Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOA WA KASKAZINI UNGUJA

0
0
 Ktibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameambatana na Wanachama wa kikundi cha Ushirika wa Tuko Imara mara baada ya kushiriki kupanda Migomba,katika Kijiji cha Banda Maji,Wilaya ya Kaskazini A mkoa wa Kaskazini Unguja mapema leo.
 katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki kupanda Mgomba katika shamba la Kikundi cha Ushirika wa Tuko Imara unaojishughulisha na Kilimo cha Migomba na Mbogamboga  katika Kijiji cha Banda Maji,Wilaya ya Kaskazini A mkoa wa Kaskazini Unguja mapema leo.
 Mbunge wa Jimbo la Chaani,Mh.Ally Juma Haji a.k.a Chepe akizungumza na baadhi ya vijana kuhusiana mambo mbalimbali ikiwemo na kuwahimiza kupiga kura ya ndio kwa katiba inayopendekezwa.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki ujenzi wa tawi la CCM Chaani Masingini,jimbo la Chaani ambapo pia alipokea taarifa ya ujenzi wa tawi hilo na kusalimiana na Wananchi,Wilaya ya Kaskazini A,mkoa wa Kaskazini  Unguja.
 Msafara wa Katibu Mkuu,Ndugu Kinana ukielekea kwenye Mradi huo wa ujenzi wa barabara unaofadhiriwa na TASAF
 Baadhi ya Wananchi wanaoshiriki kazi ya ujenzi wa barabara katika kijiji cha Kijini kwa Shauripili,jimbo la Shaani,wilaya ya Kaskazini A,mkoa wa Kaskazini Unguja inayojengwa kwa mradi wa TASAF,wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipozungumza nao mapema leo.Barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 1.7 ina thamani ya shilingi milioni 26
 Katibu mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki kazi ya ujenzi wa barabara katika kijiji cha Kijini kwa Shauripili,jimbo la Shaani,wilaya ya Kaskazini A,mkoa wa Kaskazini Unguja inayojengwa kwa mradi wa TASAF,barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 1.7 yenye thamani ya shilingi milioni 26
Mradi wa ujenzi wa Nyumba ya Madaktari inayojengwa katika Sheia ya Kijini katika jimbo la Matemwe,Wilaya ya Kaskazini A,mkoa wa Kaskazini Unguja,yenye thamani ya shilingi milioni 80 ukiendelea,Mradi huo umejengwa kwa nguvu za Wananchi na Serikali pia.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki ujenzi wa Nyumba ya Madaktari inayojengwa katika Sheia ya Kijini,jimbo la Matemwe,Wilaya ya Kaskazini A,mkoa wa Kaskazini Unguja,yenye thamani ya shilingi milioni 80.Mradi huo huo umejengwa kwa nguvu za Wananchi na Serikali pia.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na viongozi wengine wa CCM,wakitazama mchezo wa sarakasi unaofanywa na vijana mara baada ya kupokea taarifa fupi ya ujenzi wa wa jengo la  ya Nyumba ya Madaktari inayojengwa katika Sheia ya Kijini katika jimbo la Matemwe,Wilaya ya Kaskazini A,mkoa wa Kaskazini Unguja,yenye thamani ya shilingi milioni 80,nyumba mradi huo umejengwa kwa nguvu za Wananchi na Serikali pia.
 Baadhi ya viongozi wa timu za mpira wakiwa na vifaa mbalimbali walivyopokea kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,mara baada ya kukagua na kushiriki kazi ya ujenzi wa uzio wa Uwanja katika sheia ya Tazari,jimbo la Nungwi mkoa wa Kaskazini Unguja
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wananchi wa Kigunda,mara baada ya kupokea taarifa fupi ya jengo la SACCOS ya vijana yenye Wanachama 114.SACCOS hiyo imeanzishwa kwa ajili ya kuisaidia jamii katika suala zima la kuweka unafuu wa kukopa kirahisi. 
 Balozi wa Shina namba 3,Balozi Khamis Makame Faki akizungumza mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na baadhi ya wananchi na wanachama,katika jimbo la Nungwi,wilaya ya Kaskazini A,Mkoa wa Kaskazini Unguja,Ndugu Kinana alifika kwa balozi huyo na kukagua uhai wa chama na Wanachama.
katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Banda Maji mara baada ya kupokea taarifa ya kikundi cha ushirika wa Tuko Imara unaojishughulisha na Kilimo cha Migomba na Mbogamboga,pia kushiriki kazi ya kilimo cha Migomba na Mbogamboga,katika Wilaya ya Kaskazini A mkoa wa Kaskazini Unguja mapema leo.

Pata Filamu ya Mdundiko kupitia Mtandao

0
0
Katika maisha tunayoishi duniani sio vizuri kufanyiana mabaya, Kwani hujui kesho itakuaje. Malipo ni hapahapa Duniani . Fuatilia hii kupitia mtandao .......

Kwa Kuangalia Filamu hii ya Kitanzania iitwayo Fedheha au Knunua na iwe yako kupitia mtandao.

Ili kuweza kuangalia au kununua kupitia Mtandao unachotakiwa kufanya ni kutembelea tovuti hii
Pia unaweza kuangalia au kununua filamu nyingine kupitia mtandao huo huo.

ISACA TANZANIA YATOA SEMINA KUHUSU USALAMA WA MITANDAO

0
0
 Makamu wa Rais wa Isaca Tanzania Chapter ambaye pia ni Ofisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Serikali Mtandao, Dk. Jabir Bakari akitoa hotuba yake wakati akifungu semina kuhusu usalama wa mifumo ya kompyuta pamoja na ukaguzi wa mifumo hiyo kwa kuwakutanisha wataalumu na kujadiliana kuhusu ukuaji wa teknolojia na usalama.

Aidha Dk. Jabir alisema kuwa semina hiyo inawakutanisha wataalamu wa mifumo ya kompyuta kutoka ndani na nje ya nchi watakaojifunza na kuongeza utaalamu wa kulinda mifumo ya mitandao. 

Naye Mratibu wa Semina hiyo ambaye pia ni Rais wa Isaca Tanzania, alisema kuwa semina hiyo kwa ajili ya kuelezea wadau wa mitandao kuhusu mwelekeo wa teknolojia duniani na ukubwa wa tatizo katika wizi wa mitandao  'miaka ya nyuma kulikuwa na wizi wa kuvunja katika mabenki lakini siku hizi mbinu za wizi zimebadilika na wezi wanaiba kupitia mifumo ua mitandano hasa kompyuta pamoja na simu, kutoa elimu ya ajili ya mifumo ya kompyuta namna ya kuilinda na kuiendeleza.
Katibu wa Tanzania Chapter, Nemayani Kaduma (kulia)akiwa katika semina hiyo.
Baadhi ya washiriki wa semina ya ya kimataifa kuhusu usalama wa mitandao wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Taasisi ya Isaca Tanzania Chapter, Dk. Jabiri Bakari (hayupo pichani) iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Washiri wa semina wakifuatikilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa.
Washiriki wa semina hiyo.
Washiriki.
George Wahome kutoka Isaca-Kenya akitoa mada kuhusu usalama                                                 wa mitandao.
Washiriki wa semina.
Rais wa Isaca Tanzania Chapter, Boniface Kanemba akifuatilia mada katika semina hiyo.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Dun & Bradstreet Credit Bureau Tanzania, Adebowale Atobatele akitoa mada katika semina hiyo.
Rais wa Isaca Tanzania Chapter, Boniface Kanemba akizungumza na waandishi wa habari.
Washiri wa semina hiyo wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa.

MIss Universe Tanzania 2014,Nale Boniface akiwakilisha vazi la Kitaifa

0
0
Mashindano ya awali (Preliminary show)ya fainali za kumtafuta mrembo wa Miss Universe Kimataifa huko jijini Doral, Miami-Marekani yamefanyika jana tarehe 21 huku jumla ya warembo 88 kutoka nchi tofauti duniani wakipita na mavazi ya Kitaifa(National Costume), ufukweni(Swim Suit) na magauni ya usiku(Evening gown). 
Mrembo wa Tanzania, Nale Boniface (pichani)  ni mmoja wa washiriki wa mashindano hayo ambapo fainali zake zitahitimishwa jumapili, januari 25 huko Marekani. Siku chache zikiwa zimebakia kuhitimisha shindano hilo, washiriki wote walipata nafasi ya kuzungumza na kuhojiwa na vyombo mbalimbali vya habari huku wakizungumzia mawazo yao kuhusu fainali hizo.
 
 Shindano hilo la awali liliendeshwa na mrembo wa Miss Universe 2013, Gabriela Isler and Roxanne Vargas. Shindano hili la awali lilikuwa na umuhimu kwa washiriki wote kwani ndipo wanapopatikana 16 bora ambapo watatangazwa siku ya fainali za shindano hilo jumapili ya tarehe 25.Shindano hili ni la 63 kufanyika toka kuanzishwa kwake. 
Mshiriki wa Tanzania katika shindano hili alivaa vazi lililobuniwa kutokana na zao la MKONGE. Mkonge ni zao linalostahmili ambapo linaweza kustawi katika hali ya ukame na nchi zenye uoto usio na rutuba. 
Zao hili pia lina magonjwa machache sana ambayo mara nyingi halihitaji dawa yoyote. Pia zao hili linasaidia kuzuia mmomonyoko wa udongo na kupata unyevu wa anga. Zao hili linaweza kupandwa wakati wowote wa mwaka na kuvunwa kwa mwaka mzima. 
Zao hili pia haliathiriwi na moto,na ni mazao machache sana katika dunia hii yenye sifa kama hizi. Hivyo, vazi la mshiriki wetu wa Tanzania katika fainali za Miss Universe limebuniwa na kutengenezwa kutokana na zao la Mkonge.

AJALI

0
0
 Gari aina ya SCANIA likiwa limeacha njia na kupinduka eneo la Ruvu Mkoani Pwani kama lilivyokutwa na mpiga picha wetu,katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha

WANANCHI KUWENI MAKINI NA VIONGOZI WENYE TAMAA YA MADARAKA-KINANA

0
0
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia  sehemu ya wakazi wa Nungwi na Wafuasi wa CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Skuli,jimbo la Nungwi,wilaya ya Kaskazini A,mkoa wa Kaskazini Unguja.Kinana amewataka Wananchi hao kuwa makini na baadhi ya viongozi wenye tamaa ya madaraka kwa kuahidiwa mambo ambayo hayatekelezeki,pia amewataka Wananchi kujitokeza kwa wingi siku ikifika ya kupiga kura ya ndiyo kwa katiba inayopendekezwa,kwani imejaa mambo mengi na mazuri kwa Zanzibar na Tanzania bara kwa ujumla.
 Sehemu ya umati wa wakazi wa Nungwi na Wafuasi wa CCM wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipowahutubia mapema leo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Skuli,jimbo la Nungwi,wilaya ya Kaskazini A,mkoa wa Kaskazini Unguja.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia mapema leo jioni kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Skuli,Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.Nae amewataka vijana kuacha tabia  yakushabikia vyama ambavyo havina msaada kwao
 Sehemu ya Meza kuu ikifuatilia yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo.
Sehemu ya umati wa wakazi wa Nungwi akiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa hadhara,ambapo Katibu Mkuu wa CCM,aliwahutubia mapema leo jioni kwenye uwanja wa Skuli,jimbo la Nungwi,wilaya ya Kaskazini A,mkoa wa Kaskazini Unguja.
 Baadhi ya Wanachama wapya wapatao 284 waliojiunga na chama CCM wakila kiapo mara baada ya kukabidhiwa kadi za uanachama
Baadhi ya Wafuasi wa chama cha CCM wakishangilia jambo kwenye mkutano wa hadhara.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI AKAGUA KIVUKO CHA MV UTETE

0
0
 Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Gerson Lwenge(wa kwanza) akishuka ngazi  mara baada ya kukagua kivuko cha MV-Utete ambacho hakitoi huduma ya usafirishaji kutokana na kupungua kwa kina cha maji cha mto Rufiji.
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme(TEMESA), Eng. Manase Ole-Kujan (wa kwanza kushoto) akitoa taarifa ya kivuko cha MV-Utete kwa naibu waziri wa ujenzi Eng. Gerson Lwenge.
 Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Gerson Lwenge (wa pili kulia) akitoa maelekezo na maagizo kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme(TEMESA), Eng. Manase Ole-Kujan  baada ya kukagua kivuko cha Mv-Utete wilayani Rufiji mkoani Pwani
 Muonekano wa kivuko cha MV-Utete  ambacho kimeegeshwa na kusitisha huduma zake kutokana na kupungua kwa kina cha maji cha mto rufiji.
Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Gerson Lwenge (wa kwanza kulia) akimpa pole Mkuu wa mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo kufuatia mauaji ya askari polisi wawili katika kituo cha polisi cha Ikwiriri Wilayani Rufiji.

WATANZANIA WATAKIWA KUITUMIA VYEMA FURSA YA KIMATAIFAKATIKA MAONYESHO YA BIASHARA

0
0
unnamed (1)Balozi wa Tanzania nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh akitoa nasaha zake kwa Washiriki wa Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, nchini Oman,kushoto kwake ni Naibu Balozi wake Bw.Juma Othman.
unnamed (3)Baadhi ya Watanzania wanaoshiriki Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, nchini Oman wakimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini humo Bw. Ali Ahmed Saleh alipokuwa akiwanasihi Washiriki hao.
unnamed (4)Baadhi ya Watanzania wanaoshiriki Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, nchini Oman wakimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini humo Bw. Ali Ahmed Saleh alipokuwa akiwanasihi Washiriki hao.
unnamed (7)Balozi wa Tanzania nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh akiwa katika picha ya Pamoja na Wakuu wa Msafara wa Watanzania wanaoshiriki Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, nchini Oman kulia ni Masha Hussein na kushoto ni Khadija Batashy. Picha na Faki Mjaka.
unnamed (8)Balozi wa Tanzania nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh akiwa katika picha ya Pamoja na Watanzania wanaoshiriki Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, nchini Oman mara baada ya kuwapa nasaha zake. Picha zote na Faki Mjaka.
unnamed (9)Balozi wa Tanzania nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh akisalimiana na Mwandishi wa Chanel Ten Said Makala Ofisini kwake alipowaita kwa lengo la kuwapa nasaha Washiriki wa Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, nchini Oman. Picha na Faki Mjaka.unnamed (82)2 Mkuu wa Utawala Ubalozi wa Tanzania nchini Oman Abdallah Kilima kushoto akimkaribisha  Balozi wa Tanzania nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh kulia kutoa nasaha zake kwa Washiriki wa Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, nchini Oman. Katikati ni Mkuu wa Msafara wa Watanzania hao Bi Khadija Batashy.
………………………………………………………………
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar, akiwa Mascut-Oman 22/01/2015
Watanzania wanaoshiriki katika Maonesho Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea nchini Oman wametakiwa kuitumia vyema fursa ya kimataifa walioipata kwa kufuata vyema Miongozo waliyopewa ili ziara yao iweze kuleta Tija.
Miongozo hiyo ni pamoja na Mashirikiano miongoni mwao,kujituma kwa bidii na kutumia lugha nzuri katika Maonesho hayo kwa kuzingatia kuwa Wananchi wengi wa Omani wanaelewa vyema Lugha ya Kiswahili.
Wito huo umetolewa na Balozi wa Tanzania nchini Oman Mh. Ali Ahmed Saleh wakati alipokuwa akitoa nasaha zake kwa Washiriki wa Maonesho hayo Ofisini kwake Mascut nchini Oman.
Amesema Tanzania ni nchi inayoongoza kuwa na Mahusino mema na Oman hivyo Washiriki hao wanapaswa wafanye kazi zao kwa bidii na kuzingatia kanuni na Maadili ya Oman.
Balozi Saleh ameongeza kuwa kufuata kanuni na sheria za Oman kutawafanya Wajasiriamali hao wa Tanzania kufanyakazi zao kwa utulivu bila ya kupata usumbufu jambo ambalo litazidi kuimarisha mahusiano mema kati ya Tanzania na Oman.
Amebainisha kuwa Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete aliyoifanya mwaka jana nchini humo imezidi kuyaweka pazuri mahusiano na kwamba Washiriki hao wanapaswa wayatunze na kuyalinda.
“Ndugu zangu Tanzania ina nafasi ya kipekee nchi Oman,tunaheshimiwa sana kuliko nchi yoyote hasa baada ya ziara ya Rais Kikwete, naomba Mahusiano haya muyaendeleze kwa kufanya kazi zenu kwa bidii na kuchunga maneno yenu maana hawa Waoman wanakijua vyema Kiswahili Mkiwasema Wanafahamu” Alinasihi Balozi Saleh.
Ameongeza kuwa Raia wa Oman wanautamaduni wa Kumsifu na Kumtukuza Mfalme wao Sultan Qabus kwa mengi mazuri aliyowafanyia hivyo Watanzania hao wanapaswa kulifahamu hilo na kulichukulia Tahadhari.
Balozi Saleh amesema Mashirikiano miongoni mwao ni Jambo muhimu na kwamba wote wamekuja kwa Niaba ya Jamhuri ya Tanzania na Sio Bara au Visiwani.
“Kitu kingine Mufahamu kuwa hapa Tunaiwakilisha Tanzania kwa hiyo Uzanzibari na Ubara usiwepo maana mukiupa nafasi utamusumbua,Tusimameni katika Jina moja tu la Utanzania ambalo ndio uwakilishi wetu kimataifa” Alisema Balozi.
Aidha ametoa Wito kwa Wajasiriamali ambao hawakupata fursa ya kushiriki Maonesho hayo kutokata tama na kuamini kuwa ipo siku nao watapata nafasi ya kushiriki Maonesho ya kimataifa.
Kwa upande wake Mkuu wa Msafara wa Watanzania Wanaoshiriki Maonesho hayo Bi Khadija Batashy alimshukuru Balozi Saleh na Wasaidizi wake kwa Mapokezi mazuri na Nasaha alizozitoa.
Aidha Bi Khadija alimuahidi Balozi huyo kuzifanyia kazi nasaha hizo ikiwemo kujituma, kuzidisha mashirikiano na kutumia lugha nzuri ili kuwavutia wateja katika Maonesho hayo.
Awali Mkuu wa Utawala katika Ofisi ya Ubalozi Bw. Abdallah Kilima wakati akimkaribisha Balozi aliishukuru nchi ya Mascut kwa kuzidi kuongeza njanja za kuimarisha mashirikiano ikiwa ni pamoja na Mwaliko wa Maonesho hayo.
Kilima aliwataka Washiriki hao kuwa kitu kimoja na kusaidiana kwa hali na mali jambo ambalo litaipatia sifa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Maonesho hayo ya muda wa mwezi mmoja ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, huanza kila ifikapo saa 10 za jioni na kufungwa saa 04 usiku kwa majira ya nchi ya Omani ambapo Washiriki huonesha bidhaa za nchi zao na Watu kunua bidhaa hizo.

MKIRIKITI“MADIWANI ,MAAFISA TARAFA, WATENDAJI WA KATA NA WATENDAJI ACHENI KUWASINGIZIA WANASIASA WAMEWAZUIA WAZAZI KUCHANGIA CHAKULA MASHULENI”

0
0
Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti
_______________________
Na demasho.com
 Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma imefanya tahimini ya elimu ya na matokeo ya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi mwaka 2014 katika ukumbi wa EMAU Peremiho.

Katika tathimini hiyo mkuu wawilaya ya Songea Joseph Mkirikiti amewataka Madiwani ,Maafisa tarafa, Watendaji wa kata  na Watendaji wa Vijiji kuwapa elimu wazazi juu ya umuhimu wa kuchangia chakula cha kutosheleza muhula wa masomo ili kusaidia wanafunzi kufanya vizuri katika masomo.
“ Kwani kufanya hivo kutasaidia wanafunzi kujifunza muda wote wawapo shuleni na kujenga ushirikiano baina yao wanapokuwa pamoja na hali hiyo iatainua kiwango cha ufaulu” alisema Mkirikiti.

Hata hivyo Mkirikiti amewataka Madiwani ,Maafisa tarafa, Watendaji wa kata  na Watendaji kuacha kusingizia wanasiasa kuwa wamezuia suala la kuchangia chakula.
“ Tabia ya kuwasingizia wanasiasa kuwa wamezua kuchangia chakula mashuleni muache sio kila kitu kusingizia wanasiasa hivi ni kiongozi gani asiependa maendereo ?, maana saiz kila kitu wanasiasa wamezuia hasa kipindi hiki tunachoenda cha uchaguzi utasikia wanasiasa wamezuia ukiona mwanasiasa anazuia basi huyo ni SHIDAAA Alisema Mkirikiti.


Naye Kaimu Afisa elimu wilya Bw. Tanu Kameka ameomba baada ya Tathimini hiyo wakutane na waratibu wakata, wazazi , walimu pamoja na watendaje ili uongezwe muda wa ziada wa ufundishaji ili kuweza kuleta mwamko wa elimu katika halmashauri hiyo ya Songea vijijini na kuleta ufaulu mzuri.

“ Miaka yote tumekuwa tukifanya hivo na ndiyo maana tukawa tunaongoza katika matokeo , ila kwa mwaka jana hatukuweza kusimamia hili swala la muda wa ziada ndiyo maana tumeshuka ila kwa mwaka huu tunalirudisha swala la muda wa ziada hivyo tutafanya vizuri katika matokeo Alisema Bw. Kameka.


<!--[if gte mso 9]>

Waziri WA fedha Saada afanya ziara ya kushtukiza Kariakoo na Mtaa wa Namanga

0
0
 Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (wa pili kulia) akiongoza na viongozi wa mkoa wa kodi wa Ilala kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na maafisa wa Serikali alipofanya ziara ya kushtukiza leo jijini Dar es salaam katika soko la Kariakoo kujionea namna wafanyabiashara wanavyozingatia na kusimamia matumizi ya mashine za kielektroniki za EFD ambazo wanazopaswa kuzitumia mara wanapouza bidhaa zao ili kusaidia Serikali kukusanya mapato na kuboresha utoaji wa huduma za jamii nchini. Wa kwanza kulia ni Kaimu Msaidizi wa Meneja wa mkoa wa kodi wa Ilala kutoka TRA Hamidu Athmani, wa kwanza kushoto ni Kaimu Meneja wa mkoa wa kodi wa Ilala Elias Balongo na kushoto mwa Waziri ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Prof.  Adolf Mkenda.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Prof. Adolf Mkenda (wa kwanza kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (wa pili kushoto) katika ziara ya kushtukiza katika soko la Kariakoo kujionea namna wafanyabiashara wanavyozingatia na kusimamia matumizi ya mashine za kielektroniki za EFD ambazo wanazopaswa kuzitumia mara wanapouza bidhaa zao ili kusaidia Serikali kukusanya mapato na kuboresha utoaji wa huduma za jamii nchini. Aliyevaa tai kulia ni wa kwanza kulia ni Kaimu Msaidizi wa Meneja wa mkoa wa kodi wa Ilala kutoka TRA Hamidu Athmani.
. Wananchi wakifuatilia ziara ya kushtukiza ya Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum aliyofanya leo jijini Dar es salaam katika soko la Kariakoo kujionea namna wafanyabiashara wanavyozingatia na kusimamia matumizi ya mashine za kielektroniki za EFD ambazo wanazopaswa kuzitumia mara wanapouza bidhaa zao ili kusaidia Serikali kukusanya mapato na kuboresha utoaji wa huduma za jamii nchini.
(Picha na Eleuteri Mangi- MAELEZO)

Timu ya Arsenal yafanya mazungumzo na Kampuni ya TTCL

0
0

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Timu maarufu ya mpira wa miguu duniani ya Arsenal, Dam Stone (kulia) akipokea zawadi kutoka Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) iliyokabidhiwa na Meneja wa Masoko na Usambazaji wa TTCL, Robart Noel kabla ya kuanza mazungumzo ya kibiashara kati ya pande hizo mbili. Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Timu maarufu ya mpira wa miguu duniani ya Arsenal, Dam Stone (kulia) akipokea zawadi kutoka Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) iliyokabidhiwa na Meneja wa Masoko na Usambazaji wa TTCL, Robart Noel kabla ya kuanza mazungumzo ya kibiashara kati ya pande hizo mbiliKutoka kushoto ni Meneja wa Masoko na Usambazaji wa Kampuni ya Simu ya TTCL, Robart Noel, Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Timu maarufu ya mpira wa miguu duniani ya Arsenal, Daniel Willey na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Timu maarufu ya mpira wa miguu duniani ya Arsenal, Dam Stone wakiwasili kwa mazungumzo na wanahabari kabla ya kuanza kikao cha mazungumzo kibiashara kati ya TTCL na Timu ya Arsanal leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Meneja wa Masoko na Usambazaji wa Kampuni ya Simu ya TTCL, Robart Noel, Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Timu maarufu ya mpira wa miguu duniani ya Arsenal, Daniel Willey na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Timu maarufu ya mpira wa miguu duniani ya Arsenal, Dam Stone wakiwasili kwa mazungumzo na wanahabari kabla ya kuanza kikao cha mazungumzo kibiashara kati ya TTCL na Timu ya Arsanal leo jijini Dar es Salaam.Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Timu maarufu ya mpira wa miguu duniani ya Arsenal, Daniel Willey (katikati) akizungumza jambo na wanahabari kabla ya kuanza kikao cha mazungumzo ya kibiashara kati ya TTCL na Timu ya Arsanal leo jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Timu maarufu ya mpira wa miguu duniani ya Arsenal, Dam Stone (kulia) na Meneja Masoko na Usambazaji Kampuni ya Simu ya TTCL, Robart Noel (kushoto). Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Timu maarufu ya mpira wa miguu duniani ya Arsenal, Daniel Willey (katikati) akizungumza jambo na wanahabari kabla ya kuanza kikao cha mazungumzo ya kibiashara kati ya TTCL na Timu ya Arsanal leo jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Timu maarufu ya mpira wa miguu duniani ya Arsenal, Dam Stone (kulia) na Meneja Masoko na Usambazaji Kampuni ya Simu ya TTCL, Robart Noel (kushoto).
Kutoka kushoto ni Meneja wa Masoko na Usambazaji wa Kampuni ya Simu ya TTCL, Robart Noel, Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Timu maarufu ya mpira wa miguu duniani ya Arsenal, Daniel Willey na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Timu maarufu ya mpira wa miguu duniani ya Arsenal, Dam Stone wakizungumza na wanahabari kabla ya kuanza kikao cha mazungumzo ibiashara kati ya TTCL na Timu ya Arsanal leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Meneja wa Masoko na Usambazaji wa Kampuni ya Simu ya TTCL, Robart Noel, Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Timu maarufu ya mpira wa miguu duniani ya Arsenal, Daniel Willey na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Timu maarufu ya mpira wa miguu duniani ya Arsenal, Dam Stone wakizungumza na wanahabari kabla ya kuanza kikao cha mazungumzo ibiashara kati ya TTCL na Timu ya Arsanal leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Meneja Mauzo na Uendeshaji Biashara wa TTCL, Benjamin Bizere Nkaka, Meneja wa Masoko na Usambazaji wa Kampuni ya Simu ya TTCL, Robart Noel, Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Timu maarufu ya mpira wa miguu duniani ya Arsenal, Daniel Willey na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Timu maarufu ya mpira wa miguu duniani ya Arsenal, Dam Stone wakizungumza na wanahabari kabla ya kuanza kikao cha mazungumzo ibiashara kati ya TTCL na Timu ya Arsanal leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Meneja Mauzo na Uendeshaji Biashara wa TTCL, Benjamin Bizere Nkaka, Meneja wa Masoko na Usambazaji wa Kampuni ya Simu ya TTCL, Robart Noel, Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Timu maarufu ya mpira wa miguu duniani ya Arsenal, Daniel Willey na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Timu maarufu ya mpira wa miguu duniani ya Arsenal, Dam Stone wakizungumza na wanahabari kabla ya kuanza kikao cha mazungumzo ibiashara kati ya TTCL na Timu ya Arsanal leo jijini Dar es SalaamMkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Timu maarufu ya mpira wa miguu duniani ya Arsenal, Dam Stone (kulia) akipokea zawadi kutoka Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) iliyokabidhiwa na Meneja wa Masoko na Usambazaji wa TTCL, Robart Noel kabla ya kuanza mazungumzo ya kibiashara kati ya pande hizo mbili. Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Timu maarufu ya mpira wa miguu duniani ya Arsenal, Dam Stone (kulia) akipokea zawadi kutoka Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) iliyokabidhiwa na Meneja wa Masoko na Usambazaji wa TTCL, Robart Noel kabla ya kuanza mazungumzo ya kibiashara kati ya pande hizo mbili

KAMATI YA MASUALA YA UKIMWI NA MADAWA YA KULEVYA YAJADILI MUSWADA WA SHERIA YA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA DAWA ZA KULEVYA YA MWAKA 2014

0
0
unnamed (20)Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia mambo ya Bunge, Sera na Uratibu Mhe. William Lukuvi akifungua kikao cha Kamati ya Masuala ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya kujadili Muswada wa Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Dawa za Kulevya ya mwaka 2014 kilichofanyika 22/01/2015 katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
unnamed (25)Baadhi ya wajumbe toka Taasisi mbalimbali wakifuatilia kwa makini kikao cha Kamati ya masuala ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya kilichofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam kuhusu Muswada wa Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Dawa za Kulevya ya mwaka 2014.
unnamed (27)Baadhi ya wajumbe toka Taasisi mbalimbali wakifuatilia kwa makini kikao cha Kamati ya masuala ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya kilichofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam kuhusu Muswada wa Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Dawa za Kulevya ya mwaka 2014.


 (PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO, DSM)

Halmashauri ya Wilaya ya Momba yahaidi kuunda Saccoss ya Vijana kwa maendeleo ya Vijana.

0
0
 Kaimu Mkurugenzi Wilaya ya Momba Bw. Severine Chamkaga akifungua semina ya Vijana kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Ujasiriamali, Stadi za Maisha na Ujuzi jana katika Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya. Wa pili kulia ni Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa, wa kwanza kulia ni Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara hiyo Bi. Amina Sanga, na wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele.
 Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa akitoa mada wakati wa semina ya Vijana kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Ujasiriamali, Stadi za Maisha na Ujuzi jana katika Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya.
 Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga akitoa mada wakati wa semina ya Vijana kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Ujasiriamali, Stadi za Maisha na Ujuzi jana katika Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya.

 Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele akitoa mada wakati wa semina ya Vijana kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Ujasiriamali, Stadi za Maisha na Ujuzi jana katika Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya.
 Kijana Adam Zacharia Kinyakile wa pili kulia anayeinua vipaji vya vijana na kutengeneza ajira kwa vijana katika fani ya ufundi gereji Mji wa Tunduma Wilaya ya Momba akiwaonyesha maafisa waliomtembelea katika shughuli zake “Mobile Garage” aliyoitengeneza mwenyewe kwa kutumia vyuma chakavu inayoitumia kufanyia kazi za gereji mahali popote anapohitajika. Kushoto ni Mwenzeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamduni na Michezo Bibi Ester Riwa pamoja na timu kutoka Wizara hiyo.
 Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga wa pili kushoto (waliokaa) akizungumza na Vijana wa kikundi cha Matunda Wilaya ya Momba walipowatembelea wakati wa ziara ya kukagua miradi ya Vijana Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele na wa pili kushoto ni Mwenzeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Ester Riwa.
(Picha zote na Genofeva Matemu – Maelezo. Momba, Mbeya)


AK CLASSIC COSMETICS TAWI LA MLIMANI CITY SASA TUKO WAZI!!

0
0
TUNAPENDA KUWAJULISHA WATEJA WETU KUWA SASA LILE DUKA LETU LA #AKCLASSIC TAWI LA MLIMANI CITY OPPOSITE NA PETROL STATION YA TOTAL SASA TUKO WAZI. NA ILE SALE KABAMBE YA UFUNGUZI INAENDELEA NA MAMBO MAPYAMAPYA  KAMA KAWAIDA YETU YANAENDELEA... BIDHAA ZA NGOZI,KUNG'AA,CHUNUSI,WEUSI WA KWAPANI,KUKUZA NYWELE,KUNUKIA,CORSET N.K NA ZINGINE KEDEKEDE!!
BIDHAA ZETU NI ORIGINAL KABISA KUTOKA US.
INGIA HAPA KWA PICHA ZAIDI
           www.akclassic.blogspot.com
TUNAPATIKANA PIA KINONDONI MANYANYA.
PIGA
0753482909/0713468393
KUPATA BIDHAA MPAKA MLANGONI.

Utiwaji saini mkataba wa kujenga tena umoja na kukiunganisha upya Chama Tawala cha Sudan Kusini cha Sudan People’s Liberation Movement (SPLM)

0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza utiaji wa saini. Kutoka kulia ni  Mhe. Salva Kiir Mayardit  Rais wa Sudan Kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa SPLM na anayeongoza kundi linalojulikana kama SPLM in Government (SPLM-IG), Mhe Dkt. Riek Machar ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa SPLM na pia aliyekuwa Makamu wa Rais wa Sudan Kusini anayeongoza kundi la SPLM in Opposition (SPLM-IO) na Dkt. Deng Alor Kuol ambaye anaongoza kundi la SPLM Leaders- Former Detainees (SPLM Leaders – FD).
Nyuma yao ni mjane wa marehemu John Garang aliyekuwa Mwenyekiti wa SPLM Mama Rebecca Nyandeng de Mabior na Afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. Thobias Makoba. Meza kuu toka kushoto  wakishuhudia utiaji saini huo ni Makamu wwa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Naibu Rais wa Afrika Kusini Mhe Cyril Ramaphosa.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto), Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) na Bw. Deng Alor Kuol wakionesha hati baada ya kutia saini mkatana wa  makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pongezi kwa Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto), Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) na Bw. Deng Alor Kuol

baada ya kutia saini mkatana wa  makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia wakati  Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) wakipeana mikono na kubadilishana nyaraka baada ya kutia saini mkatana wa  makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA



SPEECH BY H.E. DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE,


PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA AND CHAIRMAN OF CHAMA CHA MAPINDUZI DURING THE SIGNING CEREMONY OF THE AGREEMENT ON THE RE-UNIFICATION OF SPLM OF SOUTH SUDAN, ARUSHA,

21STJANUARY, 2015



SMZ YAKIRI KUWA SKULI NYINGI ZA ZANZIBAR ZINA UPUNGUFU WA WALIMU

0
0
Na Miza Othman –Maelezo Zanzibar. 

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekiri kuwa Skuli nyingi za Zanzibar  zinaupungufu wa walimu wa masomo hasa ya  Sayansi na Hesabati.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar  Zahra Ali Hamad  huko Chukwani katika ukumbi wa  Baraza la Wawakilishi wakati alipokuwa akijibu suala la Mh. Saleh Nassor Juma

Amesema katika kukabiliana na tatizo hilo Serikali imekuwa ikitumia mbinu mbali mbali katika kuongeza idadi ya walimu wa masomo ya Sayansi na Hesabati ikiwemo kuomba msaada wa walimu wa kujitolea kutoka mataifa na mashirika ya kujitolea kutoka mataifa mbali mbali.

Baadhi ya nchi na mashirika yaliyojitokeza kusaidia ni pamoja na  Shirika la VSO la Uingereza, Peace Corps la Marekeni, JICA la Japani, Koica la Korea na Serikali ya Nigeria kupitia “Technical Aids Corps” ambalo lilikubali kuleta  walimu 14  kufundisha masomo hayo.

“Kutokana na  kubadilishana uzoefu na ujunzi katika ufundishaji wa masomo ya Sayansi na Hesabati kati ya walimu wa kigeni na walimu wazalendo, kumepelekea ufaulu wa wanafunzi wengi katika mitihani ya kidato cha nne katika miaka ya hivi karibuni”, alisema Naibu Waziri.

Hata hivyo ameeleza kuwa Wizara yake inakusudia kutumia huduma za mtandao wa mawasiliano katika kusomeshea na kufundishia masomo mbalimbali kwa kutumia  uwezo mkubwa wa mkongo wa Taifa wa mawasiliano wa simu uliopo hapa Zanzibar.

Aidha amesema hadi hivi sasa ni taasisi chache tu za elimu ndizo zilizounganishwa na mkongo wa taifa  ikiwemo Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibzr, Chuo cha Kiislamu Mazizini, Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia na Skuli ya Sekondari ya Kiembe Samaki.

Skuli hizo zimeunganishwa na mtandao kupitia kampuni ya Simu ya Zanztel.  Pia Chuo Kikuu cha Taifa Cha Zanzibar kwa ufadhili wa Benki ya Dunia imepata fedha kwa ajili ya kuandaa maabara ya kurikodia vipindi mbalimbali vya masomo ya Sayansi na Hesabati. 
                  
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR. 

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA APOKELEWA KWA MAANDAMANO MAKUBWA JIMBO LA DONGE-MKOA WA KASKAZINI B.

0
0
 Katibu Mkuu Ndugu Kinana na Ujumbe wake ukipokelewa na vijana wa CCM jimbo la Donge wakiongozwa na Mbunge wao Mh.Sadifa Juma Khamis,mapema leo alipokuwa akisili kwenye ofisi za CCM-Donge Mtambalike wilaya ya Kaskazini B.Katibu Mkuu Ndugu Kinana yupo katika ziara ya Visiwa vya Unguja na Pemba-Zanzibar akihimiza Uhai wa chama cha CCM na kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010
  Pichani kulia ni Mbunge wa jimbo la Donge na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana Taifa (UVCCM) ,Mh.Sadifa Juma Khamis akimpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana pichani kati mara baada ya kuwasili katika jimbo hilo Wilaya ya Kaskazini B,mkoa wa Kaskazini B Unguja kwa ziara ya siku moja.Ndugu Kinana aliwasili katika ofisi za CCM Donge Mtambalike na kupokea taarifa ya chama ya wilaya na utekelezaji wa Ilani,na pia alizungumza na  Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Wilaya.
 Baadhi ya Wanahabari wakihangaika kutafuta shamra shamra za kuwasili kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana katika Jimbo la Donge mapema leo,wilaya ya Kaskazini B
 Ndugu Kinana akipokelewa kwa shangwe na baadhi ya wananchi wa jimbo la Donge,wilaya ya Kaskazini B mapema leo
 Baadhi ya akina mama Wajasiliamali wa kikundi cha ushirika wa Mtambile,wakifurahia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na ujumbe wake mapema leo katika jimbo la Donge wilaya ya Kaskazini B.
 Mtunza fedha wa kikundi cha ushiriki cha akina Mama ,Saccos (kukopa na kuweka),Bi Mwatime Juma Omar akitoa ufafanuzi mfupi kuhusiana na ushirika huo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana
 Mtunza fedha wa kikundi cha ushiriki cha akina Mama,Saccos (kukopa na kuweka),Bi Mwatime Juma Omar akitoa ufafanuzi mfupi kuhusiana na namna bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na wana ushirika hao,zikiwemo sabuni,dawa zamitishamba na megineo,Wilaya ya Kaskazini B
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akizungumza na watoto wa skuli ya maandalizi ya Donge Mtambile.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pichani wa pili kushoto na Mbunge wa Jimbo la Donge,Mh.Sadifa Juma Khamis wakikabidhi mifuko ya saruji kwa Mwalimu Mkuu wa Skuli ya msingi ya Donge Mtambini,Bwa.Bakari Ame Hussein,Jumla ya mifuko  50 ya saruji ilitolewa na Mbunge Sadifa kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa skuli hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameongoza na Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Zanzibar,Ndugu Vuai Ali Vuai wakiondoka katika skuli ya Mahonda mara baada ya kupokea taarifa ya ujenzi wa madarasa na kushiriki katika ujenzi .
Baadhi ya wananchi na Wafuasi wa Muembe Jogoo wakiwa wamekusanyika nje ya Ofisi tawi la CCM Mwembe Jogoo wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipofika kuzindua ofiisi hiyo katika jimbo la Kitope-Mahonda,wilaya ya Kaskazini B
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais,na Mbunge wa jimbo la Kitope-Mahonda,wilaya ya Kaskazini B,Mh.Balozi Seif Ali Idd
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Makamu wa Pili wa Rais-Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd wakitazama shughuli mbalimbali za vijana wa Mafunzo ya Amali katika fani ya ushonaji
Baadhi ya Wafuasi wa chama cha CCM,wakifuatilia mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Maskani ya CCM Kizota,jimbo la Kitope
Mbunge wa Jimbo la Donge na Mwenyekiti wa Jumuia ya Vijana Taifa  (UVCCM),Ndugu Sadifa Juma Khamis akiwahutubia wananchi na wafuasi wa chama hicho katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Maskani ya CCM Kizota,jimbo la Kitope.
Baadhi ya Wafuasi wa chama cha CCM,wakisikiliza yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Maskani ya CCM Kizota,jimbo la Kitope
Balozi Ali Karume akihutubia katika mkutano huo wa hadhara
Sehemu ya umati wa watu uliofika kwenye mkutano huo wa hadhara.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia Wananchi na wafuasi wa CCM,katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Maskani ya CCM Kizota,jimbo la Kitope,Ndugu Kinana aliwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya kuipigia kura na Waipigie kura ya ndiyo Katiba inayopendekezwa kwa kuwa ina mambo mengi mazuri yenye faida kwa Wanzibari.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd mara baada ya mkutano wa hadhara kumalizika,shoto nyuma ya Balozi ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.

OBI KUWEKEZA KWENYE SOKO LA SMARTPHONE ZENYE GHARAMA NAFUU TANZANIA

0
0
DSC_0248
Mkurugenzi Mtendaji wa Obi Mobiles, Afrika Mashariki na Kati na Afrika, Amit Rupchandani (katikati) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari )hawapo pichani) jijini Dar leo wakati wa utambulisho wa simu za aina ya smartphone zinazotengenezwa na Obi. Kushoto ni Mkurugenzi wa DESPEC Afrika, Farouk Jivani ambao ndio wasambazaji wakuu wa bidhaa hizo Tanzania na Afrika Mashariki na Kulia Mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano wa Obi, Yusuf Khan.(Picha na Zainul Mzige).

Na Andrew Chale
Kampuni mpya ya simu za Smartphone ya Obi Mobiles imezindua bidhaa zake katika soko la Tanzania pamoja na Nchi za Afrika Mashariki, kwa ubia na kampuni ya DESPEC wasambazaji wanaoongoza katika soko la usambazaji wa bidhaa za IT.

Wakizungumza na wandishi wa habari leo katika Hotel ya Serena, jijini Dar es Salaam, wakati wa utambulisho rasmi wa kampuni hiyo ya simu ya Obi iliyoanzishwa na mtaalam wa masoko na Mkurugenzi wa zamani wa kampuni ya Apple, John Sculley, Akizumgumza kwa niaba ya Sculley. Mkurugenzi Mtendaji wa Obi Mobiles, Afrika Mashariki na Kati na Afrika, Amit Rupchandani.

Alisema kampuni hiyo kwa kushirikiana na DESPEC, Obi inategemea kuanza kusambaza bidhaa zake zenye ubora zaidi katika robo ya kwanza ya mwaka huku ikitarajia kuweza kukamata soko la Tanzania kwa asilimia tano (5%) ifikapo mwisho mwa mwaka huu.
DSC_0235
Mkurugenzi wa DESPEC Afrika, Farouk Jivani (kushoto) ambao ndio wasambazaji wakuu wa bidhaa hizo Tanzania na Afrika Mashariki, akitolea ufafanuzi wa kituo cha huduma (services centre) ya simu hizo za Obi zitakazokuwa zikishughulikiwa hapa hapa nchini.

“Nia yetu ni kutumia Obi kwenye kila soko jipya ili kutengeneza bidhaa inayokubalika Kimataifa na hasa kwenye sehemu ambazo matumizi ya Smartphone yapo juu” alisema Amit Rupchandani.

Aliongeza kuwa, Katika uzinduzi uliofanyika India na Mashariki ya Kati, umeweza kuleta mafanikio makubwa kuliko walivyotegemea hivyo Obi imejiandaa na kuwekeza nguvu kupanua wigo wa biashara zake pia kwa soko la Tanzania.

Aidha, akielezea namna walivyojiandaa kushika soko la Afrika, Amit Rupchandani alisema soko la Afrika lina nafasi kubwa kwenye bidhaa za smartphone kutokana na ongezeko kubwa katika matumizi ya Teknologia na hasa miongoni mwa vijana.

DSC_0307
Mkurugenzi wa DESPEC Afrika, Farouk Jivani (kushoto) ambao ndio wasambazaji wakuu wa bidhaa hizo Tanzania na Afrika Mashariki, akionyesha aina moja ya simu za Obi ambazo zitakuwa na garantii ya mwaka mmoja na miezi minne. 

“Wateja wanataka kutumia Smartphone zilizo nzuri zenye bei nafuu bila kuathiri ubora wake. Pia kuna ongezeko la matumizi ya Iphone ukilinganisha na Smartphone. Utafiti wetu umeonesha ya kwamba wateja wanaweza kubadilisha matumizi ya bidhaa yeyote ilmradi wana imani nayo, hivyo Obi imejiandaa kukabiliana na hilo na hakika watazifurahia”. Alisema.

Aidha, Amit Rupchandani alibainisha kuwa, licha ya soko la bidhaa za simu za mkononi kuwa bidhaa za bei kubwa, wao hawatakuwa hivyo kwani lengo lao ni kuongeza watumiaji wa simu za mkononi ambao wangependa kutumia smartphone zenye ubora bila kuingia gharama kubwa.

“Falsafa yetu ya ‘Kama ulivyo’ inamaanisha Obi haibagui, inakuwezesha ulivyo ambapo tuna bidhaa mbalimbali kwa watu wa aina tofauti”. alimalizia Amit Rupchandani.
DSC_0313
Mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano wa Obi, Yusuf Khan (kulia) akionyesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) application mbalimbali zinazopatikana kwenye simu hizo.

Kwa upande wake, Mkurugezi wa DESPEC Afrika, Farouk Jivani alisema kampuni yake inayo furaha kuwa msambazaji wa kipekee wa bidhaa za Obi Mobiles Tanzania na Afrika Mashariki kwani wamejidhatiti kuhakikisha zinawafikia watumiaji sokoni.

“Kuingia kwa kwa bidhaa za Obi Mobiles sokoni kunaashiria ongezeko la matumizi ya simu za mkononi na pia matumizi ya intaneti, hivyo tunafanya juhudi kuhakikisha Obi inatengeneza jina la kudumu kwa bidhaa zake katika hili” alisema Farouk Jivani.

Obi Smartphone kwa soko la Afrika, inatarajiwa kuziduliwa mwezi Machi mwaka huu hapa Nchini ikifuatiwa na Nchi zingine za Afrika.
DSC_0318
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakikagua ubora wa simu za Obi.
DSC_0323
Kipeperushi kikionyesha aina mbalimbali za simu za smartphone za kampuni ya Obi zitakazokuwa zikiuzwa kuanzia shilingi 120,000 mpaka 340,000.
DSC_0325

Pata Filamu ya Foolish Age kupitia Mtandao.

0
0
Katika maisha binadamu ana nyakati tatu, Wakati uliopita, wakati uliopo na wakati ujao. Wakati uliopita na ujao hana mamlaka nao bali wakati uliopo ndio hazina yake ya kujenga mustakabali wake ila kikwazo kikuu ni umri wake. Kuna umri anahitaji matunzo na ulinzi unaitwa utoto na kuna umri anahitaji heshima na matunzo  unaitwa uzee halafu kuna umri unaitwa mtu kamili ila kabla yake upo umri matata unaitwa FOOLISH AGE . Fuatilia hii kupitia mtandao .....
Kwa Kuangalia Filamu hii ya Kitanzania iitwayo Foolish Age au Knunua na iwe yako kupitia mtandao.

Ili kuweza kuangalia au kununua kupitia Mtandao unachotakiwa kufanya ni kutembelea tovuti hii
Pia unaweza kuangalia au kununua filamu nyingine kupitia mtandao huo huo

East African commercial team to train in Nigeria for six months

0
0
The Heineken team at the headquarters in Nairobi geared up for the immersion training led by the General Manager Mr.Uche Unigwe (holding Heineken bottle at the back row).   
Jan 23, 2015 - Nairobi, Kenya – It is not uncommon for top performing employees in any company to be selected for training at company headquarters for a few days or weeks. However, Heineken East Africa is taking employee training to new levels as they are sending top performing commercial team members from the Kenya, Tanzania, and Uganda markets respectively to Lagos, Nigeria for six months to participate in full immersion training in Africa’s most populous country.
The brewer’s main headquarter sits at Amsterdam in Netherlands but the training will take place in Nigeria as it is not only home to Heineken’s biggest operation in Africa but it is amongst the leading Operating Companies of Heineken worldwide. In particular, Nigeria is a source of various commercial best practices that are relevant to East African markets.
According to Heineken East Africa General Manager, Mr. Uche Unigwe, this type of immersion training is critical to embedding One Heineken operating framework in East Africa which enables Heineken to deliver a world-class experience to their loyal consumers consistently.
The immersion training will become a part of standard operating procedure for Heineken East Africa moving forward in which another set of employees will be selected every six months and sent to Lagos.
While in Lagos, the commercial teams will manage key accounts as well as trade activations throughout Nigeria where the local operations have pioneered perfect execution. Additionally, it will allow the East African commercial team to monitor external business practices and set organisational benchmarks against the best, within and beyond the Heineken organisation.
“Realistically we can only expect our people to deliver at a world class level if they have actually seen and worked in such an environment.  By sending our team to Lagos for six months they will return to
East Africa with a broader vision as to not only what is expected but also what is possible and this enhanced point of view will ultimately benefit our partners, outlets, and our consumers” added Mr. Uche Unigwe.
According to Musa Huko from Heineken Kenya he had never imagined this high level of training when he joined Heineken 3 years ago. “I am very thankful and optimistic about this opportunity not only to enhance my personal sales skills but also to use what I learn in Nigeria to better serve my home market Kenya” said Musah further stating, “I think one of the great aspects about working with Heineken is that the constant pursuit of excellence propels us to be better masters of our craft.”
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live




Latest Images