Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live

WAZIRI KIONGOZI MSTAAFU SHAMSI VUAI NAHODHA AFUNGUA SKULI YA SEKINDARI YA JUMBI.

$
0
0
Waziri kiongozi mstaafu ambae pia ni Muakilishi wa Jimbo la Mwenakwerekwe Shamsi Vuai Nahodha akikunjuwa kitambaa ikiwa ni ishara ya Ufunguzi wa Skuli ya Sekondary ya Jumbi Wilaya ya kati Unguja ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 51ya mapinduzi ya Zanzibar.Nyuma yake ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Zahra Ali Hamad.
Waziri kiongozi mstaafu ambae pia ni Muakilishi wa Jimbo la Mwenakwerekwe Shamsi Vuai Nahodha akikata utepe ikiwa ni isharaya Ufunguzi wa Skuli ya Sekondary ya Jumbi Wilaya ya kati Unguja ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 51ya mapinduzi ya Zanzibar. unnamed2q 
Waziri kiongozi mstaafu ambae pia ni Muakilishi wa Jimbo la Mwenakwerekwe Shamsi Vuai Nahodha akitembelea maeneo mbalimbali ya Skuli ya Sekondary ya Jumbi Wilaya ya kati Unguja baada ya kuifungua.Kushoto yake ni Mwalimu Mkuu wa Skuli hiyo Juma Vuai Mshamba. unnamed3q 
Waziri kiongozi mstaafu ambae pia ni Muakilishi wa Jimbo la Mwenakwerekwe Shamsi Vuai Nahodha wakwanza kulia akiangalia Madawati yaliomo katika moja ya madarasa ya Skuli ya Sekondary ya Jumbi Wilaya ya kati Unguja baada ya kuifungua,ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 51ya mapinduzi ya Zanzibar.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali  Zahra Ali Hamad.akitoa hotuba ya makaribisho kwa Waziri kiongozi mstaafu ambae pia ni Muakilishi wa Jimbo la Mwenakwerekwe Shamsi Vuai Nahodha katika ufunguzi wa Skuli ya Sekondary ya jumbi Wilaya ya kati Unguja baada ya kuifungua,ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka  51ya mapinduzi ya Zanzibar. unnamed5q 
Waziri kiongozi mstaafu ambae pia ni Muakilishi wa Jimbo la Mwenakwerekwe Shamsi Vuai Nahodha akitoa hotuba katika ufunguzi wa Skuli ya Sekondary ya jumbi Wilaya ya kati Unguja baada ya kuifungua,ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 51ya mapinduzi ya Zanzibar.PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

HUYU NA YULE........Mahojiano na Dr Talib Ali

$
0
0
Karibu katika kipindi cha HUYU NA YULE ambapo wiki hii tumeongea na Dk Talib Ali
Yeye ni mwanzilishi wa Avatar Dental Care iliyopo Leesburg Virginia.
Ameeleza mengi kuhusu kazi zake na mikakati aliyonayo baadae Pia, ametoa punguzo la 50% kwa waTanzania watakaoenda kutiiwa kwake, pamoja na mpango wa malipo ya awamu kuwzesha watu kumudu gharama hizo
Karibu
Huyu na Yule ni kipindi kinachotayarishwa na Vijimambo Blog na kuzalishwa na Kwanza Production
Kwa mawasiliano, maoni ama ushauri, tafadhali wasiliana nasi kupitia kwanzaproduction at gmail.com .

HERI YA MIAKA 51 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUTOKA NGOMA AFRICA BAND

$
0
0

Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa Band
aka FFU-Ughaibuni yenye makao yake nchi ujerumani,inawatakia kila
heri na fanaka wadau wote katika kuadhimisha miaka 51 ya mapinduzi
ya Zanzibar,mapinduzi yaliyofanyika 12 Januari 1964 ambayo  yaliwakomboa wanzibar walio wengi kutoka katika makucha ya Sultan,Mapinduzi yaliyomng'oa Sultan hadi kusahau kiremba kitandani.
Tunawapongeza wanzabar katika kuadhimisho ya miaka 51
ya mapinduzi,Amani,Upendo ,Umoja na mshikamano
ndio msingi wa maisha bora kwa wanadamu wote.
Yadumu mapinduzi ya Zanzibar ! Zidumu fikira za waasisi wa mapinduzi !
Mapinduzi haya ni yetu sote watanzania

Rais Kikwete amjulia hali Mgonjwa Bagamoyo

$
0
0

unnamed 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Mkazi wa Bagamoyo mjini Bwana Mohamed Amani anayeugua ugonjwa wa Kiharusi kutokana na maradhi ya moyo.Rais Kikwete aliyekuwa katika mapunziko ya mwisho wa wiki nyumbani kwake mjini Bagamoyo alimwona mgonjwa huyo  na kuamua kusimama kumjulia hali na kuahidi kumpatia msaada wa matibabu(Picha na Freddy Maro)

Taasisi ya WAMA Foundation imefanikiwa kupanua fursa za elimu kwa mtoto wa kike kwa mwaka 2014.

$
0
0
Hayo yamesemwa na Mke wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma Kikwete wakati Akiongea na wenza wa mabalozi kutoka nchi mbalimbali katika ghafla fupi ya kuukaribisha mwaka mpya 2015 iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam,
Mama Salma alisema kuwa baadhi ya mafanikio yaliyofikiwa na Taasisi ya WAMA ni kukamilika kwa sekondari ya WAMA Sharaf  katika Manispaa ya Lindi.
“Ninayo furaha kuwataarifu kwamba ujenzi wa shule ya sekondari ya WAMA Sharaf umekamilika, shule ambayo itaongeza idadi ya wasichana wanaofaidika na WAMA” Alisema Mama Salma.
Aidha, aliitaja Shule ya Sekondari ya Wasichana ya WAMA Nakayama kuwa sehemu ya mafanikio ya Tasisi hiyo ambayo ina idadi ya wanafaunzi zaidi ya 400 na inatarajia kuchukua wanafunzi 90 mwaka 2015, ambao ni yatima na wanaotoka kwenye mazingira magumu.
Akiongelea kuhusu mafanikio mengine Mama Salma alisema ni pamoja na kuimarisha afya ya mama wajawazito na watoto ili kupunguza vifo, kupunguza mimba za utotoni, na kupunguza kasi ya maambukizi ya HIV toka kwa mama kwenda kwa mtoto
Mama Salma aliwashukuru wadau wote wanaofanya kazi kwa kushirikiana na WAMA wakiwemo Mashirika yasiyo ya Serikali kwa misaada na kuwaomba waendelee kushirikiana ili kutoa mabadiliko chanya katika jamii husika.
Aidha, kwa niaba ya wenza wa mabalozi waliohudhuria ghafla hiyo, Mke wa kiongozi wa mabalozi nchini Bi Celine Mpango alimpongeza Mama Salma Kikwete kwa juhudi anazofanya katika kumkomboa mtoto wa kike na mwanamke kwa ujumla.

klabu za michezo za maveterani Dar es salaam zarehemu marehemu leo (Mapinduzi Day) Leaders club, Kinondoni, jijini Dar es salaam

$
0
0
 
 Sheikh Hilal Shaweji akitoa neno kwa wadau wa michezo katika ibada ya kuwakumbuka wasanii na wanamichezo mbalimbali waliotangulia mbele ya haki, ibada hiyo imefanyika katika viwanja vya Leaders Club kinondoni jijini Dar leo.
Padre John Solomon akitoa neno kwa wadau na wanamichezo katika ibada ya kuwakumbuka waliotangulia mbele ya haki  iliyofanyika leo katika viwanja vya leaders Club jijini Dar es Salaam.
Balozi Mstaafu  Sisco Mtilo Akiwakaribisha wadau katika ibada ya kuwaombea waliotangulia mbele ya haki na Ibada  hiyo imefanyika katika viwanja vya leaders Club jijini Dar es Salaam.
 Padre John Solomon akiongoza ibada ya kuwaombea wasanii na wanamichezo mbalimbali waliotangulia mbele ya haki iliyofanyika kaika viwanja vya leaders Club.
Wadau wakiwa wamesimama katika ibada ya kuwaombea wasanii na wanamichezo waliotangulia mbele ya haki iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Wadau wakifuatilia ibada maalumu ya kuwaombea wa wanamichezo na wasanii waliotangulia mbele ya haki iliyofanyika katika viwanja vya leaders Club jijini Dar es Salaam.
 Wadau wakifuatilia ibada maalumu ya kuwaombea wa wanamichezo na wasanii waliotangulia mbele ya haki iliyofanyika katika viwanja vya leaders Club jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Wadau mbalimbali waliojitokeza kwenye shughuli hiyo mapema leo katika viwanja vya leaders Club,Kinondoni jijini Dar. 
 Sehemu ya wakina mama  wakiwa wamesimama katika ibada ya kuwaombea wasanii na wanamichezo mbalimbali iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Pichani kati ni Rais wa TFF,Jamal Malinzi,kushoto ni Mbunge wa Kinondoni Idd Azzan wakisikiliza mawaidha katoka kwa Sheikh Hilal Shaweji 
 Ulifika wakati wa chakula cha pamoja. 
Wadau wakiwa katika foleni ya mnuso katika Ibada ya kuwakumbuka waliotangulia mbele ya haki .

RIDHIWANI AANZA KUTIMIZA AHADI, AWASHUKURU WANANCHI KWA KUMCHAGUA CHALINZE

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akimkabidhi Diwani wa Kata ya Miono. Senguli Mbele moja kati ya matairi manne aliyonunua kwa ajili ya gari la kubebea wagonjwa katika Kituo cha Afya cha Miono, wakati wa mkutano wa kuwashukuru wananchi kwa kumchagua miezi sita iliyopita. Mkutano huo ulifanyika jana katika Kata ya Miono, Chalinze, wilayani Bagamoyo, Pwani.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.(PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mmasai mwenye jamii ya kifugaji Andokela Okunge akiuliza swali kwa Mbunge Ridhiwani kuhsu Jamii sivyowaendea haki wafugaji ambapo alidai kuwa mkulima anaweza kuuzi shamba halafu baadaye anageuka na kusema amedhulumia jambo ambalo si kweli.

 Mwajabu Hemedambaye ambaye nyumba yake ilibomoka, akilalamik mbele ya Mbunge Ridhiwani kuwa alipotoa taarifa y kusaidiwa ujenzi wa yumba hiyo kwa Mwenyekiti wa Kitongoji, alijibiwa kwa dhiahaka kuwa amkubalie aklale naye kwanza ndipo amsaidie.
 Mzee Msoud Mhina akilalamika mbele ya Munge Ridhiwani kuwa Serikali ya CCM imewasahau wazee kwa kutowahudumia hali ambayo inawafanya waishi maisha magumu.
 Mkazi wa Miono, Sahaban Mpwimbwi akimuomba Mbunge Ridhiwani awasaidie katika Kata ya Miono kukarabati Rambo la maji ambalo limehribika. Rambo hilo lilijengwa Enzi Rais Jakaya Kikwete akiwa mbunge wa jibo la Chalinze.
 Ridhiwani akijadiliana jambo Diwani wa Kata ya Miono Senguli Mbele huku kwaya Kijiji ikitumbuiza na kutoa maneno ya matatizo yaliyopo katika Kituo cha Afya ch Miono ikiwemo kukosekana kwa chumba cha upasuaji ka waja wazito.
 Ridhiwani akisalimiana na wazee wa Miono
 Wafugaji wakijadiliana jambo a Mbunge Ridhiwani mjini Miono.
 Ridhiwani akisalimiana na watoto alipowasili katika Kijii cha Kweynkonje, Kata ya Miono
 Sehemu ya wananchi walihudhuria mkutano katika Kijiji cha Kweynkonje
 Mzee Khatib Yusufu akielezea jinsi walivyofurahi kutembelewa na Mbunge wao Ridhiwani atik Kijiji cha Kweynkonje
 Ridhiwni akisalimiana na Bibi Khadija Ibrahim lipowasili katika Kijiji cha Kweynkonje
Mkazi wa wa Kijiji cha Masimbani Kassim Mwakibindu 968) ambaye amesoma darasa moja  na Rais Jakaya Kikwete Kidato cha nane katika Shule ya Sekondari ya Lugoba, Chalinze wilayani Bagamoyo, Pwani, akimuomba Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete kuendeleza juhudi za Rais Kikwete kwa kuwajali kwa maendeleo wakazi wa kijiji hicho kilichopo kata ya Miono/

M
Saumu Bakari akimuomba rIDHIWANI KUSAIDIA KUNUNUA JOKOFU LA KUHIFADHIA CHANJO NA DAWA KATIKA zAHANATI YA KIJIJI HICHO
Ridhiwani akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Masimbani ambapo aliwashukuru na kuahidi kutekeleza ahadi mbalimbali alizoziahidi wakati wa kampeni.

Saccoss za Vijana katika Halmashauri ni Muhimu: Vijana

$
0
0
 Kijana Andrew Mlaki kutoka kikundi cha Akili ni Mwanga akielezea vijana wenzake (hawapo pichani) shughuli zinazofanywa na kikundi chake baada ya kikundi hicho kutembelewa na wawezeshaji waliofika Wilaya ya Mwanga kuhamasisha vijana na kuwapa elimu kuhusu ujuzi na stadi za maisha. Kushoto ni mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Ester Riwa.
 wa Wilaya ya Mwanga Bibi Subira Mfanga akizungumza na vijana walioshiriki semina ya uhamasishaji kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana Mkoani Kilimanjaro katika Wilaya ya Mwanga.
 Wawezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Maafisa Ushirika na Maafisa Vijana kutoka Wilaya ya Mwanga na Moshi Vijijini, katika picha ya pamoja na baadhi ya Vijana wa Wilaya hizo walioudhuria semina ya uhamasishaji kwa vijana kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana katika Wilaya ya Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga  Bw. Jamhuri David Willium (katikati) akisikiliza mrejesho kutoka kwa wawezeshaji wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo waliofika ofisini kwake baada ya kufunga semina ya uhamasishaji kwa Vijana wa Wilaya za Mwanga na Moshi Vijijini hivi karibuni.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga  Bw. Jamhuri David Willium kushoto akipokea Sera ya Maendeleo ya Vijana kutoka kwa mwezeshaji wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa baada ya kufunga semina ya uhamasishaji kwa Vijana wa Wilaya za Mwanga na Moshi Vijijini hivi karibuni.
(Picha zote na : Genofeva Matemu – Maelezo)

UFUNGUZI RASMI WA DUKA LA ZURII HOUSE OF BEAUTY WAFANYIKA LEO NDANI YA JENGO LA DAR FREE MARKET JIJINI DAR

$
0
0
 Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige  akikata utepe katika ufunguzi wa ZuRii House of Beauty duka jipya na la kisasa la vipodozi lililofunguliwa rasmi leo Jumatatu 12 Jan 2015  kulia ni Mkurugenzi wa ZuRii Fashion & Beauty Boutique, Jestina George. 
 Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akifungua duka rasmi 
   Mkurugenzi wa ZuRii Fashion & Beauty Boutique, Jestina George  akitoa ufafanuzi kwa Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige kuhusu bidhaa zilizopo kwenye duka la ZuRii Fashion & Beauty Boutique
 Mkurugenzi wa ZuRii Fashion & Beauty Boutique, Jestina George akizungumza na vyombo vya habari kwenye ufunguzi wa duka hilo la vipodozi
 Mkurugenzi wa ZuRii Fashion & Beauty Boutique, Jestina George akitoa maelezo kwa mmoja wa wateja waliofika kufanya manunuzi ndani ya duka hilo
 Mkurugenzi wa ZuRii Fashion & Beauty Boutique, Jestina George( kulia) akiwa na mwana harakati mwenzake Shamim Mwasha mmiliki wa blog ya 8020.
 Mkurugenzi wa ZuRii Fashion & Beauty Boutique, Jestina George akitoa ufafanuzi kuhusu ufunguzi na ujio wa duka hilo hapa nchini Tanzania likiwa na muonekano tofauti
 Mmoja wa wateja waliofika katika duka hilo akitizama bidhaa
Muonekano wa duka la Zurii kwa ndani

MBUNGE wa Viti Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Vijana , Mkoa wa Arusha Catherine Magige  leo amezindua rasmi  duka  jipya la vipodozi na vitu mbalimbali linalofahamika kwa jina la ZuRii lililopo katika jengo la Dar Free Market lililopo katika barabara ya Alli Hassan Mwinyi  Jijini Dar es Salaam.

Akizindua duka hilo ambalo linamilikiwa na mwana Diaspora ambaye pia ni mwanalibeneke Jestina George, Magige alisema kwamba amevutiwa na namna Jestina alivyoweza kurudi na kuwekeza  nyumbani hali ambayo imeweza kuzalisha ajira kwa watanzania na kuwa mfano wa kuigwa.

“Kabla ya yote nachukua fursa hii kumpongeza  Jestina  kwani ameonesha  mfano  wa umuhimu wa kujiajiri hasa kwa wanawake pia huu ni mfano wa kuigwa  kwa wanadiaspora , wengine warudi na kuja kuwekeza nyumbani kwani fursa nyingi zipo hivyo waje wazitumie” alisema Magige.



Aidha alitoa rai kwa wanawake wengine hapa nchini ambao wanauwezo wa kuwa na mitaji ya kuanzisha biashara wajiajiri na kutoa ajira kwa wengine  pia natoa wito kwa watanzania wengine waje katika duka la ZuRii kuja kutoa sapoti kwa Jestina, alisema Magige.

Wakati huohuo mmiliki wa duka hilo la ZuRii Jestina  alisema kwamba yeye ameona  fursa za  kuwekeza nyumbani  hivyo ameamua kuzitumia ipasavyo.

RIDHIWANI AZINDUA VYUMBA VYA MADARASA SHULE YA MAGEREZA YA BWAWANI

$
0
0

 Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi jengo la vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari ya Bwawani katika Kijiji cha Visakazi Jimbo la Chalinze. Shule hiyo inamilikiwa na Jeshi la Magereza.
 Ridhiwani akiwa na maofisa wa jeshi hilo Kaimu Mkuu wa Magereza, Emmanuel Lwinga na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Kato Luganunulauu
 Ridhiwani akihutubia wakati wa hafla hiyo. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Shule hiyo,Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Emmanuel Lwinga na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Kato Luganunula

 Ridhiwani akiwa amekaa katika moja ya madawati yaliyomo katika moja ya vyumba vipya vya madarasa
 Ridhiwani akikagua jengo hilo jipya.

 
Ridhiwani akipanda mti wa kumbukumbu mbele ya jengo hilo.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Ridhiwani akivishwa skafu na mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Bwawani alipowasili katika shule hiyo leo
 Ridhiwani akiwa amekabidhiwa shada la maua
 Ridhiwani akikgua gwaride la wanafunzi wa shule hiyo lililoandaliwa maalumu kwa ajili yake
 Ridhiwani akilakiwa na maofisa wa Jeshi la Magereza

MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MAPINDUZI ZANZIBAR LEO

$
0
0
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein akiwasili kwenye uwanja wa Aman tayari maadhimisho ya sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar leo Januari 12, 2015.
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein akipokea salamu za kijeshi mara baada ya kuwasili kwenye uwanjwa wa Aman tayari maadhimisho ya sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar leo Januari 12, 2015.
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein akikagua gwaride la vikosi mbali mbali vya kijeshi wakati wa maadhimisho ya sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar,yaliyofanyika  leo Januari 12, 2015 kwenye uwanja wa Amani,Zanzibar.
 Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein akihutubia wananchi wakati wa maadhimisho ya sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar,yaliyofanyika  leo Januari 12, 2015 kwenye uwanja wa Amani,Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein kwa hotuba yake nzuri aliyoitoa kwenye maadhimisho ya sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar,yaliyofanyika  leo Januari 12, 2015 kwenye uwanja wa Amani,Zanzibar.

UKOSEFU WA KAZI KWA VIJANA NI JANGA LA DUNIA

$
0
0
DSC_0499
Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari (UTPC), Abubakar Karsan akionyesha gazeti la "Tuwasiliane" linalochapishwa na UTPC na kusambazwa kwa wadau na maeneo mbalimbali ya jijini Mwanza kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez aliyetembelea makao ya ofisi hizo kwa ajili ya mazungumzo na kuboresha ushirikiano baina ya Umoja wa Mataifa Umoja huo wa vilabu vya waandishi wa habari nchini.

WIMBI kubwa la kuwa na vijana wasiokuwa na kazi limeelezwa kuwa tatizo duniani kote na serikali mbalimbali zinatakiwa kuliangalia hilo kwa undani na kulitatua. Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez. Mratibu huyo alisema hayo katika mazungumzo yake na Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari (UTPC) Abubakar Karsan.

Alisema ukosefu wa kazi kwa sasa ni tatizo la kijamii na kwamba, shauri hilo lisipoangaliwa kwa makini linaweza kuwa chanzo cha matatizo makubwa ya usalama na amani katika taifa. Alvaro Rodriguez ambaye alifika katika ofisi za UTPC kuangalia mambo yanayofanyika katika ofisi hiyo wakati akiwa ziarani Mwanza wiki iliyopita, alisema kama tatizo la ajira litaendelea kuwapo, vijana wanaoathirika wanaweza kufikiria njia nyingine isiyo ya kistaarabu kufanikisha mambo yao.
DSC_0440
Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari (UTPC), Abubakar Karsan akizungumza na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) aliyeambatana na Mshauri wa masuala ya haki za binadamu kutoka ofisi ya mratibu mkazi wa UN Tanzania, Bi. Chitra Massey (kulia) alipotembelea makao makuu ya ofisi hizo jijini Mwanza.

Alisema Umoja wa Mataifa unaendelea kushirikiana na serikali mbalimbali kuhakikisha kwamba tatizo la ajira kwa vijana linamalizwa ili jamii isiingie katika mtafaruku utakaokosesha amani na usalama na hivyo kusimamisha maendeleo yaliyofikiwa katika jamii. Bila kutaja makundi ya kigaidi yanayotikisa dunia kwa sasa kama Al - Qaeda na washirika wake Boko Haram, Al - Shabab, Islamic State of Iraq na Levant (ISIL) alisema makundi mengi ya kigaidi duniani yanatokana na vijana kutojua wafanye nini na mazingira waliyonayo na hivyo kuwa rahisi kushawishika.

Alisema makundi ya hatari mara nyingi ni ya vijana ambao wanashindwa kupata riziki au hawajui wafanye nini kupata riziki na serikali zimewaacha bila kuwaangalia. Aidha alisema Umoja wa Mataifa utaendelea kusaidia kuhakikisha kwamba masuala muhimu yanayowezesha maendeleo kama demokrasia yanazingatiwa ili kuiwezesha jamii kufanya maamuzi sahihi ya vile wanavyotaka kupanga maendeleo yao.
DSC_0487
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu (kulia) akichangia jambo wakati wa mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari (UTPC) Abubakar Karsan makao makuu ya ofisi za umoja huo jijini Mwanza.
Alisema Demokrasia huwezesha wananchi kujua namna wanavyoweza kutengeneza mustakabali wao katika masuala ya ustawi wa jamii na maendeleo huku haki zao za msingi zikilindwa. Mapema Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC, Bw. Karsan alimwambia mratibu huyo mambo ambayo yamefanywa na umoja huo na changamoto walizokumbana nazo kwa kuzingatia mpango mkakati wake wa mwaka 2011-2013.

Umoja huo ambao ulianzishwa mwaka 1996 na kusajili na wizara ya mambo ya ndani kama taasisi isiyokuwa ya kiserikali (NGO) mwaka uliofuata, umefanikiwa kuanzisha mfuko wa kusaidia vyombo vya habari kwa jina la Daudi Mwangosi, aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari wa Iringa (IPC).
DSC_0481
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari (UTPC), Abubakar Karsan wakati wa mazungumzo ya kuboresha mahusiano baina ya mashirika ya umoja wa mataifa na umoja wa vilabu vya waandishi wa habari nchini Tanzania.

Aidha alimwambia kwamba wamefanikisha mafunzo ya kuongeza umahiri wa uandishi wa habari na pia kuwaelezea umma juu ya uhuru wa vyombo vya habari. Pia alielezea mafanikio yaliyopatikana katika kampeni za kuelimisha umma na kuelewana miongoni mwa wadau mbalimbali wa sekta ya habari.  Alisema hata hivyo bado wanaendelea na kampeni yao kutaka mabadiliko ya malipo kwa waandishi wa habari wanaojitegemea ambao ndio wanatoa mchango wa asilimia 75 hadi 80 za habari zinazotangazwa au kuchapishwa.

Aidha wanaendelea kutoa mafunzo ya kanuni na maadili kwa waandishi wa habari na kuendelea kukabiliana na tatizo la usalama katika mpango mkakati wa mwaka 2015 – 2019. Katika ziara hiyo ya kanda ya Ziwa, mratibu huyo aliambatana na mshauri mwandamizi wa masuala ya haki za binadamu Dk Chitralekha Massey na Mtaalamu wa mawasiliano wa umoja huo hapa nchini HoyceTemu.

WASANII WANAOTAKA KUSHIRIKI TAMASHA LA MUUNGANO DAY LA WASANII WA TANZANIA ,UJERUMANI WAJIANDIKISHE

$
0
0
Tamasha litafanyika mjini Koloni,Ujerumani  April 2015

Wasanii wanaotaka kushiriki katika katamasha la kongamano la wasanii wa Tanzania na afrika mashariki linalotarajiwa kufanyika mjini Kolon,Ujermani siku ya 8 November 2014 mnaombwa mjiandikishe kwa kuwasiliana katika namba ya simu  +49(0)15778645623 .
 
Tamasha hili linania ya kutangaza sanaa za maonyesho za Tanzania nchini ujerumani,wasanii wa ngoma za asili,Sarakasi,Maigizo, Muziki n.k mnakaribishwa kujiandikisha kushiriki Tamasha hili ,Wasanii mnaombwa mtumie nafasi hii kuonyesha vipaji vyenu 
katika uwanja wa kimataifa ili kujitangaza zaidi.
 
Ushiriki wenu katika tamasha hili ndio dira ya ukombozi kwa wasanii wote!
Maelezo zaidi piga  simu  +49(0)15778645623

NAFASI ZA MAFUNZO NA KAZI.

$
0
0
Taasisi   ya  Rafiki Elimu  Foundation  inatangaza  nafasi   za  mafunzo  yafuatayo :
1.     LISHE   BORA   NA  MASAJI   :
SIFA    ZA   MWOMBAJI:
1.     Awe  wa  jinsia  ya  kike
2.     Elimu  ya  kuanzia  kidato   cha  nne  na  kuendelea
3.     Uwezo  wa  kuwasiliana   kwa  ufasaha  kwa  lugha  za  Kiswahili  na  kiingereza.
4.     Awe  anaishi  jijini  Dar  Es   salaam.
5.     Awe   tayari  kufanya    kazi   kama  mtaalamu  wa  masaji .
WAHITIMU  WA  MAFUNZO   YA  MASAJI  WATAPATA   NAFASI  YA  KUFANYA  KAZI    KAMA  WATAALAMU   WA  MASAJI   KATIKA MRADI   WA  RAFIKIELIMU  FUND  RAISING   PROJECT.
 
2.     NGO  MANAGEMENT  & OPERATION  (  USIMAMIZI  NA UENDESHAJI  WA  TAASISI  ZISIZO  KUWA  ZA  KISERIKALI  )

SIFA   ZA   MWOMBAJI:
1.     Awe   na elimu  ya  kuanzia  kidato  cha  nne  na  kuendelea.
2.     Awe   anaishi  katika wilaya  yoyote  iliyopo  ndani  ya  Tanzania bara.
3.     Awe  na  uwezo  wa  kuwasiliana  kwa  ufasaha  kwa lugha  za  Kiswahili  na  kiingereza.
WAHITIMU  WA  MAFUNZO  YA  USIMAMIZI NA UENDESHAJI  WA  TAASISI  ZISIZO KUWA  ZA KISERIKALI, WATAPATA  NAFASI   YA  KUANZISHA,KUENDESHA  NA  KUSIMAMIA    TAASISI  ISIYOKUWA  YA  KISERIKALI.
·        Kwa  waombaji   kutoka  nje  ya  mkoa  wa  Dar  Es  salaam, mafunzo  yatatolewa    kwa  njia  ya  posta.

MOTISHA KWA YEYOTE ATAKAYEFANIKISHA KUKAMATWA KWA MTU ANAYEJARIBU KUTOROSHA MADINI NJE YA NCHI


TANZANIA NA SAUDI ARABIA KUSHIRIKIANA KATIKA UHIFADHI WANYAMAPORI

$
0
0
 Ujumbe wa Serikali ya Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb) katika mazungumzo na Mwana wa Mfalme wa Saudia Prince Bandar bin Saud bin Mohammad Al-Saud ambaye pia ni Rais wa Mamlaka ya Wanyamapori ya Saudi Arabia. Wengine katika picha kutoka kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Adelhem Meru; Balozi wa Tanzania Saudi Arabia Prof. Abdillah Omari; Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. James Lembeli; Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii Mhe. Peter Msigwa; Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi;Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Herman Keraryo na Afisa wa Ubalozi Ndg. Sufian.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb) akisisitiza jambo katika mazungumzo na Mwana wa Mfalme wa Saudia Prince Bandar bin Saud bin Mohammad Al-Saud ambaye pia ni Rais wa Mamlaka ya Wanyamapori ya Saudi Arabia.
 Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Adelhem Meru (kati) akiongea katika mazungumzo baina ya ujumbe wa Tanzania na Saudi Arabia. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. James Lembeli na kushoto ni Balozi wa Tanzania Saudi Arabia Prof. Abdillah Omari.
 Mwana wa Mfalme wa Saudia Prince Bandar bin Saud bin Mohammad Al-Saud ambaye pia ni Rais wa Mamlaka ya Wanyamapori ya Saudi Arabia akiongea katika mazungumzo hayo.

Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi akichangia jambo katika mazungumzo hayo. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Herman Keraryo; Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii Mhe. Peter Msigwa; Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. James Lembeli na Balozi wa Tanzania Saudi Arabia Prof. Abdillah Omari.
 Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (wa tatu kushoto) ukiwa katika picha ya pamoja na Mwana wa Mfalme wa Saudia Prince Bandar (wa nne kushoto) jijini Riyadh, Saudi Arabia. Wengine kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania Saudi Arabia Prof. Abdillah Omari; Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Adelhem Meru; Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii Mhe. Peter Msigwa; Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. James Lembeli; Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Herman Keraryo.
 Ujumbe wa Mwana wa Mfalme wa Saudi Arabia ukifuatilia mazungumzo hayo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (kulia) akiwa na mazungumzo na (kutoka kulia) Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Adelhem Meru; Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. James Lembeli na Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii Mhe. Peter Msigwa muda mfupi kabla ya kuanza kwa mazungumzo baina ya Tanzania na Saudi Arabia jijini Riyadh, Saudi Arabia. 

KONYAGI WATEMBELEA MASHAMBA YA WAKULIMA WA ZABIBU DODOMA AMBAO WATOTO WAO WANAFADHILIWA KIMASOMO

$
0
0
 Mratibu wa Mpango wa Kampuni ya Konyagi wa kuwasomesha watoto wa wakulima wa zao la zabibu kwa masomo ya Sekondari Saimon Chibehe (katikati), akitembelea hivi karibuni shamba la zabibu la Festo Kuziganika katika Kijiji cha Mbabara, mkoani Dodoma. Kulia ni mmoja wa wakulima wa eneo hilo, Juliana Masukwi. Watoto wa wakulima hao wameingizwa kwenye mpango huo.
 Festo Kuziganika mkazi na mkulima wa zabibu katika katika Kijiji cha Mbabara, Manispaa ya Dodoma akimuelekeza jambo Mratibu wa Mpango wa Kampuni ya Konyagi wa kuwasomesha watoto wa wakulima wa zao hilo kwa masomo ya Sekondari,Saimon Chibehe (kulia) aliyekwenda hivi karibuni kuwatembelea wakulima hao.
 Mratibu wa Mpango wa Kampuni ya Konyagi wa kuwasomesha watoto wa wakulima wa zao la zabibu kwa masomo ya Sekondari Saimon Chibehe (wa pili kulia), akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkulima Juliana Masukwi (kulia), kuhusu utunzaji wa zao hilo, alipotembelea hivi karibuni shamba hilo katika Kijiji cha Mbabara, mkoani Dodoma. Wa pili kushoto ni mmoja wa wakulima wa zabibu katika Kijiji hicho, Festo Kuziganika. Watoto wa wakulima hao wameingizwa kwenye mpango huo wa kulipiwa masomo.
 Mratibu wa Mpango wa Kampuni ya Konyagi wa kuwasomesha watoto wa wakulima wa zao la zabibu kwa masomo ya Sekondari Saimon Chibehe (katikati), akitembelea hivi karibuni shamba la zabibu la Festo Kuziganika katika Kijiji cha Mbabara, mkoani Dodoma. Kulia ni mmoja wa wakulima wa eneo hilo, Juliana Masukwi. Watoto wa wakulima hao wameingizwa kwenye mpango huo.
Mkulima Juliana Masukwi mkazi wa Mbabara A', mkoani Dodoma akimuonesha  mti wa mzabibu Mratibu wa Mpango wa kuwasomesha watoto wa wakulima wa zao hilo kwa masomo ya SekondariSaimon Chibehe (hayupo pichani), ambaye hivi karibuni alitembelea shamba lake lililomwezesha mtoto wake aanze kufadhiliwa na kampuni ya Konyagi kielimu kwa masomo ya sekondari.

RAIS KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM ZANZIBAR.

$
0
0
 Pichani kati ni Mwenyekiti wa CCM Taifa,Rais Dkt Jakaya Kikwete,akiwaongoza wajumbe (hawapo pichani) wa Kikao cha kawaida cha Kamati Kuu ndani ya ukumbi ya Afisi ya CCM makao Makuu Kisiwandui mjini Zanzibar,Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na shoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM,Dkt.Ali Mohamed Shein
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwakaribisha Wajumbe wa kikao cha kawaida cha kamati Kuu ya CCM,ndani ya ukumbi ya Afisi ya CCM makao Makuu Kisiwandui mjini Zanzibar
Wajumbe wa Kikao cha Kawaida cha Kamati Kuu ya CCM,wakiwa katika ukumbi wa Afisi ya CCM makao Makuu Kisiwandui mjini Zanzibar,tayari kwa kuanza kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho,Rais Dkt Jakaya Kikwete.
 Mwenyekiti wa CCM,Rais Dkt Jakaya Kikwete akipokelewa na  Katibu Mkuu wa CCM,Ndg.Abdulrahman Kinana alipokuwa akiwasili katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM,Kisiwandui mjini Zanzibar kabla ya kuanza kwa kikao cha kawaida cha Kamati Kuu ya CCM,kilichofanyika leo mjini Zanzibar.

 Katibu Mkuu wa CCM,Ndg.Abdulrahman Kinana akizungumza jambo na Makamu Mwenyekiti wa CCM,Dkt.Ali Mohamed Shein nje ya ukumbi kabla ya kuanza kwa kikao cha kawaida cha Kamati Kuu ya CCM,kilichofanyika leo katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM,Kisiwandui mjini Zanzibar.
Makamu wa Rais,Dkt.Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na Naibu katibu Mkuu CCM-Zanzibar Ndg.Vuai Ali Vuai alipokuwa akiwasili katika kikao cha kawaida cha Kamati Kuu ya CCM,kilichofanyika leo katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM,Kisiwandui mjini Zanzibar.
 Waziri Mkuu Mh.Mizengo Pinda akisalimiana na Naibu katibu Mkuu CCM-Zanzibar Ndg.Vuai Ali Vuai alipokuwa akiwasili katika kikao cha kawaida cha Kamati Kuu ya CCM,kilichofanyika leo katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM,Kisiwandui mjini Zanzibar.
 Makamu Mwenyeki wa Chama cha CCM Bara,Ndg.Philip Mangula akipokelewa wakati alipokuwa akiwasili katika kikao cha kawaida cha Kamati Kuu ya CCM,kilichofanyika leo katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM,Kisiwandui mjini Zanzibar.
 Baadhi ya Wanahabari wakiwa nje ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM,Kisiwandui mjini Zanzibar mapema leo
 Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM pichani kulia Ndg.William Lukuvi na shoto ni Ndg.Adam Kimbisa wakiwasili katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM,Kisiwandui mjini Zanzibar

Watendaji shughulikieni masuala nyeti ya Vijana: Yenza

$
0
0
 unnamed2 
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Deogratius Yenza akifungua semina ya Maafisa Vijana na Maafisa Ushirika wa Mkoa wa Dodoma kuhusu Sera ya Maendeleo ya Vijana, Mwongozo wa kupatiwa mkopo vijana kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na ujuzi inayotolewa na wawezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Kushoto ni Mwezeshaji Bibi Ester Riwa na katikati ni Afisa Maendeleo ya Vijana Mkoa wa Dodoma Bw. Tumsifu Mwasamale
unnamed3Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa kulia akizungumza na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Deogratius Yenza walipomtembelea ofisini kwake kabla ya kukutana na Maafisa Vijana na Maafisa Ushirika kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma kuwaelimisha kuhusu Sera ya Maendeleo ya Vijana, Mwongozo wa kupatiwa mkopo vijana kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, pamoja na ujuzi leo Mkoani Dodoma.
unnamed4 
Maafisa Vijana na Maafisa Ushirika wa Mkoa wa Dodoma wakifuatilia kwa makini yaliyokua yakiendelea wakati wa semina ya kuwaelimisha kuhusu Sera ya Maendeleo ya Vijana, Mwongozo wa kupatiwa mkopo vijana kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, pamoja na ujuzi leo Mkoani Dodoma.
………………………………………………………………………..
Watendaji wanaoshughulikia masuala ya Vijana Mkoa wa Dodoma wameshauriwa kuzingatia masuala nyeti yanayowahusu vijana kwa kuyapa kipaumbele kwani vijana ndio sehemu kubwa ya nguvu kazi ya taifa.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Deogratius Yenza alipokua akifungua semina ya Maafisa Vijana na Maafisa Ushirika kutoka Wilaya ya Kondoa, Bahi, Chamwino, Mpwapwa, Kongwa, Chemba na Dodoma Mjini kuhusu Sera ya Maendeleo ya Vijana na Mwongozo wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo Mkoani Dodoma.Bw. Yenza amewataka washiriki wa semina hiyo kusoma Sera ya Maendeleo ya Vijana ili waweze kushauri, kusimamia na kufuatilia shughuli za vijana na kuwajengea uwezo utakaowawezesha kujitegemea na kujiendeleza katika jamii wanayoishi.

“Maafisa Vijana wa kila wilaya muwe na tabia ya kuwajengea uwezo vijana wa wilaya zenu na kuwashauri katika shughuli wanazozifanya ili muweze kutathmini kuona vijana wanachangiaje katika pato la taifa hivyo kuwathamini na kuwaendeleza” amesema Bw. Yenza.

Akizungumza wakati wa ufunguaji wa semina hiyo mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa amewataka Maafisa Vijana na Maafisa Ushirika wa Mkoa wa Dodoma kuwaongoza vijana wawe na ari, uwezo na kujiamini katika kushiriki masuala ya kiuchumi na kijamii ili kuweza kuondokana na vijana tegemezi bali kuwa na vijana tutakaowategemea.

Aidha Kaimu Afisa Vijana wa Wilaya ya Chemba Bibi Madlina Kalinganira amesema kuwa kundi la vijana kwa sasa ni kubwa na pesa iliyotengwa katika Mfuko wa Maendeleo Vijana ni ndogo kufikia vijana wote hivyo kuiomba serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuongeza bajeti ya fedha katika Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ili vikundi vingine vya vijana vyenye ari na uwezo viweze kupatiwa mkopo huo.

Naye Afisa Ushirika Manispaa ya Dodoma Bw. Massawe Grayson ameiomba Wizara yenye dhamana na Vijana kuendeleza elimu ya kuwahamasisha vijana na kuwapa taarifa ya mfuko huo mara kwa mara kwani vijana wengi hawafikirii jinsi ya kuweka akiba kabla ya kupewa mkopo bali hufikiria kupatiwa mkopo mapema bila kuwa na malengo ya mkopo huo hivyo kuishia kutumia mkopo huo kiholela na kushindwa kurudisha pesa hizo kwa wakati.

BENKI YA EXIM YAIPIGA JEKI HOSPITALI TABORA

$
0
0
Kamanda kikosi namba 823 cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Msange , Meja A.A Ahmed (kulia) akipokea msaada kutoka kwa Meneja wa Benki ya Exim tawi la Tabora Bw. Edwin Polle (kushoto) ulioambatana na kitanda maalum kwa kina mama wajawazito jijini Tabora hivi karibuni. Wengine ni wawakilishi wa jeshi hilo na benki. unnamed2 
Kamanda kikosi namba 823 cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Msange , Meja A.A Ahmed (kulia) akipokea msaada kutoka kwa Meneja wa Benki ya Exim tawi la Tabora Bw. Edwin Polle (kushoto) ulioambatana na kitanda maalum kwa kina mama wajawazito jijini Tabora hivi karibuni. Wengine ni wawakilishi wa jeshi hilo na benki. Picha na mpiga picha wetu. unnamed 
Kamanda kikosi namba 823 cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Msange , Meja A.A Ahmed akizungumza kutoa shukrani kwa Benki ya Exim Tawi la Tabora baada ya benki hiyo kutoa msaada wa kitanda maalum kwa kina mama wajawazito jijini Tabora hivi karibuni. Kulia kwake Meneja wa Benki ya Exim tawi la Tabora Bw. Edwin Polle. Wengine ni wawakilishi wa jeshi hilo na benki. 
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live




Latest Images