Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 451 | 452 | (Page 453) | 454 | 455 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kabwe Zitto (kulia) na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Deo Filikunjombe wakiwa katika majukumu yao. Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kabwe Zitto (kulia) na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Deo Filikunjombe wakiwa katika majukumu yao.Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) akiwa katika majukumu. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) akiwa katika majukumu.

  KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imetoa mapendekezo ya kuinusuru Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kutokana na hali mbaya ya kampuni hiyo kifedha kwa sasa ambapo inaendeshwa kwa hasara huku ikiwa na madeni makubwa. PAC imetoa mapendekezo hayo katika taarifa yao kwa bunge ya mwaka juu ya ukaguzi wa hesabu za Serikali kwa mashirika ya umma iliyotolewa Januari 28 mwaka 2015. 

   Kwa mujibu wa taarifa ya PAC hali ya mapato na matumizi ya TTCL kwa mwaka 2012 ilipata hasara ya bilioni 20.883 huku kwa mwaka 2013 ikipata hasara ya bilioni 16.258. PAC ilisema majumuisho ya hasara ya TTCL kupata hasara kwa takribani kwa miaka 10, Kampuni sasa imekuwa na hasara ambayo kwa mwaka 2013 ilifikia bilioni 334.48, jambo ambalo limeiondolea mvuto wa kukopeshwa na taasisi za fedha hata zile zenye nia ya kuikopesha.

   "...Ukosefu wa fedha za kutosha kutekeleza miradi ya Kampuni umekuwa kikwazo kwa TTCL kukabiliana na ushindani wa kibiashara. Kwa kipindi kirefu ufanisi wa TTCL kiuwekezaji na kifedha umeendelea kudorora. Tangu TTCL ibinafsishwe mwaka 2001, hakuna uwekezaji mkubwa uliofanyika na mpango wa kutafuta mkopo kutoka mabenki ya ndani na nje ya nchi unakwamishwa na masharti ya kupata udhamini wa Serikali," ilieleza taarifa hiyo ya PAC. PAC iliongeza kuwa ukiacha madeni yaliopo pia TTCL inadaiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) jumla ya bilioni 25 hivyo kufanya jumla ya deni kufikia bilioni 101.6. 

  Kamati hiyo ya bunge imesema kuna umuhimu wa Serikali kufanya maamuzi ya haraka ya kuikwamua TTCL ili iweze kuendelea kutoa huduma kwenye Sekta ya Mawasiliano ikizingatiwa kuwa ndiyo inayoendesha Mkongo wa Taifa wa mawasiliano. Katika mapendekezo ya PAC ili kuikwamua TTCL imeishauri Serikali kununua hisa asilimia 35 zinazomilikiwa na Bharti Airtel katika TTCL kwa gharama ndogo kwani Bharti Airtel haikutimiza kikamilifu masharti ya mkataba wa mauziano ya hisa hizo hapo awali kwani tangu inunue hisa hizo haijafanya uwekezaji katika Kampuni ya TTCL. 

  "...TTCL isamehewe deni la Serikali Sh. 76.6 bilioni na deni la TCRA Sh. 25 bilioni ambayo jumla yake ni Sh. 101.6 bilioni na fedha hizo zipelekwe kuongeza mtaji ili Kampuni itoke kwenye kuwa na mtaji hasi wa Sh. 87.896 bilioni na kuwa na mtaji chanya wa sh. 13.704 bilioni. Likifanyika hili basi Kampuni hiyo itaweza kukopesheka. Serikali ikamilishe taratibu zake za kuimilikisha TTCL Mkongo wa Taifa ili izidi kuuendeleza kwa ufanisi na kuongeza mapato ya TTCL," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo. Hata hivyo PAC imeshauri kuwa kuna umuhimu wa kufanya marekebisho ya muundo wa Kampuni ya TTCL kwani kwa sasa ina idadi kubwa ya wafanyakazi (1549) isiyoweza kuwalipa.

   Aidha, ilibainisha kuwa kwa sasa zinahitajika bilioni 32 kwa ajili ya kugharamia urekebishaji wa muundo wa Kampuni ili uendane na mahitaji ya utoaji wa huduma mbalimbali. Mashirika mengine yenye hali mbaya kifedha na uendeshaji ni pamoja na Shirika la Ndege Tanzania, ATCL ambayo kwa sasa ina madeni makubwa huku ikiwa na ndege moja aina ya Dash 8–Q 300, Wafanyakazi 142 na Jengo la ATC House lililoko mtaa wa Ohio, Dar es Salaam

  0 0

  DSC_0035

  Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues aliyemtembelea ofisini kwake wakati wa ziara ya kikazi ya siku nne kwenye kijiji cha Ololosokwani na halmashauri ya Ngorongoro kwa ajili ya maandalizi ya mradi wa kijiji cha digitali unaoendeshwa na Unesco kwa kushirikiana na Ki-elektronic ya Samsung unaotarajiwa kuwasili kijijini hapo mwezi februari ukitokea jijini Dar.

  Na Mwandishi wetu, Ngorongoro.
  MKURUGENZI Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues ameonesha mashaka yake juu ya ubora wa barabara ambazo magari mazito yenye vifaa vya kijiji cha digitali Ololosokwan yanaweza kupita.

  Alisema hayo kwenye mazungumzo na Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Elias Wawa Lali wakati alipomtembelea ofisini kwake. Akiwa katika ofisi za mkuu huyo wa wilaya kumwelezea shughuli za Unesco katika wilaya yake, Mkurugenzi Mkazi huyo alipata nafasi ya kuzungumzia haja ya kuboreshwa kwa maaneo kadha ya barabara kuelekea kijiji cha Olosokwan ili kuyawezesha magari hayo makubwa kufika kwa urahisi.

  Huku akimuonesha mkuu wa wilaya baadhi ya picha alizopiga akiwa njiani kukagua njia ya kupita magari hayo na kuangalia maandalizi ya mwisho ya mradi huo mkubwa na wa kipekee nchini alisema hali ya barabara si nzuri hata kidogo. Vifaa kwa ajili ya kijiji hicho vipo bandarini tayari na magari yanayoweza kubeba makontena hayo ni makubwa na barabara za kuelekea kijiji hicho ni mbaya.
  DSC_0041
  Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali (katikati) akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (kulia) aliyeambatana na wataalamu wa elimu, afya na mawasiliano pamoja na Mratibu wa Taifa wa tiba asilia na mbadala katika Idara ya Tiba Wizara ya Afya na ustawi wa jamii. Dkt Liggy Vumilia (hayupo pichani) . 


  Kutoka kushoto wa kwanza ni Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias, Afisa mipango ya Elimu wa Shirika la UNESCO, Bi. Jennifer Kotta pamoja na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph.

  Kuwapo kwa kijiji hicho ni matokeo ya mkataba uliotiwa saini kati ya UNESCO na kampuni ya elektroniki ya Samsung mwaka jana.Katika makubaliano hayo yalitiwa saini na Mwakilishi mkazi Unesco nchini, Zulmira Rodrigues na Mkurugenzi wa Samsung Electronics nchini Tanzania, Mike Seo katika Kijiji hicho kitakuwa na shule yenye Tehama ikiwa na maunganisho ya intaneti, kiliniki ya kisasa ikiwa na kituo cha teknolojia ya mawasiliano yenye kuwezesha utabibu (Telemedicine) na jenereta linalotumia nguvu za jua kwa ajili ya kijiji hicho.

  Mradi huo utawezesha UNESCO kuwapatia vijana wa Kimasai elimu kutokana na ukweli kuwa kwa utamaduni na kazi zao za ufugaji wamekuwa wakipata shida ya kupata elimu.
  DSC_0096
  Mkutano huo pia ulihudhuriwa na wataalam wa Elimu, Afya, Utamaduni na Kilimo kutoka Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro jijini Arusha. Kushoto pichani ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Dkt. Peter Kitenyi.

  Kupitia kijiji hicho vijana wataendelea na masomo hata kama wanachunga mifugo yao. Wakati wa utiaji saini Mkurugenzi wa Samsung Electronics nchini Tanzania alitaja miongoni mwa manufaa makubwa yatakayopatikana katika mradi huo wa kijiji cha digitali huko Loliondo ambayo ni pamoja na kuweza kupata nishati rahisi na iliyo rafiki kwa mazingira. Alisema kwamba Afrika imekuwa mstari wa mbele katika uanzishaji wa vijiji vya digitali. 

  Aidha kwa kitendo hicho Afrika inaonesha dunia ni kwa namna teknolojia inaweza kutumika kuleta mabadikliko chanya yanayotakiwa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi waliopo vijijini. Kijiji hicho cha Loliondo kitakuwa cha nne katika vijiji vya kidigitali barani Afrika.Inatarajiwa kwamba kijiji kingine kitajengwa mjini Zanzibar kwa ushirikiano wa UNESCO na Samsung Electronics mwaka huu.
  DSC_0080
  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akifafanua jambo kwa Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali wakati wa mazungumzo na mkuu wa wilaya hiyo kabla ya kuelekea kijiji cha Ololosokwani kwa ajili ya mkutano na wanakijiji wa kijiji hicho kabla ya kuwasili kwa mradi wa kijiji cha kidigitali mapema mwezi februari.
  DSC_0092
  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akielezea changamoto za miundo mbinu ya barabara kwa kutumia picha alizopiga akiwa njiani kuelekea kijiji cha Ololosokwan kupitia barabara ya Lake Natron kwa Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali.
  DSC_0105
  Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali akielezea jitihada zitakazofanywa na wilaya yake katika kuhakikisha miundo mbinu ya barabara inarekebishwa kuondoa usumbufu kwa magari mazito yenye vifaa vya kijiji cha digitali cha Ololosokwan yanapita bila kikwazo mapema mwezi februari.
  DSC_0136
  Wataalamu kutoka halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro, Unesco pamoja na Wizara ya afya wakitazama picha hizo kwenye kompyuta mpakato ya Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues ofisini kwa Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro.
  DSC_0136

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora Mhe. George Mkuchika, (katikati) akiwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Juma Assad (kushoto) pamoja na wajumbe wengine wakiimba wimbo wa wafanyakazi wakati wa Mkutano wa Pili wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi uliofanyika jana katika Ukumbi wa Hoteli ya Naf Beach iliyoko mkoani Mtwara.
  Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Juma Assad akisoma hotuba ya kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa Mkutano wa Pili wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi uliofanyika jana katika Ukumbi wa Hoteli ya Naf Beach iliyoko mkoani Mtwara.
  Mgeni rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora Mhe. George Mkuchika, akiwahutubia wajumbe wa Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi muda mchache kabla ya kulifungua baraza hilo jana katika Ukumbi wa Hoteli ya Naf Beach iliyoko mkoani Mtwara.


  0 0

  Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania,Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza majina ya washiriki walioingia 5 bora katika mashindano ya Airtel Trace Music Stars.Kulia ni Meneja Masoko wa Airtel,Anethy Muga.
  Meneja Masoko wa Airtel Tanzania,Anethy Muga akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza majina ya washiriki walioingia 5 bora katika mashindano ya Airtel Trace Music Stars.Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania,Jackson Mmbando.
  Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania,Jackson Mmbando (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wanne waliongia hatua ya 5 bora katika mashindano ya kuvumbua vipaji vya muziki ya Airtel Trace Music Strars . fainali za mashindano hayo zinategemea kufanyika mwanzoni mwa mwezi Airtel yatangaza tano bora ya shindano la Airtel Trace Music Starswa pili.kulia ni Meneja Masoko wa Airtel Tanzania,Anethy Muga.

  0 0

  Na Miza Othman -Maelezo Zanzibar  .
    
  Serikali  ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema Wizara ya Kilimo na Maliasili haina utaratibu wa kutoa  mikopo  kwa wakulima  ikiwemo wafugaji wa nyuki bali  suala la kuwawezesha wananchi ikiwemo mikopo ni la Wizara  ya  Uwezeshaji, Ustawi  wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto.

  Naibu Waziri wa Kilimo na Maliasili Mtumwa Kheir Mbaraka ameyasema hayo katika kikao cha Baraza la Wawakilishi wakati  akijibu suali la Mh.Saleh Nassor Juma Mwakilishi wa Jimbo la Wawi  alietaka mpango wa Serikali kupitia taasisi za fedha kutoa mikopo yenye masharti nafuu  ili wafugaji waweze kufuga nyuki kitaalamu.

  Amesema Wizara yake inajukumu la kuwashajihisha na kuwahamasisha wananchi katika ufugaji wa nyuki na kujiunga katika vikundi kwa lengo la kujikwamua na umaskini. Ameongeza kuwa  Wizara yake inatoa mizinga  ya nyuki na mafunzo ya mbinu bora za ufugaji  kwa wale wanaojishughulisha na kazi hiyo kama inavyofanya kwa  wanaushirika wa Tujiendeleze wa Jimbo la Wawi Chake chake Pemba.

  “Kinachofanyika ni jitihada za kupunguza umaskini na kuwaongezea kipato wananchi kwa kupitia shughuli zao”,  Naibu Waziri Mtumwa Kheir amesema. Alielezea kuwa  wafugaji wa nyuki wanaweza kupata mikopo binafsi kwa vikundi vya kukopa na kuweka ikiwemo vikoba au kupitia taasisi za fedha zinazotambuliwa na Serikali kitu muhimu ni kutimiza   vigezo na masharti ya taasisi hizo.

  Pia amesema nia na lengo la Wizara hiyo ni kuvitembelea vikundi vyote  vya wafugaji wa vyuki  ili kuwapatia mafunzo yaliyo bora katika kuendeleza ufugaji  wao. Wizara ya Uwezeshaji Ustawi wa Jamii, Vijana,  Wanawake na Watoto kupitia program mbali mbali hutoa mafunzo ya kusarifu mazao kwa njia mabli mbali  kwa vikundi vya  akina mama na makundi mengine katika jamii                           
                                                            
  IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0

   Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa wa pili kulia akizungumza na Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Kyela Dr. Festo Dugange jana wakati wa ziara ya kuhamasisha vijana wa Kyela. Wa kwanza kulia ni Afisa Maendeleo ya Vijana Bi. Amina Sanga, wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele na wa pili kushoto ni Afisa Vijana Mkoa wa Mbeya Bw. George Mbijima.
   Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga akiwaelimisha vijana wa Wilaya ya Kyela kuhusu mwongozo unaosimamia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana wakati wa semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyofanyika jana katika Wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya.
   Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya walioudhuria semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokua yakiendelea wakati wa semina hiyo.
   Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela wakiwa katika kikundi kujadiliana namna ya kuandika andiko la mradi baada ya kupata mafunzo ya jinsi ya kuandika andiko la mradi wakati wa semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyofanyika jana katika Wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya.
  Mwenyekiti wa Wadau Self Supporting Group Bw. Godbless Konga wanne kulia akizungumza na maafisa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo walipotembelea kikundi hicho kuangalia mradi unaoendeshwa na vijana wa kikundi hicho jana wakati wa ziara ya kukagua miradi ya vijana wa Wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya.  Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela washauriwa kutumia ujuzi kujiajiri.
  Na: Genofeva Matemu
  Tarehe: 29/01/2014
  Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela wameshauriwa kuachana na fikra potofu za kusubiria kuajiriwa na serikali mara tu wanapomaliza elimu ya chuo kikuu bali kutumia ujuzi walioupata kujiajiri wenyewe na kutoa fursa kwa vijana wengine ambao hawakupata fursa ya kujiendeleza.

  Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kyela Bibi Magreth E. Malenga alipokua akizungumza na wadau wa vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo walipofika ofisini kwake kabla ya kukutana na Vijana wa Wilaya hiyo kwa ajili ya kutoa elimu ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi, na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana jana katika Wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya.

  Akizungumza na wadau hao Bibi Malenga amesema kuwa amefurahishwa na ujio wa wadau kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwani anaamini kuwa ujio huo utawasaidia vijana wa Kyela kujitambua na kupata mbinu mbalimbali za kiujasiriamali ili waweze kujitegemea.“Vijana wa sasa hawapendi kujiajiri wanapomaliza elimu ya chuo kikuu wanabaki mitahani wakiilalamikia serikali haitaki kuwaajiri, naamini kwa semina hii vijana wa Kyela watajitambua na kutumia elimu waliyoipata kuibua miradi mbalimbali itakayowaingizia kipato” alisema Bibi Malenga.

  Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Vijana Bi. Amina Sanga amewataka vijana wa Kyela kutumia fursa mbalimbali zilizopo katika Wilaya hiyo kwani kwa kufanya hivyo watakua wameweza kujiendeleza na kujitegemea hivyo kuondokana na dhana ya kuwa tegemezi katika jamii.

  Naye mwenyekiti wa kikundi cha vijana kijulikanacho kwa jina la Wadau Self Supporting Group Bw. Godbless Konga amesema kuwa vijana wa Kyela walikua na ufikiri mdogo katika masuala ya aunzishaji na usimamiaji wa shughuli ndogondogo kutokana na kutokuwa na mbinu za kibiashara lakini kutokana na eimu waliyoipata  anaamini kuwa vijana watawekeza na kuachana na dhana ya kuwa tegemezi katika jamii. 

  Bw. Konga amewataka vijana wote nchini kuwa wabunifu na kujaribu kuanzisha miradi mbalimbali kwa kutumia mbinu za kibiashara zitakazowakwamua kimaisha ili kuachana na tabia ya kuitegemea serikali kwa kila jambo.

  0 0

  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipitia moja ya taarifa wakati akiwa kwenye Mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa,Ethiopia leo.Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh. Bernard Membe.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika (kulia) wakikutana na marais wastaafu, Thabo Mbeki wa Afrika ya Kusini(Kushoto) na Joachim Chissano wa Msumbiji(wapili kushoto) wakati wa mkutano wa 24 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika unaofanyika Addis Ababa Ethiopia leo.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Malawi Professa Peter Mutharika jijini Addis Ababa Ethiopia leo.Viongozi hao wanahudhuria mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais wa Malawi Professa Peter Mutharika(Wanne kushoto), Rais mstaafu wa Msumbiji Joachim Chissano, Rais mstaafu wa Afrika ya Kusini Thabo Mbeki(kulia) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe (kushoto)wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya kukutana wakati wa mkutano wa wakuu wan chi wanachama wa AU unaofanyika jijini Addis Ababa Ethiopia(picha na Freddy Maro)

  0 0

   Meneja wa kiwanda cha pareto mafinga (PCT) Martine Oweka
   mkulima akiwa shambani akiendelea kufanya kazi shambani.hili ni shamba lilopo mbeya
   wakulima wakiwa shambani wakiendelea kufanya kazi shambani huko mbeya.
   hii ndio pareto yenyewe ikiwa tayari kwa kuvunwa

  na Tumaini Msowoya,iringa

  KIWANDA cha Pareto (PCT), cha Mafinga wilayani Mufindi kimetumia zaidi ya shilingi milioni 400, kwa ajili ya kuwasaidia wakulima mbegu na miche ya zao hilo, ili kukuza na kuinua zao hilo.

  Kila msimu wa Kilimo, kiwanda hicho kimekuwa kikisambaza mbegu na miche ya Pareto kwa wakulima wa zao hilo katika mikoa yote ambayo zao hilo limekuwa likistawi ikiwemo Iringa, Mbeya, Njombe na Arusha.

  Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa kiwanda hicho Martine Oweka alisema kuwa lengo lao ni kuhakikisha zao la Pareto ambalo ni mkombozi kwa mkulima.

  Oweka amewataka wakulima wa mikoa hiyo  kulima zao hilo kwa wingi ili waweze kuinua kipato chao na kuondokana na umaskini kutokana na kuwepo kwa uhakika wa soko la zao hilo, tofauti na miaka ya nyuma kufuatia uwepo wa kiwanda.

  Oweka alisema ili wakulima waondokane na umaskini, lazima wajikite katika mazao ya biashara likiwemo pareto, kutokana na zao hilo kwa sasa kuwa na bei nzuri katika soko la dunia.

   Alisema kuwa endapo wakulima wa mkoa wa Iringa na mingine inayostawisha zao hilo wataamua kulima pareto kama zao mama la biashara wanaweza kuondokana na umaskini, kutokana na ukweli kwamba, zoko la pareto limekuwa na uhakika tofauti na miaka ya nyuma wakati soko la zao hilo lilipoyumba.

  Aliongeza kuwa kwa sasa kiwanda chao kinalima  zaidi ya ekari 300 za pareto, na kwamba kazi kubwa iliyopo ni kuhakikisha kuwa wakulima wanalima zao hilo na kufuatilia hatua zote za kupanda, kuvuna, kukausha na kusafirisha hadi kiwandani.

  Akizungumzia masoko ya kimataifa Oweka alisema kuwa kwa sasa zipo nchi nyingi ambazo zinauhitaji mkubwa wa zao la pareto na ndiyo maana bei yake ipo juu.

  Alizitaja nchi hizo kuwa ni Japani, India, Australia na nchi zilizopo bara la Ulaya kuwa wananunua pareto kwa wingi.

  0 0

  Baadhi ya Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakiwa katika picha ya Pamoja na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Bw. Bw.Johansen Bukwari (aliyevaa Kaunda suti) kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Bw. Assah Mwambene. Picha na Hassan Silayo.
   Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Bw.Johansen Bukwari akiongea na Maafisa Mawasiliano Serikalini ambapo alisisitiza umuhimu wa Maafisa Mawasiliano kutoa taarifa za Serikali kwa Umma.
   Mwenyekiti wa Muda wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini(TAGCO) Bw. Innocent Mungy akitoaa taarifa futi ya utekelezaji wa kazi wa chama hicho kwa Maafisa Mawasiliano wakati wa ufungaji wa kikao kazi cha Maafisa ha oleo Mkoani Mtwara.
   Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akiwaeleza Maafisa Mawasiliano Serikalini umuhimu wa kuwa na ushirikiano na vyombo vya Habari kwa dhumuni la kuieleza jamii nini serikali inakifanya, pia aliwataka kuendelea kuongeza juhudi katika utendaji kazi kupitia mafunzo waliyoyapata katika kikao kazi hiki.


   Afisa Mawasiliano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. Atley Kuni akitoa neno la Shukrani kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Bw.Johansen Bukwari

   Wawasilishaji kutoka kampuni ya PUSH OBSERVER wakiwaeleza maafisa mawasiliano huduma wanazotoa ikiwamo ufuatiliaji wa taarifa mbalimbali kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii pia utoaji wa taarifa wa jumbe kupitia mitandao ya simu(Bulk messages).


  0 0

  1
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage akijibu moja ya maswali yaliyoelekezwa kwenye wizara yake katika kipindi cha maswali na majibu Januari 30,2015  Bungeni mjini Dodoma.
  2
  Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene akijibu swali  Bungeni mjini Dodoma.
  3
  Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dkt. Pindi Chana akijibu maswali kutoka kwa wabunge  mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
  4
   Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akitoa maelezo wakati wa kipindi cha maswali na majibu Bungeni mjini Dodoma.
  5
   Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi akitoa kauli ya Serikali kuhusu Mkakati wa Serikali wa Kutatua Changamoto za Soko la Sukari nchini,  Bungeni mjini Dodoma.
  6
  Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Susan Lyimo akichangia hoja ya Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC), Kamati ya Bajeti na Kamati Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC)  Bungeni mjini Dodoma.
  7
  Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa (kushoto) akiteta jambo na Mbunge wa Kuteuliwa na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia,  Bungeni mjini Dodoma.
  8
  Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Ester Bulaya akichangia hoja ya ya Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC), Kamati ya Bajeti na Kamati Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC) jana Bungeni mjini Dodoma.
  9
  Mbunge wa Mkanyageni Mohamed Habibu Mnyaa akichangia hoja Bungeni mjini Dodoma wakati wa kuchangia hoja za Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC), Kamati ya Bajeti na Kamati Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC).
  10
  Baadhi ya wageni waliohudhuria kwenye ukumbi wa Bunge la Jamhuri bungeni mjini Dodoma.
  Picha zote na Hussein Makame-MAELEZO, Dodoma

  0 0

   Chipukizi wa Chama Cha Mapinduzi wakiwa katika mazoezi ya gwari, karate na halaiki kwenye Uwanja wa Majimaji Mjini Songea, leo wakati wa maandalizi ya maadhimisho ya miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM yanayofanyika kitaifa kesho Mkoani Ruvuma ambapo mgeni rasmi atakuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

   Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, baada ya kukagua mazoezi ya halaiki ya Chipukizi wa CCM.
   Mmoja wa Chipukizi akiwa amebebwa baada ya kuzimia akifanya mazoezi ya gwaride
   Bendi ya Vijana wa CCM kutoka Zimbabwe ikiongoza mazoezi ya gwaride

  Mkurugenzi wa TOT John Komba akizungumza na bendi ya vijana wa CCM kutoka Zanzibar

  0 0

  1
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Elimu Zanzibar (ZEDO) Ussi Said Suleiman akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Social Media huko Chuoni kwao Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar.
  2
  Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis (alie simama) akiwahutubia washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya matumizi ya Mitandao ya kijamii (Social Media), hawapo pichani yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Elimu Zanzibar kwa kushirikiana na Kigamboni Community Centre KCC kutoka Dar es Salam, huko Chuoni kwao Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar.
  3
  Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakimskiliza Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis (hayupo pichani).  
  4
  Mgeni rasmin Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis (wakatikati) waliokaa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya matumizi ya Mitandao ya kijamii (Social Media). Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar.

  0 0

   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akilakiwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Songea, jioni ya leo tayari kushiriki maadhimisho ya miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM yanayofanyika kitaifa kesho Mkoani Ruvuma ambapo mgeni rasmi atakuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete.Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.PICHA NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
   Pinda akiwapungia mkono wananchi na wana CCM waliofika kumlaki uwanjani hapo
   Vikundi vya sanaa vikitumbuiza wakati wa mapokezi ya Pinda, Kinana na Philip Mangula


  0 0

  Katibu tawala wa mkoa wa Kilimanjaro Seveline Kahitwa akiwa ameshika bendera kuashiria uzinduzi wa msimu wa 13 wa mbio za kimataifa za Kilimanjaro Marathoni,Uzinduzi uliofanyika Hotel ya Kibo Homes,Wengine ni Viongozi katika kampuni ambazo zimejitokeza kudhamini mbio hizo
  Katibu tawala wa mkoa wa Kilimanjaro Seveline Kahitwa akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa msimu wa 13 wa mbio za kimataifa za Kilimanjaro Marathoni,Uzinduzi uliofanyika Hotel ya Kibo Homes,
  Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager Pamela Kikuli ambao ndio wadhamini wakuu wa Mbio za Kilimanjaro Marathoni 2015 ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa msimu wa 13 wa mbio hizo uliofanyika Hotel ya Kibo Homes mjini Moshi.
  Baadhi ya wageni walikwa katika uzinduzi wa msimu wa 13 wa Mbio za Kilimanjaro Marathoni uliofanyika mjini Moshi.
  Mkurugenzi wa Kanda ya kaskazini wa kampuni ya Tigo Tanzania ,David Charles ambao ndio wadhamini wa Mbio za Kilimanjaro Marathoni kilometa 21 akizungumza wakati wa uzinduzi wa mbio hizo uliofanyika mjini Moshi.
  Meneja Mauzo wa Kampuni ya Mafuta na vilainishi GAPCO ,Caroline Kakwezi ambao ndio wadhamini wa mbio za watu wenye ulemavu akizungumza wakati wa uzinduzi wa mbio hizo.
  Mwenyekiti wa chama cha riadha mkoa wa Kilimanjaro (KAA) Liston Methacha akizungumza wakati wa hafla ya fupi ya uzinduzi wa msimu wa 13 wa mbio za Kilimanjaro Marathoni.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kibo Palace Hotels na Kibo Homes ,Vicent Lasway akizungumza wakati wa uzinduzi wa mbio hizo uliofanyika katika Hotel ya Kibo Homes.
  Wanariadha toka klabu ya riadha ya Holili wakifuatilia uzinduzi hhuo.

  Baadhi ya viongozi walioalikwa katika uzinduzi wa mbio hizo.
  Mkurugenzi wa kampuni ya ExecutiveSolution ,Aggrey Mareale akitoa maelezo mafupi kuhusiana na mbio za Kilimanjaro Marathoni ambazo zimeingia msimu wa 13 ,zitakazofanyika mwezi wa tatu mwaka huu.
  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya kaskazini.

  0 0

  Hatimaye kesho fainali ya Proin Women Taifa Cup itafanyika katika uwanja wa Azam Complex Chamanzi kwa kuzikutanisha timu za Pwani na Temeke huku Mshindi wa Kwanza katika Michuano hiyo ataondoka na Kitita cha Shilingi za Kitanzania Milioni 3 huku mshindi wa Pili akiondoka na Milioni 1 na Mshindi wa Tatu akiondoka na Kitita cha Milioni 1.
  Mashindano ya Women Taifa Cup ni mashindano ya kwanza kufanyika Nchini Tanzania huku yakiwa yamedhaminiwa na Kampuni ya Proin Promotions na Azam.
  Katika fainali hiyo mashabiki wataingia Bure huku mechi hiyo ikirushwa live na Azam TV.
  Mgeni rasmi katika Fainali hiyo ni Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mh Dkt Fenella Mukangara ambae atafunga mashindano hayo katika dimba la Azam Complex ambapo mechi hiyo ya fainali itaanza kutimua vumbi saa 10:15 Jioni huku Jonesia Rukyaa refarii mwenye beji ya fifa ndiye atakepuliza kipenga akisaidiwa na Hellen Mduma, Agness Alphonce na Mwanahamisi Matiku huku kamisaa wa fainali hiyo anatarajiwa kuwa Ingridy Kimaro.
  Katika Mechi ya Kumtafuta mshindi wa tatu timu ya Ilala itamenyana na Kigoma ambapo mchezo huo utaanza saa 8 Mchana. 

  0 0

   Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli amekagua barabara mkoani Mbeya na kuahidi ujenzi wa kiwango cha lami, barabara ya Mpemba-Isongole yenye urefu wa KM 58 Wilayani Ileje.

  Akizungumza mara baada ya kufungua sehemu ya barabara ya lami wilayani humo kati ya Isongole hadi Itumba KM 9, Waziri Magufuli amesema Serikali itaijenga kwa kiwango cha lami barabara ya Mpemba-Itumba KM 58, ili kufungua fursa za uchumi wilayani Ileje na kuhakikisha barabara hiyo inaungana na nchi ya malawi kwa lami na kuhuisha sekta ya uchukuzi na biashara baina ya nchi hizo.

  “Barabara ya lami ni muhimu kujengwa katika Wilaya ya Ileje ili kukuza uchumi wa wananchi ambao wana mazao mengi yanayohitaji usafiri wa uhakika kufikia masoko”, amefafanua Dkt. Magufuli.

  Waziri Magufuli amezungumzia umuhimu wa kuiunganisha Wilaya ya Ileje na mtandao wa barabara unaoanzia Bukoba –Biharamulo- Uvinza-Mpanda-Sumbawanga-Tunduma-Mpemba-Isongole hadi Chitipa nchini Malawi ambapo ikikamilika kwa lami itafungua ukanda muhimu wa biashara na kukuza uchumi wa nchi.

  Amehimiza umuhimu wa Wilaya ya Ileje kutumia fedha za mfuko wa barabara kujenga barabara za lami ili kurahisisha huduma za usafiri na kuvutia wataalam wengi kufanyakazi na kuishi wilayani humo. “Hakikisheni mnafanyakazi kwa umoja na mshikamano kwa kuepuka majungu na rushwa ili mfikie malengo na mwaka huu tutawapa shilingi milioni 721 kwaajili ya barabara”, amesisitiza Waziri Magufuli.

  Awali Waziri Magufuli alikagua mizani ya Mpemba wilayani Momba na kuhimiza wafanyakazi wa mizani hiyo kufanyakazi kwa weledi na uadilifu kwa kuzingatia elimu walizonazo na hivyo kujiepusha na vitendo vya rushwa ili kutenda haki kwa wasafirishaji na kulinda barabara zinazojengwa kwa gharama kubwa.

  Naye Katibu mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Musa Iyombe amesema barabara ya Mpemba hadi Isongole itakayojengwa kwa kiwango cha lami ilikuwa barabara ya Wilaya lakini kutokana na umuhimu wake Serikali imeipandisha hadhi kuwa ya mkoa na tayari upembuzi yakinifu kuhusu ujenzi wa barabara hiyo umekamilika.

  Naye mkuu wa wilaya ya Ileje Rosemary   Sinyamule amemhakikishia Waziri Magufuli kuwa Wilaya hiyo ina upungufu wa barabara za lami hivyo ujenzi wake utavutia watumishi kuishi na kufanya kazi katika wilaya hiyo inayopakana na nchi za Malawi na Zambia na kuhuisha fursa za uchumi zilizomo wilayani humo.

  Zaidi ya KM 11,154 za barabara za lami zinajengwa nchini kote ambapo inatarajiwa hadi mwishoni mwa mwaka huu Tanzania itakuwa na jumla ya barabara  za lami zenye urefu wa KM 18,000  zinazounganisha mikoa na nchi jirani.

  Imetayarishwa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wizara ya Ujenzi

  0 0

  2
  Mwenyekiti wa Kamati ya Viongozi wa Afrika Juu ya mabadiliko ya Tabia nchi(The Committee of African Heads of State and governments on Climate change) Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimakabidhi nakala ya Ripoti ya utendaji mwenyekiti mpya wa kamati hiyo Rais wa Misri Abdel Fattah el Sisi wakati wa Mkutano wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika uliofanyika Addis Ababa Ethiopia.Rais Kikwete alipongezwa kwa kuiwezesha kamati hiyo kupata mafanikio makubwa. (picha na Freddy Maro).1
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn muda mfupi kabla ya kumalizika kwa mkutano wa 23 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika ulifanyika katika mji Mkuu wa Ethiopia Addis Ababa,


  0 0

  Mtaalam wa TEHAMA kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Rajab Sollo akiwaonesha watendaji wa Baraza hilo (Hawako pichani) kuhusu namna mfumo wa kanzidata ya kuhifadhi kumbi za Starehe na Burudani unavyofanya kazi kwenye mafunzo ya siku mbili yaliyofanyika mwishoni mwa wiki hii makao ya BASATA yaliyo Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam.
  Mtaalam wa IT kutoka BASATA Bwana Sollo (anayeonekana kwa mbele) akitoa mafunzo kwa watendaji wa BASATA kuhusu kanzidata ya kuhifadhi kumbi za Starehe na urudani nchini.
  Sehemu ya watendaji waliohudhuria mafunzo hayo wakimfuatilia kwa makini Mkufunzi wa TEHAMA kutoka BASATA Bw. Rajab Sollo.


  0 0

  KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) ilikutana Dar es Salaam Jumatano iliyopita na kujadiliana kuhusu masuala mbalimbali.    
   
  A; Media Day
   
  Kamati ya Utendaji imepanga bonanza maalum ambalo linaandaliwa na TASWA likihusisha waandishi wa habari na wafanyakazi wa vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini lifanyike Aprili 25 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
   
  Kila mwaka TASWA imekuwa ikiandaa bonanza hilo, lakini mwaka jana kutokana na sababu mbalimbali lilishindwa kufanyika, kwa kuzingatia hilo TASWA imeamua bonanza la mwaka huu liwe la aina yake na la kihistoria likihusisha waandishi wa habari na wafanyakazi wa vyombo vya habari wasiopungua 2,000.
   
  Waandishi wa habari za afya, siasa, uchumi, michezo, mazingira na nyinginezo pamoja na wafanyakazi wa vyombo mbalimbali watapata fursa ya kukaa pamoja na kujadili masuala mbalimbali yanayowahusu na kisha kuburudika kwa pamoja.
   
  Tayari kamati maalum imeteuliwa na ishaanza kazi kwa ajili ya maandalizi ya bonanza hilo na mapendekezo lifanyike katika maeneo yenye fukwe nzuri. TASWA inawaomba wadau mbalimbali washirikiane nao katika kudhamini bonanza hilo kubwa.
   
  B; Wanachama wapya AIPS
  TASWA ni mwanachama hai wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo cha Kimataifa (AIPS) chenye makao yake makuu Lausanne, Uswisi.
  Lakini idadi wa wanachama wa TASWA ambao pia ni wanachama wa AIPS kwa hapa nchini ni ndogo sana,  hivyo AIPS tayari kwa mwaka huu imeanza kuchukua wanachama wapya wanaotaka kujiunga na chama hicho.
   
  Mfumo unaotumika kujiunga na AIPS ni wa njia ya mtandao, ambapo kwa wanaotaka kupata kadi hiyo wafungue tovuti ya AIPS ambayo ni: http://www.aipsmedia.com, kisha ukishafunguka utaona upande wa kushoto maandishi makubwa AIPS CARD bofya hapo na utafuata maelekezo rahisi sana.
   
  Wale ambao watamaliza taratibu za kujisajili ili kupata uanachama huo wataelekezwa wawasiliane na uongozi wa TASWA kwa ajili ya hatua inayofuata ambayo ni malipo ya dola 15 za Marekani na utaratibu wa kupatiwa kadi hiyo.TASWA inawahimiza wanachama wake mmoja mmoja kuchukua uanachama wa AIPS, kwani una faida nyingi maana AIPS mara kwa mara imekuwa ikitoa nafasi za mafunzo kwa wanachama wake na semina za michezo mbalimbali.Wanaopenda kujiunga wafanye hivyo kabla ya Februari 15 mwaka huu ili utaratibu wa kutuma fedha hizo ufanyike haraka, kisha kadi nazo zitumwe kwa wakati.
   
  C: Mafunzo
   
  Kamati ya Utendaji imeiagiza sekreterieti ya TASWA ifanye kila iwezalo kwa kuzungumza na wadau mbalimbali hadi kufikia Juni mwaka huu iwe imeandaa angalau semina tatu kwa wanachama wake, ili kuboresha uwezo wa namna ya kuripoti michezo mbalimbali hasa kwa waandishi chipukizi.
   
  Semina hizo ya kwanza iwe ya waandishi wa habari chipukizi, waandishi wa ngazi ya kati, na semina nyingine ihusishe wahariri wa habari za michezo pamoja na waandishi wa siku nyingi nchini.
   
  Suala hili lilitiliwa mkazo mkubwa na wapo wadau ambao wameonesha nia ya kusaidiana na TASWA kuwaweka sawa waandishi wa habari za michezo nchini, tunaamini mambo yataenda kama yalivyokusudiwa.
   
  Nawasilisha,
   
  Amir Mhando
  Katibu Mkuu TASWA
  01/02/2015
  0713-415346

  0 0

  Mwenyekiti wa Chama Tawala cha CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na maelfu ya wananchi wakati akiingia katika uwanja wa MajiMaji mjini Songea leo kuongoza kilele cha sherehe za kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM.
  Mwenyekiti wa Chama Tawala cha CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa viongozi mbali mbali wa CCM wakati akiingia katika uwanja wa MajiMaji mjini Songea leo kuongoza kilele cha sherehe za kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM.
  Mwenyekiti wa Chama Tawala cha CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na UVCCM katika uwanja wa MajiMaji mjini Songea leo katika kilele cha sherehe za kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM.


older | 1 | .... | 451 | 452 | (Page 453) | 454 | 455 | .... | 1896 | newer