Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 41 | 42 | (Page 43) | 44 | 45 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Pichani ni Ndugu Absalom Kibanda akiwa amelazwa kwenye moja ya chumba cha matibabu,hospita ya Taifa Muhimbili.Get Well soon Absalom Kibanda.Picha kwa hisani ya Mtandao wa Mabadiliko.

  Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri,na Mhariri Mkuu wa Mtendaji wa New Habari Coperations Ltd, Ndugu Absalom Kibanda, amevamiwa usiku  wa kuamikia leo akiwa anashuka nyumbani kwake Mbezi Beach na watu wasiofahamika na kumpiga kichwani. Amepata majeraha Makubwa kichwani na hasa jichoni,aidha taarifa inaeleza kuwa baada tukio hilo Kibanda alikimbizwa hospitali ya Taifa Muhimbili kwa Matibabu.

  Wadau hii ni taarifa ya kushtua sana,lakini tutazidi kutaarifiana kadiri ya habari zitakavyokuwa zinapatikana,kikubwa tumwombee Mungu amponye haraka mpiganaji mwenzetu.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Gabriel Tupa, wakifurahia kwa pamoja baada Makamu kuweka Jiwe la Msingi katika mradi wa ujenzi wa Nyumba za Watumishi wa Umma, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jana Machi 5, 2013 Wilaya ya Musoma, Mkoa wa Mara, wakati Makamu akiwa katika ziara yake ya siku mbili mkoani humo.
  Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakisikiliza maelezo na kuoneshwa Ramani za ujenzi wa nyumba za watumishi wa Umma, wakati Makamu alipofika eneo hilo kuweka jiwe la msingi Ujenzi wa nyumba hizo jana Machi 5, 2013
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati alipokutana na Wanachama wa CCM mkoa wa Mara katika Ukumbi wa CCM mkoa uliopo eneo la Nyasho Musoma mjini, wakati Makamu akiwa katika ziara yake ya siku mbili mkoani Mara. Picha na OMR.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Gabriel Tupa na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa TBA, mara baada ya Makamu kuweka jiwe la Msingi katika mradi wa ujenzi wa Nyumba za watumishi wa Umma, jana Machi 5,2013.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Musoma Mjini Mkoa wa Mara, katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Mukendo jana Machi 5, 2013 ikiwa ni siku ya mwisho ya zaiara yake mkoani Mara.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya wazee wa mkoa wa Mara wakati akiagana nao baada ya kuwahutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mukendo jana Machi 5, 2013.ikiwa ni siku ya mwisho ya zaiara yake mkoani Mara.
  Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, akizicharaza Tumba za bendi ya Msondo Ngoma, wakati bendi hiyo ilipokuwa ikitoa burudani kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mukendo Musoma mjini Mkoani Mara jana Machi 5, 2013, wakati Makamu wa Rais Dkt. Bilal, alipokuwa akiwahutubia wananchi wa mkoa huo. Kushoto ni wanamuziki wa bendi hiyo, wakimshabikia. Picha na OMR

  0 0  0 0

  Mamia ya wananchi wakijiandaa kumlaki Waziri Mkuu wa Denmark Mhe Helle Thorning-Shmidt kupitia lango la Mashariki la Ikulu Dar es salaam leo.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Denmark Mhe Helle Thorning-Shmidt wakiingia Ikulu huku wakishangiliwa.
  Msafara wa Waziri Mkuu wa Denmark Mhe Helle Thorning-Shmidt ukikaribia lango la Mashariki la Ikulu Dar es salaam leo.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu Ikulu Mhe. Sanga na maofisa wengine waandamizi wakati akimsibiri mgeni wake.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Waziri Mkuu wa Denmark Mhe Helle Thorning-Shmidt  Ikulu Dar es salaam leo.
  Waziri Mkuu wa Denmark Mhe Helle Thorning-Shmidt akisalimiana na Waziri wa kazi na  Ushirika wa Zanzibar Mhe Haroun Ali Suleiman
  Waziri Mkuu wa Denmark Mhe Helle Thorning-Shmidt akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh. Bernard Membe.  Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika maongezi ya faragha na Waziri Mkuu wa Denmark Mhe Helle Thorning-Shmidt leo Ikulu.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Waziri Mkuu wa Denmark Mhe Helle Thorning-Shmidt.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na  Waziri Mkuu wa Denmark Mhe Helle Thorning-Shmidt na ujumbe wake wakati wa mazungumzo rasmi.

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtembeza  Waziri Mkuu wa Denmark Mhe Helle Thorning-Shmidt katika viunga vya Ikulu kabla ya mgeni huyo kupanda mti wa kumbukumbu.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimueleza Waziri Mkuu wa Denmark Mhe Helle Thorning-Shmidt aina ya mti ataoupanda leo.
  Waziri Mkuu wa Denmark Mhe Helle Thorning-Shmidt akisalimiana na maafisa waandamizi wa Ikulu katika viunga vya Ikulu kabla ya mgeni huyo kupanda mti wa kumbukumbu.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtembeza  Waziri Mkuu wa Denmark Mhe Helle Thorning-Shmidt katika viunga vya Ikulu kabla ya mgeni huyo kupanda mti wa kumbukumbu.

  Waziri Mkuu wa Denmark Mhe Helle Thorning-Shmidt akipanda mti wa kumbukumbu huku mwenyeji wake akishuhudia  leo.PICHA NA IKULU

  0 0

  Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha la Pasaka kutoka Kampuni ya Msama Promotions Ltd,Bwa.Alex Msama,akizungumza mbele ya Wanahabari (hawapo pichani) ,mapema leo kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar kuhusiana na mchakato mzima wa tamasha la pasaka na kuwataja wasanii mbalimbali watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo ambalo limekuwa liwavutia wengi,ambapo mwaka huu limebeba ujumbe wa kuhimiza suala la amani na utulivu katika nchini yetu,tamasha hilo linatarajia kufanyika Machi 31 ndani ya uwanja wa Taifa na baadae kufanyika kwenye mikoa mingine kama vile Mbeya,Dodoma,Mwanza na Iringa.Kumsikiliza zaidi bofya video hapa chini.

  0 0   Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Limited, Absalom Kibanda akiwa ndani ya Ndege ya Flightlink tayari kwa kusafirishwa kwenda  South kwa matibabu zaidi baada ya kuvamiwa Nyumbani kwake 
  Mbezi Beach usiku wa kuamkia leo.
   Absalom Kibanda akiwa na mkewe ndani ya Ndege, Anjella Semaya
   Baadhi ya waandishi na viongozi wa jukwaa la wahariri wakiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbi kwa ajili ya kumjulia hali
   Absalom Kibanda akiwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili 
  kabla ya kusafirishwa kwenda South Afrika
   Wafanyakazi wa Kampuni ya Ndege ya Flightlink wakimpandisha Absalom Kibanda
   ndani ya Ndege

   Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Limited, Hussein Bashe 
  akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio la kutekwa kwa, Absalom Kibanda
   Mwenyekiti wa CHADEMA, Freema Mbowe akimjulia hali Absalom Kipanda katika Hospitali ya Taifa ya Muhumbili Dar es Salaam
   Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Regnald Mengi na OfisaMkuu Mtendaji, Hussein Bashe wakijaribu kuzungumza naye katika eneo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kabla ya kusafirishwa
  Saed Kubenea (kushoto), OfisaMtendaji Mkuu wa New Habari Huseein Bashe (kulia) wakijaribu kuzungumza naye

   Absalom Kibanda, akiwa katika eneo la Uwanja wa Ndege
   Wafanyakazi wa Kampuni ya Ndege ya Flightlink wakimpandisha Absalom Kibanda
   ndani ya Ndege.Picha zote kwa hisani ya amanitanzania.blogspot.com.

  0 0


  Clip 4

  Viongozi wa Dini (Wachungaji) wakifanya maombi ya mwisho kabla ya kuuhifadhi mwili wa aliyekuwa Mjumbe  wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (Uvccm), ngazi ya taifa  kupitia mkoa wa Arusha, Benson Mollel (26) aliyeaga dunia hivi karibu.

  Clip 5

  Baadhi ya Viongozi walio hudhuria mazishi ya Mjumbe  wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), ngazi ya taifa  kupitia mkoa wa Arusha, Benson Mollel (26) aliyeaga dunia hivi karibu katika hoteli ya Lush Garden Bussines Hotel iliyopo barabara ya vijana mkabala na  Jacaranda  mtaa wa Haile Selassie katikati ya jiji la Arusha.Picha kwa hisani ya http://jamiiblog.co.tz


  0 0

   Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori akizungumza wakati wa uzinduzi wa kujiandikisha kwa hiari kwa wanachama wa NSSF, wakulima wa Kahawa wa Ushirika wa RUMAKO Kigoma Vijijini. Zaidi ya Wanachama 500 wameandishwa Uanachama wa Hiari wa NSSF katika Kata ya Kalinzi.
  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Ramadhani Maneno akizungumza wakati wa Uzinduzi huo.
  Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga akizungumz wakati wa uzinduzi wa kujiandikisha uanachama wa NSSF wa Hiari kwa wakulima wa Kahawa wa Ushirika wa RUMAKO Kigoma Vijijini. 
  Wanakijiji wakiwa katika hafla hiyo.
  Baadhi ya wakazi wa vijiji vya Matyazo, Rusaba na Makabogo wakiwa katika hafla hiyo.   Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga akiwasili katika Kijiji cha Matyazo wakati wa uzinduzi wa kujiandikisha uanachama wa NSSF wa Hiari kwa wakulima wa Kahawa wa Ushirika wa RUMAKO Kigoma Vijijini. 
   Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kigoma Vijijini, Hamis Betese akizungumza wakati wa uzinduzi wa kujiandikisha uanachama wa NSSF wa Hiari kwa wakulima wa Kahawa wa Ushirika wa RUMAKO Kigoma Vijijini. 
  Baadhi ya wanakijiji cha Matyazo pamoja na vijiji vya jirani wakiwa katika uzinduzi huo.
  Kikundi cha ngoma za kitamaduni cha Changamoto kikitoa burudani.

  Meneja Mipango na Uwekezaji wa NSSF, Mseli Abdalah akiongoza hafla hiyo.
  Meneja wa NSSF Mkoa wa Kigoma, James Mashinga akizungumza wakati wa uzinduzi.
  Kikundi cha Ngoma cha Changamoto kikitoa burudani.
  Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga akimkabidhi kadi ya Uanachama wa hiari wa NSSF mkulima wa Kahawa wa Ushirika wa RUMAKO, Mary Wilfred wakati wa hala iliyofanyika Kogoma Vijijini.
  Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga akimkabidhi kadi ya Uanachama wa hiari wa NSSF mkulima wa Kahawa wa Ushirika wa RUMAKO, Meckrinda Enock wakati wa hala iliyofanyika Kogoma Vijijini.
  Meneja wa NSSF Mkoa wa Kigoma, James Mashinga akipokea zawadi ya Kahawa kutoka kwa Mwenyekiti wa Ushirika wa RUMAKO, Omari Mahwisa.
  Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga  akipokea zawadi ya Kahawa kutoka kwa Mwenyekiti wa Ushirika wa RUMAKO, Omari Mahwisa
  Mwenyekiti wa Ushirika wa RUMAKO, Omari Mahwisa akitoa neno la shukrani wakati wa hafla hiyo.
  Meneja Kiongozi, Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume akifurahia zawadi ya Kahawa mara baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Ushirika wa RUMAKO, Omari Mahwisa.

  0 0
 • 03/06/13--23:34: hatari lakini salama.


 • 0 0
 • 03/07/13--00:02: chezea mlege wewee..!


 • 0 0

  MWIZI WA BETRI YA GARI ANAEJULIKANA KWA JINA MOJA TU SEFA AKISURUBIWA KWA STAILI YA AINA YAKE KWA KUFUNGWA KWENYE NGAZI PAMOJA NA BETRI ALIYOIBA.
  MWIZI HUYO AKIENDELEA KUTESEKA KATIKA NGAZI HIYO

  POLISI WAMEFIKA KUMWOKOA MWIZI HUYO KATIKA MATESO HAYO
  BADO WANANCHI WANAHASIRA NA MWIZI WAO WAKIDAI WAACHIWE WAMFUNZE ADABU MAANA AMEWASUMBUA SANA ENEO HILO LA UYOLE
  POLISI WAMEZIDIWA WAMEPOKONYWA MTUHUMIWA WAO KIPIGO KINAENDELEA

  HII NDIYO NGAZI ILIYOTUMIKA KUMWADHIBU MWIZI HUYO

  PICHA ZOTE KWA HISANI YA KAMANGA MBEYA-MBEYA YETU.BLOGSPOT.COM.

  0 0


  Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akiongea katika mkutano na wanahabari leo katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa Tume Bw. Assaa Rashid.
  ========  =========  =========
  Wananchi wenye sifa za kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya na ambao wangependa kuwa Wajumbe wa Mabaraza wanaweza kuanza kuwasilisha maombi yao kwa Maofisa Watendaji wa Vijiji au Mtaa kuanzia kesho (Ijumaa, tarehe 8 Machi, 2013) hadi tarehe 20 Machi mwaka huu (2013). Kwa Zanzibar, maombi hayo yawasilishwe kwa Masheha.
   
  Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba amesema jijini Dar es Salaam leo (Alhamisi, Machi 7) kuwa ili kuhakikisha mchakato wa uundwaji na uendeshaji wa Mabaraza ya Katiba unaendeshwa kwa ufanisi, Tume imeandaa Mwongozo wa kusimamia mchakato huo na kuuchapisha katika magazeti mbalimbali na kuwekwa katika tovuti ya Tume (www.katiba.go.tz) na ukurasa wa facebook wa Tume (tumeyamabadilikoyakatiba).
   
  Jaji Warioba ameongeza kuwa Tume yake pia imechapisha vitabu vyenye mwongozo huu na kuvisambaza kwa Ofisi za Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Miji, Manispaa, Majiji na wadau wengine kwa Tanzania Bara ili wawafikishie wananchi katika mitaa na vijiji. Kwa Zanzibar, mwongozo umesambazwa kwa Ofisi za Wakuu wa Wilaya, Baraza la Manispaa na Katibu wa Halmashauri za Mji ili wawafikishie wananchi katika Shehia zao.
  “Sifa za mwananchi anayependa kuomba nafasi ya kuwa mjumbe wa Baraza la Katiba ni pamoja na kuwa raia wa Tanzania na awe na umri wa miaka 18 au zaidi,” amesema Jaji Warioba katika mkutano wake na wanahabari uliofanyika katika ofisi za Tume
  Jaji Warioba alitaja sifa nyingine kuwa ni pamoja na kuwa na uwezo wa kusoma na kuandika na pia awe ni mkazi wa kudumu wa Kijiji, Mtaa au Shehia husika. Sifa nyingine ni pamoja na kuwa mtu mwenye hekima, busara na uadilifu na ambaye ana uwezo wa kujieleza na kupambanua mambo. 
  Katika mwongozo huo, Jaji Warioba amesema, Tume pia imeelekeza kuwa wananchi wanaoomba wanapaswa kuwasilisha nakala mbili za barua ya maombi. Barua moja itabaki katika Ofisi ya Mtendaji na barua ya pili atabaki nayo mwombaji baada ya kutiwa saini na kugongwa muhuri kuthibitisha kuwa ombi lake limepokelewa.
  Aidha, baada ya muda wa kuwasilisha maombi kukamilika, Tume imeelekeza katika mwongozo wake kuwa majina ya waombaji wote yatapaswa kuwa katika sehemu za wazi na mbao za matangazo za ofisi za Watendaji wa mitaa au vijiji kuanzia tarehe 22 – 28 Machi mwaka huu ili wananchi waweze kuyapitia na kujiridhisha kuwa maombi yao yamepokelewa.
  Mwongozo wa Tume pia umeelekeza kuwa kuanzia tarehe 30 Machi hadi 3 Aprili kutafanyika Mikutano Mikuu Maalum ya Mitaa, Vijiji au Shehia kwa Zanzibar ili kufanya uchaguzi na kufuatiwa na Vikao Maalum ya Maendeleo vya Kata vitakayofanyika kati ya tarehe 5 hadi 9 Aprili mwaka huu ili kuchagua wawakilishi wa kila wa Kata. Majina hayo yatawasilishwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji, Manispaa au Jiji kwa Tanzania Bara na Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa, Katibu wa Halmashauri Mji/ Wilaya kwa Zanzibar ambao watayawasilisha kwa Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa uteuzi rasmi.
   
  Jaji Warioba amewaomba wananchi na viongozi wote kuendesha mikutano ya uundwaji wa mabaraza kwa amani na utulivu na kuzingatia mwongozo uliotolewa na Tume.

  0 0

  Pichani kati ni Mtangazaji wa kipindi cha Leo Tena, Dina Marios kutoka Clouds FM akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa mradi wa Mwanamakuka,Bi.Mariam Shamo pamoja na Mkurugenzi wa benki ya Wanawake Tanzania (TWB),Bi.Magreth Chacha,mapema leo kwenye studio za Clouds FM,Mikocheni jijini Dar.Hafla hiyo imeandaliwa na UNITY OF WOMEN FRIENDS (UWF).
  Mkurugenzi wa benki ya Wanawake Tanzania,Bi.Magreth Chacha ambao pia ni sehemu ya wadhamini wa hafla ya Tuzo za Mwanamakuka 2013 inayotarajia kufanyika hapo kesho ijumaa ndani ya hotel ya Serena jijini Dar,akifafanua zaidi kuhusiana na mambo mbalimbali yanayofanywa na benki hiyo ya wanawake inayotoa mikopo kwa riba nafuu,kushoto kwake ni  Mwenyekiti wa mradi wa Mwanamakuka,Bi.Mariam Shamo akisikiliza kwa makini.Hafla hiyo ya tu zo yakumzawadia mwanamke shujaa aliyepewa jina la Mwanamakuka inafanyika kesho ikiwa pia ni sehemu ya kuadhimisha siku wanawake duniani kote
  Mwenyekiti wa mradi wa Mwanamakuka,Bi.Mariam Shamo,pichani shoto akifafanua jambo kuhusiana na shunghuli nzima ya hafla ya kumzawadia mwanamke shujaa Mwanamakuka siku ya Wanawake Duniani inayotarjiwa kufanyika kesho Duniani kote,Bi.Mariam alisema kuwa katika hafla hiyo kutakuwepo na shunguli mbalimbali ikiwemo burudani kutoka bendi ya Tanzanite,maonesho ya mavazi na zawadi mbalimbali pia zitatolewa ukumbini humo.
  Dina Marios akitaka kufafanuliwa jambo kutoka kwa Mwenyekiti wa mradi wa Mwanamakuka,Bi.Mariam Shamo kuhusiana na shughuli nzima ya tuzo za Mwanamakuka zitakazofanyika hapo kesho ndani ya hotel ya Serena jijini Dar.

  0 0

   Timu ya Mbezi inayohusisha waendasha pikipiki maarufu kama bodaboda ikishangilia ushindi mara baada ya kuibuka washindi wa kwanza wa michuano ya Mpinga Cup iliyofanyika jana katika viwanja vya oyesterbay police. Mbezi iliifunga makondeko mabao 7-6 na kuibuka washindi
  Naibu waziri wa mambo ya ndani  Mh. Pereira Silima akikabithi mfano wa hundi ya shilingi millioni moja kwa captain wa timu ya Mbezi Ally Shila Kulola  baada ya timu yake kuibuka washindi wakwanza wa michuano ya mpinga Cup kwa kushinda Makondeko  mabao 7-6. 
   Naibu waziri wa mambo ya ndani  Mh. Pereira Silima akikabithi kombe  captain wa timu ya Mbezi Ally Shila Kulola  baada ya timu yake kuibuka washindi wakwanza wa michuano ya mpinga Cup kwa kushinda Makondeko  mabao 7-6
   Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde akikabithi zawadi kwa captain wa timu ya makondeko Stanley Peter mara baada ya kuibuka washindi wa pili wa mashindanoo ya mpinga Cup yaliyohusisha waendasha pikipiki (bodaboda)  kwa muda wa wiki moja katika viwanja vya oyesterbay polisi. Kushoto pembeni ni kiongozi wa timu ya makondeko bwana Mneke S Mneke. 
  Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga akimtambulisha  Naibu waziri wa mambo ya ndani  Mh. Pereira Silima ambaye ni mgen rasmi  wakati wa fainali za michuano ya mpinga Cup iliyofanyika jana katika viwanja vya oyesterbay police.

  Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga akibadilishana mawazo na  Naibu waziri wa mambo ya ndani  Mh. Pereira Silima ambaye  wakati wa fainali za michuano ya mpinga Cup iliyofanyika jana katika viwanja vya oyesterbay police.

  ==============  ================
  Michuano ya mpinga Cup imemalizika rasmi jana baada ya mchezo wa fainali thidi ya timu ya Mbezi na makondeko ambapo, timu  hizo zilitoka sare ya bao 2 -2 na kuingia kwenye mkwaju wa penalti ambapo timu ya kawe iliibuka na ushindi wa mabao 7 -6 Katika michuano hiyo iliyodumu kwa muda wa wiki nzima na kushirikisha timu nane kutoka katika mkoa wa kipolisi wa kinondoni timu ya  mikocheni  Iliibuka kuwa mshindi wa tatu wa michuano hiyo.

  Akiongea wakati wa kufunga michuano hiyo mgeni rasmi Naibu waziri wa mambo ya ndani  Mh. PereiraSilima alisema” tunawashukuru waandalizi wa michuano hii na wadhamini ambao ni Airtel, Mr price, home shoping center na Rotary Club Dar es Saalam kwa ushirikiano wao mkubwa na mchangao wao katika kuhakikiksha mashindano haya yanafanyika kwa mafanikio.  

  Hii nijitahada ya pekee kuunganisha michezo na elimu ya usalama barabarani. Tumegundua vipaji vingi hapa tunawaasa wachezaji hawa wajiendeleze mbali na kuendesha  pikipiki kwa muda wa ziada wataweza kucheza mpira na kupata njia nyingine ya kipato kwa michezo ni ajira. Naye Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga amewashukuru washiriki wote wa michuano hii na kusisitiza  wananchi na watanzania kwa ujumla kutii sheria bila shurutishi.

  Akiongea kwa niaba ya wadhamini Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde alisema” mashindano haya yamekuwa ya mvuto mkubwa kwa washiriki na wadau wa michezo zaidi tumeshuhudia jinsi mafunzo ya elimu ya usalama barabarani yalivyoendesha na kuelimisha watumiaji wa barabara waliokuwa wakihudhuria hapa. Tunaamini kuendelea na  juhudi hizi tutaweza kupunguza idadi za ajali barabarani. Airtel tunaahidi kuendelea kushirikiana na jeshi la  polisi  usalama barabarani katika shughuli mbalimbali za uelimishaji umma juu ya sheria za barabarani.

  Michuano ya mpinga cup kwa wilaya ya kinondoni imefika tamati hapo jana na mpango ni kuwa na michuano hii pia katika mkoa wa ilala na temeke na kisha kuendelea na michuano hii nchini nzima.


  0 0


  Kuongezeka kwa joto katika pwani ya Tanzania , kupotea kwa baadhi ya viumbe katika bahari na hindi na kumezwa kwa visiwa kumeelezwa kuwa ni miongoni mwa athari zitokanazo mabadiliko ya tabia nchi.


  Hayo yameelezwa leo na Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia Ngosi Mwihava katika warsha ya wadau ya programu ya kitaifa ya kuhimili athari zitokanazo na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi katika ukanda wa pwani inayoendelea mjini Bagamoyo.


  Injinia Mwihava ameeleza kuwa, athari nyingine zitokanazo na  madhara hayo ni pamoja navisiwa baridi kuingiliwa na maji ya chumvi, vina vya bahari kuongezeka na kwa kuwa viumbe katika bahari hupotea inaweza kupelekea uchumi wa wakazi wengi wa mwambao kudidimia kwani hutegemea zaidi uvuvi.


  Tanzania kama nchi “Ina mkakati wa kuongeza uelewa kwa kushirikiana na wadau juu ya dhana ya namna ya kukabiliana na madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi kwa kushirikiana na wadau na wananchi wa kawaida kwa kutumia sayansi na elimu asilia ikiwa ni pamoja na kufuga samaki iliwaweze kusaidiaa kipindi ambacho watakuwa wamepotea.


  Kwa upande wake mkurugenzi wa mradi wa pwani bwana Baraka kalangale ameeleza kuwa ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi mradi wake unawajengea uwezo  wananchi katika eneo hilo kupitia mafunzo na ushirikishwaji. “Vijiji vingi vimeathirika na masuala haya ya mabadiliko ya tabia nchi ikiwa ni pamoja na kijiji cha mbuyuni katika wilaya ya pwani kwani kipo katika hatari ya kumong’onyoka kabisa, alisisitiza.”

  Warsha hiyo inayohusisha wadau kutoka mashirika mbali mbali yanayojihusisha na masuala ya mazingira na serikali kuu imefadhiliwa na shirika la misaada la watu wa marekani (USAID)  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Muhamed Shein akimuagiza jambo Mkuu wa Mkoa wa mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis juu ya suala zima la uzururaji wa wanyama katika eneo la Mjini.
   Viongozi mbali mbali wa Mkoa wa Mjini  Magharibi wakimsikiliza kwa makini Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Muhamed Shein wakati akitoa majimuisho ya ziara yake katika Mkoa huo.
   Mkuu wa Wilaya ya Magharibi Hassan Mussa Takrima akitoa neno la shukurani kwa Rais wa Zanzibar huko katika ukumbi wa Chuo cha Karume Mbweni nje kidogo ya mji wa Zanzibar .Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Muhamed Shein akizungumza na viongozi mbali mbali wa Mkoa wa Mjini Magharibi katika majumuisho ya ziara yake ya Mkoa wa Mjini Magharibi huko katika ukumbi wa Chuo cha Karume Mbweni nje kidogo ya mji wa Zanzibar. 

  0 0

   Msanii, Mrisho Mpoto, akitoa burudani mbele ya jukwaa kuu, wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa pili wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), uliofanyika leo Machi 7, 2013 katika Ukumbi wa Jengo Golden Jubilee Towers, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi na watumishi wa mfuko huo, baada ya kufungua rasmi mkutano Mkuu wa pili wa mwaka wa Wadau wa PSPF, leo
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa pili wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), uliofanyika leo Machi 7, 2013 katika Ukumbi wa Jengo Golden Jubilee Towers, jijini Dar es Salaam.  
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Kitambulisho, Faridi Ibrahim Kiringi, mfanyabiashara wa duka la Nguo, ambaye ni mmoja kati ya wanachama wapya wanaochangia kwa hiyari, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao na ishara ya ufunguzi wa mkuatano huo, uliofanyika leo Machi 7, 2013, katika Ukumbi wa jengo la Golden Jubilee Towers. Kushoto ni Waziri wa Fedha, Dkt. William Mgimwa
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Hati na Nyumba na funguo, Adorat Francis Milinga, mmoja kati ya watu watano walionunua nyumba za PSPF, ambaye ni mmoja kati ya wanachama wapya wanaochangia kwa hiyari, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao na ishara ya ufunguzi wa mkuatano huo, uliofanyika leo Machi 7, 2013, katika Ukumbi wa jengo la Golden Jubilee Towers. Kushoto ni Waziri wa Fedha, Dkt. William Mgimwa. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Kitambulisho, Winfrey Ibrahim Banda, Mwalimu wa Shule ya Msingi, ambaye ni mmoja kati ya wanachama wapya wanaochangia kwa hiyari, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao na ishara ya ufunguzi wa mkuatano huo, uliofanyika leo Machi 7, 2013, katika Ukumbi wa jengo la Golden Jubilee Towers. Kushoto ni Waziri wa Fedha, Dkt. William Mgimwa.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Ukumbi wa Jubilee Towers, kwa ajili ya kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa pili wa Mwaka, wa Wadau wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), uliofanyika leo Machi 7, 2013 katika Ukumbi wa Jengo Golden Jubilee Towers, jijini Dar es Salaam

  0 0


  MAWAKALA wote walioteuliwa kuandaa mashindano ya urembo nchini mwaka huu "Redd's Miss Tanzania" leo wanatarajiwa kushiriki katika semina maalumu itakayofanyika kuanzia saa 3:00 asubuhi kwenye hoteli ya Girraffe iliyoko jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza leo jijini, Mkurugenzi wa kampuni ya Lino Agency, Hashim Lundenga, alisema kuwa mawakala watakaoshiriki semina hiyo ni wa kuanzia ngazi ya kanda, mikoa na vitongoji vyote vya mkoa wa Dar es Salaam.

  Lundenga alisema kuwa maandalizi ya semina hiyo yamekamilika na mawakala kutoka mikoani walianza kuwasili jijini tangu jana asubuhi na katika mialiko waliyotumiwa wamesisitizwa kufika bila kukosa ili kupata maelekezo kabla ya kuanza kuandaa mashindano yao ya ngazi husika.

  Alisema kuwa kila mwaka kamati yake hutoa maelekezo kulingana na kanuni na taratibu zilizopitishwa na kamati hiyo na vile vile kuwapa mwangaza mawakala ni makampuni na taasisi zipi wanazoruhusiwa kuomba udhamini ili wasiende tofauti na mdhamini mkuu wa shindano hilo ngazi ya taifa ambao ni kampuni ya bia nchini TBL kupia kinywaji chake cha Redd's original.

  "Tunaamini semina itafanyika kama ilivyokusudiwa na mawakala watapewa mbinu za kukabiliana na changamoto katika kutekeleza majukumu yao," alisema Lundenga. Mrembo kutoka katika kitongoji cha Sinza, kanda ya Kinondoni, jijini, Brigitte Alfred, ndiye mrembo anayeshikilia taji hilo la taifa aliyelitwaa kutoka kwa Salha Israel wa Ilala. Hata hivyo Brigitte ndiye atakayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya dunia mwaka huu na mrembo atakayeshinda taji hilo baadaye mwaka huu atashiriki fainali hizo za dunia mwakani

  0 0


  Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo jijini Dar es salaam.    

    ======  ========= ========= 
   Na. Aron Msigwa - MAELEZO.
   
  Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu amewataka wanawake nchini kuchangamkia fursa mbalimbali za maendeleo zinazojitokeza katika maeneo yao ili waweze kujikwamua kiuchumi na kupambana na umaskini.
   
  Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es salaam wakati akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kwa waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yatakayofanyika machi 7 mwaka huu.
   
  Amesema maadhimisho hayo yanalenga kuwezesha upimaji wa utekelezaji wa maazimio , matamko, mikataba na itifiki mbalimbali za kimataifa na kikanda zinazohusu masuala ya maendeleo ya jinsia kwa wanawake na kubainisha kuwa maadhimisho ya mwaka huu yataongozwa na kauli mbiu isemayo Uelewa wa Masuala ya Jinsia katika Jamii; Ongeza kasi"
   
  Amesema serikali ya Tanzania imekuwa na mipango thabiti ya kuhakikisha kuwa usawa wa kijinsia nchini unazingatiwa kwa kuchukua hatua mbalimbali zikiwemo kuridhia na kusaini mikataba, itifaki, maazimio na matamko mbalimbali yanayohusu maendeleo, haki na ustawi wa wanawake na utungaji wa sheria ya Ardhi Na. 4 na ile ya vijiji Na.5 za mwaka 1999 ambazo zinatoa fursa sawa za umiliki wa ardhi.
   
  Bi Ummy amefafanua kuwa kuwa Tanzania imeshasaini na kuridhia mkataba wa kuondoa aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake (CEDAW 1979), Azimio la ulingo wa Beijing (1995), mkataba wa malengo ya Milenia, Azimio la kuleta Usawa wa Kijinsia katika nchi za Afrika (2004) na Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu za Wanawake (2006).
  Mikataba mingine iliyosainiwa na kuridhiwa na Tanzania ni ule wa Itifaki ya Maendeleo ya Jinsia ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC 2008).
   
  Ameeleza kuwa serikali imepitisha Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya Mwaka 2000 ili kutoa mwongozo wa kuratibu uingizwaji wa masuala ya jinsia katika mipango, Sera, Programu, mikakati na bajeti za kisekta ili kuleta usawa baina ya wanawake na wanaume katika masuala ya maendeleo nchini.
   
  Pia amefafanua kuwa Wizara yake imeratibu kuanzishwa kwa dawati la jinsia katika Wizara, Idara za serikali zinazojitegemea, sekretarieti za mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini ili kuharakisha utekelezaji wa masuala ya jinsia.
   
  Kuhusu mafanikio ya kuleta usawa wa kijinsia nchini Bi. Ummy ameeleza kuwa kumekuwa na ongezeko la wanawake katika ngazi mbalimbali za maamuzi zikiwemo uwakilishi wa wanawake bungeni kutoka asilimia 30 mwaka 2005 na kufikia 36 mwaka 2010.
   
  "Napenda kueleza kuwa mafanikio haya kwa wanawake katika ngazi za maamuzi nchini ni makubwa kwa sasa ukilinganisha na miaka iliyopita, sasa tuna mawaziri wanawake, tuna wakuu wa mikoa na wilaya , tuna wabunge wengi tu , Majaji wa mahakama kuu, makatibu wakuu na viongozi wengi wanawake" amesema.
   
  Aidha amefafanua kuwa serikali imeendelea kuwawezesha wanawake kiuchumi na tayari imeratibu na kusimamia mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF) na kuongeza kuwa wanawake wamewezeshwa kiuchumi kwa kuwapatia elimu, mbinu za ujasiriamali na mikopo yenye masharti nafuu kupitia Benki ya Wanawake Tanzania ambapo mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 1.2 kwa wanawake 5270 na wanaume 1157.
   
  Ameeleza kuwa licha ya mafanikio yaliyopatikana bado wanawake nchini wanakabiliwa na changamoto mbalimbali hasa uwepo wa wasichana wanaokatisha masomo yao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mimba za utotoni na kuwepo kwa vtendo vya ukatili wa kijinsia katika baadhi ya jamii nchini.

  0 0older | 1 | .... | 41 | 42 | (Page 43) | 44 | 45 | .... | 1897 | newer