Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 441 | 442 | (Page 443) | 444 | 445 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwasalimia baadhi ya Wananchi hawapo pichani alipokuwa akiwasili katika uwanja wa Tawi la CCM Matarumbeta katika jimbo la Jang'ombe,ambapo Ndugu Kinana alikabidhi vifaa vya michezo kwa vijana,alikabidhi vifaa vya mradi wa maji safi,pia alikabidhi hati kwa kikundi cha vijana Jang'ombe.
   Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana pamoja na wanachama wa CCM wakiwemo na Wananchi kwa pamoja wakishiriki katika shughuli ya za uchimbaji na utandazaji wa mabomba ya mradi wa maji safi na salama katika shehia ya Kilimani,kwenye jimbo la Mjimkongwe.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata maelezo mafupi ndani ya chumba cha kufundishia Kompyuta katika kituo cha Vijana (Tanzania Youth Icon),cha kuwaendeleza na kuwawezesha katika masuala mbalimbali ikiwemo elimu,Ajira na Michezo kilichopo Shehia ya Miembeni,Mwembemadema katika jimbo la Kikwajuni.
   Mwenyekiti wa Kituo cha Tanzania Youth Icon (TAYI),Bwan.Abdullah Miraji Othman akisoma hotuba Mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kuhusiana na mambo mbalimbali yahusuyo kituo hicho cha huduma rafiki kwa Vijana kilichopo Muembemadema ndani ya jimbo la Kikwajuni sambamba na changamoto wazipatazo juu ya kituo hicho.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana  akizungumza mbele ya wanachama wa chama hicho pamoja na Wananchi nje ya Kituo cha Tanzania Youth Icon (TAYI),ambapo mlezi na mhamasishaji wake ni Mbunge wa jimbo la Kikwajuni,Mh.Hamad Yusuf Masauni.Kituo hicho cha TAYI ni Taasisi ya vyama visivyokuwa vya kiserikali,ambayo ina muelekeo wa kuwasaidiana na Wadau mbalimbali katika kufanikisha shughuli za maendeleo.Mwenyekiti wa Kituo cha Tanzania Youth Icon (TAYI),Bwan.Abdullah Miraji Othman amesema kuwa Taasisi hiyo hivi sasa ina ina wanachama wasiopungua 500 ambao tayari wameandikishwa na kuwepo katika rekodi na kumbukumbu za ofisi,Bwana Abdullah aliongeza kuwa kituo hicho kinawajenga vijana kiuchumi na pia kuwapa taaluma ya uongozi ili waje kuwa viongozi wazuri ,''kituo hiki kimekuwa kiwanda kizuri cha kuzalisha vijana wazuri kwa Taifa'',alisema Bwan.Abdullah .
  Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana ukiwasili katika tawi la CCM Mikunguni (shehia ya Mikunguni),kushiriki katika shughuli za uchimbaji na utandazaji wa mabomba ya maji na salama.
   Mbunge wa Jimbo la Kwahani,Mh.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizungumza mbele ya wakazi wa Shehia ya Mikunguni (hawapo pichani),wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana aliyoianza leo wilaya ya mjini Zanzibar.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na baadhi ya wananchi na wanachama wa Shehia ya Mikunguni ,wakati wa ziara yake aliyoianza leo wilaya ya mjini Zanzibar.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kwahani,Mh.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akishiriki uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama kwa wakazi wa Shehia ya Mikunguni ,katika jimbo la Kwahani.
    Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kwahani,Mh.Dkt.Hussein Ali Mwinyi wakishiriki katika shughuli za uchimbaji na utandazaji wa mabomba ya maji safi na salama kwa wakazi wa Shehia ya Mikunguni ,katika jimbo la Kwahani.

   Baadhi ya wakazi wa mji wa Shehia ya Makadara wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipotembelea jimbo la Rahaleo,ambapo alishiriki katika ujenzi wa Taifa za uchimbaji wana utandazaji wa Mabomba ya maji safi na salama.
   Wananchi wa mji wa Shehia ya Makadara na wanachama wa CCM,wakishangilia jambo  Katibu Mkuu wa CC,Ndugu Kinana akiwa
  Katibu Mkuu wa CC,Ndugu Kinana akishiriki ujenzi wa Ofisi ya tawi la CCM-Mwembeladu katika jimbo la Rahaleo
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na Balozi Ali Karume alipowasili katika Shehia ya Miembeni,katika jimbo la Kikwajuni,ambapo Ndugu Kinana alipokea taarifa fupi ya mradi wa Zahanati  na kushiriki katika ujenzi wa Taifa wa Ukarabati wa Zahanati ya Miembeni (Nyumba ya Yasu).Pichani kulia ni Muwakilishi wa jimbo la Kikwajuni,Mh.Mahamoud Mohamed Mussa pamoja na Mbunge wa jimbo hilo la Kikwajuni Mh.HamadiYussuf Massauni
  Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akifurahia jambo na  Balozi Ali Karume  walipokutana leo katika Shehia ya Miembeni,katika jimbo la Kikwajuni
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata maelezo mafupi ya mradi mkubwa wa kisasa alipokwenda kutembelea Tawi la CCM Vikokotoni katika jimbo la MjiMkongwe
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata taarifa fupi ya mradi wa maduka kwa vijana wajasiliamali katika Shehia ya Kilimani,ambapo Ndugu Kinana alishiriki shughuli za uchimbaji na utandazaji wa mabomba ya mradi wa maji safi na salama na ujenzi wa Maskani ya Fishamen,katika jimbo la Mjimkongwe..
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikabidhi piki piki kwa  mmoja wa makatibu wa CCM.
  Mmoja wa Mabalozi akifurahi mara baada ya kukabidhiwa baiskeli yake na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,kwa shughuli mbalimbali za kichama,baiskeli hizo ilikuwa ni ni moja ya ahadi alizoahidi kutoa Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni,Mh Masauni,ambapo pia alitoa piki piki kwa makatibu wa chama.

   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikabidhi bati kwa ajili ya ujenzi wa msikiti kwa mmoja wa wananchi kwenye uwanja wa Tawi la CCM Matarumbeta katika jimbo la Jang'ombe,ambapo Ndugu Kinana alikabidhi vifaa vya michezo kwa vijana,alikabidhi vifaa vya mradi wa maji safi,pia alikabidhi hati kwa kikundi cha vijana Jang'ombe.


  0 0


  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na kisha kuagana na Balozi wa Algeria nchini Tanzania, Mhe. Djelloul Tabel,  Ikulu jijini Dar es Salaam, Jumanne jioni January 13, 2014 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.PICHA NA IKULU

  0 0

  Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo kushoto akizungumza jambo na waandishi wa habari hawapo pichani katika uzinduzi wa huduma mpya ya Chagua chochote Bayport italipia jana jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Meneja Biashara, Thabit Mndeme.

  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
  TAASISI ya kifedha ya Bayport Financial Services, imezindua tena huduma mpya inayojulikana kama ‘Chagua chochote unachotaka Bayport italipia’, ikiwa na lengo la kuwapatia mikopo ya bidhaa mbalimbali wateja wao na Watanzania kwa ujumla.

  Huduma hiyo ni mwendelezo wa ile 'Mikopo ya Bidhaa' ambapo watu wanakopeshwa bodaboda, sambamba na Bima ya Elimu iliyozinduliwa pia mapema mwaka jana kwa ajili ya kuleta urahisi katika mfumo wa maisha ya Watanzania wengi.
   Ngula Cheyo anazungumza jambo na kulia kwake ni Thabit Mndeme.
  Akizungumza katika uzinduzi wa huduma hiyo mpya, Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, alisema huduma hiyo sasa itawapatia fursa wateja wao kukopeshwa magari, nyumba, vifaa vya ujenzi, pembejeo za kilimo, ada ya shule, pikipiki, bajaj, tv, injini ya boti na nyinginezo kwa ajili ya kuwapatia mwangaza mzuri wa kimaisha na kiuchumi.

  Alisema kuwa kuanzisha huduma hiyo mpya imetokana na ile ya mikopo ya bidhaa kufanya vizuri tangu ilipozinduliwa mwishoni mwa mwaka jana na kupatikana nchi nzima kwa kupitia matawi yaliyosambaa katika mikoa mbalimbali.
  Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme kulia akizungumza jambo katika uzinduzi wa huduma mpya ya 'Chagua chochote Bayport italipia', ikiwa ni mwendelezo wa huduma ya mikopo ya bidhaa, ambapo wateja wa Bayport wanapata fursa ya kukopeshwa bidhaa mbalimbali, kama vile nyumba, magari, vifaa vya ujenzi na nyinginezo.
  Picha zote na Mpiga Picha Wetu.

   “Bayport ilifanya mazungumzo na wateja wake mbalimbali baada ya kuzindua huduma ya Mikopo ya Bidhaa na kuona mafanikio makubwa waliyopata, hivyo mwaka huu tumeona tufike mbali zaidi kwa kuangalia namna gani Watanzania wanaweza kukopeshwa bidhaa nyingi kwa ajili ya kukuza uchumi wao.

  “Ni rahisi mno kupewa mkopo wa chagua chochote unachotaka Bayport italipia kwasababu anachotakiwa kufanya mteja ni kuchagua bidhaa anayoitaka katika duka au msambazaji yoyote aliye karibu naye, kisha atapewa fomu ya malipo na kuipeleka kwenye tawi la Bayport lililo karibu yake ili apate mkopo aliyohitaji,” alisema Mndeme.

  Alisema kuwa baada ya kuzinduliwa huduma hiyo ya Mikopo ya Bidhaa, wengi waliipenda na kunufaika nayo, hivyo aliwaomba wateja wao na Watanzania kwa ujumla kuendelea kuiunga mkono Bayport Financial Services kwa ajili ya kuwapatia maisha bora, maana ndiyo kusudio lao.

  Naye Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema kwamba taasisi yao inayojihusisha na mambo ya mikopo inatambua namna bora ya matokeo mbalimbali ya kuwaendeleza kiuchumi, hivyo huduma hizi ni mwendelezo wa juhudi za kukuza uchumi wa watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni zilizoidhinishwa.

  “Tunajivunia kufanya kazi kwa bidii na kupanua wigo wa huduma zetu kwa matawi 80 nchi nzima, jambo linalotupa shauku ya kuona nchi yetu inapiga hatua kiuchumi kwa kuwawezesha watumishi wa umma na kampuni zilizoidhinishwa na Bayport kwa kuwapatia mikopo waipendayo, huku pia tukiwaeleza kwamba tumehamia jengo jipya la Bayport House, Morocco kwa ajili ya kuwahudumia vizuri zaidi," alisema Cheyo.

  Aidha, Cheyo aliwashukuru wateja wao na Watanzania kwa ujumla kwa kuwaunga mkono miaka 9 tangu walipoanza kutoa huduma ya mikopo, huku akisema kuwa taasisi yao itaendelea kufanya kazi kwa moyo wote ili kuhakikisha kwamba pato la wananchi linakuwa kwa kuwakopesha ili wajikwamue kiuchumi.

  Bayport Financial Services ni taasisi ya isiyokuwa ya kibenki inayoongoza kutoa mikopo barani Afrika na Amerika ya Kusini, huku ikianzishwa mwaka 2001 na umiliki wake ukiwa nchini Mauriritius, ambapo pia kwa Tanzania ilianzishwa rasmi mwaka 2006, huku ikiwa na matawi 80 nchi nzima.

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Maputo usiku huu kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais Mpya wa Msumbiji Mhe.Filipe Nyusi kesho mjini Maputo. Mhe. Nyusi anachukua hatamu za uongozi kutoka kwa Rais Armando Emilio Jacinto  Guebuza anayemaliza muda wake.

  0 0

  MSANII mkongwe katika tasnia ya filamu Swahilihood Hashim Kambi ‘Ramsey’ ni moja kati ya wasanii wakubwa Bongo ambaye atawaongoza wasanii nyota na wakongwe katika filamu kubwa ya CPU inayotarajiwa kuingizwa katika Dvd baada ya kuonyeshwa katika majumba ya sinema ndani na nje ya Bongo.

  Filamu ya CPU ni kazi kubwa sana kutengenezwa na watayarishaji wa ndani na kushirikisha wasanii zaidi ya mia mbili ndio filamu kubwa yenye ubora wa kipekee awali ilionyeshwa katika ukumbi wa sinema Century Cinemax Mlimani City kwa siku kumi mfululizo na kuacha gumzo kwa wapenzi wa sinema.

  Kwa mara ya kwanza itauzwa katika Dvd ili kwa wale wapenzi wa filamu walioshindwa kuingia katika majumba ya sinema ilipoonyeshwa waweze kushuhudia teknolojia ya juu kutumika Bongo na kuwavutia wengi mtaani kwetu ambako ndio soko la filamu za kibongo lipo.

  CPU inawakutanisha wasanii nyota na wakongwe ka aKulwa Kikumba ‘Kulwa Kikumba ‘ Dude’, Richard Mshanga ‘Masinde’, Dotnata, na nyota wengine kibao ambao wanafanya vizuri katika tasnia ya filamu wakiongozwa na Hashim Kambi ‘Ramsey’ msanii aliyejijengea mashabiki wengi.

  0 0

   Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (wa pili kushoto) akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya Saudi Arabia Dk. Abdulrahman Al-Zamil (wa tatu kushoto) jijini Riyadh, Saudi Arabia. Wengine katika picha kutoka kulia ni Mshauri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Mamlaka ya Wanyamapori ya Saudia Mohammad Sulayem; Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Dk. Adelhelm Meru na Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Prof. Abdillah Omari.
   Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (kushoto) katika mazungumzo na Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya Saudi Arabia Dk. Abdulrahman Al-Zamil jijini Riyadh, Saudi Arabia.
   Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. James Lembeli (kushoto) akikaribishwa na Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya Saudia Dk. Abdulrahman Al-Zamil jijini  Riyadh, Saudi Arabia.
   Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii Mhe. Peter Msigwa (kushoto) akikaribishwa na Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya Saudia Dk. Abdulrahman Al-Zamil jijini Riyadh, Saudi Arabia. 
  Ujumbe wa Serikali ya Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (wa tano kushoto) ukiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya Saudia Dk. Abdulrahman Al- Zamil (wa sita kushoto) mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo baina ya pande mbili jijini Riyadh, Saudi Arabia. Wengine pichani kutoka kushoto ni pamoja na Mkurugenzi wa Wanyamapori Herman Keraryo; Mkurugenzi Mkuu TANAPA Allan Kijazi; Mhe James Lembeli; Mhe Peter Msigwa; Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Dk. Adelhelm Meru pamoja na maafisa kutoka Chemba ya Biashara ya  Saudia.                                                                                          

   Na Pascal Shelutete, TANAPA

  Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu amewakaribisha wafanyabiashara kutoka Saudi Arabia kuwekeza katika sekta ya utalii nchini ambayo ina fursa nyingi za uwekezaji. Nyalandu alitoa wito huo kufuatia mazungumzo yake na Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara ya Saudi Arabia Dk. Abdulrahman Al-Zamil yaliyofanyika Riyadh, Saudi Arabia jana.

  Waziri Nyalandu ambaye anaongoza ujumbe wa Wizara ya Maliasili na Utalii nchini Saudia alibainisha kuwa mazingira ya uwekezaji nchini yanavutia na kutaja maeneo hayo kuwa ni pamoja na ujenzi wa hoteli na loji za kisasa zitakazoweza kuvutia watalii wengi zaidi katika maeneo ya mijini pamoja na ndani ya maeneo ya uhifadhi.

  Alisema kuwa utalii wa Tanzania unakua kwa kasi nzuri kutokana jitihada zinazofanywa na serikali pamoja na wadau mbalimbali katika kutangaza vivutio vya utalii na kuwa juhudi hizo lazima ziende sambamba na upatikanaji wa huduma bora za malazi. “Upatikanaji wa huduma nzuri za malazi ya bei nafuu utasaidia kuvutia watalii wengi zaidi nchini na kwa maana hiyo tunawakaribisha kuja kuzitumia fursa zilizopo ili kuweza kukuza uchumi wa nchi yetu”, alisema Nyalandu.

  Waziri Nyalandu ambaye anaongoza ujumbe wa Wizara ya Maliasili na Utalii nchini Saudia, alisema kuwa Tanzania ni ya pili ulimwenguni baada ya Brazil kwa kuwa na vivutio vizuri vya asili vya utalii na kuwa rasilimali hizi zinapaswa sasa kutumiwa vema ili kuinua uchumi na njia pekee ni pamoja na kuvutia wawekezaji na mitaji kutoka Saudia ili kufikia azma hiyo.
  Kwa upande wake Dk. Al-Zamil aliahidi kuwashirikisha wafanyabiashara wenzake kutikia wito huo na kwa kuanzia timu ya wafanyabiashara pamoja na mawakala wa utalii watafika nchini katika siku chache zijazo ili kuona namna gani wataweza kuzitumia fursa zilizopo kikamilifu. Aidha, katika eneo la utalii Al- Zamil alisema kuwa Chemba yake itafanya kila liwezekanalo kubadilisha mtazamo wa Wasaudia wanaotembelea kwa wingi maeneo mbalimbali ya utalii duniani ili waweze kuitembelea Tanzania na kujionea vivutio mbalimbali vya utalii vinavyopatikana nchini.

  Aidha, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Adelhelm Meru alisema kuwa serikali itaandaa Kongamano Maalum la Uwekezaji nchini Saudi Arabia ili kuweza kutangaza fursa mbalimbali zzilizopo nchini ambazo zikitumika vema zinaweza kuinua uchumi wa taifa.

  Hivi sasa Tanzania inategemea idadi kubwa ya watalii kutoka Mataifa ya Ulaya na Amerika na kwamba japokuwa idadi ya watalii kutoka nchi za kiarabu haizidi 15,000 kwa mwaka, bado jitihada za utangazaji na uwekezaji zikifanywa vizuri idadi ya watalii kutoka mataifa ya kiarabu itaweza kuongezeka nchini.

  Ujumbe wa Tanzania unajumuisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Adelhelm Meru; Balozi wa Tanzania Saudi Arabia Prof. Abdillah Omari; Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. James Lembeli, Waziri kivuli wa Maliasili na Utalii Mhe. Mchingaji Peter Msigwa; Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Allan Kijazi pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Herman Keraryo.


  0 0

  IMG-20150114-WA0074
  Some men shirts and ladies outfit in her own design. The design collection is called WEAR SWAHILI. Her main goal is to promote our own fabric in a modern way and comfortable way. Any age can wear and still look stylish at an effective cost price.

  These are a few but also we uniforms in African Attire. Pillow case, Table mats and throws by order.
  Asanteni sana na Karibuni.

  The shop is located at Dar Free Market, Masaki 1st Floor, Shop No. 5 or Mobile no +255 784 670089
  IMG-20150114-WA0075IMG-20150114-WA0076IMG-20150114-WA0077

  0 0

  Neema Herbalist & Nutritional Foods Clinic ni wauzaji wa dawa mbalimbali za asili. Tunayo dawa nzuri ya asili inayo ondoa kitambi na kulifanya tumbo lako kuwa flat kabisa ndani ya siku kumi na nne.

  Dawa ni ya asili kabisa " Pure Herbal", haijachanganywa na kemikali yoyote na haina side effects kwa mtumiaji.

  BEI YAKE NI SHILINGI ELFU HAMSINI TU (Tsh 50,000/=)

  Kwa wasio weza kufika ofisini kwetu tunawapelekea dawa mahali walipo (DELIVERY).

  Kwa wateja wa mikoani, tunawatumia dawa kwa njia ya mabasi, kwa wateja waliopo Zanzibar tunawatumia dawa kwa njia ya meli na kwa wateja waliopo nje ya Tanzania, tunawatumia dawa kwa njia ya posta au DHL.

  Pia tunayo dawa bora kabisa ya nguvu za kiume iitwayo JIKO ambayo inatibu na kumaliza kabisa tatizo la nguvu za kiume ndani ya siku thelathini.

  Vile vile tunayo dawa ya asili inayosaidia kurudisha afya na mwili kwa mtu aliye dhoofika kwa magonjwa mbalimbali.

  Tunapatikana jijini DarEs salaam,katika eneo la Changanyikeni karibu na Chuo Cha Takwimu.

  Kufika ofisini kwetu, panda daladala za UBUNGO-CHANGANYIKENI kisha shuka kituo cha TAKWIMU halafu tembea hatua ishirini mbele kisha tazama upande wako wa kulia.

  Kwa maelezo zaidi,wasiliana nasi kwa simu 0766538384 na kwa taarifa zaidi kuhusu huduma zetu, tembelea website yetu kwa kubonyeza hapa.

  0 0

  Meneja Mkuu wa Tanzania House of Talent, Mwita Mwaikenda akizungumza kuhusiana na maadhimisho ya miaka kumi ya THT, kulia ni mwakilishi wa kampuni ya MOSAIC, Deo Masagati ambao ndio wadhamini wa shuguli hiyo, na kushoto ni mwanamziki Peter Msechu ambaye ndio mwongozaji wa burudani siku ya tamasha.
  Mbunifu wa Mavazi, Ally Remtullah akiongea na waandishi kuhusu uzinduzi wa mradi wa ubunifu na ushonaji unaonzishwa na THT. Kulia ni Peter Msechu, na kushoto ni Lameck Ditto.
  Lameck Ditto akiongea na waandishi juu ya maadhimisho ya miaka kumi ya THT
  Mkuu wa Masoko wa THT, Michael Nkya akiongea na waandishi wa habari juu ya maadhimisho ya miaka kumi ya THT.
  *Kufungua kampuni ya ushonaji na ubunifu wa mavazi
  Kituo cha kuzalisha na kukuza vipaji, Tanzania House of Talent, kinatarajia kuadhimisha miaka kumi toka kuanzishwa kwake hapo tarehe Januari 31, 2015 Escape 1 jijini Dar es Salaam.
  THT ilianzishwa mwishoni mwa mwaka 2005 kwa lengo la kuwasaidia vijana wenye vipaji, lakini wasio na uwezo wa kujiendeleza wenyewe, kwenye sekta ya sanaa hapa nchini, na toka wakati huo kituo kimekuwa na mafanikio makubwa na mchango wa pekee kwenye kukuza sanaa ya muziki nchini.
  Akizungumza wakati wa kuzindua maadhimisho hayo ambayo yatakuwa kwa mwaka mzima, Meneja Mkuu wa Kituo hicho, Mwita Mwaikenda alisema ni heshima kubwa kuweza kusherehekea miaka kumi toka imeanzishwa kwani wameweza kufanikisha mambo mengi makubwa.
  ‘Tulianzisha kituo hiki miaka kumi iliyopita kwa hakika tukiwa hatuna chochote zaidi ya imani yetu kwenye vipaji vya vijana, na tulianza hatuna hata sehemu ya maana, lakini leo miaka kumi baadaye vijana zaidi ya 3000 wamefaidika na kituo hiki kwa namna moja au nyingine na wameweza kumudu maisha yao na familia zao kutokea kuwa watoto wa mitaani’ alisema Mwita.
  THT ikiwa imeanzishwa kama kituo cha kusaidia watoto wa mtaani wenye vipaji, imeweza kukua kwa kipindi cha miaka kumi, na sasa sio tu inazalisha na kukuza vipaji bali imekuwa ikitoa huduma zote kuanzia kuratibu matamasha, kuandaa mpangilio wa burudani, kutengeneza matangazo ya radio na televisheni pamoja na makala na vipindi vya televisheni.
  ‘THT imeweza kuratibu burudani ya matamasha mbalimbali kama FIESTA, Mkutano wa Smart Partnership, Sensa ya mwaka 2013, Sherehe za miaka 50 ya Muungano pamoja na mikutano na matamasha kadha wa kadha’ alisema Meneja Masoko wa THT, Michael Nkya.
  THT imeendelea kukua kwa kuweza kuanzisha studio yake ambayo imeweza kurekodi matangazo, nyimbo za wasanii wote wa THT pamoja na wengine wengi kama Mdogomdogo na Number One Remix ya Diamond, Me and You ya Ommy Dimpoz, Prokoto ya Victoria Kimani na nyingine nyingi.Kwa sasa THT inatengeneza vipindi mbalimbali vya televisheni kama 69 Records, na vingine vingi vinavyorushwa chaneli za nje huku pia ikijivunia kuwa na maktaba ya nyimbo kubwa zaidi nchini.
  ‘Shukrani zetu za dhati kwa kweli ni kwa serikali, hasa hasa Mheshimiwa Rais Kikwete, ambaye toka mwanzo alikubali wazo na akaamini mziki unahitaji elimu ya peke yake, lakini pia makampuni mbalimbali ambayo wamekuwa wakitupa kazi pamoja na vyombo vyote vya habari kwa kutuunga mkono siku zote’ alisema Bwana Nkya.
  Akielezea kuhusu mwelekeo wa kituo baada ya miaka kumi, Mwita alisema anaamini kituo kimefanya kazi yake tayari kwa kuweza kuchagiza sanaa ya muziki nchini, na sasa ni wakati wa kuendelea kusaidia wadau au vituo vingine kama Mkubwa na Wanawe kufika THT ilipofika.
  ‘Kimsingi mwaka huu ndio mwaka wa mwisho kuendela kupokea wanafunzi wapya wa kuimba, na mpango wetu ni kuendelea kukuza kituo kwa kuanzisha kampuni ya ushonaji na ubunifu wa nguo kwa kutumia kitenge ambao tunaamini utatoa ajira kwa vijana wengi zaidi hapa nchini’ alisisitiza Mwita.
  Kampuni ya ubunifu na ushonaji kwa kutumia vitenge, tayari ishaanza mchakato wake kwa kuhusisha wadau wa biashara ya vitenge, na mbunifu mahiri Ally Remtullah, mwanamitindo Flaviana Matata wakiwa ndio walezi na wasimamizi wa mradi ambao utaanza na wabunifu wanaochipukia Neyonce pamoja na Adam Mchovu.
  ‘Kwa kuanza mradi utapeleka wabunifu nchini China ili wakajifunze zaidi juu ya ubunifu na kuongeza ubora kwenye kazi zao, wakirudi tunaamini wataweza kuwafundisha vijana wengi zaidi, na kutimiza lengo letu la kuwasaidia vijana kujiajiri’ alimaliza Mwita.

  0 0

  NAFASI  ZA  MAFUNZO   YA  UTENGENEZAJI  WA  MASHINE  ZA   KUTOTOLEA  VIFARANGA  WA  KUKU.

  Taasisi  ya  RafikiElimu  FOUNDATION,  kupitia  MRADI  WA  ELIMU  YA  UJASIRIAMALI  MIJINI  NA  VIJIJINJI , inatangaza  nafasi  za   MAFUNZO  YA  UTENGENEZAJI  WA  MASHINE  ZA  KUTOTOLEA  VIFARANGA  WA  KUKU.  ( Incubators )


  Mashine   zitakazo fundishwa  kutengeneza  ni  INCUBATOR   ( MANUAL & AUTOMATIC) ZENYE  UWEZO  WA  KUTUNZA  JOTO  KWA  SAA  48 PAMOJA  NA  KUTOTORESHA  MAYAI   KUANZIA  240  HADI  5000.


  ADA   YA   MAFUNZO   :

  Ada  ya  mafunzo  haya  ni  SHILINGI  ELFU  HAMSINI  TU. (Tshs.50,000/=)

  TAREHE  YA  KUANZA  KWA  MAFUNZO

  Mafunzo  haya  yatafanyika  kwa  muda   wa  siku  tano  kuanzia   tarehe  02  FEBRUARY  2015  hadi  tarehe  06  FEBRUARY   2015.

  MAHALI  YATAKAPO  FANYIKA  MAFUNZO  :
  Mafunzo  haya  yatafanyika  katika  madarasa  yetu  yaliyopo  katika  eneo  la  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING  nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA.

  FOMU   ZA   KUJIUNGA   NA   MAFUNZO :

  Fomu  za  kujiunga  na  mafunzo  haya  zinapatikana  ofisini  kwetu  kwa  gharama  ya  SHILINGI  ELFU  KUMI  NA  TANO  TU  ( Tshs.15,000/=).

  MWISHO   WA  KUCHUKUA  FOMU  :

  Mwisho  wa  kuchukua  fomu  ni  tarehe   31  JANUARY  2015   saa  nane  kamili  mchana.

  MAHALI  ZILIPO  OFISI  ZETU :
  Ofisi  zetu  zinapatikana  katika  eneo  la  CHANGANYIKENI karibu  na  CHUO  CHA  TAKWIMU mbele  ya  CHUO  KIKUU  CHA  DAR  ES  SALAAM  (MLIMANI )

  JINSI   YA   KUFIKA   OFISINI   KWETU:

  Kufika  ofisini  kwetu, panda  daladala za  UBUNGO- CHANGANYIKENI  kisha  shuka  kituo  cha  TAKWIMU  halafu  tembea  hatua  ishirini  mbele  kisha  tazama  upande  wako  wa  kulia utaona  ofisi  imeandikwa   RAEFO  TANZANIA.

  Kwa  maelezo  zaidi wasiliana  nasi  kwa  simu  0688 049 687

  Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  mafunzo  ya  utengenezaji  wa  mashine  za  kutotolea  vifaranga, tembelea :

  0 0

  Afisa Maendeleo ya Vijana Wilaya ya Chamwino Bw. Denis Vagela (kushoto) akizungumza na Vijana wa kikundi cha Wajasiriamali wa Wilaya ya Chamwino wanaojishughulisha na utengenezaji wa Sabuni za maji, Batiki na ufundi walipotembelewa kwa ajili ya kuangalia mradi wao leo Mkoani Dodoma. Katikati ni Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa, na aliyekaa ni Afisa Vijana Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga.
  Wakwanza mbele ni Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa akiangalia mashine ya kukamua alizeti iliyotengenezwa na Vijana wa kikundi cha Chachu ya Maendeleo Dodoma wakati wa kutembelea miradi ya vijana wa Mkoa wa Dodoma. Kulia ni kijana wa kikundi hicho Bw. Ayoub Athumani.
  Kijana Samwel Nagija kutoka kikundi cha vijana cha Chachu ya Maendeleo Dodoma kinachojishughulisha na utengenezaji wa mashine za kusaga na kukoboa, mashine za kutengeneza matofali, mashine za kukamua alizeti, na ujenzi wa vitanda na madawati ya chuma akiendelea na ujenzi wa mashine ya kusaga leo Mkoani Dodoma.
  Mwenyekiti wa kikundi cha vijana cha Iringa Promise Keepers Bw. Rashid Magule (kushoto) kinachojishughulisha na ufundi Selemala akielezea namna kikundi chake kilivyofaidika na mkopo unaotolewa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana. Wanaomsikiliza kutoka kulia ni Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa, anayefuata ni Afisa Maendeleo ya Vijana Bi. Amina Sanga na wapili kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw.Laurean Masele. (Picha na Genofeva Matemu – Maelezo, Dodoma)

  Na Genofeva Matemu

  Vijana kutoka kikundi cha Iringa Promise Keepers chenye wanachama 6 wanaojishughulisha na ufundi Selemala wameishukuru Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana unaosimamiwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuwapatia mkopo wa shilingi laki tatu mwaka 2007 ambao umeinua na kusababisha mradi wa kikundi kupanuka na kuwa mkubwa.

  Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa kikundi hicho Bw. Rashid Magule walipotembelewa na wawezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo pamoja na maafisa kutoka ofisi ya Mkoa wa Dodoma kukagua miradi ya vijana leo Mkoani Dodoma.

  “Kikundi cha Iringa Promise Keepers kinaishukuru Serikali kwa kutufaidisha na mkopo wa shilingi laki tatu kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Vijana tuliopatiwa mwaka 2007 ambao ulikua kama mtaji katika kikundi chetu hivyo kupanuka na kuwa na mtaji wa shilingi milioni nne unaotuwezesha wanakikundi kupata kipato cha kuweza kuendesha maisha yetu” alisema Bw.   Magule.

  Hata hivyo Bw. Magule ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuendelea kukipatia mkopo kikundi chake kwani bado wanakikundi wanahitaji kujiendeleza zaidi na kuwaendelezo vijana wenzao wanaohitaji utaalamu kutoka kwao hivyo kuomba kupatiwa mkopo wa shilingi milioni mbili kwa ajili ya maendeleo ya kikundi hicho.

  Kwa upande wake Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya kilichopo chini ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Laurean Masele amewapongeza wanakikundi kwa jitihada kubwa walizozifanya na kuweza kutumia mpoko mdogo waliopata kusimamia na kuendeleza mradi wao kwa kushirikiana.

  Bw. Masele amewashauri wanakikundi kufanya kazi kwa ushirikiano huo huo huku wakisimamia malengo waliyokusudia kwa kutumia ujuzi walionao kwani vijana wakiwezeshwa wanaweza.

  Naye Afisa Maendeleo ya Vijana Mkoa wa Dodoma Bw. Tumsifu Mwasamale amewapongeza wanakikundi wa Iringa Promise Keepers kwa maendeleo waliyonayo na kuwataka kutafuta eneo lao binafsi kwa ajili ya shughuli zao kwani mradi wao unahitaji nafasi kubwa na ya wazi itakayosaidia kuonyesha bidhaa wanazozalisha katika jamii.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais -Mazingira Injinia Binilith Satano Mahenge (aliyetangulia) akitembelea Kiwanda cha East Coast Oils and Fats kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Injinia Binilith Satano Mahenge (katikati) akionyeshwa ramani ya sehemu ambayo mikoko imekatwa na Baadhi ya wananchi ili kupisha Ujenzi ambao si halali katika fukwe za Bahari ya Hindi eneo la Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam. Anayemwonyesha ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Malechela Silas Malipula.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais -Mazingira Injinia Binilith Satano Mahenge (wa tatu kushoto) akitoa Maagizo ya kusitisha kwa matumizi ya magogo katika Kiwanda cha East Coast Oils and Fats, ambapo magogo hayo huyatumia katika shughuli za uzalishaji wa bidhaa mbalimbali kiwandani hapo.Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji Bw. Vijay Raghavan.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Injinia Binilith Satano Mahenge (katikati) akionyesha Bango linalokataza Ujenzi wa pembezoni mwa ufukwe likiwa limeondolewa na mmoja wa wamiliki wa nyumba za Ufukweni ili kupisha ujenzi wa nyumba yake uendelee.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Injiania Binilith Mahenge awapa miezi sita kiwanda cha East coast oil and edible kinachozalisha vipodozi na mafuta ya kupikia kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam kusimamisha uzalishaji wake unaoendeshwa kwa kutumia nishati ya magogo .

  Akiwa katika mwendelezo wa ziara zake za ukaguzi mazingira Mh. Mahenge alimtaka Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda hicho Bwana Vijay Raghavan kutumia nishati mbadala kama gesi katika uendeshaji wa mitambo ya uzalishaji wake.

  Katika ziara hiyo Mh. Mahenge alibaini kuwa tani 50 za magogo huteketezwa kila siku kiwandani hapo kwa ajili ya uendeshaji wa mashine za uzalishaji jambo ambalo huhatarisha mazingira ikiwemo Mabadiliko Tabianchi.

  Hata hivyo alikitaka kiwanda hicho kuboresha mfumo wake wa maji taka yanayotiririshwa kuelekea baharini kwa kuyatibu ili kuondoa sumu inayowaathiri viumbe hai washio baharini pamoja na watu wanaotumia samaki hao kama vitoweo.

  Wakati huo huo Mh. Mahenge alitembelea pia fukwe za Mbezi mtaa wa Malecela kuitikia wito wa malalamiko ya wananchi khusu uvamizi wa eneo la Ufukwe huo, ambapo alithibitisha kuwepo kwa uvamizi wa eneo hilo.

  Akizungumza na mwenyekiti wa mtaa huo Bwana SIlas Malipula Mh. Mahenge alisema kuwa uendeshaji wa shughuli za maendeleo uliofanyika na unaoendelea ndani ya mita 60 kutoka eneo la hifadhi ya mikoko ni kosa kisheria hivyo Wizara yake imelipokea na italifanyia kazi .

  Mheshimiwa Mahenge aliongeza kuwa swala la utunzaji wa Mazingira ni letu sote hivyo kila Mwananchi anatakiwa kuwa makini ili kuzuia uharibifu unaoendelea katika maeneo mbalimbali nchini.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Bariadi Bw. Erasto Sima akisoma Hotuba katika makabidhiano ya msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi kwa shule ya sekondari Bariadi uliotolewa na kampuni ya Airtel Tanzania.
  Mkuu wa shule ya sekondari ya Bariadi Bw. Pawa Lutema akipokea msaada wa vitabu vya sayansi kutoka kwa mkuu wa wilaya Bariadi, Vitabu hivyo vyote vinathamani ya sh milioni 6 na ni vya masomo ya sayansi kutoka kampuni ya simu ya Airtel kupitia mradi wake wa kusaidia elimu wa Airtel Shule yetu.
  Meneja wa Airtel Simiyu Bw. Ezekiel Nungwi akikabidhi msaada wa vitabu vya sayansi vyenye thamani ya milioni 6 kwa Mkuu wa wilaya ya Bariadi Bw. Erasto Sima, vitabu hivyo ni sehemu ya msaada wa Airtel kupitia mradi wake wa Airtel shule yetu.


  0 0


  0 0

    Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Halima Maulid Salum na Mshauri Muandamizi wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Bi. Kelly Hamblin wakisaini makabidhiano ya pikipiki 10 kwa ajili ya ufuatiliaji uwepo wa dawa katika vituoni vya afya Wilaya. Hafla hiyo imefanyaka Bohari Kuu la Dawa Maruhubi Mjini Zanzibar.
   Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Halima na Mshauri Muandamizi wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Bi. Kelly wakibadilishana hati ya makabidhiano.
    Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akikabidhiwa funguo ya pikipiki na Bi. Kelly Hamblin (kusho) Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bi. Halima Maulid.
  Baadhi ya Pikipiki zilizo kabidhiwa. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi na wanachama wa chama hicho,waliofika kwa wingi katika mkutano wa hadhara,wakati Ndugu Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake katika jimbo la Mpendae,wilaya ya Amani mkoa wa Mjini Magharibi.Ndugu Kinana kabla ya kuhitimisha ziara hiyo alishiriki kazi za kijamii na kukagua miradi mbalimbali ya chama.
  katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wananchi na wanachama wa chama hicho,waliofika kwa wingi katika mkutano wa hadhara,wakati Ndugu Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake katika jimbo la Mpendae,wilaya ya Amani mkoa wa Mjini Magharibi.Nape pia aliipongeza kazi nzuri inayofanywa na Dkt shein ya kuimarisha chama,amewataka viongozi mbalimbali wa chama hicho kuiga mfano wake,pia amewataka viongozi wa chama hicho kuacha kuwa na majivuno badala yake watoke na kukutana na wananchi kuwasikiliza na kuwatatulia matatizo yao kwa namna moja ama nyingine.
   Baadhi ya Wanahabari wakiwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa Binti Amran Mpendae,wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake katika Wilaya ya Amani,Jimbo la Mpendae mkoa wa Mjini Magharibi.
  Sehemu ya umati wa Wakazi wa wilaya ya Mpendae na wanachama wa CCM wa jimbo la Mpendae,wilaya ya Amani,Mkoa wa Mjini Magharibi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa Binti Amran Mpendae,wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake katika Wilaya ya Amani,mkoa wa Mjini Magharibi.
   Mkutano ukiendelea katika uwanja wa Binti Amrani Mpendae,Wilaya ya Amani mkoa wa Mjini Magharibi jioni ya leo.


   Sehemu ya Meza Kuu.
   Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar,Vuai Ali Vuai akisoma baadhi ya vifungu vilivyomo kwenye katika inayopendekezwa mbele ya wananchi (hawapo pichani) katika mkutano wa hadhara,uliofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa Binti Amrani Mpendae,Wilaya ya Amani,mkoa wa Mjini Magharibi.
   Sehemu ya umati wa Wakazi wa wilaya ya Mpendae katika jimbo la Mpendae,wilaya ya Amani,Mkoa wa Mjini Magharibi wakifautilia yaliyokuwa yakijiri katika mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa Binti Amran Mpendae,wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake katika Wilaya ya Amani,Jimbo la Mpendae mkoa wa Mjini Magharibi.
   katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwalisha kiapo baadhi ya wanachama wapya walijiunga na chama hicho sambamba na kukabidhiwa kadi za uanachama.
   Sehemu ya viongozi mbalimbali wa chama cha CCM wakishangilia jambo katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika leo kwenye uwanja wa Binti Amrani Mpendae,wilaya ya Amani mkoa wa Mjini Magharibi.
   Wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo wa hadhara.

  0 0

   Naibu waziri wa maliasili na utalii MAHAMUOD MGIMWA ambaye ni mbunge wa jimbo la mufindi kusini akiwa katika moja ya ziara zake za wizara ya maliasili na utalii
    Naibu waziri wa maliasili na utalii MAHAMUOD MGIMWA ambaye ni mbunge wa jimbo la mufindi kusini akiwa katika moja ya ziara zake za wizara ya maliasili na utalii na wengine ni viongozi wa TANAPA
  Naibu waziri wa maliasili na utalii MAHAMUOD MGIMWA ambaye ni mbunge wa jimbo la mufindi kusini akiwa ziarani 
  Naibu waziri wa maliasili na utalii MAHAMUOD MGIMWA ambaye ni mbunge wa jimbo la mufindi kusini akiwa na mkuu wa wilaya ya mufindi

  na fredy mgunda ,iringa

  Naibu waziri wa maliasili na utalii MAHAMUOD MGIMWA ambaye ni mbunge wa jimbo la mufindi kusini amewataka vijana kujituma na kutumia fursa mbalimbali ambazo zinatolewa na serikali.

  Akizungumza na mtandao huu Naibu waziri wa maliasili na utalii MAHAMUOD MGIMWA alisema kuwa vijana wengi wamekuwa wakibweteka kwa kutojituma kufanya kazi na kuendelea kuilaumu serikali.

  “Eti asubuhi unawakuta vijana wamekaa kwenye vijiwe wakizungumza siasa na kucheza mabao wakati hawajui mchana watakula wapi na jioni watarudi na nini nyumbani”alisema MAHMOUD MGIMWA

  MGIMWA ameendelea kuwaomba vijana wengi wenye fursa ya kurudi au kuingia shuleni upya warudi kwa kuwa dunia ya sasa inataka wasomi wengi kutokana na mabadiliko ya kiuchumi na sayansi na teknolojia na ndio sababu inayopelekea hata watu wazima kurudi shuleni.

  “Vijana mnatakiwakujifunza kutoka kwa watu wazima ambavyo wamekuwa wakijituma kufanya kazi kwa bidii na kujituma ilimradi kuwatengenezea watoto maisha mazuri pamoja na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla”alisema MAHMUOD MGIMWA

  Lakini Naibu waziri wa maliasili na utalii MAHAMOUD MGIMWA ambaye ni mbunge wa jimbo la mufindi kusini  amewataka wakinamama kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi mwaka huu.

  MGIMWA ameeleza kuwa wanawake waondoe hofu ya kugombea hasa kukiwa na ushindani wa wagombea wanaume kwa kuogopa kuchafuliwa kwa mambo yasiyokuwepo.

  Ameendelea kusema kuwa wananchi wasishawishiwe na propaganda za wanasiasa na badala yake wachague viongozi bora wenye uwezo wa kuongoza kutoka katika chama chochote.

  Aidha ameongeza kuwa viongozi wawe na sera za kutekelezeka ili kuwatendea haki wapiga kura wao hali itakayowafanya waaminike katika jamii.

  Mbali na hayo MGIMWA amewakumbusha vijana kutokubali kutumiwa na baadhi ya wanasiasa katika kuleta vurugu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu na badala yake wachague kiongozi mwenye weredi na sifa za kuwa kiongozi kutokana na sera za chama chake.

  Ameendelea kusema kuwa vijana wajitokeze kwa wingi katika kupiga kura ndiyo katika katiba iliyopendekezwa ili kuweza kufanya uchaguzi ulio wa haki na amani pia kujitokeza katika kujiandikisha katika daftari la wapiga kura pamoja na kupiga kura.

  Amemaliza kwa kuwataka wananchi wa jimbo la mufindi kusini kuwa na imani nae kwa kuwa amefanya yote ambayo aliwaahidi katika uchaguzi wa mwaka wa 2010 na amewaomba waendelee kuwa na imani naye katika kutekeleza mambo mapya ambayo wamejitokeza kwa lengo la kuleta maendeleo ya jimbo hilo.

  0 0

  Na Happiness Katabazi (UB)

  MAKAMU wa Rais  ,Dk.Mohammed Gharib Bilal Kesho anatarajiwa Kuwa mgeni rasmi katika sherehe za uwekwaji wa jiwe la Msingi la Chuo Kikuu  Cha Bagamoyo(UB), zitakazofanyika Jumamosi Januari 17 katika Kijiji cha  Kiromo, Bagamoyo Mkoani Pwani.


  Akizungumza na waandishi wa Habari  ofisini kwake Mikocheni Dar es Salaam, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho anayeshughulikia Fedha na Utawala, Dk.Elifuraha Mtalo  alisema  sherehe hizo zitafanyika Katika Kijiji cha Kiromo    na kwamba uwekwaji wa jiwe hilo ni ufunguzi rasmi wa ujenzi wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo Katika Kijiji hicho ambao unatarajiwa  kuanza Mwaka huu.


  Dk.Mtalo   alisema Dk.Bilal  ndiye atakuwa mgeni rasmi pia na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa naye anatarajiwa kuwa miongoni mwa wageni walioalikwa katika sherehe hiyo ya kihistoria katika Wilaya ya Bagamoyo kwasababu Somo la Historia linatufundisha kuwa  mji wa Bagamoyo watumwa walikuwa wakiishi.


  "  UB tunaifahamu historia ya Mji wa Bagamoyo ndiyo maana tukaamua kuanzisha Chuo Kikuu ambacho tumekipa jina la University of Bagamoyo.Kupitia   Mji wa Bagamoyo tulikuwa watumwa, hivyo kupitia   UB ambayo inajenga makazi yake ya kudumu   katika mji huo, binadamu wote watakuwa  huru kwasababu tutapata elimu" alisema Dk.Mtalo.


  Alisema UB ambayo ilianzishwa rasmi mwaka 2011 ambayo ina makazi yake yake ya muda ,Mikocheni  B, Dar es Salaam  na kwamba ujenzi wa Makazi ya kudumu ya UB kijijini Kilomo , utasaidia kukuza shughuli za uchumi, wananchi wa eneo hilo kupata huduma ya elimu ya ngazi ya Chuo Kikuu kwa ukaribu na ajira.

  Aidha aliwaomba wananchi Wilaya Bagamoyo na Mkoa wa Pwani kwa ujumla kujitokeza kwa Wingi Katika sherehe hiyo

  0 0

  Ofisa Habari Umoja wa Mataifa (UN), Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungumza na washiriki wa Uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini 2015, iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Ofisa Habari Umoja wa Mataifa (UN), Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungumza na washiriki wa Uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini 2015, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wananchi waslioshiriki katika Uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini 2015, iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wananchi waslioshiriki katika Uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini 2015, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali walioshirii atika Uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini 2015, iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali walioshirii atika Uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini 2015, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali wakiwakatika maumbo ya kuunda neno '2015' kuashiria uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini 2015, iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali wakiwakatika maumbo ya kuunda neno '2015' kuashiria uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini 2015, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali wakiwakatika maumbo ya kuunda neno '2015' kuashiria uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini 2015, iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali wakiwakatika maumbo ya kuunda neno '2015' kuashiria uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini 2015, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali wakiwakatika maumbo ya kuunda neno '2015' kuashiria uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini 2015, iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali wakiwakatika maumbo ya kuunda neno '2015' kuashiria uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini 2015, iliyofanyika jijini Dar es SalaamBaadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali wakiwakatika maumbo ya kuunda neno '2015' kuashiria uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini 2015, iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali wakiwakatika maumbo ya kuunda neno '2015' kuashiria uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini 2015, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

   Na Mwandishi Wetu OFISA Habari Umoja wa Mataifa (UN), Bi. Usia Nkhoma Ledama amesema bado lengo la kupunguza kiwango cha umasiki lililokuwa katika malengo ya milenia yaliyomalizika mwakani litaendelea kuwa changamoto kwa nchi mbalimbali kutokana na hali ya utekelezaji wake. Bi. Nkhoma ametoa ufafanuzi huo Uwanja wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam katika Uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini 2015 zilizozinduliwa leo Dar es Salaam. 

  Alisema jitihada zinafanyika na nchi mbalimbali zipo katika viwango tofauti katika kulitimiza lengo hilo. "...Kwanza lazima tukubali kuwa ni lengo ambalo linachangamoto kubwa kiutekelezaji karibia nchi nyingi, hivyo litaendelea kupewa uhimizaji kiutelekezaji hata katika malengo yajayo," alisema Bi. Nkhoma. Hata hivyo akizungumzia suala la kupunguza maambukizi ya Ukimwi alisema bado ni lengo ambalo linachangamoto kubwa licha ya kwamba maambukizi mapya bado yapo lakini nguvu kubwa imewekwa katika kupunguza hayo maambukizi mapya.

   "...Tupunguze maambukizi mapya na tusiwe tena na watu wanaoendelea kufa kutokana na maambukizi ya Ukimwi...hili bado ni lengo ambalo linaendelea kufanyiwa kazi kwa nguvu kubwa pia linahitaji msukumo na jitihada za mtu mmoja mmoja, lakini pia kama nchi, kama taifa na jumuiya za kimataifa katika kupambana nalo," alisema. 

  Alisema lengo la kupunguza vifo vya watoto wachanga na wajawazito bado ni lengo lenye changamoto, hii ni kutokana na suala hili utekelezaji wake unahitaji rasilimali ya kutosha kuhakiisha tuna hospitali, vituo vya afya na klinii za kutosha kuhakikisha tuna sehemu za kutolea huduma kwa akina mama na watoto. Hospitali zetu kuwa na vifaa na wahudumu wa afya waliosomea na kubobea kwenye huduma hizo. 

   "Bado kuna changamoto lakini tutatumia changamoto zilizokuwa katika utekelezaji kwa miaka iliyopita kutatua changamoto za sasa kimaboresho zaidi. Kupunguza umasikini sio suala la sera bali ushiriki wa wananchi mmoja mmoja oale alipo, pia hili ni suala mtambuka kutokana na kutegemeana na sekta nyingine. 

  Mfano mkulima hawezi kupunguza umasikini kama hana pembejeo, kama hana miundombinu imara ya kusafirisha mazao yake kutoka shambani hadi sokoni na pia kupata soko la uhakika anapoingiza mazao yake sokoni." Alisema ili kupambana na hili inabidi kujengwa mazingira kuhakikisha kila mmoja anashiriki kupambana na malengo hayo, mfano fursa za ajira na fursa za kujiajiri haiwezekani kila mtu kuajiriwa so inabidi kuandaliwa wengine kujiajiri wenyewe. 

  "...Sio lazima kila mtu aajiriwe kila mtu anakipaji chake katika uzalishaji kinaweza kutumika kwa kuendelezwa na kujikuta anafanya vizuri," alisema. Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini 2015 zimezinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam na kushiriisha makundi mbalimbali, wazee, vijana, wanafunzi wa Msingi na Sekondari, watu wenye ulemavu na makundi mengine husika. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

  0 0

  Rais Mpya wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi akila kiapo cha urais kuiongoza nchi ya Msumbiji jijini Maputo Msumbiji leo.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Rais Mpya wa Msumbiji Filipe Jacinto Nyusi muda mfupi baada ya kuapishwa jijini Maputo Msumbiji leo.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Rais Mpya wa Msumbiji Filipe Jacinto Nyusi pamoja na Rais wa Msumbiji aliyemaliza muda wake Armando Emilio Guebuza katika viwanja vya ikulu ya Maputo baada ya sherehe za kuapisha leo.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zambia Kenneth Kaunda wakati wa kuapishwa kwa Rais mpya wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi jijini Maputo Msumbiji leo.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia jambo na Mfalme Letsie III wa Lesotho(Kushoto), Rais Hifikepunye Pohamba wa Namibia(wapili kushoto) na kulia ni mke wa Rais Mama Salma Kikwete.Viongozi hao walihudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mpya wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi zilizofanyika jijini Maputo Msumbiji (picha na Freddy Maro).

older | 1 | .... | 441 | 442 | (Page 443) | 444 | 445 | .... | 1897 | newer