Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 446 | 447 | (Page 448) | 449 | 450 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Karibu katika mahojiano kati ya Mubelwa Bandio na Jhiko Manyika a.k.a JhikoMan aliyejiunga nasi moja kwa moja kutoka Bagamoyo Tanzania
  Alizungumzia wimbo wake mpya wa Africa Arise, ambao amemshirikisha Peter Morgan wa kundi la  Morgan Heritage.

  Amezungumza mengi kuuhusu
  Karibu usikilize hapa chini

  Pia unaweza kurejea mahojiano kati yao wakati JhikoMan akiwa ziarani Ulaya mwaka 2014. Alizungumza mengi kuhusu muziki wa reggae Tanzania lakini pia aligusia "projects" mbalimbali ambazo ziko njiani kuja

  0 0


   Wanafunzi wa shule ya sekondari Kiteto mkoani Manyara wakionesha vitabu baada ya kukabidhiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel chini ya mradi wake wa "Airtel shule yetu" wenye lengo la kuchangia katika sekta ya elimu nchini.
  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imepiga jeki jitihada za serikali za kuhamasisha masomo ya sayansi kwa kutoa msaada wa vitabu vya sayansi kwa shule ya sekondari ya Kiteto iliyopo mkoani Manyara.

  Msaada huo wenye thamani ya shilingi milioni 1.5 unahusisha vitabu vya fizikia, hisabati, baiolojia na kemia kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma masomo hayo katika shuleni hiyo.

  Akipokea msaada huo Diwani wa kata ya Central wilayani Kiteto Mh Yahya Masumbuko, amesema shule nyingi wilayani hapo zimekuwa zikikabiliwa na changamoto ya upungufu wa vitabu vya masomo ya sayansi licha ya kwamba kuna uhaba pia wa walimu wa masomo hayo.

  “Ni kweli kwamba uhaba wa vitabu unakwamisha kwa kiasi kikubwa wanafunzi kujifunza kwa ufasaha masomo ya Sayansi wilayani Kiteto hali inayorudisha nyuma ukuaji wa elimu ya sayansi wilayani hapa”. Alisema Mh Masumbuko.

  “Uhaba wa vitabu ni moja ya changamoto, lakini uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi pia ni kikwazo kikubwa kwa utoaji wa elimu ya sayansi kwa wanafunzi wetu hapa wilayani” aliongeza Mh Masumbuko.
  Aidha Diwani huyo ameishukuru kampuni ya simu ya Airtel  kwa kuona umuhimu wa kuboresha masomo ya sayansi ambayo  ufaulu wake umekuwa mdogo hali ambayo inayotoa fursa kwa wanafunzi kujifunza kwa umakini zaidi.

  “Msaada huu utaongeza hamasa kwa wanafunzi wetu kujifunza masomo ya sayansi hivyo tunawashukuru sana Airtel kwa kuona umuhimu wa kusaidia shule hii na hasa vitabu vya sayansi” alieleza Mh Masumbuko.
  “Sisi wa Kiteto tunaendelea na jitihada za kuhakikisha wanafunzi wetu wanajifunza masomo hayo na ndio maana hata mgao wa walimu tulioupata tumeuelekeza katika ufundishaji wa masomo ya Sayansi. Alimalizia Mh Masumbuko. 

  Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Kiteto wameishukuru kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kuwawezesha kupata vitabu vitakavyowasaidia katika masomo yao.
  Msaada huo wa vitabu vya masomo ya hisabati,kemia,fizikia na Bailojia utasaidia kupunguza uhaba wa vitabu vya sayansi kwenye shule hiyo ya wilayani Kiteto mkoani Manyara.

  Airtel shule yetu ni mpango endelevu uliodumu kwa takribani miaka 10 iliyopita mpaka sasa zaidi ya shule za sekondari 1300 nchini zimeidika na msaada wa vitabu chini ya mradi huu. Tutaendelea kushirikiana na serikali chini ya wizara ya elimu katika kuhakikisha tunaboresha sekta ya elimu na kutoa kipaombele kwenye masomo ya sayansi ili kuwa na wanasayansi wengi nchi ambao kwa sasa ni changamoto katika shule nyingi na nchi kwa ujumla alisema Meneja mauzo wa Airtel kanda ya kati Bwana  Hendrick Bruno

  0 0

  SAM_0796
  Vyombo vya habari nchini vimehimizwa kuwasilisha masuala yanayowahusu watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu. Akizungumza na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali jijini Arusha katika warsha juu ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU iliyoendeshwa na shirika liliso la kiserikali la The Foundation For Tomorrow (TFFT).
   
  Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania wa shirika hilo, Bwa. Kennedy Oulu alisema tatizo la watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu nchini Tanzania ni gumu, hivyo vyombo vya habari havina budi kuifahamisha jamii kuhusu hili suala na matatizo yanayowakabili watoto yatima na waishio katika mazingira magumu ili jamii na wadau mbalimbali waweze kushiriki vema katika kukabiliana na tatizo hili.
   
  “Kwa sasa, inakadiriwa kuwa kuna watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu wapatao 1,800,000 hapa Tanzania pekee, huku 1,300,000 kati yao wakiwa wametokana na athari za ugonjwa wa UKIMWI. Mgawanyo wa kifamilia na muundo wa kimsaada kijamii ni moja ya vinavyochangia tatizo hili. Vinapoongezwa katika umaskini unaojidhihirisha katika: ukosefu wa upatikanaji wa huduma za elimu ikiwemo elimu ya awali, ukosefu wa upatikanaji wa huduma za afya na uzalishaji kama afya ya uzazi, ukosefu wa stadi za maisha zinazoakisiwa katika mitaala ya shule zenye uwezo unaotakiwa na ubunifu ili kujenga uwezo wa watoto, si kwa yatima na waishio katika magumu pekee”. Alisema Kennedy na kuongeza.
   
  “Ni muhimu kutambua kuwa kumekuwa na hatua na mafanikio yaliyofikiwa na wadau mbalimbali ikiwemo serikali katika kuwezesha upatikanaji, kuzijengea uwezo familia za watoto hawa na kubadili mitazamo ya jamii dhidi ya watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu, hii inajenga msingi wa mwitikio endelevu.

  Kwa upande wake, shirika la The Foundation For Tomorrow limekuwa likilishughurikia tatizo hili kwa njia mbalimbali. Shirika hili hutumia njia anuai ambazo hupunguza uhitaji wa watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu kwa kuzijengea uwezo wa kiuchumi kaya zao hususani zile kaya maskini kupindukia, kutoa msaada wa kugharamia masomo ili kuwahakikishia upatikanaji wa elimu, kutoa bima za afya kwa wanafunzi yatima na wale waliotoka katika mazingira magumu, kuwajengea uwezo walimu na kuwezesha stadi za maisha kwa njia ya kuboresha mtaala.

  Bwa. Oulu amesema juhudi hizi pamoja na sauti za watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu zinapaswa kufahamika. “Changamoto za hawa watoto na mitazamo yao hutusaidia kutambua njia iliyo bora ya kulinda maisha yao. Hizo pia hutuwezesha kutambua kuwa kwa kiasi kikubwa sote tunalo jukumu la kubadili vile tunavyowachukia hawa watoto kutoka katika kudharauliwa na badala yake kuwa katika ufahamu kuwa sababu ya hali hizo na magumu yaliyopo ndiyo matatizo tunayoyashughurikia Tanzania yote: elimu, afya, umaskini, kaya na kufikia fursa zilizopo.”
   
  Inapaswa kuoneshwa ya kwamba hali hii lazima ionwe kuwa si ya kudumu wakati hatua zinazochukuliwa, kujenga kipato baina ya kaya maskini, kuwezesha upatikanaji wa mahitaji na kulinda haki na ulinzi kwa watoto, hususani kwa kuwahakikishia elimu bora na ushiriki wao usio na kikomo ni muhimu katika kutokomeza tatizo hili.
   
  Bwa. Oulu aliongeza kuwa “Uandishi wa habari wa kiuchunguzi na uwasilishaji mambo wenye malengo, suluhisho, utendaji bora na juhudi zilizoshindwa ndivyo vitaiwezesha jamii kujua ni njia gani bora ya kusaidia, kuitikia na kudumisha juhudi na fursa za kuwaondoa watoto yatima na wale wasiojiweza kutoka katika janga hilo. Inapaswa ioneshwe kuwa watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu pamoja na wanaowahifadhi na kaya zao wanayo hatua kubwa ya kuchukua.”

  Sambamba na hilo, msimamizi wa warsha hiyo Bwa. Augustine Zacharia alivishauri pia vyombo vya habari kuzingatia ni jinsi gani habari zinazotolewa katika vyombo vyao huwaathiri watoto hawa kwa upande chanya na hasi. Masuala yahusuyo watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu yanapaswa kuwasilishwa katika namna ambayo huwajenga na kuwa katika mtazamo wa kutafuta suluhisho la tatizo. Licha ya kuwa kuna uhuru wa kutoa na kupokea habari, lakini namna ambavyo habari hizi huwasilishwa, zinapaswa kwanza kuzingatia kuwa haki za watoto hazivunjwi.


  SAM_0767
  Meneja wa ushirikiano wa The Foundation For Tomorrow Bw.Anton Asukile akiwa anatoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari katika semina ya siku moja juu ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU iliyoandaliwa na shirika hilo  kwa waandishi wa habari Mkoa wa Arusha iliyofanyika katika ukumbi wa Olasiti Garden jijini Arusha
  SAM_0747
  Mwezeshaji wa Semina juu ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU Bw.Zachariah A.Babu akiwa anatoa maelekezo kwa waandishi wa habari juu ya Haki ya watoto
  SAM_0772
  Meneja wa mafunzo ya walimu wa shirika la The Foundation For Tomorrow Bi.Melissa Queyquep akiongea katika warsha juu ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU iliyoandaliwa na shirika hilo
  SAM_0751
  Mwenyekiti wa Arusha press club, Claud Gwandu
  SAM_0745
  Mwandishi mwandamizi wa kituo cha Redio 5 David Rwenyagira akiwa anafwatilia mafunzo
  SAM_0742
  Waandishi wakiwa wanafatilia sema juu ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la The Foundation For Tomorrow kulia ni Daniel Lucas mhariri wa Safina Redio na Merry Mwita kutoka gazeti la Mtanzania
  SAM_0749
  Kulia ni Queen Lema wa gazeti la Majira,Rose Jackson wa gazeti la jambo leo wakiwa katika semina hiyo
  SAM_0743
  Waandishi kutoka Habari Maalum Media Arusha,kulia ni Daniel Magulu na Edith Laizer
  SAM_0768
  Kushoto ni Jamillah Omar wa chanel Ten katikati Happy Lazaro wa mwananchi na Cynthia Mwilolezi wa gazeti la Nipashe
  SAM_0771
  SAM_0770
  Kushoto Lilian Joel wa gazeti la Uhuru na Elia Mbonea wa gazeti la Mtanzania
  SAM_0761
  Mwezeshaji wa Semina juu ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU Bw.Zachariah A.Babu akiwa anasisitiza jambo
  SAM_0787
  Waandishi mwandamizi Jamillah Omar wa chanel Ten akiwa anapokea cheti kutoka kwa Meneja wa mafunzo ya walimu wa shirika la The Foundation For Tomorrow Bi.Melissa Queyquep baada ya kuhudhuria semina ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU iliyoandaliwa na shirika hilo jijini Arusha
  SAM_0793
  Mwandishi mwandamizi wa kituo cha Redio 5 David Rwenyagira akiwa anapokea cheti kutoka kwa Meneja wa mafunzo ya walimu wa shirika la The Foundation For Tomorrow Bi.Melissa Queyquep baada ya kuhudhuria semina ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU iliyoandaliwa na shirika hilo jijini Arusha
  SAM_0764
  Mwandishi kutoka Habari Maalum Bi.Edith Laizer akiwa anachangia katika semina hiyo
  SAM_0773
  Mwandishi mwandamizi Queen Lema wa gazeti la Majira akiwa anapokea cheti kutoka kwa Meneja wa mafunzo ya walimu wa shirika la The Foundation For Tomorrow Bi.Melissa Queyquep baada ya kuhudhuria semina ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU iliyoandaliwa na shirika hilo jijini Arusha
  SAM_0794
  Mmiliki wa mtandao wa kijamii wa libeneke la kaskazini Woinde Shiza akiwa anapokea cheti kutoka kwa Meneja wa mafunzo ya walimu wa shirika la The Foundation For Tomorrow Bi.Melissa Queyquep baada ya kuhudhuria semina ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU iliyoandaliwa na shirika hilo jijini Arusha
  SAM_0779
  Mmiliki wa mtandao wa kijamii http://jamiiblog.co.tz/ Pamela Mollel akiwa anapokea cheti kutoka kwa Meneja wa mafunzo ya walimu wa shirika la The Foundation For Tomorrow Bi.Melissa Queyquep baada ya kuhudhuria semina ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU iliyoandaliwa na shirika hilo jijini Arusha
  SAM_0790
  Mwandishi wa Star TV Magessa Magessa akiwa anapokea cheti kutoka kwa Meneja wa mafunzo ya walimu wa shirika la The Foundation For Tomorrow Bi.Melissa Queyquep baada ya kuhudhuria semina ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU iliyoandaliwa na shirika hilo jijini Arusha
  SAM_0791
  Mwandishi wa mambo jambo redio Rotilinde Achimpota akiwa anapokea cheti kutoka kwa Meneja wa mafunzo ya walimu wa shirika la The Foundation For Tomorrow Bi.Melissa Queyquep baada ya kuhudhuria semina ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU iliyoandaliwa na shirika hilo jijini Arusha
  SAM_0784
  Mwandishi Peter Saramba wa Mwananchi akiwa anapokea cheti kutoka kwa Meneja wa mafunzo ya walimu wa shirika la The Foundation For Tomorrow Bi.Melissa Queyquep baada ya kuhudhuria semina ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU iliyoandaliwa na shirika hilo jijini Arusha
  SAM_0783
  Mwandishi kutoka gazeti la habari Leo Veronica Mheta akiwa anapokea cheti kutoka kwa Meneja wa mafunzo ya walimu wa shirika la The Foundation For Tomorrow Bi.Melissa Queyquep baada ya kuhudhuria semina ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU iliyoandaliwa na shirika hilo jijini Arusha
  SAM_0782
  Cynthia Mwilolezi wa gazeti la Nipashe akiwa anapokea cheti kutoka kwa Meneja wa mafunzo ya walimu wa shirika la The Foundation For Tomorrow Bi.Melissa Queyquep baada ya kuhudhuria semina ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU iliyoandaliwa na shirika hilo jijini Arusha
  SAM_0775
  Elia Mbonea kutoka Mtanznia akiwa anapokea cheti kutoka kwa Meneja wa mafunzo ya walimu wa shirika la The Foundation For Tomorrow Bi.Melissa Queyquep baada ya kuhudhuria semina ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU iliyoandaliwa na shirika hilo jijini Arusha
  SAM_0776
  Rose Jackson wa Jambo Leo akiwa anapokea cheti kutoka kwa Meneja wa mafunzo ya walimu wa shirika la The Foundation For Tomorrow Bi.Melissa Queyquep baada ya kuhudhuria semina ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU iliyoandaliwa na shirika hilo jijini Arusha
  SAM_0777
  Daniel Lucas mhariri wa Safina Redio akiwa anapokea cheti kutoka kwa Meneja wa mafunzo ya walimu wa shirika la The Foundation For Tomorrow Bi.Melissa Queyquep baada ya kuhudhuria semina ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU iliyoandaliwa na shirika hilo jijini Arusha
  SAM_0788
  Mwakilishi kutoka Habari Maalum Daniel Magulu akiwa anapokea cheti kutoka kwa Meneja wa mafunzo ya walimu wa shirika la The Foundation For Tomorrow Bi.Melissa Queyquep baada ya kuhudhuria semina ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU iliyoandaliwa na shirika hilo jijini Arusha
  SAM_0785
  Mwakilishi kutoka Habari Maalum Edith Laizer akiwa anapokea cheti kutoka kwa Meneja wa mafunzo ya walimu wa shirika la The Foundation For Tomorrow Bi.Melissa Queyquep baada ya kuhudhuria semina ya HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU iliyoandaliwa na shirika hilo jijini Arusha
  SAM_0795
  Mwenyekiti wa Arusha press club, Claud Gwandu  akitoa neno la shukrani kwa shirika hilo kuandaa semina kama hiyo kwa waandishi wa habari


  0 0

  Na Miza Othman -Maelezo Zanzibar.

  Waziri wa  Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Zainab Omar Mohammed amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kipindi chote cha utekelezaji wa awamu ya saba imejipanga vizuri katika suala zima la kukarabati na kuzifanyia matengenezo makubwa Nyumba za Wazee zilizopo Sebleni  Unguja na Limbani kwa  Pemba.

  Ameyaeleza hayo katika kikao cha Baraza la Wawakilishi, Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibzr wakati alipokuwa akijibu Suala la Mh.Jaku Hashim Ayoub alietaka kujua mpango wa Serikali  wa kuyakarabati majengo hayo ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea.

  Amesema Wizara yake tayari imeshazifanyia matenganezo makubwa nyumba mbili, Ukumbi  uliop nyumba za  wazee Sebleni na kujenga ukuta uliozunguuka eneo lote la Nyumba hizo.

  “Serikali imefanya ukarabati  mkubwa  wa miundombinu ya maji na umeme ili kuhakikisha Wazee wanapata huduma hiyo bila ya matatizo”, aliongeza Waziri Zainab.

  Aidha  amesema Serikali imeamuwa kuwapatia  wazee milo mitatu kwa siku na kuwapatia posho la shilingi Arubain Elfu (40,000/=) kwa ajili ya matumizi yao madogo madogo, chakula na posho hizo hutolewa sawa kwa wazee wote waliopo Sebleni na Limbani Pemba.

  Hata hivyo ameeleza kuwa kwa upande wa nyumba za wazee za Limbani-Pemba, Wizara tayari imeshachukuwa hatuwa ya kuandaa makisio ya matengenezo yote yanayo hitajika ikiwemo kujenga uzio pamoja na kuzifanyia ukarabati nyumba na kujenga miundo mbinu mipya ya maji na umeme.

  “Kinacho subiriwa hivi sasa ni kupata fedha kwa ajili ya mradi huo, nia ya Serikali ni kuzifanyia ukarabati nyumba zote za Sebleni na Limbani ili kuwaweka wazee wetu katika mazingira yaliyo bora zaid na kujenga ustawi wao kwa jumla”, alisisitiza Waziri.

  Aidha amesema suala la kuwapati vipando wahudumu wa nyumba hizo   ikiwemo vespa na baskeli viko katika bajeti ya Wizara yake na wakati wowote wakipata fedha suala hilo litatekelezwa kwa kila anaestahiki kupatiwa usafiri wa aina hiyo ili kuleta ufanisi wa kazi zao.


  0 0

  Watumiaji wa simu za mkononi wameendelea kukua  kadri siku zinavyo endelea na kumekua na maswali mengi jinsi gani mtu anaweza kubaki salama atumiapo simu za mkononi.
   
  Hapa nitaangazia uhalifu mtandao unao ambatana na simu za mikononi na njia za matumizi salama ya simu za mkononi.Nianze kuangazia uhalifu unaoweza kusababishwa na simu za mkononi.

  Swapping:Huu ni uhalifu mtandao unao kua kwa kasi hivi sasa maeneo mbali mbali unaotoa fursa kwa mhalifu mtandao kuwa na matumizi ya simu ya mtu bila ya mwenye simu kujua. Mara nyingi wahalifu mtandao wana lenga kuiba pesa au kuwasiliana na watu wa karibu wa mtumiaji halisi wa simu ya mkononi kwa sababu tofauti tofauti.

  Hii inatokea pale mhalifu mtandao anapo kua amepata namba yako ya simu na kusoma  ratiba yako hasa muda gani unakua hauna matumizi makubwa na simu – Baada ya kujua hivyo kupitia programu zilizopo sasa zina mpa fursa kukutoa hewani na kuanza kuitumia namba yako ya simu  ambapo anaweza kufanya mengi baada ya kua na umiliki huo ikiwa ni pamoja na kutoa au kuhamisha pesa zako na pia kuitumia vibaya simu yako.

  Shoulder surfing:Hii ni njia inayotumika na wahalifu mtandao kuweza kujua namba za siri anazotumia mmiliki wa simu kwa kuangalia pale mtumiaji wa simu anapofanya miama ya kifedha kupitia simu au kufungua simu yake.

  Mhalifu baada ya kupata taarifa hizo anaweza kukwapua simu hiyo na kuitumia vibaya kwani tayari Alisha jua namba za siri unazotumia na pia kuweza kufanya miamala na simu hiyo. Inashauriwa kuwa makini sana uwekapo namba za siri kwenye simu yako kwa kuhakikisha hakuna anayeweza kutazama ufanyacho kupitia simu yako.

  Mobile Keyloggers:kwa sasa kumekua na mtindo wa namba tofauti tofauti kut umia wenzao link ambazo maranyingi zimeambatanishwa na program inayo toa ruhusa ya kuweza kujua kila kinachoandikwa na mtumiaji wa simu mara tu baada ya kufungua link hizo.
  Kwakufanya hivyo mtumiaji anaweza kuwa kila anacho andika mhalifu mtandao anakua anafatilia au kujua – uhaifu huu umekua ukiathiri zaidi simu za kisasa maaru kama Smart phones.

  Inashauriwa unapotumiwa message yenye kiambatanishi cha link kuwa makini hasa inapotoka kwa usiye mfahamu hii ni pamoja na ujumbe unaotumiwa kwenye programu ya WhatsApp.

  mSpy:Hii niaina moja wapo  ya program ambayo inampa fursa mhalifu mtandao kuweza kufatilia kila kifanyachwa na mtumiaji wa simu za mikononi. Inaweza kutoa fursa kwa mtumiaji wa simu ya mkononi kwa simu yake kugeuzwa kuwa kipaza sauti na hatimae aliye mbali kuweza kufatilia mazungumzo yoyote yanayofanya na mtumiaji wa simu hizo.

  Aina hii ya uhalifu umekua na uwezo mkubwa wa kuathiri simu za kisasa maarufu kama smart phones haza zile zinazotumia program za Androids. Ikumbukwe situ simu kubadilishwa kuwa kipaza sauti bali hata kuweza kufanya mambo mengi na mtu aliye mbali na simu yako.

  Inashauriwa kuhakiki unakua na simu yako mara zote na kutowapa usio wafahamu kwani program iayoweza kusababisha aina hii ya uhalifu inaweza tu kuanza kufanya uharibifu maara baada ya mhalifu kuweza kuiweka mikononi simu yako.

  Manythings:Hii ni program ambayo ni mpya kwa sasa inayotoa fursa kuzifanya simu za kisasa maarufu kama smart phones kutumika kama kamera za kiusalama “Security camera” Hii inaweza ikapelekea simu hizo kuwa na matumizi salama au mabaya inategemewa na mtumiaji.

  Matumizi sahihi, Imekua inatoa fursa kwa simu za kisasa zilizo pitwa matoleo yake kuendelea kuwa na matumizi kwani program hii inayotolewa  bure inatumiwa pale mtumiaji anapokua na simu mbili ya zamani asiyo itumia  na ya sasa anayo itumia.
  Simu hizo mbili zinawekwa program ambayo itamuwezesha mtumiaji kuweza kurekodi na kufatilia kwa karibu matukio yote anayo taka kuyafatilia kama ilivyo CCTV hivi sasa.

  Matumizi mabaya, Imesadikiwa kuwa wahalifu wanaweza kuingia na simu katika maeneo ambayo wanayafanyia uchunguzi na kuziacha simu hizo kwa kigezo cha kuzisahau huku wakirejea kwenye simu zao kuhakiki wanafatilia matukio yote yanayoendelea katika eneo husika bila ya kugundulika kirahisi – Hili tayari limeweza kujiri mara tu baada ya simu hizi za kisasa kuwezeshwa kurekodi matukio na mhusika kutumia simu yake mpya kufatilia akiwa mbali kabisa na eneo.

  Sasa Niangazie njia salama za matumizi ya simu za mikononi maarufu kama “best practice”

  Namba za siri:Simu za mikononi zimetoa fursa ya kuweka maneno ya siri wakati wa kufungua simu hizo na kwa watumiaji huduma mbali mbali mfano za utumaji wa pesa kupitia simu zao. Namba hizo za siri ili kubaki salama nimuhimu ukawa muangalifu kwa kutoweka mwaka wa kuzaliwa, namba zinazo fatana au namba yako ya simu.

  Kwakufanya hivyo utatoa ruhusa kwa mtumiaji asiye husika kuwa na uwezo mkubwa wa kubashiri kirahisi na kuweza kusababisha ma dhara kwa simu yako ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya na hata kufanya vitendo vya wizi wa pesa kupitia simu yako.

  Ujumbe mfupi wa maandishi:Kumekua na wimbi la wahalifu mtandao kupitia jumbe fupi za maandishi wanaomba taarifa binafsi za watu wakijitabulisha kama watu kutoka mabenki au sehemu nyingine. Unashauriwa kuwa makini sana na usitoe kabisa taarifa zako binafsi kwa Yule usie mjua kupitia ujumbe mfupi wa maandishi.

  Pia ina shauriwa kuto sambaza ujumbe wa maandishi usio kua na uhakika nao na unaoweza kusababisha taharuki kwa wasomaji wa ujumbe huo. Kwenye hili pia inashauriwa upatapo ujumbe mfupi wa maandishi kwa mtu asiye jitambulisha na wewe kumfaham kutompatia majibu.

  Weka simu yako karibu nawe muda wote: Ifahamike aina nyingi za uhalifu mtandao unaofanywa kupitia simu za mikononi unasababishwa na mtumiaji simu kuweka simu yake mbali na yeye au kuwaazima simu kwa asiye wafahamu.

  Kwenye hili nitoe kisa kifupi sana, Kuna Mhalifu mtando alienda kwenye kibanda cha kutolea pesa na wakati yuko katika jitihada za kutoa pesa alijifanya anampigia anayehitaji kumtumia pesa na mawasiliano kutokua mazuri.

  Baadae alimuomba mhudumu wa kibanda cha miamala ya kifedha kumpatia simu yake ya mkononi ili aweze kutumia huduma ya ujumbe mfupi wa maandishi. Baada ya kupatiwa simu alicho kifanya ni ku rekebisha orodha za namba ya simu na baadae mtumiaji mwingine aliyekua amewekewa namba zake pale kuanza kutuma jumbe akimtaka mwenye kibanda kuanza kuhamisha pesa akionekana kama bosi wake tukio ambalo lilipelekea kiasi kikubwa cha pesa kupotea na uhalifu huu kuripotiwa katika vyombo vya dola.

  Funzo hapo, Umakini wa kuwa karibu na simu yako muda wote na kuto waazima usie wajua simu yako unaweza kukuepushia matatizo mengi sana ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya simu yako na hata kupoteza pesa ulizo zi hifadhi katika simu yako.

  Kuwa makini sana na huduma ya “Bluetooth” pamoja na “Wireless”: Simu nyingi za kisasa zimekua zikitoa huduma hizi ili kurahisisha mawasiliano ya kusafirisha taarifa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa haraka bila gharama yoyote.

  Bahati mbaya unapo kua umeweka huduma hizi wazi muda wote zinaweza kupelekea mhalifu mtandao kuweza kudukua simu yako kirahisi na mara nyingine kukuwekea program hatarishi kwenye simu yako ya mkononi bila ya wewe kujua.

  Hii ina mabatana na wale wanao penda kutumia huduma za Wi-Fi zinazotolewa katika viwanja vya ndege au mikusanyiko ya watu. Huduma hii inapo chukuliwa kwenye simu ikumbukwe inatoa fursa kwa mhalifu mtandao kupitia “Man in the middle attack” kuweza kupata taarifa zako na kuzitumia atakavyo.

  Inashauriwa kuwasha huduma hizi za Bluetooth na Wireless pale tu unapokua na ulazima kuzitumia na kujiepusha kabisa kutumia huduma za Wi-Fi za bure pasi na ulazima hasa usafirishapo taarifa zako binafsi na za siri.

  Kua makini na program za simu:Imekua kawaida kwa watumiaji wa simu za kisasa kupakua program mbali mbali za simu katika simu zao na wakati mwingine hata zile wasizo kuwa na matumizi nazo.

  Ikumbukwe si program zote ni salama na wakati mwingine program unayo ipakua na kuiweka kwenye simu yako inaweza kua chanzo cha simu yako kudukuliwa na wahalifu mtandao.


  Inashauriwa kuwa makini sana na kila programu unayo  ipakua katika simu zako maarufu kama Mobile Apps na uwe natabia ya kuikagua kwa karibu pale unapokua na ulazima wa kuwa na program hiyo kwa kuangalia walio whi kuipakua wameitolea maoni gani.

  0 0

   Pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bw. Hiiti Sillo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano na waandishi wa habari katika kueleza maamuzi ya TFDA kufuta usajili na kubadili matumizi ya baadhi ya dawa nchini. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa TFDA Makao Mkuu

   Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imezifutia Usajili wa Dawa tano  za Binadamu kutokana na kuwepo makosa mbalimbali.         Hayo yameelewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi mkuu   TFDA Bwana Hiiti B.Sillo  Wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo alisema Mamlaka hiyo katika kupitia mifumo ya ufuatiliaji  wa usalama na ubora wa dawa nchini wamebaini uwepo wa dawa duni kwenye soko zenye madhara na zisizofaa kwa matumizi ya Binadamu.

           Mkurugenzi Mkuu alieleza kuwa TFDA imefikia hatua ya kufuta   usajili wa aina tano za dawa za binadamu ambazo ni Dawa ya kutibu “Fungus” ya vidonge na kapsuli aina ya ketocanazole kwa sababu dawa hiyo inasababisha madhara hatarishi katika Ini kwa watumiaji.

            Dawa nyingine ni ya kutibu malaria ikiwa katika mfumo wa maji na vidonge aina ya Amodiaquine inapotumika yenyewe na sababu ya kufutia usajili na kuzuia kuingia nchini ni kutokana na mabadiliko ya mwongozo wa kisera wa kupima na kutibu malaria wa mwaka 2013 uliotolewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, na kwamba ikitumika peke yake inaleta usugu wa vimelea vya malaria.

           Bw. Sillo aliitaja dawa nyingine  ambayo ni hatari kwa matumizi ya binadamu ni Dawa ya  kutibu mafua na kikohozi ya Maji,Vidonge na Kapsuli zenye kiambato hai aina ya Phenylpropanol amine ambacho anasema kinaleta madhara hatarishi kwa binadamu kama vile kiharusi (Hemorrhagic sroke).

             Mbali na hizo Dawa zengine ni Dawa ya kuua bacteria ya Sindano aina ya Chloramphenicol Sodiam Succinate inayotengenezwa nchini India pamoja na dawa ya kuua Bakteria ya Maji na kapsuli aina ya Cloxacillin ambazo zote kwa pamoja Bw. Sillo alizitaja kwamba zina madhara kwa watumiaji ikiwemo kushindwa kupumua na kupoteza Fahamu.

          Katika Hatua Nyingine TFDA imebadili na kudhibiti zaidi matumizi ya aina nne za dawa nchini. Mojawapo ni Dawa ya kutibu malaria aina ya vidonge yenye mchanganyiko wa Sulphadoxine na Pyrimethamine (SP)ambayo imebadilishwa kutoka kutibu malaria na kuwa kinga ya malaria kwa kina mama wajawazito kwa mujibu wa mwongozo wa kisera wa kupima na kutibu Malaria wa mwaka 2013 wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

  Dawa nyingine zilizodhibitiwa zaidi ni dawa aina ya Kanamycin Amikacin na Levofloxian kwa kuruhusu dawa hizi kutumika kwa ajili ya ugonjwa wa kifua kikuu katika hospitali, vituo vya afya na zahanati pekee. Bw. Sillo alieleza sababu ya kudhibiti zaidi ni kuzuia usugu wa vimelea vya bacteria vya ugonjwa wa Kifua kikuu.

        Aidha, Bwana Sillo ametoa wito kwa wamiliki wa maduka ya Dawa pamoja wananchi kuzingatia taarifa hizi za kiudhibiti kwa lengo la kuepuka madhara yanayoweza kutokea kutokana na matumizi ya dawa hizo. Sillo alizitaka Hospitali mbalimbali nchini pamoja maduka ya dawa kuaacha kuuza dawa hizo mara moja na kuzirudisha walikozinunua kwa ajili ya kuziteketeza.

  0 0

  Waziri wa maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba (katikati) akimsikiliza Mke wa aliyekuwa Rais wa Afrika ya Kusini Bi.Gracia Machel (wa kwanza kushoto) aliyefika Wizarani hapo kujadili program maalum ya kuwasaidia watoto wa kike kupata elimu. 
  Waziri wa maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba (katikati) akisisitiza jambo wakati wa kikao chake na aliyekuwa Rais wa Afrika ya Kusini Bi.Gracia Machel (wa kwanza kushoto) aliyefika Wizarani hapo kujadili program maalum ya kuwasaidia watoto wa kike kupata elimu. Wengine kulia ni  wa kwanza kulia ni Kulia ni Naibu Katibu Mkuu , Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto , Nuru Millao na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Mtoto, Benedict Missani. 
    Waziri wa Maendeleo ya  Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba ( katikati) na  Mke wa aliyekuwa Rais wa Afrika ya Kusini Bi.Gracia Machel wa kwanza kushoto  wakiongea jambo   wakati Mama Machel alipofika wizarani wakati wa ziara yake nchini.  Kulia ni Naibu Katibu Mkuu , Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto , Nuru Millao.

   ==== =====  ======

  Mke wa aliyekuwa Rais wa Afrika ya Kusini Bi. Gracia Machel yuko nchini katika ziara fupi kusaidia kumaliza tatizo la Ndoa za utotoni kupitia programu na miradi mbalimbali atakayoifadhili ili kuwawezesha watoto wa kike kupata elimu hatimae kujikomboa na umaskini.

  Katika ziara yake mama Machel, amekutana na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba ambapo, alitumia fursa hiyo kuipongeza Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa jitihada kubwa inayofanya wizara hiyo kupambana na tatizo hilo la mimba za utotoni.

  Vilevile, aliitaka  Wizara ya  Maendeleo ya  Jamii, Jinsia na Watoto  na wadau mbalimbali hususan viongozi wa mila/jadi na dini  kushirikiana nae na kuwa mstari wa mbele katika kuleta mabadiliko chanya kupitia program hizo anazotarajia kuzianzisha, na  kuongeza kuwa, “Mkoa wa Mara ndio utakaokuwa wa kwanza kuanzishwa kwa program hiyo kwani bado mkoa huo una mila gandamizi. (mfumo dume)”,alisema Machel.

  Naye Waziri wa Maendeleo ya jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba akiongea katika kikao hicho, alieleza kuwa, ni kweli tatizo hilo lipo nchini lakini Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali yakiwemo Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Asasi za Kiraia na vyombo vya habari, wanapambana kikamilifu kumaliza tatizo hilo.

  Aidha, Waziri Simba alitumia fursa hiyo kumshukuru Mama Machel kwa jitihada anazozifanya kuwawezesha watoto wa kike kuondokana na umaskini.  

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Mbunge wa jimbo la Muyuni,Mh.Mahadhi Juma Maalim,mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Pete,jimbo la Makunduchi, Wilaya ya Kusini Unguja.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Waziri  wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Mh.Samia Suluhu Hassani na Mbunge wa jimbo la Makunduchi Samia Suluhu,mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Pete,jimbo la Makunduchi, Wilaya ya Kusini Unguja,Pichani kati ni Mwakilishi wa jimbo la Makunduchi,Mh.Haroun Ali Suleiman.

   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na Mwakilishi wa jimbo la Makunduchi,Mh.Haroun Ali Suleiman.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kusini Unguja,mara baada ya kupokea taarifa fupi ya kazi za chama na taarifa ya utekelezaji wa taarifa ya Ilani ya CCM.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana sambamba na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Mbunge wa jimbo la Muyuni,Mh.Mahadhi Juma Maalim wakishiriki ujenzi wa ofisi ya CCM katika kijiji cha Kitogani,jimbo la Muyui,wilaya ya Kusini Unguja
    Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akimjulia hali aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kusini Unguja,Ndugu Haji Abdallah Mzee,kulia ni Mwenyekiti Mkoa wa Kusini Unguja,Ndugu Ramadhan Abdallah Ali
   Baadhi ya Wakulima wa zao la Mwani wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipozungumza nao katika kijiji cha Jambiani,jimbo la Muyuni,wilaya ya Kusini Unguja.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameongozana na Mwakilishi wa jimbo la Muyuni, Mh.Jakhu Hashim Ayoub wakielekea kwenye mashamba ya zao la Mwani,ambapo pia Ndugu Kinana alishiriki kupanda Mwani na baadhi ya Wakulima wa zao hilo katika kijiji cha Jambiani,jimbo la Muyuni,wilaya ya Kusini Unguja.
  Mmoja wa Wakulima wa Zao la Mwani,akitoa maelezo mafupi namna ya zao hilo linavyopandwa na kutunzwa kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana katika kijiji cha Jambiani,jimbo la Muyuni,wilaya ya Kusini Unguja,kulia kwake ni Muwakilishi wa jimbo la Muyuni ni Mh.Jakhu Hashim Ayoub.
    Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki kupanda Mwani na baadhi ya Wakulima wa zao hilo la Mwani katika kijiji cha Jambiani,jimbo la Muyuni,wilaya ya Kusini Unguja,kulia kwake ni Muwakilishi wa jimbo la Muyuni ni Mh.Jakhu Hashim Ayoub.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Muwakilishi wa jimbo la Makunduchi,Mh.Haroun Ali Suleiman alipowasili katika tawi la CCM Kiunga Mtende,jimbo la Makunduchi wilaya ya Kusini Unguja mapema leo mchana kwa ajili ya kukagua na kushiriki ujenzi wa ukumbi wa tawi la ofisi hiyo.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua ukumbi wa mkikutano wa Tawi la CCM Kiunga Mtende,jimbo la Makunduchi wilaya ya Kusini Unguja mapema leo mchana,anaeshuhudia ni Muwakilishi wa jimbo la Makunduchi,Mh.Haroun Ali Suleiman.

  0 0

  kaymu logo copy

  From two countries to 34; Kaymu’s two year journey so far.
  January 25 marks the 2 year anniversary of Kaymu, a leading online shopping community. It’s been two years and 34 countries for Kaymu so far, which launched in Nigeria and Pakistan simultaneously and has spread rapidly through Africa, Asia and most recently, in Europe. This year will see Kaymu launching in more countries in Asia and Europe.

  Kaymu’s business model and main aim is to empower local SMEs and make shopping accessible to everyone everywhere and in the process, drive the online shift in the countries it’s in. It has achieved many milestones in the last two years but has a lot of ground to cover as a start up.

  These two years have seen Kaymu change the lives of hundreds of thousands of people. Currently, there are over 100,000 sellers on board and there have been close to 900,000 buyers who have bought products from the Kaymu platforms. Roughly eight thousand transactions take place everyday, on the platform and there are several payment options including cash on delivery and SafePay, a mobile-money-based option that protects the buyer, so as to ensure that their payment is made only after they receive their goods.

  Kaymu Tanzania Country Manager, Erfaan Mojgani says “The significant growth of Kaymu over the past two years has been great motivation for us especially with our launch in Tanzania. The consumer demand for e-commerce has pushed Kaymu to grow and as 2015 goes on, we are looking to grow even further than we already have”.

  He adds, “By entering Tanzania, one of East Africa’s largest countries, we are optimistic that Tanzanian citizens will continue to love and appreciate our presence and services, hence opting for Kaymu as the leading online shopping platform not only in Tanzania but globally.”

  Kaymu is present in three of the most prominent and populous emerging economies - Nigeria, Pakistan and Bangladesh - and is instrumental in accelerating the movement of commerce online. The combined population of all the countries Kaymu is currently in, is 1.134 billion and is focused completely on empowering SMEs in those countries and is, in a way, driving a revolution of sorts there by changing lives as a consequence.

  2015 is slated to be a year of even greater growth and progress for Kaymu and the focus is on developing the platform even further so as to help even more SMEs bring their businesses online and make shopping accessible to everyone.

  0 0

  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akizungumza na waandishi wa katika mkutano uliofanyika mchana huu kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za Wizara hiyo,zilizopo kwenye Mtaa wa Samora,Jijini Dar es salaam.

  Waziri Muhongo ametangaza kujiuzulu wadhifa wake huo,kufuatia shinikizo la muda mrefu la kumtaka afanye hivyo au awajibishwe, kufuatia mapendekezo ya Bunge lililopita, lililoagiza serikali kuchukua hatua dhidi yake na wengine kadhaa kufuatia kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow.

  Waziri Muhongo akikazia kujiuzulu kwake huko amesema kuwa yeye sio mla rushwa bali ni mchapa kazi tu na akilizungumzia swala la akaunti ya Tegeta Escrow ambalo ndilo lililopelekea kujiuzulu kwake huko,Waziri Muhongo amesema kuwa sakata hilo lilitawaliwa na mambo makuu manne ambayo aliyataja kuwa ni Mvutano wa kibiashara, Mvutano wa kisiasa, Mvutano wa uongozi na madaraka pamoja na Ubinafsi.

  Hivyo kasema ameamua kujiuzulu ili kuiachia Serikali na Bunge kusitisha malumbano ya sakata la Escrow, akidai inaonekana yeye ndiyo tatizo.Picha/habari na Othman Michuzi.
  Sehemu ya Waandishi wa kutoka vyombo mbali mbali vya habari wakifatilia kwa makini taarifa ya Waziri Muhongo.
  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akisisitiza jambo wakati akilizungumzia swala la Akaunti ya Tegeta Escrow ambalo ndilo lililopelekea kujiuzulu kwake huko,mchana wa leo.

  0 0

  Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue akizungumza na vyombo vya habari jioni hii wakati akitangaza mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri,Ikulu Jijini Dar es Salaam.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo ametangaza mabadiliko madogo katika Baraza lake la Mawaziri,ambalo Ameliapisha jioni hii Ikulu,Jijini Dar es Salaam.

  Akitangaza uteuzi huo muda mchache kabla ya Mawaziri hao kuapishwa, Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue amesema uteuzi huo unahusu pia kujaza nafasi mbili zilizoachwa wazi na Profesa Anna Tibaijuka Na Profesa Sospeter Muhongo.

  Profesa Tibaijuka, aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alieachishwa kazi kutokana na kuhusika kwake katika sakata la akaunyti ya Tegeta Escrow.

  Kwa upande wa Profesa Muhongo aliachia ngazi mwenyewe mapema leo,  kwa kile alichotaja kuipisha Serikali iendelee kuwatumikia Wananchi badala ya kuendelea na malumbano ya Escrow.

  Katika mabadiliko hayo,sura mpya za manaibu mawaziri zimeingia na baadhi ya mawaziri wamehamishwa wizara.

  Akitangaza Mabadiliko hayo,Balozi Sefue aliwataja mawaziri hao kama ifuatavyo.

  MAWAZIRI

  1. Mh. George Simbachawene - Waziri wa Nishati na Madini
  2. Mh. Mary Nagu - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Mahusiano na Uratibu)
  3.Mh. Christopher Chiza - Waziri Uwezeshaji na Uwekezaji
  4. Mh. Harrison Mwakyembe - Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
  5.Mh. William Lukuvi - Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi
  6.Mh. Steven Wasira - Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika
  7.Mh. Samwel Sitta -Waziri wa Uchukuzi
  8.Mh. Jenista Muhagama - Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge

  MANAIBU WAZIRI
  1. Stephen Masele - Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu Rais - Muungano
  2. Mh. Angela Kairuki -  Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi
  3. Mh. Ummy Mwalimu - Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
  4. Mh. Anna Kilango - Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
  5 . Mh. Charles Mwijage - Naibu Waziri wa Nishati na Madini


  0 0

  Pichani juu na chini ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia Baadhi ya wakazi wa mji wa Kizimkazi waliofika katika uwanja wa Kizimkazi Mkunguni,Wilaya ya Kusini Unguja kumsikiliza.Ndugu Kinana ambaye leo anaikamilisha ziara yake ya siku kumi katika kisiwa cha Unguja akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,katika suala zima la kuimarisha uhai wa chama na kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.
  Mkutano wa hadhara ukiendelea katika uwanja wa Kizimkazi mkunguni,Wilaya ya Kusini Unguja mapema leo jioni.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikabidhi majiko ya gesi kwa vikundi vya akina mama wa Makunduchi yaliyotolewa na Mbunge wa jimbo la Makunduchi,Mh.Samia Suluhu na Mwakilishi wa jimbo la Makunduchi,Mh Haroun Ali Suleiman.
  Ndugu Kinana akishiriki kupandisha mabomba kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji wa Kibuteni-Makunduchi unaosaidiwa na jumuiya ya Milele Zanzibar Foundation.Pichani shoto ni Afisa Maji Mkoa wa Kusini Unguja,Bwana Hafidhi Hassan  Mwinyi,ambaye alisema kuwa lengo la Mradi huo ni kuhuwisha,kuiimarisha na kuikuza miundombinu ya maji safi na salama ya Makunduchi Kibuteni ili iweze kutoa huduma vizuri na kwa ubora unaohitajika kwa walengwa wake.Mradi huo unakisiwa kugharimu kiasi cha shilingi milioni 650 na ushehe.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na wanachama wengine,wakiwaongoza wanachama wapya wapatao 518 kula kiapo mara baada ya kujiunga na chama hicho sambamba na kukabidhiwa kadi za uanachama.
  Baadhi ya wakazi wa mji wa Kizimkazi wakiwa wamekusanyika katika uwanja wa Kizimkazi Mkunguni,Wilaya ya Kusini Unguja kwa minajili ya kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana ambaye leo anaikamilisha ziara yake ya siku kumi katika kisiwa cha Unguja akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,katika suala zima la kuimarisha uhai wa chama na kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.

  0 0

  Sehemu ya wanafunzi, wazazi, mwalimu na viongozi wa jumuiya waliohudhuria siku ya kwanza ya darasa la Kiswahili DMV
  Awamu ya pili ya Darasa la Kiswahili kwa watoto waishio Washington DC na vitongoji vyake umeanza Jumamosi ya Januari 24, 2015. Rais wa Jumuiya Bw Iddi Sandaly alipata fursa ya kuzungumza nasi kwa ufupi kuhusu darasa hilo.
  Karibu umsikilize
  Sehemu ya wanafunzi wakimsikiliza Mwalimu Asha Nyang'anyi. Kushoto kwake ni Katibu wa Jumuiya ya waTanzania hapa DMV Said Mwamende
  Baadhi ya wazazi wakiwa nje ya darasa wakati watoto wakiendelea na mafunzo
  Baadhi ya wazazi waliokuwa ndani ya darasa wakati watoto wakiendelea na mafunzo

  0 0

  Kufuatia mkutano wa Watanzania waishio ujerumani na Rais wa Tanzania Mhe Jakaya Kikwete, Mweyekiti wa umoja wa watanzania Ujerumani UTU e.V Bw, Mfundo Peter Mfundo ameeleza matarajio ya Watanzania waishio Ujerumani, alifafanua kwamba japokuwa Rais Kikwete amebakisha muda mfupi katika uongozi wake lakini Umoja huo unaamini kuwa madam Rais Kikwete ameona umuhimu wa kufanya mkutano na Watanzania wanaoishi ujerumani basi anaweza akatekeleza  mahitaji ya Watanzania hao.

  Bw Mfundo alifafanua pia  hoja za msingi ambazo zitaibuka kwenye mkutano huo ni pamoja na Utekelezwaji wa upatikianaji wa fursa zilizopo Tanzania kwa watanzania wanaoishi Ujermani,(Diaspora) aidha aliendelea kueleza kwamba hoja nyingine ya msingi ni kutaka kujua msimamo wa serikali juu ya Uraia Pacha, kwani Watanzania wanaoishi ujerumani wana kiu kubwa ya kujua swala la Uraia pacha limefikia wapi.

   Akiendelea kuongea na Mtangazaji Grace Kabogo kupitia sauti ya Radio Deutsche Welle idhaa ya kiswahili Bw. Mfundo alisema kutokana na Vijana wengi wa Tanzania kujiajiri kupitia Muziki  na kuupiga vita umasikini, Umoja wa Watanzania Ujerumani Utamuomba rais Kikwete kusaidia kupitisha msamaha wa kodi kwa Vyombo vya Muziki ili kuwawezesha Vijana wa Tanzania kumudu ununuzi wa vifaa hivyo, Bw. Mfundo alieleza moja ya changamoto wanazozipata  ni pale umoja huo unapokosa mawasiliano ya moja kwa moja na Idara ya Diaspora Tanzania.

  0 0


  WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, ameendelea na jitihada za kutafuta ufumbuzi wa kudumu kuhusiana na changamoto zinazowakumba wadau wa biashara ya utalii nchini.

  Katika kuhakikisha hilo linafanyika kwa mafanikio na kwa haraka, Nyalandu ametangaza kuanza kwa vikao vitakavyowakutanisha wataalamu wa Wizara zinazohusika na maliasili na utalii za Tanzania na Kenya kwa lengo la kujadiliana masuala mbalimbali iili yapatiwe ufumbuzi kwa maslahi ya pande zote.

  Hatua hiyo imetokana na hivi karibuni Serikali ya Kenya kuyazuia magari ya utalii kutoka Tanzania kuingiza watalii kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, hivyo kusababisha usumbufu mkubwa.

  Hata hivyo, Nyalandu aliingilia kati kwa kuzungumza na Waziri wa Utalii wa Kenya, Phillys Kandie na kufikiwa kwa makubaliano ya kuruhusiwa na hapo wazo wa wizara hizo kukutana likaibuliwa.

  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Nyalandu alisema vikao ya wataalamu hao vitaanza rasmi Februari 3, mwaka huu, jijini Arusha ambapo vitahusisha pia wataalamu kutoka Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

  Alisema vikao hivyo vitajadili masuala mbalimbali ili kuhakikisha changamoto zote zinawaikabili sekta ya utalii kwa nchi hizo mbili zinapatiwa ufumbuzi.

  Aliongeza kuwa hatua hiyo pia inalenga kuimarisha ushirikiano pamoja na kuongeza ulinzi kwenye mbuga za wanyama na mapori ya akiba dhidi ya mtandao wa ujangili.

  Hata hivyo, aliweka wazi kuwa hoja kuhusiana na mpaka wa Borongoja haitajadiliwa kwenye vikao hivyo kwa kuwa si sehemu ya ajenda.

  “Nchi zetu hizi zinategemeana sana katika biashara ya utalii hivyo, kuna makubaliano tuliyafikia muda mrefu huko nyuma lakini yanaonekana kuanza kuwa na changamoto hivyo ni lazima tujadili ili tuweze kusonga mbele. Hatutaki watalii wanaokuja kupumzika wasumbuke kwani itakuwa ni hasara kwa wafanyabiashara wetu na kutahatarisha uchumi wa taifa…daima lazima tusonge mbele,” alisema Nyalandu.

  Aliongeza kuwa baada ya mkutano wa wataalamu utafuatiwa na wa makatibu wakuu wa wizara hizo utakaofanyika Februari 4 mwaka huu kisha utahitimishwa na wa mawaziri utakaofanyika Februari 5.

  Nyalandu alisema ana imani mikutano hiyo itatoka na mwanga mpya na maboresho kwa sekta ya utalii na kusisitiza maslahi ya pande zote yatazingatiwa.

  Alisema kuwa nia ya Tanzania ni kuendeleza Jumuia ya Afrika Mashariki na mahusiano yake mazuri na si kugombana na kuharibu uhusiano huo.

  Alisema daima Tanzania itakuwa makini kuhakikisha mahusiano yanakaa sawa katika majadiliano hayo na kwamba kusije kutokea jambo likaleta madhara kwa watu wengine.

  Nyalandu aliongeza Tanzania itafanya biashara za utalii na watu wengine kuhakikisha wanaendelea kulinda rasilimali za taifa sambamba na wafanyabiashara wakubwa wa kitalii na wadogo.

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akimpokea  Rais wa Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein mara baada ya kuwasili mapema leo kwenye uwanja wa Ndege wa Pemba kwa ajili ya kushiriki uzinduzi wa sherehe za maadhimisho ya miaka 38 ya CCM,ambayo Kitaifa zitaadhimishwa mjini Songea mkoani Ruvuma.
  Makamu Mwenyeki wa CCM,Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein  akisalimiana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, mara baada ya kuwasili mapema leo kwenye uwanja wa Ndege wa Pemba kwa ajili ya kushiriki uzinduzi wa sherehe za maadhimisho ya miaka 38 ya CCM,ambayo Kitaifa zitaadhimishwa mjini Songea mkoani Ruvuma.Pichani Kati ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye pia amewasili leo na Ujumbe wake kwa ajili ya  ziara ya siku tano ya Kujenga na Kukiimarisha chama cha CCM.
  Kkatibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye wakiwasili mapema leo kwenye uwanja wa Ndege wa Pemba kuanza ziara ya siku tano ya Kujenga na Kukiimarisha chama.Ndugu Kinana pia amempokea Rais wa Zanzibar Dkt.Shein mapema leo kwa ajili ya kushiriki uzinduzi wa sherehe za maadhisho ya miaka 38 ya CCM,ambayo Kitaifa zitaadhimishwa mjini Songea mkoani Ruvuma.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar Ndugu.Vuai Ali Vuai,mara baada ya kuwasili kisiwani Pemba na Ujumbe wake akiwemo Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye tayari kwa kuanza ziara ya siku tano ya Kujenga na Kukiimarisha chama.Ndugu Kinana pia amempokea Rais wa Zanzibar Dkt.Shein mapema leo kwa ajili ya kushiriki uzinduzi wa sherehe za maadhimisho ya miaka 38 ya CCM,ambayo Kitaifa zitaadhimishwa mjini Songea mkoani Ruvuma.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge a jimbo la Makunduchi na aliyewahi kuwa Makamu Mmwenyekiti wa Bunge la katiba,Mh Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwasili mapema leo kwenye uwanja wa Ndege wa Pemba kuanza ziara ya siku tano ya Kujenga na Kukiimarisha chama.Ndugu Kinana pia amempokea Rais wa Zanzibar Dkt.Shein mapema leo kwa ajili ya kushiriki uzinduzi wa sherehe za maadhimisho ya miaka 38 ya CCM,ambayo Kitaifa zitaadhimishwa mjini Songea mkoani Ruvuma.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake mara baada ya kuwasili mapema leo kwenye uwanja wa Ndege wa Pemba kuanza ziara ya siku tano ya Kujenga na Kukiimarisha chama.Ndugu Kinana pia amempokea Rais wa Zanzibar Dkt.Shein mapema leo kwa ajili ya kushiriki uzinduzi wa sherehe za maadhimisho ya miaka 38 ya CCM,ambayo Kitaifa zitaadhimishwa mjini Songea mkoani Ruvuma.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Bibi Ester Makalili akizungumza na ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo walipomtembelea ofisini kwake kabla ya kukutana na vijana wa Wilaya hiyo kutoa mafunzo ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana jana katika Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya. Kushoto ni Mwenzeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa na kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele.
  Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa akitoa mada ya Ujuzi kwa vijana wakati wa semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana jana katika Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya.
  Afisa Ushirika kutoka Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya Bw. Mwanyi Magambo akiwaelimisha vijana wa Wilaya ya Chunya umuhimu wa kuunda Saccoss ya Vijana itakayowawezesha vijana kuweka akiba na kukopeshana wakati wa semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana jana katika Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya.
  Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga kushoto akizungumza na wanakikundi wa Ngozi group wanaosindika ngozi kwa njia ya asili na kutengeneza bidhaa za ngozi kwa kutumia ngozi walizosindika walipowatembelea kukagua mradi wao jana katika kijiji cha Mkwajini Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya. Wa pili kulia ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele.
  Kijana Meshaki Ngailo kushoto kutoka kikundi cha Vijana Bush Man Works kinachofanya kazi ya kuunga vyuma akizungumza na maafisa waliofika kukagua mradi wa kikundi chake wakati wa ziara ya kukagua miradi ya vijana wa Mkoa wa Mbeya.

  (Picha zote na: Genofeva Matemu – Maelezo. Chunya, Mbeya)

  0 0  11
  Mfanyabiashara na mmiliki wa duka la dawa katika eneo la Mrombo Arusha Bi elizabeth mshana akiongea na Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde juu ya huduma ya kufanya malipo kwa kutumia kadi ya Airtel Money Near Field Communication (NFC) based solution ya  Airtel Money. kadi hii maalum inamuwezesha mteja kufanya malipo kwa haraka kwa kugusisha kwenye kifaa maalum tu mara moja, kisha kuweka nambari ya siri na kufanya malipo mahali popote. kwa sasa huduma hii imeanza kufanya kazi mkoani Arusha. Huduma hii ya Near Field Communication (NFC) yaani kulipa kwa kugusisha kadi na kifaa tu kupitia huduma za kifedha kwa njia ya mtandao ni yakwanza kuzindulia nchini na kampuni ya simu za mkoni ya airtel
  1111
  Mama elizabeth mshana mmiliki wa duka la dawa akimuuzia mteja dawa kwa kupitia kadi huduma iliyozinduliwa na Airtel mkoani Arusha inayowawezesha wateja wake kufanya malipo kwa haraka zaidi kwa kutumia kadi hiyo maalumu ya airtel Money yenye teknolojia ya Near Field Communication (NFC) based ikiwa imeunganishwa na  Airtel Money.akishuhudia ni Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde. Huduma hii ya Near Field Communication (NFC) kupitia huduma za kifedha kwa njia ya mtandao ni yakwanza kuzindulia nchini na kampuni yasimu za mkoni ya airtel.
  11111
  Afisa uhusiano wa kampuni ya simu za mkononi ya AIRTEL Jane Matinde akimuelekeza Moja ya wateja bi Merry Ngowi jinsi ya kutumia kifaa na kadi maalumu ambacho hutumika kukamilisha miamala ya malipo katika maduka mbalimbali. Huduma hii ya Near Field Communication (NFC) kupitia huduma za kifedha kwa njia ya mitandao ni yakwanza kuzindulia nchini na kampuni ya simu za mkoni ya airtel, tukio lifanyika mwishoni mwa wiki mkoani arusha eneo la muromboo wakati wa uzinduzi huduma hiyo ambayo inaleta njia salama, ya haraka na rahisi kwa wateja kufanya malipo. 
  111
  Mfanyabiashara wa duka la chakula katika eneo la Mrombo Arusha Bwana Elibariki Ngowi akipokea malipo kutoka kwa mteja kwa kupitia kadi maalum ya Near Field Communication (NFC) ya Airtel Money.  , huduma imezinduliwa na Airtel mkoani Arusha inawawezesha wateja wake kufanya malipo kwa kutumia kadi hiyo maalumu kwa haraka bila huanza kupiga *150*60# hii unagusisha tu na kulipa haraka kati kanti ni Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde akishudia huduma hiyo inavyofanya kazi.  Huduma hii ya Near Field Communication (NFC) kupitia huduma za kifedha kwa njia ya mtandao ni yakwanza kuzindulia nchini na kampuni ya simu za mkoni ya airtel.

  ……………………………………………
  Na Mwandishi Wetu
  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo (mwishoni mwa wiki) imetangaza huduma ya kwanza sokoni inayotumia kadi maalumu kwa kupitia huduma ya Airtel Money. Huduma hiyo mpya inayowawezesha wateja wa Airtel Money kufanya malipo kwa kutumia kadi  imeanza katika mkoa wa Arusha na itaendelea kufikishwa katika mikoa mbalimbali nchini.
  Akiongea kuhusu huduma hiyo, Mkurugenzi wa Airtel Money Aijaza Khan alisema” technologia inakuwa kwa kasi na tumeonelea ni muhimu kwenda sambamba na mabadiliko hayo kwa kuleta huduma za kibunifu zitakazokithi mahitaji ya wateja wetu yanayokuwa kwa kasi kila siku.  Nia yetu ni kuona wateja wetu wanapata huduma za kisasa kwa wakati wote. 

  Huduma hii mpya tunayoitambulisha leo itawawezesha wauzaji na wanunuzi kupata njia rahisi, ya uhakika na salama ya kufanya miamala na malipo yao ya kila siku.  ili kutumia huduma hii kila mteja atatakiwa kupata kadi maalum inayomuwezesha kufanya malipo kirahisi , kwa haraka na kwa usalama katika maduka mbalimbali yaliyopatiwa  vifaa maalumu kwaajili ya kupokea malipo toka kwa wateja. Huduma hii imeshaanza kufanya kazi kwa wafanyabiashara na wateja wetu Arusha. 

  “Kadi hii maalumu imeunganishwa na akaunti ya Airtel Money ya mteja, mteja anachotakiwa ni kugusisha  kadi  yake na kifaa cha kupokea malipo (POS) ili kuweza  kufanya malipo.  Malipo yatakamilika pale mteja atakapothibitisha muamala  kwa kuweka namba yake ya siri  kwenye kifaa  cha malipo.

  Tunajivunia kuwa mtandao wa kwanza Tanzania kuanzisha huduma hii ya kibunifu itakayowawezesha wateja wetu kufanya malipo ya kwa urahisi, haraka , kiusalama bila kuwa na haja ya kupiga namba ya Airtel money na kuingia kwenye orodha, Kwa kutumia kadi maalumu mteja anaweza sasa kufanya malipo. ”. aliongeza Khan.

  Akiongea kuhusu faida za huduma hiyo , Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde alisema” huduma hii inafaida nyingi kwa wafanyabishara na wateja ikiwa ni pamoja na njia salama ya kuifadhi pesa, ya kuhakiki na kukusanya pesa,mfanyabiashara anaweza kuzipeleka moja kwa moja benki kutoka kwenye kifaa hicho au kutoa pesa kwa wakala aliye karibu. Kwa upande wa wateja  faida hizo ni pamoja na kufurahia urahisi, usalama, uharaka wa kufanya malipo na pia  kuepusha wateja kutembea na pesa  nyingi mfukoni ili kufanya malipo. Mteja atakapopoteza au kuibiwa kadi yake pesa zake kwenye kadi yake zinabaki salama aliongeza” Matinde.

  Akiongelea kuhusu uzoefu alioupata a kutumia huduma hii ya kadi kupitia Airtel Money, Mfanyabiashara na milliki wa Phamarcy Bi Elizabeth Mshana alisema” Huduma hii ni ya kipekee  na imerahisisha sana namna ya kufanya biashara maana ni rahisi kutumia na ni salama. Wateja wanapokuja dukani kununua dawa na hawana pesa taslimu mfukoni wanatumia huduma hii na mimi kama muuzaji nafurahi kwakuwa pesa zangu ziko salama na sina haja ya kufikiri kuhusu kutafuta chenji. 

  Kwa kweli ni huduma nzuri na tunaifurahia na nawashauri wafanyabiashara  wenzangu na wateja kutumia huduma hii kwani inaleta ufanisi” Huduma hii inapatikana sehemu mbalimbali ikiwemo maduka ya biadhaa , maduka ya chakula, maduka ya dawa, mawakala wa Airtel Money na Baa, Mpango mkakati ni kufikisha huduma hii katika maeneo mbalimbali nchini kwa mwaka huu.

  Airtel kupitia huduma yake ya Airtel Money hivi karibuni imezindua huduma nyingine ya kibunifu ijulikanayo kama Timiza inayowawezesha wateja wake kupata mikopo rahisi  papokwa papo na kurejesha baada ya wiki moja au mwenzi huduma ambayo imewawezesha watanzania wengi kuboresha mitaji ya biashara zao na kutatua changamoto ndogondogo za kila siku

  0 0

   -Kamisaa wa Sensa ya Watu na makaazi Mwalimu Haji Ameir akitoa maelezo mafupi ya makaribisho katika Semina ya Usambazaji wa matokeo ya Sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2012 kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi huko mbweni nje ya mji wa Zanzibar.

   -Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Ikulu na Utyawala Bora Dk,Mwinyihaji Makame akitoa maelezo kuhusu Sensa na Umuhimu wake katika Semina ya Usambazaji wa matokeo ya Sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2012 kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi huko mbweni nje ya mji wa Zanzibar.
   Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk  akitoa hotuba kuhusu Sensa na Umuhimu wake katika Semina ya Usambazaji wa matokeo ya Sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2012 kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi huko mbweni nje ya mji wa Zanzibar.
   Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliohudhuria katika semina  ya Usambazaji wa matokeo ya Sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2012 wakiangalia makala fupi ya Sensa ya Watu na makaazi huko mbweni nje ya mji wa Zanzibar.
   Mtakwimu mkuu wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mohd Hafidh Rajab  akiwasilisha matokeo muhimu yanayotokana na Sensa ya Watu na Makaazi katika Semina ya Usambazaji wa matokeo ya Sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2012 kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi huko mbweni nje ya mji wa Zanzibar.
  -Mwakilishi wa Jimbo la Kitope Makame Mshimba Mbarouk akiuliza masdwali katika Semina ya Usambazaji wa matokeo ya Sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2012 kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi huko mbweni nje ya mji wa Zanzibar.

  PICHA NA YUSSUF SIMAI -MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
  Kikwete akiwasili katika Uwanja wa Ndege wan Kijeshi mjini Riyadh,
  Saudi Arabia,  asubuhi ya leo, Jumapili, Januari 25, kuhani kifo cha
  Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud aliyefariki Alhamisi na kuzikwa
  Ijumaa ya wiki iliyopita. Baada ya kuhani msiba wa Mfalme Abdullah,
  Rais Kikwete ataendelea na safari yake kwenda nchi za Ujerumani na
  Ufaransa kwa ziara za kikazi.unnamedjk 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili mjini Riyadh, Saudi Arabia,asubuhi ya leo, Jumapili, Januari 25, 2015, kuhani kifo cha Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud aliyefariki Alhamisi na kuzikwa Ijumaa ya wiki iliyopita.

  Baada ya kuhani msiba wa Mfalme Abdullah, Rais Kikwete ataendelea na safari yake kwenda nchi za Ujerumani na Ufaransa kwa ziara za kikazi.

  Mjini Berlin, Ujerumani ambako Rais Kikwete alitarajiwa kuwasili kesho, Jumatatu, Januari Ishirini na Sita, akitokea Riyadh, Saudi Arabia, anatarajiwa kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Global Alliance for Vaccines and Immunization (Gavi Alliance) ambako viongozi mbali mbali duniani watajadili jinsi ya kuboresha mipango ya utoaji chanjo kwa watoto wadogo hasa katika nchi zinazoendelea.

  Baada ya kumaliza ziara yake Ujerumani, Rais Kikwete atakwenda Ufaransa ambako miongoni mwa mambo mengine atakutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Ufaransa. Aidha, Rais Kikwete atafungua jengo jipya la Ubalozi wa Tanzania katika Ufaransa na pia nyumba ya balozi.

  Rais Kikwete baada ya kumaliza ziara zake za kikazi katika Ujerumani na Ufaransa atakwenda Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU).

  Imetolewa na:Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,Ikulu – Dar es Salaam.25 Januari, 2015

older | 1 | .... | 446 | 447 | (Page 448) | 449 | 450 | .... | 1897 | newer