Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live

MSUSI WA HK SALOON AFIA GUEST HOUSE,KIFO CHAKE CHAGUBIKWA NA UTATA

0
0

Askari polisi pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali ya mtaa kata ya Gongoni manispaa ya Tabora akiangalia mwili wa mwanaume mmoja ambaye ni Msusi katika moja ya Saloon za wanawake hapa manispa ya Tabora inayofahamika kama HK,Mwanaume huyo ambaye amefahamika kwa jina la Ramadhani amekutwa amefariki dunia akiwa chumbani kwake katika nyumba ya kulala wageni inayofahamika kwa jina la SALAMA GUEST ambapo ilidaiwa kuwa alikuwa ameishi katika nyumba hiyo kwa muda wa siku tatu na hatimaye kufikwa na umauti.
Mwili ukichukuliwa na Polisi  baada ya kuvunjwa mlango wa chumba katika  Guest House hiyo.
Dada huyu inasemekana kuwa ndiye alikuwa mpenzi wake marehemu huyo Ramadhani
Baadhi ya wananchi waliofika katika Guest house hiyo kushuhudia tukio hilo.
Hii ndio HK Saloon aliyokuwa akifanyia kazi msusi huyo maarufu wa nywele za akinamama ambapo kifo chake kimegubikwa na wimbi la utata kutokana na maelezo kuwa aliondoka Saloon hapo baada ya kufunga milango na kuelekea huko Guest house akiwa mzima wa afya.Habari kwa hisani ya http://kapipij.blogspot.com/

WASHINDI WA MASHINDANO YA DR MWAKA SPORTS XTRA NDONDO CUP 2014 WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO.

0
0
Shaffih Dauda ambaye ni Mtangazaji wa kipindi cha michezo Radio Clouds FM akizungumza jambo wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi mbalimbali wa mashindano ya Dr Mwaka Sports Xtra NDONDO CUP 2014 
Bwana Novatus Damiani ambaye ni kiongozi wa timu ya Abajalo iliyotwaa ubingwa wa michuano ya  Dr Mwaka Sports Xtra NDONDO CUP 2014 akipokea pesa taslimu shilingi milioni tano kutoka kwa Bi. Fatma Likwata ambaye ni mtangazaji wa Clouds Fm na Tv akimwakilisha Dr Mwaka.

 Shaffih Dauda ambaye ni Mtangazaji wa kipindi cha michezo Radio Clouds FM (Sports Extra) na Clouds TV (Sports Bar) akimkabidhi zawadi ya shillingi laki tano bwana Omary Hamis ambaye alitwaa tuzo ya gori kipa bora wa mashindano ya Dr Mwaka Sports Xtra NDONDO CUP 2014 
  Shaffih Dauda ambaye ni Mtangazaji wa kipindi cha michezo Radio Clouds FM (Sports Extra) na Clouds TV (Sports Bar) akimkabidhi zawadi ya laki tanomchezeshaji mzuri(refaree)  wa mashindano ya Dr Mwaka Sports Xtra NDONDO CUP 2014 .
 Shaffih Dauda ambaye ni Mtangazaji wa kipindi cha michezo Radio Clouds FM (Sports Extra) na Clouds TV (Sports Bar) akimkabidhi zawadi ya shilingi laki tano Bwana Suleiman Buji ambaye alitwaa tuzo ya mchezeji bora  wa mashindano ya Dr Mwaka Sports Xtra NDONDO CUP 2014 
  Shaffih Dauda ambaye ni Mtangazaji wa kipindi cha michezo Radio Clouds FM (Sports Extra) na Clouds TV (Sports Bar) akimkabidhi zawadi ya shilingi laki tano Bwana Ally Mango  ambao walitwaa tuzo ya kikundi bora kilichotoa burudani kwenye mashindano ya Dr Mwaka Sports Xtra NDONDO CUP 2014 .
Viongozi wa timu ya Burudani FC Bwana Hamad Mussa Chema(katikati) akiwa na mzee wa toroka Uje(wa kwanza kushoto) wakionesha kiasi cha shilingi milioni mbili walizokabidhiwa na Shaffih Dauda  kwa niamba ya Dr Mwaka baada ya timu ya Burudani FC kuibuka washindi wa tatu wa mashindano ya Dr Mwaka Sports Xtra NDONDO CUP 2014 
 Bwana Rogers Peter akionesha kitita cha shilingi milioni tatu alichokabidhiwa na mbili walizokabidhiwa na Shaffih Dauda  kwa niamba ya Dr Mwaka baada ya ya Tabata Fc kuibuka washindi wa pili wa mashindano ya Dr Mwaka Sports Xtra NDONDO CUP 2014 
Baadhi ya wadau waliofika kwenye tukio hil

WAHITINU 130 WA CHUO KIKUU CHA ARDHI (ARU), WATUNUKIWA TUZO KWA KUFANYA VIZURI KWENYE MASOMO

0
0
 Onesmo Charles ambaye ni mmoja wa wanafunzi 130 waliofanya vizuri katika masomo katika Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU), akijaribu kifaa cha kisasa cha kupimia ardhi, viwanja na ramani za nyumba alichozawadiwa Kampuni ya Hightech Systems (T) Limited katika hafla ya kuwakabidhi zawadi na tuzo wanafunzi hao bora  iliyofanyika katika chuo hicho leo ikiwa ni sehemu ya mahafali ya nane ya chuo hicho yatakayofikia kilele kesho kutwa Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam.
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi Dar es Salaam (ARU), Idrissa Mshoro (kulia) akimkabidhi mwanafunzi Onesmo Charles kifaa cha kisasa cha kupimia ardhi, viwanja na ramani za nyumba chenye thamani ya sh. mil. 35  baada ya kuwa mmoja wa wanafunzi 130 waliofanya vizuri katika masomo. Hafla ya kuwakabidhi zawadi wanafunzi hao bora  iliyofanyika katika chuo hicho leo, ni sehemu ya mahafali ya nane ya chuo hicho yatakayofikia kilele kesho kutwa kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Godfrey Ntaki wa Kampuni ya Hightech Systems (T) Limited.  iliyotoa zawadi hiyo. (PICHA ZOTE NA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
 Onesmo akipongezwa na wanafunzi wenzake

 Onesmo akiwa katika picha ya pamoja na wenzake
 Cheti alichotunukiwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
 Ipyana Mwangoka akikabidhiwa zawadi ya cheti
 Jonathan Kansheba akitunukiwa cheti
 Joyce Kasenga akipatiwa tuzo ya cheti
 Mariam Maringe akipatiwa tuzo
 Rashid Ngenyi akipatiwa tuzo ya cheti
 Rebecca Milano alipatiwa tuzo tano
 Tadeus Rudaichi akipokea tuzo
 Asha Muhali alituzwa tuzo tano
Anthony Mwashilingi akizawadiwa
 Bibian Abel akizawadiwa
 Faraja Ally akizawadiwa cheti
 Ikupa Mwakisole akipokea tuzo ya cheti


 Sehemu ya wanafunzi waliotunukiwa tuzo
 Meza kuu
 Wanafunzi wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa chuo hicho pamoja na wafadhili


MADINI MAPYA NDANI YA #AKCLASSICOSMETICS

0
0
KAMA MNAVYOWATAMBUA #AKCLASSIC WAO NI MWENDO WA VITU VYA UKWEE NA ORIGINAL KABISA..

SASA MALI MPYA IMEINGIA #TEAMNATURALHAIR MPOO? SAFARI HII HAMJASAHAULIKA!!

PIA KUNA HABARI NJEMA KWA WADAU WOTE WANAOSUMBUKA NA MATATIZO MBALI MBALI KUHUSU NGOZI ZAO KAMA VILE KUUNGUA KWA MIKOROGO,WEUSI WA MACHONI(DARK CYCLE),KUSWEAT KULIKOPITILIZA,AKCLASSIC WAMEAMUA KUCHIMBA NA KUJA NA MAJIBU YA MATATIZO YENU TENA MADINI YASIYO NA MADHARA KABISAAA KWA NGOZI YAKO!!

   WALE WALIOTOKA KUJIFUNGUA NA YALE YOTE YATOKANAYO HATUJAWASAHAU PIA KUANZIA CORSETS,NYWELE(T444Z JBCO NA HAIRFINITY),WEUSI WA KWAPA NA SHINGO NA OFCOUZ NA BIDHAA ZA KUPIGA USO MSASA!!

   TUPIGIE 0753482909/0713468393.TUPO KINONDONI KWA AMANYANYA NA SINZA KUMEKUCHA,

Ingia bloguni kujionea bidhaa zaidi na maelezo!!!
BLOG: www.akclassic.blogspot.com


 





Mahmoud Mgimwa atoa neema ya umeme jimboni mwake

0
0
Mbunge wa jimbo la mufindi wa kasikazini ambaye pia ni Naibu Waziri wa maliasili na utalii Mahmoud Mgimwa  
Mbunge wa jimbo la mufindi wa kasikazini ambaye pia naibu waziri wa maliasili na utalii Mahmoud Mgimwa akiwa na mkuu wa wilaya wa mufindi.
Mbunge wa jimbo la mufindi wa kasikazini ambaye pia naibu waziri wa maliasili na utalii Mahmoud Mgimwa akiwa amevalia 


Na fredy mgunda Iringa.

Vijiji 31 vilivyopo mufundi kaskazini mkoani Iringa vinatarajia kupokea umeme na tayari baadhi ya vijiji vipo katika hatua ya mwisho ya kufunga vikombe kwaajili ya kuanza kuvuta nyaya.
 
Akizungumza na mwandishi wetu katibu wa mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini ambae pia ni naibu waziri wa maliasili na utalii Babtist Mdende amesema kuwa, vijiji vinavyotarajia kupata umeme safari hii ni vile vijiji vilivyopo tarafa ya sadani,ifwagi na kibengu.

vijiji hivyo ni mapogoro, igomaa,kibada,ndolezi na vengine kama ugesa,vikula,ilasa na kipanga ambavyo upimaji bado unaendelea kwaajili ya kusimika nguzo, 
 
kunabaadhi ya vijiji vipo katika hatua ya awali ya kusimamisha nguzo ikiwepo kijiji cha Isalavanu ambacho mradi wake wa umeme unashughulikiwa na TANESCO wilaya ya mufindi”, alisema Mdende.

Aidha Mdende ameeleza kuwa kwa wale watakao ingazwa kwa mara ya kwanza yaani watu wa kwanza wakati wa kuzindua mladi wa umeme wataingiziwa kwa gharama ya shilingi elfu 30

MAREHEMU ELIAS ANTHONY MAPUNDA AZIKWA MAKABURI YA KINONDONI

0
0

1Kaka wa Marehemu Elias Anthony Mapunda Bw. Nesto Mapunda wa pili kutoka kulia na Mkewe Teddy Mapunda wakiwa wamesimama mbele ya jeneza la marehemu Anthony tayari kwa kiungia katika kanisa katoliki la Mtakatifu Matha Mikocheni kwa ajili ya misa maalum ya mazishi yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kinondoni jana Fullshangwe inampa pole Ndugu Nesto Mapunda pamoja na ndugu na jamaa kwa kuondokewa na ndugu yao mpendwa marehemu Elias Anthony Mapunda. Wao walimpenda lakini mungu amempenda zaidi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi AMEN.2Mwili wa narehemu Elias Anthony ukiombewa kabla ya kuingizwa kanisani.3Kaka wa Marehemu Elias Anthony Mapunda Bw. Nesto Mapunda wa pili kutoka kulia na Mkewe Teddy Mapunda pamoja na waombolezaji wengine wakiombea mwili wa marehemu.4Mwili wa marehemu Elias Anthony ukiingizwa kanisani
5Kaka wa Marehemu Elias Anthony Mapunda Bw. Nesto Mapunda wa pili kutoka kulia na Mkewe Teddy Mapunda wakiongoza waombolezaji kuingia kanisani.6Waombolezaji wakiwa kanisani7Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bi. Devotha Mdachi, Meneja masoko wa Bodi hiyo Geofrey Meena wakishiriki katika misa ya mazishi katika kanisa katoliki Mikocheni8Baadhi ya maofisa wa bodi ya utalii wakiwa katika misa hiyo9Msafara uliobeba mwili wa marehemu Elias Mapunda akiwasili katika eneo la makaburi ya Kionondozi tayari kwa mazishi10Msafara uliobeba mwili wa marehemu Elias Mapunda akiwasili katika eneo la makaburi ya Kionondozi tayari kwa mazishi11Teddy Mapunda akiwa na mama mkwe wake kushoto mama Agness Marangu tayari kwa kushiriki mazishi ya marehemu Elias Anthony Mapunda katika makaburi ya Kinondoni jana.13Waomboleza wakibeba jeneza la mwili wa marehemu Elias Tayari kwa mazishi.14151617Waombolezaji wakiwa makaburini18Teddy Mapunda na waombolezaji wengine ndugu jamaa na marafiki wakiweka mchanga kaburini19Nesto Mapunda kaka wa Marehemu Elias Mapunda akiweka mchanga kaburini wakati wa mazishi ya marehemu Elias.20Waombolezaji wakiwa na huzuni kubwa wakati wa mazishi ya Marehemu Elias Anthony Mapunda yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kinondoni jana.

WALEMAVU KILIMANJARO WAADHIMISHA SIKU YA WENYE ULEMAVU DUNIANI.

0
0
Askari Polisi wa kikosi cha Usalama barabarani mkoani Kilimanjaro ,wakiongoza maandamano siku ya watu wenye ulemavu duniania.
Kikundi cha Tarumbeta kikiongoza maandamano katika siku ya watu wenye ulemavu yaliyopita sehemu mbalimbali katika mji wa Moshi.
Taasisi mbalimbali zilishiriki maandamano hayo .
Mandamano yakipita Double Road huku waandamanaji wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali katika maadhimisho ya siku hiyo.
Vijana wenye ulemavu washiriki maandamano katika siku ya wenye ulemavu mkoani Kilimanjaro.
Kwaya ya wanafunzi kutoka shule ya msingi Mweleni ikiingia uwanjani kutumbuiza wakati wa siku ya watu wenye ulemavu dunia ambayo maadhimisho yake kwa mkoa wa Kilimanjaro yamefanyika katika viwanja vya kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi.
Baadhi ya watu wenye ulemavu wakifurahia nyimbo iliyokua ikiimbwa na kikundi cha shule ya msingi Mweleni(hakipo pichani)
Mgeni rasmi katika siku ya Wenye ulemavu duniani ,Grace Lyimo akiwa na viongozi wengine meza kuu wakati wa maadhimisho ya siku hiyo yaliyofanyika katika viwanja vya kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya kaskazini.

MAMA ALIYETELEKEZWA NA MUMEWE AOMBA MSAADA KWA WASAMALIA WEMA

0
0
WANAWAKE wengi duniani bado wananyanyaswa kijinsia kwa sababu za kijamii, kiuchumi na kipato licha ya kuwepo kwa elimu kuhusu haki zao.

Mwanamama Ester Charles ambaye ni mkazi wa Mwambani wilayani Ilemela ametelekezwa na mumewe aliyetajwa kwa jina la Albinus na kubakizwa na watoto wawili wadogo wanaohitaji uangalizi na usimamizi. Pichani mwanamama Ester akiwa na mtoto wake mdogo anayetaabika na ugonjwa wa kupooza.

KWA UFUPI
Mumewake alipopata mwanamke mwingine alihama nyumba aliyokuwa akiishi na mama huyu na kupanga eneo jingine kabisa bila kuikumbuka familia yake katika matumizi na mahitaji muhimu.
Alipomfikisha mumewe huyo mbele ya mikono ya Sheria alikubali kutoa huduma lakini ndani ya kipindi kifupi alitorokea kusikojulikana.
Amefika kuomba msaada toka kwa wasamalia wema watakaoguswa na simulizi yake. BOFYA PLAY KUSIKILIZA. 
Hali ya afya ya kwa mtoto Jr. Albinus si ya kuridhisha na haijafahamika nini kinachomsibu kwani bado hajafika hospitali kupata matibabu ya kina. Mtoto huyu pichani hawezi kutembea, hawezi kuzungumza kwa ufasaha wala kukaa, zaidi ya kulala tu muda wote.

CHANGAMOTO ALIZONAZO MAMA ESTER.

Hana pesa kwaajili ya chakula cha watoto.
Hana nguo kwaajili ya kuwavisha watoto na yeye binafsi.
Anadaiwa pesa ya kulipia nyumba anayoishi kiasi kwamba mwenye nyumba anataka kumfukuza.

Amejaribu kuomba kazi kwenye kaya mbalimbali na kukosa, akipewa majibu kuwa hawezi kuajiriwa akiwa na watoto (atashindwa kufanya majukumu ya mwajiri) naye hana sehemu ya kuwahifadhi iwe ndugu au majirani.
Jeh! Umeguswa tafadhali wasiliananaye kupitia namba 0753804881.

MUNGU AWABARIKI.

Mwasabwite kukonga Tamasha la Krismasi

0
0
MWIMBAJI wa nyimbo za injili nchini Edson Mwasabwite anayetamba kwa sasa na kibao chake kijulikanacho kwa jina la ‘Ni kwa Neema na Rehema’ amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi katika Tamasha la Krismasi litakalofanyika katika mikoa ya Mbeya, Iringa na Songea Desemba mwaka huu.

Mwasabwite alisema amejipanga kikamilifu kukonga nyoyo za mashabiki wake katika tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika Desemba 25, 26 na 28 hivyo mashabiki zake wajitokeze kwa wingi kupata burudani ya nguvu kutoka kwake.

Mwasabwite alisema mwaka huu watanzania wakae mkao wa kula kwa kusifu na kuabudu katika Tamasha la Krismasi kwani tayari amezindua albamu yake ya pili ijulikanayo kwa jina la ‘Asilimia mia Mungu amenihurumia’ yenye nyimbo tisa.

“Nimejipanga vizuri kutoa burudani kwa mashabiki wangu katika tamasha la mwaka huu la Krismasi kwani maandalizi ni mazuri, safari hii itakuwa zaidi ya mwaka jana kwa sasa nina nyimbo nyingi zitakazowabariki mashabiki zangu na tayari nimeshazindua albamu mpya,” alisema Mwasabwite. 

Aidha amempongeza Mkurugenzi wa Msama Promotions kwa kuweza kuandaa Tamasha kubwa la Kikristo lenye mafanikio makubwa kwa kuweza kuwakutanisha waimbaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania kwa lengo la kutangaza injili Tanzania.

“Makampuni ya Msama yanaaminika na kukubalika kwa watanzania na nchi nyingine za jirani ndio maana hata tamasha linafanikiwa, tunaomba wananchi waendelee kununua kazi zetu, tunaomba sapoti kutoka kwa waumini na mashabiki wa muziki wa Injili,” alisema Mwasabwite.
 

Kumbukumbu ya kifo miaka 9 ya Mzee Donati Kezirahabi

0
0

Ni miaka 9 tangu ulipotangulia katika makazi yako ya milele                                         siku ile ya huzuni 5 Dec 2005.                                                                
Tunakumbuka kwa huzuni upendo na uongozi wako katika familia.  
                Miongozo na mapenzi makubwa uliyotupa ndio yanayotuwezesha kusimama na kumsifu Bwana kila siku. 

Unakumbukwa sana na mke wako Hidaya Kezirahabi,  watoto wako wapenzi na wajukuu, ndugu, jamaa na marafiki wote.

“Bwana akupatie pumziko la milele, na mwanga wa milele akuangazie, upumzike kwa amani.”

“Bwana alitoa na bwana alitwaa. Jina lake lihimidiwe milele”
                                                                                             

Airtel yatoa vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh mil 15 kwa chuo kikuu cha Dar es saalam

0
0
 Meneja Masoko wa Airtel Tanzania, Aneth Muga (kushoto) akikabidhi jezi kwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Yunus Mgaya, wakati Airtel ilipokikabidhi chuo hicho msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya milioni 15/-, jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kuendesha mashindano yatakayoshirikisha vitivo mbalimbali inayotarajiwa kuanza Jumatatu Desema 08 mwaka huu. Wanaoshuhudia ni Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (wa pili kushoto) na Mratibu wa Michezo wa Chuo hicho, Dk. Crispian Maro.
 Meneja Masoko wa Airtel Tanzania, Aneth Muga (wa pili kushoto) akikabidhi jezi kwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Yunus Mgaya, wakati Airtel ilipokikabidhi chuo hicho msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya milioni 15/-, jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kuendesha mashindano yatakayoshirikisha vitivo mbalimbali inayotarajiwa kuanza Jumatatu Desema 08 mwaka huu. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Michezo wa Serikali ya Wanafunzi ya chuo hicho (DARUSO), Stanry Julius, Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (wa tatu kushoto) na Mratibu wa Michezo wa Chuo hicho, Dk. Crispian Maro.
 Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Yunus Mgaya kifurahia jezi baada ya kukabidhiwa na Airtel Tanzania msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya milioni 15/-, jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kuendesha mashindano yatakayoshirikisha vitivo mbalimbali inayotarajiwa kuanza Jumatatu Desema 08 mwaka huu. Wanaoshuhudia ni Meneja Masoko wa Airtel Tanzania, Aneth Muga (kushoto), Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (wa pili kushoto) na Mratibu wa Michezo wa Chuo hicho, Dk. Crispian Maro.

 Meneja Masoko wa Airtel Tanzania, Aneth Muga (wa pili kushoto) akikabidhi kikombe kwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Yunus Mgaya, wakati Airtel ilipokikabidhi chuo hicho msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya milioni 15/-, jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kuendesha mashindano yatakayoshirikisha vitivo mbalimbali inayotarajiwa kuanza Jumatatu Desema 08 mwaka huu. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Michezo wa Serikali ya Wanafunzi ya chuo hicho (DARUSO), Stanry Julius (kushoto), Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (wa tatu kushoto) na Mratibu wa Michezo wa Chuo hicho, Dk. Crispian Maro.

 Meneja Masoko wa Airtel Tanzania, Aneth Muga (wa pili kushoto) akimkabidhi Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Yunus Mgaya, wakati Airtel msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya milioni 15/-, jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kuendesha mashindano yatakayoshirikisha vitivo mbalimbali inayotarajiwa kuanza Jumatatu Desema 08 mwaka huu. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Michezo wa Serikali ya Wanafunzi ya chuo hicho (DARUSO), Stanry Julius (kushoto), Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (wa tatu kushoto) na Mratibu wa Michezo wa Chuo hicho, Dk. Crispian Maro.

Airtel yatoa vifaa vya michezo kwa chuo kikuu cha Dar es saalam
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imetoa vifaa vya michezo kwa chuo kikuu cha Dar es Salaam ili kuendesha mashindano yatakayoshirikisha vitivo mbalimbali yanayotegemea kuanza jumatatu ijayo katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Mchango huu ni mwendelezo wa dhamira ya Airtel katika kuendeleza michezo nchini inayodhirishwa kupitia mpango wake wa kuinua soka la vijana chini ya miaka 17 wa Airtel Rising Stars mpango ambao umewawezesha vijana wakitanzani na Afrika kwa ujumla kuonyesha uwezo wao wa kisoka na kuweza kufikia malengo yao.
Akiongoe wakati wa makabidhiano hayo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema” Leo tunatoa vifaa vya michezo ikiwemo seti 12 za jezi, shinguard, soksi, glovu za goalikipa pamoja na makombe yatakayowezesha kuendesha mashindano haya yanayoshirikisha wanafunzi kutoka vituvo mbalimbali chuoni hapa. Niwazi kwamba michezo ni burdani na ni sehemu ya kujenga mwili na afya hivyo ni muhimu pia kwa wanafunzi kutenga muda wao wa masomo na kushirikia katika michezo mbalimbali.  Natoa wito kwa wanafunzi wengi kujitokeza na kushiriki mashindano haya.”.
“Udhamini wetu leo ni mwanzo wa mkakati wa kutoa ofa kabambe itakayowapatia wanavyuo uhuru wa kuongea na kupata dhamani yamatumizi ya pesa zao
Ofa hii ya huduma maalumu ijulikanayo kama UN255 Itazinduliwa rasmi wakati wa kilele cha michuano hiii mwishoni mwa wiki ambapo wanafunzi watafurahi huduma zetu nyingi ikiwa ni pamoja na internet, ujumbe mfupi , kupiga simu kwa gharama nafuu. Aliongeza Mmbando
Kwa upande wake Naibu Makamu mkuu wa chuo Profesa Yunus Mgaya alisema” nawashukuru sana Airtel kwa mchango wa mkubwa na kwa kutuwezesha kupata vifaa vya michezo zitavyotuwezesha kuvitumia muda wote wa mashindano. Sisi kama chuo hatukuwa na bajeti ya kununua vifaa hivi hivyo msaada huu umekuja kwa wakati muafaka hivyo nawapongeza sana Airtel kwa mchango wao.”
“Vifaa hivi vitaleta tija kwa wanafunzi na kuinuua michezo chuoni hapa na ofa hii  UN255 itawawezesha wanafunzi na pamoja na  familia yetu yote ya chuo kikuu cha Dar es saalam kufurahia huduma za mawasiliano bora na kwa bei nafuu” aliongeza Mgaya.

Membe mgeni rasmi mahafali UB, kufanyika kesho Bagamoyo

0
0
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe, kesho Jumamosi Desemba 6 anatarajiwa Kuwa mgeni rasmi Katika Mahafali ya Pili ya  Chuo Kikuu Cha Bagamoyo (UB).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo kwa vyombo vya Habari Dar Es Salaam,  na Ofisa Habari wa  ( UB), Happiness Katabazi, inasema Kuwa Membe ndiye Atakuwa mgeni rasmi Katika mahafali hayo ambayo yatafanyika Katika Hoteli ya Kiromo  View Resort  kijijini Kiromo Wilayani Bagamoyo,Mkoani Pwani.

Katabazi alisema jumla ya wahitimu 99 wanatarajiwa kutunukiwa Vyeti Katika ngazi ya Shahada ya Uzamili, Shahada ya Kwanza, Diploma,  na cheti.

Wakati huo huo , Juzi Makamu wa Rais  Dk.Mohammed Gharib Bilal alishindwa kuhudhuria sherehe za uwekwaji  wa jiwe la Msingi wa makazi ya kudumu ya UB ikiwa ni ishara ya kuanza kwa ujenzi wa makao makuu ya UB kijijini hapo ambapo ujenzi ukikamilia majengo hayo yatakuwa na uwezo wa kuchukua zaidi ya wanafunzi 5000, yaliyopaswa yafanyike Katika kijijini Cha Kiromo ,Bagamoyo Mkoani Pwani kwasababu alikuwa amebanwa na majukumu mengine ya Kitaifa na akaomba apangiwe tarehe nyingine ya kuja kuweka jiwe Hilo la Msingi.

Akizungumza na waandishi wa Habari Katika kijijini Kiromo Juzi wakati akiiarisha sherehe za Utiaji wa jiwe la Msingi , Makamu Mkuu wa UB, Profesa Costa Ricky Mahalu alitoa historia fupi la shamba Hilo lililopo Kijijini Kiromo Alisema  familia yake ililinunua rasmi Agosti 26 Mwaka 2003.
  
Profesa Mahalu alisema Katika shamba Hilo familia yake imeamua kukata heka 100 na kuzitoa kwa UB ili UB iweze kujenga makazi yake ya kufumu katika Kijiji cha Kiromo na kwamba heka nyingine zilizosalia familia yake itazitoa  kwa Taasisi nyingine za elimu ya juu  na kwamba Tayari Taasisi nne za elimu ya juu ikiwemo Chuo Kikuu Kimoja Cha kigeni kimeishaonyesha nia ya kutaka Kuja Kujenga Taasisi yake ya elimu Katika shamba Hilo.

Profesa Mahalu Alisema shamba hilo kabla familia yake haijalinunua lilikuwa likimilikiwa na lililokuwa shirika la Serikali la NAFCO na baada ya kufirisika mwaka 1990  lilichukuliwa na LART  ambaye alikuwa na jukumu la kuchukua  kuuza Mashitaka ya serikali yalikuwa na matatizo ya kifedha.

' LART ikamkabidhi  kampuni ya PHLLIP&Ltd  iliyauza mashamba matatu  ya NAFCO  yaliyopo Kiromo. Hayo mashamba matatu ,Moja iliuziwa familia ya Mahalu na mkataba wa mauzo wa shamba Hilo la Mahalu na LART ulisainiwa Agosti 26 Mwaka 2903  na baada ya hapo  umiliki wa shamba  unachukuliwa  na familia ya Mahalu kwa mujibu wa Sheria.' Alisema Balozi Mahalu.

KUMEKUCHA Uhurumarathon 2014

0
0

 Mratibu wa Uhurumarathon Tanzania Innocent Melleck akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam juu ya kukamilika kwa maandalizi yam bio hizo zinazotarajiwa kufanyika jumapili hii jijini Dar Es Salaam katika viwanja vya Leders Club kushoto ni katibu mkuu wa shirikisho la Riadha la Taifa Selemani Nyambui.

MAANDALIZI ya mbio za Uhuru, Uhuru Marathon, zinazotarajiwa kufanyika Desemba 7  (jumapili) jijini Dar es Salaam yamekamilika, huku wanaridha kadhaa kutoka ndani na nje ya nchi wakithibitisha kushiriki mbio hizo zenye lengo la kuulinda uhuru wetu, kudumisha umoja, amani, upendo na mshikamano miongoni mwa Watanzania.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mratibu wa Uhuru Marathon, Innocent Melleck alisema, maandalizi yote yamekamilika, huku wanariadha wa hapa nchini kutoka nje ya Dar es Salaam wakiwa wamewasili tayari kwa ushiriki wao.
 
Melleck pia alisema, kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi ulinzi umeimarishwa kwa kiwango kikubwa ili kuhakikisha usalama unakuwa mkubwa kwa washiriki wote na barabara zitakazotumika zitafungwa katika kipindi hicho.
 
“Kila kitu kimekamilika na washiriki kutoka nje ya Dar es Salaam wameanza kuwasili kwa ajili ya mbio hizo na tunawahakikishia usalama utakuwa mkubwa mno katika kipindi chote cha mbio hizo n mpaka kufikia jana (juzi) tayari washiriki waliojitokeza walikuwa 4000,” alisema.
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), Selemani Nyambui alisema, wanariadha maarufu wa hapa nchini watakaoshiriki ni pamoja na Fabian Joseph na Dickson Marwa, huku Jacqueline Sekini aliyeshinda mbio hizo kwa upande wa wanawake mwaka jana, naye akiapa kutetea ubingwa wake.
 
“Wapo wanariadha wengi watakaoshiriki, lakini nataka kutoa angalizo kwa wanariadha kutoka Kenya, sisi tumetumwa mwaliko kwa wa chama husika na wao ndio watutumia majina ya wanariadha kumi, watano wa kiume na waliobaki wa kike, hatutapokea mwanariadha kutoka nchi hiyo ambaye hatujapewa jina lake,” alisema.
 
Nyambui alisema, tayari waamuzi watakaosimamia mbio hizo wapo tayari na akasisitiza ni lazima taratatibu zote zitafuatwa ili kupata mshindi halali.
 
Mbio hizo zinatarajiwa kuanzia viwanja vya Leaders Club na zitakuwa za kilomita 21, kilomita 5 na kilomita 3 ambazo ni maalumu kwa ajili ya viongozi wa kitaifa, dini na taasisi mbalimbali.
 
 
Aidha Melleck alisema, tayari namba kwa washiriki zimeanza kutolewa na wanaweza kuzipata katika viwanja vya Leaders Club.
Mgeni rasmi katika mbio hizo anatarajiwa kuwa Rais Jakaya Kikwete.

MBUNIFU WA MAVAZI,MANJU MSITA KUPEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA KATIKA MOZAMBIQUE FASHION WEEK 'MFW-2014'

0
0
Mbunifu wa Mavazi nchini Manju Msita kulia akizungumza na waandishi wa habari juu ya ushiriki wake katika Mozambique Fashion Week yatakayoanza desemba 10 mpaka 14 ambapo atakuwa akipeperusha bendera ya taifa
Mwanamitindo Matukio Chuma kulia akizungumza na wahandishi wa habari wakati wa kutangaza  upeperushwaji wa bendera ya tanzania katika nchi ya mozambique fashion week ambayo mbunifu wa mavazi Manju Msita atashiriki na kupeperurusha bendera ya Tanzania kushoto ni mwanamitindo Vivian Williams ambaye anafanya shughuli zake za uwanamitindo nchini Barcelona,Spain. 

TAMASHA LA MITIKISIKO YA PWANI KUFANYIKA DEC 13, 2014 DAR LIVE JIJINI DAR

0
0

Msama Video Productions yajipanga Tamasha la Krismasi

0
0
index
KAMPUNI ya Msama Video Productions imetoa tamko kwamba mwaka huu wamejipanga vizuri kufikisha ujumbe wa neon la Mungu katika Tamasha la Krismas kwani wanavifaa vipya na vya kisasa vyenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi katika mazingira yoyote yale na wafanyakazi wakutosha wenye weledi katika fani hiyo.

Akizungumza jijini Dar, Meneja wa kitengo hicho, Alpha Kigalla alieleza sababu za kufanikisha vilivyo katika tamasha hilo ni kwa sababu ya umahiri wa  watendaji wa kirengo hicho ndio chachu itakayofanikisha kutekeleza ibada hiyo kwa waumini na mashabiki watakaojitokeza katika Tamasha hilo.

Kigalla alitoa wito kwa wakazi wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kujitokeza kwa wingi kushuhudia kazi za kitengo hicho kilicho katika kampuni ya Msama kwani wana vifaa vya kisasa zaidi.

“Msama Video Productions ina vifaa vipya na vya kisasa zaidi  na hata watendaji wake wako makini zaidi na utekelezaji wa kazi zao, hivyo wadau wa muziki nchini kujitokeza kufanikisha kazi zao,” alisema Kigalla.

Meneja huyo alisema wakazi wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kujiandaa na kazi bora za Msama Video Productions ambazo zitafanikishwa kupitia waimbaji mbalimbali wa muziki huo.

MONTHLY NEWSLETTER OF THE DEMOCRATIC EMPOWERMENT PROJECT (DEP)

0
0

Tanzania Seeks Out Sunderland FC to Promote Its Tourism.

0
0
As Kenya grapples with insecurity and the consequent ailing tourism, her neighbor Tanzania is confidently striding across the borders to replenish its parks with international visitors.

A closer look at the once vibrant industry, the number of international tourists’ arrivals has plummeted owing to the incessant terror threats and attacks from the Al-Shabaab militant group thereupon scaring the visitors away.
The Tourism Recovery Taskforce, which is charged with the responsibility of instituting turnaround strategies to reanimate the ailing sector. On its list ‘Global Terrorism Index 2014’, the Institute for Economics and Peace ranked Kenya 12th most at risk of becoming less peaceful on its list of countries most affected by terrorism. The country also sits 132 on the Global Peace Index score and this insecurity setback has seen the numbers of tourist arrivals plummet.

When the task force took charge, Chairperson Lucy Karume revealed that the private sector has used over KES 14.7 million in local and international media familiarisation trips to showcase Kenya as a safe destination.

Amid the lukewarm reception, the government has set out to hire a foreign PR company to restore Kenya’s image abroad. During the World Travel Market held in London in August, Tanzania Tourist Board (an equal of Kenya Tourism Board) seized the chance to secure Sunderland FC’s services to “promote their beautiful country to a wider audience” and “develop sports tourism in Tanzania”. The ties are not new: they are deep-rooted.

Since then, the club has labeled all its flash tops “VISIT TANZANIA”. The club, in partnership with Tanzania Tourist Board and South African Airways, launched a competition whereby four lucky fans are set to jet off to Tanzania and experience the African savannah for a whole week this holiday.

What if Kenya employed such a strategy? In fact, Kenya has more elite sportsmen than Tanzania contracted in top class leagues in the world like Victor Wanyama who plays for Southampton FC in England. What if Kenya Tourism Board turned to such clubs whereby they are assured of reaching a wider audience than just an international PR firm? It’s up for debate.

MAKAMU WA RAIS DKT BILALI ABARIKI KANISA LA KIASKOFU LA ROHO MTAKATIFU LA JIMBO LA KONDOA MKOA WA DODOMA

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilai akizungumza na waumini wa Dini ya kikiristo wakati washerehe za kutabaruku Kuweka wakfu, kanisa la Kiaskofu la Roho mtakatifu jimbo la kondoa  jana 4/12/2014 iliofanyika Wilaya ya Kondoa Mkoa wa Dodoma.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal akipongezwa na Askofu wa kanisa katoliki Jimbo la kondoa Baba  Bernadin Mfumbusa mara baada ya kuzungumza na waumini wa kanisa la kiaskofu la Roho mtakatifu jimbo la Kondoa juzi 4/12/2014 iliofanyika walaya ya kondoa mkoa wa Dodoma.
 Makamu wa Rais wa jamhuri ya Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal akiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu na mashekh wa Wilaya ya kondoa mkoa wa Dodoma Mara baada ya kuzungumza na waumini wa Dini ya kikiristo jana tarehe 4/12/2014.
Makamu wqaa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal akiagana na Askofu mkuu wa Kanisa katoliki Tanzania Kardinali Polcarp Pengo wakati wa Sherehe za Kutabaruku kuweka wakfu ,kubariki kanisa lakiaskofu la roho Mtakatifu la jimbo la kondoa iliofanyika wilayani kondoa mkoa wa Dodoma juzi tarehe 4/12/2014.                                               

TAHADHARI KUTOKA MICHUZI MEDIA GROUP.

0
0

MKURUGENZI MTENDAJI WA KAMPUNI YA MICHUZI MEDIA GROUP ANAPENDA KUTAHADHARISHA WADAU POPOTE WALIPO KUHUSIANA NA UJUMBE (PICHANI JUU AMBAO UPO KWENYE FACE BOOK NA HATA KWENYE TWEETER),KWAMBA UJUMBE HUO  HAUHUSIANI KWA LOLOTE NA ANKAL MUHIDIN ISSA MICHUZI,HIVYO TUNAWASIHI TUSIHUSISHWE NAYO NA PIA TUNAWAOMBA KUWA MACHO NA MAMBO KAMA HAYA,MAANA ULAGHAI NA UTAPELI MITANDAONI NI MWINGI MNO.
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live




Latest Images