Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MJINI MOSHI (MUWSA) YATEKELEZA MIRADI YAKE

$
0
0
MAKALA MAALUMU YA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MJINI MOSHI (MUWSA) .KUONESHA UTEKELEZAJI WA MIRADI MBALIMBALI YA MAJI PAMOJA NA JITIHADA ZA MAMLAKA HIYO KATIKA KUHAKIKISHA INAFIKISHA HUDUMA YA MAJI KWA WAKAZI WA MJI WA MOSHI NA MAENEO JIRANI INAYO HUDUMIA KWA MUDA WA SAA 24.

Video ya Makala haya imeandaliwa na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

WASANII WANAOTAKA KUSHIRIKI TAMASHA LA MUUNGANO DAY LA WASANII WA TANZANIA ,UJERUMANI WAJIANDIKISHE

$
0
0
Tamasha litafanyika mjini Koloni,Ujerumani  April 2015

Wasanii wanaotaka kushiriki katika katamasha la kongamano la wasanii wa Tanzania na afrika mashariki linalotarajiwa kufanyika mjini Kolon,Ujermani mwezi April  2015 mnaombwa mjiandikishe kwa kuwasiliana katika namba ya simu  +49(0)15778645623 .
 
Tamasha hili linania ya kutangaza sanaa za maonyesho za Tanzania nchini ujerumani,wasanii wa ngoma za asili,Sarakasi,Maigizo, Muziki n.k mnakaribishwa kujiandikisha kushiriki Tamasha hili ,Wasanii mnaombwa mtumie nafasi hii kuonyesha vipaji vyenu 
katika uwanja wa kimataifa ili kujitangaza zaidi.
Ushiriki wenu katika tamasha hili ndio dira ya ukombozi kwa wasanii wote!
Maelezo zaidi piga  simu  +49(0)15778645623

YOUTH CAMPAIGNERS MEET VICE PRESIDENT DR. MUHAMMAD BILAL IN DAR-ES-SALAAM

$
0
0
  Vice President of Tanzania, Dr Gharib Bilal answering youth questions.
   Dr Sipho Moyo, ONE Afrika Executive Director giving opening remarks at action/2015 launch
   Margaret Mliwa, Restless Development Country Director speaking at the event.
 Some of the youth telling the Vice President their priorities           
 Deputy Minister of Culture, Information, Sports and Youth, Juma Nkamia welcoming Vice President Dr Bilal. 
 According to new research, almost a billion extra people face a life of extreme poverty if leaders do not make key decisions on poverty, inequality and climate change at two crucial summits in New York and Paris later this year.

That's the warning by more than a thousand organisations around the world which are launching a new campaign called action/2015, calling on local and world leaders to take urgent action to halt man-made climate change, eradicate poverty and address inequality.

The new calculation released by the action/2015 coalition shows that the number of people living in extreme poverty – on less than $1.25 a day – could be reduced dramatically from over a billion to 360 million by 2030.

However, if leaders fail to deliver and build on the growing momentum for ambitious deals at the UN Special Summit on Sustainable Development in September and the UN Climate talks in Paris in December, and scale back their efforts, the number of people living in extreme poverty could actually increase to 1.2 billion by 2030. This increase would be the first in a generation (since 1993) and almost a billion higher (886million) than if resolute action is taken. Under this scenario, 1 in 3 of the world’s population would live under $2 a day.

Malala Yousafzai, Nobel Prize winner who put her life on the line for the right to education said; 

2015 must be the year the world wakes up and delivers a safer, more just future for children and young people. We all must play our part in ensuring this is the case. Do not let this opportunity go to waste.”

Alongside Malala, dozens of high profile activists including Archbishop Desmond Tutu, Mo Ibrahim, Angelique Kidjo, D’banj, Queen Rania of Jordan, Bono, Ben Affleck, Bill and Melinda Gates and Ted Turner have backed the coalition of over a thousand organisations in more than 120 countries around the world. The campaign is calling on world leaders to agree plans to eradicate poverty, prevent dangerous climate change and tackle inequality at these summits.

action/2015 – announced by Malala when she accepted the Nobel Peace Prize – is one of the biggest campaigns ever to launch – combining environmental, human rights, development organisations and faith networks. From household names like Amnesty International and Save the Children, to campaign and advocacy organisations like ONE, to grassroots NGOs working with local communities, the movement aims to make sure the agreements of 2015 are shaped by the people.

In Tanzania, youth campaigners have meet with His Excellency Vice-President of Tanzania Dr. Mohamed Gharib Bilal at Hyatt Regency Hotel in Dar es Salaam for a discussion on their aspirations for the future and the action they want from their political leaders in 2015.

One of the campaigners, 14-year-old Eva of Malinzanga, in Tanzania, told the Vice President;

“This year, as I turn 15, our leaders will agree a new plan for a better world. If they make it really good, and then actually stick to it, there could be almost no extremely poor people – anywhere – by the time I am 30. It’s our future that’s at stake. That’s why I and thousands like me are demanding they make the right choices in 2015”

Dr Sipho S. Moyo, Africa Executive Director of the ONE Campaign, giving opening remarks at the event said;

“Tanzania's Development Vision 2025 is an ambitious plan to move from low-income to middle-income status by 2025. For this to be achieved, the right policy priorities have to be put in place to tackle in particular extreme poverty and growing inequality by providing basic social opportunities like good education and fostering an environment  that creates what the International Labour Organization (ILO) calls decent employment. It is imperative, therefore, that the government moves rapidly and efficiently through its Big Results Now (BRN) strategy that is aimed at scaling up government’s focus and commitment to eradicating poverty and hunger and thus ensures that 2015 becomes the year that brings this great country closer to a safe and prosperous future for everybody. 

Margaret Mliwa - Country Director Restless Development Tanzania, also addressing the event said:

The launch of action/2015 is significant for young people of Tanzania. It paves the way for dialogue with their leaders from now and throughout the years. With coordinated action and unity in pushing for ambitious decisions in 2015 to address poverty and inequality, we can all work to make Tanzania a better place.
With so much at stake, this is truly the year for young people to mobilise and ensure that the decisions made by their government are representative of the Tanzania they wish to see.


As part of the launch, activities are taking place in over 50 countries all around the world.  Many of these are spearheaded by 15 year olds – a constituency who will be among the most affected by the agreements:

·        In Uganda young people will challenge the Foreign Affairs minister to listen to their demands when they hand over a petition signed by over 10,000 young people;
·        In Nigeria, 15 year olds will quiz the finance minister Ngozi Okonjo-Iweala on national television;
·        In South Africa, 15 year old campaigners from across the country will meet with Sports Minister Fikile Mbalula in the historic township of Soweto to challenge him to play a part securing a safer future for their generation.
·        In New York, the Secretary- General of the United Nations Ban Ki- moon will meet a group of 15 year olds to discuss why we need global action in 2015.
·        In the UK, some of Britain’s leading youth activists will meet Prime Minister David Cameron and Ed Miliband, the Leader of the Opposition, to urge them to seize the opportunities of 2015.

 action/2015 is calling on the public to join them in their calls to ensure world leaders commit to a better world.  Throughout 2015 the campaign will provide ways for everyone everywhere to get involved in influencing the outcomes of these global debates that could achieve:

      An end to poverty in all its forms
      The meeting of fundamental rights, tackling inequality and discrimination.
      A world where everyone can participate and hold their leaders accountable.


Watanzania Waishio Nje ya Nchi sasa Kupata Filamu za Kitanzania Kupitia Mtandao

$
0
0

Mheshimiwa Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara akisoma hotuba fupi mbele za waandishi wa habari na wageni waalikwa waliohudhuria hafla fupi ya Uzinduzi wa Mpango wa Kuuza Filamu za Proin Mtandaoni.
Mkurugenzi wa Makampuni ya Proin, Mh Johnson Lukaza akisoma hotuba fupi kwa Mgeni rasmi ambae pia Ni Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Mh Dkt Fenella Mukangara wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kuuza filamu za Proin mtandaoni.
 Muigizaji Emmanuel Muyamba Akiteta jambo na Mkurugenzi Wa Bodi ya Filamu Tanzania, ms Joyce Fissoo wakati wa hafla ya uzinduzi wa uuzaji wa filamu za kitanzania kupitia mtandao uliozinduliwa na kampuni ya Proin Promotions Leo katika hoteli ya Southern Sun.

Na Josephat Lukaza - Lukaza Blog
Mwishoni mwa Wiki Kampuni ya Utengenezaji na Usambazaji wa Kazi za Filamu Tanzania ya Proin Promotions imezindua mpango wake wa kuuza filamu za Kitanzania kupitia Mtandao wa http://www.proinpromotions.co.tz  Filamu hizo za Kitanzania Kuanzia jana zimeanza kuuzwa katika mtandao wa Kampuni ya Proin Promotions (www.proinpromotions.co.tz) ambapo mpaka sasa tayari filamu zaidi ya kumi zipo mtandaoni.
Mbali na kuuza Filamu hizo Mtandaoni mteja pia anaweza kuangalia filamu hizo mtandaoni kwa masaa 48 huku akilipia gharama ndogo kabisa au akaamua kununua kabisa na kuimiliki filamu anayoitaka. Kampuni ya Proin Promotions imeamua kufanya hivyo ili kuweza kuwawezesha Watanzania wanaoishi ndani na nje ya Tanzania kuweza kupata filamu za Kitanzania kupitia mtandao.
Kampuni ya Proin Promotions imeamua kuuza filamu za kitanzania kupitia mtandao kwa lengo la kutanua wigo wa kuuza kazi zetu na kuwafikia wadau wengi zaidi duniani pamoja na kuzitangaza kazi zetu kimataifa.
Ili mteja aweze kununua filamu zetu anachotakiwa kufanya ni kutembelea tovuti ya http://www.proinpromotions.co.tz na kufungua akaunti yake ambapo kwa kufanya hivyo ni bure kabisa mara baada ya kufungua akaunti yake mteja ataweza kuchagua filamu anayotaka kuiangalia mtandaoni au kuinunua kabisa na baada ya hapo atakachotakiwa kufanya ni kufuata maelekezo.
Kampuni ya Proin Promotions inawakaribisha Wadau wote wa filamu nchini ambao wangependa kazi zao kuuzwa mtandaoni ili kuweza kuzitangaza  na kuwezesha watanzania waishio ndani na nje ya nchi kupata filamu hizo kwa urahisi zaidi.
Proin Promotions imekuwa ni Kampuni ya kwanza nchini Tanzania ambayo imezindua huduma ya kuuza filamu za kitanzania kupitia mtandao huku wadau wengi wakitarajiwa kujiunga na Kampuni ya Proin Promotions kwa ajili ya Kuuza kazi zao kupitia mtandao.Kwa maelezo zaidi jinsi ya Kununua Filamu za Kitanzania kupitia Mtandao tembelea tovuti ya http://www.proinpromotions.co.tz

TANZANIA YASHIRIKI MAONESHO YA KIMATAIFA YA SANAA,UBUNIFU NA UTAMADUNI NCHINI OMANI

$
0
0

Naibu Balozi wa Tanzania nchini Oman Juma Othman kushoto akimsikiliza Mkuu wa Msafara wa Watanzania wanaoshirikia Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Mascut nchini Oman Bi Khadija Batash, katikati ni Afisa wa Ubalozi Bw. Abdallah kilima. unnamed1 
Mbunifu na mchongaji wa Milango maarufu kama “Zanzibar Door” Bw. Abdul-Rahman akipaka rangi baadhi ya kazi zake katika Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Mascut nchini Oman unnamed2 
Naibu Balozi wa Tanzania nchini Oman Juma Othman kulia akibadilishana mawazo na mmmoja ya Wajasiriamali kutoka Tanzania anayeshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Mascut nchini Oman unnamed3 
Salum Ameir Muchi Mchoraji akiwaonesha baadhi ya kazi zake Wageni waliotembelea Banda la Tanzania katika Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Mascut nchini Oman. unnamed4 
Mbunifu na Mchongaji “Big Mama” akionesha kazi zake Wageni waliotembelea katika Banda la Tanzania katika Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Mascut nchini Oman.
unnamed5 
Shamra shamra za ufunguzi wa Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Mascut nchini Oman. unnamed7 
Waziri wa Kilimo na Mifugo wa Oman Dkt. Fuad bin Jaafar al Sajwan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Maonesho ya Mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Mascut nchini Oman. Picha na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar .
…………………………………………………………………..
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanziabr
Jumla ya Wajasiriamali 20 kutoka Tanzania, Taasisi mbalimbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zimeshiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Mascut nchini Oman.

Taasisi hizo ni pamoja na Kamisheni ya Utamaduni Zanzibar, Baraza la Sanaa Zanzibar, Hoteli ya Bwawani, Shirika la Biashara la Taifa la Zanzibar (ZSTC) Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania na Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Nchini Omani.

Maonesho hayo ambayo yatadumu kwa muda wa Mwezi mmoja yamefunguliwa usiku wa Jana na Waziri wa Kilimo na Mifugo wa Oman Dkt. Fuad bin Jaafar al Sajwan.

Akizungumzia Maoneosho hayo Naibu Balozi wa Tanzania nchini humo Juma Othman amesema Maonesho yana leongo la kuzikutanisha nchi Rafiki za Omani kutangaza Vipaji vyao na  fursa za kimaendeleo zinazopatikana katika nchi husika.

Amesema ni fursa ya kipekee kwa Tanzania kuitumia katika kutangaza vivutio vyake, Vipaji vyake na Utamaduni wake jambo ambalo kama litatumika vyema linaweza kuipandisha hadhi zaidi Tanzania.

“Kwa ujumla tumejiandaa na nawaomba Wageni na wenye asili ya Tanzania kuja katika Banda letu kujionea mambo mbali mbali na bidhaa zinazotengenezwa na vipaji vya watu wetu” Alisema Naibu Balozi.
Bwa Othman amesema Nchi ya Omani imekuwa na kawaida ya kufanya Tamasha hilo na kualika nchi Rafiki ambapo China, India, Iran na Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoshiriki Tamasha hilo litakalochukua muda wa mwezi mmoja.

Kwa upande wake Mkuu wa Msafara huo kutoka Tanzania Bi Khadija Batash amesema Watahakikisha kuwa wanazitangaza vyema Fursa za kimaendeleo  zinazopatikana Bara na Zanzibar ili kuifanya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kusonga mbele kimaendeleo.

Amesema Tanzania imejaaliwa Raslimali nyingi ikiwemo Mbuga za Wanyama, Fukwe nzuri za Zanzibar na utamaduni wa kipekee na kwamba kama utatangzawa vyema Sekta ya Utalii itapiga hatua zaidi ya kimaendeleo.

Ameongeza kuwa Vipaji vya ubunifu wa Kuchora, Kuchonga na kufuma vinaweza kuwasaidia sana Watanzania na kuitangaza vyema kimataifa iwapo Wabunifu hao watawezeshwa vyema na Serikali au taasisi binafsi.
Aidha amewataka Washiriki kuzidisha Mashirikiano miongoni mwao ili kuiletea Sifa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Maonesho hayo ya muda wa mwezi mmoja yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, huanza kila ifikapo saa 10 za jioni na kufungwa saa 04 usiku kwa majira ya nchi ya Omani.

MSAJILI WA VYAMA AVIAS VYAMA VYA SIASA

$
0
0
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO.

MSAJILI wa Vyama Vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amevitaka vyama vyote vya siasa kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria , katiba na kanuni ili kuepusha migogoro. Aidha msajili huyo amevitaka vyama hivyo mfano mzuri wa kwa jamii kwa kudumisha amani na utulivu ndani ya vyama vya siasa.

Kauli hiyo imetolewa leo na Msajili huyo katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari kufuatia kuwepo kwa wimbi kubwa la migogoro ndani ya vyama hivyo. “Endapo kwa bahati mbaya mgogoro ukiibuka, unatakiwa utatuliwe kwa utaratibu na namna ambayo itadumisha amani na utulivu ndani ya chama,” alisema Jaji Mutungi.

Jaji Mutungi amewataka wanachama wa kawaida wa vyama vya siasa kupenda amani na utulivu ndani ya chama na kuepuka migogoro kwa kuheshimu na kufuata mfumo au taratibu za kuwasilisha malalamiko uliopo ndani ya chama au taasisi husika. Pia wawe wavumilivu mpaka watakapopata majibu ya malalamiko yao kutoka katika utaratibu huo uliowekwa na taasisi husika.

Aliongeza kuwa ofisi yake inajitahidi kuepusha na kutatua migogoro ndani ya vyama kwa kuchukua hatua zifuatazo, ambazo ni kuvihimiza vyama vya siasa kuheshimu sheria,kuzingatia misingi ya demokrasia na utawala bora,katiba na kanuni zake, kusuluhisha mgogoro unapoibuka,“Na hivi sasa tumewasilisha Serikalini mapendekezo ya marekebisho ya sheria yatakayosaidia kuepusha migogoro ndani ya vyama,” alisisitiza.

Ameiomba jamii ikemee tabia ya migogoro isiyo na tija ,inapoona vyama vya siasa havitekelezi wajibu wake, badala yake vinajikita katika migogoro ndani ya ndani.

RAIS KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI CHA KWANZA KWA MWAKA HUU WA 2015

$
0
0
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri cha kwanza kwa mwaka huu wa 2015 Ikulu jijini Dar es salaam leo January 16, 2015. Kulia kwake ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali na kushoto kwake ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda. PICHA NA IKULU

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA-KUNA MATUMAINI MAKUBWA YA KUFIKIWA MAKUBALIANO YA KUKIUNGANISHA CHAMA CHA SPLM

$
0
0


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana jana  aliwasili Arusha kwa lengo la kufanya mazungumzo na makundi matatu ya chama cha SPLM ya Sudani ya Kusini, mashauriano hayo yalilenga kukamilisha makubaliano baina ya makundi hasimu. 

Baada ya Mazungumzo Ndugu Kinana alisema ana matumaini ya kufikiwa makubaliano ya kukiunganisha chama cha SPLM katika siku chache zijazo 
Kutoka kushoto ni Balozi David Kapya,Abdulrahman Kinana,Mwenyekiti wa Mazungumzo Dk.John Samuel Malecela na Makamu Mwenyekiti wa mazungumzo Dk. Hassan Kibelloh mazungumzo hayo yalifanyika Ngurdoto Arusha. 
Viongozi wa Makundi matatu kutoka chama cha SPLM kutoka Sudani ya Kusini wakiwa kwenye mazungumzo ya kufikia makubaliano ya kuunganisha chama chao cha SPLM. Hapa wakiwa  na viongozi wa Tanzania wanaosaidia kumaliza tofauti na yakiwa yanasimamiwa na Chama Cha Mapinduzi chini ya uongozi wa Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana.

======  ======  ===== =======
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alitangaza kuwa Tanzania imekubali kuwa msuluhishi wa mgogoro wa kisiasa ndani ya chama tawala cha Sudan Kusini cha Sudanese People’s Liberation  Movement (SPLM), mgogoro ambao ulisababisha kuzuka kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Hata hivyo, Rais Kikwete alisema kuwa usuluhishi huo utakuwa wa kichama na Chama cha Mapinduzi (CCM) ndicho kitaongoza usuluhishi huo katika mazungumzo yatakayofanyika Arusha na kuwa jitihada hizo za Tanzania hazitaingilia mazungumzo ya kujaribu kusimamisha mapigano nchini humo yanayoendelea huko Addis Ababa, Ethiopia.

Rais Kikwete alisema kuwa ulikuwa uongozi wa SPLM na hasa Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais Salva Kiir ambao wameiomba Tanzania kusaidia jitihada za kisiasa za kupatanisha pande ambazo zinavutana na kutofautiana ndani ya SPLM wakiamini kuwa mapatano ndani ya chama yatafanikisha kumaliza mgogoro wa kisiasa katika Serikali ya nchi hiyo ambayo  imegawanyika na kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Rais Kikwete alitangaza jitihada hizo za upatanishi za Tanzania wakati alipohutubia maelfu kwa maelfu ya wananchi na kupitia kwao Taifa kwenye Sherehe ya Kuzima Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Kilele cha Wiki ya Vijana kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.

“Ni fahari kwetu kwamba wananchi wa Msumbiji, Zimbabwe, Angola, Namibia na Afrika Kusini nao wako huru na tumetoa mchango wetu.  Ni jambo la faraja kubwa kwamba nchi yetu imeweza kupatia hifadhi ndugu zetu wa nchi jirani na hata mbali wakati maisha yao yalipokuwa hatarini kwa sababu ya kukosekana kwa amani ama kukimbia mateso ya uongozi wa kidikteta. Ndugu zetu wa Kongo, Burundi, Rwanda, Kenya na Comoro wanaujua ukweli huo. Na, kwa Uganda tuliwasaidia kuling’oa Dikteta Idd Amin na Comoro tulisaidia kuunganisha nchi yao tena.”


VIJANA WATAKIWA KUJITUMA NA KUFANYA KAZI KWA KWA MAENDELEO YAO

$
0
0
Ndugu Elly David Akitoa Mada Kuhusu Vijana kujituma na kufanya kazi kwa Bidii Kwa maendeleo ya taifa.Mtoa Mada huyo amesema kutokana na Ukosefu wa ajira hususani kwa vijana ni vyeme vijana kujituma na kuwa wabunifu na waweze kujiajiri kwa lengo la Kupambana katika Maisha.Katika Kongamano hilo la Vijana lililofanyika Jijini dar es salaam Liliwapa Fursa vijana kueleza Changamoto zinazowakabili na namna ya Kuzikabili.Kongamano hilo lililoandaliwa na Elly David mara baada ya ya kuona changamoto zinazowakabili vijana wa kitazania ili kuwapa fursa vijana kukutana kubadilishana mawazo Pamoja na Kuangalia namna ya kutatua changamoto zinazowakabili vijana wa Kitanzania/

Historia ya Tanzania na nchi za GCC yawa chachu ya uwekezaji nchini.

$
0
0
 
 Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
Serikali ya Tanzania itaendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na kuendeleza ushirikiano na mahusiano mzuri uliopo kati yake na nchi zinazounda umoja wa nchi za Ghuba (GCC).

Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es salaam na Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima alipokuwa akifunga mkutano wa siku mbili wa wafanyabishara kutoka Tanzania na nchi za GCC ambao ulianza Januari 15 hadi 16 mwaka huu.

Malima alisema kuwa Watanzania umefika wakati wa kuboresha biashara zetu ili kuweza kuuza bidhaa bora ndani na nje ya nchi na kukabiliana na changamoto za soko la kimataifa.

“Viwango vya mazao yetu vinapaswa viewe bora, ambapo ubora huo utaruhusu bidhaa zetu ziuzike nchi nyingine” alisema Malima.

Akitolea mfano, Malima alisema Tanzania imejaliwa kuwa na mifugo mingi inayoweza kuzalisha nyama ambayo soko lake tunalo tayari ambalo ni nchi za GCC na kusisitiza kuwa nyama hiyo inapaswa kuandaliwa  katika machinjio salama na ya kimataifa ili kufungua fursa ya kuuza nyama hiyo maana milango sasa ipo wazi kwa serikali ikishirikiana na wafanyabiashara nchini.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Shirikisho la Wafanyabiashara kutoka nchi za Ghuba (FGCCC) Abdulrahman Bin Saleh Al- Otainshan alisema kuwa jumuiya ya wafanyabiashara wan chi za Ghuba  wameona na wanatarajia kufanya biashara Tanzania katika sekta ya kilimo na mifugo ambapo wanategemea kupata mzao mbalimbali yanayohitajika nchi za Uarabuni.

Mazao hayo yanayohitajika ni pamoja na mchele, matunda, mboga mboga, asali na nyama.Zaidi ya hayo, Rais hyo wa FGCCC alisema kuwa nchi zianazounda umoja huo zinatarajia kuwekeza Tanzania katika sekta za  kilimo, mifugo, elimu, maji, afya, ufundi na utalii.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa benki ya BADEA alisema kuwa Abdel Aziz Khelef alisema kuwa benki yake itaendelea kuwa kiunganishi muhimu kati ya wafanyabiashara wa Tanzania na nchi za GCC ambapo wamekuwa na uhusiano mzuri kwa zaidi ya miaka 40.

Nchi zinazounda umoja wa GCC ni Kuwait, Oman, Bahrain, Qatar, UAE na Saud Arabia zinauhusiano wa karibu na Tanzania kihistoria, lugha pamoja mila na desturi.

TAARIFA YA MSIBA WA DADA LETICIA MATTEI RWECHUNGURA

$
0
0
 Tunasikitika kutangaza kifo cha ghafla cha  dada yetu mpendwa Leticia Mattei Rwechungura kilichotokea hapa Ujerumani tarehe 06.01.2015.Mazishi yatafanyika hapa Ujerumani Königswinter, karibu na mji wa Bonn tarehe 24.01.2015. Misa itaanza saa tano asubuhi (11:00 a.m.), katika Kanisa la St. Michael Niederdollendorf, Petersbergerstr. 14, 53639 Königswinter.

Dada Leticia Mattei alikuwa mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa huko South Sudan (UNMIS) - United Nations Mission in Südan, Eastern Equatoria State of Torit-Sudan. Aliugua muda mfupi na kufariki dunia katika hospitali iliyoko mjini Bonn hapa Ujerumani. 

Watanzania wote walioko hapa Ujerumani, nyumbani Tanzania na ulimwenguni kote wameshtushwa na kifo hiki cha ghafla cha kuondokewa na mama yetu na dada yetu mpenzi Leticia Mattei. Tutamkumbuka daima kwa kazi kubwa alizoifanyia nchi yetu ya Tanzania, bara la Afrika na dunia nzima kwa ujumla. Mungu amlaze mahali pema Peponi - Amin!
Kwa yeyote atakayependa kutoa sanda yake, tunaomba michango itumwe moja kwa moja kwa mtoto wa marehemu:

Diana Kajuna
IBAN: DE76 3806 0186 5501 3030 13
BIC: GENODED1BRS
Kreditinstitut: Volksbank Bonn Rhein-Sieg eG

Tunaomba sana ili tuweze kutekeleza mipango hii vizuri ya kumsindikiza dada yetu kwa heshima zote, wale wanaopenda kuhudhuria mazishi haya wawasiliane na mratibu wa shughuli hizi Nd. Majura, ili tupate orodha kamili ya wale wanaokuja ili itusaidie kuandaa mambo mengi ya muhimu. Kwa wale watakaopenda kupata malazi (ya hoteli), kadhalika tunaomba wawasiliane na Dr. Isack Majura kuanzia sasa kupitia:

Tel. +49 173 7089513
e-Mail: IMajura@aol.com
Germany

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA YAFANA WILAYA YA DIMANI MKOA WA MAGHARIBI.

$
0
0
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Idd mara baada ya kumaliza kikao cha halmashauri kuu ya wilaya ya Dimani. 
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kufyeka majani mbele ya Chuo cha Sayansi ya Bahari (IMS), alipotembelea chuo hicho kilicho chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam eneo la Buyu, Unguja Zanzibar leo wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM pamoja na kusikiliza kero za wananchi ili zipatiwe ufumbuzi. PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win
 Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana ukielekea katika jimbo la Fuoni kushiriki upandaji wa mikoko katika hifadhi ya Baahari,kaa na ufugaji nyuki  katika eneo la Fuoni Bondeni. 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Dimani mkoa wa Magharibi Zanzibara na kuataka wana CCM kushikamana huku akiwaambia vijana kuwa wasiwewanyonge katika kukitetea chama chao.
  Mamia ya watu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM kwenye viwanja vya Magereza ,Tomondo wilaya ya Dimani mkoa wa Magharibi Zanzibar.
   Katibu wa NEC Itikadi Na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa wilaya ya Dimani mkoa wa Magharibi ambapo aliwaeleza hesabu na sayansi ya kisiasa imewamaliza wapinzani hivyo CCM itashinda uchaguzi ujao.
 Baadhi ya Wanahabari wakiwa kazini .
 katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake wakielekea kukagua na kupata maelezo juu ya ujenzi wa Chuo cha sayansi ya Bahari na kutoa nasaha kwa chuo hicho.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikata utepe kuzindua rasmi gari la wagonjwa lililotolewa na Mbunge wa jimbo la Fuoni kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa katika jimbo hilo.
 Mamia ya watu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM kwenye viwanja vya Magereza ,Tomondo wilaya ya Dimani mkoa wa Magharibi Zanzibar.

PICHA NA MICHUZI JR-WILAYA YA DIMANI-UNGUJA

Ridhiwani Kikwete ashiriki mazishi Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Mkoa Pwani, SALEHE MPWIMBWI

$
0
0

 MBUNGE Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akiweka mchanga kwenye kaburi la Salehe Mpwimbwi aliyezikwa katika makaburi yaliyopo nje kidogo ya kijiji cha Miono, mazishi yaliyofanyika juzi baada ya Mpwimbwi kupata ajali akiwa kwenye gari yake binafsi akitokea kijiji
> cha jirani kumpeleka mgonjwa ambapo njiani gari lake lilipasuka taili na kupinduka
KAKA wa Rais Jakaya Kikwete Selemani Kikwete akiweka mchanga katika Kikwete akiweka mchanga kwenye kaburi la Salehe Mpwimbwi aliyezikwa katika makaburi yaliyopo nje kidogo ya kijiji cha Miono, mazishi yaliyofanyika juzi baada ya Mpwimbwi kupata ajali akiwa kwenye gari yake binafsi akitokea kijiji cha jirani kumpeleka mgonjwa ambapo njiani gari lake lilipasuka taili na kupinduka. (PICHA NA OMARY SAID).

Matukio Picha Hafla ya Wanahabari na Kampuni ya Afrika Internet Holding

$
0
0

Meneja wa Kampuni ya Lamudi nchini Tanzania, Godlove Nyagawa akizungumza na wageni waalikwa wanahabari na wadau wengine wa kampuni hiyo kwenye hafla ya kufahamiana iliyoandaliwa na Afrika Internet Holding. Meneja wa Kampuni ya Lamudi nchini Tanzania, Godlove Nyagawa akizungumza na wageni waalikwa wanahabari na wadau wengine wa kampuni hiyo kwenye hafla ya kufahamiana iliyoandaliwa na Afrika Internet HoldingMeneja wa Kampuni ya Kaymu.com nchini Tanzania, Erfam Mosgani (kushoto) akizungumza na baadhi ya wageni waalikwa katika hafla ya kufahamiana na kubadilishana uzoefu na wanahabari iliyoandaliwa na kampuni ya Afrika Internet Holding. Meneja wa Kampuni ya Kaymu.com nchini Tanzania, Erfam Mosgani (kushoto) akizungumza na baadhi ya wageni waalikwa katika hafla ya kufahamiana na kubadilishana uzoefu na wanahabari iliyoandaliwa na kampuni ya Afrika Internet Holding.Kutoka kushoto ni Meneja wa Kampuni ya Kaymu.com nchini Tanzania, Erfam Mosgani (kushoto), Meneja Mwendeshaji wa Mo Blog, Mr. Zainul M. na Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Mahusiano Kaymu.com, Angaza Nkurlu wakibadilishana uzoefu katika hafla ya kufahamiana iliyoandaliwa na kampuni ya Afrika Internet Holding. Kutoka kushoto ni Meneja wa Kampuni ya Kaymu.com nchini Tanzania, Erfam Mosgani (kushoto), Meneja Mwendeshaji wa Mo Blog, Mr. Zainul M. na Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Mahusiano Kaymu.com, Angaza Nkurlu wakibadilishana uzoefu katika hafla ya kufahamiana iliyoandaliwa na kampuni ya Afrika Internet HoldingBaadhi ya wanahabari na wadau wa kampuni ya Afrika Internet Holding wakiwa katika hafla hiyo. Baadhi ya wanahabari na wadau wa kampuni ya Afrika Internet Holding wakiwa katika hafla hiyo.
Ofisa Msaidizi Kitengo cha Uhusiano wa Kampuni ya Lamudi Tanzania, Lilian Kisasa (katikati) akibadilishana uzoefu na baadhi ya wanahabari katika hafla ya kufahamiana iliyoandaliwa na kampuni ya Afrika Internet Holding. Ofisa Msaidizi Kitengo cha Uhusiano wa Kampuni ya Lamudi Tanzania, Lilian Kisasa (katikati) akibadilishana uzoefu na baadhi ya wanahabari katika hafla ya kufahamiana iliyoandaliwa na kampuni ya Afrika Internet Holding.Meneja wa Kampuni ya Jumia nchini Tanzania, Sabrina Dorman (kushoto)akizungumza na baadhi ya wageni waaliwa (wanahabari) katika hafla ya kufahamiana na wadau wa kampuni ya Afrika Internet Holding. Meneja wa Kampuni ya Jumia nchini Tanzania, Sabrina Dorman (kushoto)akizungumza na baadhi ya wageni waaliwa (wanahabari) katika hafla ya kufahamiana na wadau wa kampuni ya Afrika Internet Holding.IMG_0032IMG_0027
[caption id="attachment_54815" align="aligncenter" width="800"]Baadhi ya wanahabari na wadau wa kampuni ya Afrika Internet Holding wakiwa katika hafla hiyo. Baadhi ya wanahabari na wadau wa kampuni ya Afrika Internet Holding wakiwa katika hafla hiyo.[/caption] [caption id="attachment_54816" align="aligncenter" width="800"]Meneja wa Kampuni ya Jumia nchini Tanzania, Sabrina Dorman (katikati) akizungumza na baadhi ya wageni waaliwa (wanahabari) katika hafla ya kufahamiana na wadau wa kampuni ya Afrika Internet Holding. Meneja wa Kampuni ya Jumia nchini Tanzania, Sabrina Dorman (katikati) akizungumza na baadhi ya wageni waaliwa (wanahabari) katika hafla ya kufahamiana na wadau wa kampuni ya Afrika Internet Holding.[/caption] [caption id="attachment_54817" align="aligncenter" width="751"]Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Carmudi Afrika Mashariki, William Day (kushoto) akibadilishana mawazo na mmoja wa maofisa wa kampuni yake. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Carmudi Afrika Mashariki, William Day (kushoto) akibadilishana mawazo na mmoja wa maofisa wa kampuni yake.[/caption] [caption id="attachment_54818" align="aligncenter" width="800"]Baadhi ya wanahabari na wadau wa kampuni ya Afrika Internet Holding wakiwa katika hafla hiyo. Baadhi ya wanahabari na wadau wa kampuni ya Afrika Internet Holding wakiwa katika hafla hiyo.Baadhi ya wanahabari na wadau wa kampuni ya Afrika Internet Holding wakiwa katika hafla hiyo. Baadhi ya wanahabari na wadau wa kampuni ya Afrika Internet Holding wakiwa katika hafla hiyo.

Waziri Fenella akutana na Jukwaa la wahariri

$
0
0
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akiwaeleza wahariri wa vyombo vya habari nchini wajibu na umuhimu wa  vyombo vya habari katika mchakato huu wa upatikani wa katiba mpya ikiwemo kutoa elimu kuhusu umuhimu wa mchakato huu kwa mustakabali wa Taifa pia alivipongeza vyombo vya habari katika elimishaji wa wananchi katika mchakato wa Bunge Maalum la Katiba, Wakati wa Mkutano na Wahariri wa Vyombo vya Habari Leo Jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Absalom Kibanda akiongea wakati wa mkutano uliowakutanisha wahariri wa vyombo na Waziri wa Habari, Vijana, Utamduni na Michezo ambapo Dkt. Fenela Mukangara ambapo waliwataka wahariri kuwa wamoja katika masuala ya kitaifa hasa yatakayopelekea kuibomoa nchi yetu pia aliwaasa wahariri kutumia kalamu zao vizuri kuwaelimisha wananchi katika mchakato huu wa kuelekea upatikaji wa Katiba Mpya kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw. Assah Mwambene, Naibu Waziri Wizara ya Katiba na Sheria Mh.Angela Kairuki  na Mwisho ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara Leo Jijini Dar es Salaam.
 Mzee Kingunge Ngombale-Mwiru akiongea na wahariri wa vyombo vya habari ambapo ambapo aliwaeleza kuhusu umuhimu wa upatikanaji wa katiba mpya kwa maendeleo ya Taifa ikiwa katiba iliyopendekezwa imezingatia Masuala muhimu ya ukuzaji uchumi wan chi pia uzingatiaji wa makundi mbalimbali katika jamii na alisisitiza umuhimu wa vyombo vya habari kuendelea kutoa elimu kuelekea upatikanji wa katiba mpya kwani katiba ni chombo cha ukombozi wa nchi.
 Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Absalom Kibanda akisalimiana na Mzee Kingunge Ngombale-Mwiru wakati wa mkutano wa wahariri wa vyombo vya Habari na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara.
 Mh. Hamadi Rashid Muhamed akiwaeleza wahariri wa vyombo vya habari ambapo alieleza furaha yake kwa katiba inayopendekezwa kujikita katika kutatua changamoto za muungano zitakazopekea kuimarika kwa muungano wa Tanzania bara na Zanzibar.
Baadhi wa Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini Wakifuatilia Mada zilizokuwa zinawasilishwa katika mkutano huo

TAZAMA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2015 HAPA

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, AHUDHURIA SHEREHE ZA KUSIMIKWA ASKOFU MKUU JIMBO LA DODOMA LEO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia kwenye Sherehe ya Kumsimika Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dodoma Beatus Kinyaiya iliyofanyika leo Januari 18, 2015 katika Kanisa la Mt. Paulo wa Msalaba Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dodoma Beatus Kinyaiya baada ya kusimikwa rasmi kwenye Sherehe iliyofanika leo Januari 18, 2015 katika Kanisa la Mt. Paulo wa Msalaba Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katikati akiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu mbalimbali waliohudhuria sherehe ya kusimikwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dodoma Beatus Kinyaiya kwenye Sherehe iliyofanika leo Januari 18, 2015 katika Kanisa la Mt. Paulo wa Msalaba Dodoma. (Picha na OMR)

Chama cha uzazi na malezi bora (UMATI) chatembelea kituo cha watoto yatima kurasini

$
0
0
 Mkufunzi wa vijana kutoka kituo cha vijana umati temeke akiwafundisha vijana kuhusu hatua za ukuaji na athari zake.

Mwerimishaji rika kutoka kituo cha vijana umati temeke ambaye pia alikuwa mtoto yatima kituoni hapo akiwaeleza vijana umuhimu wa elimu.

 Afisa Vijana wa Kituo cha Vijana UMATI Temeke akikabidhi zawadi kwa mwakilishi wa watoto yatima wa kituo cha Kurasini jijin Dar es Salaam walipotembelea kituoni hapo jana.
 Wafanyakazi wa umati wakiwa na watoto yatima pamoja na walezi wa watoto yatima katika kituo cha watoto yatima Kurasini.Picha kwa Hisani ya Kituo cha Vijana,UMATI-TEMEKE

WANANCHI MKURANGA WAASWA KUCHANGIA DAMU.

$
0
0
unnamedMkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Emanuel Mjema (kulia) akimkabidhi Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga Dkt. Anwar Milulu (kushoto) msaada wa mashuka yenye 90 yaliyotolewa na chuo hicho kusaidia wagonjwa katika hospitali hiyo.Makabidhiano hayo yalifanyika jana wilayani Mkuranga kama  sehemu ya Chuo hicho kuadhimisha miaka 50 toka kianzishwe mwaka 1965.unnamed1Baadhi ya Wauguzi na wahudumu wa afya wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga wakiangalia moja ya shuka kati ya mashuka 90 yaliyotolewa na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kusaidia wagonjwa wanaolazwa katika hospitali hiyo.unnamed2Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Emanuel Mjema (katikati) akitoa ufafanuzi kuhusu msaada wa mashuka  90 yaliyotolewa na chuo hicho katika hospitali ya wilaya ya Mkuranga ikiwa ni sehemu ya mpango wa chuo hicho kutoa huduma kwa jamii.
unnamed4Baadhi ya viongozi wa Chuo cha Elimu ya Biashara CBE wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga jana.
 ……………………………………………………………………………..
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
 Mkuranga, Pwani.
 
Wananchi wilayani Mkuranga wametakiwa kujenga utamaduni wa kuchangia  damu kwenye  benki ya damu iliyoko katika hospitali ya wilaya hiyo ili kupunguza tatizo la uhaba wa damu linaloikabiri hospitali hiyo.
Kauli hiyo ilitolewa jana wilayani Mkuranga na Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya  hiyo, Dkt. Anwar Milulu wakati akipokea msaada wa mashuka 90 yaliyotolewa na Chuo cha Elimu ya Biashara Dar  es salaam (CBE) kwa lengo la kuwasaidia wagojwa wanaolazwa katika hospitali hiyo.
 
Alisema kuwa hospitali hiyo kwa sasa inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa damu kutokana na mwamko mdogo wa wakazi wa wilaya hiyo wanaojitokeza kuchangia damu jambo linalosababisha upungufu wa damu na usumbufu kwa wagonjwa wanaohitaji kuongezewa damu .
 
“Kama mnavyoona hospitali yetu iko barabarani kwa sasa tunakabiliwa na tatizo la upungufu wa damu, baadhi ya wagonjwa hutufikia wakiwa katika hali mbaya  ya kuhitaji kuongezewa damu kiasi cha  kutufanya tuwapeleke katika hospitali ya Taifa Muhimbili  kuokoa maisha yao” Alisema Dkt. Milulu.Alieleza kuwa lishe duni na kutozingatia ulaji wa mboga za majani kama inavyoshauriwa na wataalam wa afya ni miongoni mwa sababu zinazochangia kuendelea kwa tatizo la upungufu wa damu kwa akina mama wajawazito na watoto.
 
Dkt. Milulu alifafanua kuwa hospitali hiyo imekuwa ikitoa elimu kwa wagonjwa hususan akina mama wajazito na watoto pindi wanapohudhuria Kliniki kwa lengo la kuwaeleza umuhimu wa uzingatiaji wa lishe bora na namna ya  kukabiliana na tatizo la upungufu wa damu miongoni mwa jamii.
 
Aidha, alisema Serikali inaendelea kuyatafutia ufumbuzi matatizo ya ukosefu wa maji,uhaba wa miundombinu  na dawa yanayoikabili hospitali hiyo kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa wa kawaida na wale walio katika makundi maalum wanaohudumiwa na hospitali hiyo ikilinganishwa na uwezo wake.“Serikali inaendelea kushughulikia tatizo la maji,miundombinu na upungufu wa dawa unaoikabili hospitali yetu maana idadi ya wananchi tunaowahudumia ni wengi ikilinganishwa na uwezo wa miundombinu ya hospitali”
 
Kuhusu changamoto ya rasilimali watu na wataalam wa kada mbalimbali alisema kwa sasa hospitali hiyo  ina idadi inayoridhisha ya  Madaktari, Wauguzi, wahudumu, wataalam wa maabara na madereva ikilinganishwa na miaka iliyopita.Alitoa wito kwa uongozi wa chuo hicho kuendelea kuisaidia hospitali hiyo katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha wanafunzi wa chuo cha CBE kujitokeza kuchangia damu mara kwa mara  ili  kuokoa maisha ya wagonjwa.
 
Nao baadhi ya wananchi waliokuwa wakipatiwa huduma katika hospitali hiyo wakizungumza kwa nyakati tofauti licha ya kuushukuru uongozi wa chuo cha CBE kwa kuwakumbuka kwa kuwapatia msaada wa mashuka hayo walikiri kuwepo kwa mwamko mdogo wa wananchi  kuchangia damu katika benki ya damu ya hosptali hiyo.
 
Aidha, waliiomba Serikali kulishughulikia tatizo la  maji , miundombinu na uhaba wa dawa uliopo katika hospitali hiyo na kuwaomba wadau wengine wajitokeze kuisaidia hospitali hiyo ili iweze kutoa huduma bora kwa wananchi.
 
Awali akizungumza msaada huo Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Emanuel Mjema alisema kuwa chuo chake ifikapo Januri 21, 2015 Chuo cha  Elimu ya Biashara kinatimiza miaka 50 hivyo msaada walioutoa ni sehemu ya huduma kwa jamii.
 
Alisema katika kuelekea kutimiza  miaka 50 ya chuo cha CBE mbali na kujikita katika masuala ya kuelimisha jamii katika taaluma  mbalimbali ikiwemo Biashara, Ugavi na manunuzi, Vipimo, TEHAMA na Utawala katika biashara kimekua kikitoa huduma mbalimbali kwa jamii.
 
Alisema katika kuelekea maadhimisho ya miaka 50 chuo hicho kimekuwa kikitoa misaada ya vitu mbalimbali na elimu ya ujasiriamali kwa wananchi katika mikoa yote ambayo kina matawi yake ikiwemo Dar es salaam, Mbeya, Zanzibar, Mwanza na Dodoma.

timu ya wataalamu kutoka wizara ya uchukuzi watembelea kampuni ya kutoka huduma za ndege,mizigo na abria ya swissport

$
0
0
 Meneja wa Huduma za Mizigo, ndege na Abiria wa Swissport, Stella Kitali, akiwaonyesha wataalam kutoka Wizara ya Uchukuzi, karatasi inayotumika kuonyesha aina za mizigo inayopakiwa kwenye ndege  wakati wataalam hao walipotembelea Kampuni hiyo,  mwishoni mwa wiki kuona huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
 Meneja wa Huduma za Mizigo, ndege na Abiria wa Swissport, Stella Kitali, akiwaonyesha wataalam kutoka Wizara ya Uchukuzi, ngazi mbalimbali zinazotumika wakati abiria wanaposhuka kutoka kwenye ndege,  wakati wataalam hao waliotembelea Kampuni hiyo,  mwishoni mwa wiki kuona huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
 Moja ya magari yanayomilikiwa na Kampuni ya kudumia ndege, abiria na Mizigo ya Swissport, yanayotumika kushusha mizigo kutoka kwenye ndege, kama lilivyokutwa mwishoni mwa wiki wakati wataalam kutoka Wizara ya uchkuzi, walipotembelea kampuni hiyo kuona huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni hiyo kwa ndege mbalimbali zinazotua katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA).
 Ndege za mashirika mbalimbali zinazofanya safari zake kutoka Tanzania kwenda Nchi za nje, zikiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA). Idadi ya abiria wanaowasili na kuondoka katika viwanja vya ndege nchini imeendelea kuongezeka kutoka abiria  2,172, 519  mwaka 2005 hadi abiria  4,670,380  mwaka 2013, sawa na  ongezeko la asilimia 14.8.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi).

Moja ya magari yanayomilkiwa na kampuni ya kuhudumia mizigo, ndege na abiria ya Swissport, likitumika kuitoa ndege na kuiweka kwenye Barabara ya kiungio (tax way) kabla haijaondoka, kama lilivyokutwa mwishoni mwa wiki.
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images