya juu kupata yao sasa, ili na wao waweze kupata nafasi ya kushinda safari ya kwenda China na kukamilisha furaha ya maisha yao.”