Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46193 articles
Browse latest View live

DKT. KIGODA AZINDUA BODI YA UONGOZI YA CHUO CHA CBE LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

0
0
 Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Abdallah Kigoda akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Chuo cha CBE na menejimenti ya chuo hicho kabla ya kuzindua rasmi Bodi mpya ya uongozi ya chuo hicho leo.
 Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Abdallah Kigoda (kulia) akimkabidhi mwongozo wa utendaji kazi Mwenyekiti wa Bodi iliyoteuliwa ya uongozi wa Chuo cha Elimu ya Biashara, Prof. Mathew Luhanga (kushoto) leo jijini Dar es salaam.
 Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Abdallah Kigoda (katikati) akizungumza jambo na viongozi na wajumbe wa Bodi mpya ya uongozi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) iliyoteuliwa alipokuwa akitembelea maeneo mbalimbali ya chuo hicho leo jijini Dar es salaam. Kutoka kushoto ni Mkuu wa chuo hicho Prof. Emanuel Mjema akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi Prof. Eleuther Mwageni na Prof. Mathew Luhanga ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi ya CBE (kulia).
 Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Emanuel Mjema (kushoto) akimwonesha Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Abdallah Kigoda baadhi ya maeneo ya chuo yaliyokuwa yamevamiwa na watu na kujengwa majengo yakiwa wazi baada ya kubomolewa kufuatia uongozi wa chuo hicho kuendelea na juhudi za kuyarudisha maeneo yote yaliyokaliwa kinyume cha sheria chini ya umiliki wa chuo.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Abdallah (katikati)Kigoda akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Uongozi wa Chuo cha CBE na Menejimenti ya CBE leo jijini Dar es salaam. 

 Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Abdallah Kigoda akisalimiana na viongozi na wafanyakazi wa Chuo cha Elimu ya Biashara kampasi ya Dar es salaam alipowasili chuoni hapo kuzindua Bodi mpya ya uongozi ya Chuo hicho leo.Picha na Aron Msigwa- MAELEZO.

DKT. KIGODA AZINDUA BODI YA UONGOZI YA CHUO CHA CBE LEO JIJINI DAR ES SALAAM.
Na.Aron Msigwa –MAELEZO.
13/1/2015. Dar es salaam.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Abdallah Kigoda amezindua rasmi Bodi ya Uongozi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na kuitaka bodi hiyo kufanya kazi zake kwa kuzingatia sheria na kushirikiana na menejimenti ya chuo hicho kuweka mikakati na mipango ya maendeleo itakayokiwezesha chuo hicho kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.

Akizungumza na viongozi na wajumbe wa bodi hiyo leo jijini Dar es salaam, Dkt. Kigoda amesema  serikali inayo imani kubwa  na Mwenyekiti na wajumbe wa Bodi hiyo walioteuliwa na kwamba  watatimiza majukumu yao kikamilifu na kukiwezesha chuo hicho kufikia malengo na matarajio ya  watanzania ya kuendelea kuzalisha wataalam  bora wa fani za biashara.

“Ninaamini kuwa Bodi niliyoizindua leo itasimamia shughuli za chuo hiki kwa kufuata misingi ya uadilifu,utawala bora na kuongeza chachu ya kuleta huduma bora kwa wananchuo na umma” Amesisitiza Dkt. Kigoda.

Amesema viongozi na wajumbe wa Bodi walioteuliwa wanalojukumu la kusimamia ustawi wa chuo hicho wakiwa chombo cha juu cha utoaji wa maamuzi  na usimamizi wa masuala mbalimbali  ya chuo hicho ikiwemo uidhinishaji wa matumizi ya chuo yanayoendana na mapato ya chuo, uteuzi wa Mkuu wa Chuo na watumishi wengine na uidhinishaji wa viwango vya ada.

Akizungumzia mabadiliko ya  chuo hicho toka kuanzishwa kwake mwaka 1965 Dkt. Kigoda  amesema yamehusisha  mabadiliko makubwa ya mitaala ya kufundishia ili kuwafanya wanafunzi na wahitimu waweze kupanua ufahamu wao kwa kuwa na uwezo wa kukabiliana na ushindani wa soko la ajira kwa  kuongeza fursa za ajira katika  sekta ya umma na binafsi pamoja kuwajengea uwezo wahitimu waweze kujiajiri wenyewe.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo  hicho Prof. Emanuel Mjema akizungumza wakati wa kuwakaribisha wajumbe walioteuliwa  chuo hapo amesema  kuwa wao kama viongozi wa chuo hicho wataendelea kusimamia  msingi wa kuanzishwa kwa chuo  wa  kuendelea kuzalisha wataalam bora katika nyanja za biashara na sekta ya uendeshaji viwanda nchini.

Amesema kuwa wao kama menejimenti ya chuo hicho watashirikiana na uongozi na wajumbe wa bodi iliyoteuliwa kusimamia rasilimali na miundombinu ya chuo hicho ili kiendelee kutoa huduma bora kwa wanafunzi na wananchi wengi Zaidi kwa wakati.

Naye Makamu mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi ya Chuo hicho Prof. Eleuther Mwageni akizungumza kwa niaba ya uongozi na wajumbe wa bodi iliyoteuliwa amesema kuwa  Bodi iliyoteuliwa  itatekeleza majukumu  yote yaliyoanishwa kwa mujibu wa sheria.

TANZANIA YASHIRIKI KATIKA MKUTANO WA KUMI WA MAENDELEO YA TAKWIMU AFRIKA NCHINI UGANDA.

0
0
 Waziri Mkuu wa Uganda Mhe. Ruhakana Rugunda akiwahutubia washiriki mbalimbali kutoka barani Afrika (hawapo pichani) wakati wa Mkutano wa Kumi wa Maendeleo ya Takwimu Afrika uliofanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Speke Munyoyo Kampala, Uganda. 
 Washiriki kutoka Tanzania wakisikiliza kwa makini mambo yanayoendelea katika Mkutano wa Kumi wa Maendeleo ya Takwimu Afrika uliofanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Speke Munyoyo Kampala, Uganda.  Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Prof. Innocent Ngalinda, katikati ni Meneja wa Takwimu za Kilimo Titus Mwisomba kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu na kulia ni Mwenyekiti wa  Bodi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu Prof. Milline Mbonile.
 Washiriki wengine kutoka Tanzania wakisikiliza kwa makini mambo yanayoendelea katika Mkutano wa Kumi wa Maendeleo ya Takwimu Afrika uliofanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Speke Munyoyo Kampala, Uganda.  Kushoto ni Meneja wa Sensa ya Watu na Makazi Irenius Ruyobya akifuatiwa na Dkt. Camilius Kasalla kutoka Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika.
 Waziri Mkuu wa Uganda Mhe. Ruhakana Rugunda akimpongeza Mwandishi wa Kitabu cha Mapinduzi ya Takwimu Afrika Prof. Ben Kiregyera baada ya kukizindua leo kwenye Mkutano wa Kumi wa Maendeleo ya Takwimu Afrika uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Speke Munyoyo Kampala, Uganda. (PICHA NA VERONICA KAZIMOTO - KAMPALA)

RIPOTI KAMILI YA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM KUJULIKANA KESHO.

0
0
 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akizungumza jambo na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,Ndugu Adam Kimbisa,wakati akitoka nje mara baada ya kumaliza kikao cha kawaida cha Kamati Kuu ya CCM Taifa usiku huu,kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Unguja,Zanzibar,kikao hicho kilianza mnamo majira ya saa sita mchana na kumalizika usiku mnamo saa mbili na ushehe hivi huku mambo mbalimbali yakiwa yamejadiliwa ikiwemo suala la sakata la Akaunti ya Escrow,Hali ya kisiasa nchini,uchaguzi Mkuu na mambo ya Maadili na mengineyo.
Pichani ni Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na Wanahabari usiku huu baada ya kikao cha kamati kuu cha CCM kuisha nje ya ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM,Kisiwandui mjini Unguja kisiwani Zanzibar.Nape ameeleza kuwa taarifa rasmi ya yaliyohusu kikao hicho atayaweka wazi mapema kesho asubuhi.

MASANGA COMMUNITY TAKES A STAND AGAINST FGM

ASKOFU MPYA DAYOSISI YA KASKAZINI AWEKWA WAKFU NA KUSIMIKWA

0
0
Waumini wakiwa katika ibada ya kuwekwa Wakfu na kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Dayosisi ya Kaskazini ,Dkt Fredrick Shoo ibada iliyofanyika Usharika wa Moshi Mjini.
Askofu ,Dkt Paul Akyoo akimvisha kofia Askofu Mpya wa Dayosisi ya Kaskazini ,Dkt Fredrick Shoo ikiwa ni alama ya ukuhani wake  Yesu Kristo katika kanisa lake.
Maaskofu wakiwa wamemzunguka huku wakimwekea mikono Askofu Mpya wa Dayosisi ya Kaskazini Dkt Fredrick Shoo na kumbariki kwa baraka ya Haruni wakati wa ibada ya kuwekwa Wakfu na Kusimikwa kwake.
Baadhi ya waumini na viongozi mbalimbali wakiwa katika ibada hiyo iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Usharika wa Moshi mjini 
Askofu Mpya wa Dayosisi ya Kaskazini,Dkt Fredrick Shoo akitoa hotuba yake ya kwanza muda mfupi baada ya kuwekwa Wakfu na Kusimikwa kuwa Askofu Mpya wa Dayosisi hiyo akichukua nafasi ya Dkt Martin Shao aliyemaliza muda wake.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini ,kwa PICHA ZAIDI BONYEZA HAPA.

FLAVIANA MATATA FOUNDATION YATOA VIFAA VYA SHULE SHULE YA MSINGI MSINUNE

0
0
Taasis ya Flaviana Matata 'FMF' ya Mwanamitindo Flaviana Matata aishie New York ,Nchini Marekani. Mwaka jana ilisaidia watoto 3000 kwa kuwapa vifaa vya kujifunzia.Mwaka huu itaendelea kuwasaidia Watoto hao hao wakati inaangalia namna ya kutatua matatizo mengine yanayozikabili Shule hizo ili kuboresha elimu nchini Yakiwemo mavazi, majengo na hata vyakula vya shule kwa shule za pembezoni Zoezi litaendelea kwa shule zingine za mikoani ukiwemo Mkoa wa Shinyanga, Lindi na Arusha kwa kuanzia. 

Bado Flaviana Matata Foundation inahamasisha yeyote akataeguswa ikiwa ni shirika , kampuni au mtu binafsi atakaeguswa kuwasiliana nao kupitia info@flavianamatatafoundation.org au piga simu +255 784 200 680 .Pichani ni wanafunzi wa Shule ya Msingi Msinune iliyopo kata ya Kiwangwa katika wilaya ya Bagamoyo leo team ya FMF ilopotembelea Shule hiyo kuendelea zoezi lake flaviana matata 2015IMG_6600IMG_6607IMG_6609IMG_6594 Msimu wa wanafunzi kurejea mashuleni ndio kwanza umeanza ukiwa kama kampuni, mtu binafsi ukiguswa na ungependa kusaidia tafadhali wasiliana na info@flavianamatatafoundation.org au piga simu +255 784 200 680

Waumini wa Mwembetanga kwa Karagosi waadhimisha Maulidi ya Mfunga Sita

0
0
Vijana na wazee wa kiIslamu wa M/Tanga wamefanikisha kuadhimisha Maulid ya Mtume Muhammad Salallahu alayhi wasalam, yaliosomwa Siku ya Jumanne Jan 13 ,2015 sawa na Rabii Awal 143.

Maulidi hayo walioaza rami mida ya Saa tatu usiku maraa tu baada kusaliwa sala ya Ishaa, katika Mtaa wa Mwembetanga maarufu (Kwa Karagosi) Zanzibar ambapo Wazee na vijana hao huuandaa maulidi kila mwaka, ifikapo mwezi wa kuzaliwa Mtume Muhammed S.A.W 
Mapambo ya jukwaa: Maandalizi ya jukwaa maalumu kwaajili ya KUMSIFU na kumsalia MTUME Muhammed S.A.W katika Maulidi ya Mfungo Sita yaliofanyika rasmi mtaa wa M/Tanga Siku ya Jumanne Jan 13, 2015 sawa  Rabii Awal 1436 (Picha na  Mussa Yussuf)
Wanafunzi wa Madrasa Ya Sharif Aboud kutoka vikokotoni  wakisoma kasida za Kumsifu Mtume Muhammed S.A.W katika Maulidi ya Mfungo Sita yaliofanyika rasmi mtaa wa M/Tanga 
Muongozaji Maulidi ya Mwembetanga kwa karagosi MC Imam Sadat Fadhil Abdullah akiongea Mipangilio ya maulid kwa ratiba maalumu iliopangwa na wana kamati Ya maandalizi ya Maulidi hayo.
Wazee wa mtaa wa M/Tanga Hajji AbdulAziz akiea na Sheik Ahmed wakiwa makini kusikiliza maulid ya Mtume Muhammad Salallahu alayhi wasalam, yalioandaliwa na  vijana pamoja na wazee wawa M/Tanga Siku ya Jumatatu Jan 13, 2014 Zanzibar. Maalim: Dr. Muhidin Siasa (kulia) na mwazake wakisikiliza Mtume Muhammad Salallahu alayhi yaliofanyika rasmi mtaa wa M/Tanga Siku ya Jumanne Jan 13, 2015 sawa Rabii Awal 1436
Maulidi ya kizidi kuendelea na ustadhi Kombo Muhammed akisoma mlango wa pili wa Mualidi Ya Mtume Muhammed s.a.w Yalioandaliwa Rasmi na Wazee pamoja na vijana wa M/Tanga, Zanzibar
Waumini wa kiIslamu kutoka maeneo mbali mbali wakiwa katika  maulid ya Mtume Muhammad Salallahu alayhi wasalam, yalioandaliwa na  vijana pamoja na wazee wawa M/Tanga Siku ya Jumatatu Jan 13, 2014 Zanzibar
Waandaaji wa maulid hayo Imam Sadat akipata picha ya pamoja na Hudheif A Shatry katika maulidi Ya mfungo sitta yaliofanyika Siku ya Jumatatu Jan 13, 2014 Zanzibar katika Mtaa wa M/Tanga Zanzibar
Waumini wa kiIslamu kutoka maeneo mbali mbali wakiwa katika  maulid ya Mtume Muhammad Salallahu alayhi wasalam, yalioandaliwa na  vijana pamoja na wazee wawa M/Tanga Siku ya Jumatatu Jan 13, 2014 Zanzibar
Waalikwa wageni mbalimbali wakisikiliza Maulidi ya mfungu sita Mwembetanga Maulidi yaaza rasmi kwa kasida ilivyokuwa ikisomwa na wanafunzi wa Madrasa Ya Sharif Aboud Vikokotoni kutoka.
Maalim: Dr. Muhidin Siasa akiongea neno kuhusu  Maulid ya Mtume Muhammad Salallahu alayhi  yaliofanyika rasmi mtaa wa M/Tanga Siku ya Jumanne Jan 13, 2015 sawa  Rabii Awal 1436
Maalim Abuu akihitimisha Dua ya Maulidi ya Mtume Muhammad Salallahu alayhi wasalam, yalioandaliwa na  vijana pamoja na wazee wawa M/Tanga Siku ya Jumatatu Jan 13, 2014 Zanzibar

Mmoja kati ya wanakamati ya maandalizi ya Maulidi Mussa Yussuf Mussa akiwa katika usimamizi wa kuweka mambo sawa katika kusimamia maulidi.

Maalim Afrif Abdallah Shatry akiwa katika usimamizi wa maulidi 
Mwanakamati ya maandalizi ya Maulidi  Masoud Masoud   akiwa katika usimamizi wa kuweka mambo sawa katika kusimamia Maulid ya Mtume Muhammad Salallahu alayhi wasalam, yaliosomwa Siku ya Jumanne Jan 13 ,2015 sawa na mwezi 11 Rabii Awal 1436
Kijana Muhammed Hassan akipata picha ya pikee katika maulid ya Mtume Muhammad Salallahu alayhi wasalam, yalioandaliwa na  vijana pamoja na wazee wawa M/Tanga Siku ya Jumatatu Jan 13, 2014 Zanzibar.

HAYA NDIYO MAAZIMIO YA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM KILICHOFANYIKA JANA MJINI UNGUJA-ZANZIBAR.

0
0
Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na Wanahabari mapema leo akifafanua kuhusiana na ripoti na maadhimio ya kikao cha kamati kuu cha CCM kilichofanyika jana katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM,Kisiwandui mjini Unguja kisiwani Zanzibar.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Jana tarehe 13/01/2015 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa chini ya uongozi wa Mwenyekiti wake wa Taifa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete ilifanya kikao chake cha kawaida cha siku moja Kisiwandui Mjini Zanzibar.

Pamoja na mambo mengine baadhi ya mambo yaliyojadiliwa na Kamati Kuu ni pamoja na:-

1. SAKATA  LA  AKAUNTI  YA ESCROW.
 
Chama Cha Mapinduzi kimesikitishwa sana na sakata hili. Baada ya kulijadili kwa muda mrefu na kwa kina Kamati Kuu imeamua yafuatayo:-,
i). Pamoja na yale ambayo yameshatekelezwa na serikali, Kamati Kuu imeitaka serikali na vyombo vinavyohusika kuendelea kutekeleza maazimio ya bunge juu ya swala hilo.

ii). Kamati Kuu imewataka wote wanaopewa dhamana wajenge utamaduni wa kuwajibika kwa dhamana zao, na wasipowajibika waliowapa dhamana wachukue hatua za kuwawajibisha.

iii). Aidha Kamati Kuu imeiagiza Kamati Ndogo ya Maadili kuchukua hatua za kimaadili kwa wale wote waliohusika na ukiukwaji wa maadili kwenye sakata la Escrow na wako kwenye vikao vya maamuzi vya Chama. Kikao cha Kamati Ndogo ya Maadili kitafanyika tarehe 19/01/2015 kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hilo.

2. WALIOPEWA  ADHABU KWA KUKIUKA MAADILI YA CHAMA.
 
Itakumbukwa kuna makada sita wa CCM walipewa adhabu kwa kuhusishwa na ukiukwaji wa maadili kwenye mchakato wa kutaka kuteuliwa na CCM kugombea urais, watamaliza muda wa adhabu zao mwezi wa pili mwaka 2015.

Baada ya muda wa adhabu zao kuisha, itafanyika tathimini kuona kama walizingatia mashariti ya adhabu zao. Na kama kuna ambao watakutwa hawakuzingatia mashariti ya adhabu zao wataongezewa adhabu.

3. SOKO LA MAHINDI.
 
Kamati Kuu imepokea taarifa ya mwenendo wa soko la mahindi nchini. Baada ya tathimini na uchambuzi,  pamoja na kazi iliyofanywa na serikali, Kamati Kuu imeiagiza serikali kuangalia upya mfumo unaotumiwa na Hifadhi ya Taifa ya Chakula ( NFRA)katika ununuzi wa mahindi, ili unufaishe zaidi wakulima badala ya utaratibu wa sasa ambao kwa kiasi kikubwa unanufaisha zaidi mawakala badala ya wakulima moja kwa moja.

4. RATIBA YA VIKAO VYA CHAMA.
 
Kamati Kuu imepitisha ratiba ya shughuli mbalimbali za Chama kwa mwaka 2015.Aidha ratiba ya mchakato wa kuwapata wagombea wa CCM ndani ya dola utapangwa na vikao vijavyo  vya Chama.

Nape Moses Nnauye
CCM Secretary for Ideology & Publicity.

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (KAZI MAALUM), MHESHIMIWA PROF. MARK MWANDOSYA AFANYA ZIARA YA KIKAZI NCHINI SUDANI

0
0

New Picture (1) 
Mhe. Prof. Mark Mwandosya akifafanua jambo wakati wa mkutano wa pamoja na Waziri wa Maji na Umeme wa Sudan Mhe Mutaz Moussa Abdallah Salim. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Bwana Felix Ngamlagosi ambaye ameongozana pamoja na maafisa wengine na Waziri Prof. Mwandosya
New Picture (2) 
Mhe. Prof. Mark Mwandosya akitoa maelezo katika mkutano wa pamoja na Waziri wa Maji na Umeme wa Sudan Mhe Mutaz Moussa Abdallah Salim.
New Picture (3) 
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Mhe. Prof. Mark Mwandosya katika mkutano wa pamoja na ujumbe wa Sudan ulioongozwa na Waziri wa Maji na Umeme wa Sudan Mhe Mutaz Moussa Abdallah Salim.
New Picture 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Mhe. Prof. Mark Mwandosya akikaribishwa na mwenyeji wake Waziri wa Maji na Umeme wa Sudan Mhe. Mutaz Moussa Abdallah Salim mara alipowasili katika Ofisi za Wizara hiyo Jijini Khartoum.
……………………………………………………………………………………………………………………………………..
12 – 17 JANUARI 2015Mheshimiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Mark Mwandosya yuko ziarani nchini Sudan ambako atatembelea miradi mbalimbali ya maendeleo nchini humo ikiwemo miradi mikubwa ya mabwawa yaliyojengwa katika bonde la Mto Nile pamoja na kubadilishana uzoefu na taasisi za Sudan zinazojihusisha na udhibiti wa huduma katika sekta za maji, nishati, mawasiliano na usafirishaji.

Ujumbe wa Mhe. Prof. Mwandosya umejumuisha wataalamu kutoka Wizara ya Maji, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) na Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA).

Mhe. Prof. Mwandosya alianza ziara yake Jumatatu ya tarehe 12 Januari, 2015 kwa kutembelea Wizara ya Rasilimali za Maji na Nishati ya Umeme ya Jamhuri ya Sudan. 
 Katika ziara hiyo Mhe. Prof. Mwandosya alieleza kuwa pamoja na shughuli zingine, ameandamana na taasisi za udhibiti kutoka Tanzania ili kujifunza na kubalishana uzoefu katika shughuli za udhibiti kutoka kwa taasisi kama hizo katika nchi ya Sudan. 

Waziri alieleza kuwa shughuli za udhibiti Tanzania zimekuwa zikifanyika kwa kipindi cha takribani miaka 10 sasa. Waziri alieleza kuwa pamoja na mafanikio yaliyopatika katika kutekeleza majukumu yao, Mamlaka za Udhibiti bado zina changamoto nyingi ambazo inabidi kukabiliana nazo kwa kujifunza na kubadilisha uzoefu na taasisi kama hizo katika nchi kama Sudan.

ASKOFU MPYA DAYOSISI YA KASKAZINI AWEKWA WAKFU NA KUSIMIKWA

0
0
Waumini wakiwa katika ibada ya kuwekwa Wakfu na kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Dayosisi ya Kaskazini ,Dkt Fredrick Shoo ibada iliyofanyika Usharika wa Moshi Mjini.
Askofu ,Dkt Paul Akyoo akimvisha kofia Askofu Mpya wa Dayosisi ya Kaskazini ,Dkt Fredrick Shoo ikiwa ni alama ya ukuhani wake  Yesu Kristo katika kanisa lake.
Maaskofu wakiwa wamemzunguka huku wakimwekea mikono Askofu Mpya wa Dayosisi ya Kaskazini Dkt Fredrick Shoo na kumbariki kwa baraka ya Haruni wakati wa ibada ya kuwekwa Wakfu na Kusimikwa kwake.
Baadhi ya waumini na viongozi mbalimbali wakiwa katika ibada hiyo iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Usharika wa Moshi mjini 
Askofu Mpya wa Dayosisi ya Kaskazini,Dkt Fredrick Shoo akitoa hotuba yake ya kwanza muda mfupi baada ya kuwekwa Wakfu na Kusimikwa kuwa Askofu Mpya wa Dayosisi hiyo akichukua nafasi ya Dkt Martin Shao aliyemaliza muda wake.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini ,kwa PICHA ZAIDI BONYEZA HAPA.

RAIS KIKWETE NA MAMA SALMA KIKWETE WAMJULIA HALI MBUNGE WA NAMTUMBO MHE VITA KAWAWA ALIYELAZWA HOSPITALI YA AMI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

0
0

unnamed 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakimjulia hali Mbunge wa Namtumbo Mhe. Vita Kawawa aliyelazwa katika hospitali ya AMI jijini Dar es salaam akipatiwa matibabu ya tumbo. Katikati yao ni Mhe Adam Malima, naibu Waziri wa Fedha na kushoto ni Daktari katika wodi hiyo.

TAKWIMU SAHIHI NA ZA WAKATI ZITASAIDIA KULETA MAENDELEO KWA HARAKA BARANI AFRIKA.

0
0
 WITO umetolewa kwa washiriki wote wa Mkutano wa Kumi wa Maendeleo ya Takwimu Afrika kuelendelea kutoa takwimu sahihi na kwa wakati ili kuleta maendeleo yanayokusudiwa ya kiuchumi na kijamii barani Afrika.
 
Wito huo umetolewa jana na Waziri Mkuu wa Uganda Mhe. Dkt. Ruhakana Rugunda wakati akifungua Mkutano wa Kumi wa Maendeleo ya Takwimu Afrika uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Speke Munyoyo Kampala, Uganda.
 
Dkt. Rugunda amesema kuwa, ili kupata maendeleo kwa haraka, ni lazima takwimu zitolewe kwa wakati na ziwe sahihi kwa ajili ya kusaidia kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo.
 
“Ili Bara la Afrika liweze kuendelea kwa haraka, linahitaji takwimu sahihi na zinazotolewa kwa wakati ili takwimu hizo zisaidie katika kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo”, amesema Waziri Mkuu Rugunda.
 
Dkt. Rugunda ameongeza kuwa ili kuweza kufanikisha hilo, kuna umuhimu kwa nchi za Afrika kusaidia program mbalimbali za uzalishaji wa takwimu na matumizi yake kwa ajili ya kupanga mipango ya maendeleo.
 
Kwa upande wa Waziri wa Fedha wa Uganda Matia Kasaija amesema kuwa, ili kuweza kulinganisha takwimu za nchi mbalimbali, ni vyema takwimu zinazozalishwa zikafuata mbinu bora za uzalishaji wa takwimu.
 
Matia Kasaija amesema mbinu bora za uzalishaji wa takwimu ni zile  zinazofuata viwango vinavyopendekezwa na Umoja wa Kimataifa – Kitengo cha Takwimu.  
 
Mkutano wa Kumi wa Maendeleo ya Takwimu Afrika umewakutanisha washiriki takribani 400 kutoka nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo Tanzania. Mkutano huu ni wa siku tatu na unatarajia kumalizika kesho tarehe 15 Januari, 2015.
 
NA: VERONICA KAZIMOTO
14 JANUARI, 2015
KAMPALA.
 
SIMBA YAIBUKA KINARA KOMBE LA MAPINDUZI CUP UWANJA WA AMANI

0
0
unnamed4 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi kombe Nahodha wa Timu ya Simba Hassan Izhaka baada ya kuifunga Mtibwa kwa matuta 4-3 mchezo wa Fainali ya kombe la Mapinduzi uliofanyika jana ikiwa ni kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar katika uwanja wa Amaan Studium.
unnamed 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Wachezaji wa Timu ya Simba kabla ya mpambano wa Fainali ya Kombe la Mapinduzi na Timu ya Mtibwa Sugar katika kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar mchezo uliofanyika jana Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]
Kikosi kamili cha Timu ya Simba kikiwa katika picha ya pamoja Uwanja wa Amaan Studium jana wakati wa Mpambano wa mchezo wa fainali ya kombe la Mapinduzi Cup na Timu ya Mtibwa Sugar mchezo huo ikiwa ni kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo mgeni rasmi alikuwa  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein [Picha na Ikulu.]
unnamed3 
Wananchi na Mashabiki wa timu ya Simba wakifuatilia kwa makini mchezo wa fainali ya kombe la Mapinduzi Cup kati ya Simba na Mtibwa Sugar uliochezwa jana katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja ikiwa ni katika kusherehekea miaka 51 ya mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ambapo simba iliweza kutokakifua mbele kwa kuwafunga Mtibwa matuta 4-3.
unnamed5 
Wachezaji wa Timu ya Simba wakisherehekea ushindi wao baada ya kuwafunga kwa matuta timu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro katika mchezo wa fainali ya kombe la Mapinduzi 4-3 katika uwanja wa Amaan studium Mjini Unguja jana katika kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.]
unnamed6 
Mashabiki wa Timu ya  Simba Wengundu wa Msimbazi walipokuwa katika jukwa la   Saa katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja wakishangilia timu yao ilipocheza na Mtibwa Sugar ya Morogoro katika fainali ya kombe la Mapinduzi,Timu hiyo ya Simba ilishinda kwa matuta 4-3ikiwa ni kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.]
Bendera ya Shirikisho la mchezo wa Mpira wa Miguu FIFA iliyobebwa na Vijana wakiwepo na waamuzi wa Mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi kati ya Timu ya Mtibwa Sugar na Simba katika Uwanja wa Amaan Studium katika kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar katika mchezo huo Simba iliibuka kwa ushindi wa matuta 4-3 dhidi ya Mtibwa, [Picha na Ikulu.]
unnamed 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo Said Ali Mbarouk (kushoto) wakiangalia mchezo wa Fainali ya kombe la Mapinduzi Cup kati ya Simba na Mtibwa Sugar uliochezwa jana katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja ikiwa ni katika kusherehekea miaka 51 ya mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ambapo simba iliweza kutokakifua mbele kwa kuwafunga Mtibwa matuta 4-3 , [Picha na Ikulu.]

RIDHIWANI KIKWETE ASHIRIKI MAZISHI YA MGOMBEA UNEC, NJOMBE

0
0
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM-NEC), Ridhiwani Kikwete akitoa salamu za CCM, wakati wa mazishi ya, aliyekuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM Taifa, marehemu Christian Fwalo ambaye alikuwa akiwakilisha mkoa wa Iringa mwaka 2007-2012,  katika makaburi ya Kijiji cha Ihalula, mkoani Njombe juzi. Fwalo pia alikuwa mgombea wa NEC, ili kuziba pengo la marehemu Lupyana Fute aliyefariki mwak jana.

Vice President Bilal to host youth discussion on post-2015 goals

0
0
 Vice President of Tanzania, His Excellency Dr. Mohamed Gharib Bilal will be joining The ONE Campaign and Restless Development on Thursday 15, January, 2015, for a dialogue with 15-year-olds,aimed at giving an opportunity for the youths to share their views with policy makers on what the next set of development goals should look like for them to have a better future by 2030.

The event is part of action2015, a citizen’s movement of nearly 1,000 organisations around the world coming together to raise awareness of how important 2015 is and to demand truly ambitious agreements to end poverty and inequality in the world.

The vice president’s dialogue with the youth will be held at Hyatt Regency Hotel in Dar es Salaam, where the youth selected from all over the country will raise their voice to what they feel are top priorities ahead of the 2015 UN Summit that will come up with a new set of development goals.

2015 is a unique opportunity for world leaders to accelerate progress towards the eradication of extreme poverty and preventable, treatable child and maternal death by 2030 where Leaders meeting at the UN will agree a new set of goals on development targets that will replace the Millennium Development Goals (which ran from 2000 to 2015).

Speaking ahead of the event, Oscar Kimaro of Restless Development said youth in Tanzania comprise about 60% of the total population and those who are 15 years old now were born when the Millennium Development Goals were unveiled.

“The post-2015 development agenda is about building a better future for these people, who will be 30 years old at the end of the second set of the development goals in 2030. These are the people who will hold our leaders accountable for decisions being taken this year. Their voice and perspective is important in this process” he said.
Those expected at the event include the Deputy Minister of Information, Youth and Culture, Dr Fenella Mukangara, ONE Africa Executive Director Dr Sipho Moyo, ONE Campaign ambassador in Tanzania, Diamond Platnumz, AY and many other government and civil society leaders.
The event will be broadcasted live on Clouds TV and participants will be able to share questions via social media through Facebook and Twitter, using the hashtags #action2015 and #DemandBetter.
As part of the launch of action2015, similar activities are taking place in over 50 countries all around the world, including South Africa, Liberia, Nigeria, Lebanon, Norway, the United Kingdom, USA and Sri Lanka

Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa wafanyabiashara kutoka Tanzania na nchi za Ghuba (GCC)

0
0
 Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Oman Ali Ahmed Saleh akieleza umuhimu wa mkutano wa kimataifa wa wafanyabiashara kutoka Tanzania  na nchi za Ghuba (GCC) utakafanyika kwa siku mbili kuanzia Januari 15 hadi 16, 2015 jijini Dar Es Salaam.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara kutoka Oman na nchi za Ghuba (GCC)   Saeed Saleh Saeed Al Kiyumi (katikati) akizungumza na baadhi ya wajumbe wa mkutano wa kimataifa wa wafanyabiashara kutoka Tanzania  na nchi za Ghuba (GCC) utakafanyika kwa siku mbili kuanzia Januari 15 hadi 16, 2015 jijini Dar Es Salaam. Kulia ni Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Oman Ali Ahmed Saleh na kushoto ni mkalimani aliyetafsiri maelezo ya mwenyekiti GCC Sudi Ahmed Rawahi.
 Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria mkutano wa matayarisho wa mkutano wa siku mbili wa kimataifa wa wafanyabiashara kutoka Tanzania  na nchi za Ghuba (GCC) utakafanyika kwa siku mbili kuanzia Januari 15 hadi 16, 2015 jijini Dar Es Salaam. 
 Baadhi ya wajumbe  kutoka Oman waliohudhuria mkutano wa matayarisho wa mkutano wa siku mbili wa kimataifa wa wafanyabiashara kutoka Tanzania  na nchi za Ghuba (GCC) utakafanyika kwa siku mbili kuanzia Januari 15 hadi 16, 2015 jijini Dar Es Salaam. 
 Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria mkutano wa matayarisho wa mkutano wa siku mbili wa kimataifa wa wafanyabiashara kutoka Tanzania  na nchi za Ghuba (GCC) utakafanyika kwa siku mbili kuanzia Januari 15 hadi 16, 2015 jijini Dar Es Salaam.

PRESIDENT KIKWETE MEETS MILLICOM INTERNATIONAL CELLULAR EXECUTIVE VICE CHAIRMAN IN DAR ES SALAAM

0
0

 unnamed3 
President Jakaya Mrisho Kikwete shakes hands with the Millicom
International Cellular South Africa Executive Vice President for
Africa, Mr Arthur Bastings, who and his delegation  paid a courtesy
call on him Wednesday January 14, 2015 at the State House in Dar es
salaam. Second left is Ambassador Ami Mpungwe and right the Chairman
of MIC Tanzania (TIGO)  Mr Diego Gutierrez. Others second right are
TIGO’s Head of regulatory Ms Sylvia Balwire and extreme left is Tigo’s
Public Retations Manager MS Halima Okash.unnamed 
President Jakaya Mrisho Kikwete chats  with the Millicom
International Cellular South Africa Executive Vice President for
Africa, Mr Arthur Bastings, who and his delegation  paid a courtesy
call on him Wednesday January 14, 2015 at the State House in Dar
  unnamed1 
President Jakaya Mrisho Kikwete chats with the Millicom
International Cellular South Africa Executive Vice President for
Africa, Mr Arthur Bastings, who and his delegation  paid a courtesy
call on him Wednesday January 14, 2015 at the State House in Dar es
salaam
Viewing all 46193 articles
Browse latest View live

Latest Images