Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

Pata Filamu ya Jenipher Kyaka FIGO kupitia Mtandao

$
0
0
Filamu ya Figo
Kumsikiliza mzazi ni jambo la kawaida kwa kila mtoto, Lakini wakati mwengine lazima mtoto achague lipi jema, Lipi baya. Kijana Sila alijikuta kwenye pigo kubwa sana katika maisha yake nakujiuliza swali " Nani ni mzazi wangu kati yako na yule"Fuatilia kisa hiki..
Kwa Kuangalia Filamu hii ya Kitanzania iitwayo FIGO au nunua na iwe yako kupitia mtandao.Ili kuweza kuangalia au kununua kupitia Mtandao unachotakiwa kufanya ni kutembelea tovuti hii
Pia unaweza kuangalia au kununua filamu nyingine kupitia mtandao huo huo

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AFANYA ZIARA YA MAJIMBO MANNE LEO MKOA WA MAGHARIBI.

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akimtwisha ndoo ya maji mama mkazi wa sheia ya Mbuzini,Bi.Khadija Issa Kibwana mara baada ya kuzindua mradi wa maji safi na salama katika jimbo la Mfenesini,Mkoa wa Magharini.Katika ziara hiyo ambayo ni ya kukagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2010,kinana leo ametembele majimbo Manne likiwemo Mfenesini,Dole,Bububu pamoja na Mtoni.Ndugu Kinana amefuatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM,Nape Nnauye.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki kazi ya kupanda miti katika shamba la Spice Solution Farm,lililopo katika kijiji cha Mwakaje,wilaya ya Mfenisini,mkoa wa Magharibi.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki ujenzi wa madarasa katika skuli ya Kidichi,Wilaya ya Mfenesini mkoa wa Magharibi.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana pichani shoto na Waziri Kiongozi Mstaafu Mh.Shamsi Vuai Nahodha wakishriki katika ujenzi wa Ofisi ya CCM tawi la Bububu,katika wilaya ya Mfenisini mkoa wa Magharibi
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipanda moja ya kiungo katika shamba la Spice Solution Farm lililopo Mwakaje,Wilaya ya Mfenesini mkoa wa Magharibi.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiangalia viungo mbalimbali vilivyosagwa na kusindikwa tayari kwa kuuzwa kwa wateja. 
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na Vijana wajasiliamali walioko katika shamba la viungo (spice Spice Solution Farm),lililopo katika kijiji cha Mwakaje,wilaya ya Mfenisini,mkoa wa Magharibi.Ndugu Kinana amelitembelea shamba hilo la kujionea shughuli mbalimbalizi zifanywazo na vijana hao wapatao 2600.

  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiangalia bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na kikundi cha  akina mama Wajasiliamali cha Mshikamano Daima kilichiopo Mtopepo,jimbo la Mtoni,wilaya ya Mfenesini mjini Unguja,mkoa wa Magharibi.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar,Ndugu Vuai Ali Vuai,wakati Ndugu Kinana alipowasili katika jimbo la Mfenesini,ambapo alipokea taarifa ya kazi za chama cha CCM  pamoja na kuzungumza na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Wilaya,mkoa wa Magharibi.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipeana mkono na Balozi Ali Karume,wakati Ndugu Kinana alipowasili katika jimbo la Mfenesini,ambapo alipokea taarifa ya kazi za chama cha CCM pamoja na kuzungumza na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Wilaya,mkoa wa Magharibi.

SERIKALI YA KENYA YAKUBALI KUYARUHUSU MAGARI YA ABIRIA NA WATALII KUTOKA TANZANIA.

$
0
0
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amesema serikali ya Kenya imekubali kuyaruhusu magari ya abiria na watalii kutoka Tanzania, kuingia ndani ya Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.
Awali, Serikali ya Kenya iliyazuia magari hayo kuingia uwanjani hapo huku ukiyatoza ushuru kwa yale yanayoingia, jambo ambalo lililalamikiwa na wafanyabiashara wa Tanzania.
Marufuku hiyo ya Kenya kwa magari ya Tanzania, ilidumu kwa zaidi ya wiki mbili, ambapo katika kusaka suluhu hiyo Nyalandu alikutana na wafanyabiashara hao jijini Arusha kisha kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Biashara na Utalii wa Kenya, Phyllis Kandie.
Katika mazungumzo yake na Kandie, Nyalandu alisema kwa sasa magari ya Tanzania yataendelea kuingia uwanjani hapo wakati ufumbuzi wa kudumu ukitafutwa.
Alisema kutakuwa na vikao vya kazi baaina ya Wizara ya Utalii ya Kenya na wizara yake, ambapo vitaanzia ngazi ya watandaji, watalaamu, makatibu wakuu na mawaziri.Alisema katika mikutano hiyo masuala mbalimbali kuhusiana na biashara ya utalii yatazungumzwa baina ya nchi hizo mbili.
Hata hivyo, alisema katika vikao hivyo suala la mpaka wa Bolongoja halitajaliwa wala kuwepo kwenye ajenda.
“Kwa sasa wafanyabiashara wetu wataingia Jomo Kenyatta kama ilivyokuwa awali. Tumezungumza na kupanga kuwa na vikao kujadili na kuzipatia ufumbuzi changamoto zote kuhusiana na sekta ya utalii.“Niwahakikishie tu katika vikao hivyo maslahi ya pande zote yatazingatiwa, lakini suala la mpaka wa Bolongoja halitajadiliwa wala kuwemo kwenye ajenda za vikao vyetu.“Wataalamu na watendaji wa wizara yangu watakutana na wenzao jijini Arusha na maofisa wa Jumuia ya Afrika Mashariki watashiriki ili kutafuta ufumbuzi wa kudumu,” alisema Nyalandu.
Kupatiwa ufumbuzi kwa tatizo hilo kumekuwa faraja kubwa kwa wafanyabiashara na wadau wa utalii katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, ambapo walipongeza jitihada za haraka zilizofanywa na Nyalandu.Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, wadau hao wa utalii walisema Nyalandu ameonyesha utendaji kazi kwa vitendo na kwamba, hilo linapaswa kuwa mfano kwa viongozi wengine.
Walisema waziri huyo baada ya kupata taarifa za wafanyabiashara wa Tanzania kuzuiwa kuingiza magari Jomo Kenyatta, aliwafuata kwenye maeneo yao na kuwasikiliza kero zinazowakabili kisha kufunga safari kukutana na waziri Kandie jijini Nairobi.
“Hawa ndio aina ya viongozi ambao Tanzania ya sasa na inayokuja inawahitaji, wanaposikia wananchi wana kero na wananyimwa haki ama kunyanyaswa wanakwenda kuwasikiliza na kutafuta ufumbuzi wa haraka. “Kwa hili Waziri Nyalandu anastahili pongezi na viongozi wengine waige mfano huu, wangekuwa wengine wangeanza kuleta siasa na tatizo kuchukua muda mrefu kupata ufumbuzi,” alisema John Mlay, ambaye ni mmoja wa wafanyakazi kwenye kampuni za usafirishaji watalii.

JAJI MUTUNGI AVIONYA VYAMA VYA SIASA VINAVYOENDEKEZA MIGOGORO

$
0
0
Hivi Karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la Migogoro ndani ya vyama vya Siasa. Jambo hili linaleta Taswira mbaya kwa jamii, hasa kipindi hiki ukielekea katika uchaguzi Mkuu wa nchi.

Athari za migogoro hii ni nyingi, ikiwemo chama cha kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa, kupoteza mvuto kwa jamii na wanachama wake, ukosefu wa amani na utulivu ndani ya chama na kupoteza sifa za usajili.
Hivi sasa mfumo wa demokrasi ya vyama vingi vya siasa una takribani miaka 23 tangu urejee tena mwaka 1992. Hivyo jamii inategemea kuwa mwanasiasa na vyama vya siasa kuonyesha ukomavu na busara katika kuokuongoza na kushiriki shughuli za chama.
Mojawapo ya ukomavu na ustarabu huo ni kuweka mifumo, kuongoza na kushiriki shughuli za chama katika namna ambayo itaepusha migogoro. 
Mojawapo ya Mambo ya kuzingatia ni chama kudhibiti tofauti za wanachama na baina ya viongozi kwa njia ya kidemokasia na utawala bora katika kuongoza na kushiriki shughuli za chama na kuheshimu na kufuata sheria, katiba na kanuni za chama.
Hivyo natumia nafasi hii kama ninavyotambulika na jamii kuwa ni mlezi wa vyama vya siasa, kuvisihivyama vyote vya siasa, kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria, katiba na kanuni zake. Pia kuwa mfano mzuri kwa jamii kwa kudumisha amani na utulivu ndani ya vyama vya siasa.

TBL YAFADHILI UCHIMBAJI VISIMA BAGAMOYO

$
0
0
 Mhandisi wa Kampuni ya Al Water Well Drillers, Mohamed Aboud (katikati), akielekeza jambo kwa mmoja ya wafanyakazi wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi ya miradi ya uchimbaji wa visima vya maji unaofafadhiliwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), katika vijiji vya Nianjema C na Mianzini B, wilayani Bagamoyo, Pwani mwishoni mwa wiki. Kulia ni Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu.
 Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu (kulia) akielekeza jambo kwa fundi alipokuwa akikagua ujenzi wa mradi wa uchimbaj wa visima vya maji katika vijiji vya Nianjema C na Mianzini B, wilayani Bagamoyo, Pwani mwishoni mwa wiki.Miradi hiyo itagharimu sh. mil.51.7.

 Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu, akijadiliana jambo na  na mkandarasi wa  ujenzi wa visima vya maji katika vijiji vya Nianjema C na Mianzini B,Mohamed Aboud, mwishoni mwa wiki wilayani Bagamoyo, Pwani. TBL inafadhili miradi hiyo kwa gharama ya sh. mil. 51.7.

Mhandisi wa Kampuni ya Al Water Well Drillers, Mohamed Aboud (katikati), akielekeza jambo kwa mmoja ya wafanyakazi wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi ya miradi ya uchimbaji wa visima.

Obi sets sights on Africa smartphone market; brand by former Apple CEO to launch in Tanzania in Q1 2015.

$
0
0
·         New venture led by former Apple CEO, former president of PepsiCo, and renowned tech investor John Sculley aims for rapid global expansion
·         Following its successful launch in India and the Middle East, Obi Mobiles plans substantial investments in to the Tanzania smartphone market
·         Signs on renowned regional IT distributor DESPEC as exclusive channel partner in Tanzania and other African countries

Dar es Salaam, Tanzania: 19 January, 2015  Obi Mobiles, the new smartphone brand co-founded by veteran marketer and former Apple CEO John Sculley, is preparing an ambitious launch in Tanzania and other countries in East Africa, and has signed on DESPEC, the leading IT distributor as its exclusive channel partner in the region. The firm is set to roll out a superior line-up of Obi devices suited to consumers in the region in Q1 2015, with an aim to capture 5% market share by the end of this year.

John Sculley is an internationally renowned marketing expert, entrepreneur and investor in high-tech startups. He was vice-president (1970–1977) and president of PepsiCo (1977–1983), until he became CEO of Apple in 1983. He held that position till 1993 and, under his management, annual sales at Apple increased from $800 million to $8 billion.

A new entrant in the consumer technology sector, Obi Mobiles is a venture of Sculley’s Toronto-based Investment and Acquisition Company, Inflexionpoint. It marked its global launch in India, followed by the Middle East markets in 2014. The brand, which aims to attract the growing segment of young and trendy smartphone users, confirmed that Tanzania is an important market in Obi’s rapid global expansion strategy.

John Sculley, co-founder and managing partner at Inflexionpoint, says: “Our vision is to use Obi’s success in each new market to create an international brand, especially targeted at the feature-rich and trendy smartphone segment. Having launched in India and the Middle East, with a better-than-anticipated response, has helped us set the pace for the Obi expansion blueprint, and now we are expanding our strategy of effective brand building and marketing for superior mobile devices in other regions.

“The African markets present a huge opportunity for new smartphone devices, with a growing population of technology- and fashion-savvy youth. Consumers today want the best feature-rich smartphone experience at desirable price points, without compromising on quality. There is also a growing trend of feature phone users moving towards smartphones. Our analysis has revealed that consumers today are more likely to switch brands as long as they have sufficient incentive. Obi is uniquely positioned to leverage all these changing market dynamics.”


Designed to capture the minds of the younger demographic, Obi devices are packed with style and superior features. The range includes mobile devices that run on the efficient Android Kit Kat platform, powered by multi-core processors, including an octa-core option, dual-SIM capabilities, large screen sizes and high quality camera options, all packaged in a robust and stylish exterior.

Amit Rupchandani, Managing Director for the Middle East and Africa region at Obi Mobiles, adds: “While the mobile industry is often associated with highly expensive products sold using technical jargon, at Obi Mobiles the belief is that it doesn't have to be this way. Obi is perfect for the growing number of mobile phone users in this region who desire the best smartphone experience without a huge financial investment.

“Added to that is our brand philosophy of ‘Whoever you are’. What it essentially means is that Obi doesn’t judge you, it lets you be you. In keeping with that, we have a broad range of quality products to suit the different personalities and preferences of smartphone users.

“We are charting out our entry in to the East Africa market currently, and aim to rapidly grow in the region by forging synergies with effective channel partners. Obi will continue to expand extensively through 2015, with Latin America and the former CIS region up on the list of priority markets.”

As a value-added reseller to Obi Mobiles for Tanzania, Kenya and other African markets, DESPEC will manage the distribution of Obi devices to all key retailer and independent retailer channels in these countries.

Farouk Jivani, CEO, DESPEC Africa, says: “DESPEC is excited to be appointed as the exclusive channel partner for Obi Mobiles in Tanzania and other East African markets. Obi has paid special attention to creating an image that resounds with the large section of young and aspirational smartphone users in Africa. Their entry in these markets will additionally be buoyed by trends such as increased mobile internet usage and penetration among target consumers. We look forward to working with Obi and establishing the brand as one to reckon with in the region.”

The Obi smartphones for the African markets will be unveiled in March in Tanzania followed by a phased roll-out across other markets in the region.

Huyu na Yule...........Mahojiano na Dr na Mama Williams

$
0
0
Karibu kwenye mahojiano ya Dr na Mama Williams.
Waasisi wa AHEAD Inc. Taasisi ambayo iliasisiwa mwaka 1985 na inajishughulisha kubadili maisha ya wengi nchini Tanzania kupitia Elimu, Stadi za Maisha, Afya ya Mama na Mtoto na pia kuzisaidia jamii mbalimbali..
Wamezungumzia mengi kuhusu namna walivyofika Tanzania kwa mara ya kwanza 1974. Kilichowapeleka, walivyoamua kubaki huko mpaka sasa, shughuli za Taasisi yao na mengine mengi
Karibu
Huyu na Yule ni kipindi kinachotayarishwa na Vijimambo Blog na kuzalishwa na Kwanza Production . Kwa mawasiliano, maoni ama ushauri, tafadhali wasiliana nasi kupitia kwanzaproduction at gmail.com

DORIS MOLLEL KATIKA UZINDUZI WA BWENI LA KWANZA KWA WATOTO WA JAMII YA HADZABE, SINGIDA

$
0
0
Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15,Doris Mollel (wa pili kushoto) akiongea na waandishi wa habari wakati alipohudhuria kwenye hafla ya ufunguzi wa bweni jipya maalum kwa watoto wa jamiii ya hadzabe katika shule ya msingi Munguli, wilaya ya Mkarama mkoani Singida. Uzinduzi wa bweni hili ni matunda ya jitihada za Serikali ya wilaya hiyo na mkoa wa Singida kuwahamasisha watoto hao kuhudhuria madarasa bila kukosa na kujifunza maisha ya kawaida kama watoto wa jamii nyingine. Doris alichangia vitabu na ma-blanketi vyenye thamani ya Tsh 1,000,000/=. Hafla hiyo iliandaliwa na Mkuu wa Wilaya Ndg Edward Ole Lenga na mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dk. Paseko Kone (Wa kwanza kushto).
Mlezi wa watoto wa jamii ya Hadzabe katika shule ya msingi Munguli, wilayani Mkarama mkoani Singida akimpongeza Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15,Doris Mollel baada ya kumteua kuwa ‘balozi wa elimu’ wa watoto wa jamii ya Hadzabe kwenye shule hiyo. Doris ambaye ni Miss Singida na Kanda ya Kati 2014/15 alichangia vitabu na ma-blanketi vyenye thamani ya Tsh 1,000,000/=. Hafla hiyo iliandaliwa na mkuu wa Wilaya Ndg. Edward Ole Lenga na mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dk. Paseko Kone (mwenye suti nyeusi).
Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15,Doris Mollel akikabidhi Blanketi kwa watoto wa jamii ya Hadzabe waliojengewa Bweni na Serikali ya Wilaya na Mkoa wa singida katika shule ya msingi Munguli Wilayani Mkarama ikiwa ni jitihada za Serikali kuwahamasisha kuduhuria madarasa bila kukosa na kujifunza maisha ya kawaida kama watoto wa jamii nyingine. Doris alichangia vitabu na ma-blanketi vyenye thamani ya Tsh 1,000,000/=. Akishuhudia tukio hilo ni Dk. Paseko Kone, Mkuu wa Mkoa wa Singida na Mgeni rasmi kwenye hafla hiyo.

Pata Filamu ya Kigodoro kupitia Mtandao.Kantangaze

$
0
0
Mtaani kuna vituko vingi vyenye kusisimua, kuhuzunisha na kufurahisha unaweza Fuatilia uko vilivyopo katika filamu hii kupitia mtandao .......
Kwa Kuangalia Filamu hii ya Kitanzania iitwayo KIGODORO au Knunua na iwe yako kupitia mtandao.

Ili kuweza kuangalia au kununua kupitia Mtandao unachotakiwa kufanya ni kutembelea tovuti hii
Pia unaweza kuangalia au kununua filamu nyingine kupitia mtandao huo huo.

UFAHAMU MTANDAO WA MALEZI MAKUZI NA MAENDELEO YA WATOTO WADOGO TANZANIA (TECDEN)

$
0
0
unnamed
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Bruno Ghumpi
...........................................................................................................
Mtandao wa Malezi Makuzi na Maendeleo ya Watoto Wadogo Tanzania – TECDEN ni chombo kinachoundwa na mashirikia mbalimbali yanayofanya kazi za kuhudumia watoto wadogo Tanzania. Mtandao huu ulianzishwa mwaka 2000 na kusajiliwa rasmi mwaka 2004. Makao makuu ya Mtandao huu yapo Jijini Dar es salaam. Hadi kufikia mwaka 2014 Mtandao huu una jumla ya mashirika wanachama wasioungua 200 katika mikoa 14 ya Tanzania bara na Visiwani yanayotoa huduma kwa watoto wadogo Tanzania Lengo kuu la Mtandao ni kuboresha huduma za watoto wadogo Tanzania ili waweze kukua na kufikia utimilifu waoShughuli Kuu za 

Mtandao ni pamoja na:-• Kufanya ushawishi na utetezi wa masuala yanayohusu uboreshaji wa huduma na kulinda haki za watoto wadogo ikiwa ni pamoja na kushawishi maboresho ya sera na kufuatilia utekelezaji wa sheria na miongozo mbalimbali inayohusu uboreshaji wa huduma kwa watoto wadogo Tanzania.• Kuhamasisha jamii na watoa huduma kutambua umuhimu wa kuimarisha na kuwezesha watoto wadogo kupata mahitaji na haki zao za msingi. • Kuimarisha mifumo ya upashanaji habari na kuelimishana katika ngazi zote za huduma kwa watoto wadogo. • Kutafiti na kutumia matokeo ya utafiti katika kushauri uboreshaji wa huduma kwa watoto wadogo Tanzania.

Dhana ya Malezi Makuzi na Mendeleo ya Awali ya Mtoto (MMMAM)Malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto ni istilahi ya jumla ya programu na vitendo vinavyoandaliwa kuwasaidia watoto (kuanzia mimba, kuzaliwa hadi miaka 8) ili kukua vizuri kimwili, kiakili, kijamii, kihisia, kimaadili na kiroho. Watoto wanahitaji kuchangamshwa katika nyaja na hatua zote za ukuaji, kiakili kwa michezo, kujifunza kuzungumza, kukaa, kutambaa, kutembea na kupatiwa fursa ya kuanza kujifunza mambo mbalimbali pamoja na utamaduni wao.

Utoaji wa huduma jumui za MMMAM.Huduma hizi hujumuishwa ili kuwawezesha watoto wengi kupata huduma jumuishi za MMMAM zitolewazo na sekta mbali mbali katika mkabala jumui. Huduma hizi zinapaswa kupatikana kuanzia ngazi ya familia ,vituo vya afya ya msingi,vituo vya kulelea watoto mchana, vituo vya Malezi Makuzi ya awali ya mtoto vinavyomilikiwa na Jamii, madarasa ya awali na madarasa ya msingi hususani darasa la kwanza na la pili.

Katika kutekeleza shughuli zake Mtandao wa TECDEN umekuwa ukishirikiana na mashirika mbalimbali ya wabia wa maendeleo ikiwemo shirika la Children in Crossfire kutoka nchini Ireland na shirika la Better Way Foundation kutoka nchini Marekani
Ili kujua habari zaidi za TECDEN na masuala ya utoaji huduma kwa watoto wadogo na faida zake, unaweza kutembelea ofisi ya Mtandao makao makuu iliyopo Jengo la Posta mkabala na Wizara ya Mambo ya Ndani Nchi na Makao Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam.
Unaweza pia kuwasiliana kwa njia ya simu au barua pepe na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Bruno Ghumpi kwa namba 0754 690 556 na barua pepe ecdnetwork@gmail.com na ghumpibr@yahoo.com

Benki ya Exim yatambulisha Kadi ya Faida EMV kuwezesha miamala salama

$
0
0
 Mkuu wa Hazina wa Benki ya Exim, George Shumbusho, akikata utepe kutambulisha kadi ya “Faida EMV Debit Card” itakayochukua nafasi ya “Magnetic Stripe Faida Debit Card” iliyokua ikitumika hapo awali. Ameambatana na Mkuu wa Kitengo cha kudhibiti majanga wa Benki ya Exim, David Lusala (kulia) na Afisa masoko wa benki hiyo, Noel Tuga.  Kadi hiyo hutoa usalama wa hali ya juu kutokana na uwepo wa ‘embedded chip’ inayodadavua taarifa za mteja kwa kutumia mfumo madhubuti wa kiusalama hivyo kutoruhusu unakili wa taarifa za mteja husika.
 Mkuu wa kitengo cha kudhibiti majanga wa Benki ya Exim, David Lusala (kulia),akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, kutambulisha kadi ijulikanayo kama “Faida EMV Debit Card” kuchukua nafasi ya “Magnetic Stripe Faida Debit Card” iliyokua ikitumika hapo awali. Kushoto ni Mkuu wa Hazina wa benki hiyo, George Shumbusho. Kadi hiyo hutoa usalama wa hali ya juu kutokana na uwepo wa ‘embedded chip’ inayodadavua taarifa za mteja kwa kutumia mfumo madhubuti wa kiusalama hivyo kutoruhusu unakili wa taarifa za mteja husika.
Mkuu wa Hazina wa Benki ya Exim, George Shumbusho (kushoto), akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, kutambulisha kadi ijulikanayo kama “Faida EMV Debit Card” kuchukua nafasi ya “Magnetic Stripe Faida Debit Card” iliyokua ikitumika hapo awali. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha kudhibiti majanga wa Benki hiyo, David Lusala. Kadi hiyo hutoa usalama wa hali ya juu kutokana na uwepo wa ‘embedded chip’ inayodadavua taarifa za mteja kwa kutumia mfumo madhubuti wa kiusalama hivyo kutoruhusu unakili wa taarifa za mteja husika.
 
Katika jitihada za kurahisisha upatikanaji wa huduma za kibenki kwa wateja wake katika mazingira salama zaidia Benki ya Exim imetambulisha kadi mpya ya kimataifa ijulikanayo kama “Faida EMV Debit Card” kuchukua nafasi ya “Magnetic Stripe Faida Debit Card” zilizokua zikitumika hapo awali.

Kadi hiyo mpya hutoa usalama wa hali ya juu kutokana na uwepo wa ‘embedded chip’ inayodadavua taarifa za mteja ikiwa na mfumo madhubuti wa kiusalama hivyo kutoruhusu unakili wa taarifa za mteja husika. Hii itasaidia wateja wa benki hiyo kutekeleza miamala yao katika mfumo ulio salama zaidi.  

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana,  Mkuu wa Hazina wa Benki ya Exim, Bw. George Shumbusho alisema kadi hiyo mpya ina usalama ulioimarishwa zaidi kutokana na uwepo wa ‘embedded chip’ na kufanyika kwa ukaguzi wa ziada wa namba ya siri.

“Tunatambua hitaji la wateja wetu kuweza kufanya miamala yao kwa usalama zaidi. Kwa kutumia kadi hii mpya ya kimataifa kutoka Benki ya Exim, mteja anaweza kuwa na uhakika kwamba miamala yake inafanyika katika mazingira salama kabisa,” alisema Bw. Shumbusho.

Aliongeza kuwa, Kadi hiyo mpya ya kimataifa inamuwezesha mteja kufanya miamala duniani kote katika mashine za ATM na POS zilizothibitishwa na MasterCard.

“Kama Benki ya Exim, tunaamini kuwa ugunduzi ni maisha. Hivyo basi, tutaendelea kugundua teknolojia mpya zitakazoendana na kasi ya ukuaji wa utandawazi katika dunia hii ya sasa ili kuweza kukabiliana na changamoto zilizopo katika usalama wa kimtandao.

“Ni matumaini yetu kuwa wateja wetu watazifurahia zaidi kadi zao mpya za “Faida EMV Debit card,” alisema.

KINANA AMALIZA ZIARA KATIKA JIMBO LA UZINI MKOA WA KUSINI UNGUJA

$
0
0
 Mfuasi wa CHADEMA,Bi.Fatma Hassan akikabidhi kadi yake kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na kujiunga na chama hicho,ambapo wanachama watano wa CHADEMA walirudisha kadi na kujiunga na CCM.
 Baadhi ya Wanachama wapya wakila kiapo
 Sehemu ya Umati wa watu wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Tunduni,Jimbo la Uzini,Mkoa wa Kusini Unguja
 Sehemu ya Umati wa watu waliofika kwenye mkutano wea hadhara uliofanyika katika kijiji cha  Tunduni,Jimbo la Uzini,Mkoa wa Kusini Unguja.PICHA NA MICHUZI JR-KUSINI UNGUJA-ZANZIBAR

ARSENAL FC YATEMBELEA PSPF KWA LENGO LA KUSAKA FURSA ZA MAHUSIANO YA KIBIASHARA.

$
0
0
 Mkurugenzi wa Mahusiano ya kimaendeleo wa Klabu ya Arsenal Bw. Sam Stone (Kulia) akimkabidhi jezi ya timu hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bw. Adam Mayingu. Kushoto ni Bw. Daniel Willey, Meneja wa Mahusiano ya Kimaendeleo ya Arsenal. Maafisa hao wapo nchini kwa lengo la kukutana na wadau mbalimbali ili kufungua mahusiano ya kibiashara, katika mpango huo makocha wa timu hiyo na baadhi ya nyota waliowahi kuchezea timu hiyo watapata fursa kutembelea Tanzania. Klabu ya Arsenal ni kati ya klabu maarufu ulimwenguni ambayo inashiriki ligi maarufu duniani ya Barclyas.
Mkurgenzu Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu (kushoto) akimkabidhi zawadi Afisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group, Bw Imani Kajura ambaye ni mwenyeji wa maafisa kutoka klabu ya Arsenal ambao wapo nchini kwa ajili ya kukutana na wadau mbalimbali kwa lengo kufungua mahusiano ya kibiashara.

Elimu kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana yawafikia Vijana wa Mbeya Vijijini

$
0
0

unnamedMkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Vijijini Bibi Upendo Sanga akifungu semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyoandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo jana katika Mkoa wa Mbeya. Waliokaa katikati ni Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa na kulia ni Afisa Vijana kutoka Wizara hiyo Bi. Amina Sanga.
unnamed1Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga akiwaelimisha vijana wa Wilaya ya Mbeya Vijijini kuhusu mwongozo unaosimamia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana wakati wa semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyofanyika jana katika ukumbi wa Halmashauri hiyo Mkoa wa Mbeya.
unnamed2Afisa Ushirika wa Wilaya ya Mbeya Vijijini Bw. Isaya Mwamarobo akifafanua jambo wakati wa semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyotolewa kwa vijana wa wilaya hiyo jana katika Mkoa wa Mbeya.
unnamed3Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Vijijini Mkoa wa Mbeya walioudhuria semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana wakiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji wa semina hiyo. unnamed4Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga wapili kulia akizungumza na wanakikundi wa Wasamba Saccoss Wilaya ya Mbeya Vijijini walipowatembelea kukagua mradi wanaouendesha. Wakwanza kulia ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele na watano kulia ni Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa.
……………………………………………………………………………………….

Na: Genofeva Matemu – Maelezo, Mbeya.
Vijana wa Mkoa wa Mbeya Wilaya ya Mbeya Vijijini wametakiwa kutokuwa na tafsiri hasi kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kuwa ni takrima inayotolewa na serikali kwa vijana hivyo kuchezea fedha hizo na kushindwa kurejesha mkopo watakaouomba kupitia mfuko huo.

Hayo yamesemwa na Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa wakati wa semina iliyotolewa kwa Vijana wa Mbeya Vijijini kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Stadi za Maisha, Ujuzi na Ujasiriamali jana Mkoani Mbeya.Bibi Riwa amesema kuwa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana unahudumia vijana wote nchini bila kuangalia itikadi za kisiasa ukiwa na lengo la kuwakomboa vijana na kuinua vipaji vya vijana nchi nzima.

“Vijana ni taifa la leo na kesho likiwezeshwa taifa zima limewezeshwa, Wizara yenye dhamana na Vijana inalenga kuwafikia vijana wote nchini bila kuangalia itikadi za kisiasa kwani vijana wote ni wetu na tunatamani kuona vijana wanajiendeleza kufikia ndoto walizonazo” amesema Bibi Riwa.

Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbeya Vijijini Bibi Upendo Sanga amesema kuwa ni bahati ya pekee kutembelewa na ugeni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo hivyo kuwaomba vijana wa Wilaya yake kuzingatia elimu watakayoipata na kusambaza elimu hiyo kwa vijana wengine wa Wilaya yake ambao hawakuweza kufika katika semina hiyo.

Bibi Sanga ameiomba Wizara yenye dhamana na Vijana kuendeleza programu ya kuwaelimisha vijana mara kwa mara na kuwahamasisha vijana kujiunga katika vikundi kwani ni raisi kusaidia vijana wakiwa katika vikundi kuliko kumsaidia kijana mmojammoja.
 Akichangia wakati wa semina hiyo kijana Evans Bembeja kutoka Shirika la Efao linalojishughulisha na kilimo cha mbogamboga amesema kuwa vijana wengi hawaangalii mbele wamekua kwenye mwamko wa kisiasa wakiamini kuwa siasa ndio sehemu ya kupata pesa za haraka hivyo kuachana na fursa nyingine kama vile kilimo na ufugaji.

BARAZA LA WATUMIAJI HUDUMA SUMATRA LASHIRIKI KIKAMILIFU MAONESHO YA MIAKA 40 YA CHUO CHA NIT JIJINI DAR

$
0
0
Afisa wa Elimu kwa Wateja kutoka Baraza la Ushauri la Watumiaji Huduma za Usafi wa nchi kavu na Majini, Nicholous Kinyariri  akitoa maeklezo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Monica Mwamunyange (kulia) wakati alipotembelea banda la SUMATRA katika maonesho ya kuazimisha miaka 40 tangu kuanzishwa kwa chupo cha Usafirishaji Tanzania (NIT) kwenye viwanja vya chuo hicho jana. Kushoto ni Afisa wa Baraza hilo la Sumatra, Doatha Kabyemela.
Naibu Katibu Mkuu wa Uchukuzi, Monica Mwamunyange (kulia) akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Usafirishaji  (NIT) Mhandisi Priscilla Chilipweli baada ya kupokea maelezo ya kina na yanayoeleweka ipasavyo kuhusu shughuli za baraza hilo kutoka kwa  Afisa wa Elimu kwa Wateja kutoka Baraza la Ushauri la Watumiaji Huduma za Usafi wa nchi kavu na Majini, Nicholous Kinyariri.
Maafisa wa Baraza la Ushauri la Watumiaji Huduma za Usafi wa nchi kavu na Majini, wakitoa elimu kwa wananchi.
 Wananchi wakipata elimu katika baraza hilo.
 Maafisa wa Baraza la Ushauri la Watumiaji Huduma za Usafi wa nchi kavu na Majini, wakitoa elimu kwa wananchi.
 Afisa wa Elimu kwa Wateja kutoka Baraza la Ushauri la Watumiaji Huduma za Usafi wa nchi kavu na Majini, Nicholous Kinyariri akielezea takwimu za utafiti uliofanywa na baraza.
Afisa wa Elimu kwa Wateja kutoka Baraza la Ushauri la Watumiaji Huduma za Usafi wa nchi kavu na Majini, Nicholous Kinyariri akitoa elimu kwa vijana.

MWENYEKITI WA SITTI TANZANIA FAUNDATION, SITTI MTEMVU AWATEMBELEA WATU WENYE ALIBINIZIM NA KUTOA MSAADA

$
0
0
Mwenyekiti wa Sitti Tanzania Faundation, Sitti Mtemvu (wa pili kushoto), akiuangalia mkono wa Adam Robert (aliye vaa flana ya njano) alipo tembelea kituo cha watu wenye   Albinizim mwishoni mwa wiki Dar es Salaam, ambaye alikatwa kidole katika kijiji cha Nyaruguguna Geita na kupelekwa Vancouver, Canada kwa matibabu. Adam Robert alipandikizwa  kidole cha kati cha Mguu wa kulia  kwenye kiganja chake cha  mkono wa  kulia kuwa kidole gumba, wakwanza ni Mariam Staford kushoto ambaye alitokea kijiji cha Ntobeye Wilaya Ngara Karagwe na Kurwa Lusana toka kijiji cha mbizi Kahama   (kulia)  (PICHA NA KHAMISI MUSSA).  

CCM YEW YORK INAWAKARIBISHA WATANZANIA WOTE KWENYE BASHHHH LA MIAKA 38 YA CCM...TEGA SIKIO KWA HABARI ZA NANI KUTUMBUIZA FEB 21 !

Vijana waendelea kupata ajira katika Utumishi wa Umma

$
0
0

unnamedKatibu Msaidizi Idara ya Ajira kutoka Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Malimi Muya akiwaeleza waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam (hawapo pichani) sababu zinazopelekea Vijana wengi kupenda kufanya kazi katika Utumishi wa Umma ikiwemo uboreshaji wa mishahara,kuboreshwa kwa mazingira ya kazi,usalama wa kazi unaotokana na kuwepo kwa taratibu za kazi zinazotabirika ,kuwepo kwa taratibu maalum zinazomhakikishia mwajiriwa maslahi au malipo bora baada ya kuhitimisha ajira yake.kushoto ni Afisa Habari wa Sektetarieti hiyo Bw. Kassim Nyaki na kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Frank Mvungi.unnamed1Afisa Habari toka Ofisi ya Rais Sektetarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Kassim Nyaki akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam,Katikati ni Katibu Msaidizi Idara ya Ajira kutoka Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Malimi Muya na kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Frank Mvungi.           
unnamed3 
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Katibu Msaidizi Idara ya Ajira kutoka Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Malimi Muya leo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano uliolenga kutoa taarifa ya mafanikio ya Sekretarieti hiyo ikiwemo kuwapangia vituo vya kazi jumla ya waombaji kazi 12,858 walioshinda usaili kufikia Novemba 2014.
(Picha zote na Idara ya Habari Maelezo )
……………………………………………………………………………………
Frank Mvungi- MaelezoSerikali imewapangia vituo vya kazi waajiriwa 12,858 katika Utumishi wa Umma kufikia Novemba mwaka 2014 ambao walifuzu usaili kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya ajira katika Utumishi wa Umma.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Katibu Msaidizi Idara ya Ajira kutoka Sekretarieti hiyo Bw. Malimi Muya wakati wa mkutano na Waandishi wa habari uliolenga kueleza mafanikio ya Sekretarieti hiyo hadi mwishoni mwa mwaka jana.

Akizungumzia suala la maombi ya ajira yaliyowasilishwa katika Sekretarieti hiyo, Muya alibainisha kuwa jumla ya barua za maombi 191,844 zilifikishwa na kupokelewa na Sekretarieti hadi Septemba 2014 ambapo jumla ya waombaji 71,124 walikidhi vigezo na waliitwa kwenye usaili baada ya uchambuzi kufanyika.

“Kati ya waombaji 71,124 waliotwa kwenye usaili huo, ni waombaji 12,858 ndio waliofuzu na waliopangiwa vituo vya kazi ambapo wanaume walikuwa 7,598 sawa na asilimia 59.1 na wanawake walikuwa 5,260 sawa na asilimia 40.9.” alisisitiza Muya.

Aidha kati ya waajiriwa 12,858 waliopangiwa vituo vya kazi Muya alibainisha kuwa Vijana wenye umri kati ya miaka 21-25 ni 1045 sawa na asilimia 8.1 wenye umri kati ya miaka 26-30 ni 6,346 sawa na asilimia 49.4 ambapo kati ya mwaka 2010 hadi 2014 utumishi wa umma umeajiri 57.5 ya vijana wenye umri wa miaka 21-30.

Akizungumzia sababu zinazowavutia na kuwasukuma vijana kuingia katika Utumishi wa Umma, Muya alisema kuwa uboreshaji wa mishahara, kuboreshwa kwa mazingira ya kazi, usalama wa kazi unaotokana na kuwepo kwa taratibu za kazi zinazotabirika ndizo mojawapo ya sababu zinazowavutia vijana wengi kuomba kazi katika utumishi wa umma.
 Sababu nyingine zinazowavutia vijana kupenda kuajiriwa katika utumishi wa umma ni kuwepo kwa mabadiliko ya mara kwa mara ya kanuni na taratibu za kazi zinayofanywa kukidhi mahitaji ya watumishi kwa wakati unaohusika, kuwepo kwa taratibu maalum zinazomhakikishia mwajiriwa maslahi bora baada ya kuhitimisha ajira yake.
 Akizungumzia kada zenye fursa pana ya ajira, Muya alisema kuwa kada ya gesi, petrol, Madaktari wa mifugo, wahandisi, na mafundi mchundo katika sekta za maji,umeme na afya,hivyo kuwataka vijana kusoma masomo ya Sayansi.

Aidha Muya alitoa wito kwa wale wote ambao wameshapangiwa vituo vya kazi katika Utumishi wa Umma kujituma, kuwa wabunifu katika sehemu zao za kazi kwani Taifa linawategemea vijana katika kufikia maendeleo endelevu kwa manufaa ya sasa na ya baadae.
 Kwa upande wake Afisa Habari wa Sekretarieti hiyo Bw. Kassim Nyaki alibainisha kuwa waombaji kazi waliofanya usaili mwezi Desemba, 2014 kuwa waliofaulu na kupangiwa vituo vya kazi jumla yao ni 572 ambapo watapangiwa vituo hivyo kabla ya mwisho wa mwezi Januari 2015.

Pata Filamu ya Never Give Up kupitia Mtandao.

$
0
0
" And in her smile I see something more beautiful than the stars " Fuatilia hii kupitia mtandao ..

Kwa Kuangalia Filamu hii ya Kitanzania iitwayo NEVER GIVE UP au Knunua na iwe yako kupitia mtandao.

Ili kuweza kuangalia au kununua kupitia Mtandao unachotakiwa kufanya ni kutembelea tovuti hii
Pia unaweza kuangalia au kununua filamu nyingine kupitia mtandao huo huo

CCM HAITASITA KUWACHUKULIA HATUA KALI WALE WOTE WANAOSAMBAZA HABARI ZA UZUSHI HASA WANAOWANIA NAFASI YA URAIS.

$
0
0
Mwaka huu 2015 ni mwaka wa uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Rais wa Jamhuri ya Muungano. Hii ni kwa mujibu wa katiba ya nchi. Ratiba ya mchakato wa kuwapata wagombea wa CCM kwa nafasi hizo haijatolewa bado.

Itakumbukwa Kamati Kuu iliyopita ya tarehe 13/01/2015, iliyoketi Kisiwandui Zanzibar ilipitisha ratiba ya shughuli za kawaida za Chama kwa mwaka 2015 na kupanga kushughulikia ratiba ya mchakato wa uteuzi wa wagombea wa CCM vikao vijavyo.

Pamoja na kutotolewa kwa ratiba hiyo, bado zimekuwepo harakati nyingi za wanaotaka kuteuliwa na CCM kugombea nafasi mbalimbali hasa ya urais wa Jamhuri ya Muungano. Harakati hizo baadhi halali, nyingi haramu.

Pamoja na kutaadharishwa mara nyingi juu ya madhara ya harakati hizo kwa umoja na mshikamano wa Chama bado baadhi yao wamekuwa wakiendelea na harakati hizo.

Kwa muda sasa kumekuwepo na uzushi mwingi juu ya baadhi ya wanaotaka kuwania nafasi hizo kujadiliwa na hata kuchukuliwa hatua na vikao vya chama. Maneno haya kwa sehemu kubwa yamekuwa yakisambazwa na wagombea wenyewe au wapambe wao.

Uzushi huu, hauna nia njema kwa CCM, unalengo la kukigawa Chama na kuonyesha kama vile Chama hakina kazi nyingine ila kujadili na kushughulika na watu hao. Kwa mara nyingine CCM inapenda kuwataadharisha wagombea hao na wapambe wao kujiepusha na kusambaza taarifa zisizokuwa za kweli. Kwa kuwa vitendo hivi vinakigawa Chama chetu.

CCM haitasita kuchukua hatua kali dhidi ya wote wanaosambaza taarifa hizi. Ni vyema wagombea wakawadhibiti wapambe wao na wakajichunga wenyewe dhidi ya hujuma hizi kwa Chama kwani zitawapotezea sifa ya kugombea.

Wengi wa wanaosambaza taarifa hizi ni wagombea au wapambe wasiojiamini kutokana na matendo yao, ambayo hata wao wana mashaka na uadilifu wao. Hatuoni sababu ya mgombea anayefuata sheria, kanuni na taratibu za Chama kuhofia kuchukuliwa hatua kila vikao vya Chama vinapofanyika.

Ukitenda kwa haki huna haja ya kuogopa vikao na kuzusha uongo na uzushi usio na ukweli. CCM inaamini matendo haya hayatajirudia.

Aidha Chama Cha Mapinduzi kinawaomba wanachama na wananchi kuzipuuza taarifa zinazosambazwa kwa kuvinukuu vyanzo visivyo rasmi, kama kuna hatua au taarifa kwa umma juu ya hatua yoyote katika mchakato huu basi itatolewa na wasemaji halali wa Chama na si kutoka vyanzo vya barabarani.

Itakumbukwa pia baada ya Kamati Kuu iliyopita kukutana tulitangaza kufanyika kwa kikao cha Kamati Ndogo ya Maadili kwa ajili ya kushughulikia masuala ya kimaadili kwenye sakata la Escrow kwa viongozi wa Chama walioko kwenye vikao vya Chama vya maamuzi.

Jana kumekuwepo na harakati nyingi za vyombo vya habari na watu binafsi kujaribu kupata taarifa ya nini kimetokea kwenye kikao hicho cha Maadili.

Tunapenda kuwakumbusha kuwa kwa mujibu wa taratibu taarifa za kilichotokea kwenye kikao cha Kamati Ndogo ya Maadili huwa hazitolewi kwa umma mpaka baada ya kufikishwa kwenye Kamati Kuu. Hivyo basi tunawaomba kutulia na kusubiri taarifa rasmi baada ya kufikishwa kwenye Kamati Kuu kuliko kuhangaika sasa hivi, jambo linaloweza kusababisha kuokotwa kwa habari za barabarani ambazo nyingi si za kweli. Tulieni subirini taarifa rasmi.


KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Imetolewa na;-
Nape Moses Nnauye
Katibu wa Itikadi na Uenezi.
20/01/2015
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images