Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46371 articles
Browse latest View live

WAKENYA WAWAFUNIKA WATANZANIA MICHUANO YA TENISI DAR OPEN

$
0
0
DSC_0453
Mmoja wa wadhamini kutoka kampuni ya mawikili ya IMMA ya Dar es Salaam, Alexander Sarac, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa michuano ya tenisi ya walemavu ya kimataifa kutoka Tanzania kwa udhamini mkuu wa kampuni ya magari ya CFAO Motors kupitia brandi ya magari ya Mercedes Benz. (Picha na Zainul Mzige wa MOblog).
Na Mwandishi wetu

WACHEZA tenisi kutoka nchini Kenya wamewafunika watanzania katika michuano ya kimataifa ya kwanza ya tenisi kwa walemavu (Dar Open ). Michuano hiyo inatarajiwa kuhitimishwa kesho katika viwanja vya Gymkhana, majira ya saa 10 ambapo washindi watapewa tuzo zao.

Kwa mujibu wa matokeo ya hadi mchana wakati mwandishi wa habari hizi anaondoka viwanjani hapo, mechi saba zilienda kwa wakenya kwa nafasi ya wanaume na wanawake na mbili ndio walishinda Watanzania.

Michuano hiyo ambayo inadhaminiwa na kampuni ya magari ya CFAO, Mercedes-Benz na kampuni ya mawakili ya Dar es salaam ya IMMMA imelenga pia kuandaa wachezaji kwa ajili ya mechi za kufuzu michezo ya dunia zinazotarajiwa kupigwa nchini Kenya Februari mwakani.
DSC_0413
Mshiriki wa michuano ya tenisi ya walemavu ya kimataifa kutoka Tanzania, Rehema Selemani akirusha mpira wakati akichuana na mshiriki kutoka Mombasa, Phoebe Masika (hayupo pichani).

Kwa mujibu wa msemaji wa wadhamini wa michuano hiyo Alexander Sarac, michuano hiyo yenye washiriki wanaume 17 na wanawake watano walioitwa kutoka Tanzania na Kenya, imelenga kuwezesha walemavu kuendeleza vipaji vyao vya kucheza tenisi.

Pamoja na kuwa na ushindi dhaifu wa watanzania kocha wa timu ya Tanzania amesema bado ana bunduki zake mbili na ana hakika kesho vikombe vitabaki Tanzania. Fungua dimba ya michuano hiyo ilianzishwa na watanzania Novatus Temba na Moses Sebastian ambapo Temba alimchapa Sebastian kwa seti 2-0; mkenya Itaken Timoi alimvuruga Bernad Antony kwa seti 2-0 huku Mkenya mwingine Peter Mnuve akimtoa Mtanzania Albert John kwa seti 2-0.
DSC_0376
Katika michezo mingine Rajab Abdallah kutoka Kenya alimtoa Adil Hashim kwa seti 2-0 huku Yohana mwila wa Tanzania akimpa taabu Kenya ambaye alimuondoa kwa seti 2-1. Muingereza anayeishi nchini Ian Artetiel alimtoa Mtanzania Voster Peter kwa seti 2-1.
 
Mkenya Caleb Odisyo alimchapa Mtanzania Wiston Sango kwa seti 2-0 wakati katika mechi za wanawake, Mtanzania Rehema Seleman alimsulubu bila huruma Asia Mohamed wa Kenya seti 2-0.Katika mechi nyingine Asia Mohamed alimchapa Bihawa Mustafa kwa seti 2-1.

Naye Lucy Shirima wa Tanzania alitandikwa na Phoebe Masika wa Kenya kwa seti 2-0.
Timu ya Tanzania ambayo kwa sasa ndiyo inayotamba Afrika Mashariki kutokana na michuano ya mwisho iliyofanyika Nairobiu kutwaa ushindi ina kazi ya ziada kulinda heshima yake.
DSC_0404
Mshiriki kutoka Mombasa, Phoebe Masika akishiriki mashindano hayo.
DSC_0418
Mtinange ukiendelea.
DSC_0499
Mshiriki wa michuano ya tenisi ya walemavu ya kimataifa kutoka Tanzania Yohana Mwila (kushoto) akipeana mkono na mshiriki mwenzake kutoka Mombasa, Rajabu Abdallah mara baada ya kumaliza mchezo wa seti 3 ambapo seti ya kwanza Rajabu Abdallah ameshinda 4-3 na seti ya pili ameshinda Yohana Mwila 4-3 na ya tatu ubingwa ukienda kwa Yohana Mwila 10-3 katika kutafuta mshindi wa robo fainali kwenye michuano hiyo iliyodhaminiwa na kampuni ya magari ya CFAO Motors, kupita brandi ya Mercedes-Benz kama wadhamani wakuu na kampuni ya mawakili ya Dar es salaam ya IMMMA.
DSC_0421
Ofisa wa Kitengo cha masoko na huduma wa CFAO Motors Ltd, Angel Ndege akiwa amejumuika na washiriki hao uwanjani hapo.
DSC_0423
Baadhi ya washiriki kutoka Tanzania na Mombasa wakishuhudia wenzao wakiumana uwanjani.
DSC_0436
Vikombe vitakavyokabidhiwa hapo kesho kwenye fainali za michuano hiyo.
DSC_0488
Ofisa wa Kitengo cha masoko na huduma wa CFAO Motors Ltd, Angel Ndege na Kocha wa timu ya wachezaji tenesi Tanzania, Riziki Salum wakiangalia vikombe vitakavyokabidhiwa kwenye fainali za michuano hiyo itakayorindima hapo kesho kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
DSC_0433
Mmoja wa wadhamini kutoka kampuni ya mawikili ya IMMA ya Dar es Salaam, Alexander Sarac (kulia) akibadilishana mawazo na baadhi ya wadau wa mchezo wa tenesi waliofika uwanja hapo kushuhudia michuano hiyo.

Call Out for Artists

$
0
0


Call Out for Artists


ZIFF is East Africa’s largest film, music and arts festival, bringing together talent from all over the world for a Zanzibar Tamasha! ZIFF puts together the island’s best parties. Bringing live music, dance, DJs and performances on a number of platforms. A carnival fever hits Zanzibar for 10days! We bring musicians together from all over Africa, and the world at large.
 
Zanzibar International Film Festival is currently calling for Musicians and Performing Artists to send their request in order to be part of ZIFF 2015. Applying is free. Please submit you sample works by sending a YouTube link, Vimeo, Sound Cloud, pictures and Artist profile to 
mpa@ziff.or.tz.
Deadline: 31st January, 2015 at 12Noon.

TAASISI ZA NPS NA TYCEN ZAWAKUTANISHA VIJANA KWENYE MKUTANO WA MABADILIKO YA TABIANCHI

$
0
0
Picha ya pamoja ya washiriki wa mkutano wa Vijana wa Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika kwenye ukumbi wa Eco Sanaa, Mikocheni Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umeandaliwa na Global Power Shift Tanzania Chapter (NPS) kwa kushirikiana na Tanzania Youth Cultural Exchange Network (TYCEN).
Afisa Mwandamizi Mazingira, Abela Muyungi kutoka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) akifafanua jambo wakati wa mkutano huo
Mratibu wa Mtandao wa mabadiliko ya Tabianchi CAN Tanzania, Sixbert Mwanga akitoa mada wakati wa mkutano wa vijana wa mazingira.
 Baadhi ya washiriki wakifurahia jambo wakati wa mkutano huo uliowakutanisha vijana kutoka kwenye taasisi na mashirika mbalimbali yanayopambana na mabadiliko ya tabianchi.

 Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa makini mada wakati wa mkutano huo uliowakutanisha vijana kutoka kwenye taasisi na mashirika mbalimbali yanayopambana na mabadiliko ya tabianchi.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa makini mada wakati wa mkutano huo
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada

Rose Muhando na Kamata Pindo la Yesu kutawala Tamasha la krismass

$
0
0
JINA la Rose Muhando ni mojawapo ya majina yanayofanya vizuri katika muziki wa Injili barani Afrika  hasa kutokana na uwezo wake jukwaani pindi anapofikisha uinjilishaji kwa waamini na mashabiki mbalimbali.
 
Muhando ni mzaliwa wa kijiji cha Dumila, wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro, Tanzania, Afrika Mashariki na ni mwimbaji wa nyimbo za injili kwa lugha ya Kiswahili ambaye umahiri wake awapo jukwaani umefanikisha kutambulika barani Afrika. 
 
Rose atakayepanda jukwaani kuanzia Desemba 25, Agosti 3 mwaka huu alizindua albamu yake Kamata Pindo la Yesu yenye nyimbo za ‘Facebook’, ‘Bwana Niongoze’, ‘Wewe Waweza’, ‘Usiniache’, ‘Nibariki na Mimi’, ‘Usivunjike Moyo’ na ‘Kwema’. 
 
Awali Rose kabla hajawa Mkristo alikuwa Muislam na ni mama wa watoto watatu. Alimpokea Yesu Kristo pale alipokuwa anaumwa na yuko kitandani akiwa na umri wa miaka 9, aliugua kwa muda wa miaka mitatu na baadae alipona na kubadili dini na kuwa Mkristo.Rose alizama kwenye muziki katika kwaya iliyoko Dodoma na alikuwa mwalimu wa Kwaya katika kwaya ya Dodoma St. Mary’s katika kanisa la Kianglikana la Chimuli.
 
Januari 31 mwaka 2005, Rose Muhando alizawadiwa tuzo ya Mtunzi bora wa nyimbo za Injili, Mwimbaji Bora na albamu Bora ya Mwaka. Tuzo hizo zilitolewa katika Tamasha Tanzania Gospel Music Awards, 2004.Desemba mwaka 2005 alihudhuria katika tamasha la Nyimbo za Injili katika kusaidia kuchangia kwa watoto na wajane Dar es Salaam ambapo alitekeleza ipasavyo uchangiaji huo.
 
Februari 2011, Rose Muhando alisaini mkataba na Mult Album Recording Deal na Kampuni ya Sony Music ya Afrika Kusini. Kusaini huko kulitangazwa katika mkutano wa waandishi wa habari Dar es Salaam, Tanzania na hiyo ni mara ya kwanza kufanyika Afrika Mashariki.

Baadhi ya albamu za Rose Muhando ni:
1. Mteule uwe macho, 2004
2. Kitimutimu, 2005
3. Jipange sawasawa, 2008
4.Utamu wa Yesu 2012
4.Kamata Pindo la Yesu 2014

Tuzo alizopata

2005 -Tanzania Music Awards: Mwimbaji Bora wa Kike Nyimbo za Dini (“Mteule uwe macho”) 
2009 - Mwimbaji Bora wa Nyimbo za Injili
2008- Alitunukiwa tuzo nchini Kenya ya Mwimbaji Bora wa Injili Afrika
Amewahi kuzawadiwa kitita cha Sh200,000 na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC).

PSPF YAPATA TUZO YA KIMATAIFA KWA KUTOA HUDUMA BORA KWA WATEJA WAKE

$
0
0

unnamedBalozi wa PSPF Bw.Mrisho Mpoto alionesha tuzo iliyotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya kusimamia Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (ISSA) kwa Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa ajili ya kwa  kutumiaTeknolojia ya Habari na Mawasilino katika utunzaji wa kumbukumbu za wateja na kwa kuwasiliana na wateja wake kwa kutumia simu za mikonono, kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu.

RAIS MSTAAFU,ALLI HASSAN MWINYI AIMWAGIA SIFA NSSF KWA KUWA WABUNIFU WA KUBUNI MIRADI YENYE UBORA

$
0
0
 Rais  Mstaafu wa awamu ya pili Alli Hassan Mwinyi akibadilishana jambo na Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi ya Jamii NSSF, Ramadhan Dau alipotembelea miradi mitatu ya shirika hilo mwishoni mwa wiki ambayo ni daraja la Kigamboni, ujenzi wa nyumba za kisasa Kijichi na Mradi wa kijiji cha Dege Kigamboni jijini Dar es Salaam (Picha na Mpigapicha Wetu) 

RAIS Mstaafu wa awamu ya pili Alli Hassan Mwinyi ameumwangia sifa uongozi  wa Shirika la Hifadhi ya Jamii nchini NSSF, kwa kuwa wabunifu  katika kubuni miradi  yenye ubora ambayo inaendeleshwa  katika maeneo ya Kijichi na Kijiji  cha Dege (Dege Eco Village), kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

Mwinyi aliyasema hayo  Jana Jumamosi alipotembelea  miradi hiyo kwa mara ya akwanza  ambapo alionekana kuvutiwa sana  na kusema “Nimeshukuru  kupata  nafasi hii ya kutembea miradi mitatu ya NSSF kuanzia ujenzi wa daraja la Kigamboni , ujenzi wa nyumba za Kijichi na kijiji cha Dege  wallah nimesikia raha” alisema Mwinyi.

Aliongeza kwa kusema kuwa anawapongeza  NSSF kwa kuwa na fikra yakinifu ambazo zimezaa matunda ya kujivunia katika serikali , ni jambo la fahari  kwa nchi yetu  kwani haya ndiyo amendeleo ambayo tuliyokuwa  tunayaota siku zote.

Mwinyi aliongeza kwa kusema kuwa ifike wakati  watanzania waachane na  maisha ya kuishi  kinyonge na katika nyumba ambazo ni za kimasikini na zisizokuwa na hadhi  ya kuishi binaadamu.

Nina imani kubwa kwamba ipo siku watu wanaoishi Manzese, Buguruni na kwingineko watahama  na kuhamia katika nyumba za bei nafuu za mradi huu wa Dege na Kijichi na haya ndiyo maendeleo yenyewe.

Aidha alisema kwamba tofauti iliyopo katika nyumba hizo ni  bei na gharama hivyo mtu ataweza kuishi kwa nyumba ambayo ni kubwa ama ndogo ya kiasi cha familia anayohitaji .

“Narudua tena kuwa nawapongeza  viongozi wa NSSF wakiwa chini ya Mkurugenzi wao Ramadhan Dau  kwa kuwafikiria yaliyomema Watanzania waliowengi kwa kujenga nyumba zaidi ya 7,000 pia nawaombea maisha marefu na yenye afya njema”, ifike wakati Watanzania wote waishi katika hali ya maisha ya kufanana hasa katika makazi na tofauti itakuwepo katika kipato cha kila mmoja tu  na siyo mahali pa kuishi” alisema Mwinyi.

Akiuzungumzia mradi wa daraja la Kigamboni alisema kwamba jana ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza  kwenda kutembelea mradi huo na kuahidi kuwa katika mstari wa mbele  katika kuchangia hasa kwenye ulipaji  katika kuvuka pindi kivuko hicho kitakapokamilika Julai mwakani.

Alimalizia kwa kusema kuwa anakumbuka wakati alipokuwa  madarakani aliweza kutembelea nchi ya Netherlands ambako walikuwa waking’oa madaraja yao nay eye akapafikiria sana Kigamboni lakini alipowaomba madaraja ili wampe pamoja na wajenzi wao wakamwambia kuwa alichelewa kwa sababu walikwisha  yagawa madaraja hayo kwa  makoloni yao hivyo  anaona  ujenzi wa daraja hilo umetimiza njozi yake.

Tamko La ACT-Tanzania Kuhusu Uchaguzi Unaoendelea Wa Serikali Za Mitaa

Gwiji wa masuala ya mtangamano EAC afariki

$
0
0
Balozi Ndayiziga katika mojawapo ya warsha ya EAC hivi karibuni. Kulia ni mtaalamu wa habari na mratibu wa mafunzo ya wandishi wa habari EAC, Bw. Sukhdev Chhatbar.

Mkufunzi katika Mafunzo hayo, Balozi  Jeremy Ndayiziga (kushoto enzi za uhai wake) akimkabidhi cheti Mroki Mroki, kutoka Father Kidevu Blog ambaye pia ni Mpigapicha wa Masuala ya Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,  kwa kushiriki kikamilifu mafunzo hayo ya masuala ya Mtengamano wa EAC. Anaeshuhudia Katikati ni Elizabeth Wanyoike wa GIZ ambao walifadhili mafunzo hayo na Jumuia ya Afrika Mashariki.
**********
 Na Mtua Salira, EANA
Mshauri Mtaalamu wa muda mrefu wa Masuala ya Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Balozi Jeremy Ndayiziga (54) amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi ugonjwa wa kisukari mjini Bujumbura,Burundi.
Balozi huyo raia wa Burundi kwa mujibu wa marafiki wa karibu na ndugu zake alifariki Jumatano wiki iliyopita na anatarajiwa kuzikwa nchini Burundi Jumanne ijayo, Shirika Huru la Habari la Afrika Mashariki (EANA) limeripoti.
Kutokana na hali yake ya afya kuendelea kudorora, Balozi Ndayiziga alilazimika kukatwa mguu wake wa kulia  katika Hopsitali ya Nairobi kutokana kuzidiwa na ugonjwa wa kisukari na hivyo kubaki hospitalini kwa miezi ipatayo minne. Afya yake ilionekana kuimarika kidogo na alikuwa anakaribia kupona.
Mara ya mwisho alionekana makao makuu ya EAC mjini Arusha, Tanzania katikati ya Novemba mwaka huu katika mkutano wa Maofisa Mawasiliano wa EAC.
Jina la Balozi Ndayiziga ni maarufu kwa watendaji wa EAC kutokana na umahiri wake wa uchapaji kazi,uongozi wa busara na kuwa muumini wa itikadi ya Shirikisho la EAC. Ndiye aliyeiongoza nchi yake katika harakati za kujiunga na EAC 2007.
‘’Marehemu Balozi Ndayiziga alikuwa mtu maarufu, mchapakazi mwenzangu na kwa kweli, zaidi ya yote alikuwa rafiki yangu wa karibu sana,’’ alisema Jean Rigi,Katibu Mkuu wa Wizara ya Afrika Mashariki  nchini Burundi na kuongeza kuwa wengi watamkosa na ni pigo kubwa kwa wote wanaopigania kujenga Afrika Mashariki na raia wake.
Mkongwe wa masuala ya habari nchini Tanzania Jenerali Ulimwengu kufuatia taarifa ya kifo hicho alisema: ‘’Nimepata mshtuko mkubwa! Nilijua kwamba alikuwa anaugua lakini nilifikiri kwamba ni jambo la kawaida tu linaloweza kudhibitiwa.Nimesikitishwa sana kwa sababu alikuwa ni mtu makini na mwalimu mwenye uelewa wa hali ya juu na alikuwa mwakilishi mzuri wa masuala ya mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.Nilifanya naye kazi kwa karibu sana kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitano.’’
Naye mmoja kati wafanyakazi aliokuwa anafanya nao kazi kwa karibu ni Sukhdev  Chhatbar, Mtaalamu wa Masuala ya Habari, ambaye alielezea kusitishwa na kifo Balozi Ndayiziga.
‘’Tulikuwa tunawasiliana vyema katika uekelezaji wa miradi mbalimbali.Alikuwa mtu maarufu, mwenye msimamo thabiti,mwenye busara na alikuwa tayari kufanya lolote kuimarisha mchakato wa mtangamano wa kikanda,’’ alisema Chhatbar, mwandishi wa habari maarufu aliyekuwa anasafiri na kusimamia miradi ya pamoja ya EAC na marehemu Balozi huyo katika nchi wananchama wa jumuiya.
Marehemu ameacha mjane na watoto wanne.

SECURITYGROUP (T) LTD (SGA) WAFANYA USAFI KUADHIMISHA MIAKA 30 YA UTENDAJI KAZI NCHINI

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya ulinzi ya Security Group (T) Ltd (SGA), Eric Sambu akizungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo muda mfupi kabla ya kuanza kuufanyia usafi ufukwe wa Bahari ya Hindi, eneo la Mbezi Beach, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kuadhimisha miaka 30 ya utendaji kazi wa kampuni hiyo nchini.
Wafanyakazi wa kampuni ya ulinzi ya ulinzi ya Security Group (T) Ltd (SGA), wakifanya usafi katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, Mbezi Beach, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kudhimisha miaka 30 ya kampuni hiyo tangu kuanza kufanya kazi zake hapa nchini.
Meneja Mawasiliano wa kampuni ya ulinzi ya Securty Group (T) Ltd (SGA), Sofia (kushoto) akitoa maelekezo kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati wa zoezi la kufanya usafi katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, eneo la Mbezi Beach, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ikiwa ni kuadhimisha miaka 30 ya utendaji kazi wa kampuni hiyo hapa nchini.
Wafanyakazi wa kampuni ya ulinzi ya Security Group (T) Ltd (SGA) akifurahia katika picha ya pamoja baada ya kukamilisha zoezi la ufanyaji usafi katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kuadhimisha miaka 30 ya utendaji kazi wa kampuni hiyo nchini.
Wafanyakazi wa kampuni ya ulinzi ya Security Group (T) Ltd (SGA) wakionesha sehemu ya taka ngumu walizookota katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, eneo la Mbezi Beach, Dar es Salaam wakati walipoufanyia usafi ufukwe huo kuadhimisha miaka 30 ya utendaji kazi wa kampuni hiyo hapa nchini.

ONYESHO LA ELIMU

NEWZ ALERT;MGOMBEA CHADEMA MTAA WA MIGOMBANI SEGEREA, JAPHET KEMBO AWAGARAGAZA WAPINZANI WAKE KWA KUPATA KURA 510

$
0
0
Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Migombani Kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema) Japhet Kembo akifurahia huku akipongezwa na wanachama na wapenzi wa Chadema mara baada ya kuibuka mshindi wa Kiti cha Mwenyekiti kwa Kupata Kura 510 huku CCM wakiwa wamepata kura 215 na NCCR kupata kura 205
 Mawakala wa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Migombani wakihesabu kura ambapo sanduku hilo ndio lilikuwa sanduku la mwisho kuhesabiwa katika Kituo cha Kupigia kura cha Migombani ambao wakazi wa Mtaa wa Migombani walikuwa wakisubiria matokeo
 Askari Polisi wakiwa katika kituo cha Kupigia Kura cha Migombani kwaajili ya kuimarisha ulinzi na mpaka zoezi la kuhesabu kura likimalizika kwa Mgombea wa Chadema kuibuka Mshindi hakuna fujo zilizotokea.
Baadhi ya wakazi wa Mtaa wa Migombani Wakisubiria Matokeo ya Uchaguzi wa Serikali ya Mtaa wa Migombani ambapo mpaka matokeo yanatangazwa Chadema iliibuka na Kura 510, CCM ikiwa imepata kura 215 na NCCR wakiwa na kura 205.
Baadhi ya wapita njia nao ilibidi wasimame maana uchaguzi huu ulivuta hisia za watu wengi kutokana na hali iliyoonyeshwa na wakazi wa mtaa huo kukaa mpaka dakika za mwisho
 Msimamizi wa Uchaguzi katika Kituo cha Kupigia Kura cha Migombani akitangaza Mshindi wa Uchaguzi huo uliomalizika kwa Mgombea wa Chadema akiwa ameibuka Mshindi kwa Kupata Kura 510 huku wapinzani wake wakiwa na Kura 215 za CCM na Kura 205 za NCCR
 Wakazi wa Mtaa wa Migombani wakishangilia ushindi mara baada ya Mgombea wa Chadema Kutangazwa Mshindi wa Kiti cha Mwenyekiti wa Mtaa wa Migombani
 Wakazi wakishangilia kwa Ushindi,
 Mgombea wa Nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Migombani Japhet Kembo (Kushoto aliyenyoosha mkono) akipongezwa na wakazi wa Mtaa wa Migombani kwa kuibuka Mshindi wa uchaguzi
Wakazi wa Mtaa wa Migombani Segerea wakishangilia mara baada ya mgombea wao kuibuka mshindi katika kinyanganyiro hiko.Picha Zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

UPDATES: UCHAGUZI WA SERIKALI YA MTAA WA MIGOMBANI WAINGIA KWIKWI MARA BAADA YA AFISA MTENDAJI WA KATA YA SEGEREA KUJA KUTANGAZA KUSITISHA UCHAGUZI

$
0
0
Wakazi wa Mtaa wa Migombani, Uliopo Katika kata ya Segerea Manispaa ya Ilala Jijini Dar Es Salaam wakiwa wamelizunguka gari la Afisa Mtendaji wa Kata ya Segerea aliyefika majira ya saa tisa kamili mchana huu na kutangaza kusitisha uchaguzi wa serikali ya mitaa kimya kimya.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Segerea (katikati mwenye shati la draft) akiwa kawekwa mtukati mara baada ya kuja na kutaka kusitisha uchaguzi bila sababu ya msingi. waliomzunguka ni wakazi wa mtaa wa segerea wakimuhoji afisa mtendaji huyo sababu ya kutaka kusitisha uchaguzi huo wakati hakukuwa na vurugu wala kero ya aina yoyote iliyojitokeza katika kituo cha kupigia kura cha Migombani.
 Wakazi wa Mtaa wa migombani wakumzuia afisa mtendaji kuondoka hadi pale atakapotangaza tena kuwa uchaguzi unaendelea
 Msimamizi wa Uchaguzi wa serikali ya Mtaa wa Migombani katika Kituo cha uchaguzi wa Migomabni akielezea sababu za kusimamisha uchaguzi huo kwa muda kutokana na kusubilia barua ya kumtaka kuendelea na uchaguzi kutoka kwa afisa mtendaji wa Kata ya Segerea aliyetaka kujaribu kusitisha Uchaguzi huo kwa kisingizio cha Kutumwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Segerea, Akiandika barua ya kutamka kuwa uchaguzi unaendelea mara baada ya wakazi wa mtaa wa migombani kutaka afisa huyo kueleza sababu za msingi za kutaka kujaribu kusitisha uchaguzi huo.Pembeni ni wakazi wa Mtaa wa Migombani wakishuhudia kuwa afisa mtendaji huyo anaandika ipasavyo hiyo barua.
Hii ndio barua aliyokuwa akiandika afisa mtendaji wa kata ya segerea inavyosomeka ambapo baadae alienda nayo ofisi kwa kuongozana na wakazi wa migombani kwaajili ya kugonga muhuri wa kata kuthibitisha kuwa uchaguzi unaendelea
Afisa mtendaji wa Kata ya Segerea (Mwenye shati la drafti) akiongea na wakazi wa mtaa wa migombani mara baada ya vurugu kutaka kutokea mara baada ya afisa mtendaji wa kata ya segerea kujaribu kusitisha uchaguzi bila sababu za msingi
Wakazi wa Mtaa wa migombani, Kata ya Segerea wakimzuia Afisa mtendaji huyo kuondoka mpaka atangaze tena kuwa uchaguzi unaendelea.Picha na Josephat  Lukaza wa Lukaza Blog
Na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog.
Hali ya Kushtusha imetokea katika uchaguzi wa Serikali ya Mtaa wa Migombani Mara baada ya Afisa Mtendaji huyo kuja na kutangaza kimyakimya Kuwa UChaguzi huo umesitishwa, Mara baada ya wakazi wa mtaa wa migombani kusikia ndipo walipoanza sasa kutafuta mchawi na kumtia nguvuni afisa mtendaji huyo wa mtaa kwa kutaka kujua sababu za msingi zinazopelekea yeye kuja kutangaza kusitisha uchaguzi huo.
Afisa mtendaji huyo baada ya kuulizwa sababu za msingi alijitetea kuwa ameagizwa na Mkurungenzi wa Uchaguzi wa Manispaa ya ilala. Mara baada ya Kutoa sababu hiyo ndipo wakazi wa mtaa wa migombani walipoona kuna dalili za kuchakachuliwa kwa kura zao ndipo walipomuweka mtu kati na kumtaka Afisa mtendaji huyo kutangaza kwa maandishi kuwa uchaguzi unaendelea ndipo wakazi hao walipomuweka mtu kati na kuhakikisha anaandika barua hiyo ya kutaka kuendelea na uchaguzi.
Mara baada ya wakazi wa mtaa wa migombani kwenda nae katika ofisi ya kata kwaajili ya kugonga muhuri kuthibitisha Uchaguzi huo kuendelea ndipo uchaguzi ukaendelea na muda huu zoezi la kuhesabu kura linaendelea

6TH ANNIVERSARY GROOVEBACK PARTY 2014 YAFANA NA BIA YA WINDHOEK DRAUGHT NDANI YA THE ARCADE HOUSE.

$
0
0
 Dj Pierra Kutoka Nchini Kenya nae hakuwa nyuma kuendeleza Burudani ya Muziki kwa ajili ya Kusherekea Grooveback Party iliyotimizia Miaka sita
 Ni mwendo wa ku party.
 
 Dj KT kutoka Tanzania akiwa anaangusha bonge la moja Burudani .....
 
 Hakuna kulala full ku party ...
 DJ Pinye Mkali kutoka nchini Kenya .. akiangusha Burudani ... Hii ilikuwa hatare sana Mashabiki walifurahia Burudani hii ya nguvu.
 Twende Dj Pinye...
.
 Dj Crusia Toni kutoka Nchini Kenya akiendelea na Burudani ya Nguvu ... Party inaendela..
Meneja Biashara wa Bia ya Windhoek Joseph Boniface akielezea kuhusiana na Grooveback Party ambayo wao wamekuwa wadhamini wakuu kwa mwaka 2014 katika kutimiza miaka sita ya Grooveback
 Wa pili kushoto ni Msimamizi  wa Windhoek Salum Kabanda akielezea ni jinsi gani wanavyotoa fursa kwa vijana na kuweza kuitumia hususani kwa wanamuziki ambapo wanaandaa matamasha mbalimbali na kuweza kuwa wadhamini wakuu hivyo kuwapa changamoto vijana kwa kuweza kuandaa michanganuo mbalimbali ya kazi kuifikisha kwao na kuifanyia kazi kwa kuwasaidia.
 
 Wahudumu wa The Arcade wakiwa katika Pouzi wakati wakiwahudumia wateja wao waliofika katika Sherehe ya Miaka Sita ya Grooveback iliyofanyia jana
 Dj JB akiendelea kumwaga Burudani ya nguvu ya ngoma za Zamani na kukuna nyoyo za watu wengi waliofika katika Sherehe hiyo.
 Wapambe wa Windhoek wakiwa wanapata Picha ya pamoja wakati wa Sherehe ya kuadhimisha Miaka sita ya Grooveback
 
 Wadau Mbalimbali wa Mabibo Beer and Wine wakiwa wanapata Kinywaji cha aina ya Windhoek Draught huku Burudani ya nguvu ikiendelea kutoka kwa Dj JB
 Mashabiki wa Grooveback na watumiaji wa Windhoek Draught wakiwa katika Tabasamu la Hatari ..

 Dj Nijo ambaye aliingia kwa awamu ya pili na kubadirisha radha ya muziki wa Lingara zile za Kitambo na kukonga nyoyo za wengi
 6th Anniversary Grooveback  Party 2014  Cheers ! na Windhoek Draught
Party ikiwa inaendelea huku Windhoek Draught zikiwa zimezagaa kwa kila Meza!

WANANCHI WAFURIKA KATIKA BANDA LA DEGE ECO VILLAGE, MLIMANI CITY- DAR

$
0
0
Muuzaji kutoka Hifadhi Builders Ltd akiongea na mteja kuhusu mradi wa Dege Eco Village jijini Dar es salaam hivi karibuni
Adam Jusab, Afisa Masoko akihojiwa na waandishi wa habari hivi karibuni na kulia kwake Bwana Nyenshile, Afisa Mauzo wa Hifadhi Builders
Muuzaji kutoka hifadhi Builders Ltd akiongea na mteja na kufafanua juu ya mradi huu wa Dege Eco Village iliyopo Kigamboni.
Banda lililopo Mlimani City la Dege Eco Village jijini Dar es salaam  Na Mwandishi Wetu. Wananchi wa jiji la Dar es Salaam wamepata nafasi ya kutembelea banda la Dege Eco Village na kufahamu juu ya mradi huo wa makazi bora unaofanyika Kigamboni eneo la Ras Dege. Akizugumza na wananchi waliotembelea banda hilo .

Afisa Masoko wa Hifadhi Builders Ltd inayosimamia mradi huo bw. Adam Jusab alisema kuwa mradi huo ni kwa ajili ya wananchi wanao hitaji makazi bora na mpaka sasa nyumba elfu mbili zimekamilika kati ya nyumba elfu saba. Mradi huo utajumlisha aina mbili ya nyumba yaani appartments na villas. Pia kutakuwa na huduma za shule, kituo cha polisi, maeneo ya burudani, kituo cha zimamoto na huduma za usafiri wa mabasi kwa uchache.'

 Aidha aliendelea kusema kwamba mradi huo utakamilika mwaka 2018. Pia aliendelea kusisitiza kwamba kama sehemu ya mazimio ya mwaka 2015 waTanzania wanashuariwa kununua nyumba zilizo kwenye makazi bora kama mradi huu wa Dege Eco Village. Kwa kumalizia aliwataka wale wote watakayohitaji kuwasiliana nao kufika kwenye ofisi zao zilizo mtaa wa Azikiwe Posta pembeni ya Benki ya NMB au kutembelea kwenye mtandao wa Dege Eco Village, www.degeecovillage.com au ukurasa wa facebook www.facebook.com/degeecovillage

Martha Mwaipaja apania kutumbuiza tamasha la krismass.

$
0
0
“TAMASHA linafanyika siku maalum ambayo Yesu Kristo amezaliwa, nitatoa huduma kwa njia ya uimbaji naomba wakazi wa mikoa yote mitatu wafike kwa wingi wale ambao hawanifahamu pia watanifahamu siku hiyo na wataguswa na kupata ujumbe uliotukuka,” anasema mwimbaji Martha Mwaipaja.
 
Mwimbaji huyo anasema kuwa amejipanga vilivyo ikiwa pamoja na kufanya maandalizi ya hali ya juu huku akisistiza kuwa atafanya makubwa katika tamasha la Krismasi ambalo litakuwa la pili kufanyika.
 
Mwaipaja anasema kuwa anawaomba mashabiki wafike kwa wingi kwa sababu amepewa nafasi hiyo ya kulihubiri neno la Mungu kupitia uimbaji hivyo yupo kwa ajili yao ni vema wakajitokeza kwa wingi kupata upako.
 
“Naimba kwa ajili ya kumtumikia Mungu, natoa huduma kwa njia ya uimbaji hivyo watanzania wajitokeze siku hiyo muhimu ya kuzaliwa kwa Yesu naamini watafurahi kwa jinsi ninavyofanya maandalizi ya tamasha hili kubwa ambalo limepangwa kufanyika siku yenye Baraka za Mungu,” 
Mwimbaji huyo anayevuma na nyimbo zake nyingi ambazo anatarajia kuziimba katika tamasha hilo la aina yake aliziita atakazoimba kuwa ni pamoja na Tusikate ‘Tamaa’ ambako alisema kuwa anaupenda wimbo huo kwa sababu wengi unawatia moyo.
 
Anasema kuwa  mbali ya wimbo huo ambao  upo kwenye albamu yake ya kwanza pia anatarajia kuimba wimbo wa ‘Ombi langu’ambao unapatikana katika albamu yake ya pili huku akifafanua kuwa maana ya wimbo huo kuwa mungu ametengeneza njia katikati ya aliowakumbuka nay eye yumo.

Wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma mjii wa Nanchang nchini China waanzisha umoja wao

$
0
0
Viongozi wa NATATA, toka kushoto ni Katibu Mkuu Halima Guga,Mwenyekiti Given Massawe na mratibu wa Elimu Abdulkarim Baksh.
  Mwenyekiti wa NATASA ,Given Massawe akipozi kwa picha na wadau wa NATASA, toka kushoto  ni Henry Mzava,Evance,Letitia Smith ambae yeye anatoka Namibia, Henry,Hamza Riyani, Charles na Mercy.
 M/kiti wa NATASA Given Massawe akikata keki ya ya kuzindua umoja huo pamoja kuazimisha miaka 53 ya Uhuru wa Tz huku katibu wake Halima Guga akishuhudia.

 Wakina dada wa Kitanzania wanaosoma kwenye mjii wa Nanchang ambao ni wanachama wa NATASA wakipozi kwa picha wakiwa na bendera zao za Tanzania siku ya uzinduzi huo.
 .Wakina dada wa Kitanzania wanaosoma kwenye mjii wa Nanchang ambao ni wanachama wa NATASA wakipozi kwa picha wakiwa na bendera zao za Tanzania siku ya uzinduzi huo.

 wadau wa NATASA wakiwa ndani ya ukumbi  wa Hotel ya XIN DIAN TI wakibadilisha mawazo mawili matatu na kukumbushana story mbali mbali za nyumbani Tanzania.
 Mzee wa Shekeli Geofrey Njalangi  na kitamba chake cheupe mkononi mbele kabisa akisataka rhumba siku ya uzinduzi huo wa NATASA pamoja na Charles kulia na Elvis kushoto kwake  ndani ya ukumbi wa  XIN DIAN TI HOTEL kwenye mjii wa Nanchang nchini CHINA.
Mo van der Mhando,Nanchang, China.
Wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma kwenye mjii wa  Nanchang nchini China wameanzisha umoja wao na  Jumamosi iliyopita wameuzindua rasmi umoja huo wenye lengo la kuwasaidia kwa mambo mbali mbali wakiwa kwenye nchi ya kigeni.
Jumla ya wanafunzi 54 wa Kitanzania wapo kwenye mjii huo wakiwa wanasoma kwenye vyuo mbali mbali na walikuwa hawana kitu chochote kinachowaweka karibu kama Watanzania na ndio maana wakaanzisha umoja huo.
Umoja huo unaojulina kwa jina la Nanchang, Tanzanian Students Association (NATASA) ulizinduliwa rasmi na mwenyekiti wake Given Massawe ambae alisema kuanzishwa kwa umoja huo lilikuwa ni wazo la muda mrefu na hatimae hivi sasa ndoto imetimia.Massawe alifafanua kuwa kwenye mingine ya nchini China ambako kuna wanafunzi wa Kitanzania nao wanajumuia zao ambazo zinawasaidia hivyo kwa wanafunzi wa Nanchang kuwa na umoja huo ni sehemu ya fungua milango kwao.
Mwenyekiti huyo amesema hivi sasa wapo kwenye harakati za kutengeneza katiba yao ambayo ndio itakuwa dira ya uongozi wao na pia kuzinduliwa kwa chama hicho ni msaada tosha kwa wanafunzi hao wa Kitanzania kuanzia kwenye masomo hadi maisha ya kila siku.
Uzinduzi wa umoja huo ulienda sambamba za sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania bara na hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa wanafunzi wa Nanchang kusherekea siku yao ya Uhuru wakiwa pamoja.

VITUO VITATU VYA WATOTO WENYE UHITAJI MAALUM VYAPOKEA ZAWADI ZA KRISMASI KUTOKA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF.

$
0
0
 Kulia ni Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Mkoa wa Shinyanga Erick Chinimbaga na wa kwanza kushoto ni Afisa Fedha kutoka PSPF Makao Makuu Samweli Haule wakiwakabidhi zawadi za Krismasi watoto wenye ulemavu wa ngozi katika kituo cha Buhangija kilichopo Shinyanga  zawadi za Sikukuu ya Krismasi hapa watoto wenzao wakipokea zawadi hizo kwa niaba.  

Akikabidhi Msaada huo Afisa Fedha wa PSPF kutoka Makao Makuu alisema kwamba Mfuko wa Pensheni wa PSPF unalo lengo la kuwasaidia watoto wenye Uhitaji Maalum ili nao waweze kujisikia wapo katika jamii kama watoto wengine na kwamba kuwa hapo sio ndio kwamba wametengwa, alisisitiza kuwa Hata watakapo kuwa wakubwa wengine wataikuta PSPF na watakuwa wanachama na wengine watakuja kufanya kazi kabisa katika mfuko huo.
 Mlezi wa Kituo cha Kulelea watoto yatima cha  Buloma Foundation kilichopo Picha ya Ndege Kibaha Bi Simphania Aidan wa kwanza kushoto akipokea Zawadi za Sikukuu ya Krismasi kwa niaba ya Msimamizi na Mwenye kituo hicho Bi.Fransisca Kyando Kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF , wa katikati ni Meneja wa PSPF Mkoa wa Pwani Msafiri Mugaka na wa kwanza kulia ni Afisa Mahusiano wa PSPF Coleta Mnyamani.  

Akikabidhi Msaada huo Meneja wa PSPF Mkoa wa Pwani Msafiri Mugaka alisema kuwa PSPF inatoa zawadi za Sikukuu ya Krismasi kwa watoto yatima ili nao washerekee vizuri na wasijisikie vibaya , aliongeza kuwa pamoja na PSPF kuwa na wanachama watu wazima lakini pia inafanya hivyo kwa watoto ili waanze kuijua PSPF wakiwa wadogo na wakiwa watu wazima waje kuikumbuka na kujiunga na Mfuko huo Bora wa Pensheni na hata kuja kufanya kazi katika Mfuko huo.

Nae Afisa Mahusiano wa PSPF kutoka Makao Makuu Coleta Mnyamani  Aliongeza neno kuwa Watoto yatima ni kama watoto wengine ambao wanahitaji kupata huduma na malezi Bora kama watoto wengine wenye wazazi au wanaolelewa bila shida yotote, alimalizia kwa kusema kuwa PSPF ipo pamoja na watoto hao wenye uhitaji na itaendelea kuwasaidia .
 Watoto wakipokea zawadi za Krismasi kwa Niaba ya wenzao
 Picha ya pamoja ya Ma Afisa wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF na watoto pamoja na Mlezi wao baada ya kupokea zawadi hizo kwa ajili ya Sikukuu ya Krismasi
 Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Mkoa wa Shinyanga wa pili kushoto  Erick Chinimbaga akimkabidhi zawadi Mmoja wa walezi wa watoto hao bwana Revocatus Robert   wa kwanza Kulia zawadi za Sikukuu ya Krismasi kwa Wasichana waliotoka katika Mazingira magumu wanaolelewa na Kituo cha Agape Mkoani shinyanga, wasichana hao walipata zawadi za Mafuta, Mbuzi, Mchele, Sabuni,Sukari pamoja na vitu.

Bodi ya Filamu Nchini yatoa wito kwa wamiliki wa Filamu kuweza kuwasilisha Filamu.

$
0
0
 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu , Joyce Fisoo  akiamwandikia kibali cha filamu mwakilishi wa kampuni ya Al- Riyamy Production Bakari Kassim almaarufu Mzee Jangala,(kulia) baada ya kufanya malipo ya filamu zao zote zikiwemo za zamani na mpya,leo jijini Dar es Salaam.
 Mwakilishi wa kampuni ya Al- Riyamy Production Bakari Kassim almaarufu Mzee Jangala,(kulia) akimuonyesha stakabadhi ya malipo Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu , Joyce Fisoo baada ya kufanya malipo ya kupata kibali kwa ajili ya filamu za kampuni hiyo,leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu , Joyce Fisoo  akimkabidhi kibali cha filamu mwakilishi wa kampuni ya Al- Riyamy Production Bakari Kassim almaarufu Mzee Jangala,(kulia) baada ya kufanya malipo ya filamu zao zote zikiwemo za zamani na mpya,leo jijini Dar es Salaam.
 Afisa Utamaduni wa Bodi ya Filamu Clarence Chelesi(kulia) akimpa mkono wa pongezi mwakilishi wa kampuni ya Al- Riyamy Production Bakari Kassim almaarufu Mzee Jangala,(kushoto) baada ya kupata kibali cha filamu,leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Utamaduni wa Bodi ya Filamu Simon Peter (kulia)  akimpa mkono wa pongezi mwakilishi wa kampuni ya Al- Riyamy Production Bakari Kassim almaarufu Mzee Jangala,(kushoto) baada ya kupata kibali cha filamu wanaotazama ni Afisa Utamaduni wa Bodi ya Filamu Clarence Chelesi(katikati) na   Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu , Joyce Fisoo (kushoto) ,leo jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Lorietha Laurence-Maelezo).


=======  ======  ======
Bodi ya Filamu Nchini yatoa wito kwa wamiliki wa Filamu kuweza kuwasilisha Filamu.
Lorietha Laurence -Maelezo
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu , Joyce Fisoo  ametoa wito kwa kampuni za Filamu nchini kuwasilisha filamu zao ili ziweze kuhakikiwa na kulipiwa  kwa kupata kibali cha kuingia sokoni  kama sheria ya filamu ya mwaka 1976 kifungu namba 4 inavyoeleza.

Akizungumza  katika ofisi za Bodi leo jijini Dar es Salaam, Fisoo ameipongeza  kampuni ya Al-Riyamy Production  ambayo imeweza kutimiza wajibu wake na kulipia filamu 134 ambazo zimepata kibali cha kupatiwa stamp za  TRA na hivyo kuwa tayari kuingia sokoni. Aliongeza kuwa kuna baadhi za  kampuni za filamu nchini zimekiuka utaratibu na kushindwa kuwasilisha filamu zao kwa Bodi ikiwemo filamu zile zilizoigizwa  miaka ya zamani ambazo zimekuwa zikionyeshwa bila kibali.

 “Nimefurahishwa sana  kwa namna ambavyo kampuni ya Al-Riyamy  Production kwa kufuata sheria na kanuni za filamu nchini, hivyo natoa wito kwa kampuni nyingine pia kuweza kufanya  hivyo ili kukuza uchumi wetu na wao waweze kufanya biashara bila usumbufu” alisema Fisoo.

Naye mwakilishi wa kampuni ya Al- Riyamy Production Bakari Kassim almaarufu Mzee Jangala, amewaomba wasanii wenzake wenye kampuni za filamu waweze kufuata taratibu na sheria za bodi ya filamu ili kukuza soka la filamu na kuinua uchumi wa nchi yetu.

“Nawasiii wasanii wenzangu na wamiliki wa kampuni za filamu nchini waweze kufuata sheria na kanuni za filamu ili tuweze kwenda vizuri kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake katika ulimwengu huu wa filamu” alisema Mzee Jangala. 

Baadhi ya kampuni ambazo zimeweza kuwasilisha kazi zao katika Bodi ya filamu ,ni pamoja na kampuni ya  Wananchi wote wamewasilisha filamu 119, Game First Quality filamu 35, steps Entertainment filamu 739, na Al-Riyamy Production  filamu 134.
  

FAINALI YA Airtel UNI255 UDSM INTER-COLLEGE CHAMPIONS LEAGUE YAHIMITISHWA

$
0
0
  Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Betram Mapunda akikagua wachezaji wa Chuo cha Uhandisi na Teknolojia, kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali ya mashindano ya vitivo mbalimbali vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, yaliyodhaminiwa na Airtel Tanzania kupitia huduma yake ya Uni 255, yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam juzi. Timu hizo zilitoka sare ya magoli 1-1 katika mpambano huo, uliomalizika kabla ya muda kufuatia giza kuingia na uwanja kukosa taa.Kushoto ni Meneja Masoko wa Airtel, Aneth Muga.
Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Betram Mapunda akikagua wachezaji wa Chuo cha Sayansi za Jamii, kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali ya mashindano ya vitivo mbalimbali vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, yaliyodhaminiwa na Airtel Tanzania kupitia huduma yake ya Uni 255, yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam juzi. Timu hizo zilitoka sare ya magoli 1-1 katika mpambano huo, uliomalizika kabla ya muda kufutia giza kuingia na uwanja kukosa taa.
 Wachezaji wa timu ya Chuo cha Sayansi za Jamii, wakijifua kwa mazoezi kabla ya mchezo wao dhidi ya timu ya Chuo cha Uhandisi na Teknolojia katika fainali ya mashindano ya vitivo mbalimbali vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, yaliyodhaminiwa na Airtel Tanzania kupitia huduma yake ya Uni 255, yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam juzi. Timu hizo zilitoka sare ya magoli 1-1 katika mpambano huo, uliomalizika kabla ya muda kufutia giza kuingia na uwanja kukosaa taa.

  Wachezaji wa timu za Chuo cha Sayansi za Jamii (jezi nyeusi) na Chuo cha Uhandisi na Teknolojia, wakigombea mpira wakati wa mchezo wa fainali ya mashindano ya vitivo mbalimbali vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, yaliyodhaminiwa na Airtel Tanzania kupitia huduma yake ya Uni 255, yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam juzi. Timu hizo zilitoka sare ya magoli 1-1 katika mpambano huo, uliomalizika kabla ya muda kufutia giza kuingia na uwanja kukosa taa.



======  ======  ========
Fainali ya Mashindano ya mpira wa miguu kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) yanayojulikana kama Airtel UNI255 yaliyoshirikisha wanafunzi wote wa schools na Colleges zilizopo chuoni hapo yamemalizika siku ya jumamosi ya tarehe 13/12/2014 Katika Fainali iliyovikutanisha vyuo vya Sayansi ya Jamii(College of Social Science)na Chuo cha Uhandisi na Teknolojia (College of Engineering and Technology) ambapo hadi dakika tisini(90) zinamalizika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) zilikuwa zimefungana bao 1-1.

Timu ya kitivo cha CoET iliyokua na upinzani mkali kwa jumla ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 20 ya kipindi cha kwanza mfungaji akiwa ni Justin Rupia kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa CoSS Chawaka Francis na kumfanya mwamuzi wa mpambano huo Wema Ngota pamoja na wasaidizi wake Benjamini Mbughi, Hellen Mduma, Iddi Mfaume, Ramadhan Pondamali,Jackison Msilombo, Ally Sarehe na Faraji Gaibu,walioichezesha michezo hiyo tangu tarehe 8 mwezi huu kuwa katika hali tete kutokana na shangwe, nderemo na vifijo kutoka kwa Mashabiki wa CoET kucharuka uwanja mzima.

Kipindi cha Pili kila timu ilifanya mabadiliko ambapo CoSS iliwatoa Emmanuel George na Morrison Ng’owo na nafasi zao kuchukuliwa na wachezaji Rashidi Hussen na Ramadhan Hussen dakika ya 67 na 75 huku wenzao wa kitivo cha CoET aliingia mchezajji Tibe Mario kuchukua nafasi ya mchezaji George Michael katika dakika ya 62 mabadiliko yaliyowanufaisha zaidi CoSS waliposawazisha bao dakika za Majeruhi baada ya kutokea piga nikupige na hivyo kuleta mtafaruku kutokana na Muda(Kiza) kuingia ambapo timu hizo zilishindwa kupigiana Penalti ili kupata mshindi wa kwanza na mshindi wa pili.

Katika michezo ya awali timu hizo za College of Social Science waliokuwa kundi B lililokuwa katika viwanja vya chuo kikuu za Mabibo maarufu kama Mabibo Hostel ilifanikiwa kuongoza vizuri ambapo ilicheza mechi 3 ikashinda moja na kutoa sare ya bila kufungana mechi 2. matokeo yalioyowapa pointi 5 na goli 2 na kufanikiwa kutinga hatua ya fainali.

Katika michezo ya awali timu ya Chuo cha Uhandisi na Teknolojia-College of Engineering and Technology(CoET) iliyokuwa kundi A lililokuwa katika viwanja vya chuo kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) ilifanikiwa kuongoza pia vizuri na kupata pointi zilizoiweka kwenye nafasi ya kucheza Fainali baada ya kushinda hatua ya nusu fainali dhi ya timu ya UDBS.

Timu iliyochukua nafasi ya tatu ni kitivo cha UDBS waliofanikiwa kuwafunga Kitivo cha SoED kwa njia ya penalty baada ya kumaliza dakika 90 kwa kufungana 2-2 katika mchezo uliokuwa wa upinzani mkubwa kutokana na timu ya SoED kuwa na wachezaji wengi wakongwe waliokaa muda mrefu hapo chuoni na wameshiriki michuano mingi na wamefanya vizuri na ndiyo timu pekee iliyokuwa ikipewa nafasi kubwa ya kunyakua Uchampioni huo wa Chuo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti timu Capateni wa Timu zilizoshiriki hatua ya nusu fainali, Bodoo Oduon wa Timu ya CoET, Michezo hiyo imeleta changamoto kubwa kwa wanafunzi na kuwataka wadhamini kujitokeza kudhamini michezo ya vyuo vya mkoa wa Dar es Salaam.

“Tumefurahi pamoja, tumecheza na kuruka ruka hii ni shangwe, tena mimi nasema hawa Airtel hakika wanatakiwa kuwa mfano wa kuigwa, ni pesa ngapi wamewekeza hapa, na hii ni kwa Chuo Kimoja tu ch UDSM na bado kuna hiyo michuano ya vyuo vya Dar es Salaam, ni muunganiko mzuri unaoletwa na hawa Airtel kwa kutuunganisha kati ya vyuo na vyuo”alisema Bodoo Oduon.

Kuhusu kutopata matokeo ya Mshindi wa kwanza timu kampteni wa CoSS  Elias Mshomba alisema kuwa ni kawaida kutokea jambo hilo, maana Fainali ilihusisha watoto wa baba mmoja, kwamba jambo kubwa ni juu ya hizo College zilizoingia fainali kuwa wawakilishi wa College Championship Dar es Salaam inayotazamiwa kuunguruma mapema kuanzia mwezi wa tatu mwakani.

“Wewe unadhani kuna jambo limeharibika hapa kwa kutopata mshindi wa kwanza ama wa pili, sisi tulikuwa katika mchujo wa kupata wawakilishi wa chuo, kama ni zawadi zote ni za UDSM, hivyo nawaomba wachezaji wote waliofanikiwa kuzifikisha timu zao hatua ya nusu fainali, kuendelea na maandalizi makali ya kuhakikisha tunatwaa hizo zawadi zinazokuja za ushindani wa vyuo vya Dar es Salaam, mwenyewe umeona kiza kimeingia hivyo wachezaji wasingekuwa na uwezo wa kumaliza penalty tano kabla ya usiku na hapa hakuna taa, tusubiri hiyo michuano ambayo sijui wadhamini ni nani kama watakuwa ni Airtel basi itakuwa Raha sana maana tumefurahishwa na Airtel” alisema Elias Mshomba.

Akiongea kuhusiana na mwenendo wa mashindano hayo kwa Waziri wa michezo wa jumuiya ya wanafunzi chuo kikuu cha Dar es salaam STANLRY JULIUS alisema “Mashindano ya mwaka huu yamekuwa na mvuto wa kipekee hasa kutokana na wadhamini wetu Airtel kutupatia vifaa vya kutosha na kwa namna moja yameongeza hari sana kwa washiriki wote, na Pengine hii imekuwa ni changamoto kwetu kutokana na Uwepo wa Michuano ya Wanavyuo, College Championship Tanzania” alisema.

 Na kuongeza kuwa “sisi kama UDSM tumepewa heshima kubwa ya kutoa wawakilishi wane watakaoungana na College zingine Kuunda jumla ya Timu 32 za College Kanda ya Mashariki,hivyo tumefaidika sana sisi kama chuo, kwa kuwa jambo lingine tumeweza kufanya Selection (Usahili) wa kupata timu ya chuo (UDSM ALLY STARS)ambayo inaweza kuwakilisha chuo kwenye michezo ya EAST AFRICAN UNIVERSITIES COMPETITION, inayoshirikisha nchi za Afrika mashariki kwa michezo ya Vyuo Vikuu,lakini pia nichukue Fulsa hii kuwaomba tena Airtel, kupitia hii hii Airtel UNI255 kuweza kudhamini hatua inayofuata ya Michezo ya Vyuo kwa Mkoa wa Dar es Salaam, NACTE & Inter College Championship-Dar es Salaam,itakayoshirikisha jumla ya vyuo 32, Kama ulivyoona mwenyewe jinsi ushindani ulivyomkubwa na hata soka lenyewe lipo vyuoni,shamra shamra zote hizi hapa ni chuo kimoja je itakapokuwa imekutanisha vyuo vingine kama vile IFM,DIT,NIT,TRA,ISW,IAE,BANDARI COLLEGE,CBE, DACICO, HEDEN HILL, NJUWENI, MUHIMBILI MEDICAL SCHOOLS, KIBAHA COTC na St. JOSEPH UNIVERSITY ambazo tayari zimefuzu hatua ya Makundi yake ya Michuano ya Bonanza la NACTE INTER COLLEGE DAR ES SALAAM BONANZA unadhani shamra shamra zitakuwaje, na tunaomba hiyo Fainali ya College za Dar es Salaam ifanyike Uwanja wa Taifa ili TFF na Makocha wa Timu ya Taifa waje wachague wachezaji watakaoisaidia Tanzania katika michuano ya Taifa na kimataifa”alisema STANLRY.
    
Timu iliyoonyesha nidhamu  na Ushindani mkubwa wa kuwania hizo nafasi wakati wa mchujo huo wa College ya UDSM ili kuingia kwenye ushiriki wa michuano ya Vyuo vya Dar es Salaam ni SJMC iliyokuwa kinara wa kundi A katika viwanja vya ndani ya chuo kikuu cha Dar es salaa ni (School of Journalism and Mass Communication) ilicheza mechi mbili na kushinda zote na kujitengenezea pointi 6 na huku akiongoza kwa kuwa na bao 5 za kufunga.

Akizungumzia michezo hiyo kwa upande wa College za UDSM mratibu  wa College za chuo hicho bwana. Albert Kimaro alisema kuwa “ Kundi B ambalo mechi zake zilichezewa katika viwanja vya chuo kikuu za Mabibo maarufu kama Mabibo Hostel, ndilo lililokuwa na timu zenye wachezaji wakongwe na liliongozwa na COSS (College of Social Science) timu iliyokuwa na mashabiki wengi na ambayo imeweza kucheza Fainali, lakini pia ndani ya UDSM zimeshiriki College kama CONAS, ambayo pia ilikuwa na wachezaji wazuri, UDSL,  COET, COICT,ISK,na COHU” alisema Albert.

Mgeni Rasmi katika Fainali hiyo Profesa Mapunda Mapunda baada ya ukaguzi wa wachezaji aliwaasa kuwa na utulivu, Upendo, mshikamano,  wakati wote wa michezo na waepuke ugomvi wakati wote kwani michezo ujenga na kuimarisha mahusiano mwao.

“kikubwa hapa ni jinsi ya kujenga misingi imara ya michezo ndani ya vyuo vyetu, sina maana katika chuo hiki pekee, bali vyuo vyetu vyote, lakini pia niseme kwamba miaka ya nyumba hatukuwa na hamasa ya michezo vyuoni kutokana na miundo mbinu, lakini wakati huu nadhani kwamba michezo ama vipaji vipo vingi vyuoni, nimesikia kuna kampuni ya MIDETA entertainment imeanza harakati za kuanzisha hii michezo ya vyuo vyote vya Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla,inayojulikana kama College Championship Dar es Salaam, ambapo kwa sasa kuna mtowano mwingine unaendelea wa vyuo vingine kupitia mfumo uliowekwa wa Bonanza la Nacte inter College Dar Es Salaam ili kupata timu zitakazoshiriki ligi hiyo itakayokuwa na timu 32, nina hakika kwamba michuano itakuwa mizuri na itapendwa sana na pia itazalisha vijana wengi watakaokuwa wasomi kasha wawakilishi wetu kimichezo” alisema Profesa Mapunda.

 Naye Meneja Uhusiano wa Airtel Jackison Mbando alisema kuwa kuwa Mashindano yalikuwa mazuri na timu na kwamba imewapa changamoto ya kuongeza udhamini kwenye michezo ya vyuo, “ kama unavyoona mwenye jinsi Fainali ilivyosheheni watu utadhani mechi yay a Mtani Jembe, upinzani ni mkubwa sana na imeleta changamoto sana, lakini kubwa ni kuhakikisha kwamba Airtel inawafikia Watu wote kwa namna ya pekee,

Tupo katika harakati za kuboresha maisha ya wanavyuo kwani tunatambua kwamba wanahitaji kusoma kwa kutumia Mitandao katika ulimwengu huu wa sasa ambao Airtel kama unavyoona ni zaidi ya mitandao mingine, tunaanza sisi kisha wanafuata wengine nah ii tumeanza kwa kuwa karibu na wanavyuo ili tuwape nafuu katika usomaji na upataji wa mawasiliano, lakini si hivyo tu kama unavyoona hapa leo mambo yamenoga katika kuwapa pia afya wanafunzi wa vyuo kwani Michezo inaleta afya ndiyo maana tumeamua kuingia sasa kusaidia na kudhamini hii michezo ya Vyuo, na sasa tumeanza na College za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, tunatarajia kufanya mazungumzo na waandaaji wa Michezo ya vyuo kwa Mkoa wa Dar es Salaam (MIDETA entertainment) tupate mahitaji yao tuangalie, uwezekano upo wao waje tuzungumze na ikibidi hata kupata timu bora ya College za Tanzania,(College Championship Tanzania”alisema Jackison Mbando.

Aidha katika kilele cha tamasha hilo Airtel ilizindua kwa wanafunzi wa chuo kikuu huduma ya UNI255 itakayowawezesha kuwasiliana , kuperuzi internet kwa gharama nafuu.

CCM YAONGOZA UWENYEKITI WA MTAA MKOA WA ARUSHA

$
0
0
Na Woinde Shizza,Arusha

Chama cha mapinduzi kimeibuka kidedea katika uchaguzi wa uwenyekiti wa mitaa katika mitaa yote iliopo ndani ya mkoa wa Arusha baada ya kuvishinda vyama vingine vya upinzani .

Akitangaza  matokeo ya uwenyeviti wa mitaa Mkurugenzi wa jiji la Arusha Iddi Juma alisema kuwa mpaka sasa uchaguzi wa uwenyekiti umekamilika katika mitaa yote na vituo vyote isipokuwa kituo kimoja ambacho uchaguzi wake utarudiwa siku ya kesho.

Alisema kuwa   katika uchaguzi huu jumla ya wananchi  1,13909 walijiandikisha kupiga kura na jumla ya vyama sita vilisimamisha wagombea katika kila mtaa ambapo alitaja vyama ambavyo vilisimamisha wagombea kuwa ni pamoja na ACT,chama cha mapinduzi CCM,NCCR mageuzi ,CUF pamoja na TLP   .

Akitaja matokeo ya uwenyekiti wa mitaa alisema kuwa ccm imeweza kuongoza kwa kupata mitaa mingi zaidi ambapo alisema kuwa CCM imeweza kupata kura 78 ambapo kati ya kura hizo kura sita ni za kupita bila kupigwa, ikifuatiwa na chadema ambao wana kura 75 ,ACT ikiwa aijapata kura ,NCCR ikiwa aijapata kura ,CUF ikiwa aijapata kura pamoja na TLP

Aidha alibainisha kuwa jumla ya vituo 154 vilikuwa wepo kwa ajili ya kupigia kura na vyote vimekamilisha uchaguzi isipokuwa kimoja ambapo kilifutiwa matokeo hayo na kulazimika kurudiwa ambapo alisema kuwa katika kituo hicho uchaguzi utarudiwa hapo kesho .

mpaka sasa uchaguzi wa uwenyekiti umemalizika ila tumelazimika kurudia uchaguzi katika vituo vitatu ambapo katika vituo hicho kituo kimoja ambacho ni cha Oysterbay uchaguzi utarudiwa kwa watu wote na maanisha uchaguzi wa kuanzia kwa mwenyekiti wa mtaa ,wajumbe  watano pamoja na wajumbe watatu wa viti maalumu huku katika kituo cha AICC -Sekei uchaguzi utarudiwa kwa wajumbe watatu wa viti maalumu ambapo hii inatokana na kura za kufungana kwani wote walipata 31 kwa 31  na katika kituo cha Oldpolisi line ambapo napo uchaguzi utarudiwa kwa watu wawili ambao nao pia  ni wajummbe wa viti waamaalu  walifungana kwa kura 64 kwa 64.

Juma alisema katika uchaguzi wakesho ambao  wanarudia wamejipanga vizuri kusimamia kwani nguvu zote wanazielekeza katika vituo hivyo ambapo alibainisha kuwa katika kila kituo kutakuwa na wasimamizi nane pamoja na ulinzi wa kutosha  .

Aidha alitumia fursa hii kuwashukuru wananchi wate na viongozi kwa kufanya uchaguzi wa amani na kistarabu  pamoja na kuvumiliana huku akiongeza kuwaanamatumaini utulivu huu na uvumilivu walionyesha utaendelea hata katika vituo hivi ambavyo vinarudiwa.
Viewing all 46371 articles
Browse latest View live




Latest Images