Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

Watanzania waaswa kuendelea kusaidia sekta ya Michezo nchini

$
0
0

unnamed
WaziriwaHabari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akizungumza na wadau wa michezo ya Ngumina na Karate wakati wa hafla ya kukabidhiwa msaada wa Ulingo wa Ngumi wa Kimataifa pamoja na hundi yenye thamani ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya kusaidia mchezo wa Karate kutoka kwa Kampuni ya Mawasiliano ya Simu ya Zantel Tanzania leo jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Pratap Ghose.
unnamed1Ulingo wa kisasa kwa ajili ya Mchezo wa Ngumi uliotolewa kama msaada na Kampuni ya Mawasiliano ya Simu ya ZANTEL na kupokelewa naWaziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara leo jijini Dar es Salaam.
unnamed3Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (Kulia) akijaribu baadhi ya vifaa vya mchezo wa ngumi (Gloves) wakati wa hafla ya kukabidhiwa msaada wa Ulingo wa Ngumi wa Kimataifa pamoja na hundi yenye thamani ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya kusaidia mchezo wa Karate kutoka kwa Kampuni ya Mawasiliano ya Simu ya ZANTEL leo jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Pratap Ghose na katikati yao mwenye suruali nyekundu ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) Bw.Lukelo Willilo.
unnamed4Afisa Mtendaji Mkuu wa ZANTEL Pratap Ghoe akisalimiana na Bingwa wa mchezo wa ngumi Tanzania Bondia Francis Cheka (kushoto) wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa Ulingo wa Kimataifa kwa ajili ya mchezo huo leo jijini Dar es Salaam, Kulia ni wa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Picha zote na: Frank Shija, WHVUM

Mshindi wa Big Brother Africa 2014,idris sultan awasili nchini

$
0
0
Mshindi wa Big Brother Africa 2014,Idris Sultan akiongea na waandishi wa habari.
Mshindi wa Shindano la Big Brother Africa 2014,Idris Sultan akishangilia wakati alilakiwa na Washabiki wake waliojitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere,Jijini Dar es salaam leo akitokea nchini Afrika Kusini yalikokuwa yakifanyika mashindano hayo.Kushoto kwake ni Laveda aliekuwa mshiriki mweza wa Idris.
Idris akionekana ni mwenye furaha kubwa sana baada ya kuwasili nchini.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Barbara Kambogi (kati) akijadiliana jambo na Mshindi wa Big Brother Africa 2014,Idris Sultan pamoja na aliekuwa mshiriki wa shindano hilo,Laveda katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Mama Mzazi wa Idris Sultan akijiandaa kumpokea mwanae.

UN YATAKA SERIKALI KUFANYIA KAZI MIANYA INAYOTISHIA HAKI ZA BINADAMU

$
0
0
DSC_0102
Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bibi Mary Massay akitambulisha meza kuu wakati wa maadhimisho ya Siku ya haki za binadamu yaliyoenda sambamba na mkutano wa kujadili utekezaji wa makubaliano ya haki za binadamu nchini na maandalizi ya ripoti ijayo yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog). 


MRATIBU Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez ameitaka serikali ya Tanzania pamoja na mafanikio makubwa katika kufanikisha amani na kutia saini mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu, kufanyia kazi maeneo kadhaa ambayo bado yanatishia sifa nzuri ya taifa hili. Maeneo hayo ni mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, wanawake vikongwe na ukatili kwa watoto.

Alisema taifa hili ambalo limekuwa kimbilio la wakimbizi,kuukubali kuwa makao ya mahakama mbili kubwa za kimataifa zinazoshughulikia haki za binadamu (ICTR na African Court of Human rights) sasa linashuhudia madhila kwa baadhi ya wananchi wake ambao huuawa kwa imani za kijinga.

Akizungumza katika siku ya mataifa ya haki za binadamu mjini hapa, Mratibu huyo pamoja na kutoa ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, alisema ili Tanzania iweze kutekeleza kwa umakini kauli mbiu ya mwaka huu “haki kwa wote siku zote 365” maeneo yaliyotajwa yanastahili kufanyiwa kazi kwani ni changamoto kubwa.
IMG_6700
Mgeni rasmi Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mh Ali Hassan Rajab akizungumza wakati wa akifungua mkutano wa kujadili utekezaji wa makubaliano ya haki za binadamu nchini na maandalizi ya ripoti ijayo ulioenda sambamba na maadhimisho ya siku ya haki za binadamu duniani.

Alisema Tanzania ambayo imetia saini na kuridhia mikataba ya haki za binadamu kama ya kuwatambua walemavu, kukabili ubaguzi dhidi ya wanawake (CEDAW) na ule wa kulinda haki za watoto (CRC) inaposherehekea siku ya haki za binadamu inakabiliwa na doa hilo la ukatili miongoni mwa watu wake.

Alisema ipo haja ya kuimarisha usalama wa makundi hayo kwa kuhakikisha kwamba mashauri yao mahakamani yanamalizika na haki kuonekana kutendeka . Alisema familia ambazo zimepoteza watu wake kwa namna ya kikatili wanahitaji si tu kuona haki inatendekea bali wahusika wake wakichukuliwa hatua na ulinzi kwa makundi hayo ukiimarishwa.

Aidha alisema kwamba anapata maumivu makubwa anaposikia kuwapo na taarifa nyingi za ukatili kwa watoto na kuendelezwa kwa mila mbaya zinazofunika haki za msingi huku wahusika wakiwa hawachukuliwi hatua au upelelezi ukidaiwa bado kukamilika.
DSC_0110
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisoma hotuba kwenye maadhimisho ya siku ya haki za binadamu duniani yaliyoenda sambamba na mkutano wa kujadili utekezaji wa makubaliano ya haki za binadamu nchini na maandalizi ya ripoti ijayo.


Alisema kitendo cha kuchelewesha haki kutokana na upelelezi kutokamilika au kushindikana kutokana na kukosekana kwa fedha au familia zenyewe kushindwa kutafuta haki kutokana na kutokuwa na fedha kunavuruga jina zuri la nchi hii ambayo ina makabila mengi na tamaduni tofauti.

Alisema pamoja na ukweli kuwa matendo hayo kisheria ni haramu kukosekana kwa utashi kwa viongozi kukabiliana na changamoto zilizopo na kuachwa kwa mila mbaya kunawafanya wananchi wabaki katika mazingira ya kutotendewa haki. Alisema mfumo wa sheria lazima uonekane kufanya kazi ili kukabiliana na wavunjaji wa haki za binadamu.
“Ni matumaini yangu kwamba serikali ya Tanzania itaonesha kuwajibika kwake na kuhakikisha inaangalia changamoto hizi na kuziondoa ili kuwezesha kutekeleza haki za binadamu saa 24, siku saba za juma na siku 365 za mwaka” alisema na kuahidi kwamba Umoja wa mataifa katika hilo utaendelea kutoa ushirikiano.
IMG_6647
Mkuu wa Balozi za Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania na Afrika Mashariki, Mh. Filiberto Ceriani-Sebregondi akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya haki za binadamu duniani yaliyoenda sambamba na mkutano wa kujadili utekezaji wa makubaliano ya haki za binadamu na maandalizi ripoti ijayo.

Aidha alisema kwamba UN itaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kuimarisha kamisheni ya haki za binadamu na utawala bora (CHRAGG) na taasisi nyingine za kijamii kuhakikisha kwamba kuna mfumo wa kulinda haki za biandamu.
Aidha mratibu huyo ameitaka serikali ya Tanzania kukamilisha uongozi wa CHRAGG na pia kuangalia watetezi wa haki za binadamu wanapata ulinzi wa kutosha dhidi ya watu wanaowatishia maisha.

Naye Mkuu wa Balozi za Umoja ya Ulaya (EU) nchini Tanzania na Afrika Mashariki Filiberto Ceriani-Sebregondi ameitaka serikali ya Tanzania kuangalia mapendekezo matatu iliyokataa ambayo yanagusa haki za binadamu. Mapendekezo hayo yalikuwamo katika mfumo wa Umoja wa mataifa wa kupitia mambo mbalimbali yanayohusu haki za binadamu (UPR).
DSC_0108
Meza kuu kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bibi Mary Massay, Mkuu wa Balozi za Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania na Afrika Mashariki Filiberto Ceriani-Sebregondi, mgeni rasmi Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mh Ali Hassan Rajab na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez katika maadhimisho ya siku ya haki za binadamu duniani yaliyoenda sambamba na mkutano wa kujadili utekezaji wa makubaliano ya haki za binadamu na maandalizi ripoti ijayo.
Balozi huyo alitaja mapendekezo hayo ni pamoja na kufuta adhabu ya kifo, kuweka umri unaoruhusu ndoa na kuchukua hatua za kulinda waandishi wa habari na kulinda utamaduni wa wananchi wake.
Alisema mambo hayo ni sehemu muhimu ya kutekeleza maazimio ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu.
Aidha balozi huyo pia aliitaka serikali kukamilisha kamisheni ya haki za binadamu na utawala bora na kuiwezesha kufanyakazi zake zinazopaswa ikishirikiana na asasi za kiraia na wadau wengine wa haki za binadamu.
Hata hivyo alisema jumuiya hiyo itaendelea kufanyakazi na serikali katika kuhakikisha kwamba haki za binadamu zinazlindwa.
Hata hivyo balozi huyo amesema ni vyema kuendelea kuyafanyia kazi mapendekezo mengine 119 ambayo serikali ilikuwa imeyakubali na kuonesha mafanikio yake katika majadiliano yajayo.
IMG_6732
Pichani juu na chini ni baadhi ya mabalozi, wadau wa haki za binadamu na wageni waalikwa wakifuatilia hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika maadhimisho ya siku ya haki za binadamu duniani yaliyoenda sambamba na mkutano wa kujadili utekezaji wa makubaliano ya haki za binadamu na maandalizi ripoti ijayo.
IMG_6638
IMG_6633
IMG_6630
IMG_6739
Nkason Sarakikya kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali akitoa tathmini ya hali ya haki za binadamu Tanzania kwenye maadhimisho ya siku ya haki za binadamu duniani yaliyoenda sambamba na mkutano wa kujadili utekezaji wa makubaliano ya haki za binadamu na maandalizi ripoti ijayo.
DSC_0193
Balozi Mdogo anayeshughulikia masuala ya habari na siasa kutoka Jumuiya ya Ulaya Tanzania, Bi. Laura REALE, akiuliza swali kuhusiana na uboreshaji wa sheria ya ndoa za utotoni kwenye mkutano wa kujadili utekezaji wa makubaliano ya haki za binadamu na maandalizi ripoti ijayo wakati maadhimisho ya siku ya haki za binadamu duniani.
DSC_0176
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem akizungumza kwenye mkutano huo wa kujadili utekezaji wa makubaliano ya haki za binadamu na maandalizi ripoti ijayo.
IMG_6584
DSC_0186
Dr. Khoti Kamanga kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Kitivo cha sheria akitoa maoni kwenye mkutano wa kujadili utekezaji wa makubaliano ya haki za binadamu na maandalizi ripoti ijayo.
IMG_6762
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu (katikati), Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama pamoja na Afisa Habari wa Umoja wa ulaya Tanzania (EU), Susanne Mbise (kushoto) katika picha ya pamoja.
DSC_0089
Mkuu wa Balozi za Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania na Afrika Mashariki, Mh. Filiberto Ceriani-Sebregondi (kushoto) akiteta jambo na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati). Kulia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bibi Mary Massay.
IMG_6556
Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu THRDC Taifa, Bw. Onesmo Olengurumwa akiteta jambo na Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mh. Lennarth Hjelmaker wakati wa mkutano wa kujadili utekezaji wa makubaliano ya haki za binadamu na maandalizi ripoti ijayo ulioenda sambamba na maadhimisho ya siku ya haki za binadamu duniani.
IMG_6533
Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe,Egon Kochanke ( wa pili kushoto) akibadilishana mawazo na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mh. Diana Melrose (wa pili kulia) pamoja na wakili wa serikali ya mapinduzi Zanzibar, Bw. Othman Suleiman wakati wa maadhimisho hayo.
DSC_0128
Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bibi Mary Massay (kushoto) akiongozana na Mkuu wa Balozi za Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania na Afrika Mashariki, Mh. Filiberto Ceriani-Sebregondi (katikati) pamoja na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez kuelekea sehemu maalum kwa ajili ya picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa kujadili utekezaji wa makubaliano ya haki za binadamu na maandalizi ripoti ijayo katika kuadhimisha siku ya haki za binadamu duniani.
DSC_0136
Mgeni rasmi Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mh Ali Hassan Rajab (wa pili kulia waliokaa) katika picha ya pamoja na wadau waliohudhuria mkutano wa kujadili utekezaji wa makubaliano ya haki za binadamu na maandalizi ripoti ijayo ulioenda sambamba na maadhimisho ya siku ya haki za binadamu duniani.
DSC_0144
Balozi wa Ireland Nchini Tanzania, Mh. Fionnuala Gilsenan (kulia) akibadilishana mawazo na Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bibi Mary Massay (kushoto) mara baada ya zoezi la picha ya pamoja. Katikati ni Mshauri mwandamizi wa haki za binadamu kutoka Umoja wa Mataifa Tanzania, Chitralekna Massey.

HABARI NJEMA, WATANZANIA TUSICHOKE KUPIGA KURA ZIMEBAKI SIKU CHACHE #Happiness4MissWorld

$
0
0
10614252_800789863300579_6044778737800766960_n
NEW TOP 10 on the Miss World People's Choice!
AUSTRALIABARBADOSHAITIINDIANEPAL NETHERLANDS PHILIPPINES SOUTH AFRICA TANZANIA - NEW ENTRY!THAILAND
TANZANIA jumps up into the top 10 today, with Russia dropping out!
Voting closes 15:30 on Sunday 14th December, so there is only 96 to go!
Download the Miss World App for free to register your vote now!
10846445_10152970401239974_5092824672817370692_n

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHUTUBIA WAWAKILISHI WA AFRIKA KATIKA MKUTANO WA MAZINGIRA DUNIANI (COP20) JIJINI LIMA, PERU

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Wawakilishi wa Afrika katika mkutano wa Mazingira wa Dunia (Cop20) (hawapo pichani) alipokuwa akiwahutubia leo Desemba 11, 2014. Katikati ni Waziri wa Mazingira wa Sudan, (kushoto) ni Mwenyekiti wa Kamati ya Wataalam ya Afrika katika masuala ya Majadiliano ya Mabadiliko ya Tabianchi kutoka nchini Sudan, Nagmeldin El-Hassan
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Wawakilishi wa Afrika katika mkutano wa Mazingira wa Dunia (Cop20) (hawapo pichani) alipokuwa akiwahutubia leo Desemba 11, 2014. katika mkutano wa Mazingira wa Dunia unaoendelea Jijini Lima, nchini Peru.Katikati ni Waziri wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Tanzania, Dkt. Binilith Mahenge. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Wataalam ya Afrika katika masuala ya Majadiliano ya Mabadiliko ya Tabianchi kutoka nchini Sudan, Nagmeldin El-Hassan, wakati alipokuwa akiwasili katika ukumbi wa mikutano kwa ajili ya kuzungumza na wawakilishi wa Afrika katika mkutano wa Mazingira Duniani (Cop20) unaoendelea jijini Lima, nchini Peru.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya wawakilishi wa Afrika katika mkutano wa Mazingira wa Dunia (Cop20) baada ya kuwahutubia leo Desemba 11, 2014, katika Mkutano wa Mazingira Duniani na majadiliano kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, unaoendelea jijini Lima, nchini Peru.

  Sehemu ya Wawakilishi wa nchi za Afrika katika mkutano wa Mazingira Duniani, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akiwahutubia leo, Desemba 11, 2014, mkutano wa Mazingira Duniani (Cop20) unaoendelea jijini Lima, nchini Peru. Picha na OMR

MHESHIMIWA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AHUTUBIA WAWAKILISHI WA AFRIKA KATIKA MKUTANO WA MAZINGIRA DUNIANI (COP20) JIJINI LIMA, PERUDESEMBA 11, 2014

Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal jana Desemba 10, 2014, amewahutubia wawakilishi wa Afrika katika Mkutano wa Mazingira Duniani (Cop20) unaofanyika jijini Lima, nchini Peru. Mheshimiwa Makamu wa Rais anahudhuria mkutano huu akimuwakilisha Rais Jakaya Kikwete ambaye ni Kiongozi wa Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi. Mkutano huo wa jana ulikuwa na dhima ya Afrika baada ya mwaka 2015: Makubaliano Mapya kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi.

Awali Mheshimiwa Dkt. Bilal aliwaambia wawakilishi wa Afrika katika mkutano uliojumuisha Mawaziri wa Afrika wanaoshughulikia masuala ya Mazingira katika nchi zao kuwa, Afrika licha ya unyonge wake bado inalo jukumu la kusimama kidete katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na ili kufanikiwa katika jambo hilo ni muhimu kwa Bara hili kuwa na sauti ya pamoja. 

Mheshimiwa Makamu wa Rais aliendelea kusema kuwa, Bara la Afrika lina kila sababu ya kuwa na mipango yake ambayo itatumika kushirikisha nchi za nje ya Afrika ili kwa pamoja Dunia iweze kuwa na kauli inayofanana yenye kulenga kukabiliana na majanga yanayotokana na mabadiliko ya Tabia Nchi licha ya kuwepo tofauti za kimaendeleo kati ya Afrika na nchi za mabara mengine.

Awali akizungumza kabla ya Mheshimiwa Makamu wa Rais, Waziri wa Mazingira wa Sudan ambaye ni Mwenyekiti wa kundi hili la Afrika Dkt.  Hassan Albdelgadir Hillal alisema, kundi la Afrika linapongeza uongozi wa Tanzania kupitia kwa Rais Jakaya Kikwete kwa namna unavyosimamia agenda hizi za mabadiliko ya Tabia Nchi na kusimamia upatikanaji wa sauti moja kutoka kwa nchi za Afrika. Dkt. Abdelgadir aliendelea kusema kuwa, Afrika inatakiwa kutumia mkutano huu wa Lima kwa umakini ili kuhakikisha mipango inayofikiwa inapata kutambulika na kuonekana mwakani wakati mkutano kama huu utakapofanyika jijini Paris.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Binilith Mahenge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mawaziri wa Mazingira kwa nchi za Afrika yeye alibainisha kuwa, viongozi wa nchi za Afrika wamekuwa mstari wa mbele kabisa kuhakikisha kuwa Afrika inasikika na kwamba anatarajia ushirikiano katika ngazi ya Mawaziri kuendelea hata pale atakapokuwa anakabidhi nafasi hiyo kwa Waziri wa Mazingira wa Misri.

Katika mkutano mwingine ambao pia ulikuwa mwendelezo wa Siku ya Afrika katika COP20, Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal alisisitiza kuwa Afrika inatakiwa kuhakikisha vijana na akina mama wanakuwa mstari wa mbele katika kukabiliana na hali hii ya mabadiliko ya tabia nchi. 

“Makundi haya ni muhimu sana kwa kuwa ndiyo yanayohusika moja kwa moja na shughuli za kila siku. Hatutaweza kufanikiwa kama tutayaacha makundi haya nyuma,” alisema Mheshimiwa Makamu wa Rais katika Mkutano huo ambao pia ulihutubiwa na Dkt. Fatima Denton, Mkurugenzi wa Harakati Maalum kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kamishenbi ya Uchumi kwqa Afrika (UNECA).

Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Lima, Peru

DK. REGINALD MENGI AZINDUA TASWE SACCOSS JIJINI DAR

$
0
0

Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Media, Dk. Reginald Mengi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs ( TASWE - Saccoss) uliofanyika katika ukumbi wa St. Peter's jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE - Saccoss), mama Anna Matinde na  Balozi Mdogo wa India, Baluinder Humpal. Picha zote na Cathbert Angelp Kajuna wa Kajunason Blog.

Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Media, Dk. Reginald Mengi akishirikiana na Balozi Mdogo wa India, Baluinder Humpal.
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Media, Dk. Reginald Mengi akikabidhiwa zawadi kwa mchango wake anaoutoa katika jamii.
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Media, Dk. Reginald Mengi akiongea machache.

Mwenyekiti wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs ( TASWE - Saccoss), mama Anna Matinde alisema "Tumeanzisha Saccos hii ili kupambana na changamoto za upataji wa mikopo kwa riba kubwa na kuwajengea watanzania tabia ya kuweka akiba.

Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Media, Dk. Reginald Mengi akikagua miradi mbali mbali inayoendeshwa na akina mama wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs ( TASWE - Saccoss) wakati wa uzinduzi uliofanyika katika ukumbi wa St. Peter's jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Media, Dk. Reginald Mengi akionyeshwa jiko la kisasa linalopunguza matumizi. Pembeni kwake ni Balozi Mdogo wa India, Baluinder Humpal katikati wakiongozwa na mwenyeji wao Mwenyekiti wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs ( TASWE - Saccoss), mama Anna Matinde.
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Media, Dk. Reginald Mengi leo Disemba 10, 2014 amezindua Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs ( TASWE - Saccoss) itakayowawezesha watanzania na wanachama kuweka akiba, kukopa na kununua hisa kwaajili ya kupata mitaji ya kuboresha shughuli zao za kijamii na kiuchumi.
Akiongea wakati wa uzinduzi Dk. Mengi aliwataka wanachama watumie fursa hii kupata mikopo kwaajili ya kutanua biashara zao, lakini pia wahakikishe wamejipanga mathubuti na kujiwekea malengo endelevu ambayo yataleta tija katika maendeleo yao.
"Nanawatia moyo wote, na pia ninapenda kuwapongeza sana na nawatakia kila lakheri" Alisema Mengi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs ( TASWE - Saccoss), mama Anna Matinde alisema "Tumeanzisha Saccos hii ili kupambana na changamoto za upataji wa mikopo kwa riba kubwa na kuwajengea watanzania tabia ya kuweka akiba. Mpaka sasa tuna wanachama zaidi ya 200 hapa Dar es Salaam na tumejipanga kutanua wigo na kufungua matawi zaidi Kanda ya Kaskazini, mikoa ya Dodoma, Mtwara, Lindi, Mwanza hadi ifikapo mwezi wa tatu mwakani.
Lakini pia ipo miradi tuliyonayo yenye lengo la kuinua na kukuza chama hiki cha saccoss na kunufaisha wanachama wake.Ofisi zetu ziko Oysterbay, Dar es Salaam hivyo nawakaribisha wanachama wapya kujiunga
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa email annamatinde@gmail.com au 0754692994.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais,Mh.Ummy Mwalimu afanya ziara ya ukaguzi wa mazingira kiwanda cha Ok Plastic jijini Dar

$
0
0
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu amefanya ziara ya ukaguzi wa mazingira katika kiwanda cha OK Plastic kilichopo jijini Dar Es Salaam. Ziara hiyo ni muendelezo wa ziara za kuangalia hali ya mazingira kwenye viwanda mbalimbali hapa Nchini.
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu akipata maelezo ya uendeshaji wa kiwanda cha OK Plastic kutoka kwa Menejimenti ya kiwanda hiko.Wengine wanaofuatia ni Mkurugenzi Msaidizi-Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais bi Magdalena Mtenga, Bwana Anacleto Pereira Mkuu wa Idara ya sheria wa OK plastic, Fadl Ghaddar Mkurugenzi Mtendaji wa OK plastic na Martin Msamba Meneja wa kiwanda.

  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu akimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Magdalena Mtenga wakati wa ziara hiyo.
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu akiangalia jinsi betri chakavu zinavyohifadhiwa kiwandani hapo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalim akielekeza jambo wakati wa ziara ya kutembelea kiwanda cha OK Plastic kilichopo jijini Dar Es Salaam

tuzo ya mbunifu bora wa mwaka swahili fashion week

$
0
0
Mkurugenzi Msaidizi wa Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Leah Kihimbi akimkabidhi Tuzo mshindi wa kipengele cha Mbunifu Bora wa mwaka wa Swahili Fashion Week mwaka huu Kiki Zimba


Na Evance Ng'ingo
WIKI iliyopita hapa nchini ilifikia tamati ya Onesho kubwa la mavazi kwa Afrika Mashariki na Kati la Swahili Fashion Week ambapo kwa mwaka huu onesho hilo limetimiza  miaka saba.

Onesho hilo linaloandaliwa na kampuni ya 361 degree lilishirikisha wabunifu 24 kutoka ndani na nje ya Tanzania ambao walijikita zaidi katika ubinifu wa mavazi ya aina mbalimbali.

Onesho hilo lililoendana na utoaji wa Tuzo kwa washindi wa vipengele mbalimbali waliokuwa wakishindanishwa pia katika onesho hilo.

Meneja wa onesho hilo Washington Benbella anasema kuwa kwa mwaka huu onehso limeongezewa ubunifu zaidi kwa kuwa kwanza limefanyika katika eneo jipya ambalo ni hoteli ya Sea Cliff pia kumekuwa na mwamko zaidi kutoka kwa wabunifu hasa wabunifu wa ndani.
Anaongeza kuwa kwa mwaka huu hata katika kipengele cha Mbunifu Bora Chipukizi kimeboreshwa zaidi na kujikuta kikiongeza hamasa kwa wabunifu wnegi chipukizi kujitokeza zaidi kuonesha vipaji vyao.

"Kila mwaka Swahili Fashion inajitaidi kuja na kitu kipya kwa mwaka huu tumeona kuwa ni vema tukaja na mambo mengi zaidi kwa lengo la kuwapatia mwanya wabunifu wa kitanzania na wa nje ya nchi kubadilishana uzoefu ambapo wameshirikiana kwa kiasi kikubwa katika hilo"anasema Washington.

Onesho hilo la siku mbili lilianza tangia Desemba 5 na kumalizika Desemba  7 liliendana na mauzo ya bidhaa mbalimbali nje ya eneo la onesho na pia mchana wa siku ya mwisho wa kulikuwa na mauzo ya bidhaa mbalimbali za wabunifu nyumbani kwa Balozi wa Canada Masaki, Dar es salaam.

Onesho lilifunguliwa na Mbunifu Mkongwe katika tasnia ya ubunifu wa mavazi hapa nchini Ailinda Sawe Afrika ambapo alionesha nguo zake za aina mbalimbali kabla ya kuja mbunifu wa lebo ya H & A Dress to Impress.Pia siku hiyo ya kwanza hiyo hiyo pia zilishuhudiwa kazi za wabunifu kama vile kutoka lebo la Kiarasheba inayomilikiwa na Mbunifu Boke Chacha, The Mabinti Centre Handmade, Tanzania & Can Wear Designs na  Sabina Mutsvati kutoka nchini Zimbabwe.

Shoo hiyo ilichukua takribani saa mbili na kisha ikafungwa kwa siku ya kwanza huku siku ya pili pazia lilifunguliwa na Lucky Creations  kisha ikaja zamu ya mbunifu  Jamilla Vera Swai na baadae Asia Idarous Khamsin.

Pia ikaja zamu ya Mkomanile Craft na wakafuata akina Jose Rui Lopez  kutoka nchini Angola, Jacquelines Collection, Taati Sibolile Maison kutoka nchini Namibia na  Kiki's Fashions.
Siku ya tatu ilionekana kuwa ndio nzuri zaidi kwa kuwa wabunifu wengi wa mavazi wakubwa akina Martin Kadinda, Manju Msita, Innocent Dorkenoo wa Ghana,  Gabriel Mollel, Anisa Abayas na Palse wa Afrika Kusini walionesha mavazi yao.

Kwa upande wa Tuzo zilizokuwa zikishindaniwa , mbunifu wa mavazi Kiki Zimba ametunukiwa tuzo ya kuwa mbunifu bora wa mavazi kwa mwaka huu iliyotolewa katika onesho la mavazi la Swahili Fashion 2014.
Pia Mwanamitindo wa kimataifa mtanzania aishie Marekani Millen Magese alishinda tuzo ya mtu mwenye mvuto zaidi nchini ijulikanayo kama  Mercedes - Benz Style Icon of the Year iliyotolewa kwenye tuzo za Swahii Fashion 2014.
Katika kipengele hicho alikuwa akishindanishwa na akina Nasib Abdul, Diamond Platinum, Mohamed Dewji   na Wema Sepetu.
Millen pia alitunukiwa tuzo ya kutambua mchango wake kama mwanadada mwenye  mchango mkubwa katika kusaidia jamii yake.
Tuzo hizo zilizoandaliwa na kampuni ya 361 degree ambayo pia imeandaa onesho hilo, kulikuwa na utoaji wa tuzo nyingine mbalimbali zilizotolewa kwa wadau wa mitindo nchini kwa lengo la kutambua mchango wao katika kuendeleza fani hiyo.
Mbunifu wa mavazi Martin Kadinda alichaguliwa kuwa mbunifu bora wa mavazi ya kiume huku Jamila Nyangassa akichaguliwa kuwa mwanamke wa mwaka.

Gazeti tando (blog) ya Missie Populaar ilichaguliwa kuwa blog bora ya mwaka  huku mbunifu wa mavazi Husna Tandika akitajwa kuwa ndio mbunifu bora  anaechipukia.
Pia mwandishi wa habari wa kituo cha Eatv Deogratius Kithama alichaguliwa kuwa mwandishi bora wa mavazi ya kiume, na Albert Manifester alichaguliwa kuwa mpiga picha bora wa masuala ya Mitindo.
Wengine walioshinda tuzo ni pamoja na Rehema Samo alietajwa kuwa mrembaji bora wa mwaka na Irfan Rizwanali kuwa mtaalamu bora wa kuwapendezesha watu mbalimbali.
Akizungumzia ushindi wa kuwa mbunifu bora wa mavazi kwa mwaka huu, Kiki Zimba alisema kuwa ushindi huo unatokana na nia ya dhati katika tasnia hiyo hasa kwa kujituma kwa hali na mali katika kutengeneza nguo bora zaidi.

"Mwaka huu nimefanya kazi kubwa zaidi kwa kuwabunia watu mbalimbali hadi nimeweza kushinda tuzo hii ninaomba na watu wengine wajitokeze zaidi katika kutuunga mkono wabunifu wa ndani kwa kushona nguo kwetu"alisema Kiki.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Leah Kihimbi alisema kuwa serikali itaendelea kusaidia tasnia ya Mitindo nchini huku akiipongeza kampuni ya 361 degree kwa kutimiza miaka saba katika kuandaa onesho hilo la Swahili Fashion Week.
Swahili Fashion Week na Tuzo za mwaka 2014 zinaandaliwa na 361 Degrees kwa usaidizi wa Hotel Sea Cliff, Sea Cliff Court, chini ya udhamini wa EATV, East Africa Radio, Basata, Baileys, Mercedes-Benz,  2M Media, Tanzania Printers LTD and Syscorp Media.

 



KATIBU WA CCM MKOANI IRINGA AWAONYA WANAVYUO KUJIHUSISHA NA MASWALA YA SIASA

$
0
0



katibu wa chama cha mapinduzi mkoani iringa HASSANI MTENGA akiwahutubia wananchi wa mataa wa semtema mjini iringa
 wananchi wa mtaa wa semtema wakimsikiliza katibu wa  ccm mkoa HASSAN MTENGA
 hapa wakiwa makini wakisikiliza maneno matamu wakati wa mkutano huo

Na Fredy Mgunda, Iringa.
 
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Iringa HASSANI MTENGA, amefungua rasmi kampeni za uchaguzi wa Serikali za mitaa katika mtaa wa semtema  mkoani iringa.


Akiwahutubia mamia ya wananchi wa mtaa wa semtema MTENGA aliwataka wananchi wa eneo hilo kuwa makini wakati wa kuchagua kiongozi katika uchaguzi utakao fanyika tarehe 14/12/2014.

MTENGA alisema kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi na watu binafsi kwa kuwa kila maendeleo yanaanzi chini ndio yanaenda juu,hivyo wananchi wanatakiwa kuwa makini sana na kumchagua kiongozi anayefaa.

 aidha MTENGA aliwataka wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani iringa kuacha kuiga siasa chafu ambazo waiga kutoka kwa wapinzani wao kwa kuwa wanaiga kitu ambacho hawakijua ambacho kitawaletea madhara baadae.

alisema kuwa IRINGA ni ya watu wa iringa hivyo kuwaambia wanafunzi wa vyuo vyote mkoani iringa kuwaachia siasa wana iringa na wao waendelee na walicho kifuata hapa na sio isasa.

kwa upande wake wanafunzi waliohudhuria mkutano huo walimsifu katibu huyo wa chama cha mapinduzi kwa kuwa na sera zinazotekeleza na kuwaambia ukweli vijana waliopo vyuoni kwqa kuwa wananfunzi wengi wamekuwa wakiiga mambo mengi bila kujua nini kipo mbele yao.

lakini wananchi waliojitokeza eneo hilo walimuita katibu huyo kwa jina dawa ya muarobaini kwa maneno aliyoyatoa katika mkutano huo na kumsifu kiongozi huyo kuwa ni kiongozi ayefaa kuigwa hapa mkoani iringa.

 pia kunabaadhi ya wananchi walisikika wakisema kwa sera za katibu MTENGA mbunge wa jimbo la iringa mjini atake asitake ataondoka tu na kumwomba aanze kukusanya kilicho chake.

GROOVEBACK NITE YASHEREKEA MIAKA 6 JUMAMOSI HII- EAST 24/ARCADE-PARKING PLACE

Mshindi wa Big Brother 2014,Idris Sultan azungumza na wanahabari jijini dar leo

$
0
0
 Mshindi wa Big Brother 2014,Idris Sultan akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es salaam leo,wakati akizungumzia ushindi wake na uzoefu alioupata katika Jumba hilo la Big Brother huko nchini Afrika Kusini.Kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Furaha Samalu na kushoto ni Meneja Uhusiano wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Barbara Kambogi.
  Mshindi wa Big Brother 2014,Idris Sultan akisisitiza jambo wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es salaam leo.
Idris akizungumza.
 Alikuwa Mshiriki mwenza wa Idris Sultan,Irene Laveda akizungumza machache kwenye Mkutano huo.
 Meneja Uhusiano wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Barbara Kambogi akizungumza jambo wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo.
 Sehemu ya Waandishi wa habari waliofika katika Hoteli ya Hyatt Regency kumsikiliza Mshindi wa Big Brother 2014,Idris Sultan.
Mshindi wa Big Brother 2014,Idris Sultan (pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja Masoko wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Furaha Samalu (pili kulia),Meneja Uhusiano wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Barbara Kambogi (kushoto) pamoja na Mwanalibeneke Othman Michuzi a.k.a Mzee wa Mtaa kwa Mtaa
 Wadau wakipiga picha ya pamoja na Idris na Laveda.
 Mpiga picha na Blogger,Salma Msangi kazini.

Na   Bakari   Issa,Dar  es  Salaam

Mshindi  wa  Big  Brother  Africa   2014,Idris  Sultan ameeleza  siri  ya mafanikio yake  katika  shindano lililomalizika hivi karibuni  nchini  Afrika   ya  Kusini mbele ya waandishi wa habari waliofika kumsikiliza leo kwenye hoteli  ya  Hyatt Regency jijini  Dar  es  Salaam.

Idris  alifanikiwa kupata  ushindi  huo  baada  ya  kupigiwa kura  na nchi tano ambazo   ni  Tanzania,Kenya,Uganda,Rwanda pamoja na Namibia  na  kutwaa  Dola  za  Kimarekani 300,000  sawa  na  shilingi  Milioni 500 za Kitanzania na kufanikiwa kumbwaga mpinzani wake,Tayo kutoka  nchini Nigeria.

Idris  amesema  kuwa  ushindi   huo  ni  kwa  ajili  ya  mashabiki  hususan   waliompigia  kura  wakati  akiwa  katika  jumba   la  Big  Brother  huko  Afrika  ya  Kusini  na  kutoa  shukrani  kwa  nguvu,bidii  ambazo  watu  walimuekea  yeye na  kupata  ushindi  huo.

“Ushindi huu si wa kwangu peke yangu bali ni ushindi wa mashabiki ambao waliniwekea nguvu  pamoja na bidii na kufanikisha ushindi huu,”alisema Idris.

Pia  Idris  amezitaja  changamoto  alizokutana nazo  katika  jumba  la  Big  Brother  kuwa ni  kutokumjua mtu kama anakurekebisha au anakutoa kwenye njia,hivyo basi kushindwa kujua njia  sahihi ya kushindana.

“Kutokujua Waafrika wanafikiriaje, hauwezi   kujua    mtu    anakurekebisha     au  anakupotosha au  anakutoa  kwenye  njia,unashindwa kufahamu hiyo ndiyo changamoto niliokutana nayo,”alieleza  Idris

Aidha, amewataka  washiriki wa Tanzania watakaokuja kushirika shindano hilo,wasifikirie watu  wanafanya nini ndani ya jumba bali wafanye wao kama wao na sio kumuiga mtu mwingine.

MASHINDANO YA MPIRA WA MIGUU KWA COLLEGE NA SCHOOL ZA UDSM YAPAMBO MOTO

$
0
0
Wachezaji wa timu ya COSS (College of Social Science) ya chuo kikuu cha Dar es salaam kwenye picha ya pamoja wakati wa kujiandaa kucheza. Kikosi hiki ndicho kinachoongoza kundi B la wanaoshindana chuoni hapo.

*       SJMC (School of Journalism & Mass communication)  wanaongoza kilele cha group A
*       COSS (College of Social Science)  wanaongoza kilele cha group B
*       Mechi zingine nne kuendelea leo hadi Jumamosi

Mashindano ya mpira wa miguu kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) yanayojulikana kama Airtel UNI255 yanayoshirikisha wanafunzi wote wa schools na Colleges zilizopo chuoni hapo yameendelea kwa  kasi yakiwa leo yameingia siku ya tatu toka kuanza kwake huku baadhi ya washiriki wakijichukulia ushindi na kuongozo msimamo wa mchezo huo na wengine kuendelea kusuasua .

Akiongea kuhusiana na mwenendo wa mashindano hayo kwa sasa Waziri wa michezo wa jumuiya ya wanafunzi chuo kikuu cha Dar es salaam STANLRY JULIUS alisema "Mashindano ya mwaka huu yamekuwa na mvuto wa kipekee hasa kutokana na wadhamini wetu Airtel kutupatia vifaa vya kutosha na kwa namna moja yameongeza hari sana kwa washiriki wote

Hadi sasa kinara wa kundi A ambao mechi zao zinachezwa pale katika viwanja vya ndani chuo kikuu cha Dar es salaa ni SJMC (School of Journalism and Mass Communication) alicheza mechi mbili na kushinda zote na kujitengenezea pointi 6 na huku akiongoza kwa kuwa na bao 5 za kufunga.

Kundi B ambao mechi zao zinazochezewa katika viwanja vya chuo kikuu za Mabibo maarufu kama Mabibo Hostel linaongozwa na COSS (College of Social Science) ambapo imecheza mechi 3 ikashinda moja na kutoa sare ya bila kungana mechi 2. Kwa matokeo hayo wanapointi 5 na goli 2.

Mashindano haya ya Airtel UNI255 yanaendelea tena leo na yatafikia tamati siku ya jumamosi kwa fainali itakayokutanisha mshindi wa kundi A na kundi B na baadae Airtel imeandaa tamasha maalum la vipaji maalum kwa wanafunzi wa  chuo hicho litakalofuatiwa burudani kali toka kwa wasanii maarufu wa kizazi kipya nchini akiwemo shilole, Ney wa Mitego, Roma na wengineo. Aidha katika kilele cha tamasha hilo Airtel itazindua kwa wanafunzi wa chuo kikuu huduma ya UNI255 itakayowawezesha kuwasiliana , kuperuzi internet kwa gharama nafuu.

MIUNDOMBINU YA BANDARI YA KIGOMA KUBORESHWA NA KUPANULIWA

$
0
0
 Sehemu ya chelezo zinazotumika kwa ajili ya matengenezo ya meli na boti katika Bandari ya Kigoma.
 Mkuu wa Bandari ya Kigoma, Bw. Athuman Malibamba (Katikati mbele) akifafanua jambo kwa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango mara walipofika kujionea shughuli za maendeleo kiwanjani hapo.
 Mratibu wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Senya Tuni (Wapili kushoto) akiuliza jambo kwa Mkuu wa Bandari ya Kigoma, Bw. Athuman Malibamba (Wapili kulia) walipofanya ziara bandarini hapo.

 Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Aliyenyanyua mkono) akionesha kufurahia jambo wakati walipofanya ziara katika Bandari ya Kigoma.
 Mkuu wa Bandari ya Kigoma, Bw. Athuman Malibamba (Wapili kulia) akifafanua jambo kwa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango mara walipofika kujionea shughuli za maendeleo kiwanjani hapo
 Afisa utekelezaji wa Bandari Kigoma, Bw. Teophil Luoga (Kulia aliyechuchumaa) akiwaonesha eneo la upanuzi wajumbe wa timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango mara walipofika kujionea shughuli za maendeleo kiwanjani hapo.
 Mkuu wa Bandari ya Kigoma, Bw. Athuman Malibamba (Kulia) akimkaribisha Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) mara alipofika kujionea maendeleo ya bandari hiyo.
Boti na meli zikipandisha shehena kwenye Bandari ya Kigoma.PICHA ZOTE NA SAIDI MKABAKULI
Na Saidi Mkabakuli, Kigoma
Serikali imeazimia kuendelea kuboresha miundombinu ya bandari hususan miradi iliyoibuliwa katika Programu ya Matokeo Makubwa Sasa ikiwemo kuanza kufanya upanuzi wa Bandari ya Kigoma  na kuendelea kuboresha miundombinu na ununuzi wa vifaa mbalimbali vya kuhudumia shehena katika Bandari ya Kigoma ili kuweza kukidhi mahitaji yanaongeza siku baada ya siku katika bandari hiyo.
Ahadi hiyo imetolewa na Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miundombinu katika Bandari ya Kigoma.
Bibi Mwanri alisema kuwa serikali kupitia Mamlaka ya Bandari nchini nchini ipo kwenye mkakati wa kuiendeleza bandari hiyo ili iwe ya kiwango kizuri kwa kuhudumia watumiaji wa wa bandari hiyo.
“Kama munavyokumbuka Serikali katika mwaka huu wa fedha ilipanga kuiendeleza na kuboresha miundombinu ya usafiri wa majini na anga ili kuongeza ufanisi wa sekta hizi, ambapo Bandari ya Kigoma ni mojawapo ya bandari zilizopewa kipaumbele kwa ajili ya uendelezaji,” alisema Bibi Mwanri.
Kwa mujibu wa Bibi Mwanri, upanuzi wa bandari hiyo upo kwenye hatua za upembuzi yakinifu kwa ajili ya kuboresha bandari ya Kigoma na kutwaa maeneo zaidi kwa ajili ya upanuzi wa bandari hiyo.
Akitoa taarifa ya maendeleo ya Bandari hiyo, Mkuu wa Bandari hiyo Bw. Athuman Malibamba alisema kuwa mpaka kufikia Juni 2014 hatua ya utekelezaji iliyofikiwa ni kukamilika kwa kazi ya uthamini wa mali eneo la Kibirizi lenye hekta 10 kwa ajili ya upanuzi wa bandari hiyo. “Pia, Mamlaka imempata Mtaalam Mshauri (M/S Royal Haskoning H.D.V Nederland, B.V) atakaefanya kazi ya Upembuzi Yakinifu. Aidha, kazi ya uthamini wa mali imekamilika kwa eneo la Katosho lenye hekta 69 kwa ajili ya kujenga bandari kavu,” alisema.
Kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi katika nchi za jirani kunatoa fursa ya kuimarisha miundombinu ya bandari ya Kigoma ili kuwa na uwezo wa kuhudumia shehena inayoongezeka na kukuza uchumi katika mkoa na Taifa kwa ujumla. Aidha kuanzishwa kwa Eneo Maalum la Kiuchumi, katika mkoa wa Kigoma ni kichocheo muhimu kwa Mamlaka ya Bandari (TPA) kuimarisha huduma katika bandari ya Kigoma na hivyo kuweza kuzitumia fursa zitakazojitokeza mara baada ya shughuli mbalimbali za kiuchumi kuanzishwa.

TASWIRA ZA BONDE LA MTO MSIMBAZI

$
0
0
Katika pita pita za kila siku mtaani,hivi karibuni kamera yetu ilikatiza maeneo ya Vingunguti pembezoni mwa bonde la Mto Msimbazi na kukutana na hali kama ionyekanavyo pichani hapa.kiukweli mambo si shwari katika eneo hili hasa usalama wa afya kwa wakazi waliozunguka eneo hilo.ukiangalia kwa makini utabaini kuwa kuna watoto wadogo wakiendelea na michezo katika eneo hilo bila kufahamu kuwa wapo hatarini kiafya.

PSPF YAZINDUA HUDUMA MPYA ZA MIKOPO KWA WANACHAMA WAKE.

$
0
0
 Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, (Wapili kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, (Wapili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta, (TPB), Sabasaba Moshingi, (Wakwanza kushoto) na Balozi wa PSPF, Mrisho Mpoto, wakishikana mikono kuashiria uzinduzi wa huduma mpya za mikopo kwa wanachama wa Mfuko huo kupitia TPB jijini Dar es Salaam, leo Alhamisi Desemba 11, 2014
 Balozi wa PSPF, Mrisho Mpoto, akielezea huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akitoa hotuba yake

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta, TPB, Sabasaba Moshingi, akitoa hotuba yake
 
 Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa PSPF, Masha Mshomba, akitoa shukrani kwa walkiohudhuria hafla hiyo
Mgeni rasmi Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, na viongozi wa juu wa PSPF,na TPB, wakiwa katika picha ya pamoja

 Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo, akitoa hotuba yake
 Baadhi ya wafanyakazi wa TPB, na PSPF, waliohudhuria hafla hiyo wakifuatilia mambo yanavyokwenda
Waziri Kabaka (Katikati), Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, (Kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi, wakibadilishana mawazo baada ya uzinduzi huo




Leo Desemba 11, 2014 Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa kushirikiana na Benki ya Posta Tanzania wamezindua huduma mpya kwa wateja wake, huduma hizo ni Mkopo wa kuazia Maisha na Mkopo wa elimu.

Kwa upande wa mkopo wa elimu mwanachama anaweza kukopa kwa ajili ya kujiendeleza kielimu katika ngazi yoyote ile ya elimu, mfano stashahada, shahada, shahada ya uzamili na hata mafunzo ya ufundi. Katika huduma hii PSPF imetenga jumla ya shilingi bilioni 4.

Kwa upande wa mkopo wa kuanzia maisha, mwanachama aliyepata ajira kwa mara ya kwanza huwa ana mahitaji muhimu, kwa kutambua hilo PSPF imeanzisha mpango huu ambapo mwanachama anaweza kukopa mishahara yake ya miezi miwili ili aweze kujipanga na maisha mapya ya ajira. Katika huduma hii PSPF imetenga jumla ya shilingi bilioni 2.

Lengo kubwa la PSPF kuanzisha mikopo hii ni kuhakikisha kila mtanzania anatimiza ndoto yake ikiwa ni katika masomo kwa kupitia mkopo wa elimu au ndoto yake nyingine kwa kupitia mkopo wa kuanzia maisha, hivyo natoa wito kwa watanzania  wenzetu kujiunga na PSPF ili waweze kufaidika na fursa hizi.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri wa Kazi na Ajira Mheshimiwa Gaudentia kabaka alisema amefurahishwa na PSPF jinsi ilivyoshirikiana na Benki ya Posta Tanzania katika Kubuni, Kupanga, kuandaa na hatimaye kuteleza utratibu huu, alisema hili ni jambo sahihi na mwafaka kwani kwa mujibu wa taratibu za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii duniani kote, kazi za Mifuko hii sio kutoa mikopo bali ni kuwawezesha wanachama wake kupata mafao yao stahili pale wanastaafu. 

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Bw. Sabasaba Moshingi alisema mwanachama wa PSPF anayetaka kukopa anatakiwa kwenda kwenye tawi lolote la Benki ya Posta lililopo karibu yake. Huduma za utoaji wa mikopo hii ni za haraka sana na bora.

BARAZA LA UWEZESHAJI LAWANUFAISHA WAKULIMA WA MPUNGA

$
0
0
 Anchali Seleman Mmoja wa wakulima wa mpunga katika bonde la Madibira akiandaa mbegu ya mpunga katika kitalu chake baada ya kuwezeshwa na udhamini wa Baraza la Uwezeshaji Taifa kupitia bank ya CRDB pamoja na Madibira Saccos.
 Baadhi ya wakulima waliodhaminiwa na serikali kupitia baraza la uwezeshaji la Taifa wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi kutoka baraza hilo.
Mmoja ya Mkulima aliyefanikiwa kupata udhamini wa baraza la uwezeshaji akielezea mafanikio yake baada ya udhamini huo ikiwa pamoja na ujenzi wa nyumba ya kisasa na kununua trekta na vifaa kazi vingine.(Picha na Denis Mlowe).
 
NA DENIS MLOWE, MADIBIRA
 
BARAZA la uwezeshaji Taifa limewanufaisha jumla ya wakulima 400 wa kilimo cha Mpunga wa bonde la Madibira wilayani Mbarali mkoani Mbeya kwa kuwadhamini kupitia benki ya CRDB tawi la Iringa na Madibira Saccos baada ya kupatiwa mkopo wa shilingi milioni 400 ambazo zimeweza kuwanufaisha katika kilimo cha mpunga kwa kununua vifaa vya kilimo na kukuza kipato.
 
Akizungumza na Tanzania Daima wakati walipowatembelea wakulima hao na kufanya ukaguzi wa udhamini huo mwishoni mwa wiki, Afisa Mwandamizi Mawasiliano ya Umma na Ushawishi kutoka Baraza la Uwezeshaji Taifa, Edward Kessy alisema kuwa lengo la udhamini wa serikali kwa wakulima hao ni kutekeleza mpango wa taifa wa matokeo makubwa sasa kuwawezesha wakulima kuinua kipato chao na kukuza uchumi wa nchi kupitia kilimo.
 
Kessy alisema kuwa kupita benki ya CRDB tawi la Iringa serikali wamewadhamini wakulima hao fedha hizo ambazo wanazikopa kupitia Madibila Saccos inayofadhiliwa na benki hiyo na wamepatiwa elimu ya kilimo cha kisasa ambacho kimewasaidia kuongeza uzalishaji mazao na kudhibiti tatizo la njaa wilayani humo.
 
“Baraza la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi chini ya mfuko wake wa uwezeshaji mwananchi ambao unatekelezwa kwa kushirikiana na benki ya CRDB imeweza kuwadhamini wajasiriamali mbalimbali  kwa kupitia vyama vya kuweka na kukopa nchini kuweza kupata mikopo ambayo inakuwa mitaji katika kuendeleza biashara zao na kilimo kwa ujumla na itaendelea kutoa udhamini zaidi kwa mwaka wa fedha ujao’ alisema Kessy.
 
Alisema baraza hilo hadi sasa limeweza kutoa mikopo yenye thamani zaidi ya shilingi bilioni 7 kwa wajasiriamali mbalimbali na wakulima wa mazao mbalimbali na wakulima wa mpunga Madibira wamedhaminiwa shilingi milioni 400 ikiwa ni awamu ya kwanza kwa wakulima hao.
 
Awali wakulima hao waliishukuru serikali kwa udhamini huo uliowawezesha kujikwamua kiuchumi na kuongeza kipato cha familia sambamba na kuongeza mavuno ya mpunga kwa mwaka jana.
 
Mmoja wa wakulima wa mpunga katika bonge la Madibila, Anchila Seleman alisema kuwa mkopo huo umewawezesha kukuza kipato na mavuno ingawa wanakumbana changamoto ya soko la zao la mpunga hapa nchini.
 
Alitoa wito kwa baraza la uwezeshaji kuendelea kutoa mikopo kwa wakulima kwa lengo la kuwanufaisha na kuwatafutia masoko nje ya nchi kuweza kuuza mpunga kwa faida tofauti na sasa ambapo soko limekuwa likiwadidimiza wakulima wadogo.
 
Kwa upande wake,Bruno Theodory Meneja Mahusiano wa benki ya CRDB tawi la Iringa alisema kuwa benki hiyo imekuwa ikitoa mafunzo mbalimbali kwa wakulima hao kupitia mahusiano mazuri waliyoweka na Madibira Saccos ambapo wakulima hujipatia mikopo kila mwaka kutokana na uanachama waliokuwa nao.
 
Alisema kuwa msimu wa 2013/2014 wakulima walionufaika na udhamini wa baraza la uwezeshaji ni zaidi ya 400 waliojipatia mkopo wa shilingi milioni 1 kwa kila mkulima na kuwasaidia wakulima kuzalisha mazao mengi zaidi tofauti na misimu iliyopia..

MAADHIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI YAFANYIKA MKOANI DODOMA

$
0
0
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi David Misime akiongea jambo wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili kwa wanawake na watoto yaliyofanyika Bwalo la polisi Dodoma.
 Kamanda wa polisi wilaya ya Dodoma mjini Malingumu akizungumza akizungumza katika maadhimisho hayo.
 Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Dodoma Bi. Amina Mfafaki akifafanua jambo wakati alipokuwa akiongea wakati wa kufunga maadhimisho ya siku 16 ya kupinga ukatili kwa wanawake na watoto katika ukumbi wa Bwalo la polisi Dodoma.(Picha na John Banda).
 Staff Sajent Mwanajuma Mtuli wa polisi Dodoma akisisitiza jambo kwenye ufungaji huo wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili kwa wanawake na watoto.
 Baadhi ya Askari wakifuatilia jambo kwenye kilele hicho.

Wakina mama wajawazito wa wodi ya chikande walioalikwa kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukeketaji kwa wanawake na watoto uliofanyika katika Bwalo la polisi Dodoma.

MKUTANO MKUU WA CAMFED TANZANIA WAFANYIKA MJINI DODOMA

$
0
0
Mgeni rasmi Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma, Juma Kaponda akizungumza katika Mkutano mkuu wa shirika lisilo la kiserikali la CAMFED TANZANIA ambalo linahusiana na kuwafadhili Watoto wa Kike wa Shule za Sekondari na Vyuo Vikuu hapa Nchini wenye mazingira magumu.
Mgeni rasmi Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma, Juma Kaponda akikaribishwa katika Mkutano mkuu wa shirika lisilo la kiserikali la CAMFED TANZANIA ambalo linahusiana na kuwafadhili Watoto wa Kike wa Shule za Sekondari na Vyuo Vikuu hapa Nchini wenye mazingira magumu.
Mkurugenzi kutoka Wizara ya Elimu, akiongea katika Mkutano mkuu wa shirika lisilo la kiserikali la CAMFED TANZANIA ambalo linahusiana na kuwafadhili Watoto wa Kike wa Shule za Sekondari na Vyuo Vikuu hapa Nchini wenye mazingira magumu.
Mgeni rasmi akiwa na Wafanyakazi pamoja na Wanafunzi wanaofadhiliwa na Camfed Tanzania.
Wanafunzi wa Sekondari wanaosomoshwa na shirika la Camfed Tanzania.
Wanafunzi wa vyuo vikuu wanaosomeshwa na shirika la Camfed Tanzania.

CCM INA MTAJI WA KUTOSHA KUSHINDA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

RUSSELL SIMMONS AMSHIKA MKONO TENA FLAVIANA KUITAMBULISHA FLAVIANA MATATA FOUNDATION MAREKANI

$
0
0
Flaviana Matata Mwanamitindo wa kitanzania afanyae shughuli zake za Mitindo Nchini Marekani, Jana alijiunga na rafiki, mshauri, mwekezaji na hip- hop legend , Russell Simmons, Na kuitambulisha rasmi Flaviana Matata Foundation 'FMF' nchini Marekani katika hafla fupi ilofanyika jijini New York City kwenye mgahawa wa Beautique. Nia ikiwa ni kusaidia suala la FMF katika - kuhamasisha , kuwawezesha na kuwasaidia watoto wa Tanzania katika masomo yao - wageni walioudhulia waliburudishwa na cocktail; wengi wakiwa ni models Wilhelmina Models. Kwa habari zaidi juu Flaviana Matata Foundation na jinsi ya kuchangia , bonyeza hapa.   #unamfuatilia Flaviana MatataInstagram: @FlavianaMatataFoundation Twitter: @FMFoundflavianamatatafoundation.orgtumblr_ngdxj7AcPp1swsaplo1_1280  tumblr_ngdxj7AcPp1swsaplo2_400  tumblr_ngdxj7AcPp1swsaplo3_400      tumblr_ngdxj7AcPp1swsaplo5_400  tumblr_ngdxj7AcPp1swsaplo6_400  tumblr_ngdxj7AcPp1swsaplo7_400
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images