Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 42 | 43 | (Page 44) | 45 | 46 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri Mkuu wa Denmark Mhe. Hell Thorning-Shmidt wakiangalia ngoma za utamaduni za kundi la JKT  katika dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu jana usiku.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Waziri Mkuu wa Denmark Mhe. Hell Thorning-Shmidt  katika dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu jana usiku.
   ais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi ya kinyago cha 'Shetani,  Waziri Mkuu wa Denmark Mhe. Hell Thorning-Shmidt  wakati wa dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu jana usiku
   Waziri Mkuu wa Denmark Mhe. Hell Thorning-Shmidt akiongea wakati wa dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jana usiku.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akigonganasha glasi ya kutakiana afya njema na  Waziri Mkuu wa Denmark Mhe. Hell Thorning-Shmidt  katika dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu jana usiku.

  Waziri Mkuu wa Denmark Mhe. Hell Thorning-Shmidt  akifurahia zawadi ya kinyago cha 'Shetani' alichopewa na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete jana usiku Ikulu.PICHA NA IKULU.


  0 0


   Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF.Juma Duni Haji amewataka Wazanzibar kuwa makini katika mchakato mzima wa Katiba Mpya.

  Hayo aliyasema leo huko katika uwanja wa mkutano magogoni wakati akiwahutubia wananchi wa jimbo hilo . Alisema kuwa wazanzibar wakae pamoja kuweza kutafakari kupata katiba iliyobora wao na vizazi vijavyo 

  Aidha alisema katiba mpya itakuwa ina nguvu na ndio katiba mama hivyo wananchi wasikubali kutumiwa na watu wachache kwa masilahi yao .  “tunataka nchi yetu kama iliyokuwa 1964 yenye mamlaka yake kamili alisema Babu Duni.

  Aidha alisisitiza kuwa wazanzibar lazima watetee nchi yao kwanza na Dunia itaheshimu maamuzi ya wananchi ambayo wanayataka . Alisema kuwa Masheha wa shehia mbali mbali wawe walimu kwa wananchi ili kuelimisha wananchi wao isiwe ni miongoni mwa kuwapotosha .

  Duni aliwataka wananchi kusimama kidete kuokoa nchi yao ambayo wao wameridhi kwa wazee wao na wao waweza kuwasaidia virembwe na vijukuu vyao ili kuikuta na kuweza kuitumia nchi hii ya Zanzibar

  Alisema kuwa wasikubali kutekwa nchi yao iwe huru na yenye mamlaka kamili  nje na ndani ya nchi bila ya kuingiliwa na nchi nyengine

  Nae Mbunge wa Jimbo la Magogoni Hamad Ali Hamad ameeleza kuwa ataendeleza kutekeleza ahadi zake mbali mbali alizoahidi yeye pamoja na mwakilishi na diwani katika kuiletea maendeleo jimbo lao la magogoni .

  Alisema katika ahadi hizo baadhi wamekwisha zitekeleza ikiwemo kuwapatia wananchi maji safi na salama kujenga madarasa mbali mbali .kuvichangia vikundi mbali mbali vya akinamama na kadhalika.

  Na Khadija  Khamis –Maelezo Zanzibar  .

  0 0


  Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu ambao ni kusanyiko la zaidi ya asasi 70 za kiraia  zinazotetea haki za binadamu (THRD-Coalition) , kwa kushirikiana na Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habati Tanzania (UTPC) pamoja na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini kwa Africa (MISA-Tan) tunalaani vikali shambulio la kinyama alilofanyiwa mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda usiku wa kuamkia jana Jumatano tarehe 6 Machi, 2013.

  Bw. Kibanda alivamiwa wakati alipokuwa anarudi nyumbani kwake Mbezi juu. Watu hao walimteka na kisha wakamtesa kinyama kwa kumng’oa meno, kucha,  kidole na kuliharibu vibaya sana jicho la upande wa kushoto. Huu ni ukatili, unyama dhidi ya utu wa binadamu. Baada ya kutekeleza azma yao walimtupa umbali wa mita 30 toka alipokuwa amepaki gari lake.

  Uchunguzi tulioufanya bado haujatujapatia habari za undani zaidi na za uhakika wa tukio hilo. Lakini kwa taarifa za awali kwa asilimia kubwa  linahusiana na kazi yake ya utetezi wa haki za binadamu kupitia katika taaluma yake ya uandishi wa habari. Hii ni kwa sababu pia tayari alishafunguliwa kesi mahakamani inayohusu uandishi wake.

  Tunasema hivyo kwa sababu vitisho dhidi ya wanahabari na watetetezi wengine wa haki za binadamu vinataka kuzoeleka sasa hapa nchini jambo ambalo halikuwapo katika miaka ya nyuma. Takribani ndani ya miezi 10 sasa zaidi ya watetezi wa haki za binadamu 10 wakiwamo waandishi wa habari  wameshajeruhiwa,  wamepata vitisho  au kuuwawa.

  Matukio haya yanaashiria lengo la kutaka kuzima sauti za watetezi wa wanyonge kwa visingizio mbali mbali huku matukio ya aina hii wakati mwingine yakipewa sura tofauti tofauti ikiwamo uhalifu wa kawaida, visa vya kudhulumiana na  visasi vya kimapenzi. Ni dhahiri wanaofanya hivyo wana malengo mabaya ya kuchafua jina na taswira nzuri ya nchi yetu  katika Jamii ya Kimataifa kwa malengo binafsi.

  Wakati tukio hili linapojitokeza sasa, bado Mtandao wetu unafuatilia kwa karibu kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi na mazingira ya kukamatwa na kuhojiwa kwa waandishi wa gazeti la Tanzania Daima kulikofanywa na Jeshi la Polisi hivi karibuni kwa kile kilichoitwa kwamba ni kuandika habari za uchochezi.

  Tunajiuliza je nini Jeshi la Polisi na Serikali kwa ujumla wamelifanya kuhusiana na kutekwa na kuteswa kwa Dkt Ulimboka zaidi ya Kulifungia Mwanahalisi ambalo lilijitoa mhanga kuchunguza suala hili? Ndugu Kibanda katekwa na kufanyiwa kile kile alichofanyiwa Ulimboka, Je tume iliyoundwa  itaanzia kwa Ulimboka ama itarukia moja kwa moja tukio hili ambalo ni muendelezo wa matukio lukuki dhidi ya watetezi wa haki na waandishi kwa ujumla.


  Hatupendi kuingilia wala kukwamisha utendaji kazi wa jeshi hilo, lakini pia hatupendi wanahabari na watetezi wengine wafanye kazi yao katika mazingira ya woga. Tunaamini kwamba zipo njia muafaka zaidi za kushughulikia masuala yanayohusu taaluma ya habari. Kwa mfano lipo Baraza la Habari Tanzania (MCT) ambalo linajukumu ya kusuluhisha migogoro inayohusiana na taaluma hiyo na iwapo itashindikana basi mhusika au wahusika bado wanakuwa na nafasi ya kwenda mahakamani.

  Kinachoshangaza ni kuona kwamba Jeshi la Polisi limefikia mahali pa kwenda kuwakamata waandishi na wahariri waTanzania Daima ndani ya chumba chao cha  habari na kuwakagua hadi katika makazi yao na kuchukua nyaraka kadhaa kama ilivyotokea kwaa Bw. Josephat Isango.

  Hali hiyo ya mahojiano ya kushtukiza na kuogofya imefanyika pia kwa wahariri Charles Misango na Edson Kamukara wote wa gazeti hilo, ambapo hatima yao bado haifahamiki mpaka sasa. Hali hii inaweza kusababisha woga kwa wanataaluma wengine na hivyo kuleta athari kubwa katika sekta ya habari nchini.

  Waandishi hao kwa sasa wanaishi kwa woga. Je kwanini tufikie hatua hii ya kufanya wenzetu waishi  kwa hofu kama swala kwenye mbuga iliiyojaa simba?. Je ulinzi wa vyombo vya usalama upo kwa ajili ya nani? Kwanini wengine wauawe, watekwe, wateswe na kudhalilishwa  huku vyombo vya usalama vikichukulia ni jambo la kawaida na kutupiana mpira?

  Rai Yetu
  1.     Tunawataka watu wote  wanaotumika au wanaoendeleza wimbi la mashambulizi kwa wanahabari na watetezi wote wa haki za binadamu kwa ujumla, waache kufanya hivyo kwani wataliingiza nchi katika machafuko makubwa.
  2.    Tunalisihi Jeshi la Polisi na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kubeba jukumu lao la kuhakikisha usalama wa watetezi wa haki za binadamu, na raia na watu wote waliomo ndani ya mipaka ya nchi hii kwa ujumla bila ubaguzi.
  3.    Tunaomba uchunguzi wa kina ufanyike ili kubaini wahusika wa mtindo huu wa kuteka kutesa na kutelekeza kwani tukio hili la Kibanda linashabihiana kwa kiwango kikubwa na lile la Dkt Stephen Ulimboka.
  4.    Tunaiomba jamii yote ya watu waliostaarabika, makundi mbalimbali kutuunga mkono katika jitihada zetu la kupigania amani, haki na uhuru kwa watu wote hasa hasa watetezi wa haki za binadamu na waandishi  wa habari.
  5.    Tunawakumbushia waandishi wa habari kujitahidi kupata mafunzo ya usalama ambayo yanaratibiwa na kutolewa na Mtandao huu wa watetezi.
  6.    Vyombo vyote vya habari  na  waandishi kwa ujumla wazidi kuwa pamoja katika kipindi hiki kigumu cha kuelekea chaguzi za serikali za mitaa mwakani pamoja na uchaguzi mkuu 2015. Pia wajieupushe na makundi ya kisiasa ili kujiweka vizuri katika kufanya kazi zao kwa kufuata misingi ya taaluma zao.

  Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania!

  Imeletwa kwenu na

  sign.png
  Onesmo Olengurumwa
  Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa
  Haki za Binadamu Tanzania (THRD-Coalition)
  K.n.y Watetezi Wote wa Haki za Binadamu Tanzania 
  -- 

  0 0
 • 03/07/13--12:39: 16th ZIFF- FILM SUBMISSION

 • Inline image 1


  0 0  Join the Dar-es-Salaam Cycle caravan to raise awareness about sickle cell disease in Tanzania.

  From Mnazi Mmoja grounds Dar es Salaam, through Bibi Titi Rd, Ali Hassan Mwinyi, Kawawa, Uhuru then Mnazi Mmoja.

  On Sunday 10th March 2013,8am till Noon

  It is not a competition, it is a slow ride. All bicycles, disabled, normal, cargo bikes, children, elders, youths, roller blades and skateboards are all welcome.

  Come and help promote donations for the Sickle Cell Foundation of Tanzania.
  3 Brand New Bicycles will be given away as part of a raffle, plus plenty of other prizes too! Hire a bicycle for Tsh 25,000 or buy a jacket for 5,000 and win yourself a prize from Afriroots.  All the profits from the sale go to the Sickle Cell Foundation of Tanzania  http://lms.muhas.ac.tz/sicklecelltz

  To be part of the event: Call Now on 0713 652 642/ 0714 132 782 or Email: 
  uwabadar@yahoo.co.uk

  From January to May 2013, Alan Knight is riding the Tour d'Afrique Cycle Adventure which crosses the African Continent from Cairo to Cape Town, over a distance of 11,718km. He is hoping to raise Tsh 80 Million to help build a Centre for Sickle Cell Disease in Tanzaniahttp://alanknighttourdafrique.com

  Join him in Dar es Salaam to support the fund raising event and Cycle for Sickle Cell

  0 0
 • 03/07/13--12:59: MISA YA KUMBUKUMBU

 • CHARLES PIUS LUKAMILWA
  Mwaka mmoja umepita (8 Machi 2012) tangu utangulie katika makazi yako ya milele. Tunakumbuka upendo, ucheshi na mapenzi yako kwetu sisi sote hasa watoto wako Christina na Sindy. "Tulikupenda sana lakini Mungu alikupenda zaidi. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe"
  Kwa kumbukumbu hii, Familia ya Marehemu Donati Kezirahabi na Bibi Hidaya Kezirahabi Wanawakaribisha ndugu, jamaa na marafiki kwenye misa ya kumbukumbu ya kijana wao mpendwa itakayofanyika nyumbani Mbezi Luisi Dar es Salaam siku ya Jumamosi (9 Machi 2013) kuanzia saa tano asubuhi.
  Wote mnakaribishwa.
  Taarifa zaidi wasiliana nasi 0716838188 au 0758868628

  0 0


  Moja ya shughuli maalum iliyompeleka Mhe. Thorning-Schmidt kijijini Lepurko ni kuzungumza na kina mama na kusikiliza matatizo na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika maisha yao ya kila siku kama anavyoonekana.
  Mmoja wa kina mama katika Kijiji cha Lepurko akimweleza Mhe. Thorning-Schmidt matatizo yanayowakabili wanawake wa kikiji hicho ikiwa ni pamoja na uhaba wa maji na elimu bora kwa watoto wao.
  Moja ya nyumba  maarufu kama "Boma" zilizopo kijijini hapo
  Mhe. Thorning-Schmidt akimsikiliza mmoja wa watoto wa kike ambaye ni mwanafunzi katika kijiji hicho.
  Mhe. Thorning-Schmidt akihutubia wananchi (hawapo pichani) wa Kijiji cha Lepurko.
  Mhe. Thorning-Schmidt akiangalia bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa kwa shanga na kina mama wa kijijini hapo.
  Mmoja wa kina mama wa Kijiji cha Lepurko akimvisha ushanga Mhe. Thorning-Schmidt.
  Sehemu ya Wananchi wa Kijiji cha Lepurko wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mhe. Thorning-Shmidt (hayupo pichani) ambapo aliahidi kuwasaidia katika kutatua tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama.
  Mhe, Thorning-Schmidt akitoka ndani ya nyumba "Boma" aliyoitembelea kijijini hapo.
  Mhe. Thorning-Schmidt akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Mhe. Edward Lowassa  mara baada ya kuhitimisha ziara yake katika kijiji cha Lepurko.picha zaidi bofya hapa

  0 0

  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete akifungua kitambaa na baadaye akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi kisima cha maji kilichochimbwa katika hospitali ya mkoa wa Mwanza, Sekou Toure,kwa msaada wa kampuni ya bia ya Serengeti. Kisima hicho kimegharimu shilingi milioni sabini. Kushoto kwa mama ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ndugu Paschal Mabiti na kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kampuni ya bia ya Serengeti Jaji Mark Bomani na wamwisho ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dr. Valentino Bangi.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisaidiana na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dr. Valentino Bangi  kumtwisha ndoo ya maji ndugu Getrude Ndaweka ambaye ni afisa muuguzi katika hospitali ya Sekou Toure wakati wa sherehe za uzinduzi wa kisima cha maji hospitalini hapo tarehe 
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifungua koki ya maji wakati wa kuzindua rasmi kisima cha maji katika hospitali ya mkoa wa Mwanza, Sekou Toure .
  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, Mama Salma Kikwete akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi kisima cha maji kilichochimbwa katika hospitali ya mkoa wa Mwanza, Sekou Toure.

   Mwenyekiti wa WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikewte akimjulia hali mtoto Juma Joseph, 6 , kutoka katika kijiji cha Karumo, wilayani Sengerema aliyelazwa katika hospitali ya Sekou Toure jijini Mwanza akisumbuliwa na ugonjwa wa malaria`.
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na wafanyakazi na wananchi wa jiji la Mwanza waliohudhuria shaerehe ya kuzindua kisima cha maji katika hospitali ya Sekou Toure

  Mwenyekiti wa WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikewte akiwahutubia mamia ya wafanyakazi na wananchi wa jiji la Mwanza baada ya kuzindua rasmi kisima cha maji katika hospitali ya Sekou Toure leo. PICHA ZOTE NA JOHN LUKUWI

  0 0

  Bingwa wa Taifa mchezo wa Masumbwi nchini, Japhet Kaseba Katikati akilishwa keki na mwanae Suzan Kaseba wakati wa sherehe ya mtoto huyo kutimiza miaaka 11 iliyofanyika katika shule ya msingi St. Joseph.  Dar es alaam juzi kulia ni mama yake mzazi Wema Kaseba nae akilishwa keki hiyo.
  Mtoto Zuzan Kaseba akimlisha keki mama yake Wema Kaseba wakati wa kushelekea sikukuu yake ya kuzaliwa iliyofanyika shuleni kwao St. Joseph.  katikati ni baba yake mzazi Japhet  Kaseba bingwa wa taifa wa mchezo wa masumbwi nchini
  Baba na Mama wakiwa katika picha ya pamoja.

  Bingwa wa ngumi za kulipwa uzito wa kati Japhet Kaseba (kulia)  akiwa amemshika mtoto wake Suzan Kaseba wakati wa sherehe ya mtoto huyo kutimiza umri wa miaka 11 iliyofanyika shuleni kwao wengine ni mama yake mzazi Wema Kaseba (shoto) pamoja na wanafunzi wanaosoma nao darasa moja katika shule ya msingi St. Joseph .

  0 0
 • 03/07/13--22:41: tangazo.


 • 0 0

  Mshindi wa Tigo smart card promotion Bw.Julius Kanza akiwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius K Nyerere akitokea Hispania alikoenda kushuhudia mechi kati ya Real Madrid na Fc Barcelona iliyopigwa mwishoni mwa wiki iliyopta safari hiyo iligharamiwa na kampuni ya simu za mkononi Tigo.

  0 0

  MWIMBAJI wa muziki wa Injili kutoka Zambia, Ephraim Sekeleti amethibitisha kushiriki tamasha la Pasaka litakalofanyika Sikukuu ya Pasaka Machi 31 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

  Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ambaye ni Mkurugenzi wa Msama Promotions, waandaaji wa tamasha hilo, Sekeleti amekubali kushiriki baada ya mashabiki wengi kumpendekeza.


  Msama alisema Dar es Salaam jana kuwa mwimbaji huyo wa nyimbo za kumsifu Mungu anatamba na albamu mbalimbali zikiwemo Acha Kulia na Mungu Mwenyewe. Baadhi ya nyimbo zilizomo kwenye albamu hizo ni Uniongoze na Kidonge cha Yesu. Wasanii wengine ambao tayari wamethibitisha ushiriki wao ni Upendo Nkone na Rose Muhando kwa Tanzania, wakati wan je ya Tanzania ni Solomon Mukubwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) anayeishi Kenya.


  Tamasha la Pasaka litafanyika Dar es Salaam Machi 31 na  litaendelea Aprili mosi kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati Aprili 3 ni Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Tamasha la mwaka jana baadhi ya waimbaji mahiri waliokuwepo ni Rose Muhando, Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava, Ephraim Sekeleti na kundi la Glorious Celebration.

  Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilikuwa miongoni mwa burudani zilizokuwepo siku hiyo.

  0 0

    Washiriki wa Miss Utalii Tanzania Fainali za Taifa 2012/13 wakiwa katika mazoezi ya nguvu ya kujiandaa na Shindano lao la Vipaji ndani ya Ukumbi wa Dar Live.
  Washiriki wa Miss Utalii Tanzania Fainali za Taifa 2012/13 wakiwa katika picha ya pamoja Ukumbi wa Dar Live.
  ======  =========== ============


  MISS UTALII TANZANIA VIPAJI 2012/13 KUPATIKANA KESHO DAR LIVE

  Shindano la Taifa la Miss Utalii Vipaji 2012/13  linafanyika kesho katika ukumbi wa Dar Live Mbagala, ambapo Warembo  40 kutoka Tanzania Bara, Zanzibar na Kanda Maalum vyuo Vikuu Tanzania , watapanda stejini kushindana kucheza Ngoma za asili  kutoka Mikoa ambayo wanawakirisha,watapita na mavazi mbalimbali.

  Katika shindano hilo mbali na Burudani kutoka kwa Warembo wa Miss Utalii Tanzania 2012/13  kutakuwa na Burudani zaidi za Ngoma za Asili, Muziki wa kizazi Kipya pamoja na Burudani kutoka kwa Mwanamuziki wa Kimataifa Che Mundugwao, Atakuwepo pia mwanamuziki chipukizi wa Bongo Flava Dogo Genius ambeye ametokea kuwa mpinzani mkubwa wa Dogo Janja na Asley.

  Shindano hili ni la awali ambalo litapata Mshindi wa Vipaji kabla ya kufanyika fainali kuu ambalo litampata Miss Utalii Tanzania litakalo Fanyika Tarehe 17.03.2013 katika ukumbi wa Dar Live. Mshindi wa Tuzo hilo la Vipaji atajipatia zawadi ya Kusomeshwa Bure katika ngazi ya Cheti au Diploma kulingana na Sifa zake. Mshindi wa Mwaka jana na ambaye anashikiria taji Hilo kwa sasa ni Daisy Msumbusi Miss Utalii Kutoka Mkoa wa Kagera.

  Katika Shindano hilo , ulinzi utakuwa umeimarishwa ambapo kutakuwa na Polisi na Ninja, usalama wa Magari pamoja na vitu vyote  utakuwa ni wakutosha, kutakuwa na eneo la kutosha la kuegesha Magari na walinzi muda wote watakuwepo katika eneo hilo.

  Viingilio katika Shindano hilo itakuwa kama ifuatavyo, Viti vya kawaida Tsh 5,000 na Viti Maalum 10,000

  0 0


  0 0

   Mlinzi wa Chipukizi, Leon Kimath (kushoto)  akipambana na mshambuliaji Juma Faki wa KMKM.  Timu zilitoka sare bila bila.
    Wachezaji wa Chipukizi na KMKM wakiwania mpira.
  Wachezaji wa KMKM na Chipukizi wakichuana kuwania mpira kwenye uwanja wa Amaan jana. Pambano la ligi kuu ya Grand Malt ya Zanzibar kati ya KMKM na Chipukizi kwenye uwanja wa Amaan jana ambapo timu hizo zilitoka nguvu sawa bila kufungana. 

  0 0


  Mmiliki na Mweneshaji wa kipindi cha 'Ongea na Janet' Bi. Janet Sosthenes Mwenda. Sasa ‘Ongea na Janet’ inaonyeshwa katika Dstv kufuatia kuingia nao mkataba.

  MO BLOG:Tulishuhudia uzinduzi wa ‘Ongea na Janet’ tukaanza kuona vipindi vikienda hewani hebu tuweke wazi yapi mafanikio uliyopata mpaka sasa..?

  JANET: Mafanikio nilianza kuyaona kwenye vipindi 13 tu vya mwanzo ambavyo vilitengeneza ‘Season One’. Nashukuru Mungu ‘Ongea na Janet’ ilijulikana haraka sana, ikapata watazamaji wengi, ‘comments’ nazo zikawa nyingi, ‘changes’ zikawa nyingi nikajikuta kila ninapokwenda siitwi tena Janet naitwa ‘Ongea na Janet’.

  Hilo lilikuwa ni fanikio la kwanza kwamba niliondoka kwenye media muda mrefu na niliporudi nikapokewa vizuri kwa hiyo nawashukuru kwanza watanzania wenzangu kwa hilo, nawashukuru sana mashabiki wa Janet kwa kunipa ‘love’ ukweli.

  Lakini pia fanikio lingine lilikuja kujitokeza ambalo sikulitegemea kwa kipindi kile lilikuja kama ‘surprise’ kwangu kwani nikiwa sina hili wala line nikapata simu kutoka MNet-Dstv Nairobi wakaniambia kwamba shoo yangu wameipenda na wataichukua, wakati huo nikuwa nimesha ‘apply’ siku nyingi sana mpaka nimesahau.

  Wakanipa na ‘amount’ nikakubali wakaniuliza unazo ngapi? Wakati huo ndio nimemaliza ‘Season One’ nikawaambia ziko 13 wakasema wangependa kama zingekuwa 26 nikasema sawa nitakaporudi ‘Season Two’ nitawapatia wakakubali.

  Hivyo niliporudi ‘Season Two’ nikawa nimeingia kibiashara zaidi na Dstv wakawa wameni-‘support’ nikaweza kubadilisha set up nzima ya ‘Ongea na Janet’ na wakanipa hamasa zaidi na nikapata nafasi ya kuitangaza nchi yangu kwa na kwa sababu naoneka katika nchi nane (8) tofauti.
  Pia nikagundua moja kwa moja kuwa sasa nimeingia kwenye ‘competition’ na watu nane wanaoziwakilisha nchi zao kwa maana ya kwamba Tanzania iko kwenye ‘competition’ ya‘talk show’ na nchi nane za Afrika. Mashabiki wangu nataka niwaambie kwamba nitajitahidi kuboresha kazi zangu na natamani Talk Show bora East and Central Africa itoke Tanzania.

  Mmiliki na Mwendeshaji wa Kipindi cha Ongea na Janet Bi. Janet Sosthenes Mwenda katika moja ya vipindi walivyofanya na Bondia maarufu nchini Tanzania Japhet Kaseba.
  MO BLOG: Ni nchi zipi ambazo ‘Ongea na Janet’ inaonekana Afrika..?

  JANET:‘Ongea na Janet ‘ inaonekana hapa nyumbani Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi, Sudan Kusini, Malawi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), hivyo naweza kusema ‘Ongea na Janet’ bado ina kazi kubwa ya kufanya si kwa ajili yangu bali kwa ajili ya watanzania wote.
  MO BLOG: Baada ya kuingia mkataba na Dstv nini kilifuata..?

  JANET: Baada ya kuingia mkataba nao fanikio la kwanza ilikuwa ni kubadilisha ‘set up’ ya kipindi kama nilivyosema na fanikio lingine ambalo lilikuwa ni ndoto yangu ya siku nyingi ni kuanzisha kampuni yangu mwenyewe ambayo itafanya vitu ambavyo natamani kuvifanya na tayari nimeshaifungua.
  ‘Soon’ itaanza ku-produce yenyewe kipindi cha ‘Ongea na Janet’, lakini sasa hivi tuko kwenye production ya kipindi kingine ambacho ni product ya ‘Ongea na Janet’ kwa hiyo watanzania wakae katika mkao wa kula kwani nitawaletea vipindi vingine viwili japo sita tangaza mimi.
  Kwa sasa hivi kampuni yangu inafanya ‘production’ kwa hiyo nimekuwa na Media House, kwa mfano ukija na movie yako tunakurekodia, ukiwa na series zako tunakurekodia, dokumentari yako tunakutengenezea.

  Kitu kingine namshukuru Mungu Dstv wamezidi kunifungulia milango kwani wamenifanya kuwa ‘agent’ wao kwa hapa nyumbani Tanzania. Kwa hiyo nimekuwa katikati ya mpishi na mlaji upande wa filamu, series na vipindi kwa hiyo kama kuna mtu sasa hivi ana kipindi anataka kiende Dstv anakileta kwangu, sisi tunakihariri upya, tunakifanyia ‘sub title’ kisha tunakipeleka Dstv.
  Ilimradi hiyo kazi iwe ni ya kwake mwenyewe na ameisajili COSOTA.
  Kusoma Mahojiano yote Bofya Hapa

  0 0

   Mwakilishi wa Vodacom Tanzania Bw.Nguvu Kamando, (Kulia), akiweka saini makubaliano ya pamoja ya kampuni nne za simu za mkononi, kushiriki mfuko wa mawasiliano ya umma jijini Dar es Salaam . Katika mkataba huo makampuni ya Tigo, TTCL, Airtel ambapo Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa Mnyaa,(Watatu kulia waliosimama),  alishuhudia.
   Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa Mnyaa,akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusiana na makampuni ya simu za mkononi Vodacom  Tanzania.Airtel,Tigo,TTCL  kuweka saini makubaliano ya pamoja ya kushiriki mfuko wa mawasiliano ya umma.
    Baadhi ya wawakilishi wa kampuni za simu za mkononi wakimpigia makofi ,Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa Mnyaa,mara baada ya kumaliza kutoa spichi yake wakati wa kuweka saini  makampuni ya simu za mkononi Vodacom Tanzania,Airtel,Tigo,TTCL kuhusiana na  makubaliano ya pamoja ya kushiriki mfuko wa mawasiliano ya umma.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Kamugisha Kazaura (Kushoto)Mwakilishi wa Vodacom Tanzania, Nguvu Kamando, akizungumza  baada ya hafla ya kusaini mkataba wa ushiriki wa mfuko wa mawasiliano ya umma, jijini Dar es Salaam, ambapo makampuni manne ya simu za mkononi yameshiriki. Makampuni hayo ni Vodacom Tanzania, Tigo, TTCL na Airtel .

  0 0

   Rais Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na ujumbe wa Airtel pamoja na Waziri wa Sanyasi, Mawasiliano na Tekenolojia, Profesa Makame Mbarawa. PICHA NA IKULU

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete jana jioni amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Bharti Airtel ya India Bw. Sunil Mittal aliyemtembelea na ujumbe wake kuzungumzia maswala mbalimbali ya sekta ya Mawasiliano. Bw. Mittal aliongozana na Bw. Manoj Kohli, CEO Internationa wa kampuni hiyo, Bw. Jayant Khosla, CEO Anglophone Africa, Bw. Sam Elangallor, Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania anayemaliza muda wake, Bw Sunil Colaso, Mkurugenzi Mkuu mpya wa Airtel Tanzania pamoja na Bi Beatrice Singano, Corporate Affairs Director  wa Airtel Tanzania.

  Katika mazungumzo hayo ujumbe wa serikali ulikuwa ni pamoja na Waziri wa Sanyasi, Mawasiliano na Tekenolojia, Profesa Makame Mbarawa, Mwenyekiti wa CHC Profesa Marcelina Chijoriga, Kaimu Mtendaji wa CHC Bw. Dome Malosha, Msajili wa Hazina Mama Mlaki na Mhandisi Clarence Isokeleza.


  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mwenyekiti wa kampuni ya Airtel India Bw. Sunil Mittal alipokutana naye Ikulu, Dar es salaam, jana jioni
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na ujumbe wa Airtel na wa Serikali jana jioni Ikulu Dar es salaam
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mwenyekiti wa kampuni ya Airtel India Bw. Sunil Mittal alipokutana naye Ikulu, Dar es salaam, jana jioni


   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa kampuni ya Airtel India Bw. Sunil Mittal alipokutana naye Ikulu, Dar es salaam, jana jioni
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa kwa Mkurugeni Mkuu mpya wa Airtel Tanzania Bw Sunil Colaso na aliyemaliza muda wake Bw Sam Elangallor (kulia)

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mwenyekiti wa kampuni ya Airtel India Bw. Sunil Mittal alipokutana naye Ikulu, Dar es salaam, jana jioni
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu mpya wa Airtel Tanzania Bw Sunil Colaso

  Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania aliyemaliza muda wake Bw. Sam Elangallor

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mwenyekiti wa kampuni ya Airtel India Bw. Sunil Mittal alipokutana naye Ikulu, Dar es salaam, jana jioni

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua kwa kipindi kingine Balozi Christopher Liundi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa-Arusha (AICC).

  Aidha, kufuatia uteuzi huo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Kamillius Membe (Mb.) amewateua Wajumbe wa Bodi hiyo kama ifuatavyo:-

  Bw. Aggrey Mlimuka
  1. Bw. Dash-Hood Mndeme
  2. Dkt. Ali Mndali
  3. Mhe. Balozi Abdi Mshangama (Mstaafu)
  4. Mhe. Faith Mtambo (Mbunge wa Viti Maalum)
  5. Mhe. Dkt. Hamis Kigwangala (Mbunge wa Nzega)
  6. Mhe. Mary Chatanda (Mbunge wa Viti Maalum)
  7. Mhe. Ali Mzee Ali, (Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi - Zanzibar)
  8. Bw. Wilson Masilingi (Mbunge Mstaafu)

  Uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe hao ni kwa kipindi cha miaka mitatu (3) kuanzia tarehe 06 Machi, 2013.
     
  IMETOLEWA NA: WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM

  8 MACHI, 2013

  0 0

   Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angellah Kairuki (katikati) akifafanuliwa jambo na Mh.Sofia Mwaipopo (kushoto) Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Mwanzo Magomeni wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea mahakama hiyo jana jijini Dar es salaam.Hapo waliposimama ni jengo la mahabusu la Mahakama hiyo. Aliyeko kulia ni  Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Kinondoni Mh. Aniceta Wambura.
  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh: Angellah Kairuki (mwenye nguo ya njano) akioneshwa kiwanja kitakachojengwa Mahakama ya Mwanzo Kawe wakati wa ziara yake ya kutembelea Mahakama za Mwanzo jijini Dar Es Salaam iliyomalizika jana. Wa kwanza kushoto ni Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Kinondoni Mh. Aniceta Wambura na wapili kushoto ni Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Kawe Mh. Mary Katabi.

older | 1 | .... | 42 | 43 | (Page 44) | 45 | 46 | .... | 1898 | newer