Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

WANAJESHI KUTOKA CHUO CHA KIJESHI CHA KENYA WATEMBELEA TBL

$
0
0
 Mpishi Mkuu wa Bia wa Kiwanda wa cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dar es Salaam, Kelvin Nkya akitoa maelezo ya jinsi bia inavyochachuliwa wakati wanajeshi kutoka Chuo cha Jeshi Kenya walipotembelea kiwanda hicho jana, wakiongozwa na maofisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)
Wanajeshi kutoka Chuo cha Jeshi Kenya, wakipata maelezo kutoka kwa Mpishi Mkuu wa Bia wa Kiwanda wa cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dar es Salaam, Kelvin Nkya (kushoto),  kuhusu mitungi inayotumika kupikia bia  walipotembelea kiwanda hicho jana, wakiongozwa na maofisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
 Wanajeshi wakioneshwa   shayiri inayotumika kutengenezea bia
 Mpishi Mkuu wa Bia wa Kiwanda wa cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dar es Salaam, Kelvin Nkya akitoa maelezo ya jinsi bia inavyopikwa kwa kutumia njia ya kisasa ya kompyuta wakati wanajeshi kutoka Chuo cha Jeshi Kenya walipotembelea kiwanda hicho jana, wakiongozwa na maofisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Wanajeshi kutoka Chuo cha Jeshi Kenya, wakipata maelezo kutoka kwa Mpishi Mkuu wa Bia wa Kiwanda wa cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dar es Salaam, Kelvin Nkya (kushoto),  jinsi bia inavyopimwa ubora katika maabara  walipotembelea kiwanda hicho jana, wakiongozwa na maofisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)
 Askari hao wakitembelea maabara ya kiwanda hicho
 Wakiwa katika moja ya mitambo ya kutengenezea bia
Wanajeshi kutoka Chuo cha Jeshi Kenya, wakitembelea Kiwanda cha Bia cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dar es Salaam jana, wakiambatana na maofisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
 Nkya akijibu maswali ya askari hao
Oriyo akielezea mafanikio ya TBL na jinsi kampuni hiyo inavyoongoza katika pato la Taifa
 Kanali Jimmy Mutai kutoka Chuo cha Jeshi Kenya akitoa shukurani kwa TBL BAADA UJUMBE WAO KUTEMBELEA KIWANDA
 Kanali Mutai akikabidhi zawadi kwa Meneja wa Kiwanda hicho, Carvin Martine
Meneja wa Kiwanda cha Bia cha TBL Dar es Salaam, Calvin Martine akimkabidhi zawadi Ofisa wa Jeshi la JWTZ,  aliyeongoza ujumbe huo, Brigedia Jenerali Dominic Mrope
Martine akimkabidhi zawadi Ofisa kutoka Ofisi ya Rais Mipango na Ugatuzi, Purity Masikombe
 Meneja wa Mawasiliano-Mambo ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania, Emma Oriyo (kulia), akiagana na baadhi ya wanajeshi kutoka Chuo cha Jeshi Kenya baada ya kutembelea kiwanda cha TBL Dar es Salaam jana, wakiongozwa na maofisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Ujumbe huo ukitembelea idara ya ujazaji bia kwenye chupa na makopo

Viongozi wa TBL wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa wanajeshi hao

MDAU ANGELA AKILIMALI NA WENZAKE WALA NONDO YA MAWASILIANO YA UMMA

$
0
0
Kaimu Mgukurugeni wa Uhuru FM, Angela Akilimali (katikati) akiwa na wahitimu wenzake wa Shahada ya Mawasiliano ya uma ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) katika mahafali yaliyofanyika hivi katibuni mkoani Kibaha mkoani Pwani.  Kushoto ni Hemed Mbaraka na Mganwa Nzota.
 Wanahabari wa morogoro nao walikula nondo zao katika mahafali hayo.
 Angela Akilimali akiwa na mumewe Hassan Hemedi Chamshama baada ya kumkabidhi shada la maua wakati akimpongeza.
 Toka kushoto ni Idda Mushi wa ITV/Redio One - Morogoro, Angela Akilimali wa Uhuru FM na Hana Mayige  wa TBC wakipozi kwa picha wenye furaha baada ya kula nondo zao. PICHA ZAIDI BOFYA>>>>KIDEVU BLOG.

BW. GEORGE SHINGA MTAMBALIKE KUUFANYA MTAA WA MOGO KIPAWA KUWA WA KISASA

$
0
0
1
 Mgombea wa Uenyekiti wa Mtaa wa Mogo kupitia Chama cha Mapinduzi Bw. George Shinga Mtambalikeakizungumza na waandishi wa habari huko Ukonga majumba siti wakati akizungumzia juu ya kameni za uchaguzi huo ambazo zinatarajiwa kufungwa kesho kabla ya uchaguzi kufanyika jumapili Desemba 14.
2
Mgombea wa Uenyekiti wa Mtaa wa Mogo kupitia Chama cha Mapinduzi Bw. George Shinga Mtambalikeakizungumza  na vijana mbalimbali wakati alipokutana nao katika ukumbi wa Kiota Ukonga jijini Dar es salaam.

………………………………………………………………………
IMEBAINISHWA kuwa endapo wananchi wa kata ya Kipawa Mtaa wa mogo watakichagua Chama cha Mapinduzi CCM kupitia  Mgombea wake George Shinga Mtambalike,basi mtaa huo anampango wa kuufanya kuwa mtaa wa kisasa kama ilivyokuwa mitaa  mingine Duniani.

Kauli hiyo imetolewa Dar es Salaam jana na Mgombea wa Chama cha hicho kwa nafasi ya uwenyekiti wa Serikali ya Mtaa  wa Mogo,wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini.

Alisema kuwa wananchi kama watampa nafasi ya kuwa kiongozi wao katika mtaa huo wa mogho basi malengo yake ni kuona  Mtaa wa Mogo unakuwa katika sura ya tofauti ambapo pia atahakikisha mtaa huo unapimwa na kuwa katika mipango miji.

“Kimsingi wananchi wa Mtaa huu wanatakiwa wasifanye makosa wahakikishe wanakichagua chama cha Mapinduzi ili kuweza 

kutimiza ndoto za maendeleo katika mtaa huu wa Mogo ambao kwa muda mrefu umekuwa ukikabiliwa  na changamoto za 

kutosha,’alisema Mtambalike

Alisema kuwa mbali na kubadilisha mtaa huo pia atahakikisha kuwa makundi yote yaliyopo katika mtaa huo yanakuwa 

katika utambuzi ili kuweza kuzifikia kwa uhalaka fursa zinazojitokeza kupitia Ofisi ya Serikali ya Mtaa.

Akizungumzia miundombinu alisema kuwa kumekuwepo na changamoto kubwa ya miundombinu hivyo hatua ya kwaza baada ya 

kuingia madarakani ni kuhakikisha mazingira yanakuwa safi kwa maana ataunda vikundi mbalimbali ya kuzoa taka pamoja 

na kuimarisha ulinzi shiriki na utekekelezaji huo wote utafanywa na wakazi wa mtaa husika wa mogo.

Alisema kuwa malengo yake mengine ni kuona mtaa huo unamiliki Studio kwa ajili ya vijana,wanajenga Soko la kisasa 

ambalo kwa sasa wananchi wanapata shida na wanalazimika kwenda Buguruni kwa ajili ya kufata mahitaji yao muhimu ya 

nyumbani.

“Katika kuhakikisha haya yote tunakwenda kuyafanya basi ni muhimu wakazi kukichagua Chama cha Mapinduzi Disemba 14 

siku ya Juma pili ambapo vituo vitafunguliwa kuazia saa 2 asubuhi,’alisisitiza

TIMU YA TANZANIA WAICHAPA EALA MABAO 4-0

$
0
0
SAM_0069Timu ya Tanzania.
 
Timu ya Tanzania jana wailiichapa timu ya EALA mabao 4 kwa 0 ambapo Mh. Joshua Nassari alifunga bao la kwanza na bao la pili kufungwa na na mchezaji mahiri Yusuph Gogo na la tatu kufungwa na Ahmed Ngwali na bao la  nne timu ya EALAwalijifunga wao wenyewe kupitia kwa beki wao Wyclif Keto katika harakati za kuokoa mpira
SAM_0070Timu ya EALA
SAM_0073Naibu Waziri   wa  Fedha   Adam  Malima kiongozi wa timu ya Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na waamuzi wa mechi kati ya Tanzania na EALA jana katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha
SAM_0077
Mashabiki wakiwa wanafatilia mpambano kati ya Tanzania na Bunge la EALA jana katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
SAM_0080Mlinda malango timu ya Tanzania Mh.Idd Azan akijiweka sawa golini kuhakikisha magoli hayaingii
SAM_0079Mlinda mlango timu ya EALA akiwa anajiandaa kudaka mpira
SAM_0098Dk Hamisi Kigangwala mchezaji wa Tanzania akiwa uwanjani
SAM_0086Mh.Joshua Nassari mchezaji wa timu ya Tanzania  akiwa amenyanyua t-shart yake juu mara baada ya kuipatia timu yake bao la kwanza ujumbe ulikuwa ukisomeka hivi"ESCROW hela zetu"
SAM_0109Muonekano wa wachezaji uwanjani
SAM_0105Mabalozi kutoka Model of Tourism Tanzania wakiwa wanashangilia wakati timu ya Tanzania na EALA wakipambana uwanjani.(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)

Wateja wa TTCL Kununua Salio Kupitia ‘Mobile Banking’

$
0
0
Meneja Mipango na Mauzo wa TTCL, Benjamin Bizere (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya uzinduzi wa huduma ya kuongeza salio kwa kupitia simu za mkononi (Mobile Banking) ambapo sasa mteja wa TTCL ataweza kuongeza salio kupitia simu yake ya mkononi (TTCL top-up). Meneja Mipango na Mauzo wa TTCL, Benjamin Bizere (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya uzinduzi wa huduma ya kuongeza salio kwa kupitia simu za mkononi (Mobile Banking) ambapo sasa mteja wa TTCL ataweza kuongeza salio kupitia simu yake ya mkononi (TTCL top-up).Meneja Mipango na Mauzo wa TTCL, Benjamin Bizere (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya uzinduzi wa huduma ya kuongeza salio kwa kupitia simu za mkononi (Mobile Banking) ambapo sasa mteja wa TTCL ataweza kuongeza salio kupitia simu yake ya mkononi (TTCL top-up). Kulia ni Mkuu wa Mauzo wa TTCL, William Chamla. Meneja Mipango na Mauzo wa TTCL, Benjamin Bizere (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya uzinduzi wa huduma ya kuongeza salio kwa kupitia simu za mkononi (Mobile Banking) ambapo sasa mteja wa TTCL ataweza kuongeza salio kupitia simu yake ya mkononi (TTCL top-up). Kulia ni Mkuu wa Mauzo wa TTCL, William Chamla.Kutoka kulia ni Meneja Mipango na Mauzo wa TTCL, Benjamin Bizere, Mkuu wa Mauzo wa TTCL, William Chamla, Ofisa Habari wa TTCL, Edwin Mashasi wakizungumza na wanahabari (hawapo pichani) juu ya uzinduzi wa huduma ya kuongeza salio kwa wateja wa TTCL kupitia simu za mkononi 'Mobile Banking'. Kutoka kulia ni Meneja Mipango na Mauzo wa TTCL, Benjamin Bizere, Mkuu wa Mauzo wa TTCL, William Chamla, Ofisa Habari wa TTCL, Edwin Mashasi wakizungumza na wanahabari (hawapo pichani) juu ya uzinduzi wa huduma ya kuongeza salio kwa wateja wa TTCL kupitia simu za mkononi 'Mobile Banking'Ofisa Habari wa TTCL, Edwin Mashasi (aliyesimama) akiwatambulisha waandishi wa habari (hawapo pichani) maofisa wa TTCL, Kutoka kulia ni Meneja Mipango na Mauzo wa TTCL, Benjamin Bizere na Mkuu wa Mauzo wa TTCL, William Chamla kabla ya uzinduzi wa huduma ya kuongeza salio kwa wateja wa TTCL kupitia simu za mkononi 'Mobile Banking'. Ofisa Habari wa TTCL, Edwin Mashasi (aliyesimama) akiwatambulisha waandishi wa habari (hawapo pichani) maofisa wa TTCL, Kutoka kulia ni Meneja Mipango na Mauzo wa TTCL, Benjamin Bizere na Mkuu wa Mauzo wa TTCL, William Chamla kabla ya uzinduzi wa huduma ya kuongeza salio kwa wateja wa TTCL kupitia simu za mkononi 'Mobile Banking'.

 KAMPUNI ya Simu nchini Tanzania (TTCL) sasa imerahisisha upatikanaji wa vocha zake baada ya kuingia makubaliano kuishirikiano na benki 13 nchini zinazotoa huduma zake pia kwa kupitia simu za mkononi (Mobile Banking) ambapo sasa mteja wa TTCL ataweza kuongeza salio kupitia simu yake ya mkononi (TTCL top-up).

 Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Meneja Mipango na Mauzo wa TTCL, Benjamin Bizere alisema huduma hiyo ya kununua salio kwa njia ya simu kupitia mabenki 13 imeanza kufanya kazi hivi sasa hivyo mteja wa TTCL anaweza kununua salio lake popote alipo kwa kutumia simu yake. 

 Alisema TTCL imeingia makubaliano ya kiushirikiano katika uuzaji wa muda wa maongezi kwa benki za Standard Chartered, Akiba Commercial (ACB), Tanzania Postal Bank (TPB), Exim Bank, Dar Es Salaam Community Bank (DCB), Mkombozi Bank, KCB Bank pamoja na Bank of Africa ambazo wateja wa beki hizo wanaweza kununua salio kupitia simu zao popote walipo kwenye akaunti zao. “…Jumla ya benki 13 zimeingia ubia wa kibiashara na TTCL kwa ajili ya kuuza vocha za TTCL kupitia benki zao…hapo juu nimetaja majina ya benki zote ambazo zinatumika kwa ajili ya kufanya miamala mbalimbali ikiwemo TTCL TOP-UP,” alisema Bw. Bizere. 

Akifafanua zaidi juu ya huduma hiyo Mkuu wa Mauzo wa TTCL, William Chamla alisema huduma ya TTCL TOP-UP na Mobile banking ni njia ambayo TTCL imeanzisha kwa wateja wake kwa ajili ya kuongeza salio la muda wa maongezi kwa simu za mezani, mkononi na kununua vifurushi vya intaneti hivyo mteja ataweza kununua salio lake muda wowote na popote. “…Mteja atakayenufaika na huduma hii ni yule mwenye akaunti ya benki, na amejisajili katika huduma ya kibenki kupitia simu ya mkononi yaani 'mobile banking'.

 Hata hivyo alisema ili kuwarahisishia upatikanaji wa huduma kwa wateja wa wao vocha za TTCL pia zinapatikana katika vituo vya Maxmalipo na Selcom ‘wireless Point’ na kwenye Ofisi za TTCL, pamoja na vituo vya huduma kwa wateja ambako viko katika kila mkoa na wilaya.

Tanzania yasaini mkataba wa Sh. bilioni 15.5 kutoka benki ya ADB kuboresha kituo cha utafiti MUHAS.

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya fedha Bw. Servacius Likwalile (kushoto) akisaini Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa ajili ya kuboresha kituo cha utafiti wa magonjwa ya moyo kinachosimamiwa na Chuo Kuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Muwakilishi wa Benki ya ADB nchini Tonia Kandiero akisaini mkataba huo kwa niaba ya Rais wa benki hiyo Dkt. Donald Kaberuka.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donan Mmbando (kushoto) akitoa neno la shukurani baada ya kusainiwa  Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa ajili ya kuboresha kituo cha utafiti wa magonjwa ya moyo kinachosimamiwa na Chuo Kuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) leo jijini Dar es salaam. Wa kwanza kulia ni Muwakilishi wa Benki ya ADB nchini Tonia Kandiero na katikati ni Katibu Mkuu Wizara ya fedha Bw. Servacius Likwalile.

 Katibu Mkuu Wizara ya fedha Bw. Servacius Likwalile (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam wakati wa kusaini Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa ajili ya kuboresha kituo cha utafiti wa magonjwa ya moyo kinachosimamiwa na Chuo Kuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
(Picha zote na Eleuteri Mangi – MAELEZO).

Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
12/12/2014.
Serikali ya Tanzania imetiliana saini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 9.4 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 15.5 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa ajili ya kuboresha kituo cha utafiti wa magonjwa ya moyo kinachosimamiwa na Chuo Kuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).

Mkataba huo wa makubaliano umesainiwa leo jijini Dara es salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Muwakilishi wa Benki ya ADB nchini Tonia Kandiero kwa niaba ya Rais wa benki hiyo Dkt. Donald Kaberuka.

Dkt. Likwelile alisema kuwa kituo hicho kitasaidia kupunguza tatizo la wataalam wa afya nchini na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na hivyo kupunguza idadi kubwa ya  wagonjwa wanaotibiwa nje ya nchi.

Kwa upande wake Muwakilishi wa Benki ya ADB nchini Tonia Kandiero ameipongeza Tanzania kuwa nchi ya kwanza kusaini mkataba huo kati ya nchi nne za jumuiya ya EAC zinazokusudiwa kujenga kituo kama hicho.

Bi Tonia alisema kuwa benki ya ADB imejiwekea lengo kuboresha rasilimali watu katika fani ya afya ambapo mradi wa ujenzi wa kituo kinachojengwa MUHAS upo katika mkakati wa benki hiyo ambao uulianza 2011 hadi 2015, mpango mkakati wa benki wa 2013 hadi 2017 na mfumo mpya wa elimu katka nchi za Afrika.

Mfumo huo unalenga kutatua tatizo la utaalaam katika soko la ajira kwa kupitia vituo bora vya kanda vya afya ili kuendana na dira ya maendeleo ya Taifa na mkakati wa kupunguza umasikini ifikapo mwaka 2025.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donan Mbando ameushukuru uongozi wa benki ya ADB kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania na kuahidi fedha hizo zitatumiwa kwa malengo yaliyokusudiwa.

Hadi kukamilika kwa kituo hicho cha afya kinachojengwa katika chuo cha MUHAS kitagharimiwa na benki ya ADB kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania.


MBATIA AWANADI WAGOMBEA WA CHAMA NCCR-MAGEUZI KATIKA JIMBO LA VUNJO.

$
0
0
Kikundi cha Nyimbo cha Mlimbo Uwo kikitoa burudani wakati wa kampeni za Chama cha NCCR-Mageuzi za kuwanandi wagombea wa nafasi mbalimbali katika kijiji cha Mlimbo Uwo katika jimbo la Vunjo.
Wananchi katika kijiji cha Mlimbo Uwo wakijibu salamu ya chama cha NCCR-Mageuzi katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha Mlimbo Uwo. 
Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi,James Mbatia akimtambulisha mwenyekiti wa kitongoji cha Pangara ,Humphrey Machange aliyepita bila kupingwa katika kitongoji hicho kwa tiketi ya chama cha NCCR-Mageuzi.
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi James Mbatia akihutubia wananchi katika kijiji cha Mlimbo Uwo wakati akiwanadi wagombea katika kampeni za kuwania nafasi mbalimbali za ungozi katika kijiji hicho.
Diwani wa kata ya Mwika Kusini kwa tiketi ya TLP,Meja Jesse Makundi akizungumza katika mkutano wa kampeni wa kuwanadi wagombea wa chama cha NCCR-Mageuzi katika kijiji cha Mlimbo Uwo.
Diwani wa kata ya Kilema Kusini kupitia TLP akisalimiana na Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi James Mbatia wakati wa mkutano wa kampeni za kuwanadi wagombea wa nafasi za Uenyekiti katika kijiji cha Mlimbo Uwo.
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi ,James Mbatia akionesha kitabu alichoandika kuhusu Uwajibikaji katika Uongozi ,kitabu ambacho amekigawa jimbo zima la Vunjo.
Wananchi katika kijiji cha Maring'a wakimpokea Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi James Mbatia kwa majani ya Masale wakati alipofika kuwanadi wagombea wa nafasi za Uenyekiti kupitia chama hicho.
Diwani wa kata ya Miwka Kusini kwa tiketi ya TLP ,Meja Jesse Makundi akihutubia katika mkutano wa kampeni wa chama cha NCCR-Mageuzi akiwanadi wagombea wa chama hicho katika kijiji cha Maring'a.
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi ,James Mbatia akiwahutubia wananchio katika kijiji cha Maring'a katika jimbo la Vunjo.
Wananchi katika kijiji cha Maring'a wakimshangilia mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi wakati alipohutubia katika mkutano wa hadhara katika kijiji hicho.
Mh Mbatia akimnadi mgombea wa nafasi ya uenyekiti katika kijiji cha Maring'a.
Wagombea wa nafasi ya Wajumbe wa Halmashauri wakiwa na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi wakati wa mkutano wa kuwanadi wagombea wa chama hicho uliofanyika katika kijiji cha Maring'a.
Wananchi katika Jimbo la Vunjo wakiwa wamembeba ,Mwenyekiti wa taifa wa chama cha NCCR-Mageuzi ,James Mbatia aliyefika jimbooni humo na kufanya mikutano katika vijiji mbalimbali kuwanadi wagombea wa chama hicho na wale wanaotokana na UKAWA .Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya kaskazini.
Mh,Mbatia akitoka katika uwanja wa ofisi za kijiji cha Maring'a mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kampeni katika kijiji hicho.
Mh Mbatia akipokewa na wakazi wa kijiji cha Lole alipofika kwa ajili ya kuwanandi wagombea wa nafasi auenyekiti katika kijiji hicho
Mh Mbatia akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Lole katika jimbo la Vunjo.

KATIBU MKUU WA UVCCM NDUGU SIXTUS MAPUNDA AWALIPUA CHADEMA, ADAIWA KUNYAKA TAARIFA ZA SIRI ZA MIPANGO YA VURUGU SIKU YA KUPIGA KURA.

$
0
0
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (M-NEC) Ndugu Sixtus Mapunda amesema kuwa Chadema wamepanga njama haramu za kuvuruga uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa kuwaandaa vijana wa kufanya vurugu na kuwazuia akina mama na wazee wasiende katika maeneo ya kupigia kura.

Mapunda ameyasema hayo leo majira ya saa tano na nusu asubuhi wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwanzugi Kata ya Igunga , mkoani Tabora ambako yupo katika ziara ya Kikazi ya siku kumi na nne katika mikoa ya Tabora, Shinyanga, Geita na Kagera.

“..tumepata taarifa za kuaminika kuwa Chadema wameandaa vijana na kuwaandalia viroba na bangi ili waweze kufanya vurugu siku ya uchaguzi na kuwazuia wananchi kwenda kupiga kura katika vituo vilivyoandaliwa.,tunawataka waache mpango huo mara moja kwani vyombo vya dola viko macho na vitawachukulia hatua wote watakaofanya hujuma hizo..”

alisema Mapunda katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Mwanzugi stendi na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa kijiji cha Mwanzugi.

Pia, Mapunda amewataka wananchi kuwachagua Viongozi wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi kwani ni waaminifu, wakweli na wenye anuani kamili kwa maana ya kuwa wanazo ofisi zinazotambulika katika kila kijiji na Kata ambako wananchi wanaweza kupeleka malalamiko yao na kusikilizwa tofauti na vyama vingine ambavyo havina ofisi wala anuani ya Kudumu.

Mapunda ameendelea na mikutano yake ya hadhara katika Mkoa wa Tabora ambako anatarajia kuzungumza na wananchi wa wilaya za Kaliua, Urambo na Nzega.

FILAMU MBILI ZA PROIN PROMOTIONS ZAINGIA KWENYE KINYANG'ANYIRO CHA TUZO ZA AFRICA MAGIC VIEWERS CHOICE AWARD

$
0
0
Two Tanzanian movies Mdundiko and Network have been nominated for Nigeria Awards, the 2015 Africa Magic Viewers Choice Awards which will take place early next year. Both movies are nominated in the category of  Best Indigenous Language – Swahili and they are competing with Kenyan films. Mdundiko which is directed by Timoth Conrad stars Lumolwe Matovolwa, Dokii,Tino, Rado, Masinde and Bi. Mwenda while Network directed by John Kalaghe stars Monalisa Yvonne Cherryl in the lead.
Jinsi ya Kupiga Kura Unachotakiwa kufanya ni kufungua website hii www.amvca2015-awards.dstv.com and start voting! Unaweza kupiga kura mpaka 100 kwa Siku na vilevile unaweza kupiga kura kwa Kutuma Sms mpaka 100 pia kwa Siku pindi Tuzo hizo zitakapoanza
Vilevile Unaweza kupiga kura kwa kutumia program iitwa WE CHAT ambapo utatakiwa kuidownload kwenye simu yako na kuanza kupiga kura
Sasa ni zamu ya Filamu kuleta Tuzo Nyumbani Maana Muziki na BBA tayari na sasa tuweke nguvu zetu Huku hadi Davido Apaniki tena.

Kamanda Mpinga apokea stika za Usalama Barabarani

$
0
0

Mkurugenzi wa Masoko wa Benki ya Posta Tanzania, Deo Kwiyukwa (kulia) akimkabidhi Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga stika za taarifa za usalama barabarani zilizotolewa na Benki ya Posta Tanzania (TPB). Mkurugenzi wa Masoko wa Benki ya Posta Tanzania, Deo Kwiyukwa (kulia) akimkabidhi Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga stika za taarifa za usalama barabarani zilizotolewa na Benki ya Posta Tanzania (TPB).Mkurugenzi wa Masoko wa Benki ya Posta Tanzania, Deo Kwiyukwa akibandika kwenye basi moja ya stika za taarifa za usalama barabarani zilizotolewa kwa msaada na TPB. Pembeni yake ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga. Mkurugenzi wa Masoko wa Benki ya Posta Tanzania, Deo Kwiyukwa akibandika kwenye basi moja ya stika za taarifa za usalama barabarani zilizotolewa kwa msaada na TPB. Pembeni yake ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga.Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga akibandika kwenye basi moja ya stika za taarifa za usalama barabarani zilizotolewa kwa msaada na TPB. Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga akibandika kwenye basi moja ya stika za taarifa za usalama barabarani zilizotolewa kwa msaada na TPB.
Zoezi la utoa stika za taarifa za usalama barabarani zilizotolewa kwa msaada na TPB kwenye mabasi ya abiria likiengelea. Zoezi la utoa stika za taarifa za usalama barabarani zilizotolewa kwa msaada na TPB kwenye mabasi ya abiria likiengelea.Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga akizungumza na wanahabari leo mara baada ya kupokea msaada wa stika za taarifa za usalama barabarani zilizotolewa na Benki ya Posta Tanzania (TPB). Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga akizungumza na wanahabari leo mara baada ya kupokea msaada wa stika za taarifa za usalama barabarani zilizotolewa na Benki ya Posta Tanzania (TPB)Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga (kulia) akiiangalia moja ya stika za taarifa za usalama barabarani zilizotolewa kwa msaada na TPB kwenye mabasi ya abiria, akiwa pamoja na wafanyakazi wa Benki ya Posta Tanzania walioshiriki katika hafla Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga (kulia) akiiangalia moja ya stika za taarifa za usalama barabarani zilizotolewa kwa msaada na TPB kwenye mabasi ya abiria, akiwa pamoja na wafanyakazi wa Benki ya Posta Tanzania walioshiriki katika hafla.Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Kinondoni, Mkaguzi wa Polisi, Awadhi Haji akizungumza na wanahabari leo katika zoezi la utoaji wa stika za taarifa za usalama barabarani zilizotolewa na Benki ya Posta Tanzania (TPB). Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Kinondoni, Mkaguzi wa Polisi, Awadhi Haji akizungumza na wanahabari leo katika zoezi la utoaji wa stika za taarifa za usalama barabarani zilizotolewa na Benki ya Posta Tanzania (TPB).Zoezi la utoa stika za taarifa za usalama barabarani zilizotolewa kwa msaada na TPB kwenye mabasi ya abiria likiengelea. Zoezi la utoa stika za taarifa za usalama barabarani zilizotolewa kwa msaada na TPB kwenye mabasi ya abiria likiengelea. 

NGOMA AFRICA BAND NA MZIMU WAO WA MZIKI WA DANSI ! WENYE MVUTO MKUBWA BARANI ULAYA

$
0
0
Bendi maarufu ya mziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band,ni bendi ya kwanza ya kiafrika iliyojiwekea nafasi ya pekee katika nyoyo za washabiki uko ughaibuni.
 
Bendi hiyo ambayo imetajwa kuwa ndio bendi ya kwanza ya kiafrika kutumia muziki wake kutoka uswahilini kama daraja la kuwafikia washabiki wake  katika kona zote duniani,pia imetajwa na vianzo vya habari vya kimataifa  kuwa  mdundo wa mziki wake umekuwa ni urimbo unao wanasa na kuwatia kiwewe washabiki, popote pale duniani.
 
Bendi ya Ngoma Africa band aka FFU yenye maskani yake nchini Ujerumani ilianzishwa mwaka 1993 na mwanzilishi kwake mwanamziki Ebrahim Makunja almaarufu pia kwa majina kama Ras Makunja kamanda wa FFU,Mtawala wa himaya ya Anunnaki Empire "ambaye  pia ndiye mtunzi,mwimbaji na kiongozi wa bendi hiyo,bendi yenye utajili wa wanamziki wenye vipaji baadhi yao wakiwemo mpiga solo gitaa Christian Bakotessa aka Chris-B aka “Mshenzi” wa solo gitaa ambae pia yupo katika safu ya uimbaji,Wengine ni  Matondo Benda,Aj Mbongo na Saidi Jazbo Vuai wapiga bass gitaa ,Jonathan Sousa aka “Jo Jo” (Drum),wapo akina dada FrolaWilliam,Jessica Oyah ,bendi hiyo maarufu ina wanamziki takriban kumi ,bendi hiyo pia imezungukwa na wataalamu .
 
Ngoma Africa band ni bendi iliyo pachikwa majina mengi mengi ya utani au usanii kama vile FFU, Mzimu wa Muziki, Wazee wa kukaanga mbuyu, majina ambayo bendi hiyo haiwezi kuyakwepa !  Jina lingine ambalo lilikua gumu kwao kulikubali ni  “Watoto wa Mbwa” bendi hiyo ilibandikwa jina hilo na baadhi ya wadau wa mziki, kuwa nyimbo zao ni sawa  vitisho vya mbwa wanao bwaka katika kila sekta na kugusa nyoyo za walio wengi !

Ngoma Africa band imefanikiwa kufyatua CD nyingi ambazo nyimbo zilizomo katika santuri hizo zinatawala anga za redio za kimataifa..na kulitangaza kwa kasi kubwa jina la Tanzania kanji ya muziki , baadhi ya nyimbo zao ni pamoja “Rushwa ni adui wa haki” , Album “Mama Kimwaga”,Single CD “Apache wacha Pombe” , CD “Jakaya Kikwete 2010”,CD "Miaka 50 ya uhuru" na CD Bongo Tambarare na Uhuru wa habari, ambazo zote ni Utunzi wake kiongozi wa bendi hiyo kamanda Ras Makunja wa FFU,mjeshi wa ambaye kufanya nae kazi inataka uwe na tabia za ki FFU, yaani uwe tayari tayari wakati wowote kwenda kutumbuiza hata ikiwa katika nchi za vita ! 
 
Na mdundo anautaka yeye lazima uwe na mwendo wa kasi na magitaa Lazima yalie milio ya kushambulia mashabiki katika ulingo wa dansi, mdundo ambao umepewa jina “Extra Ordinary” Bongo Dance mdundo ambao umefanikiwa kuwateka , kuwanasa na kuwatia kiwewe watu wengi katika kila kona duniani,Wasikilize katika  website yao at www.ngoma-africa.com au pia http://www.itunes.apple.com/us/album/mama-kimwaga-sugar-mum/id947329929 ambayo mpenzi au mshabiki anaweza ku log in na kujumuika nao kama mwanachama wa bendi hiyo.
 
Ngoma Africa band inaonekana kuwa na mfumo tofauti sana ! Kuwa washabiki wanasauti kubwa ya kuweza kulazimisha maonyesho kuliko uongozi wa bendi !? Mashabiki mara nyingi wamekua tishio hadi kwamaporomota na waandaaji wa maonyesho makubwa ya mziki…kama bendi ya Ngoma Africa haikualikwa au kupangwa katika ratiba ya onyeshoFulani basi wapo tayari kususia onyesho hilo…au pengine wakalivunja !
 
Tena washabiki  hao wa umri wa lika na mataifa mbali mbali hawaoni wala hawasikii kitu kingine chochote mbele Bongo dansi la Ngoma Africa band aka FFU,ukipenda    waite  “Watoto wa Mbwa” au "Anunaki Elien" viumbe wa ajabu kutoka sayari majina yote size yao !
Maporomota au waandaaji wa maonyesho mengi ya mziki huko ughaibuni wanalazimika Kuandaa  ulinzi wa kutosha mara tu wanapoialika bendi hiyo   kushiriki katika maonesho yao....hapa ndipo vianzo vingi vya habari vya ndani na nje  ya nchi vinapofika katangaza kuwa FFU wa Ngoma Africa band “jino kwa           jino” au “Jicho kwa Jicho” na washabiki .
 wasikilize katika tovuti yao www.ngoma-africa.com 

pia unaweza kuwasiliana nao at contact@ngoma-africa.com

MWANZA KUFIKIA MALENGO YA MILENIA KUKABILIANA NA AFYA YA MAMA NA MTOTO IFIKAPO DESEMBA 2015.

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga akifungua Mkutano huo.
 Mratibu wa Afya ya mama na Mtoto mkoani Mwanza Secilia Mrema akitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari.
 .Bw. Stanley Matowo, mataalam wa maji kutoka sekretarieti ya mkoa wa mwanza akichangia katika kikao hicho.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Drt. James Kengia akitoa ufafanuzi wa maswali ya wadau waliokutana.

Na: Atley Kuni-(Afisa habari Mwanza).

Mkoa wa Mwanza umejiwekea malengo makubwa ili kukabiliana na afya ya uzazi na malezi bora kwa mtoto ili kuweza kufikia malengo ya milennia ifikiapo Desemba 2015.

Hayo yamesemwa na bibi Secilia Mrema wakati akiwasilisha mada kwenye kikao cha pamoja kilichokutana katika ofisi ya mkuu wa mkoa na wadau wa masuala ya afya mkoani hapa kwa ajili yakupitia mipango waliojiwekea lakini pia kupeana majukumu ili kuweza kufikia azma yao hiyo.

Mrema amesena, kutokana na hali ya uzazi salama kuwa chini ukilinganisha na mikoa jirani kama vile Kagera ndio maana wameamua kukaa pamoja ili waone kwa namna gani wanaweza kutoka mahali walipo na kufikia malengo waliojiwekea ifikiapo  mwishoni mwa 2015.

Amesema kutokana na Uelewa mdogo juu ya njia za uzazi salama kwa watoa huduma na kwa jamii, Mila na desturi zinazofanya utumiaji mdogo  wa huduma za afya ya uzazi na uzazi wa mpango, ushiriki mdogo wanaume ni  baadhi sababu kubwa iliyo wasukuma kuja na mikakati hiyo, lakini pia kutokana na mpango wa Tekeleza sasa kwa matokeo makubwa (BRN) ni njia moja wapo ya visababishi vilivyo wafanya kuja na mikakati hiyo “ Tunajua suala la afya ya uzazi ni jukumu la jamii nzima ndio maana tumeona ni vema tuka kaa wadau wote tunao husika ili tuweze kuangalia kiunaga ubaga mikakati hii tuliojiwekea.

Kutokana na changamoto hizi mkoa kwa kupitia halmashauri za wilaya umejiwekea malengo yafuatayo.

Kupiga vita mila na desturi zinazofanya utumiaji mdogo  wa huduma za afya ya  uzazi kama  vile, uzazi wa mpango, ushirikishwaji wa wanaume, Kuongeza kiwango cha wajawazito kujifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za afya  kutoka 68%-80% ifikapo desemba 2015, kuongeza  kiwango cha huduma baada ya kujifungua ndani ya siku 7 kutoka 21% mpaka 62% ifikapo  Decemba  2015, kuongeza kiwango cha watoto wanaozaliwa na kina mama wenye maambukizi ya VVU kutumia  ARV (prophylaxis) kutoka 45% to 65% ifikapo Decemba 2015 kuongeza namba ya vituo vinavyotoaa huduma ya IMCI kutoka 69%-80% ifikapo Desemba 2015, mbali ya mikakati hiyo vilevile mkoa umedhamiria Kuboresha utoaji wa taarifa kwa wakati kutoka 66%-100% ifikapo Decemba 2015.

Mrema amekwenda mbali zaidi nakusema ili waweze kufikia malengo waliojiwekea watatoa mafunzo kwa watoa huduma kuhusu (njia za kisasa za uzazi wa mpango, huduma za dharura wakati wa uchungu na kujifungua, huduma ya kumsaidia mtoto mchanga kupumua baada ya kuzaliwa, IMCI, mtuha). Aidha kupitia vyombo vya habari watatumia mwanya wakutoa elimu kwa umma ili wajue umuhimu wa afya ya uzazi lakini pia kufanya mikutano mingi ya uraghabishaji kwa umma ili ufahamu umuhimu wa masuala ya afya ya uzazi kwa mama na mtoto.

Mkoa wa Mwanza ni mojawapo ya  mikoa 6 inayo unda kanda ya Ziwa ambao una wilaya ziapatazo saba  zenye visiwa 68. Huku mkoa huo kwa mujibu wa sensa ya watu na  makaazi ya mwaka 2012 ikiwa jumla ya watu wapatao 2,772,509, idadi ya watoto chini ya mwaka mmoja ikiwa ni 104,507, na watoto  watoto chini ya miaka 5 ikiwa ni 516,998 huku  wanawake wenye umri wa kuzaa kwa maana ya umri kati ya miaka (14-49yrs)  ni 677,100.

Mrema amesema, wastani wa watoto katika familia ni 5.4 (Fertility rate), na ukuaji wa wakazi kwa maana ongezeko la watu kimkoa ikiwa ni 3.2% kwa mujibu wa sense ya 2012, aidha mkoa pia  una jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya 360 kati ya hivyo vituo 263 (73) % vinatoa huduma za afya ya uzazi na mtoto.

Awali akifungua kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo katika hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa Wilya ya Nyamagana alisema ni jukumu la kila mmoja wetu “kujihoji ni kwa vipi mama apoteze maisha ili hali kila mmoja wetu anajua kuwa mama ndiye anaye tengeneza maisha”? 

Aidha  amesema kuwa kutokana na lengo la nne la millennia kugusa suala nyeti kama hili ndio maana kama taifa tayari tathimini ilifanyika ambapo Wakuu wa Mikoa yote Tanzania Bara, Makatibu Tawala na Waganga Wakuu wa Mikoa Tanzania walikutana na Mheshimiwa Rais tarehe 15 Mei, 2014 na kupewa taarifa ya tathimini hiyo na kujadili mkakati mpya ulioboreshwa wa kitaifa katika kufikia lengo la 4 na la 5. Ifikapo mwishini mwa mwaka 2015, “Pamoja na mengine tuliyokubaliana mbele ya Mheshimiwa Rais, suala la uwajibikaji lilipewa kipaumbele ambapo kila mmoja wetu aliweza  kupata uzoefu wa mikoa mingine, mfano Singida na Mara jinsi walivyofaulu katika suala la afya ya uzazi.

Kikao hicho cha siku moja kimewakutanisha Viongozi wa dini, wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa halmashauri, wenyeviti wa halmashauri, waganga wakuu wa wilaya na waratibu wa afya ya uzazi wa wilaya pamoja na wataalam kutoka sekretarieti ya mkoa wa Mwanza.

Imeandaliwa na Afisa habari- Mwanza- ofisi ya Mkuu wa mkoa. soma zaidi na picha kupitia: www.mwanzareview.blogspot.com

BASATA kuwapiga msasa waimbaji Desemba 17 Na Mwandishi Wetu

$
0
0
WAIMBAJI watakaoimba kwenye Tamasha la Krismasi katika mikoa ya Mbeya, Iringa na Songea  wanatarajia kupigwa msasa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), kupitia semina itakayofanyika Desemba 17 katika ofisi za Msama Promotions, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Abihud Mang’era semina hiyo itahusisha baadhi ya watendaji  wa Basata ambao watafikisha ujumbe wa serikali katika tasnia ya muziki.

Mang’era alisema ni muhimu kwa waimbaji kuhudhuria semina hiyo ambayo ina lengo la kuwapa mwangaza waimbaji ambao watashiriki kutoa huduma ya neno la Mungu.

“Ni muhimu kwa waimbaji kuhudhuria katika semina hiyo ambayo itaongozwa na watendaji wa Basata ambao watashirikiana na watendaji wa Msama Promotions,” alisema Mang’era. Mang’era alisema semina hiyo itawasaidia waimbaji kukumbuka masuala ya msingi pindi wawapo jukwaani  ambako alisisitiza waimbaji kuhudhuria semina hiyo.

DIWANI MATHIUS WA KATA YA MALANGARINI AFUNGA KAMPENI ZA UCHAGUZI KATANI KWAKE

$
0
0
Diwani wa kata ya Mlangarini, Mathius Manga akizungumza na wananchi wa kata hiyo katika mkutano wa hadhara wa kuhitimisha kampeni za uchaguzi wa CCM kwa ajili ya kuwachagua viongozi wa  serikali za mitaa utakaofanyika jumapili Desemba 14 mwaka huu.

Diwani Manga amewaasa wananchi wote kujitokeza kwa wingi kuwapigia kura wagombea wa CCM kwani wanasifa stahiki za kuwaongoza. 

Aidha amesisitiza kulimnda amani kipindi cote cha uchaguzi na hata matokeo yatakapo tangazwa na kuepuka vitendo vya vurugu. 
 Wananchi wa kata ya Manyire wakimsikiliza diwani wa kata hiyo hayupo pichani wakati wa kuhitimisha kampeni za uchaguzi wa serukali za mitaa.

 Diwani wa kata ya mlangarini Mathius Manga akizungumza huku makada wa CCM wakicheza kwa furaha.
 Viongozi wa CCM wakiwa katika mkutano huo.
 Diwani wa kata ya mlangarini Mathius Manga akiwa na viongozi wenzake wa CCM katika mkutano huo.

Article 1


MFUKO WA PENSHENI WA LAPF WASAIDIA UJENZI WA MAABARA KATIKA SHULE YA MIHANDE WILAYANI KIBAHA MKOA WA PWANI

$
0
0

Kaimu Meneja wa LAPF Kanda ya Mashariki, Isaya Mwakifulefule (kushoto), akimkabidhi, Ofisa Elimu wa Vifaa na Takwimu wa Wilaya ya Kibaha, Doris Semkiwa (kulia), bati na rangi zenye thamani ya sh.milioni 3.5 zilizotolewa na mfuko huo jana, kusaidia ujenzi wa maabara katika Shule ya Sekondari ya Mihande ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais Jakaya Kikwete za kuhakikisha kila shule ya sekondari nchini inakuwa na maabara. Anayeshuhudia makabidhiano hayo katikati ni Mkuu wa shule hiyo, Flora Masha.
Kaimu Meneja wa LAPF Kanda ya Mashariki, Isaya Mwakifulefule (kushoto), akipeana mkono na Mkuu wa shule hiyo, Flora Masha wakati akikabidhi msaada huo. Kulia ni   Ofisa Elimu wa Vifaa na Takwimu wa Wilaya ya Kibaha, Doris Semkiwa. 
Kaimu Meneja wa LAPF Kanda ya Mashariki, Isaya Mwakifulefule (kushoto), akipeana mkono na Ofisa Elimu wa Vifaa na Takwimu wa Wilaya ya Kibaha, Doris Semkiwa. Kulia ni Mkuu wa shule hiyo, Flora Masha.   
Hapa ni kubadilishana mawazo baada ya makabidhiano hayo.
Kaimu Meneja wa LAPF Kanda ya Mashariki, Isaya Mwakifulefule (kushoto), akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo.
Jengo la maabara la shule hiyo lililokamilika ujenzi wake.
Jengo la maabara ambalo ujenzi wake unaendelea.
Baadhi ya majengo ya shule hiyo yanvyoonekana.
Jengo la utawala la shule hiyo.
 
Dotto Mwaibale
 
MFUKO wa Pensheni wa LAPF umeunga jitihada za Rais Jakaya Kikwete za kuhakikisha kila shule ya sekondari nchini inakuwa na maabara kwa kutoa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya sh.milioni 3.5 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa maabara katika Shule ya Sekondari ya Mihande iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha.
 
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa hivyo Mlandizi wilayani humo jana, Kaimu Meneja wa Kanda ya Mashariki wa mfuko huo, Isaya Mwakifulefule alisema mfuko huo umejiwekea utaratibu wa kusaidia kutoa misaada mbalimbali katika  shughuli za maendeleo ya kijamii.
 
“Mfuko wetu kila kanda nchini wamekuwa wakishiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo na katika hilo mnaweza kuwa mashuhuda kwani siku za hivi karibuni mmeweza kuona tulivyotoa msaada kwa ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi (albino)” alisema Mwakifulefule.
 
Alisema ujenzi maabara katika shule hapa nchini ni muhimu sana katika wakati huu wa ulimwengu wa sayansi na teknolojia ambapo wanahitaji wanayansi wengi kwa utaalamu wa aina mbalimbali hasa katika masuala ya utafiti.
 
Alitaja vifaa vilivyotolewa na mfuko huo kuwa ni mabati na rangi kwa ajili ya kukamilishia ujenzi wa maabara hizo na alitoa mwito kwa wadau wa maendeleo na mifuko mingine kujitokeza kusaidia eneo hilo kwani kuna mahitaji makubwa ya maabara nchini.
 
Akipokea msaada huo kwa niana ya Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo, Ofisa Elimu Vifaa na Takwimu wa wilaya hiyo, Doris Semkiwa alisema msaada huo utapunguza changamoto ya ujenzi wa maabara kwenye shule hiyo.
 
Alisema ujenzi wa maabara katika wilaya hiyo umekamilika kwa asilimia 67 na kuwa ujenzi huo unaendelea kwa kasi ambapo wanatarajia kukamilisha kazi hiyo mapema iwezekanavyo.
 
Alisema kwa wilaya nzima yenye shule za sekondari 8 mahitaji ni kuwa na maabara 24 na tayari wamejenga 14 na kuwa fedha zinazotumika kwa ujenzi huo zinatoka katika mapato ya ndani ya Halmshauri, wadau mbalimbali na nguvu za wananchi.
 
Aliongeza kuwa ujenzi huo utagharimu zaidi ya sh, milioni 400 na kuwa changamoto kubwa ni mapato ya ndani kuwa kiduchu na kuwa kama wangekuwa na fedha za kutosha wangeweza kumaliza kwa wakati ujenzi huo.
 
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Flora Masha aliwashuku LAPF kwa msaada huo pamoja na Halmsahauri kwa fedha za luzuku inazozitoa kila mwezi kusaidia mambo mbalimbali katika shule hiyo na zingine sanjari na ujenzi wa maabara hizo.
“Naishukuru Halmshauri kwa fedha hizo ambazo imekuwa ikitupa kila mwezi kusaidia katika maeneo mbalimbali” alisema Masha.

MAHAFALI YA 12 YA CHUO CHA UHASIBU TANZANIA (TIA) YAFANA, JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Kikosi cha band cha Jeshi la Magereza kikiongoza maandamano kuelekea uwanjani kwenye mahafali hayo.
 Wahadhiri wa Taasisi hiyo pamoja na mgeni rasimi wakiandamana kwenda uwanjani tayari kwa hafla hiyo.
 Wahitimu wakiandamana kwenda uwanjani tayari kwa hafla hiyo.
Meza kuu
 Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo, Shah Hanzuruni akizungumza jambo
 
 Wahitimu wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA), wakiwa katika mahafali yao hayo.

 Baadhi ya wahitmu wa Chuo hicho, wakitunukiwa shahada zao wakati wa mahafali yao hayo.
 Wahitmu wakitunukiwa shahada zao wakati wa mahafali yao hayo.
 Wahitmu wakitunukiwa shahada zao wakati wa mahafali yao hayo.
 Wahitmu wakitunukiwa shahada zao wakati wa mahafali yao hayo.
 Mdau wetu Nicko Anthony baada ya kula nondo kwenye mahafali ya 12 ya Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA)
 
Mdau wetu Nicko Anthony(wa kwanza kushoto)  akiwa kwenye picha ya pamoja wahitimu wenzake
 Baadhi ya wahitimu wakiwa kwenye picha ya pamoja
  Mdau wetu Nicko Anthony akiwa kwenye picha ya pamoja na Teddy mara baada ya kumalizika kwa sherehe hizo
Baadhi ya wananchi waliofika kwenye mahafari hayo
Justine Kajerero(kushoto) akiwa pamoja na mdau wetu Nicko Anthony 

Mgodi wa Resolute wakabidhi eneo la Mgodi kwa Chuo cha Madini Dodoma, Masele asema tukio hilo limefungua ukurasa mpya

$
0
0



unnamedNaibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Stephen Masele (aliyesimama katikati) akishuhudia halfa fupi ya kusaini makabidhiano ya eneo la Mgodi wa Resolute kwa Chuo cha Madini Dodoma. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Madini Dodoma, Mjiolojia Mwandamizi Subian Chiragwile, katikati ni Kaimu Kamishna wa Madini Mhandisi Ally Samaje, na kushoto ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Resolute Peter Beilby. Wengine wanaoshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Nzega Bintuni Msangi (wa pili kuchoto aliyesimama),Mkurugenzi Kampuni ya Resolute Rose Aziz na baadhi ya waliohudhuria.
unnamed1Meneja Mazingira   baada Mgodi wa Resolute Jackie Sinclair (Kulia), akimkabidhi funguo mbalimbali za majengo ya eneo la mgodi wa Resolute Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Madini) Stephen Masele (Kushoto) mara makabidhiano ya eneo la mgodi.
unnamed2Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Chuo cha Madini Dodoma Mjiolojia Mwandamizi Subian Chirangilwe funguo mbalimbali za majengo ya mgodi wa Resolute kwa ajili ya Chuo cha Madini Dodoma.
unnamed4Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele akiangalia chumba cha Computer ambacho ni miongoni mwa vifaa ambavyo Mgodi wa Resolute umekabidhi kwa ajili ya Chuo cha Madini Dodomaunnamed5Pichani Meneja Mazingira wa mgodi wa Resolute Jackie Sinclair (mbelea) akieleza jambo wakati akikiabidhi baadhi ya vifaa vya maabara kwa Chuo cha Madini Dodoma. Wanaomsikiliza ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele ujumbe alioambatana nao.
unnamed6Meneja Mazingira wa Mgodi wa Resolute Jackie Sinclair akikabidhi moja ya vifaa ambavyo vitatumiwa na Chuo cha Madini Dodoma kwa wanafunzi kujifunza kwa vitendo wakati wa halfa ya kukabidhiana eneo la mgodi wa Resolute. Wanaoangalia kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele, Kaimu Kamishna wa Madini Mhandisi Ally Samaje na Mkuu wa Wilaya ya Nzega Bintuni Msangi
unnamed7Sehemu mgodi ambao shughuli za uchimbaji zilikuwa zikifanywa na mgodi wa Resolute ambao pia umekabidhiwa kwa Chuo cha Madini Dodoma. Kwa mujibu wa Mkuu wa Chuo Madini Dodoma Mjiolojia Mwandamizi Subian Chirangilwe ameeleza kuwa,mgodi huo utatoa fursa kwa wanafunzi kujifunza kwa vitendo kuhusu shughuli za uchumbaji.
…………………………………………………………………………..
Na Asteria Muhozya, Nzega.

Mgodi wa Resolute uliopo Wilayani Nzega Mkoani Tabora jana tarehe 12 Desemba, 2014, ulikabidhi eneo la Mgodi kwa Chuo cha Madini Dodoma katika hafla fupi iliyofanyika na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, anayeshughulikia madini Stephen Masele aliyekuwa mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Nzega aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Bituni Msangi, Viongozi Waandamizi wa Wilaya ya Nzega, Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje, Kamati ya Kitaifa ya uchimbaji, Uongozi wa Juu wa kampuni ya Resolute na wananchi.

Akihutubia katika hafla hiyo, Naibu Waziri Masele alieleza kuwa, tukio la kukabidhiwa eneo hilo la Mgodi kwa Chuo ni tukio ambalo limefungua ukurasa mwingine kutokana na kwamba Chuo cha Madini Dodoma kitaiwezesha Tanzania kuzalisha wataalamu zaidi waliobobea katika tasnia hiyo ambao mchango wao kwa taifa unahitajika katika kuendeleza sekta ya madini. “Tunataka wanafunzi wasome kwa vitendo, hii itawezesha kupata wataalamu waliobobea. 

Ni nafasi kwa wanafunzi na Chuo cha Madini kuitumia fursa hii vizuri. Najua kuna mawazo mchanganyiko ya kupoteza mapato kwa Halmashauri na mengine ya kupata Chuo lakini, kufunga mgodi ni sehemu ya Sheria ya madini”, aliongeza Masele.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nzega Bintuni Msangi, akizungumza katika halfa hiyo, alieleza kuwa, Mgodi wa Resolute una historia ya kuwa mgodi wa kwanza nchini kuzalisha madini ya dhahabu na kuogeza kuwa, ndani ya kipindi cha miaka 12 cha uhai wa mgodi huo umeweza kuchangia kiasi cha shilingi bilioni 290 za Kitanzania ikiwa ni kodi mbalimbali zilizotolewa na mgodi huo kama mrahaba.

Aliongeza kuwa, Halmashauri iliweza kupata kiasi cha shilingi bilioni 6 ikiwa ni kodi na kiasi cha Tsh bilioni 6 kilitumiwa na mgodi huo kuwezesha za kijamii ikiwemo ujenzi wa zahanati, shule, upatikanaji wa huduma safi ya maji katika eneo linalozunguka mgodi huo.
 Pamoja na eneo la mgodi huo kukabidhiwa kwa Chuo cha Madini Dodoma, vilevile mgodi umekabidhi majengo, mitambo, maabara ambapo, kwa mujibu wa Mkuu wa Chuo cha Madinini Dodoma, Mjiolojia Mwandamizi Subian Chiragwile alieleza kuwa, eneo hilo litatumiwa na wanafunzi wa mwaka wa pili kwa ajili ya masomo ya vitendo.

Mgodi wa Resolute umefunga rasmi shughuli zake za uchimbaji madini ya dhahabu katika eneo hilo, ambapo ulianza kazi zake mwaka 1998. Kabla ya makabidhiano hayo, mgodi huo umefanya ukarabati, ujenzi wa madarasa, na uhifadhi wa mazingira.

WAZIRI MKUU PINDA AKUTANA NA BALOZI WA SWEDEN NCHINI, ASHIRIKI CHAKULA CHA JIONI NA AKINA MAMA WA (New Millenium Women Group)

$
0
0

unnamed2Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katka picha ya pamoja na washiriki wa maonyesho ya mavazi yaliyoandaliwa na  Umoja wa wake wa viongozi ( New Millenium Women Group) katika chakula cha jioni kilichoambatana na burdani mbalimbali kwenye ukumbi wa Kardinal Rugambwa, Oysterbay jijini  Dar es salaam, Desemba 12, 2014.  Chakula hicho  kiliandaliwa ili kuchangisha fedha kwa ajili ya maboresho ya kituo cha  kulea watoto yatima cha Buhangija mkoani Shinyanga.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)unnamed4Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katka picha ya pamoja na washiriki wa maonyesho ya mavazi yaliyoandaliwa na  Umoja wa wake wa viongozi ( New Millenium Women Group) katika chakula cha jioni kilichoambatana na burdani mbalimbali kwenye ukumbi wa Kardinal Rugambwa, Oysterbay jijini  Dar es salaam, Desemba 12, 2014.  Chakula hicho  kiliandaliwa ili kuchangisha fedha kwa ajili ya maboresho ya kituo cha  kulea watoto yatima cha Buhangija mkoani Shinyanga.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)unnamed5 Baadhi ya  washiriki wa maonyesho ya mavazi yaliyoandaliwa na  Umoja wa wake wa viongozi ( New Millenium Women Group) katika chakula cha jioni kilichoambatana na burdani mbalimbali kwenye ukumbi wa Kardinal Rugambwa, Oysterbay jijini  Dar es salaam, Desemba 12, 2014 wakijitambulisha baada ya onyesho hilo.  Chakula hicho  kiliandaliwa ili kuchangisha fedha kwa ajili ya maboresho ya kituo cha  kulea watoto yatima cha Buhangija mkoani Shinyanga.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)unnamed6 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na na nalozi wa Sweden nchini, Bw.Lennarth Hjelmaker, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Desemba   13, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

HIVI NDIVYO YANGA ILIVYOKUNWA GOLI 2-0 NA SIMBA ISHU YA NANI MTANI JEMBE

$
0
0
Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi akiwa amenyanyua juu Kombe la Ubingwa wa mechi ya Nani Mtani Jembe msimu wa pili uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba imeshinda 2-0. 
 Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Mchezo, Dk. Fenella Mukangala akimkabidhi nahodha wa Simba, Emmanuel Okwi Kombe la Ubingwa wa mechi ya Nani Mtani Jembe.
Wachezaji wa Simba wakishangilia ushindi wa timu yao.
 Umati wa mashabiki wa Yanga.
 Umati wa mashabiki wa Simba.
Mashabiki wa Simba wakiwa wamebeba mfano wa jeneza kuwakejeli watani zao.
 Beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro'

 Beki wa Yanga, Kelvin Yondan akimiliki mpira.
 Mwamuzi wa mchezi akimuonyesha kadi ya njano mshambuliaji wa Simba, Simo Serunkuma.
 Kpah Sherman akiokoa moja ya hatari langoni mwake huku Elius Maguri akimzonga.
 Mshambuliaji wa Simba Emmanule Maguri akichuana na beki wa Yanga, Nadir Haroub.
Wachezaji wa Simba wakishangilia bao lao la kwanza.
 Hassan Isihaka (kushoto) ana Ramadhani Singano 'messi' wakishangilia bao la kwanza la timu yao.
Beki wa Yanga, Oscar Joshua akimtoka Elius Maguri wa Simba.
Shabiki wa Yanga akipata msaada baada ya kuzimia jukwaani.
 Mashabiki wa Simba wakiwa na bango lenye idadi ya mabao waliyowahi kufungwa Yanga.
Leo ni 2-0.....
Burudani zikitolewa uwanjani.
 Mashabiki wakitolewa uwanjani baada ya kuzimia.
 Hali ilikuwa ngumu kwa mashabiki mpaka baadhi yao kuzimia.
Huduma ya kwanza kwa waliozimia ikitolewa.
 Beki wa Yanga, Kpah Sherman akichuana na beki wa Simba, Hassan Isihaka.
 Danny Mrwanda akiwa ameshika kichwa baada ya kukosa bao la wazi.
Ivo Mapunda akiokoa moja ya hatari langoni mwake.
 Simon Msuva akichuana na Issa Rashid.
Ivo Mapunda (katikati) akishangilia ushindi na wenzake.
Wachezaji wa Yanga wakiwa na huzuni baada ya kumalizika kwa mchezo.
Yanga wakiwa vichwa chini.
 Medali za washindi. 
 Kocha wa Simba, Patrick Phir akisalimiana na kocha wa Yanga, Marcio Maximo kabla ya mchezo. (Picha zote na Francis Dande)
 Emmanue Okwi akiomba dua wakati akiingia uwanjani.
 Mgeni rasmi akisalimiana na wachezaji wa Yanga.
 Mgeni rasmi akisalimiana na wachezaji waSimba.
Kikosi cha Yanga.
Kikosi cha Simba.
Kocha wa Yanga akitafakari.
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images