Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

WAZIRI WA MAJI JUMANNE MAGHEMBE ATOA SIKU 90, KWA MKANDARASI MEGHA ENGINEERING

0
0

Waziri wa Maji Jumanne Maghembe wapili kulia akioneshwa mchoro wa mradi wa bomba la maji  mlandizi kimara linalopitia makongo juu na Mhandisi wa Mradi huo, Bw Severin Mkendala jinsi mabomba  mradi wa mlandizi kimara yalipopita .
unnamed (10) 
Mashine aina ya Catterpilar la kampuni ya Megha Enginearing Infastructure Limited, likiwa linasafisha eneo ambalo linatakiwa kulazwa mabomba ya yanayotoka Mlandizi Kimara kwenda Ruvu JUU.unnamed (7) 
Kushoto ni Meneja Mradi kutoka Kampuni ya Megha Engenearin Infastructure Limited Mural Mohan, akimweleza maendeleo ya mradi huo Waziri wa Maji Jumanne Maghembe,aliyekuwa katika ziara  ya kutembelea miradi  inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka.unnamed (8) 
Waziri wa Maji Jumanne Maghembe akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukamilisha ziara hiyo.
 
unnamed (5)Wafanyakazi wa kampuni ya WABAG Constraction wakiendela na ujenzi wa wa kituo cha kuasfisha maji cha ruvu juu .
Waziri wa maji Jumanne Maghembe wa kwanza kulia akizungumza na wakandarasi wanaojenga bomba la maji la Mlandizi Kimara Januari 20, 2015 mkoani Pwani wakati alipotembelea tembelea miradi ya maji inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na maji Taka (DAWASA),  kwalengo la kupata tathimini ya mradi huo ulipofikia sasa.

…………………………………………………………………………………….
WAZIRI wa maji Jumanne Maghembe ametoa siku 90, kwa mkandarasi Megha Engineering Infrastructure Limitedi anaesambaza bomba la maji mradi wa Mlandizi Kimara kufanikisha mradi huo na kupeleka ripoti ya maradi,mamlka ya maji safi na maji taka (Dawasco), kwalengo la kupata tathimini ya mradi.

Alitoa agizo hilo Januari 20, 2015 mkoani Pwani wakati akikagua miradi minne ya Dawasco,yakusambaza maji Ruvu juu na Ruvu Chini kufikisha Jijini Dar es Salaam.
 Alisema,mpaka sasa mkandarasi alitakiwa aweamelaza kilomita 20,lakini chakushangaza mkandarasi huyo amelaza kilomita 12,tu.Maghembe alisema utendaji kazi wa mkandarasi huyo ni mbovu na nimewaagiza wabadilike na nitakuja kuwatembelea baada ya siku 90,na kama hakutakuwa na maendeleo itabidi tuwafukuze.

“tumempatia mkandarasio huyu kiasi cha dola za kimarikani 59,ambao nisawa na bilioni 96 za kitanzani fedha hizi watanzania watazilipa hivyo ni vema mkandarasi huyu afanye kazi iliyomleta,”alisema Maghembe

Kwaupande wa maradi wa Ruvu juu wa kusafisha maji Waziri Maghembe aliridhika na utendaji kazi wa mkandarasi anayejenga mradi huo na kumtaka amalizie kufunga pampu mpya ili mgao wa maji upungue Dar es Salaam.

Aidha alimwagiza Mkurugenzi Mkuu wa DAWASA Arcado Mutalemwa kuhakikisha pampu zilizokwama bandarini zinafika leo na kufungwa siku ya Alhamisi.

Statement on SPLM Agreement in Arusha

0
0


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
 Telephone:255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz              

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      STATE HOUSE,
              1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

The warring factions of the Sudanese Peoples Liberation Movement (SPLM) of South Sudan will tomorrow (Wednesday, January 21, 2015) sign an agreement on the re-unification of their movement, in a major step towards resolving the current political crisis that has plunged the country into a tragic and unprecedented civil war.

          The Presidents of South Africa, Uganda and Kenya and the Prime Minister of Ethiopia will join Tanzanian President Jakaya Mrisho Kikwete in witnessing the signing to take place at the Ngurdoto Mountain Lodge in Arusha. 

          Both President Salva Kiir and Former Vice President Dr. Rick Machar will sign for their respectful SPLM factions. A leader of the SPLM-Former Detainees will also sign on behalf of his faction.

The agreement is result of an intra–SPLM Dialogue attended by delegations of the three SPLM Groups which has been taking place in Arusha under the auspices of Tanzania’s ruling party, Chama cha Mapinduzi (CCM).

Following a request by the chairman of SPLM, President Salva Kiir,  CCM agreed, last year, to mediate between SPLM groups – SPLM in Government, SPLM in Opposition and SPLM – Former Detainees – which appeared as a result of the political crisis.

 The talks in Arusha, which first took place between 12-20 October, last year, were chaired by former Chairman of CCM, John Samwel Malecela and facilitated by CCM Secretary General, Mr. Abdulrahman Kinana.

The latest talks, which resulted in the agreement, took place in both December last year and beginning January 8th this year. The agreement will be followed by the process of implementation during which time CCM will continue assisting.

The Process in Arusha sought at re-uniting SPLM and was therefore complimentary to the Peace Talks taking place in Addis Ababa, Ethiopia.
President Kikwete arrived in Arusha this evening (Tuesday, January 20, 2015) ready for the signing ceremony tomorrow.

Ngoma Africa band na Jinamizi lao la Bongo Dansi barani ulaya lazidi kuwanasa washabiki

0
0
Muziki wa Bongo Dansi unapogeuka mzimu na kuwapeleka puta washabiki !

Pia wanamuziki FFU-Ughaibuni kukosa Usingizi.

Ujerumani,

Imebainika kuwa bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU-ughaibuni almaarufu viumbe wa ajabu Anunnaki Alien,inayoongoza na mwanamuziki Ebrahim Makunja aka kamanda Ras Makunja,bendi hiyo imejukuta ipo katika hali ya kukosa usingizi tena baada ya kutakiwa kutumbuiza maomyesho zaidi katika msimu ujao wa joto.
 
watayarishaji wa maonyesho makubwa ya nje barani ulaya wanashinikizwa na washabiki wao lazima waipandishe jukwaani Ngoma Africa Band kutokana na mdundo wao Bongo dansi,maporota hao baada kuweka roho juu na washabiki wao nao wamedhamiria kuwapambanisha washabiki hao na bendi maarufu Ngoma Africa band yenye makao yake nchini ujerumani.
 
Habari za uhakika zimetonya kuwa bendi hiyo imekubali kuenda kutumbuiza katika nchi za Latvia na Austria na maonyesho mengine katika msimu wa joto. habari zimetonya kuwa hali hiyo tabia za washabiki kushinikiza katika maonyesho inaifanya bendi ya Ngoma Africa band kuwa katika mzunguko wa maonyesho makubwa na wanamuziki kukosa muda wa kupumzika.Lakini inasemekana kamanda Ras Makunja na kikosi chake wanauwezo wa aina yake wa kuwamudu washabiki wao waliodata akili na jinamizi la muziki wa dansi wa bongo kule barani ulaya.ffu-ughaibuni pia wanasikika online at www.ngoma-africa.com.



 

.Dr. Binilith Mahenge fanya ziara bandari ya Tanga

0
0

unnamed (2)5 
Sehemu ya Bandari ya Tanga ikionesha kisiwa cha Toten kilichopo Mkoni hapo ambacho kipo hatarini kuzama. unnamed (2)1 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Mhe.Dkt.Injinia Binilith Satano Mahenge (wa pili kushoto) akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Tanga Bw. Fred Liundi (kushoto) pamoja na viongozi wa Mkoa wa Tanga wakielekea kupanda Boti  kwenda kuangalia kisiwa cha Toten ambacho kiko hatarini kuzama.
unnamed (2)3 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Mhe.Dkt.Injinia Binilith Satano Mahenge (kulia), akikagua Kisiwa cha Toten kilichopo mkoani Tanga. unnamed (2)4 
Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Tanga Bw. Fred Liundi akitoa maelezo kwa Waziri wa  Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Mhe.Dkt.Injinia Binilith Satano Mahenge,kuhusu umuhimu wa kisiwa hicho.

KUTOKA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR.

0
0
 Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho katikati akisindikizwa na Askari wake kutoka katika ukumbi wa Baraza Baada ya kuhairishwa kwa kikao hicho kilichoanza  leo Mbweni nje ya mji wa Zanzibar.
 Waziri wa Miundo mbinu na mawasiliano Juma Duni Haji kushoto akiwa pamoja na Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Nasor Ahmed Mazrui nje ya ukumbi wa Baraza la Wawaklilishi Mbweni nje ya mji wa Zanzibar.
 Mwakilishi wa Jimbo la Wawi Saleh Nasor Juma akibadilishana mawazo na mwakilishi wa kuteuliwa nafasi za wanawake Wanu Hafidh Ameir nje ya ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbwenu nje ya mji wa Zanzibar.
 -Mwakilishi wa Jimbo la Wawi Saleh Nasor Juma wakizungumza jambo na Mwakilishi wa Jimbo la Mji mkongwe Ismail Jussa Ladhu nje ya ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni nje ya mji wa Zanzibar.
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Ikulu na Utawabora DKT Mwinyihaji Makame kulia akibadilishana mawazo na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Saidi Hassan Saidi nje ya ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni nje ya mji wa Zanzibar.PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

Pata Filamu ya FEDHEHA kupitia Mtandao.

0
0
Katika maisha tunayoishi duniani sio vizuri kufanyiana mabaya, Kwani hujui kesho itakuaje. Malipo ni hapahapa Duniani . Fuatilia hii kupitia mtandao .......

Kwa Kuangalia Filamu hii ya Kitanzania iitwayo Fedheha au Knunua na iwe yako kupitia mtandao.

Ili kuweza kuangalia au kununua kupitia Mtandao unachotakiwa kufanya ni kutembelea tovuti hii


Pia unaweza kuangalia au kununua filamu nyingine kupitia mtandao huo huo.

MAAFISA WA JESHI LA MAGEREZA WAPEWA MAFUNZO KUHUSU TAKWIMU RASMI

0
0
 Meneja Tawala wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Gabriel Madembwe (katikati) akiwahutubia Maafisa wa Ngazi za Juu wa Jeshi la Magereza kutoka vitengo mbalimbali vya Makao Makuu ya Jeshi hilo wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Takwimu Rasmi yaliyofanyika leo mkoani Morogoro. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Dkt. Frank Mkumbo  na kulia ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Magereza Makao Makuu Bw. Edward Kaluvya.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari wakichukua habari wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Takwimu Rasmi kwa Maafisa wa Ngazi za Juu wa Jeshi la Magereza kutoka vitengo mbalimbali vya Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Amabilisi uliopo mkoani Morogoro.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Dkt. Frank Mkumbo  akiwa katika mahojiano na Waandishi wa Habari mara baada ya ufunguzi wa Mafunzo ya Takwimu Rasmi kwa Maafisa wa Ngazi za Juu wa Jeshi la Magereza kutoka vitengo mbalimbali vya Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Amabilisi uliopo mkoani Morogoro.

MAAFISA WA JESHI LA MAGEREZA WAPEWA MAFUNZO KUHUSU TAKWIMU RASMI
 
Na Veronica Kazimoto
Morogoro
21 Januari, 2015.
 
Wito umetolewa kwa Maafisa wa Ngazi za Juu wa Jeshi la Magereza kutoka vitengo mbalimbali vya Makao Makuu ya Jeshi hilo kuwahimiza maofisa waliopo chini yao kutumia takwimu mbalimbali zinazozalishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ili zisaidie katika kuandaa mipango na kutoa maamuzi mbalimbali ya kazi zinazofanywa na jeshi hilo.
 
Wito huo umetolewa leo na Meneja Tawala wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Gabriel Madembwe wakati akifungua Mafunzo ya Takwimu Rasmi kwa Maafisa wa Ngazi za Juu wa Jeshi hilo yaliyofanyika katika ukumbi wa Amabilisi uliopo mkoani Morogoro.
 
Madembwe amesema kuwa maafisa wengi katika Jeshi la Magereza wakijua umuhimu wa matumizi ya takwimu itasaidia kuleta mabadiliko hasa katika kupanga mipango yao kwenye maeneo yao ya kazi.
 
"Napenda kusisitiza kuwa ili mabadiliko yatokee sehemu yoyote ile; iwe nyumbani,  kazini au katika jamii, ni lazima kuwepo na kichocheo cha mabadiliko hayo, hivyo ninyi mtakuwa kiungo muhimu katika kuleta mabadiliko yenye kutoa maamuzi kwa kuzingatia matumizi ya takwimu rasmi", amesema Madembwe.
 
Nae Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Magereza kutoka Makao Makuu Dar es Salaam Bw. Edward Kaluvya amesema mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka ambapo kwa sasa wamekuwa wakitumia sana takwimu katika maeneo mengi ya kazi zao.
 
"Mafunzo haya yatatusaidia kujenga uelewa wa pamoja na kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayohusiana na uzalishaji, uhifadhi na utumiaji wa takwimu kwa usahihi katika kutoa maamuzi na kupanga mipango endelevu katika Jeshi letu la Magereza'', amefafanua Kaluvya.
 
Mafunzo haya ya siku tatu yanatolewa na Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika kilichopo jijini Dar es Salaam na yamefadhiliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kupia Mpango Kabambe wa Kitaifa wa Kuboresha na Kuimarisha Takwimu Tanzania (TSMP).
 
Lengo kuu la Mpango huu ni kuhakikisha Tanzania inakuwa na mfumo imara wa kitaifa wa kuratibu, kukusanya, kuhifadhi na kusambaza takwimu nchini.
 

Mh.Ummy Mwalimu afanya ziara ya kikazi ya siku moja ya kutembelea baadhi ya viwanda jijini Arusha

0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Ummy Mwalimu amefanya ziara ya kikazi ya siku moja katika baadhi ya viwanda vya Arusha lengo likiwa ni  kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya Serikali kuhusu viwanda kutotumia magogo kama nishati ya uzalishaji viwandani.
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Ummy Mwalimu (Katikati) akipata taarifa fupi kutoka kwa kwa uongozi wa Mkoa wa Arusha mara baada ya kufanya ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani hapo kuangalia masuala ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Felix Ntibenda na Katibu Tawala wa Mkoa Bw. Mapunda.


 Moja ya boiler inayotumia makaa ya mawe katika Kiwanda cha Sunflag. Awali Kiwanda hicho kilikuwa kinatumia nishati ya Magogo katika shughuli za uzalishaji kiwandani hapo. Serikali imepiga marufuku matumizi ya magogo ili kuhifadhi mazingira
 Shehena ya magogo iliyobaki katika Kiwanda cha Sunflag. Kiwanda hicho kwa sasa kimebadilisha matumizi ya nishati ya uzalishaji kutoka kwenye magogo na kutumia makaa ya mawe.
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Ummy Mwalimu akiongea na Bw. Binesh Haria Afisa Mwendeshaji wa Kiwanda cha A to Z cha Jijini Arusha. Naibu Waziri alikuwa na ziara ya ukaguzi wa masuala ya Mazingira kiwandani hapo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Ummy Mwalimu akiongea na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha Bw.  Fidelis Lumato mara baada ya kutembelea kiwanda cha A –Z cha Jijini hapo kukagua masuala ya Mazingira.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeshatayarisha kanuni za usalama wa barabarani za kutoza faini za papo kwa papo-Mh.Mohamed Aboud

0
0
Na Abdulla Ali Maelezo- Zanzibar  .
                             
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mhe. Mohamed Aboud Mohamed amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeshatayarisha kanuni za usalama wa barabarani za kutoza faini za papo kwa papo kama ilivyo sasa kwa upande wa Tanzania Bara.

Hayo ameyaeleza katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar wakati akijibu swali la mwakilishi wa Jimbo la Kwahani Mhe. Ali Salum Haji.

Waziri Mohamed amesema kuwa kanuni za sheria ya usalama  barabarani kwa upande wa Zanzibar zipo kwa Mwanasheria Mkuu  kwa hatua za mwisho na zitaanza kutumiwa na Jeshi la Polisi mara baada ya kukamilika rasmi kwa kutoza faini ya papo kwa papo kwa wote watakaofanya makosa ya usalama wa barabarani.

Waziri Aboud ametanabahisha kuwa kwa sasa Zanzibar Sheria Nambari 7 ya Mwaka 2003 (R.E 2006) ndio inayosimamia masuala ya usalama barabarani na kwa mujibu wa sheria hiyo kifungu namabari 180 hadi 184 vimeelezea kuhusiana na utaratibu wa faini ya papo kwa papo kwa vyombo vya moto vinavyovunja sheria za usalama wa barabarani Nchini.

Aidha amesema Jeshi la Polisi lina jukumu la kusimamia na kutekeleza Sheria zilizotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar  ambapo kwa upande wa Tanzania Bara Sheria inayohusika na usalama wa barabarani ni Sheria nambari 168 ya Mwaka 2002.

“Miongoni mwa majukumu ya Jeshi la Polisi ni kusimamia na kutekeleza Sheria zilizotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar”, alieleza waziri Mohamed.

Hivyo ameeleza kuwa kupitia Sheria hiyo Jeshi la Polisi hutekeleza sheria za faini ya papo kwa papo kwa vyombo vya moto vinavyovunja sheria za usalama barabarani na kusaidia Serikali kukusanya fedha nyingi zinazotokana na makosa hayo.

Jeshi la polisi ni Jeshi la Jamhuri ya muungano wa Tanzania na limeundwa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 chini ya ibara ya 147 ya kuanzishwa kisheria chini ya kifungu nambari 3 cha sheria ya polisi na polisi wasaidizi Cap.322 R.E ya mwaka 2002.

kutokuwepo mashine za kisasa za kupimia bidhaa ndiko kunakopelekea kukosekana kwa vipimo vya kisasa-Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko

0
0
Na Abdulla Ali Maelezo- Zanzibar    .
                         

Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Mhe. Nassor Ahmed Mazrui amesema kutokuwepo kwa mashine za kisasa za kupimia bidhaa ndiko kunakopelekea kukosekana kwa vipimo vya kisasa, vya kitaalamu na vya uhakika vya bidhaa hizo na kupelekea uingizwaji wa bidhaa feki.



Hayo ameyaeleza katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani Mhe. Ali Salum Haji. 



Waziri Mazrui ametanabahisha kuwa kutokana na ukosefu wa vifaa hivyo ikiwemo mashine ya ICP kunafanya baaadhi ya bidhaa kushindwa kufanyiwa vipimo wakati zinapoingizwa nchini na kusababisha hasara na madhara makubwa kwa watumiaji wa bidhaa hizo kwani nyingi zao huwa ni feki. 




Waziri Mazrui amesema kutokana na ukuaji wa biashara nchini kumejitokeza baadhi ya wafanyabiashara ambao huingiza bidhaa feki za kulainisha vyombo vya moto kama vile Girisi na Oil pamoja na vyakula vilivyokwisha muda wake.



“Kwanza naomba kukiri kuwa kwa hivi sasa Wizara yangu haina utaratibu wa kukagua bidhaa za vilainisho ingawa nakubaliana na mjumbe kuwa hii ni mojawapo ya bidhaa au huduma nyengine zinazopaswa kusimamiwa”, alieleza Waziri Mazrui.



Aidha Waziri Mazrui amewaomba viongozi na Wajumbe wa Baraza hilo kushirikiana na taasisi nyengine za serikali kuangalia mfumo bora wa kusimamia biashara hizo ambazo kwa sasa hazina mfumo mzuri wa kuzisimamia sambamba na kuwataka wananchi kutoa taarifa kwa Wizara yake pale ambapo wanagundua uingizwaji au uuuzwaji wa bidhaa feki madukani.

Vitendo vinavyokwenda kinyume na maadili ya kijamii vyashamiri kwa kasi miongoni mwa vijana wa Zanzibar .

0
0
Na Abdulla Ali Maelezo- Zanzibar .
                             

Vitendo vinavyokwenda kinyume na maadili ya kijamii vimekuwa vikishamiri kwa kasi miongoni mwa vijana wa Zanzibar licha ya viongozi wa Dini, Wazee na Walimu kuvikemea vitendo hivyo.



Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mhe. Bi Hindi Hamad Khamis wakati akijibu swali la mwakilishi wa Jimbo la Muyuni Mhe. Jaku Hashim katika mkutano wa  18  wa Baraza la Wawakilishi ulioanza leo Chukwani Zanzibar.



Amesema kuwa hivi sasa imekuwa ni jambo la  kawaida kwa baadhi ya vijana wa kiume hususan wa Kizaanzibari kutoboa masikio, kusuka nywele na kujipodoa jambo ambalo ni kinyume cha sheria, Silka na Utamaduni wa Mzanzibari.



Mhe Bi Hindi amesema Serikali imechukua hatua mbalimbali katika kupambana na tatizo la uvunjifu wa Mila, Silka na Desturi ikiwa ni pamoja na kushajihisha kutolewa elimu ya Dini na Malezi, Kulinda na Kuhimiza uendelezaji wa Utamaduni pamoja na kusambaza ustaarabu wa Mzanzibari kwa njia ya Sanaa ya Maonyesho, Semina na Makongamano.




Mhe. Bi Hindi ametanabahisha kuwa ili kuondokana na vitendo hivyo viovu, Serikali inapitia upya sheria zilizopo zinazohusiana na mambo ya Mila, Silka na Desturi kwa lengo la kuzipa nguvu ili kupunguza kasi ya vitendo vinavyoipaka matope Zanzibar ambavyo kwa kiasi kikubwa vinachangiwa na uwepo wa utandawazi duniani kote.



Aidha amesema tatizo liliopo sio kutokuwepo kwa sheria bali ni usimamizi wa sheria hizo na kuthibitishwa kwa makosa mbele ya vyombo vya sheria ili kuweza kuchukuliwa hatua zinazofaa.



 “Kwa kulipatia ufumbuzi tatizo hili, sisi sote hapa ni viongozi na wananchi kwa ujumla tunatakiwa kushirikiana kupiga vita vitendo hivyo na kutilia nguvu usimamizi wa sheria tunazozitunga”, alieleza Naibu waziri Bi hindi.



Mhe. Bi Hindi amewataka Viongozi, Walimu, Viongozi wa Dini  na Wananchi kwa ujumla kushirikiana pamoja katika kupiga vita vitendo hivyo viovu na kutilia mkazo usimamizi wa sheria ili kulipatia ufumbuzi tatizo hilo.



IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR


VIDEO MPYA: Y-TONY FT BARNABA - MAMA

0
0

Wilaya ya Rufiji yapokea vifaa tiba

0
0
 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Seif Rashid (aliyevaa shati la batiki) akishirikiana na wananchi wa kijiji cha Nyamwage  kata ya Mbwala wilayani Rufiji mkoa wa Pwani kufungua kitanda kwa ajili ya akinamama kujifungulia hivi karibuni wakati anakabidhi vifaa tiba kwa ajili ya wilaya hiyo. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Giant Surgical and Pharmaceutical inayojishughulisha na masuala ya afya na tiba Peter Joseph Karia ambayo imechangia kufanikisha upatikanaji wa baadhi ya vifaa tiba vilivyokabidhiwa katika zahanati Nyamwage kata ya Mbwala hivi karibuni.
 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Seif Rashid akimshukuru Mkurugenzi wa kampuni ya Giant Surgical and Pharmaceutical inayojishughulisha na masuala ya afya na tiba Peter Joseph Karia ambayo imechangia kufanikisha upatikanaji wa baadhi ya vifaa tiba vilivyokabidhiwa katika zahanati Nyamwage kata ya Mbwala hivi karibuni.
Baadhi ya akina mama wakimshukuru Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Seif Rashid kwa kuwapatia vifaa tiba kuwalinda na  kuimarisha afya ya mama na motto. (Picha zote na Eleuteri Mangi- MAELEZO).




 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Seif Rashid akiongea na wananchi wa kata ya Mbwala wilayani Rufiji mkoa wa Pwani Juma Ligomba hivi karibuni kabla ya kukabidhi vifaa tiba ambavyo vitakavyotumika katika zahanati mbalimbali wilayani humo.
 Diwani wa kata ya Mbwala wilayani Rufiji mkoa wa Pwani Juma Ligomba akimkaribisha Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Seif Rashid kuongea na wananchi wa kata hiyo hivi karibuni kabla ya kukabidhi vifaa tiba ambavyo vitakavyotumika katika zahanati mbalimbali wilayani humo.
 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Seif Rashid (kushoto) akiteta jambo na diwani wa kata ya Mbwala wilayani Rufiji mkoa wa Pwani Juma Ligomba (kulia) wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa tiba ambavyo vitakavyotumika katika zahanati mbalimbali wilayani humo. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Giant Surgical and Pharmaceutical inayojishughulisha na masuala ya afya na tiba Peter Joseph Karia ambayo imechangia kufanikisha upatikanaji wa baadhi ya vifaa tiba vilivyokabidhiwa katika zahanati Nyamwage kata ya Mbwala hivi karibuni.
 Wananchi wa kijiji cha Nyamwage kata ya Mbwala wilayani Rufiji mkoa wa Pwani wakimkasikiza Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Seif Rashid hivi karibuni kabla ya kukabidhi vifaa tiba ambavyo vitakavyotumika katika zahanati mbalimbali wilayani humo.

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALLY IDD AHUDHURIA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA CBE LEO.

0
0
 Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Emanuel Mjema (wa pili kutoka kulia) akimtambulisha viongozi wa chuo cha CBE ,Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd (katikati) leo jijini Dar es salaam wakati wa maadhimisho ya chuo hicho kutimiza miaka 50. Kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdallah Kigoda.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd akipata maelezo kutoka kwa  Bi. Esther Kibua, mwanafunzi wa mwaka wa 3 wa chuo cha Elimu ya Biashara CBE kampasi ya Dar es salaam juu ya namna chuo hicho kinavyowaandaa kuitumia elimu wanayoipata chuoni hapo pindi watakapomaliza masomo yao.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd akimuuliza swali Bi. Esther  Kibua, mwanafunzi wa mwaka wa 3 wa chuo cha Elimu ya Biashara CBE kampasi ya Dar es salaam  alipotembelea banda la maonesho la wanafunzi wa Chuo cha CBE leo jijini Dar es salaam wakati wa sherehe za  kilele cha miaka 50 ya chuo hicho.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd akifafanua akifafanua jambo alipotembelea banda la maonesho la Idara ya Mizani na Vipimo la Chuo cha CBE leo jijini Dar es salaam wakati wa sherehe za  kilele cha miaka 50 ya chuo hicho.Kushoto ni Mwalimu wa Idara ya Mizani na Vipimo wa Chuo hicho Bw. Faraja Nyoni.Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.
 

NHC LAFANYA KONGAMANO LA MAMENEJA WA MIKOA NA WATENDAJI WENGINE JIJINI ARUSHA.

0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza jambo katika kongamano hilo ambapo alisisitiza umuhimu wa Watendaji wa NHC kuongeza ubunifu katika kazi zao ili kuongeza ufanisi wa kazi zao.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akikabidhi zawadi ya simu ya kisasa ya I Phone 6 kwaajili ya kuboresha ufanisi kwa Ofisa Mwandamizi Uendelezaji Biashara Fatima Rajabu ambaye aliibuka mshindi wa jumla wa maigizo ya vitendo kwenye kongamano la Mameneja wa Mikoa na Watendaji wengine linalofanyika katika hoteli ya Naura Springs, Arusha. Kongamano linakusudia kuwajengea uwezo wa kiuongozi wa kusimamia uuzaji wa nyumba zinazojengwa na NHC katika maeneo mbalimbali nchini. Katika kongamano hilo, mada mbalimbali zinaendelea kutolewa ikiwemo kuwajali wateja, misingi ya uhusiano na ujenzi wa taswira ya Shirika na uwekezaji katika sekta ya usimamizi na uendelezaji wa Miliki.
Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba (NHC), David Shambwe akitoa mada kwenye kongamano hilo. Shambwe alizungumzia hatua muhimu za kuibua miradi kuitekeleza na hatimaye kuiuza kwa ufanisi kwa wateja na kufuatilia malipo baada ya kuuza nyumba zinazojengwa maeneo mbalimbali nchini. 
  Mkurugenzi mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu alipata nafasi ya kujadiliana na  mameneja na watumishi wa shirika la Nyumba la Taifa waliohudhuria kongamamo la Arusha kuhusiana na mafanikio na changamoto zinazowakabili  .


Mhadhiri Mwandamizi na Mtalamu Mshauri wa masuala ya Uhasibu, Usimamizi wa Fedha na Menejimenti wa Chuo Kikuu cha Uongozi Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI) Felix Kariuki Kamau akitoa somo kwenye kongamano hilo ambapo alizungumzia kwa kina masuala ya usimamizi wa Fedha na kuboresha tafiti kabla ya kuwekeza katika maeneo mbalimbali, lakini pia michakato muhimu ya kuzingatia ili kuweza kuuza nyumba nyingi zaidi.
 Meneja wa NHC mkoa wa Mtwara, Joseph John akielezea mikakati ya uendelezaji ujenzi katika mkoa wake mafanikio pamoja na changamoto.
Meneja wa NHC mkoa wa Kinondoni, Benith Masika akielezea mikakati ya uendelezaji ujenzi katika mikoa minne ya Shirika mafanikio pamoja na changamoto.
Meneja wa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa, Tuntufye Mwambusi akizungumza kwenye kongamano hilo.
 Washiriki wakifuatilia kwa makini kongamano hilo linalofanyika katika hoteli ya Naura Springs, linafanyika kwa wiki nzima.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi NHC TAMICO, Danny Nkya akifuatilia kwa makini kongamano hilo.
 Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa Felix Maagi na Haikamen Mlekio wakifuatilia mada na mijadala inayoendelea katika kongamano hilo 
 Washiriki wakifuatilia kwa makini kongamano hilo linalofanyika katika hoteli ya Naura Springs, linafanyika kwa wiki nzima.
  Mkurugenzi mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu alipata nafasi ya kujadiliana na  mameneja na watumishi wa shirika la Nyumba la Taifa waliohudhuria kongamamo la Arusha kuhusiana na mafanikio na changamoto zinazowakabili  .
  Mkurugenzi mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu alipata nafasi ya kujadiliana na  mameneja na watumishi wa shirika la Nyumba la Taifa waliohudhuria kongamano la Arusha kuhusiana na mafanikio na changamoto zinazowakabili  .
  Mkurugenzi mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu alipata nafasi ya kujadiliana na  mameneja na watumishi wa shirika la Nyumba la Taifa waliohudhuria kongamano la Arusha kuhusiana na mafanikio na changamoto zinazowakabili  .
Mkurugenzi mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu alipata nafasi ya kujadiliana na  mameneja na watumishi wa shirika la Nyumba la Taifa waliohudhuria kongamano la Arusha kuhusiana na mafanikio na changamoto zinazowakabili  .
Wakurugenzi wa NHC, DAvid Shambwe, Issack Peter na Raymond Mndolwa wakijadiliana jambo nje ya kongamano hilo .
  Mkurugenzi mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu alipata nafasi ya kujadiliana na  mameneja na watumishi wa shirika la Nyumba la Taifa waliohudhuria kongamano la Arusha kuhusiana na mafanikio na changamoto zinazowakabili .
 Mhadhiri wa  Chuo Kikuu cha Uongozi Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI), Jackson Kilimba akitoa mada kuhusiana na majadiliano, michakato yake na namna ya kuitekeleza.
Washiriki wakifuatilia kwa makini kongamano hilo linalofanyika katika hoteli ya Naura Springs, linafanyika kwa wiki nzima.
  Washiriki wakifuatilia kwa makini kongamano hilo linalofanyika katika hoteli ya Naura Springs, linafanyika kwa wiki nzima.
 Washiriki wakifuatilia kwa makini kongamano hilo linalofanyika katika hoteli ya Naura Springs, linafanyika kwa wiki nzima.
Washiriki wakifuatilia kwa makini kongamano hilo linalofanyika katika hoteli ya Naura Springs, linafanyika kwa wiki nzima.

PINDA AKUTANA NA WAWEKEZAJI KUTOKA RUSSIA

0
0

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na ujumbe wa Kampuni kutoka Russia ya Mantra Tanzania Limited inayokusudia kuwekeza katika Mradi Uranium wa Mto Mkuju, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Januari 21, 2014. Kushoto ni Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Uwekezaji na Uwezeshaji, Dr. Mary Nagu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)unnamed (37) 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dr. Mary Nagu  (kulia)  akiteta na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Bibi Tonia  Kandiero baada ya mazungumzo yao, Ofisini kwa Dr. Nagu jijini Dar es salaam  Januari 21, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MKUTANO WA UPATANISHI WA CHAMA CHA SPLM YA SUDAN KUSINI JIJINI ARUSHA LEO

0
0

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi wenzie  leo JumatanoJanuray 21, 2015 kabla ya kuanza kwa mkutano wa utiaji sainimakubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusinikatika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha. Kutoka kushoto ni Makamu waRais Dkt Mohamed Gharib Bilal,, Naibu Rais wa Afrika Kusini,  MheCyril Ramaphosa, Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Kikwete, RaisSalva Mayardit Kiir, wa Sudani ya Kusini, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenyana Makamu wa Rais wa Zamani wa Sudani ya Kusini Dkt Riek Machar,unnamed (48) 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
leo Jumatano Januray 21, 2015 kabla ya kuanza kwa mkutano wa utiaji
saini makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani
Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha. unnamed (49) 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Yoweri Museveni  leo
Jumatano Januray 21, 2015 kabla ya kuanza kwa mkutano wa utiaji saini
makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini
katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.
unnamed (52) 
unnamed (50) 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mjane wa Mwenyekiti waZamani wa SPLM Mama Rebecca Nyandeng Garang de Mabior leo JumatanoJanuray 21, 2015 kabla ya kuanza kwa mkutano wa utiaji sainimakubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusinikatika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.

UVCCM ZANZIBAR WAFANYA MATEMBEZI YA MSHIKAMANO KUUNGA MKONO HOTUBA YA DKT.SHEIN

0
0
Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar, Shaka Hamdu Shaka akiwahutubia mamia ya vijana baada ya kupokea matembezi ya mshikamano na kufanya mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Magogoni Kwa Mabata mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kupongeza hotuba ya Rais wa Zanzibar na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibr Dr. Ali Mohamed Shein aliyoitoa tarehe 12/1/2015 katika viwanja vya Amani mjini Zanzibar.

 Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar, Shaka Hamdu Shaka akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mjini Ndugu Borafya Silima wakati akiwasili katika viwanja vya Magogoni kwa Mabata kwa ajili ya kupokea matembezi ya vijana mshkamano na kuwahutubia.
  Vijana kutoka majimbo mbalimbali wakiwa wamekaa katika mkutano huo.
Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye viwanja vya Magogoni kwa Mabata wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo wa kuipongeza hotuba ya Rais Dkt.Shein aliyoitoa hivi karibuni.
Wadau.Wanahabari kutoka Unguja wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo.
 4 
Umati wa vijana ukiwa kwenye mkutano huo uliofanyika kwenye viwanja wa vya Magogoni kwa Mabata. 5 
Umati wa vijana kutoka mikoa mbalimbali ukiwa kwenye mkutano huo uliofanyika kwenye viwanja wa vya Magogoni kwa Mabata.2 
Baadhi ya vijana wakiwasili katika viwanja vya Magogoni Kwa Mabata kwa matembezi ya mshikamano.

MKOA WA MBEYA WAIOMBA IDARA YA MAMBO YA KALE KUWAKABIDHI MAKUMBUSHO YA MAMBO YA KALE YA KIMONDO

0
0
Hiki  ndicho  kimondo  kina tani 12
Na Matukiodaima Blog.
MKOA  wa  mbeya   umepania  kuboresha miundo  ya  kituo cha mambo ya  kale  cha  Kimondo wilayani Mbozi mkoani hapa  iwapo Idara ya Mambo ya kale iliyopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii itakubali  ombi la mkoa   huo  kukabidhi  kivutio  Halmashauri  ya  Mbozi.

Hatua   hiyo   imekuja  kufuatilia ziara ya  wanahabari  mkoani Iringa wanaotembelea vivutio  vya  utalii  mikoa ya  Mbeya, Njombe na Iringa  kama  njia ya  kuhamasisha  utalii  mkoa ya nyanda  za  juu  kusini na pia  kubaini sababu  za  utalii kutokua kwa kasi katika  mikoa   hiyo  .

Mhifadhi  msaidizi  wa  kituo  cha makumbusho ya  mambo ya kale ya  Kimondo  wilayani  Mbozi Bw Mussa Nsojo alisema  kuwa  mbali  ya  watalii wengi  kupenda  kutembelea  eneo  hilo la Kimondo ila miundo  mbinu ya  eneo  hilo si rafiki kwa  watalii kuendelea  kutembelea  kutokana na  serikali  kushindwa  kuboresha  majengo na  eneo  hilo kwa  ujumla.

Alisema  kuwa  kimondo  hicho  ambacho mwaka kilipoanguka  eneo  hilo haufahamiki ila  utafiti wake ulianza kati ya  mwaka 1930 -1931 na kubainika  kuwa  si  jiwe la kawaida  bali ni sayari iliyoanguka  kutoka angani  toka  wakati   huo  kimendelea  kupata  umaarufu  wa  watalii kufika  kutembelea  eneo hilo japo katika  eneo  hilo mazingira  yake ni mabovu  zaidi.

Mhifadhi   huyo  akielezea  historia  ya  kimondo  hicho  alisema  kabla  ya  watafiti  kubaini  kuwa ni  kimondo miaka  ya  nyuma kulikuwa na wenyeji  ambao walikuwa  wakiishi  eneo  hilo na  mkazi  mmoja aliyefahamika  kwa jina la Harele  ambae  alikuwa akifanya kazi  ya uhunzi kuweza kubaini jiwe  hilo la ajabu wakati akitafuta  udongo chuma kabla  ya  kumega kipande  kidogo na kutengenezea shoka .

Alisema  kutokana na wakati   huo chuma kuwa na dhamani  kubwa alipeleka taarifa  kwa chifu  wa  eneo  hilo na  kulifanya  eneo hilo  kuwa  la tambiko kabla utawala  wa Waingereza  kuchukua eneo  hilo na  kulihifadhi kabla  ya  serikali ya  Tanzania  kupitia idara ya mambo ya  kale  kuhifadhi  eneo  hilo.

Kuhusu  changamoto  kubwa  zilizopo eneo  hilo alisema ni pamoja na kukosekana kwa  nyumba  bora  za watumishi ,jengo la ofisi  ya makumbusho  kutokana na kibanda  kilichopo  kutokuwa na sifa ya utalii ,pia miundo mbinu  ya barabara  kufika  kituoni hapo.


Afisa  utalii ofisi ya utalii kanda  ya kusini Bi Risala Kabongo akielezea  kivutio   hicho  alisema  kuwa  ni  moja kati ya  vivutio  visivyo  vya kawaida  hapa  nchini na kuwa  iwapo  serikali itaboresha  zaidi  eneo hilo upo uwezekano  wa uchumi  wa  mkoa  wa Mbeya kukua  zaidi  kupitia kivutio  hicho .

" Kivutio   hiki kinavutia   zaidi ila ushauri  wangu  kwa serikali ni kuboresha  miundo  mbinu ikiwa ni pamoja na kutenga eneo la banda la  wageni na eneo la kujenga mahema kwa  wageni.....Kimondo  hiki  kimetoka katika  sayari ya Mars na  hivyo ni  kivutio  cha ajabu  zaidi"

Katibu  tawala msaidizi (miundombinu)  mkoa  wa  Mbeya  Kastory Msigala  alisema  kuwa mkoa  huo  kupitia  kikao  chake  cha kamati ya ushauri ya  mkoa  kimeiandikia  barua  idara ya mambo ya kale  ili kuipa eneo hilo  la Kimondo Halmashauri ya  Mbozi  ili  kusimamia kwa lengo la  kuiboresha  zaidi.

Kwani  alisema  shida  kubwa ya  Halmashauri  hiyo na mkoa  kushindwa  kuboresha  majengo na miundo  mbinu  inayozunguka  makumbusho hayo ni  kutokana na kutokuwa na mamlaka ya  kufanya  hivyo kutokana na usimamizi wa eneo  hilo  kuwa  chini ya idara ya mambo ya kale ila pale  idara  hiyo  itakapokabidhi katika serikali ya  wilaya  upo uwezekano wa  wilaya  kusimamia  vizuri  zaidi.

Alisema katika mkoa   huo kuna  jumla  ya  vivutio 13  vilivyotambuliwa kikiwemo  kivutio   hicho  cha Kimondo  na  kuwa mbali ya  vivutio   hivyo  bado  mkoa  umejipanga zaidi  kutangaza  utalii  kufuatia ushirikiano mkubwa  uliopo kati ya  mkoa huo na ofisi ya SPANEST  , bodi ya utlii ,wizara  ya utalii na wadau mbali mbali  kukuza  utalii mkoani  humo .
Wanahabari  wakitazama  Kimondo
Mwanahabari  wa Habari  leo  Iringa na mwenyekiti wa chama  cha waandishi wa habari  mkoa  wa Iringa Frank  Leonard  akitoka  kutazama  Kimondo
Mgeni  akisaini kitabu cha wageni katika  ofisi ya makumbusho ya mambo ya kale  ya  Kimondo Mbeya
Wanahabari wakitoka katika  Kimondo  kulia na Slvanus  Kigomba  (ITV) na kulia ni Iren Mwakalinga (TBC),nyuma yao ni ofisi ya makumbusho  hayo
Mhifadhi  akionyesha  jiko  ambalo  linatumika  eneo  hilo
Nyumba ya  wahifadhi  wa makumbusho ya mambo ya kale ya  Kimondo Mbeya
Mhifadhi  msaidizi  wa makumbusho ya  Kimondo  akiingia katika nyumba  yake
Hii  ndio  nyumba  ya  mhifadhi mkuu na mhifadhi msaidizi wa Kimondo  Mbeya

Mwanahabari  wa ITV Iringa  Slvanus Kigomba  akijipumzisha kando ya  Kimondo
Mwanahabari  wa Star Tv Iringa  Mawazo Marembeka  kushoto akiwa na mzee  wa matukiodaima katika Kimondo
Wanahabari  wakimhoji mhifadhi msaidizi  wa makumbusho ya mambo ya kale ya Kimondo Mbeya  Bw Mussa Nsojo
Hiki  ndicho  kimondo  kina tani 12
Afisa utalii kanda  ya  kusini Tanapa  Bi Risala kabongo akiwa katika kibao  cha Kimondo

MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA YATOA ELIMU KWA VIONGOZI WA SACCOS ZA WAJASIRIAMALI MANSIPAA YA ILALA

0
0
 Mkugenzi wa CHF Bima ya Afya, Bw.Rehan Athumani (katikati) akifungua semina ya siku tatu Januari 21, 2015 jijini Dar es Salaam ya viongozi wa SACCOS za wajasiriamali zilipo Mansipaa ya Ilala iliyoandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) lengo la semina hiyo kuwapa elimu viongozi hao kuhusu Mfuko Taifa wa Bima ya Afya ili wapeleke ujumbe kwa wanachama wa SACCOS waweze kujiunga na mfuko huo (kushoto) Afisa Ushirika Mansipaa ya Ilala, Ladislaus Mwamanswao (kulia) Meneja wa CHF Bima ya Afya, Costantine Makala.
 Afisa Matekelezo wa NHIF, Godfrey Tumaini akiwakilisha mada yake kuhusina mpango wa kikoa ambapo amesema mpango huo ni mpya na umeanzishwa kwa malengo ya kukidhi haja ya kundi la watu wa kati ambao hawawezi kujilipia bima kama watu binafsi na hawaridhiki kujiunga katika mfumo wa CHF katika mfuko huo.
 Afisa Matekelezo NHIF Mansipaa ya Ilala, Hipoliti Lello akisisitiza jambo wakati wa semina ya siku tatu Januari 21, 2015 jijini Dar es Salaam ya viongozi wa SACCOS za wajasiriamali zilipo Mansipaa ya Ilala iliyoandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) lengo la semina hiyo kuwapa elimu viongozi hao kuhusu Mfuko Taifa wa Bima ya Afya ili wapeleke ujumbe kwa wanachama waweze kujiunga na mfuko huo.
 Afisa Matekelezo na Uratibu NHIF, Catherine Masinisa akielezea sheria za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakati wa semina hiyo.
 Mshiriki wa Semina hiyo, Juliana Richard akichangia mada.
 Viongozi wa SACCOS wakipitia vipeperushi.
 Viongozi mbalimbali wa SACCOS wakifuatilia mada wakati wa semina hiyo iliyoandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Viewing all 46202 articles
Browse latest View live


Latest Images