Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 457 | 458 | (Page 459) | 460 | 461 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la marehemu Bi.Tajiri Abdallah Kitenge wakati wa mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Chumbageni mjini Tanga.Marehemu Bi.Tajiri ni mama wa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama Bwana Rashid Othman.jk2 
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Bwana Rashid Othman wakati wa mazishi ya Mama yake Bi.Tajiri Abdallah Kitenge yaliyofanyika katika makaburi ya Chumbageni mjini Tanga jana(picha na Freddy Maro)

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akivunja Bunge. bu2Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge, Christopher Ole Sendeka, akijibu hoja za wabunge kuhitimisha mjadala.Kamati hiyo iliundwa kuchunguza na kuchambua Sera mbalimbali zinazohusu masuala ya Aridhi, Kilimo, Mifugo,Maji na Uwekezaji ili kubaini kasoro zilizomo katika matumizi ya Ardhi.
  bu3 
  Aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maenedeleo ya Makazi na Mbunge wa Mbunge wa Manyoni Mashariki, Kapteni Mstaafu John Chiligati, akichangia hoja.
  Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo, akichangioa taarifa ya kamati teule. bu5 
  Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Sabrina Sungura aichangia hoja.
  Mbunge wa Gando, Khalifa Suleiman akichangia taarifa.bu7 
  Wabunge wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge baada ya mkutano wa Bunge kuvunjwa.bu8 
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini Charles Mwijage, akisalimiana na Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda(kulia) baada ya Bunge kuvunjwa.Katikati ni Mbunge wa Viti maalum (CCM) mkoa wa Singida Diana Mkumbo Chilolo.
  bu9Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji George Masaju akibadilishana mawazo na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Martha Mlata.
  bu10 
  Baadhi ya wafugaji waliohudhuria Bungeni wakizaungumza na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) baada ya kuvunjwa kwa Bunge.
  ……………………………………………………………………
  Na Lorietha Laurence-Maelezo,DodomaWAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ametoa rai kwa wakulima na wafugaji nchini kujikubali kuwa wote ni Watanzania na wanahaki ya kuishi popote bila kuvunja sheria. Amesema hayo Bungeni Dodoma alipokuwa akipokea na kukubali taarifa na mapendekezo iliyotolewa na kamati teule ya Bunge ya kuchunguza na kuchambua sera mbalimbali zinazohusu masuala ya Ardhi,kilimo,mifugo,maji na uwekezaji.

  “Nimepokea mapendekezo yote yaliyotolewa na kamati na ninaahidi yatafanyiwa kazi kwa maslahi ya wananchi wa Tanzania” alisema PindaAliongeza kuwa kwa utekelezaji wa awali serikali itauunda tume maalum ya wataalum mchanganyiko na tume ya makatibu wakuu ili kuweza kupitia taarifa hizo na baadaye kuwasilisha kwa ajili ya utekelezaji.

  Aidha alisema ni wajibu wa Wizara ya Ardhi kupima ardhi katika maeneo mbalimbali na kwa wale wanaokiuka taratibu wachukuliwe hatua madhubuti ya kuwawajibisha.Hata hivyo Waziri Pinda alisema kuwa kuna umuhimu wa kutolewa kwa elimu ya kuwahamasisha wananchi umuhimu wa kulinda na kuitunza amani ya nchi yetu katika kuleta mabadiliko na kuondokana na mgawanyiko.

  Vile vile alizitaka Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa pamoja na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kuwachunguza watendaji wake wanaokiuka sheria na taratibu za utendaji na baadaye kuweza kuwawajibisha.  Naye Mwenyekiti wa kamati hiyo teule Mbunge wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka alisema kuna haja ya kuwatengea maeneo yaliyopimwa wafugaji na wakulima ili kuepusha vurugu kwa jamii hizo mbili.

  “Naiomba serikali iweze kushughulikia suali hili la wafugaji na wakulima ili kuepukana na migogoro inayojitokeza mara kwa mara katika maeneo hayo” alisema Ole Sendeka.

  0 0


  ..Kufanyika Nyumbani Lounge  Ijumaa Februari 13
  Na Andrew Chale.
   
  MBUNGE  wa Bunge la Afrika Mashariki, Mh. Shy rose Bhanji anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye usiku maalum wa Lady In Red 2015, Ijumaa ya Februari 13, kwenye ukumbi wa M.O.G Bar (Zamani Nyumbani Lounge) huku mitindo ya nguo nyekundu zitauzwa kwa ajili ya siku ya wapendanao ‘Valentine day’.
   
  Mwaka huu ni wa 11, tokea kuanzishwa kwa  Lady in red, ambapo itajumuisha wanamitindo mbalimbali pamoja na wabunifu tofauti katika redcapert iliyotayarishwa maalum kwa ajili ya usiku huo.Kwa mujibu wa wandaaji wa Usiku huo wa Lady in red 2015, Asia Idarous Khamsin ‘Mama wa Mitindo’  akishirikiana na Fashionnews  Tanzania, alieleza kuwa usiku huo utapambwa na Gusa Gusa Min Band,  kundil la Ngoma za asili na wengineo.
   
  “Ijumaa  ya Februari 13 ni siku maalum ya usiku wa Lady in red. Kwa kiingilio cha sh 10,000 kawaida na sh. 20,000 kwa upande wa V.I.P. Nguo nyekundu za Valentine day zitauzwa sambamba na kufurahia   burudani mbalimbali” alisema Asia Idarous na kuongeza kuwa vazi maalum la usiku huo ni rangi nyekundu na tiketi za usiku zinapatikana Fabak fashions, Mikocheni kwa Mwalimu Nyerere na Kobaz shop, Nyumbani Lounge.
   
  Aidha, usiku huo wa Lady in red  2015, mdhamini mkuu ni Maji Poa, wengine ni Darling hair, , Vayle Spring,  Eventlite, michuzi media group, chaneli ten, magic fm, sibuka tv, profile and style, Jambo Leo, mashughuli  blog, vijimambo blog, Voice of America, Mo blog, Supernewstz blog na wengine wengi.

  0 0

  3
  Mke wa Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bibi. Daniela Schadt (mwenye nguo nyekundu) akisikiliza maelezo mafupi kuhusu Shirika lisilo la Kiserikali la DSW Tanzania kutoka kwa Mkurugenzi wa shirika hilo Bw. Peter Owaga mara baada ya kuwasili katika ofisi za Shirika hilo zilizopo Tengeru Munasa jijini Arusha juzi.Wa mwisho kushoto ni Mkuwa Wialaya ya Arumeru Mhe. Nyirembe Munasa.
  4
  Mkurugenzi wa DSW Tanzania Bw. Peter Owaga akizungumza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa BEYOND 2015 juzi jijini Arusha. Kutoka kushoto ni Mke wa Rais wa Shirikisho wa Jamii Dkt. Elizabeth Mapella. BEYOND 2015 ni mradi uliolenga kuongeza hamasa na ushawishi kwa wadau wa maendeleo kutoa kipaumbele kwa vijana husasni katika Elimu, Afya ya uzazi na Ajira.la Ujerumani Bibi. Daniela Schadt, Mke wa Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bibi. Wenday Marshall – Kochanke na Mratibu wa Programu za Vijana kutoka Wizara ya Afya, na Ustawi.
  5
  Baadhi ya washiriki wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa BEYOND 2015 wakimsikiliza Mkurugenzi wa DSW Tanzania Bw. Peter Owaga (hayupo pichani).
  7
  Mke wa Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bibi. Daniela Schadt akifuarahi mara baada ya kukata utepe na kuzindua rasmi mradi wa BEYOND 2015, juzi jijini Arusha.Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa DSW Tanzania ambao ndiyo watekelezaji wa mradi huu Bw. Peter Owaga. Wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Nyirembe Munasa (nyuma ya Mke wa Rais wa Ujerumani) na Mratibu wa Mradi huo Bi. Ester Mwanjesa aliyeshika kitabu.
  8
  Mke wa Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bibi. Daniela Schadt akiteta jambo na Mkurugenzia wa DSW Tanzania(katikati) pamoja na Mratibu wa Mradi wa BEYOND 2015 Bi. Esther Mwanjesa mara baada ya kuzindua mradi huo juzi jijini Arusha
  9
  Mke wa Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bibi. Daniela Schadt akipokea zawadi ya Kimasai kutoka kwa Mwanamke mjasiriamali Bibi.Salome Samwel wakati alipotembelea maonyesho ya biaadha zao katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa mradi wa BEYOND 2015, juzi jijini Arusha.1
  Picha ya pamoja 
  2
  Mke wa Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bibi. Daniela Schadt (mwenye nguo nyekundu) akisalimiana na Mkurugenzi wa DSW Tanzania Bw. Peter Owaga mara baada ya kuwasili katika ofisi za Shirika hilo zilizopo Tengeru jijini Arusha alipoenda kuzindua mradi wa BEYOND 2015 hivi karibuni.

  …………………………………………………………………………
  Na Mwandishi Wetu, Arusha

  Mke wa Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bibi. Daniella Schadt ametoa wito kwa jamii kuhakiksha wanatoa kipaumbele katika kushirikisha vijana kwenye nyanja mbalimbali za maendeleo.
   Wito huo umetolewa juzi jijini Arusha wakati Mke huyo wa Rais wa Ujerumani alipokuwa akizindua mradi wa utetezi na ushawishi wa jamii katika kutoa vipaumbele katika sekta za Elimu, Afya na Ajira kwa vijana ujulikanao kama BEYOND 2015 ambapo mradi huo unaratibiwa na Shirika lisilo la Kiserikali la DSW Tanzania.
   Bibi. Daniela alisema kuwa jamii inapaswa kutoa mkazo katika sekta za Elimu, Afya na Ajira kwa vijana kwa kuwa duniani kote vijana ndiyo nguvu kazi katika kuletea maendeleo ya taifa lolote lile. ‘Tunapaswa kuweka mkazo kwa vijana wadogo, maisha yao ya baadaye yanaanza kuanzia sasa, tuweke mkazo katika Elimu na Afya kwa vijana wetu ili waeze kutambua fursa na kuzitumia.’’ Alisema Bibi. Daniela.
   Kwa upande wake Mkurugenzi wa DSW Tanzania Bwana Peter Owaga amesema kuwa ni wao kama asasi ya kirai wanashirikia na Serikali katika kuhakikisha utekelezaji wa sera zinazohusu vijana nchini zinaleta tijaOwaga ameongeza kuwa Serikali kama msimamizi imepiga hatu kubwa kwa kuwa na Sera na miongozo mbalimbali inayohusu vijana kama vile Sera ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007 inayotoa fursa kwa kijana kujitambua.
   Aidha Owaga aliongeza kuwa mradi wa BEYOND 2015 ambao umezinduliwa na Mke wa Rais wa UjerumaniBibi. Daniela Schadt umelenga kuongeza ushawishi na hamasa kwa washirika wa maendeleo ili kutoka kipaumbele kwa kutenga bajeti kwa ajili ya Elimu , Afya ya Uzazi na Ajira kwa vijana.
   Akizungumzia mikakati na namna mradi huo utakavyotekelezwa Afisa Muhamasishaji na Mawasiliano Bi. Ester Mwanjesa amesema kuwa mradi huo utatekelezwa kwa mwaka mmoja katika mikoa yote nchini ambapo mijadala mbalimbali itakuwa ikifanyika ili kuongeza hamasa ya uashawishi utakaopelekea kutoa kipaumbele kwa vijana hususan katika nyanja za Elimu, Afya ya uzazi na Ajira.
   Mradi huu wa BEYOND 2015 ambao ni kifupi cha maneno Building Expert Youth and Organisation for National Postion on the Post 2015 Development umelenga kutatua changamoto za vijana asa baada ya kumalizika kwa muda wa Malengo ya Melenia mapema mwaka huu.

  0 0

  jky4 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiweka shada kwenye kaburi la  Marehemu Bibi Bridget Ramadhani, mama Mzazi wa Jaji Augustino Ramadhani,  wakati wa mazishi Ijumaa February 6, 2015 huko Kimara King’ongo jijini Dar es salaam. PICHA NA IKULU
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Bibi Bridget Ramadhani, Mama Mzazi wa Jaji Augustino Ramadhani,  wakati wa mazishi Ijumaa February 6, 2015 huko Kimara King’ongo jijini Dar es salaam.jky2 
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakijumuika na
  waomboilezaji wengine  katika mazishi ya Marehemu Bibi Bridget
  Ramadhani, mama Mzazi wa Jaji Augustino Ramadhani,  wakati wa mazishi
  Ijumaa February 6, 2015 huko Kimara King’ongo jijini Dar es salaam.
  jky3 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiweka udongo
  kwenye kaburi la  Marehemu Bibi Bridget Ramadhani, mama Mzazi wa Jaji
  Augustino Ramadhani,  wakati wa mazishi Ijumaa February 6, 2015 huko
  Kimara King’ongo jijini Dar es salaam.


  0 0

  Itakumbukwa kuwa mnamo tarehe 26/01/2015 Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) lilisaini mkataba maalum na timu ya Real Madrid ya Nchini  Hispania ya kuanzisha na kuendesha kituo cha michezo (NSSF- REAL MADRID Sports Academy) kwa lengo la kuibua, kuendeleza na kukuza vipaji kwa mpira wa miguu. 

  Shirika la NSSF litajenga kituo hicho katika eneo la Mwasonga Kigamboni nje kidogo ya mji wa Dar es Salaam na wataalamu kutoka timu ya Real Madrid watatoa mafunzo kwa vijana wa umri wa miaka13 hadi 19 kwa madhumuni ya kukuza mpira wa miguu nchini, kupata wachezaji bora wanaouzika nje na ndani ya nchi pamoja na kulipatia mapato shirika na nchi kwa ujumla .

  Akizungumza na Waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya Habari Nchini, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Dr. Ramadhani K. Dau alisema mradi huo ukiwa kama sehemu ya uwekezaji wa NSSF ulianza maramoja baada ya kusaini mkataba.   

  NSSF imeanza utaratibu wa kuwabaini vijana walengwa ambapo kwa kuanzia utafutaji wa vipaji vya mpira wa miguu utaanzia mkoa wa Dar es Salaam kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 14. Utafutaji wa vipaji utafanyika kiwilaya kwa Wilaya za mkoa wa dar es salaam na utakuwa unafanyika  katika viwanja vya Karume. Zoezi hilo litakuwa linafanyika kati ya saa 1 asubuhi hadi saa 9 alasiri  kwa tarehe zilizoainishwa.

  Uandikishaji  wa washiriki utakuwa unafanyika siku za mwisho wa wiki ili kutoathiri wanafunzi watakaopenda kushiriki na utaanza rasmi tarehe 14 na 15,na tarehe 22 na 23  Februari 2015, na kufuatiwa na michezo ya majaribio tarehe 28 Februari,na Tarehe 1 Machi 2015 kwa wilaya  zote za mkoa wa Dar es salaam ambapo kituo kitakuwa viwanja vya Karume kuanzia saa moja asubuhi hadi saa 9 alasiri.

   Zoezi la Uandikishaji halitahusisha gharama zozote kwa washiriki, na uandikishaji wa washiriki utafanyika kwa kujaza fomu maalum na kupewa namba ya ushiriki na kila mshiriki atapata fursa ya kucheza katika awamu mbili za dakika 30. Kwa kuanzia washiriki watatakiwa kuja na vifaa vyao vya michezo. 

  Zoezi la awali litafanywa na wataalam wa ndani ya nchi ambapo Vijana 500 kati ya wote watakaofanyiwa majaribio  wataingia katika awamu ya pili ya majaribio na  watadahiliwa na wataalamu kutoka Klabu ya Real Madrid na hatimaye kupatikana vijana 30 amabo ndio wataingia katika  shule maalum ya mafunzo kwa awamu ya kwanza. 

  Wakati wa uandikishwaji washiriki watatakiwa kuja na wazazi/walezi wao wakiwa na vitambulisho vyao,na kijana husika awe na Cheti  halisi cha kuzaliwa  na kopi  yake pamoja na picha mbili za pasport  rangi ya blue.Muda wa uandikishaji na majaribio unaweza kuongezwa kulinagana na mahitaji.

  Shirika la NSSF linatoa wito kwa vijana kujitokeza kwani ni fursa kwao ya kuweza kujiendeleza kimichezo na kujiajiri katika tasnia hiyo

  0 0

   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Benard Membe akifanya mazungumzo na Rais wa Baraza Kuu la Makanisa ya Sabato Duniani Askofu Ted Wilson wakati wa siku ya ufungaji wa Kongamano hilo lililofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam siku ya tarehe 7 Februari, 2015.
   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Benard Membe ambaye alikuwa mgeni rasmi akiwahutubia wananchi pamoja na wageni wengine waalikwa (hawapo pichani) wakati wa siku ya ufungaji wa Kongamano hilo lililofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam siku ya tarehe 7 Februari, 2015.
   Watoto wakitoa burudani mbele ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa siku ya ufungaji wa Kongamano hilo lililofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam siku ya tarehe 7 Februari, 2015.
   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Benard Membe (aliyesimama katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Makanisa ya Wasabato (SDA) wakati wa siku ya ufungaji wa Kongamano hilo lililofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam siku ya tarehe 7 Februari, 2015.

  (PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO-DSM)
   
   
  Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dar es Salaam.
   
  WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe amelipongeza Kanisa la Wasabato (SDA) kwa kuwa mfano mzuri wa ustahimilivu, uvumilivu wa kidini na imani katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Mhe. Membe ameyasema hayo leo wakati alipokuwa akifunga rasmi Kongamano la siku 4 (4-7 Februari, 2015) Kimataifa la Utume kwa Kanisa la Sabato  lililofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambalo lilishirikisha Mataifa zaidi ya 20 Duniani.

  Alisema kuwa, katika kipindi chote cha uongozi wake kama Waziri hajawahi kusikia mgogoro wala matatizo yakioongozwa na SDA dhidi ya madhehebu mengine ya dini hapa nchini na hata dhidi ya wananchi.

  “Mpo mnafanya kazi zenu, mnachapa shughuli zenu kwa amani na utulivu, hamjachokoza mtu na hiyo ni sifa ya dini mojawapo yenye amani duniani”, alisema Mhe. Membe.

  Alisisitiza kwa kuwataka wananchi wa dini zote nchini kuiga mfano wa wana SDA ili Tanzania iendelee kuwa nchi yenye amani na utulivu.

  Aidha, alieleza kuwa, Dini na Diplomasia vina husiana pale masuala ya amani, ulinzi na usalama yanapoguswa huku akiwataka wananchi wa dini zote nchini kushiriki katika kutengeneza viongozi bora katika jamii kwa misingi ya uadilifu ambao watasimamia amani na kujiepusha na vitendo viovu ikiwemo rushwa.

  Aliongeza kuwa dhamira ya Serikali ya kuendelea kushirikiana nalo kwa ajili ya ustawi wa nchi huku akieleza kuwa, Serikali itaendelea kulinda uhuru wa kuabudu kwa dini zote kama inavyoelezwa kwenye Katiba ya Jamhuriu ya Muungano wa Tanzania.

  Naye Rais wa Baraza Kuu la Makanisa ya Sabato Duniani, Askofu Ted Wilson alisema kuwa anawaombea  Viongozi wa Tanzania waendelee na maono kwa lengo la kuwatumikia wananchi  na kwamba wakimtumaini Mungu atawawezesha kupata maono mapya kwa ajili ya kulitumikia Taifa zima.

  Kongamano hilo lilishirikisha Mataifa zaidi ya 20 ambapo Kanisa hilo la Wasabato ni Kanisa linalokua duniani likiwa na Waumini milioni 307 huku Waumini milioni 30 wakiwa Afrika na takriban milioni 5 wakiwa Tanzania.

  0 0

  *Ataka AZISE zishirikishwe kikamilifu
   
  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amezindua Mpango wa Kitaifa wa Kukuza Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) unaolenga kukuza viwango vya uelewa kwa watoto wa darasa la kwanza na la pili kwa nchi nzima.

  Mpango huo wa miaka mitatu ulioanza kutekelezwa 2014/2015 hadi 2016/2017 umelengwa kuwahusisha watoto wenye umri wa miaka mitano hadi 13 walio kwenye mfumo rasmi wa elimu na usio rasmi (MEMKWA).

  Akizungumza na wadau wa elimu, walimu na wanafunzi walioshiriki uzinduzi huo jana jioni (Jumamosi, Februari 7, 2015) Waziri Mkuu Pinda alisema mpango huo ni mkubwa na umeandaliwa mahsusi kujibu changamoto zilizojitokeza miaka ya nyuma.

  Aliwataka watekelezaji wakuu wa mpango ambao ni Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) pamoja na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kuhakikisha kuwa wanazishirikisha asasi zisizo za Kiserikali ambazo zinajihusisha na masuala ya elimu.

  “Kuna mashirika mengi yasiyo za kiserikali ambayo ni chachu ya kuhimiza elimu nchini... jaribuni kuwashirikisha sababu wao ni wadau wazuri sana wa suala hili. Pangeni utaratibu wa kukaa na hawa wadau na kuwapa mrejesho wa mpango huu mzima,” alisema Waziri Mkuu.

  Hata hivyo, Waziri Mkuu aliwataka wahusika wakuu wa mpango waangalie mgawanyo wa mikoa iliyoingizwa kwenye mpango huo kwa kuzingatia kanda ili kuleta matokeo ya mtawanyiko badala ya hali ilivyo sasa. “Nimeangalia jinsi mlivyogawa mikoa yenu, inanipa taabu kidogo... kuna mikoa inahitaji msukumo wa pekee, mikoa ya wadugaji, mikoa iliyoko pwani ya bahari na maziwa, yote inahitaji msukumo wa tofauti,” alisema.

  Katika taarifa yao, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilisema mpango huo wa KKK au LANES (Literacy and Numeracy Support Programme)  unafadhiliwa na Ushirika wa Kimataifa wa Maendeleo ya Elimu (Global Partnership for Education – GPE) na wahisani wengine.

  Wahisani hao ni pamoja na Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID) kupitia mradi wa EQUIP-T unaotekelezwa katika mikoa saba ya Kigoma, Shinyanga, Mara, Simiyu, Lindi, Dodoma na Tabora; Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Elimu kwa Mtoto (UNICEF) wanaofadhili utelekezaji wa Mpango wa LANES katika mikoa ya Iringa, Mbeya na Njombe; na Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID) kupitia Mradi wa TZ-21 unaotekelezwa katika mkoa wa Mtwara.

  Mapema, akisoma taarifa ya mpango huo mbele ya Waziri Mkuu, Kamishna wa Elimu nchini, Prof. Eustella Bhalalusesa alisema mpango huo umelenga kuongeza ufanisi katika stadi za KKK, kurahisisha kazi ya walimu wanaofundisha watoto wa darasa la kwanza na la pili pamoja na kuongeza ushiriki wa jamii katika kuboresha elimu na hasa ujifunzaji wa stadi za KKK.

  Alisema mpango huo utachangiwa sh. bilioni 150 ambazo zitaingizwa moja kwa moja kwenye mfuko wa elimu kupitia Wizara ya Fedha.

  Alisema maandalizi yote ya utekelezaji wa mpango huu yamekamilika ikiwa ni pamoja na mtaala wa darasa la kwanza na darasa la pili, muhtasari wa KKK kwa darasa la I & II, pamoja na Mwongozo wa Mwalimu wa kufundisha kusoma kuandika na kuhesabu.  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 980,
  DODOMA.
  JUMAPILI, FEBRUARI 8, 2015.

  0 0
 • 02/08/15--14:00: Watch "MALAIKA - MWANTUMU"

 • 0 0

  Bunduki ni miongoni mwa zana zinazotumika katika ngoma ya Asili kutoka nchini Moroko. Pichani Wasanii hao wakitumbuiza nje ya banda lao kuvutia wateja kujionea bidhaa mbalimbali za nchi yao katika maonesho ya Kimataifa ya Sanaa,ubunifu na utamaduni. Picha na Faki Mjaka-Mascut Oman
  Wasanii wa Ngoma za Asili kutoka Tanzania wakitumbuiza nje ya Mlangoni wa Banda lao la Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa Ubunifu na Utamaduni Mascut nchini Oman. Utumbuizaji wa ngoma ni mfumo wanaoutumia katika kuwavutia na kuwafurahisha Wateja kuingia katika Banda la Tanzania kwenye Maonesho hayo. Pichani ni Ngoma ya Msewe yenye asili ya Zanzibar. 

  Warembo kutoka Thailand wakiwa Wametulia nje ya Mlango wa Banda lao ikiwa ni ubunifu wa kuwavutia na kuwafurahisha Wateja wanaoingia katika Banda lao kujionea bidhaa mbalimnali za nchi yao katika Maonesho ya Kimatifa ya Sanaa,ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Mascut-Oman
  .Picha na Faki Mjaka.

  0 0


   Mwenyekiti wa Tamasha la tunzo za wasanii bora Zanzibar mwaka 2014/15  Seif Mohd Seif akizungumza na waandishi wa habari  juu ya maandalizi ya tamasha hilo  Ofisini kwake mtaa wa Mombasa nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.Picha Na Makame Mshenga –Maelezo Zanzibar.
   Mratibu wa Tamasha hilo Ramadhani Senga akijibu masuala ya waandishi wa habari kuhusu tunzo za mwaka huu katika mkutano uliofanyika Jengo la Zanzibar Media Corporation Limited mtaa wa Mombasa nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

   Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo katika jengo la Zanzibar Media Corporation Limited wakifuatilia mazungumzo hayo.
   Meneja Masoko wa Zanzibar Media Corporation Limited Said Khamis akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari  katika Mkutano wa  maandalizi ya Tamasha la tunzo za wasanii bora Zanzibar mwaka huu uliofanyika jengo la Zanzibar Media Cortporation Limited mtaa wa Mombasa. Picha Na Makame Mshenga –Maelezo Zanzibar.


  Na Ramadhani Ali-Maelezo Zanzibar  .            
  Taratibu za Tamasha la kuwatafuta wasanii bora wa Zanzibar (Zanzibar Music Awards) zinazosimamiwa na Kampuni ya Zanzibar Media Corporation  inayomiliki kituo cha Zenj Fm radio na kitengo cha Zenj Entertainment kwa mwaka 2014/2015 zimeanza rasmi leo.

  Akizungumza na waandishi wa habari katika jengo la Zanzibar Media Corporation, mtaa wa Mombasa nje kidogo ya Mji wa Zanzibar, Mwenyekiti wa Tamasha  hilo Seif Mohd Seif amesema maandali yamekamilika. Amesema tunzo hizo ambazo zinalengo  la kuwanyanyua wasanii wa Zanzibar kibiashara zitafikia kilele chake siku ya Ijumaa tarehe 27.2.2015 katika ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani.

  “Lengo la tunzo hizi ni kuweza kuwatangaza wasanii wetu wa hapa Zanzibar kibiashara, kuona thamani ya kazi zao na mchango wa sanaa zao unavosaidia jamii kuipa taaluma kupitia sanaa hizi,” alisisitiza Seif Mohd Seif.

  Ameongeza kuwa tamasha la mwaka huu ambalo ni la nane, kama yalivyo matamasha yaliyopita  yanasaidia kuinua sekta ya utalii kutokana na wageni mbali mbali kuhudhuria. Ametoa shukrani kwa wasanii wote wa Zanzibar kwa kuonyesha moyo wa kuziimarisha kazi zao ambazo zinakuwa na mvuto kwa jamii kwa kuendeleza sanaa nchini.

  Pia ameipongeza Kamati ya  majaji kwa kazi kubwa waliyofanya ya kupitia kazi za wasanii, na wadau mbali mbali kutoka vyombo vya habari vya Zanzibar ikiwemo Baraza la sanaa kwa michango mikubwa waliyotoa kufanikisha maandalizi ya Tamasha hilo.

  Mwenyekiti wa  Zanzibar Music Award amesema katika Tamasha hilo jumla ya makundi 18 yatawania tunzo hizo kwa wasanii wa Zanzibar pekee.
  Ameyataja makundi hayo kukwa ni  Video bora ya mwaka muziki wa kizazi kipya, video bora ya mwaka taarab ya kisasa, Mwanamuziki bora wa mwaka wa hip hop, Mwanamuziki wa mwaka wa R&B, Mwanamuziki bora wa Afro pop na Mtaarishaji bora wa mwaka.

  Wengine ni Mwanamuziki bora wa kiume  na wa kike taarab ya kisasa, Wimbo bora wa taarab ya kisasa ya mwaka, Mwanamuziki bora wa kiume na wa kike taarab asilia, Mwanamuziki bora wa kike na kiume muziki wa kizazi kipya na wimbo bora wa mwaka wa kizazi kipya.

  Katika makundi hayo pia kutakuwa na tunzo ya Mwanamuziki bora chipukizi wa mwaka, Mwanamuziki bora wa mwaka na Mshairi bora wa mwaka. Seif Mohd Seif amewataka watu wote wanaopenda kushiriki tunzo za mwaka huu kuwa upigaji  wa kura umeanza rasmi leo Jumapili na utamalizika siku ya Jumatano tarehe 25.2.2015 na matangazo ya kupiga kura yatarushwa na vyombo mbali mbali na katika Gazeti la Nipe Habari na kupitia website yao www.zenjifmradio.com

  IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

  0 0

   

  DSC_0200
  Kiongozi wa mila tarafa ya Ngorongoro, Augustino Pakai Olonyokei akizungumza na Meneja uendeshaji wa mtandao wa habari wa modewjiblog, Zainul Mzige aliyefika eneo hilo kwa ajili ya kuangalia miradi mbalimbali inayoendeshwa kusaidia jamii ya wafugaji wa kimasai hivi karibuni.

  Na Mwandishi wetu, Ngorongoro
  KIONGOZI wa mila tarafa ya Ngorongoro Augustino Pakai Olonyokei ameitaka serikali kusimamisha uwekezaji katika Mamlaka ya Ngorongoro ili kupunguza shinikizo la raslimali katika eneo hilo.

  Alisema kuendelea kuwekeza katika mahoteli,makambi ya watalii, miundombinu katika hali ilivyo sasa ni kuzidisha migogoro iliyopo kati ya wakazi wa eneo hilo na mamlaka ambayo tayari ipo. Olonyokei alisema hayo hivi karibuni wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi ambaye alifika eneo hilo kwa ajili ya kuangalia miradi mbalimbali inayoendeshwa kusaidia jamii ya wafugaji wa kimasai.

  Alisema hali ya sasa ni ngumu na inayosikitisha hasa kutokana na sheria iliyoanzisha mamlaka ya Ngorongoro kuwanyang’anya umiliki wa eneo ambalo wao wamelilinda miaka yote ndiyo maana wanyama wanapatikana na utalii unakuwepo. Aidha alisema mabadiliko ya hali ya hewa yanafanya mazingira yao kuwa magumu , wanakuwa na njaa huku wakiwa wamekatazwa kulima hata eneo dogo.

  “Tuna changamoto nyingi…hatuna ajira, ushiriki wetu katika bodi ni mdogo na baraza la wafugaji linapewa hela kidogo katika mazingira ya kuwa na miradi mingi,” alisema Olonyokei.

  Alisema Baraza hilo kupewa sh bilioni moja tu haitoshi wakati utalii ukiingiza mabilioni ya fedha. Pamoja na kuelezea changamoto hizo na kuitaka serikali kuzuia kuongezeka kwa shughuli zaidi katika eneo hilo, aliwataka watanzania kujua mazingira ya jamii ya wafugaji na adha wanazokutana nazo.

  Hata hivyo Mhifadhi wa mamlaka ya Ngorongoro Dk. Freddy Manongi amesema kwamba pamoja na malalamiko hayo, mamlaka hiyo iliyoanzishwa mwaka 1959 kwa ajili ya kutoa huduma kwa jamii, utalii na kuhifadhi mazingira mwaka jana pekee ilitumia sh bilioni 60.
  Fedha hizo ni kwa ajili ya kuhifadhi, kuendeleza jamii na utalii. Alisema msaada mkubwa wanaoufanya ni katika sekta ya elimu ambapo imejenga shule 21 na kila mwanafunzi anayekwenda sekondari kutoka katika eneo hilo hupatiwa udhamini wa masomo.

  Aidha alisema kutokana na wananchi kuzuiwa kulima, huwapatia mahindi kwa ajili ya chakula na ingawa kunatakiwa kuangaliwa namna bora zaidi endelevu ya wananchi kupata chakula lakini kwa sasa hilo ndilo wanalofanya.

  DSC_0041
  Mhifadhi wa mamlaka ya Ngorongoro, Dk. Freddy Manongi katika mahojiano maalum na Meneja uendeshaji wa mtandao wa habari wa modewjiblog. Zainul Mzige (hayupo pichani).

  “Mahindi ya bure yanapokosekana anagalau yawepo ya kununua kwa bei ya chini, na tunauza kwa shilingi 5000 kwa debe” alisema. Dk. Manongi alisema pia kwamba fedha nyingine zinatumika katika sekta ya afya na pia kuboresha hali ya mifugo kwa kuwezesha uharamishaji mifugo na kujenga majosho.

  Alisema ongezeko kubwa la watu katika eneo ambalo haliongezeki ni dhahiri linaleta migongano lakini mamlaka hiyo inafanya shughuli zake kwa kushirikiana na Baraza la wafugaji ili kupunguza migongano. Wakati mamlaka inaanzishwa 1959 eneo hilo lilikuwa na wakazi 8,000 baada ya wengine 4000 kuhamishiwa hapo kutoka Serengeti. Kwa sasa eneo hilo lina watu takaribani 90,000 katika eneo lilelile la kilomita za mraba 8,262.

  Alisema baraza hupewa sh bilioni 2 kwa mwaka wakati shughuli nyingine za maendeleo zinazofanywa na Mamlaka hugharimu sh bilioni 11. Kuhusu changamoto za elimu amesema kwa mwaka jana hali haikuwa njema kwa ufaulu lakini sasa wametafuta sababu na kuanza kuhakikisha kwamba walimu wanapewa motisha na pia wanafunzi wanapata mlo wa mchana ili kuwafanya wasitoroke.

  Kuhusu suala la ajira Dk. Manongi amesema ni tatizo la tafsiri tu lakini kila nafasi zinazpopatikana hujitahidi kuajiri watu kutoka katika eneo hilo. Alisema kuna mambo mengi yanayofanywa kuimarisha eneo hilo kuendeleza jamii na kuendeleza hifadhi ili kuwezesha utalii ambao ndio unatoa fedha kwa ajili ya mambo yote.

  0 0

   Kutoka kushoto Enock, Maromboso, Beka na Aslay wakiwa wameshikilia ticket zao za ndege  ambazo walikabidhiwa rasmi na mkurugenzi wa Zurii house of Beauty Jestina George Meru.
  Yamoto Band wanatarijiwa kufanya Live show kwenye jiji London siku ya tarehe 21.02.2015 katika ukumbi wa Royal Regency Banguet Hall 
   Zuri House of Beauty CEO Jestina George Meru akiwa kwenye picha ya pamoja na timu nzima ya Yamoto Band 
  Kama kawaida Ukitembelea Zurii House of Beauty huondoki mkono mtupu
  UK na Europe yote Siku ya Jumamosi tarehe 21 Feb 2015 tukutane pale kwenye ukumbi wa Royal Regency Manor Park London Kwani Hiyo ndio sehemu pekee kwenye jiji la London utapopata Burudani ya kukata na shoka kutoka kwa No1 band ya Tanzania Hakuna wengine ni wale wale vijana wetu wanne machachari wanaoitikisha East Africa sasa hivi YAMOTO BAND aka MKUBWA na WANAWE. Tickets are on sale now Standard ticket £25, VIP £35 kama unahitaji Meza ya watu 10 basi wasiliana nasi  kwenye number hizi  07853482158 @bongodeejays or whatsapp +447557304940 
  Also if you are in

  Northampton,you can get your tickets 

  Kass's Grill 01604621567/07527283219 
  And for people in Milton Keynes you can Get your tickets by 

  Calling  Cobby ...07448416240 London Chris Chagula 07405889880 /Hakim 07931 526622

  VjOj on 07940 679201and Exposed Uganda on  07931 119346 


  0 0

   Mshambuliaji wa zamani wa FC Barcelona na timu ya Taifa ya Uholanzi Patrick Kluivert alizungumzia ujio wa magwiji FC Barcelona nchini mwezi wa tatu mbele ya waandishi wa habari kwenye mgahawa wa Sports Lounge uliopo jijini Dar Es Salaam ,Pembeni ya Kluivert ni mwenyekiti wa DRFA Ndugu Almas Kasongo. Magwiji hao wa Barcelona wanataraji kucheza na wachezaji nyota wa Tanzania kwenye uwanja wa Taifa mnamo mwezi wa machi tarehe 28. 
  Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Dar Es Salaam,Almasi Kasongo akizungumza kwenye mkutano huo katikati na mwakilishi wa FC Barcelona pamoja na Mwakilishi wa kampuni ya Prime Time Promotions Stuart Kambona ambao ni waratibu wa mchezo huo.
   Baadhi ya Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo mapema leo asubuhi

  Timu ya wachezaji nyota wa zamani wa Barcelona FC watacheza na wachezaji wa zamani wa Tanzania, Tanzania All Stars Machi 28 kwenye uwanja wa Taifa jijini.Mwakilishi wa wachezaji wa zamani wa Barcelona, Patrick Kluivert alisema jana kuwa mechi hiyo itawahusisha wachezaji nyota wa Barcelona wakiwemo, Edgar Davids, Gaiza Mandieta, Ludovic Giuly, Francesco Coco na wengine wengi waliopitia klabu hiyo kwa miaka tofauti.Kluivert alisema kuwa kikosi chao kina wachezaji nyota ambao ni maarufu duniani na wanaamini mechi itakuwa nzuri na yenye ushindani mkubwa.

  Alisema kuwa yeye ni mwenyeji sana hapa Tanzania kwani huu ni ujio wake wa tatu na anaamini kuwa jinsi mashabiki wanapenda sana mpira wa miguu, itakuwa fursa kubwa kwao kuona vipaji vya zamani ambavyo  vimetukuka.“Ninafurahi kuja nchini Tanzania kwa mara ya tatu, ni faraja kubwa pia kucheza hapa nchini kwa mara ya kwanza, naomba mashabiki wa soka wajae uwanjani kuona mpira wenye ushindani,” alisema Kluivert.

  Mwakilishi wa kampuni ya Prime Time Promotion inayoratibu mechi na ziara ya timu hiyo ya Barcelona, Stuart Kambona alisema kuwa madhumuni ya mchezo huo ni kudumisha mahusiano ya kibiashara ya mpira wa miguu baina ya Tanzania na Hispania, kutangaza utalii na kuendeleza mahusiano mazuri baina ya nchi hizo mbili.

  Kambona alisema kuwa pamoja na kucheza soka siku hiyo, ujio wao pia utaitangaza nchi nje ya mipaka yake na kuleta fursa nyingi hapa nchini.“Wachezaji wa Barcelona wanataingia nchini siku mbili kabla ya mechi na watakuwa zaidi ya 20, majina ya wachezaji wengine yatatangazwa baadaye, ila tunaomba wadhamini wajitokeze kufanikisha na kufaidika na  mechi hiyo,” alisema Kambona.

  Mwenyekiti wa Chama cha soka cha mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)  Almasi Kasongo aliwaomba mashabiki wa soka kujiandaa kuangalia mechi hiyo  kwa kufika uwanjani.

  Kasongo alisema kuwa DRFA imefarijika sana kwa ziara hiyo na kuiomba Prime Time Promotion kuhakikisha kuwa inapanua wigo kwa kuandaa mechi nyingi ambazo zitakuwa chachu ya maendeleo ya soka nchini.

  0 0

  Si Kila Unayemkuta Kijijini ni mshamba wengine wanajua na wanaweza kuliko wewe. Mzee Mbunda na wajukuu zake jembe na Edo Madirector Kutoka mjini wanaingia kijijini na kuwa na maisha ya kimbulu yaani Paka liloshindikana ila wnakwaa visiki baada ya kukutana na wanakijiji wanajua zaidi yao.
  Pata Filamu hii ya Kimbulu Kupitia Mtandao Taarifa nzuri zaidi ni kwamba Filamu zote za Kiswahili unaweza Kuzipata kupitia mtandao au ukaziangalia kupitia mtandao au kununua pia popote pale duniani
  Tembelea Tovuti hii kwa kuangalia au kununua filamu hii ya KIMBULU na nyingine nyingi tu.

  0 0

  ARTIST: DAT
  VIDEO: EKIGAMBO
  GENRE: TAULA TAMADUNI
  PRODUCTION: WHITE, CONCEPT MEDIA

  0 0

  Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Siemens, Bi.  Sabine Dall’Omo, wakati akifafanua jambo, alipomtembelea Waziri wa Uchukuzi akiwa na ujumbe wake, kutaka kufahamu fursa za uwekezaji katika sehemu ya reli, leo asubuhi.
   Wakurugenzi wa Wizara ya uchukuzi, na ujumbe wa kampuni ya Siemens kutoka nchini Afrika Kusini wakimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Siemens, Bi Sabine Dall’Omo( wa nne kutoka kulia), wakati Afisa huyo na Ujumbe wake walipotembelea Wizara ya Uchukuzi, kufahamu fursa mbalimbali za uwekezaji katika sehemu ya reli leo asubuhi.


  Makamu wa Rais wa Kampuni ya Siemens, Bw. Kevin Pillay, akiwasilisha mada, wakati ujumbe wa Kampuni hiyo ulipomtembelea Waziri wa Uchukuzi, leo asubuhi kufahamu fursa mbalimbali za uwekezaji katika sehemu ya reli. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi).

  0 0

     MWANAHABARI FRANK KIBIKI  AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI OFISINI KWAKE
    MWANAHABARI FRANK KIBIKI  AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI OFISINI KWAKE.

  MWANAHABARI Frank Kibiki, aliyewahi kuwa Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) ngazi ya wilaya kwa zaidi ya miaka 10.

  Akizungumza na mtandao huu MWANAHABARI FRANK KIBIKI  alisema kuwa vijana wengi wamekuwa wakibweteka kwa kutojituma kufanya kazi na kuendelea kuilaumu serikali.

  “Eti asubuhi unawakuta vijana wamekaa kwenye vijiwe wakizungumza siasa na kucheza mabao wakati hawajui mchana watakula wapi na jioni watarudi na nini nyumbani”alisema MWANAHABARI  FRANK KIBIKI

  MWANAHABARI  FRANK KIBIKI  ameendelea kuwaomba vijana wengi wenye fursa ya kurudi au kuingia shuleni upya warudi kwa kuwa dunia ya sasa inataka wasomi wengi kutokana na mabadiliko ya kiuchumi na sayansi na teknolojia na ndio sababu inayopelekea hata watu wazima kurudi shuleni.

  “Vijana mnatakiwakujifunza kutoka kwa watu wazima ambavyo wamekuwa wakijituma kufanya kazi kwa bidii na kujituma ilimradi kuwatengenezea watoto maisha mazuri pamoja na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla”alisema MWANAHABARI  FRANK KIBIKI

  Lakini MWANAHABARI  FRANK KIBIKI  amewataka wakinamama kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi mwaka huu.

  MWANAHABARI  FRANK KIBIKI  ameeleza kuwa wanawake waondoe hofu ya kugombea hasa kukiwa na ushindani wa wagombea wanaume kwa kuogopa kuchafuliwa kwa mambo yasiyokuwepo.

  Ameendelea kusema kuwa wananchi wasishawishiwe na propaganda za wanasiasa na badala yake wachague viongozi bora wenye uwezo wa kuongoza kutoka katika chama chochote.

  Aidha ameongeza kuwa viongozi wawe na sera za kutekelezeka ili kuwatendea haki wapiga kura wao hali itakayowafanya waaminike katika jamii.

  Mbali na hayo MWANAHABARI  FRANK KIBIKI  amewakumbusha vijana kutokubali kutumiwa na baadhi ya wanasiasa katika kuleta vurugu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu na badala yake wachague kiongozi mwenye weredi na sifa za kuwa kiongozi kutokana na sera za chama chake.

  Ameendelea kusema kuwa vijana wajitokeze kwa wingi katika kupiga kura ndiyo katika katiba iliyopendekezwa ili kuweza kufanya uchaguzi ulio wa haki na amani pia kujitokeza katika kujiandikisha katika daftari la wapiga kura pamoja na kupiga kura.

  0 0

    MWIMBAJI mahiri wa  nyimbo za Injili nchini, Upendo Kilahiro amesema kuwa endapo atapata nafasi ya kushiriki kwenye miaka 15 ya Tamasha la Pasaka mwaka huu, ataimba nyimbo zilizopo katika albamu yake mpya inayotarajia kukamilika hivi karibuni.
   
  Kwa mujibu wa Kilahiro tamasha hilo ni maalum kwa sababu  linatimiza miaka 15 tangu kuanzishwa kwake hivyo akipata nafasi katika tamasha hilo ataimba nyimbo mpya kama zawadi kwa watanzania.
   
  Alipotakiwa kuitaja albamu hiyo na baadhi ya nyimbo zilizomo humo alisema ni mapema kuitaja hata hivyo nia yake ni kuwashitukiza watanzania watakaopata fursa ya kushiriki tamasha hilo ambalo litakuwa la aina yake.
   
  Alisema iwapo atapata nafasi katika tamasha la mwaka huu ataimba nyimbo hizo mpya na zile za zamani ambazo zinatamba katika ulimwengu wa muziki wa injili huku akiwaomba watanzania kufika kwa wingi katika tamasha hilo litakuwa tofauti na mengine yaliyowahi kufanyika.

  0 0

   Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo akitoa taarifa ya kupungua kwa mfumuko wa bei nchini kwa mwezi Januari, 2015 leo jijini Dar es salaam.

  Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
  9/2/2015, Dar es salaam.

  Ofisi ya Taifa ya Takwimu imesema kuwa Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Januari, 2015  umepungua hadi kufikia asilimia 4.0 kutoka asilimia 4.8 ya mwezi Desemba, 2014 kutokana na kuendelea kupungua kwa kasi ya bei ya bidhaa na huduma mbalimbali nchini.

  Akitoa taarifa ya mfumuko huo leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraim Kwesigabo amesema kuwa kupungua kwa mfumuko wa Bei katika maeneo mbalimbali nchini kumesababishwa na kupungua kwa kasi ya bei ya bidhaa za vyakula na  zile zisizo.

  Amesema kiwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya kimeonyesha kupungua katika maeneo mbalimbali nchini kikihusisha bei ya mahindi, Unga wa mahindi , ndizi, ndizi za kupika na mihogo.

  Aidha, Bw. Kwesigabo ameeleza kuwa bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei nchini ni pamoja na mafuta ya taa asilimia 8.4, dizeli asilimia 10.2, Petroli kwa asilimia 6.8 na  gesi ya kupikia kwa asilimia 2.9.

  Akitoa ufafanuzi kuhusu  kiwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi kwa kipimo cha mwezi kati ya mwezi Desemba 2014 na Januari 2015 , amesema kuwa mwezi Januari umekuwa na ongezeko la asilimia 1.0 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 2.0 la mwezi Desemba , 2014.

  Kuhusu Fahirisi za bei kwa maana ya kiwango cha badiliko la kasi ya bei  za makundi ya bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na Kaya binafsi kwa kuzingatia kipimo cha mwezi zimeonyesha kuongezeka hadi kufikia 152.43 kwa mwezi Januari 2015 kutoka 150.92 za mwezi Desemba, 2014.
   
  Amebainisha kuwa kuongezeka kwa Fahirisi hizo kumechangiwa na bidhaa za mchele, nyama, samaki ,lishe kwa watoto, mbogamboga, mavazi ya wanawake, kodi ya pango na mkaa kwa asilimia 1.6 .

  Kwa upande wa uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma za mlaji kwa mwezi Januari , 2015 Kwesigabo amesema kuwa umefikia shilingi 65 na senti 60 ikilinganishwa na kiasi cha shilingi 66 na senti 26 za mwezi Desemba 2014.

  “Uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma zilezile kwa mlaji kwa mwezi Januari 2015 na Desemba 2014 umepungua kidogo, hii inamaanisha sasa mtu hahitaji kuongeza ziada ili aweze kununua bidhaa na huduma anazozihitaji”

  Kwa upande wa mfumuko wa Bei wa mwezi Novemba 2014 katika nchi za Afrika Mashariki amesema una mwelekeo unaofanana , Kenya ukipungua  na kufikia  asilimia 5.53 kwa mwezi Januari 2015, kutoka asilimia 6.02 za mwezi Desemba 2014, Uganda  mfumuko wa bei kwa mwezi Januari 2015 umepungua hadi asilimia 1.3 kutoka asilimia 1.8 za mwezi Desemba 2014.

older | 1 | .... | 457 | 458 | (Page 459) | 460 | 461 | .... | 1897 | newer