Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU ATAKA VETA IANDAE VIJANA STADI YA MADINI

$
0
0

*Akabidhi vyerehani 20 kwa wahitimu wa VETA Songea

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameutaka uongozi wa Bodi ya Mamlaka ya Vyuo.Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) nchini uelekeze jicho lake Nyanda za
Juu Kusini na kuandaa vijana wenye weledi na stadi ya uchimbaji madini
ili kukabili changamoto za soko.

Ametoa wito huo jana jioni (Jumamosi, Januari 31, 2015) wakati
akizungumza na walimu na wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi
(VETA) cha Songea mjini, mkoani Ruvuma ambako pia alikabidhi vyerehani
20 vyenye thamani ya sh. milioni 4/- kwa wanafunzi 20 waliohitimu kozi
ya ushonaji mwaka jana.

Waziri Mkuu ambaye aliwasili Songea mjini jana jioni akitokea Dodoma,
alifanya kazi hiyo ya kukabidhi vyerehani ikiwa ni utekelezaji wa
ahadi aliyoitoa Julai 20, 2013 wakati akizindua chuo hicho alipofanya
ziara ya kikazi kwenye mkoa huo.

“Katika kipindi kifupi, mkoa wa Ruvuma umeanza kubadilika kwa kasi ya
haraka. Kuna madini ya urani, makaa ya mawe na dhahabu. VETA inapaswa
iangalie fursa hii kwa kuandaa vijana wenye stadi za uchimbaji madini
ili wakati wawekezaji wakianza kuchimba tayari muwe na watu wa kufanya
hiyo kazi kutoka kwenye mkoa huu,” alisema Waziri Mkuu.

“Wasilianeni na Wizara ya Nishati na Madini ili mjue mahitaji yao
kwenye eneo hili ni yapi. Wakianza uchimbaji watataka watu wa kufanya
kazi hizo. Andaeni vijana... siyo mkae tu na kuja kushtukizwa au
mjikute vijana kutoka mbali wanapata hizo ajira wakati wa kwenu
wangeweza kunufaika na fursa hii,” alisema.

Aliwataka vijana wanaosoma katika chuo hicho wasome kwa bidii na
kuacha kasumba ya kuchagua kazi na kuonea aibu baadhi ya kazi.
“Someni, someni sana kwa sababu ustawi wa maisha ya Mtanzania hapo
baadaye unategemea elimu ya ufundi. Tuachane na fikra potofu za
kuchagua kazi. Kama ni mpishi fanya kazi ya upishi vizuri sababu
walaji wapo, hawaishi,” alisisitiza.

Alisema VETA inaweza kuwa suluhisho la ukosefu wa ajira hapa nchini
kwa sababu ufundi na stadi wanazopata wahitimu wa vyuo hivi vinapaswa
kuwapatia ajira. “Tanzania ina wakazi milioni 45 na wote hawa wanataka
kuvaa. Mkianzisha kikundi kidogo kuamua kushona tu sare za shule,
tayari mtakuwa mmetoa jibu kwa hitaji la sare za wanafunzi. Wamachinga
watanunua kwenu na kuuza lakini na ninyi pia mtapata fedha kuendeshea
mradi wenu,” aliwasisitizia wahitimu hao.

Mapema, akisoma risala ya chuo hicho, Mwenyekiti wa Bodi ya VETA Kanda
ya Nyanda za Juu, Bw. Kabaka Ndenda alisema chuo hicho kimekwishatoa
wahitimu wa kozi fupi 2,627 katika fani mbalimbali za mafunzo ambapo
kati yao wavulana ni 2,202 na wasichana ni 425.

Aliiomba Serikali iiangalie VETA kisera zaidi kama mkombozi wa ajira
hasa wakati huu ambapo vijana wengi wanakabiliwa na ukosefu wa ajira.
Alizitaja baadhi ya kozi zinatoloewa chuoni kuwa ni mafunzo ya udereva
wa magari na pikipiki; uhazili; utengenezaji wa kompyuta; umeme wa
jua; umeme wa majumbani; ulimbwende (cosmetology) na upishi.

Alisema chuo hicho kwa sasa kina wanafunzi 298 wanaoendelea na kozi
mbalimbali na mwaka huu kinatarajia kudahili wanafunzi 306.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, FEBRUARI MOSI, 2015.

Makamo mwenyekiti wa UTU kuwasili Tanzania

$
0
0
 Makamo mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania  Ujerumani UTU e.V  Mheshimiwa Peter Kazaura kuwasili nchini Tanzania Kesho 02.02.2015

Makamo mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania  Ujerumani UTU e.V  Mheshimiwa Peter Kazaura kuwasili nchini Tanzania Kesho 02.02.2015 kwa ajili ya kufanya mazungumzo na kiongozi wa juu wa Taifa. akiwa Tanzania atafanya mazungumzo na uongozi wa mashirika  yafuatayo TIC, Basata, Wizara ya Ardhi, NSSF, NHC,  Tanzania Diaspora Initiative na Wizara ya Utamaduni Michezo na Vijana.  

Mazungumzo hayo yatalenga upatikanaji wa Fursa zilizopo Tanzania kwa Diaspora. akiendelea kueleza msemaji wa Umoja huo Watanzania wanaoishi ujerumani wangependa pia kuhusishwa kikamilifu katika shughuli za maendeleo nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na Afya, Elimu.naye  Mwenyekiti wa  Umoja huo Mhe. 

Mfundo Peter Mfundo alithibitisha kuwepo kwa safari ya Makamo Mwenyekiti Mhe Peter Kazaura na  alisema  UTU e.V umechukua uamuzi huo  baada ya Watanzania nchini Ujerumani kukosa nafasi ya kuongea na Rais wa Tanzania  wakati wa ziara ya Rais nchini Ujerumani.Pia watanzania wanaoishi ujerumani wanaulalamikia ubalozi kuwa viongozi wa umoja wao walinyimwa nafasi ya kuonana na kumsalimia Mhe.Rais Dkt.Jakaya Kikwete.--

Mfundo Peter Mfundo
Vorsitzender U T U e.V

Chipukizi wa UVCCM wa Songea watia fora katika maadhimisho ya miaka 38 ya CCM uwanja wa Majimaji

$
0
0
 Mawenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisimama kikakamavu wakati wimbo wa Taifa ukipigwa kwenye kilele cha sherehe za miaka 38 ya CCM katika uwanja wa Majimaji mjini Songea ziliziopambwa vilivyo na chipukizi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)
 Chipukizi wa UVCCM wakipia saluti huku wakiimba  wimbo wa Taifa
 Saluti kwa wimbo wa Taifa
 Bendi ya Chipukizi kutoka Zanzibar ikipiga wimbo wa Taifa
 Rais Kikwete akikagua gwaride la chipukizi wa UVCCM
 Kamanda wa gwaride la chioukizi wa UVCCM akimshukuru Rais Kikwete kwa ukaguzi
 Chipukizi wakakamavu wa UVCCM Songea wakiwa kazini huku wakishangiliwa
 Wanahabari wakirekodi tukio zima
 Gwaride la chipukizi wa UVCCM songea
 Gwaride likijiandaa kwa mwenzo wa pole
 Kikosi cha Bendera
 Chipukizi wa UVCCM Songea wakionesha ukakamavu wa hali ya juu
 Nidhamu na ukakamavu
 Gwaride likipita mbele ya jukwaa kuu
 Meza kuu ikipokea gwaride kwa furaha

 Rais Kikwete akionekana kufurahishwa na gwaride la chioukizi wa UVCCM Songea
 Sehemu ya maelfu ya wananchi wa Songea
 Gwaride kazini
 Ukakamavu na nidhamu
 Heshima kulia
 Hakuna mchezo hapa
 Kiapo cha utii baada ya hatua 15 mbele
 Kikosi cha "makomandoo" wavulana
 Kikosi cha "makomandoo" wasichana
 Sanaa ya kujilinda kwa mikono mitupu.
 Kamanda msaidizi akitoa amri
 Makamanda wa gwaride
 Wapiganaji wa TBC One wakirusha live tukio zima
 Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Dkt John Nchimbi akisema machache
 Sehemu ya wageni kutoka mikoa yote
 Wageni kutoka chama tawala cha Uganda wakiteta jambo
 Sehemu ya waalikwa kutoka mikoa yote
 Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana akiongea na umati
 Mwakilishi wa cha tawala cha Uganda akisema machache
 Sehemu ya jukwaa kuu ikishangilia
 Makamu Mwenkeyikiti wa chama tawala cha Uganda akisalimia
 Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete akicheza kwa furaha jukwaa kuu
 CCM Oye!
 Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete akihutubia umati wa wananachi
 Rais Kikwete akimpongeza Mwenyekiti wa CCM Songea kwa maandalizi mazuri 
 Sehemu ya maelfu ya wananchi
 Rais Kikwete akiendelea na hotuba
 Nyomi
 Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete akigawa kadi kwa wanachama wapya akiwa na Mbunge wa Songea Mjini Dkt Emmanuel Nchimbi na Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana
  Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete akigawa kadi kwa wanachama wapya akiwa na Mbunge wa Songea Mjini Dkt Emmanuel Nchimbi na Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana
  Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete akigawa kadi kwa wanachama wapya akiwa na Mbunge wa Songea Mjini Dkt Emmanuel Nchimbi na Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana
  Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete akigawa kadi kwa wanachama wapya akiwa na Mbunge wa Songea Mjini Dkt Emmanuel Nchimbi na Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana
  Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete akigawa kadi kwa wanachama wapya akiwa na Mbunge wa Songea Mjini Dkt Emmanuel Nchimbi na Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana
  Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete akigawa kadi kwa wanachama wapya akiwa na Mbunge wa Songea Mjini Dkt Emmanuel Nchimbi na Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana
 Msanii Diamond na kundi lake la Wasafi wakitumbuiza
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernad Membe akiongea na Naibu Waziri wa Fedha Mhe Mwigulu Nchemba
 Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana na Katibu Mwenezi na Itikadi Ndg Nape Nnauye wakisalimia umati
 Diamond na kundi lake wakitumbuiza
Diamond na Abddul Misambano na kikundi cha TOT wakitumbuiza
PICHA NA IKULU

BARABARA YA IGAWA – UBARUKU KUJENGWA KWA LAMI.

$
0
0

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli amesema serikali itajenga barabara ya Igawa hadi Ubaruku KM 18 kwa kiwango cha lami ili kuinua fursa za uchumi za wilaya ya Mbarali na kuwezesha magari makubwa kupita kwa urahisi kufuata mazao katika eneo hilo.
Waziri Dkt. Magufuli amesema hayo katika ziara yake inayoendelea mkoani Mbeya ambapo leo ameweka jiwe la msingi  ujenzi wa barabara ya igawa-ubaruku  yenye urefu wa KM 18 na kusisitiza barabara hiyo ni muhimu kwa uchumi wa mkoa wa Mbeya na taifa kwa ujumla.
“Nitahakikisha barabara hii inajengwa kwa kiwango cha lami na kukamilika mapema ili kuunga mkono juhudi za wananchi wa Mbarali wanaotekeleza sera ya kilimo kwanza kwa kuzalisha mpunga na mahindi kwa wingi”, amesisitiza waziri Magufuli.
Amewataka wananchi waliojenga katika hifadhi ya barabara kupisha eneo la barabara ili kuwezesha kazi ya ujenzi huo kufanyika kwa haraka na kumalizika kwa wakati.
Amemwagiza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini TANROADS Eng. Patrick Mfugale kufanya usanifu ili kuwezesha madaraja kumudu kupitisha magari yenye uzito wa tani 40 yatakayochukua mazao katika maeneo ya Rujewa na Ubaruku.
Eng. Mfugale amesema barabara ya Igawa-Ubaruku kwa sasa ni barabara ya mkoa na ujenzi wake utazingatia vigezo vya barabara za mikoa ili kukidhi mahitaji ya uzito wa magari yatakayopita katika barabara hiyo.
Kuhusu barabara ya Igawa –Madibira yenye urefu wa KM 153 ambayo upembuzi yakinifu na usanifu wake umekamilika waziri Magufuli amesema Serikali inatafuta fedha ili kuijenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami na hivyo kuifungua kiuchumi wilaya ya Mbarali.
Amesisitiza umuhimu wa umoja,mshikamano na uaminifu kwa wananchi wa Mbarali na kuwataka vijana watakaopata kazi wakati wa ujenzi wa barabara hiyo kuwa waaminifu.
Naye mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amemshukuru Waziri wa Ujenzi kwa kuamua kujenga kwa lami barabara za Mpemba hadi Isongole wilayani Ileje ,Igawa hadi Ubaruku wilayani Mbarali na Kikyusa hadi Matema wilayani Kyela na kusisitiza barabara hizo zitakapokamilika zitaimarisha usafiri na kuibua fursa za ajira na uchumi kwa wakazi wengi wa mkoa wa Mbeya.
Imetayarishwa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Wizara ya Ujenzi.

HOTUBA YA RAIS KIKWETE KWENYE MAADHIMISHO YA MIAKA 38 YA KUZALIWA KWA CCM

$
0
0
HOTUBA YA MWENYEKITI WA CCM TAIFA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, KATIKA SHEREHE ZA KUTIMIZA MIAKA 38 YA CCM, KWENYE UWANJA WA MAJIMAJI, SONGEA - RUVUMA,
TAREHE 01 FEBRUARI, 2015
 
 Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete akihutubia umati wa wananachi

Ndugu Philip Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM;
Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda, Waziri Mkuu na mjumbe wa Kamati Kuu;
Mheshimiwa Anne Makinda, Spika wa Bunge na Mjumbe wa Kamati Kuu;
Ndugu Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM;
Ndugu Mike Mukula, Makamu Mwenyekiti wa NRM ya Uganda na ujumbe wake;
Waheshimiwa Wajumbe wa Kamati Kuu;
Mheshimiwa Oddo Mwisho, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma;
Waheshimiwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa;
Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM;
Ndugu Verena Shumbusho, Katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma;
Wenyeviti wa Jumuiya za CCM;
Viongozi, wananchama na wapenzi wa CCM;
CCM Oyee!
          Naomba nianze kwa kuwashukuru na kuwapongeza wenyeji wetu kwa mapokezi  mazuri, hususan napenda kuwatambua wananchi, viongozi na wana-CCM wa Mkoa wa Ruvuma wakiongozwa na Mwenyekiti wao ndugu Oddo Mwisho, Katibu wa Mkoa Mama Verena Shumbusho, Mkuu wa Mkoa na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Ndugu Said Mwambungu. Nawapongeza kwa maandalizi mazuri ya sherehe hizi. Hakika zimefana sana.  Hii ni mara ya pili sherehe hizi kuadhimishwa mkoani hapa.  Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1991 wakati wa kuazimisha miaka 14 ya CCM. 
 
Tunatambua kuwa mmefanya kazi kubwa ya maandalizi  mpaka mmeweza kufanikisha shughuli ya leo kwa kiwango cha juu. Waswahili wanasema “Usione vinaelea Vimeundwa”. Napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi maalum kwa Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana kwa uongozi wake makini uliowezesha mambo kuwa mazuri kiasi hiki.  Hongera sana kwa hili na kwa kazi nyingi nzuri unazofanya kwa maslahi ya Chama chetu na nchi yetu.
Leo ni siku ya furaha kwangu na kwa viongozi na wanachama wenzangu wa CCM kote nchini ya kusherehekea na kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi. Tunastahili kuisherehekea siku hii kwa nderemo na vifijo kwa sababu ya mafanikio makubwa ambayo Chama chetu kimeendelea kupata ndani ya Chama na katika kuliongoza taifa letu. Katika miaka 38 ya uhai wake Chama chetu kimezidi kuimarika na kimeendelea kuliongoza vyema taifa letu: kuna amani, utulivu na maendeleo yanayoonekana.
Tumeeendelea kuaminiwa na kutumainiwa na Watanzania. Kama ilivyothibitika na ushindi wa kishindo katika chaguzi zote tangu mfumo wa vyama vingi uanze mwaka 1995 mpaka sasa.  Hata mwaka huu itakuwa hivyo hivyo. Dalili ya mvua ni mawingu: ushindi mnono tulioupata kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni dalili tosha kwamba Oktoba, 2015 watani zetu hawana chao.
Ninaposema hivyo nawaomba wana CCM wenzangu tusibweteke tukadhani kwamba ndiyo tumekwishafika. Bado safari ndiyo kwanza tumeianza na inaweza kuwa na changamoto zake.  Lazima tufanye kazi tena kazi kubwa sana ndipo tutakapojihakikishia ushindi.  Nguvu ya ushindi inaanzia kwenye Chama.  Huu ni mwaka ambao kazi ya Chama ndani ya Chama na kazi ya Chama ndani ya umma inatakiwa ifanyike kwa nguvu zaidi na kwa ari kubwa zaidi.  Lazima tuhakikishe tunao umoja wa dhati na kwamba  wanachama wetu wanakuwa na mwamko wa hali ya juu wa kukipigania Chama katika kutafuta na kupata ushindi kwa Udiwani, Ubunge, Uwakilishi, Urais wa Zanzibar na Urais wa Muungano.
Huu ni mwaka ambao wanachama na viongozi wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanakutana mara kwa mara kwa mujibu wa Katiba na hata zaidi kuzungumzia mikakati ya kupata ushindi na kuitekeleza.  Huu ni mwaka ambao lazima tuhakikishe kuwa tunazo rasilimali na nyenzo za kutuwezesha kufanya kazi ya Chama ndani ya umma na kuwapatia ushindi wagombea wa Chama chetu.
Huu ni mwaka ambao kazi ya Jumuiya za Chama ya kukiwezesha Chama kuungwa mkono na jamii pana ya Watanzania walio vijana, wanawake na wazazi inafanyika kwa umahiri na ufanisi wa hali ya juu.
Bila ya shaka, ndugu zangu mtayakumbuka maneno niliyoyasema kwa kuyarudia kuwa “Mwisho wa uchaguzi mmoja ndiyo mwanzo wa uchaguzi mwingine”. Najua baadhi yenu mmezingatia na kuchukua hatua za kufanya maandalizi mapema ya uchaguzi wa mwaka huu mara   baada ya kumaliza uchaguzi wa mwaka 2010. Hao nawapongeza.  Lakini wapo viongozi na wanachama ambao hawajafanya chochote.  Hawa, wananisikitisha kwa athari mbaya na hatari ya kupoteza ushindi wanayokiletea Chama chetu. 
Naomba kila mmoja wetu ajipime yupo fungu gani. Kama upo kwenye kundi la kwanza lililokwishaanza maandalizi natoa pongezi nyingi.  Nawaomba muendelee kukamilisha ipasavyo. Kwa wale ambao wapo kundi la wale ambao maandalizi yao ni ya kiwango kidogo au hawajaanza kabisa lazima waanze na wakati ni huu.  Usikawie, unatakiwa kufanya kazi kwa ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi kama ilivyo kauli mbiu ya CCM. Yapo mambo kadhaa ya kufanya ambayo tulikwishaambiana tufanye.  Miongoni mwao ni lile agizo la kutaka kila ngazi ya Chama na hasa Wilaya na Mikoa kuwa na Mfuko wa Uchaguzi. Wakati wake ndio huu sasa wa mfuko huo kufanya kazi iliyokusudiwa.  Naomba tujiulize wangapi wanayo mifuko hiyo na wangapi hawana.  Kwa wale walionayo wahakikishe ina rasilimali za kutosha.  Kama hazitoshi waweke mikakati ya kuitunisha mifuko hiyo.  Kwa wale ambao hawajaanzisha wachune bongo kuhusu namna ya kupata fedha za kuendeshea shughuli za uchaguzi. Sina budi kuwatahadharisha kuwa msichukue fedha ambazo zitazua matatizo.


Ndugu viongozi na ndugu wanachama;
Huu ni mwaka wa kutambua ahadi zipi tulizotoa zimetimizwa na zipi bado.  Kwa zile ambazo hazijakamilika wajibu wetu ni kuweka mikakati ya kuzikamilisha.  Kwa zile ambazo hazitakamilika tutafute maelezo sahihi ya kutoa kwa wadau wa huduma hiyo.  Naamini hazitakuwa nyingi za kuchosha. Mwaka huu siyo mzuri kwenda na madeni lukuki ya ahadi.  Yanaweza kutupunguzia ushindi wetu.
Huu ni mwaka wa kuongeza ukubwa wa jeshi letu la ushindi kwa kuongeza wananchama wapya. Natambua tatizo la upungufu wa kadi lakini najua mipango thabiti iliyopo ya kuleta kadi nyingi za kutosha wale waliopo nje. Tujiepushe na kuingiza mamluki hivyo taratibu za kuingiza wanachama zizingatiwe ipasavyo.
Ndugu Viongozi;
Ndugu Wananchi;
Jambo lingine kubwa na muhimu sana kufanya mwaka huu ni kuwatembelea wanachama na wananchi na kuzungumza nao. Hatujaifanya vizuri sana kazi hii lakini hatujachelewa.  Sina budi kutoa pongezi maalum kwa Katibu Mkuu wa CCM kwa ufanisi mkubwa aliopata kwa jambo hili.  Sote hatuna budi kuiga mfano wake mzuri.  Tuache kukaa maofisini tutoke kuzungumza na watu kuwashawishi waunge mkono na kuipigia kura CCM katika uchaguzi ujao. Kila Ofisi ya Mkoa na kila Ofisi ya Wilaya inalo gari la kuwawezesha kufanya kazi hiyo. Tafadhali fanyeni hivyo, kwani bila ya kufanya hivyo hakuna uhakika wa kupata ushindi.  Kilichobakia kwa upande wetu ni kutafuta vipando kwa Ofisi za Kata na Matawi. Tusaidiane pale inapowezekana.



Uandikishaji wa Wapiga Kura
Ndugu wana CCM na ndugu Wananchi;
          Jambo lingine muhimu katika kutafuta ushindi ni kupatikana kwa wapiga kura.  Chama chetu kama vilivyo vyama vingine, hatuna budi kuwahimiza wanachama wetu, wapenzi wetu na wananchi wengine wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kupiga kura.  Mwaka huu wenye kadi mpya za mpiga kura ndiyo watakaoruhusiwa kupiga kura katika uchaguzi mkuu na katika kura ya maoni kuhusu Katiba Inayopendekezwa.
Asiyejiandikisha hatapata fursa ya kushiriki kura ya maoni na uchaguzi mkuu.  Kwa sababu hiyo nawaomba viongozi na wanachama wa CCM wawe ndiyo wa kwanza kujitokeza kujiandisha.  Pia wawe mstari wa mbele kuwahimiza wananchi wengine kujiandikisha.  Nawaomba jambo hili mlipe uzito mkubwa kwani safari ya kutafuta na kupata ushindi inaanzie kwenye kupata wapiga kura hususani wapiga kura wanaounga mkono Chama chetu na wagombea wetu.
Kura ya Maoni
Ndugu wananchi;
          Kama mjuavyo, jambo kubwa lililo mbele yetu ni kura ya maoni kuhusu Katiba Inayopendezwa itakayofanyika tarehe 30 Aprili, 2015. Maandalizi yote husika yanaendelea kufanyika ili kuwezesha kura hiyo kutekelezwa kama ilivyopangwa. Kama nilivyokwishaeleza hivi punde uandikishaji wa wapiga kura ni miongoni ma maandalizi hayo. Mengine ni uchapishaji na usambazaji wa Katiba Inayopendekezwa.
Yapo mambo kadhaa ambayo nawasihi viongozi na wanachama wenzangu mfuatilie kwa karibu ili yasiwapite. Yale tunayoyajua tuwaambie. Miongoni mwa mambo muhimu sana ambayo Chama hakina budi kujipanga vizuri ni kuhusu kutoa elimu kwa umma kuhusu Katiba Inayopendekezwa na kampeni ya Kura ya Maoni. Watani zetu watatoa elimu hasi kuhusu  Katiba Inayopendekezwa, sisi tutoe elimu chanya. Wenzetu watataka Katiba Inayopendekezwa  isipite. Sisi tupige kampeni ikubalike.  Nilisema siku ileDodoma wakati wa kukabidhiwa Katiba Inayopendekezwa na narudia tena leo kwambaKatiba Inayopendekezwa imebeba maslahi mapana ya taifa letu. Hatujawahi kuwa na Katiba kama hii Inayopendekezwa.  Misingi ya historia ya nchi yetu yaani kule tulikotoka, tulipo sasa na tuendako imezingatiwa vizuri. Katiba hiyo inatambua maslahi ya makundi yote nchini na kuyawekea utaratibu mzuri wa kutekelezwa. Wakulima, wafugaji, wavuvi, wanawake, vijana, wasanii, wafanyakazi, wazee na watoto wametambuliwa kwa kina na upana zaidi kuliko Katiba ya sasa. 
Katiba Inayopendekezwa imeshughulikia kero za Muungano na kujenga mazingira bora zaidi kwa Muungano wetu kuimarika. Yale mambo yaliyokuwa yanaikwaza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuukwaza Muungano yamepatiwa ufumbuzi mwafaka. Sasa Zanzibar itaendesha na kushughulikia mambo yake kwa uhuru mkubwa zaidi.
Ndugu wananchi;
          Kwa maoni yangu sioni sababu ya kuikataa Katiba Inayopendekezwa. Hatuna budi kutambua kuwa tukiikataa Katiba Inayopendekezwa, Katiba ya sasa itaendelea kutumika mpaka hapo mchakato mwingine utakapomalizika miaka mingi ijayo. Viongozi wa vyama vinne vya siasa wamesikika wakisema watasusia kushiriki katika kura ya maoni na kuwataka wanachama wao wasishiriki. Kauli hiyo imenisikitisha sana ingawaje haikunishangaza hasa tukikumbuka waliyoyafanya wakati wa Bunge la Katiba. Mimi nawaomba washiriki.
Nawasihi wananchi wasiwasikilize. Wao wakitaka kususia waacheni wasusie lakini nyie jitokezeni kupiga kura.  Nawasihi msikubali kupoteza mema mengi yaliyo katika Katiba Inayopendekezwa ati kwa sababu tu hakuna Serikali Tatu walizokuwa wanazitaka. Kama kweli wananchi wa Tanzania wanakereketwa na Serikali Tatu watathibitisha hiyo kwenye kura ya maoni.
Naomba msibabaishwe wala kudanganywa na watu wanaotaka kuturudisha nyuma kutoka katika hatua kubwa muhimu tutakazopiga kwa kuikubali Katiba Inayopendekezwa. Tusikubali kubaki nyuma.
Uchaguzi Mkuu
Ndugu wananchi;
          Kama mjuavyo mwezi Oktoba, 2015 nchi yetu itafanya uchaguzi mkuu wa Madiwani, Wabunge, Wawakilishi, Rais wa Zanzibar na Rais wa Jamhuri ya Muungano. Uchaguzi wa mwaka huu ni wa kihistoria kwa nchi yetu kwani tunachagua Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mimi nataka Rais huyo awe mwana CCM.  Sisi sote katika CCM tunataka Rais atoke katika Chama chetu  kwa sababu kama alivyousia Baba Wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere “Rais wa nchi yetu anaweza  kutoka Chama chochote lakini Rais bora atatoka CCM”.
Huu ni usia mzito wenye maono ya mbali.  Tusiupuuze wosia huu bali tuuenzi.  Sisi katika Chama cha Mapinduzi tuwe mstari wa mbele katika kuuenzi wosia huu kwa kupata mgombea aliye bora wa kupeperusha bendera ya CCM  katika uchaguzi ujao. Mgombea ambaye wananchi wakisikia jina lake likitajwa watasema naam, hapo sawa, hapo barabara.  Lakini tukiteua mgombea ambaye watu wataguna na kusema hata huyu? Tutakuwa tumemuangusha  Muasisi wa Chama chetu na taifa letu katika wosia wake. Bila shaka laana yake tutaipata. Na hilo likitokea itakuwa hasara kubwa kwa taifa letu na msiba kwa CCM.  Nchi itayumba.
Lazima tuhakikishe kuwa hatutafika huko.  Watu wazuri wapo wa kutosha katika CCM na naamini  tunawajua. Kama hawajajitokeza tuwashawishi wafanye hivyo. Ndugu zangu, tusifanye ajizi katika jambo hili kubwa na la msingi kwa Chama chetu.  Kushinda chaguzi za dola katika sehemu zetu mbili za Muungano ndiyo madhumuni makuu ya kuundwa na kuwepo kwa CCM.      
          Napenda kuwahakikishia wanachama wa CCM na wananchi kuwa, Chama cha Mapinduzi ni Chama kilichokomaa, kilicho makini na imara. Tunao utaratibu  unaoeleweka na kutabirika wa kuwapata wagombea. Inazo kanuni na vigezo vya wazi vya kuwapata viongozi walio bora, na tunavyo vikao rasmi vya kuchuja na kuteua wagombea kwa kuzingatia kanuni, taratibu na maadili ya Chama chetu. Hivyo basi, hapataharibika jambo.
Naomba niwahakikishie kwamba CCM itawapatia Watanzania wagombea bora ambao hawatawapa wananchi mashaka wala kigugumizi cha kuwachagua.  Tutafanya hivyo kwa nafasi ya Rais wa Muungano, Rais wa Zanzibar, Wabunge, Wawakilishi na Madiwani. Nawaomba wagombea wazingatie na kuheshimu masharti ya Katiba ya Chama, Kanuni na Madili ya uteuzi kwa wanaotaka kuteuliwa kugombea nafasi katika chaguzi za dola. Asiyezingatia hayo asije akakilaumu Chama bali ajilaumu mwenyewe kwa makosa aliyoyafanya.
Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa CCM
Ndugu wananchi;
          Miezi minne iliyopita nilifanya ziara ya mkoa huu wa Ruvuma kukagua shughuli za maendeleo.  Nimefurahishwa sana na jitihada za kujiletea maendeleo zinazofanywa na wananchi wa mkoa huu na mafanikio mnayoendelea kuyapata. Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na mipango mbalimbali ya serikali unakwenda vizuri, kiasi cha kuwastajabisha hata wale waliokuwa na mashaka na wasio tutakia mema.
Yako mambo mengi tuliyoahidi kufanya ambayo tumeyakamilisha na mengine utekelezaji wake unaendelea vizuri. Kilio cha miaka mingi cha wananchi wa mkoa huu kuhusu barabara kimefanyiwa kazi vya kutosha. Ujenzi wa barabara ya Namtumbo – Songea na  Peramiho - Mbinga kwa kiwango cha lami umekamilika. Tunaendelea na ujenzi wa barabara ya Namtumbo – Tunduru na Tunduru – Mangaka ili kuunganisha mkoa wa Mtwara na Ruvuma kwa barabara za lami. Aidha, mipango ya kujenga barabara ya Mbinga – Mbambabay kwa mkopo wa Benki ya Maendeleo ya Afrika imefikia mahali pazuri.  Kwa upande wa usafiri katika Ziwa Nyasa hivi sasa mchakato wa ujenzi wa chelezo cha kujengea meli ya ziwa hilo kule kwenye bandari ya Itungi, Kyela unaendelea vizuri. Ujenzi wa chelezo ukishakamilika ujenzi wa meli utaanza.
Kwa upande wa umeme tunaendelea na ujenzi wa njia ya umeme ya msongo wa Kv 220 kutoka Makambako kuja Songea na hadi Mbinga na Namtumbo.  Ujenzi wa njia hii ya umeme utakapokamilika utawahakikishia wakazi wa mji wa Songea na mkoa wa Ruvuma umeme wa uhakika. Tumechelewa kidogo kwa sababu ya kubadilisha ukubwa wa njia kutoka msongo wa Kv 132 tuliyotaka kujenga awali hadi Kv 220. Aidha, usambazaji wa umeme vijijini unaendelea kwa kasi katika maeneo yote nchini. Tunataka ifikapo June, 2015 zaidi ya vijiji 5,336 viwe vimepatiwa umeme. Kati ya vijiji hivyo zaidi ya vijiji 300 ni vya mkoa wa Ruvuma. Haya ni mafanikio makubwa na ya kutia moyo.
Kuhusu sekta ya Afya nako pia tumepata mafanikio makubwa katika utoaji wa huduma ya afya kwa Watanzania. Kwa hapa Songea nimekwishatoa maelekezo kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuanza mchakato wa ujenzi wa hospitali mpya ya Mkoa wa Ruvuma na hii iliyopo sasa iwe ni hospitali ya Manispaa ya Mji wa Songea. Halmashauri ya Manispaa ya Songea iharakishe kutenga eneo la kutosha kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo ya mkoa ambayo itakuwa ni ya rufaa kwa yale ambayo hospitali za Wilaya zitashindwa kumudu.
Haya ni maeneo machache tu ambayo yanaonyesha hatua kubwa tuliyopiga katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi na maendeleo ya mkoa huu. Ukweli ni kwamba Ruvuma ya miaka 10 iliyopita siyo Ruvuma ya leo. Ninyi nyote ni mashahidi wa mambo haya. Mwenye macho haambiwi tazama.
Ndugu wananchi;
Jambo la mwisho ambalo napenda kulizungumzia ambalo nilishalizungumzia kwenye hotuba yangu ya mwaka mpya inahusu ununuzi wa mazao ya wakulima. Nilieleza siku ile kuwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ilikuwa bado haijalipa shilingi bilioni 89 kwa wakulima kwa mazao yao iliyonunua. Nilielezea kutokufurahishwa  kwangu na hali hiyo na kuagiza Wakala kulipa deni hilo. 
Nimeambiwa kuwa tayari shilingi bilioni 15 zimeshatolewa na hapa Ruvuma mmepata shilingi bilioni 8.  Hivi karibuni shilingi bilioni 36 zitatolewa na kubaki shilingi bilioni 38 ambazo zitalipwa mwezi Machi.
Jambo lingine ambalo tunaendelea nalo kulishughuikia katika Serikali ni kupata masoko mengine kwa mazao ya wakulima.  Kama nilivyosema NFRA haiwezi kununua mazao yote ya wakulima nchini. Uwezo wake ni kuhifadhi tani 240,000 wakati uzalishaji wa mahindi hapa Ruvuma ni tani 993,350.  Hata kama NFRA ingeamua kununua mahindi yote kutoka mkoa wa Ruvuma peke yake isingeweza kuyamaliza.
Nimewaagiza viongozi wa mkoa wa Ruvuma  na mikoa yote nchini washirikiane na Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika na Wizara ya Viwanda na Biashara kutafuta masoko mengi kwa ajili ya mahindi, mpunga na mtama wa wakulima ndani na nje ya nchi.
Tunakokwenda
Ndugu wana CCM;
          Mafanikio ya miaka 38 ya Chama chetu yasitufanye tubweteke. Bado tunayo kazi kubwa mbele yetu.  Ili tuendelee kuongoza dola hatuna budi tuendelee kuwa tumaini na kimbilio la wananchi wetu. Inatupasa kuwa waaminifu kwa ahadi zetu na watiifu kwa matakwa yao.  Kubwa sana, tunatakiwa tuwe tayari wakati wote kubadilika na kwenda na wakati. Tunaweza kufanya hivyo ikiwa tutaendelea kukuza demokrasia ndani ya Chama chetu na kuruhusu na kuvumilia tofauti za mitazamo.  Hiyo ndiyo siri ya uhai wa CCM ambayo hatuna budi kuendeleza.
          Tunapoanza safari ya kuelekea mwaka wa 39, hatuna budi sasa kuelekeza nguvu zetu kwenye kuondoa utegemezi wa kifedha kutoka kwenye ruzuku na michango ya wafanyabiashara.  Kutegemea misaada na michango si mambo endelevu na huo hauwezi kuwa ni mkakati wa kutumainiwa wa kuimarisha Chama chetu.  Wakati mwingine michango hii imetugharimu ndani ya Chama chetu.  Lazima tuwe wabunifu katika kutafuta vyanzo vya mapato ikiwa ni pamoja na rasilimali zetu nyingi tulizonazo ili kuwezesha Chama kujitegemea. Tayari yako mawazo yaliyoibuliwa kutokana na kazi nzuri ya Kamati iliyoongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu na Mweka Hazina wetu Mheshimiwa Zakhia Meghji tumeagiza yatekelezwe. Naomba mtimize ipasavyo wajibu wenu.
Hitimisho
Ndugu wana CCM;
          Leo ni siku ya furaha kwetu sote. Wakati tukisherehekea mafanikio yetu tuwakumbuke pia waasisi wetu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliyekuwa Mwenyeti wa TANU na Ndugu Sheikh Aboud Jumbe aliyekuwa Mwenyekiti wa ASP kwa busara, hekima na uamuzi wao uliotukuka uliowezesha kuzaliwa kwa CCM.  Tunawakumbuka pia wale wote waliotangulia mbele ya haki ambao walijitoa maisha yao kujenga CCM.  Hatuna budi kuwaenzi kwa kutoa  mchango mkubwa zaidi mwaka ujao na miaka mingi ijayo. Tuhakikishe kuwa tunaimarisha Chama chetu na kutenda mema kwa ajili ya nchi yetu na watu wake. Hili linawezekana ikiwa kila mtu atatimiza wajibu wake. Kidumu Chama cha Mapinduzi!
Asanteni sana kwa kunisikiliza.

JUMUIYA YA BLUE HEALTH ZANZIBAR YATOA TAALUMA KWA WANAFUNZI WA MASOMO YA SAYANSI KUHUSU KENSA.

$
0
0
 Docta Aboubakar kutoka Blue Health Organisation,  akiwaeleza wanafunzi wa  masomo ya Sayansi wa Skuli za Sekondari walioshiriki semina ya  kutoa taaluma juu ya maradhi ya Kensa iliyofanyika Skuli ya sekondari Haillesselassie, Mjini Zanzibar.
 Rais wa Blue Health Organisation Gora Faki Haji akiwaeleza wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi pamoja na walimu wao tatizo la maradhi ya Kensa Tanzania katika semina iliyofanyika Skuli ya Haillesselassie. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
 Baadhi ya viongozi wa Blue Health Organisation wakifuatilia kwa karibu watoa mada katika semina ya kutoa taaluma ya maradhi ya Kensa iliyofanyika Skuli ya Haillesselassie.
 Picha ya pamoja ya viongozi wa Blue Health Organisation na baadhi ya walimu wa masomo ya Sayansi walioshiriki semina ya taaluma ya maradhi ya Kensa katika Skuli ys Sekondari Haillesselassie.(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).


Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar  .
              
Wanafunzi  wa skuli za sekondari wanaosoma masomo ya Sayansi na walimu wao Tanzania wamesisitizwa kuongeza juhudi katika  masomo yao  na kufanya tafiti zitakazosaidia kugundua matatizo ya afya yanayoikabili nchi hivi sasa ikiwemo maradhi ya Kensa.

Rais wa Jumuiya ya wataalamu wa fani mbali mbali za Afya Zanzibar yenye lengo la kutoa taaluma ya maradhi tofauti kwa wananchi (Blue Health Organisation) Gora Faki Haji ametoa ushauri huo katika semina ya  kuelimisha tatizo la maradhi ya Kensa iliyowashirikisha baadhi ya wanafunzi wa  masomo ya Sayansi wa skuli za sekondari katika skuli ya Haillesselassie.

Amewaeleza wanafunzi hao kwamba  Kensa ni miongoni mwa maradhi hatari yanayosumbua wananchi wengi Tanzania na idadi kubwa ya watu wanaopata maradhi hayo hupoteza maisha.

“Takwimu  za maradhi ya Kensa  kutoka Hospitali ya Ocean Road, inayoshughulikia maradhi hayo, zinaonyesha kuwa  asilimia 14 tu ya watu waliopata Kensa  waliweza kupona,” alisema Gora Faki Haji.

Rais  huyo wa Blue Health Organisation omeongeza kuwa asilimia 66 ya wagonjwa wa kensa  waliofika  Ocean Road  kupatiwa matibabu ni wanawake na asilimia 24 ndio wanaume na hiyo inaonyesha wanawake  wanaosumbuliwa zaidi na maradhi hayo.

Amesema pamoja na kuwa hakuna sababu  rasmi inayopelekea  kupata kensa moja kwa moja lakini amesema matumizi ya bidhaa zinazotokana na tumbaku, utumiaji wa pombe na mpangalio usioridhisha wa chakula unachangia kupata tatizo la maradhi hayo. Amewataka wananchi kujiepusha na viashiria  vinavyoweza kupelekea kupata kensa na kuwa na utaratibu mzuri wa chakula ikiwemo kutumia zaidi matunda na  mboga za majani.

Amewashauri watu kujenga tabia ya kufanya uchunguzi wa afya zao mara kwa mara na kuwa na  tahadhari  wanapopata tatizo la mivimbe katika miili yao.

Amewahakikishia wananchi  kuwa Blue Health Organisation itaendeleza lengo la kutoa taaluma  ya masuala ya afya kwa makundi tofauti  ili waweze kujua sababu zinazopelekea maradhi na njia za kujiepusha nayo.

Semina hiyo iliwashirikisha wanafunzi wa skuli za Sekondari Lumumba, Benbella, Hamamni na baadhi ya walimu wa skuli hizo wanaosomesha masomo ya Sayansi.
                                               mwisho
 IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

MWANAHABARI FRANK KIBIKI AENDELEA KUCHASHA FEDHA ZA KUCHULIA FOMU YA UBUNGE JIMBO LA IRINGA

$
0
0
Kibiki akibadilishana mawazo na mmoja wa wanachama wa tujiwezeshe cha kituo kikuu cha mabasi mjini Iringa
Katibu wa kikundi cha tujiwezeshe chenye wanachama zaidi ya 560, wa kituo kikuu cha mabasi mjini Iringa Manet Charles akizungumza baada ya kumkabidhi sh 110,000 mwanachama mwenzao Frank Kibiki, ambaye ni mwanahabari baada ya kutangaza nia wa kuomba kuwania ubunge wa jimbo la Iringa mjini kupitia CCM.
Kibiki mwenye koti jeusi, akiwashukuru viongozi wa tujiwezeshe kwa msaada huo, na kuomba wavumilie muda ufike kwani fedha hiyo ataitunza

NA FREDY MGUNDA, IRINGA

NYOTA ya mwandishi wa Habari wa gazeti la Uhuru, Frank Kibiki ambaye hivi karibuni alitangaza nia ya kuwania ubunge katika jimbo la Iringa mjini, endapo chama chake cha CCM kitampitisha imeendelea kuwaka baada ya vijana wa stendi kuu ya mabasi mjini Iringa, kumchangia fedha, kwa ajili ya kuchukulia fomu wakati ukifika.

Vijana hao wamesema wameamua kuchangishana fedha ili kufanikisha zoezi la Mwandishi huyo kuchukua fomu, wakiamini ni mwenzao.

Kibiki amechangiwa fedha hizo, ikiwa ni siku chache tu zimepita, tangu wasanii wa muziki wa kizazi kipya manispaa ya Iringa wakiongozwa na ‘One lee’kumkabidhi zawadi ya wimbo ambao, tayari umeanza kusikika kwenye vituo mbalimbali vya redio mjini humo.

Kiongozi wa vijana hao, Maneti Charles alisema ni wakati wa kijana wa kawaida, kutoka miongoni mwao kuongoza jimbo la Iringa mjini na kuitaka CCM manispaa ya Iringa, ihakikishe inampitisha mtu anayekubalika kwa jamii.

Amesema mpaka sasa wamefikisha kiasi cha Sh 110,000 ambazo wamemkabidhi wakitaka azitunze mpaka wakati wa kuchukua fomu ukifika.

“Kibiki ni mwenzetu, siku zote tumekuwa tukishinda naye na tunaujua uwezo wake, tumechangishana fedha mwenye mia moja, miambili, miatano ili tumsaidia wakati ukifika tumchukulie fomu.” Alisema.

Tangu kutangaza nia, Kibiki ambaye ni Mjumbe wa Mkutano mkuu wa CCM taifa, na Katibu mwandamizi wa UVCCM kwa miaka zaidi ya miaka 10, anadaiwa kuharibu upepo wa vigogo wa chama hicho ambao walikuwa wakitajwa kunyemelea jimbo la Iringa mjini.

Vijana hao, wamemtaka Kibiki kutoogopa wala kukata tamaa badala yake, wao watamsemea mahali popote wakidai kuwa sifa kuu ya kiongozi ni kukubalika kwa watu wa riza zote na kushirikiana na wananchi bila kujali matabaka yao.

“Tunamkubali kaka, wala asiogope sisi ndio tutakuwa mbele yake, tunachotaka ubunge urejee kwetu sisi wana Iringa wenye ubunge kwani huu ni utumishi ambao sisi ndio tunaowatuma hawa wabunge,”alisema Enos Mgala, muuza pipi wa kituo cha mabasi, Iringa mjini.

Jimbo la Iringa mjini ni mionngoni mwa majimbo yenye upinzani mkali, tangu Mbunge wa jimbo hilo, Mchungaji Peter Msigwa(chadema), alipolipokonya kutoka kwa wapinzani wake chama cha mapinduzi (CCM).

Benki ya CRDB na kampuni ya Bima ya Heritage zanyakua tuzo za BBLA 2014

$
0
0

 Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Charles Kitwanga, (Kushoto) akimkabidhi tuzo mshindi wa Tuzo za Bodi yenye Uongozi Bora za 2014 (BBLA) katika sekta ya kibenki, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB Bw. Martin Mmari (kulia). Benki ya CRDB iliibuka mshindi katika sekta ya kibenki wakati kampuni ya Heritage Insurance iliibuka kinara katika sekta ya bima katika tuzo hizo zilizofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Charles Kitwanga, (Kushoto) akimkabidhi tuzo mshindi wa Tuzo za Bodi yenye Uongozi Bora za 2014 (BBLA) katika sekta ya bima, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya kampuni ya Heritage Insurance, Bw. Yogesh Manek (kulia). Heritage Insurance iliibuka mshindi katika sekta ya bima wakati Benki ya CRDB iliibuka kinara katika sekta ya kibenki katika tuzo hizo zilizofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Mwenyekiti wa jopo la majaji waliosimamia Tuzo za Bodi yenye Uongozi Bora za 2014 (BBLA), Bw. Leonard Mususa akizungumza katika hafla ya kutangaza washindi wa tuzo hizo ambapo kampuni ya bima ya. Heritage iliibuka mshindi katika sekta ya bima wakati Benki ya CRDB iliibuka kinara katika sekta ya kibenki katika tuzo hizo zilizofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Charles Kitwanga akizungumza katika hafla ya kutangaza washindi wa Tuzo za Bodi yenye Uongozi Bora za 2014 (BBLA), ambapo kampuni ya bima ya. Heritage iliibuka mshindi katika sekta ya bima wakati Benki ya CRDB iliibuka kinara katika sekta ya kibenki katika tuzo hizo zilizofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

=========  ========  ========
Benki ya CRDB pamoja na kampuni ya Bima ya Heritage mwishoni mwa wiki zilifanikiwa kuibuka washindi wa tuzo za bodi bora katika sekta ya fedha kwa mwaka 2014 tukio lililofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Benki ya CRDB ilifanikiwa kutwaa tuzo hiyo dhidi ya benki ya Exim iliyofanikiwa kuwa mshindi wa pili huku benki ya Posta (TPB) nayo ikiibuka mshindi wa tatu katika tuzo hizo zilizofanyika kwa mara ya kwanza hapa nchini.

Kwa upande wa makampuni ya Bima, Kampuni ya Bima ya Alliance Insurance Corporation ilifanikiwa kutwaa tuzo hiyo baada ya kuibuka mshindi wa kwanza huku ikifuatiwa na kampuni za Alliance Insurance Corporation, Alliance Life Assurance pamoja na Strategies Insurance (T) Limited kwa mtiririko mahususi.

Akizungumzia mchakato mzima wa kupatikana kwa washindi hao, Mwenyekiti wa timu ya majaji wa tuzo hizo Bw. Leonard Mususa alisema, jopo lake liliundwa na watu wenye uzoefu mkubwa katika masuala ya uongozi katika sekta za fedha akiwamo Mkaguzi mkuu na mdhibiti wa hesabu za serikali (CAG) aliyestaafu, Bw Ludovick Utouh.

Wengine ni pamoja na Bw. Mwaremi Marwa, (Mkurugenzi Mkuu wa soko la Hisa la Dar es Salaam( DSE), Bw. Yona Killaghane (Mkurugenzi mkuu mstaafu wa shirika la maendeleo la Petroli nchini (TPDC).

Aidha akizungumza kwenye hafla hiyo Mwenyeki wa taasisi ya sekta binafsi (TPSF), na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dr Reginald Mengi alisema tuzo zimekuja wakati muafaka kwa kuwa sekta za fedha na Bima nchini zinapitia mabadiliko makubwa ya kimaendeleo.

Awali akizungumza kwenye hafla hiyo, mratibu wa tuzo hizo Bi Neema Gelard alisema tuzo hizo zitatoa mwanga zaidi kuhusuana na namna jinsi bodi bora katika sekta za fedha na bima hapa nchini zinatakiwa kujiendesha.

Zaidi Bi Neema aliwashukuru wadhamini wa tuzo hizo ambao ni kampuni za Capital Plus International (CPI), IPP Media, Real PR Solutions Limited, Afrimax Strategic Partnerships Limited, Serena Hotel, Fix Agency Ltd, Lilacnshades na Excel Management and Outsourcing.

Aidha akizungumza kwenye hafla hiyo naibu waziri wa nishati na makini Bw Charles Kitwanga alitoa wito kwa taaisisi nyingine za fedha na mashirika ya bima kujitokeza na kushiriki katika tuzo zijazo.

''Wakati nawashukuru waandaaji wa tuzo hizi kwa kuja na wazo hili lenye tija kubwa kwa taifa... Naomba nitoe wito kwa bodi za mifuko yetu ya jamii pia ziangalie uwezekano wa kushiriki kwenye tuzo hizi kwa manufaa ya wanachama wa mifuko hiyo''alisema Mhe. Kitwanga.

Temeke mabingwa Wa Proin Women Taifa Cup mara baada ya kuifunga Pwani katika fainali

$
0
0
Waziri wa habari utamaduni na Michezo, Mh Dkt Fenella Mukangara akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya Temeke mara baada ya kuibuka washindi wa Mashindano ya Proin Women Taifa Cup ambayo yalichezwa katika Dimba la Azam huku Proin Promotions na Azam wakidhamini mashindano hayo.
Nahodha wa Timu ya Pwani akipokea Mfano wa hundi ya Shilingi Milioni Mbili ambazo ni zawadi ya Mshindi wa pili katika Mashindano ya Proin Women Taifa Cup na kuwamalizika kwa Temeke kuwa Mabingwa kwa kuifunga Pwani goli 1 kwa 0.
Nahodha wa Timu ya Ilala ambao ni washindi wa tatu akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi Milioni 1 ambayo mshindi wa tatu katika Mashindano hayo ni Ilala
Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara (wa kwanza kulia) na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF Jamal Malinzi wakishuhudia fainali ya Mashindano ya Proin Women Taifa Cup mechi iliyochezwa katika dimba la Azam Complex kwa kuzikutanisha timu za Pwani na Temeke na Temeke Kuibuka Bingwa wa Proin Women Taifa Cup kwa kuichapa Pwani goli 1 kwa 0.

Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo, Mh Dkt Femella Mukangara (wa pili kushoto) akiwasili katika uwanja wa Azam Complex Chamanzi wakati wa fainali ya Mashindano ya Proin Women Taifa Cup yaliyofikia Tamati leo kwa kuzikutanisha Timu za Temeke na Pwani.

Kikosi cha Timu ya Pwani
Kikosi cha Timu ya Temeke ambacho kimeifunga Kikosi cha Timu ya Pwani kwa goli 1 kwa 0 katika Mchezo wa Fainali ya Mashindano ya Proin Women Taifa Cup, mchezo uliomalizika kwa Temeke kuibuka mabingwa wa Proin Women Taifa Cup katika Dimba la Azam Complex
 Waziri Mukangala akisalimiana na timu ya Temeke pamoja na timu ya Pwani kabla ya Mechi ya Fainali ya Proin Women Taifa Cup kuanza katika dimba la Chamanzi Complex. Temeke iliibuka Mshindi kwa kuifunga Pwani Goli 1 kwa 0
Hatari langoni mwa timu ya Pwani
 Wakichuana vikali
Wachezaji wa timu ya temeke wakishangilia goli lililofungwa katika kipindi cha Kwanza cha Mchezo na kupelekea kudumu kwa dakika tisini na kuwapa ubingwa temeke.
 Mashabiki waliojitokeza kushuhudia mtanange huo 
 Mlinda mlango wa timu ya Temeke akiokoa moja ya hatari iliyopelekwa katika lango lake
 
 Wachezaji wa Pwani wakisikitika kwa kufungwa na Temeke
Picha zote na Josephat Lukaza - Lukaza Blog

RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA PILI, ALI HASSAN MWINYI AZINDUA MAADHIMISHO YA WIKI YA SHERIA NCHINI

$
0
0
 -Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (wa pili kushoto) akiongozana na jaji mkuu wa Tanzania, Mohamed Othaman Chande  (watatu kushoto) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki (wa kwanza kushoto), Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu,Shabani Ally LILA  wakiwa katika matembezi ya kuadhimisha wiki ya sheria nchini matembezi hayo yalianzia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuishia katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam February 1, 2015.
 Bendi ya polisi ikiongoza matembezi ya wiki ya sheria nchini.
 Watumishi wa Mahakama nchini pamoja na watumishi wa taasisi zingine wakiwa wakiwa katika matembezi ya kuadhimisha wiki ya sheria nchini matembezi hayo yalianzia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuishia katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam February 1, 2015.

 Matembezi yakiwasili katika uwanja wa mnazi mmoja.
 Vijana kutoka katika vikundi mbali mbali wakitoa burudani wakati wa kuadhimisha wiki ya sheria nchini.
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (wa kwanza kushoto),akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bw. Michael Mhando kuhusiana huduma wanazotoa NHF alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho ya kuadhimisha wiki ya sheria nchini (kushoto katikati), jaji mkuu wa Tanzania, Mohamed Othaman Chande, na kulia Meneja Masoko na Elimu kwa Umma NHF, Bi. Anjela Mziray.
 Wtumishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),wakiendelea kutoa elimu kwa washiriki wa maonesho hayo namna ya kujiunga na NHIF (wakwanza kulia),  Afisa Masoko na Elimu kwa Umma wa NHIF, Bi. Catherine Kameka, na katikati  Afisa Masoko na Elimu kwa Umma NHIF, Bi Hawa Duguza.
 Washiriki wa maonesho hayo wakipata huduma mbalimbali kutoka kwenye banda la NHIF.
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi akimsikiliza Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa, Bi. Zahra Maruma juu ya huduma zinazotolewa alipotembelea banda hilo (wa kwanza kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki.
  jaji mkuu wa Tanzania, Mohamed Othaman Chande akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi kuzindua wiki ya sheria nchini yanayofanyika katika uwanja wa mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi akitoa hotuba yake wakati akizindua wiki ya sheria nchini katika uwanja wa mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi pamoja na Majaji waliokaa mbele wakiwa kwenye picha ya pamoja na wakuu wa taasisi mbalimbali zilizoshiriki katika wiki ya sheria nchini.

Rais Mstaafu wa awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi ameitaka jamii kuacha kuchukua sheria mkononi na badala yake waviache vyombo vya dola vifanye kazi yao kwa mujibu wa sheria kwani kufanya hivyo ni jambo la dhuluma na aibu.
 
Aliyasema hayo February 1, 2014 jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakati akizindua maadhimisho ya wiki ya sheria nchini ambapo kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni "Fursa ya kupata haki: wajibu wa serikali,mahakama na wadau."
 
Alisema kuwa katiba Ibara ya 107 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzanuia inae lekezakuwa mahakama ndio muhimili pekee uliopewa jukumu na dhamana ya kuwafikishia haki.
 
"ili Mahakama kutekeleza majukumu hayo lazima wananchi wajengewe uelewa juu ya shughuli za mahakama zinavyoendeshwa na hilo ndio lengo la maadhimisho haya,"Alisema Mwinyi
Aliongeza kuwa ni vema wananchi wakajijengea utaratibu wa kuisadia mahakama pindi panapo hitajika ushahidi ili kuepuka kuachiliwa huru kwa wahalifu wao kwa kukosa ushahidi wa kutosha.

Alisema kuwa sheria pia inahitaji Majaji na Mahakimu watoe haki kwa kuzingatia sheria hivyo ni wajibu wa wananchi na jamii nzima kushirikiana na  mahakama kupata haki halali kwa watuhumiwa wetu.Kwaupande wake Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman alisema kuwa mahakama imedhamiria kutoa elimu kwa ummma kuhusu masuala mbalimbali ya kimahakama.
 
Alisema kuwa wamejipanga katika kutoa elimu kuhusu ufunguaji na uendeshaji wa mashauri mbalimbali,utatuzi wa migogoro kwa njia ya suluhu muafaka pamoja na mfumo mpya wa kulipa tozo za mahakama kwa njia ya benki. "kwa mara ya kwanza mahakama ya tanzania imeamua kushirikisha jamii katika kujifunza jinjsi utendaji kazi wa mahakama unavyofanya kazi ni matumaini yetu kuwa jamii itajifunza vyema na kutii sheria za nchi"alisema Chande
.

WAKALI WA MAPENZI VALENTINE'S DAY DAR LIVE

NEW VIDEO: BARAKAH DA PRINCE - SIACHANI NAWE

Vijana Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali wameishukuru Serikali kutoa elimu ya Ujasiriamali

$
0
0
 Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Bibi Mariam A. Mtunguja (katikati) akizungumza na maafisa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakati wa ziara ya kutembelea vijana wa Mkoa wa Mbeya na kutoa elimu ya Ujasiriamali, Ujuzi, Stadi za Maisha na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
 Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Bw. Gullamhussein S. Kifu (katikati) wakati wa ziara ya kutoa mafunzo ya Ujasiriamali kwa vijana wa Wilaya hiyo. Kulia ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele na anayefuata ni Kaimu Afisa Vijana Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Bw. Athuman Mustafa Kinza.
 Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele akiwaelekeza vijana wa Mbarali namna ya kuandika andiko la mradi wakati wa semina ya Ujasiriamali, Ujuzi, Stadi za Maisha na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyotolewa kwa vijana wa Mbarali hivi karibuni.
 Maafisa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo pamoja na vijana wa Kikundi cha Umati Sanaa Group wakiburudika na muziki uliokua ukitumbuizwa na vijana wa kikundi hicho wakati wa ziara ya kutembelea vikundi vya vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Mkoa wa Mbeya.
 Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa (waliokaa kushoto) akizungumza na vijana wa Umati Sanaa Group wanaofanya kazi za sanaa walipofika kuangali kazi zinazofanywa na kikundi hicho wakati wa ziara ya uhamasishaji kwa vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Mkoa wa Mbeya

(Picha zote na: Genofeva Matemu – Mbarali, Mbeya)


Wabunge wapewa Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012

$
0
0
 Mgeni Rasmi katika Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 kwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iliyofanyika leo mjini Dodoma.
 Waziri wa Fedha Saada Mkuya akitoa ufafanuzi juu ya maswali ya wabunge.
 Kamishna wa Sensa Tanzania, Hajjat Amina Mrisho.
 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akiwasilisha mada.

 Waziri wa Uchukuzi Samuel Sitta ambaye amemuwakilisha Mgeni Rasmi wa Semina hiyo Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akiwa na Waziri wa Fedha Saada Mkuya.
 Mbunge wa jimbo la Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye akichangia
 Mbunge wa jimbo la Mkanyageni, Mohamed Habibu Mnyaa.
 Waziri wa Sheria na Katiba Selina Kombani akichangia kwenye semina hiyo.
Baadhi ya wabunge waliohudhutia semina hiyo. Picha zote na Hussein Makame-MAELEZO, Dodoma

Bondia wa kulipwa Farncis Cheka atupwa jela miaka mitatu, familia yapanga kukata rufaa

$
0
0
 
Na Ripota wetu, Morogoro
 
Bondi wa kulipwa nchini, Francis Cheka ambaye maarufu kwa jina la SMG, amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela na faini ya Sh milioni moja kwa kosa la kumpiga meneja waje wa baa, Bahati Kibanda.
 
Cheka alitiwa hatiani Julai 2 mwaka jana kwa kumpiga na kumsababishia maumivu makali Kibanda ambaye alikwenda hapo kudai fedha zake katika baa aliyokuwa anaifanyia kazi  ijulikanayo kwa jina la Vijana Social Hall.
 
Hakimu Mwanamizi wa mahakama ya mkoa wa Morogoro Said Msuya alikubaliana na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na kuthibitisha shitaka hilo.
 
Hakimu Msuya alisema kuwa adhabu hiyo ni fundisho kwa mshitakiwa na watu wengine wanaotumia vibaya nguvu zao kwa watu wengine na anatakiwa kumlipa mlalamikaji fidia ya Sh milioni moja.
 
Pamoja na Cheka kupewa nafasi ya kujitetea, bondia huyo hakutoa maelezo yoyote na kuiachia mahakama hiyo kutoa adhabu inayostahili kwa bondia huyo aliyejizolea sifa kemkem katika ngumi za kulipwa nchini.
 
Hata hivyo, taarifa zilizotufikia wakati tunakwenda mitamboni, familia ya Cheka inampango wa kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.
 

WASANII KUTOKA TANZANIA WATUMBUIZA OMAN

$
0
0
 Na Faki Mjaka, Mascut Oman.

Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa,Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea Mascut nchini Oman yamechukua sura mpya baada ya Nchi Washiriki kupeleka Wasanii wake wa Ngoma za Asili kwenda kutumbwiza katika wiki mbili za mwisho ya Maonesho hayo. Tanzania ni moja ya nchi washiriki ambapo Wasanii wake 15 Usiku wa jana walipata nafasi ya kuburudisha kwenye Jukwaa kuu la Maonesho hayo.

Akizungumza kuhusu ujio wao Kiongozi wa Wasanii hao wa Ngoma Bi Asha Khatib amesema wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanazikonga vyema nyoyo za Waomani kwa burudani ya nguvu. Amefafanua kuwa Waoman wengi wanapenda Ngoma zenye asili ya Zanzibar hivyo wamefanya Mazoezi ya kutosha ili kuwafurahisha Mashabiki wao pale wanapopanda Jukwaani kwa ajili ya kutumbuiza.
 
“Kwa kweli tumejiandaa vizuri tu na tumekuja hapa Mascut kwa kazi moja tu ya kutoa Burudani hivyo Waoman wazidi kuja kwa wingi kuja kujionea burudani ya aina yake yenye Asili ya Tanzania-Zanzibar”Alisema Bi Asha. Bi Asha amebainisha kuwa katika Jukwaa watapiga baadhi ya Ngoma zenye Asili ya Zanzibar kama vile Msewe, Uringe, Gonga, Kyaso,Kitua tua,Kibunguu na Kidumbaki ambapo anaamini zitakidhi kiu ya burudani kwa Waomani.

Jana ikiwa ni siku ya mwanzo kwa Watanzania hao hivyo walipewa muda wa nusu saa kwa ajili ya kusalimia jukwaa na kutumbuiza ambapo walipiga Ngoma ya Msewe na Kitua tua.

Kabla ya Watanzania kupanda Jukwaani kwenda kutumbuiza walitanguliwa na Wasanii kutoka Ufaransa ambapo baada ya Watanzania kumaliza Wasanii kutoka Urusi ndio waliochukua nafasi kutumbuiza. Nchi nyingine zilizopata nafasi ya kutumbuiza katika Jukwaa kwenye Maonesho hayo ya Kimatifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni ni pamoja na China, Iran, Thailand, India, Uzbekistani na Misri.

Kwa wiki mbili mfululizo kuanzia jana Wasanii wa Nchi hizo zinazoshoriki Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa,Ubunifu na Utamaduni watakuwa wakipanda katika Jukwaa kuonesha vipaji vyao vya Muziki wa Asili ya nchi zao husika.

Wasanii hao wa Ngoma waliofika Juzi kutoka Tanzania wanaungana na Wenzao waliokuwepo Oman kwa zaidi ya wiki mbili sasa kushiriki Maonesho hayo ambapo Wasanii huonesha bidhaa zao wanazozitengeneza kwa Mikono na kuwauzia Wateja mbalimbali wanaofika katika Maonesho hayo.

BODI YA MICHEZO YA BAHATI NASIBU YAKABIDHI LESENI KWA KAMPUNI YA MURHANDZIWA KUENDESHA MICHEZO HIYO

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya bahati nasibu , Bw Abbass Talimba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi leseni ya kuendesha bahati nasibu ya Taifa kwa Kampuni ya Murhandziwa.
Bodi ya Michezo ya bahati nasibu ya Taifa leo imetoa leseni ya kuendesha Bahati nasibu ya Taifa kwa Kampuni ya Murhandziwa ambayo itakuwa ikiendesha bahati nasibu hiyo hapa nchini ambapo Bahati nasibu hiyo itaanza mnamo tarehe 4 Julai 2015.Bei ya tiketi zitakazouzwa itagharimu shilingi za Kitanzania shilingi 500 kwa kila tiketi.
 Baadhi ya viongozi wa Kampuni ya Murhandziwa pamoja na viongozi wa Bodi ya Michezo ya Bahati nasibu ya Taifa wakitazama video ya Mwenyekiti wa kampuni ya Kampuni ya Murhandziwa amaye hakuweza kufika kwenye hafla hiyo
 Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya bahati nasibu, Abbass Talimba (wa pili kutoka kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa wa Bodi ya Michezo ya bahati nasibu, William Mdundo  wakikabidhi leseni kwa viongozi wa Kampuni ya Murhandziwa ambao ndio wamepewa kibali cha kuendesha bahati nasibu ya Taifa nchini Tanzania. Aliyeshika Leseni hiyo ni Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Murhandziwa, Lucien D Avece( wa tatu kutoka kulia).
 Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya bahati nasibu , Bw Abbass Talimba akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo Pichani)
 Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Murhandziwa, Lucien D Avece akiyatolea ufafanuzi maswali yaliyoulizwa na waandiahi wa habari (hawapo pichani)
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo uliofanyika katika hoteli ya Double Tree by Hilton - Masaki

Wageni wabainika wakitengeneza Filamu bila Kibali

$
0
0
 Katibu Mtendaji  Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fisoo( wakwanza  kushoto) akitoa ufafanuzi kuhusu filamu hiyo iliyokuwa ikirekodiwa na raia wa Norway katika Ofisi ya Bodi ya Filamu mwishoni mwa wiki.
 Raia hao wa Norway katika picha wakiwa katika kikao kuhusu filamu waliyokuwa wakirekodi  kwenye Ofisi  ya  Bodi ya Filamu hivi karibuni.
 Bw.Torshin Nodland  raia wa Norway (watatu kulia)akijitetea kuhusu filamu hiyo waliyokuwa wakirekodi mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya vifaa walivyokuwa wakitumia raia hao wa Norway katika kurekodi filamu hiyo vikiwa katika Ofisi ya Bodi ya Filamu mwishoni mwa wiki.

MH.HAMAD RASHID AWAASA WANAFUNZI KUJIUNGA NA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF ILI KUPATA MIKOPO YA ELIMU NA MIKOPO YA KUANZIA MAISHA

$
0
0

Mgeni rasmi Hamad Rashid ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Wawi kupitia CUF akizunguza na wanafunzi walioudhuria kwenye siku ya Career Day iliyofanyika kwenye viwanja vya chuo cha Biashara (CBE) jijini Dar es Salaam
Rais wa Serikali ya Wanafunzi Katika Chuo cha Biashara,(CBE),Ramadhani S Kirungi akiwakaribisha wageni mbalimbali katika siku ya "CAREER DAY" iliyofanyika katika viwanja vya Chuo hicho Jijini Dar es salaam
Afisa wa PSPF Hadji Jamadary akiwa anafafanua na kuelezea  kuhusu na uchangiaji wa hiari wa PSS kwa wanafunzi wa Chuo Cha Biashara (CBE) jijini Dar es salaam
Maseko Kodalo Afisa wa Mfuko wa pensheni Wa PSPF akiwa anatoa maelekezo ya kujiunga na mfuko huo kwa mpango wa lazima, Mikopo ya Elimu na mikopo ya kuanzia maisha.
Mgeni rasmi Mh. Hamad Rashid ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Wawi kupitia CUF akitolewa ufafanuzi kufusu kazi za mfuko wa PSPF na Afisa wa PSPF Hadji Jamadary (wa pili kutoka Kushoto)
Mbunge wa Jimbo la Wawi kupitia CUF, Mh. Hamad Rashid akiwa ndani ya banda la PSPF ambao walikuwa wadhamini wakuu katika Career Day
Mgeni rasmi Mh. Hamad Rashid ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Wawi kupitia CUF akipata ufafanuzi kutoka kwa wanafunzi wa Chuo kikuu cha biashara (CBE) wa kozi mbalimbali kuhusu kazi zao na maendeleo ya masomo yao.
Afisa wa PSPF Hadji Jamadary akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa wanafunzi waliotembelea banda la mfuko wa PSPF.

Wanafunzi wakiwa kwenye banda la Mfuko wa PSPF wakipatiwa elemu kuhusu mikopo ya kuanzia maisha na fao la elimu.
Afisa wa  mfuko wa Pesheni (PSPF) Abdallah Ahamed akitoa maelekezo kwa mmoja wa wanachuo waliotembelea kwenye banda la PSPF
Wanafunzi wa Chuo cha Biashara (CBE) jijini dar es Salaam wakijaza fomu za kujiunga na mfuko wa PSPF
Baadhi ya washiriki ya washiriki wa Cereer Day
Baadhi ya wanafunzi walioweza kutembelea banda la PSPF na kuweza kulimishwa juu ya fao la elimuna mikopo ya kuanzia maisha wakitizama mtandao wa Mfuko huo kwa njia ya simu
Mgeni Rasmi na PSPF wakiwa kwenye picha ya pamoja na Baadhi ya viongozi wa Chuo cha Biashara (CBE)  jijini Dar 



Mbunge wa Jimbo la Wawi kupitia CUF Mh.Hamad Rashid ameupongeza mfuko wa pensheni wa PSPF kwa kuwa wadhamini katika Career Day ya Chuo cha biashara (CBE) iliyofanyika katika viwanja vya chuo hicho  siku ya ijumaa ambapo mbunge huyo aliweza kuwa mgeni rasmi wa tukio hilo na kuwapa hongera PSPF kwa kitendo cha kuweza kuwa pamoja na wanafunzi kwa ajiri ya kuwaandaa kuwa washiriki wazuri katika uchangiaji wa mafao mbalimbali na kuweza kupata mikopo ya elimu na ile ya kuanzia maishi

Rais wa Serikali ya Wanafunzi Katika Chuo cha Biashara,(CBE) Bw.Ramadhani S Kirungi amewashukuru wanafunzi wote walio weza kushiriki katika sherehe hizo kwani ni za kwanza toka chuo hicho kianze yapata miaka hamsini (50) hazijawahi fanyika lakini katika uongozi wake amepata bahati ya kuweza kuifanya siku hiyo, pia amewapongeza wanafunzi wa kozi mbalimbali walio weza kufanya maonesho katika viwanja vya chuo hicho kwaajiri ya kuwaonesha wahudhuriaji ufasaha wa masomo yao.

Pia Mfuko wa Pensheni wa  PSPF kupitia Maafisa wao walio weza kujitoa kwa ajiri ya kuwapa elimu ya jinsi na namna ya kujiunga na mfuko huo hususani katika fao la elimu na fao la kuanzia maisha ambapo ni mfuko mojawapo wenye manufaa makubwa kuliko mifuko mingine unaoweza kutoa huduma kulingana na mahitaji wa watanzania pasipo na ubaguzi wala upendeleo

Maseko Kodalo Ambaye ni Afisa wa Mfuko wa pensheni Wa PSPF yeye aliweza kutoa rai kwa wanafunzi wote na wananchi wote waweze kujiunga na mfuko huo ili kuweza kupata mafanikio, alitoa mifano michache ambayo inawezekana ukaimudu pindi unapo jiunga na mfuko huo ambapo kwa mwanafunzi alitaja kuwa unaweza kupata mikopo na kujiwekea akiba ili kuweza kukusaidia katika masomo, vilevile kuna mikopo ya kuanzia maisha  ambayo itakuwezesha kupata nyumba ambazo wamezijenga kwa ajiri ya mtanzania aweze kununua au kukopeshwa na baadae kuweza kurejesha mkopo huo wanyumba, pia aliongeza kwa kusema nyumba zote zimewekewa bima endapo tatizo lolote likitokea basi nyumba hizo zitakuwa salama .

Dkt Kigoda anastahili kupumzika jimbo la Handeni

$
0
0
NA KAMBI MBWANA, DAR ES SALAAM.

UKWELI unauma. Na ili ufahamu hilo, mara nyingi watu wanaosema ukweli huwa hawapendwi. Watazushiwa na kusemwa mno kutokana na misimamo yao ya ukweli wanayosema mbele ya hadhira.

Wakati nasema haya, najipa moyo kuwa hata kama wapo watakaochukizwa na ukweli wangu, ila ipo siku jamii itaishi vizuri kutokana na kukombolewa na harakati za ukweli zinazoweza kupingwa na wachache wao waliokuwa kwenye nafasi mbalimbali za kiutawala.

Ndio, bora niseme tu Dkt Abdallah Omary Kigoda anastahili kupumzika kuongoza kama Mbunge wa Handeni, mkoani Tanga. Kigoda ni mbunge wa Chama Cha Mapinduzi CCM kwa miaka 20 sasa.

Kigoda aliingia madarakani kwa mara ya kwanza kama mbunge mwaka 1995. Watoto waliozaliwa miaka ya 1995 mwaka 2015 wametimiza miaka 20. Ni kipindi kirefu mno kuongoza katika nchi inayojipambanua kuwa inaongozwa kwa misingi ya kidemokrasia.

Aidha, watoto hao waliozaliwa miaka ya 1995 na kukuta kero nyingi kama vile kukosa maji safi na salama, umeme vijijini, elimu duni, afya na mengineyo wanashangaa kama hadi leo kero hizo hazijatatuliwa ipasavyo licha ya kuongozwa na mbunge aliyekaa madarakani kwa muda mrefu.
Kwanini Kigoda anastahili kupumzika? Licha ya Handeni kuwa wilaya kongwe na kubwa mno, lakini wananchi wake wanaishi maisha magumu na kuvumilia shida mbalimbali, jambo lililowachosha.

Wilaya hii haina maji. Wananchi wake wanalazimika kununua ndoo ya maji kwa Sh 700 hadi 1000 yanapotoka mbali zaidi. Kwa mtu mwenye familia ya watu wanne, atalazimika kununua ndoo tatu hadi tano. Endapo atanunua ndoo tano, basi atalazimika kulipia Sh 3500 kama atayanunua kwa Sh 700. Lakini kama atanunua kwa Sh 1000, basi mwananchi huyo atayanunua maji kwa Sh 5000. Je, pato lake kwa siku lipoje?

Mbaya zaidi, licha ya kuwa wilaya kongwe, lakini Hospitali ya wilaya ya Handeni haina chumba cha kuhifadhia maiti. Watu wanalazimika kupelekwa Hospitali ya wilaya Korogwe (Magunga) kuhifadhiwa kabla ya kuzikwa au kusafirishwa kwa wale wenye utaratibu huo. Aidha wilaya pia haina gari la kuzimia moto. Ulipotokea moto uliowatia hasara wananchi wengi, msaada ulizimika kutoka Korogwe. Hadi gari hilo lilipofika Handeni, moto huo ulishateketeza nyumba nyingi na kuwapa hasira wananchi kiasi cha kulipopoa kwa mawe gari hilo.

Huduma za afya ni mbovu. Na yote hayo yamesababishwa na utawala mbovu usiokuwa rafiki kwa wananchi dhidi ya mbunge Kigoda, ambaye pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara. Kumbuka Kigoda sit u ni mbunge wa muda mrefu, bali pia amewahi kuwa Waziri wa wizara tofauti kwa vipindi tofauti. Wakati yeye ni Waziri wa Viwanda na Biashara, lakini wakulima wake wa matunda wilayani Handeni wanapata hasara kubwa mno.


Maeneo ya Michungwani, Segera na kote wanapolima machungwa hawana kwa kuyapeleka na mara kadhaa wanayouza si yale yanayozaliwa. Hii ni aibu kubwa mno. Wilaya ya Handeni ipo ipo tu. Hata elimu ya sekondari ya kidato cha tano na sita ni mtihani mzito.

Licha ya ukongwe huo lakini hakuna cha kujivunia. Wakulima wanadhulumiwa mashamba yao na wenye nacho. Watu wachache wamegawana maeneo makubwa ya ardhi, hali kadhalka uwapo wa dhahabu na madini mengine hakuonekani dalili njema za kuwakomboa wananchi wa Handeni, wanaoishi kwa kupiga miayo. Ni mifano hii michache tu kati ya mingi ninayoweza kuisema hapa, nadiriki kusema Mbunge Kigoda hana cha kumfanya agombee tena jimbo hilo kwa kipindi cha tano kijacho.

Bali anastahili kupumzika na abaki kuwa mshauri tu. Watu wanaishi kwa tabu kwenye wilaya yao yenye kila aina ya matunda. Wananchi wa Handeni wataendelea kutaabika hadi lini?

Hili ni jambo la kuliangalia. Mfumo wa kiutawala wilayani Handeni umekufa na hauna mwamko tena. Mbaya zaidi, kitu chochote ambacho mbunge hakitaki aidha kwa woga wake kisiasa au vinginevyo hakubali kifanyike hata kama kina manufaa na wananchi wake.

Katika hali ya kushangaza na kuogopesha, hakuna mtu yoyote anayeweza kutoa sauti yake kumkemea au kumkosoa mbunge. Hii ni mbaya. Kumuogopa huku kunasababisha hasara kwa wilaya.

Haiwezekani mbunge akawa anajua yote. Lakini pia haiwezekani kuona mbunge analalamikiwa bila sababu za msingi. Ingawa baraza la madiwani ndio lenye mamlaka ya kisheria ya kupanga bajeti na kuisimamia, ila mbunge naye ni mjumbe kutokana na kofia yake. Na kwakuwa tumekuwa na utawala wa kuogopana, madiwani hawa wameshindwa kupaza sauti yao kusimamia mambo yenye manufaa na wilaya ya Handeni.

Leo hii ni aibu iliyoje? Ukongwe wa Handeni na rasilimali zote ilizokuwa nazo, hakuna chuo chochote kinachoweza kuwapa elimu ya juu wanafunzi wanaotokea kidato cha nne au sita.
Lini Handeni itakuwa na mwangaza? Mwangaza huo utakuja siku Kigoda atakapoamua kwa ridhaa yake au kulazimishwa kupumzika kwasababu ameshindwa kuwaongoza watu wake.

Kwa bahati mbaya, leo hii wananchi wamekuwa wakali. Wamekuwa na mtazamo chanya wa kuhoji maendeleo yao na wale wanaochelewesha mikakati inayoweza kuwakwamua kiuchumi. Wakati nasema haya, nadiriki kuona hatari ya kudhalilika juu ya mbunge huyu, hasa kama ana ndoto za kutetea kiti chake. Wananchi wamekuwa wakihoji udhaifu wake hadharani.

Mengi yanayosemwa ni kama matusi kwake. Mbunge aliyekaa madarakani miaka 20, anapoambiwa ameshindwa kufanyia kazi hata chumba cha kuhifadhia maiti ni aibu isiyokuwa na kifani.
Ni budi kwa viongozi wa juu wa CCM kuvuta taswira halisi ya ugumu wa maisha ya wana Handeni. Lakini pia viongozi hao lazima wajuwe chama chao kipo rehani kwasababu ya kumng’ang’ania mtu mmoja.
Yeye ni nani? Hakuna mwingine? Mfumo wa upatikanaji wa viongozi wa CCM hususan wa kuangalia asiyependwa ndiyo anayepita umepitwa na wakati kwa Dunia ya leo ya Sayansi na teknolojia.

Tunachokiona sasa ni tatizo kubwa la kimfumo kama nilivyojaribu kulieza hapo juu kwenye makala haya. Kama leo tunawaza namna gani ya kuleta maji, umeme vijijini, afya jua tumeshindwa.

Na udhaifu huu utachukuliwa kama tahadhari katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu kuhakikisha kuwa mgombea wa CCM, hasa kama akiwa Kigoda aenguliwe. Na kama watashindwa basi hata wale wasioaamini upinzani watashawishika na kupiga kura za chuki dhidi ya Kigoda na chama chake CCM.

Bora ukweli useme bila woga. Ukweli usemwe ili watu wajirekebishe katika harakati za kuikomboa wilaya ya Handeni ambayo si wote wanaiheshimu kutokana na kiwango kibovu cha viongozi wake, wakiongozwa na mbunge wa miaka 20 madarakani jimbo halina maji, huduma za afya mbovu, elimu ya kusua sua, malalamiko ya wakulima na kadhalka.

Ajabu, wanaopita pembeni wakimsifia mbunge ni viongozi wachache wa CCM wilayani, ambao kwa namna moja ama nyingine wana manufaa naye, aidha kuwekwa wao madarakani katika Uchaguzi wa ndani wa CCM, hivyo kuendelea na sera ya kulipana fadhira.

Hilo haliwezekani. Tunahitaji kuzaliwa upya kwa wilaya ya Handeni, tukianzia na kuona namna gani mfumo uliooza chini ya Kigoda unaondolewa kwa ajili ya kuibua ari mpya, kasi mpya na vitendo vyote vya kupigania maendeleo kwa jimbo hili linaloonekana la mwisho kimaendeleo.
kambimbwana@yahoo.com+255712053949
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images